Wakati Idd anaamka peke yake pale nyumbani, na kushindwa kufanya lolote, akiishia kufunga mlango na kuchukuwa baskeri yake, kisha anaelekea mjini, mke wake Ashura alikuwa bado kitandani, mtupu kama alivyo zaliwa, pembeni yake alikuwa Shaban, nae alikuwa mtupu kama alivyo zaliwa, anachezea tumbo la mke wake.
“mpaka hapo Ashura, lazima uombe taraka mapema, maana siri ya Idd itaanza kufichuka” alisema Shaban, ambae siku zote uwa ataki kuona Ashura anaendelea kuishi kwenye nyumba ya Idd, wakati tayari alisha zaa nae watoto watatu, na walikuwa wanapendana sana.
“Shaban jamani, vumilia kidogo nijifungue, kisha nianze kuomba taraka” alisema Ashura, kwa sauti ya kumbembeleza Shaban, “nisawa Ashura, lakini itakuwaje kama akigundua kabla ajakupatia taraka?” aliuliza Shaban akionyesha wazi kuwa, alicho itaji kwa Ashura, ni kuondoka salama kwa Idd bila aibu ya kuzaa nje ndoa.
“wala usiwe na wasi wasi, Idd kwa ubishi wake na akili yake ndogo, awezi kujuwa chochote, mpaka atakapo nipatia taraka na kusikia naishi na wewe ndio, au nimwambie mwenyewe” alisema Ashura, ambae mpaka sasa alikuwa na week tatu tu, ili aingie kwenye tarehe za matazamio, ya kujifungua.*******
Siwema alifika ofisini kwa mkurugenzi wa wizara ya afya, ambapo aliambiwa aache ile barua yake ya kuachishwa kazi, kisha aka elekezwa aende ofisini kwa waziri wa afya.
Akiwa mwenye furaha iliyochanganyika na hofu, Siwema anatembea kwa haraka, kuelekea kwenye ofisi ya waziri wa afya, ambako anakaribishwa na wasaidizi na kuluhusiwa kuingia ndani.
“asalam aleykum” anasalimia Siwema kwa sauti iliyo jawa na hofu, na wasi wasi, japo tayari alisha hisi alicho itiwa, “aleykum salaam” aliitikia mwanamama aliekaa kwenye kiti chake kizuri nyuma ya meza kubwa, yenye vitu vingi vinavyo ashiria kuwa ofisi hii akuwa ndogo.
“Siwema nimekuita hapa, kwa mambo mawili” alianza waziri wa afya, huku anamtazama Siwema, “la kwanza ni kukurudisha kazini, lakini nakupangia kituo kidogo cha magomeni” alisema mwanamama huyu, ambae kwa mwonekano wa nje, alionekana mwenye kujipenda na kujijari, ukichangia kuwa na kipato kikubwa anacho pata kwa uwaziri wake. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA THEMANINI NA TISA
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NANE: “Siwema nimekuita hapa, kwa mambo mawili” alianza waziri wa afya, huku anamtazama Siwema, “la kwanza ni kukurudisha kazini, lakini nakupangia kituo kidogo cha magomeni” alisema mwanamama huyu, ambae kwa mwonekano wa nje, alionekana mwenye kujipenda na kujijari, ukichangia kuwa na kipato kikubwa anacho pata kwa uwaziri wake. ......... ENDELEA….
“Jambo la pili Siwema, nimekurudisha kazini kwa sababu ya heshima ya shemeji barozi Edgar, na yako na dada yako Radhia, hivyo na wewe ujitaidi kuwa makini basi, kwanza unajitia aibu, na pia unamwaibisha mdogo wako, ambae anaenda kuwa mtu mkubwa” alisema waziri wa afya, huku Siwema akimsikiliza na kichwa ameinamisha chini.
“ata sisi wengine tuna onja pombe, lakini kunywa kistaarabu, ukijifungia nyumbani kwako unakunywa pombe, nani atakuchukuwa video, na mbaya zaidi nasikia unamume, na huku unamlilia hawara, uoni kuwa ni vibaya” aliongea yule mama, huku akimsisitiza Siwema kubadirika kitabia, asirudie tena makosa aliyo yafanya mwanzo.
Baada ya kutoka ofisini kwa waziri, Siwema akaelekea ofisini kwa mkurugenzi, kuchukuwa barua ya uamisho, kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani, akiwa mwenye mawazo mengi sana, akionekana kukosa amani moyoni mwake.
Unaweza kushangaa, kwanini Siwema akose amani, wakati amerudishiwa kazini, ila jibu lake aunaweza kulikataa, maana ukweli aufurahisi ata kidogo, “pia unamwaibisha mdogo wako, ambae anaenda kuwa mtu mkubwa” ilo neno sijuwi kwanini lilimkosesha raha Siwema, “yani mimi ndio wa kumwaibisha Radhia, eti anakuwa mtu mkubwa” alijisemea Siwema akiwa kwenye dala dala.
“kwahiyo ata mawaziri wanajuwa kuwa Radhia ni mpenzi wa yule Edgar” anajiwazia Siwema ambae kila dakika zilivyosonga nae alizidi kukosa amani, “tutaziweka wapi sura zetu” aliwaza Siwema, ambae aliona ni rahisi kukabiliana na aibu ya kurekodiwa video, akiwa amelewa na kulilia mchepuko, kuliko mdogo wake kufanikiwa kimaisha.********
Mida hii Radhia alikuwa nyumbani kwa Edgar, anajiandaa kuondoka kwenda nyumbani kwao, hii ni toka alipo ondoka usiku wa juzi, yani jumamosi, na mpango ulikuwa ni kurudi tena jioni, wakati Edgar akiwa amesha rudi toka kazini.
Radhia akiwa mwenye furaha na amani moyoni mwake, alichukuwa mkoba wake, ambao ndani ulikuwa na kiasi flani cha fedha, nyaraka ambazo zilikuwa na maelekezo ya maitajio na mpango wa wageni wa wanamichezo wa timu ya mpira wa kikapu, toka #Mbogo_Land, watakao kaa kwa week moja hapa kisiwani, yeye akiwa kama msimamizi na mratibu wa ziara hii ya wanamichezo.
Radhia anatoka nje na kuaga kwa wahudumu waliokuwepo, maana Monica alikuwa ameenda ofisini kwa Edgar, maana licha ya kuwa msimamizi wa shughuri zote za nyumbani, pia ni msimamizi wa shughuri za ofisini pia.
Radhia anasalimiana na kuwaaga wafanyakazi na walinzi wa nyumba ya barozi Edgar, nao wanaitikia kwa furaha na heshima, wanaonekana kumpenda mwanamke huyu, ambae anawaheshimu kama wanavyo mheshimu, kama ungewaona wakati huo ungesema, nae ni mfanyakazi wa mle ndani, au amekuja mala moja, na kwamba akukaa hapa kwa siku mbili, labda ungetofautisha kwa mavazi yake ya kifahari, na ya kipekee.
Radhia aliependeza kwa vazi na ung’aavu wa sura yake, anatoka nje na kukutana na walinzi wa wili, mmoja akiwa ni wakike na mmoja wakiume, wakiume akiwa amevalia suit nyeusi, kama wavaa avyo walinzi wa Edgar, huku yule wakike, akiwa amevalia gauni refu hijab na vatu vya kutumbukiza, wakiwa wamezimama pembeni ya gari dogo, yani BMW, lile la rangi nyeusi, ambalo ndani pia kulikuwa na dereva wakike, alie valia kama huyu mlinzi wakike.
Radhia anawasalimia kwa nidhamu, kama alivyofanya kwa wengine, “asalm aleykum” ndivyo alivyo salimia Radhia, “aleykum salam” wanaitikia wale walinzi wawili, ambao mwanzo Radhia akujuwa kama ni walinzi, “aya tutaonana jioni” alisema Radhia kwa maana ya kuwaaga, huku kichwani mwake akiwa anajionea aibu, kamaana alijuwa fika kuwa nyumba nzima, ilikuwa infahamu kuwa usiku wa leo pia alikuwa anafanya nini na Edgar.
“samahani mama gari ili hapa lipo tayari” alisema yule mlinzi wa kike, kwa sauti iliyojaa nidhamu, huku anafungua mlango wa nyuma wa habiria wa upande wa kushoto.
Radhia anashangaa kidogo, maana ilikuwa ya kipekee, ni kama anavyoona wanafanyiwa wake wa viongozi au viongozi wenyewe, “kwahiyo mnataka kunipeleka nyumbani, kwanini mjisumbue hivyo, maana mimi nataka kupitia sokoni” alisema Radhia, ambae alikuwa amesimama anawatazama wale walinzi.
“naitwa Jasmin, ni msaidizi wako na mwangalizi wa usalama wako, aitokuwa usumbufu kutimiza jukumu langu” alisema yule mlinzi wa kike, aliejitambulisha kwa jina la Jasmin.
Inamshangaza kidogo Radhia, ambae anaingia kwenye gari, Jasmin anafunga mlango na kwenda kuingia kwenye gari, seat ya mbele upande wa seat ya abiria, Radhia akiwa mwenye uso wa uoga na utulivu, anajiuliza maswali mengi sana, kwanini Edgar muwekee ulinzi.
Safari inaanza taratibu na kimya kimya, gari linatoka nje yageti, huku Radhia aliekaa seat ya nyuma peke yake anazungusha mawazo kichwani mwake, akijiuliza swali ambalo jibu lake la haraka alilolipata likiwa ni, sababu Edgar anahisi kuwa yeye siyo mwaminifu, anahisi bado anatembea na Idd, kutokana na juzi kupiga simu na kumwita mke wake.
“samahani mama tunaelekea wapi kwa sasa” Radhia anashtuliwa na sauti tulivu ya kike, toka kwa mlinzi wake Jasmin, “darajani, huko mjini, nataka kupitia sokoni” alisema Radhia, ambae pia anawatazama wale wanawake walioko mbele ya gari, na kujiuliza kwanini wao wanakaa mbele wakati yeye amekaa nyuma, kama kweli wao ni wapo kwaajili yake.
“mama huyu ni dereva wako, anaitwa Nadia, muda wowote yupo tayari kukupeleka sehemu sehemu yoyote” alisema Jasmin, kwa sauti tulivu yenye nidhamu, “sawa na mie si mnanifahamu jina langu?” aliuliza Radhia, akijaribu kuangalia anawezaje kuwazowea wale wanawake wenzake.
“ndiyo mama” wanajibu wote kwa pamoja, kwa sauti zenye nidhamu, Radhia anachekecha kidogo, namna ya kuwaingia waschana hawa ambao umri wao ni kati ya miaka 20 hadi 22, “sawa basi msiniite mama, niiteni wifi au dada, au Radhia” alisema Radhia, na hapo maongezi mepesi yakaanza.********
Mzee Abeid Ally Makame, anakaribishwa na wasimamizi na waangalizi wa usalama kwenye ofisi ya rais, ambao wanamwelekeza aingie ndani ya ofisi ya mheshimiwa rais.
Mzee Makame anaingia ofisini huku akitamani angalau angekuwepo mtu ata mmoja anae mfahamu, kama vile Edgar, ili angalau aweze kuwa na ujasiri wa kuonmgea na mheshimiwa rais.
Mzee Makame anakanyaga zuria jekundu, anaingia ndani ya ofisi, na kuibukia ndani ya ofisi kubwa, ambayo kwa haraka ungesema ni sebule ya nyumbani kwa tajiri flani, maana kulikuwa na makochi mazuri ya kifahari, yaliyokaa juu ya dhuria lile jekundu, mbele kabisa kuna meza kubwa nzuri yenye vitu vichache vya kiofisi.
Ndani kuna watu kadhaa, ukiachilia wafanya kazi wawili, ambao walikuwa wanahudumia, huku chai na vitafunwa mbali mbali vikiwa mezani, pia kulikuwa na mheshimiwa rais mwenyewe, pamoja na waziri wa elimu, wote walikuwa wanamtazama kwa tabasamu, kama vile wanamfahamu, nyuma yao wakiwepo walinzi na wanahabari wawili wa ikuru, mmoja wao akiwa ameshika camera. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums