Simulizi - DYLAN

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★

Mwanaume huyo akasimama na kumtazama Dylan usoni kwa hasira.

"Unaingiaje kwenye chumba private bila kugonga hodi? Wewe ni mpumbavu?" mwanaume huyo akafoka tena.

Leila akaanza kuvaa T-shirt yake haraka haraka akiwa ameingiwa na hofu kubwa. Dylan akajifuta tena chozi taratibu na kumwangalia jamaa usoni.

"Samahani kaka...nime...nimekosea chumba," Dylan akamwambia kiupole.

"Unakoseaje chumba we mtu mzima bwana! Em' toka!" jamaa akasema kwa ukali.

Dylan akageuka ili aanze kuondoka, lakini Leila akamwahi na kumshika mkono.

"Ethan... Ethan... subiri... ona... nitakuelekeza... nitakueleza kila kitu..." Leila akawa anasema kwa hofu.

"We vipi? Nani huyu?" jamaa akamuuliza Leila.

Dylan akautoa mkono wa Leila kutoka kwenye wake, kisha akamwambia jamaa, "Samahani tena kuwaharibia muda wenu. Mnaweza kuendelea."

"Ethan nisikilize... Ethan!"

Leila akaishia kuita jina tu baada ya Dylan kuondoka humo. Akajishika kichwani na kuanza kulia, akamwachia jamaa anamshangaa.

"Una matatizo gani? Huyo mwanaume ni mtu wako eti?" jamaa akamuuliza Leila.

Leila hakumjibu hata kidogo na kuanza kuchukua vitu vyake ili aondoke kumwahi Dylan. Alishuka kwa kutumia ngazi kutoka jengoni hapo na kwenda mpaka nje akitafuta uwepo wa Ethan (Dylan), lakini hakumwona. Leila alichoka. Hakujua ni nini kingetokea baada ya hapo kwa sababu alitambua mambo yalikuwa yamevurugika haswa. Akabaki kutaharuki tu na kutafuta sehemu ya kukaa kwanza, kisha akaanza kumpigia simu Dylan, lakini hakupokea hata mara moja. Akaamua tu kuondoka hapo na kurudi nyumbani ili akaendelee kuigiza kwamba anaumwa.

★★★

Dylan alirudi mpaka jijini kwao, kule alikoishi na Grace, lakini hakwenda mpaka upande wao wa mji. Alikuwa anaendesha gari kwa mwendo wa taratibu sana, akiwa na huzuni nzito moyoni mwake. Simu yake iliita mara nyingi lakini hakujali kuangalia ni nani aliyepiga, kilichokuwepo akilini mwake ni picha ile aliyotoka kuiona hotelini kule. Ilijirudia mara nyingi kichwani kwake kumkumbusha kwamba Leila hakuwa mwanamke aliyemdhania kuwa hata kidogo. Ndiyo alikuwa na mapungufu yake, lakini hakutazamia kamwe kwamba angemtendea kwa njia hiyo, kwa sababu alijitahidi sana kumwonyesha upendo mwingi. Akaona aelekee sehemu ya starehe tu kwanza ili apige vileo kama vyote kupoteza mawazo, akiona hiyo ndiyo ingekuwa njia rahisi ya kuepukana nayo.

Alifika nje ya bar kubwa, iliyokuwa kama club pia, naye akaegesha gari hapo. Ilikuwa kwenye mida ya saa 2 na nusu hivi usiku, na bila kujali yeyote akaenda zake kule ndani mpaka sehemu ya bartender na kuagiza kinywaji. Kulikuwa na watu wengi kiasi wakijitumbuiza kwa vinywaji na muziki pia ndani hapo. Alikaa hapo mpaka inafika saa tatu akinywa kistaarabu tu huku akiwa amezama kwenye fikira za ni nini ambacho alipaswa kufanya sasa. Bado alimpenda Leila, lakini baada ya kumwona leo, ilikuwa ni kama asilimia zote za upendo aliokuwa nao kumwelekea zilipotea ghafla. Hakuhisi chochote kile tena zaidi ya majuto, na hii ilimvunja sana moyo.

"Hey, Ethan?"

Alisikia sauti hiyo ya mwanamke kutokea nyuma yake, na mkono wa mtu ukimshika mgongoni. Aligeuka na kukuta ni Sarah, yule rafiki yake Grace. Akatabasamu baada ya kumwona.

"Hey Sarah, what's up?" Dylan akasema.

"Poa tu."

Sarah akajibu hivyo na kumkumbatia Dylan (Ethan). Baada ya kumwachia na kumwangalia usoni, akatambua Dylan hakuwa sawa.

"Vipi my friend, mbona unaonekana... pale?" Sarah akamuuliza.

"Aahh...ni uchovu tu wa kazi. Ndiyo nimekuja kujichimbia huku mwenyewe," Dylan akasema kiutani.

"Aaaa... sawa. Nikafikiri umekuja na demu huku ama nini?"

"Ahahah... hapana. Na wewe je? Umekuja na jembe huku ama vipi?"

"Akha! Nilikuwa nimekuja na wakina Asia tu kujifurahisha. Sasa wakati tunataka kuondoka nimekuta gari langu lina pancha...halafu mbili kabisa."

"Mh! Wakati umefika halikuwa na hizo pancha?"

"Hamna! Yaani ni kama kuna mtu amefanya hivyo makusudi... nikimjua atanikoma," Sarah akasema.

"Pole sana. Kwa hiyo... unasubiria linatengenezwa au?"

"Eeee nimetafuta fundi ndiyo amekuja kwo' sina jinsi ila kusubiri. Halafu nilikuwa nataka niwahi pia."

"Si ungeondoka na Asia?"

"Yaani... wenyewe walitangulia. Mimi nilibaki hapa kwa sababu kuna mtu mwingine nilikuwa nakutana naye kumpa mzigo, kwa hiyo alivyoondoka na me ndiyo nikawa nataka kuondoka... nikakuta pancha."

"Ungechukua hata taxi. Gari lingemaliza kutengenezwa ungelifata baadae."

"Mh! Hapana. Mimi taxi siwezi. Halafu gari langu wanaweza hata kulichakachua ni bora nisubiri tu."

"Ahahahah... hawawezi bwana. Liache tu me nikupeleke maana umesema unahitaji kuwahi si ndiyo?"

"Mmmm... ndiyo lakini, idea ya kuliacha bado siioni kuwa sawa."

"Sarah kweli unataka kuniambia fundi wako hauwaamini au basi tu unajishaua?"

"Siyo kujishaua..."

"Nakujua vizuri wewe, ulikuwa tu unataka kuendelea kuenjoy huku kwo' hicho kikawa kisingizio kizuri ili Laurent asizingue...mmmm... sema," Dylan akauliza kichokozi.

"Ahahahah... hamna bwana. Ila... uko sahihi, nahitaji kuwahi, kwanza palikuwa pameshaniboa hapa. Kwa hiyo tuondoke sasa hivi?" Sarah akauliza.

"Ndiyo. Me mwenyewe nahitaji kuondoka maana nikilewa kuendesha itakuwa shida," Dylan akasema.

"Poa. Nisubirie hapa nakuja sasa hivi," Sarah akamwambia na kuelekea upande mwingine ndani hapo.

Dylan akasimama na kulipia kinywaji chake kwa bartender, naye akageuka nyuma na kutoa simu yake. Alikuta missed call nyingi kutoka kwa Leila, na ujumbe wake mwingi pia wa kumwomba waongee kwa kusema alichoona hakikuwa jinsi alivyofikiria. Dylan akatikisa kichwa kwa kusikitika sana. Alijiona mpumbavu kwa kiasi fulani kwa sababu kama isingekuwa ya Fred kumwambia jambo lile, mpaka sasa angekuwa anaendelea kufanywa kuwa mpenzi kipofu na Leila. Akampigia simu Baraka kumuuliza mambo yalikwendaje kwenye mechi. Baraka akamsimulia jinsi timu zilivyotoka suluhu ya magoli mawili mawili, na jinsi familia yake ilivyofurahia matembezi hayo na chakula kizuri. Baada ya kuagana naye, Dylan akairudisha tu simu mfukoni kwake.

Wakati akiwa amesimama bado akimsubiria Sarah, aliona jambo fulani lililovuta umakini wake. Kutokea upande mwingine wa bar hiyo, kulikuwa na watu wamechanganyikana wakijifurahishakwa kucheza muziki, na hapo akawa amemwona mwanamke fulani mzuri sana. Kulikuwa na wengi waliovutia ndani hapo, kutia ndani huyu aliyemwona, lakini ilikuwa ni kama sura yake haikuwa ngeni sana machoni kwa Dylan. Alipendezwa na tabasamu lake kila mara rafiki yake wa kike alipocheza karibu yake kwa furaha, naye angecheza pia kuendana na muziki.

Dylan akaendelea kumtazama tu, na kwa mpigo mmoja wa macho, mwanamke huyo akawa amemwangalia Dylan pia. Lakini akaacha kucheza na kumwangalia vizuri zaidi Dylan machoni. Dylan akaona akwepeshe tu macho yake na kuangalia upande ule alikoelekea Sarah, ila hakumwona. Wakati aliporudisha macho yake kwa mwanamke yule, alikuta bado anamwangalia tu, tena kwa njia fulani kama amezubaa. Dylan akabaki kumtazama pia asielewe kwa nini aliangaliwa kwa njia hiyo; ijapokuwa ni yeye ndiye alianza kumwangalia sana.

Ni hapa ndipo Sarah akawa amerejea na kumvuta mkono Dylan ili waondoke. Fikira zote juu ya mwanamke yule zikaishia hapo, naye Dylan akatoka na Sarah na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake Dylan. Alimpeleka Sarah mpaka kule alikohitaji, kisha yeye akageuka kuelekea nyumbani kwa Grace pia.

★★★

Dylan alikuja kufika nyumbani mida ya saa 5 usiku. Baada ya kuegesha gari, akaelekea ndani, akiwa bado amevunjwa moyo na kitendo alichotoka kumwona Leila amefanya kule hotelini. Hakumkuta Grace pale ndani, na baada ya Matilda kumuuliza kama angependa kupata chakula, Dylan akakanusha na kusema alikuwa ameshiba. Matilda akamwambia kwamba Grace alikuwa chumbani pia, hivyo Dylan akaanza kupanda kuelekea juu. Akafikiria aende kumsalimu Grace kabla ya kwenda kupumzika, hivyo akaelekea mpaka chumba chake kilipokuwa.

Wakati amefika mlangoni, alianza kusikia sauti ya Grace akiongea na mtu mwingine, bila shaka kwenye simu, kwa kuwa mlango wa chumba chake ulikuwa umeacha uwazi kidogo.

"....na haitakiwi kuwa hivyo kwa sababu ni mpaka Dylan aweze kujua kila kitu kwanza, ndiyo tutaweza ku-proceed na mpango huu. Ninachotaka kujua kutokana na hiyo info ni wapi hasa anapokuwa anatoa huo msaada, umeelewa Jafari? Kwa sababu ni muhimu tujue NANI anamsaidia so this doesn't just blew up in our faces, 'cause he'll still be one step ahead of us..."

Grace akawa anaendelea kuongea.

"Hapana, bado kumbukumbu yake haijarudi, na sitaki kukurupuka, kwa hiyo fanya ku-dive ndani zaidi ili tuwe full on EVERYTHING... na hapo ndiyo tutaweza kumwangusha chini huyo mpumbavu..."

Dylan alishangazwa sana na maneno yake. Huyo mtu ambaye Grace alikuwa anaongea naye kwenye simu hakumfahamu, lakini Grace alimweleza vitu kuhusu yeye ambavyo hata Dylan mwenyewe hakuwa na chembe ya ujuzi kuvielekea. Hii ilikuwa ni mara ya pili kumsikia Grace anatumia jina "Dylan" kumhusu yeye, na hakujua ni mpango gani aliokuwa anauzungumzia. Lakini haikuonekana kuwa jambo zuri kwake, na kwa sababu alitambua anahusika hapo, akataka kujua ni nini hasa kilichokuwa kinaendelea.

Baada ya Grace kushusha simu yake kutoka sikioni, Dylan akaufungua mlango na kuingia chumbani hapo. Grace alishtuka na kugeuka nyuma kutokea alipokuwa amesimama. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza Dylan kuingia kwenye chumba chake bila kupiga hodi, na kwa kumwangalia tu usoni, Grace alijua bila shaka kijana alikuwa amemsikia. Dylan akaanza kuelekea kwa Grace taratibu na kusimama mbele yake, huku anamwangalia kwa uso wa kawaida tu. Grace akatoa tabasamu bandia ili kuficha hisia zake za wasiwasi.

"Ethan... sikujua umerudi. Umetokea kule ulikoniambia ulienda?" Grace akauliza ili kuficha mambo.

"Ndiyo," Dylan akajibu huku anamtazama kwa makini.

"Okay. Aam... let's go down, nikuwekee something to eat... najua unahisi njaa, halafu mimi mwenyewe sijala bado... au ulikuwa umeshakula?" Grace akasema huku akianza kuondoka.

Dylan akaushika mkono wake mmoja na kumfanya asimame alipokuwa amefika tu nyuma yake. Mapigo ya moyo ya Grace yakaanza kukimbia kwa kasi.

"Haikuwa rahisi kwangu kuishi bila kujua kihalisi mimi ni nani. Kwa hiyo unaweza kuelewa kwamba... ilikuwa ngumu pia kuamini watu kwa kadiri fulani," Dylan akasema kwa sauti tulivu.

Hawakuwa wamegeukiana bado, lakini Dylan akaendelea kuushikilia mkono wake.

"Ila kwako wewe... sijui tu. Ilikuwa rahisi sana kukuamini kwa sababu... kwa sababu ambayo hata sielewi kiukweli, yaani, ninakuamini tu. Tafadhali niambie kwamba bado naweza kukuamini Grace..." Dylan akaongea kwa hisia.

Grece akafumba macho yake huku akizuia hisia nyingi sana. Dylan akamgeukia na kuugeuza mkono wake taratibu ili waangaliane. Grace alikuwa anamtazama kwa njia yenye wasiwasi kwa kiwango kikubwa, naye Dylan alitaka kujua ni kwa nini.

"I'm sorry, ni... ni ngumu sana..."

"Niko tayari kukusikiliza. Kwa hizi siku chache zilizopita nimetambua hauko sawa Grace. Na sasa unaongea vitu ambavyo vinaweza kutia shaka mtu yeyote. Sitaki niwe na shaka juu yako Grace, ninakuamini sana," Dylan akamwambia kwa upole.

Grace akawa anamwangalia machoni kwa hisia.

"Lakini nahitaji kujua nini kinaendelea...mpango gani huo unaouongelea? Wewe unataka kumwangusha nani, na kwa nini?" Dylan akamuuliza.

Grace akashusha pumzi huku anaangalia kuelekea chini, kisha akamwangalia tena Dylan machoni.

"Nililelewa kwenye familia ya kimasikini sana. Mama yangu...alikufa nilipokuwa na miaka mitano...akituacha mimi na dada yangu ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi...na baba yangu aliyekuwa mlevi kupindukia..." Grace akaanza kusimulia.

Dylan alijua bila shaka mambo ambayo Grace alikuwa ameanzisha kumwambia yangepelekea moja kwa moja kwa yeye kupata majibu, hivyo akaendelea kumsikiliza kwa makini.

".... Baba yetu hakujali ikiwa tunakula, tunavaa, masomo yanakwendaje...yeye ilikuwa ni pombe na wanawake tu. Ningeachwa kwa jirani kukaa mpaka muda ambao dada yangu angetoka shule ili niweze kurudi naye nyumbani. Niliishi kwa majirani kwa kusimangwa sana na ijapokuwa nilikuwa bado mdogo mno lakini nilielewa hilo. Baadae dada hakuweza kuendelea kusoma kwa kuwa baba aliacha kutoa hela kwa ajili yake, hivyo akarudi nyumbani tu na kuomba msaada ili awe anafanya kazi ndogondogo kwa ajili ya kupata pesa ya chakula. Alipitia hali nyingi ngumu sana, hivyo pamoja na umri wangu mdogo nikawa namsaidia, kama ni kumsaidia kutembeza maandazi, kuokota-okota mikaa ya kuuza, kufanya kitu chochote kile ambacho kingetusaidia, nilifanya..." akaendelea kusimulia huku akitokwa na machozi.

Dylan akamfuta machozi akimwonea huruma sana.

".... Siku moja dada yangu...akiwa anatembeza...maandazi...alikamatwa na wanaume fulani ambao walimbaka kwa zamu mpaka akafa! Alikuwa na miaka 12 tu!" Grace akasema huku machozi yakimtoka kwa huzuni nyingi aliyohisi.

Dylan aliumia sana. Grace alianza kulia kwa uchungu mwingi, hivyo Dylan akamkumbatia ili kumbembeleza. Bado hakujua haya yote yangeelekea wapi, lakini alijua simulizi hili lenye kusikitisha sana kutoka kwa Grace bila shaka lilikuwa limechangia uzito wa kile kilichokuwa kinaendelea. Akaketi pamoja naye kwenye kitanda akiwa amemshikilia, kisha akamfuta machozi kwa wororo huku anamtazama kwa kujali. Grace akawa anarudisha hali ya utulivu kutokana na kulia.

"Pole sana Grace..." Dylan akamfariji.

"Yaani kiukweli niliumia sana, lakini maumivu hayakuishia hapo. Baada ya kumzika dada, baba yangu alinichukua na kunipeleka kwa mwanamke wake mmoja. Mpaka kufikia kipindi hicho sikuwa nikisoma, na niliomba sana nipelekwe shule lakini sikukubaliwa. Niliishi kwa mwanamke wake kama..mfanyakazi fulani hivi... nililazimishwa kufanya kazi ngumu ambazo hazikuendana na umri wangu. Ilifikia hatua nikawa hadi nazimia kutokana na kulemewa na uchovu mwingi, lakini hawakujali hilo. Baada ya muda fulani... ni kama baba aliona jinsi navyoteseka, kwa hiyo akanitoa hapo ili nikakae kwa mtu mwingine ambaye hata sikumjua. Aliniacha kwake na kusema angerudi, lakini hakurudi tena. Baadae nilikuja kujua kwamba aliniuza kwa mwanaume huyo kwa pesa ndogo sana..." Grace akaendelea kusimulia.

"Oh my God!" Dylan akasikitika sana.

"...ahah... yaani ni kama nilikuwa bidhaa tu kwake. Mwanaume huyo niliyeuzwa kwake alikuwa mwenye pesa, naye alikuwa anajihusisha na biashara za wanawake waliouzwa kwa watu wenye pesa kwa ajili ya kujinufaisha. Wakati huo nilikuwa na miaka 15, nilikuwa mdogo, niliogopa sana, sikufanya mambo kwa njia aliyotaka yeye na hakujali umri wangu. Kwa hiyo akanipeleka kwenye nyumba yake ili niwe kama mtumwa wake. Alinitendea kwa ukatili, alinilazimisha kufanya naye mapenzi... kwa kuniumiza sana... sikujua nilipokuwa, sikujua wa kumwomba msaada, yaani..." Grace akaongea huku analia na kujifunika uso kwa mikono yake.

Dylan akaanza kutokwa na machozi pia, lakini akayafuta haraka na kuanza kumbembeleza kwa kuusugua mgongo wake kwa wororo.

"....nyumba yake ililindwa na watu walioonekana kuwa wakatili kama yeye tu. Kuna wakati alikuwa akitoka na hasira zake huko nje, anarudi na kuzimalizia kwangu kwa kunipiga au kunitendea vibaya kimwili. Nilichoka sana. Kuna siku nikajaribu kuchukua simu yake na kupigia mtu yeyote ili nipate msaada, lakini akajua. Aliniambia kwamba kwa sababu nimefanya hivyo, angehakikisha hakuna mwanaume yeyote yule ambaye angetaka kuja kuwa nami kamwe. Kwa hiyo... akanikamata na kunipiga sana... akachukua pasi ya umeme yenye moto mkali.... mgongo wangu...." Grace akashindwa kuendelea na kuanza kulia tena.

Dylan alisononeka sana kiasi kwamba hakuweza kuyazuia machozi yake tena. Grace akamtazama Dylan huku machozi mengi yakiwa yanatiririkia mashavuni mwake.

"....nililetewa daktari hapo hapo ambaye alisisitiza nipelekwe hospitali, lakini wale watu wakamtisha anipe tiba hapo hapo la sivyo wangemfanyia jambo baya. Kwa siku nyingi baadae hali yangu ikawa nafuu zaidi, lakini nilijua alinipa tiba tu ili niendelee kuwa mtumwa wake hapo, kwa hiyo nikafikiria njia ya kutoroka, na nikafanikiwa. Walinitafuta sana wakihofia nilikuwa nimeenda polisi labda, lakini haikuwa hivyo. Wakati nakimbia ilikuwa usiku na nikajikuta nadumbukia mtaroni kwa sababu ya kutoona gizani. Nilipoteza fahamu na kuja kujikuta hospital nikipatiwa matibabu... na aliyenisaidia alikuwa mwanaume fulani mwenye umri mkubwa sana. Baada ya kupata nafuu... akanipeleka kwake... yaani kwenye hii nyumba..."

"Oooh... okay..."

"....yeah, akanitunza hapa, yeye na mke wake... na wote walikuwa ni wazungu. Aliitwa Smith, na alikuwa ndiyo mwenye kampuni hii. Nilimweleza kila jambo lililonipata, na kufikia wakati huo nilikuwa nina miaka 16, na bado sikuwa nimewahi kukanyaga shule hata mara moja. Kwa hiyo, akanisomesha, nje ya nchi, mpaka nilipomaliza elimu aliyonichagulia. Mke wake alikufa miaka miwili baada ya mimi kurudi huku, na nilikuwa nimeshaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake Smith. Kwa kuwa umri wake ulikuwa mkubwa sana, hakutaka kufa akijua angeiacha kampuni bila mrithi, kwa sababu hakuwa na watoto, na yeye alikuwa amejitenga na familia yake ya kiukoo. Kwa hiyo... akanioa," Grace akaeleza.

Dylan akaendelea kumsikiliza kwa makini.

"Alijua angeweza kuniamini kwenye suala la kuitunza na kuikuza zaidi kampuni yake. Nafikiri yeye ndiyo mwanaume wa kwanza kunitendea kwa njia nzuri sana, hata aliponioa, aliendelea kunionyesha heshima kama binti yake... kwa hiyo nilimuahidi nisingemwangusha katika hilo. Alikuwa ana uvimbe kichwani uliomsumbua kwa muda mrefu ijapokuwa alijaribu kuutibu; kwa kufanyiwa upasuaji... lakini hali hiyo iliendelea kumsumbua tu na hakutaka watu waijue. Mwaka mmoja baada ya kuwa amenioa... he passed away... akiacha kila kitu huku mikononi mwangu. Bado kumbukumbu zote za mambo mengi mabaya niliyopitia maishani zilikuwepo, nami nilikuwa nimeazimia kumtafuta yule mwanaume ili nimlipe kwa mambo yote aliyonifanyia..." Grace akasema kwa hisia kali.

Dylan akamtazama kwa uelewa sana. Alijua bila shaka mwanamke huyu alihisi maumivu sana moyoni, lakini bado hakuwa na uhakika Grace alitaka kulipiza kisasi kwa njia gani.

"Grace... hakuna maneno yoyote yatakayotosha kukueleza ni jinsi gani nilivyoumia na yote uliyosema. Umepitia hali nyingi ngumu sana... haukustahili kabisa kutendewa namna hiyo..." Dylan akamwambia kwa hisia za huruma.

Grace akaanza kudondosha machozi tena, kisha akasema kwa njia yenye hasira, "Nitahakikisha yeye pamoja na wote waliohusika kuyafanya maisha yangu yawe kama kuzimu wanaanguka. Ninajua Mungu amewaacha waendelee kuishi ili nije niwaonyeshe ni nini maana ya mateso."

Dylan aliiona vyema hasira ya Grace usoni mwake. Bila shaka alikuwa akipanga mambo yenye kuumiza sana kwa ajili ya watu wote aliowaona kuwa wabaya wake, na kitu hicho kilimfanya awe mwenye kuogopesha.

"Grace..." Dylan akamwita kiupole.

Grace akawa anatazama tu mbele huku anapumua kwa hasira.

"...najua una maumivu. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuelewa hilo vizuri zaidi yako, kwa sababu ni wewe ndiyo ulipitia hali hizo zenye kuumiza sana. Lakini... kulipiza kisasi hakuta..."

"No!"

Grace akamkatisha huku anamwangalia machoni kwa hisia kali. Dylan akatulia tu.

"You have no idea what those bastards made me go through! Walinitendea kama mnyama... yule mwanaume mpumbavu alikuwa ananinyima chakula kwa siku nyingi, kisha angenipa chakula alichokikanyaga kwa miguu yake na kukitemea mate ili nile!" akasema Grace kwa mkazo sana, huku machozi yakiwa yanamtiririka.

Dylan akamwonea huruma sana.

"Alinifanyia vitu ambavyo sidhani ikiwa mama yake au dada yake angefanyiwa angemwacha salama mtu aliyemfanyia hivyo. Huwezi kuniambia nisimlipe kwa yote aliyoyafanya!" akasema kwa sauti ya juu sana.

Dylan akatazama chini kwa huzuni. Pumzi za Grace zilikuwa zinatetemeka kwa hasira aliyohisi, hivyo akajitahidi kujituliza kiasi.

"Mimi kama wanawake wengine... nilikuwa nina ndoto zangu. Nili... nilitaka... nilitaka kuwa na familia... nilitaka kuwa na boyfriend... kama wasichana wenzangu. Lakini alinifanya nikawa nawaona wanaume kama wanyama tu... yeye na baba. Ni nani angetaka kuwa nami baada kujua mambo haya yote? Nisingeweza kuficha hata kidogo! Wameniharibia maisha yangu Ethan.... siwezi kuwaacha," akasema Grace kwa uhakika huku akilia.

Dylan akawa anakaribia kutokwa na machozi tena huku anamwangalia Grace kwa simanzi, naye Grace akaanza kujifuta machozi kwa njia ya kujikaza na kuonyesha yuko imara. Simu yake Grace ilianza kuita, naye akaichukua kutoka pembeni kwenye kitanda alipoiweka muda ule wameketi hapo. Baada ya kuona ni yule mwanaume aliyekuwa anaongea naye muda mfupi uliopita, yaani Jafari, akageukia upande wa pembeni na kupokea ili amsikilize.

Dylan akawa anamtazama kwa hisia nyingi sana. Alikumbukia wakati ule alipomwambia kwamba aache kujibana sana na atafute mwanaume mzuri maana anazeeka, na ijapokuwa alimwambia kiutani tu, sasa akawa ametambua kuwa maneno yake yalimuumiza sana mwanamke huyu. Alihitaji kupendwa pia, lakini hali zake alizopitia zilifanya ajione kuwa hafai kama mwanamke wa kawaida, naye Dylan alitaka kumwonyesha kwamba hilo halikuwa kweli.

Wakati Grace alipokuwa akiongea na simu, alikuwa amempa mgongo Dylan, naye Dylan akawa anamwangalia kwa nyuma akitathimini mwili wake. Grace alikuwa amevaa gauni nyeupe yenye kubana mwili kuanzia juu mpaka magotini mwake, na kama kawaida, sikuzote nguo zake ziliuficha mgongo wake. Dylan akaanza kuupeleka mkono wake polepole kuelekea sehemu ya bega la Grace iliyokuwa wazi, naye akaigusa taratibu kwa wororo sana.

Grace alihisi kiganja cha Dylan kilipomgusa, naye akajikaza asigeuke, bila kuelewa Dylan alikuwa anataka kufanya nini. Dylan alikuwa anamwangalia kwa hisia za upendo ambazo zilikuwa zimeshajengeka siku nyingi, naye akaanza kukishusha kiganja chake taratibu kuelekea chini kwenye mkono wa Grace. Mwanamke huyu alisisimka sana, na mkono wake uliokuwa umeweka simu sikioni ukashuka taratibu bila kuwa amemaliza kuongea na Jafari.

Mwili wa Grace ulikuwa katika hali yenye kumtia hofu, na wasiwasi kwa wakati mmoja. Dylan alilielewa hilo vizuri, lakini alitaka Grace ajue kwamba hakuwa na sababu ya kuogopa, kwa kuwa sasa alimwelewa vizuri. Akaishika zipu ya gauni kwa nyuma karibu na shingo ya Grace, kisha polepole akaanza kuishusha chini. Pumzi za Grace zilipanda, akawa anahema juu juu huku ameachama mdomo kama anajaribu kusema kitu fulani lakini akawa anashindwa.

Dylan akaishusha zipu mpaka usawa wa kiuno chake, kisha kwa mikono yake yote akaliachanisha gauni hilo kutokea katikati. Grace alifumba macho huku machozi yakiwa yanamtoka, akijua wazi kwamba Dylan aliweza kuona jambo ambalo hakutaka mtu yeyote alione kamwe. Dylan aliutazama mgongo wa Grace kwa simanzi sana. Ulikuwa na alama nyingi za kukatwa na vitu kama visu, alama nyingi nyeusi za vidonda vya kuunguzwa na pasi, na mikwaruzo mingi iliyotuna kwenye mbavu zake kuelekea chini.

Grace akawa analia kwa sauti ya chini. Dylan pia, kwa simanzi kubwa aliyohisi, alitokwa na machozi. Akaanza kutembeza kidole chake akizigusa alama hizo, huku Grace akijiona kama kitu chenye kutia kinyaa, na akifikiri Dylan angemwona kama kitu kisichofaa. Lakini mawazo hayo hayakuwa sahihi, na Dylan alitaka Grace alitambue hilo.

Mwanaume akapeleka mdomo wake polepole mpaka mgongoni kwake Grace, naye akambusu kwa wororo sana.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)


★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★★


Grace akafumbua macho yake kwa kutotegemea jambo hilo, na hisia nyingi zikaanza kujengekea mwilini mwake; hisia ambazo kwa miaka mingi hakuwa amewahi kuwa nazo. Dylan akaibusu tena sehemu ya bega lake kwa wororo, naye Grace akashtuka kiasi baada ya kuhisi msisimko. Hakuwa amefikiria kwamba Dylan angeweza kufanya hivyo, na kwa sababu alikuwa mwanamke wa malengo tu, haingekuwa rahisi kwa yeyote kufanya kitu cha namna hiyo mwilini mwake na yeye amwachie tu; kwa sababu hakuwa hata na muda wa kuwazia jambo hili.

Lakini ni kama Dylan alimfanya ajihisi tofauti... udhaifu fulani hivi. Sikuzote Grace alikuwa mwanamke imara na thabiti, asiyependa michezo ya kitoto na yeyote kabisa. Lakini kwa huyu kijana ambaye alikuwa ametoka kumsimulia kuhusu maumivu yake, ilionekana kwamba alikuwa na aina fulani ya upendezi kumwelekea ambao ungempa ruhusa kijana huyu kufanya kitendo hicho.

Dylan naye hakujua kihalisi ikiwa jambo hili lingempendeza mwanamke huyo, lakini yeye sikuzote alifata moyo wake, na moyo wake wakati huu ulimwambia amwonyeshe Grace kwamba anapendwa. Akaanza kuubusu mgongo wa Grace hapa na pale kwa wororo sana, naye Grace akawa anasikilizia jinsi midomo ya Dylan ilivyompatia hisia zenye kusisimua. Kuna sehemu ya akili yake ilikuwa inataka kumwambia Dylan aache, lakini alilegea sana na kushindwa kujua kwa nini alikuwa tu hata amemwachia aifungue zipu; sembuse kuubusu mgongo wake!

Dylan akaanza kuishusha chini sehemu ya gauni iliyokuwa begani taratibu kuelekea chini kidogo kwenye mkono wake Grace. Grace alisisimka sana, naye akawa amekunja sura kwa hisia za kimahaba asijue la kufanya. Kusema kweli alikuwa akiogopa pia, kwa kuwa alifikiri wanaume wengi wangemtendea kwa njia ile ile kama yule aliyemnunua, hivyo hata kwa Dylan alihisi woga. Lakini njia ya Dylan ya kufanya mambo ilikuwa bila papara, na angalau jambo hili ni kama liliutuliza woga wake kwa kadiri fulani.

Dylan akaibusu sehemu ya bega lake Grace, kisha akaanza kupandisha taratibu kuelekea shingoni. Grace alifumba macho huku midomo yake ikitetemeka kwa mbali kutokana na hisia nyingi alizopata, naye Dylan akaendelea kuibusu shingo yake kwa upendo sana. Grace akageuka nyuma taratibu, na sasa midomo yao ikawa karibu sana huku wanatazamana kwa hisia. Hisia zilizokuwa zimempanda Grace zilimfanya awe na mzuka mwingi, naye akawa anapumua kwa kutetemeka sana.

"Its okay... its okay... I got you..." Dylan akamwambia kwa sauti yenye kubembeleza ili kumtuliza.

Grace akajitahidi kutuliza hisia zake za juu, naye Dylan akatabasamu kidogo na kuushika uso wake kwa kiganja chake. (.......).

(........).

(........).

(........).

(........).

Ijapokuwa kweli mgongo wa Grace uliwekewa makovu ya maisha, hii haikuwa sababu kwa Dylan kumwona hafai, na mpaka kufikia hatua hii alikuwa amemthibitishiahilo, na angeendelea kuthibitisha.

(........).

(........).

(........).

(........).

Dylan alijua alikuwa akishughulika na mwanamke ambaye alipitia maumivu ya kimwili zamani, na ambaye tokea wakati huo hakuwahi kujihusisha tena na mapenzi. Hivyo kwa njia fulani angepaswa kumtendea kama... bikra... ahakikishe anamrudishia hali ya kawaida ya kimahaba kwa uangalifu.

(........).

Grace alihisi maumivu, kama msichana kwa mara yake ya kwanza, na hii ilieleweka kwa kuwa hakuwahi kufanya tena mapenzi na mtu yeyote tokea alipotibiwa na Smith alipokuwa na miaka 16; hiyo ikimaanisha alikaa miaka 18 mpaka leo ndiyo akaweza kujiachia kwa Dylan kimapenzi. (.......).

(........).

(........).

(........).

Ilionekana wazi sasa kwamba Dylan alikuwa anamfurahisha mwanamke huyu. Dylan alifarijika sana kuona kwamba hatimaye Grace aliondoa hofu aliyohisi kwa miaka mingi kuelekea jambo hili, na sasa alichohisi kilikuwa ni raha badala yake. Dylan hakuvunja moyo hata kidogo kwenye kutoa mapenzi.

(.........).

(.........).

(.........).

Dylan pia alikuwa amezama kwenye raha nyingi aliyohisi kutoka kwa mwanamke huyu, hadi akawa amesahau mambo yenye kuvunja moyo aliyopitia siku hiyo. Hata alipohisi matambi yake yanakaribia kutoka, hakutaka kuacha kwa kuwa alihitaji raha hiyo iendelee tu. Kisha, baada ya kufikia mahala pazuri, Dylan alijiachia ndani kabisa kwa Grace.

Grace alipumua kwa uchovu sana, huku akiwa amelegea kitandani hapo. Dylan akamwangalia kwa sekunde kadhaa, akiona kuwa kweli mwanamke alikuwa ametua zigo zito la kipindi kirefu. Akambusu kwa wororo sana shavuni, na kuelekea mdomoni, huku Grace bado akiwa amefumba macho yake, kisha akambusu mdomoni na kuanza kuinyonya kwa upendo. Akaichomoa mashine yake taratibu kutoka kitoweoni mwa bibie na kumfanya agune kwa pumzi ya chini.

Ilikuwa ni kama wamechukua muda wa milele kumaliza safari ya mahaba yao, kwa sababu walipeana penzi kistaarabu na kihisia sana. Dylan aliona fahari kumsaidia Grace aondoe hofu yake, naye Grace hakuwa akiamini kama kweli aliweza kupita kwenye sehemu hiyo tena ambayo hakutaka kamwe kuipita. Alihisi usalama na imani kubwa kumwelekea Dylan.

Kutokana na mridhiko na uchovu aliohisi, Grace hakusema lolote ila kujilaza tu hapo kitandani akiwa amefumba macho. Dylan aliendelea kumbusu hapa na pale, huku akicheza na sehemu za mwili wake kwa kutumia vidole. Baada ya dakika chache, Dylan akatambua kuwa usingizi ulikuwa unamjia Grace, hivyo akasogeza shuka na kuufunika mwili wake. Grace akajigeuza kivivu upande mwingine ili aweze kusinzia vizuri, na kumwacha Dylan anautazama mgongo wake kwa huruma.

Kweli mwanaume huyo aliyemnunua kutoka kwa baba yake alikuwa amemfanyia mambo mengi mabaya sana ambayo hakuna msichana yeyote anastahili kufanyiwa. Alijua hata kama ingekuwa ni yeye, asingefikiria kuacha kulipiza kisasi, kama alivyotaka kumshauri Grace muda ule hajauona mgongo wake bado. Akajisogeza na kujiingiza ndani ya shuka, kisha akaukumbatia mwili wa Grace kwa nyuma na kulala miili yao ikiwa imegusana. Akaibusu shingo yake kwa nyuma, kisha naye akaanza kuutafuta usingizi pia.

★★★

Asubuhi ya saa mbili ilipofika siku iliyofuata, Grace akafumbua macho yake taratibu kutoka usingizini. Fikira za haraka zikaingia kwenye akili yake na kukumbuka jinsi alivyopeana mapenzi matamu na kijana Dylan usiku uliopita. Akaachia tabasamu la mbali na kugeukia upande wa pili wa kitanda, kukuta Dylan hayupo kitandani. Akajiuliza yuko wapi, na kwa haraka akakisia huenda Dylan alikuwa amekwishaamka na kuelekea kazini akimwacha yeye amelala.

Akajinyanyua kivivu na kuketi vizuri kitandani, akianza kujishika mwilini mwake huku akikumbukia kila mguso wa Dylan. Angetabasamu huku akiwa amefumba macho kwa kuvuta hisia nzuri alizopata jana kutoka kwa mwanaume huyo.

"Good morning sunshine."

Akatazama upande wa mlangoni baada ya kuisikia sauti hiyo. Ilikuwa ni Dylan, akiwa amesimama hapo huku ameshikilia sahani pana yenye vyakula mbalimbali na chai, huku anamwangalia Grace kwa tabasamu la furaha. Grace akatabasamu kwa mbali pia huku anamtazama Dylan kwa hisia. Kisha jamaa akaanza kuelekea hapo alipoketi bibie na kuiweka sahani hiyo kitandani katikati yao.

"Breakfast in bed... kama wazungu," Dylan akasema.

Grace akatabasamu na kusema, "Asante."

Hakufanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kumwangalia tu Dylan, hivyo jamaa akachukua yai kidogo na kumwekea mdomoni ili ale. Grace alijihisi vizuri sana kwa kuwa Dylan alimtendea kwa njia yenye upendo. Akala, naye Dylan akaendelea kumlisha taratibu.

"Mbona wewe hauli?" Grace akamuuliza.

"Msosi wa jana usiku ulikuwa mtamu mno. Bado nimeshiba," Dylan akasema kichokozi.

Grace akatabasamu kwa haya kiasi na kutazama chini. Dylan akatabasamu pia, akifurahia jinsi ma-dimple yalivyochoreka kwenye mashavu ya Grace. Akaendelea kumlisha bibie mpaka aliposema kwamba inatosha, naye Dylan akamwambia ajitoe kitandani ili akajisafishe, kisha angemkuta kule chini. Grace akakubali, naye Dylan akabeba vitu alivyokuja navyo na kurudi navyo kule chini jikoni.

Grace akatoka kitandani na kuelekea bafuni ili ajisafishe. Baada ya kusafisha kinywa, akaingia 'shower' na kuanza kujimwagia maji. Wakati akiendelea kujiogesha, akahisi mikono ikimgusa kwenye mbavu zake na kumfanya ashtuke sana.

"Its okay... ni mimi."

Dylan akamtuliza kwa kumwambia hivyo. Grace akatulia kiasi, huku sasa akihisi jinsi mwili wa Dylan, ambao haukuwa na nguo, ukimgusa na kuubana wake kwa nyuma. Dylan akaanza (........).

(..........).

(..........).

(..........).

(..........).

Raha aliyopata Grace ilimfanya ajihisi ni kama hakuwa na matatizo kwa wakati huo, naye alitaka sana waendelee na mapenzi yao matamu licha ya mambo mengi waliyohitaji kushughulika nayo. Baada ya kutoka bafuni, walielekea kitandani na kuendeleza penzi lao murua; Grace akimwachia Dylan autawale mchezo wote na yeye aipate tu raha ambayo hakufikiria angewahi kuja kuifurahia namna hii.

Dakika kadhaa baadae wote walijiachia na kumwaga misisimko yao kwa pamoja, kisha wakajisafisha tena na kuanza kuvaa. Dylan aliwahi kutoka chumbani, akimwacha Grace anajiandaa, maana wanawake hutumia muda mrefu zaidi. Akashuka mpaka kule chini na kukaa kumsubiri Malkia wake mpya ashuke ili waweze kuondoka pamoja.

Grace alishuka kutoka juu ya ngazi taratibu baada ya dakika kadhaa, akiwa anaongea na Jafari kwenye simu. Alikuwa amevaa blauzi nyekundu ya kitambaa na suruali yake pana, na miguuni alivaa viatu vyeupe virefu, huku nywele zake akizitengeneza kwa mtindo wa kuzilaza mpaka kufikia mgongoni. Usoni alikuwa amependeza sana kwa kupaka lipstick nyekundu mdomoni na kuyaremba macho yake mazuri.

Baada ya kufika mwisho wa ngazi, akamalizia maongezi yake na Jafari, kisha akakata simu na kuangalia upande wa masofa sehemu ya sebule ile pana. Akamwona Dylan hapo akiwa ameketi huku anamwangalia kwa hisia. Jamaa akatabasamu kidogo kumwelekea, naye bibie akaachia tabasamu la upendo pia. Dylan akanyanyuka na kumfata Grace mpaka aliposimama.

"Umependeza mrembo," akamwambia.

"Asante," Grace akajibu huku anatabasamu.

"Ofisini?" Dylan akauliza.

"Yeah."

"Unajua... bado kuna mambo mengi tunahitaji kuzungumzia, siyo?"

"I know. Twende kazini, then we'll talk later. I'll tell you everything you wanna know (twende kazini kisha tutaongea baadae. Nitakueleza kila kitu unachotaka kujua)," Grace akamwambia.

Dylan akatikisa kichwa kukubali.

Kisha Grace akamwita Matilda ili kumwachia maelekezo fulani. Baada ya kumaliza, akakishika kiganja cha Dylan na kuvibana vidole vyao kwa pamoja, huku akimwangalia Dylan kwa upendo. Dylan akatabasamu, kisha wakatoka pamoja kuelekea nje ili wachukue gari na kuelekea kwenye kampuni.

★★★★★

"...bado tuko huku kwa nini? Kwa sababu tumekaa tu bila kufanya lolote!" Jaquelin akafoka kwa hasira.

"Jaquelin... kuna mambo mengine tunayoweza kukazia fikira na kujitahidi kuyakuza zaidi ili yatupe faida angalau kwa wakati huu," Gilbert akamwambia kwa upole.

"Mambo gani? Unataka tuendelee kutegemea restaurant hiyo ya kipumbavu wakati tuna kampuni kubwa ambayo WEWE umeipoteza? Huo haukuwa mpango wetu Gilbert... ulikuwa mpango wa Dylan. Kwa hiyo umeridhika kabisa sasa unajifanya kama maisha yako poa tu... wakati kila kitu umepoteza?!" Jaquelin akaendelea kulalamika.

Mambo hayakuwa yakienda shwari upande wa wazazi wake Dylan. Ilionekana kuwa sasa kampuni waliipoteza kabisa baada ya Mr. Bernard kutambuliwa kuwa raisi mpya wa kampuni hiyo miezi michache iliyopita. Hawakujua ni kwa nini mambo mengi waliyofanya ili kurudisha haki yao yalishindikana,lakini ni Mr. Bernard pamoja na MTU yule aliyeshirikiana naye ndiyo waliohusika kuhakikisha wanamkandamiza Gilbert ili apoteze kila kitu.

Mgahawa wa Dylan uliendeshwa vyema, lakini Jaquelin hakutosheka kabisa na mambo aliyoyaona kuwa madogo madogo sana waliyopata kutoka hapo. Alikuwa amepoteza uhusiano mzuri pamoja na marafiki zake wa zamani ambao walimtenga baada ya yeye kushuka kipesa; isipokuwa labda Beatrice, ambaye alimsaidia mara kwa mara vitu fulani na ushauri pia kama rafiki.

Gilbert alikuwa amewaza kuwa waendeleze biashara hiyo ya mgahawa, na kadiri ambavyo siku zingepita, wangetumia faida wanayopata kuukuza zaidi na hata kuifanya iwe hoteli kubwa. Alikuwa na matumaini sana kwamba jambo hili lingefanikiwa, lakini kwenye masikio ya Jaquelin ilikuwa ni kama kumpigia kelele zilizomuumiza. Ndiyo sababu iliyofanya mzozo huu kutokea wakati wako nyumbani.

"....kuna maisha mengine Jaquelin, usifikiri kwamba kuwa na pesa nyingi ndiyo kila kitu. Nilikwambia tupunguze gharama za matumizi ili tuishi maisha rahisi, lakini unang'ang'ania kuishi maisha kama hayo tuliyokuwa nayo. Hakukuwa hata na uhitaji wa kuwa na msaidizi wa kazi hapa, tungezifanya weny..."

"Unasema? Yaani nianze kujiumiza mimi mwenyewe kwa sababu tu wewe umefeli kurekebisha mambo? Hakuna kitu chochote kilichobaki tena, najua, lakini siwezi kuanza kuishi maisha ya kitumwa!"

"Hakuna kitu kingine kilichobaki? Jaquelin kwa nini unakosa shukrani?"

"Shukrani gani? Maisha gani haya umefanya tuanze kuishi? Miaka yote hiyo ya kazi ngumu kuijenga kampuni kuwa ilivyo leo eti imepotea ndani ya dakika mbili tu. Unafikiri Dylan angekuwepo angekuonaje?"

"Jaquelin funga mdomo wako."

"Ahah... ukweli unauma eeh? Umejitahidi sana kuweka mambo sawa hata aliporudi huku, lakini bado umeishia kuanguka..."

"Jaquelin nimesema funga mdomo wako! Usimwingize Dylan kwenye haya..."

"...bila shaka kama angekuwa hai angekuona kama baba yako tu... you are a failure! Umeshindwa kuongoza kampuni, baba yako kakugeuzia mgongo, familia ikavurugika kwa sababu ya..."

"Usiongelee masuala ya mimi kuku-cheat! Unajua wazi kwamba ni WEWE ndiye ulisababisha hilo! Usiigeuzie hatia yako mwenyewe kwangu, kwa sababu ijapokuwa unanidharau, bado sikukuacha... na hata kama nilifanya makosa, nilijitahidi kurekebisha hali lakini ni wewe ndiyo ukaendelea kuleta matatizo!"

Maneno hayo ya mwisho ya Gilbert aliyasema kwa hasira sana, naye Jaquelin akawa anamwangalia kwa hasira pia huku machozi yakimtoka. Walikuwa chumbani kwao wakiongea hivi kwa hisia zilizovurugika, naye Gilbert akatoka chumbani hapo kwa hasira na kushuka chini. Bado walikuwa wakiishi kwenye ile nyumba ya Dylan ambayo Gilbert alimrithisha, na mambo mengi hayakuwa yakienda vizuri tokea "kifo" cha mwanao.

Gilbert akaenda mpaka kwenye friji na kutoa maji kisha kunywa ili atulize hisia zake, huku msaidizi wao wa kazi akiwa hapo jikoni anaandaa chakula. Jaquelin akatoka chumbani ili amfate Gilbert waendelee kuongea, maana hakuwa amemalizana naye. Ni wakati alipofika sebuleni, pale mlango wa geti la nje uliposikika ukigongwa; kuonyesha kulikuwa na mtu nje aliyetaka kuja ndani.

Dada wa kazi akahakikisha kwamba mambo yako sawa ili aende kufungua, lakini Gilbert akamwambia angeenda kufungua yeye mwenyewe. Akampita Jaquelin bila kumwangalia wala kumsemesha na kwenda nje moja kwa moja. Jaquelin alimkata jicho la ukali sana, naye akaamua kutoka mlangoni aweze kuona ni nani alikuwa anagonga getini wakati huu kwa kuwa kulikuwa na giza nje na tayari ilikuwa imetimia saa 2 usiku. Gilbert alipoufungua mlango mdogo wa geti, aliachia tabasamu dogo kwa kuwa aliyesimama hapo alimfahamu.

"Fetty... hujambo?" akamwambia.

"Sijambo. Shikamoo?" Fetty akamsalimu.

"Marahaba. Karibu sana. Za huko kwenye harusi? Ndiyo umerudi leo?" Gilbert akasema.

Uso wa Fetty ulionyesha wasiwasi ambao ulimtaarifu Gilbert kwamba mambo hayakuwa sawa kwa binti huyo.

"Vipi Fetty? Kila kitu kiko sawa?" Gilbert akauliza.

"Yaani sijui nisemeje..." Fetty akajibu kwa kuonyesha wasiwasi.

Gilbert akaona amkaribishe ndani ili waweze kuongea vizuri. Fetty akamkuta Jaquelin akiwa amesimama mlangoni na kumsalimia, kisha wote wakaingia ndani. Walipofika usawa wa masofa, Gilbert akamwomba Fetty aketi, lakini binti akaendelea kusimama tu akionyesha hofu fulani usoni.

"Una tatizo gani? Mbona hukai?" Jaquelin akamuuliza.

"Kuna jambo fulani nahitaji kuwaambia... yaani sielewi imekuwaje..." Fetty akasema huku anafikicha viganja vyake kwa wasiwasi.

Gilbert na Jaquelin wakaangaliana, kisha wakamtazama tena Fetty.

"Ni jambo gani hilo?" Gilbert akauliza kwa upole.

Fetty akawa anataka kusema lakini anababaika tu.

"Ongea basi, una shida gani?" Jaquelin akamshurutisha.

"Nimemuona Dylan!" Fetty akasema.

Gilbert alibaki kumwangalia tu usoni asielewe anamaanisha nini. Jaquelin akakunja sura kimaswali huku pumzi zake zikianza kuongezeka kasi.

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★

"Nimemuona Dylan jana." Fetty akarudia tena.

"Unamaanisha nini?" Jaquelin akauliza.

"Nimemuona sehemu fulani... alikuwa na mtu mwingine... yaani..."

"Wewe!" Jaquelin akamkatisha.

Fetty akamtazama kwa woga.

"Una kichaa eti?" Jaquelin akasema.

"Jacky..." Gilbert akataka kumzuia.

"Nini? Huyu binti ana matatizo gani? Umemuona Dylan wapi wakati unajua sehemu pekee aliyopo ni huko chini?" Jaquelin akasema kwa hisia.

"Hapana, nimemuona kweli! Nisingekuja hapa kuwaambia jambo kama hili... najua siyo utani huu. Lakini nina uhakika nimemuona... ninajua ilikuwa ni yeye..." Fetty akasema huku machozi yanamtoka.

Wazazi wote wa Dylan walishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Wakabaki kumtazama Fetty kwa kushangazwa na kile alichosema.

"F..Fetty una... una uhakika na unachokisema?" Gilbert akamuuliza.

Fetty akatikisa kichwa chake kukubali.

Jaquelin akaanza kutokwa na machozi huku anapumua kwa kasi. Hakuweza kuamini kama kweli jambo hili lilikuwa kweli.

"Umemwona wapi?" Gilbert akamuuliza.

"...nilikuwa na Patricia... rafiki yangu... tulienda kwenye bar fulani kubwa... tulipokuwa tumetoka kwenye sherehe... ni kama club... nikamuona hapo..." maneno ya Fetty yakatoka kwa kubabaika.

"Alikuwaje? Uliongea naye?"

"Si... sikuweza. Nilikuwa nashangaa kumwona... na yeye akaniangalia sana... lakini kuna mtu akamvuta mkono na wote wakaondoka. Nilipowafatilia nikaona... nikaona wanaingia kwenye gari halafu... wakaondoka... sijui walielekea wapi..."

Jaquelin akakaa kwenye sofa kwa kuishiwa nguvu. Gilbert akachuchumaa kumwelekea Jaquelin ili amwangalie kama yuko sawa. Alikuwa amechoka.

"Gilbert.... Dylan yuko hai! Yuko hai!" akasema Jaquelin kwa shauku yenye huzuni huku analia.

Gilbert akamkumbatia Jaquelin ili kumtuliza. Fetty alikuwa amesimama hapo pembeni akilia pia.

Baada ya Jaquelin kutulia kidogo, akamwomba Fetty awaeleze tena jinsi mambo yalivyokuwa, naye akafanya hivyo. Walitafakari sana ni nini ambacho kingekuwa kimetokea siku ile Dylan kapanda helicopter, lakini hawakuweza kupata jibu sahihi. Ndipo hapa Fetty akakumbuka kuhusu Mr. Bernard. Alimsikia akiongelea kuhusu mpango fulani wa kumwangusha Gilbert, na ungefanyika muda ule ule ambao Dylan alitakiwa kupanda helicopter. Gilbert na Jaquelin wote walishangaa kujua ukweli huu ambao Fetty hakuweza kuwaambia kutokana na majanga mengi yaliyotokea.

"Mshenzi mkubwa yule! Bila shaka ni yeye ndiye amesababisha mambo yote yale kutokea!" Jaquelin akasema kwa hasira.

"Kwa hiyo alisema mwisho wangu umekaribia... ndiyo maana akajaribu kumuua mwanangu!" Gilbert akasema kwa hisia za huzuni sana.

"Kwa nini hukutuambia mapema?" Jaquelin akamfokea Fetty.

"Sikuwa naelewa... nilitaka kumwambia Dylan lakini akawahi..."

"Usijali Fetty... Jaquelin... mtoto hana makosa... mambo mengi yalituvunja sisi sote..." Gilbert akasema.

"Ndiyo! Na ni kwa sababu ya huyo mpumbavu! Ngoja nimfate..."

Jaquelin akanyanyuka ili aondoke, lakini Gilbert akamwahi na kumzuia kwa kuushika mwili wake.

"Jacky.. Jacky... nisikilize..."

"Gilbert niachie... nimesema niache!"

"Tulia!" Gilbert akamfokea kwa sauti kubwa mno.

Jaquelin akatulia na kumwangalia usoni.

"Unataka kufanya nini? Uende ili na wewe akuue?" Gilbert akamuuliza.

"Ikiwa ataniua ni sawa tu... si ndo' mpango wake? Amuue Dylan... basi na mimi..."

"Hiyo siyo akili Jaquelin!" Gilbert akamkatisha.

Jaquelin akatulia.

"Tumetoka tu kujua mtoto wetu yuko hai... kitu cha kwanza kabisa cha kutanguliza inapaswa kuwa yeye," Gilbert akasema kwa hisia.

Jaquelin akaanza kulia kwa uchungu sana. Gilbert akaushika uso wake kwa upendo ili watazamane.

"Jaquelin... unahitaji kuwa strong kama jinsi navyokufahamu ili tuweze kumshinda adui yetu. Ni wazi kabisa kwamba kila kitu kilichotupata haikuwa coincidence... ilipangwa. Kwa hiyo tunahitaji kufanya kila jambo kwa akili sana... kwa sababu hawa watu ni wakatili, wanaweza kufanya lolote lile kutimiza haja zao. Hatupaswi kuhatarisha usalama wetu na... na usalama wa Dylan kwa mara nyingine tena..." Gilbert akamweleza kwa upole.

Jaquelin akaishika mikono ya Gilbert usoni mwake huku akimwangalia kwa hisia.

"...kwa hiyo tufanye nini?" akamuuliza mume wake.

Gilbert akamwangalia Fetty, ambaye alikuwa akiwatazama kwa simanzi wazazi hao wa Dylan, kisha akamwangalia Jaquelin tena.

"Tumtafute mwana wetu," Gilbert akamwambia kwa uhakika.

Jaquelin akatikisa kichwa kukubali, naye Gilbert akamkumbatia kwa ajili ya faraja.

Wenzi hawa hawakujua kilichofanya Dylan asirudi nyumbani au kuwatafuta mpaka wakati huu, lakini walikuwa na matumaini hakika moyoni kwamba wangeungana na mwanao tena ili waweze kujipanga kupambana na maadui zao.

★★★

Grace akawa ameketi pamoja na Dylan kitandani chumbani kwake, akimwambia kuhusu kila jambo alilohitaji kujua kuhusu mipango yake ya kisasi. Dylan alimsikiliza kwa makini na kupata kutambua ukweli muhimu ambao hakujua wala kukumbuka.

"Dylan ndiyo jina langu?" akauliza.

"Ndiyo. Jina lako halisi ni Dylan Gilbert," Grace akajibu.

"Kwa hiyo... muda wote huu ulikuwa unafahamu mimi ni nani... kwa nini hukuniambia?"

Grace akawa kimya tu akimwangalia Dylan kwa hisia.

"Grace nieleze. Nahitaji kujua ninahusika vipi kwenye mpango ulio nao mpaka ukaamua kunifichia jambo hili," Dylan akamsihi kwa upole.

"Well... ukweli ni kwamba... haukuwa sehemu ya mipango yangu mpaka miezi michache iliyopita. Kitu kilichosababisha upoteze kumbukumbu ni kwamba... ulipata ajali ya helicopter. Inaonekana ulianguka na kuumia mpaka kupoteza kumbukumbu yako, lakini watu waliokufahamu walifikiri umekufa. Ijapokuwa wengi waliiona kuwa accident, mimi nilifanya uchunguzi zaidi na kutambua kwamba haikuwa accident..." Grace akaeleza.

Dylan alikuwa ameshangazwa na ufunuo huu. Maswali yaliyopita kichwani kwake yalikuwa mengi mpaka akashindwa kujua aulize lipi aache lipi. Ni hapa ndipo Grace akachukua simu yake na kuanza kutafuta picha fulani. Dylan alikuwa anamwangalia kwa makini sana, naye Grace alipopata picha aliyoitaka, akampa Dylan simu aitazame.

Dylan alipoiangalia, aliona mwanaume fulani mwenye umri mkubwa akiwa amevaa suti na akitoa tabasamu kubwa. Lakini aliutazama sana uso wake, na hii ilikuwa ni kwa sababu alihisi kama anamfahamu.

"Looks familiar... doesn't he?" Grace akasema.

Dylan akauliza, "Ni nani huyu?"

"Huyo ndiyo yule mwanaume aliyenitendea kwa ukatili kipindi kile. Anaitwa Yakobo Bernard Sizwe. Wengi humfahamu kama Mr. Bernard," Grace akajibu.

"Mr....Bernard?" Dylan akauliza, akiwa kama analifahamu jina hilo.

"Yeah. Mnafahamiana. Amefanya kazi kama investor mkubwa kwenye kampuni ambayo ilikuwa ya baba yako, na sasa ameikwapua kutoka kwa baba yako na kuifanya iwe yake kwa sababu ya tamaa yake kutaka kuwa in control. Nimemfatilia kwa kitambo sasa, na ninajua hangeweza kufanya jambo hilo yeye mwenyewe; kuna mtu anamsaidia," Grace akaeleza.

Dylan alichanganyikiwa. Mambo ambayo Grace alikuwa akimtaarifu yalikuwa mengi mno kuweza kuyameza yote akilini kwa wakati mmoja.

"Anajihusisha na mambo mengi illegal: madawa ya kulevya, magendo, human trafficking, na ulaghai wa hali ya juu ambao umesababishia wengi matatizo. Kwa miezi michache iliyopita nilijitahidi kufichua maovu yake, kwa njia isiyo ya moja kwa moja, lakini kuna mtu fulani yuko nyuma yake ambaye anahakikisha Mr. Bernard hafikiwi na udhuru anaostahili. Nikiweza tu kujua mtu huyu ni nani, basi nita-attack haraka iwezekanavyo," akasema Grace.

Dylan akakaa kimya kwa sekunde chache, kisha akamuuliza, "Ulijuaje kwamba... kilichonipata hakikuwa accident?"

"Kama nilivyokwambia, nimekuwa nikimfatilia mwanaume huyo tokea Smith alipokufa. Mwanzoni, sikujua jinsi ya kutafuta vigezo vya kunisaidia ili nimwangushe, hivyo nikaamua ku-hire private investigator... jina lake ni Jafari. Alinisaidia kujua kuhusiana na operation za huyo mtu zilizofanywa kwa usiri wa hali ya juu, na mara kwa mara alikuwa anabadilisha njia zake za kufanya mambo yake mengi mabaya. Hivyo nikaamua kuweka focus kwenye kampuni yenu pia, na hasa kwa sababu ilikuwa inafanya kazi kama ya kwangu tu. Jafari alikuja kunipatia info baadae kuwa Mr. Bernard alikuwa anapanga kumwangusha Gilbert, baba yako, lakini hakujua ni jinsi gani angefanya hivyo."

Dylan akaendelea kumsikiliza.

"Nilikuja kutazama taarifa ya habari baada ya helicopter uliyopanda kuanguka, na hapo nikawa nimetambua huo ulikuwa ni sehemu ya mpango wake, kwa sababu inaonekana alihofia uwepo wako pale ulikuwa unairudisha nyuma mipango yake. Kwa hiyo nikamwamuru Jafari afatilie zaidi kuhusiana na kisa cha helicopter hiyo, na baadae akaja kuniambia kuwa inaonekana kuna tatizo lilitokea mkiwa huko huko juu. Jafari alipata taarifa baadae kuhusu parachute iliyoangukia maeneo fulani, kwa hiyo akaenda kuchunguza huko. Alikuja kupata wallet yako ambayo nafikiri ilidondokea sehemu fulani wakati unaanguka, na baada ya kuniletea, tukaanza kufatilia zaidi ikiwa uli-survive. Ndiyo miezi michache baadae Jafari akanitaarifu kuhusu habari zako za kujenga lile daraja, na alipokufatilia akatambua ilikuwa ni wewe, yaani Dylan."

Dylan akatulia kidogo, kisha akauliza, "Kwa hiyo kumbe ulipo...nitafuta, haukuwa na lengo la kunisaidia tu kimaisha... ila ulinifata kwa lengo la kunifanya niwe sehemu ya mipango yako?"

"I'm sorry Dylan... najua hii yote inakuumiza. Lakini kutoka ndani ya moyo wangu, nilitaka kukusaidia na kukulinda ili uwe salama; maana kama wale watu wangejua ulikuwa hai, wangekutafuta kukumaliza. Nilikuwa ninafahamu mambo kadhaa kukuhusu... na mengi yalikuwa kuhusu jinsi ulivyo mwerevu na jasiri. Kwa hiyo nilitaka kukufunulia kila jambo polepole ili uwe upande wangu... kwa pamoja tuweze kumwangusha huyo mpumbavu," Grace akajieleza.

Dylan akashusha pumzi na kusema, "Usijali, Grace. Kiukweli, haya yote yamenichanganya sana.... I feel so... lost. Lakini ijapokuwa bado sikumbuki mambo mengi, angalau sasa siko gizani. Kwa hiyo... mpaka sasa... wazazi wangu.... na kila mtu anayenifahamu huko... wanafikiri nimekufa, siyo?"

Grace akatikisa kichwa taratibu kukubali.

Dylan akatikisa kichwa kwa kusikitika sana, naye akanyanyuka na kuelekea upande wa dirishani na kutazama nje. Grace alikuwa anamwangalia kwa hisia za huruma, kwa kuwa alielewa mambo mengi yalimchanganya mpenzi wake huyo mpya. Yeye pia akanyanyuka na kumsogelea Dylan karibu akiwa nyuma yake, kisha akamshika begani kwa kujali.

"Mr. Bernard..." Dylan akasema kwa sauti yenye mkazo.

Grace akawa anamwangalia kwa kujali.

"Tamaa... tamaa ni kitu kibaya sana. Ni watu kama yeye ndiyo wanaosababisha maisha ya wengine yaharibike bila haki. Anaua... analaghai... anawatendea watu kama wanyama... halafu anafurahia maisha mazuri...."

Dylan aliyasema hayo yote kwa hisia nzito sana. Kisha akamgeukia Grace na kumwangalia machoni.

"I'm in!" akasema kwa hisia kali sana.

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Gilbert yupo calm sana, anaishi na mwanamke asiye mvumilivu kabisa na asiyejali kuumiza hisia za mumewe.

Hongera sana mtunzi kwa simulizi kali
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★

Zilipita siku mbili baada ya Grace kumweleza Dylan ukweli huo wote. Sasa walikuwa pamoja nyumbani usiku, wakiwa na Jafari, ambaye aliitwa na Grace ili waongelee kuhusiana na mipango yao. Ni hapa ndipo Dylan alipata kujua kuwa Jafari ndiye yule mwanaume aliyekuwa akimwona mara kwa mara akimfatilia kule alikoishi kwa Baraka. Ndiyo huyu aliyemwona kipindi kile saluni, kwenye mechi, na akitokea hapo nyumbani kwa Grace. Alikuwa mpelelezi wake wa kibinafsi ambaye pia alitaka sana kufichua uovu mwingi wa Mr. Bernard.

Jafari alikuwa akieleza mambo mengi ambayo alipata kufahamu kutokana na uchunguzi alioufanya, naye Dylan akawa anapitia baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa kama ushahidi wa yale waliyoyaona kuwa ni matendo ya hila kutoka kwa Mr. Bernard. Wote walikuwa wameketi kwenye viti ndani ya ofisi ya Grace ya nyumbani, wakijadiliana na kupanga mambo mengi vizuri kwa kuwa sasa timu yao ilikamilika.

"....uliungua sana ndiyo sababu haikuwezekana kujua mwili ule ulikuwa ni wa nani. Wakauzika wakifikiri ni wako," Jafari akawa anamweleza Dylan.

"Advantage kubwa tuliyonayo ni kifo chako. Hawawezi kuona nini kinakuja ikiwa hawajui ni nani anakuja... ndiyo maana wewe ni wa muhimu sana kwenye hili Dylan," Grace akasema.

Dylan alikuwa anaangalia baadhi ya picha za helicopter ile iliyoanguka, ambazo Jafari alichukua wakati ule anafanyia uchunguzi.

"Boss... umesubiri kwa muda mrefu sana... na najua una uwezo mkubwa wa kumshusha Bernard chini. Kwa nini bado unasubiri?" Jafari akamuuliza Grace.

"Ni muhimu tujue kwanza nani yuko nyuma ya mgongo wake. Na pia ni kwa sababu maumivu nayotaka kumpa siyo kumshusha tu ki-mali... ila kumfanya ahisi maumivu yote aliyonifanya nipitie," Grace akajibu kwa hisia yenye mkazo.

"Usijali, Grace. Tutahakikisha anayapata," Dylan akasema kwa uhakika.

Grace akashusha pumzi kutulia.

"Walisema chanzo ni nini cha helicopter kuanguka?" Dylan akamuuliza Jafari.

"Kwamba iliishiwa fuel kwa hiyo ikapoteza mwelekeo na kuanguka," Jafari akajibu.

"Ni uwongo tu," Grace akasema.

"Ndiyo. Fuel kuisha siyo jambo lililofanya ianguke, kwa sababu inaonekana tatizo lilipotokea bado helicopter iliendelea kukaa juu kwa muda mrefu, bila shaka pilot akijaribu kuirudisha kwenye control," Jafari akaeleza.

"Story mbovu sana ku-cover jambo zito namna hiyo. Kweli... waseme tu eti fuel iliisha... ina maana wenye hiyo helicopter hawana mafunzo kujua mapema mambo yanayohitajika kabla chombo hakijapanda juu?" Grace akasema.

Dylan akazitazama picha tena, kisha akamwangalia Jafari na kuuliza, "Uliweza kuipata CVR?"

Jafari alishangazwa kidogo na swali la Dylan.

"CVR ndiyo nini?" Grace akauliza.

"Aam... ni ufupisho wa Cockpit Voice Recorder; kifaa fulani cha kurekodi sauti ndani ya helicopter. Umejuaje kuhusu hilo?" Jafari akaeleza na kumuuliza Dylan hivyo.

"Sijui... yaani sikumbuki lakini... najua tu kwamba najua," Dylan akasema.

Jafari akatabasamu na kusema, "Okay. Ninacho hapa."

Akakitoa kwenye boksi ambalo alikuja nalo lililokuwa na vifaa vingi vya upelelezi wake. Simu ya Dylan ikaanza kuita. Ilikuwa mezani, kwa hiyo yeye pamoja na Grace waliweza kuona jina la aliyepiga, naye alikuwa Leila. Dylan akamtazama Grace machoni, naye Grace akamwangalia pia. Kisha Dylan akakata na kuipotezea kabisa.

"Uliwaibia?" Dylan akauliza kiutani.

"Chochote kwa ajili ya boss," Jafari akajibu kiutani pia.

Dylan akatabasamu na kukichukua.

"Hiki kifaa huwa useful sana hasa kwa ma-investigatorwanaochunguza helicopter zilizoanguka. Nilihitaji kutumia resource nyingi ili nikichukue, lakini kila kitu alichosema rubani humo hakikunisaidia kujua nini hasa lilikuwa tatizo, ijapokuwa inaonekana tatizo hilo ni kitu ambacho hakuweza ku-solve," Jafari akamwelezea Grace.

Dylan akakiwasha, na wote wakaanza kusikiliza maneno ya mwisho ya rubani ya kuomba msaada wakati chombo kilipoanza kuleta shida mpaka kuanguka. Grace hakuona ulazima wala umuhimu wa kusikiliza mambo hayo, lakini akamwacha tu Dylan afanye utafiti wake ili aone kama angegundua kitu. Baada ya Dylan kuwa amesikiliza kwa makini, akaizima na kumtazama Jafari.

"Ni rotor," akasema kwa uhakika.

"Nini?" Grace akauliza.

"Yaani... kuna kifaa kinaitwa rotor ambacho huwa kinapokea nguvu kutoka kwenye engine ndani ya helicopter. Ndege za kawaida huwa zina redundancy kwenye vifaa muhimu ndani yake, na huwa zinasaidia flight control ili kama system moja ikifeli, basi nyingine inachukua nafasi ili kuisaidia ndege. Helicopter mara nyingi HAINA redundancy kwenye vifaa vyake muhimu. Ndege ya kawaida inaweza kupoteza engine moja na bado ikaendelea kwenda angani, lakini helicopter haingeweza. Nafikiri engineer aliyeishughulikia alifanya kui-crack kwa njia fulani ili baada ya muda ikiwa angani ipoteze mwelekeo," Dylan akaeleza kwa njia iliyomfanya Jafari astaajabu sana kuhusu ujuzi wake.

"Kimakusudi, si ndiyo?" Grace akamuuliza Dylan.

"Ndiyo," Dylan akajibu.

"Kwa hiyo tutumie vipi jambo hilo?" Jafari akauliza.

"Tutapaswa kujua helicopter ilitokea wapi na ni nani aliyeishughulikia tofauti na rubani aliyekufa. Mtu huyo ndiye aliyepewa maagizo ya kuifanya ifeli. Tukimpata na kuthibitisha kupitia yeye kuwa Mr. Bernard alihusika, huo utakuwa sehemu ya mwanzo mzuri wa kumwangusha mwanaume huyo," Dylan akasema.

Simu ya Dylan ikaanza kuita tena. Ilikuwa ni Leila kwa mara nyingine tena, naye Dylan akakata na kumwangalia Jafari.

"Nafikiri sehemu nzuri ya kuanzia ni kule helicopter ilikotokea asubuhi ile," Dylan akamwambia Jafari.

"Ndiyo... nitachunguza hilo. Boss, una jambo lingine la kuongeza?" Jafari akauliza.

"For now hapana. Just... give me updates on that if you get anything (utanipa taarifa za mapema ukipata chochote)," Grace akasema.

Jafari akakubali, kisha akakusanya vitu vyake na kuwaaga. Walikuwa wamemsihi akae ili apate chakula, lakini akawashukuru na kusema alikuwa anawahi sehemu nyingine. Hivyo akaondoka na kuwaacha wawili hao ofisini humo. Wakabaki wakiangaliana kwa sekunde kadhaa, kisha Grace akanyanyuka na kusogea mpaka usawa wa kiti alichokalia Dylan na kuanza kutembeza vidole vyake kwenye nywele zake.

"Twende tukapate chakula," akasema kwa sauti yenye kubembeleza.

Dylan akatabasamu na kusimama, kisha akamwangalia usoni kwa ukaribu sana na kutikisa kichwa kukubali. Grace akaondoka ofisini hapo, huku akimwacha Dylan anawaza bila shaka huenda Grace alihisi vibaya baada ya kuona Leila anampigia simu. Yeye pia akatoka ofisini humo na kuelekea sebuleni. Walikula pamoja mezani, kisha baadae Grace akarudi ndani ya ofisi yake ili apangilie mambo yake.

Dylan alielekea chumbani kwake, akitafakari mambo kadhaa kuhusu maisha yake. Alijiona kuwa kama mtu aliyepotea katikati ya msitu mkubwa, bila kujua aelekee wapi kwa sababu sehemu nyingi zilikuwa hatari. Lakini hakufa moyo; akaamua kuendelea kuwa imara kwa ajili ya yale ambayo yeye na Grace walidhamiria kufanya.

Baada ya masaa mawili hivi, Grace akawa chumbani kwake tayari, akiwa amesimama usawa wa dirisha pana la chumba hicho, akimtafakari Dylan. Hisia zake kumwelekea zilikuwa zenye nguvu kufikia wakati huu, lakini bado moyoni mwake alikosa amani kwa kufikiria uwezekano wa Dylan kuendelea kutoka kimapenzi na Leila. Dylan alikuwa amemfanya aijue raha ya kupenda, hivyo hangetaka kuwazia hata kidogo kumpoteza kijana huyo kwa mwanamke mwingine.

Ni wakati akiendelea kuwaza, pale Dylan alipoingia chumbani kwake na kusimama umbali mfupi kutokea aliposimama Grace. Grace alijua Dylan alikuwa nyuma yake, lakini hakugeuka. Dylan akawa anamwangalia kwa upendo, jinsi 'night dress' yenye kung'aa aliyovaa ilivyoupendezesha mwili wake ulionawiri vyema.

"Mbona bado hujalala?" Dylan akauliza kwa sauti ya chini.

"Usingizi haunitaki," Grace akajibu.

Dylan akatabasamu na kumsogelea karibu zaidi.

"Umeongea na Leila?" Grace akauliza.

"Ndiyo."

"And?"

"Alikuwa... anaomba samahani... anataka nimsamehe na tukutane ili tuongee vizuri," Dylan akasema.

Grace akakwazika kiasi. Dylan tayari alikuwa amekwishamwambia kuhusu usaliti wa Leila, kwa hiyo alijua vizuri mwanamke yule alihitaji msamaha wa nini.

"Kwa hiyo umeamuaje?" akauliza.

"Wewe unafikiri nimeamuaje?" Dylan akamuuliza pia.

"Nitajuaje sasa? Ni wewe ndiyo mwenye maamuzi. Najua... unampenda... kwa hiyo..." Grace akasema kwa njia ya kuvunjika moyo.

Dylan akawa ameelewa hilo. Akatabasamu na kusogea mpaka nyuma yake na kuizungushia mikono yake kiunoni mwa Grace. Grace akasisimka na kufumba macho yake, huku Dylan akiwa ameweka kichwa chake nyuma ya kichwa cha Grace.

"Kujua kwamba nimeongea na Leila kumekufanya uone wivu eti?" Dylan akauliza kiutani.

"Wivu? Unanitania?" Grace akakanusha.

"Aaah come on... usikatae, kubali tu nijue."

"Hakuna kitu kama hicho. Ukitaka m...mrudiane... ni wewe tu, me siwezi kuku..."

Kabla Grace hajamailiza kuongea, Dylan akamgeuza na kuanza kumpiga denda kwa wororo sana. Kama kawaida ya Grace, alilegea na kuanza kurudisha pigo za jamaa kwa upendo, akiunyonya ulimi wake kwa raha zote. Kisha Dylan akaiachia midomo yake taratibu na kumtazama machoni akiwa ameushika uso wake.

"Usiogope Grace.... mimi ni wako sasa," akamwambia kwa hisia.

Grace akatabasamu kwa hisia, akifurahia kujua kuwa Dylan alikuwa wa kwake peke yake. Akaifata midomo ya mwanaume wake sasa na kuendelea kudendeshana naye, akimwonyesha dhahiri kuwa alifurahia penzi lake. Dylan kama kawaida hakukwaza; aliendelea kuinyonya midomo ya bibie kimahaba huku mikono yake ikiishusha mikanda myepesi ya night dress aliyovaa Grace. (.......).

(........).

Haikuchukua muda mrefu hata kidogo, na wote wakawa mawinguni kihisia, wakionyeshana mapenzi ya dhati kwa vitendo vingi. Dylan alimpeleka Grace kitandani na hapo akahakikisha anapiga show ya kibabe mpaka Grace akatosheka. Wote walipitiwa na usingizi baada ya karibia masaa mawili ya kupeana malavidavi pamoja kitandani hapo.

★★★

Siku zilizofuata zilikuwa ni siku zenye ubize mwingi wa kimipango ya kazi na kisasi cha wawili wale ambao sasa walikuwa wapendanao; Grace na Dylan. Dylan alisoma kila kitu kuhusu kampuni ya baba yake na kupata kujua mambo mengi kuihusu. Kama Grace alivyomwambia, jambo kuu lilikuwa kupanga kila jambo vyema na kutambua anayemsaidia Mr. Bernard ni nani hasa, ili waweze kupiga hatua yao kwa usahihi. Dylan aliongeza mambo kadhaa kwenye mipango ya Grace kwa kutoa mawazo ya nyendo zitakazofaa zaidi ili kumwangusha Mr. Bernard na kumfichua msaidizi wake.

Upande wa wazazi wake Dylan, walikuwa wakiendelea kupambana kurudisha nafasi zao kwenye kampuni, huku wakitafuta mambo yatakayowasaidia kuweza kumpata Dylan kimya kimya. Gilbert alikazia mara kwa mara kwa Jaquelin kuwa hakupaswa kumwambia YEYOTE kuhusiana na jambo hilo, kwa sababu alifikiria bila shaka Dylan alikuwa na maana yake kutojitokeza kwao mapema.

Jaquelin alikuwa na hamu sana ya kumwona mwanae tena, hivyo wakati mwingine angehisi kukosa subira kwa kuwa bado hawakuweza kujua Dylan yuko wapi. Fetty alienda mara kwa mara kwenye club ile nje ya jiji lao ili kuona kama Dylan angefika tena, lakini aliambulia kuvunjika tu moyo. Ila hakukata tamaa. Aliamini kutoka moyoni mwake kuwa angemwona tena mwanaume huyo aliyekuwa ameanza kumpenda kwa dhati muda mfupi kabla ya taarifa za "kifo" chake.

Kwake Jafari, mambo yalipamba moto. Aliweza kumpata mwanaume yule ambaye alihusika pamoja na rubani wa helicopter katika udumishaji mzuri wa chombo hicho. Alimfatilia na kujua alikuwa mwanaume aliyeitwa Pius, mtu mzima mwenye miaka 54, ambaye alikuwa amesomea masuala ya vyombo vya angani na alifanya kazi kama mekanika wa vifaa vikubwa vya ndege.

Jafari alipopata nafasi ya kumbana na kumhoji kuhusu yeye kuihujumu helicopter ile (sabotage), mwanaume huyo alipinga vikali na kumwambia asimsumbue tena. Lakini Jafari alimhakikishia kuwa ushahidi anao kutoka kwenye kifaa cha kurekodi maneno ya rubani, ambayo yalionyesha kuwa kweli kuna 'sabotage' ilifanywa ambayo rubani huyo mzungu hakuitambua kwa sababu mwanaume huyu ndiye aliyeshughulikia eneo hilo la chombo.

Jafari akahusisha jina la Mr. Bernard pia, na hapo akaona jinsi mwanaume huyo alivyotangatanga kuonyesha dhahiri kwamba kuna jambo alificha. Ikabidi Jafari amwambie kuwa angempatia pesa nyingi zaidi ya pesa alizopatiwa na Mr. Bernard kwa ajili ya jambo lile ikiwa atasema ukweli, lakini Pius akakanusha na kusema haelewi lolote Jafari analosema. Pius akamkwepa Jafari na kuondoka eneo walilokuwepo ili asiendelee kumhoji tena, hivyo Jafari akawataarifu Grace na Dylan kuhusu yaliyojiri upande wake. Aliwaambia aliona bila shaka Pius kuna jambo alificha, na asingeishia hapo kumshawishi mpaka aseme ukweli.

Pius aliwasiliana na Mr. Bernard baada ya kumkimbia Jafari, kumjulisha kuwa kuna mtu alikuwa anafatilia jambo hilo ambalo alihusika kumsaidia. Ikawa wazi sasa kwamba, kweli Mr. Bernard alimlipa Pius aikwamishe rotor ya helicopter kitaalamu siku ile Dylan alipotumiwa helicopter hiyo. Kwa kuwa mpango wao ulifanikiwa, na wote walifikiri kwamba Dylan na wengine waliokuwemo mule walikufa, suala hili la mtu kumpeleleza Pius lilimshangaza Mr. Bernard. Alijiuliza ni nani ambaye angetaka kufufua jambo hilo kwa wakati huu; na kwa nini. Akamwambia Pius awe makini zaidi na akimwona tena mpelelezi huyo basi amjulishe haraka sana ili ashughulike naye.

Mr. Bernard akamjulisha jambo hili MTU yule ambaye amekuwa akimsaidia ili kuyaharibu maisha ya Gilbert na Jaquelin. Yeye pia hakuwa na wazo la ni nani ambaye alitaka kujua ukweli, lakini alitambua muda si mrefu jambo hili lingeweza kuzua tatizo kubwa. Hivyo akawa anaitengenezea akili yake mipango mingi zaidi ya kushughulika na hali hii, bila kumwambia Mr. Bernard lolote zaidi tu ya kumsihi awe mwangalifu zaidi. Hivyo, Mr. Bernard akamwambia Pius ahame eneo aliloishi haraka sana, na pale Jafari alipomtafuta kwa mara nyingine, akashangazwa kujua mwanaume huyo alitoroka na kuiacha familia yake. Kwa hiyo akafanya mpango wa kuendelea kumtafuta mpaka ampate tena; na zamu hii kingeeleweka.

Wakati hayo yakiendelea, Dylan alikuwa anafanya baadhi ya mipango yao yeye na Grace kuanza kazi. Kwa akili ya hali ya juu, alifichua siri nyingi za utendaji wa mambo haramu ya Mr. Bernard ambayo alijitahidi kuficha kwa siri kwa muda mrefu.

Mr. Bernard alifanya biashara nyingi haramu zilizohusisha uuzaji wa bidhaa ambazo zilikuwa zimeibiwa, kisha yeye angezibadili kwa njia ya kificho kupitia majengo yake ya biashara zisizo haramu ili kutovuta umakini wa vyombo vya usalama, na kuviingiza sokoni kwa bei nzuri tu. Kwa sababu Mr. Bernard alitenda kama mwasilishi wa kati baina ya wale waliomletea bidhaa zilizoibiwa na wateja ambao wangezinunua, aliwekeza pesa nyingi kwenye suala hili ambalo kwa muda mrefu lilimpatia faida. Zamani alihusika kwenye biashara ya watoto na wanawake kwa kuwaiba au kuwanunua na kuwauza kwa wenye pesa, lakini kwa wakati huu alikazia fikira zaidi magendo.

Kwa hiyo Dylan alipofanikisha kufichua kazi hizi haramu, ilikuwa ni jambo lililompiga Mr. Bernard kwa kishindo sana. Sehemu kadhaa zilizoendesha biashara hizo zilikamatwa na kukomeshwa. Lakini kwa sababu Mr. Bernard alikuwa amesafisha jina lake kupitia kazi rasmi kwenye kampuni ya Gilbert, hangeweza kutambuliwa kirahisi kwamba yeye ndiye aliongoza biashara hizo, kwa sababu pia hakutaka kujionyesha wazi kwa waliohusika nazo. Lakini mambo haya yalimpa hasara kubwa sana kwa sababu bidhaa nyingi za magendo zilipotaifishwa na kuteketezwa na mapolisi, ilimwacha bila pesa ya kuweza kugharamia potezo hilo.

Kwa kuharakisha mambo, akatumia pesa nyingi zilizowekezwa ndani ya kampuni ya Gilbert kujaribu kulipia makosa yake, na sasa kampuni ikaanza kutenda kwa njia mbovu sana baada ya hisa kushuka na kuporomoka kimapato. Ilikuwa ni kama ndoto kwake jinsi mambo yalivyobadilika upesi. Alipomwomba msaada MTU wake yule, alimwambia kwenye suala hilo angepaswa kushughulika nalo yeye mwenyewe kwa kuwa kwenye hilo hakuhusika; ilikuwa mzigo wa Mr. Bernard peke yake. Kampuni kuanza kuporomoka kidogo kidogo kuliwafanya washiriki wengi wa bodi ya kampuni wajiulize shida ilikuwa nini mpaka kusababisha hisa zao zilike, bila kutambua ni kiongozi waliyemchagua ndiye aliyechakachua.

Jambo hilo lilikuwa ndiyo lengo la Grace na Dylan. Walijua bila shaka Mr. Bernard angefanya kila awezalo kutafuta suluhisho, hivyo wao ndiyo wangekuwa suluhisho hilo. Mpango wa Grace ulikuwa kununua hisa ZOTE za kampuni ya Gilbert, ili iwe chini yake, kwa kuwa pesa ndefu alikuwa nayo. Hivyo wawili hawa walitumia mwakilishi aongee na kumshawishi Mr. Bernard kwa niaba yao kuwa kuna mwekezaji mkubwa aliyetaka kununua hisa hizo ili kuiinua kampuni zaidi kwa kuiwekezea pesa nyingi pia.

Mr. Bernard aliongea na washiriki wa bodi ili kuwashawishi, ambao nao pia waliona ni bora kukubali kwa kuwa mambo kweli yalikuwa yakienda vibaya. Alipoulizwa ikiwa alimjua mnunuzi, alisema ndiyo anamfahamu, na kwamba anajua ni mtu mwenye pesa na ana kampuni kubwa zilizoendelea hivyo angekuwa msaada mkubwa kwa kampuni yao pia.

Yote haya Mr. Bernard aliyafanya kwa papara kwa sababu alikuwa anahitaji suluhisho la haraka, hivyo hangeweza kutambua kwamba alijiingiza kwenye mtego ambao ungeyabadili kabisa maisha yake.

★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★

Jafari alifanikiwa kumpata Pius, yule mwanaume aliyemkimbia ili asiendelee kupelelezwa kuhusiana na ajali ile ya helicopter. Jafari aliweza kutambua kwamba Pius alifanya ionekane kama amekimbilia sehemu ya mbali, lakini akajua hiyo haikuwa kweli kupitia kusikiliza mawasiliano baina yake na watu wa familia yake. Pius alikuwa amekwenda kujificha nje ya wilaya aliyoishi, na mara kwa mara aliwasiliana na mke wake kuulizia hali nyumbani. Jafari alitumia utaalamu kuweza kuunganisha namba ya mke wake kwenye simu yake, ili atakapopokea au kupiga simu yoyote, aweze kuyasikiliza maongezi.

Baada ya Jafari kufanya utafiti na kugundua sehemu hususa Pius aliyokuwa, akawajulisha Dylan na Grace. Wakati huu, Grace alimwambia wanatakiwa kufanya mambo kwa umakini zaidi, ili kuweza kumnasa mwanaume huyo vizuri. Hivyo, Jafari akapiga hatua ya kwanza kwa kumfata eneo la sokoni, ambako Pius alikuwa na kawaida ya kwenda kununua chakula, kisha akaendelea kumfatilia polepole. Hakujionyesha kwake mpaka Pius aliporudi kwenye nyumba aliyokuwa amepanga chumba.

Pius alikuwa analipia chumba kidogo kwenye nyumba ya wapangaji, ambako aliweka godoro moja, neti na ndoo. Kutokana na kazi yake na hela nyingi alizolipwa kusababisha ajali ya Dylan, pesa ya kujikimu wakati amejificha alikuwa nayo. Ila bado aliogopa kwa kuwa hakujua ikiwa mambo haya yangeendelea au yangekwisha.

Wakati alipofika ndani kwake, akarudishia mlango na kuketi kwenye godoro chini; tayari kwa kuanza kula. Ila kabla hajaanza kula, mlango wake ukagongwa kuashiria kuna mtu nje alihitaji kuonana naye. Kwa haraka akafikiri ni mpangaji wa hapo, hivyo akaweka chakula pembeni na kwenda kufungua mlango. Macho yake yalitanuka kwa mshangao baada ya kumwona Dylan akiwa amesimama hapo. Alianza kurudi nyuma akiwa anatetemeka na kupumua haraka haraka kwa woga sana.

Dylan akapiga hatua na kuingia ndani mule, akifuatiwa na Jafari nyuma yake. Mwanaume huyo mwenye umri mkubwa aliogopa na kushindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Jafari akapandisha T-shirt yake juu kidogo kumwonyesha Pius bastola kiunoni, kisha akaweka kidole chake kimoja mdomoni mwake kumwonyesha Pius kwamba asifanye fujo zozote.

Pius aliogopa sana. Alimwangalia Dylan kwa kutoamini kabisa kwamba ilikuwa ni yeye. Dylan akasogea karibu yake zaidi akiwa anamwangalia kwa njia ya kawaida.

"Habari yako Mr. Pius?" Dylan akasema kwa utulivu.

Pius akawa anamwangalia kwa wasiwasi.

"Najua me ni mdogo kwako lakini... shikamoo siyo kitu yangu kabisa," Dylan akatania, naye Jafari akatabasamu.

"Mnataka nini?" Pius akauliza.

"Wow! Tunataka nini? Yaani hauonyeshi hata woga kuona maiti inaongea?" Dylan akakejeli.

"Naombeni mniache... mimi sijui lolote mnalotaka..."

Kabla hajamaliza kuongea, Dylan alimpiga ngumi nzito usoni na kumfanya ajigonge ukutani. Ilimuumiza sana mpaka damu ikaanza kuvuja kutokea puani mwake. Jafari, akiwa nyuma ya Dylan, akatoa bastola yake na kumnyooshea Pius, kama anataka kumfyatulia risasi.

"Tafadhali... tafadhali... nina familia... jamani msiniue..." Pius akasema kwa woga.

"Kimya!" Jafari akamfokea.

Pius akaendelea kutetemeka kwa woga.

"Sema ukweli wote... kuanzia mwanzo hadi mwisho," Jafari akamwambia kwa mkazo.

*Mimi... mimi sijui..."

Hapo hapo Dylan akaishika shingo yake kwa nguvu na kumkaba huku amemkandamizia ukutani. Uso wa Dylan ukawa karibu na uso wa Pius, akimwangalia kwa hasira sana.

"Kuna vitu huwa nafanya wakati mwingine mpaka nakuwa sijielewi. Lakini naomba uelewe kuwa nimetokea kuzimu sasa hivi ambako wewe ndiyo ulikuwa njia ya kuhakikisha nafika, kwa hiyo nina hasira kidogo..." Dylan akasema kwa kejeli yenye ukali sana.

Pius akawa anahangaika kupumua na kutoa sauti za kukabwa.

"Una familia? Mimi pia nina familia. Lakini wakati wewe na mafala wenzako mnapanga kifo changu, haukujali hilo. Sikujui, hunijui, na sijali wewe ni nani. Ninakupa sekunde 10 uanze kuongea ukweli wote... zikipita sekunde kumi hujasema... Jafari mtandike risasi popote pale lakini asife... mpaka aseme," Dylan akasema kwa mkazo.

Jafari akaikoki bastola yake vizuri, naye Dylan akamwachia Pius na kusogea nyuma kidogo. Pius akawa anarudisha utaratibu kwenye kupumua, na sasa Jafari akawa anahesabu kama jinsi ambavyo sekunde hutembea.

"T...kkhohh.. tafadhali... tafadhali..usi..."

"...tano... sita... saba... nan...."

"Ni Bernard! Ni Yakobo Bernard! Ulikuwa mpango wake! Alinilipa pesa tu mimi nifanye vile... sikuwa na ubaya na mtu yeyote mimi..." Pius akaanza kuongea.

"Tutakuwaje na uhakika kwamba unachosema ni kweli? Je kama unamsingizia?" Jafari akauliza.

"Hapana... ni yeye ndiye aliyeniagizia bomu dogo na kunilipa ili nilipachike mule.... kwa njia ambayo halingeweza kuonekana..."

"Ili iweje?" Jafari akamuuliza.

"Ali... alitaka kumuua... kumuua huyu kijana... Mimi nilikubali tu kwa kuwa sikuwa na jinsi..."

"Hukuwa na jinsi? Angekuwepo mwanao kwenye hiyo helicopter ungekubali?" Dylan akamuuliza.

"Haiko hivyo... mwanzoni sikutaka lakini... Mr. Bernard alitishia usalama wa familia yangu..."

"Ulishindwa kwenda polisi?" Dylan akamuuliza kiukali.

"Mambo siyo rahisi kihivyo mwanangu..."

"Usiniite mwanao! Mambo siyo rahisi... kwa hiyo kuua mtoto wa mtu mwingine ni sawa eti kwa sababu wa kwako katishiwa? Hata kama jambo hilo lilikuwa gumu, hiyo hailifanyi liwe justified... aaaigh...." Dylan akashindwa hata kuendelea kutokana na hasira nyingi aliyohisi.

"Nisamehe kijana wangu... tafadhali nisamehe... nitafanya lolote lile..tafadhali..." Pius akaomba kwa huzuni.

Jafari akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni. Akatoa kifaa cha kurekodia sauti alichokuwa amekiweka mfukoni, ambacho kilikuwa kinarekodi kila kitu walichoongea muda huo wote.

"Mambo yote uliyosema yako hapa. Hiyo ni moja," Jafari akamwambia.

Pius akashangaa kwa kuwa hakujua alikuwa akichukuliwa sauti.

"Mbili, kwa kuwa umesema kwamba alikuagizia bomu, nahitaji uniambie aliliagiza kutokea wapi," Jafari akamwambia.

"...aam..." Pius akasita.

"Umesema utafanya lolote... ongea," Dylan akamwambia.

"Bla...black market," Pius akajibu.

"What?! Black market! Tanzania wana hizo?" Dylan akamuuliza Jafari kiutani.

"We acha tu," Jafari akajibu.

"Tafadhali nawaomba msinichukulie hatua mbaya..."

"Kaa kimya," Jafari akamkatisha.

Pius akatulia akiwa mwenye wasiwasi bado. Dylan alianza kumwonea huruma kwa kiasi fulani, lakini hakutaka hisia hizo zipite kiasi.

"Bila shaka ikiwa wewe ulihusika kwenye hili, basi najua kuna mkataba mfupi ulipewa, si ndiyo?" Jafari akamuuliza Pius.

"Ndiyo...unamaanisha wa kuafikiana na...kuagiziwa..."

"Ndiyo, namaanisha hivyo. Karatasi hizo unazo bado?"

"Aam...nilizificha kwenye..."

"Nitahitaji unipe," Jafari akamwambia.

"Lakini...haziko hapa...yaani..."

"Sijali ziko wapi. Unapaswa unipatie haraka sana...leo leo," Jafari akamwambia kwa uthabiti.

Pius akawa hana neno lingine la kipingamizi kabisa. Alijua kufikia hapa hakuwa na njia ya kutoroka tena kwa sababu mambo yalikuwa yamevurugika sana upande wake. Dylan akamgeukia Jafari.

"Contract ya nini unaongelea?" akamuuliza Jafari.

"Siyo kama mikataba ya kawaida inavyokuwa. Yaani kwa black market za huku, hasa kwa nature ya Bernard, najua atakuwa aliagiza kwa njia isiyo ya moja kwa moja...na ili imfikie huyu bila shaka kuna vitu vilifanywa vya kuthibitisha muamala huo. Ikiwa vilipita kwanza kwa Bernard, lazima tutapata disclosure ya physical description yake, au mfano wa mwandiko wake kwenye sahihi au kitu chochote alichoandika ambacho kitatusaidia kupata background info kuhusu uhusiano wake na ajali hiyo; ili ikihitajika kuthibitisha..."

"Uthibitisho tunakuwa nao," Dylan akamalizia.

"Yeah."

Dylan akamgeukia Pius na kusema, "Uko tayari kunisaidia?"

"Ndiyo. Nitafanya unachotaka," Pius akajibu.

"Kweli? Hata ijapokuwa nimekupiga ngumi usoni?" Dylan akatania.

Pius, akiwa kama mtu mzima, aliona aibu sana kutendewa namna hii na kijana ambaye kiumri alimwacha sana. Lakini kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya makosa yake, alijua malipo yangepaswa kuwa makubwa, hata kama angepelekwa jela. Hakuwa na njia ya kuepuka mkasa huu tena.

Dylan alimhimiza asiseme lolote kwa yeyote kwa kuwa angejiletea matatizo. Alimwahidi kwamba adhabu yake haingekuwa kubwa sana, hasa ikiwa angethibitisha kwa vyombo vya kisheria kuwa alilaghaiwa ili afanye mpango ule wa Mr. Bernard utimie. Jafari akamwambia kwa muda huu angepaswa kuacha kuwasiliana na Mr. Bernard mpaka wahakikishe wameweza kumdhibiti ipasavyo, kwa kuwa mipango yao ilikuwa imeanza kazi.

Pius alikubali, na alionyesha kweli anataka kurekebisha makosa yake kwa kumwambia Jafari angekwenda naye hiyo hiyo siku kufata kila kitu alichohitaji. Kwa hiyo Dylan akawaacha wawili hao waelekee huko, akiwa anajihisi vizuri kwamba mpango huo wa kumshawishi Pius ulifanikiwa, kisha yeye akaondoka na kuelekea kwa Grace.

★★★

Gilbert alipigiwa simu asubuhi moja na kuambiwa kwamba mwakilishi wa kampuni ambayo ilikuwa yake angekuja sehemu aliyoishi ili amletee ujumbe fulani muhimu. Aliuliza ilihusu nini, lakini akaambiwa asubiri tu mpaka mwakilishi huyo afike, naye angepata kujua ujumbe huo ulikuwa ni nini hasa. Akamwambia Jaquelin kuhusu hilo, ambaye pia hakuwa na wazo la ni nini ambacho watu hao walitaka kusema.

Walikaa nyumbani kusubiri mpaka ilipofika mida ya jioni saa 10, pale mwanaume fulani alipofika kwao, akiwa na mwonekano nadhifu wa suti. Gilbert wala Jaquelin hawakuwahi kumwona, kwa hiyo wakafikiri labda alikuwa mwajiriwa mpya kwenye kampuni. Lakini kihalisi, mtu huyu alikuwa mwakilishi wa kampuni ya Gilbert kwa niaba ya Grace, ambaye ndiye aliyekuwa amemtuma hapo. Wakamkaribisha ndani, lakini akasema hakuwa na muda mrefu sana wa kuweza kukaa, hivyo angewapatia taarifa aliyowaletea na kuondoka.

Mwanaume huyo akampa Gilbert faili fulani, kisha akamwambia, "Hongera Mr. Gilbert. Umekuwa raisi wa kampuni yako tena."

Gilbert na Jaquelin walibaki kushangaa sana. Wakatazamana kwa kuchanganywa na habari hizo za ghafla.

"Unamaanisha nini... imekuwaje... kivipi yaani?" Gilbert akauliza kwa kutoelewa.

"Nafasi yako kama raisi wa kampuni imerudishwa. Mambo utakayosoma humo yatakuelewesha kila kitu. Share zote za kampuni ziko chini yenu sasa; wewe na Mrs. Gilbert," mwanaume huyo akasema.

Jaquelin akatoa macho kwa kushangaa.

"Shares zote?!" akauliza.

"Ndiyo. Karibuni sana tena," mwanaume huyo akajibu.

Ilikuwa ni taarifa ambayo ingepaswa kuwafanya wafurahi sana, lakini ikawaacha wakiwa wamepigwa na butwaa. Mwakilishi huyo akawaambia watie sahihi karatasi fulani ya uthibitisho kuwa wameafiki jambo hili, nao wakasaini na kisha mwanaume huyo akawaaga na kuondoka zake. Wawili hao wakarudi ndani wakiwa wana maswali mengi vichwani mwao.

"Isije ikawa kwamba tunazungukwa tena Gilbert?" Jaquelin akasema.

"Sidhani Jacky. Tazama... kila kitu kiko in perfect order....yaani... we're in control of all shares... I can't believe this!" Gilbert akasema kwa hisia.

"Ni nani aliyefanya hivi? Una uhakika kweli..."

"Ndiyo, Jaquelin. Angalia...100% ya share zote ziko chini yetu sasa. Kampuni ilikuwa ikiperform vibaya... kuna mtu hapa anaitwa Smith Morgan amenunua zote, na corporate law imemsaidia kuhakikisha hakuna mtu yeyote anapinga jambo hilo. Kazihamishia kwetu... yaani ni kama..." Gilbert akaishia hivyo baada ya kuingiwa na wazo fulani.

Jaquelin akabaki kumwangalia kwa umakini, naye Gilbert akamgeukia na kumwangalia kwa njia iliyoonyesha alikuwa na jambo fulani kichwani kwake.

"Nini?" Jaquelin akamuuliza.

"Ni Dylan!" Gilbert akasema kwa uhakika.

Jaquelin akabaki kumtazama tu.

"Jaquelin, ni Dylan. Dylan ndiyo anafanya hivi... ahah..." Gilbert akaonyesha shauku.

"Unajuaje hilo?"

"Sijui lakini... think about it. Haiwezekani tu kampuni irudishwe kwetu kinagaubaga bila mtu anayeirudisha kwetu kuwa na nia fulani. Ni wazi kabisa kwamba Dylan amefanya hivi."

"Gilbert tutawezaje kuwa na uhakika kwamba ni yeye? Najua ingekuwa ni yeye angetuambia lakini hajajitokeza hata mara moja kwetu, unawezaje kuamini tu kwamba..."

"Sijaamini tu ovyo ovyo. Jaquelin, Dylan hajui kwamba sisi tunafahamu yuko hai. Ana... bila shaka amekuwa akifatilia maisha yetu... na sijui amewezaje kuzinunua hisa hizo zote lakini... anatusaidia bila kujulikana kwamba yuko hai. Jaquelin hiyo inamaanisha anafanya mpango fulani wa kumwondoa adui yake... na hii ndiyo njia ya kwanza..."

"Mr. Bernard," Jaquelin akasema kwa utambuzi.

"Ndiyo. Inaonekana anajua kuhusu Bernard ku-compromise helicopter, kwa hiyo Jaquelin, tunapaswa kumsaidia pia Dylan kwa kumhandle Bernard... kwa sababu sasa nguvu yetu imerudi," Gilbert akasema kwa uhakika.

"Ndiyo. Kwa hilo tuko pamoja. Mr. Bernard ni lazima aanguke," Jaquelin akasema kwa mkazo pia.

Wawili hawa wakaendelea kupitia masuala mbalimbali kwenye makaratasi ya faili waliloletewa, nao wakajiweka sawa kiakili ili waweze kurudi kwenye kampuni yao kwa kishindo.

Kutokana na furaha aliyokuwa nayo, Jaquelin akampigia rafiki yake, Beatrice, na kumwambia amerejea ngazi ya juu kwa mara nyingine tena. Beatrice alishangaa na kumuuliza alimaanisha nini, naye Jaquelin akamwambia angekuja kusikia tu matendo yake yeye mwenyewe wala asiwe na haraka. Ikabidi Beatrice amwambie angefika kwake kesho kumtembelea ndiyo angemsimulia vizuri, kwa kuwa alikuwa na muda hajamwona. Kwa mambo mengi, Jaquelin alipenda sana kujisifia, na sasa kurudishiwa kampuni yao lilikuwa ni jambo la kumfanya atambe; yaani wote waliomwonyesha dharau wangemtambua!

Gilbert alijipanga vyema kwa ajili ya kesho. Kwenye makaratasi aliyoletewa alipata kujua kuwa aliyenunua hisa za kampuni yao na kumrudishia nafasi yake alimtaka afanye kazi kwa njia yake anayojua ni bora ili kuirudisha kampuni kwenye mstari ulionyooka tena. Jina lilikuwa ni Smith Morgan, lakini Gilbert aliamini kabisa moyoni mwake kuwa ilikuwa ni Dylan. Alijua Dylan angetaka atoe jambo ambalo ni kikwazo kikubwa pale kwenye kampuni yao, kwa hiyo bila shaka angeanza na Mr. Bernard.

Kwa upande wa Mr. Bernard, ilikuwa ni wasiwasi tupu uliomjaa baada ya kuhangaika sana kumtafuta Pius bila mafanikio. Alijua mwanaume yule alikuwa akifatiliwa na mtu fulani na alikwenda kujificha kutokana na aliyemtafuta kumhoji kuhusu siri yao, lakini sasa kila alipomtafuta Pius kwa simu hakuweza kumpata. Ikambidi atume mtu wake mmoja (kama jambazi) ili aweze kumtafuta na akishampata amlete kwake; atake asitake.

Sasa Pius akaanza kusakwa na mtu huyo ambaye alikuwa ni mwanaume mwenye roho ya kikatili, aliyemfanyia Mr. Bernard mambo mengi mabaya kwa muda mrefu sana.

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI

★★★★★★★★★★★★★★


Moja kwa moja mpaka kwenye chumba kikuu cha mikutano cha kampuni ya Gilbert, ambayo sasa ilikuwa ndani ya mikono ya Grace, washiriki wote wakuu wa bodi ya kampuni, kutia ndani Mr. Bernard akiwa kama raisi, walikuwa humo wakijadili suala fulani ambalo liliwafanya wote washangae. Taarifa ilikuwa imeletwa na wawakilishi wa Grace (wenyewe walifikiri wawakilishi ni wa Smith Morgan), kwamba amebadilisha mfumo wa uongozi na kumpa mtu mwingine ndiyo awe raisi wa kampuni sasa.

Mr. Bernard alitaharuki sana kwa kuwa alishtushwa na habari hizi, naye akawa akiwaambia wawakilishi hao kuwa angehitaji kuonana ana kwa ana na "Smith" ili wazungumze kwa kuwa jambo hilo kwake halikukubalika hata kidogo. Wawakilishi wale walimwambia hakuna chochote angefanya ambacho kingebadili uamuzi wa mkubwa wao, hivyo angepaswa kutulia kwa sababu sasa kampuni ilikuwa ni yake (yaani Grace). Wote walikuwa humo wakisubiria raisi mpya afike, kwa hiyo Mr. Bernard akakaa kusubiri pia kwa shingo upande.

Baada ya dakika chache, Gilbert pamoja na Jaquelin waliingia kwenye chumba hicho cha mikutano wakionekana kuwa makini na tayari kikazi. Wengi walishangaa na kusimama kuwatazama, huku Mr. Bernard akiwa amekunja sura kwa mshangao asiamini kuwaona hapo. Baadhi ya washiriki waliokuwa na mioyo minyoofu kuwaelekea wawili hao walifurahi sana kuwaona na kuwakaribisha kwa shauku, huku wanafiki wakibaki kukunja sura tu. Mr. Bernard akatoa tabasamu bandia huku akiwa na wasiwasi, naye akasogea karibu na walipokuwa wamesimama.

"Jaquelin....Gilbert... karibuni sana...ni muda umepita," Mr. Bernard akajifaraghua.

Gilbert na Jaquelin wakamwangalia kwa mkazo sana.

"Aam...sikujua kama militakiwa kuwepo kwenye huu mkutano," Mr. Bernard akasema.

"Everyone, huyu ndiyo raisi mpya wa kampuni, Mr. Gilbert Mushi," mwakilishi mmoja akasema.

Mr. Bernard alitoa macho kwa kushangaa mno! Washiriki wengine walifurahi na kuanza kumpigia makofi ya hongera Gilbert pamoja na mke wake, ambao walionyesha shukrani pia. Wawakilishi wale wa Grace wakaongea kifupi na Gilbert, kisha wakawaaga wote na kuondoka. Gilbert akamwangalia Mr. Bernard kwa mkazo, kisha akampita na kwenda mpaka kwenye kiti cha mbele zaidi cha kiongozi na kuketi. Jaquelin pia akampita Mr. Bernard huku anamwangalia kwa dharau, na kufanya jamaa ahisi hapa kuna mchezo lazima umefanywa. Lakini yote kwa yote, akajirekebisha kwa kuliweka koti lake sawa na kwenda kuketi pia.

Gilbert aliongea na washiriki wa bodi ya kampuni kuhusiana na matatizo yaliyoipata kampuni, na kuwafanya watambue kwamba bila shaka Mr. Bernard hakuwa akifanya kazi kama alivyotakiwa. Jamaa alijitetea sana na kuwaomba wapambe wake wampe kichwa, lakini ni kama wengi wao walihofia kutoa support kwake tena kutokana na ukweli wa mambo ambayo Gilbert aliwaambia. Mwishowe, Gilbert akaanza kuwataarifu watu hao kuhusu mipango mingi ambayo "Smith" alikuwa amempa ili kusaidia kuirudisha kampuni juu tena. Mawazo hayo yangeanza kufanyiwa kazi haraka sana ili matokeo mazuri yaweze kuja mapema pia.

"Pia, kuna jambo la mwisho la muhimu nalotaka kusema," akasema Gilbert.

Wote wakakaa tayari kumsikiliza raisi wao alitaka kusema nini.

"Mr. Bernard..." Gilbert akaita.

"Ndiyo..." jamaa akaitika kwa shauku.

"Kaisafishe ofisi yako," Gilbert akamwambia.

Wengi walibaki kumtazama Mr. Bernard kimaswali, wakiwa wameelewa kuwa Gilbert alikuwa anamfuta kutoka kwenye kampuni yao. Mr. Bernard alichanganyikiwa na kuanza kuuliza sababu ni nini ya Gilbert kufanya hivyo, na kwa kejeli Gilbert akasema ni kwa sababu tu amependa. Akamwambia kama aliona shida kubeba vitu vyake na kuondoka, basi angeita walinzi ili waje kumtoa yeye pamoja na vitu vyake. Hakuwa na ujanja tena. Akanyanyuka na kuondoka akiwa anahisi aibu kubwa sana.

Wakati akitoka alikuwa anatazamwa mno na wafanyakazi wa hapo, ambao hawakupenda uongozi wake tokea alipowekwa kuwa raisi wa kampuni miezi michache iliyopita. Akaenda mpaka kwenye gari lake na kuingia akiwa na hasira, kisha akampigia yule mtu aliyesaidiana naye ili kumwangusha Gilbert. Akamweleza kuhusu kilichotokea na kusema alishindwa kuelewa iliwezekanaje mpaka wawili wale wakaweza kurudi namna hiyo, kwa kuwa aliwawekea vikwazo vingi sana ili wasifanikiwe.

Mtu huyo alikasirika sana na kusema haiwezekani, ni lazima angejua nini kinaendelea na kama kuna mtu amewasaidia basi yeye angeshughulika naye. Baada ya kukata simu, Mr. Bernard akaondoka akiwa ameudhika na kujiahidi kutoacha mpaka ahakikishe Gilbert anaanguka kwa mara nyingine tena.


★★★


Mambo yalikwenda vizuri kwa wazazi wa Dylan siku yao ya kwanza kurudi tena kwenye kampuni yao. Wafanyakazi wengi walifurahi kuona wamerejea, naye Gilbert aliwaahidi mambo yangekwenda vizuri zaidi wakati huu. Aliongea na wengi wao kuweza kujua kuhusu uzoefu, furaha, hofu na kero zao, ili ajipange kuwasaidia kwa njia nzuri na kuwafanya wafurahie kuendelea kufanya kazi hapo.

Jaquelin alikutana na rafiki yake Beatrice baadae. Kihalisi walitakiwa kuonana nyumbani kwake, lakini mambo yakabadilika hivyo wakaamua kukutana kwenye mgahawa mkubwa wa kisasa. Lilikuwa ni wazo la Jaquelin kwa sababu sasa alikuwa amerudi kwenye mahali alipoona alistahili kuwa...kwenye pesa. Akamsimulia rafiki yake kuhusu jinsi walivyorudi kwenye kampuni yao kwa kishindo na kumfukuza Mr. Bernard bila kukawia. Beatrice alikuwa anashangaa bado kuhusu mambo haya.

"Mmewezaje...yaani best mmenishangaza sana!" Beatrice akasema.

"Unashangaa nini nawe? Ndiyo sisi. Walisema ooh wamepotea, mara ooo hawatarudi...yako wapi? Alaah..." Jaquelin akajisifia.

"Ahahahah...ama kweli malipo hapa hapa duniani," Beatrice akasema.

"Ndiyo maana yake. Yaani tena huyo Bernard nilikuwa natamani kumpiga kofi la usoni kwa alichokifanya! Ana bahati tu kwamba..." Jaquelin akaishia hivyo.

"Ana bahati kwamba?" Beatrice akauliza.

"Aagh... achana naye," Jaquelin akasema.

"Unajua...huwa unasema tu jinsi unavyomchukia huyo...Mr. Bernard, lakini hujawahi kuniambia ni kwa nini. Na...wakati huu...kwa nini mmemfukuza namna hiyo?" Beatrice akauliza.

"We acha tu Tris. Mambo ni mengi sana."

"Mh...unanifanya nijali hata zaidi sasa. Niambie ni nini kinaendelea maana jamaa inaonekana aliwachokonoa pabaya."

"Siyo kutuchokonoa..yaani yule mshenzi ameyafanya maisha yetu yawe magumu...ni yeye ndiye aliyefanya mpaka hayo mambo yote yakatupata."

"Wewee...kumbe?" Beatrice akashangaa.

"Ndiyo. Tulipoteza kila kitu kwa sababu yake, na ni yeye ndiye alifanya mpango ili ile helicopter imwangushe Dylan!"

"Eh!" Beatrice akashangaa zaidi.

"Yaani wakati mwingine sipendi hata kulisikia jina lake huyo kinyago," Jaquelin akasema kwa hisia kali.

"Kwa nini sasa afanye vile huyo baba? Halafu kipindi kile nilipokutanaga naye pamoja na Alfred alionekana mstaarabuu...kumbe ndo'...."

"Mstaarabu? Heh...yaani yule ni nyoka. Na hapo bado...tutahakikisha anapoteza kila kitu kama alivyotaka kutufanyia mpuuzi yule," Jaquelin akasema.

"Aisee! Kwa hiyo sasa...mmewaambia polisi kuhusu alichofanya?"

"Hatujafanya hivyo."

"Kwa nini sasa? Mnatakiwa muwaambie mapolisi ili wamkamate kwa sababu alifanya kosa la mauaji!"

"Najua. Lakini mapolisi na wenyewe washamba tu. Sisi wenyewe tutadili naye...kwa sababu sasa hivi nguvu yangu imerudi," Jaquelin akasema kwa uhakika.

"Unamaanisha kuirudisha kampuni? Hicho tu ndiyo kitakufanya umlipizie kisasi? Je ukitoka hapa sasa hivi ukashtukia tu gari lako linalipuliwa?"

"Wewee hana ubavu huo. Na hata alipojaribu kumuua mwanangu hakufanikiwa."

"Nini?" Beatrice akashangaa.

Jaquelin akatazama pembeni kwa njia ya kuudhika.

"Best unamaanisha nini? Sote tunajua kwamba Dylan ame..."

"Hajafa!" Jaquelin akamkatisha.

Beatrice akabaki kumtazama kwa kuchanganyikiwa.

"Ahah...Jaquelin... samahani lakini...najua kifo cha Dylan kilikuumiza sana na ulipitia wakati mgumu ila...mimi ni rafiki yako...lazima nikwambie ukweli na uukubali. Dylan hatuko naye tena Jaquelin," Beatrice akamwambia kwa hisia.

"No. Dylan yuko hai. Unafikiri ni nani aliyetusaidia mpaka tukaipata kampuni tena?" Jaquelin akasema kwa uhakika.

"What...yaani...Dylan ndiyo amewasaidia mkaipata kampuni tena?"

"Ndiyo maana yake."

"Jaquelin...umeweka nini kwenye kinywaji chako?"

Jaquelin akazungusha macho yake. Ni wazi Beatrice alishindwa kuelewa nini kinaendelea.

"Rafiki yangu usi..."

"Tris nisikilize. Dylan hakufa. Sijui ilikuwaje lakini alisalimika kwenye ile ajali. Tumekuja kujua yuko hai wiki iliyopita, na sasa bila shaka ametusaidia ili mambo yakae sawa tena kwetu. Sijajua anapanga nini, lakini anaonekana kuwa makini kwa sababu hataki mtu ajue kwamba yuko hai...na ndiyo maana sisi pia hatusemi kwa yeyote kuhusu hilo," Jaquelin akaeleza.

Beatrice alimwangalia kimaswali sana, naye akatikisa kichwa chake taratibu kuonyesha kwamba jambo hilo lilimshangaza sana.

"Mh! Makubwa jamani. Kwa hiyo Dylan wangu yuko hai! Masikini..." Beatrice akasema kwa hisia.

"Mwanangu atarudi tu. Na akifika wote watamtambua. Hizi ni cheche tu najua anakuja na moto," Jaquelin akasema kwa ujasiri.

"Umeshamwona?" Beatrice akauliza.

"Hapana. Ametulia huko aliko bila shaka anaunda mipango yake kwa umakini zaidi."

"Lakini unawezaje kuwa na uhakika kwamba ni yeye? Je kama kuna mtu anawafanyia mchezo...halafu mnaingia mtegoni," Beatrice akasema kwa kujali.

"Beatrice usijali. Mambo mengi hayaeleweki kirahisi najua...lakini wewe tulia tu utaona. Dylan atawashusha WOTE wanaojaribu kumzingua...hawamjui mwanangu vizuri," Jaquelin akasema kwa uhakika sana.

Beatrice akabaki anamtazama rafiki yake kama vile ni mtu aliyerukwa na akili, lakini uhakika wa Jaquelin ulikuwa wa hali ya juu sana kupuuzia jambo hilo zito. Simu ya Beatrice ikaita, naye akapokea huku Jaquelin akiendelea kunywa juice yake. Beatrice akamaliza kuongea na simu na kurudisha umakini wake kwa Jaquelin tena.

"Boyfriend eeh?" Jaquelin akauliza.

"Mm hamna...hahahah...ni Harleen," akasema.

"Eee afu' kweli, Harleen ni muda sasa sijamwona. Anaendeleaje?"

"Mh...we acha tu. Walikorofishana na mchumba wake huko sijui wakaachana ghafla."

"Wewe! Kisa?"

"Aagh yaani me hata sikuwaelewa kwa kweli. Harleen anaingiaga kwenye mahusiano, lakini baada ya muda mfupi tu...wameachana. Nishamzoea."

"Lakini ni mtoto wako, unatakiwa kumwongoza mara nyingine hata kama amekua."

"Siyo mtoto huyo, anaweza kufanya maamuzi yake mwenyewe. Na kwanza huyo mwanaume hata sikumpenda ni basi tu Harleen anapenda kulazimisha mambo."

Jaquelin akacheka.

"Tena unajua nini...nafikiri Harleen atafurahi sana kama atajua Dylan ni mzima, maana..."

"No Beatrice, hapana. Usimwambie yeyote kuhusu Dylan. Ninakuamini wewe tu, usiseme kwa yeyote yule please," Jaquelin akamsihi.

"Okay sawa usijali, my lips are sealed. Ila maisha yenu yalivyo best kama movie vile..."


Jaquelin akacheka na kuendelea kupiga story na rafiki yake kipenzi. Baada ya muda fulani kupita, waliagana na wote kuelekea makwao baada ya kufurahia kiburudisho hicho cha urafiki pamoja.


★★★


Mr. Bernard alipigiwa simu usiku na yule jamaa aliyemtuma kumtafuta Pius, ambaye alimwambia alifanikiwa kumpata na kumfanya apoteze fahamu kwa kumnusisha madawa kwenye kitambaa. Kwa hiyo, alimweka kwenye gari lake na kumleta upande huu wa jiji; kwenye jumba la kutunzia nafaka ambalo halikuwa likitumiwa kwa muda mrefu. Hivyo, Mr. Bernard akamwambia amsubirie hapo na amchunge ili afike na kuzungumza naye. Mambo mengi yalikuwa yameanza kwenda vibaya kwa Mr. Bernard, kwa hiyo alitaka kujua kisa cha Pius kumkwepa kilikuwa ni kwa sababu gani.

Dakika chache baadae, Mr. Bernard akawa amefika sehemu ile na kuegesha gari lake nje. Akaingia ndani ya jumba hilo, lililokuwa tupu na lenye giza kiasi, huku kwa mbele chemli ikionekana kumulika sehemu ndogo ya humo ndani. Akasogea mpaka sehemu hiyo na kufika usawa wa ukingo wa ukuta na kukata kona. Ni hapo ndiyo akawa amefika kwenye chumba ambacho hakikuwa na mlango, na ndani palimulikwa na taa kutokea juu, hivyo aliweza kumwona Pius akiwa amelazwa chini akionekana kusinzia. Akaingia na kumkuta yule mwanaume na kumpongeza kwa kazi nzuri, kisha akamwambia amwamshe. Jamaa akaenda kujaribu kumwamsha Pius kwa kumpiga makofi, ambaye alianza kurejewa na fahamu polepole.

Pius alikurupuka baada ya kumwona Mr. Bernard akiwa hapo. Akasimama na kurudi nyuma kidogo, akishangaa alifikaje sehemu hii.

"Unaweza kunieleza ni nini maana ya wewe ku-dodge simu zangu?" Mr. Bernard akamuuliza kwa mkazo.

"Sija-dodge simu zako. Ni kwamba tu...nilikuwa nimejificha..."

"Kwa hiyo?"

"...nilifikiri ingekuwa busara kuwa makini..nisipokee maana...huwezi jua..mtu fulani angeweza ku-tap simu yangu," Pius akatoa kisingizio.

Mr. Bernard akatabasamu na kumsogelea karibu zaidi.

"Unaniona mimi kama mjinga mwenzako, si ndiyo?" akamuuliza.

"Hapana. Kwa nini useme hivyo? Mimi naku...nakuheshimu siwezi kukudanganya..." Pius akasema.

"Ahahahah... Kwa hiyo bado unaniona mimi mtoto mdogo sivyo?" Mr. Bernard akauliza.

Pius akabaki kumtazama tu.

"Pius...tusitaniane. Ninataka uniambie ukweli...nini kinaendelea?"

"Hakuna chochote..wala mimi sikutanii..siwezi..."

"Kimya! Niambie ukweli sasa hivi la sivyo..."

Mr. Bernard akafoka kwa hasira na kulishika shati la Pius kwenye kola huku akimvuta. Pius alijawa na hasira pia, naye akaitoa mikono ya Mr. Bernard kwa nguvu kutoka kwake. Mr. Bernard akashangaa.

"Unataka kujua ukweli? Sawa. Ukweli ni kwamba sitaki tena kujihusisha nawe kwa lolote. Ninajuta kukubali unitumie kwenye jambo lile la kikatili...sitaki tena!" Pius akasema kwa hisia kali.

"Hutaki nini? Una matatizo? Siyo wewe uliyenipigia simu ukasema unafatiliwa na unahitaji kujificha? Mnyoo gani amekuingia kichwani mpaka unanipandishia sauti namna hiyo? Umenisahau eeh?" Mr. Bernard akafoka.

"Sikuogopi. Wewe fanya mambo yako na mimi uniache kwa amani. Nimeshasema sitaki tena kujihusisha nawe...kama kufatiliwa sasa hivi sifatiliwi kwa hiyo sihitaji msaada wako," Pius akasema.

"Nini?" Mr. Bernard akauliza kimshangao.

Pius akampita Mr. Bernard akitaka kuondoka lakini yule mwanaume akamzuia kwa kusimama mbele yake. Mr. Bernard akamgeukia Pius na kumwangalia akiwa anahisi hasira sana.

"Mwacheni aende."

Wote walisikia sauti hii ikitokea sehemu ya kuingilia ndani ya chumba hicho. Wakageuka na kutazama ni nani aliyesema hivyo kwa utulivu mno, na hapo Mr. Bernard akatambua kwamba ilikuwa ni yule mtu muhimu aliyesaidiana naye kufanya mpango wa kumwangusha Gilbert. Alikunja uso kimaswali, akishangaa mtu huyo aliwezaje kujua walikuwa hapo. Akaingia ndani ya chumba hicho na kufika usawa wa mwanaume yule aliyemzibia njia Pius, na hapo mwanaume huyo akampisha na kusimama pembeni, kama kumwonyesha heshima. Pius hakujua mtu huyo alikuwa nani, lakini kufikia hapa akaweza kujiongeza kwamba alifahamiana na hawa watu.

"Pius Kimambo...habari yako?" mtu huyu akamsalimu.

Pius akawa anamwangalia tu kwa mashaka.

"Unafanya nini hapa? Umejuaje tuko hapa?" Mr. Bernard akauliza.

"Oh ninajua mambo mengi yanayonizunguka Bernard...nafikiri unajua hilo," mtu huyo akasema.

Pius akawatazama wote kwa makini, kisha akamkazia uangalifu zaidi mtu huyo.

"Kwa nini mnamzuia baba wa watu? Hii ni nchi huru...kama anataka kuondoka mwacheni aondoke," mtu huyo akasema.

"Nini? Aondoke kivipi...unaju..."

"Nimesema mwacheni aondoke!" mtu huyo akamkatisha Mr. Bernard kwa uthabiti.

Mr. Bernard pamoja na yule mwanaume mwingine walitazamana kimaswali sana, huku Pius akijipa ukakamavu wa kuonyesha bado ni jasiri.

"Pius...kama ulivyosema, hakuna lolote ulilobakiza hapa. Kwa hiyo waweza kwenda nyumbani...hawa wasikuzingue kabisa...nenda baba," akasema mtu huyo.

Pius akamwangalia kwa sekunde chache, kisha polepole akaanza kupiga hatua na kumpita ili aondoke zake. Mr. Bernard alikuwa amepigwa na butwaa, asielewe nini ilikuwa maana ya mtu huyu kumwachia Pius. Ni mpaka Pius alipokaribia sehemu ya wazi ya mlango pale wanaume wawili wenye miili mikubwa ya mazoezi walipomzibia njia ili asiweze kupita. Pius alishtushwa nao sana na kubaki kuwatazama kwa hofu, kwa sababu walikuwa na sura zilizoonyesha walitaka kumdhuru. Mtu yule, akiwa anamwangalia Mr. Bernard, akaachia tabasamu la hila, na hapo Mr. Bernard akawa ametambua kwamba alikuwa akimfanyia tu Pius mchezo; hatoki mtu hapo!

Mtu huyu akageuka taratibu na kumwangalia Pius, ambaye alikuwa anababaika asijue pa kwenda. Wanaume wale wakamkamata kwa nguvu na kumpiga tumboni, kisha usoni, na kumtupa chini mbele ya miguu ya mtu huyo. Akacheka kwa dharau, na wale wanaume wake wakacheka pia. Mr. Bernard alihisi ahueni kwamba hawakumwachia Pius aondoke, lakini hakujua kihalisi watu hawa wangeupeleka wapi mchezo huu. Pius akajitahidi kusimama huku analia na kutetemeka, akiomba wasimtendee kwa ukatili.

"...tafadhali...niachieni...mimi...mimi ni..."

"Wewe ni msaliti!" mtu huyo akamkatisha.

Mr. Bernard hakuelewa alimaanisha nini kumwita Pius msaliti.

"Na unajua dawa ya wasaliti huwa ni nini?" mtu huyo akauliza.

Kisha akarudisha mkono wake nyuma ya kiuno chake na kutoa bastola. Mr. Bernard akashtushwa kiasi, kwa sababu hakuwa na lengo la kumuua Pius, kwa hiyo hakujua atazamie nini kutoka kwa mtu huyo ambaye hakueleweka ikiwa alikuwa anatania au anamaanisha anachotaka kufanya.

"Dada tafadhali...usiniue...nina familia...wananihitaji...mwanangu ni mgonjwa...ana...ana...ananihitaji...tafa..." Pius akaendelea kuomba kwa huzuni.

"Dawa ya wasaliti huwa ni kifo. Hujasoma kuhusu Yuda Iskariote? Alimsaliti Yeshu Krishto kwa shilingi 50 tu! Akaweka mfano kwa kujiua yeye mwenyewe...na mfano huo mpaka leo unapaswa kufatwa; usaliti, kifo. Lakini...kwa kuwa hukujiongeza kujiua, naona bora nikusaidie...au unasemaje?" mtu huyo akasema kwa kejeli na kufanya wanaume wake wacheke.

"Please dada...usi...mimi ni binadamu mwenzako...usitende unyama huu..."

Mtu huyu, anbaye ni mwanamke, akawa anatabasamu kwa kejeli tu na kumwangalia Pius bila kujali hata kidogo. Akamnyooshea Pius bastola kama anataka kumfyatulia risasi, naye Pius akanyoosha mikono yake juu kidogo kumwonyesha kwamba anahitaji amwonee huruma. Mwanamke huyo akamwangalia Pius sana, kisha akashusha bastola yake.

"Agh! Kwa nini huwa mnatia huruma sana mkiomba tusiwaue? Umenifanya hadi nimeshindwa kukupiga," mwanamke huyu akasema.

"Tafadhali dada yangu...usiniue. Mimi ni baba...nina binti...nina watoto...ndugu wananitegemea...tafadhali..." Pius akaomba kwa huzuni zaidi.

Mwanamke huyo alimwangalia kwa hisia sana, kisha akawaambia wanaume wale wampishe ili aondoke. Wakatii, naye Mr. Bernard akazidi kupandwa na hofu kiasi.

"Ondoka haraka! Sitaki kukuona tena...harakisha!" mwanamke huyo akamwamuru Pius.

Pius akaanza kurudi nyuma huku anatetemeka, kisha akageuka na kuanza kuelekea mlangoni upesi. Alipofika tu mlangoni, mlio wa risasi ulisikika kwa nguvu na kumfanya ashindwe kuendelea kujongea baada ya risasi hiyo kuupiga mgongo wake. Watu fulani husema kwamba, bora risasi ikupige ukiwa unatazama sehemu ilipotokea, lakini ikikupiga bila kutarajia, huwa ni kama maumivu yake yanakuwa mara mbili zaidi.

Pius alihisi maumivu makali sana kwa kuwa risasi hiyo ilimtoboa mgongoni mpaka sehemu ya mbele ya upande wa ini lake. Hakuweza hata kufikiria lolote, na hapo hapo risasi nyingine ikampiga mgongoni tena na kutoboa mpaka sehemu ya tumbo lake. Baba wa watu akaishiwa nguvu na kudondokea magoti yake, kisha mwili wa juu ukaangukia tumbo, naye akawa anashtuka-shtuka huku damu nyingi zikimtoka mwilini mwake na kutapakaa chini, kisha mwili wake ukatulia kabisa.

Mr. Bernard alishindwa kuelewa kwa nini mtu wake huyu aliamua kufanya hivyo. Mwanamke huyo akawa anatabasamu kikatili, akiwa ameridhishwa kabisa na kile alichofanya.

"Nini maana yake Beatrice? Kwa nini umefanya hivi?" Mr. Bernard akauliza.

Ndiyo. Mwanamke huyu alikuwa ni Beatrice, rafiki kipenzi wa Jaquelin!

Tokea mwanzo, ni yeye ndiye aliyekuwa akimsaidia Mr. Bernard ili kuharibu maisha ya Gilbert na Jaquelin. Alikuwa na sababu iliyomwongoza atake kuyafanya maisha ya wawili hao kuwa mabaya sana........



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Kama hii simulizi haijakopiwa kutoka watunzi wakubwa wa nje bhasi hakika tumefikia viwango vya kimataifa. Kuiweka kwenye mfumo wa movies, budget yake ni kubwa na producers wengi wakibongo hawataweza. Yote juu ya yote hongera mtunzi
 
Aisee, sio mchezo. Beatrice miyeyusho sana, sema nae Jaquline misifa inamponza
 
Kama hii simulizi haijakopiwa kutoka watunzi wakubwa wa nje bhasi hakika tumefikia viwango vya kimataifa. Kuiweka kwenye mfumo wa movies, budget yake ni kubwa na producers wengi wakibongo hawataweza. Yote juu ya yote hongera mtunzi
Asante kaka. Matumaini one day my talent will be realised and I'll go far
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…