Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 3,506
- 6,305
Abou Shaymaa tunakusubiri huku
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naaaaam shushaaaaa tuuu vitu kaka usiku mrefu huuuuu sheikhASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO: Mpaka hapo Shani akajuwa kuwa kinachofwata nikupigwa kwa mala ya kwanza na mume wake, “namimi nataka kuzaa” alisema Shani kwa sauti yenye kilio cha chini chini, “kwahiyo ndio unajiliza liza kama mjinga” alisema Idd sambamba na mvumo wa mkanda uliotuwa kwenye mgongo wa Shani, ambae apiga yowe la nguvu. . ......... ENDELEA….
“mpuuzi sana, sasa hivyo mimba unataka nikubebea mimi, siubebe mimba sasa” Idd akainua tena mkanda na kuuleta kwa Shani, safari hii Shani akuacha mnda ufike mwili mwake, alivulumisha miguu yake na kumsukuma Idd, ambae akutegemea ktendo kile, na kujikuta akisukumwa na kujibwaga chini.
Idd akainuka akiwa na hasira kali, na kuokota mkanda wakeambao ulikuwa umemtoka mkononi, Shani anapata nafasi ya kutoka mle chumbani akiwa na chupi, tu, kifua kipo wazi.
Idd ana tembea kuelekea sebuleni, huku anasikilizia maumivu, aliyo yapata kutokana na kuanguka, akiwa amevaa kaptula iliyoishia magotini, “vipi tena jamani, mbona mnapigana usiku usiku namna hii?” alieuliza alikuwa ni Ashura, yani mke mkubwa wa bana Idd, ambae alikuwa amesimama kwenye mlango wa chumba chake, ilikuwa baada ya kusikia kelele za mke mdogo.
Shani akuwepo pale seuleni, “mpuuzi sana huyu, anajifanya kiburi, ssa ngoja nimwonyeshe” alisema Idd huku anaelekea kwenye mlango wa chumba cha Ashura, ambako alizania Shani amekimbilia, “umwonyeshe nani?” ilisikika sauti ya Shani, aliekuwa ametokea upande wa jikoni.
Idd anageuka kwa hasira, na kumwona Shani, akiwa ameshika panga mkononi mwake, huku uso umefura kwa hasira, “yani nakukumbusha wajibu wako wakunipa haki yangu, baada ya kunitimizia wewe uanipiga” alisema Shani kwa sauti iliyojaa hasira kali.
Idd anatoa macho ya mshangao na uoga, kisha ana geuka na kukimbilia chumbani kwa mke mkubwa, kisha akamsukuma mke wake mkubwa, ambae kama siyo Shani kumdaka, basi angeanguka vibaya sana.
Idd pasipo kujari alichokifanya, aka akafunga mlango haraka, “yani Shani umefikia hatua ya kunishikia panga, walahi na kurudisha kwenu” alisema Idd, kwa sauti yenye uoga na wasi wasi, “unazani ningeendelea kukaa hapa, ilinipate nini, mtu mwenyewe mwanaume suruali, nashangaa ata Ashura uliwezaje kumpatia mimba, wakati unalolote unalo lifanya, na ukiambiwa una kimbilia kunipiga” alisema Shani kwa sauti ya juu yenye hasira, huku maneno yake yakiwashtua watu wawili, yani Idd na Ashura.
Idd aliona mke wake anamchafua, kwa kuongea vile kwa sauti ya juu, na pengine majirani wanaweza kuwa wanasikia, lakini mshtuko wake, aukuwa mkubwa kama ule wa Ashura, ambao ulimfanya ahisi kuwa, mchezo wake unaenda kufichuka muda siyo mrefu.
“mwanamke gani uliziki, unataka mpaka nife” alisema Idd, ambae akuwai kufikilia wala kuwaza kuhusu shida aliyonayo, ya kushindwa kutimiza tendo la ndoa kwa wake zake, “ufe kwa lipi, wakati ni mwezi wapili sasa utaki ata nikuguse, utazani tumegombana, sijuwi kitu gani kilikufanya umzunguke Yasin na kuja kunichumbia, wakati uwezo wa kulala na mwanamke mmoja hauna” alisema Shani ambae ni wazi alikasirika kweli kweli.
Hapo Idd, ana umia moyoni mwake, ni kwamaana Shani anaingea ukweli mtupu, kwamaana anavuta kumbu kumbu, na kuona ni kweli sasa anamiezi miwili, ajagusa kitumbua cha mke wake mdogo, achana na mke mkubwa ambae akumbuki imepita muda gani ajamgusa,
Nikweli anagundua akuwa na sababu yakumchukuwa Shani toka kwa Yasin, lakini yeye lengo lake likuwa ni kuona Yasin anamkosa Shani, “hapo nikimwacha lazima aende akaseme kwao, huyu ni tofauti na Radhia alie nivumilia” waza Idd, ambae anajuwa fika kuwa, swala ili linaweza kuwa kashfa kubwa kwake.
Lakini basi kabla ajaongea lolote, akamsikia Shani akiongea toka sebuleni, “taraka utaniletea nyumbani” alisikika Shani, huku anaelekea chumbani kwake, akiwa na panga mkononi, mke mkubwa akimsindikiza kwamacho, akiombea mume wake aishie hapo kuongea, isje kuweka wazi janja yake ya kuzaa na Shaban watoto watatu.
Hapo Idd anadharau “nani kakuambia nakutariki, we nenda lakini utarudi mwenyewe” alisema Idd akiongea toka chumbani, “tena nikuambie kitu, uje na taraka tatu, sababu sitokaa nirudi tena hapa kwako, na ukichelewa kesho, nitaenda kutoa taarifa msikitini, kama ulivyo kuja kunifanyia fitina” alisikika Shani ambae sasa alikuwa chumbani, anavaa nguo na kuweka nguo zake kwenye mfuko wake mkubwa.
Ashura anakumbuka jinsi Idd alivyo mfanyia yeye, kwa tamaa ya mcho, lakini akashindwa kutimiza ya chumbani, na kumfanya sasa aishi kitembea na wanaume wawili, yani Idd na Shaban.
Idd anaona mambo yanaenda kuwa mabaya kwake, niwazi Shani ataeleza kila kitu, ata kisichotakiwa kuelezwa adharani, “Ashura mzuwie asindoke huyo” alisema Idd, kwa sauti ya juu, “alafu nikimzuwia mimi ndie nita mlala, nani alikuambia tendo la ndoa nikumpiga mwanamke” alijibu kwa hasira Ashura, akiwa namaana mbili.
Moja ni hasira alizokuwa nazo, juu ya matendo ya Idd, kuvuruga mapenzi ya watu, na kuwatenganisha, pili ni kutoa mwanya kwa Shani kuondoka, ilikuepusha kufichuka kwa siri ya uzaifu wa mume wake, maana kama Ashura akiendeleakuishihapa, kunasiku wanganza kueleza madhaifu ya Idd, napengine watu kuanza kuingiwa na mshaka juu ya ulijari wa Idd, na kuhoji juu ya namna alivyoweza kumpatia mimba Ashura.
Ilimshtua sana Idd kauri ya mke wake mkubwa, “ashura na wewe umekuwaje lakini, usimsikilize huyo, ebu mzuwie asiondoke bwana” alipaza sauti Idd, ambae akusikia jibu lolote toka kwa Ashura,
Nae anatoka chumbani kwa Ashura kimya kimya, na kuibukia sebuleni, mbako anakuta papo tupu, hivyo anasogelea mlango wa chumba cha mke mdogo, kwa kunyatia.
Idd anapofika kwenye mlango wa chumba kile, anasikia maongezi yanaendelea ndani ya chumba hicho, “lakini mdogo wangu, ukiona hasira zimepungua rudi hapa nyumbani, siunajuwa mimi mwenyewe siwezi kumhudumia mume wetu” ilikuwa sauti ya Ashura ikimbembeleza Shani, “dada mimi siwezi, yani sijuwi kwanini aliingia tamaa ya kuniachanisha na Yasin, wakati mwenyewe anajijuwa dhaifu” maneno ya Shani yaliuchoma moyo wa Idd.
“Shani ndoa zina mambo mengi, ni uvumilivu tu, mbona mimi mwenzio navumilia kwa muda mrefu” alisema Ashura, ambae kichwani mwake alikuwa amesha pata njia ya kwenda kwa Shaban, kuendelea kula raha.
Naaaaaam!, mpaka Shani anamaliza kupanga mizigo na kuomba kaka yake mwagizie taxi ya kumpeleka nyumbani kwao, hapakuwa na mwafaka mzuri juu ya ndoa ile, na wakati wanasubiri gari, ndipo Ashura nae alipotoa ombi lake, “Idd siunajuwa sasa nitakuwa mwenyewe, basi naomba niende kwa dada, ata likitokea lolote aweze kunisaidia, maana hapa nilipo ata kupika siwezi” alisema Ashura, na Idd akupiga lolote, akamkubaria Ashura aondoke na Shani, kwa makubaliano ya kwamba, ata rudi siku mbayo Shani atarudi nyumbani.
Nusu saa baadae gari likaja, Ashura na Shani wakaondoka zao, pasipo Shani kujuwa kuwa, mke mwenzie anaelekea kwa mwanaume wake, anae mpatia raha nakujihisi kuwa ni mwanaume. ********
Naaaaaaam!, kwa upande wa Edgar na Radhia, usiku wao ulikuwa mzuri zaidi ya jana, maana ukiachilia kula nakuongea kwa pamoja, huku wakinywa juice ya matunda harisi, pia walioga pamoja na kunyaduana kweli kweli zaidi ya ilivyokuwa jana, wakianza kwa kifanyiana michezo ya kimahaba. . ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA jamii forums
😅😅Naaaaam shushaaaaa tuuu vitu kaka usiku mrefu huuuuu sheikh
Shushaaaaaaaa vituuuu tupo machooooMushalala sio?
Aiseeeeee hapo sijasoma hata moja but uko vizuri kaka we shushaaaa sisi tutazisomaaaaaa haswaaaaaaaKama Hujasoma Simulizi Hizi Kutoka Kwa Edgar Mbogo Basi Usicheze Mbali
1,KIFO CHA HAWARA
2,KIAPO CHA DAMU KWA DAMU CAPTAIN CHUI MCHAFU
3,MLANGO WA ADUI
Na Nyingine Nyingi Tu Kama
Tembele La Uwani
Kitumbua Cha Buku
Mwalimu Anataka
Mama Mwenye Nyumba
Aaah Acha Tu
DondoshaaaaaaaaaaaaaaASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA THEMANINI NA NANE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA: Naaaaaaaam!, wakati Ashura anaamkia mlandege kwa Shaban, Shani aliamkia nyumbani kwao, akiwa amesha waeleza kila kitu wazazi wake, “yule kijana waovyo sana, lazima niongee na baba yako alipeleke kwa wazee wenzake, wamweleze atoe taraka” alisema mama Shani. ......... ENDELEA….
Pia siku hii ilikuwa fupi sana kwa Edgar na Radhia, ambao walikuwa pamoja muda wote, kuanzia ofisini, ambako waliingia mala tu baada ya kunywa chai, ambako walikaa lisaa limoja tu, Edgar akikagua nyaraka alizo letewa mezani kwake, na kusoma baadhi ya barua pepe, huku Radhia akiwa amevalia kikaptulah kifupi kilichoishia pajani, na tishert refu la Edgar, ambae alivaa kaptulah ndefu mpaka magotini na tishert la kubana.
Ofisini pia walitumia muda wao kupanga utaratibu na mipangilio ya mapokezi na huduma za wageni huku wakihakikisha wanapata bajeti za maitajio ya vyakula ambavyo wachezaji na walimu wao watakula kwa week nzima, sehemu ya kufikia, na mafuta kwajili ya usafiri watakao utumia muda wote wakiwa hapa unguja.
Baada ya hapo wakaamia jikoni, ambako Radhia atoa maitajio yake ya vyakula alivyoitaji kupika, na walipika wakisaidiana na Edgar, muda wote wakicheza na kufanyiana michezo ya kimahaba, wafanyazi wao walifanya mambo madogo madogo, pasipo kuingilia mapishi.
Hakika ata wafanyakazi na watu wengine wlifurhia mapishi, huku wakitoa pendekezo la kwamba Radhia awafundishe upishi ule, ili siku nyingine waweze kupika wenyewe sehemu yoyote, ikiwa na nchini kwao #Mbogo_Land.
Jioni ya saa kumi na mbili Edgar na Radhia wakatoka nakwenda kutembea kule forodhani, ambako walifanya kama jana, leo wakiwa wamekaa muda mrefu sana, na kurudi nyumbani mida ya saa mbili usiku, na walipofika ilikuwa kama jana, mwendo wa kula na kupeana dudu.*******
Jumatatu ilikuwa nisiku ya kwanza makazini, hii ni baada ya mapumziko marefu ya eid, siku ile ilimkuta Siwema kitandani, ikiwa nisiku ya kwanza bila kwenda kazini.
Mawazo yame mshika roho, inamuuma kweli kweli, akizingatia siyo kazi pekee, pia ameachwa kwa aibu, ikiwa kosa ni uzinzi, na kilichomuumiza zaidi nikwamba, wakati yeye anaumia kwa kuachwa, ndogo wake Radhia ndio anaanza kufaidi maisha.
Wakati anaendlea kuwaza ili na lile, mala akasikia simu yake inaita, akatazama ilikuwa namba ngeni, Siwema anahisi pengine atakuwa ni Said, yani hawara yake alie mtoroka bwawani hotel, na kisha kumleta mke wake.
Siwema anapokea simu kwa shahuku, “hallo asalam aleykum” alisalimia Siwema, kwa sauti ya upole na tahadhari kubwa sana, “aleykum salam, bila shaka naongea bi Siwema Makame” ilisikika sauti ya kike toka upande wapili wa simu.
Mapigo ya moyo ya Siwema yanaanza kwenda mbio, kichwani kwake anahisi pengine ni mke wa Said ndie alie mpigia, “ndiyo ni mimi” anaitikia Siwema, kwa sauti yenye uoga mwingi, “unatakiwa report kwa mkurugenzi haraka iwezeka navyo, ukiwa na barua yako ya kuachishwa kazi” alisema mwanamke upande wapili wa simu.
“sawa nakuja sasa hivi” alisema Siwema, huku anajiinua toka kitandani na kukimbilia bafuni haraka kujiandaa, huku kichwani mwake akianza kikumbuka aliachoongea Edgar juzi, wakati wamlo wa mchana.**********
Mida hii, huko shule ya sekondari ya mwankwelekwe A, mwalimu Makame, ndio kwanza alikuwa anaingia darasani, na kitabu chahe cha biology kwamaana ya sayansi ya viumbe hai, ambayo ni moja kati ya masomo aliyo yasomea.
Mwalimu Makame anaingia darasani na wanafunzi wanasimama na kumsalimia, anaitikia na kuwa luhusu wakae, lakini kabla ajaongea chochote, kingine yeye na wanafunzi wake wakajikuta wanatazama nje, kuona magari mawili meusi aina ya Toyota V8. Yakija na kusimama mbele ya jengo la ofisi.
Mzee Makame anakumbuka kabisa kuwa, magari kama aya yalikuja juzi nyumbani kwake, lakini namba azikuwa hizo namba zilikuwa ni zaubarozi, lakini hii ya leo, ni namba za serikazi, yani SMZ, ambayo mala baada ya kusimama, walishuka watukadhaa wakiwa wamevalia suit yeusi, maarufu kama Kaunda suit.
“aya mmesha yaona magari zaidi ya hapo ni kujitaidi darasani, ili uweze kuyapanda na kuyaendesha” alisema mwalimu Makame kwa sauti iliyojaa utani, wanafunzi wanacheka kwa pamoja, ucheshi na utani, ni moja kati ya vitu ambavyo vinawafanya wanafunzi wampende sana mwalimu Makame.
Naaaaaaam! ile mwalimu Makame anataka kuanza kufundisha tu, mala akasikia mchakato wa vishindo vya watu zaidi ya mmoja vikija upande wa darasa alikuwepo yeye, wanafunzi nao wakatazama upande wa madirisha yalipo kolidoni, na yeye mwalimu Makame akatazama, upande huo, ambao waliweza kuwaona watu wanne wakilio shuka kwenye lile gari, wakiwa wameongozana na mwalimu mkuu, wakija mpaka kwenye mlango wa darasa alilokuwepo yeye, na kufungua mlango, kisha mwalmu kuu peke yake akachungulia na kumwita mwalimu Makame kwa ishala ya mkono.
Mwalimu Makame akusubiri aitwe mala mbili akatoka nje na kumfwata mwalimu mkuu aliekuwa na wale jamaa wanne, wenye Kaunda suit, “asalam aleykum” alisamia mzee Makame, huku anawatazama wale jamaa kwa macho ya tahadhari, “aleykum salaam” waliitikia wale jamaa, kisha mwalimu mkuu akaongea, “ugeni wako huu bwana Makame” alisema mwalimu mkuu, akionyesha mwenye tabasamu usoni.
“sawa nawasikiliza” alisema mzee Makame, akiwatazama kwa zamu wale jamaa wanne, “mzee huu ni ujumbe toka ikulu, tumetumwa kuja kukuchukuwa unatakiwa kuonana na rais” sauti ya mmoja kati ya wale jamaa ilipenya masikioni mwa mzee Makame na kulipua moyo wake kwa furaha, ambayo aliizuwia isionekane wazi wazi.
“sina pingamizi, maana yeye ndie mwenye mamlaka na inchi hii na sie ni watumishi wake” alisema mzee Makame, kabla ajaomba kwenda kuchukuwa mkoba wake ofisini, kwa ajili ya kujiandaa kuondoka****
tunazipata wapi hizi mkuuKama Hujasoma Simulizi Hizi Kutoka Kwa Edgar Mbogo Basi Usicheze Mbali
1,KIFO CHA HAWARA
2,KIAPO CHA DAMU KWA DAMU CAPTAIN CHUI MCHAFU
3,MLANGO WA ADUI
Na Nyingine Nyingi Tu Kama
Tembele La Uwani
Kitumbua Cha Buku
Mwalimu Anataka
Mama Mwenye Nyumba
Aaah Acha Tu
Leta hizi mkuu hizi ndiyo zinaonekana noma sana full mizagamuanoNa Nyingine Nyingi Tu Kama
Tembele La Uwani
Kitumbua Cha Buku
Mwalimu Anataka
Mama Mwenye Nyumba
Aaah Acha Tu