ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA MIA MOJA NA MBILI
MTUNZI:
edgar MBOGO
WHATSAPP: 0717924403 au 0743632247.
ILIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA MOJA: Radhia akiwa amelala fofofo juu ya kifua cha Edgar, ambae pia alikuwa amepitiwa na usingizi mzito, kutokana na kuchelewa kulala jana usiku, kwa kazi waliyoifanya mala baada ya kurudi toka kwa mzee Makame. ......... ENDELEA….
Awakujuwa kama Siwema na Idd wapo njiani wanaelekea kwa babu chongo, kufanya kitu ambacho kiliaminiwa kuwa, kinaweza kuwatenganisha, yeye na mpenzi wake Edgar.
Saa saba mchana, ndio mida ambayo Siwema na Idd, walipata nafasi ya kuongia kwa mganga, baada ya kukaa sana, wakisubiri zamu yao, hii nikutokana na uwingi wawatu, waliokuwepo eneo pale, wakisubiri huduma.
Naaaaaam!, sasa walikuwa mbele ya mganga maarufu kwa ulozi na visasi, anae fahamika kwa jina la babu Chongo, hii ni kutokana na jinsi analo tumia kwenye ulozi wake, lilifahamika kwa jina la jinni chongo.
Ukweli sifa za huyu mzee ni kwamba, akuwai kushindwa kufanya alicho kusidia kufanya, hakuna mteja aliefika kwake akarudi na malalamiko, kwamaana hukumu zake, ni ngumu na zauhakika.
Babu chongo anawatazama Siwema na Idd, kwa sekunde kadhaa, akitumia macho yake mekundu ya kuogofya, kabla ajapiga chafya kubwa, na kutikisa kichwa kama anasisimwa na jambo baya, “nyie siyo wanandoa, na huyu mwanamke hana shida yoyote katika mwili wake, ila wewe mwanaume ndie mwenyewe shida” alisema yule babu, kwa sauti yenye mkromo wa kutisha.
Siwema na Idd wanatazamana, kwa mshangao, kabla awaja mtazama babu chongo, “hapana babu, wote hatuna shida katika miili yetu, ila tuna shida imetuleta wote kwa pamoja” alisema Siwema, lakini babu akafumba macho na kufanya kama anavuta hisia za jambo flani, kisha akatoa ngurumo moja nzito.
“sikia binti, mwenzio anatatizo kubwa sana, alisha owa wake watatu, na bado ajabahatika kupata mtoto mpaka sasa” alisema yule babu kwa sauti ya mkazo, na safari hii, akiwafanya Siwema na Idd, kutazamana kwa mshangao kubwa sana.
Siwema akiingiwa na mashaka juu ya sifa za huyu mganga, huku Idd akianza akikumbuka mambo mambo mawili kwa haraka, moja ni kwamba, toka jana asubuhi ajarudi tena kumwona Ashura kule hospital, pili alikumbuka kuhusu ukaribu wa mke wake na mpenzi wake wa zamani, yani kijana Shaban Uss.
Kabla Siwema ajasema au kuuliza chochote, akamsikia ganga akiendelea, “tatizo halipo kwa wake zako, tatizo unalo mwenywe, unatakiwa kupata tiba za hospital siyo kwa mganga” alisema babu Chongo, na kumfanya Idd aamini kuwa kweli alipaswa kufwatilia nyenendo za mke wake na siyo kumfwatilia Radhia.
“lakini babu sisi tumekuja kwa swala jingine, kunamtu tunaitaji kumtengeneza ili aache jeuri” alisema Siwema, na kumfanya babu atulie kidogo, kabla ajampatia karatasi nyeupe, na karamu ya risasi, yani pensel, “andika majina yake matatu” alisema babu chongo na Siwema akafanya hivyo na kupatia babu lile karatasi, “usinipe mimi, weka kwenye hicho chungu, kisha kimoyo moyo unachotaka kitokee” anasema babu chingo, huku anasogeza chungu mbele ya Siwema.
Siwema analikunja kunja lile katarasi na kuliweka kwenye chungu, kisha anaanza kuongea kimya kimya, kama anakinong’onoeza kile chungu, adi alipo maliza, “tayari babu” alisema Siwema.
babu chongo anachukuwa nuga flani na kuumwagia kwenye chungu hicho, unalipuka moto mkubwa, na karatasi linaanza kuungua, “anaitwa Radhia Abeid Makame, liachika, lakini sasa anamwanaume, mwingine, na anaujauzito, anapendwa sana na mchumba wake, sasa anajiandaa kwenda nje ya nchi” anasema babu chongo, huku Siwema anaitikia kwa uthibitisho, “tawile”.
Hapo mganga anatuia kidogo, kama vile kuna kitu akipo sawa, kisha anamtazama Idd, “kwanini unataka kumdhuru mtu ambae ajakukosea kitu, wewe ndie ulie mwacha mkeo kwa kosa lako mwenyewe?” anauliza mganga chongo, kwa sauti ile ile nzito yenye mikoromo.
Idd pasipo kupepesa macho akajibu, “babu roho inaniuma kuona anakuwa na mwanaume mwingine, sitaki aishi kwa raha baada ya kutoka kwangu” ilo ndilo lilikuwa jibu la Idd.
Babu chongo anamtazama Siwema, “ulifukuzwa kazi yeye akakusaidia kurudi kazini, na sasa unataka kumdhuru kwanini, maana bado anawasadia wadogo zako?” aliuliza babu chingo, “sababu ananinyanyasa sana, anamalingo na majivuno, anajiona yeye ndio kila kitu, nataka akose kila kitu” alisema Siwema, bila kuona aibu yoyote.
Babu chingo anatulia kidogo, kama vile anasikiliza jambo toka sehemu, “sikilizeni wajukuu zangu, huyo mtu ajawakosea jambo lolote, hivyo basi mashariti ya kumfanyia mnacho taka ni magumu sana, je mpo tayari kuya tekeleza?” aliuliza babu chongo, huku anawatazama kwa hawamu wawili awa.
Sijuwi kwakuwa walikuwa na chuki na Radhia, amawivu na kuto kufikilia, wote wawili bila kujiuliza ata kidogo, waka itikia “tupo tayari babu” walijibu kwa pamoja.
“kwanza wekeni laki tano kwenye hapo kwenye gamba la kasa” alisema babu Chongo, huku anaonyesha kwenye gamba la kumbe cha baharini, kinachofanana na kobe, Idd bila kinyongo anatoa kibunda cha fedha na kuhesabu kwa mafungu matano ya noti za elfu kumi kumi, na kuweka sehemu aliyo elekezwa.
Baada ya hapo babu chongo anachanganya dawa zake pamoja na majivu ya lile kratasi lililoandikwa jina la Radhia, kisha akaweka funga kwenye kitambaa cheupe, na kumpatia Siwema, “zingatia ya fuatayo binti, endapo utayakosea basi usinilahumu kwa lolote” sawa babu” anaitikia Siwema.
“hakikisha unaweka kwenye chakula atakacho kula, asile mtu mwingine asie usika, zaidi ya yeye mwenywe” alisema babu chongo, kwa msisitizo, “sawa” anaitikia Siwema, “hakikisha dawa aishikwi na mtu mwingine” alisema babu chongo, kwa sauti ya msisitizo, “sawa babu” anaitikia Siwema.
“na utakapo igusa hii dawa wakati wa kumwekea, hakikisha hupo msafi, yani ujatoka kukutana na mwanaume, na umevaa nguo safi ya ndani” alisisitiza babu chongo, kabla awajaluhusiwa kuondoka zao.
Waliondoka hapo huku wakiambizana kuwa mganga aliwatisha bule, kuhusu mashariti ya dawa ile, kwamaana ayakuwa magumu, kama alivyosema, kwamaana waliamini kuwa watayamudu bila shida yoyote. *******
Saa moja za jioni, ndio mida ambayo, Idd na Siwema waliachana na maeneo ya dukani kwa dukani kwa sharif, nakuelekea majumbani kwao, kila mmoja akiamini kuwa mwisho wa Radhia unakaribia, na sasa anaenda kushi maisha magumu ya shida na dhiki.
Idd hakuwa na mpango wowote wa kwenda hospital, na wala akutaka kuamini maneno ya mganga, kuhusu yeye kuto kuwa na watoto, japo alimini kuwa atawafanikishia swala la Radhia kupoteza mimba na haliki, kwamaana ya kuwachizi, kitu ambacho kitamfanya Edgar amwache.
Siwema anatembea huku dawa hupo kwenye mkoba wake, anapokaribia kufika nyumbani kwake, mala anasikia simu yake inaita, akaitoa kwenye mkoba na kuitazama, ilikuona mpigaji ni nani.
Siwema alishangaa na kushtuka kwanguvu sana, maana akumini alicho kiona, “Said” anasema Siwema kwa sauti ya chini yenye kujawa na mshangao, “amekumbuka nini huyu mpuuzi” anajiuliza Siwema, huku anaachia tabasamu laini.
Siwema anaipokea simu, huku anaendelea kutembea, “aya niambie, umekumbuka nini kwangu?” anauliza Siwema, japo sauti yake aikumaanisha anacho sema, maana ilionyesha wazi kuwa mwenye furaha, “haaaa!, jamani bila ata salamu, niambie tukutane wapi ili tuongee” ilisikika sauti yakiume yenye kumbeleza.
“Siwema anatabasamu kidogo, “alafu mke wako utamuaga vipi?” anauliza Siwema, “ameshapanda meli leo asubuhi” alisema Said, “ok! mie ndio naingia hapa nyumbani, ukiweza njoo nyumbani kwangu michenzani, siunajuwa sasa hivi sina cha kuogopa, cha msingi njoo na bia” alisema Siwema, pasipo kujuwa anatafuta janga la kitaifa, “ok! nikikaribia nitakupigia” alisema Said na kukata simu.
Hakika Siwema alijihisi kuwa dunia inakuwa upande wake, maana aliona kila kitu kinamwendea vyema, ukizingatia Radhia anaenda kuwa chizi, alafu said anajileta mwenywe, “tena safari hii namwendea kwa Chongo yeye na baba Khadija, wakizubaa nitaishi nao wote wawili kama mume na mume mwenza” alijisemea Siwema, ambae asa alisha karibia nyumbani kwake.
Siwema anaingia ndani ya nyumba yake na weka mkoba juu ya meza, anaingia chumbani ambako anavua nguo zake na kuelekea bafuni, ambako anatumia nusu saa, akioga na kusafisha kiufasaha maeneo ya kitumbua, ambayo yalikuwa na mwezi aya jatumika, akiamini kuwa Said lazima ata kitumia kitumbua kile.
Siwema anatoka bafuni, na kujiweka sawa, kisha anavaa gauni jepesi na fupi bila nguo ya ndani, kisha ana elekea sebuleni, ambako anafungua mkoba wake, na kutoa chips na urojo, sambamba na mishikaki, anaanza kula huku anashushia pombe kari.
Wakati anaendelea kula na kunywa pombe yake, ambayo ilikuwa inamchangamsha kwa kasi, huku kigauni chake kikishindwa kufunika chungu, mala akasikia simu yake inaita, mpigaji akiwa Said, anaipokea haraka, huku anatabasamu, “vipi umesha fika?” anauliza Siwema. ......... ENDELEA…. KUFWATILIA HADITHI HII YA #ASALI_AITIWI_KIDOLE, HAPA HAPA
jamii forums