ndo mwisho apo manana umeahid apo ni bandika bandua mpk mwisho na leo naona haujatuma kabisa inakuaje mkali
HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE: Baba yake akuwepo sebuleni, mida hii upenda kukaa uwani, na kujisomea kitabu cha riwaya za Mbogo, “hoooooo!, mambo Radhia, siamini kama umepokea simu yangu, kitambo sana sijakupigia kukujulia hali” Radhia anasikia sauti ya kiume iliyo changamka, toka upande wapili wa simu, “mh!” anaguna Radhia, huku anatoa simu sikioni na kutazama jina la mpigaji. . ENDELEA….
Radhia anajikuta anaatoa macho kwa mshangao, huku anarudisha simu sikioni, “salama habari” anaitikia Radhia, kwa sauti yenye tadhari, huku anajiuliza sababu ya mtu huyu kupiga simu, “usalama utoke wapi, yani sikukuu hii, imenifanya nikukumbuke sana” ilisikika sauti ya mwanaume huyo, mwenye rafudhi ya watu wakisiwa hiki cha Zanzibar.
Huyo alikuwa ni bwana Idd Kiparago, mume wa zamani wa Radhia, ambae uongeaji wake wa kuchangamka ulimshangaza Radhia, maana ukiachilia kuto kuwasiliana nae toka siku alipopewa taraka, ila pia walisha kutana mala akdhaa njiani, na ata yeye alipomsalimia Idd akuwai kuitikia salamu yake.
Inamshangaza kidogo Radhia, ambae ajaelewa cha kupigiwa simu hii, na mume wake wa zamani, “anasemaje dada yangu, ajambo?” anauliza Radhia akimaanisha mke kubwa wa mume wake wa zamani, “yeye mzima, sema ujauzito wake wa safari hii, umejia vibaya kidogo” alisikika Idd, akiongea kwa uchangamfu.
Hii ni taarifa mpya kwa Radhia, ambae anakumbuka tatizo lake la kuto kushika ujauzito, anakosa amani kidogo, lakini anajikaza, “hooo!, mpe hongera zake” amaongea Radhia kwa sauti ya uchangamfu kama vile, akuwa anahisi chochote moyoni mwake, “naanzaje kumwambia, wakati sitaki ajuwe kama tumewasiliana” alisema Idd huku anacheka kidogo.
Hapo Radhia anacheka kicheko cha mguno, maana anashangazwa na maneno ya mume wake wa zamani, ambae mpaka sasa ajajuwa lengo la kumpigia simu, “kwanini sasa, kwani zambi kusalimiana, na wakati anajuwa umesha nipa taraka tena tatu?” anauliza Radhia, kwa sauti ya uchangamfu, huku bado amesimama sebuleni.
Hapo kinafwata kicheko cha kibwege, toka upande wapili wasimu, “siunajuwa anafahamu jinsi ulivyo mzuri, unazani atashindwa kuwa na wivu, mimi mwenyewe nimeshindwa kuvumilia, mpaka nimeamua nikupigie” alisema Idd na kumshangaza Radhia, ambae sasa alianza kuhisi kitu.
Lakini kabla ajaongea chochote Idd akamuwai, “sasa inakuwaje, baadae si unaweza kuja sehemu tuongee kidogo?” aliuliza Idd kwa sauti tulivu, ya kubembeleza, Radhia anatikisa kichwa kwa masikitiko, huku anaachia tabasamu pana la ushindi, maana alisha hisi mume wake wa zamani anaitaji nini kwake.
Ukweli ni kwamba, licha ya kuwa alikuwa anaitaji mtu wa kumbeleza, na pia alikuwa anahamu ya dudu, kitu ambacho siyo tu kukaa mwaka bila kupata, ila pia akuwai kuipata kisawa sawa, lakini siyo kwa mume wake huyo wa zamani, “hapana Idd, atuwezi kuonana, labda kama unamaongezi nikupigie uongee, nina salio la kutosha” ajibu Radhia, kwa sauti tulivu, yenye uchangamfu.
Hapo Idd anacheka kidogo, na weye unakuwa kama mtoto, maongezi gani ya kwenye simu, ebu fanya baadae tuonane bwana” alisema Idd, nakuweka wazi anacho itaji.
Ilimfanya Radhia atikise kichwa kwa masikitiko, huku sura yake inaonyesha kuchukia, lakini anajikaza kidogo, “baadae kuna sehemu naenda, sitoweza kuonana na wewe” alijibu Radhia, kwa sauti tulivu ya chini, akizuwia hasira zake.
Hapo nikama Idd aamini anacho ambiwa, “unaenda wapi bwana, ebu tukutane tukumbushiane jambo, mwenzio nimekumbuka sana mambo yako” alisema Idd kwa sauti ya kubembeleza, “mpuuzi huyu anammambo gani ya kufanya namimi” anawaza Radhia kwa hasira, akishindwa kutamka neno kwa Idd, ambalo lingemchukiza sana, nalo ni kwamba, Idd akuwa na chochote kitandani.
Maana ata alipokumbuka wakati anamchumbia, akiwa katika harakati za kwenda Dar es salaam kujiendeleza kimasomo, kwa ushawishi wa rafiki zake, ambao kwa sasa wapo huko, ndipo aliposhtuka akiletewa barua ya posa, toka kwa kijana ambae alisha wai kumkataa kimapenzi, nae akahapa kumpata kwa namna yoyote.
Ata baada ya kuingia kwenye ndoa, na kushuhudia kinachofanyika kitandani na mwanaume huyu, ambae alimwalibia mpango wa kwenda kujiendeleza kimasomo, ilibidi azowee na kuona kuwa ndvyo mambo yalivyo, japo alisha wai kusikia kuwa mwanamke uwa anafurahia tendo la ndoa na kukata kiu yake, kitu ambacho kwake akuwai kukishuhudia.
Ukweli ataleo anavyo pigiwa simu na Idd, akimtaka kwenda kukumbushia enzi za ndoa yao, inazidi kumchukiza Radhia, ambae kama ungemwona tu, unge gundua kuwa amekasirishwa na maongezi yale, maana Radhia alitafthiri kuwa, ile nidharau kubwa toka kwa Idd, ambae amemwona kuwa yeye afai kuwa mke na kumpa taraka, ila anafaa kuwa mchepuko, na ata kisema akampatie kitumbua, angeishia kumwacha na hamu zake.
Radhia anajikaza, asitukane wala kuongea neno baya, lakini anaamua kuondoa usumbufu, “nikweli siwezi kuja sehemu yoyote, naenda kukutana na mpenzi wangu” alisema Radhia akijuwa kuwa Idd angeacha dharau zake, “mpuuzi kweli wewe, mwanamke anae jiheshimu anaweza kutamka upuuzi kama huo, eti naenda kuonana na mpenzi wangu, bila ata aibu” alisema Idd kwa sauti yenye hasira.
Idd akuishia hapo “huyo ni mwanaume anaetaka kuni owa” alisema Radhia, akijuwa fika anadanganya, lakini sikusaidia kitu, “kwahiyo hiyo siku hizi umeanza ukahaba, umeacha kabisa kujiheshimu siyo, unawezaje kutembea na mwanaume ambae auna uhakika kama atakuowa, unanitia aibu sana, nasema jitaidi tuonane aiwezekani uwe na tabia za hovyo kama hizo, na nitakuja kwa baba yako kumweleza” alisema Idd kwa sauti ya ukali, akionekana amechukia kweli kweli.
Ilizidi kumshangaza Radhia, ambae sasa aliacha kukasirika na kushangaa matusi aliyokuwa anashushiwa, “samahani Idd, unaongea hivyo kama nani wangu, au umesahau kuwa mimi na wewe tulisha tarikiana, kwahiyo unaona niwe mchepuko wako, kuliko mimi kuwa na mume wangu?” anauliza Radhia kwa sauti tulivu ya taratibu.
Hapo nikama Idd alikosa jibu wala swali, japo akukaa kimya, “mimi na wewe bado atujamalizana, na uwezi kuolewa na mwanaume mwingine yoyote, ingali nipo hai” alisema Idd kwa sauti yenye hasira, ilimshangaza sana Radhia, ambae aelewi chanzo nini mpaka haya yatokee leo.
Radhia akaona nivyema akimaliza mjadara, “Idd naomba siku nyingine usinipigie simu kama hauna lamaana la kuongea, kumbuka mimi siyo mkeo, na wala atuna cha pamoja, atuja zaa wala atuja jenga kwa pamoja, niliondoka kwako na nguo zangu tu, unidai siku dai” alisema Radhia na kukata simu, kisha akaingia chumbani kwenda kujiweka sawa, maana uso wake ulikuwa na udhuni kiasi.
Lakini akiwa anajiweka sawa, mala akasikia simu yake inaita tena, mwanzo alijuwa ni Idd, lakini akakumbuka kuitazama ilikuona jina la mpigaji, asije kufanya kosa kama la mwanzo, “afadhari amepiga” anajisemea Radhia, huku anaachia tabasamu pana la furaha, ni mala baada ya kuona jina la mpigaji.
Radhia anapokea simu haraka, “asalam aleykum Edgar” alisalimia Radhia kwa sauti ya nyororo yenye kusikika vizuri na kuleta utamu masikoni mwa msikiliazaji, asa akiwa ni mwanaume, “aleykum salaam bi Radhia, habari za toka jana?” alisalimia mwanaume mwenye sauti nzito, toka upande wapili wasimu.
Radhia anajikuta anapata raha flani moyoni mwake, kiasi cha kuendelea kutabasamu, karibia kuchekelea, “nashukuru mungu, nipo salama, sijuwi wewe wajionaje na hali yako?,” alijibu Radhia, “kwasasa najihisi afadhari, maana nilikuwa na hofu juu yenu, auku nipigia simu, kunijulisha kama umesha fika nyumbani” alisema Edgar ambae daima uongea taratibu, kwa ie sauti yake nzito.
Sijuwi kwanini Radhia alijihisi raha zaidi, “niliogopa kukupigia nije kukugombanisha na mpenzi wako” siyo kwamba alikuwa na maana hiyo, ila ukweli ni kwamba, Radhia alimchokoza makusudi Edgar, kuona kama ata zungumzia mapenzi kuhusu yeye. . ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA
jamii forums