ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA THEMANINI NA TATU
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI: “sikia Radhia, wewe ni mke wangu, siwezi kuluhusu mpuuzi mwingine awe na wewe, chakufanya achana na huyo mjinga, mimi nitakupatia unacho taka, acha kuzuzuka na hayo magari ya serikali, huyo nifisadi tu” alisikika Idd, akiongea kwa kujinasib. ......... ENDELEA….
Hapo ata Edgar alimtazama Radhia, ambae sasa alionekana kukunja uso kwa hasira, machozi yanamtoka, “sikia jaribu kutumia muda wako kufwatIlia na wake zako, inaweza kukusaidia, kuliko kunigombanisha na mchumba wangu, aitokusaidia, ata kama nikiachana nae……” anasema Radhia ambae kabla ajamaliza kuongea tayari Edgar anaiwai simu na kuikata.
“Edgar naomba usiamini anacho sema Idd, ni wazi anataka kutugombanisha…” alisema Radhia huku analia, lakini akupewa muda wa kumaliza alicho kusudia kueleza, edha akamshika na kumvutia ubavuni kwake, kisha akamkumbatia, “Radhia bwana, mbona mimi nakuona ni mwanamke mwelewa na umepitia mengi sana, sasa hapo inacho kuliza nini?” ilikuwa sauti nzito na tulivu.
Radhia analia kwa kwikwi, huku anatumia kifua cha Edgar, alie kuwa tumbo wazi na bukta chini, kujifutia machozi, “sasa anaongopa makusudi ili unichukie, alafu uniache” alisema Radhia, huku anaendelea kulia kilio cha kwikwi, “sikia Radhia, mimi nilisha juwa toka jana, kuwa huyo mtu anampango wa kunishawishi nikuone ufai” alisema Edgar, na kuanza kumsimulia, jinsi Idd alivyo mfwata na kuanza kumweleza, kuhusu yeye Radhia kuwa bado mke wa mtu, huku akishauri amwache mala moja.
Mpaka Edgar anamaliza kusimulia tayari Radhia alikuwa amesha acha kulia, “kumbe alikufwata jana baada ya kuachana na sisi?” anauliza Radhia kwa mshangao, “ndiyo alinifwata, ila sikutaka kukueleza sababu nilisha ona kuwa akuwa na ukweli wowote, pia na kuamini sana, alafu nakupenda sana” alisema Edgar, huku anapapasa bega la Radhia, ambae alikuwa ameachia tabasamu la raha.
“asante Eddy, nitakupenda na kukuheshimu daima, naomba uendelee kunitunzia utu wangu” alisema Radhia, kwa sauti yenye usifu wa furaha ya wazi kabisa, “vyote utapata, nakuongezea amani na ufuraha pia, na kila kitu cha thamani ambacho unastahili kama mke wangu” alisema Edgar, na kumfanya Radhia atabsamu kwa sauti.
Naaaam!, baada ya kumaliza kubembelezana, na Radhia kutulia, sasa akionekana kuwa na furaha, Edgar anabadirisha maongezi, “nilikuambia nataka usimamie mpango wa mwaliko wa timu ya mpira wa kikapu ya King Eugen sekondari, kuanzia sehemu ya kufikia wanafunzi na vyakula watakavyo kula na sehemu ambazo wataenda kutembelea baada ya kumaliza mechi zao” alisema Edgar, akionyesha hakuwa nautani katika swala ilo.
Radhia anamtazama Edgar kwa mshangao mkubwa, “mbona swala kubwa sana ilo, nitawezaje kusimamia hayo yote?” anauliza Radhia, akuonyesha kuto kuamini anachoongea Edgar, “wala usiwe na wasi wasi, nitakuelekeza cha kufanya, ni jambo la week moja tu, katika michezo mitatu, itakuwa kama biashara ndogo kwako, ambayo itakuingizia fedha nzuri, na kujijengea jina na uaminifu kwa watu wengi” alisema Edgar, kisha akaanza kumwelekeza baadhi ya vitu, ambavyo Radhia angetakiwa kuvifanya katika mpango huo.*******
Bwana Makame yupo sebuleni amekaa mbele ya wake zake wawilina binti yake mkubwa, yani Siwema, huku Mariam na Zuhura wakiwa wamejibanza karibu na mlango wa sebuleni wakitaka kusikia kinachoongelewa huko ndani.
Mama Mariam na Siwema walitegemea kuwa, wange mkuta mzee Makame amefura kwa hasira, kutokana kile kilicho tokea, aidha kumchukia Radhia, au kumchukia Siwema alie ongea kwa sauti, lakini baada yake wanamkuta baba huyu akiwa katika hali ya utulivu, yani siyo hasira wala furaha.
“Siwema nimesikia ukiongea na simu, ebu ielezee vizuri, kwamba Radhia amefanya nini?” anauliza mzee Makame, kwa sauti tulivu huku anamtazama Siwema, ambae sasa anaona ndio wakati wa kumkomoa Radhia, na kumchonganisha kwa baba yake, ikiwezekana apigwe marufuku kuwa karibu na Edgar.
“alinipigia shemeji Idd, amenieleza kuwa kamwona Radhia anaenda kwa mwanaume, na siyo kwa mama mdogo kama alivyosema” alisema Siwema kwa sauti ya upole na tulivu, kisha akatulia subiria bomu lilipuke.
Wote wanamwona mzee Makame anamtazama mama Radhia, “ebu nieleze mama Radhia, huyu Radhia ameaga anaenda wapi?” aliuliza mzee Makame, huku anamtazama mke mdogo, yani mama Radhia, “mume wangu, kiukweli Radhia aliniaga anaenda Edgar, lakini nisingeweza kusema anaenda huko, sababu bado Edgar ajaja kujitambulisha hapa nyumbani” alisema mama Radhia kwa sauti yenye wasi wasi mwingi, hakuwa na na sababu ya kuficha chochote, maana tayari siri ilisha fichuka.
Mzee Makame bado amelekeza uso wake, kwa mke mdogo, “hivi Radhia ameolewa?” anauliza mzee Makame, swali ambalo lina utata kidogo, lakini Siwema anaona niswali ambalo lina muumbua mama Radhia, huku mama yake anatabasamia pembeni.
“Radhia ajaolewa mume wangu” alijibu mama Radhia, ambae pia akujuwa maana ya swali la mume wake, sasa mzee Makame, anamtazama Siwema, “siyo mala moja nimekusikia unasema Radhia anatia aibuhuko mitaani, ni nani na nani wamekupa taarifa za Radhia kuonekana na wanaume mtaani?,” aliuliza mzee Makame, na kumfanya Siwema ainue uso kumtazama mama yake, ambae alikuwa amekodoa macho anamtazama Siwema.
Siwema anajaribu kutafuta mtu wapili zaidi ya Idd, ambae alimweleza kuhusu Radhia kuonekana na wanaume, “ni Idd peke yake” anajibu Siwema kwa sauti ya chini, yenye kukosa nguvu ya kujiamini, mzee Makame anamtazama mke mdogo, “mama Radhia, huyu Idd ni nani kwa Radhia, si walisha achana, au bado wanaurafiki wa siri?” aliuliza mzee Makame, ambae bado alikuwa anamtazama mama Radhia.
Lakini licha ya kuwa, swali lilimlenga mama Radhia, lakini Siwema alijuwa fika jibu lake lina muumbua, Ilikuwa hiyo hivyo kwa mama Siwema, ambae aliamua awai kulijibu swali ilo, “lakini baba Siwema, ata kama walisha achana, lakini anafanya mambo ya aibu mpaka mwenzie anamwonea huruma” alisema mama Siwema, kwa sauti ya kukosoa, na kupingana na mwazo ya mume wake.
Mzee Makame anamtazama mke mkbwa, “kwa hiyo mnaimani kuwa Idd ni mtu mwema kwa Radhia, mwanaume ambae alishindwa kumtunzia siri ya uzazi, na kumwacha kwa taraka tatu, huku akimsimanga mtaani kote?” aliuliza mzee Makame akimtazama mama Siwema, ambae ni mke mkubwa.
Siwema na mama yake wanakosa majibu, wanatazama chini, kwa asibu, “sikia Siwema, jifunze kuwa na shukrani ata mala, Radhia sijuwi ata aliongea nini na mwenzie, adi kwenda kwa waziri kukuombea urudishwe kazini, hivi mtumwingine angekubari kuibeba aibu uliyoifanya kwenye ile video, na kwenda kukuombea urudishwe kazini?” anauliza mzee Makame, kwa sauti ya chini yenye kusisitiza amani.
“nimekusikia unaongea kwa sauti kubwa ili majilani wakusikie, hivi uoni kuwa kuna siku Radhia atakuchoka na kuacha kukushika mkono?” anauliza mzee Makame, pasipo jibu lolote toka kwa Siwema, “kuanzia leo kama unawasiliana na Idd, wasiliana kwa mema, lakini usishirikiane na huyo kijana kuaribu amani ya mwenzio, na kikubwa ni kwamba, kwako na kwa Radhia, nyie mlisha lelewa na kuolewa mktokea mikononi mwetu, sasa siwezi tena kuwalea kama watoto wadogo, kikubwa ni kwamba, nita pokea mwanaume anae kuja kuowa” alisema mzee Makame, kabla ya kuwaluhusu waondoke.*********
Idd anaingia ndani ya nyumba yake amfura kwa hasira, huku kichwani mwake akijiuliza maana ya maneno ya Radhia, ambayo uyarudia mala kwa mala, “bora utumie muda wako kumfwatilia mkeo” maneno ambayo yana mchanganya sana Idd, ambae leo alimwona mke wake mkubwa, yani Ashura, amebeba jwebte vesper, na mwanaume wake wa zamani, ukizingatia leo ni siku ya tatu Ashura akuwa nyumbani, na akuwai kuwasiliana nae wala kwenda kumwona.
“lakini Ashura awezi kunisaliti, maana ni mjamzito na atamimi mwenyewe siluhusiwi kulala nae, itawezekanaje kwa mwanaume mwingine” anawaza Idd, ambae anajisahaulisha kuwa Ashura anapenda sana Shaban. . ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums