Elton Tonny
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 396
- 2,976
- Thread starter
- #101
Kweli kabisa kaka πMkuu tuombe uzima hapo mbele tunaweza kuwa angel investors wa entertainment industry
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli kabisa kaka πMkuu tuombe uzima hapo mbele tunaweza kuwa angel investors wa entertainment industry
Duuu, Beatrice ni Mnyambisi kabisaDYLAN
Story by Elton Tonny
Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
(R-rated 18+)
Enjoy!
β β β β β β β β β β β β β β β β β β
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
β β β β β β β β β β β β β β β β β β
2012
"Kwa nini unakuwa hivi lakini Gilbert? Hakuna chochote kinachopotea zaidi ya sisi kuwa na furaha..."
"No..hapana. Yaani...kiukweli ninachohisi tu ni hisia za hatia...siwezi kuendelea kufanya hivi..."
"Kwa nini?"
"Kwa sababu sisi sote tuna familia, Beatrice. Una mume nami nina..."
"Acha kujifanya kama vile mambo yako sawa kwenye ndoa zetu. Unajua vizuri kwamba Jaquelin anaku-cheat...na mimi vile vile Alfred anani-cheat..."
"...ndiyo lakini huoni kwamba na sisi tunafanya hivyo hivyo pia? Ni sawa kwao kutoka na watu wengine...lakini mimi kiukweli sitaki kuendelea kuwa kama wao, ijapokuwa inaumiza..."
Maongezi haya yalikuwa ni baina ya Gilbert na Beatrice. Wawili hawa walikuwa wamekutana kwenye chumba cha hoteli moja ya kifahari ili kuzungumzia uhusiano wao huu uliokuwa unaendelea kwa muda fulani sasa. Gilbert alikuwa akimwambia Beatrice kuwa walitakiwa kuacha, lakini Beatrice hakutaka kukatisha uhusiano wao bila kujali sababu zilizomfanya Gilbert afikie uamuzi huu.
"Ahah...kwa hiyo nini, utarudi nyumbani na kumsubiri "mke" wako umpokee kwa furaha, ukijua wazi ametoka kuliwa huko nje?" Beatrice akasema kwa hisia kali.
"Jaquelin amepoteza mwelekeo wake kwa muda mrefu...lakini bado ni mama wa mtoto wangu...sidhani Dylan atafurahi kujua ninaishi maisha yaliyojaa upotovu wa..."
"Upotovu? Unamaanisha kwamba unaniona mimi kama uchafu?"
"Hapana...hapana Beatrice. Ninathamini jambo hili kati yetu... lakini wewe na mimi tuko kwenye commitment..."
"To hell with that! Gilbert ninakupenda sana...niko tayari kumtaliki Alfred ili tuwe sote kwa njia unayotaka."
"Beatrice..."
"...ni kitu cha kawaida sana mbona. Wala usiumize kichwa...wewe fanya hivyo hivyo pia kwa kuwa..."
"Beatrice tafadhali...hatupaswi kuchukua maamuzi kwa njia hiyo. Tuna watoto...sidhani kama watafurahi kujua tunatenda namna hii. Pia tuko ndani ya kifungo cha ahadi za ndoa tulizotoa..."
"Who cares?!"
"Beatrice..."
"Usiniambie masuala ya ahadi za ndoa. Gilbert, tumerudiana ndani ya muda mfupi tu baada ya miaka yote hiyo, tumeonyeshana jinsi gani ilivyokuwa makosa sisi kufunga ndoa na watu wengine, na unajua tumependana tokea vidato. Kwa muda mrefu sana nilikuwa nataka itokee njia ili turudiane, na sasa nimekupata tena...siwezi kukuachia kirahisi-rahisi...hapana..."
"Beatrice..."
"Mm-mm..."
"...nisikilize. Sifanyi hivi kwa sababu labda najiona kuwa mtakatifu..."
"Ila kumbe? Tumefurahia mapenzi pamoja halafu sasa unataka tu kusema eti ahadi ya ndoa ndiyo inakuzuia?"
"...ni kwa sababu jambo hili ni kubwa zaidi yako na mimi. Mambo mengi yanahusika Beatrice...tayari tuna familia...hata kama tukiachana na wenzetu kisheria, bado itashangaza wengi ikiwa tutaungana na kuwafanya hata watoto wetu wafikiri kwamba sisi ndiyo tumewatendea ubaya wazazi wenzetu..."
"Basi kama ni hivyo, tutafute njia ya kuwafichua wenzetu usaliti wao, tuutumie kama ushahidi..."
"Beatrice no...haita..."
Beatrice akaushika uso wa Gilbert na kumwangalia usoni kwa hisia.
"Nimeshasema sitaki kukupoteza tena Gilbert...tutapata tu njia mpenzi wangu...nakuomba tafadhali...I love you so much..." Beatrice akasema.
Gilbert akawa anamwangalia tu kwa hisia, naye Beatrice akamsogelea mdomoni na kumpiga busu laini.
Mambo yalikuwa hivi: Gilbert alikutana na Beatrice kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake wakati anasoma kidato cha pili. Beatrice alikuwa amehamishiwa shuleni alikosomea Gilbert, na mwanzoni walizoeana kama marafiki tu wa kawaida mpaka walipofika kidato cha tatu, ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi. Walipendana sana kwa kuwa waliendelea kuwa pamoja mpaka walipomaliza kidato cha nne na kutengana, siyo kuachana, ila kurudi kwa familia zao ambazo ziliishi mikoa tofauti.
Waliendelea kuwasiliana, na mara kwa mara hata Gilbert alifanya mipango kwa jitihada nyingi ili wakutane na kuonyeshana upendo. Baadae, walishindwa kabisa kupatana tena baada ya Beatrice kupoteza njia ya kuwasiliana na Gilbert, hivyo mpaka wakati wanaingia chuo, hawakuwa wamewasiliana tena kwa zaidi ya miaka mitano. Kwa hiyo wote walijikuta wakiingia kwenye mahusiano mapya yaliyopelekea mpaka kufunga ndoa.
Kilichokuja kuwakutanisha ilikuwa ni siku ya sendoff ya Jaquelin, wakati Gilbert alipomwona Beatrice kwenye ukumbi wa sherehe yao hiyo. Baadae Jaquelin alipomfichua bwana harusi, Beatrice pia alishangaa kumwona Gilbert kuwa ndiye bwana harusi. Hadi unafika ule muda wa kuwasalimu maharusi pale mbele, Beatrice alimkumbatia Gilbert kwa hisia sana, bila yeyote kujua historia ya wawili hawa. Baadae, ilibidi Gilbert amuulize Jaquelin ikiwa alifahamiana na Beatrice, naye akamwambia ndiyo ni rafiki yake sana ambaye alimwacha akiendelea na chuo walichosomea pamoja.
Gilbert aliweza kupata namba mpya za Beatrice kwa ajili ya mawasiliano, na baada ya kuwasiliana naye akawa ametambua kwamba Beatrice pia aliolewa. Mume wa Beatrice, Alfred, alikuwa mwenye miradi mikubwa ya uuzaji wa madawa muhimu kutoka nje na kusambazia 'pharmacy' nyingi nchini. Kwa hiyo ujuani wao ukasaidia kujenga urafiki wa karibu kati ya wanne hawa; Alfred, Beatrice, Gilbert, na Jaquelin, nao wakawa karibu na kusaidiana kwa mambo mengi bila ya wenzi wa Gilbert na Beatrice kujua historia ya kimapenzi ya wawili hawa (ijapokuwa baadae waliweka wazi kuwa walisoma sekondari pamoja).
Kufikia wakati huu sasa ambao Gilbert alikuwa kwenye chumba cha hoteli na Beatrice, ndoa yake pamoja na Jaquelin ilikuwa na matatizo mengi sana. Gilbert alipata kujua kwamba Jaquelin alikuwa akitoka kimapenzi na mtu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake wa zamani, na ilikuwa ni kama hakujali kwa sababu ijapokuwa waliishi kama mume na mke, uhusiano wao wa ndoa haukuwa mzuri kipindi hiki. Gilbert aliamua kumwacha Jaquelin afanye analotaka, naye akaazimia kusonga tu mbele na mambo yake mengine.
Ndipo siku moja Gilbert akiwa anaongea na Beatrice, alimwambia kuwa rafiki yake (yaani Jaquelin) alikuwa anatoka nje ya ndoa, na hapa Beatrice pia akamwambia kuwa mume wake alifanya hivyo hivyo. Kwa hiyo, wawili hawa wakaanza kujenga ukaribu zaidi kwa kuwasiliana mara nyingi mpaka mwisho wa siku wakajikuta wanazama upya kwenye penzi lao lililoishia njiani miaka mingi iliyopita.
Lakini dhamiri ya Gilbert ilimsumbua sana ijapokuwa Jaquelin alikuwa amemkosea, kwa sababu bado aliheshimu cheo chake kama mama wa mwanae, Dylan. Hakutaka siku moja Dylan arudi akute ndoa yao imevurugika namna hiyo, lakini pia hakujua angeweza kushughulika vipi na mama yake. Beatrice akawa ndiyo kama njia ya kumfanya aondoe mikazo yake, kwa sababu bado ndani ya moyo wake alikuwa na hisia za upendo kumwelekea, lakini alijua kuendeleza uhusiano huu usio halali kungeleta shida zaidi, hivyo ni lazima angetafuta njia ili kuweka mambo kwenye mpangilio mzuri.
Beatrice akaendelea kumpiga denda Gilbert kimahaba huku anampapasa-papasa mwilini taratibu chumbani hapo, na sasa wote wakawa wamepandwa na hisi za mahaba kuelekeana. Ijapokuwa Gilbert aliona haikufaa, bado moyo wake ulitaka sana kuwa na Beatrice, hivyo akaruhusu penzi hili Beatrice alilotaka kumpatia hapo liendelee.
Wawili hawa hawakutambua kuwa walikuwa wakifatiliwa na mtu fulani kwa muda sasa. Kihalisi aliyekuwa akifatiliwa ni Beatrice, na sasa mtu huyo aliyekuwa anawafatilia alipata kuwaona wakiwa pamoja na mara kwa mara wakiingia hotelini hapo, hivyo alikuwa amekitafuta mapema chumba hiki walichopenda kukitumia na kutegesha camera ndogo sana (micro camera) ambayo ilirekodi kila jambo walilofanya wakati huu. Gilbert na Beatrice walikaa kama nusu saa baada ya kupeana mapenzi motomoto, kisha wakaisafisha miili yao na kuondoka. Sikuzote alianza kutoka kwanza Gilbert na kumwacha Beatrice akae kama dakika 15 hapo, kisha na Beatrice angeondoka baadae; wakifanya hivi kujilinda. Lakini sasa mambo yalikuwa yameharibika.
Kufikia kipindi hiki, Beatrice alikuwa mkuu (principal) wa chuo kikuu cha biashara. Alfred, mume wa Beatrice, alikuwa ameikuza miradi yake miaka mingi ya karibuni na kufanya familia yote kwa ujumla iwe yenye pesa nyingi sana. Binti yao, Harleen, alikuwa ameanza kusomea udaktari kwenye chuo kikuu nje ya nchi; akiwa na miaka 19 tu, na mwana wao David mwenye miaka 7 alikuwa masomoni kwenye shule nzuri ya international, ambako aliishi huko huko pia (boarding).
Baada ya Beatrice kurudi nyumbani akitokea chuoni, alikopita baada ya kuondoka kwenye hoteli ile, alimkuta Alfred akiwa chumbani. Alikuwa amekaa kitandani akionekana kuwaza jambo fulani. Beatrice akamsalimu, naye Alfred akamwangalia na kutabasamu, kisha akasimama na kuitikia salamu yake.
"Za chuo?" Alfred akauliza.
"Safi tu. Ndiyo nimetoka huko, panaboa kweli," Beatrice akadanganya.
"Pole. Ndiyo kazi," Alfred akamwambia.
"Mbona mapema leo?" Beatrice akauliza.
"Hakukuwa na mambo mengi leo. Pia...nilikuwa nataka kukuona," Alfred akajibu.
"Kama ni hivyo si ungenipigia simu halafu ukanitoa out?" Beatrice akasema kwa maringo huku anamsogelea.
"Kwa nini twende out wakati nyumbani ni pazuri zaidi? Tuifanyie hapa hapa tu," Alfred akajibu.
"Ahah...hiyo itakuwa date ya aina gani sasa?" Beatrice akauliza kimadoido.
"Hakuna kinachoshindikana...ndiyo maana hadi kuna breakfast in bed," Alfred akatania.
"Ahahah... kwa hiyo ungependa tuianze vipi hiyo date?" Beatrice akauliza huku anamsogelea Alfred mdomoni.
"Mhm...namna hii..."
Alfred akasema hivyo kisha kumwasha kofi la nguvu usoni! Beatrice alianguka chini na kuanza kulia, akishika uso wake kusitiri maumivu aliyohisi.
"Alfred! Kwa nini unanipiga?"
"Oh pole...nilifikiri ungefurahia zaidi tukiianza date yetu namna hiyo...hujapenda?" Alfred akamuuliza kikejeli huku anachuchumaa na kumshika shavu.
"Usiniguse! Umepatwa na kichaa!" Beatrice akasema kwa hasira.
Alfred akamtandika kofi lingine usoni na kufanya Beatrice aendelee kulia.
"Wewe ndiye mwenye kichaa, malaya mkubwa wewe!" Alfred akafoka.
"Alfred...nimekukosea nini? Kwa nini unanionea?"
"Nakuonea? Nakuonea eeh?"
Alfred akachukua simu yake na kuweka video fulani, kisha akamwonyeshea Beatrice. Macho ya Beatrice yalimtoka kwa mshangao baada ya kujiona kwenye video akiwa kwenye chumba kile cha hoteli pamoja na Gilbert. Alishindwa kuelewa Alfred alipata vipi video hiyo ambayo hakujua hata ilichukuliwa vipi. Maongezi yake pamoja na Gilbert yalisikika, naye Alfred akaipeleka mbele kufikia sehemu waliyokuwa wanafanya mapenzi kitandani. Beatrice alichoka! Akabaki kulia tu huku woga mwingi ukimwingia.
"Nini hiki Beatrice?"
Beatrice akaendelea kulia tu.
"...unadiriki kutoka nje ya ndoa yetu bila sababu yoyote! Unakosa nini kwangu Beatrice? Kuna kitu ambacho unahisi sijakutoshelezea? Eeh? Nijibu mpumbavu wewe!" Alfred akasema kwa hasira.
"Alfred...mume wangu..."
"Usiniite mume wako! Beatrice nimejitoa kadiri gani kwako ili kuifanya familia yetu iwe yenye furaha? Pesa zipo, watoto wapo, mapenzi nakupa jinsi utakavyo...leo hii unamvulia nguo mwanaume mwingine? Nimekukosea nini?"
Beatrice akaishika miguu ya Alfred huku akilia kwa huzuni.
"Usiniguse...don't..don't touch me! Endelea kusema sasa kwamba ninakuonea...ongea!"
Beatrice akainamisha kichwa chake chini huku akilia.
"...eti Alfred anani-cheat...nimeku-cheat lini mimi Beatrice? Na nani? Sema nimeku-cheat na nani...unanisingizia jambo lisilo la kweli ili kuhalalisha ufedhuli wako sivyo? Halafu huyu mpumbavu kumbe anajifanya ni rafiki yangu lakini na yeye ni mshenzi tu kama wewe! Mnafanya usali...aisee!"
"Alfred... Alfred... mimi...sija...nahitaji unielewe..."
"Nikuelewe vipi? Oh..principal wa chuo kikuu nieleweshe somo hili tafadhali..."
"...Alfred nakupenda...please...ni...ni..."
"Ni nini? Unataka kusema ni shetani ndiyo amekupitia tu? Why didn't he JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala you himself then?! Ilikuwa vipi ukafika kwa Gilbert?"
Beatrice akaendelea kulia kwa kuhisi hatia kuu moyoni.
Kwa upande wa Gilbert, ilikuwa ni kweli kwamba Jaquelin alifanya usaliti uliomchanganya akili mpaka akajikuta anaingia kwenye penzi na Beatrice, ambaye alimwambia pia kwamba Alfred alitoka nje ya ndoa. Lakini kwa upande wa Beatrice ilikuwa ni uwongo, Alfred hakuwa akitoka nje ya ndoa, bali ni kwa sababu ya tamaa yake ya kibinafsi ya kutaka kuwa na Gilbert tena ndiyo iliyomfanya amdanganye vile.
Kwa muda fulani, Alfred alianza kuingiwa na mashaka kuhusu nyendo za mke wake, hivyo aliamua kuajiri mtu wa kumfatilia kwa ukaribu ili ajue kama kulikuwa na kitu anaficha. Sasa akawa ametambua kwamba mke wake na rafiki yake walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, kitu ambacho kilimuumiza sana.
"Sasa nisikilize..." Alfred akasema huku akiwa ameshasimama.
Beatrice akamwangalia huku analia.
"...kuanzia sasa...sitaki tena kuwa na wewe!"
"No...Alfred..."
"...umesema kwamba unachotaka ni kunitaliki ili uwe na huyo mtu wako si ndiyo? Usijali...utaipata..."
"Alfred tafadhali...usifanye hivi...tuongee please my..."
"Don't touch me..don't touch me! Haujui ni kiasi gani umeniumiza we mwanamke! Nimekupa kila kitu... Usijali mama, kama ni talaka unayotaka, basi utaipata. Lakini kwanza kabisa ni lazima niwaonyeshe wazazi wako huu upuuzi..."
"Nooo...Alfred please... usi..."
"...na KILA MTU nitahakikisha anaiona video hii ili wajue jinsi gani unavyotia kinyaa!"
"...Alfred mume wangu..."
"Nimesema usiniguse! Mshenzi mkubwa wewe!" Alfred akafoka na kumpiga teke la begani.
Beatrice akaanguka chini huku analia sana.
"....ninaondoka sasa hivi kwenda kuhalalisha unachokitaka...nikirudi...nisikukute wewe au chochote kinachokuhusu ndani ya hii nyumba...la sivyo nitakuua!"
Alfred alikuwa amekasirika sana. Beatrice alimsihi sana asifanye hivyo, lakini mwanaume hakujali. Akaifata droo na kutoa vitu fulani, kisha akaanza kuuelekea mlango. Beatrice akanyanyuka na kumfata kisha kumkumbatia kwa nyuma huku akilia, lakini Alfred akamtoa mwilini kwake kwa nguvu na kumsukuma, naye Beatrice akadondokea chini huku analia. Alfred akatoka akiwa na hasira kali na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake, kisha akaondoka upesi.
Beatrice akabaki kutaharuki asijue la kufanya. Aliwaza mengi; ikiwa Alfred angeionyesha video hiyo kwa wazazi, watoto, marafiki, na watu wengi waliomheshimu, mambo mengi sana yangeharibika. Akaona hapaswi kuendelea kukaa na kulia tu, bali afanye jambo fulani ili kuibadili akili ya mume wake. Lakini hakujua la kufanya. Alitangatanga sana chumbani hapo kama ana kichaa, akipiga mito ya kitanda na kuvuruga vitu vingi vya humo kwa hasira nyingi. Akaelekea kwenye makabati na droo akitafuta kitu ambacho hata hakikueleweka, na kwa kukosa chochote cha kumsaidia aliivuta droo ya mwisho ya kabati kwa hasira na kuirusha pembeni kwa nguvu; ikisababisha vitu vingi vilivyokuwemo kudondokea na kutapakaa chini.
Akapiga magoti akilia kwa uchungu sana, kisha macho yake yakaganda juu ya kitu kimoja kilichokuwa chini hapo baada ya droo hiyo kuangukia chini. Ilikuwa ni bastola ya Alfred. Alikuwa na bastola kwa ajili ya kujilinda, lakini hakuwa na kawaida ya kuitumia. Kufikia wakati huu, mara ya mwisho kuitumia ilikuwa ni miaka 9 iliyopita, alipomtishia mfanya fujo fulani. Ni Beatrice peke yake ndiye aliyejua kuhusu bastola hiyo kuwa ndani humo, lakini hakuwa ameifikiria hata kidogo.
Ila sasa, baada ya kuiona hapo, wazo lile, lile wazo la kishetani, likaingia akilini mwake. Alijua hangeweza kumshawishi Alfred hata kidogo aache kuchukua hatua aliyomwambia, lakini vipi kama angeweza kumnyamazisha kabisa?
Akaifata bastola hiyo na kuichukua, kisha akasimama polepole huku anaitazama kwa umakini. Alikuwa anapumua kwa kwikwi nyingi za kilio, lakini sasa akajituliza na kufuta machozi yake. Akili mbaya ya kutaka kufanya ubaya mbaya sana ilivaa kichwa chake kwa ghafla, naye akaenda kwenye kabati na kutoa sweta lake kubwa, lililokuwa na kofia ya kufunika kichwa kutokea mgongoni, kisha akalikunja vizuri na kuliweka ndani ya mfuko, pamoja na ile bastola. Akatoka chumbani hapo na kuelekea nje kwenye gari lake.
Beatrice alikuwa mwanamke mwenye akili sana. Alichofanya, alimpigia simu Harleen na kumwambia kwamba hawezi kumpata baba yake kwa simu, hivyo yeye (Harleen) ajaribu kumpigia ili aone kama anaweza kumpata, kwa kusema huenda namba yake (Beatrice) kwenye simu ya Alfred ilijifunga. Bila Harleen kujua, Beatrice alikuwa ameunganisha simu yake na ya Harleen ili akimpigia baba yake simu, pale tu atakapopokea, Beatrice aweze kuangalia sehemu aliyopo Alfred (location) kwa kutumia app ya ufatiliaji kwenye simu yake. Alijua wazi ikiwa yeye ndiyo angempigia Alfred, asingepokea na hata kum-block. Hivyo, baada ya Harleen kumpigia baba yake, Beatrice akaweza kujua kule alikokuwa. Alianza kuendesha gari kuelekea huko huku bado akiwasikiliza walivyokuwa wanaongea.
Harleen alimwambia baba yake kwamba mama yake alikuwa akimtafuta lakini anashindwa kumpata, hivyo amtafute na pia aangalie simu yake huenda alimfungia kimakosa. Kwa busara, Alfred alimwambia angefanya hivyo, bila kusema chochote kilichotokea. Beatrice aliwasikiliza walipoagana kwa kuambiana mambo yenye kugusa hisia, naye akawa analia tu kwa kufikiria jinsi gani jambo alilotaka kufanya lingewaumiza sana watoto wake. Lakini alikuwa ameshaiwekea akili yake fikira ya kwamba hakukuwa na njia nyingine; hii ndiyo iliyoonekana kuwa suluhisho pekee.
Maeneo ambayo Alfred alikwenda yalikuwa yenye wapita njia wachache sana. Mwanaume huyo alikuwa kwenye bar kubwa akinywa pombe, kutokana na kuwa na mawazo mengi. Alijawa na huzuni nyingi pia, hivyo alikuwa amejipeleka hapo ili atafakari vitu huku anashushia pombe taratibu. Pombe ilikuwa imeshaanza kukigonga kichwa chake, naye aliona haingekuwa busara kuendelea kunywa kwa kuwa angehitaji kuendesha, hivyo akatumia muda mwingi kukaa tu hapo bila kuendelea kunywa.
Beatrice alikuwa ameegesha gari lake umbali mfupi kutoka kwenye bar hiyo, akiwa ameliona gari la mume wake hapo nje. Alijua bila shaka Alfred angekuwa mule ndani, hivyo akakaa kusubiri akiwa mwenye wasiwasi mwingi sana. Kufikia sasa, alikuwa amevaa sweta lake lile na kuishika bastola mikononi mwake, huku akipumua kwa msisimko mkubwa wa kile ambacho angefanya.
Ilifika mida ya saa 2 usiku, naye Alfred akaona atoke tu hapo na kuelekea nyumbani; na alikuwa ameshaiwekea akili yake jambo moja kuwa, kama angekuta Beatrice bado yuko huko, basi angemfungashia virago na kumfukuza yeye mwenyewe. Watoto wake wangemwelewa tu; aliwaza hivyo. Ile amefika nje na kuanza kulielekea gari lake, alisimama baada ya kuona gari ambalo alijua ni la mke wake. Alishangaa kiasi na kujiuliza Beatrice alijuaje alikokuwa, lakini alijua tu kwamba alimfata hapo bila shaka ili kumwomba samahani hata zaidi.
Beatrice akajikaza baada ya kumwona Alfred, kisha akavalia kofia ya sweta lake kichwani, ambayo iliufunika uso wake kiasi, na bastola akaificha nyuma ya kiuno chake, kisha akatoka na kuanza kumfata. Alfred alimwangalia kwa hisia kali sana, akikumbukia mambo yote aliyoyaona kwenye video ile. Wakati huu, Beatrice alikuwa amejipa ujasiri wa hali ya juu sana kiasi kwamba yeye mwenyewe alijiuliza aliutolea wapi. Kihalisi alikuwa na woga uliopitiliza wa kupoteza kila kitu ikiwa Alfred angefanya alichosema, kwa hivyo hiyo ikawa sababu ya kutosha kwake kuamua auondoe uhai wake.
"Unafanya nini hapa?" Alfred akamuuliza baada ya Beatrice kusimama umbali mfupi.
Mwanamke akawa anamwangalia tu huku anapumua haraka-haraka. Alfred akatikisa kichwa chake kwa kusikitika, kisha akashika mkono wa kufungulia mlango wa gari lake.
"Nadhani nilijieleza vizuri. Sitaki kukuona tena...natumaini sitakuta uchafu wako wowote kwenye nyumba yangu," Alfred akasema.
Kisha akauvuta mlango wa gari nao ukafunguka, na hapo Beatrice akamwita kwa jina lake. Alfred alipomtazama, akakuta ameshikilia bastola kwa mikono miwili huku amemwelekezea. Alishtuka na kuingiwa na hofu kubwa kwa kuwa hakutegemea hilo.
"Beatrice... unafanya nini?" Alfred akauliza.
"Hata mimi sitaki kukuona tena!" Beatrice akasema kwa sauti tetemeshi.
Na hapo hapo akafyatua risasi iliyompata Alfred katikati ya kifua chake!
β β β β β β β β β
ITAENDELEA
β β β β β β β β β
WhatsApp +255 787 604 893
Oyaaa nawe unaunga mkono akufe? [emoji23][emoji23] asife, azinduke aseme halafu apalaraizi atunzwe kwa wema wakeBaraka has gone so soon, he paid the big and major sacrifice towards the Dylan's observation. Missed calls na sms aliyomtumia Dylan ni alert na information nzuri na za wazi kabisa
Beatrice aliact vizuri ndani ya ukumbi baada ya kugundua ulinzi wa mule ndani na mejiexpose kijinga kabisa kupiga simu ya madhara katika eneo la wazi.