Simulizi - DYLAN

Simulizi - DYLAN

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

ILIPOISHIA....

Dylan anakwenda kwenye chumba alichopo shangazi yake mdogo, Camila, na kuingia humo kwa uangalifu ili asifanye yeyote amsikie. Anamkuta shangazi yake akiwa ameketi kitandani, na baada ya Camila kumwona, akanyanyuka akishangaa uwepo wa mpwa wake hapo. Dylan akamfata na kumkumbatia kwa upendo, akimwambia maneno mazuri kukumbushia wakati ule walipojiingiza kwenye mapenzi kule Brazil. Lakini shangazi yake akamwambia kuwa sasa alipata mchumba, hivyo Dylan ajitahidi kuzifuta kumbukumbu hizo za wakati uliopita.

Dylan akavunjika sana moyo na kurudi nyuma kidogo. Camila akamwangalia kwa hisia za huruma, na uso wa Dylan kweli ulionyesha huzuni. Kijana akageuka na kupiga hatua kuurudia mlango, lakini akasita na kusimama. Kisha akamgeukia tena shangazi yake.

"Kwa nini umeniruhusu nikubusu?" Dylan akauliza.

Camila hakutoa jibu, bali macho yake yakaanza kujawa na machozi. Dylan akatikisa kichwa taratibu kwa huzuni, kisha akaona ni bora ajiondokee tu. Lakini wakati ameugeukia mlango, akapatwa na machale kuwa kulikuwa na mtu nje ya mlango. Ilikuwa ni kama hatua zinakaribia mlangoni hapo, na kwa kasi sana Dylan akaelekea mlangoni upesi na kuipandisha miguu yake kwa kukanyaga kuta za pembeni, akipanda juu kama vile spiderman!

Camila alishtushwa kiasi na jambo hilo, kwa kuwa hakuelewa Dylan alikuwa na maana gani kufanya hivyo. Akawa anamwangalia jinsi alivyojikaza juu hapo, na hapo hapo mlango ukafunguliwa taratibu. Mapigo ya moyo ya Camila yakaanza kupiga kwa kasi pale alipomwona Jaquelin akiwa amesimama mlangoni hapo, lakini hakuingia mpaka ndani baada ya kumwona Camila amesimama usawa wa kitanda.

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★

"Cammy... bado hujalala?" Jaquelin akamuuliza.

Camila akameza mate na kusema, "..aam... yeah. Sijalala bado..."

"Nimesikia kama ulikuwa unaongea mtu," Jaquelin akasema.

Camila akazidi kuingiwa na wasiwasi, lakini akajitahidi kujidhibiti.

"Aam... yeah. Nilikuwa... nilikuwa naongea na simu," akadanganya.

"Aaaa... sawa."

Camila akamtazama kifupi Dylan na kuona jinsi alivyojitahidi kujikaza pale juu. Jaquelin akaongeza hofu ya Camila baada ya kuanza kuingia chumbani akimfata. Dylan akasema kwa sauti ya chini 'shit!' maana alijua vizuri kwamba endapo mama yake angegeuka, basi angemwona. Jaquelin akafika karibu zaidi ya Camila akiwa anatabasamu.

"Alikuwa Felipe bila shaka," akasema Jaquelin.

Camila akatabasamu kihofu-hofu tu.

"Nilikuwa nataka kuuliza, huwa anapenda lobsters (yaani kaa)? Kuna maduka huku makubwa wanauza. Ikiwa na yeye anakula hizo, basi kesho niagize," Jaquelin akasema.

"Ndiyo... huwa anakula. Anapenda," akajibu Camila.

"Ahah... sawa. Dylan asingekuwa anaondoka angekula pia. Anazipenda sana."

Wakati wakiendelea kuongea, Dylan akaona aanze kushuka taratibu bila kutoa sauti yoyote. Alitumia umakini sana, na Camila akatumia akili kwa kuuliza mambo fulani ili kumkengeusha Jaquelin asigeuke nyuma. Dylan akawa amefika chini bila kutoa sauti, na sasa akaanza kuelekea nje ya mlango taratibu mno ili atoke kimya kimya. Baada ya kufanikiwa kutoka ndani hapo, akajibanza kwa nje na kushusha pumzi ya utulivu, kwa kuwa mapigo ya moyo yalimdunda kwa nguvu. Akacheka kidogo kutokana na jinsi jambo hilo lilivyosisimua, kisha akarejea chumbani kwake.

Alikaa kitandani kwa dakika kadhaa, akiwaza kuhusu kilichokuwa kimetokea chumbani kwa shangazi yake. Alijua kwamba jambo sahihi ilikuwa kumwachia Camila kutoka moyoni mwake, lakini bado roho ilimuuma kwa sababu hisia zake kumwelekea mwanamke huyo zilikuwa zenye nguvu sana.

Kimahusiano, Dylan alikuwa amepita kwa wasichana kadhaa ambao mwisho wa siku walimtendea kwa njia yenye kuvunja moyo ijapokuwa alijitahidi kuwaonyesha upendo mwingi. Kwa hiyo kwa kutegemea mambo aliyopitia kutokea kwa mpenzi wake wa kwanza mpaka kufikia kwa Harleen, tayari alikuwa ameshaondoa wazo la kufatilia mwanamke mdogo kwa kuwa wana mambo mengi mno ambayo yalifanya kipimo chake cha imani kuwaelekea kipungue. Lakini alimjua Camila vizuri sana. Aliupenda utu wake. Na kiukweli, ni kama vile alikuwa anatafuta mtu aliye kama Camila ili awe naye, lakini hakuona bado, ijapokuwa Fetty alikaribia. Kwa hiyo hisia zake kwa shangazi yake bado zilikuwa zenye nguvu mno, ila hali waliyokuwa ndani yake haikuruhusu aweze kuzishiriki pamoja naye.

Kijana akaona asiendelee kukazika sana kiakili kuhusiana na jambo hili kwa kuwa haingekuwa na faida yoyote. Akatazama muda na kukuta ni saa 8 usiku tayari, hivyo akajilaza na kuanza kutafuta usingizi.

★★★

Ilikuwa ni asubuhi yenye pilika-pilika upande wa Fetty. Aliwahi mgahawani mapema na kuanza kazi kama kawaida; kusafisha vitu mbalimbali hapo, kusaidia mapishi na kuhudumia wateja. Kwa kuwa walikuwa na kawaida ya kuwapelekea wateja fulani vyakula sehemu mbalimbali za karibu mjini hapo, alisaidizana na wenzake kufanya hivyo.

Ilipofika mida ya saa nne, Dylan akampigia simu kumkumbusha kuwa alipaswa kumpelekea chakula ofisini, kitu ambacho Fetty hakuwa amesahau. Alimwambia angefika ndani ya dakika 15 tu, hivyo akakata simu na kuanza kumwandalia rafiki yake chakula na kukiweka kwenye makontena madogo na masafi sana. Fetty alikuwa mwenye bidii, na hakutaka nafasi hiyo ya kupata pesa impite hata kama aliyemwagiza alikuwa rafiki yake na ilikuwa mbali. Baada ya kuviweka kwenye mfuko, akawaaga wenzake wa hapo mgahawani na kuanza kuelekea huko.

Ilimchukua dakika kadhaa kufika maeneo ya kampuni yao Dylan. Akamlipa dereva wa bajaji, kisha akaanza kuelekea ndani kule, akipendezwa na urefu na umaridadi wa jengo la kampuni hiyo. Akiwa anaelekea juu, alipishana na watu kadhaa ambao walisalimiana naye vizuri, naye akaelekea mpaka kwenye lifti na kuingia ndani. Alikumbukia jana walipokuja na Dylan hapa, jamaa alibonyeza kitufe chenye namba 7, yaani ghorofa ya saba, hivyo akanyoosha kidole chake ili abonyeze kitufe hicho.

Lakini wakati akiupeleka mkono wake hapo, simu yake ikaanza kuita na kumfanya aangalie kuielekea ilipokuwa mfukoni mwa suruali yake; kitu kilichofanya kidole chake kikosee pa kubonyeza, na kubonyeza namba 6 badala ya 7. Milango ya lifti ikafunga, nayo ikaanza kumpeleka juu, akifikiri alibonyeza 7. Akaitoa simu yake mfukoni na kukuta anayepiga ni Dylan, naye akatabasamu kisha kupokea.

"Nini kinakutafuna wewe? Mbona hufiki tu?" Dylan akalalamika.

"Ahahahah... nakaribia bwana," akasema Fetty kwa furaha.

"Umeweka nyama kama zote?"

"Kama zote."

"Okay. Unapakumbuka ofisini kwangu?"

"Ndiyo. Napakumbuka. Si nitakukuta humo?"

"Yah. We ukifika ingia tu, sawa?"

"Haya."

"Haya. Waisha hizo nyama."

Fetty akacheka, na kisha Dylan akakata simu.

Lifti ilipofunguka, Fetty alianza kutembea akivipita vyumba kwa kuhesabu jinsi alivyokumbuka chumba cha ofisi ya Dylan kilipojipanga. Alijua kilikuwa mwishoni, hivyo akapita moja kwa moja mpaka mwisho huko na kuufikia mlango. Kulikuwa na watu wachache hapo, na wengi hawakumkazia uangalifu, hivyo akausukuma mlango na kuingia ndani. Alianza kwa kuchungulia, lakini hakuona mtu. Alipoingia ndani zaidi, aliona ni kama vile mwonekano wa ofisi hii ulikuwa tofauti na jinsi alivyoikumbuka ofisi ya Dylan. Hakukuwa na mtu hapo, naye akawaza huenda amekosea ofisi, au Dylan anamfanyia mchezo.

Alitembea taratibu kuelekea mlango ambao ulikuwa wa chumba chenye makolokolo mengi ya kiofisi. Akafungua mlango na kuingia kuchungulia humo, lakini hakukuwa na mtu. Kwa haraka akawaza bila shaka alikuwa amekosea ofisi, na sasa akataka ageuze ili kurudi nje. Lakini ile anageuka nyuma, akaona mtu anaingia ndani ya ofisi hii, akiwa amevalia suti nyeusi na miwani ya macho. Alikuwa ni Mr. Bernard mwenyewe.

Fetty akaingiwa na wasiwasi sasa, naye akajirudisha ndani ya chumba hicho kidogo. Akashindwa kujua afanye nini maana ameingia kwenye ofisi ya mtu bila ruhusa, huenda hata angeitwa mwizi. Lakini alijua ilikuwa ni kimakosa tu kwamba ameingia hapo, na akawaza kama angemweleza, basi angeelewa.

Bado Mr. Bernard hakuwa amemwona Fetty kwa sababu binti alikuwa ndani kidogo ya chumba kile kingine, akijifikiria atoke ili aongee na huyo mtu mzima. Wakati anataka kutoka, akamwona Mr. Bernard amesimama usawa wa mlango wa chumba hiki alichokuwa ndani yake, akiwa ameweka simu sikioni huku amempa mgongo. Ikabidi Fetty atulie kwanza.

"Ndiyo..." sauti ya Mr. Bernard ikasikika.

"...hakikisha kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga... umeelewa?" akaendelea kusema kwa sauti yenye mkazo.

Fetty akaendelea kumsikiliza.

"...vizuri. Itakuwa kwenye mida ya saa sita. Hakikisha hakuna mtu hata mmoja anayetoka..."

Fetty akakunja uso wake kimaswali. Hakuweza kuelewa mwanaume huyo alikuwa anazungumzia nini, lakini hakikuonekana kuwa kitu kizuri. Akamwona ameshusha simu yake kutoka sikioni.

"Your downfall begins now, Gilbert (kuanguka kwako kunaanza sasa, Gilbert)," akasema Mr. Bernard kwa sauti ya kikatili.

Fetty alishangaa sana, na alijiuliza maswali mengi mno. Hakuwa na ma-degree ya kisomi lakini alielewa kile ambacho Mr. Bernard alisema. Alielewa jina hilo la Gilbert ni la baba yake Dylan, na bila shaka mwanaume huyu alipanga kufanya jambo fulani ambalo lingemdhuru baba ya rafiki yake. Kilichokuwepo ilikuwa ni kuhakikisha anamfikishia Dylan jambo hili ili kumwonya kuhusu hatari ambayo ingeweza kumkabili baba yake.

Mr. Bernard akaelekea mezani kwake na kupitia mafaili fulani, bila kutambua kulikuwa na mtu ofisini kwake. Fetty akaendelea kutulia humo humo ndani, akiombea jambo fulani litokee ili mwanaume huyo aondoke, ili naye aweze kutoka. Ilikuwa ni kama Mungu alijibu sala yake, kwa kuwa ndani ya dakika chache, Mr. Bernard alitoka ofisini hapo na kuelekea alikojua yeye.

Bila kupoteza wakati, Fetty akatoka kwenye chumba hicho na kwenda mpaka mlangoni. Akachungulia nje, na hakuweza kumwona Mr. Bernard, hivyo akatoka haraka na mifuko yake akielekea upande wa ngazi za jengo. Akatulia hapo na kutoa simu yake, kisha akampigia Dylan. Akamwambia alikuwa amefika lakini alisahau ofisi yake ilipokuwa, hivyo Dylan akamwelekeza vizuri, na sasa Fetty akaelewa cha kufanya.

Haikuchukua dakika nyingi, naye akawa amefika ofisini kwa jamaa. Alimkuta ameketi kwenye sofa lake huku anaangalia muziki wa kilatini (aina ya reggaetón), na baada ya kumwona Fetty, Dylan akanyanyuka akiwa anatabasamu.

"Finally!" Dylan akasema kwa shauku.

"Ahah... pole nimechelewa. Nilipotea," akasema Fetty.

"Si nilikuuliza kama bado unapakumbuka ukasema 'ng'weee,' kilichokupoteza nini sasa?" Dylan akamtania.

"Ahahahah... lione kwanza," Fetty akamwambia na kumpiga ngumi nyepesi begani.

"Mmmm... hapa nitakamua mpaka nisahau kula siku nzima," akasema Dylan baada ya kuvitoa vyakula.

"Kwa hiyo kweli ilikuwa lazima ule chakula hiki?" akauliza Fetty.

"Ndiyo. Nilikuwa nataka nikuone na wewe pia," Dylan akasema bila kumtazama.

Fetty akamwangalia kwa hisia sana. Aliyapenda sana maneno ya Dylan, na kila siku ilikuwa ni kama jamaa alikuwa anampa sababu ya kuvutiwa naye hata zaidi. Akawa anauangalia uso wake, huku Dylan akitoa chapati na kuikunja, kisha akaichovya kwenye supu na kuanza kula kwa hamu kubwa.

"Mmmm... delicioza (tamu)," akasifia.

"Ahahah..." Fetty akacheka huku anamwangalia.

"Nitabeba na nyama kwenye helicopter. Nikifika kule nazila zote," akasema Dylan.

"Wacha! Unaenda kwa helicopter kumbe?"

"Yeah. Usingechelewa ningekula huku nimekaa."

"Kwani unatakiwa uondoke saa ngapi?"

"Ilikuwa niondoke saa 6, ila ratiba imebadilika. Chopper inatua hapa saa 5... ikiwezekana nitarudi leo leo," Dylan akatania, kwa kuwa asingerudi kwa siku kadhaa.

"Saa 6?" Fetty akauliza.

Dylan akatikisa kichwa kukubali na kubugia nyama.

Kitendo cha Dylan kusema saa 6 kilimkumbusha Fetty kuhusu Mr. Bernard. Aliongelea kuhusu jambo fulani ambalo lingetokea saa 6 pia, na lilihusiana na Gilbert. Akatambua huu ulikuwa muda mwafaka wa kumwambia Dylan alichosikia.

"Dylan..." akamwita.

"Mmm..." jamaa akaitika huku anakunywa supu.

"Wakati ule...wakati nimepotea ofisi...niliingia kwenye ofisi ya..."

"Umeingia kwenye ofisi ya mtu? Ahahahah... usiniambie umetimuliwa!" Dylan akamtania.

"Ahah... hapana. Hakuniona. Nilijificha."

"Wewee! Ilikuwa ofisi ya nani?"

"Simjui...ni mbaba mtu mzima. Ni...mnene kiasi, mweusi afu'...amevaa miwani ya macho hivi...ana kipara..."

"Aaaaa unamwongelea Mr. Bernard," Dylan akamjuza.

"Nafikiri ndiyo huyo."

"Huwaga ananikera na kitambi chake huyo! Ni vizuri hajakuona maana angeanzisha timbwili."

"Well... nilimsikia alikuwa anaongea kwenye simu... na mtu fulani sijui nani..." Fetty akaanza kufunguka.

"Mm-hmm..." Dylan akatega sikio kwa makini.

"Walikuwa wanaongelea kuhusu..."

"Mr. Dylan..."

Sauti hiyo ikamkatisha Fetty ghafla. Wote wakatazama mlangoni na kumwona Mr. Bernard akiwa amesimama hapo. Fetty aliingiwa na wasiwasi kiasi, huku Dylan akimpuuzia jamaa na kuendelea kula. Mr. Bernard akaweka tabasamu la bandia na kuwasogelea. Fetty akarudi nyuma kidogo ili kuwaachia nafasi.

"Nani huyu?" Mr. Bernard akauliza.

"Ni rafiki yangu. Unasemaje?" Dylan akamuuliza.

"Aam... najua unaondoka, nilikuwa nimekuja kukuaga," Mr. Bernard akasema kinafiki.

"Kila mara nikiondokaga ofisini huwa hauniagi, kulikoni leo?"

"Ahahahah... ni kwa sababu unaenda mbali Mr. Dylan."

"Okay. Asante. Kuna kingine?"

"Aaaa... kuna paperwork nyingi sana za kufanyia kazi kutokana na mambo uliyoyaingiza hapa, sanasana insurance certificates na material orders. Process ziko slow kwa hiyo..."

"Kampuni kufanya kazi primarily paperless ni kitu ambacho mlikuwa mnatakiwa kuwa mmefanya kitambo sana. Mbona ziko njia na system nyingi za ku-deal na document management, iwe ni categorization, due dates, project deadlines.... acheni uvivu...em'...niache tu kwanza maana napata msosi hapa. Kadili na hayo masuala mwenyewe," Dylan akamwambia kwa kukereka.

Mr. Bernard alichukizwa sana na Dylan, kwa kuwa alihisi kwamba Dylan ni mtoto mdogo sana kuweza kumzidi akili namna hiyo, na hasa kwa sababu hakuwa ameitumikia kampuni kwa muda mrefu kama yeye. Akatoa tabasamu bandia, akijifanya mwema sana.

"Sawa nimeelewa.... boss," akasema Mr. Bernard kikejeli.

Dylan akamtazama kwa ukali, naye Mr. Bernard akageuka na kumwangalia Fetty. Akamshusha na kumpandisha, kisha akatoka ofisini hapo akiwa ameudhika. Dylan akatikisa kichwa chake na kuendelea kula.

"Si ndiyo huyo weasel uliyekuwa unamsemea?" akamuuliza Fetty.

Fetty akasogea karibu zaidi na kukubali.

"Anajifanyaga anajua sana huyo. Yaani huwa namnyoosha, mpaka nitahakikisha hicho kitambi kinaporomoka," akasema Dylan.

"Ndiyo, anaonekana ni mwenye hila sana. Nilikuwa nakwambia..."

"Sir Dylan... helicopter imefika."

Fetty akakatishwa tena na sauti hiyo nyingine mlangoni pale. Alikuwa ni mfanyakazi wa hapo.

"Already?" Dylan akashangaa.

"Ndiyo sir."

Dylan akashusha pumzi kwa kukwazika, kisha akasema, "Okay fine nakuja. Nenda waambie ninakuja."

"Okay sir."

Mfanyakazi huyo akaondoka, kisha Dylan akamwangalia Fetty.

"Time's up (muda umekwisha)," Dylan akasema huku anatabasamu.

Fetty akawa anamwangalia machoni kwa hisia.

"Asante kwa chakula. Nimefurahia ijapokuwa hawa wahuni wananiwahisha mno," akasema Dylan huku anatoa wallet yake.

Akampatia Fetty laki moja. Binti akashangaa.

"Dylan nini hiki?" akamuuliza.

"Najua, najua. Haijafika milioni moja uliyosema jana. Usijali nikirudi nitamalizia deni," Dylan akatania.

"Lakini Dylan... mbona unapenda kuchezea pesa sana?" Fetty akauliza.

"Sijazichezea. Nimekupa wewe. Ikiwa huzitaki fanya lolote lile unaloona ni sawa, maana siyo zangu tena... ni zako," Dylan akamwambia huku anachukua simu yake.

Fetty akakosa cha kusema. Dylan akamshika shavu lake la kushoto, kisha akambusu la kulia.

"Tutaonana tena my friend... ngoja niwahi," akamuaga.

Fetty alikuwa anamtazama kwa hisia nyingi sana. Hata lile wazo la kumwambia kuhusu alichosikia Mr. Bernard anasema kwenye simu, likatoweka. Akili yake na hisia zake zilikuwa zimesharuka mbali kutokana na kupenda sana mambo yote Dylan aliyoyafanya kwa ajili yake. Jamaa akachukua rimoti na kuzima TV, kisha akaelekea mlangoni na kumgeukia Fetty, akiachia tabasamu la kirafiki.

"Usipotee tena ukitoka," Dylan akasema, kisha akaondoka sehemu hiyo.

Fetty alibaki ofisini hapo, akiwaza kuhusu jinsi Dylan alivyokuwa mwenye kumfanya ajihisi wa pekee sana. Akajishika shavu lake, akikumbukia jinsi midomo ya jamaa ilivyolipiga busu laini iliyomsisimua kwa kiasi fulani. Akakusanya vyombo vyake, kisha akaondoka kutoka kwenye jengo hilo ili arudi kule mgahawani.

Njia nzima kurudi kule alimfikiria tu Dylan, na sasa jambo moja likawa wazi kwake... alimpenda. Akatabasamu kwa hisia nyingi sana za upendo wa dhati aliohisi kumwelekea, akijishauri akilini mwake kuwa pindi ambapo kijana huyo angerudi, angemfunulia kilicho moyoni mwake.

★★★

Upande wa juu kabisa wa ghorofa, helicopter ilisimama hapo huku chuma lake la juu likizunguka kwa kasi. Dylan akawa amefika hapo na kumkuta baba yake, Gilbert, akiwa pamoja na wanaume wengine watatu. Wakaongea naye kuhusu safari hiyo, wakimtakia mkutano na kazi njema huko ambako angeenda. Akaagana na baba yake pia, akimwambia amfikishie heri zake mama yake pia, ambaye alikuwa bize na mambo fulani.

Kisha, Dylan akaongozana na mwanaume mmoja kati ya wale waliokuwa hapo mpaka kwenye helicopter na kupanda pamoja naye. Rubani alikuwa ni mwanaume mzungu, naye akasalimiana nao, kisha akaanza kuinyanyua helicopter angani. Gilbert akawa anampungia mkono mwanae, na baada ya helicopter kufika mbali, akarejea kwenye ofisi yake.

Zilipita dakika chache wakiwa angani, nayo helicopter ikatua chini. Dylan akauliza mbona kama wamewahi sana, naye rubani akasema kuna mtu fulani alikuwa anampitia hapo. Na kweli akafika mwanaume fulani, ambaye alijitambulisha kuwa rafiki wa rubani huyo ambaye alikuwa akielekea mkoa walioenda pia, hivyo wakamkaribisha vyema na helicopter ikarudi angani. Dylan alijitahidi kuongea nao na kuwafanya wapendezwe naye sana kwa kuwa alifurahisha mno. Wakaendelea kupiga story huku mara kwa mara wakiangalia jinsi mwonekano wa kule ardhini ulivyopendeza kutokea angani.

"Naona kama vile ni ngumu sana," akasema mwanaume wa kwanza.

"Hapana siyo ngumu wala," Dylan akajibu.

"Ulishawahi kujaribu?" mwanaume wa pili akamuuliza.

"Ndiyo tayari. Ni rahisi mno kama hauogopi kupita kiasi," Dylan akasema.

Walikuwa wanaongelea kuhusu jinsi ya kutumia parachuti. Mwanaume wa kwanza hakujua jinsi ya kutumia, na alifikiri ni ngumu sana.

"Hata humo kwenye hilo begi imo," akasema mwanaume wa kwanza.

"Eee ndiyo. Yaani unavaa, halafu... ngoja nikuonyeshe," akasema Dylan.

Kisha akafungua mikanda ya usalama aliyokuwa ameifungia mwili wake, na kulichukua begi la parachuti ili awaonyeshe mfano.

"Mr. Dylan, kuwa mwangalifu!" mwanaume wa kwanza akamwonya.

"Usihofu niko sawa."

Akalivaa begi hilo.

"Okay, umeona... hizi kanda unazifunga tu ili kubana mwili wako na begi, halafu hiki kikamba ndiyo unachotakiwa kukivuta wakati unataka kulifungua parachuti," Dylan akawaelezea.

"Eee ndiyo naonaga wanafanya hivyo. Wanapovuta begi linakuwa kama linachanika," akasema mwanaume wa pili.

"Ahahah... siyo kuchanika, per say, yaani inakuwa ni kama inaifungua zipu ili parachuti litoke," akasema Dylan.

"Aaaa... kwa hiyo unapovuta, inafunguka halafu inatoka?"

"Ndiyo. Kwa mabegi mengine inakuwa kama inaisukuma kwa juu, kwa hiyo ukivuta ina...."

Ghafla helicopter ikatoa kishindo cha nguvu sana kutokea juu! Wote walishikwa na taharuki kwa kutoelewa nini kilikuwa kinaendelea. Helicopter ikaanza kupoteza mwelekeo mzuri na kuanza kuzunguka bila mpangilio maalumu, huku rubani akijitahidi kuidhibiti bila mafanikio.

Kwa kuwa Dylan alikuwa ameifungua mikanda maalumu ya usalama kutoka mwilini mwake, aliweweseshwa huku na huku, akijitahidi kujiweka sawa ili atulie sehemu moja, lakini akawa anashindwa. Wengine walipiga kelele wakiuliza nini kinatokea, na sasa kasi ya kuzunguka ya helicopter ikazidi. Hii ikasababisha lock ya mlango wa helicopter ijifungue na kumrusha Dylan nje kwa nguvu sana!

Kwa kuwa wengine walikuwa wamekazwa na mikanda kwenye siti zao, hawangeweza kutoka hapo hata kidogo. Walihofia sana kuhusu uhai wa Dylan, na usalama wao pia.

JE, WATI DO YU SINKI WILI HAPENI?

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★

Dylan aliendelea kudondoka kuelekea chini kwa kasi, huku mwili wake ukizunguka-zunguka ovyo ovyo sana. Alikuwa akijaribu kuishika kamba ya kuvutia parachuti ili lifunguke kutoka kwenye begi, ambalo bado lilikuwa mgongoni kwake, lakini akawa anashindwa kuipata kutokana na upepo kuirusha huku na huku. Alianza kuona kuwa alikaribia chini zaidi sasa, na kwa ustadi akajikunja na kujiviringisha angani hapo ili aweze kuuweka mwili wake sawa, kisha akafanikiwa kuishika kamba hiyo na kuivuta kwa nguvu.

Parachuti lilifunguka, lakini kutokana na kasi yake lilipofunguka, ilifanya mwili wa Dylan urudi juu kidogo kwa kushtukiza, hivyo kasi yake ya kudondoka ikapungua, lakini tatizo lingine likatokea. Kwa kuwa hakuwa ameifunga mikanda ya begi kifuani, ilifanya mikono ya begi iteleze kutoka mabegani kwake na hivyo begi hilo kumtoka mgongoni! Alikuwa amekaribia chini sana, na baada ya begi kumtoka, akaanza kuanguka huku anapiga kelele za hofu.

Mwili wake ulidondokea kwenye kamba nene iliyokuwa ya kivuko/daraja refu la kamba, ambalo lilikuwa juu katikati ya miamba miwili mikubwa ya bwawa pana sana la maji yenye kina kirefu. Baada ya kujigonga hapo, akaanza kuangukia chini huko na kudumbukia ndani ya bwawa kwa nguvu sana, na mwili wake ulipokuwa unazama chini, kichwa chake kikajigonga kwa nguvu kwenye jiwe kubwa ndani ya maji hayo.

Upande wa helicopter, rubani alijitahidi sana kurudisha chombo hicho kwenye utaratibu mzuri, lakini jitihada zake zikaendelea tu kugonga mwamba. Helicopter iliendelea kuzunguka na kwenda ovyo ovyo, na kwa dakika kadhaa baadae, ikaishiwa nguvu yote na kuanza kuelekea chini kwa kasi sana; hapo ikiwa imevuka mikoa michache toka ilipoanza kuleta shida. Kwa kusikitisha sana, iliangukia sehemu ya mbali ambayo ilikuwa na mlima, na yote ikalipuka.

★★★

Huzuni, simanzi na majonzi vilitawala familia nzima ya Dylan baada ya kuwa wamepata taarifa kuhusu ajali iliyompata kijana huyo. Walisafiri haraka kuelekea mkoa ambao helicopter iliangukia, na baada ya kufika huko, waliweza kuonyeshwa miili mitatu ambayo ilikuwa imeungua sana na kuwa myeusi yenye kutisha. Gilbert alikumbuka kuwa, Dylan alipanda helicopter pamoja na mwanaume mwingine wa kampuni yao, hivyo ukijumuisha na rubani bila shaka walikuwa watatu. Kwa hiyo kwa haraka wote wakajua kwamba Dylan pia alikuwa amepoteza maisha kwenye ajali hiyo. Walilia sana.

Camila pamoja na mchumba wake walikuwepo pia, naye alimwombolezea mpwa wake kwa uchungu mwingi sana moyoni, ukitegemea hawakuwa wameachana kimtazamo mzuri.

Walifanya msiba baada ya siku chache, kukiwa na ndugu na marafiki wa karibu waliofika kuwafariji. Aliyepoteza matumaini kabisa alikuwa ni Jaquelin. Hakula vizuri, hakuongea, angelia mara kwa mara na kuanza kupiga-piga vitu walipokuwa nyumbani, na hakutoka nyumbani kwa siku nyingi. Muda mwingi angelala tu kitandani akiwa anaangalia picha za Dylan huku analia kwa huzuni, na mambo yote haya yalimvunja sana Gilbert.

Fetty aliumia sana. Alihisi ni kama mikosi kwake isingeisha kamwe. Dylan alikuwa ni kitu kizuri sana kuwahi kuingia kwenye maisha yake. Kuna msemo wa kwamba mtu huwa hatambui umuhimu wa kitu alichonacho mpaka anapokuja kukipoteza, naye Fetty alihisi ni kama msemo huo ulimfaa yeye kwa sababu ijapokuwa nafasi ilikuwepo kabisa ya kuwa pamoja na Dylan kimahusiano, hakupiga hatua hiyo. Hivyo alijilaumu kuwa alikuwa akichezea muda tu wakati angekuwa ameshamwambia mapema kuwa alimpenda. Kutokea hapo, mwanadada huyu hakuwa na furaha tena moyoni, kwa kuwa kitu kilichompatia furaha kilikuwa kimepotea.

Camila alirudi Brazil na mchumba wake baada ya miezi mitatu. Hawakuwa wamepanga kukaa muda mrefu hivyo, lakini baada ya mambo hayo yasiyotazamiwa kutokea, Camila alihitaji kuwa na ndugu zake karibu zaidi. Lakini kwa kuwa walihitaji kuendelea na kazi, ilibidi warudi Brazil sasa; Camila akimuahidi Jaquelin kuwa angeendelea kuwasiliana naye kila siku.

Kufikia wakati huu, Gilbert alikuwa anaendelea kujitahidi kuweka mambo sawa kwenye kampuni, kwa kuwa baada ya Dylan "kufa," mipango mingi iliyokuwa ikiendeshwa naye iliharibika. Ijapokuwa Gilbert alijitahidi sana kuongoza mambo vyema, vizuizi vya kimakusudi kutoka kwa watu waliotaka aporomoke vilimrudisha nyuma; na wakati huu ilikuwa ni kama anapoteza mwelekeo kwa kuhisi yuko mwenyewe. Jaquelin alianza tena kwenda kwenye kampuni, lakini akili yake haikukazia fikra kabisa kazi, bali ni mwili wake tu ndiyo ulikuwa pale.

Maisha ya wawili hao yaliendelea kuwa yenye misukosuko zaidi kadiri siku zilivyoendelea kwenda, na haikuonekana kama wangeweza kupata ahueni tena.

★★★

Dylan anafumbua macho yake taratibu, akiwa anahisi kama ametoka kwenye usingizi mzito. Anatazama sehemu aliyopo na kutambua ni chumba fulani. Anapojaribu kugeuza shingo, anahisi maumivu yanayofanya akunje sura yake kwa hisia za kuumia. Kichwa chake kinamuuma sana, naye haelewi kwa nini iko hivyo.

Kisha anasikia sauti pembeni yake ikisema, "...ameamka... nyie... ameamka..." naye anatambua sauti hii ni ya mvulana mdogo, lakini hawezi kumwona kwa kuwa hawezi kuigeuzia shingo yake upande huo.

"Emmy, kamwite dokta..."

Anasikia sauti hiyo nyingine ikisema hivyo. Hii ni ya mwanaume mtu mzima, lakini hatambui ni nani. Kisha hapo hapo mwanaume fulani anasogea karibu na uso wake na kuanza kumwangalia-angalia usoni mwake. Hamtambui hata kidogo, kisha anakuja mwanaume mwingine na kuanza kumkagua usoni; analimulika jicho lake kwa tochi ndogo, anatumia kifaa cha kusikilizia mapigo ya moyo kusikiliza ya kwake, kisha anamuuliza Dylan anahisije mwilini.

Dylan akaanza kuzungusha macho huku na huku bila kutoa jibu lolote. Mwanaume huyo, daktari, akaanza kuongea na yule mwanaume mwingine pembeni. Alikuwa anamwambia kwamba mgonjwa anaonekana kuwa na shida kwenye ubongo, hivyo angehitaji kupelekwa hospitali kubwa zaidi. Dylan akamsikia mwanaume huyo mwingine akimwambia daktari kuwa hana pesa ya kumgharamia na kumpeleka kwenye hospitali kubwa, kwa kuwa alimpata tu akiwa kwenye hali mbaya, hivyo akamsaidia na kumleta hapo kwenye zahanati hii.

Mwanaume huyo akamuuliza daktari shida ya mgonjwa kwenye ubongo ni nini, naye daktari akasema atahitaji kumfanya mgonjwa aongee ili aweze kuwa na uhakika zaidi, ndipo atoe jibu. Dylan alisikia vizuri walichokuwa wanasema, lakini HAKUELEWA kilichokuwa kinaendelea. Daktari akamsogelea tena, kisha akanyanyua vidole viwili mbele ya uso wa Dylan huku anamwangalia kwa makini.

"Hii ni ngapi?" daktari akauliza.

Dylan akaukazia macho mkono wa daktari, kisha akasema, "Mbili."

Daktari akafurahi kuona ameweza kuongea na kutoa jibu kwa usahihi, kisha akamwangalia macho tena kwa kuyavuta-vuta.

"Unaitwa nani?" daktari akamuuliza tena huku anamwangalia.

Dylan akafungua mdomo ili ajibu, lakini akabaki ameachama bila kutoa neno lolote. Akaanza kupeleka macho huku na huku, akionekana kutafuta jibu. Daktari akarudia tena kumuuliza jina lake ni nani, lakini Dylan akawa amekunja tu uso huku anaonyesha kutangatanga kiakili. Daktari akamtuliza kwa kumwambia asijilazimishe maana kichwa kingeanza kumuuma, kisha akamgeukia yule mwanaume aliyemsaidia Dylan.

"Inaonekana atakuwa amepoteza kumbukumbu," daktari akamwambia.

"Mh! Sasa itakuwaje?" mwanaume huyo akauliza.

"Tumchukue tumpeleke nyumbani," akajibu mvulana yule mdogo.

Mwanaume huyo akamwangalia Dylan kwa wasiwasi.

"Sasa dokta, ikiwa anaweza kukumbuka namba mbili, anashindwaje kukumbuka jina lake?" akamuuliza.

"Aam... kumbukumbu ni pana. Na mara nyingi kwenye visa vya kupoteza kumbukumbu, watu husahau hasa mambo mengi kuhusu maisha waliyoishi, lakini vitu vichache walivyofundishwa mara nyingi hubaki kwenye ubongo. Ndiyo maana unaona hajasahau kiswahili," daktari akaeleza.

"Ee ndiyo baba. Ndo' maana unaona anaweza kuongea, la sivyo asingesema chochote," akasema binti ya mwanaume huyo, aliyeitwa Emilia.

"Hahah... angekuwa kama litoto anafanya bhabhabha..." akasema mvulana yule, na wote wakacheka kidogo (isipokuwa Dylan).

"Nini kinaendelea? Nimefikaje hapa? Kwa nini sikumbuki vitu?" Dylan akauliza kwa wasiwasi.

Daktari akamsogelea na kusema, "Pole sana. Inaonekana ulipatwa na ajali, na sasa... ukaangukia vibaya jiwe kubwa na kukipiga kichwa chako kwa nguvu. Kwa hiyo sehemu kubwa ya ubongo wako iliyotunza kumbukumbu imevurugika," daktari akaelezea.

"Ajali? Jiwe? Mbona sikumbuki?" akasema Dylan kwa huzuni.

"Usijali. Tatizo hili litaisha baada ya muda fulani kupita. Atahitaji dawa za kusaidia maumivu ya mishipa ya shingo, nitakuandikia," daktari akamwambia mwanaume yule.

Kisha daktari akaondoka kwenda kwa wagonjwa wengine, akiwaacha wote hapo.

"Sasa baba, kama amepoteza kumbukumbu atarudije kwao?" Emilia akamuuuliza baba yake kwa sauti ya chini.

"Nitamsaidia kutafuta alikotokea. Nafikiri kuna watu eneo hili wanaomfahamu," akajibu.

Dylan alikuwa anaangalia huku na huku kwa wasiwasi, akijaribu kuvuta picha ya mambo mengi, lakini anashindwa kukumbuka. Mwanaume huyo akamsogelea na kuketi kitandani akimwangalia, naye Dylan akamwangalia pia.

"Hujambo? Naitwa Baraka, mimi ndiyo nilikusaidia na kukuleta hapa," mwanaume huyo akasema.

"Asante. Nini kilinipata?" Dylan akauliza kwa hisia.

"Sijui kwa kweli. Nilikuwa kwenye mtumbwi na mwenzangu, tukijaribu kuvua dagaa wachache bwawani. Nikakuona ukiwa chini ya maji kwa sababu ya... shati lako jeupe, kwa hiyo tukakutoa, na ulikuwa umepoteza fahamu. Kichwa chako kilikuwa kimevimba kwa nyuma huku damu zinakutoka, kwa hiyo tukakuwahisha hapa kwa sababu bado ulikuwa hai..." Baraka akaelezea.

Dylan akanyanyua mkono wake na kujishika kichwani. Akatambua alikuwa amefungwa bendeji kuzungukia kichwa chake, kisha akafumba macho kwa huzuni.

"Haukumbuki kitu chochote kabisa?" akauliza Emilia.

Dylan akafumbua macho na kumtazama Emilia. Aliweza kumwona akiwa amesimama pembeni kidogo, huku akiwa ameikunjia mikono yake kifuani.

"Kuna vitu najua. Najua wewe ni msichana... najua hiki ni kitanda... najua hapa tuko hospitali...aam, zahanati..." Dylan akasema.

Baraka akatabasamu kwa kutambua kuwa Dylan alikuwa mwerevu.

"Lakini vitu vingi vya maisha yangu sivijui... aah... ni hisia mbaya sana," akasema Dylan.

Wote walimwonea huruma sana.

"Usihofu. Kama dokta alivyosema, usijilazimishe... itarudi yenyewe. Jipe tu muda," Baraka akamtia moyo.

Dylan akashusha pumzi taratibu, kisha akauliza, "Nimekuwa hapa kwa muda gani?"

"Siku...6. Tokea tulivyokutoa kwenye maji," Baraka akajibu.

"Haionekani kwamba nilikuwa humo muda mrefu?" Dylan akauliza.

"Hapana. Inaonekana ulidumbukia siku hiyo hiyo tuliyokutoa, la sivyo tungekuta umekufa," Baraka akamwambia.

Dylan akatulia kidogo.

"Hawa ni wanangu. Huyu ni Emilia, na huyu mdogo ni Steven," Baraka akawatambulisha wanae kwa Dylan.

Dylan akatabasamu kidogo, na watoto wa Baraka wakatabasamu pia kirafiki.

Waliendelea kukaa na Dylan kwa muda fulani, kisha wakaondoka na kumwacha chini ya uangalizi wa wauguzi.

★★★

"Hivi kweli baba Leila... unawezaje kufanya uamuzi huo?"

"Kwa hiyo unataka nimwache tu kijana wa watu?" akajibu Baraka.

"Ina maana hana familia? Waje wamchukue! Wewe unataka kutuletea hapa mtu ambaye hatumfahamu hata kidogo. Unajua vipi tabia zake? Je kama ni jambazi?"

"Mama Leila, usiwe hivyo. Yule kijana anahitaji msaada. Hana pa kwenda kwa sababu hakumbuki maisha yake. Siwezi kumwacha tu mpaka nimsaidie arudi kwao..."

"Lakini si kuna watu maalumu wa kumtafutia? Kwa nini wewe? Umemmwokoa asizame, umempeleka zahanati, umemtolea hela ya matibabu ambayo tungetumia hapa nyumbani, inatosha. Sasa sa'hivi unataka tena kumleta hapa ili iweje? Aagh..."

Haya yalikuwa ni maongezi kati ya Baraka na mke wake. Ilikuwa imepita wiki moja sasa tokea Dylan alipoamka, na daktari alisema yuko vizuri kimwili kuweza kutoka zahanati hapo. Lakini shida ilikuwa kwamba Dylan hakukumbuka vitu, kwa hiyo hangekuwa na pa kwenda. Baraka alikuwa ametumia muda huo wa wiki kuulizia sehemu za maeneo yao ikiwa kuna kisa cha mtu kupotea, lakini hakupata mtu aliyeonekana kufahamu upotevu wa Dylan.

Baadhi ya watu waliofahamiana na Baraka walikuwa wameenda pamoja naye zahanati ili kumwona Dylan, lakini wote hawakumtambua hata kidogo. Sasa kijana huyo angetakiwa kuondoka zahanatini kesho, na Baraka alikuwa anafikiria kumpa hifadhi nyumbani kwake wakati wakiendelea kutafuta watu ambao wangemfahamu. Jambo hill lilikuwa limemkera sana mke wake, ambaye aliona ingekuwa kuongeza mzigo tu kwenye maisha yao ikiwa wangemleta Dylan hapo.

"Mimi ndiye nitakayewajibika kwa ajili yake. Wewe niamini mimi," Baraka akamwambia.

"Maisha yetu kama unavyojua ndiyo hivyo... hayaeleweki. Wewe kuanza kujifanya msamaria mwema kutaongeza tu..."

"Aagh mama Leila! Nimeshasema anahitaji msaada, na nitamwajibikia mimi. Hebu acha basi kulalamika... agh!" Baraka akamwambia akiwa ameudhika.

"Sawa, utajua mwenyewe," mke wake akamwambia kwa kukerwa.

Akatoka hapo kwenye kochi walilokuwa wameketi na kuelekea chumbani akiwa amekasirika. Baraka akabaki sebuleni akitafakari mambo kwa makini, bila kujua kwamba binti yake mkubwa, Leila, alikuwa akiwasikiliza kutokea pembeni akiwa amejibanza.

Baraka alikuwa na familia yenye mke mmoja na watoto watatu. Binti yake wa kwanza ndiye aliyeitwa Leila, na alikuwa na umri wa miaka 22. Binti yake wa pili aliitwa Emilia, naye alikuwa mwenye miaka 18. Mwana wake wa tatu aliitwa Steven, naye alikuwa na umri wa miaka 11. Jina la mke wake lilikuwa Shani, lakini alizoea kuitwa mama Leila na wengi.

Baraka alikuwa mwanaume mstaarabu sana. Alikuwa ana ujuzi wa masuala ya makarai; alitengeneza majiko ya vyuma, mageti, nguzo za chuma, na alirekebisha mambo mengi yaliyohusisha vyuma. Hii ndiyo iliyokuwa kazi yake tokea zamani sana ambayo ilimpatia kipato kidogo kwa ajili ya kutegemeza familia yake. Eneo waliloishi lilikuwa mbali kutokea na sehemu aliyofanyia kazi, ambayo ilikuwa kama soko dogo la biashara ambako watu wengi walifanya kazi zao.

Mke wake, Shani, alikuwa mwanamke mwenye kujiamini na mkali kiasi. Mara nyingi ungekuta akiwafokea-fokea watoto wake kwa vitu vidogo vidogo tu, nao walikuwa wameshamzoea. Alikuwa anafanya kazi ya upishi, yeye kama maman'tilie, kwenye mgahawa wake mdogo eneo la soko lile la biashara. Alikuwa mwenye mwili mnene kiasi, lakini haukuwa na manyama mengi, bali uliofanya umbo lake lionekane vyema kwa kutokeza kalio lake kubwa vizuri kwa nyuma. Alipenda sana kuvaa nguo za kujiachia na kujiremba; ili kufanya aonekane kama binti mdogo bado!

Leila, binti mkubwa wa Baraka, alikuwa mwanamke mwenye kujiamini, mkaidi, na mwongeaji sana. Alikuwa amemaliza kidato cha nne miaka kadhaa nyuma na kwenda kwenye chuo cha ufundi, lakini akaachana na masuala ya shule ili akazie fikira biashara. Kwa kukosa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara, alianza kufanya kazi kama muhudumu kwenye mgahawa fulani, tofauti na wa mama yake, na aliendelea kuwa hapo kwa miezi kadhaa. Leila alikuwa mwenye umbo zuri, nene kidogo lakini lililojikata kike sana, na hips na kalio lake vilitokeza vyema. Alikuwa na uso mzuri, naye alipenda kusuka rasta za kuchanganya rangi, na nguo nyingi alizopendelea kuvaa zilikuwa ni dera.

Emilia, binti wa pili, alikuwa msichana mstaarabu, mpole na mwenye akili sana. Wakati huu alikuwa kidato cha nne, akikaribia kumaliza masomo ya sekondari. Alikuwa mzuri pia kisura na kitabia, huku umbo lake lililonona pia likiwatamanisha wanaume wengi, ambao walikuwa wamejaribu sana kupita hapo ila binti akawagomea. Alikuwa anajiheshimu, na alipatana vizuri sana na baba yake.

Kisha kuna dogo Steven, ambaye ni mwana, na mtoto wa mwisho wa Baraka na Shani. Alikuwa mvulana mjanja, mtundu, mwongeaji, na mwerevu pia. Alikuwa darasa la 6 wakati huu, na alisoma kwa bidii pia ili afanikiwe kuingia darasa la 7 mwaka ujao.

Hiyo ndiyo ilikuwa familia ya bwana Baraka. Alikuwa amejenga nyumba ya kawaida yenye vyumba vinne ndani; kimoja kama sebule, kimoja cha kulala yeye na mke wake, kimoja cha kulala Leila na Emilia, na kingine cha kulala Steven. Walikuwa na jengo lingine dogo kwa nje ambalo lilitumiwa kama jikoni, na choo na bafu vilikuwa nje pia.

Walikuwa na shamba kwenye eneo hilo hilo ambalo walipanda mazao fulani waliyotumia kama chakula na kufanyia biashara kwenye kazi ya Shani. Nyumba za majirani wengi hapo zilikuwa kwa umbali fulani kutoka kwa moja na nyenzake, hivyo hawakubanana hata kidogo. Ilikuwa ni eneo kwenye mwinuko mkubwa sana, ambao ulikuwa na bwawa kubwa sehemu za mbele, lililotenganisha mwamba wa eneo hilo na mwamba mwingine kufikia upande wa pili wa mtaa huo; ambao ndiyo ulikuwa wenye eneo la biashara.

Katikati ya bwawa hilo, kutokea kwenye kingo za miamba hiyo, lilijengwa daraja refu la kamba na shaba ngumu kama kivuko kufika upande mwingine, lakini kivuko/daraja hili lilikuwa limeharibika katikati kwa muda mrefu sasa, na halikuwa limetengenezwa. Wenyeji wa upande huu wa eneo hili waliloishi familia ya Baraka walikuwa wameshajaribu kuomba msaada kutoka kwa diwani wao, lakini kwa sababu fulani hakuwa ametoa msaada na kuwapuuzia tu.

Ni daraja hili ndiyo ambalo Dylan aliangukia juu ya kamba yake ya kulishikilia siku ile aliporushwa nje kutoka kwenye helicopter, na wakati amedumbukia bwawani, Baraka alikuwa pamoja na rafiki yake kwenye mtumbwi wakitafuta dagaa kwa ajili ya chakula, ndiyo akaweza kumtoa baada ya kumwona kwenye maji.

Baada ya muda fulani, Baraka pia akaelekea chumbani ili kupumzika, baada ya kuwa amekorofishana na mke wake kuhusu kumleta Dylan hapo kwao. Ilikuwa ni usiku, hivyo walijua watoto walikuwa wamelala, pasipo kujua Leila alikuwa anasikiliza maongezi yao.

★★★

Asubuhi ilipofika, Baraka alielekea zahanati ili kumfata Dylan. Dylan angeweza kutembea vizuri, lakini kwa uangalifu sana ili asitie kichwa chake mtikiso ambao ungemuumiza, kwa kuwa alikuwa na kidonda kikubwa bado kichwani kilichofanya sehemu kubwa ya kichwa chake kufunikwa kwa bendeji. Baraka alimtoa huko na kumpeleka kwake, wakitembea mwendo mrefu sana.

Alimkaribisha vyema kwake, kisha akamwekea maji ya kunywa, na baadae ya kuoga. Akamwelekeza chumba ambacho angetumia, nacho kilikuwa kile alicholalia Steven. Kwa kuwa Baraka alikuwa na godoro la ziada, alimwambia Dylan kuwa angelala chini, kwa sababu hakukuwa na kitanda, na kitanda cha Steven kilikuwa kidogo. Dylan akasema hakuna shida, na kwamba anapenda kulala chini. Baraka akabaki anamwangalia kwa makini.

"Umejuaje kwamba unapenda kulala chini?" akamuuuliza.

Dylan akamtazama Baraka, akiwa hajatambua kwamba alisema kitu fulani kuhusu utu wake bila kukaza sana fikra.

"Amm... sijui. Ahah... hiyo ni ishara nzuri, siyo?" Dylan akasema kwa shauku kiasi.

Baraka akatabasamu na kusema, "Ndiyo. Pole kwa pole... kumbukumbu yako itarudi."

Dylan akamshukuru sana Baraka kwa msaada wake wote aliompatia.

Baada ya hapo alienda kuoga, kisha akarejea na kupata chakula. Baraka alikuwa amempatia baadhi ya nguo zake ili awe anavaa, naye alimwelezea Dylan kuhusu watu wa familia yake, na baadae kijana akapata kuwatambua vizuri baada ya kuwa wamerudi. Emilia na Steven walimwonyesha Dylan roho ya ukarimu kwa kumkaribisha vizuri, lakini Shani pamoja na Leila hawakuonyesha upendezi wowote kumwelekea Dylan. Ijapokuwa alitambua kwamba siyo wote wangempokea vyema, alijitahidi kuwa mtaratibu na mwelewa; akitumaini kuweza kukumbuka maisha yake ya zamani haraka ili asiwabane tena.

"Kaka haitatosha baba. Tumtungie jina," akasema Steven wakati wote wakiwa wameketi sebuleni pamoja usiku.

"Ahahah... tumtungie jina gani sasa?" akauliza Baraka.

"Lolote tu. Kumwita kaka haifai kwa sababu siyo kaka yao," akasema Shani kwa njia yenye kuvunja moyo.

Leila alikuwa bize ku-chat tu, nao wengine walitambua Shani alisema hivyo kwa nia mbaya.

"Achague Steven. Ungependa uniiteje?" Dylan akasema.

"Mmmm... jina gani, jina gani, jina ganiii.... Tumwite ISHENGOMA!" akasema Steven kwa uhakika.

Wote wakacheka, huku Dylan akishangaa jina hilo.

"Ishwegwama?" Dylan akauliza.

"Ahahahah... kwa nini unataka tumwite hivyo?" Emilia akamuuuliza Steven.

"Jina la kibabe. Kama yule Ishengoma mvuta bangi kule sokoni," akasema Steven, na wote wakacheka.

"Ahah... kumbe nafanana naye?" Dylan akauliza.

"Hamna, wewe mzuri. Yeye ana sura ngumu, huwa tukimwona tunakimbia. Sema ana marasi kama wewe, ndiyo maana nikaona tukuite hivyo," Steven akajibu.

"Mhm... linamfaa," akasema Leila kikejeli huku akiendelea ku-chat.

"Hamna bwana, baya. Tutafute la kizungu," akasema Emilia.

"Ili iweje?" akauliza Shani.

"Tumwite... Brian," akasema Baraka ili kumpotezea Shani.

"Mm-mm," Emilia akakataa.

"Kendrick?" akasema Baraka.

"Mm-mm."

"Sebastian?" akasema Steven.

"Mm-mm."

"Sasa we unataka lipi?" Shani akamuuuliza Emilia.

"Ishengoma," akajibu Leila, na wote wakacheka.

"Hamna bwana," Emilia akasema.

Dylan alikuwa anamwangalia Emilia huku anatabasamu.

"Basi wewe mchagulie, maana unayajua majina ya wazungu kuliko hadi wazungu," Leila akamwambia Emilia.

"Ndiyo, Emilia. Nichagulie jina," Dylan akamwambia.

Wote wakamtazama Emilia, naye akawa anamwangalia Dylan kwa makini, kama anatafakari jina ambalo litamfaa.

"Mmmm... Ethan. Tumwite Ethan," akasema Emilia.

Dylan akatabasamu.

Leila akasonya kidogo na kusema, "Me nikafikiri labda utasema Pipindopolupsykapolis."

Baraka akacheka kidogo, kisha akasema, "Ni zuri. Tutakuita Ethan mpaka utakapokumbuka jina lako."

"Na asipolikumbuka milele?" Shani akauliza.

"Haiwezekani. Saa zile alikumbuka kwamba huwa anapenda kulala chini. Atakumbuka vitu vingine tu taratibu," Baraka akasema.

"Kweli?" Steven akauliza.

"Ahahah... ndiyo," Dylan akajibu.

Akamwangalia sana Emilia huku akitabasamu, naye binti akatabasamu pia. Kisha akamshukuru kwa kumpa jina zuri, na kuanzia sasa, Dylan angeanza kufahamika kama ETHAN.

★★★★★★★★★

Mwama amepata dhahama mbaya sana, bila shaka atatoboa tu
 
DYLAN ▶ ‎

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

ILIPOISHIA....

Dylan, baada ya kuwa amepoteza kumbukumbu ya maisha yake ya zamani, anakaribishwa nyumbani kwa mwanaume aliyemsaidia kuokoka kifo kwenye maji, yaani Baraka. Anampatia baadhi ya nguo zake ili awe anavaa, naye anamwelezea Dylan kuhusu watu wa familia yake, na baadae kijana akapata kuwatambua vizuri baada ya kuwa wamerudi.

Emilia na Steven, watoto wadogo wa Baraka wanamwonyesha Dylan roho ya ukarimu kwa kumkaribisha vizuri, lakini Shani, mke wa Baraka, pamoja na Leila, binti yao mkubwa, hawaonyeshi upendezi wowote kumwelekea Dylan. Ijapokuwa Dylan anatambua kwamba siyo wote wangempokea vyema, anajitahidi kuwa mtaratibu na mwelewa; akitumaini kuweza kukumbuka maisha yake ya zamani haraka ili asiwabane hapo tena.

Usiku wakiwa wamekaa pamoja sebuleni wanaongelea kuhusu jina litakalomfaa Dylan kwa sababu alikuwa amelisahau la kwake. Baada ya kutafuta majina kadhaa, Emilia anachagua jina fulani zuri kwa ajili yake.

"Ethan. Tumwite Ethan," akasema Emilia.

Dylan akamwangalia sana Emilia huku akitabasamu, kisha akamshukuru kwa kumpa jina zuri, na kuanzia sasa, Dylan angeanza kufahamika kama ETHAN.

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★

"Steven, Emmy, em' nendeni mkalale, kesho shule," Shani akawaamrisha wanae wakiwa bado sebuleni hapo.

"Aah lakini mama, story zimenoga," akasema Steven.

"Em' nyanyuka huko. Unataka kuanza kusumbua asubuhi-asubuhi wakati unajua palivyo mbali," Leila akamwambia mdogo wake.

"Shule mnayosomea iko mbali?" Dylan akauliza.

"Wee! Yaani kila siku kutembea ni kama kifo," akasema Steven.

Leila akatabasamu kidogo na kusema, "Kifo unakijua wewe?"

"Ndiyo. Kila siku tunapotembea tunakifa," akasema Steven, na Dylan akacheka.

"Haya twende tukalale," Emilia akamwambia Steven, nao wakanyanyuka na kuelekea vyumbani.

Wakabaki wanne sebuleni hapo, Baraka, Shani, Leila, pamoja na Dylan. Nyumba yao ilikuwa na umeme lakini hawakuwa na TV. Hivyo mara nyingi waliketi pamoja kupiga story kama hakukuwa na fujo za Shani na Leila.

"Shule iko mbali kweli au Steven ametia tu chumvi?" Dylan akaanzisha mada.

"Hazikuwa... mbali... mwanzoni. Zimekuwa mbali sasa hivi kwa sababu daraja liliharibika," Baraka akaeleza.

"Kwa nini?" Dylan akauliza.

"Yaani... daraja hilo lilikuwa ndiyo njia ya kuvukia ule upande wa pili... si umeliona wakati tunakuja?" Baraka akamuuuliza.

"Ndiyo..." akajibu.

"Basi, kwa hiyo ilikuwa njia iliyorahisisha watu kwenda na kurudi. Lilipoharibika, ikatubidi tuwe tunazunguka mpaka upande wa mwisho wa bwawa ili kufikia upande wa pili... hata leo, ikiwa lingekuwa halijaharibika tusingechukua muda mrefu hivyo kufika," Baraka akaeleza.

"Mh! Kwa hiyo... Emilia na Steven huwa wanaenda shule kila siku kwa kutembea... wakizunguka namna hiyo?"

"Ndiyo. Inawabidi waamke saa 11 kuanza kujiandaa ili waondoke saa 12 kamili. Kila siku."

"Siyo Emilia na Steven peke yao. Sisi wote," akasema Leila huku anaendelea ku-chat.

"Liliharibikaje?" akauliza Dylan.

"Haijulikani. Yaani lilikuwa zima halafu tukashtukia limenyofoka-nyofoka tu. Ni kama kuna mtu alifanya hivyo," akasema Baraka.

"Mh baba Leila! Yaani mpaka leo bado unaamini hivyo? Nani angeliharibu katikati ya maji mengi bila sisi kumwona? Hata angesimamaje hapo?" Shani akamuuuliza mume wake.

Ni wakati huu ndipo Leila alinyanyuka na kwenda zake chumbani. Shani akanyanyuka pia na kwenda kuandaa mambo kwa ajili ya kesho, kisha akatangulia chumbani, akiwaacha wanaume wameketi hapo.

"Wewe pia unahitaji kupumzika. Ingia chumbani ukalale," Baraka akamwambia Dylan.

"Na wewe?" akauliza Dylan.

"Mimi huwa nakaa-kaa kidogo ndiyo naenda kulala."

"Basi nitakaa nawe kidogo pia."

"Hauhisi maumivu sehemu yoyote?"

"Hapana, niko sawa. Aam.... kwa nini unafikiri kuna mtu aliharibu daraja kimakusudi?" Dylan akauliza.

"Mhmm... ni mambo mengi. Wengi hawaniamini nikiwaambia hilo," akasema Baraka.

"Mimi niko tayari kukusikiliza," Dylan akamhakikishia.

Baraka akashusha pumzi, kisha akaanza kumwambia Dylan alichofikiri.

"Hapa kwenye maeneo yetu, kuna mashamba mazuri sana yanayomilikiwa na watu kadhaa wa huku. Mimi pia ninalo moja, na huwa nalitumia pamoja na familia yangu kwa ajili ya matumizi yetu binafsi..."

"Ndiyo..."

"Sasa, kuna watu fulani ambao walikuwa wanataka kuyachukua kwa kutoa kiwango fulani cha pesa, lakini watu wa huku, kutia ndani mimi, tulikataa. Hatukutaka kuyauza mashamba yetu kwa sababu yanatusaidia sana, na ukitegemea pesa yenyewe waliyotaka kutoa ilikuwa ndogo ukilinganisha na faida ambayo wangepata kutokana na mashamba yetu..."

"Walikuwa wanataka kuyachukua ili..."

"Ili wajengee miradi yao huku. Na wengi walifahamiana na diwani, kwa hiyo tulipokataa inaonekana walikasirika mno..."

"Mh! Kwa hiyo ikawaje?"

"Zilipita siku kadhaa baada ya wao kuahirisha kutulazimisha tulegeze msimamo wetu. Usiku mmoja...mvua kubwa ilikuwa inanyesha. Nilikuwa nimekuja sebuleni kuangalia usalama, usiku huo wa manane, nikaanza kusikia sauti za mlio wa helicopter...unafahamu helicopter?"

"Nd..ndiyo..."

"Ndiyo, nilizisikia. Zilikuwa zinatokea upande huo wa huko bwawani. Mwanzoni nikafikiri labda ilikuwa inapita tu, lakini zikaendelea tu kutoa hiyo sauti. Nikajiuliza mh... kulikoni? Labda helicopter imetua chini? Maana kwa karibu zinakuwa zinatoa makelele, lakini kwa sababu ya mvua kelele nyingi zilikuwa zinazibwa. Baada ya dakika chache, zikaacha. Hapo nikajua tayari ilizima au iliondoka, kwa hiyo nikakaa kidogo kuangalia kama jambo fulani lingetokea. Niliporidhika hakuna kitu nikarudi kulala. Asubuhi inafika wote tunaelekea huko, tunakuta watu wengi upande huu na upande ule wamekwama, wanashindwa kuvuka kwa sababu tayari daraja lilikuwa limeharibika. Wengi wakasema ooh ni mvua inaonekana iliharibu... mbona kamba na chuma za chini za kulishikiza hazikutoka? Mh.. Tukaomba msaada, wapi. Ahadi, ahadi, ahadi, wapi. Hapo nikawa nimeshatambua kulikuwa na jambo limejificha..." akasimulia Baraka kwa hisia.

"Mh! Poleni sana kwa kweli," Dylan akasema kwa kujali.

"We acha tu," akasema Baraka kwa huzuni.

"Hiyo ilikuwa ni lini?"

"Ni kama miaka miwili sasa hivi imepita. Hebu niambie, miaka miwili kweli, wameshindwa kutusaidia? Hmmm... inasikitisha sana."

Dylan aliendelea kusimuliwa mambo mengi kuhusu maeneo haya, akipata kujua maisha ya wakazi wa huko na changamoto ambazo wengi wa upande huu walikabili kutokana na daraja kuharibiwa. Lakini Baraka alimwambia kuwa bado waliendelea kuishi, na hilo lilitosha kwa sababu waliendelea kuwa pamoja kama familia na ni hicho tu ndicho kilijalisha. Dylan alipendezwa sana na utu wa Baraka, naye akaendelea kupatana vizuri na mwanaume huyo kadiri siku zilivyoendelea kusonga.

★★★★

Miezi minne ilipita baada ya hapo (mitatu ilipoisha ndiyo Camila alirudi Brazil), naye Dylan bado aliendelea kuishi kwa bwana Baraka. Jitihada za Baraka za kutafuta alikotokea kijana huyu bado hazikufanikiwa, na kwa kadiri kubwa hakutaka kumwacha tu Dylan bila msaada, hivyo aliendelea kumpa hifadhi kwake.

Wakati huu, Dylan alikuwa amezoeana vyema na wote, ijapokuwa Shani na Leila bado hawakupendezwa na uwepo wake hapo. Shani alimwona Dylan kuwa kama kitu fulani chenye kuwanyonya sana, na Leila alimwona Dylan kama mtu fulani wa hali ya chini asiyekuwa na faida yoyote kwake. Lakini yote kwa yote, Dylan aliendelea kuwa mtulivu na kujitahidi kuishi nao kwa amani.

Emilia ndiye aliyejenga ukaribu sana na Dylan, kwa kuwa Dylan alimwonyesha staha nzuri, na mara nyingi maneno yake yalimsaidia sana msichana huyu kihisia, ijapokuwa Dylan hakutambua hilo. Alimwona Dylan kuwa kama kaka mzuri, naye alitamani dada yake mwenye kutojali awe kama hivyo. Mitihani ya kuhitimu kidato cha nne ilikuwa ikikaribia sana, hivyo Emilia aliongeza bidii ya kusoma ili aweze kufanya vizuri.

Mara kwa mara, Dylan angeenda pamoja na Baraka kule alikofanyia kazi. Aliona jinsi baba huyo alivyojituma sana na ugumu wa kazi yake ulivyokuwa, na mara kadhaa alimsaidia kwa mambo machache ambayo hayakumuumiza kichwa. Kufikia wakati huu, kidonda chake kichwani kilikuwa kimeacha kutoa maumivu, lakini bado alivaa bendeji kichwani ili tu kuweka usalama. Rasi zake zilikuwa zimeongezeka na uso ulikuza ndevu nyingi, hivyo alionekana kama mtu fulani mwenye umri mkubwa sana. Alizoeana na watu kadhaa maeneo ya kule kwenye soko, ambao walipendezwa sana na upole na ustaarabu wake.

Ilikuwa ni siku fulani mida ya jioni, Dylan alikuwa akirudi nyumbani mwenyewe baada ya Baraka kumwambia atangulie, pale alipofika usawa wa daraja lile na kusimama kulitazama. Aliangalia jinsi chini kule palivyokuwa mbali, na jinsi maji kufikia upande wa pili yalivyokuwa mengi. Ngome nene za kulishikiza kule chini bado zilisimama, lakini sehemu yote ya kutembelea katikati mpaka mwishoni kwa pande zote ilikuwa imebomoka-bomoka vibaya sana.

Wakati alipogeuka akitaka kuondoka, kichwa chake kikapatwa na taswira ya mchoro fulani ambao ulikuwa na mwonekano wa daraja hilo. Alitulia kidogo, kisha akalitazama tena. Alipoendelea kuliangalia, mchoro huu ukazidi kujitengeneza kwenye akili yake; yaani ni kama akili yake ilikuwa inalichora daraja hilo.

Hakutambua ni kwa nini hii ilikuwa inatokea, lakini sababu ilikuwa ni kwamba alisomea masuala ya ukandarasi kwa miaka mingi, hivyo akili yake ilikuwa imeshazoea michoro mingi ya ujenzi kipindi cha nyuma. Bila yeye kutambua, akili yake ilikuwa inafanya kazi kumwonyesha jinsi ambavyo daraja hilo lingeweza kukarabatiwa, lakini akawa haelewi jambo hilo. Akageuka zake tu na kuendelea kuelekea nyumbani, akihisi labda kichwa chake kilikuwa kinamwonyesha vitu alivyoona tu zamani.

Alipofika nyumbani, alimkuta Steven nje akiwa anafua shati lake la shule, naye akatabasamu na kumfata pale.

"Steven..." akamwita.

"Naam... shikamoo kaka Ethan?" Steven akamsalimia.

"Marahaba, hujambo?" akamwitikia.

"Sijambo," Steven akajibu kivivu.

"Vipi, mbona kinyonge hivyo jembe?"

"Nimechoka. Mbali kweli."

"Pole."

"Asante."

Steven akainama ili atoe shati lake aanze kulikamua maji, pale Dylan alipoona alama fulani ya uvimbe kwenye mkono wake kutokea begani.

"Steven, nini hicho mkononi?" akamuuuliza.

"Naam? Wapi?"

"Hapo hivi. Umefanyaje, mbona pamevimba?"

"Aaaa... mwalimu alinipiga stick," Steven akajibu.

"Kwa nini amekupiga vibaya hivyo?"

"Nilikuwa nimesinzia darasani wakati anafundisha. Kwa hiyo akaniwasha fimbo kwa nguvu mgongoni... inauma!"

"Aisee... pole. Kwa nini unalala darasani wakati anafundisha?"

"Sifanyi makusudi kaka Ethan. Usingizi wa saa 11 mtamu, kila siku kuamka muda huo, kutembea, nakuwa nachoka. Najitahidigi nisilale lakini mara nyingine usingizi unakuwa unanilemea," Steven akaeleza.

"Dah, ila walimu na wenyewe bana! Wako kama wanyama, sijui wakoje..."

"Wakuda tu. We subiri, nami nikija kuwa mwalimu nitakuwa nafumua mtoto wake! Heeee..."

Dylan akacheka kidogo. Alimwonea huruma sana Steven, kwa kuwa alikuwa mdogo mno, na inaonekana kuna mambo mengi magumu alipitia shule kutokana na shida hiyo ya umbali.

"Umekula?" akamuuliza.

"Eee angalau nimekuta chapati na maharage kwenye hotpot. Zimetuliza maumivu," Steven akajibu.

Dylan akatabasamu na kumwambia akaanike nguo sasa. Yeye akaelekea ndani ili aweze kutoka kuoga na kubadili nguo.

Ilifika usiku, na wote wakawa nyumbani tayari. Wanawake walikaa nje mara nyingi hasa kwa sababu ya kupika, naye Baraka pamoja na Dylan wangekaa ndani wakiongea, au nje kama kungekuwa na uhitaji wa kufanya hivyo. Baraka alikuwa akimsimulia Dylan kuhusu mtu fulani mwenye fujo sana aliyeitwa Lazaro kule anakofanyia kazi, ambaye alitokeza ugomvi muda ule Dylan ametangulia kuja nyumbani. Dylan akamwambia ikiwa angehitaji msaada kumdhibiti basi amwambie, naye Baraka akacheka na kumwambia alisuluhisha jambo hilo. Wakaendelea na story mpaka muda wa kula ulipofika.

Ilikuwa ni wakati Leila anaingia ndani akiwa amebeba chombo kilichokuwa na chakula, pale alipoteleza kutokana na maji yaliyomwagika kidogo chini wakati Steven ameleta maji ya kunawa. Dylan alikuwa amepatwa na machale ya haraka yaliyomfanya atende upesi mno; akanyanyuka kutoka alipoketi na kumwahi Leila kabla hajadondokea kichwa chake chini. Alikishika kiuno chake kwa kasi na kukigeuza ili awe kwa chini yake, hivyo miili yao ilipoanguka, wa Dylan ukawa chini ya mwili wa Leila ili asiumie.

Wote walishtuka na kwenda hapo wakiwaangalia. Hotpot alilobeba lilikuwa na mboga za majani, nayo yote ikawa imemwagika. Leila akanyanyua uso wake na kumwangalia Dylan, ambaye alikuwa amemshikilia bado chini hapo.

"Uko sawa?" Dylan akamuuliza.

"Unafanya nini... em' niachie!" Leila akamwambia kwa ukali, huku akijitoa mwilini mwa Dylan.

"S..samahani..." Dylan akasema.

Shani akamshika Leila akimwangalia kwa makini, kisha akamuuliza, "Umekuwaje?"

"Sijui nani amemwaga maji hapa..." akasema Leila kwa kuudhika na kusonya.

"Muwe mnakuwa waangalifu bwana. Ethan asingekudaka, ungeumia vibaya," Baraka akawaambia.

"Ethan uko sawa?" Emilia akamuuliza Dylan.

Dylan alikuwa amejishika kichwa, huku akikaza meno yake. Kichwa chake kilikuwa kimepiga chini wakati anamdaka Leila, hivyo alihisi maumivu kiasi.

"Ndiyo niko sawa," akajibu kwa kuficha ukweli.

"Aagh mboga yote imemwagika jamani!" Shani akasema kwa kukwazika.

Emilia akatoka kwenda kuchukua dekio, naye akarejea na ndoo yenye maji ili apasafishe.

Wengine wakakaa ili kujiandaa kula, wakiwa wanamsubiria Emilia amalize. Kwa kuwa kulikuwa na mboga nyingine, wangetumia hiyo hiyo kulia ugali, kwa hiyo hakukuwa na shida sana upande wa chakula. Shida ikawa upande wa Dylan. Kichwa kilimsumbua, siyo kuuma, bali alianza kuona vitu vingi kama maruerue yaliyokuwa yanachanganya sana, nayo yalimnyima raha. Hata hamu ya kula ikamtoka kabisa.

Akala chakula kidogo sana, kisha akawaaga kuwa anaingia kulala, akiwaacha wanamwangalia wasijue amepatwa na nini. Muda wote ambao Dylan alikuwa amejilaza, alijaribu kuviunganisha vipande vidogo vidogo alivyoona kichwani ili atengeneze taswira nzuri, lakini akawa anashindwa. Mwishowe alipitiwa na usingizi baada ya muda mfupi akiwa kwenye msukosuko huo wa kichwani.

★★★

Dylan aliamka alfajiri mapema sana. Kulikuwa na giza nje bado, naye aliweza kuwasikia Emilia na Steven wakiwa katika harakati za kujiandaa. Steven sikuzote alikuwa mzito alipoamshwa mapema namna hiyo, lakini baada ya kuoga angejisikia afadhali na kujiandaa vyema kwa ajili ya shule. Walipomaliza, walitoka kwa pamoja baada ya Emilia kuonana na baba yake, kama ilivyokuwa kawaida. Dylan alitoka na kumkuta Baraka akiwa ameshaamka tayari, naye Baraka akashangaa kidogo kwa sababu Dylan hakuwa na kawaida ya kuamka alfajiri mno; sanasana mida ya saa moja au saa mbili asubuhi.

Dylan aliwaangalia Emilia na Steven wakiondoka, naye aliwaonea huruma sana kwa kuwa alijua vizuri jinsi ilivyokuwa ngumu kwao kila siku kutembea. Baadae, maman'tilie na dadan'tilie wakawa wameamka pia. Walikuwa na kawaida ya kusaidizana kuandaa vitu usiku kwa ajili ya siku inayofuata, hivyo asubuhi wangeondoka wakiwa wamevibeba kichwani, halafu baada ya kumfikisha mama yake mgahawani, Leila angeelekea alipofanyia kazi.

Baraka alikuwa na kawaida ya kwenda mgahawani kwa Shani aidha asubuhi au mchana ili kupata msosi, kwa hiyo tokea Dylan alipoanza kuwa anaenda naye kazini kwake, mara kwa mara walienda pamoja pale. Ijapokuwa Baraka na mke wake hawakuwa na maisha ya hali ya juu, walijitahidi sana kuwaandalia mahitaji watoto wao kwa kila kitu ambacho waliweza kufanya; na walijitoa kwa moyo wote, haijalishi ni changamoto zipi walipitia.

Asubuhi hii, Dylan alimwambia Baraka atangulie, naye angefata ndani ya muda mfupi ili kwenda kumsaidia kazi kadhaa huko.

Baada ya Baraka kuwa ametangulia, Dylan akafunga nyumba kisha akaelekea sehemu ile yenye lile daraja. Alisimama hapo, akilitathmini kwa makini sana. Ilikuwa ni kama aliingiwa na kitu fulani kilichomwambia kwamba angeweza kulitengeneza, naye alitaka kujihakikishia kwamba kweli angeweza. Akarudi tena nyumbani na kuanza kutafuta kalamu na karatasi. Alifanikiwa kupata penseli ndogo iliyochongwa vizuri, na daftari ambalo alitambua halikutumika tena. Baada ya kukuta karatasi kadhaa zilizokuwa bila maandishi, akalichukua pia, kisha akarejea darajani pale.

Alifika na kuketi kwenye jiwe dogo pembeni ya mwingilio wa kivuko hicho. Akafumba macho na kuvuta pumzi kisha kuishusha taratibu ili kutuliza akili yake. Akayafumbua macho na kuanza kulitazama daraja hilo kwa umakini tena. Jinsi lilivyokuwa limebomoka kuanzia katikati mpaka mwishoni, haikuonekana kuwa mvua ndiyo iliyoharibu, bali ni KITU fulani ndiyo kiliharibu. Akili yake yenye werevu mwingi ilimsadikishia kabisa kwamba daraja hilo lilikuwa limebomolewa kwa kutumia mashine fulani, hivyo Baraka alikuwa sahihi aliposema liliharibiwa kimakusudi.

Kadiri alivyoendelea kulitazama, ndivyo njia za michoro (patterns) zilivyoendelea kujichora kwenye akili yake. Hivyo, akawa anachora kwenye daftari mambo yote ambayo taswira yake ilimwonyesha, na mara nyingi hata alikuwa haangalii daftari! Alitumia saa zima akiwa ameketi hapo anachora, kisha akatazama daftari na kuona alikuwa ameweza kuchora njia za kulitengeneza daraja hilo. Alitabasamu, akitambua kwamba alikuwa ana ujuzi fulani kuhusu ujenzi, lakini bado hakukumbuka vizuri ilikuwa kutokea wapi.

Muda mfupi baadae akaondoka na kuelekea kwa Baraka, akiwa amelikunja daftari alilochorea na kuliweka nyuma kwenye mfuko wa suruali yake. Mambo kule yalikuwa kama kawaida; vyuma. Alimsaidia kukata, kurekebisha, kuunganisha, na kutengeneza vitu mbalimbali. Dylan alikuwa amejifunza mambo haraka kwa hiyo miezi michache aliyoanza kumsaidia kazi Baraka, na hata watu kadhaa waliomfahamu huko walimpelekea vitu vyao arekebishe, wakimwita yeye pia fundi. Kujifunza kwake haraka kulitokana hasa na kichwa chake chepesi kushika mambo, hivyo aliwapendeza wengi kwa ustadi wake mwingi.

Ilipofika mida ya jioni baada ya wawili hao kuwa wametoka kwa Shani kula, wakawa wameketi kwa nje mbele ya ofisi yake Baraka. Walikuwa wakipiga story na watu wengine wa eneo hilo, na wengi walimzungumzia yule jamaa aliyemletea fujo Baraka jana. Kisha baadae, wakawa wamebaki watatu tu hapo; Baraka na Dylan, wakiwa na kijana mwingine aliyeitwa Konde, ambaye aliuza nguo za dukani maeneo hayo.

"Weweee! Michepuko ndiyo dili! Hivi wewe huwonagi jinsi michepuko inavyojuwa kupendeza? Yaani malavidavi kama yowte... ahmm hoowney, karibu, mwaah... jamani baby nimeku-miss... mke ataweza hayo?" akasema Konde, akiwa anabishana na Baraka, huku Dylan anasikiliza akicheka.

"Mke wako tu ndiyo hawezi! Na tena siyo kwamba hawezi, ni wewe tu ndiyo umepoteza akili kwa michepuko yako!" Baraka akamwambia.

"Aa wapi! Mchepuko baba... acha kabisa. Yaani hee, hee, hee, mpaka unatamani kubaki naye tu! Kwanza wanajua kupendeza, ni wazuri sana," akasema Konde.

"Ni mzuri kwa sababu pesa zako zote unapeleka huko akatumie wakati kwa mke wako unaacha buku tu. Unamkomaza mkeo na majukumu af' humtunzi, atakuwa mzuri saa ngapi mbwa wewe?" akasema Baraka.

Dylan na Konde wote wakacheka.

"Eti jamani? Matunzo zero. Tunza mkeo achana na michepuko fala wewe. Angekuwa mbaya usingemwoa," akasema Baraka.

"Hakuna kitu wewe," Konde akakanusha.

"Tatizo wakishagaoa wanachukulia ndiyo basi tena na matunzo hawatoi, wakati waliwakuta wadada wa watu wanang'aa," Dylan akasema.

"Umeona?" akasema Baraka.

"Dah! Ethan! Yaani na wewe unamsapoti huyu mbabu wa kale?" Konde akasema.

"Kwenda huko bwege wewe!" Baraka akamwambia kiutani.

Wote walifurahia sana maongezi yenye kujenga lakini yenye utani mwingi. Ni wakati huu ndipo mteja alifika kwenye duka la Konde, hivyo akatoka hapo akiharakisha kumfata.

"Yaani vijana wa siku hizi!" akasema Baraka.

"Ahahah... wanajua kuhusika," akasema Dylan.

"Ahahah... Vijana wa kiume wapo kwa ajili ya kuonja-onja tu. Hata kama ameoa, anataka kuhalalisha kuonja, unafikiri wataacha kuwadharau wake zao?" akasema Baraka.

"Ahahah... zamani walikuwaga hawaonji-onji?"

"Aah... zamani wazee walionja nje lakini kwa siri sana. Mahusiano kwa vijana siku hizi ni fashion tu siyo stara tena, hawana hata hofu ya Mungu. Hawajui kutofautisha tamaa na upendo," akasema Baraka.

"Kweli kabisa."

Baraka akashusha pumzi, kisha akasema huku akisimama, "Naona tufunge tu tupandishe."

"Sawa. Aam... Baraka..." Dylan akaita.

"Naam..."

"...kuna jambo nataka kuongea nawe."

"Ahah... mbona serious sana? Ni jambo baya?"

"Hamna, ni... zuri. Nahitaji tu msaada wako."

"Sawa... niambie," Baraka akaweka umakini.

"Nahitaji kuwa nachukua vyuma kwenye hicho chumba chenye vyuma vingi ambavyo havitumiki," akasema Dylan.

"Kwa nini? Unataka kuvifanyia nini?"

"Nataka... kulitengeneza daraja."

"Eti? Daraja hilo lililoharibika?"

"Ndiyo."

Baraka alishangazwa na uhakika wa Dylan.

"Nini kimekufanya ufikie uamuzi huo?" Baraka akamuuliza.

Dylan akatazama chini.

"Kuna vitu umekumbuka? Ulikuwa... fundi wa madaraja au?" Baraka akauliza.

"Hapana...sijui...ila..." Dylan akashindwa amwelezee vipi.

Baraka alikuwa anamwangalia kwa maswali mengi sana. Dylan akamshika begani kwa kiganja chake.

"Najua inaweza kuwa ngumu kunielewa. Lakini... ninaomba tu uniamini. Ninajua ninaweza kufanya hili jambo," akamhakikishia.

Baraka akatafakari kidogo, kisha akasema, "Lakini ni refu. Utawezaje kulitengeneza mwenyewe?"

"Nahitaji tu muda, na kibali chako. Nikiwa na kila kitu nitakachohitaji, nitafanikisha," Dylan akasema kwa uhakika.

Baraka akashusha pumzi tena, kisha akatikisa kichwa kwa kustaajabishwa na kijana huyo.

"Sawa. Siyo kwamba vyuma hivyo huwa situmii, lakini unaweza kuchukua unavyohitaji," akamwambia.

"Ahah... asante sana," Dylan akafurahi.

"Kwa hiyo unataka kuanza lini?"

"Haraka iwezekanavyo. Na... nahitaji kufanya maandalizi kwanza, kwa hiyo jambo hili liwe kati yetu wawili mpaka nitakapomaliza," Dylan akasema.

Baraka akatikisa kichwa taratibu kukubali, akiona kwamba kweli kijana huyu alikuwa na nia hiyo ya kufanya jambo ambalo halingefikirika kwa yeyote. Dylan aliamini kabisa kwamba angeweza kuleta badiliko, na sasa kile ambacho kingefuata ilikuwa ni kazi tu.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN ▶ ‎

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★

Wawili hawa wakafunga ofisi na kuanza kurejea nyumbani. Dylan alimsimulia Baraka wakiwa njiani kurudi nyumbani kuhusu michoro aliyoona kichwani kwake. Alimweleza kwamba mambo mengi aliyohitaji kufanya yalichochewa na "maono" yake hayo, na ijapokuwa yalikuwa ni mambo yenye kuchanganya kidogo, Baraka alimwamini na kumwacha tu ili afanye alichoona ni sahihi.

Asubuhi ya siku iliyofuata, Dylan alibaki nyumbani ili aweze tena kwenda kwenye daraja lile. Wakati huu alikuwa anachora jinsi ambavyo alitaka ujenzi wa daraja ukae, ili ajue vyuma na vifaa ambavyo vingefaa kwa ajili ya matengenezo aliyotaka kufanya. Baada ya kumaliza kupangilia michoro yake, alienda kwa Baraka baadae, naye akaanza kupekua vyuma vingi ambavyo havikutumiwa. Baraka sanasana alimchagulia vyuma vingi, kwa kuwa baadhi alivihitaji. Dylan akamshukuru, kisha akaenda kuazima toroli kubwa na kuviweka humo ili arudi navyo nyumbani.

Alifanya safari tatu za kupeleka vyuma nyumbani, na kisha akarudisha toroli kwa wamiliki. Alirudi nyumbani akihisi uchovu kiasi kutokana na umbali, lakini alikuwa mwenye uchangamfu moyoni. Baadae wengine waliporejea, walishangaa kukuta vyuma vingi nje, nao ikabidi waulize kulikoni. Baraka aliwaambia kuna kazi atakuwa akisaidizana na Ethan (Dylan) hapo nyumbani. Shani alishangaa kwa kuwa Baraka hakuwa na kawaida ya
kufanyia kazi nyumbani, hivyo alitaka kujua ilikuwa kazi gani hasa. Baraka alipiga chenga maswali yake mengi, akikazia kwamba ni masuala ya kiufundi ambayo asingeelewa.

Dylan akaanza kazi upesi. Angesubiria wote waondoke asubuhi, kisha angeshughulika na vyuma vile; akivinyoosha, kuvipindisha, kuviunganisha, kwa njia ambayo ilipatana na jinsi alivyotaka daraja liwe. Alitumia muda mwingi sana kufanya kazi hii, na mara kwa mara Baraka alimsaidia wakati ambao Dylan angefanya kazi usiku.

Bado wawili hawa hawakuwa wamemwambia yeyote kuhusu mpango wa Dylan wa kulitengeneza daraja, hivyo watu wa familia ya Baraka hawakuelewa Dylan alichokuwa anafanya, na hasa Shani na Leila ndiyo ambao waliona kazi hizo kuwa hazina maana na zenye kupoteza muda.

Zilipita wiki mbili, na sasa Dylan akawa amemaliza kuvitengeneza vyuma vile kwa mpangilio aliotaka. Baraka alikuwa amemwongezea vyuma vingine wakati akiendelea na kazi, naye Dylan alikuwa ametafuta pia kamba nyingi nene, ndefu, na ngumu, misumari mikubwa, nati nyingi, na makolokolo mengine mengi. Baraka alikuwa amechangia kwa kiasi kikubwa sana kumpatia vitu alivyohitaji, akiwa na imani ndani ya kijana huyo kuwa angefanya maajabu kweli. Hivyo Dylan alikuwa na rundo kubwa la vifaa; vikiwa tayari kwa ajili ya kazi yenyewe.

★★★

"Kwani Misha kasemaje?" akauliza Dylan.

"Anabanwa na chuo. Eti wakati huo watakuwa na mitihani. Anazingua sana msela," akasema Fred.

"Siyo lazima tucheze na Misha bwana," akasema Omari.

"Jamaa anajua boli. Kocha mwenyewe anamkubali sana, sa' sijui ndo' itakuwaje...maana mechi inakaribia, hatutaki kuaibishwa tena," akasema Fred.

"Ish... kwenye mechi anacheza Misha peke yake kwani? Sisi tutacheza na tutashinda," akasema Omari.

"Kipa wa kwetu atakuwa nani?" Dylan akauliza.

"Lazima iwe Anatory. Akikaa pale hawapitishi goli hata moja... afu' jamaa anang'ang'ania Misha, Misha..." akasema Omari.

Haya yalikuwa maongezi baina ya Dylan pamoja na vijana wenzake, ambao walikuwa rafiki zake pia. Ilikuwa ni Jumapili, jioni, nao walikuwa wamekaa kwenye kijiwe chao wakiongea baada ya kutoka kufanya mazoezi ya mpira. Dylan alipendelea kwenda kupasha mwili kwa mazoezi hayo pia, lakini kwenye masuala ya mechi hakushiriki.

Mechi hii muhimu waliyokuwa wanaizungumzia, ilikuwa ni mechi ya kirafiki kati ya wachezaji wa eneo lao na wachezaji wa mjini, ambayo ingechezwa mwezi ujao mwishoni. Mara nyingi walishindanishwa ili kusaka vipaji zaidi, na wadhamini kadhaa wangekuwepo kutazama. Timu ya eneo lao Dylan iliitwa Cotable FC, na ya mjini iliitwa Town City FC, ambayo ilikuwa timu nzuri yenye mafanikio sana. Mara nyingi walipocheza, Cotable ilifungwa tu, hivyo walikuwa wana hamu kubwa ya kuishinda ya mjini siku moja ili iache kujigamba.

Wakati wakiwa wanarudi makwao kutoka huko, walikutana na rafiki yao mwingine, aliyeitwa Shija.

"Oyo, oyo, mzee baba..." akasema Omari.

"Aa niaje?" Shija akawasalimu.

"Fresh, wapi iyo?" akauliza Omari.

"Skani.' Nkuwa' nimetoka kusaga mahindi, si mnaona hii ndoo?" akasema Shija.

"Aaaa... ni mwendo wa nguna tu!" akatania Fred.

"Usiulize," akasema Shija, na wote wakacheka.

"Mechi hiyooo, kombe tunabeba," Omari akajigamba.

"Aa wapi, nyie mtakunyugwa tu," Shija akasema.

"Angecheza Misha, jamaa angesaidia sana. Sema anabanwa na chuo," akasema Fred.

"Dah, mwanangu, an' huyu fala amekomaa na Misha kama demu wake vile. We kama jamaa huwa anahemea mgongoni kwako, sema tu," Omari akamtania Fred.

Fred akamfata Omari, nao wakaanza kufanya kama wanapigana kiutani, huku Dylan na Shija wakicheka.

"Niaje mbabe?" Shija akamwambia Dylan.

"Poa tu. Ungekuja tizi bwana," Dylan akamwambia.

"Aah, msosi lazima, tizi hiari."

"Ahahah... kweli."

"Nimemuona dada yako yule anapandisha mlimani," akasema Shija.

"Dada yangu? Nani... Leila?" Dylan akauliza.

"Eee huyo."

"Mlima gani?" akauliza Dylan.

"Huu wa huko hivi, ukiwa unaelekea Banza."

"Yaani hajaenda Banza kabisa, ila amepandisha kwenye huo mlima?" akauliza Fred.

"Eee," Shija akajibu.

"Mh! Demu mkali vile ameenda huko kufanya nini?" Omari akamuuliza Dylan.

"Kwenda huko kuna uhusiano gani na yeye kuwa demu mkali?" Fred akamuuliza Omari.

"Eeeheheh... huyu jamaa ndo' wale wanaovizia huyu," akasema Shija.

Dylan alikuwa akiwaza ni nini ambacho kilimpeleka Leila juu ya mlima huo, ukitegemea ilikuwa ni saa 12 jioni tayari.

"Ngoja nikamcheki," Dylan akasema.

"Poa. Me naingia skani'. Tizi kesho kama kawa?" Shija akauliza.

"Kama kawaida," akajibu Fred.

"Poa poa. Bro, nyoa hizo ndevu, unaonekana kama yule Duma," Shija akamwambia Dylan, na wengine wakacheka.

"Ndiyo nani huyo? Me simjui," Dylan akasema.

"Yule mwigizaji mbaya mbaya yule," akasema Shija.

"Ngoja aje akusikie," Fred akamwambia Shija.

"Mwite! Yule ntamkunja' tu na kumtafuna," Shija akajigamba.

Kisha akawaacha vijana hao watatu na kuelekea kwao.

"Oy kwo' unaingia mlima wa Banza?" Omari akamuuliza Dylan.

"Ndiyo. Usiku unaingia, nataka kuhakikisha huyo yuko salama," akajibu Dylan.

"Haya poa, sisi tunaingia home. Tutaonana man."

Wote wakamuaga Dylan, kisha yeye akaanza kuelekea upande wa mlima ule ambao aliambiwa Leila alikuwa amekwenda.

Alipofika maeneo hayo, alianza kupandisha moja kwa moja kupitia njia iliyoelekea huko juu. Ulikuwa mlima mdogo, lakini kuupanda ilichosha. Alitazama huku na huku akitafuta uwepo wa Leila, na baada ya mwendo fulani, akaanza kusikia sauti iliyomshtua.

Ilikuwa ni sauti ya Leila, naye alilia na kusema kwa sauti iliyosikika kwa mbali kwamba anahitaji msaada. Dylan akaanza kuelekea upande ambao sauti ya Leila ilitokea, akiwa hajui ni nini kimemsibu. Aliamua kutomwita Leila, ili kama kuna mtu alikuwa anajaribu kumtendea vibaya kimwili, labda kumbaka, asitambue ujio wake ili aweze kumshughulikia ipasavyo.

Alipofika karibu zaidi na kelele za Leila, aliweza kumwona akiwa ndani ya shimo lenye mawe madogo-madogo, naye kwa haraka akawa ametambua kuwa binti alidondokea shimoni humo. Akawahi na kusogea karibu zaidi ili amsaidie kutoka humo.

"Ethan... Ethan... em' nitoe humu..." akasema Leila huku anajifuta machozi.

"Nipe mkono," Dylan akamwambia huku ameinama na kumnyooshea mkono wake.

Akafanikiwa kumvuta na kumtoa kutoka kwenye shimo hilo. Leila alikuwa amevalia T-shirt ya rangi nyeusi na suruali ya jeans, ambayo ilichafuliwa na vumbi la kwenye shimo hilo.

"Pole. Ulikuja kufanya nini huku Leila? Ulidondokeaje humo?" Dylan akamuuliza.

"Hayakuhusu..." Leila akasema huku anajipangusa vumbi.

"Iih... wewe! Hiyo ndiyo asante?" Dylan akasema akimshangaa.

"Nikikwambia asante utapata faida gani?" Leila akamuuliza kwa dharau.

Dylan akabaki anamwangalia tu, akiwa anashangazwa na mtazamo huo mbaya wa dada huyu.

Leila akageuka na kuanza kuondoka.

Dylan akawa anamfata nyuma huku anamsihi amwambie alikuja kufanya nini huku, lakini binti hakutaka kusema. Alimjibu ovyo tu, na kiukweli Dylan alijisikia vibaya kwa kuwa alijitahidi sana kuwa mwelewa na mstaarabu, lakini bado Leila na mama yake hawakumtendea vizuri mpaka kufikia kipindi hiki.

Wakafika sehemu fulani ambayo ilianza kushuka, na kwa tukio baya Leila akaukwaa mguu wake na kuutegua vibaya kwa chini. Alihisi maumivu sana, naye akakaa chini akiwa amekunja sura yake. Dylan akawahi hapo ili auangalie mguu wake.

"Niache usiniguse!" Leila akamfokea Dylan.

"Nataka kuangali..."

"Nimesema uniache, sitaki unisaidie!" Leila akamkatisha.

Dylan alimshangaa sana.

"Una matatizo gani?" akamuuliza.

"Ahssss... hayakuhusu," Leila akajibu huku akisikilizia maumivu mguuni.

"Kwa nini uko hivi? Najua hujanipenda toka nilipokuja kwenu, lakini mbona unanitendea kama vile nimekufanyia jambo fulani baya? Mimi nataka kusaidia tu..."

"Nyooo... umsaidie nani wewe? Toka umekuja unalishwa, unavalishwa, upo upo tu, halafu unasema kusaidia tu..." Leila akasema kwa dharau.

Dylan akawa anaelewa hayo ni masimango tu, lakini ni wazi Leila alisumbuliwa na jambo fulani. Alipotazama mguu wake, aliweza kuona damu ikitoka kidogo sehemu iliyokwanguka, hivyo akachukua kitambaa chake na kutaka kumfuta taratibu, lakini Leila akaupiga mkono wake ulioshika kitambaa hicho ili asimfute. Dylan aliingiwa na hasira, naye akampiga nacho tumboni, kisha Leila akakichukua na kumpiga nacho usoni. Dylan alimwangalia sana, akiwa ameudhiwa sana na tabia ya Leila.

"Una shida gani? Ni nini kinakufanya unakuwa na kiburi sana?" Dylan akamuuliza.

"Ambacho huna, na ambacho hujawahi kuona," Leila akajibu kwa ukali.

"Una nini wewe ambacho mimi sijawahi kuona?" Dylan akamuuliza, akiwa amekerwa sana sasa.

"K(...)!" Leila akamjibu kwa dharau.

"Hicho tu? Ndiyo kinakufanya ujione uko juu zaidi kwenye dunia? Ya kwako ina utofauti upi labda... ina miba au?" Dylan akamuuliza kwa kukereka.

Leila akawa anamwangalia usoni huku anapumua kwa hasira.

"Basi endelea kukaa hapo Ikiwa hicho ulichosema ndiyo kitakusaidia kunyanyuka," akasema Dylan kwa mkazo.

Kisha jamaa akainuka na kuanza kuondoka, akimwacha Leila amekaa chini hapo. Dylan aliudhika sana, kwa kuwa ni wazi Leila hakumheshimu hata kidogo. Kilichomkera ilikuwa ni kwamba alijitahidi kuonyesha roho ya upole na kuwajibika kwa mwanamke huyo, lakini akamrudishia mateke kama shukrani. Hivyo aliona amwache tu ili matatizo yamfunze vyema.

Dylan alifika mpaka sehemu ya chini na kutulia hapo. Alikuwa anafikiria mambo yote ambayo Leila alimwambia, naye alikuwa amevunjika moyo kiasi. Lakini akaanza tena kufikiria hali yake; ameumia mguu, yuko mlimani, na usiku umeanza kuingia. Alijua isingekuwa jambo zuri kumwacha tu huko, ijapokuwa kiburi chake kilimuudhi. Hivyo akaamua kurudi tena ili amfate, na wakati huu asingejali kelele zake, kama ni kumbeba kwa lazima angefanya hivyo.

Giza lilikuwa limeingia zaidi, na sasa mvua ikaanza kunyesha. Dylan alifanya upesi sana kumfata Leila, na alipomfikia akamkuta anajiburuza chini huku analia. Alimwonea huruma sana. Mvua ilikuwa kubwa yenye kutia baridi mno, hivyo Dylan akamfata chini hapo na kumnyanyua juu, kisha akambeba mgongoni kwake. Leila alikuwa kwenye huzuni nzito, na ijapokuwa alitaka kuendeleza kiburi chake, zamu hii hangeweza kwa kuwa alihitaji sana msaada.

Dylan akajitahidi kushuka naye chini kwa uangalifu kwa kuwa maji mengi yalitiririka na ardhi ilipatwa na utelezi, mara kwa mara ikisababisha ateleze lakini angeweza kujidhibiti ili wasianguke. Akafanikiwa kutoka kwenye mlima huo na kufika kule chini barabarani, kisha akaanza kuelekea upande wa eneo la Banza. Walifika sehemu fulani ambayo Dylan alijua kulikuwa na nyumba ndogo iliyoachwa, hivyo akaelekea humo ili watoke kwenye mvua. Ilikuwa ni nyumba ya mbao ambayo zamani ilitumiwa kama sehemu ya starehe, hivyo ilikuwa pana kiasi.

Baada ya kuingia hapo, Dylan alimweka Leila chini na kumkalisha, binti akiwa anatetemeka sana. Akamuuliza ikiwa simu yake iko mfukoni, lakini kutokana na baridi aliyohisi hakuweza kujibu. Dylan akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali ya Leila na kuitoa simu yake, kisha akaifungua yote na kutoa betri ili isiharibike. Akavua T-shirt yake na kuikamua maji, kisha akaitandaza kwenye mlango kwa juu. Giza lilikuwa zito, lakini mianga ya radi iliwamulika mara kwa mara, hivyo wangeweza kuona mambo kwa kadiri fulani.

Dylan alipomgeukia Leila, angeweza kuona jinsi baridi ilivyomchoma sana binti. Akamsogelea, yeye pia akihisi baridi, kisha akaanza kuvipulizia viganja vyake joto la mdomo kwa ukaribu. Dylan angefikicha viganja vyake na kumwekea kwenye uso, au angechukua viganja vya Leila na kuvifikicha kwa vyake, yaani alijaribu jambo lolote ili kumsaidia, lakini bado Leila alitetemeka sana. Dylan akasimama na kuangalia huku na huku, lakini hakukuwa na kitu chochote kilichompa wazo zuri.

Kisha akamtazama tena Leila. Wakati akiwa anamwangalia, akili yake ikaanza kumwonyesha taswira nyingine ya mwanamke, ambaye hakuonekana uso vizuri. Alikuwa anamwangalia Leila lakini aliona mwanamke mwingine akiwa amevaa taulo, huku anatetemeka, kisha akamfata na kumkumbatia. Alifumba macho yake na kutikisa kichwa chake kidogo, kisha akafumbua tena na kumtazama Leila. Hakujua kuwa kumbukumbu yake ilikuwa inamwonyesha jambo ambalo liliwahi kutokea kipindi cha nyuma, lakini taswira hiyo ikawa imempa wazo.

Akamfata Leila hapo chini, kisha akamshika usoni na kumtazama machoni.

"Leila... najua..hhautakubaliana na jambo hili... lakini naomba ujue tu kuwa... nalifanya ili kukusaidia..."

Dylan akamwambia hivyo. Leila, akiwa amejishikilia huku anatetemeka mdomo, alimwangalia Dylan usoni asielewe alichomaanisha, na hapo hapo, Dylan akaishika T-shirt ya binti kwa chini na kuanza kuivuta juu. Alipoifikisha usawa wa kifua, akamwangalia binti machoni, na kwa kushangaza, Leila akalegeza mikono yake na kuinyanyua juu, ili kuruhusu avuliwe.

Dylan akaitoa yote na kuikamua maji kisha kuiweka pembeni, na aliporudisha macho kumwangalia, akakuta alikuwa amevalia sidiria nyeusi iliyoyaonyesha matiti yake kwa juu kidogo. Lakini kwa wakati huu, Dylan hakukazia fikra mwili maridadi wa mwanamke huyu, bali kumpatia msaada, hivyo akaketi karibu yake na kumkumbatia ili miili yao itengeneze joto kadiri ambavyo muda ungepita.

Mwanzoni wote waliendelea kuhisi baridi tu, lakini dakika kadhaa baadae miili yao ikazoeana na hali na kuanza kutulia zaidi. Dylan alikuwa anasugua-sugua mkono wa Leila kwa wororo, ili mtoto apate joto kiasi. Baada ya muda mfupi mvua ikapungua na kubaki kudondosha manyunyu, huku wawili hawa wakiwa wameshikiliana bado kwa zaidi ya dakika 40.

"Samahani Leila. Nisingekuacha hii isingetokea," Dylan akasema kwa sauti ya upole.

Leila, akiwa amemsikia vizuri sana, akabaki kimya tu.

"Nisamehe pia... kwa kukusemesha namna ile," akasema Dylan.

Leila alikuwa ameanza kutambua jinsi gani Ethan (Dylan) alivyokuwa mwanaume mstaarabu. Sikuzote alimwona kuwa dhaifu tu, lakini udhaifu huu sasa akatambua ni utu mzuri wa kijana huyu. Sasa mvua ikawa imekata, huku anga bado likitoa mianga ya radi, nao wakaendelea kukaa namna hiyo kwa nusu saa zaidi.

"Nafikiri tunaweza kwenda nyumbani sasa... unaonaje?" Dylan akauliza kwa sauti yenye upole.

Leila hakutoa jibu, lakini akajitoa mwilini mwa Dylan na kukaa sawa. Alikuwa ametulia zaidi sasa, naye Dylan akanyanyuka na kufata simu yake; aliyokuwa ameisambazia vitu vyake chini. Akarudi nayo karibu ya Leila na kuanza kuiunganisha.

"Tuombe Mungu isiwe imeharibika..."akasema Dylan.

Alikuwa ameikung'uta maji vyema muda ule, hivyo akaweka betri na kuifunga vizuri, kisha akampa Leila aiwashe. Leila akaichukua taratibu na kujaribu kuiwasha, nayo ikawaka. Dylan akatabasamu huku anamwangalia, naye Leila akawa anamwangalia Dylan usoni kwa njia ya kawaida.

"Sasa... utaweza kuvaa hiyo T-shirt? Maana bado haijakauka," Dylan akamwambia.

Leila akamwangalia kidogo machoni, kisha akatikisa kichwa chake taratibu kukataa. Dylan akamwangalia kwa kujali, naye akanyanyuka na kuzifata nguo zao. Akarudi kwa Leila tena na kumnyanyua ili asimame, kisha akageuka na kuushusha mwili wake chini kidogo, akimwambia apande mgongoni. Leila akatii, na baada ya kupanda mgongoni kwa jamaa, Dylan akamwomba ampatie simu ili awashe tochi kwa ajili ya kumulikia njia. Baada ya kuwasha wakaondoka hapo ili kuelekea nyumbani.

Njia nzima, Leila alikuwa mgongoni tu kwa Dylan, hakushushwa hata mara moja. Dylan alitembea kwa uangalifu, na taratibu ili asianguke kutokana na sehemu zenye utelezi. Hawakuongeleshana chochote kile. Leila alikuwa ametulia tu, akihisi vyema joto la mgongo wa Dylan, kwa kuwa yeye pia hakuvaa chochote juu. Upepo wa baridi ulipuliza, hivyo miili yao ilihisi baridi mara kwa mara, lakini Dylan alikomaa kutembea tu akiwa na Leila mgongoni.

Walifika nyumbani mida ya saa 4 usiku. Wote pale waliwashangaa sana, na pia walikuwa wenye hofu kwa sababu hawakujua walikokuwa wakati wa mvua hiyo kubwa. Emilia akaleta khanga upesi na kumfunika Leila, naye Steven akamfatia Dylan shati ili avae. Shani alikuwa amekasirika sana na kumsema sana Leila.

"....na mbona mmerudi hivi, eeh? Nimempigia mama Conso simu akaniambia ulikuwa umeshaondoka kule mapema... ulienda wapi?" Shani akawa anaendelea kumfokea Leila.

Leila akawa amekaa kimya tu akiwa ameudhika.

"Mama Leila..." Dylan akamwita.

Shani pamoja na wengine wakamtazama.

"...samahani... haikuwa makosa yake. Ni mimi ndiyo nilimchelewesha," Dylan akamtetea Leila.

Leila akamwangalia Dylan, akishangaa kwa nini kadanganya.

"Unamaanisha nini?" Shani akamuuliza kwa ukali.

"Nilikuwa nafanya zoezi nika... nikamwona. Nikamwita nikamwambia... anisubirie ili tuje wote nyumbani. Lakini nikamchelewesha sana, mpaka mvua ikaanza," Dylan akasema.

"Na mbona mmerudi bila kuvaa nguo?" Shani akauliza.

"Mvua ilitunyeshea wakati tunarudi na... Leila akawa ameumia mguu... kwa hiyo ikabidi tutafute sehemu ya kujikinga mpaka mvua ilipoisha. Alikuwa akihisi baridi sana, kwa hiyo hakuweza kuvaa nguo yake... ndiyo nikaja naye hivyo hivyo," akaeleza Dylan.

Shani akamwangalia binti yake, kisha akamtazama tena Dylan kwa mashaka.

"Baraka, mama Leila... naombeni mnisamehe sana kwa jambo hili... nitahakikisha halitokei tena," Dylan akasema kwa unyoofu.

Baraka akamshika begani huku anamtazama kwa kujali.

"Usijali Ethan. Poleni sana kwa kila kitu. Mama Leila alikuwa anawawaza sana kwa hofu maana hatukujua mko wapi. Kaa ili mle. Emilia, wapakulie," Baraka akasema.

Emilia akaenda kuwapakulia chakula.

Leila alikuwa akimwangalia Dylan (Ethan) kwa kuchanganywa sana. Alijiuliza ikiwa alifanya vile kumsaidia au kujifanya yeye ni mtu mzuri sana. Ijapokuwa bado alijawa na kiburi, hakuweza kuzizuia hisia za shukrani kumwelekea Dylan. Sasa ni kama alianza kumwangalia kwa njia tofauti na jinsi alivyomchukulia mwanzoni.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN ▶ ‎

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

ILIPOISHIA....

"....na mbona mmerudi hivi, eeh? Nimempigia mama Conso simu akaniambia ulikuwa umeshaondoka kule mapema...ulienda wapi?" Shani akawa anamfokea Leila.

Leila akawa amekaa kimya tu akiwa ameudhika.

"Mama Leila..." Dylan akamwita.

Shani pamoja na wengine wakamtazama.

"...samahani...haikuwa makosa yake. Ni mimi ndiyo nilimchelewesha," Dylan akamtetea Leila.

Leila akamwangalia Dylan, akishangaa kwa nini kadanganya.

"Unamaanisha nini?" Shani akamuuliza kwa ukali.

"...nilikuwa nafanya zoezi nika...nikamwona. Nikamwita nikamwambia...anisubirie ili tuje wote nyumbani. Lakini nikamchelewesha sana, mpaka mvua ikaanza," Dylan akasema.

"Na mbona mmerudi bila kuvaa nguo?" Shani akauliza.

"Mvua ilitunyeshea wakati tunarudi na...Leila akawa ameumia mguu...kwa hiyo ikabidi tutafute sehemu ya kujikinga mpaka mvua ilipoisha. Alikuwa akihisi baridi sana, kwa hiyo hakuweza kuvaa nguo yake...ndiyo nikaja naye hivyo hivyo," akaeleza Dylan.

Shani akamwangalia binti yake, kisha akamtazama tena Dylan kwa mashaka.

"Baraka, mama Leila...naombeni mnisamehe sana kwa jambo hili...nitahakikisha halitokei tena," Dylan akasema kwa unyoofu.

Baraka akamshika begani huku anamtazama kwa kujali.

"Usijali Ethan. Poleni sana kwa kila kitu. Mama Leila alikuwa anawawaza sana kwa hofu maana hatukujua mko wapi. Kaa ili mle. Emilia, wapakulie," Baraka akasema.

Emilia akaenda kuwapakulia chakula.

Leila alikuwa akimwangalia Dylan (Ethan) kwa kuchanganywa sana. Alijiuliza ikiwa alifanya vile kumsaidia au kujifanya yeye ni mtu mzuri sana. Ijapokuwa bado alijawa na kiburi, hakuweza kuzizuia hisia za shukrani kumwelekea Dylan (Ethan). Sasa ni kama alianza kumwangalia kwa njia tofauti na jinsi alivyomchukulia mwanzoni.

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★

"Steven rudi ukalale, kesho shule," Shani akamwambia mwanae.

"Yaagh... kulala mapema! Yaani naombea mvua kubwa inyeshe kesho nilale mpaka jioni," Steven akaondoka huku analalamika.

Baraka akasogea karibu na mguu wa Leila ulioumia na kujaribu kuunyoosha, lakini Leila alilia kwa maumivu sana, hivyo Baraka akaacha. Emilia alikuwa ameleta vyakula alivyowapakulia kwenye sahani mbili na kuviweka mezani.

"Hamna hata dawa ya kuchua, sasa tutafanyaje?" Shani akauliza kwa kujali.

"Nisaidieni kwenda chumbani," akasema Leila.

"Kula kwanza," Baraka akasema.

"Hapana, sijisikii kula," akasema Leila.

"Chakula kimeshapakuliwa sasa, em' kula bwana," Shani akasema kwa ukali.

"Sijisikii kula, nataka kulala," Leila akasema huku machozi yanamlenga.

Baraka akatazamana machoni na Dylan, wakiambiana bila maneno kuwa Leila ana tatizo fulani bila shaka. Lakini ilibidi Dylan atulize hisia zake kwa kuwa aliwasimulia story tofauti kidogo na ukweli wenyewe. Ikabidi Baraka na Shani waanze kumsaidia Leila anyanyuke ili wampeleke chumbani, lakini akawa analia kwa maumivu aliyohisi mguuni. Shani alikuwa akimwambia ajikaze, lakini Leila aliendelea kuonyesha hangeweza kwenda kwa mtindo huo.

Ndipo Dylan akasogea karibu na kuwaomba wazazi wake ambebe mikononi ili ampeleke chumbani. Wakakubali, naye akamnyanyua taratibu na kufanya binti awe kama amelalia mikononi mwake, huku nyuso zao zikitazamana, kisha akaanza kumpeleka chumbani. Alimlaza kitandani kwa uangalifu, kisha yeye na Baraka wakaondoka humo, wakiwaacha Leila na mama yake.

"...najua wewe siyo wa kukaa na kumsubiria Ethan, labda uwe umerogwa. Niambie ukweli, mlikuwa wapi?" Shani akawa anamshawishi Leila aseme ukweli.

"Mama... naomba uniache. Sijisikii vizuri. Udadisi wako haunisaidii," Leila akamjibu akiwa amelala huku amegeukia upande mwingine.

Shani akamwangalia kwa ufupi, kisha akasonya na kusema, "Utajua mwenyewe sasa."

Akaondoka chumbani hapo baada ya Emilia kuingia. Leila aliendelea kujilaza kimya tu akitafakari matukio ya siku hiyo, na baada ya muda fulani akawa amesinzia.

Dylan alibaki na Baraka sebuleni akipata msosi. Baraka aliongea naye kuhusiana na ishu yake ya kulitengeneza daraja, naye Dylan akamwambia alikuwa anataka kuanza kesho. Baraka alimuuliza kwa mara nyingine kama kweli alikuwa anajua anachokifanya, na kijana huyu akamwambia ijapokuwa bado hakujua ni kwa nini, moyo wake ulimwambia anafahamu vizuri kile ambacho angefanya. Pia, alidokeza kuwa huenda hii ikawa njia nyingine ya kumsaidia ili arudishe kumbukumbu yake mapema.

Baada ya Dylan kumaliza kula, wote walielekea vyumbani ili kupumzika kwa ajili ya kesho.

★★★

Asubuhi kama kawaida, wote waliondoka, isipokuwa Leila na Dylan. Leila aliumwa mguu bado, hivyo hangeweza kwenda kufanya kazi. Shani alikuwa ameongea na mama Conso, mwenye mgahawa ambao Leila alifanyia kazi, akimwombea ruhusa kwa kumtaarifu kuwa Leila alipatwa na ajali ndogo. Ijapokuwa mguu wake uliuma, asubuhi hii alijitahidi kwa kuwa alitembea taratibu kwa kuchechemea. Dylan alimsaidia mara kwa mara kumpa egemeo kama angehitaji kwenda nje, na Leila alijihisi vizuri kila mara kaka huyo alipomsaidia. Hakuleta kiburi tena, ijapokuwa bado moyoni hakuwa amemzoea.

Ilipofika mida ya saa 5, Baraka alimpigia simu Leila kumuuliza mguu unaendelea vipi. Akasema bado anahisi maumivu, lakini Ethan (Dylan) anamsaidia sana. Baraka akamwambia ampe simu "Ethan" ili waongee, naye akamuuliza ikiwa alianza kazi. Dylan alimwambia kuwa bado hakuanza kwa sababu alihisi alihitajika kumwangalia Leila, lakini Baraka akamhakikishia kuwa Leila angekuwa sawa, hivyo kama angetaka kuanza kazi, aanze tu.

Baada ya Dylan kumrudishia simu Leila, alimuuliza ikiwa ingekuwa sawa akimwacha kwenda kufanya kazi fulani.

"Haina shida. Nenda tu," Leila akasema.

"Naona kama... inaweza ikatokea dharura," Dylan akasema kwa kujali.

"Usijali niko sawa. Kila kitu kipo vizuri, chakula kipo, mimi nakuwa chumbani tu, kwo' we nenda wala usiwaze," Leila akamwambia kistaarabu.

"Sawa. Wacha... ngoja niende. Ikitokea...ikitokea dharura nipigie...aagh...sina simu kweli..." Dylan akawa anababaika.

Leila akacheka kwa sauti ya chini.

Hii ndiyo mara ya kwanza Leila anacheka kutokana na kitu alichosema Dylan. Dylan akafarijika sana moyoni kuona badiliko hilo.

"Okay. Baadae," akamuaga.

"Poa," Leila akamjibu.

Kijana akaondoka na kubeba vifaa alivyohitaji kwa siku hiyo. Akafika usawa wa daraja, kukiwa hamna mtu hata mmoja eneo la hapo, naye akaanza kazi sasa. Alifanya vitu jinsi kichwa chake kilivyomwongoza, na alijitahidi kuweka umakini wa hali ya juu ili kufanya mambo kwa njia iliyo bora kabisa.

Baadae, watu fulani waliopita eneo hilo wakiwa wanatokea eneo la upande wa pili walimwona akikomaa na matengenezo, nao wakamuuliza alikuwa anafanya nini. Ndiyo hapa akawaambia alikuwa kwenye harakati za kulitengeneza daraja hilo, na baadhi yao walimwona kuwa mjinga. Wengine walifikiri ameanza kuvuta bangi kama Ishengoma, wakiangalia marasi yake na ndevu zake nyingi, hivyo wakampuuzia tu na kuendelea na mambo yao. Kwa siku hiyo, Dylan alifanikiwa kutengeneza msingi imara wa mwingilio wa daraja hilo, ulioingia chini ya ardhi sana kwa kuuunganisha na ule wa zamani.

★★★

Kila siku baada ya hapo aliendelea kwenda kwenye kivuko hicho, akiongeza vitu, akipunguza vitu, akitengeneza na kulirudisha daraja katika mwonekano wake mpya na uliofaa. Watu wengi walimwambia aache kwa kuwa anajisumbua, na haingechukua muda angekata tamaa. Shani alimvunja sana moyo kuwa hatafanikiwa, lakini Dylan hakuacha kufanya kazi hiyo.

Kadiri siku zilivyozidi kusonga, aliendelea kuwashangaza watu kwa sababu alizidi kulisogeza daraja mbele tu. Baraka angemsaidia mara kwa mara, akifurahia sana utendaji wa kijana huyu. Dylan hakuogopa hata kudondokea kule chini; alijitoa kwa moyo wake wote ili kuwasaidia watu hao.

Wenyeji wa eneo hilo walipoona Dylan amelifikisha daraja nusu ndani ya wiki mbili tu, walishangaa sana. Wengi waliomwona mwanzoni kama mjinga, wakaanza kusaidiana naye kuendeleza ujenzi. Muundo wa daraja wakati huu ulikuwa tata zaidi, kwa sababu mwanzoni vikanyagio vyake vilikuwa vya chuma nyepesi sana (kama bati) na mbao nene, lakini wakati huu Dylan aliweka ZOTE ziwe za chuma ngumu. Hivyo, watu wengi walisaidia kwa kuleta vyuma vingine vingi zaidi na vifaa mbalimbali; wakifata maelekezo yake alipowaongoza jinsi ya kuvipangilia.

Ilikuwa ni wakati wenye kusisimua wengi, kwa sababu bila kutarajia, Dylan alikuwa amewaunganisha watu wote washirikiane kufanya jambo ambalo walitegemea mpaka kupewa msaada na watu wa juu. Sasa wakawa wametambua kuwa walihitaji mkandarasi mmoja tu, tena aliyepoteza kumbukumbu, ili waweze kujenga tena matumaini yaliyokuwa yamebomoka.

Daraja likawa limekamilika ndani ya wiki tano tokea Dylan alipoanza kulitengeneza, kwa kuwa nguvu kazi ilikuwa ya mikono tu. Sasa alichokuwa akifanya ni kuhakikisha sehemu zote muhimu za kulikaza ziko imara.

★★★

Ilikuwa ni Jumamosi moja mida ya jioni watu kadhaa walipokuwa eneo hilo la daraja. Walikuwepo wanaume kwa wanawake na watoto, wakifurahia kutembea-tembea hapo huku Dylan na wenzake baadhi wakihakikisha daraja liko vizuri. Familia yote ya bwana Baraka ilikuwepo pia, na kufikia wakati huu hata Shani alikuwa amemkubali sana jamaa.

Wakati Dylan alipokuwa anaangalia sehemu fulani ya chini ya daraja hilo katikati, aliteleza na kupindukia upande wa pili kama anadondokea kuelekea chini, lakini mkono wake mmoja ukashika kamba nene ya kushikia daraja, hivyo akawa amening'inia. Wengi walishtuka na kuanza kumkimbilia, huku akijitahidi kuendelea kulishikilia kwa utulivu, maana kama angetikisika kidogo tu, mkono ungeteleza. Walifika rafiki zake wawili haraka na kuanza kumvuta, nao wakafanikiwa kumrudisha kwa juu.

Watu walimtazama kwa wasiwasi, wakimuuliza kama yuko sawa, lakini Dylan akaanza kucheka. Wote walimshangaa sana, wakishindwa kuelewa angewezaje kucheka ndani ya hali hiyo. Akanyanyua kidole gumba juu huku anacheka, kuwaonyesha kwamba yuko sawa. Wote wakaanza kucheka pia wakitambua kweli jambo hilo liliburudisha. Watu wengi walipendezwa na kufurahishwa na Dylan, na sasa akawa anaonwa kama mtu mwenye kutegemeka sana.

Uhusiano wake pamoja na Shani na Leila ulizidi kuwa wa kirafiki zaidi. Leila alipendezwa sana na Dylan na hata kumsimulia mara nyingi kwa rafiki zake. Alikuwa amemzoea zaidi sasa, hata walikuwa wanataniana kama kaka na dada wanavyofanya. Shani naye alimwonyesha Dylan heshima zaidi, akitambua kijana huyo alikuwa baraka kwao. Baraka kwa upande mwingine, alimsifia sana kijana wake huyo kwa marafiki, akiwaambia jinsi ambavyo alisaidiana naye mpaka kufanikisha mpango huo. Alijivunia sana.

Baada ya Dylan kuwa ametulia kutokana na kukaribia kuanguka, aliwatangazia watu kuwa daraja lilikuwa limekamilika. Wengi walishangilia, huku baadhi ya wanawake wengi wakimkimbilia na kumkumbatia. Walifurahi sana, na watu wote wakakubaliana kufanya sherehe ndogo kesho kwa Baraka ili kuweza kufurahia mafanikio yao.

Watu wangepita hapo mara kwa mara, wakifurahia kivuko chao kipya baada ya miaka miwili ya kusota wakizunguka kwa kutumia njia ndefu sana. Steven alimsifia sana Dylan kwa kuwa alifurahi kwamba hangewaza tena kuhusu kuamka mapema mno. Habari hizo za daraja kujengwa zilikuwa zimesambaa mpaka maeneo ya mjini zaidi, na watu kadhaa walitaka kuja hapo kujua ni nini kilichofanya mpaka daraja lilioachwa ukiwa kwa miaka miwili na zaidi, litengemae.

★★★

Asubuhi iliyofuata, Jumapili, watu kadhaa walikuwa wamefika hapo kwa bwana Baraka, wakipangilia masuala ya sherehe. Michango ilikuwa imekusanywa kwa uharaka sana, na hii ilionyesha jinsi gani watu walivyokuwa na hamu ya kusherehekea siku hii. Wanawake wengi walikuja na vyombo vyao, wakianza kuandaa mambo ya upishi. Kulikuwa na vyakula mbalimbali ambavyo vilinunuliwa na kuletwa na vijana, ambao walifanya kazi upesi kutokana na kurahisishiwa mambo kwa sababu ya daraja kutengenezwa. Wenye mifugo walileta mbuzi na ng'ombe wa kuchinja kwa ajili ya nyama, na mboga mbalimbali zikaanza kupikwa pia.

Dylan alikuwa pamoja na rafiki zake, hasa sehemu waliyounganishia sabufa kubwa na kompyuta ndogo kwa ajili ya muziki. Fred, yule rafiki yake, alikuwa ni DJ pia na alimiliki ofisi ndogo ya kubani na kuuza CD, na kuwekea watu movie na miziki. Watoto wadogo walicheza muziki pamoja, na maandalizi ya misosi yakaendelea kuwekwa sawa na wanawake. Dylan akaamua kuwaacha ili aelekee saluni kwa ajili ya kutengeneza nywele. Zilikuwa nyingi na ndefu sana wakati huu, hivyo aliona ni bora akiweka mwonekano mpya, hasa baada ya rafiki zake kumwambia mara nyingi kwamba anaonekana kama mtumwa wa wakati ujao!

Alikwenda kwenye saluni eneo la pili na kutengeneza nywele na ndevu zake kwa njia nzuri. Hakuwa amekumbuka chochote kuhusu jinsi alivyopenda kunyoa zamani, lakini alinyoa kwa mtindo kama ule alioupenda. Alizikata rasi mpaka kufikia shingoni, naye alihakikisha anazitengeneza kwa njia ambayo zile nene zingeondolewa na kubaki nyembamba kiasi. Pande za kichwa chake alizinyoa na kuacha nywele laini kidogo sana, na ndevu alizipunguza na kuacha kidogo; zikichongwa vizuri kutokea kwenye timba. Kisha, akatafuta 'rubber band' na kuzifunga rasi zake kwa nyuma ili chache zimwagikie kichwani kama mkia (ponytail) na chache za mbele akaziacha zidondokee pembeni ya uso. Alikuwa na style nzuri sana Dylan hata kama hakukumbuka mambo mengi vizuri.

Akiwa bado mbele ya kioo cha saluni, aliona jambo fulani ambalo lilivuta umakini wake. Kupitia hicho hicho kioo, aliona mwanaume fulani upande wa nje, akiwa amevalia kofia iliyofunika uso wake kiasi, na akiwa kama anamtazama sana. Ilibidi Dylan aendelee kujifanya kama anatengeneza tu mwonekano wake kwa kujiangalia kwenye kioo, lakini kwa kuibia akawa anamwangalia mwanaume huyo.

Hakumjua, na hakuwahi kumwona kabla, kwa nini alikuwa anamtazama sana? Alijiuliza bila kupata jibu. Kisha, akamwona mwanaume huyo anatoa simu yake mfukoni na kuiweka sikioni, naye akaondoka eneo hilo. Dylan hakujua afikie mkataa gani kuhusu mtu huyo; ikiwa labda alikuwa anamtazama kwa nia nzuri au mbaya, ama ikiwa yeye mwenyewe (Dylan) ali-panick tu. Kwa kuwa mwanaume huyo aliondoka eneo hilo, jamaa akaona ampotezee tu.

Baada ya kuridhishwa na mwonekano wake mpya, akatoka zake saluni na kuanza kurejea nyumbani. Watu wengi aliopishana nao walimwangalia sana kutokana na jinsi mwonekano wake mpya ulivyombadilisha. Alipofika kule kwenye sherehe, watu walimsifia sana kwamba amependeza, wengine wakishangaa jinsi mtindo wake wa nywele ulivyomfanya aonekane mdogo. Wanawake na wasichana kadhaa walivutiwa naye, na wengi walikuwa wanajishebedua sana ili aelekeze uangalifu wake kwao, lakini jamaa hakuwa na muda.

Kama ni mwanamke aliyevutiwa zaidi na sura ya Dylan wakati huu kuliko wote, basi hakuwa mwingine ila Leila. Mwanzoni alipomwona alishindwa hata kuendelea na kazi ya kupika, akibaki kumtazama tu mpaka aliposhtuliwa na sauti ya 'Leila si ukoroge hayo maharage!' Uzuri wa Dylan ni kwamba alikuwa mwanaume aliyetulia sana, hivyo mambo kama wanawake hayakumpa presha hata kidogo.

Muda wa msosi uliwadia. Watu walikula, walikunywa, na kuserebuka kupita maelezo. Ilikuwa ni kama eneo lile lote liliishiwa na nafasi kutokana na watu kuwa wengi mno. Hadi vyombo vya kuwekea chakula viliisha, hivyo ikabidi wengine wasubirie waliomaliza kula wawape sahani ili nao wapate msosi. Kutokana na wingi wa chakula, wengi walikuja kumaliza kula saa 11, ndipo muziki wa kujiachia ukaanza. Watu walicheza kwa mbwembwe sana, huku wengine wenye ustaarabu wakifurahia kuwatazama tu.

Watu walicheza sana, na kama ilivyo kawaida ya ma-DJ, Fred alibadili muziki kila mara na kuwapa ladha nyingi nzuri, na sasa akawa akiweka muziki wa nyimbo za aina ya singeli. Wanawake wengi walipenda nyimbo hizo, nao walizicheza kwa furaha sana. Leila na rafiki zake wengi walikuwa wamevaa madera, hivyo walizungusha viuno na kutikisa makalio kwa njia yenye kusisimua. Wanaume kadhaa vijana walijumuika nao kucheza, lakini kwa uangalifu ili wasiguse mke wa mtu.

Baraka na wengine walikuwa wakimshawishi Dylan aende kucheza pia, lakini kwa unyoofu alisema hakujua kucheza; hasa kwa sababu aliona haya. Huyu alikuwa Dylan aliyepoteza kumbukumbu yake, mstaarabu, na mpole. Ingekuwa ni Dylan yule wa zamani aliyekuwa mtundu sana, wote hapo wangemshangaa kwa kuwa angewaonyesha jinsi gani alivyojua mambo.

Fred alipoweka wimbo wa singeli wa msanii Rayvanny akimshirikisha Dulla Makabila, ulioitwa Miss Buza, wanawake walipiga kelele kwa shangwe nyingi. Hata wengine waliokuwa wamekaa pembeni walijiunga nao hapo ili kuonyesha upendo wao kwa wimbo huu. Ilipofika kwenye daraja la wimbo huo (bridge), sauti za juu za wanawake zilisikika zaidi, wakifatisha maneno aliyoimba msanii Rayvanny.

"....ana msitu kwapani, ndala kifuani... Kwenye daladala anapita dirishani... Ghetto anazima taa, vipele mapajani... Ana dera jipya, chupi la zamani... Ayoo yoo yoooh.. huyo Miss Buza...."

Wakaanza kusasambua sasa! (twerking)

"...mama Miss Buza..."

Wanasasambua tu!

"....jamani Miss Buza... Nampenda Miss Buza...."

Mambo haya yote yalimchangamshasana Dylan. Na pia, muda mwingi alimkazia fikra Leila, kwa kuwa mwanamke huyo alicheza huku akimtazama pia. Alifanya mambo kwa njia iliyoonyesha kwamba alimchezea Dylan, kutia ndani na wanawake kadhaa ambao walivutiwa na Dylan. Dylan alipenda sana jinsi Leila alivyoonyesha ufundi wa viuno na usasambuaji.

Baada ya usiku kuwa umeingia, wakubwa waliwasihi vijana wengi waelekee majumbani kwao, na watu baadhi wakaanza kuviondoa vitu kadha wa kadha eneo hilo. Kila mtu alihisi kuburudishwa sana, na sasa bila shaka wangetarajia mambo mengi mazuri yaendelee kutawala eneo hilo baada ya kulirekebisha daraja lao.

★★★

Mambo hayakuwa mazuri upande wa wazazi wake Dylan. Ni kama kila jambo walilofanya baada ya "kifo" cha mwanao halikufanikiwa hata kidogo.

Mr. Bernard pamoja na mtu yule aliyekuwa anashirikiana naye ili kumwangusha Gilbert, walifanikiwa kwa kiwango kikubwa kumharibia sifa yake nzuri kwenye kampuni na kumwondoa kwenye uongozi; tena kwenye kampuni aliyoijenga na kuikuza mwenyewe! Mambo waliyoyafanya watu hawa sanasana ilikuwa ni kusambaza porojo za uwongo kuhusu kifo cha Dylan, kuharibu baadhi ya mipango mingi ya Gilbert, na hasa kuporomosha utendaji kwa kuiba vifaa vingi ambavyo Gilbert alitumia pesa nyingi kuviweka hapo; lengo lao likiwa kukwamisha miradi ya kampuni.

Hivyo, mapato yalishuka kwa kiwango kikubwa, na wafanyakazi wengi walilalamika kutolipwa jinsi walivyostahili. Kwa hiyo washiriki wa bodi ya kampuni, wakiwa na nguvu kubwa ya usemi hapo kutokana na kushikilia hisa za juu zaidi, walimwondoa Gilbert kwenye nafasi ya uraisi wa kampuni na kumweka Mr. Bernard, ambaye alitumia hila nyingi kuwashawishi washiriki hao wafikie uamuzi huo bila Gilbert kujua.

Ilifikia hatua mpaka ikawabidi Gilbert na Jaquelin kuondoka kwenye nyumba yao kwa kuwa waliimudu kupitia pesa zao ambazo ziliunganishwa (linked) na kampuni moja kwa moja; kwa sababu kampuni ilikuwa yao. Lakini sikuzote watu wenye nia mbaya hufanya kila wanachoweza ili kuwaporomosha wengine, na watu hao walifanikiwa kwa hilo. Ikawabidi wazazi hao wa Dylan wahamie kwenye ile nyumba ambayo Gilbert alimpa Dylan, kwa kuwa ilikuwa chini ya jina la mwanao, ambaye aliweka kila jambo lililomhusu kwa kibinafsi sana na siyo kutegemea kampuni.

Jaquelin alikutana na watu wengi aliowafahamu ili wamsaidie kuweza kutatua tatizo lao, hasa wanasheria, lakini kila sehemu ikawa ni kutokufanikiwa tu. Gilbert alitaifishwa kampuni ndani ya muda mfupi sana, na roho ilimuuma mno. Hawakuwa na njia nyingine tena ya kulazimisha mambo, hivyo wakageukia mradi mwingine ambao ungewasaidia kwa wakati huo, yaani mgahawa wa Dylan, Dy-Foods.

Wakati ule alipoondoka na kupatwa na ajali, Dylan alikuwa ameuacha mgahawa wake chini ya uangalizi wa msimamizi wake aliyemwajiri kipindi kile, aliyeitwa Tony, na alikuwa amekwishampatia maelekezo ya kumwajiri Fetty kama msimamizi msaidizi (assistant manager). Kufikia wakati huu, mgahawa huu uliendelea kuingiza pesa nzuri tu, na hata idadi ya waajiriwa iliongezeka. Fetty alikuwa hapo pia kama msimamizi msaidizi, akiwa ameiacha kazi yake ya zamani miezi michache nyuma.

Kwa muda huo wote waliofikiria kwamba Dylan alikuwa amekufa, Gilbert, kabla hajaondolewa kwenye kampuni, alikuwa akiwasiliana na Tony ili kujua maendeleo ya mgahawa huo, na aliongoza mambo bila Jaquelin kujua kwa sababu yeye hakuujali. Lakini wakati huu mambo yalibadilika, naye Jaquelin akawa tayari kujihusisha nao na kusaidia kuupanua zaidi, huku wenzi hao wa ndoa wakijitahidi kutafuta suluhisho la tatizo lao bila kupata matokeo mazuri.....

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN [emoji666] ‎

Muendelezo
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★

Siku chache zikawa zimepita baada ya sherehe ile kufanyika kwa Baraka. Watu waliendelea na mambo yao kama kawaida, naye Dylan aliendelea kumsaidia kazi Baraka na kujipatia pesa ndogo ndogo ambazo zilisaidia familia na mambo yake kadhaa.

Ilikuwa ni Jumamosi tena, naye Dylan akawa uwanjani kwenye eneo la pili, akifanya mazoezi na vijana wenzake. Walinyoosha viungo, walikimbia, na kuchezeshwa mpira na kocha wao pia. Cotable FC ilikuwa ikidhaminiwa na watu wa mitaa yao, sanasana wanaharakati waliopenda mpira. Hawakuwa na mdhamini mkubwa wala nini, lakini walijiendeleza kwa muda mrefu sana. Wakati vijana hao walipokuwa wamemaliza zoezi kwenye mida ya saa 12 jioni na kocha wao kuongea nao, akamwita Dylan pembeni ili azungumze naye.

"Ndiyo nitakuwepo," Dylan akamwambia.

"Ulifikiria kuhusu nilichokwambia?" kocha akamuuliza.

"Kocha... napenda kucheza. Lakini... sijafikiria kucheza mechi kabisa kwa sababu..."

"Najua. Umeshaniambia kwamba unafanya mazoezi nasi kujifurahisha tu," kocha akamkatisha.

Dylan akatikisa kichwa kukubali.

"Nisikilize Ethan. Wewe ni kijana mwenye kipaji sana. Unajua vitu vingi na huwa unafanya mambo mengi hapa ambayo mtu yeyote anajua lazima uhitajike. Sawa unafanya kujifurahisha tu, lakini huwezi jua kipaji chako kitakupeleka wapi usipokionyesha kwa watu," kocha akamwambia.

"Kocha... mimi nakuelewa. Ningeweza kufanya hivyo, lakini maisha yangu yanachanganya. Nahitaji utulivu wa kiakili ili..."

"Ethan... hili suala halihitaji kuwaza saaana. Mwanangu, una kipaji. Siyo cha kutengeneza madaraja tu, ila una kipaji kama zawadi kutoka kwa Mola. Usiipuuze. Cheza mechi ya kesho... ninajua unaweza, na utaweza kutusaidia sana tuwafumue wale mafala," kocha akamsisitizia.

"Ahahahah... kocha bwana! Aam...kiukweli...bado sijui..."

"Usijali. Sitakulazimisha. Lakini nataka ucheze japo kipindi cha kwanza tu dogo langu. Unaonaje?"

"Sidhani kama hiyo itakuwa busara maana kuna vijana wengi ambao wanajua hapa... kipindi cha kwanza sitaweza.."

"Ethan nisiki..."

"Kocha usijali, nimekuelewa. Nachoweza kufanya...ni kuwa sub... angalau hivyo tu... kwa kuwa bado sina uhakika sana kama hata ikiwa natakiwa kucheza," akasema Dylan.

"Wewe ni kijana unayejiamini. Ila unapaswa kuacha kujishusha mno, kuna fursa nyingi kwa ajili yako. Vijana wenzako hao huwa wanatamani kucheza kwa mtindo wako ila hawakwambii tu..." kocha akamsifia.

Dylan akatabasamu na kutikisa kichwa chake.

"Sawa basi. Kwa kuwa unaona kuwa sub ndiyo itafaa kwako nitakuweka uwe sub," kocha akamwambia.

"Wengine watashangaa! 'Ethan si alisemaga hachezi, leo vipi?'" Dylan akasema kiutani.

"Hahahah... usijali, niachie mimi. Ila nikikuweka dakika ya 90 usilalamike."

"Ahah... itakuwa vizuri."

Baada ya wawili hawa kuongea hayo, wote wakaanza kuelekea makwao. Mechi aliyokuwa anaizungumzia kocha ni ile mechi kati ya timu yao na timu ya mjini, iliyokuwa inasubiriwa na wadau wa huku kwa muda sasa. Timu ya Town City FC ingekuja kuchezea kwenye uwanja wa eneo la huku, hivyo Dylan na wenzake ndiyo wangekuwa wenyeji wakiwakaribisha wageni.

Kocha huyo alikuwa amemshawishi Dylan tokea kitambo kuwa ajiunge na timu yao kama mchezaji, lakini Dylan alikataa mara zote kwa kuwa kama alivyosema, alicheza mpira na kufanya mazoezi ili kujifurahisha tu, na siyo kwa ajili ya mashindano. Kocha alipendezwa sana na uchezaji wa Dylan, kwa kuwa sikuzote alicheza kwa ufundi mzuri wa kuwachanganya waliomkaba, mambo ambayo alizoea kufanya kule Brazil kwa miaka mingi aliyokuwa huko. Hiyo ndiyo sababu kocha aliamini Dylan angekuwa msaada mkubwa kwa mechi hiyo ya kesho.

Dylan alifika nyumbani mida ya saa 1 kasoro, usiku, naye alimkuta Leila akiwa pamoja na rafiki zake wawili pale nje, wakiwa wanapiga story. Alipowasalimia, wote walimwitikia huku wanatabasamu kwa shauku, kisha akaingia ndani na kuwaacha rafiki za Leila wakimwambia kwa sauti ya chini jinsi Ethan (Dylan) alivyo wa moto. Haikuchukua dakika nyingi, naye Dylan akatoka nje akiwa kifua wazi na kuvalia kaptura, kisha akafata maji kwenye ndoo na kuingia bafuni kuoga; wanawake hao wakimtazama tu.

"Jamani shosti...ah aaahh! Mmzuri! Nipe namba yake bwana!" akasema rafiki ya Leila aliyeitwa Sada.

"We naye! Nitakuja kumwambia Enock... we subiri," Leila akamtishia.

Sada akasonya, kisha akasema, "Enock na mimi wapi na wapi?"

"Hee! Makubwa! Unakana buzi lako kwa kuwa umeona tu kifua hiko?" akasema rafiki mwenza, aliyeitwa Pili.

"Ndo' namshangaa na mimi," akasema Leila.

"Mmm...huna lolote... eti 'namshangoo na mimi,' we mwenyewe hapo unamtaka Ethan," Sada akamwambia Leila.

"Inahusu? Umemkana Enock kwa nini?" Leila akamuuliza.

"Hayakuhusu," Sada akasema.

"Aa-aaah jibu swali. Mara ya mwisho alipokunyandua nini kilitokea?" Leila akamuuliza.

"Ahahah...inaonekana aligeuka nyuma akaona mtako wake," Pili akatania.

"Hahahahah... kweli shosti? Tuambiane..." Leila akasema huku anacheka.

"Nimewaambia hayawahusu..." Sada akasema huku anawarembulia.

"Tulikuwa tutako tudogo tumebanana... tumepaukaaa!" akasema Pili, na wote wakacheka kwa sauti ya juu.

"Nyie em' acheni umbea," Shani akasema kutokea ndani.

"Yaani! Kila tukipandana kananipiga makofi tu kwenye tako," akasema Sada, na wenzake wakacheka kidogo.

"Halafu sipendagi hiyo yaani!" akasema Pili.

"Ukiona unapigwa mikofi ujue tu hela aliyokupa ulitakiwa kurudisha chenji ila mshkaji kusema anaona jau," akasema Leila kiutani.

"Ahahahah... utakuta kimekazana kupiga mikofi wakati maajabu yenyewe zero," akasema Pili.

"Mwenzangu!" akasema Sada.

Marafiki hawa waliendelea kupiga umbea mpaka Dylan alipotoka bafuni. Wakati anaianika boxer yake kwenye kamba, Sada na Pili wakawa wanamfinya-finya Leila kwa kumwonyesha atazame jinsi mashine ya jamaa ilivyojichora kwenye kaptura yake nyepesi kwa mbele. Kisha alipoanza kuelekea ndani, wakajifanya walikuwa wanaendelea na mambo yao tu.

Dylan hata hakuwa na muda wa kufikiria walichokuwa wanajadili hapo. Upendezi wa Leila kumwelekea Dylan ulizidi kuongezeka, lakini bado hakuonyesha hilo, kwa kuwa ni kama alimsubirishia Dylan apige hatua ya kwanza; ijapokuwa rafiki zake wengi walimfanya aone kama anachelewa, nao wangemwahi jamaa ikiwa angeendelea kujichelewesha.

Emilia alikuwepo ndani pia akijisomea kwa utulivu. Mitihani yao ilipangwa kuanza Jumatatu, hivyo hizi zilikuwa dakika za mwisho. Kwa sababu asizozijua, Dylan alikuwa na kawaida ya kumsaidia Emilia hasa kwa masomo ya Mathematics, Physics, Geography, na mengine; akimfundisha mambo kadha wa kadha tokea alipoanza masuala ya ujenzi wa daraja. Hii ilitokana na ubongo wake kuwa tayari unajua vitu vingi kuhusiana na masomo hayo, hivyo wakati huu walikuwa pamoja wakipitia mambo mengi wakiwa pamoja na Steven.

★★★

Jumapili jioni ikafika. Watu wengi walikuwepo uwanjani kwa ajili ya kushabikia timu za maeneo yao. Timu ya Town ilifika mapema na wachezaji wake kuanza kupasha miili yao, wakiwakuta wachezaji wa Cotable wanapasha pia. Baraka, Leila, Emilia, Steven na marafiki wengi wa Dylan walikuwepo pia, huku Shani akibaki nyumbani kwa sababu alizozijua yeye.

Watu walifurahia kumwona Dylan akiwa anafanya mazoezi hapo, na wengi walitamani kumwona akicheza. Watu fulani wenye pesa kutoka maeneo ya mjini walikuja pia kuangalia vipaji hivi, ili kutazama ubora wa timu hizi na kuweza kutoa michango yao katika kuviendeleza. Baadae, wachezaji walijiweka tayari kwa ajili ya mchezo sasa, na refa akapuliza filimbi ili mechi ianze.

Dylan alikuwa ameketi pamoja na wachezaji wenzake nje ya uwanja wakitazama mpira huu, na kwa watu ambao walitaka kumwona akicheza, jambo hilo liliwakwaza sana. Hata kocha mwenyewe alitaka sana kumweka Dylan kipindi cha kwanza, lakini aliheshimu maamuzi ya kijana huyo ya kuomba acheze cha pili. Timu zilicheza kwa kujituma sana, huku kwa asilimia kubwa timu ya mjini ikionekana kuwa na nguvu zaidi. Lakini Cotable walijitahidi sana kulinda upande wao, hivyo mashambulizi mengi ya Town yaligonga mwamba. Dakika za kipindi cha kwanza ziliisha timu zikiwa bila magoli.

Kipindi cha pili kilipoanza, watu wengi walitarajia bila shaka kungekuwa na mabadiliko. Pande zote zilijituma sana, na bado hawakufungana mpaka inafikia dakika ya 70. Kocha alikuwa amebadili wachezaji wachache, na sasa akamwambia Dylan aingie kwa kumpumzisha mchezaji mwingine mfungaji.

Baada ya rafiki zake na watu wengine wa kwao kuona anaanza kuingia, walishangilia sana, na kufanya wapinzani wajiulize ni nani huyo. Hawakuwahi hata kumwona akicheza, lakini kutokana na umaarufu wake kule kwao wa kutengeneza daraja, walihisi tu kwamba na hapo angeweka maajabu; hasa wanawake. Alipoingia aliongea kifupi na nahodha wa timu kuhusu ujumbe ambao kocha alimwambia ampe, kisha akajiweka tayari kuanza kazi.

Mpira uliendelea bila Dylan kuwa ameugusa, na sekunde kadhaa baadae ukatoka nje kutokea katikati ya uwanja. Ilikuwa ni Cotable ndiyo walitakiwa kurusha ndani, hivyo Dylan akasogea karibu na mrushaji huku anafatwa nyuma na mkabaji, na baada ya kurushiwa tu, akaupiga mpira upesi kwa kisigino na kugeukia upesi upande wa nyuma, akikutana nao nyuma ya mkabaji huyo ambaye hakutarajia kasi hiyo.

Watu walishangilia jambo hilo, naye Dylan akatoa pasi kwa mwenzake huku akikimbilia mbele. Mwenzake aliutanguliza mpira mbele ili Dylan akutane nao, na sasa wapinzani wakaona kuna hatari kwa sababu Dylan alikuwa na kasi sana. Wawili walimkaribia kumkaba baada ya yeye kuufikia mpira, lakini akatoa pasi ya haraka kwa mwenzake pembeni na kuwaruka, na hapo hapo mwenzake akaiunganisha pasi hiyo kwa kuupiga mpira akitumia kisigino kumwelekea Dylan kwa mbele; karibu kabisa na mstari wa dimba la nje la wapinzani. Dylan alikutana na mpira huo na hapo hapo kuupiga kwa nguvu sana kulielekea goli, huku akiwa amezungukwa na wakabaji. Mpira ulifanikiwa kuupita mkono wa golikipa aliyejitahidi kuurukia ili auzuie, nao ukaingia ndani ya nyavu.

Wenyeji walipiga kelele nyingi za shangwe! Ilikuwa imemchukua Dylan dakika tatu tu kuubadili mchezo huu kwa kuonyesha ustadi wa hali ya juu sana. Akiwa kwenye furaha nyingi, alikimbilia ukingoni mwa uwanja na kuruka sarakasi kwa kuuviringisha mwili wake hewani. Alipotua chini, alijishangaa sana amewezaje kufanya hivyo, kwa kuwa hakukumbuka kwamba alijihusisha na masuala ya sarakasi kipindi cha nyuma. Akiwa bado anajishangaa, alirukiwa na rundo la wachezaji wenzake ambao walikuwa wamemkimbilia kwa kufurahia goli lake zuri.

Walipoanza kurejea katikati ya uwanja, Dylan alimsonta Baraka na kumpigia saluti, naye Baraka akafurahi sana. Mechi iliendelea, huku wanawake na wanaume wa upande wa timu ya Cotable wakiimba na baadhi kupuliza mavuvuzela ili kuwatia moyo wachezaji wao. Goli la Dylan liliandikwa kuwa ni la dakika ya 73, na sasa wakawa wakiendelea kupambana ili ikiwezekana waongeze lingine.

Wachezaji wa timu ya Town walianza kucheza kwa hasira kwa kuwa walihofia wangeaibishwa na timu ya Cotable waliyoidharau kwa muda mrefu. Kuna wakati ugomvi ulitokea baina ya wachezaji pale mchezaji wa mjini alipomchezea vibaya Dylan na kumwangusha kimakusudi, lakini akapewa adhabu na mechi ikaendelea. Cotable walijitahidi sana kuongeza bidii katika mashambulizi na ulinzi, huku Dylan akiwafurahisha watu kwa kuwasumbua sana wakabaji akiwapiga chenga zilizowafanya waonekane duni.

Mechi ilimalizika hatimaye; Cotable 1-0 Town. Mashabiki wa Cotable walivamia uwanja wakishangilia sana, huku Dylan akikimbiliwa na wanawake wengi ili wamkumbatie. Ijapokuwa ilionwa kuwa mechi ya kirafiki, kwa wenyeji ilikuwa mechi ya kuwanyamazisha wageni baada ya kuwatandika goli siku hiyo. Watu wengi waliotazama mechi walimpongeza sana Dylan, naye akawa anaelekeza sifa zote kwa timu nzima.

Kuna wakati ambao Dylan alitambua kwamba mwanaume yule aliyemwona siku ile ameenda kunyoa, ambaye alimwona akimtazama sana kupitia kioo, alikuwepo hapo pia. Alijitahidi kumwangalia mara kwa mara ili kuona ikiwa alikuwa amemkazia fikira sana kama siku ile, lakini wakati huu hakuona hali ya namna hiyo.

★★★

"Ulifanyaje vile... kuruka soti? Ilikuwa noma sana!" Steven akasema kwa shauku.

"Ahahah... me mwenyewe hata sijui. Nashangaa tu niliweza," Dylan akasema kwa unyoofu.

"Labda zamani ulikuwaga unaruka sarakasi eti?" akauliza Leila.

"Inawezekana. Yaani kuna wakati nafanya vitu...automatically mpaka najishangaa," akasema Dylan.

"Eee kweli, hata hiyo 'automatically'umeisema automatically..." Steven akatania, na wote wakacheka.

Hayo yalikuwa ni maongezi yao wakati wanarudi nyumbani wakiwa wenye furaha sana. Steven alimtungia jina lingine Dylan na kumwita Ronaldo, kwa kuwa alicheza kwa ufundi sana kama mchezaji huyo aliyempenda. Walimsimulia Shani jinsi mambo yalivyokwenda uwanjani, na jinsi Ethan (Dylan) alivyowaaibishawakabaji. Shani akampongeza sana Ethan, kisha baada ya hapo kijana akaingia bafuni kuoga.

★★★

Siku iliyofuata, kama kawaida Emilia na Steven walikwenda shuleni, Shani na Leila migahawani, Baraka na Dylan kazini kwao.

Wakati wa mida ya mchana, kuna gari fulani ya rangi ya shaba (silver), aina ya Volkswagen Touareg, ilifika maeneo hayo kwenye barabara iliyoelekea nyumbani kwa Baraka, na kusimama usawa wa daraja lile. Alishuka mwanamke fulani, mrefu, aliyevalia gauni iliyofikia magotini yenye kubana mwili wake wenye umbo zuri, na usoni akiwa amevaa miwani nyeusi ya urembo, kisha akasogea kwenye mwingilio wa daraja hilo na kusimama hapo.

Alilitazama kwa makini sana. Alipendezwa na muundo wake tata ambao ulimwambia kuwa bila shaka aliyeongoza ujenzi huu alikuwa ni mtu mwenye ujuzi na ustadi mwingi sana. Mwanamke huyu alikuwa amesikia habari kuhusu kijana fulani aliyefanya jambo hilo lenye kusisimua sana, naye alitaka kujua ni nani huyo. Kwa kuliangalia wakati huu, aliridhika sana na mtindo huo wa ujenzi, naye akapanga kwenye akili yake kumtafuta kijana huyo ili ikiwezekana aweze kushirikiana naye katika mambo fulani.

Upande wa Baraka na Dylan, mambo yalikwenda kama kawaida kazini kwao, na sasa ilikuwa imefika mida ya jioni pale Baraka alipopewa ujumbe fulani na mke wake kupitia simu.

"Ethan..." Baraka akamwita Dylan.

"Naam..." akaitika na kumfata.

"Kuna jambo naomba unisaidie..." Baraka akasema.

"Ndiyo..."

"Mama Leila amenipigia. Amenikumbusha kuhusu jambo fulani muhimu ambalo Leila alitakiwa kufanya leo, linawahusu wanawake hawa. Sasa...Leila alikuwa anatakiwa kulishughulikia, na ni muhimu sana, lakini inaonekana amesahau kwa kuwa alikuwa anatakiwa kumpelekea taarifa mama Theodota yule..."

"Ndiyo..."

"...eeeh, lakini mpaka sasa hivi hajafika kule. Mimi na mama yake tumejaribu kumpigia, simu yake haipatikani, inaonekana imezimika sijui... Sasa nilikuwa naomba umwahi pale kwa ma' Conso anapofanyia kazi ili umkumbushe hilo..."

"Umejaribu kumpigia mama Conso? Mpigie ili ampe simu uongee naye," Dylan akashauri.

"Ndiyo nimejaribu lakini na yeye hapokei simu yake. Na muda unaenda sasa. Mama Leila amekosa mtu wa kutuma pale ndiyo akaniambia nikuagize, maana anajua una spidi," Baraka akasema.

"Ahahah... sawa haina shida. Ngoja nimuwahi."

"Eee fanya hivyo kijana wangu. Ukimkuta we mwambie kwamba mama yake amesema aende kwa mama Theodota kuhusu ile ishu... ataelewa," Baraka akasema.

"Sawa sawa. Kwa hiyo... nitakukuta au?" Dylan akauliza kabla ya kuondoka.

"Aa...hamna nafunga muda siyo mrefu. Kama vipi msindikize kule kabisa ili mrudi wote nyumbani," Baraka akamwambia.

"Haya sawa."

Dylan akatoka haraka na kuanza kuelekea kule kwenye mgahawa wa mama Conso ili amfikishie Leila ujumbe ule upesi.

★★★

Leila alikuwa akimalizia kazi kadhaa kwenye mgahawa aliofanyia kazi, kama vile usafi wa viti, eneo la ndani, vyombo, na mambo mengine madogo-madogo; akisaidiana na wenzake wawili ukiachilia mbali mama Conso. Walikuwa na kawaida ya kufunga mgahawa saa 12 au saa 1 jioni, lakini kama kungekuwa na wateja zaidi wangeendelea mpaka mida ya usiku; ikitegemea kama bado kuna chakula.

Ilikuwa wakati alipotoka kwenye meza kuifuta, pale aliposikia sauti anayoifahamu ikimwita. Baada ya kugeuka kuthibitisha, alikuta kweli ilikuwa ni 'ex' wake, aliyeitwa Fabian. Baada ya Leila kuwa amesimama, jamaa alimfata na kumwambia alikuwa amekuja eneo hilo kutembea na marafiki zake. Alianza kumwambia jinsi gani amem-miss sana na kwamba hakuna mtu mwingine mtamu kama Leila kitandani. Leila hakutaka kabisa wazo la kutoka tena na Fabian liingie akilini; mara mia atoke na mtu mgeni. Aliachana naye na kwenda kuendelea na kazi zake.

Baada ya kumaliza kazi na mama Conso kuanza mipango ya kufunga, Leila pamoja na wengine waliondoka pia. Yeye alitoka kuelekea nyumbani, na wakati akiwa njiani kabla hajafika, akavutwa mkono nyuma kwenye sehemu ambayo ilikuwa na kichaka ambacho kiliingia kwenye eneo la wazi kidogo. Alipomtazama aliyemvuta, akakuta ni 'ex' wake huyo, na kwa kuudhika akauvuta mkono wake na kuutoa kwenye mkono wa Fabian kwa nguvu.

"Leila sikiliza bwana. Me sikutegemea kukutana nawe huku kabisa. Me naona ilikuwa mipango ya Mungu tukutane. Nimekumiss sana babe. Tusahau tu yale turudiane mpenzi wangu," Fabian akambembeleza.

"Me nilishasahau mbona! Nilishasahau kila kitu kabisa, kutia ndani wewe," akajibu Leila kwa uthabiti.

"Aaaaa baby...usiwe hivyo. Najua bado unani-feel sana," Fabian akasema kwa kujitutumua.

Fabian alijaribu kufanya Leila aonekane kama dhaifu; asiyemaanisha anachosema, na jambo hilo lilimuudhi sana binti. Akamsogelea karibu na kumshika kiuno, akijaribu kumpiga busu. Leila akajitoa mikononi mwake na kutaka kuondoka, lakini jamaa akamvuta mkono wake tena na kumweka kinywani mwake akimpiga busu; akifanya hivyo kama mapenzi ya tamthilia za wahindi.

Ni kufikia hapo ndipo Leila alipokasirika haswa. Hakuhisi kitu chochote kumwelekea Fabian tena zaidi ya kumwonea huruma kwa sababu ya utu aliokuwa nao. Alimsukuma na kumwasha kofi usoni ili kumwonyesha kwamba hakuwa akitania. Fabian alishtuka sana. Kama mtu ambaye anafikiri 'aaah huyu demu anajishaua tu, nikimpa mate kidogo atalegea,' hatua hiyo Leila aliyochukua ilimshangaza sana.

Alimvuta binti kwa nguvu akijaribu kumpiga busu la lazima; huku Leila akijitahidi kujinasua kwa nguvu pia. Fabian alikuwa na kiburi sana hivyo alitaka kuonyesha kuwa hawezi kushindwa na binti huyo. Ni wakati huo ndipo alihisi akivutwa nyuma kwa nguvu na kuangushwa chini. Aliponyanyua uso juu, alitambua kuwa ilikuwa ni Ethan, yaani Dylan. Leila alijihisi usalama wa ghafla baada ya kumwona Dylan pale, naye akasimama nyuma yake.

"Oooh..Ethan... ahahah...kaka mtu. Kumbe mlikuja wote huku eeh..." akasema Fabian kwa kujishaua huku akinyanyuka.

Fabian alikuwa na mwili mkubwa kidogo zaidi ya Dylan, hivyo alikuwa anamdharau. Dylan hakusema lolote lile zaidi ya kumtazama kwa makini. Alijua kuwa Leila alitoka kimapenzi na Fabian, lakini hakujua kwamba walikuwa wameachana wiki kadhaa nyuma. Wakati huu alikuwa akielekea kule kwa mama Conso ili amwahi Leila kumpatia ujumbe wa mama yake, ndipo akawasikia kwenye kichaka cha hapo. Hali iliyokuwa ikiendelea hapo baada ya yeye kufika ilitosha kumwambia kwamba kulikuwa na tatizo.

"Hayakuhusu mambo yangu na Leila, kwo' potea," Fabian akamwamrisha Dylan.

"Sina chochote nilichobakiza kwako. We ni fala sana Fabian. Una girlfriend halafu una-cheat. Bado tena unajifanya kama unaweza kuya-control maisha yangu; we umekuwa nani?" akasema Leila kwa hisia.

Fabian akajaribu kumfata Leila ili amshike, lakini Dylan akamsukuma. Akarusha ngumi ili impige Dylan, lakini Dylan akainama na wakati huo huo kumpiga kwenye tumbo kwa kutumia goti, kisha kumtandika usoni kwa kiwiko. Fabian alipokuwa akiyumba kidogo, Dylan akamwongezea ngumi ya pua usoni. Alifanya hayo yote kwa kasi sana na Fabian akadondoka chini huku Leila anatazama akiwa ameziba mdomo.

"Basi Ethan, mwache. Hafai huyo," Leila akajaribu kumtuliza jamaa.

Ni wakati huo Fabian aliona chupa tupu ya bia ikiwa chini na kuichukua kisha kuipasua. Akanyanyuka, huku damu ikivuja puani mwake, na kuanza kumfata Dylan akiwa ameshika kipande cha chupa chenye makali.

Dylan alimwonyeshea kwa mkono Leila kuwa asogee pembeni, na baada ya Leila kwenda pembeni kwa hofu, Dylan alimwahi Fabian kwa njia yenye ustadi na kuupiga mkono wake kwa nguvu. Hii ilisababisha kidole cha mwisho cha mkono wa Fabian kivunjike, naye akatoa kelele ya maumivu. Kuanzia hapo, Dylan alimshushia kipondo cha maana sana, mpaka jamaa akalegea. Wapita njia kadhaa walisogea eneo hilo na kumzuia Dylan (Ethan) asiendelee, huku jamaa akipumua kwa hasira.

Leila alimwangalia Dylan kwa hisia nyingi zenye hofu, kwa kuwa jambo hilo lilikuwa lenye kushtua. Baada ya kuwauliza nini kinaendelea, Leila aliwaambia kila kitu kuanzia jinsi Fabian alivyomfatilia na kujaribu kumlazimisha mapenzi. Watu walimfukuza Fabian hapo na kumtishia kuwaambia polisi ikiwa wangemkamata tena anajaribu jambo hilo. Alikuwa amejaa damu usoni, naye akaondoka akijivuta-vuta kutokana na maumivu aliyohisi.

Baada ya hapo, Dylan alimgeukia Leila na kumshika mkono, kisha wakaanza kuondoka. Giza lilikuwa limeingia, lakini taa za nyumba mbalimbali ziliangaza maeneo ya nje. Alipomfikisha sehemu nzuri, akampa pole kutokana na kitendo cha Fabian. Leila akamshukuru sana kwa kumwokoa, naye Dylan akampatia ujumbe wa mama yake. Leila alishtuka kwa sababu alikuwa ameshasahau, na kusema hakupatikana kwa kuwa simu yake ilikuwa imezima na alitaka kwenda kuichajishia nyumbani.

Hivyo ikabidi wawili hao wachukue bodaboda upesi na kuelekea kule. Kweli Leila alikuta anasubiriwa, naye akaomba samahani na kuanza kuongea na wanawake waliokuwepo, huku Dylan akimsubiri nje. Baada ya kama nusu saa, wanawake wakatoka nje na kusalimiana na Dylan. Baadhi wakaondoka, naye Leila akawa anamuaga mama Theodota kwa kumpa shukrani, kisha yeye na Dylan pia wakaanza kurejea nyumbani.

Wakati wa kurudi hawakupanda bodaboda na kuamua kutembea kwa kuwa Leila alikuwa amewasiliana na mama yake kupitia simu ya mama Theodota kumjulisha alikuwa anarudi pamoja na Dylan. Wakiwa njiani, Leila alimfungukia Dylan kwa mambo mengi sana. Alimweleza kuhusu usaliti wa Fabian wiki kadhaa zilizopita alipomkuta na mwanamke mwingine wakipeana denda. Dylan alipata kujua kuwa, siku ile ambayo Leila alipanda kwenye ule mlima na kudumbukia shimoni, ndiyo ilikuwa siku ambayo Leila alimkamata Fabian na mwanamke wake huyo, ndiyo kwa hasira kali akawa ameenda huko ili awe peke yake.

Leila alieleza pia kwamba, kwa sababu alimpenda Fabian, alilia sana siku hiyo kwa kuhisi maumivu mengi ya usaliti, ndiyo maana hata alimtendea Dylan kwa hasira. Akaomba samahani kuhusu hilo, naye Dylan akamhakikishia haikuwa na shida tena kwa kuwa yalikuwa mapito. Walipofika usawa wa daraja, Leila akasimama na kuuangalia mkono wa Dylan aliotumia kumpiga ngumi nyingi 'ex' wake.

"Mkono wako unauma?" akamuuliza kwa kujali.

"Hapana...niko sawa," Dylan akajibu.

"Nisamehe sana Ethan. Yaani...we ndo' mtu pekee ambaye sikutaka huyo fala akuingie kabisa," akasema Leila kwa sauti yenye hisia.

"Leila, acha kuomba samahani. Haujafanya kitu chochote cha kujihisi hatia. Tena kiukweli, nimefurahia sana kum-punch huyo 'fala,' na sijui hata ni kwa nini," Dylan akatania.

"Najua. Ila....kuna hali fulani yaani... ile hali ya kutotaka uwepo sehemu ambayo ingenifanya nitambue jinsi gani nilivyokuwa mpumbavu kutoka kimapenzi na mtu kama yeye... japokuwa tayari nalijua hilo," Leila akaongea kwa hisia za huzuni.

"Leila... usiwaze kabisa juu ya hilo. Mimi huwa sijaji mtu kabisa. Mmeachana muda siyo mrefu sana kwa hiyo naelewa kuwa hisia nyingi zinahusika. Kiukweli, me natumaini hautarudiana na huyo 'fala' kamwe baada ya kukufanyia alichokufanyia.Lakini, bado mwisho wa siku mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe, na mimi nitaheshimu hilo," Dylan akamtia moyo kwa upole.

Leila alifarijika sana baada ya rafiki yake huyu kumfariji namna hiyo. Hata alianza kujiuliza ni nini ambacho kilimfanya amdharau kaka wa watu kipindi kile. Akamsogelea karibu zaidi, kisha akashika rasi zake mbili za mbele na kuzivuta-vuta kwa wororo. Dylan alikuwa anamtazama tu, akijua bila shaka mwanamke huyu alipenda yale aliyomwambia. Leila akamkumbatia Dylan kwa furaha, naye Dylan akazungusha mikono yake kiunoni kwa binti na kuwa kama anamnyanyua, akionyesha amelikubali kumbatio lake. Leila akashusha pumzi na kumbana zaidi jamaa.

"Nataka uendelee kuwa upande wangu Ethan," Leila akamwomba kwa sauti yenye deko.

Dylan akatabasamu na kusema, "Ondoa shaka," huku akimbana kidogo tena akiwa amefumba macho.

Leila akatoa mguno kwa pumzi iliyosikika kwa mbali, na bila kufikiri, akainamisha midomo yake kwenye shingo ya Dylan na kuibusu taratibu sana kimahaba!

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom