Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
- Thread starter
- #201
ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA SABINI NA TATU
MTUNZI: edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA MBILI: Ni wazi Edgar aliigundua swala ilo, “sasa mbona kama umeshtuka sana niliposema kufanya taratibu, au bado ujapanga kuwa mke wa mtu kwasasa?” aliuliza Edgar kwa sauti nzito na tulivu, swali ambalo lilimshtua sana Radhia, ambae akuamini kama ni kweli alichosikia au ni wenge, “siamini kama ni kweli wachaniamke nijuwe kama ni ndoto” alisema Radhia akijihisi kuwa yupo ndotoni. ......... ENDELEA….
Edgar akajikuta anacheka kidogo, “kwanini Radhia, au nimefanya haraka kukuambia?” analiuliza Edgar kwa sauti yenye msisitizo, nakuzidi kumshangaza Radhia ambae sasa alianza kuhisi machozi yanamtililika machoni mwake, “jamani Eddy, mbona wanifanyia hivyo, mwenzio sijawai kuwa na bahati hiyo, au unataka nipige kelele za furaha” alisema Radhia, kwa sauti ambayo iliyo ambatana na dalili ya kilio cha furaha.
“una stahili kuwa mke wamtu, naimani uliachwa ili nikupate, zaidi tutaongea kesho, nazani tutakuwa na muda mwingi wa kukaa pamoja” sauti nzito ya Edgar ilipenya masikioni mwa Radhia, na kwenda kuutekenya moyo wake, uliozalisha furaha kubwa sana.
Ukweli Radhia akuwa na wazo la kwamba ataolewa tena, asa baada ya kuachika kwa kuto kushika mimba, sasa Edgar anataka kumchumbia, je ata mkubarije, ilihali anajijuwa ashiki mimba, “Eddy baba, niliamua kukuachia mwili wangu, kwa kuwa na kupenda sana, lakini sizani kama nitakufaa, siunajuwa sina uwezo wa kushika mimba, nitakuwaje mke kwako, au na wewe utaniacha” alisema Radhia huku anashindwa kuzuwia machozi ambayo yalizidi kutililika, safari hii siyo kwa furaha, ila alijuwa wazi kabisa yakuwa, huo ndio mwanzo wa kumpoteza Edgar, mwanaume aliemwonjesha mapenzi.
“Radhia mama yangu, nani kasema uwezi kuzaa, achana na mawazo hayo, hakika tutapata watoto kwamajiliwa ya muumba wetu” alisema Edgar kwa sauri ya kubembeleza, ambayo ili zidi kumtoa machozi Radhia, kwa kuona kuwa, kunamwanaume anaupendo wa dhati juu yake, tena ni mwanaume ambe anauwezo wakumpata mwanamke yoyote ampendae.
“asante Edgar, nakupenda sana, hakika nitakutendea yote apaswayo kutendewa mume” alisema Radhia, kwa sauti yenye hisia toka moyoni, “asante sana Radhia, hivi umeona watu walivyo sema kuhusu picha yetu, niliyo iweka kwenye account yangu?” anauliza Edgar, kwa sauti tulivu, hapo Radhia anaacha kulia na kutoa macho kwa mshangao, “weeeee!, umepost picha yetu, mbona sijaiona?” aliuliza Radhia kwa sauti ya mshangao, maana licha ya kutokuwa mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii, ila pia alikuwa anajuwa kuwa, mwanaume akikupost ni moja ya dalili za kuwa wewe ndie mpenzi pekee.
“yaaah!, angalia jinsi watu walivyo comment” alisema Edgar kabla awajaagana na kukata simu, kisha Radhia akaingia kwenye account yake, ambayo kwanza alikuta wafuasi wake wamengezeka mala dufu, wakiwepo watu mashuhuri na baadhi ya viongozi wakubwa, wa nchini kwao na nchi nyingine nyingi.
Radhia ambae akujuwa maana ya wafuasi wengi, akatazama picha ambayo alishikizwa, ni picha iliyopostiwa na Edgar, picha ambayo ilimwonyesha yeye akiwa na Edgar, kule bwawani hotel.
Radhia anatabasamu kwa furaha, huku anatazama maoni ya mengi ya watu, ambayo anaanza kuyasoma moja baada ya jingine, akitamani kujibu baadhi ya maoni, lakini anakumbuka kuwa, maoni yale yalikuwa katikapicha ambayo alipost Edgar, na siyo yeye.
Radhia alifurahi kuona maoni yote yalikuwa mazuri, yaki wapongeza na kuwatakia ndoa njema, na kikubwa zaidi, aliona baadhi ya watu maarufu wakiwa wametoa maoni yao, katika picha yao.
Na kubwa kuliko zote ni kwamba, ata Radhia alipotazama picha yake, ambayo alipostiwa na Edgar, mala baada ya kumfungulia account kwenye mtandao maarufu wa kijamii, na kuona imetolewa maoni mengi sana, tena na watu wakila aina, marafiki zake wa shule, marafiki wa ukubwani, ambao sasa hakuwa nao karibu, pia na watu maarufu, ambao akutegemea kama wanaweza kufanya hivyo.
Hakika mpaka Radhia anapitiwa na usingizi, ata yeye akujijuwa ni saangapi, ila alishtuka asubuhi akiwa amelala na simu yake, bahati akuivunja, wala kuilalia, alie mwamsha ni mama yake, akimtaka akajumuike na mapishi.********
Naaaaaam! siku ya pili, yani siku ya jumamosi, ilianza vizuri sana kwa baadhi ya wanafamilia wa mzee Abeid Makame, pilika pilika za jikoni, ambalo leo liliamia upande wa uwani, huku mzee Makame akiwa amekaa upande wa mbele, yani kibaradhani.
Harufu nzuri tofauti tofauti za vyakula, zilisikika na kutawanyika eneo lote la nyumba na jilani zao, kitu ambacho wenyeji wa mtaa huu, wamezowea kuona vitu kama hivi nyakati za sikuu kama eid au maurid, na sherehe za harusi na sherehe nyinginezo.
Wanawake wote kuanzia Zahara, adi mke mkubwa wa mzee Makame, walikuwa wanaendelea na mapishi, wapo walio shugurika na biliyan, wapo walioshughurika na kuku, ambao waliandaliwa kwa mitindo miwili tofauti, yani wakukaangwa na wale wa mchuzi mzito, ambao unge tumika kwenye biliyan.
Hiyo hivyo iliwa kwenye samaki, ambao wapo walio kaangwa na walio tengenezwa kwa rost la hatari, maandazi chapati na vitu vingine vingi, juice za matunda na vinywaji vingine vingi lakini visivyo na ulevi.
Kila mmoja alionekana kuwa mwenye furaha, ata Mariam na Zuhura nao walionekana kuwa na furaha, japo kuna wakati mioyo yao ulipatwa, na ugumu asa baada ya kukumbuka kuwa mwanaume anaekuja, anakila dalili ya kuwa mpenzi wa Radhia.
Ilikuwa tofauti sana ka Siwema, ambae licha kujilazimisha kuongea na kucheka, huku akiendelea kushugurika na mapishi, lakini bado alimwona Radhia kama amemwondolea bahati zake zote, na kumsababishia majanga kwa mume wake na kazini, hivyo alikuwa amejawa na chuki kubwa moyoni mwake, na siyo tu alimchukia Radhia peke yake, ata mama yake mdogo, yani mama Radhia na baba yake, kwa kuluhusu ugeni ule uje pale nyumbani, lakini alijikaza tu.
Ukweli maandalizi yalikuwa makubwa kiasi cha kumfanya mzee Abeid ashinwe kuuliza na kusibiri kitakacho endelea, maana ukiachilia kuwa mgeni huyu ni rafiki wa kijana wake Mukhsin, lakini pia ni mheshimiwa, yani mwenye wadhifa mkubwa, na anaiwakirisha nchi tajiri yenye sifa nzuri duniani.
Achana na maandalizi ya upande wa vyakula na vinywaji, pia kuna wakati Radhia alijadiliana na mama yake, kisha wakaagiza mazuria ya kisasa, na mito mizuri kubwa, ambayo ilitandikwa sebuleni. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA jamii forums
USIKOSE KUFUATILIA MKASA UJAO WA (KIAPO CHA DAMU KWA DAMU NA CAPTAIN CHUI MCHAFU)
HAPA HAPA JAMII FORUMS
NIWATAKIE USIKU UNONO