SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

SIMULIZI: Asali haitiwi kidole

ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: Tuanze na huko ndani, ambako mama Zuhura aliwaita wakina Mariam, ambao aliingia nao chumbani kwake, “nimewaita wote wawili, kuna kitu nataka tuongee” alisema mama Mariam kwa sauti ya chini, kiasi kwamba, ata kama kunamtu alikuwa amekaa nje ya chumba iki yani mlangoni asinge sikia. ENDELEA….

Wakina Mariam wakatega masikio kwa umakini, kumsikiliza mama yao ambae ni kama rafiki yao linapokuja swala la upinzani na mke mwenzie, ya ni mama Radhia.

Mama riam aliwaimulia kikao chake na mzee Abeid na mama Radhia, akiwaeleza jinsi baba yao alivyo kataza kumsimanga Radhia, “lakini kama akiwachokoza wala msimwache msemeni kama kawaida, kwani uongo siyo mjane, yeye alipoolewa si aliwaona nyie amfai na kwamba yeye ndie mwenye bahati sana, na yeye peke yake ndie anae faa kuolewa, sasa kikowapi?” alisema mama Mariam, na kuwafanya watoto wake wazibe midomo wakizuwia vicheko, kuogopa baba yao asije kusikia.

“alafu sijuwi amepata kibwana gani, kinashindwa ata kununulia nguo” alisema Mariam, na kumfanya mama Mariam aache mdomo wazi kwa mshangao, “weee! Usiniambie, au ndio huyo alie mpa hiyo ela mnayosema?” aliuliza mama Mariam, huku anwatazama watoto wake kwa hawamu, “mh! sizani kama ni huyo, amtoe wapi mwanaume mwenye fedha kiasi hicho, si ange mnunulia nguo za siku kuu, baada ya kuwapa ela wakina Mu, wachezee” alisema Mariam, kwa sauti yenye mashaka na zarau, lakini kumbuka kuwa, Mariam na Radhia wamepishana mwaka mmoja tu wakuzaliwa.

Wakati ndani maongezi ya kiwa hayo, huku nje nako, mambo yalikuwa hivi, “vipi tena mbona kama wamechukia?” anauliza mama Radhia, ambae aliona hali ya Mariam na Zuhura, wakati anapishana nao, “ata siwaelewi, walikuwa wanajiongelesha hapa, nashangaa ghafla wamebadirika” alisema Radhia, ambae uso wake ulikuwa ujawa na furaha.

Mama Radhia anaona hali ya furaha ya Radhia, anakosa uvumilivu, maana nikawaida yao kushiriki furaha kwa pamoja, “vipi mwenzetu, naona ume amka naunyonge ghafla umapatwa na furaha” anaongea mama Radhia kwa sauti iliyojaa utani, “walaaa hakuna kitu” anasema Radhia na wakati huo anaonekana Mukhsin akiwa anakuja kwa mwendo wa haraka, huku amebeba mifuko mitatu mikubwa na zuri, maalumu toka kwenye maduka ya nguo.

Wote wanamwona, Zahara anatimka mbio kumfwata kaka yake, maana anajuwa zile ni nini, na zinatoka wapi, maana anakumbuka jana waliahidiwa na Edgar, ambae alisema kuwa wanamtoko wa pamoja, “he! Radhia huyu nae ametoa wapi hivyo vitu” anauliza mama Radhia, huku anamtazama Radhia kwa macho ya udadisi.

Radhia kabla ya kujibu anacheka kidogo, huku anamtazama Mukhsin, ambae alikuwa amesha mfikia, “rafiki yake Mu, amesema leo tumealikwa sehemu, hivyo akasema ata nunua nguo kwaajili yetu” alisema Radhia kwa sauti ya chini, yenye aibu ya kike, aibu ambayo ilimfanya mama yake ahisi kitu, lakini anashindwa kusema maana Mukhsin na Zahara waliwepo pale.

“dada wewe wakwako huu na Zahara huu hapa, amesema saa sita gari linakuja kutuchukuwa” alisema Mukhsin, akiwa katika hali ya furaha, huku anampatia Radhia mifuko miwili, kisha akaingia ndani.

Radhia akiwa ameshikilia mfuko mwili, anatulia kusubiri swali toka kwa mama yake, “unasubiri nini sasa, ebu twendeni ndani tukajionee hivyo vilivyomo ndani, au mpaka waje hao wenye maneno mengi” anasemama Radhia huku anainuka na kuchukuwa ile mifuko miwili na kuingia nayo ndani, akifwatiwa na Zahara kisha Radhia.

Mpaka wanaingia ndani, bado Mariam Zuhura na mama yao walikuwa awajatoka, chumbani walikokuwa wanakikao cha muda, kikao ambacho ata mama Radhia alikuwa anakifahamu.

Aliekuwa anatoa nguo kwenye mfuko ni mama Radhia mwenyewe, akiwa ameanza na mfuko ambao ulisemekana kuwa ni wa Zahara, ambao ulikuwa na nauni zuri sana lenye rangi ya blue, na nakshi za mauwa ya rangi ya silver, na dhahabu, pia hijab na mtandio wa rangi ile ile, ya blue na nakshi kama ilivyo kwenye gauni, viatu zuri vya mikanda, vyenye rangi nyeusi na fito za blue.

Hakika zilikuwa nzuri sana, japo hawa kujuwa gharama yake, lakini zilivutia sana machoni pa kila mmoja wao, na kuwapa hapa hamu ya kuangalia mfuko wa Radhia, ambao pia licha ya kuwa na nguo iliyofanana na lile gauni la Zahara, na viatu kama vyake, ila pia, kulikuwa na pea gauni jingine, lenye rangi nyekundu ya kung’aa, huku likiwa na nakshi za bulue na silver, hijab na viatu pea mbili, zilizo fanana rangi na nguo zake, kama ilivyokuwa kwa Zahara.

Licha ya vitu hivyo vyote, lakini pia bado kuna vitu ndani ya mfuko, mama Radhia anaingiza mkono na kutoa rangi ya mdomo wanja na manukato mbali mbali, pia kimkebe cha mkufu mzuri wenye kipambo cha rubi, lakini bado kuna vitu vingine ndani ya mfuko.

Mama Radhia anaingiza mfuko na kuibuka na komkoba mpya wakike, uliotuna kweli kweli, anaufungua na kuingiza mkono ndani yake, anaibuka na kubunda cha nguo, wote wanatoa macho ya mshangao.

Zilikuwa ni nguo za ndani, yani chupi na sidilia, kiwa ni tatu tatu kwa rangi tofauti, nyeupe pink na nyekundu, zenye maua tofauti tofauti, zikiwa zinafanana na kwa pea ya chupi na sidilia, “Radhia umesema ni rafiki wa Mu?” anauliza mama Radhia kwa mshangao, “ndiyo mama, ni rafiki yake Mu, niyule alie mnunulia viatu vya mpira, mwulize ata Zahara” anasema Radhia kwa namna ya kujitetea.

Mama Radhia anatulia, lakini bado anamashaka, anatumia sekunde kadhaa kuwaza jambo, kabla ajamtazama binti yake mdogo, “aya nenda kaoge si mmeambiwa saa sita mna kuja kuchukuliwa” anasema mama Radhia akimtazama Zahara, ambae haraka sana aanza kujiandaa, anatumia dakika tatu, mpaka kutoka nje na kwenda bafuni.

Chumbani sasa wamebakia wawili, “Radhia auna aja ya kunificha lolote, ebu niambie, huyo mwanaume ni yupi na anakazi gani?” anauliza mama Radhia, kwa sauti tulivu huku anamtazama Radhia usoni, ambae akuonyesha wasi wasi wowote, zaidi ni nijiaibu kwambali, “mama huyu ni rafiki yake Mu, anaitwa Edgar, wala sijuwi lolote kuhusu yeye” alisema Radhia, kisha akamsimulia kuhusu kukutana kwao, na jinsi iilivyokuwa, mpaka kuletewa nguo leo hii.

Radhia alimweleza mama yake kila kitu, kwamba yeye alitoka kwa lengo la kuwapeleka wakuna Zahara, wakakutane na kijana huyo, ambae ata yeye anamfahamu, “lakini nilipotaka kuondoka Edgar akasema nibakie kwanza, maana pake yake asingeweza kukaa na wakina Zahara” alieleza Radhia, na pia akaeleza kuhusu mwaliko, “nilimweleza kuwa mimi sitoweza kwenda, akauliza kwanini, ndio Zahara akamweleza kuwa sababu sikuwa na nguo, nae akasema kuwa atatnunua nguo za kila mtu” alieleza Radhia.

Mama Radhia alisikiliza kwa umakini maelezo ya binti yake, kisha akamweleza, “Radhia, wewe ni mkubwa sasa, na wala ukataliwi kufanya unacho taka, lakini angalia thamani yako na usalama wako” alisema mama Radhia, kisha akamweleza kuhusu maongezi yao na baba yake jana usiku.******

Naaaaaaam!, saa sita na nusu, Mariam na Zuhura wakiwa kibarazani, wakisubiri kula chakula cha mchana, ili wakatembee wanako kujuwa wao, wapo pamona mama Radhia na mama yao, ambae ndie alie kuwa anapika, huku wakina Khadija wanacheza pale mbele ya nyumba yao, hakuwepo Radhia wala Zahara.

“kwahiyo nyie leo mnatoka wenyewe, watoto mtawaacha na nani?” anauliza mama Mariam, “watacheza na wakina Zahara” anajibu kwa haraka Mariam, “Zahara ana toka na Mukhsin na dada yao” anajibu mama Radhia, na kuwafanya Mariam na Zuhura watazamane kwa mshangao. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JamiiForums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: “kwahiyo nyie leo mnatoka wenyewe, watoto mtawaacha na nani?” anauliza mama Mariam, “watacheza na wakina Zahara” anajibu kwa haraka Mariam, “Zahara ana toka na Mukhsin na dada yao” anajibu mama Radhia, na kuwafanya Mariam na Zuhura watazamane kwa mshangao. ENDELEA….

“jamani dada Radhia, mbona anajiaibisha hivyo, anatoka na gauni moja siku mbili” alisema Mariam, na kumfanya Zuhura acheke kidogo.

Inaonyesha imemkela mama yao, maana aliwakata jicho kali, lenye kuonya, “nyie wenyewe leo mnavaa nguo gani, si ile ile ya jana?” anauliza mama Mariam, na kumfanya mama Radhia atabasamu kidogo, “lakini bira magaui yetu mapya, yeye lakwake lina mwaka sasa, analivaa ilo ilo kila mtoko” anasema Zahara, na wakati huo huo wanaliona gari dogo, la kukodi likisimama mbele ya nyumba yo, mita chache toka kibarazani, yani pale walipokaa.

Wote wanalitazama kwa macho ya mashaka, kasoro mama Radhia peke yake, gari lime simama lakini milango aifunguliwi, kuonyesha mtu anashuka, Mariam anainuka na kulifwata gari, akiitaji kujuwa shida ya mwenye gari, lakini kabla ajalifikia anasikia arufu nzuri ya manukato, tokea ndani, anageuka na kutazama kama wenzake walivyofanya.

Hapo wanaonekana watu watatu, wote wakiwa wamependeza kweli kweli, yani Zahara alie pendeza kwenye gauni lake la blue lililofanana na lile la dada yake, kwamaana walikuwa wamevaa sale sale, huku kijana mdogo Mukhsin akiwa amevalia kanzu ya blue bahari, yenye nakshi ya nyuzi nyeupe na njano, kama ilivyo kwenye balaghashia yake, ambayo ilikaa vyema kichwani, sambamba na kiatu cha wazi cha mikanda, yani sendo za ngozi.

Kwa upande wa Radhia, ukiachilia kuvaa kwa mfanano na mdogo wake Zahara, pia alikuwa amependeza na kuonekana mzuri mala dufu ya alivyo kuwa ata kabla ya kuolewa, huku mkufu mzuri wa rangi ya dhahabu ukining’inia shingoni mwake, huku akinging’niza mkoba wa blue kwapani mwake.

Hakika ilikuwa ni jambo la ghafla sana, kwa wakina Mariam na Zuhura, ambao walitoa macho ya mshangao kama ilivyokuwa kwa mama yao, “jamani baadae” anasema Radhia, huku anashuka ngazi, “aya nawatakia mwaliko mwema” aliejibu ni mama Radhia pekee, huku wengine wakiwasindikiza kwa macho, na kuwaona wakina Radhia wakiingia kwenye gari na gari likaondoka zake.

“hapana lile litakuwa feki siyo lile tulilo liona siku ile” anasema Zuhura, kama vile yupo kwenye wenge, “nini itakuwa fake?” anauliza mama Mariam, ambae pia bado yupo katika mshangao, “lile gauni alilovaa da Radhia, tuliliona dukani, linauzwa elfu semanini” anasema Mariam, “mh!, anaguna mama Radhia, ambae anazidi kuingiwa mashaka na huyo rafiki wa Mu, kwa Radhia, “nitamwuliza baadae, lakini atakuwa ametowa wapi ela?” anauliza Zuhura, huku anamtazama mama Radhia, akizingatia kwamba, ata ile kanzu aliyo ivaa Mukhsin, inathamni kubwa sana, sawa na pea mbili au tatu, ya nguo walizo vaa wakina Mahadhi ile jana.

Mama Radhia anatabasamu kidogo, “ni rafiki yake Mu” anajibu kwa kifupi mama Radhia, na kuwafanya Mariam, Zuhura na mama yao, watazamane kwa macho ya mshangao, na mashaka, “jamani situambizane kama ameshapata mchumba, kuliko kuficha ficha” alisema mama Mariam, kwa sauti yenye mashaka na kusuta.

Mama Radhia anacheka kidogo, “kama ni mchumba atatueleze mwenyewe, maana mpaka sasa mie najuwa ni rafiki yake Mu” anasema mama Radhia, kwa sauti ya upole, lakini alionekana wazi kuwa alikuwa mwenye furaha, “au ni mume wamtu, maana wakati ule tulijuwa amepata mume wake, kumbe mume wamtu” alisema Mariam, na hapo mama Radhia, akahisi kuwa, maneno ya mama Mariam na binti zake, ayakuwa na nia njema, ni wazi wanamaanisha kuwa, binti yake atakuwa ameanza kutembea hovyo na wanaume za watu.

Hivyo akawaza jambo la haraka, ambalo ni kumweleza mume wake, kuhusu urafiki wa watoto wake na huyo kijana, japo lilikuwa ni jambo gumu kidogo, lakini alipanga japo amgusie ata kuhusu mwaliko waliopewa, watoto wake, hakika alijuwa kama akichelewa kufanya hivyo, mama Mariam ata tangulia kuongea na mumwake na kumweleza anavyojuwa yeye.

Hivyo mama Radhia anainuka na kuelekea ndani, huku wakina Mariam wakimtazama kwa jicho la chuki, na mioyo yao ilishaanza kupoteza hamu ya kwenda kwa wawapenzi wao, kwa kuzingatia wanarudia nguo na mbaya zaidi nguo zao azikuwa na thamani kama ilivyo nguo ya Radhia, ambayo thamani yake ingefaa kununua pea nne za magauni yao.*******

Naaaaaam!, taxi inaingia barabara tulivu ya njia mbili, ya uwanja wa ndege darajani, kupitia maisala gymkana, nalo lina shika ualekeo wa kilimani, linapita kwenye ile nyumba ambayo walimwona Edgar anatokea, lakin awakupazinga tia, ila wanashangaa mioyoni mwao, sababu walitegemea kuwa wataelekea mjini.

Wanazidi kushangaa wanapo liona gari ili dogo la kukodi likisimama kwenye lango la kuingilia ikulu, ya rais wa Zanzibar, waninua shingo zao kuchungulia nje ya gari, wanaona getini kuna skari kadhaa wa jeshi la polisi, wakike na wakiume, wenye bunduki zao mikononi, pamoja na watu waliovalia suit yeusi na miwani meusi.

Wanaona magari yanaingia mle ndani ya jumba lile, ambalo ni makazi na ofisi za rais, wanatazamana usoni, kama vile wanaulizana kitu kwa mshangao, “jamani huku wapi?” ni Zahara pekee ndie anapata ujasiri wa kuuliza, siyo kwamba awapajuwi, ila wanashangaa wamekujaje hapa, wakati wao wanajuwa wanaenda kwenye mwaliko wa sikuu.

Lakini kabla awajapeana majibu, dereva wa taxi anaongea, “shemeji amesema mkisuka mpigie simu, anasema dereva wa taxi, na wao wanapunguza hofu na mshangao kisha wanashuka toka kwenye gari, na kusimama pembeni.

Radhia anatoa simu na kupiga namba ya Edgar, nayo inaanza kuita, huku wanashuhudia magari kadhaa ya yakiingia katika msafara unao ongozwa na magari ya polisi, baadhi yake, yakiwa na bendera za taifa, Mukhsin anajaribu kutazama ndani ya geti, anaona magari mengi yakiwa yamejipanga, sambamba na askari kadhaa wajeshi la polisi na jeshi la ulinzi, pamoja na watu kadhaa walio valia suit na nguo nadhifu za kiraia, waliosimama karibu na magari.

Simu inapokelewa, “hallow dada Radhia asalam aleykum” inasikika sauti nzito toka upande wapili wasimu, sambamba na sauti za music wa quaswida, na sauti za watu walipo katika maongezi na vicheko, “aleykum salaam, sie tupo hapa nje” anasema Radhia kwa sauti tulivu pia, lakini yenye uoga, huku anamtazama mmoja kati ya askari aliekuwa anawasogelea.

“ok!, dakika moja” anasema Edgar, kisha simu ikakatika, Radhia anawatazama wadogo zake, na ambao walikuwa wanamtazama pia kwa uoga, maana tayari askari alisha wafikia, “vipi nyie mnaitaji nini hapa?” anauliza yule askari wa jeshi la polisi, na wakati huo baadhi ya magari yanaelea kuingia. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JamiiForums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA NANE
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: “ok!, dakika moja” anasema Edgar, kisha simu ikakatika, Radhia anawatazama wadogo zake, na ambao walikuwa wanamtazama pia kwa uoga, maana tayari askari alisha wafikia, “vipi nyie mnaitaji nini hapa?” anauliza yule askari wa jeshi la polisi, na wakati huo baadhi ya magari yanaelea kuingia. ENDELEA….

Radhia anamtazama Mukhsin kwamba atoe jibu, “tuna mwitaji Edgar, amesema tuletwe hapa” anajibu Mukhsin, kwasauti yenye utulivu wakujiamini, lakini wakashangaa kuona yule askari anakunja uso kwa mshangao, “Edgar ndio nani, amewaambia anakaa hapa?” anauliza yule askari kwa sauti yenye mashaka.

Safari hii Mukhsin anamtazama Radhia, ambae ni dada yake, akimjulisha safari hii zame yake kutoa jibu, lakini hakuna anae weza kuelekezea Edgar ni nani, hivyo wanabakia kutoa macho kwa mshangao, ata yule askari anajuwa kuwa watu awa awakuwa wanamjuwa wanae mfwata, hivyo ni wababaishaji.

Laki kabla yule askari ajasema lolote, anasikia sauti toka getini, “shabani, ebu njoo nao” ilikuwa ni sauti ya askari mmoja, kati ya wale waliokuwepo pale getini, wote wanatazama kule getini, wanawaona wale wote waliokuwepo getini wanawatazama, kwa macho ya udadisi, “aya twendeni mkajieleze” anasema yule askari wa jeshi la polisi, na wakaanza kutembea kuongozana na yule askari, kusogelea getini, ambako sasa alikuwa ameongezeka mwanamke mmoja alie valia tofauti na wale wengine, yeye alikuwa amevalia gauni refu na hijab.

Radhia na wadogo zake wanatembea kwa tahadhari, huku akiwa tofauti na wadogo zake, ambao awakuwa na uoga mwingi, maana waliamini kuwa Edgar awezi kuwadanganya, Radhia yeye alikuwa anawaza mengi sana, juu ya Edgar na huu mwaliko wake, “ni kweli yupo hapa, na kama yupo hapa yeye ninani mpaka atuarike ikuru, na sijuwi nitaenda kuwajibu nini awa, na huyu mbona atokei au nimpigie tena” anawaza Radhia ambae anawatazama wale watu waliopo getini, ambao pia, walikuwa wanawatazama kwa mwacho ya udadisi.

Naaaaam!, Radhia akiwa anajiandaa kujibu maswali, anafika pale geni akiwa na wadogo zake, lakini anashangaa anapokelewa tofauti, “karibu dada karibuni sana” anasema mwanamke mwenye gauni refu, huku anawapatia viambata jina ambavyo uvaliwa shingoni, “asante sana” anajibu Radhia, huku anapokea kiambata jina chake na kukivaa shingoni kama vile mkufu, hivyo hivyo walifanya wadogo zake, ni Radhia pekee ndie alie kumbuka kusoma kilicho andikwa kwenye hiyo name tag.

Wote wanaingia ndani, na kukuta kiofisi ndogo, palikuwa na watu wanne, nyuma ya meza kubwa na computer, huku wengine wawili wakiwa amesimama, kikaguzi hisisha, yani ditector, walikuwa ni mwanaume na mwanamke, “aya akikisheni majina yenu hapo” anasema yule mwanamke alie wapokea, na hapo mmoja kati ya wale watu waliopo kwenye ile ofisi, akaanza kuuliza jina moja baada ya jingine, nao wakayataja, kisha wakwasogelea wale wenye kikaguzi, wakakaguliwa kutokana na jinsia, yani Mukhsin alikaguliwa na mwanaume, na Radhia na Zahara walikaguliwa na yule wakike.

Walipo maliza kukaguliwa, wakaendelea na safari ya kuingia ndani, wakiongozwa na yule mwanamke, waliweza kuona majengo makubwa mazuri yenye pambo na bustani nzuri mbele ya majengo yale, ambayo yalikuwa na mwonekano wa kiofisi.

Magari mazuri ya kifahari na yakawaida yalionekana mbele ya majengo yale, yakiwepo magari binafsi na yale ya selikari, magari ambayo mala nyingi uyaona yakikatiza barabarani chini ya ulinzi mkali wa askari polisi.

Wanaachana na magari yale, ambayo yalikuwa pamojana watu waliovalia suit na nguo za kawaida, pamoja naaskari wa jeshi la polisi, jeshi la ulinzi, JKU, KVZ, KMK na mafunzo, wao wanaendelea kutembea, huku macho yao yakiwa yanaendelea kushangaa vitu vingine, mle ndani, kiasi kwamba Radhia anatamani kama angekuwa na simu yenyekuweza kupiga picha basi angepiga picha nyingi sana.

Sauti za music zinaanza kusikika, sambamba na sauti za watu, arufu tamu ya ya vyakula, inayo zidisha njaa inasikika, na kupenya kwenye pua za wageni hawa ambao ni mala yao ya kwanza kuingia kwenye eneo ili, ambalo uwa wanalipita kila siku kwa nje.********

“yaaaap! Mama Radhia anaingia ndani moja kwa moja anapitiliza uwani, anamkuta mume wake akiwa ametulia anasoma kitabu cha KIFO CHA HAWARA, “samahani mume wangu, tunaweza kuongea kidogo” anaomba mama Radhia, kwa sauti tulivu yenye nidhamu ya hali ya juu, mala tu baada ya kukaa kwenye mkeka, uliopo pembeni ya mume wake, aliekuwa amekaa kwenye kiti cha uvivu.

Mzee Abeid anamtazama mke wake, “bila shaka mke wangu, hakuna kitu kinaweza kunizuwia kuongea na wewe, nini unataka kunieleza, ni kuhusu kile nilicho kutuma kuongea na Radhia?” anauliza mzee Abeid Ally Makame, huku anafunika kitabu chake na kuweka kidole kwenye kurasa aliyo ishia.

Hapo mama Radhia anatabasamu kidogo, uwa anapenda sana ukarimu wa mume wake, maana toka aolewe nae miaka iishilini na nane iliyopita, ajawai kubadirika, na kuwa mbaya kwake, “ndiyo mume wangu, niliongea na Radhia, ila kuna kitu nimegundua, nikaona nikujulishe mapema, usije kumkuta mtaani ukamfikilia vibaya” alisema mama Radhia, kwa sauti yenye tahadhari, maana akujuwa tafsiri ya mume wake katika jambo lile itakuwaje.

“madamu unanitoa wasi wasi, ondoa shaka mke wangu, naomba unieleze, kuliko kunilambisha ndimu na kuniacha na ugwadu wa kutaka kujuwa” anasema mzee huyu, ambae elimu yake yajuu ya sayansi ya viumbe hai na mimea, aliichukulia SUA, yani Sokoine Univarsity Of Agricalture.

Hapo mama Radhia akajituliza kidogo na kujiweka sawa, maana licha ya kuwa mpole na mpenda amani, lakini mzee huyu akuwai kupenda mambo ya kipuuzi ata siku moja, ata ujinga wa binti zake wakina Mariam, ulikuwa unafanyika bila yeye kujuwa.

“ni mwezi sasa, naona kuna ukaribu na kijana mmoja anaitwa Edgar, mala ya kwanza nilimsikia kama rafiki wa Mukhsin, anacheza nae mpira wakikapu, lakini kwa sasa naona amezidisha upendo kwa Radhia na wadogo zake” alisema mama Radhia, ambae alielezea kuanzia kununuliwa viatu kwa Mukhsin kwaajiya mashindano ya mapinduzi, na pia kununua viatu vya shule vya Zahara, na ile ya jana ya kuwatoa mtoko wa sikuu, na kuwapatia fedha wakina Mukhsin.

Kubwa kuliko ilikuwa hii ya leo, ambayo licha kwenda nao kwenye mwaliko ambao hakuna anae juwa wanako elekea, ila pia ni nguo za thamani walizo nunuliwa, nguo ambazo zina gharama kubwa, yani kwa wote watatu, nikama iligjaribu lakini tatu kasolo.

Mzee Abeid ambae alisikiliza kwa umakini mkubwa, mwishoni akauliza, “ulimwuliza kuhusu ilo?” aliuliza mzee Makame, “nilimwuliza, lakini akasema hakuna uhusiano wowote kati yake na huyo kijana zaidi ya kuwa ni rafiki wa mdogo wake” alijibu mama Radhia, ambae lengo la kumweleza mume wake mambo aya ni kwamba, yasije kutangulia maneno ya uzushi, ya kumchafua biti yao.

Mzee Abeid akatulia kidogo, kama anatafakari jambo, kabla ajamtazama mke wake, “lakini kama ni rafiki yake Mukhsin, anawezaje kuwa na uwezo wa kununua nguo zenye thamani kubwa sawa na mshara wa mtu?” anauliza mzee Abeid, mke wake anakosa jibu, maana ata yeye aelewi lolote ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA JF
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KUMI NA TISA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: Mzee Abeid akatulia kidogo, kama anatafakari jambo, kabla ajamtazama mke wake, “lakini kama ni rafiki yake Mukhsin, anawezaje kuwa na uwezo wa kununua nguo zenye thamani kubwa sawa na mshara wa mtu?” anauliza mzee Abeid, mke wake anakosa jibu, maana ata yeye aelewi lolote ENDELEA….

“sawa mke wangu, Radhia kwa sasa ni mtu mzima, na amesha wai kuishi maisha ya ndoa, naamini anajitambua na anaweza kujisimamia, cha msingi kama ni kweli huyo bwana ata kama ni rafiki wa kawaida, basi aje tumfahamu, na tujuwe anafanya kazi gani, na anaishi wapi” alisema mzee Abeid kwa sauti yenye busara, kabla ajamluhusu mke wake akaendelee na mambo mengine.*********

Naaaaaaam!, upande wapili ikulu, ukiachilia upande wa maofisini, sasa upande wa makazi ya rais wa Zanzibar na familia yake, mida hii panaonekana pakiwa pamechangamka sana, sauti ya music wa quaswida, na arufu nzuri ya vyakula vya kila aina, huku wandishi wa habari toka mashirika mbali mbali ya habari, ya serikali na binafsi, wakiwa wanaendelea kuchukuwa matukio kwa camera zao maridadi zenye uwezo tofauti.

Wanaonekana watu wengi kiasi, waliopendeza kwa mavazi mazuri ya kupendeza, wasio pungua sabini, wake kwa waume na watoto wa lika zote, yani watoto wachanga walio bebwa au baba zao, watoto wasio zidi ishilini wenye umri wa kati ya mwaka mmoja, mpaka miaka kumi na tatu.

Pia walikuwepo vijana wachache sana wakiume na wakike, wenye umri wa kuanzia miaka kumi na tano mpaka kumi na saba, wote wakiwa wamekuja na baba zao, au mama zao, au ndugu yoyote alie alikwa, kama ilivyokuwa kwa wakina Radhia, na wadogo zake.

Lakini pia idadi kubwa ya wanaume waliokuwepo pale, walikuwa ni viongozi, wa serikali, yani mawaziri, makamo wa rais na rais mwenyewe, pia palikuwa na mabarozi wachache wenye barozi zao hapa Zanzibar, walikuwepo pia wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ambao awakuzidi sita.

Pia walikuwepo wakuu wa idara mbali mbali, kama vile tanesco, wasimamizi wa barabara, wakuu wa idara ya mapato, na Doctor mkuu wa hospitar kuu ya taifa ya mnazi mmoja, pamoja na wafanya biashara wakubwa wa ksiwani Zanzibar.

Ila pia, palikuwa na wanawake kadhaa wenye madaraka juu, japo wengine walikuja kama familia, yani walikuja na waume zao, ambao ndio walio alikwa, lakini walikuwepo wabunge na maziri wakike, ambao waliudhulia pale ikuru, ambapo palikuwa na afla ya chakula cha mchana.

Wanawake na watoto wakike, walionekana kuvalia magauni marefu na hijab zao vichwani, ilipendeza sana, wanaume wengi wakiwa wamevalia kanzu nzuri za rangi tofauti tofauti, na baraghashia zao, pia wapo wanaume waliovalia suruali za vitambaa na mashati ya vifungo, nao vichwani mwao walivalia baraghashia zao.

Licha ya kuwa na viwanja vingi vyenye michezo ya watoto, lakini hakuna mtoto aliekuwa anacheza mchezo wowote, zaidi kila mmoja alikuwa amesimama karibu na baba yake, au mama yake, ambae alikuwa anasalimiana na wenzake, huku wakiongea ili na lile, na rais pamoja namke wake wakiwa wamejichanganya nao.

Pia kila alie ilingia eneo lile, alienda kumsalimia rais, kisha akaenda kusalimiana na watu wengine, akiwepo mke wa rais na mawaziri wengine na wake zao, kisha angeendelea maongezi na mtu anae mfahamu au mume wake, au ndugu yake, ila idadi kubwa ilikuwa ni mke na mume.

Upande wa mbele kidogo chini ya mahema yaliyojengwa vizuri, na kutandikwa mazuria, palikuwa panaandaliwa vyakula vingi na zuri, katika sahani nyingi sana, zenye pilau, bilyani, viazi mbatata, mabakuli ya urojo, mabakuri yamapaja ya kuku, sotojo la ng’ombe na vitafunwa vya maandazi bagia sambusa, na vinginevyo.

Hayo yote yalionwa na wafanyakazi kumi wa idara ya afya, waliokuwepo pembeni ya magari mawili ya wagonjwa, yani ambulance, yaliyo simama mita chache toka pale walipo kuwepo wageni waarikwa na wenyeji wao, na mmoja kati ya wahuguzi waliokuwepo pale, alikuwepo Amina, rafiki mkubwa wa Siwema, ambae alikuwa amesimama na mwenzie mmoja, akifwatilia kwa umakini mkubwa kila kilichokuwa kinaendelea.

Amina akiwa anafwatilia wageni waharikwa, alitazama sana watu ambao akuwai kuwaona kwa ukaribu, na pia alifwatilia sana mavazi ya wanawake wenzie, ni kawaida kwa wanawake, “lile gauni bei yake ni laki mbili, lakini alija mpendeza sana” alisema mwenzie na Amina, huku wanaendelea kutazama, hicho ndicho walichokuwa wanakifanya toka walipofika mapema saa nne.

Ila pia ukiachilia kufwatilia aina na mitindo ya magauni na viatu, kuna kitu Amina na mwenzie, kiliwavutia zaidi, “yani mwenzio yule mkaka nashindwa ata kujizuwia” alisema yule mwenzie na Amina, huku wanamtazama kijana mmoja mwenye urefu wa wastani, mweusi kiasi, na mwili ulio jengeka kimazoezi, alie jaliwa sura nzuri na uso wenye tabasamu, alie valia kanzu ya blue, na yenye nakshi ya nyuzi nyeupe na rangi ya dhahabu, kama ilivyo baraghashia yake, chini akiwa amevalia viatu vya ngozi vya wazi, yani sendo.

“sema tu, ni mheshimiwa, na ajichanganyi mitaani, vingenevyo angesababisha niachike” alisema Amina, na hapo wote wawili wakacheka kwa pamoja, “unataka polisi wa watu apate kesi ya mauwaji” alisema mwenzie na Amina, wakacheka sana, “mh!, polisi na barozi wapi na wapi” alisema Amina akizidi kumsifia yule kijana, ambae alionekana kuwa na umri mdogo, kuliko wageni wote waalikwa wenye nyadhifa zao, na sasa alikuwa amesimama karibu kabisa na rais, pamoja na viongozi wengine watatu, wakionegea na kucheka kwa pamoja.

“lakini kwanini #Mbogo_Land wameleta barozi mdogo namna hii?” anauliza yule mwanamke mwingine, huku anageuza shingo yake kutazama kule wanako ingilia wageni waalikwa, “Amina unakumbuka lile gauni nililokuambia kuwa nilitaka kununua nikashindwa bei, lile paleeee” alisema yule mwenzie na Amina, huku anatazama kule wanako ingilia, amina nae anatazama upande huo.

Naaaaaaam! Amina anajikuta anatoa macho ya mshangao, akiwatazama watu wanne, mmoja akiwa ni mwanamke ambae walisha mwona hapo mwanzo, akiwa pale kwenye afla, ila watatu walikuwa ni wageni walioingia mida hii, ambao walikuwa ni wanawake wawili, yani dada mkubwa na mschana mdogo, waliovalia magauni mazuri ya kufanana, na kijana mmoja wa miaka kumi na saba, alie valia kanzu iliyofanana na yule balozi wa #Mbogo_Land.

“Tooooba!, toba!, toba!, toba, hivi naota au macho yamgu yameweuka?” anauliza Amina kwa sauti ya chini yenye mshangao mkubwa Amina, na kumfanya mwenzie amshangae, “siyo macho tu, ila utakuwa umeweuka mwili mzima, sasa nini kinakufanya ushangae lile gauni ni elfu semanini, na yule lazima atakuwa mke wa waziri au mwakilishi” alisema mwenzie na Amina, kwa sauti ya kumshangaa Amina. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA KWA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ISHIRINI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: “Tooooba!, toba!, toba!, toba, hivi naota au macho yamgu yameweuka?” anauliza Amina kwa sauti ya chini yenye mshangao mkubwa Amina, na kumfanya mwenzie amshangae, “siyo macho tu, ila utakuwa umeweuka mwili mzima, sasa nini kinakufanya ushangae lile gauni ni elfu semanini, na yule lazima atakuwa mke wa waziri au mwakilishi” alisema mwenzie na Amina, kwa sauti ya kumshangaa Amina. ENDELEA….

Amina anashindwa acheke au alie, “hivi unajisikia unacho sema wewe, nani kasema yule ni mke wa mtu, yule ni mjane, tena ni mdogo wake Siwema Makame, ni mtoto wa bi mdogo, aliachika mwaka jana, alikuwa anakaa pale michenzani, tena kisa ugumba, nashangaa amekujaje hapa” anasema Amina, huku wanamtazama Radhia, alie ongozana na wadogo zake Zahara na Mukhsin, ambao nyuso zao zilikuwa zimejawa na furaha na matabasamu pana mapana.

“labda Siwema ndio ata nifafanulia, anasema Amina, huku anatoa simu yake haraka, “sasa utaharibu, ebu kuwa makini unapopiga picha” anasema yule mwenzie na Amina, huku wote wawili wanawatazama wakina Radhia, ambao leo walionyesha uharisia wao wa uchotara wa kiarab.

Tuachane na wakina Amina, tusogee kwa wageni waalikwa, ambako Radhia ana wadogo zake wanakiwa wanamfwata yule mwanamke, alie wafwata getini, wanajikuta wanaibukia kwenye eneo la wazi, lenye watu wengi, lakini shida ni moja tu, watu wanao waona mbele yao, ni watu ambao mala zote wanaona kwenye magari wakipita na ving’ora, au kwenye TV, akiwepo mheshimiwa rais, na mke wake.

Uoga unawavaa Radhia na Mukhsin, kasoro Zahara, ambae akuwa anaelewa lolote, kwamaana alijionea kawaida tu, alicho waza ni ile misosi iliyokuwa inaandaliwa, na bembea zilizokuwa zinawasubiri wamalize kula, “jama Edgar akuona kwa kutupeleka zaidi ya hapa, tukivukzwa itakuwaje?” analalamika Radhia kwa sauti ya chini,

Radhia mwenye wasi wasi na hofu kubwa, anamwona Edgar mbele yao mita kama ishilini hivi, akiwa amevalia kanzu inayo fanana na kanzu ya Mukhsin, aliekuwa anaongea na kucheka na watu aliokuwa nao, kitu ambacho Radhia akukijuwa ni kwamba, uingiaji wake pale ulishaanza kuvuta macho ya watu wengi, asa wanaume.

Lakini wanapo msogelea, wanagundua kuwa kati ya watu wale ambao ni viongozi wakubwa wa serikalini, mmoja wao ni mheshimiwa rais, “mtumeee roho yangu mie!” anasema Radhia, kwa sauti ya chini, wakati huo tayari alikuwa amesha karibia kabisa, alipokuwa amesimama Edgar, ambae alikuwa bado ajawaona wakina Radhia.

“samahani mheshimiwa, wageni wako hawa hapa” alisema yule mwanamke, kwa sauti ya unyenyekevu, na yenye nidhamu ya hali ya juu, Edgar anageuka na kuwatazama wakina Radhia, anapo waona anatabasamu kwa furaha.

Ukweli nikama Radhia anashikwa na mshangao, lakini anashindwa kushangaa wazi wazi, maana ni aibu kushangaa mbele ya waheshimiwa, lakini bado anajiuliza Edgar ni mheshimwa kivipi, “ujuwe niliwaona mkiwa kuleee, lakini siku watambua kabisa, hakika leo mmependeza sana” anasema kijana Edgar, na kuwafanya ata wale wengine, yani rais na wale mawaziri wawatazame wakina Radhia, asa macho yote yakikwama kwa Radhia mwenyewe.

Hapo wakajikuta wanakubariana na Edgar, kuwa Radhia amependeza sana, wote wanatikisa vichwa vyao juu chini, huku nyuso zao zikiunda tabasamu na vicheko laini, kitendo ambacho kilifanya Radhia ajisike aibu zaidi, na kuishia kutabasamu, huku anatazama chini.

“Asalam Aleykum” anasalimia Radhia kwa sauti tulivu na nyenyekevu, hapo wote wanaitikia kwa pamoja, “Aleykum Salaam” huku rais akimalizia kwa kusema, “karibu sana, naona bwana Edgar, alikuwa anawasubiri kwa hamu kubwa, yeye peke yake, ndio alikuwa bachela, bila familia” alisema mheshimiwa rais, kwa sauti iliyo ashilia utani, ikifwatia nakicheko toka kwa wengine waliokuwa pamoja, yani wale watatu pamoja na Edgar mwenyewe, ata wakina Radhia wakajikuta wanacheka pia.

“hamku amini niliposema nina ndugu zangu hapa Zanzibar, nazani mmejionea wenyewe” alisema Edgar kwa sauti ya ucheshi, na wote wakacheka kwa pamoja, “aya bwana Edgar, tumesha amini sasa” anasema mmoja kati ya wale mawaziri, “Radhia hapa Zanzibar ni mwenyeji wa mtaa gani?” anauliza mheshimiwa rais, huku anamtazama Zahara.

Niwazi alitajiwa majina lakini aliyachanganya, “tunaishi jang’ombe, mtaa wa jang’ombe kwa soud” anajibu Radhia mwenyewe, hapo mheshimiwa anamtazama Radhia mwenyewe, “kumbe Radhia ni huyu mkubwa, na huyu ndie Zahara, nilichanganya majina” anasema mheshimiwa, huku wote wanacheka.

Lakini bado rais naonekana kuwa na maswali, “ok! pale jang’ombe kwa mzee nani?” anauliza rais, akiwa anamtazama Zahara, ikiwa ni sehemu ya maongezi ya kawaida, “sisi ni watoto wa mwalimu Abeid Ally Makame, anafundisha shule ya sekondari Mwanakwelekwe A” anajibu Radhia, na hapo waziri mmoja kati ya wale watatu waliokuwepo pale, akaonekana kufahamu jambo.

“namfahamu huyo mwalimu, ni mkongwe sana pale mwanakwelekwe, anaelimu ya juu ya sayansi ya viumbe na kilimo, alisomea chuo kikuu cha sokoine” alisema yule waziri, ambae kimajukumu ni waziri wa elimu.

“he! kumbe tuna wataalamu wakilimo, ebu angalia taarifa zake, kisha nizipate ofisini kwangu” anasema mheshimiwa rais, na wakati huo mke wa rais akasogea karibu yao, “asalaam Aleykum” anasalimia mke wa rais kwa maana ya kumsalimia Radhia, huku anampatia mkono, “aleykum salaam,” anaitikia Radhia, huku wanapeana mikono.

Ilikuwa ni mala ya kwanza kushikana mkono mkono, kiongozi au mke wakiongozi mkubwa kama huyu, “karibu sana, isiwe mwisho leo, tena si unakaa hapo jirani, kwa barozi Edgar?” aliuliza mke wa rais, ambae anaonekana ni mcheshi sana, tofauti na anavyo onekana kwenye TV, ambae ni wazi aliamini kuwa, Radhia ni mke wa Edgar, na wanaishi pamoja.

Hapo Radhia anamtazama Edgar, kwa macho yaliyo jaa staajabiko na aibu, ni kama anauliza ajibu nini, lakini mheshimiwa rais ndie anajibu, “bila shaka bado awajaowana, ila na amini mala hii, tutapeleka binti yetu #Mbogo_Land, kama tulivyo mpeleka Doctor Irine kwa king Eric wa 25” alisema rais, na wote wakaangua kicheko cha furaha.

Hii kauri ya mheshimiwa rais iliingia moyoni kwa Radhia, na kutamani iwe kweli, japo akujuwa barozi Edgar kwa maana hipi mpaka aitwe barozi, ila alichoelewa ni kwamba, Edgar ni mtu mwenye hasiri ya #Mbogo_Land, Radhia anamtazama Edgar, ambae pia anamtazama, Radhia anakwepesha macho na kumtazama Mukhsin, ambae akuonekana kujari.

“ama hakika ndoa yao itakuwa kubwa sana, nazani mungu akipenda, itakutanisha tena kama hivi” alisema mwingine, na hapo Radhia alitabasamia chini, huku anamtazama tena Edgar, lakini safari hii kwa jicho la wizi, lililojaa aibu, akamwona kijana huyu anatabasamu. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI: “ama hakika ndoa yao itakuwa kubwa sana, nazani mungu akipenda, itakutanisha tena kama hivi” alisema mwingine, na hapo Radhia alitabasamia chini, huku anamtazama tena Edgar, lakini safari hii kwa jicho la wizi, lililojaa aibu, akamwona kijana huyu anatabasamu. ENDELEA….

Maongezi anaendelea, wanazungumzia kuhusu harusi ya Edgar na Radhia, Edgar naonekana kawaida, lakini Radhia anajisikia aibu, Mukhsini anahisi kuwa ni utani wa mheshimiwa rais na mawaziri, hivyo achukulii kama jambo la kweli, lakini anastaajabu kugundua kuwa rafiki yake ni mtu kubwa serikalini.

Ilikuwa tofauti kwa Zahara, ambae muda wote alikuwa anatabasamu kwa furaha, huku anawatazama kwa hawamu, Edgar na Radhia, “mimi mtanituma kwa kwa mwalimu Makame, kupeleka barua” alisema yule waziri wa Elimu, na wote wakacheka, “siku ta pili baada harusi nitaandaa chai” alisema mhe Rais, na mke wa Rais akadakia, “aswaaaa!, hapo umenena” alisema mke wa rais, na kumfanya Radhia ajisikie raha, utazani tayari kuna ukweli juu ya lile linalo ongelewa pale.

Labda tuelewane kidogo, kuhusu hii chai inayo zungumziwa, ambayo ni utamaduni wa nchi za bara la ulaya, na nchi nyingi za kiarabu, wakitumia kama afla ndogo ambayo inafanyika jioni, kuanzia mida ya saa kumi, ikiwa na vyakula vingi sana, lakini ikimbatana na chai harisi.

Katika afla hii ambayo ingeandaliwa na muhusika mwenyewe kwa kuwaarika watu ambao awakuweza kuhudhuria katika harusi ile, au ingeandaliwa na mtu mwingine wakaribu, na kukaribisha watu ambao kwa namna moja au nyingine wanaitaji kuwapongeza maharusi.

Naaaaam! sasa Edgar anaona kama wanamchanganyia mambo, ataonekana kuwa lengo siyo urafiki na Mukhsin ila ni kumvizia dada yake, hivyo haraka anabadirisha mwendo wa maongezi, “mheshimiwa, huyu ndie kijana niliekuambia kuwa, nitamfadhiri akasome chuo cha king Augen wa pili, ili aweze kuchezea mpira wakikapu kwenye ligi ya MBA” alisema Edgar akimaanisha kuwa akacheze ligi kubwa yenye nguvu ya baskert Africa, yani #Mbogo_Land Baskert Ball Assosiation.

Habari ile siyo tu inamfurahisha Mukshin na dada yake Radhia, ila pia ata mheshimiwa rais na wale mawaziri, wanaonekana kufurahishwa na jambo ilo, “itakuwa safi sana, atakuwa barozi wetu katika mpira wa kikapu, cha msingi ajitaidi kusoma” anasema raisi, huku anamtazama Mukhsin, ambae aliitikia kwa sauti yenye nidhamu, “ndiyo mheshimiwa” ilikuwa ni sauti tulivu, yenye hofu kubwa, huku akitikisa kichwa juu chini, kukubariana na raisi.

Maongezi yaliendelea kwa dakika chache, huku kila kiongozi akimweleza Mukhsin faida ya huo mpango, na kumsisitiza asome, huku Edgar akisema kuwa ataomba kibari cha kuarika timu ya baskert ya shule mmoja ya sekondari ili iweze kucheza na kombain ya wacheza wa mpira huo wa shule za hapa Zanzibar, mheshimiwa akaafiki, na kuaidi kuwa television ya taifa itarusha moja moja michezo huo, ambao aliomba usiwe mmoja, ili wanafunzi wengi washiriki.

Dakika chache baadae, mke wa rais ana wachukuwa Radhia na Zahara, anaodoka nao kuelekea upande ambao ulikuwa na wanawake wengine, ambao baadhi yao ni viongozi na wengine ni wake wa viongozi, wakimwacha Mukhsin akiwa na Edgar, pamoja na wale viongozi wengine.

Radhia akiwa anajiona kuwa yupo pale kwa bahati mbaya, anafika kwenye kundi la wanawake, anasalimiana nao, huku mke wa rais akifanya utambuliso, Wjamani huyu ni jilani yangu wa hapo baadae, yeye ni mchumba wa barozi Edgar wa #Mbogo_Land, ila ni mwenyeji wa hapa hapa kisiwani” japo mapaka dakika hii utambulisho ulikuwa ni wauongo, lakini ulikuwa mtamu kwa Radhia, ambae akujuwa kama kuna flash disc inameza matukio na maneno.

“hongera sana, mnaendana sana, fanyeni hima mfunge ndoa” anasema mama mmoja ambae ni mke wa waziri kiongozi, mwingine ambae ni mke wamfanya biashara mkubwa pame unguja na Tanzania kwa ujumla anadakia “tena wewe ndiyo wakulisimamia ilo, maana wanaume nao uangalia sisi tunavyotaka” alisema yule mwanamke, ambae kiukweli mume wake anaheshima kubwa nchini Tanzania na nchi za jilani.

Wanawake wengine wanaunga mkono, kwakile kilichosema, “tena ukihamia #Mbogo_Land, utakuwa mwenyeji wangu, kila nikija kutembea huko, nitafikia kwako” anasema waziri wa afya, ambae ni mwanamke, na wote wanacheka wengine wakisema “umaniwai kidogo tu, nilitaka kusema hivyo hivyo” japo ilikuwa ni kama burudani kwa wengine, akiwepo Zahara, lakini ilikuwa ni mshangao na sitofahamu kwa Radhia, ambae alitamani lile swala lingekuwa kweli, na yeye kuwa mke wa Edgar.

“wacha mimi nijiwekee kumbu kumbu” alisema waziri wa afya, huku anachukuwa simu yake, na kupiga picha na Radhia, “nitaweka kwenye kurasa yangu, ili baadae nije niwakumbushe watu” alisema yule waziri, mala baada ya kupiga picha, nawezake wakacheka kidogo, huku wengine wakifanya jambo lile lile alilofanya waziri wa afya.

Hapo baadhi ya wanawake wakapiga picha na Radhia, wakiamini kuwa ni mchumba wa barozi Edgar, toka #Mbogo_Land, huku yeye licha ya kutamani kupiga picha za kwenda kuwaonyesha nyumbani, lakini alikosa camera ya kupigia picha, ni kama Edgar alililona swala ilo, na kufahamu kinamchotokea Radhia, akamtuma Mukhsin akampige picha dada yake, kwa kutumia camera yake ndogo.

Hakika yalikuwa ni matukio ya kupendeza na kumstaajabisha Radhia, ambae aliona kuwa, kama ile itakuwa ni ndoto, basi aliomba alale ata siku tatu, ili afaidi maisha na matukio yale, ambayo akutegemea kama kunasiku itatokea, akajikuta yupo ndani ya jumba lile ambalo ni makazi ya mheshimiwa raisi.

Aliongea kwa karibu na kuuuhuru na mke wa raisi, ata wale wake wa viongozi na matajiri wakubwa waliokuwepo pale, ambao baadae aliwasikia wakizungumzia kuwa, kesho usiku kuanzia saa nne, kutakuwa na tamasha la music wa taharab, litakao fanyika bwawani hotel, na kwamba kuna bendi moja maarufu yenye nyimbo zinazo tamba kwa sasa, toka kwa waimbaji wakubwa wa music huo bara na visiwani.

Ukweli music huo wa taharab, ndiyo music pendwa katika visiwa hivi Zanzibar, hakuna mtu siependa kwenda kwenye onyesho la music huo, tukio mbalo yeye Radhia licha ya kutamani kuhudhuria, lakini akuwai kuhuduria ata siku moja.

Huku nako Amina alifwatilia na kuyashuhudia, matukio yote yaliyo muhusu Radhia na wadogo zake, huku wakati mwingine akijaribu kupingana naukweli kwambayule hakuwa mdogo wake Siwema, yani Radhia, lakini alipo mwona Zahara, alijiwasha data, na kurejea kwenye hakili zake, “lakini imekuwaje waje hapa, wanaumaarufu gani” moja ya swali ambalo Amina alijiuliza.

Japo maswali ayakuishia hapo, “na wanafahamiana wapi na yule barozi wa #Mbogo_Land” anajiuliza Amina, ambae sasa nikama alikuwa anaugulia moyoni mwake, kwa sababu ambazo anazijuwa yeye mwenyewe, “ila yule dada lile gauni limempendeza kweli kweli, na limeenda nae, nazani ni kutokana na uzuri wa shape yake na uzuri wake” anasema mwenzie Amina, na kumtoa Amina kwenye wenge.

Kauri ya mwanamke huyu, inaonyesha kumchukiza Amina, “kwa uzuri gani, bwana au huo uarabu koko wake” anasema Amina kwa sauti yenye chuki, huku anachukuwa simu yake na kutuma picha na video kadhaa, zinazo mwonyesha Radhia akiwa kwenye matukio mbali mbali. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA jamii forums
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA: Kauri ya mwanamke huyu, inaonyesha kumchukiza Amina, “kwa uzuri gani, bwana au huo uarabu koko wake” anasema Amina kwa sauti yenye chuki, huku anachukuwa simu yake na kutuma picha na video kadhaa, zinazo mwonyesha Radhia akiwa kwenye matukio mbali mbali. ENDELEA….

Inamshangaza rafiki yake Amina, ambae anamtazama Amina kwa macho ya mshangao, anamwona yupo busy anatuma picha, video sambamba na ujumbe, “maajabu ya mwaka, mbona jawai kuniambia kuhusu ili” ndivyo ulivyosema ujumbe huo.

Rafiki yake Amina anatafsiri kuwa, ni wivu wakumwona kijana wanae mtamani akiwa na mwanamke mwingine, na mbaya zaidi ni mwanamke anae mfahamu.*******

Saa tisa na dakika kumi, ziliwakuta Mariam na Zuhura, wakiwa wanaingia forodhani, wakiwa na wapenzi wao, yani Mahadhi na Mahamud, wote wanne wakiwa katika sura zenye furaha, japo zilikuwa ni furaha tofauti.

Wakati Zuhura na Mariam wanafurahia offer watakayo pewa ya urojo, ambao wamepanga kuubeba nyumbani wakati watakaporudi, kama ilivyokaiwda yao, ili wakaonekane kwa wale walioko nyumbani, kwamaana ya kuwa lingishia, na kuwatamanisha watakapokuw wanakula.

Lakini Mahadhi na Mahamud, wao walikuwa wepesi tayari walikuwa wamesha maliza kula vitumbua, japo awakutumia ata dakika kumi kukamilisha zoezi lile, ambalo walilifanyia kwenye chumba kimoja, walicho azima kwa rafiki yao, ambapo alianza Mariam na Mahamud, ambao awakutumia ata dakika tano wakatoka na kuanza mipango ya kuoga, kisha wakafwata Mahadhi na Zuhura, ambao pia hawakuchelea, walimaliza na kuoga kisha wakaanza safari ya kuja forodhani.

Wakiwa forodhani, walifanya yale waliyo yafanya jana, ikiwa ni kukaa sehemu na kuwatazama wenzao waliokuwa wanaburudika kwa vinywaji na vitafunwa mbali mbali, wao wakipiga picha na kuzipost tandaoni, wakiambatanisha na vichwa vya habari walivyoona vinafaa.

Wakiwa wanaendelea kushangaa wenzao waliokuwa wamekuja kuburudika, mala wakamwona bwana Idd Kiparago, akiwa anawasogelea, huku ameongozana na wanawake wawili, yani mke wake mkubwa, ambae wanamfahamu toka zamani, na sasa alionekana kuwa na tumbo kubwa la ujauzito, na mwanamke mwingine, ambae ni mgeni macho pao, ambae kwa umri alikuwa analingana na Mariam.

Wanamtazama sehemeji yao, ambae aliwafikia pale walipokuwepo, akiwa na wake zake wawili, wakasalimiana vizuri kabisa, maana siku za nyuma bwana Idd akiwa anaishi na dada yao, hakika walikuwa kama maadui, walitokea kumchukia sana shemeji yao huyu, lakini baada ya kumtariki dada yao, urafiki na mazoewea yakaanza nakuwa makubwa sana.

“naona mmekuja kutembea” alisema Idd, mla baada ya kumaliza kusalimiana nao, “siunajuwa tena mambo ya siku kuu” alijibu Mariam, kwa sauti ye uchangamfu, huku anamtazama mke mkubwa wa bwana Iddi, ambae tumbo lake la ujauzito lilionekana wazi kabisa.

“vipi lakini, wote wazima huko nyumbani?” anauliza Idd, ambae mpaka sasa nikama analengo flani kwa ujio wake ule, “huko wazima tu, labda mkeo wa zamani, yeye ndio anamawazo mengi sana, anazurula tu na wadogo zake” anasema Zuhura, kwa sauti iliyo jaa uchokozi na umbea, na kuwafanya wote wacheke, siyo bwana Idd na wale wake peke yao, ata wakina Mahadhi pia walicheka.

Idd anataachia tabasamu la ushindi, “nilijuwa tu, awezi kupata mwanaume kama mimi, lakini ndiyo hivyo tena, mimi nimesha owa mke wapili” alisema Idd, kwa sauti yenye kiashirio cha mafanikio, huku anamtazama yule mwanamke mwingine, ambae kimwonekano, akuweza kugusa ata arufu ya uzuri wa Radhia.

Hapo wakina Mariam wanamtazama yule mwanamke, huku wameachia matabasamu ya furaha, “hongera shemeji, lakini ulishindwa ata kutu harika kwenzio” alilalamika Mariam, ambae siyo kwamba alilalamikia mwaliko kwaajili ya kuudhuria, ila alilalamika sababu amekosa fimbo ya kumnyanyasa Radhia, maana angemsimnga kipindi chote cha ndoa.

Ukweli habari za Iddy kuowa mke wapili, na mke mkubwa kupata ujauzito, ziliwafurahisha sana wakina Mariam, ambao walisahau kuhusu nguo mpya ya Radhia, “ata hivyo atajuta kuachika, leo lazima nikasimulie nyumbani, najuwa ataumia roho na ugumba wake” anasema Mariam, baada ya idd kuondoka na wake zake.*********

Siwema akiwa nyuki club na mpenzi wake, pamoja na sehemeji yake, yani mume wa rafiki ya ke Amina, pale nyuki, kwenye bar ya jeshi, wanakunywa pombe, na kuburudika kwa matukio mbali mbali, mala akasikia ujumbe unaingia kwenye simu yake, lakini akaupuuzia.

Ata hivyo baada ya dakika mbili, akasikia ujumbe mwingine ukiingia, safari hii aukuwa mmoja, ziliingia jumbe nne mfululizo, akaamua atoe simu na kuitazama kuona mtumaji wa ujumbe alikuwa na shida gani.

Ulikuwa ni ujumbe uliotumwa kwanjia ya whatsapp, toka kwa rafiki yake mkubwa Amina, akafungua na chakwanza kuona ni picha na video nne, zilizo tanguliwa na ujumbe, “maajabu ya mwaka, mbona jawai kuniambia kuhusu ili” ndivyo ulivyosomeka ule ujumbe.

Hapo siwema yani dada mkubwa wa Radhia, kwa mama yake mkubwa, yani mke mkubwa wa baba yake, akiwa na kihoro akaanza kufungua picha na zile video moja baada ya nyingine, na kujionea maajabu ya mwaka, ambayo aliambiwa na Amina.

Kwanza aliiona picha ya mwanamke mmoja mzuri, alie valia gauni zuri, lililomkaa vyema, akiwa amesimama na rais wa Zanzibar, na waheshimiwa wengine, sambamba na kijana mmoja mwenye umbo zuri la kiume, alie valia kanzu iliyofanana na kanzu aliyovaa kijana mdogo pembeni yao.

Mwanzo hakumtambua mwanamke yule, ila baada ya kumwona vizuri yule kijana mdogo pembeni, na kumtambua kuwa ni mdogo wake Mukhsin, yani mtoto wa mke dogo wa baba yake, ndipo alipo mtazama vizuri binti mdogo alie simama pembeni ya yule mwanamke mrembo wa kiarabu, ambae alivaa nae gauni la kufanana, na kumtambua kuwa ni Zahara, mdogo wa Mukhsin, Siwema anarusdisha macho kwa yule mwanamke. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA Jamii furoms
 
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI: Mwanzo hakumtambua mwanamke yule, ila baada ya kumwona vizuri yule kijana mdogo pembeni, na kumtambua kuwa ni mdogo wake Mukhsin, yani mtoto wa mke dogo wa baba yake, ndipo alipo mtazama vizuri binti mdogo alie simama pembeni ya yule mwanamke mrembo wa kiarabu, ambae alivaa nae gauni la kufanana, na kumtambua kuwa ni Zahara, mdogo wa Mukhsin, Siwema anarusdisha macho kwa yule mwanamke. ENDELEA….

Hapo mapigo ya moyo yakamlipuka Siwema, na kumtazama vizuri yule mwanamke ambae kwa mwonekano alikuwa mzuri kupita kiasi, na mwenye umbo zuri la kupendeza.

“Radhia amefikaje hapo, na ameenda kufanya nini na awa wadogo zake?,” anajiuliza Siwema, ambae anakosa jibu, anaamua kutazama video, ambayo inamwonyesha Radhia anasalimiana na mheshimiwa rais, awasikii maongezi, lakini wanawaona wakicheka na kuongea kwa furaha, huku mala kwa mala akiusishwa yule kijana wakuvutia.

Siwema, akiwa aamini kile anacho kiona, anaendelea kutazama video na picha alizo tumiwa, na anaweza kumwona Radhia katika matukio tofauti tofauti, kama vile akiwa anasalimiana na mke warais, ata wakati anaondoka nae akiwa ameongozana na Zahara, pia akiwa anapiga picha na wake waviongozi mbali mbali, pamoja na viongozi wakike, huku wakiongea na kucheka kwapamoja.

“Jamani eeeee!, hivi nikweli tumesha amka au bado tumelala?” anauliza Siwema, kwa sauti ya kilevi yenye mshangao, wanaume wawili wanamshangaa Siwema, ambae anagundua alicho kifanya, anaamua kupotezea, “Amina amenitumia ujumbe kunamtu kamwona huko kwenye afla ikuru, mpaka nimeshangaa amefwata nini” anasema Siwema huku anaweka simu kwenye mkoba wake, na kuendelea na kinywaji, lakini kichwani mwake anajiuliza maswali mengi sana.*******

Naaaaaaam!, siku ilikuwa nzuri sana kwa Radhia na wadogo zake, nazani pia ata kwa kijana Edgar kwa kuwa karibu na familia hii, ambayo nikama ndugu zake huku ugenini, maana baada ya kula, Zahara akajiunga na watoto wenzake kuelekea kwenye bembea, na michezo mingine, huku Mukhsin akijiunga na vijana wa umri wake, ambao walikuwa ni watoto wa viongozi na wafanya biashara wakubwa wa pale Zanzibar.

Watu wengine waliendelea kuongea ili na lile, wapo waliokaa na wake zao, ila wengi walijitenga kwa jinsia, wanaume walikaa kivyao wakiongea ili na lile, na wanawake walikaa kivyao wakiongea ili na lile.

Radhia akiwa amejichanganya na wanawake wengine, mala kwa mala alikuwa anamtazama Edgar, ambae pia alikuwa anaonge ana wanaume wenzake, Radhia aliona kama wanaupoteza muda wa kuwa pamoja, lakini kiukweli moyoni mwake alikuwa anajuwa kabisa, hakuwa na mausiano ya kimapenzi na wanaume huyu, ambae pia akuwa amemtamkia neno lolote la kimapenzi.

Mwisho zilitolewa zawadi mbali mbali kwa watoto walio udhuria ule mwaliko, toka kwa wafanya biashara na baadhi ya viongozi, akiwepo rais mwenyewe, Radhia na Mukhsin ndio walio nufaika na zawadi zile, ambazo azikuwa husu watu wazima, kundi ambalo Radhia alikuwepo, na kama ujuwavyo wakipata wadogo zake, na yeye amepata.

Saa mbili kasoro za usiku, ndio mida ambayo, wageni walimalizika kuondoka pale ikulu, na ndio wakati ambao, wakina Radhia waliagana na Edgar, ambae alimpatia fedha Radhia, kiasi cha elfu hamsini, akiwaeleza kuwa aitumie kesho kwenye matembezi, yeye kesho anaitaji kufanya mazoezi maana ilishapita siku tatu, bila kufanya mazoezi.

Japo aikuwa habari nzuri kwa Radhia, lakini alikubariana nae sababu akuwa na uwezo wa kulazimisha chochote, ukichukulia akuwa na mausino ya kuweza kumpa haki hiyo.

Baada ya hapo, wakina Radhia wakaingia ndani ya gari moja zuri jeusi, aina ya Toyota land cruzer, V8, na kuanza safari ya kuelekea nyumbani, huku wakimwacha Edgar anatembea taratibu kuelekea kwenye nyumba anayo ishi, akiwa ameongozana watu wawili, waliovalia suit nyeusi.

Wakati wanaondoka, Radhia alitamani kama wangeongozana na Edgar ili akapajuwe kwao, na pengine kusalimiana na mama yake, lakini ndio vyo tena anashindwa kumweleza maana akujuwa anaanzia wapi, na anamweleza kama nani wake, ikiwa ni swala la urafiki, kwa leo ingetosha kuishia hapa, labda angekuwa mpenzi wake, ndio angeweza kumwomba waende wote.******

Saa mbili za usiku, licha ya shamla shamla za sikuu kuwa zinaendelea, lakini baadhi ya watu, asa wanaume watu wazima na vijana wapenda utulivu, sasa walikuwa sebuleni wanatazama taarifa ya habari, kwenye kituo cha television cha shirika la habari la Zanzibar.

Mida hii Bwana Idd Kiparago pia alikuwa sebuleni kwake na mke mkubwa, ambae ni mjamzito, wamekaa kwenye makochi tofauti, wakati bwana Idd akiwa busy anatazama television, mke wake alikuwa busy na simu, kwa haraka haraka bwana Idd anajuwa mke wake anatazama matukio kwenye mitandao ya kijamii, ila ukweli ni kwamba, alikuwa anapokea na kutuma ujumbe, kwenda kwa mtu flani alie mseve kwa jina la dada Aziza.

Nikweli Ashura yani mke mkubwa wa Idd, anadada yake mkubwa anae itwa Aziza, lakini pale unaposoma ujumbe uliokuwa unatumwa na yeye anaupoke, zilikuwa ni jumbe zenye maudhui tofauti kwa mwanamke kutumiwa na mwanamke mwenzie, alafu ukizinga tia ni dada yake.

Mfano sasa Ashura alipokea ujumbe ulio andikwa hivi, “kwahiyo na leo ulikuwa na Idd, sasa kesho utaniletea Cuma, nimkuze mtoto wetu?” ndiyo ulivyosema ujumbe toka kwa Aziza, ujumbe ambao kwa haraka ata mtoto mdogo angejuwa kuwa unatumwa na mwanaume, au inafaa uandikwe na mwaume, nasiyo Aziza kama inavyoonekana.

Hapo mke mkubwa aliekuwa amejilaza kwenye kochi, anamtazama mume wake, anamwona yupo busy na TV, anamtazama na kumsikiliza mtangazaji alie kuwa anasoma vichwa vya habari za leo, ikiwepo habari ya tukio la, viongozi mbali mbali na watu mashuhuri, kula cha kula cha mchana na rais wa Zanzibar, Ikulu leo mchana. ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPAHAPA jamii forums
 
Back
Top Bottom