Simulizi - DYLAN

Simulizi - DYLAN

DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


2012

"Kwa nini unakuwa hivi lakini Gilbert? Hakuna chochote kinachopotea zaidi ya sisi kuwa na furaha..."

"No..hapana. Yaani...kiukweli ninachohisi tu ni hisia za hatia...siwezi kuendelea kufanya hivi..."

"Kwa nini?"

"Kwa sababu sisi sote tuna familia, Beatrice. Una mume nami nina..."

"Acha kujifanya kama vile mambo yako sawa kwenye ndoa zetu. Unajua vizuri kwamba Jaquelin anaku-cheat...na mimi vile vile Alfred anani-cheat..."

"...ndiyo lakini huoni kwamba na sisi tunafanya hivyo hivyo pia? Ni sawa kwao kutoka na watu wengine...lakini mimi kiukweli sitaki kuendelea kuwa kama wao, ijapokuwa inaumiza..."

Maongezi haya yalikuwa ni baina ya Gilbert na Beatrice. Wawili hawa walikuwa wamekutana kwenye chumba cha hoteli moja ya kifahari ili kuzungumzia uhusiano wao huu uliokuwa unaendelea kwa muda fulani sasa. Gilbert alikuwa akimwambia Beatrice kuwa walitakiwa kuacha, lakini Beatrice hakutaka kukatisha uhusiano wao bila kujali sababu zilizomfanya Gilbert afikie uamuzi huu.

"Ahah...kwa hiyo nini, utarudi nyumbani na kumsubiri "mke" wako umpokee kwa furaha, ukijua wazi ametoka kuliwa huko nje?" Beatrice akasema kwa hisia kali.

"Jaquelin amepoteza mwelekeo wake kwa muda mrefu...lakini bado ni mama wa mtoto wangu...sidhani Dylan atafurahi kujua ninaishi maisha yaliyojaa upotovu wa..."

"Upotovu? Unamaanisha kwamba unaniona mimi kama uchafu?"

"Hapana...hapana Beatrice. Ninathamini jambo hili kati yetu... lakini wewe na mimi tuko kwenye commitment..."

"To hell with that! Gilbert ninakupenda sana...niko tayari kumtaliki Alfred ili tuwe sote kwa njia unayotaka."

"Beatrice..."

"...ni kitu cha kawaida sana mbona. Wala usiumize kichwa...wewe fanya hivyo hivyo pia kwa kuwa..."

"Beatrice tafadhali...hatupaswi kuchukua maamuzi kwa njia hiyo. Tuna watoto...sidhani kama watafurahi kujua tunatenda namna hii. Pia tuko ndani ya kifungo cha ahadi za ndoa tulizotoa..."

"Who cares?!"

"Beatrice..."

"Usiniambie masuala ya ahadi za ndoa. Gilbert, tumerudiana ndani ya muda mfupi tu baada ya miaka yote hiyo, tumeonyeshana jinsi gani ilivyokuwa makosa sisi kufunga ndoa na watu wengine, na unajua tumependana tokea vidato. Kwa muda mrefu sana nilikuwa nataka itokee njia ili turudiane, na sasa nimekupata tena...siwezi kukuachia kirahisi-rahisi...hapana..."

"Beatrice..."

"Mm-mm..."

"...nisikilize. Sifanyi hivi kwa sababu labda najiona kuwa mtakatifu..."

"Ila kumbe? Tumefurahia mapenzi pamoja halafu sasa unataka tu kusema eti ahadi ya ndoa ndiyo inakuzuia?"

"...ni kwa sababu jambo hili ni kubwa zaidi yako na mimi. Mambo mengi yanahusika Beatrice...tayari tuna familia...hata kama tukiachana na wenzetu kisheria, bado itashangaza wengi ikiwa tutaungana na kuwafanya hata watoto wetu wafikiri kwamba sisi ndiyo tumewatendea ubaya wazazi wenzetu..."

"Basi kama ni hivyo, tutafute njia ya kuwafichua wenzetu usaliti wao, tuutumie kama ushahidi..."

"Beatrice no...haita..."

Beatrice akaushika uso wa Gilbert na kumwangalia usoni kwa hisia.

"Nimeshasema sitaki kukupoteza tena Gilbert...tutapata tu njia mpenzi wangu...nakuomba tafadhali...I love you so much..." Beatrice akasema.

Gilbert akawa anamwangalia tu kwa hisia, naye Beatrice akamsogelea mdomoni na kumpiga busu laini.

Mambo yalikuwa hivi: Gilbert alikutana na Beatrice kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake wakati anasoma kidato cha pili. Beatrice alikuwa amehamishiwa shuleni alikosomea Gilbert, na mwanzoni walizoeana kama marafiki tu wa kawaida mpaka walipofika kidato cha tatu, ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi. Walipendana sana kwa kuwa waliendelea kuwa pamoja mpaka walipomaliza kidato cha nne na kutengana, siyo kuachana, ila kurudi kwa familia zao ambazo ziliishi mikoa tofauti.

Waliendelea kuwasiliana, na mara kwa mara hata Gilbert alifanya mipango kwa jitihada nyingi ili wakutane na kuonyeshana upendo. Baadae, walishindwa kabisa kupatana tena baada ya Beatrice kupoteza njia ya kuwasiliana na Gilbert, hivyo mpaka wakati wanaingia chuo, hawakuwa wamewasiliana tena kwa zaidi ya miaka mitano. Kwa hiyo wote walijikuta wakiingia kwenye mahusiano mapya yaliyopelekea mpaka kufunga ndoa.

Kilichokuja kuwakutanisha ilikuwa ni siku ya sendoff ya Jaquelin, wakati Gilbert alipomwona Beatrice kwenye ukumbi wa sherehe yao hiyo. Baadae Jaquelin alipomfichua bwana harusi, Beatrice pia alishangaa kumwona Gilbert kuwa ndiye bwana harusi. Hadi unafika ule muda wa kuwasalimu maharusi pale mbele, Beatrice alimkumbatia Gilbert kwa hisia sana, bila yeyote kujua historia ya wawili hawa. Baadae, ilibidi Gilbert amuulize Jaquelin ikiwa alifahamiana na Beatrice, naye akamwambia ndiyo ni rafiki yake sana ambaye alimwacha akiendelea na chuo walichosomea pamoja.

Gilbert aliweza kupata namba mpya za Beatrice kwa ajili ya mawasiliano, na baada ya kuwasiliana naye akawa ametambua kwamba Beatrice pia aliolewa. Mume wa Beatrice, Alfred, alikuwa mwenye miradi mikubwa ya uuzaji wa madawa muhimu kutoka nje na kusambazia 'pharmacy' nyingi nchini. Kwa hiyo ujuani wao ukasaidia kujenga urafiki wa karibu kati ya wanne hawa; Alfred, Beatrice, Gilbert, na Jaquelin, nao wakawa karibu na kusaidiana kwa mambo mengi bila ya wenzi wa Gilbert na Beatrice kujua historia ya kimapenzi ya wawili hawa (ijapokuwa baadae waliweka wazi kuwa walisoma sekondari pamoja).

Kufikia wakati huu sasa ambao Gilbert alikuwa kwenye chumba cha hoteli na Beatrice, ndoa yake pamoja na Jaquelin ilikuwa na matatizo mengi sana. Gilbert alipata kujua kwamba Jaquelin alikuwa akitoka kimapenzi na mtu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake wa zamani, na ilikuwa ni kama hakujali kwa sababu ijapokuwa waliishi kama mume na mke, uhusiano wao wa ndoa haukuwa mzuri kipindi hiki. Gilbert aliamua kumwacha Jaquelin afanye analotaka, naye akaazimia kusonga tu mbele na mambo yake mengine.

Ndipo siku moja Gilbert akiwa anaongea na Beatrice, alimwambia kuwa rafiki yake (yaani Jaquelin) alikuwa anatoka nje ya ndoa, na hapa Beatrice pia akamwambia kuwa mume wake alifanya hivyo hivyo. Kwa hiyo, wawili hawa wakaanza kujenga ukaribu zaidi kwa kuwasiliana mara nyingi mpaka mwisho wa siku wakajikuta wanazama upya kwenye penzi lao lililoishia njiani miaka mingi iliyopita.

Lakini dhamiri ya Gilbert ilimsumbua sana ijapokuwa Jaquelin alikuwa amemkosea, kwa sababu bado aliheshimu cheo chake kama mama wa mwanae, Dylan. Hakutaka siku moja Dylan arudi akute ndoa yao imevurugika namna hiyo, lakini pia hakujua angeweza kushughulika vipi na mama yake. Beatrice akawa ndiyo kama njia ya kumfanya aondoe mikazo yake, kwa sababu bado ndani ya moyo wake alikuwa na hisia za upendo kumwelekea, lakini alijua kuendeleza uhusiano huu usio halali kungeleta shida zaidi, hivyo ni lazima angetafuta njia ili kuweka mambo kwenye mpangilio mzuri.

Beatrice akaendelea kumpiga denda Gilbert kimahaba huku anampapasa-papasa mwilini taratibu chumbani hapo, na sasa wote wakawa wamepandwa na hisi za mahaba kuelekeana. Ijapokuwa Gilbert aliona haikufaa, bado moyo wake ulitaka sana kuwa na Beatrice, hivyo akaruhusu penzi hili Beatrice alilotaka kumpatia hapo liendelee.

Wawili hawa hawakutambua kuwa walikuwa wakifatiliwa na mtu fulani kwa muda sasa. Kihalisi aliyekuwa akifatiliwa ni Beatrice, na sasa mtu huyo aliyekuwa anawafatilia alipata kuwaona wakiwa pamoja na mara kwa mara wakiingia hotelini hapo, hivyo alikuwa amekitafuta mapema chumba hiki walichopenda kukitumia na kutegesha camera ndogo sana (micro camera) ambayo ilirekodi kila jambo walilofanya wakati huu. Gilbert na Beatrice walikaa kama nusu saa baada ya kupeana mapenzi motomoto, kisha wakaisafisha miili yao na kuondoka. Sikuzote alianza kutoka kwanza Gilbert na kumwacha Beatrice akae kama dakika 15 hapo, kisha na Beatrice angeondoka baadae; wakifanya hivi kujilinda. Lakini sasa mambo yalikuwa yameharibika.

Kufikia kipindi hiki, Beatrice alikuwa mkuu (principal) wa chuo kikuu cha biashara. Alfred, mume wa Beatrice, alikuwa ameikuza miradi yake miaka mingi ya karibuni na kufanya familia yote kwa ujumla iwe yenye pesa nyingi sana. Binti yao, Harleen, alikuwa ameanza kusomea udaktari kwenye chuo kikuu nje ya nchi; akiwa na miaka 19 tu, na mwana wao David mwenye miaka 7 alikuwa masomoni kwenye shule nzuri ya international, ambako aliishi huko huko pia (boarding).

Baada ya Beatrice kurudi nyumbani akitokea chuoni, alikopita baada ya kuondoka kwenye hoteli ile, alimkuta Alfred akiwa chumbani. Alikuwa amekaa kitandani akionekana kuwaza jambo fulani. Beatrice akamsalimu, naye Alfred akamwangalia na kutabasamu, kisha akasimama na kuitikia salamu yake.

"Za chuo?" Alfred akauliza.

"Safi tu. Ndiyo nimetoka huko, panaboa kweli," Beatrice akadanganya.

"Pole. Ndiyo kazi," Alfred akamwambia.

"Mbona mapema leo?" Beatrice akauliza.

"Hakukuwa na mambo mengi leo. Pia...nilikuwa nataka kukuona," Alfred akajibu.

"Kama ni hivyo si ungenipigia simu halafu ukanitoa out?" Beatrice akasema kwa maringo huku anamsogelea.

"Kwa nini twende out wakati nyumbani ni pazuri zaidi? Tuifanyie hapa hapa tu," Alfred akajibu.

"Ahah...hiyo itakuwa date ya aina gani sasa?" Beatrice akauliza kimadoido.

"Hakuna kinachoshindikana...ndiyo maana hadi kuna breakfast in bed," Alfred akatania.

"Ahahah... kwa hiyo ungependa tuianze vipi hiyo date?" Beatrice akauliza huku anamsogelea Alfred mdomoni.

"Mhm...namna hii..."

Alfred akasema hivyo kisha kumwasha kofi la nguvu usoni! Beatrice alianguka chini na kuanza kulia, akishika uso wake kusitiri maumivu aliyohisi.

"Alfred! Kwa nini unanipiga?"

"Oh pole...nilifikiri ungefurahia zaidi tukiianza date yetu namna hiyo...hujapenda?" Alfred akamuuliza kikejeli huku anachuchumaa na kumshika shavu.

"Usiniguse! Umepatwa na kichaa!" Beatrice akasema kwa hasira.

Alfred akamtandika kofi lingine usoni na kufanya Beatrice aendelee kulia.

"Wewe ndiye mwenye kichaa, malaya mkubwa wewe!" Alfred akafoka.

"Alfred...nimekukosea nini? Kwa nini unanionea?"

"Nakuonea? Nakuonea eeh?"

Alfred akachukua simu yake na kuweka video fulani, kisha akamwonyeshea Beatrice. Macho ya Beatrice yalimtoka kwa mshangao baada ya kujiona kwenye video akiwa kwenye chumba kile cha hoteli pamoja na Gilbert. Alishindwa kuelewa Alfred alipata vipi video hiyo ambayo hakujua hata ilichukuliwa vipi. Maongezi yake pamoja na Gilbert yalisikika, naye Alfred akaipeleka mbele kufikia sehemu waliyokuwa wanafanya mapenzi kitandani. Beatrice alichoka! Akabaki kulia tu huku woga mwingi ukimwingia.

"Nini hiki Beatrice?"

Beatrice akaendelea kulia tu.

"...unadiriki kutoka nje ya ndoa yetu bila sababu yoyote! Unakosa nini kwangu Beatrice? Kuna kitu ambacho unahisi sijakutoshelezea? Eeh? Nijibu mpumbavu wewe!" Alfred akasema kwa hasira.

"Alfred...mume wangu..."

"Usiniite mume wako! Beatrice nimejitoa kadiri gani kwako ili kuifanya familia yetu iwe yenye furaha? Pesa zipo, watoto wapo, mapenzi nakupa jinsi utakavyo...leo hii unamvulia nguo mwanaume mwingine? Nimekukosea nini?"

Beatrice akaishika miguu ya Alfred huku akilia kwa huzuni.

"Usiniguse...don't..don't touch me! Endelea kusema sasa kwamba ninakuonea...ongea!"

Beatrice akainamisha kichwa chake chini huku akilia.

"...eti Alfred anani-cheat...nimeku-cheat lini mimi Beatrice? Na nani? Sema nimeku-cheat na nani...unanisingizia jambo lisilo la kweli ili kuhalalisha ufedhuli wako sivyo? Halafu huyu mpumbavu kumbe anajifanya ni rafiki yangu lakini na yeye ni mshenzi tu kama wewe! Mnafanya usali...aisee!"

"Alfred... Alfred... mimi...sija...nahitaji unielewe..."

"Nikuelewe vipi? Oh..principal wa chuo kikuu nieleweshe somo hili tafadhali..."

"...Alfred nakupenda...please...ni...ni..."

"Ni nini? Unataka kusema ni shetani ndiyo amekupitia tu? Why didn't he https://jamii.app/JFUserGuide you himself then?! Ilikuwa vipi ukafika kwa Gilbert?"

Beatrice akaendelea kulia kwa kuhisi hatia kuu moyoni.

Kwa upande wa Gilbert, ilikuwa ni kweli kwamba Jaquelin alifanya usaliti uliomchanganya akili mpaka akajikuta anaingia kwenye penzi na Beatrice, ambaye alimwambia pia kwamba Alfred alitoka nje ya ndoa. Lakini kwa upande wa Beatrice ilikuwa ni uwongo, Alfred hakuwa akitoka nje ya ndoa, bali ni kwa sababu ya tamaa yake ya kibinafsi ya kutaka kuwa na Gilbert tena ndiyo iliyomfanya amdanganye vile.

Kwa muda fulani, Alfred alianza kuingiwa na mashaka kuhusu nyendo za mke wake, hivyo aliamua kuajiri mtu wa kumfatilia kwa ukaribu ili ajue kama kulikuwa na kitu anaficha. Sasa akawa ametambua kwamba mke wake na rafiki yake walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, kitu ambacho kilimuumiza sana.

"Sasa nisikilize..." Alfred akasema huku akiwa ameshasimama.

Beatrice akamwangalia huku analia.

"...kuanzia sasa...sitaki tena kuwa na wewe!"

"No...Alfred..."

"...umesema kwamba unachotaka ni kunitaliki ili uwe na huyo mtu wako si ndiyo? Usijali...utaipata..."

"Alfred tafadhali...usifanye hivi...tuongee please my..."

"Don't touch me..don't touch me! Haujui ni kiasi gani umeniumiza we mwanamke! Nimekupa kila kitu... Usijali mama, kama ni talaka unayotaka, basi utaipata. Lakini kwanza kabisa ni lazima niwaonyeshe wazazi wako huu upuuzi..."

"Nooo...Alfred please... usi..."

"...na KILA MTU nitahakikisha anaiona video hii ili wajue jinsi gani unavyotia kinyaa!"

"...Alfred mume wangu..."

"Nimesema usiniguse! Mshenzi mkubwa wewe!" Alfred akafoka na kumpiga teke la begani.

Beatrice akaanguka chini huku analia sana.

"....ninaondoka sasa hivi kwenda kuhalalisha unachokitaka...nikirudi...nisikukute wewe au chochote kinachokuhusu ndani ya hii nyumba...la sivyo nitakuua!"

Alfred alikuwa amekasirika sana. Beatrice alimsihi sana asifanye hivyo, lakini mwanaume hakujali. Akaifata droo na kutoa vitu fulani, kisha akaanza kuuelekea mlango. Beatrice akanyanyuka na kumfata kisha kumkumbatia kwa nyuma huku akilia, lakini Alfred akamtoa mwilini kwake kwa nguvu na kumsukuma, naye Beatrice akadondokea chini huku analia. Alfred akatoka akiwa na hasira kali na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake, kisha akaondoka upesi.

Beatrice akabaki kutaharuki asijue la kufanya. Aliwaza mengi; ikiwa Alfred angeionyesha video hiyo kwa wazazi, watoto, marafiki, na watu wengi waliomheshimu, mambo mengi sana yangeharibika. Akaona hapaswi kuendelea kukaa na kulia tu, bali afanye jambo fulani ili kuibadili akili ya mume wake. Lakini hakujua la kufanya. Alitangatanga sana chumbani hapo kama ana kichaa, akipiga mito ya kitanda na kuvuruga vitu vingi vya humo kwa hasira nyingi. Akaelekea kwenye makabati na droo akitafuta kitu ambacho hata hakikueleweka, na kwa kukosa chochote cha kumsaidia aliivuta droo ya mwisho ya kabati kwa hasira na kuirusha pembeni kwa nguvu; ikisababisha vitu vingi vilivyokuwemo kudondokea na kutapakaa chini.

Akapiga magoti akilia kwa uchungu sana, kisha macho yake yakaganda juu ya kitu kimoja kilichokuwa chini hapo baada ya droo hiyo kuangukia chini. Ilikuwa ni bastola ya Alfred. Alikuwa na bastola kwa ajili ya kujilinda, lakini hakuwa na kawaida ya kuitumia. Kufikia wakati huu, mara ya mwisho kuitumia ilikuwa ni miaka 9 iliyopita, alipomtishia mfanya fujo fulani. Ni Beatrice peke yake ndiye aliyejua kuhusu bastola hiyo kuwa ndani humo, lakini hakuwa ameifikiria hata kidogo.

Ila sasa, baada ya kuiona hapo, wazo lile, lile wazo la kishetani, likaingia akilini mwake. Alijua hangeweza kumshawishi Alfred hata kidogo aache kuchukua hatua aliyomwambia, lakini vipi kama angeweza kumnyamazisha kabisa?

Akaifata bastola hiyo na kuichukua, kisha akasimama polepole huku anaitazama kwa umakini. Alikuwa anapumua kwa kwikwi nyingi za kilio, lakini sasa akajituliza na kufuta machozi yake. Akili mbaya ya kutaka kufanya ubaya mbaya sana ilivaa kichwa chake kwa ghafla, naye akaenda kwenye kabati na kutoa sweta lake kubwa, lililokuwa na kofia ya kufunika kichwa kutokea mgongoni, kisha akalikunja vizuri na kuliweka ndani ya mfuko, pamoja na ile bastola. Akatoka chumbani hapo na kuelekea nje kwenye gari lake.

Beatrice alikuwa mwanamke mwenye akili sana. Alichofanya, alimpigia simu Harleen na kumwambia kwamba hawezi kumpata baba yake kwa simu, hivyo yeye (Harleen) ajaribu kumpigia ili aone kama anaweza kumpata, kwa kusema huenda namba yake (Beatrice) kwenye simu ya Alfred ilijifunga. Bila Harleen kujua, Beatrice alikuwa ameunganisha simu yake na ya Harleen ili akimpigia baba yake simu, pale tu atakapopokea, Beatrice aweze kuangalia sehemu aliyopo Alfred (location) kwa kutumia app ya ufatiliaji kwenye simu yake. Alijua wazi ikiwa yeye ndiyo angempigia Alfred, asingepokea na hata kum-block. Hivyo, baada ya Harleen kumpigia baba yake, Beatrice akaweza kujua kule alikokuwa. Alianza kuendesha gari kuelekea huko huku bado akiwasikiliza walivyokuwa wanaongea.

Harleen alimwambia baba yake kwamba mama yake alikuwa akimtafuta lakini anashindwa kumpata, hivyo amtafute na pia aangalie simu yake huenda alimfungia kimakosa. Kwa busara, Alfred alimwambia angefanya hivyo, bila kusema chochote kilichotokea. Beatrice aliwasikiliza walipoagana kwa kuambiana mambo yenye kugusa hisia, naye akawa analia tu kwa kufikiria jinsi gani jambo alilotaka kufanya lingewaumiza sana watoto wake. Lakini alikuwa ameshaiwekea akili yake fikira ya kwamba hakukuwa na njia nyingine; hii ndiyo iliyoonekana kuwa suluhisho pekee.

Maeneo ambayo Alfred alikwenda yalikuwa yenye wapita njia wachache sana. Mwanaume huyo alikuwa kwenye bar kubwa akinywa pombe, kutokana na kuwa na mawazo mengi. Alijawa na huzuni nyingi pia, hivyo alikuwa amejipeleka hapo ili atafakari vitu huku anashushia pombe taratibu. Pombe ilikuwa imeshaanza kukigonga kichwa chake, naye aliona haingekuwa busara kuendelea kunywa kwa kuwa angehitaji kuendesha, hivyo akatumia muda mwingi kukaa tu hapo bila kuendelea kunywa.

Beatrice alikuwa ameegesha gari lake umbali mfupi kutoka kwenye bar hiyo, akiwa ameliona gari la mume wake hapo nje. Alijua bila shaka Alfred angekuwa mule ndani, hivyo akakaa kusubiri akiwa mwenye wasiwasi mwingi sana. Kufikia sasa, alikuwa amevaa sweta lake lile na kuishika bastola mikononi mwake, huku akipumua kwa msisimko mkubwa wa kile ambacho angefanya.

Ilifika mida ya saa 2 usiku, naye Alfred akaona atoke tu hapo na kuelekea nyumbani; na alikuwa ameshaiwekea akili yake jambo moja kuwa, kama angekuta Beatrice bado yuko huko, basi angemfungashia virago na kumfukuza yeye mwenyewe. Watoto wake wangemwelewa tu; aliwaza hivyo. Ile amefika nje na kuanza kulielekea gari lake, alisimama baada ya kuona gari ambalo alijua ni la mke wake. Alishangaa kiasi na kujiuliza Beatrice alijuaje alikokuwa, lakini alijua tu kwamba alimfata hapo bila shaka ili kumwomba samahani hata zaidi.

Beatrice akajikaza baada ya kumwona Alfred, kisha akavalia kofia ya sweta lake kichwani, ambayo iliufunika uso wake kiasi, na bastola akaificha nyuma ya kiuno chake, kisha akatoka na kuanza kumfata. Alfred alimwangalia kwa hisia kali sana, akikumbukia mambo yote aliyoyaona kwenye video ile. Wakati huu, Beatrice alikuwa amejipa ujasiri wa hali ya juu sana kiasi kwamba yeye mwenyewe alijiuliza aliutolea wapi. Kihalisi alikuwa na woga uliopitiliza wa kupoteza kila kitu ikiwa Alfred angefanya alichosema, kwa hivyo hiyo ikawa sababu ya kutosha kwake kuamua auondoe uhai wake.

"Unafanya nini hapa?" Alfred akamuuliza baada ya Beatrice kusimama umbali mfupi.

Mwanamke akawa anamwangalia tu huku anapumua haraka-haraka. Alfred akatikisa kichwa chake kwa kusikitika, kisha akashika mkono wa kufungulia mlango wa gari lake.

"Nadhani nilijieleza vizuri. Sitaki kukuona tena...natumaini sitakuta uchafu wako wowote kwenye nyumba yangu," Alfred akasema.

Kisha akauvuta mlango wa gari nao ukafunguka, na hapo Beatrice akamwita kwa jina lake. Alfred alipomtazama, akakuta ameshikilia bastola kwa mikono miwili huku amemwelekezea. Alishtuka na kuingiwa na hofu kubwa kwa kuwa hakutegemea hilo.

"Beatrice... unafanya nini?" Alfred akauliza.

"Hata mimi sitaki kukuona tena!" Beatrice akasema kwa sauti tetemeshi.

Na hapo hapo akafyatua risasi iliyompata Alfred katikati ya kifua chake!



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


2012

"Kwa nini unakuwa hivi lakini Gilbert? Hakuna chochote kinachopotea zaidi ya sisi kuwa na furaha..."

"No..hapana. Yaani...kiukweli ninachohisi tu ni hisia za hatia...siwezi kuendelea kufanya hivi..."

"Kwa nini?"

"Kwa sababu sisi sote tuna familia, Beatrice. Una mume nami nina..."

"Acha kujifanya kama vile mambo yako sawa kwenye ndoa zetu. Unajua vizuri kwamba Jaquelin anaku-cheat...na mimi vile vile Alfred anani-cheat..."

"...ndiyo lakini huoni kwamba na sisi tunafanya hivyo hivyo pia? Ni sawa kwao kutoka na watu wengine...lakini mimi kiukweli sitaki kuendelea kuwa kama wao, ijapokuwa inaumiza..."

Maongezi haya yalikuwa ni baina ya Gilbert na Beatrice. Wawili hawa walikuwa wamekutana kwenye chumba cha hoteli moja ya kifahari ili kuzungumzia uhusiano wao huu uliokuwa unaendelea kwa muda fulani sasa. Gilbert alikuwa akimwambia Beatrice kuwa walitakiwa kuacha, lakini Beatrice hakutaka kukatisha uhusiano wao bila kujali sababu zilizomfanya Gilbert afikie uamuzi huu.

"Ahah...kwa hiyo nini, utarudi nyumbani na kumsubiri "mke" wako umpokee kwa furaha, ukijua wazi ametoka kuliwa huko nje?" Beatrice akasema kwa hisia kali.

"Jaquelin amepoteza mwelekeo wake kwa muda mrefu...lakini bado ni mama wa mtoto wangu...sidhani Dylan atafurahi kujua ninaishi maisha yaliyojaa upotovu wa..."

"Upotovu? Unamaanisha kwamba unaniona mimi kama uchafu?"

"Hapana...hapana Beatrice. Ninathamini jambo hili kati yetu... lakini wewe na mimi tuko kwenye commitment..."

"To hell with that! Gilbert ninakupenda sana...niko tayari kumtaliki Alfred ili tuwe sote kwa njia unayotaka."

"Beatrice..."

"...ni kitu cha kawaida sana mbona. Wala usiumize kichwa...wewe fanya hivyo hivyo pia kwa kuwa..."

"Beatrice tafadhali...hatupaswi kuchukua maamuzi kwa njia hiyo. Tuna watoto...sidhani kama watafurahi kujua tunatenda namna hii. Pia tuko ndani ya kifungo cha ahadi za ndoa tulizotoa..."

"Who cares?!"

"Beatrice..."

"Usiniambie masuala ya ahadi za ndoa. Gilbert, tumerudiana ndani ya muda mfupi tu baada ya miaka yote hiyo, tumeonyeshana jinsi gani ilivyokuwa makosa sisi kufunga ndoa na watu wengine, na unajua tumependana tokea vidato. Kwa muda mrefu sana nilikuwa nataka itokee njia ili turudiane, na sasa nimekupata tena...siwezi kukuachia kirahisi-rahisi...hapana..."

"Beatrice..."

"Mm-mm..."

"...nisikilize. Sifanyi hivi kwa sababu labda najiona kuwa mtakatifu..."

"Ila kumbe? Tumefurahia mapenzi pamoja halafu sasa unataka tu kusema eti ahadi ya ndoa ndiyo inakuzuia?"

"...ni kwa sababu jambo hili ni kubwa zaidi yako na mimi. Mambo mengi yanahusika Beatrice...tayari tuna familia...hata kama tukiachana na wenzetu kisheria, bado itashangaza wengi ikiwa tutaungana na kuwafanya hata watoto wetu wafikiri kwamba sisi ndiyo tumewatendea ubaya wazazi wenzetu..."

"Basi kama ni hivyo, tutafute njia ya kuwafichua wenzetu usaliti wao, tuutumie kama ushahidi..."

"Beatrice no...haita..."

Beatrice akaushika uso wa Gilbert na kumwangalia usoni kwa hisia.

"Nimeshasema sitaki kukupoteza tena Gilbert...tutapata tu njia mpenzi wangu...nakuomba tafadhali...I love you so much..." Beatrice akasema.

Gilbert akawa anamwangalia tu kwa hisia, naye Beatrice akamsogelea mdomoni na kumpiga busu laini.

Mambo yalikuwa hivi: Gilbert alikutana na Beatrice kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake wakati anasoma kidato cha pili. Beatrice alikuwa amehamishiwa shuleni alikosomea Gilbert, na mwanzoni walizoeana kama marafiki tu wa kawaida mpaka walipofika kidato cha tatu, ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi. Walipendana sana kwa kuwa waliendelea kuwa pamoja mpaka walipomaliza kidato cha nne na kutengana, siyo kuachana, ila kurudi kwa familia zao ambazo ziliishi mikoa tofauti.

Waliendelea kuwasiliana, na mara kwa mara hata Gilbert alifanya mipango kwa jitihada nyingi ili wakutane na kuonyeshana upendo. Baadae, walishindwa kabisa kupatana tena baada ya Beatrice kupoteza njia ya kuwasiliana na Gilbert, hivyo mpaka wakati wanaingia chuo, hawakuwa wamewasiliana tena kwa zaidi ya miaka mitano. Kwa hiyo wote walijikuta wakiingia kwenye mahusiano mapya yaliyopelekea mpaka kufunga ndoa.

Kilichokuja kuwakutanisha ilikuwa ni siku ya sendoff ya Jaquelin, wakati Gilbert alipomwona Beatrice kwenye ukumbi wa sherehe yao hiyo. Baadae Jaquelin alipomfichua bwana harusi, Beatrice pia alishangaa kumwona Gilbert kuwa ndiye bwana harusi. Hadi unafika ule muda wa kuwasalimu maharusi pale mbele, Beatrice alimkumbatia Gilbert kwa hisia sana, bila yeyote kujua historia ya wawili hawa. Baadae, ilibidi Gilbert amuulize Jaquelin ikiwa alifahamiana na Beatrice, naye akamwambia ndiyo ni rafiki yake sana ambaye alimwacha akiendelea na chuo walichosomea pamoja.

Gilbert aliweza kupata namba mpya za Beatrice kwa ajili ya mawasiliano, na baada ya kuwasiliana naye akawa ametambua kwamba Beatrice pia aliolewa. Mume wa Beatrice, Alfred, alikuwa mwenye miradi mikubwa ya uuzaji wa madawa muhimu kutoka nje na kusambazia 'pharmacy' nyingi nchini. Kwa hiyo ujuani wao ukasaidia kujenga urafiki wa karibu kati ya wanne hawa; Alfred, Beatrice, Gilbert, na Jaquelin, nao wakawa karibu na kusaidiana kwa mambo mengi bila ya wenzi wa Gilbert na Beatrice kujua historia ya kimapenzi ya wawili hawa (ijapokuwa baadae waliweka wazi kuwa walisoma sekondari pamoja).

Kufikia wakati huu sasa ambao Gilbert alikuwa kwenye chumba cha hoteli na Beatrice, ndoa yake pamoja na Jaquelin ilikuwa na matatizo mengi sana. Gilbert alipata kujua kwamba Jaquelin alikuwa akitoka kimapenzi na mtu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake wa zamani, na ilikuwa ni kama hakujali kwa sababu ijapokuwa waliishi kama mume na mke, uhusiano wao wa ndoa haukuwa mzuri kipindi hiki. Gilbert aliamua kumwacha Jaquelin afanye analotaka, naye akaazimia kusonga tu mbele na mambo yake mengine.

Ndipo siku moja Gilbert akiwa anaongea na Beatrice, alimwambia kuwa rafiki yake (yaani Jaquelin) alikuwa anatoka nje ya ndoa, na hapa Beatrice pia akamwambia kuwa mume wake alifanya hivyo hivyo. Kwa hiyo, wawili hawa wakaanza kujenga ukaribu zaidi kwa kuwasiliana mara nyingi mpaka mwisho wa siku wakajikuta wanazama upya kwenye penzi lao lililoishia njiani miaka mingi iliyopita.

Lakini dhamiri ya Gilbert ilimsumbua sana ijapokuwa Jaquelin alikuwa amemkosea, kwa sababu bado aliheshimu cheo chake kama mama wa mwanae, Dylan. Hakutaka siku moja Dylan arudi akute ndoa yao imevurugika namna hiyo, lakini pia hakujua angeweza kushughulika vipi na mama yake. Beatrice akawa ndiyo kama njia ya kumfanya aondoe mikazo yake, kwa sababu bado ndani ya moyo wake alikuwa na hisia za upendo kumwelekea, lakini alijua kuendeleza uhusiano huu usio halali kungeleta shida zaidi, hivyo ni lazima angetafuta njia ili kuweka mambo kwenye mpangilio mzuri.

Beatrice akaendelea kumpiga denda Gilbert kimahaba huku anampapasa-papasa mwilini taratibu chumbani hapo, na sasa wote wakawa wamepandwa na hisi za mahaba kuelekeana. Ijapokuwa Gilbert aliona haikufaa, bado moyo wake ulitaka sana kuwa na Beatrice, hivyo akaruhusu penzi hili Beatrice alilotaka kumpatia hapo liendelee.

Wawili hawa hawakutambua kuwa walikuwa wakifatiliwa na mtu fulani kwa muda sasa. Kihalisi aliyekuwa akifatiliwa ni Beatrice, na sasa mtu huyo aliyekuwa anawafatilia alipata kuwaona wakiwa pamoja na mara kwa mara wakiingia hotelini hapo, hivyo alikuwa amekitafuta mapema chumba hiki walichopenda kukitumia na kutegesha camera ndogo sana (micro camera) ambayo ilirekodi kila jambo walilofanya wakati huu. Gilbert na Beatrice walikaa kama nusu saa baada ya kupeana mapenzi motomoto, kisha wakaisafisha miili yao na kuondoka. Sikuzote alianza kutoka kwanza Gilbert na kumwacha Beatrice akae kama dakika 15 hapo, kisha na Beatrice angeondoka baadae; wakifanya hivi kujilinda. Lakini sasa mambo yalikuwa yameharibika.

Kufikia kipindi hiki, Beatrice alikuwa mkuu (principal) wa chuo kikuu cha biashara. Alfred, mume wa Beatrice, alikuwa ameikuza miradi yake miaka mingi ya karibuni na kufanya familia yote kwa ujumla iwe yenye pesa nyingi sana. Binti yao, Harleen, alikuwa ameanza kusomea udaktari kwenye chuo kikuu nje ya nchi; akiwa na miaka 19 tu, na mwana wao David mwenye miaka 7 alikuwa masomoni kwenye shule nzuri ya international, ambako aliishi huko huko pia (boarding).

Baada ya Beatrice kurudi nyumbani akitokea chuoni, alikopita baada ya kuondoka kwenye hoteli ile, alimkuta Alfred akiwa chumbani. Alikuwa amekaa kitandani akionekana kuwaza jambo fulani. Beatrice akamsalimu, naye Alfred akamwangalia na kutabasamu, kisha akasimama na kuitikia salamu yake.

"Za chuo?" Alfred akauliza.

"Safi tu. Ndiyo nimetoka huko, panaboa kweli," Beatrice akadanganya.

"Pole. Ndiyo kazi," Alfred akamwambia.

"Mbona mapema leo?" Beatrice akauliza.

"Hakukuwa na mambo mengi leo. Pia...nilikuwa nataka kukuona," Alfred akajibu.

"Kama ni hivyo si ungenipigia simu halafu ukanitoa out?" Beatrice akasema kwa maringo huku anamsogelea.

"Kwa nini twende out wakati nyumbani ni pazuri zaidi? Tuifanyie hapa hapa tu," Alfred akajibu.

"Ahah...hiyo itakuwa date ya aina gani sasa?" Beatrice akauliza kimadoido.

"Hakuna kinachoshindikana...ndiyo maana hadi kuna breakfast in bed," Alfred akatania.

"Ahahah... kwa hiyo ungependa tuianze vipi hiyo date?" Beatrice akauliza huku anamsogelea Alfred mdomoni.

"Mhm...namna hii..."

Alfred akasema hivyo kisha kumwasha kofi la nguvu usoni! Beatrice alianguka chini na kuanza kulia, akishika uso wake kusitiri maumivu aliyohisi.

"Alfred! Kwa nini unanipiga?"

"Oh pole...nilifikiri ungefurahia zaidi tukiianza date yetu namna hiyo...hujapenda?" Alfred akamuuliza kikejeli huku anachuchumaa na kumshika shavu.

"Usiniguse! Umepatwa na kichaa!" Beatrice akasema kwa hasira.

Alfred akamtandika kofi lingine usoni na kufanya Beatrice aendelee kulia.

"Wewe ndiye mwenye kichaa, malaya mkubwa wewe!" Alfred akafoka.

"Alfred...nimekukosea nini? Kwa nini unanionea?"

"Nakuonea? Nakuonea eeh?"

Alfred akachukua simu yake na kuweka video fulani, kisha akamwonyeshea Beatrice. Macho ya Beatrice yalimtoka kwa mshangao baada ya kujiona kwenye video akiwa kwenye chumba kile cha hoteli pamoja na Gilbert. Alishindwa kuelewa Alfred alipata vipi video hiyo ambayo hakujua hata ilichukuliwa vipi. Maongezi yake pamoja na Gilbert yalisikika, naye Alfred akaipeleka mbele kufikia sehemu waliyokuwa wanafanya mapenzi kitandani. Beatrice alichoka! Akabaki kulia tu huku woga mwingi ukimwingia.

"Nini hiki Beatrice?"

Beatrice akaendelea kulia tu.

"...unadiriki kutoka nje ya ndoa yetu bila sababu yoyote! Unakosa nini kwangu Beatrice? Kuna kitu ambacho unahisi sijakutoshelezea? Eeh? Nijibu mpumbavu wewe!" Alfred akasema kwa hasira.

"Alfred...mume wangu..."

"Usiniite mume wako! Beatrice nimejitoa kadiri gani kwako ili kuifanya familia yetu iwe yenye furaha? Pesa zipo, watoto wapo, mapenzi nakupa jinsi utakavyo...leo hii unamvulia nguo mwanaume mwingine? Nimekukosea nini?"

Beatrice akaishika miguu ya Alfred huku akilia kwa huzuni.

"Usiniguse...don't..don't touch me! Endelea kusema sasa kwamba ninakuonea...ongea!"

Beatrice akainamisha kichwa chake chini huku akilia.

"...eti Alfred anani-cheat...nimeku-cheat lini mimi Beatrice? Na nani? Sema nimeku-cheat na nani...unanisingizia jambo lisilo la kweli ili kuhalalisha ufedhuli wako sivyo? Halafu huyu mpumbavu kumbe anajifanya ni rafiki yangu lakini na yeye ni mshenzi tu kama wewe! Mnafanya usali...aisee!"

"Alfred... Alfred... mimi...sija...nahitaji unielewe..."

"Nikuelewe vipi? Oh..principal wa chuo kikuu nieleweshe somo hili tafadhali..."

"...Alfred nakupenda...please...ni...ni..."

"Ni nini? Unataka kusema ni shetani ndiyo amekupitia tu? Why didn't he JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala you himself then?! Ilikuwa vipi ukafika kwa Gilbert?"

Beatrice akaendelea kulia kwa kuhisi hatia kuu moyoni.

Kwa upande wa Gilbert, ilikuwa ni kweli kwamba Jaquelin alifanya usaliti uliomchanganya akili mpaka akajikuta anaingia kwenye penzi na Beatrice, ambaye alimwambia pia kwamba Alfred alitoka nje ya ndoa. Lakini kwa upande wa Beatrice ilikuwa ni uwongo, Alfred hakuwa akitoka nje ya ndoa, bali ni kwa sababu ya tamaa yake ya kibinafsi ya kutaka kuwa na Gilbert tena ndiyo iliyomfanya amdanganye vile.

Kwa muda fulani, Alfred alianza kuingiwa na mashaka kuhusu nyendo za mke wake, hivyo aliamua kuajiri mtu wa kumfatilia kwa ukaribu ili ajue kama kulikuwa na kitu anaficha. Sasa akawa ametambua kwamba mke wake na rafiki yake walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, kitu ambacho kilimuumiza sana.

"Sasa nisikilize..." Alfred akasema huku akiwa ameshasimama.

Beatrice akamwangalia huku analia.

"...kuanzia sasa...sitaki tena kuwa na wewe!"

"No...Alfred..."

"...umesema kwamba unachotaka ni kunitaliki ili uwe na huyo mtu wako si ndiyo? Usijali...utaipata..."

"Alfred tafadhali...usifanye hivi...tuongee please my..."

"Don't touch me..don't touch me! Haujui ni kiasi gani umeniumiza we mwanamke! Nimekupa kila kitu... Usijali mama, kama ni talaka unayotaka, basi utaipata. Lakini kwanza kabisa ni lazima niwaonyeshe wazazi wako huu upuuzi..."

"Nooo...Alfred please... usi..."

"...na KILA MTU nitahakikisha anaiona video hii ili wajue jinsi gani unavyotia kinyaa!"

"...Alfred mume wangu..."

"Nimesema usiniguse! Mshenzi mkubwa wewe!" Alfred akafoka na kumpiga teke la begani.

Beatrice akaanguka chini huku analia sana.

"....ninaondoka sasa hivi kwenda kuhalalisha unachokitaka...nikirudi...nisikukute wewe au chochote kinachokuhusu ndani ya hii nyumba...la sivyo nitakuua!"

Alfred alikuwa amekasirika sana. Beatrice alimsihi sana asifanye hivyo, lakini mwanaume hakujali. Akaifata droo na kutoa vitu fulani, kisha akaanza kuuelekea mlango. Beatrice akanyanyuka na kumfata kisha kumkumbatia kwa nyuma huku akilia, lakini Alfred akamtoa mwilini kwake kwa nguvu na kumsukuma, naye Beatrice akadondokea chini huku analia. Alfred akatoka akiwa na hasira kali na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake, kisha akaondoka upesi.

Beatrice akabaki kutaharuki asijue la kufanya. Aliwaza mengi; ikiwa Alfred angeionyesha video hiyo kwa wazazi, watoto, marafiki, na watu wengi waliomheshimu, mambo mengi sana yangeharibika. Akaona hapaswi kuendelea kukaa na kulia tu, bali afanye jambo fulani ili kuibadili akili ya mume wake. Lakini hakujua la kufanya. Alitangatanga sana chumbani hapo kama ana kichaa, akipiga mito ya kitanda na kuvuruga vitu vingi vya humo kwa hasira nyingi. Akaelekea kwenye makabati na droo akitafuta kitu ambacho hata hakikueleweka, na kwa kukosa chochote cha kumsaidia aliivuta droo ya mwisho ya kabati kwa hasira na kuirusha pembeni kwa nguvu; ikisababisha vitu vingi vilivyokuwemo kudondokea na kutapakaa chini.

Akapiga magoti akilia kwa uchungu sana, kisha macho yake yakaganda juu ya kitu kimoja kilichokuwa chini hapo baada ya droo hiyo kuangukia chini. Ilikuwa ni bastola ya Alfred. Alikuwa na bastola kwa ajili ya kujilinda, lakini hakuwa na kawaida ya kuitumia. Kufikia wakati huu, mara ya mwisho kuitumia ilikuwa ni miaka 9 iliyopita, alipomtishia mfanya fujo fulani. Ni Beatrice peke yake ndiye aliyejua kuhusu bastola hiyo kuwa ndani humo, lakini hakuwa ameifikiria hata kidogo.

Ila sasa, baada ya kuiona hapo, wazo lile, lile wazo la kishetani, likaingia akilini mwake. Alijua hangeweza kumshawishi Alfred hata kidogo aache kuchukua hatua aliyomwambia, lakini vipi kama angeweza kumnyamazisha kabisa?

Akaifata bastola hiyo na kuichukua, kisha akasimama polepole huku anaitazama kwa umakini. Alikuwa anapumua kwa kwikwi nyingi za kilio, lakini sasa akajituliza na kufuta machozi yake. Akili mbaya ya kutaka kufanya ubaya mbaya sana ilivaa kichwa chake kwa ghafla, naye akaenda kwenye kabati na kutoa sweta lake kubwa, lililokuwa na kofia ya kufunika kichwa kutokea mgongoni, kisha akalikunja vizuri na kuliweka ndani ya mfuko, pamoja na ile bastola. Akatoka chumbani hapo na kuelekea nje kwenye gari lake.

Beatrice alikuwa mwanamke mwenye akili sana. Alichofanya, alimpigia simu Harleen na kumwambia kwamba hawezi kumpata baba yake kwa simu, hivyo yeye (Harleen) ajaribu kumpigia ili aone kama anaweza kumpata, kwa kusema huenda namba yake (Beatrice) kwenye simu ya Alfred ilijifunga. Bila Harleen kujua, Beatrice alikuwa ameunganisha simu yake na ya Harleen ili akimpigia baba yake simu, pale tu atakapopokea, Beatrice aweze kuangalia sehemu aliyopo Alfred (location) kwa kutumia app ya ufatiliaji kwenye simu yake. Alijua wazi ikiwa yeye ndiyo angempigia Alfred, asingepokea na hata kum-block. Hivyo, baada ya Harleen kumpigia baba yake, Beatrice akaweza kujua kule alikokuwa. Alianza kuendesha gari kuelekea huko huku bado akiwasikiliza walivyokuwa wanaongea.

Harleen alimwambia baba yake kwamba mama yake alikuwa akimtafuta lakini anashindwa kumpata, hivyo amtafute na pia aangalie simu yake huenda alimfungia kimakosa. Kwa busara, Alfred alimwambia angefanya hivyo, bila kusema chochote kilichotokea. Beatrice aliwasikiliza walipoagana kwa kuambiana mambo yenye kugusa hisia, naye akawa analia tu kwa kufikiria jinsi gani jambo alilotaka kufanya lingewaumiza sana watoto wake. Lakini alikuwa ameshaiwekea akili yake fikira ya kwamba hakukuwa na njia nyingine; hii ndiyo iliyoonekana kuwa suluhisho pekee.

Maeneo ambayo Alfred alikwenda yalikuwa yenye wapita njia wachache sana. Mwanaume huyo alikuwa kwenye bar kubwa akinywa pombe, kutokana na kuwa na mawazo mengi. Alijawa na huzuni nyingi pia, hivyo alikuwa amejipeleka hapo ili atafakari vitu huku anashushia pombe taratibu. Pombe ilikuwa imeshaanza kukigonga kichwa chake, naye aliona haingekuwa busara kuendelea kunywa kwa kuwa angehitaji kuendesha, hivyo akatumia muda mwingi kukaa tu hapo bila kuendelea kunywa.

Beatrice alikuwa ameegesha gari lake umbali mfupi kutoka kwenye bar hiyo, akiwa ameliona gari la mume wake hapo nje. Alijua bila shaka Alfred angekuwa mule ndani, hivyo akakaa kusubiri akiwa mwenye wasiwasi mwingi sana. Kufikia sasa, alikuwa amevaa sweta lake lile na kuishika bastola mikononi mwake, huku akipumua kwa msisimko mkubwa wa kile ambacho angefanya.

Ilifika mida ya saa 2 usiku, naye Alfred akaona atoke tu hapo na kuelekea nyumbani; na alikuwa ameshaiwekea akili yake jambo moja kuwa, kama angekuta Beatrice bado yuko huko, basi angemfungashia virago na kumfukuza yeye mwenyewe. Watoto wake wangemwelewa tu; aliwaza hivyo. Ile amefika nje na kuanza kulielekea gari lake, alisimama baada ya kuona gari ambalo alijua ni la mke wake. Alishangaa kiasi na kujiuliza Beatrice alijuaje alikokuwa, lakini alijua tu kwamba alimfata hapo bila shaka ili kumwomba samahani hata zaidi.

Beatrice akajikaza baada ya kumwona Alfred, kisha akavalia kofia ya sweta lake kichwani, ambayo iliufunika uso wake kiasi, na bastola akaificha nyuma ya kiuno chake, kisha akatoka na kuanza kumfata. Alfred alimwangalia kwa hisia kali sana, akikumbukia mambo yote aliyoyaona kwenye video ile. Wakati huu, Beatrice alikuwa amejipa ujasiri wa hali ya juu sana kiasi kwamba yeye mwenyewe alijiuliza aliutolea wapi. Kihalisi alikuwa na woga uliopitiliza wa kupoteza kila kitu ikiwa Alfred angefanya alichosema, kwa hivyo hiyo ikawa sababu ya kutosha kwake kuamua auondoe uhai wake.

"Unafanya nini hapa?" Alfred akamuuliza baada ya Beatrice kusimama umbali mfupi.

Mwanamke akawa anamwangalia tu huku anapumua haraka-haraka. Alfred akatikisa kichwa chake kwa kusikitika, kisha akashika mkono wa kufungulia mlango wa gari lake.

"Nadhani nilijieleza vizuri. Sitaki kukuona tena...natumaini sitakuta uchafu wako wowote kwenye nyumba yangu," Alfred akasema.

Kisha akauvuta mlango wa gari nao ukafunguka, na hapo Beatrice akamwita kwa jina lake. Alfred alipomtazama, akakuta ameshikilia bastola kwa mikono miwili huku amemwelekezea. Alishtuka na kuingiwa na hofu kubwa kwa kuwa hakutegemea hilo.

"Beatrice... unafanya nini?" Alfred akauliza.

"Hata mimi sitaki kukuona tena!" Beatrice akasema kwa sauti tetemeshi.

Na hapo hapo akafyatua risasi iliyompata Alfred katikati ya kifua chake!



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
Duuu, Beatrice ni Mnyambisi kabisa
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Mlio wa risasi ulishtua watu wengi eneo hilo, na baadhi ya wapita njia waliokuwa wakija upande huu wakarudi walikotoka kwa kutimua mbio!

Alfred aliachama mdomo wake kwa mkazo sana kutokana na maumivu aliyohisi mwilini mwake. Risasi ilipompata ilifanya ajibamize kwenye mlango wa gari na kuanza kushuka chini taratibu, kisha akawa amelala chali baada ya mwili wake kufika chini. Mikono ya Beatrice ilitetemeka, na mapigo yake ya moyo yalikimbia kwa kasi sana, lakini akajikaza ili kuhakikisha lengo lake alilokuwa nalo akilini linatimia. Akamfata haraka-haraka hapo chini na kuanza kuitafuta simu ya Alfred kwenye mifuko yake ya suruali. Alfred alivuja damu nyingi sana zilizomfanya Beatrice ashindwe kumwangalia.

"Why...."

Sauti ya mbali ya Alfred ikasikika akisema hivyo. Beatrice akawa ameipata simu ya mume wake na kuichukua, akiyapotezea maneno yake kwa kuwa alihitaji kuondoka eneo hilo haraka sana. Akakimbia kurudi kwenye gari, kisha akaondoka eneo hilo upesi sana. Alikuwa anaendesha huku analia mno, na sehemu fulani ya akili yake ilimlaumu mno kwa kitendo alichofanya. Lakini akajikaza na kuisafishia akili yake mawazo yote ya kujutia, kwa kuwa maji yalikuwa yameshamwagika, hangeweza kuyazoa.

Aliendesha gari mpaka sehemu ya msituni, kisha akashuka na kwenda kuvua sweta lake haraka sana. Akalichoma moto, ili kuhakikisha haliwi chanzo cha ushahidi endapo uchunguzi ungefanywa, kisha akaichukua simu ya Alfred na kutafuta uwezekano wa kuipata namba ya mpelelezi aliyeajiriwa na Alfred kumfatilia.

Beatrice alijua ni mpelelezi huyo pekee zaidi ya mume wake aliyejua kuhusu ishu yake na Gilbert, hivyo angehitaji kumpata ili arekebishe mambo. Baada ya kutosheka na namba aliyojua bila shaka ndiyo yenyewe, akamtumia ujumbe kwa simu hiyo hiyo ya Alfred kwamba wakutane sehemu fulani kisiri kwa sababu alikuwa na jambo muhimu la kumwambia. Mpelelezi huyo akajibu kwa ujumbe kukubali kwenda, akifikiri aliyetuma ujumbe ni Alfred. Akili ya Beatrice aliyeijua ni yeye mwenyewe tu!

Beatrice, kwa kutumia simu ya mumewe, alikuwa amemwelekeza mpelelezi afike sehemu fulani ambayo ilikuwa kama msitu huo; hakukuwa na watu eneo hilo, zaidi ni magari machache tu ndiyo yalipita kwenye barabara ya lami. Mpelelezi alipofika, alishuka kutoka kwenye gari na kwenda moja kwa moja mpaka sehemu ambayo alielekezwa. Kwa ujanja Beatrice alikuwa amemwambia wasipigiane simu kwa maana kulikuwa na jambo fulani linaendelea lililohitaji umakini. Lakini mpelelezi huyu alianza kuingiwa na mashaka baada ya kufika hapo na kumkuta Beatrice. Akatambua kwamba huu ulikuwa ni mtego, naye akataka kuondoka upesi lakini Beatrice akamnyooshea bastola na kumwambia atulie.

Mpelelezi akanyoosha mikono yake juu kumwonyesha Beatrice kwamba asimdhuru, huku Beatrice akipumua kwa kasi sana.

"Alikuwa anakulipa shi'ngapi?"

Beatrice akamuuliza, lakini jamaa akakaa kimya tu.

"Nijibu...alikulipa shilingi ngapi ili unifatilie?"

"Milioni tano," mpelelezi akajibu.

"Video tape...naitaka video tape yote...iko wapi..?"

Jamaa akakaa kimya. Beatrice akashusha bastola kuelekea miguu ya mpelelezi na kufyatua risasi iliyompiga gotini na kupasua mfupa wake. Alitoa sauti ya maumivu na kudondoka chini, kisha Beatrice akaanza kumsogelea karibu zaidi.

"Niambie...la sivyo..."

"Aagh... ssss...sijui...ssss...aaaagh..."

"Niambie ukweli mpuuzi wewe! Wewe ndiyo uliwashwa kuitega camera mule ndani...niambie iko wapi!"

"..aaah...aaagh...."

Beatrice akampiga risasi nyingine begani.

"Aaaaaagh!" mpalelezi akapiga yowe la maumivu.

"Sema!" Beatrice akafoka.

"...aaagh...aaagh...ssss...nilimpa..vyote...sijui kaweka wapi...aaagh.. ssss..."

"Hutaki kusema? Ngoja nikupasue goti lingine!"

"...hapana... ssss...aaagh..
me nilimpelekea..ssss...ofisini.kwake...sijui alipoviweka..."

Beatrice akawa anamwangalia kwa hasira sana. Aliona ni kama mwanaume huyo ndiye aliyesababisha mambo yote haya yatokee.

"...aaah...dada..sss...tafadhali..usi..."

Kabla hajamaliza kuongea hapo hapo Beatrice akamfumua risasi ya kichwa iliyofanya sehemu ya juu ipasuke na kurusha damu hewani. Mpelelezi akaanguka chini na kutulia tuli! Beatrice alipumua kwa hasira na hofu kwa wakati ule ule, yaani alikuwa ameua watu wawili ndani ya masaa machache! Akaanza kuangalia huku na huko kama kuna mtu, lakini hangeweza kuona vizuri pande za mbali kutokana na giza. Hivyo, akaondoka eneo hilo na kuanza kuelekea nyumbani.

Alifika nyumbani kwenye mida ya saa 5 usiku, naye akaelekea chumbani kwake moja kwa moja. Aliingia bafuni akiwa anatetemeka, kisha akajimwagia maji kwa zaidi ya nusu saa. Alipotoka humo, akaketi kitandani akipumua kwa presha sana, kisha akafumba macho na kuanza kulia upya. Hazikupita dakika nyingi, simu yake ikaita, na namba ilikuwa ngeni. Akapokea na kupewa taarifa ya kifo cha mume wake kutoka kwa polisi, hivyo ikabidi aondoke kwenda kule walikouhifadhi mwili; kana kwamba hakujua kuhusu hilo.

Baada ya muda, kifo cha Alfred kiliwafikia ndugu zake, watoto wake, marafiki, na wafanyakazi wengi aliokuwa amewaajiri. Msiba ulifanywa, watoto wote wa Alfred wakiwepo, na hata Jaquelin na Gilbert pia. Uchunguzi uliendelea kufanywa na mapolisi kuhusu muuaji, lakini Beatrice alihakikisha anatumia kila njia kuweza kuficha ukweli. Kwa kuwa sasa mume wake alikufa, sehemu kubwa ya mali zake ilikuwa chini yake na watoto wake. Yeye ndiye angepaswa kuongoza mambo ilipohusu mali na pesa za familia; kitu ambacho kwa muda akaanza kuona kilikuwa ni chenye faida sana.

Kwa hiyo maisha yaliendelea hivyo hivyo, watoto wake wakiendelea na masomo baada ya maombolezo, naye Beatrice akawa ndiyo malkia wa milki aliyoiacha Alfred. Mara kwa mara alijaribu kumshawishi Gilbert wawe pamoja, lakini kutokana na mambo yote yaliyotokea, hasa kifo cha Alfred, Gilbert hangeweza kukubaliana naye kwa jambo hilo kabisa kwa kuwa angefanya hisia zake za hatia ziwe za juu hata zaidi. Mara kwa mara Beatrice alitafuta njia za kumlazimisha wawe hata na uhusiano wa siri, lakini Gilbert alikataa kwa busara na hata kumshauri atafute mtu mwingine wa kuwa naye atakayewajibikia upendo kwake kwa asilimia zote.


β˜…β˜…β˜…


Miaka sita ilipita tokea kifo cha mume wake Beatrice, yaani Alfred, na sasa ilikuwa ni 2018, mwaka ambao tatizo fulani kubwa lilizuka baina ya Gilbert na Jaquelin. Jaquelin alikuwa anadai kwamba Gilbert ndiye aliyetoka nje ya ndoa, lakini Gilbert akamhakikishia kwamba alijua ni yeye Jaquelin ndiye aliyefanya usaliti na kijana aliyeitwa Thomas, ambaye alikuwa ni mwanamitindo mwenye sura nzuri na mwili wa mazoezi. Alimwambia Jaquelin alijua kuhusu hilo na kwamba alichoka kugeuziwa lawama za hatia ya maovu mke wake aliyoyafanya, na kwamba upendo wake kwake ulikuwa umezimika siku nyingi sana lakini aliamua tu kuendelea kuwa naye ili kuokoa picha yake nzuri ya hadharani (reputation).

Ugomvi huu ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba Gilbert akaondoka kwenye nyumba yao mpya na kwenda kukaa kwenye ile waliyoiacha kwa ajili ya Dylan. Sikuzote matatizo yalipotokea baina ya wanandoa hawa, Jaquelin alimweleza Beatrice, kama rafiki yake wa karibu, kwa kuwa mara nyingi angempa ushauri wa kinafiki kuhusiana na jinsi ya kutatua matatizo. Lakini wakati huu, baada ya Jaquelin kumweleza jinsi tatizo hilo lilivyokuwa kubwa, Beatrice akaona huenda hii ikawa nafasi nzuri ya kumzuzua Gilbert na kumwingiza kwenye anga zake tena. Akamwambia Jaquelin angeenda kumwona kwake ili amfariji, kisha ndiyo wangepanga jinsi ya kumlainisha Gilbert. Lakini Beatrice alichofanya ilikuwa ni kutafuta Gilbert alipokuwa, na baada ya kupajua, akaamua kumfata huko huko ili wayajenge.

Beatrice alifika kwenye nyumba ya Gilbert usiku, naye Gilbert alishangaa uwepo wa mwanamke huyu hapo. Beatrice akamwomba aingie ndani ili waweze kuongea kuhusiana na matatizo yake; kama rafiki tu. Gilbert alikuwa peke yake ndani ya nyumba hii, naye akamkaribisha Beatrice kwa kumwekea wine kwenye glasi na wote wakaketi na kuendelea na mazungumzo.

"...siyo rahisi lakini mwisho wa siku najua nitahitaji kutafuta amani...for Dylan's sake," Gilbert akawa akisema.

"For all these years that you chose to stay with her...ilikuwa kwa ajili ya Dylan tu?" Beatrice akauliza.

"Yeah," Gilbert akajibu kishingo upande.

"Ahah...Gilbert... Dylan siyo mtoto tena. Umejilazimisha kuwa na mtu mpumbavu asiyejua thamani yako, na ambaye moyo wako uko mbali naye muda wote huu, matokeo yake ni nini sasa?" Beatrice akauliza.

"Ahah...yaani utafikiri unayemwongelea hivyo siyo rafiki yako," Gilbert akamwambia.

"Yaani ni kama haujui ni kwa nini ninasema hivyo," Beatrice akasema.

Gilbert akaangalia upande mwingine.

Beatrice akanyanyuka kutoka kwenye sofa aliloketi na kwenda kukaa alipoketi Gilbert; kwa ukaribu sana. Kisha akaushika mkono wa Gilbert na kuanza kuusugua taratibu kwa njia ya kubembeleza. Gilbert akawa anamwangalia kwa hisia, naye Beatrice akaanza kuifata midomo yake taratibu akikusudia kumpiga busu. Lakini alipoikaribia zaidi, Gilbert akaangalia chini na kufanya busu hiyo isifanikiwe. Lakini Beatrice akakinyanyua kidevu cha Gilbert kwa wororo na kumpiga denda laini. Akaanza kuinyonya midomo yake kimahaba sana, huku akitembeza mkono wake mmoja mwilini mwa Gilbert. Akaanza kuvifungua vifungo vya shati la mwanaume, na ni hapa ndipo Gilbert akajitoa mdomoni mwake na kumshika mkono huo kwa kumzuia.

"Beatrice... we can't do this," akamwambia.

"Why not? Nakuhitaji...and I know you want me too..." Beatrice akasema kwa deko.

"Ni mambo mengi yanahusika...."

"Sikuzote huwa unasema hivyo Gilbert...acha kuzunguka sana. Niko hapa...kwa nini hunioni?"

"Siyo hivyo...Beatrice...maisha yetu yako ndani ya rubble kubwa sana...tuki..."

Beatrice akamkatisha kwa kuanza kumpiga denda kwa mara nyingine tena.

Wakati huu alifanya hadi kumlalia kifuani huku akiendelea kuinyonya midomo yake kwa njia ya kumpandishia hisia za kimahaba, lakini Gilbert akajitoa tena kwake na kusimama kutoka kwenye sofa. Beatrice alivunjika moyo sana, lakini hakutaka kukata tamaa. Akanyanyuka na kumfata aliposimama kisha kuanza kuitafuta denda nyingine. Lakini Gilbert akamdhibiti na kumshikilia mikononi.

"Beatrice..."

"Kwa nini lakini? Kwa nini?"

"...sidhani ikiwa itafaa...Beatrice tulichokuwa nacho kipindi kile ni cha kipindi kile...muda umepita sasa...mambo mengi yamebadilika..."

"Kwa nini...nimeharibikia? Unaona kama simfikii Jaquelin kwa uzuri now...nitafanya chochote kwa ajili yako Gil..."

"Beatrice please..please...please...jaribu kuelewa..."

"...achana naye! Kwa nini unalazimisha tu...ana nini ambacho mimi sina Gilbert? Niambie sababu moja inayokufanya usitake kabisa kuwa na mimi...niambie..." Beatrice akasema huku machozi yanamtoka.

Gilbert akawa anamwangalia kwa hisia za huruma.

"...niambie...amenizidi nini? Mimi naweza kukupa vitu bora zaidi ya vile ambavyo yeye anagawa nje...niambie Gil...kwa nini umemng'ang'ania tu?" Beatrice akauliza kwa hisia.

Gilbert akaangalia chini kidogo kisha akamtazama tena Beatrice machoni na kusema, "Nampenda."

Beatrice alianza kulia bila kutoa sauti, kwa kuhisi kama amechomwa na kitu kikali sana moyoni mwake.

"I'm sorry Beatrice... Jaquelin is a lot of things but....alikuwa nami kwa kipindi fulani ambacho...kila mtu alinigeuzia mgongo wake na kunitenga..lakini yeye alisimama na mimi na...tukapita kwenye changamoto nyingi pamoja. Mtoto wetu wa kwanza alikufa siku aliyozaliwa...maumivu aliyopata Jaquelin yalimsababishia PPD...ugonjwa ambao ulikuwa unafanya mood yake inabadilika-badilika. Beatrice... imenichukua muda na jitihada nyingi kumwonyesha upendo Jaquelin..na wakati mwingine nilihitaji tu kuelewa kwamba mambo mengi yenye kuudhi aliyofanya...hakudhamiria kwa asilimia zote...." Gilbert akaeleza.

Beatrice akajifuta machozi na kusema, "Kwa hiyo, hiyo inamaanisha hata kama akitoka na wanaume wengine ni sawa tu kwa sababu ana PPD?"

"Hapana. Unajua ilifika kipindi nikahisi kukata tamaa...mpaka nikaanza kutoka na wewe tena. Matibabu tumefanya ila...bado hali hiyo hutokea mara kwa mara. Lakini kila wakati ambapo angerudi kuwa stable...nilichokiona kwake ilikuwa ni yule Jaquelin wangu nayempenda...na bado ninampenda," Gilbert akasema kwa hisia sana.

Beatrice akawa anatikisa kichwa kwa kutoamini kama kweli Gilbert alimkataa. Akaufata mkoba wake kwa hasira na kuanza kuondoka haraka kutoka sehemu hiyo.

"Beatrice... Beatrice..."

Gilbert alimsindikiza kwa macho huku akimwita.

Mwanamke akatoka upesi na kuondoka eneo hilo huku akilia sana. Alihisi ni kama alionwa hafai, na hapa kumbukumbu za jinsi Gilbert alivyompa mapenzi matamu miaka ya nyuma zikawa zinajirudia akilini mwake. Hakutaka kukubali kumpoteza jumla mwanaume huyo; iwe isiwe, ni lazima angehakikisha anampata tena Gilbert. Hivyo akaunda mpango mpya wa kuweza kuondoa kikwazo kilichozuia penzi lake na Gilbert lisiwe hai tena, yaani Jaquelin.


β˜…β˜…β˜…


Ilipofika kesho jioni, Beatrice alikwenda nyumbani kwa Jaquelin kwa kigezo cha kumtembelea ili amfariji na kumpa mawazo ya kirafiki. Alimkuta akiwa na rundo la hisia za huzuni, upweke na majuto pia. Postpartum depression (PPD), ni ugonjwa ambao huathiri tabia za hisia (mood) kwa watu fulani, hasa wanawake pindi za kujifungua watoto. Unasababisha hisia zao zinakuwa katika hali ya kubadilika-badilika sana, na kwa Jaquelin hilo ndiyo lilikuwa tatizo ambalo mara nyingi lilifanya atende kwa njia ambazo angejutia baadae. Wakati huu ambao Beatrice alimtembelea, Jaquelin alikuwa katika hali ya kujuta kwa nini amesababisha mpaka Gilbert akamtenga, naye akamwomba rafiki yake huyo amsaidie la kufanya ili aweke mambo sawa.

Beatrice sasa, akiwa anajua vizuri jinsi ya kuikoroga akili ya Jaquelin, akamwambia Jaquelin afanye kitu ambacho kingemlazimu Gilbert arudi yeye mwenyewe na asije kumwacha tena. Alimwambia kwa uwongo kwamba ajifanye ametaka kujiua, na hapo Gilbert ataona thamani yake. Jaquelin aliogopa, lakini Beatrice akamtuliza kwa kusema ana njia rahisi ambayo haitamdhuru, na akamwambia njia hiyo ilikuwa ni dawa fulani ambayo akinywa anapoteza fahamu kwa muda mrefu, lakini haingemuua. Kwa hiyo angeinywa na kufanya Gilbert achanganyikiwe kwa kujua maisha ya mke wake yako hatarini, na baada ya kumrudisha kwenye hali ya kawaida, amwambie mume wake kwamba hawezi kuishi bila yeye hivyo akimwacha tu, anajiua.

Jaquelin alimwamini rafiki yake huyo, na kwa jinsi ambavyo alikuwa na uharaka wa kutaka suluhisho, akaona akubali msaada huo aliopatiwa na shoga yake. Beatrice akampatia chupa ndogo ya dawa na kumwambia iko humo, kwa hiyo yeye anywe tu na kutulia ili imfanye azimie, kisha bila shaka msaidizi wa kazi angempigia simu Gilbert ili aje kumwokoa. Lakini Jaquelin hangeweza kujua kwamba huo ulikuwa ni mpango mbaya dhidi yake, kwa sababu ndani ya chupa hiyo ndogo haikuwa dawa ya kumfanya azimie kwa muda mrefu, bali Beatrice alikuwa ameiwekea dawa ambayo ilikuwa sumu kali pia. Mwanamke huyo mwenye moyo mbaya wenye wivu akamwacha Jaquelin akitafakari kuhusiana na jambo hilo, naye alijua bila shaka angekunywa tu kwa kuwa alimwamini.

Kweli ilipofika kesho, Jaquelin alifikia uamuzi wa kuinywa ili mambo yaende jinsi rafiki yake alivyoyapanga, bila kujua alikuwa anachukua hatua ya kujiangamiza. Gilbert alipatwa na wasiwasi kiasi kwa kuwa Jaquelin hakuwa ameenda kazini, na hata alipompigia hakupokea. Jaquelin aliziona simu zote za Gilbert lakini alizipuuzia, na sasa Gilbert akawa ameamua kumfata nyumbani ili waweze kuongea. Aliwaza huenda wakati huu Jaquelin angekuwa ametulia zaidi, hivyo labda hata angeyatengeneza mambo kati yao vizuri kwa kuwa kwa kiasi fulani alim-miss sana.

Ilikuwa ni kama Mungu tu ndiyo alisaidia kufanya wazo la Gilbert kwenda kwa Jaquelin limwingie, kwa sababu ilikuwa ni wakati amefika tu nje ya geti la nyumba yao, ndiyo Jaquelin alikuwa ameinywa sumu ile akiwa chumbani kwake. Gilbert akafunguliwa geti baada ya mlinzi kuona ni boss karudi, naye akaliingiza gari ndani na kushuka, kisha akaelekea ndani ya nyumba. Alipokelewa kwa salamu na msaidizi wao wa kazi, naye akamuuliza ikiwa Jaquelin alikuwepo, na kujibiwa kwamba alikuwa chumbani. Akapanda ngazi kuelekea mpaka mlango wa chumba chake, kisha akashusha pumzi ndefu na kuufungua mlango. Alishtuka sana baada ya kumwona Jaquelin akiwa amelala chini huku mdomoni akitokwa na povu zito jeupe. Akawahi chini pale na kuanza kujaribu kumwamsha, lakini Jaquelin alikuwa ametulia tu huku amefumba macho. Akaiona chupa ile ndogo ikiwa kitandani, naye akatambua kuwa mke wake alikuwa amekunywa sumu.

Upesi sana akambeba na kumwahisha mpaka kwenye gari, kisha akalikimbiza kwa kasi sana kuelekea hospitali. Aliishiwa raha kabisa na kuanza kujilaumu mno kwa tukio hilo. Hakumjulisha mtu yeyote kuhusu jambo hilo, lakini wa kwanza kufika hapo hakuwa mwingine ila Beatrice mwenyewe. Akawa anamfariji kinafiki sana, akionyesha kama ana huzuni usoni, lakini kumbe anafurahia moyoni. Madaktari walimwambia Gilbert kuwa mke wake alihitaji matibabu ya hali ya juu zaidi kwa sababu sumu ilisababisha ini lake lianze kuharibika, na walikuwa wamefanya yote wawezayo ili kumwongezea muda zaidi, lakini kama angecheleweshwa basi angepoteza maisha.

Uzuri ni kwamba pesa ilikuwepo, hivyo Gilbert akafanya mpango wa haraka ili Jaquelin asafirishwe kwenda kutibiwa nje ya nchi upesi. Jambo hili halikumfurahisha Beatrice kwa sababu ikiwa wangefanikiwa kumtibu Jaquelin, basi mpango wake ungekuwa wa kazi bure tu. Gilbert aliondoka na Jaquelin kwa ndege ya kibinafsi mpaka Ulaya, ambako angetibiwa kwenye hospitali kubwa yenye kila aina ya vifaa. Lakini baada ya kufika kule, Gilbert aliambiwa kwamba hali ya Jaquelin ilikuwa mbaya sana na ingehitajika atolewe ini lake na kupandikiziwa lingine kwa njia ya OLT (Orthotopic Liver Transplant), la sivyo angekufa. Mwanaume akaweka pesa yote iliyohitajika ili maisha ya mke wake yaokolewe kwa gharama zote.

Madaktari walianza kufanya kazi yao, na ni kipindi hiki Harleen alikuwa kwenye hospitali hii pia akisaidia kwenye masuala ya upasuaji, kwa sababu alikuwa ni daktari mchanga lakini mwenye ustadi sana kiasi kwamba alialikwa hapo ili afanye kazi. Ndiyo kipindi hiki alipata kutambua kuwa mgonjwa huyo alikuwa mama yake Dylan, hivyo alitia bidii kwenye mambo aliyoweza kufanya ili ahakikishe anasaidia pia kuokoa uhai wa mwanamke huyo. Lakini hakuweza kupata nafasi ya kuonana na Gilbert kutokana na kuwa na wagonjwa wengine wa kushughulika nao kwa mida fulani hususa.

Gilbert aliendelea kukaa huko, na baadae Dylan pamoja na Camila walifika pia baada ya kusikia taarifa hizo, wakiwa wametokea Brazil. Dylan alihuzunishwa sana na kilichompata mama yake, lakini hakuwa na muda mrefu wa kukaa hapo kwa sababu walikuwa karibu kuanza mitihani ya mwisho chuoni kule. Alimsihi baba yake amweleze ni nini hasa kilichosababisha mpaka mama yake akanywa sumu, lakini Gilbert alikosa jibu la kumpa.

Kwa akili ya haraka, Dylan alichukulia bila shaka huenda ni kwa sababu ya baba yake ndiyo Jaquelin alikunywa sumu, kwa kuwa pindi kadhaa nyuma Jaquelin alipowasiliana na Dylan, mara kwa mara angemwambia kuwa baba yake anatoka nje ya ndoa, kwa hiyo jambo hili zito likaanza kufanya Dylan awe na chuki kumwelekea baba yake.

Baada ya miezi kama miwili, Jaquelin alirejewa na fahamu, na wakati huu tayari Dylan alikuwa amerudi Brazil, akiwaacha Gilbert na Camila huko Ulaya. Wawili hawa waliendelea kumtunza kwa upendo kwa miezi mingine michache mpaka alipoweza kuruhusiwa kuondoka huko.

Waliporudi nyumbani, kila mtu aliyejua kuhusu Jaquelin kupelekwa Ulaya kimatibabu alipewa taarifa kwamba Jaquelin alikuwa tu na shida ya ini, lakini ukweli kwamba alikunywa sumu ukafichwa ili kuepuka porojo nyingi. Gilbert alimshauri Jaquelin wajitahidi kuishi kwa amani wakati huu, na asirudie tena kufanya kitu kama hicho, kwa kuwa inaonyesha alikuwa akijifikiria yeye mwenyewe tu bila kuwafikiria watu waliompenda wangehisije kama angewaacha namna hiyo. Akamwomba samahani ya kila jambo ambalo alifanya lililomuumiza, nao wakaendelea kuwa pamoja kama wanandoa.

Baada ya wiki chache kutokea hapo, Camila alirudi Brazil. Beatrice, rafiki mnafiki, akawa amefika kwa Jaquelin kumsalimu, akisema alikuwa safari ya mbali ndiyo maana hakuweza kuwa hapo mapema. Yeye na Jaquelin mwanzoni walionekana kama kuwa na utengano kidogo kutokana na akili ya Jaquelin kufikiria sana kuhusu utata wa jambo lililomkuta baada ya Beatrice kumshauri achukue hatua ile ya kunywa sumu, lakini baadae Jaquelin akaachia kukaza na kuendelea kumwamini rafiki yake huyo. Dylan alikuwa anataka sana kurudi nchini lakini tatizo likawa limezuka baada ya gonjwa baya sana kuibuka kule na kusababisha watu wengi wafe, hivyo alitakiwa kuwa ndani tu kwa muda mrefu akiwa huko ili kujilinda mpaka wakati ambao lingeisha.

Kwa hiyo maisha yakaendelea tu vizuri, naye Jaquelin akazidi kurudia hali njema ya kiafya kadiri miezi ilivyopita. Beatrice bado alikuwa na kinyongo sana kuwaelekea wanandoa hao wawili, naye aliazimia kufanya yote awezayo kuwaangusha. Wakati huu alikuwa na hasira na Gilbert pia kwa sababu alimkataa na kuamua kumwokoa mke wake kwa hali na mali, hivyo akatafuta njia ya kuanza kuwavurugia mambo yao, na pa kuanza kukawa kwenye kampuni yao. Aliona aungane na Mr. Bernard, ambaye alikuwa amemfatilia na kujua mambo yake mengi haramu aliyoyaficha kisiri, hivyo akafanya makubaliano naye na kuwa anamsaidia kuyaendesha mambo hayo haramu, na kumuahidi faida nyingi nzuri ambazo angepata kwa kujiunga naye ili kuwaporomosha Gilbert na Jaquelin; lengo lake likiwa ni kumtumia ili kufanikisha mpango wake.......


β˜…β˜…β˜…


2021

BAADA YA BEATRICE KUWA AMEMPIGA RISASI PIUS


"Nini maana yake Beatrice? Kwa nini umefanya hivi?" Mr. Bernard akauliza.

Beatrice akamgeukia akiwa anamtazama kwa macho makali sana, kisha akainyanyua bastola ile kumwelekea Mr. Bernard pia. Mwanaume huyo alitumbua macho yake kwa kushtuka sana, akiwa haelewi ni nini iliyokuwa maana ya Beatrice kufanya haya.

"We...Beatri....acha masihara basi...kwa nini una-point gun kwangu?" Mr. Bernard akauliza kwa hofu.

Yule mwanaume wa Mr. Bernard alikuwa amesimama kando yake, na yeye akiwa anashangazwa na jambo hilo. Kisha papo hapo Beatrice akavuta kifyatulio cha risasi akiwa bado ameielekezea bastola kwa Mr. Bernard!



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Beatrice, pamoja na wale mabaunsa wake wawili aliokuja nao, wakaanza kucheka sana. Mr. Bernard akabaki ameduwaa baada ya kutambua bastola ya Beatrice haikuwa na risasi tena, hivyo mwanamke huyo alikuwa anajaribu kumwogopesha tu kwa kuwa hakikutoka kitu. Mr. Bernard alibaki kumtazama kwa njia iliyoonyesha kwamba kitendo hicho kilimuudhi, kwa kuwa alikuwa ameua mtu mbele yake na kumfanyia masihara tena. Ijapokuwa Beatrice alikuwa mwenye nguvu kwa kadiri kubwa, bado alikuwa ni mdogo kwa Mr. Bernard, kwa hiyo kwa kiasi kikubwa dharau hizo mwanaume huyu alizichukia.

"Vipi? Ulikuwa unafikiri safari yako ya motoni imewadia? Ilikuwa na risasi mbili tu, tuliza boli," Beatrice akasema kwa kejeli huku akicheka.

"Mambo gani haya eeh? Kwa nini umemuua huyu mwanaume? Sikutaka tum..."

"Nimejisikia tu kum-shoot," Beatrice akamkatisha.

"Lakini alikuwa na info muhimu niliyotaka kujua! Sasa nitaijua vipi sasa hivi baada ya wewe kujisikia tu kutaka kumuua? Na umeshamuua, nitaipataje?" Mr. Bernard akaendelea kulalamika.

Beatrice akampa baunsa wake mmoja bastola yake, kisha akamsogelea karibu Mr. Bernard. Wakati huu alikuwa anamwangalia kwa njia iliyoonyesha yuko serious, naye Mr. Bernard akaweka umakini zaidi.

"Kwa huu muda wote ambao nimekuwa pamoja nawe Bernard, nilishawahi kufanya jambo lolote ambalo...haukupenda?" Beatrice akamuuliza.

Mr. Bernard akatikisa kichwa kukanusha.

"Basi ni kwa nini wewe umefanya jambo ambalo mimi sijapenda?" Beatrice akamuuliza tena.

"Unamaanisha nini?" Mr. Bernard akauliza.

"Ilikuwa ni kazi ndogo...ndogo sana...lakini ukashindwa! Naanza kujiuliza ikiwa kufanya nawe mpango huu kutaniletea manufaa au hasara, maana nimeanza kuziona hasara mapema sana," Beatrice akamwambia.

"Sikuelewi Beatrice. Unaongelea nini? Kama ni kuhusu kampuni, usijali. Nitafanya mpango ili..."

"Yaani na ujanja wako wote bado mpaka sasa hujatambua kinachoendelea! Unbelievable," Beatrice akamkatisha.

"What? Nini...una...nini kinaendelea?" Mr. Bernard akauliza akiwa amechanganyikiwa.

"Dylan is alive," Beatrice akasema kwa mkazo.

Mr. Bernard akabaki kumwangalia kama mtu aliyepigwa na bumbuazi kutokana na maneno hayo ambayo yalishangaza sana.

"Dylan?!" Mr. Bernard akauliza.

"Wewe na mpuuzi mwenzako huyo mlishindwa kutekeleza jambo dogo tu namna hiyo," Beatrice akamwambia kwa ukali.

"Dylan yuko hai? Umevuta marijuana ya wapi Beatrice?"

"Usinisemeshe hivyo Bernard, nitakuumiza!" Beatrice akamwambia.

"Unanishangaza sasa! Dylan amekufa kwenye ile plan yetu...unachosema ni nini?" Mr. Bernard akasema.

"Nyie wote ni wapumbavu tu!" Beatrice akamwambia kwa sauti ya juu.

Mr. Bernard alikuwa haelewi jambo hili hata kidogo. Kwenye kichwa chake akawa anafikiria labda Beatrice amerukwa na akili, lakini hakujua alikuwa anaambiwa ukweli mtupu. Beatrice akapiga hatua chache kuelekea mlangoni, kisha akawaangalia wale mabaunsa wake.

"Ondoeni mwili huu haraka, mlio wa risasi umesikika sana, umevuta attention. Wewe...nifate," akasema hivyo na kumwambia Mr. Bernard amfuate.

Wale jamaa wakaanza kushughulika na mwili wa Pius, naye Mr. Bernard akamfuata Beatrice nyuma akiwa bado kwenye sintofahamu kubwa sana. Walifika na kuingia pamoja ndani ya gari lake Beatrice, kisha mwanamke akaliondoa hapo na kumpeleka Mr. Bernard sehemu ya mbali ili amjuze vizuri ni nini kilichokuwa kinaendelea. Alifika naye sehemu ile ile ya msitu ambayo alimuulia mpelelezi wa Alfred kipindi kile, na hapo akaanza kumweleza kuwa ni Dylan ndiye aliyewasaidia wazazi wake waweze kuirudisha kampuni yao tena na kumwondoa yeye hapo.

Mr. Bernard alishangazwa sana na jambo hili, naye akauliza iliwezekanaje Dylan kusalimika kwenye ajali ile ya helicopter waliyokuwa wameipangia ianguke. Beatrice akasema hakujua ni jinsi gani kijana huyo alivyookoka, lakini kuona kwamba hajaja mpaka sasa na kufanyia mambo mengi akiwa gizani ilimaanisha bila shaka alijua ile haikuwa ajali kama wenyewe walivyotaka kufanya ionekane na alikuwa na mipango mingi ya kuwaangusha wabaya wake. Beatrice hakuwa na uhakika kama Dylan alijua na yeye alihusika katika hilo, lakini akamwambia Mr. Bernard ni lazima wamtafute haraka ili wamwangamize.

Mambo yote haya yalimwacha Mr. Bernard katika taharuki nzito, kwa kuwa alihofia kuwa Dylan anaweza kufanya jambo baya kumwelekea; ukitegemea ameweza kuirudisha kampuni ya wazazi wake mikononi mwao tena, bila shaka hilo lilimaanisha kijana huyu alikuwa na nguvu nyingi sana wakati huu. Beatrice akamwambia Mr. Bernard aache kujilizaliza na atende kama mwanaume kweli, kwa kuwa kijana huyo angeweza kuwa popote pale hivyo walihitaji kujua ni wapi hasa ili wafanikishe mipango yao maana kikwazo kikubwa wakati huu ingekuwa ni yeye.

"Lakini sasa....kwa nini umemuua Pius? Kama unavyosema, Dylan ndiyo anayetuandama sasa..yule mzee alikuwa na...."

"Bernard, you need to think with your head, not your balls all the time! (unatakiwa kufikiria na kichwa chako, siyo mipira yako kila mara!)" Beatrice akamkatisha.

Mr. Bernard akabaki kumwangalia.

"Hata hujiulizi baada ya kujua haya yote ni kwa nini Pius alikuwa anakukwepa? Dylan got to him. ANAJUA ulimlipa kuiangusha chopper, ndiyo maana tako lako liko broke sasa hivi. Biashara zako zote zimeanguka, kampuni umefukuzwa, isingekuwa ya mimi kuku-back ungekuwa umeshachukuliwa hatua na polisi. Hujiongezi ni nani kafanya hayo yote?" Beatrice akasema kwa mkazo.

Mr. Bernard akawa amechanganyikiwa haswa.

"Pius alikuwa daraja. Nimelivunja sasa. Nataka kuucheza mchezo huu na Dylan, mimi na yeye. Ahahahah... anafikiri atashinda kwa sababu anadhani hatujui yuko hai. Sasa nitamwonyesha kwenye mchezo huu mshindi huwa ni mmoja tu....na huyo ni Beatrice," Beatrice akasema huku akiwa anatabasamu kwa kiburi.

Kuanzia wakati huo, lengo la wawili hawa likawa ni kutafuta kimya kimya njia za kujua Dylan alikuwa wapi ili waweze kumwangamiza, na wakati huu walitaka kuhakikisha kwamba wanafanya hivyo kwa umakini zaidi ili safari hii wasirudie makosa ya kipindi cha nyuma ambayo ndiyo yaliyosababisha matukio haya mabaya upande wao kuanza kutokea.


β˜…β˜…β˜…


"Bado tu?" Grace akauliza.

"Yeah," Dylan akajibu.

Grace akatazama pembeni akiwa na uso wenye mashaka.

"It's weird isn't it? (ni ajabu siyo?)" Dylan akauliza.

"Yeah. Sijui ni kwa nini lakini, kuna kitu nahisi kinaendelea," Grace akasema.

"Mimi pia. Lakini ni mpaka tumpate ndiyo itajulikana. Jafari's working on it," Dylan akasema.

Haya yalikuwa ni maongezi baina ya wawili hawa wakiwa pamoja nyumbani siku chache baada ya tukio lililompata Pius. Walikuwa wanamwongelea mwanaume huyo ambaye alipotea ghafla tu, na wote walijua bila shaka kulikuwa kuna jambo limejificha kwa sababu Jafari alikuwa ametia juhudi nyingi kumpata lakini hakuwa amefanikiwa bado. Wakati huu ilikuwa Jumapili mchana, nao walikuwa wameketi kwenye meza ya chakula huku Matilda akiwa analeta vyakula mbalimbali hapo kwa ajili yao waweze kupata lunch pamoja.

"Umeshafikiria kuhusu ni lini utakutana na wazazi wako?" Grace akauliza.

"Sija...sijafikiria bado. Kukutana nao tena inamaanisha itanibidi ni-act kwamba nakumbuka kila kitu...sijui hata kama itafaa maana sitaki niwafanye kuwa target rahisi mpaka tumjue mtu anayemsaidia yule mwanaume," Dylan akaeleza.

"Uko sahihi kwa kiasi fulani lakini...unafikiria mambo mengi mbali sana. Kuna njia ya kuonana nao bila adui kutambua uwepo wako...na hata kama itawezekana, uwaambie kuhusu mpango wetu ili wasijikwae kwenye lolote kwa ajili ya kujilinda," Grace akamshauri.

"Sidhani kama kuwaingiza sana kwenye mpango huu kutakuwa ni wazo zuri. Wamepitia mambo mengi magumu, hasa baada ya kufanywa wafikiri nimekufa. Singependa nirudi halafu niwaambie kuwa bado kuna rundo la matatizo yananiandama."

"Except wakati huu hauko bila msaada. Dylan, niko pamoja nawe. Uwe na uhakika hii vita tunashinda."

"Unavyoongea ni kama unasema umerishishwa na yaliyompata Bernard," Dylan akasema.

Grace akaanza kujiwekea chakula huku akionyesha kukerwa baada ya kusikia jina hilo.

"Bado Dylan. Bado sijaridhika," akajibu kwa uhakika.

Dylan akamtazama kwa uelewa, kisha naye akaanza kuweka chakula kwenye sahani yake.

Wote kwa pamoja walianza kula huku wanapeana tabasamu kufurahia chakula chao. Lakini baada ya Grace kula mboga fulani ya majani aliyotengeneza Matilda, akakunja sura yake na kuanza kutafuna kwa njia yenye kuonyesha ilikuwa ni mbaya. Dylan akamwona, naye akasitisha kula na kubaki kumtazama kwanza. Grace alipojaribu tena kuionja, akakunja sura yake zaidi kwa njia iliyoonyesha kinyaa.

"Grace...what's wrong?" Dylan akauliza.

"Hii mboga....Matildaaa..." Grace akamwita.

"Beee..." Matilda akaitikia kutokea jikoni.

Kisha baada ya sekunde chache msaidizi huyo wa kazi akawa amefika.

"Umeweka nini kwa hii mboga, mbona mbaya?" Grace akauliza kwa kuudhika.

Matilda akawa anababaika.

"Ni mbaya?" Dylan akauliza.

"Ndiyo...please onja uone," Grace akamwambia.

Dylan akachukua kijiko na kutoa mboga hiyo kidogo, kisha akaionja, huku Grace akiwa anakunywa maji. Lakini ilikuwa ni mboga nzuri na tamu sana. Akamwangalia Grace baada ya kuionja.

"Naona iko vizuri tu," akamwambia.

"Nini?" Grace akashangaa.

Matilda naye pia akaonja na kuona mboga kweli ilikuwa nzuri sana.

"Labda umetafuna ulimi wako," Dylan akatania.

"Hamna bwana, siyo masihara," Grace akasema.

"Okay, ngoja."

Dylan akachukua kijiko na kuchota mboga hiyo kidogo, kisha akamsogezea mdomoni Grace ili kumlisha. Grace kwa mashaka akaila mboga hiyo, naye Dylan akauliza alihisije wakati huu. Bado Grace aliendelea kuitafuna kama vile ilimtia kinyaa sana, kisha akajilazimisha kumeza. Lakini baada tu ya hapo ndipo akaanza kujihisi vibaya hata zaidi.

"Mm-mm...hii mboga mbaya....mbaya sana...yaani..."

Grace akawa anaongea kwa njia yenye kuonyesha hisia mbaya. Dylan na Matilda wakashindwa kuelewa alikuwa amepatwa na nini, naye Grace akasema angeenda chumbani kwanza. Lakini wakati amesimama, akakaribia kudondoka baada ya kuyumba kidogo, na hapo hapo Dylan akasimama ili akamshike. Ila kabla hajamfikia Grace akaanza kutapika hapo hapo! Dylan alishtuka sana na kumwahi haraka, kisha akamshikilia huku anamsugua mgongo wake kwa kasi. Grace akaanza kuyumba haswa kutokana na kuhisi kizunguzungu, hivyo taratibu Dylan akamwongoza mpaka kwenye sofa moja na kumwacha ajilaze hapo.

Matilda aliharakisha kuanza kupasafisha pale chini, naye Dylan akawa anaangalia joto la mwili wa Grace kuona kama alikuwa na homa kali. Kisha akatoa simu yake na kumpigia Hamisa; yule yule rafiki wa Grace, ambaye alikuwa ni daktari pia. Akamweleza kuhusu hali ya Grace na kumwomba afike hapo nyumbani ili kumwangalia, kwa kuwa alikoishi hapakuwa mbali sana na nyumba ya Grace. Hamisa akakubali, na baada ya hapo Dylan akaketi kumwangalia mwanamke wake kwa ukaribu.

Grace alionekana kuishiwa nguvu na hata hakufumbua macho yake kila mara Dylan alipomsemesha, hivyo mwanaume akamnyanyua na kumpeleka mpaka chumbani kwake; akimlaza kitandani. Matilda naye akafika akiuliza ni nini ambacho kilikuwa kinamsumbua boss wake, naye Dylan akasema ingewapaswa wamsubirie Hamisa ili waweze kuwa na uhakika zaidi. Grace wakati huu alikuwa amesinzia, na ulikuwa ni usingizi uliomjia kwa uharaka sana.

Baada ya kama dakika 10 hivi, simu yake Dylan iliita, naye akamwomba Matilda akae humo humo ili akaongee na aliyempigia nje ya chumba. Akatoka na kusogea hatua chache mbele kisha akapokea.

"Jafari," Dylan akasema.

"Yeah, Dylan, nimefanikiwa kumpata Pius...na nilichokuta siyo habari nzuri," Jafari akasema upande wa pili.

"Nini kimetokea kaka?" Dylan akauliza.

"Pius ameuawa," Jafari akasema.

Dylan akashangaa sana.

"What?"

"Yeah. Nilipata taarifa za mwili uliotolewa kwenye ziwa ukiwa na risasi mbili ndani yake, nikaona ni-check. Nimekuta ni yeye aisee," Jafari akamtaarifu.

Dylan akafumba macho na kushusha pumzi ndefu.

"Hii siyo coincidence," Dylan akasema.

"Ndiyo najua. Bila shaka ni Mr. Bernard ndiyo amemuua."

"Huenda na mtu anayemsaidia pia."

"Ndiyo kaka."

"Hii inamaanisha kwamba watakuwa wamejua kuhusu sisi kumfikia, na kama iko hivyo, basi huenda wanajua pia kwamba niko hai," Dylan akamwambia.

"Kwa hiyo tufanyaje?" Jafari akauliza.

Ni wakati huu ndipo Dylan akasikia sauti ya horn ya gari nje ya geti la nyumba hii. Akajua bila shaka ilikuwa ni Hamisa ndiyo amefika.

"Tutaongea vizuri zaidi baadae. Kuwa makini sana Jafari kuanzia wakati huu," Dylan akasema.

"Wewe pia mkuu. Mfikishie boss salamu zangu," Jafari akamwambia.

"Okay."

Mambo yalikuwa yameanza kuchemka haswa, na yalikuwa yaaelekea kuiva! Dylan alijua maadui wake bila shaka ndiyo waliohusika na mauaji ya Pius, na kuona ni jinsi gani ambavyo walikuwa wakatili, alitambua ilikuwa ni muhimu sana kuweza kumfichua mbaya wao mwingine haraka iwezekanavyo, kwa kuwa kusubirishia mpaka wakati mwafaka isingewapa faida yoyote tena. Akashuka mpaka chini na kumfungulia Hamisa mlango wa ndani, baada ya kuwa ameliingiza gari na kuegesha nje hapo. Walisalimiana tena vizuri, kisha akaenda pamoja naye mpaka kwa Grace.

Dylan na Matilda waliamua kumwacha Hamisa ashughulike na kumpa tiba Grace. Matilda akaenda chini kuendelea na kazi, huku Dylan akisubiri nje ya chumba cha Grace. Baada ya dakika kadhaa, Hamisa akamwita Dylan ndani mule, na sasa akakuta Grace amekwishaamka na kuketi kitandani akiwa ameegamia mto mwanzoni mwa kitanda. Bado Hamisa hakuwa amesema kilichomsumbua Grace, na kumwita Dylan ndiyo lililokuwa lengo.

"Kwa hiyo....ninaumwa nini?" Grace akauliza.

"Unafikiri nini? Malaria labda? Huwa haulali na neti mpenzi unategemea nini?" Hamisa akatania, naye Dylan akatabasamu.

"Acha masihara bwana. Ilikuwa kidogo nizimie...au nimezimia kweli?" akamuuliza Dylan.

"Ulikaribia," Dylan akajibu.

Hamisa akawa anazilaza-laza nywele za Grace kwa upendo.

"Kwa hiyo? Nina Malaria kweli?" Grace akauliza.

"Hapana. Umepatwa na shida fulani kubwa sana...itachukua muda mrefu kui-overcome," Hamisa akamwambia kwa u-serious kiasi.

"Ni nini?" Grace akauliza.

Hamisa akatazama chini na kushusha pumzi kwa huzuni.

"Hamisa...nina shida gani?

Hamisa akamwangalia Dylan, ambaye pia alikuwa ana wasiwasi wa ni nini ambacho daktari huyu angesema, kisha akamtazama tena Grace machoni.

"Yaani sijui nisemeje....ni...ni shida fulani ambayo itachukua mpaka miezi tisa ndiyo utakuwa sawa tena," Hamisa akasema kwa huzuni fulani hivi.

Dylan, aliyekuwa amekunjia mikono kifuani, akaishusha na kubaki amezubaa kumwangalia tu Grace baada ya kuwa amekisia ni nini ambacho Hamisa alimaanisha. Grace akakunja uso kimaswali sana. Bado hakuwa ameelewa rafiki yake alichomaanisha.

"Congratulations sis, you're pregnant! (Hongera dada, una ujauzito!)" Hamisa akamwambia kwa shauku kubwa sana.

Maneno yake yalimwacha Grace mdomo wazi. Hamisa yeye akawa anaonyesha furaha tele kwa ajili ya rafiki yake huyu.

"I'm pregnant?" Grace akauliza kwa sauti ya chini.

Hamisa akatikisa kichwa taratibu kukubali.

Grace akamwangalia Dylan machoni, na wote wakawa wanatazamana kwa njia iliyoonyesha hawakuwa wametarajia hili. Hamisa akawaangalia wote kwa kuelewa kwamba bila shaka ujauzito huo ulikuwa ni zao la wawili hawa, naye akatabasamu kwa furaha. Grace alionekana kuchanganywa kwa kiasi kikubwa na jambo hili.

"Unamaanisha nini Ham...nawezaje....nilifikiri siwezi...." Grace akawa anababaika.

Dylan akaangalia chini.

"Well, inaonekana haukuwa sahihi. Una katoto humo sweety...emumumuuumwaahh...ahahahah... nitafaidi kuitwa aunty," Hamisa akasema kwa shauku.

Kisha, baada ya kuwa amemweleza Grace jinsi ya kuanza kujitunza kuanzia wakati huu, akawaaga wawili hawa, akimpongeza na Dylan pia kwa kuwa angekuwa baba. Kutoka ndani ya moyo wake, Dylan alifurahi kujua kwamba angeweza kuitwa baba wa mtoto wa Grace, lakini hakuwa na uhakika mwanamke huyu alichukuliaje suala hili kwa kuwa uso wake tu ulionyesha wazi kabisa kwamba hakutarajia, na wala hakupendezwa kabisa na jambo hilo. Akamsogelea mpaka karibu na kuketi kitandani karibu yake, nao wakawa wanatazamana kwa hisia machoni. Grace alionyesha wasiwasi wa hali ya juu, naye Dylan akataka kumtuliza.

"Grace...."

"Dylan, what have I done?!" Grace akasema kwa huzuni.

"What do you mean?"

"Dylan...huu....huu siyo wakati...oh my God.... huu...."

"Okay Grace, calm down. Calm down..."

Grace akawa anapumua kwa kasi kiasi.

"Najua haukuwa umetarajia hili...lakini kama Hamisa alivyokwambia usi-stress sana ni mbaya kwa..."

"Dylan hii haikupaswa kutokea!" Grace akamkatisha.

Dylan akabaki kumtazama tu machoni.

"This is a mistake. Siwezi kuruhusu jambo hili litokee," Grace akasema kwa hisia.

"Grace...hatuwezi kubadili kilichotokea. Na pia....I think hii ni sababu ya kuwa na shangwe Grace. Ahah...utakuwa mama...nami nitakuwa..."

Grace akanyanyuka upesi na kusimama pembeni. Alionekana kuhangaishwa sana na jambo hili. Dylan akasimama pia na kumshika ili watazamane.

"Grace..."

"Dylan....please. Usi....usianze kuniambia jinsi gani jambo hili lilivyo zuri, kwa sababu hilo halitabadili navyoliona," Grace akasema.

"Hakuna sababu yoyote ya kuogopa Grace. Mimi...."

"Ni rahisi kwako kusema hivyo, Dylan. Huwezi kuelewa ni jinsi gani nimevunjika moyo," Grace akamwambia huku machozi yakianza kumtoka.

"Umevunjika moyo kujua kwamba utakuwa mama wa mtoto wetu?" Dylan akauliza.

"Don't...do that, Dylan. Huwezi kunielewa hata siku moja," Grace akasema kwa huzuni.

"Okay. Sawa. Siwezi kukuelewa. Kwa hiyo...unataka tufanye nini sasa? Mmm?" Dylan akamuuliza.

Grace akatulia kidogo, kisha akasema, "Naitoa."

Dylan akabaki kumtazama Grace kwa kushangazwa na maneno yake. Alikuwa amemshika mikono, lakini akamwachia na kurudi nyuma kidogo akiwa haamini kama kweli alichosikia kilikuwa sahihi.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


"Unasemaje?" Dylan akauliza kwa sauti ya chini.

Grace akajifuta machozi na kumwangalia usoni.

"I'm aborting this pregnancy. Ndiyo njia pekee ya ku-solve hili," akasema.

"Ku-solve? Ku-solve nini Grace? Unaelewa kwamba kilicho tumboni kwako ni uhai? Unataka kuutoa uhai kwa sababu gani Grace?" Dylan akauliza kwa hisia kali.

"Dylan... tuko kwenye kipindi ambacho sote tunatakiwa kuwa imara ili kuwashinda adui zetu. I can't afford kuwa dhaifu wakati huu. Adui zetu wakijua nina udhaifu huu si ndiyo watapata njia ya kuniangusha kirahisi? Unafikiri..."

"Grace!" Dylan akamkatisha kwa sauti ya chini.

Grace akawa anapumua kwa kasi huku analia. Dylan akatikisa kichwa kwa kusikitika kiasi.

"Grace mtoto ni baraka kwetu...siyo udhaifu. Huyo ndiyo atakufanya uwe imara zaidi, kwa sababu mambo yote utakayofanya yatakuwa kwa ajili yake pia," Dylan akasema kwa hisia.

"Dylan hatuko kwenye movie, okay? Naomba uache ku-act all sainty na mimi na u-face reality. Masuala ya watoto wakati huu sikuwa na muda nayo kabisa. Usijihisi hatia hata kidogo Dylan kwa sababu ninafanya hivi ili kuhakikisha wewe na mimi hatutikiswi. Haujui jinsi inavyokuwa? Mara nitaanza kuhitaji hiki, mara kile, usumbufu mwingi tu na mambo yasiyo ya muhimu, mwisho wa siku nitasababisha tupoteze morale ya juu tuliyofikia katika mpango wetu kwa sababu kila kitu itakuwa ni mtoto, mtoto, mtoto," Grace akaeleza kwa hisia sana.

Dylan akamwangalia tu usoni bila kusema lolote. Ijapokuwa Grace alijiona kuwa sahihi, bado Dylan aliona sababu zake hazikutosha kuhalalisha uamuzi huu mbaya ambao alitaka kuchukua. Akamsogelea mpaka karibu na kumshika usoni kwa mikono yake.

"Grace...hicho ni kitu ambacho siwezi KAMWE kukubaliana nacho. Najua unaogopa. Lakini hauna sababu ya kuogopa Grace, kwa kuwa niko pamoja nawe pia. Umetoka kuniambia muda mfupi uliopita kwamba uko pamoja nami...na mimi pia nakuhakikishia nitakuwa pamoja nawe katika hili Grace. Tafadhali usifanye hivi. Hili ni jambo ambalo litauvunja sana moyo wangu ikiwa utalifanya Grace. Please....please don’t have an abortion.”

Maneno haya yalisemwa na Dylan kwa hisia sana, naye Grace akawa anadondosha tu machozi huku anamwangalia jamaa kwa hisia nyingi zilizovurugika. Dylan akamkumbatia ili kumwonyesha kwamba alimjali sana, na angekuwa pamoja naye kupitia kipindi hiki ambacho kilimhofisha mwanamke wake huyu. Lakini Grace akajitoa kutoka kwenye kumbatio la Dylan na kuingia bafuni kisha kujifungia; akimwacha Dylan anamwangalia tu.

Mwanaume akaketi kitandani akiwa na msongo wa mawazo mengi sana. Pamoja na kwamba Grace alikuwa aina ya mtu ambaye angefanya lolote lile aliloona kuwa sawa, Dylan asingeruhusu achukue hatua hii. Akajihakikishia kwenye akili yake kuwa angefanya yote ndani ya uwezo wake kuepusha balaa ambalo Grace angejisababishia kwa kuchukua uamuzi huo.

Ilifika mpaka usiku Grace akiwa bado chumbani kwake tu. Dylan angejaribu kurudi ili waongee tena, lakini Grace hakutaka kuzungumza naye. Hivyo, Dylan akaamua kusaidizana na Matilda kuandaa chakula, kisha akapanda nacho mpaka chumbani kwa Grace na kumkuta akiwa amejilza kitandani. Akamkaribisha ale, lakini mwanamke akaendelea tu kuwa kimya. Kwa hiyo akakiweka chakula pembeni, kisha akapanda kitandani hapo na kulala nyuma yake; akiibana miili yao kwa njia ya kumkumbatia kwa upendo. Grace hakutenda kwa njia yoyote ile na kubaki ametulia tu.

"Hisia ulizonazo....ninazielewa. Nilipotambua kwa mara ya kwanza kwamba nimepoteza kumbukumbu, nilijihisi nimepotea sana. Nilihisi kuna mambo mengi mno nimepoteza. Najua hata wewe pia...unahisi ni kama kuna vitu vingi utapoteza kwa sababu ya jambo hili ambalo....hukupangia. Lakini unajua hiyo ni kwa nini? Ni kwa sababu una akili ya msichana mwenye miaka 18."

Dylan alikuwa anamwambia maneno hayo kwa sauti yenye utulivu, na baada ya kufika hapo, Grace akajiuliza ni nini iliyokuwa maana yake kumwambia kwamba ana akili ya msichana. Dylan alitia ndani utani huo ili kupata itikio fulani kutoka kwa Grace, na hilo likafanikiwa.

"Unamaanisha nini?" Grace akauliza.

Dylan akatabasamu baada ya kujua umakini wa Grace bado ulikuwepo.

"Msichana wa namna hiyo akipata ujauzito bila kupangia...kitu cha kwanza anachoangalia kuliko vyote huwa ni MATATIZO yatakayompata. Hali huwa hazifanani kwa wote najua, lakini kwa wewe, unaangalia sana matatizo UNAYOFIKIRI yatakupata na siyo baraka ambazo umepewa," Dylan akamwambia.

Grace akakaa tu kimya.

"Grace, tafadhali nakusihi ujitahidi kutoliona jambo hili kama tatizo. Usichukue maamuzi ya haraka bila kutafakari matokeo ya mbeleni. Abortion....ni jambo baya sana Grace. Kuna wanawake wanaolia kwa sababu hawapati mtoto, na hivyo wanajiona kama vitu vya kudharauliwa. Lakini wewe, una nafasi nzuri ya kuwa mzazi bora kwa sababu najua utajitahidi kumtunza mwanao kwa njia ambayo hatapitia kamwe mambo ambayo wewe ulipitia utotoni..."

Grace akaanza kulia bila kutoa sauti. Maneno ya Dylan yalimgusa sana moyoni, kwa kuwa kumbukumbu nyingi za maisha magumu ambayo yeye na dada yake walipitia utotoni zilimwingia tena.

"Grace, ninakujali sana. Ninataka uwe na maisha ambayo yatakuridhisha baada ya mambo haya yote tunayopitia. Lakini ikiwa utatoa mimba, utajiathiri kwa njia mbaya sana kihisia kwa maisha yako yote. Ila mimi niko pamoja nawe Grace, hilo nakuhakikishia. Tutamlea mtoto wetu pamoja. Sikuzote kumbuka kwamba niko pamoja nawe. Usiogope Grace. Nijajua unaweza, na utaweza kuwa mama bora kwa huyu kijacho," Dylan akanena kwa hisia sana.

Grace akakaza macho yake kwa nguvu akilia kwa hisia nyingi sana. Kisha taratibu akaugeuza mwili wake na kuutazamisha na wa Dylan, naye Dylan akamkumbatia kwa kumbana kwake zaidi huku Grace akiwa amefichia uso wake kifuani kwa mwanaume kitandani hapo.

Waliendelea kulala hivyo hivyo pamoja kwa dakika kadhaa, kisha Dylan akajinyanyua taratibu na kumnyanyua Grace pia akae. Akaanza kumfuta machozi kwa upendo, huku Grace anamwangalia kwa hisia nyingi, kisha Dylan akamfinya shavu kwa wororo. Grace akatabasamu kidogo na kuangalia chini, kisha akamkumbatia tena Dylan. Alihisi wasiwasi, msisimko, na faraja kwa wakati mmoja, na sasa akawa tayari kufuata kile ambacho Dylan alimsihi asifanye.

"Nimekuelewa Dylan. I won't do it," akasema akiwa bado amemkumbatia.

Dylan akashusha pumzi ya kuridhika na kumbusu nyuma ya shingo yake, huku akimbana zaidi kumwonyesha furaha.

Baada ya kumwachia, Dylan akakichukua chakula kile na kuanza kumlisha taratibu mwanamke wake huyu kitandani hapo. Grace alijihisi fahari sana, naye akawa anamlisha pia. Walikula bila kusemeshana neno lolote, zaidi ilikuwa ni kutazamana tu wakipeana tabasamu za furaha na upendo. Walipomaliza, Dylan akaweka vyombo pembeni, kisha akaketi karibu yake tena na kuvishika viganja vyake. Alikuwa na uso ulioonyesha aliwaza sana jambo fulani, naye Grace akataka kujua ni nini.

"Kuna tatizo?" Grace akauliza.

Dylan akamtazama machoni, kisha akatikisa kichwa kukubali.

"Ni nini?" Grace akauliza kwa kujali.

"Jafari amempata Pius. Lakini amemkuta akiwa amekufa," Dylan akasema.

"What?!" Grace akashangaa.

"Ameuliwa, Grace."

Grace akabaki mdomo wazi. Ni jambo ambalo hakuwa ametarajia, lakini kwa kiasi kikubwa halikumshtua sana kwa sababu alijua ni aina gani ya watu waliokuwa wanashughulika nao.

"Ni huyo mwanaume mpumbavu ndiyo amefanya hivi,'" Grace akasema kwa hasira.

"Inaonekana. Unajua hayo yote yanamaanisha nini Grace?" Dylan akauliza.

"Kwamba Benard amejua Pius alitoboa siri yake...ndiyo maana amemuua," Grace akajibu.

"Ndiyo. Na kama ni hivyo, hiyo pia inamaanisha anajua niko hai," Dylan akasema.

Grace akafumba macho na kutikisa kichwa kwa kusikitika.

"Oh God! This is too much. Hatuwezi kumwacha Mr. Bernard aendelee kuwa free tena Dylan. Ninachotaka kufanya sasa ni kumtia mikononi mwangu na kumlipa kwa mabaya yote aliyofanya...maana anaua mpaka na watu waliokuwa wanahitaji redemption," Grace akasema kwa hisia.

"Mimi pia Grace. Mimi pia. Lakini....nafikiri itakuwa vyema tukishughulika naye kwa njia ambayo itatusaidia kumpata mtu anayemsaidia kwanza," Dylan akasema.

"Lakini hicho si ndiyo ambacho tumekuwa tunafanya muda huu wote Dylan? Matokeo yake ni haya sasa! Naanza kuona ni kama Jafari alikuwa sahihi kabisa. Nimesubiria kuchukua hatua za haki, lakini matatizo ndiyo yanazidi...."

"Grace, calm down. Okay? Naelewa. Hata mimi nataka sana kuwashusha watu hawa. Ila kutokana na haya yote nimetambua kitu fulani kuwahusu maadui zetu," Dylan akasema.

"Nini hicho?"

"Ni waoga. Na watu waoga wenye nguvu sikuzote hutumia njia za vitisho ili kuwafanya watu wafikiri kwamba wao ni imara sana na wanapaswa kuogopwa, lakini kumbe wao ni wadhaifu tu. Nataka tuutumie woga wao kuwafichua na kukomesha uovu wao mwingi Grace...kwa hiyo tunahitaji kuchukua hatua mpya sasa," Dylan akaeleza.

Grace akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa, kisha akamuuliza, "So what should we do? (kwa hiyo tufanye nini sasa?)"

Dylan akatazama pembeni kwa umakini, akianza kuunda mpango mpya kwenye akili yake ili waweze kuupeleka mchezo huu kwa njia ambayo ingewasaidia kuwaangusha wabaya wao.


β˜…β˜…β˜…


Beatrice alikuwa akitafuta kila njia kuweza kujua Dylan alipokuwa, lakini hakuweza kujua kirahisi. Alitafuta habari zilizohusiana na huyo Smith Morgan ambaye alifanya yote mpaka kufanikiwa kampuni inarudi mikononi kwa Gilbert na Jaquelin, lakini hakuweza kupata taarifa zenye kutegemeka kutokana na jinsi taarifa hizo zilivyofichwa vyema.

Mara kwa mara aoipoongea na Jaquelin, aliuliza kwa ujanja ikiwa Dylan alikuwa amejitokeza kwao, lakini jibu la Jaquelin kama kawaida lilimfanya akwazike sana. Alianza hadi kufikiria ingekuwa bora kama tu angekatisha maisha ya Jaquelin moja kwa moja, lakini tena akafikiria kuhusu lengo lake la kisasi kwao. Lengo lilikuwa ni kuwaumiza kihisia sana wawili wale, na kwa kiasi fulani alifanikiwa kipindi kifupi nyuma, lakini sasa tena mambo yakamwendea ovyo. Lakini yote kwa yote, mwanamke huyu alikuwa ameazimia kumpata Dylan na kumwangamiza tu, iwe isiwe.

Mr. Bernard aliendelea kukaa kwa kujificha kiasi, akihofia kwamba Dylan angeweza kuwa popote pale na huenda hata alikuwa anapanga kumuumiza kwa njia fulani. Hivyo alipiga hatua zake kwa umakini sana ili asije tu kutoka nje na kushtukiza analambwa risasi ya kichwa. Aliendelea pia kuwasiliana na Beatrice kujua harakati zake za kumpata Dylan zilifikia wapi, na kwa kuwa jibu lilikuwa hasi, alipaswa kuendelea kufanya mambo yake mengi kwa kujificha.

Kwa upande wa Gilbert na Jaquelin, waliendelea kuongoza kampuni huku wakisubiri kwa hamu kumwona tena mwana wao. Muda ulionekana kuwa unazidi kwenda na ni kama matumaini yao yalikuwa yanafifia kwa kadiri fulani. Lakini waliamini kabisa kwamba wangemwona tu tena kijana wao, hivyo subira ilikuwa ni muhimu sana.

Kwenye siku hii, Gilbert alipigiwa simu akiwa ofisini kwake, na namba ngeni kabisa, naye akapokea na kujua ilikuwa ni mwakilishi wa Smith Morgan. Alimjulisha kwamba mnunuzi huyo wa hisa za kampuni hii alikuwa anataka wakutane kesho, sehemu fulani ambayo ingekuwa ni ya kibinafsi ili waweze kuongea. Hii ndiyo ingekuwa mara ya kwanza kwa Gilbert kuweza kukutana naye, na hamu kubwa ilimjaa kwa sababu alitarajia mambo mengi sana, ikiwemo uwezekano wa kukutana na Dylan tena.

Gilbert akakubali na kuuliza ingekuwa ni wapi, na mwakilishi huyo akamwambia kwamba alichopaswa tu kufanya ni kuondoka kwenye mji huu na kwenda mpaka kwenye mji ambao angeelekezwa, na huko taratibu zingine zingefuata. Mwendo wa kufika huko ingekuwa ni masaa manne, hivyo alipaswa kuondoka mapema asubuhi. Baba huyu wa Dylan hakuwa na kipingamizi, hivyo wakaagana, kisha akampigia simu Jaquelin na kumwambia aje kwenye ofisi yake ili wazungumze.

Baada ya Jaquelin kufika, Gilbert alimweleza kila jambo alilotoka kuambiwa na mwakilishi yule, naye Jaquelin akalipuka kwa hamu kubwa kwa kuwa na matarajio yale yale aliyokuwa nayo mme wake. Gilbert akamweleza kwamba angepaswa kuondoka kesho asubuhi ili kuwahi huko, na hapa Jaquelin akaanza kuomba kwamba na yeye aende huko pia. Ilikuwa ni wazi kwa Gilbert kwamba alitakiwa kwenda mwenyewe, lakini hangeweza kumdhibiti Jaquelin kwa sababu ya jinsi alivyokuwa mwenye king'ang'anizi sana, ukitegemea na hali zake, hivyo akamkubalia na kusema wangeenda pamoja lakini bila kumwambia mwakilishi yule jambo hilo.

Kwake Dylan, alitumia wakati huu mfupi uliobaki kabla ya kuanza mipango yake kumtembelea Baraka kule kwenye mji wao alikoishi zamani. Familia ya Baraka ilifurahi sana kumwona tena alipofika huko. Wakati huu watoto wawili wa Baraka, yaani Emilia na Steven, hawakuwa wakienda shule kwa kuwa Emilia alimaliza kidato cha nne na Steven pia alikuwa amemaliza darasa la sita na kufunga masomo mpaka mwakani, hivyo walikuwepo tu nyumbani. Ujio wake kwenye mji ule ulifanya watu kadhaa waende kumwona ili kumsalimu kwa kuwa alikuwa maarufu huko.

Walifurahia sana uwepo wake huko tena, hata Shani, mama Conso, na Leila waliacha kazi ili kwenda kumwona. Leila hakuweza kumsemesha hata kidogo zaidi ya kumwangalia tu, kwa kuwa bado alihisi hatia sana moyoni. Lilikuwa ni jambo lenye uajabu kiasi kwa sababu hakuna mtu mwingine hapo aliyejua kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa wawili hawa isipokuwa Emilia na Fred pekee. Dylan alimsalimu vizuri tu binti huyo, wala hakuonyesha kuwa na kinyongo, kwa sababu wakati huu mambo mengi yalikuwa yamebadilika.

Shani, Emilia pamoja na Leila walipika chakula kizuri sana, na wote wakafurahia mlo wa pamoja. Waliongelea mambo mengi yenye kufurahisha na kubaki wakiwa wamechangamka sana. Dylan alikaa hapo mpaka jioni, kisha akatoka na Baraka kuzungumza naye kibinafsi. Alimwambia ukweli wote kuhusu maisha yake, na kwamba ni Grace ndiye aliyemsaidia kujua yeye ni nani kihalisi. Kwa kuwa alimwamini sana Baraka, alimweleza pia kwamba Grace alikuwa na ujauzito wake, na mwanaume huyo akafurahi na kumpongeza sana. Dylan hakuwa na ujuzi wa mambo mengi ilipohusu kuwa mzazi, hivyo Baraka akampatia ushauri mwingi sana.

Ilipofika saa mbili usiku, Dylan akawaaga wote an kuwaambia jinsi alivyofurahi sana kuwa pamoja nao wakati huu. Akawaahidi kwamba wangeonana tena, nao wakamsindikiza kufikia gari lake na kisha akaondoka eneo hilo. Roho ilimuuma sana Leila kwa kuwa hakupata nafasi aliyopangia kuweza kuongea na Dylan kwa faragha. Alijua ndiyo alikuwa amempoteza jumla, na hakukuwa na mtu yeyote wa kulaumu kwa hilo isipokuwa yeye mwenyewe.


β˜…β˜…β˜…


Gilbert na Jaquelin walianza safari saa 3 asubuhi kuelekea mkoa ambao wangekutana na "Smith" kwa mara ya kwanza. Walikuwa wameelekezwa kufika kwenye hoteli fulani na kuegesha hapo, kisha kusubiria ndani ya gari lao. Walifika huko kwenye mida ya saa 7 mchana na kuelekea mpaka nje ya hoteli hiyo; ambayo ilikuwa kubwa na ya kifahari sana. Gilbert akampigia mwakilishi wa boss wake kumjulisha kwamba alikuwa amefika, naye akaambiwa asubiri kwa dakika chache. Jaquelin alikuwa na wasiwasi uliotokana na hamu kubwa ya matarajio yake mengi mno, hivyo Gilbert akamtuliza kwa kumwambia wasubiri kuona nini kingefuata.

Baada ya dakika chache, lilifika gari jeusi aina ya Noah new model lililong'aa sana na kusimama hapo, kisha Gilbert akapigiwa simu tena na kuambiwa kwamba aende humo ili apelekwe kwa boss mkuu. Mwanaume akatoka pamoja na mke wake kulifata, lakini kwa tahadhari pia maana hali hii ilichanganya kiasi, kisha mlango mrefu wa gari hilo ukajifungua walipoufikia, nao wakaingia ndani. Alikuwepo mwanaume fulani kwenye siti hizo za nyuma, naye akajitambulisha kuwa ndiyo huyo mwakilishi ambaye aliwasiliana na Gilbert muda wote huu. Gilbert alimtambulisha mke wake kwake pia na kusema kwamba alikuja naye ili yeye pia apate kumjua Mr. Smth.

Basi safari ikaanza kuelekea kwa boss mkubwa. Njiani waliongelea vitu vingi kuhusiana na kazi, mwakilishi huyo akiwapongeza wawili hao kwa kazi nzuri waliyokuwa wakiifanya kwenye kampuni yao. Iliwachukua kama dakika 10 hivi kufika nje ya nyumba ya Grace, na kiukweli wenzi hawa walipendezwa SANA na mpangilio, ukubwa, umaridadi wa nyumba hii. Kwa kuwa Gilbert alijua vizuri masuala ya ujenzi, kwa haraka angeweza kutambua kwamba nyumba hii ilikuwa ghali ya juu kupita maelezo, kwa kuwa ilikuwa pana sana iliyojazwa vitu vingi vya gharama; hapo bado hawajaingia ndani.

Gari liliegeshwa, na watatu hawa wakashuka pamoja wakimwacha dereva ndani yake. Mwakilishi huyo akawaongoza wenzi hawa mpaka kwenye mwingilio wa jumba hilo la kifahari, kisha akabonyeza kengele ya mlangoni na kusubiri. Sekunde hazikupita nyingi na mlango huo mpana ukafunguliwa, aliyefungua akiwa ni Matilda. Akawakaribisha vizuri ndani hapo, na wote wakaingia. Jaquelin alistaajabishwa sana na ukuu wa nyumba hii, kwa kuwa vitu vingi hapo vilikuwa vya gharama sana, na vilipangiliwa kwa ustadi mno.

Matilda akawakaribisha waketi kwenye masofa, kisha akawaambia angekwenda kumtaarifu boss wake kuhusu ujio wao. Alipanda ngazi upesi akiwaacha wanasubiri hapo. Mara kwa mara Gilbert na Jaquelin waliangaliana, kama kuulizana ikiwa kweli mwanao ndiye ambaye angekuwa mwenye mambo yote haya, na kama ilikuwa hivyo, swali ni alitoa wapi vitu hivi vyote? Vitu walivyowaza vingejibiwa ndani ya muda mfupi, hivyo kwa uvumilivu wakaendelea kusubiri.

Matilda alirudi chini na kuwataarifu kwamba boss wake anakuja, naye akaenda jikoni na kurudi akiwa na sahani pana ya shaba iliyowekewa glasi tatu zenye juice ya embe na kuwapatia wageni hao. Ukaribishaji-wageni huu ulikuwa mzuri sana, nao wakaanza kunywa juice zao taratibu huku wakimsubiri Mfalme au Malkia wa jumba hili la dhahabu.

"Hivi kweli Dylan anaweza kuwa ndiyo mwenye hii nyumba?"

Jaquelin akamnong'oneza Gilbert hivyo, naye Gilbert akaangalia tu chini kwa mashaka.

"Welcome everyone!"

Wote walinyanyua juu baada ya kusikia sauti hiyo kutokea upande wa ngazi. Waliweza kumwona Grace hapo, mwanamke mrembo na aliyejua kupendeza haswa. Alikuwa anashuka kutokea juu huko akiwa anatabasamu, na mwilini alivalia gauni nyepesi ya rangi ya pink yenye maua-maua iliyoishia magotini na kuufunika mgongo wake kwa nyuma. Mwakilishi wake akasimama kuonyesha heshima, na jambo hilo likafanya wazazi wake Dylan wasimame pia kwa kutambua kuwa huyo ndiye aliyekuwa Malkia wa hapo.

Grace akafika mpaka chini na kuwafuata walipokuwa.

"Good afternoon boss," mwakilishi akamsalimu.

"Afternoon, John," Grace akajibu.

"Good afternoon."

"Good afternoon."

Gilbert na Jaquelin wakamsalimu pia, wakifikiri huenda alikuwa mmarekani mweusi. Grace akaachia tabasamu zuri na kusogea karibu yao.

"Good afternoon. Karibuni sana," akawaambia.

"Oh...kumbe unajua Kiswahili..." Jaquelin akasema.

"Ndiyo najua. Nafurahi sana kukutana nanyi in person. Gilbert.... Jaquelin," Grace akasema huku anawapa wote mkono.

Wazazi wa Dylan walitegemea kukutana na mtu tofauti kabisa, kwamba kama haingekuwa Dylan, basi ingekuwa ni mwanaume mwingine ambaye ndiye Smith Morgan. Lakini huu ndiyo ukawa mwanzo wa utambuzi kwao kujua ni nani hasa waliyekuwa wanashughulika naye. Kuona ametaja majina yao ilimaanisha aliwafahamu vizuri sana, hivyo ilibaki zamu yao kujua yeye ni nani hasa.

"Boss, wacha me nirudi kule factory. Mizigo inaanza shipment, nahitaji kuwepo huko," yule mwakilishi, John, akamwambia Grace.

"Okay. Thanks for everything. Utanipa update basi," Grace akamwambia.

John akakubali, kisha akawaaga na wazazi wa Dylan pia na kuondoka. Gilbert alitambua kwamba watu waliomfanyia kazi mwanamke huyu walimwonyesha heshima yenye staha sana, na hilo lilimaanisha walimpenda. Grace akawaambia waketi ili waweze kuanza mazungumzo yao.

"Kwa mara nyingine tena, karibuni sana," Grace akawaambia.

Wote wakashukuru.

"Naelewa mimi siye ambaye mlitarajia mngekuta hapa, siyo?" akawauliza.

"Ndiyo. Tulitegemea ku...kukutana na Mr. Smith," akajibu Gilbert.

"Well, ni mimi ndiye ambaye nimewaita hapa. Smith alikuwa ni mume wangu," Grace akasema.

"Alikuwa?" Jaquelin akauliza.

"Yeah. He passed away a few years ago (alikufa miaka michache iliyopita)," Grace akasema.

Gilbert na Jaquelin wakaangaliana kimaswali.

"Najua mna maswali mengi, na msijali, nitayajibu yote. Ndiyo sababu mko hapa. Jina langu ni Grace Morgan. Jisikieni kuwa huru kabisa kwenye kanyumba kangu haka."

"Kanyumba? Yaani hili jumba lote unaliita kanyumba!" Jaquelin akasema kimshangao.

Grace akatabasamu.

"Nimefurahi sana kukufahamu Mrs Gra...."

"Oh please, niite tu Grace," Grace akamkatisha Gilbert.

"Sawa....Grace. Ninahitaji kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa mambo yote ambayo umetufanyia...mimi na mke wangu. Tulipitia kipindi kigumu mpaka kuipoteza kampuni, lakini ni kwa sababu ya msaada wako ndiyo tumerejea tena. Shukrani zangu za dhati kwako dada," Gilbert akamwambia.

"Gilbert! Yaani unamwita dada kweli...." Jaquelin akawa anamsahihisha.

"Oh no, haina shida kabisa. Mr. Gilbert tafadhali usiwe formal namna hii, mimi ni mdogo sana kwako. Asante pia kwa shukrani yako na bidii uliyonayo ya kuiinua zaidi kampuni. Ijapokuwa nimenunua shares za kampuni hiyo, bado itaendelea kuwa ya kwako tu. Nilifanya hivyo ili kukusaidia wewe na Jaquelin kutoka kwenye uonevu uliokuwa unawapata," Grace akaeleza.

Wazazi wa Dylan wakawa makini zaidi kuanzia hapo kwa sababu Grace alisema mambo kwa njia iliyoonyesha alijua mambo mengi sana kuhusu maisha yao.

"Nilifurahi sana kujua kwamba hatua ya kwanza uliyochukua baada ya kurudi kwenye kampuni ilikuwa ni kumfukuza Yakobo Bernard. Right on reflex," Grace akamwambia Gilbert.

"Yeah...aam....nilifanya hivyo. Nilifanya hivyo kwa sababu...mwanaume huyo alikuwa ndiye chanzo cha matatizo yetu. Lakini samahani, naomba niulize....kwa nini jambo hilo lilikufurahisha?" Gilbert akauliza.

"Ni kwa sababu hiyo hiyo pia. Mwanaume huyo alinisababishia matatizo mengi kipindi cha nyuma. Ni mtu mbaya sana mwenye roho iliyojaa ukatili na umwagaji wa damu pia," Grace akasema.

Gilbert na Jaquelin wakatazamana kwa hisia, wakitambua kuwa huyu alikuwa ni mtu mwingine aliyeathiriwa na ubaya wa mwanaume yule. Lakini kujua kwamba Mr. Bernard alijihusisha kwenye umwagaji mwingine wa damu kulikuwa jambo lenye kuhangaisha sana.

"Kwa hiyo ulitusaidia vile ili...kumlipizia kisasi?" Jaquelin akauliza.

"Kisasi? Hapana. Bado kisasi changu kumwelekea mpumbavu yule hakijaanza. Kuwasaidia ilikuwa sehemu ya mpango wangu mwingine tu. Naelewa mwana wenu alipatwa na ajali ya helicopter miezi kadhaa nyuma," Grace akasema.

"Ndiyo," Gilbert akajibu.

"Tumekuja kugundua kwamba ilikuwa ni Mr. Bernard ndiye aliyefanya mpango wa kuiangusha ili kumuua mwanangu," Jaquelin akasema.

"Mlijuaje hilo?" Grace akauliza.

"Siku hiyo kabla Dylan hajaondoka, rafiki yake alimsikia Bernard kwa simu akiongea na mtu fulani akimwambia ahakikishe mpango wao unafaulu...mpango ambao ungemwangusha Gilbert. Kwa sababu hakuelewa vizuri kilichosemwa alishindwa kutuonya mapema, ndiyo akaja kutuambia baadae....ajali ilipokuwa imeshatokea," Jaquelin akaeleza kwa huzuni.

"Pole Jaquelin. Poleni nyote kwa kila jambo lililowakuta," Grace akasema.

Wote wakashukuru.

"Nimekuwa hesitant kushughulika na Bernard moja kwa moja kwa sababu kuna mtu fulani anayemsaidia kufanya mambo haya. Nimefanikiwa kuangusha mambo mengi illegal aliyokuwa anafanya lakini mtu huyo amemsafishia jina lake ili aendelee kuwa huru. Mnapaswa kutambua kuwa adui yenu siyo Bernard pekee; kuna mtu mwingine nyuma yake," Grace akawataarifu.

Wawili hao waliyaona maneno ya Grace kuwa hakika na ya kweli kabisa. Hawakujua ni nani mwingine aliyekuwa adui yao, hivyo walilichukulia jambo hilo kwa uzito sana.

"Anaweza akawa ni nani huyo?" Jaquelin akauliza.

"Haijafahamika bado," Grace akawaambia.

"Mr. Bernard alikuwa anajihusisha na biashara nyingine haramu?" Gilbert akauliza.

"Ndiyo. Kuanzia vandalism, madawa ya kulevya, fencing, human trafficking, yote alikuwa anahusika nayo," Grace akasema.

"Human trafficking?!" Jaquelin akashangaa.

"Yeah. Unaweza ukawasha tu TV yako ukakuta ITV wanatangaza sijui fulani wa fulani kapotea kwa muda mrefu sana bila kupatikana. Baadhi ya watu hao huwa wanashikwa na kuuzwa kwa wengine kisiri sana, na Bernard ni mmoja wa wauzaji hao," Grace akawaambia.

"Oh my God!" Jaquelin akasema kwa mshangao.

"Lakini nilifanikiwa kuzimisha operation zake hizo. Kwa hiyo sasa kinachobaki ni kumfunua mtu huyo mwingine anayejificha kama kobe," Grace akasema.

"Kwa nini tusiwaambie polisi kuhusu hili?" Gilbert akauliza.

"Polisi ni washamba Gilbert. Wataanza kuingiza na masera yao na kutuchanganyia tu habari," Jaquelin akamwambia.

Grace akatabasamu, kisha akasema, "Uko sahihi Jaquelin. Police watataka kujua mengi na mambo hayo kwa kiasi kikubwa yataturudisha nyuma. Juzi hapo, Bernard, pamoja na mwenziye inaonekana, wamemuua mwanaume fulani aliyekuwa akitusaidia kupata ukweli muhimu juu ya kilichompata Dylan..."

Wazazi wa Dylan wote wakashtuka.

"Yeah. Kwa hiyo nimewaita hapa ili kuwaandaa vizuri kwa ajili ya mpango WETU wa kuwafichua watu hawa na kuhakikisha tunawakalisha chini ipasavyo," Grace akasema.

"Mpango wenu? Wewe na nani?" Gilbert akauliza.

Grace akageukia upande wa ngazi zile alizoshuka nazo kutokea chumbani, nao wazazi wa Dylan wakaangalia huko pia. Macho yaliwatoka kwa mshangao mkubwa sana baada ya kumwona Dylan akiwa amesimama hapo huku akiwatazama!



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Jaquelin akanyanyuka polepole akiwa amepigwa na butwaa zito. Gilbert pia akanyanyuka akiwa anashangaa kumwona Dylan hapo. Pumzi za Jaquelin zilianza kupanda, na machozi yakaanza kumtoka akiwa kwenye furaha nzito iliyobebwa na huzuni kubwa aliyokuwa nayo kipindi chote alichofikiri mwanae alikufa.

"Dylan.... D...Dylan...."

Akawa anasema kwa sauti tetemeshi huku akipiga hatua chache kumwelekea mwana wake. Dylan pia akaanza kutembea taratibu kumfata mama yake, akiwa na uso wa kawaida tu ulioonyesha uelewa mwingi wa hisia za wazazi wake. Jaquelin alimfikia karibu, naye akaanza kumshika mwilini huku viganja vyake vikitetemeka kwa msisimko mkubwa sana, naye Dylan akawa anamwangalia kwa hisia pia.

Gilbert alikuwa amesimama pale pale akishangaa, naye akamwangalia Grace kimaswali sana kwa sababu jambo hili lilikuwa kuu kupita maelezo. Grace akamtikisia kichwa taratibu kumhakikishia kwamba mambo ndivyo yalivyokuwa, naye Gilbert akaanza kuwafata Jaquelin na Dylan pia.

Jaquelin alikuwa ameanza kuushika uso wa Dylan huku analia kwa furaha sana, kisha akamkumbatia kwa upendo huku anaita jina lake mara nyingi. Dylan hakusema lolote lile, zaidi alipokea kumbatio la mama yake na kumbembeleza kwa kuusugua mgongo wake kwa wororo. Alilia sana Jaquelin. Kuona jinsi alivyokuwa analia kulimfanya Grace adondoshe machozi pia, hivyo akajifuta haraka na kuutafuta utulivu wa kihisia.

Gilbert alifika nyuma ya Jaquelin na kuushika mgongo wake, hivyo Jaquelin akamwachia Dylan taratibu huku akiwa bado karibu naye. Dylan akamwangalia baba yake usoni, akitambua kwamba uso huu aliujua, lakini bado ikawa ngumu sana kwake kumkumbuka kwa asilimia zote. Gilbert akamshika Dylan begani, huku naye akitokwa na machozi kiasi, kisha akawakumbatia wawili hao kwa pamoja. Ilikuwa ni muungano wa familia yao ndogo wenye kugusa hisia sana.

Waliendelea kukumbatiana kwa dakika chache, kisha wote wakaanza kuelekea kwenye masofa tena. Waliketi pamoja, Jaquelin akiwa karibu kabisa na Dylan, na Gilbert akiwa pembeni yake Jaquelin. Grace alikuwa ameketi kwenye sofa la upande mwingine akiwatazama kwa hisia.

"Dylan jamani....yaani eeh....nimeku-miss sana mwanangu..." Jaquelin akasema huku analia.

Dylan akaanza kumfuta machozi huku anamwangalia kwa upendo, kisha akamlaza kifuani kwake kwa njia ya kukumbatia. Grace akatazama upande mwingine na kumwona Matilda akiwa amesimama huko huku akijifuta machozi. Grace akampa tabasamu la mbali, naye Matilda akatabasamu pia na kurudi kwenye kazi zake.

Jaquelin akakaa sawa tena na kumwangalia mwanae usoni.

"Nini kilitokea? Eeh? Sisi wote tulifikiri ume...." Jaquelin akaishia hivyo.

"Kwamba nilikufa? Ndiyo. Kwa watu wengi nimekufa. Lakini baada ya ile ajali... zilipita tu siku nne Yesu akaniita nirudi tena," Dylan akatania.

Grace akashindwa kujizuia na kucheka kidogo. Jaquelin akakunja uso kimaswali, huku Gilbert akielewa kwamba Dylan alitania tu.

"Yesu? Yesu gani? Alikuita kutoka wapi?" Jaquelin akauliza.

Swali lake lilimfanya Gilbert atabasamu pia.

"Aam...ni...kitu fulani kiko kwenye Biblia kwa hiyo... anatania tu," Grace akamwambia Jaquelin.

"Nini?" Jaquelin akawa haelewi.

"Hiyo inaonyesha hujawahi kusoma Biblia," Gilbert akamtania.

Dylan na Grace wakachekea kwa chini. Dylan alikuwa anamtazama sana mama yake kwa upendo.

"Yaani... pamoja na haya yote yaliyotokea bado hujaacha kuwa mtundu tu!" Jaquelin akamwambia Dylan.

"Kumbe me... ni mtundu?" Dylan akauliza.

Jaquelin akatikisa kichwa na kutabasamu kwa kuhisi furaha sana.

"Nilijua tu tutakuona tena. Nilikuwa nina uhakika kabisa kwamba ni wewe ndiye uliyekuwa unatusaidia," Jaquelin akasema.

"Kweli? Lakini umesema mlifikiri nimekufa... ungewezaje kuwa na uhakika tena kwamba niko hai?" Dylan akauliza.

"Fetty alikuona siku moja... sijui wapi huko... ndiyo akaja kutuambia," Jaquelin akamwambia.

"Fetty?" Dylan akauliza kiudadisi.

"Ndiyo," Jaquelin akajibu.

"Anasema alikuona, na wewe ukamwangalia kabisa lakini kuna mtu mwingine... labda rafiki yako, akakuvuta mkaondoka sehemu hiyo. Kwa hiyo akakukosa," Gilbert akamwambia.

Dylan hangeweza kujua waliyekuwa wananwongelea ni nani, lakini jambo hili alilikumbuka kwa ufupi. Siku ile alipomfumania Leila na mwanaume mwingine, alikwenda kwenye 'club' moja hivi, na hapo akamwona mwanamke ambaye alimtazama sana kabla ya Sarah kumvuta ili waondoke eneo hilo. Sasa akawa ametambua kuwa mwanamke huyo alimfahamu, lakini bado yeye hakuweza kumkumbuka. Jaquelin akaona ni kama Dylan amezama kwenye fikira za jambo fulani, hivyo akamshika usoni kwa upendo ili watazamane.

"Dylan....ni nini kilitokea mwanangu? Hiyo ajali... walipata miili mitatu iliyounguzwa vibaya baada ya helicopter kulipuka... tukafikiri ilikuwa ni mwili wako pia kwa sababu siku hiyo mliondoka watatu. Ulipona vipi?" Gilbert akauliza.

Dylan akamtazama Grace, akimpa kiashirio cha kuuliza kitu fulani, kisha Grace akamtikisia kichwa mara moja kama kumwambia aendelee. Dylan akawageukia wazazi wake tena.

"Mama, baba, kuna mambo mengi yametokea baada ya hiyo ajali kunipata, lakini... mambo mengi ya kabla siyakumbuki," Dylan akasema.

Wazazi wake wakamtazama kwa umakini sana.

"Unamaanisha nini?" Jaquelin akauliza.

"Niliangukia kwenye maji... nika..piga kichwa kwenye jiwe kwa hiyo... nikapoteza kumbukumbu," Dylan akasema.

Wazazi wake walifadhaika sana. Jaquelin akaanza kulengwa na machozi.

"Mama... usilie. Cha muhimu ni kwamba niko hai. Kumbukumbu itarejea tu polepole," akawahakikishia.

"Kwa hiyo Dylan... unataka kusema kwamba hata na sisi hautukumbuki?" Gilbert akauliza.

Dylan akaangalia chini na kutikisa kichwa taratibu kukubali.

Jaquelin akaziba mdomo wake kwa huzuni.

"Hata ijapokuwa hakumbuki mengi, la muhimu ni kwamba ANAJUA nyie ni wazazi wake, na mambo yote atakayohitaji kujua kuhusu maisha yake ya awali, basi you guys will fill him in," Grace akasema.

Dylan akaanza kuzilaza-laza nywele za mama yake kwa upendo.

"Mambo mengi niliyofundishwa naweza kuyakumbuka... na wakati mwingine huwa yanakuja tu kichwani bila me kujaribu sana kuyatafuta. Lakini inapokuja kwenye suala la watu na vitu nilivyofanya kabla ya ajali... bado memory inasua," Dylan akaeleza.

"Pole sana Dylan," Gilbert akamwambia.

"Kwa hiyo... Grace ndiyo alikusaidia mpaka ukafika huku?" Jaquelin akamuuliza.

"Mwanzoni, kuna mwanaume fulani ndiyo alinisaidia. Alinitoa nilipozama kwenye bwawa la huko kwao na kunipeleka kutibiwa. Ni mwanaume mmoja nayemwona kama baraka kubwa sana kwangu... na jina lake ni Baraka pia," akasema Dylan.

"Okay..." akasema Jaquelin.

"Ndiyo kwa hiyo... nilikaa kwake kwa miezi kadhaa ndipo Grace akaja na kunichukua. Aliniweka wazi kuhusu mambo yote ambayo sikuwa nafahamu, na akanisaidia sana kwa kunipa hifadhi ili kunilinda maana sikujua kwamba kulikuwa na hatari nikijiachia sana," Dylan akasema.

Wazazi wake wakaanza kumshukuru sana Grace. Mwanamke akawaambia wasijali, na kitu cha muhimu wakati huu ingekuwa ni kuupeleka mpango wao kwenye mwendo ili kuwanasa kisawasawa wabaya wao.

"Kwa hiyo sasa... tunatakiwa tufanye nini kuhusu Mr. Bernard?" Gilbert akauliza.

"Nina mpelelezi wangu maalumu ambaye huwa anafuatilia mambo haya kwa ukaribu. Tokea kifo cha mwanaume huyo niliyewaambia, inaonekana ni kama Mr. Bernard anajificha kwa kuwa hata kwenye nyumba yake hakanyagi, na sababu inaweza ikawa kwamba tayari anajua Dylan yuko hai, hivyo huenda anaogopa kwamba Dylan anaweza kumfanya kitu fulani kibaya," Grace akawaelezea.

"Yaani huyo mwanaume ana roho mbaya! Haitoshi kwamba anauza hadi binadamu, lakini mpaka kuua anaua!" Jaquelin akasema kwa mkazo.

"Kilichopo wakati huu ni kumtoa huko anakojificha, kumkamata, na kumfanya aseme ni nani anayeshirikiana naye kumpa kichwa kwenye maovu yao," akasema Grace.

"Okay sawa. Ni njia gani tutakayotumia ili kumvuta?" Gilbert akauliza.

"Mimi," Dylan akasema.

Wazazi wake wakamtazama kwa makini.

"Nimepanga pamoja na Grace kwamba nitajitokeza upya kwa watu wote wanaofikiri nilikufa, nami nitaweka wazi kwamba tukio lililonipata halikuwa ajali, bali lilipangwa kimakusudi na mtu fulani. Ninajua nitamvuta Mr. Bernard au msaidizi wake kwa sababu watahofia kama nitawasema basi wamekwisha. Wakati huo huo, tutakuwa tumeweka watu wetu special ambao watakuwa makini kutambua nyendo zozote zile zenye hila, na hapo tutawadaka watu hao," Dylan akaeleza.

"Dylan subiri... mbona naona kama hiyo ni hatari? Je kama... je waki...wakiweka sniper labda akufyatue kwa mbali... itakuwaje? Mimi sitaki kukupoteza tena Dylan!" Jaquelin akasema kwa wasiwasi.

Dylan akamshika mama yake usoni.

"Usijali mama. Kila kitu ulichosema ni kati ya mambo mengi ambayo tumeshafikiria. Kila kitu tumeandaa vizuri tayari, kwa hiyo nakuhakikishia hakuna kitu kibaya kitakachonipata tena. Mbaya wetu mwingine anaweza kuwa mtu yeyote yule, huenda hata rafiki wa karibu au adui wa zamani, kwa hiyo ninahitaji ushirikiano wenu kwa mambo yote tutakayowaambia ili kuweza kufanikiwa katika hili," Dylan akasema kwa utulivu.

Wazazi wake wakakubaliana na hilo, na watatu hawa wakakumbatiana tena kwa faraja.

Baada ya hapo, Dylan pamoja na Grace walianza kuwapanga wenzi hawa kuhusiana na mpango wao ambao ulikuwa mwepesi tu. Kikubwa katika haya yote kilikuwa ni rejeo la Dylan tena, kutoka kwa wafu, jambo ambalo ndiyo walitaka kulitumia vizuri kwa ajili ya faida yao.

Muda mfupi kutokea hapo Matilda akawa amemaliza kuandaa meza kwa ajili ya chakula, na wote wakaenda hapo ili kupata msosi pamoja. Dylan kuketi katikati ya wazazi wake kuliwapa faraja sana, nao wakawa wakila huku wakiongelea mambo mbalimbali kuhusu maisha ya mwanao. Dylan alipata kujua kwamba aliishi Brazil kwa miaka zaidi ya 10, na alifungua mgahawa mzuri sana wa kisasa ambao uliendelea kukua hata wakati alipopotea.

Dylan pia aliwasimulia kuhusu jinsi alivyowasaidia watu wa kule kwao Baraka kutengeneza daraja, jinsi alivyomdunda mtu mmoja ambaye alimfanyia fujo mtoto wa Baraka, na mambo mengine tokea alipoanza kufanya kazi kwenye kampuni ya Grace. Kwa kadiri fulani ilikuwa kama ndoto vile kwa wazazi wake, lakini ilikuwa ni ukweli mtupu kwamba mwana wao alikuwa hai muda wote huo.

Walipomaliza kula waliketi tena kwenye masofa yale kuongelea tena kuhusiana na mambo ambayo wangefanya kuanzia wakati ambao Dylan angerudi nyumbani. Grace aliwasihi sana kutomwambia YEYOTE yule kuhusu haya, hata kama ingekuwa ni rafiki wa karibu, mpaka wakati ambao mpango wao ungeanza kazi. Grace aliwaambia wangewasiliana tena, lakini kwa tahadhari ili kuepusha ufatiliwaji wowote, kama walivyofanya leo.

Ilifika mpaka mida ya saa 1 jioni wakiwa bado hapo, hivyo wakaagana na mwanao ili waweze kurudi nyumbani; ijapokuwa Jaquelin alitaka sana kubaki ili kuwa na mwanae zaidi, lakini walitakiwa kuwa waangalifu ili kutowapa maadui njia ya kuwafikia mapema kiurahisi maana hakuna ajuaye, huenda hata walikuwa wameanza kufatiliwa.

Dylan na Grace wakawasindikiza mpaka nje, na wenzi hao wakaingia kwenye Noah ile tena ili kurudishwa kule walikoacha gari wakiwa na furaha kubwa sana moyoni. Wazazi wake walifika kwao kabisa kwenye mida ya saa 5 usiku, wakionekana kama walitoka kwenye fungate vile kwa sababu nyuso zao zilikuwa na shauku iliyojaa sana. Walitazamia kwa hamu kubwa kumwona mwanao tena, hivyo wangesubiri mawasiliano kutoka kwake ili awapange juu ya mambo ambayo wangefanya siku za hivi karibuni.

Mida hiyo hiyo, Dylan na Grace walikuwa chumbani wakiongea kuhusu jinsi mkutano huu na wazazi wake ulivyokuwa. Dylan alieleza jinsi ambavyo, ijapokuwa hakuweza kuwakumbuka vizuri, lakini aliguswa sana moyoni kuona kwamba wazazi wake walikuwa pamoja kipindi chote kile kigumu ambacho walipitia. Akamwahidi Grace kufanya kila kitu ili kuwapatia wote haki, yaani wazazi wake na yeye Grace.

"Ungependa tuwaambie wakati gani?" Dylan akamuuliza Grace.

"Mmmm... ingependeza kama tungewaambia mambo yakitulia zaidi, lakini kama bado haitakuwa hivyo basi tutawaambia mapema tu," Grace akasema.

"Najua watafurahi sana."

"Kujua kwamba watakuwa babu na bibi?"

"Ahahahah... ndiyo."

"Mhm... mama yako anaonekana kupenda sana urembo. Haitakuwa rahisi kum-convince kwamba ameanza kuzeeka," Grace akatania.

"Ahahahah... Uzee huja tu. Ila... pamoja na mambo mabaya yanayotuzunguka, najua hii itakuwa sababu nzuri sana ya kuwa na shangwe. Wakijua watapata mjukuu watafurahi sana maana watapata kaDylan kengine ka kucheza nako," Dylan akasema.

"Mm? Hamna bwana. Katakuwa kaGrace haka," Grace akasema.

"Hamna... hako ni kajembe kama mimi mzee wake."

"Nakwambia ni kaGrace haka, usibishe."

"Unajuaje?"

"Ninajua tu. I can feel it," Grace akasema huku analishika tumbo lake.

Dylan akatabasamu kwa furaha, kisha akambusu Grace mdomoni.

Grace alipandwa na hisia nyingi ghafla zilizosababisha msisimko wa hali ya juu ambao hakuwa ameutarajia, naye akaiendeleza busu ya Dylan na kuigeuza kuwa denda ya kimahaba sana. Kadiri walivyoendelea Dylan akawa ametambua kuwa mwanamke huyu alitaka mambo mengi zaidi ya busu. Grace akaendelea kumpiga denda huku anatoa miguno ndani ya mdomo wake kwa huba nzito.

Moja ikawa mbili mpaka tatu na Dylan akakishusha kigauni chake chepesi na kuanza kuyanyonya matiti yake yaliyosimama kwa hamu. Kufikia wakati huu angalau Grace alijua jinsi ya kuonyesha hulka ya kimapenzi baada ya kumzoea zaidi Dylan, hivyo naye akawa analivuta T-shirt lake ili amvulishe. Mwanaume akatii na kumruhusu afanye hivyo, kisha naye akamnyanyua na kumweka katikati ya kitanda kwa kumlaza. (.......).

(........).

(........).

(........). Hii ilikuwa ni njia nzuri ya kuondoa mikazo kwa wawili hawa, kwa sababu nao walihitaji muda wa kuonyeshana upendo na kuondoa misongo kiasi.

Baada ya kama saa zima la mechi hiyo, wawili hawa waliridhiana bila kusukumwa, kwa raha zao, na kisha wakalala pamoja kuweza kujipumzisha.


β˜…β˜…β˜…


Usiku huo huo, Beatrice, akiwa kwake chumbani, alipigiwa simu na Mr. Bernard. Akaipokea ili amsikilize mwanaume huyo.

"Nini kinaendelea? Umempata?" Mr. Bernard akauliza.

"Nani, Alikiba au?" Beatrice akauliza kwa kejeli.

"Dylan bwana! Acha mambo yako Beatrice," Mr. Bernard akasema.

"Ningekuwa nimempata ungekuwa umeshajua. Acha kunisumbua usiku usiku bwana."

"Sasa tunafanyaje?"

"Tunafanyaje nini?"

"Usichukulie hili kirahisi Beatrice. Huyo kijana anaweza kuwa popote pale na anaweza kutuzingua muda wowote ule."

"Mmmm ndiyo maana umeenda kuficha tako lako huko eeh? Na ujanja wote ukakimbia na kujificha, hiyo ndiyo itakusaidia kumpata?"

"Lakini si tuli..."

"Usiniambie hayo masuala Bernard. Unatarajia nimtafute, nimpate, nimuue, wewe umekaa tu? Usitegemee mimi nitaendelea kukuficha maisha yako yote kondoo wewe! Act like a man not like a bitch that you are!"

"Aaaa Beatrice... mambo gani tena hayo kupeana kashifa? Eeh...mimi pia namtumia kijana wangu afatilie mambo kwa ukaribu," Mr. Bernard akasema.

"Umepata chochote?" Beatrice akauliza.

"Alifanikiwa kupachika tracking device kwenye gari za Gilbert na Jaquelin..."

"Keep talking..."

"Leo kaniambia kwamba gari la Gilbert lilienda nje ya mkoa kufikia kwenye hoteli fulani halafu likasimama hapo," Mr. Bernard akamwambia.

Beatrice alikuwa amekaa kitandani, lakini baada ya Mr. Bernard kumpa taarifa hiyo akasimama chini na kuweka umakini zaidi.

"Alienda kufanya nini kwenye hiyo hoteli?" Beatrice akauliza.

"Sijajua sasa..."

"Aagh c'mon Bernard, what the f(..)k?! Yaani umeshindwa kujua nini kilichoendelea huko? Je kama ile ndiyo sehemu ya kukutana na Dylan?" Beatrice akauliza kwa mkazo.

"Kama ni hivyo basi natakiwa kumweka kijana wangu huko ili akimwona tu Dylan ammalize," Mr. Bernard akasema.

"Kwa nini hukuniambia mapema kuhusu hili? Afu' unaanza maswali ya ooh umempata Dylan, ulikuwa unataka nini sasa?"

"Beatrice usiwe mkali. We ndiyo Malaika wangu, nakutegemea kwa sababu umenisaidia sana. Nilikuwa nataka kuhakikisha tu ikiwa nawe umepata kitu, siyo kwamba mimi kujihami inamaanisha nimejificha kazi bure. Nitalifanyia kazi hilo usihofu. Nami najua wewe pia unafatilia huko," Mr. Bernard akasema.

"Ndiyo fanya hivyo. Mtu wako huyo akae nje ya hiyo hoteli hata kama ni masaa 24 asubirie na kuwa makini kutambua ikiwa huyo mpumbavu atakuwepo. Mpe maagizo mapema ili akimwona tu asibakize bullet yoyote kwenye bastola yake! Zote zimwishie mwilini, sijui unanielewa?"

"Ndiyo inaeleweka. Lakini Beatrice, ninahitaji pesa nyingine tena kwa ajili ya..."

Beatrice akazungusha macho yake kwa kukerwa na kusema, "Yaani wewe kila saa ni pesa tu! Za kwako umezipeleka wapi? Hivi unajua ni mambo gani amba....."

"Mommy?"

Sauti hiyo kutokea nyuma yake Beatrice ilimshtua SANA. Akaacha kuzungumza akiwa ameganda hivyo hivyo, kisha akageuka taratibu na kukuta ni Harleen akiwa amesimama mlangoni kwake. Alikuwa anamtazama kwa njia iliyoonyesha maswali mengi sana.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
DYLAN

Story by Elton Tonny

Familia, Kazi, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Unyanyasaji, Usaliti, Visasi, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

(R-rated 18+)

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA THELATHINI NA SITA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Beatrice akashusha simu kutoka sikioni mwake huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi. Alijiuliza Harleen alikuwa amesimama pale kwa muda gani, na kama ulikuwa mrefu basi alisikia kila jambo ambalo alisema.

"Ulikuwa unaongea na nani?" Harleen akauliza.

Beatrice akatoa tabasamu la bandia kuonyesha mambo yalikuwa sawa.

"Nilikuwa naongea na mtu fulani tu. Vipi, mbona bado hujalala?" Beatrice akasema.

"Nilienda kunywa maji," Harleen akasema huku akiwa ameweka uso wa kimaswali.

Beatrice akamfata mlangoni hapo akiwa anatabasamu kwa wasiwasi.

"Umekuja hapa zamani?" akamuuliza.

"Ndo' nimekuja sa'hivi, nimesikia unafoka nikajiuliza unamfokea nani?" Harleen akajibu.

"Ah... ni bwege mmoja tu ananisumbua tu usiku usiku. Usijali wala, we nenda tu ukalale baby," Beatrice akamwambia huku anazilaza-laza nywele za bintiye.

Harleen akageuka na kuondoka kuelekea chumbani kwake.

Beatrice akashusha pumzi ya ahueni na kuufunga mlango. Akamwandikia Mr. Bernard ujumbe mrefu kumwambia jinsi anavyotakiwa kushughulika na mambo yote haya na kwamba pesa angemtumia pia. Kisha baada ya hapo akaenda kitandani kulala.


β˜…β˜…β˜…


Siku iliyofuata, Dylan aliwajulisha wazazi wake kuwa angetoka alikokuwa na kwenda nyumbani kwao kwa mara ya kwanza tokea alipopotea na ajali ile iliyowafanya wengi wafikiri amekufa. Bado aliwaambia wasiseme kwa yeyote kwanza kuwa anarudi, hivyo walijiandaa kumpokea kwa kuwa waangalifu kutomwambia yeyote kuhusu ujio wake.

Jaquelin hakwenda kazini siku hiyo; alibaki nyumbani kutayarisha chakula na vitu ambavyo mwana wake angehitaji kutumia atakapofika. Gilbert alikwenda kwenye kampuni kama kawaida, akiwa pia anajua kwamba Dylan anarudi. Alipomuuliza ikiwa angepakumbuka, Dylan alimwambia alikuwa akija kwa kufata ramani ya kitaalamu (GPS) ya kwenye gari, hivyo ingemleta mpaka kwenye nyumba aliyojua ilikuwa ya wazazi wake.

Ilipofika mida ya saa 8 mchana, Dylan akawa amefika nyumbani kwao kwa mara nyingine tena. Kwa kuangalia mazingira ya hapo alitambua kwamba vitu vingi havikuwa vigeni sana machoni pake ijapokuwa hakuweza kukumbuka mambo mengi vizuri. Baada ya kufunguliwa geti, kuingiza gari ndani na kushuka, alipokelewa kwa furaha sana na Jaquelin ambaye alimkumbatia kwa upendo.

Wawili hao wakaingia ndani ya nyumba pamoja, naye Jaquelin akaanza kumwonyesha vitu vingi vya hapo na kumkumbusha mambo mengi ambayo aliwahi kufanya akiwa nyumbani. Dylan alifurahi kuijua historia yake kwa kiasi fulani, kwa kuwa mambo mengi ambayo hakukumbuka yalionekana kuwa mambo yaliyompa furaha kipindi hicho. Msaidizi wa kazi wa hapo alishangaa sana baada ya kumwona mtoto wa boss akiwa hai, naye Jaquelin akamwambia kwa ufupi kuwa alipona kwenye ile ajali. Gilbert alifika nyumbani pia baada ya muda mfupi, naye akamkaribisha mwana wake kwa furaha kubwa. Wakapata mlo pamoja, kisha wakaelekea kwenye ofisi ndogo ya baba yake ya hapo ili wazungumzie mpango wao.

Dylan aliwaeleza kwamba, walitakiwa kufanya mpango wa party, ambayo wangealika ndugu, marafiki, wafanyakazi wa kampuni na wengine waliojuana nao ili kusherehekea jambo fulani muhimu sana. Aliwaambia kwamba Grace alikuwa tayari ameanza kushughulikia suala la mialiko, na ilikuwa ni juu ya wazazi wake kuamua ni nani wangealikwa kwa sababu wenyewe ndiyo waliojua watu wengi wa huku vizuri sana.

Alitaka party hii iwe yenye uhuru sana, na jambo kuu kuhusu party hii lingekuwa ule wakati ambao wazazi wake wangewatangazia watu wote kwamba mwana wao hakufa kwenye ile ajali, bali alipona na alikuwa mzima. Na hapo hapo ndipo Dylan angejitokeza sasa na kuanza kuwaambia watu kile kilichotokea haswa. Alisema ilikuwa ni lazima wahakikishe taarifa za sherehe hiyo zinamfikia Mr. Bernard.

Gilbert na Jaquelin waliuliza ikiwa kufanya hivyo kungekuwa salama, naye Dylan akawaeleza kuwa anajua huenda mbaya wake akawa eneo hilo, lakini kwa kumfanya afikiri kwamba amejiachia tu ndiyo itakuwa rahisi kumnasa kwa sababu Dylan atakuwa ameweka watu maalum wa kuangalia nyendo zozote zile za hila. Akawahakikishia kabisa wazazi wake kuwa wasiwe na wasiwasi kwa sababu kila jambo walikuwa wamelipangilia kwa umakini sana, hivyo suala hili la party lilipaswa kushughulikiwa upesi.

Basi baada ya hayo Dylan akawa amewapa tarehe ambayo walitakiwa kufanya party hiyo, nayo ingekuwa ni ndani ya siku saba. Muda huo ungetosha kuwafikishia taarifa wabaya wao, kwa kuwa kwa sasa walijua Dylan yuko hai, hivyo ni wazi wangeweza kuwa na hamu ya kutaka kujua ni nini hasa kilichokuwa cha muhimu kwa sherehe hii wakikisia Dylan angehusika hapo.

Jaquelin akamwomba mwanae alale hapo siku hiyo, lakini Dylan akasema alihitaji kurejea kule jijini kwao hasa kwa kuwa walitakiwa kuwa waangalifu. Akamwahidi mama yake kwamba haingechukua muda mrefu nao wangeungana kama familia tena; kwanza wamalize ishu hii muhimu. Jaquelin akaridhia na kumkumbatia kwa dhati kubwa sana mwanae, naye Gilbert akafanya hivyo hivyo pia. Kijana akatoka zake hapo kwao huku wazazi wake wakiwa wanamsindikiza kwa macho mpaka geti lilipofungwa, kisha wakarejea ndani tena.

Dylan aliingia barabarani na kuanza kuelekea kule alikoishi na Grace. Mwendo ungekuwa ni mrefu sana lakini ilihitajika afanye hivi kwa ajili ya kuwa mwangalifu na mipango yao. Alifika maeneo fulani na kutambua kwamba mafuta kwenye gari lake yalikuwa yamekaribia kuisha, hivyo akatafuta kwa ramani yake kuona ikiwa kulikuwa na kituo cha kuwekea gari mafuta pande za karibu na hapo. Baada ya kupata kimoja, akaelekea upande huo ili aweke mafuta upesi ili kurejea safarini.

Wakati amefika hapo na kuliegesha gari lake liwekewe bomba la mafuta, kishindo kilisikika kutokea nyuma ya gari lake kilichofanya litikisike kwa nguvu. Alipoangalia kupitia kioo cha juu, aliona gari lingine nyuma yake likiwa linarudi nyuma. Akatambua kwamba lilikuwa limegonga kidogo sehemu ya nyuma ya gari lake. Akatikisa kichwa kwa kusikitika maana kihalisi gari hii haikuwa YA KWAKE kabisa, bali ya Grace, hivyo alijihisi vibaya kwamba amesababisha litiwe jeraha 😁.

Kupitia kioo hicho hicho aliweza kumwona dereva wa gari hilo akishuka na kuonekana kama anarushiwa maneno na mhudumu wa kituo hicho cha mafuta, kwa sababu uzembe wake ulisababisha agonge gari ya mtu mwingine. Dylan akashuka ili aende kuangalia sehemu ambayo iliharibiwa na ajali hiyo ndogo. Alipofika nyuma ya gari akakuta taa moja imepasuka na sehemu ya chini kukunjika kiasi.

"....haraka ya nini? Huu ni usiku, na hapa inatakiwa kuwa sehemu salama..." mhudumu akaendelea kufoka.

"...najua, najua. Kama kuna faini natakiwa kutoa, nitalipa. Sikufanya makusudi," mwanaume huyo akasema.

Dylan alikuwa bado analikagua gari lake hivyo hawakuwa wametazamana bado.

"Bro...tusameheane tu mimi...."

Mwanaume huyu alikuwa ameanza kumwambia Dylan hivyo lakini baada ya Dylan kumwangalia akaishia hapo na kutoa macho kimshangao. Dylan alipomwangalia, aliweza kutambua kwamba sura hiyo haikuwa ngeni sana kwake, lakini bado hakukumbuka mtu huyu alikuwa ni nani. Mwanaume huyo akaachama na mdomo wake huku anapiga hatua chache kumfata Dylan akiwa anashangaa. Dylan akakunja uso wake kimaswali.

"D...Dylan!" mwanaume huyo akaita.

Sasa Dylan akagundua kwamba mtu huyu alimfahamu. Akawaza huenda alikuwa anajuana naye wakati bado anaishi huku, lakini kumkumbuka ikawa shida.

"Dylan ni wewe?" mwanaume huyo akauliza tena.

Dylan akatikisa kichwa taratibu kukubali. Mtu huyo akajishika kichwa akiwa haamini.

"Aam... niwekee mafuta ya laki moja tafadhali," Dylan akamwambia mhudumu yule.

Baada ya mhudumu kwenda kufanya alivyoambiwa, Dylan akamwangalia tena mwanaume huyu.

"Dylan... lakini... nilipata... niliambiwa umekufa kwenye ajali! Nini kilitokea bro?" mwanaume huyo akauliza.

Kuona kwamba mtu huyu alimwita "bro" kulimjulisha Dylan kuwa walikuwa ni marafiki. Hivyo, akamsogelea karibu na kumshika begani.

"Mambo ni mengi rafiki yangu, siyo rahisi kueleweka haraka hapa, kwa hiyo unaonaje tukienda sehemu private kidogo ili tuongee?" Dylan akasema.

"Aa... sawa, haina shida. Dah! Aisee mbona kama ndoto vile!" huyo mwanaume akasema.

Baada ya Dylan kuwekewa mafuta kwenye gari lake, alilisogeza mbele kumpa nafasi "rafiki" yake huyo awekewe mafuta pia. Kisha akamwongoza kuelekea mpaka kwenye sehemu ambayo haikuwa na nyumba wala watu ili wakazungumzie huko. Waliegesha tu magari yao na kusimama kwa kuegamia gari la Dylan ili waweze kuongea.

Dylan alianza kumwelezea kuhusu "ajali" ile mpaka aliposaidiwa na Baraka kukiokoka kifo. Alimweleza pia kwamba kutokana na hayo yaliyompata kumbukumbu yake ilipotea, hivyo vitu vingi hakukumbuka. Alijitahidi kutomwambia kuhusu masuala ya Mr. Bernard na adui yake mwingine maana hakuwa na uhakika ikiwa angeweza kumwamini namna hiyo.

"Kwa hiyo kumbe.... unataka kusema kwamba... hata mimi haukumbuki ni nani?" mwanaume huyo akauliza.

Dylan akatikisa kichwa kukubali.

"Aisee!" jamaa akasikitika.

"Ndiyo hivyo bwana. Ni ngumu kwa kiasi fulani lakini memory itarudi tu eventually," Dylan akasema.

"Dah! Pole sana mwanangu. Hayo yote yaliyokukuta yaani, nilihuzunika sa-na. Taarifa za kifo chako zilimchanganya mpaka Queen yaani. Me ni rafiki yako tokea primary, naitwa Bosco," akajitambulisha.

"Bosco?"

"Yeah."

"Kumbe tunajuana tokea zamani eeh?"

"Kitambo sana. Sema we darasa la sita uliondokaga ukaenda....wapi Brazil kule, ila tulionanaga tena mitandaoni tukawa tunachekiana. Kwo' uliporudi tukakutana tena. Tumefanya mishe nyingi sana mwana," Bosco akaeleza.

"Dah! Natamani ningekumbuka hayo yote rafiki yangu."

"Itarudi tu hiyo kumbukumbu kama wewe ulivyorudi kutoka kwa wafu kaka."

Dylan akacheka kidogo.

"Umesema jina Queen... ndiyo nani?" Dylan akauliza.

Bosco alianza kumsimulia jinsi alivyomuunganisha kwenye mtandao ule wa mapambano ya mieleka ambao ulifanywa kwa siri sana. Alimsimulia kuhusu jinsi alivyopendwa sana kwa kuwa alipigana kwa mtindo wa Capoeira na mara zote alizopigana aliibuka mshindi. Hata yeye Bosco alipotishiwa kuumizwa na Queen, Dylan alimsaidia kwa kupigana na watu watatu na kuwashinda wote. Mambo haya yalimshangaza Dylan kwa sababu hangekaa kufikiri hata mara moja kwamba aliwahi kufanya mambo yote hayo.

"Ahahahah... kweli?"

"Usipime! Yaani huyo jamaa ulimchemsha mpaka akalainika alikuwa ana mauzo mengi sana lakini pamoja na kuchoka ukamfumua," Bosco akaendelea kusimulia.

"Ahahahah... umesema alijiita nani?"

"The Crusher! Ye' ndo' akawa crushed."

"Aisee, hiyo kweli noma."

"Yaani Dylan tokea ulipopotea, haya mashindano yamelala sana. Watu walikuwa wanalipa mihela mingi kwa ajili ya Killmonger ila sa'hivi ni kama panaboa sana bila wewe."

"Kuna kipindi kweli nilipigana na mwanaume fulani mhuni hadi nikamvunja mkono. Wakati mwingine nilipokaa nikawaza hilo nilijiuliza niliwezaje kufanya vile yaani," Dylan akasema.

"Mwili wako tayari ulikuwa umeshazoea kupigana zamani ndiyo maana."

"Yeah, inaonekana."

"Kwa hiyo, hapa ulikuwa unaenda wapi?" Bosco akauliza.

Dylan akamwambia ilikuwa ni sehemu alikoishi ambako palikuwa nje ya mkoa.

"Si bora ukalala hotelini, sa'hivi ishakuwa....saa tano sa'hivi, utafika huko saa ngapi? Tena si ungelala tu 'skani kwenu?" Bosco akashauri.

Ni wakati huo ndipo simu ya Dylan ikaanza kuita. Alipoiangalia, akakuta ni Grace ndiye anampigia.

"Grace..." Dylan akasema baada ya kupokea.

"Dylan... uko wapi sasa?" Grace akauliza.

"Aam...niko... niko huku bado, nili...nimepatwa na ajali ndogo kwenye..."

"Ajali! Oh my God, what happened? Are you hurt?!" Grace akaongea kwa hofu.

"Grace calm down, niko sawa. Ni... scratch tu kwenye gari basi. Litahitaji repair kidogo," Dylan akamtuliza.

Bosco akatabasamu akiwa ameshajua ni mtu ampendaye Dylan.

"Nitakwambia kila kitu kesho, inaonekana leo sitarudi maana muda umeenda," Dylan akamwambia Grace.

"Okay. Pole kwa ajali. And be careful, okay?" Grace akasema.

"Usijali. Nifinyie Dylan Jr. hapo, mwambie nampenda sana," Dylan akasema.

"Ahahah... ni Gracious wa pili bwana. Haya zimefika. Baadae," Grace akaaga.

"Okay."

Baada ya kukata simu, Dylan akakuta Bosco anatabasamu kwa njia yenye utundu. Naye pia akatabasamu.

"Nini?" akamuuliza.

"Huyo ni baby mama kama sikosei!" Bosco akasema.

"Ahahah... yeah."

"Nilijua tu, we huwa huchelewi," Bosco akatania.

Dylan akatabasamu na kurudisha simu mfukoni.

"Okay, nimefurahi kukutana nawe Bosco."

"Mimi pia bro."

"Ninakuomba kitu kimoja. Usimwambie YEYOTE kuhusu mimi kuwa hai, YEYOTE YULE."

"Vipi, kuna kitu kinaendelea?"

"Ndiyo. Kuna mambo nafatilia kimya kimya kwa hiyo sitakiwi kujulikana kuwa niko hai. Naweza kukuamini kwenye hilo?"

"Kabisa Dylan, yaani usiwe na shaka. Niachie namba yako halafu nitaku-beep u-save na ya kwangu."

Dylan akafanya hivyo, naye Bosco akam-save "Killmonger."

Baada ya hapo, wawili hawa wakaagana na kila mmoja kuelekea upande tofauti. Dylan alitafuta hoteli moja na kulipia chumba ili apumzike hapo. Akawasiliana na Grace tena na kuongea naye kifupi kuhusu wazazi wake na kukutana kwake na Bosco, kisha baada ya hapo akaingia kulala.


β˜…β˜…β˜…


Siku zilizofuata zilikuwa ni zenye pilika kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya Gilbert na Jaquelin. Waliifanya iwe kama sherehe kwa ajili ya mafanikio ya kampuni, lakini marafiki zao pia walialikwa hapo, ikiwemo Beatrice, Harleen, Fetty, Tony, na wengine. Baba yake Gilbert, ambaye kwa muda mrefu alikuwa nchini Nairobi, alirejea pia baada ya kuitwa na Gilbert kwa kuw kuambiwa jambo hili lilikuwa ni la muhimu sana hivyo alitakiwa kuwepo pia.

Taarifa hizi zilipomfikia Beatrice, moja kwa moja akahisi huenda jambo kuu hapo lilihusiana na Dylan, hivyo hii haingekuwa ya kukosa. Aliwasiliana na Mr. Bernard na kumwambia atulie huko huko alikokuwa kwa sababu yeye ndiye ambaye angekwenda kwenye sherehe, hivyo angejua la kufanya endapo kungetokea jambo ambalo lingewaathiri vibaya.

Dylan alikuwa amefanya mpango ili kuwaleta watu kadhaa kutokea kule kwao, wakiwemo baadhi ya wafanyakazi kwenye kampuni ya Grace, familia ya Baraka, mama Conso, Fred, Bosco, marafiki zake Grace, na Grace mwenyewe. Party hii ingekuwa kubwa, ambayo ingefanywa kwenye ukumbi wa hoteli ya kifahari jijini kwa wazazi wa Dylan. Hivyo Dylan alikuwa amefanya mipango na Grace ili waliotoka mbali waweze kurudishwa majumbani kwao kwa usafiri wa kibibafsi baada ya party kuisha.

Grace aliongea na Jafari kumpanga kuwa aweke vijana wengine mahiri katika kufatilia nyendo za watu pale, ambao wangejifanya kama waalikwa wa kawaida tu. Wachache wangekuwa ukumbini, na wachache wangekuwa kwenye chumba binafsi chenye TV nyingi zilizoonyesha CCTV camera zilizowekwa kuzunguka ukumbini hapo mpaka sehemu ya nje ili kuangalia kila mtu kwa makini. Alikuwa amelipa uongozi wa hoteli hiyo ili kwa sehemu kubwa ya shughuli ambazo zingefanyika hapo siku hiyo iongozwe kwa njia aliyotaka yeye.

Kwa hiyo watu wake wangekuwa makini sana kuona mambo yote na kuwasiliana kimya kimya kupitia vifaa vidogo vya masikioni ili kuweza kupeana taarifa muhimu.


β˜…β˜…β˜…


Hatimaye siku ya party ikawadia. Mpaka kufikia wakati huo bado Jafari hakuwa amempata Mr. Bernard, hivyo walijua walipaswa kuwa chonjo sana kwenye mambo ambayo yangefanyika siku hiyo. Watu wengi wa huko walifika mapema na kukuta ukumbi ukiwa umepambwa kwa mitindo tofauti tofauti yenye kupendeza sana. Meza zilizungukwa kwa viti vilivyopambwa pia, na muziki ulipigwa kuwapa wahudhuriaji ladha nzuri ya uwepo wao hapo. Kama kawaida, watu walivaa kwa kupendeza sana, na kila mmoja wao alikaribishwa kwa kinywaji na kuchagua sehemu ya kuketi.

Beatrice alifika mida ya saa 12 jioni, akiwa pamoja na wanae, Harleen na David. David pia alikuwa amemaliza kidato cha pili hivyo wakati huo alikuwepo nyumbani. Walikaribishwa vizuri na kwenda kusalimiana na wazazi wa Dylan, ambao tayari walikuwepo wakifurahia maongezi na watu, pamoja na kupata vinywaji. Rafiki za Dylan; Fetty, Bosco, Fred, na wengine walikuwepo pia hapo.

Kulikuwa na mtumbuizaji aliyeimba nyimbo zake zenye kuvutia, nyingi zikielekezwa kwa wazazi wa Dylan, pindi ambazo DJ angezimisha mziki wa kwenye mitambo. Hakuna yeyote yule isipokuwa Gilbert na Jaquelin aliyejua kwamba Dylan alikuwepo muda wote huo; akiwa kwenye chumba binafsi peke yake kufanya maandalizi kwa ajili ya wakati ambao angejitokeza mbele ya wengi.

Baada ya muda, Baraka pamoja na familia yake wakawa wamefika pia. Walivalia vizuri sana kwa kuwa Grace alikuwa amewagharamia nguo na viatu vizuri sana. Walisalimiana na wengi hapo kisha kuketi, wakifurahia vinywaji na vitumbuizo kadhaa kule mbele kwenye jukwaa. Shani na Steven ndiyo waliokuwa na mzuka sana kwa kuwa walipenda sana maisha ya namna hiyo; bata.

Leila alimuuliza baba yake kwa nini Ethan, yaani Dylan, hakuwepo bado. Baba yake akawa amemwambia tu kijana angekuja hivyo alitakiwa kuwa na subira. Ijapokuwa Baraka hakujua kihalisi kilichokuwa kinaendelea HAPO, alijua huenda kulikuwa na jambo kuu lingefanyika kwenye sherehe hii kwa sababu Dylan alikuwa ameshamweleza ukweli kuhusu maisha yake, lakini Baraka alikuwa makini kutosema kwa yeyote kuhusu mambo hayo. Watu walipiga story, walikunywa, na kufurahia vitumbuizo mbalimbali vilivyoandaliwa hapo. Baba yake Gilbert alifika pia akiwa na rafiki yake mmoja kutokea huko huko Nairobi.

Saa 2 ilipofika, Grace akaingia. Watu wote walimwangalia kana kwamba ni mtu fulani maarufu ndiye alikuwa ameingia. Alipendeza sana. Alivaa gauni refu lililofika hadi chini na kuburuza kwa nyuma, lenye rangi ya maroon yenye kung'aa na lililokuwa la kitambaa kizito kilicho na manyoya yenye kuteleza. Mpasuo wake ulifikia pajani, na mkononi alishika pochi nene ya rangi hiyo hiyo pia. Nywele zake zilikuwa zimesukwa kwa njia ya rasta nyeusi, alizoziachia zimwagikie kufikia mgongoni kwake. Alitembea taratibu na viatu vyake virefu akielekea upande ambao wazazi wa Dylan walikuwa.

"Baba, huyo hapo ni mke wake Dayamondi," Steven akamwambia Baraka.

Baraka na Shani wakacheka sana.

"Siyo bwana, huyo ni Grace. Umemsahau?" Emilia akasema.

"Aaaa... mchumba wake Ethan? Eh, anamfanana Zari!" Steven akasema.

Wazazi wake wakacheka tena. Leila akaudhika na kumwangalia mdogo wake kwa kukereka.

"Siyo mchumba wake!" Leila akamwambia Steven.

"Iiiih...kwani kuna nini akiwa mchumba wake?" Shani akasema.

"Anaona gere!" Emilia akatania.

Leila akasonya na kuangalia pembeni.

Wazazi wa Dylan, wakiwa wameketi kwenye meza moja na baba yake Gilbert, walisimama baada ya kumwona Grace. Akawafata akiwa anatabasamu, kisha akawasalimu na kuwakumbatia mmoja baada ya mwingine. Hawakuwa wametarajia hilo, kwa sababu walimwona Grace kama mtu fulani asiyeguswa kabisa, bila kujua mwana wao tayari alikuwa ameshavuruga mitambo!

Beatrice alimtazama sana Grace. Hakuwahi kumwona sehemu yoyote ile, na uwepo wake hapo mpaka kujuana na Gilbert na Jaquelin kulimaanisha kwamba alikuwa mtu fulani muhimu sana sehemu hii. Akajiwekea akilini mwake kuwa ni lazima angemfanyia utafiti mwanamke huyo ili kujua ikiwa ana uhusiani fulani na mipango yao kuvurugwa.

Baada ya hapo, MC aliwakaribisha wenye sherehe ili waweze kuongea machache kuhusiana na dhumuni la tafrija hiyo. Gilbert na Jaquelin wakapanda jukwaani pamoja, na kusimama wakiwa karibu sana. Hilo lilimchukiza mno Beatrice ambaye bado alikuwa ana hisia kumwelekea Gilbert. Gilbert akaanza kusema maneno ya shukrani kwa wafanyakazi wa kampuni na marafiki kwa support kubwa ambayo wamewapa kwa kipindi kirefu. Akaongelea kuhusiana na panda shuka walizokutana nazo katika safari yao, lakini Mungu aliweza kuwasaidia kwa njia ambazo hawangeweza kutarajia kiukweli.

Jaquelin akachukua kikuza sauti (mic) ili naye aanze kuongea baada ya Gilbert kuwa ameongea hayo. Akaanza kuongelea kuhusu jinsi anavyohisi kuwa mwenye pendeleo kubwa sana kwa sababu ya baraka ambazo Mungu amewashushia baada ya kipindi kile kigumu kuwapata. Akaelekeza sifa zake kwa Grace, kwa kusema kwamba mwanamke huyu amekuwa ni msaada mkubwa sana kwao. Akawafahamisha watu wote hapo kuwa VIP maalumu wa sherehe hii alikuwa ni yeye (Grace), na kwamba ni kwa sababu ya msaada wake mkubwa wameweza tena kuongeza na VIP mwingine ambaye ni wa muhimu hata zaidi.

Grace alichekea chini kwa kufurahishwa na jinsi Jaquelin alivyojua kupamba maneno yake. Wengi hawakuelewa ni nini alichokuwa anamaanisha hasa kwa kusema hivyo, hivyo akawaambia wangeelewa ndani ya muda mfupi. Ni hapa ndipo mapigo ya moyo wa Beatrice yalianza kwenda kwa kasi kwa kuwa alianza kuyaona matarajio yake yanafikia penyewe. Jaquelin akamwangalia Grace, naye Grace akampa ishara kwa macho kuwa aendelee.

"Nina furaha kubwa sana kuwaambia nyote mlioko hapa kwamba...Dylan... mwanangu kipenzi... yuko hai!"

Maneno ya Jaquelin yangepaswa labda kuwafanya watu waanze kupiga makofi kwa shangwe, lakini wote wakatulia na kumwangalia kama vile ni mtu aliyerukwa na akili. Gilbert akacheka kidogo kutokana na kuona jinsi watu walivyoshangazwa na maneno yake. Beatrice alianza kupumua kwa hofu lakini akijizuia asionekane waziwazi.

"Ni kweli. Mwanangu alisalimika kwenye ajali ile iliyompata, naye amerudi kwetu tena kwa mara nyingine. Na huyo ndiyo VIP special wa party hii."

Watu waliendelea kumwangalia, na kuangaliana kimaswali sana. Waliochanganywa zaidi na maneno yake walikuwa ni Fetty na Harleen. Fetty tayari alikuwa amemwona Dylan, hivyo kuhakikishiwa kwamba alikuwa amerudi kulifanya hisia zake zipande maradufu. Kwa upande wake Harleen, lilikuwa ni jambo lenye kushtua sana na kushangaza kwa sababu rafiki yake huyo wa kitambo, ambaye pia alimpenda, alikuwa amekufa kwenye akili yake, na sasa tena akaambiwa yuko hai. Alitaka kujua ikiwa huu ulikuwa ni ukweli au kulikuwa na tatizo kwenye akili za wazazi wa Dylan.

Jaquelin akasema hivi, "Nyote mlio hapa, napenda kuwakaribishia mwanangu mpendwa, DYLAN!"

Alisema hivyo huku akiwa amenyoosha mkono wake kuelekea kwenye milango ya kuingilia, na watu wote wakageuka kutazama huko.

Hapo hapo akaingia mwanaume! Wote ambao walifikiri Jaquelin amerukwa na akili walisimama wakiwa hawaamini kile macho yao yalichoona. Dylan alikuwa hai, mzima wa afya kabisa.

Beatrice alinyanyuka pia akiwa anahisi woga uliofanya damu yake ichemke na mapigo yake ya moyo kukimbia kwa kasi. Harleen, Fetty, baba yake Gilbert (babu yake Dylan), wote walisimama wakiwa wanashangaa kumwona tena mwanaume huyu waliyempenda sana. Fetty alikuwa analia huku anacheka kwa furaha, naye Harleen akawa anadondosha machozi akiwa ametulia kwa mshangao wake.

Dylan alikuwa anatembea kuelekea mbele kule huku anawapa watu wote tabasamu la kirafiki, huku wengi wakitoa minong'ono ya kustaajabishwa na jambo hilo. Alikuwa amependeza kwa kuvalia suti nyeusi na kuziweka nywele zake kwa mtindo ule ule aliopenda. Baba yake Gilbert akamfata kabla hajafika kule jukwaani na kumshika mabegani, akimwangalia kama haamini alikuwa ni yeye kweli. Akamkumbatia kwa furaha sana, kitu kilichofanya Jaquelin aanze kulia. Kisha baada ya kumwachia, Dylan akaelekea kule jukwaani na kukumbatiana na wazazi wake pia.

"Watu tafadhali jamani, mnaweza kukaa. Dylan atawaeleza kila kitu mnachohitaji kujua," Jaquelin akasema.

Watu wakaanza kurudi kwenye viti vyao ili wakae na kumsikiliza kwa makini mtoto wa Gilbert na Jaquelin.

"Kwa nini anamwita Ethan, Dylan?" Steven akamuuliza baba yake.

"Dylan ndiyo jina lake kabisa. Unakumbuka alipokuja nyumbani alikuwa hadi amesahau jina lake?" Baraka akasema.

"Eeee," Steven akajibu.

"Ndiyo. Sasa hivi amejua kwamba anaitwa Dylan, na huyo ndo' mama'ake, na yule baba'ake," Baraka akaeleza.

"We ulijua lini?" mama Conso, ambaye alikuwa ameketi meza moja pamoja nao, akamuuliza hivyo Baraka.

"Aliniambia juzi kati hapo," Baraka akajibu.

Jaquelin Na Gilbert walimwacha Dylan akiwa ameshika kikuza sauti na kwenda kuketi kwenye viti. Watu walikuwa makini sana kumwangalia Dylan, wakisubiri kusikia ni nini ambacho kilikuwa kimempata kijana huyo.

"Za wakati huu? Aam... samahani kwa kuwa siko vizuri sana kwenye salamu... namaanisha habari za wakati huu?"

Dylan akaanza kuongea namna hiyo, na baadhi ya watu wakaitikia salamu yake.

"Wengi wenu hapa mnanifahamu, na labda mimi pia niliwafahamu...."

"Labda?" Harleen akauliza akiwa amemgeukia mama yake.

Beatrice akatikisa mabega kuonyesha hakuelewa mambo vizuri.

Dylan akawa anaendelea kusimulia, "...kwa sababu kilichotokea ni tofauti na kilichokuja kusikika. Wengi mnajua kuwa nilipatwa na ajali, na ikasemekana kwamba nilikufa humo pia. Lakini la, haikuwa hivyo. Bado sijui ilikuwaje nikasalimika kwa sababu... nilipiga kichwa changu vibaya inaonekana baada ya kuanguka, na hivyo nikawa nimepoteza kumbukumbu yangu..."

Watu wengi walimwonea huruma baada ya kutambua ukweli huo. Kwa Beatrice, maneno ya Dylan yalimpa tumaini kuwa huenda alikuwa hafahamu chochote, lakini bado alijua angepaswa kummaliza tu iwe isiwe.

Dylan akawa anaendelea, "...mwanaume huyu ni kama baba, kaka, na baraka kubwa kwangu kwa sababu badala ya kuniacha tu nifie majini, alinitoa, akanipeleka kupata matibabu na kunitunza kwa miezi mingi nyumbani kwake. Naweza kusema bila yeye huenda nisingekuwa nimesimama hapa leo. Tafadhali Baraka, nakuomba uje usimame nami..."

Baraka akanyanyuka akiwa anafurahi sana na kwenda kule mbele. Grace alianzisha kupiga makofi, na watu wote wakaanza kumpigia makofi Baraka. Akafika mbele pale na kukumbatiana kiume na kijana wake, kisha Dylan akaendelea kuzungumza.

"....kwa yote niliyopitia, yote niliyohitaji msaada, sikuzote Baraka alini-support sana. Ilikuwa ni kama upendo alionionyesha ni wa baba kwa mwanae, kwa hiyo mwanaume huyu ni mtu mmoja ambaye ni muhimu sana kwangu. Baraka... nakushukuru sana kwa yote uliyonitendea kwa wema. Mama alisema me ndiyo VIP mwingine special, na wewe pia ni VIP special kwenye party hii," Dylan akamwambia.

Watu wengi wakatabasamu kwa kuguswa sana na hilo. Baraka akamkumbatia tena kijana wake, kisha akaanza kurudi kuketi tena huku akipigiwa makofi.

"Maisha yangu yaliendelea kuwa kama movie, maana kwa sababu fulani kila wakati jambo fulani lilitokea kwa njia ambazo zilinibomoa au kunijenga zaidi nikiwa bado kama Ethan. Lakini zinazochukua sehemu kubwa ndani ya moyo wangu ni zile zilizonijenga, na moja iliyo muhimu kati ya hizo zote ni huyu mwanamke.... Grace," Dylan akasema.

Grace akatabasamu akiwa ameketi pembeni ya wazazi wake Dylan, na watu wote wakamwangalia Grace. Hapa sasa Beatrice akawa ameunganisha vipande vingi na kupata kitu kizima. Huyu Grace ndiye aliyewasaidia Gilbert na Jaquelin kuirudisha kampuni, halafu ni huyo huyo ndiye ambaye Dylan anamsifia kwamba alimsaidia. Bila shaka huyo ndiye aliyekuwa tatizo kwake.

Dylan akamnyooshea kiganja Grace kuashiria apande kule mbele, naye Grace akanyanyuka na kuelekea huko. Dylan akampokea kwa mkono na kisha kumkumbatia kwa upendo. Watu kadhaa walisikika wakinong'ona, na ilieleweka wengi walikuwa wanakisia kwamba mwanamke huyo mwenye kuvutia alikuwa ni mtu wake Dylan; na hawakuwa wamekosea.

Dylan akawageukia watu huku akiwa amemshika mkono Grace. na kusema, "...huyu ndiye ambaye amenisaidia pia kuweza kurudi hapa. Ni mwanamke mrembo sana kama mnavyoona. Ni mkali sana, na ana kichwa kigumu pia..."

Grace pamoja na watu wengine wakacheka.

"Lakini ni mtu mmoja mkarimu, mstaarabu, na anayejua kuchukua hatua zinazofaa ili kuondoa ukosefu wowote wa haki unaomzunguka. Grace....asante sana kwa kila jambo ulilofanya kwa ajili yangu..."

Dylan akasema hivyo na kumshika Grace kwenye shavu. Watu wote wakawa wanasubiri kwa hamu kuona nini kingefuata maana hata wazazi wake hawakuwa wamefikiri wawili hawa wana ukaribu namna hiyo.

"Wewe ni wa muhimu sana kwenye maisha yangu Grace....nakupenda."

Wazazi wake Dylan wakaangaliana kwa kushangazwa na hilo. Harleen na Fetty walitamaushwa mno kujua kwamba Dylan alikuwa kwa mwingine sasa. Bora hata Harleen ambaye alionjeshwa penzi la Dylan kwa muda mfupi; Fetty ndiye aliyehisi kumkosa kabisa jamaa daima. Dylan akamkumbatia Grace, na watu wakaanza kupiga makofi kwa shangwe kubwa. Dylan akamwachia Grace na kushuka naye kuanza kusalimiana na watu hapo, na wengi walikuwa wakimfata ili kuweza kuongea naye na kumwambia jinsi walivyomkosa sana.

Muda wote, kupitia vifaa vyao vya masikioni, waliweza kuambiwa na sauti za wafatiliaji wao kuhusu nyendo za watu hapo ili kuwapa umakini. Walikuwa waangalifu sana kutokaribiana karibu mno na yeyote ili kuepusha athari za ghafla. Ni mpaka wakati ambapo Harleen alimfata Dylan kwa kasi na kujaribu kumkumbatia, pale mmoja wa waliokuwa wanamlinda Dylan kisiri alipomzuia asiendelee kumfata.

Hii iliwasha taa nyekundu kwenye akili ya Beatrice na kumfanya atambue kwamba Dylan alikuwa anajilinda hapo. Wazazi wa Dylan walienda na kumtambulisha Harleen kwa Dylan, akipata kujua sasa kwamba huyu alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu. Alitambulishwa kwa wengi ambao walikuwa marafiki zake na alifanya nao kazi pia, lakini pamoja na hayo yote bado Dylan alihitaji kuwa mwangalifu kwa sababu alijua hata mtu asemaye kuwa ni rafiki angeweza kuwa ndiye adui.

Wakiwa wanaendelea kusalimiana na wengi, chakula kilikuwa tayari na wote wakaambiwa wanaweza kwenda kufata. Dylan na Grace walienda kukaa pamoja na wazazi wake, wakionekana kama wanandoa fulani hivi. Harleen na Leila waliona wivu sana, lakini ni Fetty ndiye aliyehisi maumivu mengi mno moyoni mwake, kwa sababu ilikuwa ni kama hakuwahi kujuana naye kabisa. Alimwangalia jinsi alivyoonekana kuwa na furaha sana akiwa na Grace, naye akajikaza sana asionyeshe simanzi yake nzito.

Beatrice alikuwa makini kutazama watu kwenye ukumbi huo, akipiga jicho lake la tai huku na huku, na kwa akili yake yenye hila aliweza kutambua kwamba kulikuwa na watu maalum waliowekwa ili kufatilia wengine hapo. Hivyo kwa ujanja akajitahidi kuonyesha utulivu wa hali ya juu, lakini akilini akiwa anajipanga ni jinsi gani angeweza kushughulika na Dylan.

Baada ya chakula, watu waliwekewa muziki ili waanze kucheza kwa raha zao. Harleen alikuwa akicheza pamoja na Bosco, baada ya wawili hawa kukumbukana tena kwa kuwa walisoma pamoja na Dylan wakati wako wadogo. Dylan aliendelea kukaa pamoja na Grace, kwa utulivu tu wakisikilizia jinsi ambavyo mambo yalikuwa yanakwenda. Ni hapa ndipo Beatrice akaamua kuwafata ili aongee nao, akijifanya kuwa mtu ambaye anampenda sana Dylan kwa sababu ya kuwa rafiki ya mama yake. Aliwachangamkia sana na kupiga nao story kuhusu mambo mengi yaliyohusiana na kule kwao, sanasana akimhoji Grace kuhusu maisha yake kwa njia ya kijanja.

Grace alianza kuona ni kama Beatrice alikuwa mchokonozi sana; kupita kiasi. Hili likamfanya na yeye aanze kumuuliza maswali yenye udadisi kuhusu maisha yake, naye Beatrice akawa akitumia mikato tu baada ya kuanza kuona kwamba Grace alikuwa mwenye akili sana. Hivyo akaamua kuwaacha ili aende kwa Jaquelin. Baada ya kuwaacha, Grace akawaambia watu wake wamwangalie kwa ukaribu mwanamke huyo kwa kuwa alimpa hisia fulani mbaya.

Dylan alimfata Fetty baada ya hapo. Alikuwa anamkumbuka kutokea usiku ule alivyomwona kwenye ile bar alipokwenda, na alijua anamfahamu vizuri baada ya wazazi wake kumwambia yeye ndiye aliyewajulisha kuwa yuko hai.

"Mambo vipi?" akamsalimu baada ya kumfikia.

Fetty akasimama kutoka alipokuwa amekaa, akimwangalia Dylan kwa hisia sana.

"Safi tu," akamjibu.

"Fetty, si ndiyo?" Dylan akasema.

"Ndiyo."

"Mama aliniambia sisi ni marafiki. Nilipokuona siku ile nilihisi kama nakujua lakini pff... kumbukumbu ikawa inanisaliti hahah..."

Dylan alisema hivyo kwa njia yenye utani kiasi, lakini akashangaa kuona kwamba Fetty hata hakutabasamu. Alikuwa anamwangalia kwa njia ya huzuni, na jinsi pumzi zake zilivyopanda, macho yake kulengwa na machozi, kulimwambia Dylan kwamba kuna kitu Hakukuwa sawa.

"Aam... samahani, kuna tatizo?" Dylan akauliza kwa kujali.

Fetty akameza mate kwa njia ya kujikaza na kutikisa kichwa kukataa.

"Najua sikumbuki mambo vizuri, kama kuna jambo fulani ambalo... unaweza kuniambia chochote kile..."

Dylan akawa anajaribu kumsihi, lakini Fetty akajifuta tu machozi haraka na kuuchukua mkoba wake kisha kuondoka hapo. Alimwacha Dylan anawaza ikiwa kulikuwa na jambo lolote lenye kukwaza alilosema, au labda jambo fulani ambalo alifanya hapo zamani. Alijionea huruma kwa kiasi fulani kwa sababu ya kutokumbuka mambo mengi, lakini hakuwa na jinsi ila kusubiri wakati ambao mambo mengi ya maisha yake ya zamani yangerejea tena kichwani kwake.

Masaa yalikuwa yamekwenda, na sasa ikawa inakaribia saa 6 usiku. Watu kadha wa kadha walikuwa wakiondoka, na wengi wao walimuaga Dylan wakionyesha jinsi walivyofurahi kumwona tena. Harleen aliondoka pamoja na David, akimwacha Beatrice akiwa na "rafiki" yake, Jaquelin. Familia ya Baraka ilihitaji kuondoka pia, na kwa kuwa Grace alikuwa amefanya mpango ili walale kwenye hoteli fulani ndani ya mji huo, wangeenda kwenye gari lao walilokodishiwa kisha kupelekwa huko. Fred pia angeambatana pamoja nao, hivyo baada ya wote kumuaga Dylan, wakaondoka ukumbini hapo.

Upelelezi uliofanywa na watu wa Grace haukuwa umetokeza jambo lenye kuvuta uangalifu wao, lakini yote kwa yote walijua maadui zao wameshajua kuwa Dylan yuko hai, hivyo muda siyo mrefu wangejitokeza tu kujaribu kufanya kitu ambacho kingewanasisha mtegoni. Dylan alimwambia Grace kuwa na yeye (Grace) alihitaji kwenda kupumzika mapema hasa kwa sababu alikuwa mjamzito, hivyo angempeleka kwenye hoteli fulani ambayo tayari walikuwa wameshalipia chumba maalumu cha kupumzikia kwa ajili yao.

Hivyo Dylan akatoka na Grace ili watangulie; na wakiwa makini sana walipoelekea kule nje, huku Beatrice akiwatazama kwa hisia kali sana.


β˜…β˜…β˜…


Wakiwa bado njiani kuelekea kwenye hoteli, familia ya Baraka ilizungumzia mambo mengi mazuri waliyofurahia kwenye party ile. Hoteli hii haikuwa mbali sana na hoteli waliyokuwa wanafanyia sherehe ile, hivyo walifika na kushuka kutoka ndani ya gari hilo. Fred alimbeba Steven kwa kuwa alikuwa amesinzia, lakini Shani akabaki ndani ya gari hilo akitafuta kitu fulani. Baraka akarudi hapo na kuuliza ni nini alikuwa anatafuta, naye akamwambia inaonekana alikuwa amesahau pochi yake kwenye kiti alichokalia kule hotelini walikotoka.

Walikuwa wamepewa walinzi wawili waje nao, yaani watu wa Grace, na ijapokuwa familia ya Baraka haikuelewa kikamili sababu ilikuwa ni nini, waliridhia kulindwa namna hiyo kwa kuwa iliwafanya wajihisi kama watu wa matawi ya juu. Msaidizi ambaye alikuwa amewaleta hapo kama dereva aliwahakikishia kwamba pochi yake angeikuta tu kule kule ikiwa angerudi kuifata, lakini ikaonekana ni kama isingewezekana kwa sababu alihitaji kuwapeleka kwenye vyumba walivyolipiwa ili yeye aondoke pia.

Hivyo, Baraka akamwambia Shani asijali; angemfatia pochi yake yeye mwenyewe kwa kuchukua usafiri wa bodaboda, kwa sababu Shani alisisitiza kulikuwa na mambo ya muhimu mule. Mlinzi mmoja aliposhauri aende pamoja naye, Baraka akasema haikuwa na shida kwa maana alikuwa akifata pochi tu haraka na kurudi.

Kwa hiyo Baraka akawaacha na kwenda kuita bodaboda karibu na hapo. Alihakikisha anakariri jina la hoteli hiyo waliyoletwa ili wakati wa kurudi asije kupotea. Baada ya kupata bodaboda moja akaanza kurudi kule ili kumfatia mke wake kipenzi pochi yake.


β˜…β˜…β˜…


Wazazi wa Dylan, pamoja na Beatrice, waliendelea kuwepo kwenye hoteli ile kwa muda mrefu zaidi, wakipiga story, huku furaha kubwa ya Jaquelin ikimfanya anywe wine nyingi mpaka kulewa. Hivyo Gilbert akaamua kumpeleka nyumbani kupumzika, akimwacha Beatrice pamoja na wengine baadhi hapo. Ilimbidi Gilbert ampe egamio mke wake kwa kuwa hakuweza kutembea vizuri. Mpaka wanafika ndani ya gari Jaquelin alikuwa amedebweda haswa, naye Gilbert akawaondoa hapo kuelekea nyumbani.

Beatrice pia alijiondokea na kwenda usawa ambao gari lake lilikuwa limeegeshwa, naye akatoa simu baada ya kuhakikisha hakukuwa na mtu hapo karibu wa kumsikia, kwa kuwa alikuwa anataka kumpigia Mr. Bernard. Moyoni alihisi hasira kali sana kwamba mambo mengi yalikuwa yameharibika, hivyo akataka kumjulisha Mr. Bernard dhumuni lake kuanzia sasa.

"Beatrice..." Mr. Bernard akasema kutokea upande wa pili.

"Dylan yuko hai! Amejitokeza leo hapa kwenye party," Beatrice akasema kwa mkazo.

"Damn!" Mr. Bernard akasema kwa hasira.

"Kuna huyu mwanamke... anaitwa Grace sijui, ndiyo amefanya mpaka ukanyang'anywa kampuni. Ni malaya wake sijui alimtoa wapi," Beatrice akasema.

"Ndiyo, hata mimi nilijua lazima Dylan awe anasaidiwa na mtu tu. Sasa... tunafanyaje? Ingewezekana hata si ungem-handle we mwenyewe fasta hapo...."

"Acha ujinga Bernard, hawa watu wana akili. Unafikiri angejitokeza tu bila kujiandaa kwa lolote? Anajua ana maadui, kulikuwa na watu wao wanachunguza hapa, hata kwa kumwangalia tu kifuani niliweza kutambua alikuwa amevaa bulletproof. Nisingeweza kufanya lolote."

"Sawa nimeelewa. Mpango ni nini sasa? Kama vipi nirudi ili..."

"Kalisha tako lako huko huko Bernard. Faida tuliyonayo ni kwamba hawajui ni mimi, lakini wewe wameshakujua. Nitadili na huyu mbwa me mwenyewe, halafu kila kitu ninachotaka kitokee nitahakikisha tu kinafanikiwa, hakuna makosa ya kijinga tena."

"Namna hiyo! Hapo umeongea Beatrice, nakukubali sana mama'angu," Mr. Bernard akamsifia.

Beatrice akatabasamu kwa kiburi, kisha akakata simu yake.

Ile anageuka nyuma, akashtuka sana baada ya kumwona mwanaume mmoja nyuma yake. Mapigo ya moyo yalianza kumkimbia kwa kasi kwa sababu alimtambua haraka, naye alikuwa ni Baraka. Alimkumbuka kutokana na jinsi Dylan alivyomsifia kwamba alimwona kama baba yake, hivyo ikiwa alikuwa amesikia maongezi yake na Mr. Bernard, basi alijua hiyo isingekuwa jambo zuri kwake.

Baraka alikuwa amesimama hatua chache kumfikia Beatrice, akiwa ametokea kwenye bodaboda ili arudi tena ndani ya hoteli ile. Beatrice akajitahidi kuzuia hofu yake isionekane wazi, naye Baraka akaachia tabasamu dogo na kuanza kumfata Beatrice taratibu. Hii ikamwambia Beatrice kwamba huenda mwanaume huyo hakuwa amemsikia.

"Habari," Baraka akamsalimu.

"Nzuri," Beatrice akasema huku akitoa tabasamu bandia.

"Watu bado wapo huko ndani?" Baraka akauliza.

"Wachache sana.... wengi organisers. Wanapatengeneza na kushughulikia usafi."

"Dah me nilifikiri watafanya asubuhi, inabidi niwahi mke wangu amesahau pochi yake, ndo' nimemfatia."

"Oooh sawa."

Baraka akamwangalia kwa sekunde chache Beatrice, naye Beatrice akatilia maanani hilo.

"Wewe ni... rafiki yake na mama yake Ethan. Yaani Dylan... si ndiyo?" akamuuliza.

"Ndiyo."

"Aaa... sawa. Unaitwa nani kweli...jina limenitoka pombe hiyo hahahah...." Baraka akasema kirafiki.

Beatrice akakaza meno yake kidogo, kisha akasema, "Aam... wahi kwanza pochi ya mkeo usikute imetolewa."

"Oooh sawa sawa. Ngoja niwahi huko sasa," Baraka akasema na kumpita Beatrice hapo.

Beatrice alimgeukia na kumpiga jicho kwa umakini sana, na hapo aliweza kumwona Baraka akigeuka nyuma mara kwa mara kumwangalia na kisha kuelekea kule ndani ya hoteli. Beatrice akatukana kwa sauti ya chini akiwa ametambua kwamba mwanaume huyo alimsikia, ila akajifanya tu kama vile hakumsikia. Hapo sasa ilikuwa ni hatari kwake maana bila shaka angeweza kumwambia Dylan kila kitu alichosikia. Akaingia ndani ya gari lake na kuanza kuupiga usukani akitumia mikono yake kwa hasira, akijiuliza afanye nini sasa. Akiwa anapumua kwa hasira, akatazama sehemu ya mbele ya gari ya kutunzia vitu vichache, naye akaweka uso ulio serious na kutazama tena upande wa ile hoteli.

Akiwa kule ndani ya hoteli, Baraka alimpigia sana simu Dylan, lakini kijana wake huyo hakupokea hata mara moja. Alitaka kumwambia kuhusu mambo yote aliyosikia kutoka kwa mwanamke yule, kwa kuwa sasa alitambua wazi kwamba huyo ndiye adui mkuu wa kijana wake aliyemsababishia matatizo mengi sana, na ambaye bado alitaka kumwongezea mengine. Jitihada yake ya kumfikishia ujumbe huo kijana iligonga mwamba, na kwa kuchukulia kwamba huenda tayari alikuwa amelala, akaona amwandikie ujumbe mfupi ili akiamka ausome na kujua umuhimu wa jambo alilotaka kumwambia.

Baada ya hapo akaingia tena ukumbini kule, naye alipofika kwenye viti walivyokalia alishukuru kuikuta pochi ya mke wake pale, lakini ikiwa imedondokea chini karibu na miguu ya meza. Akaiokota, kisha akaanza kurudi nje ili aelekee hotelini. Alipofika usawa wa barabara, aliangalia pande tofauti kuona kama angeweza kupata bodaboda mwingine, maana alisahau kumwambia yule aliyekuja naye amsubiri. Aliona mmoja akiwa kwa mbali, naye akamwita.

Lakini kabla boda hajafika, gari likafika pembezoni mwa barabara kumwelekea Baraka na kusimama hapo. Kioo cheusi cha mlango wa mbele kikashuka, naye Baraka akapata kumwona Beatrice kwenye usukani.

"Baraka... unaelekea nyumbani?" Beatrice akamuuliza huku anatabazamu.

Baraka pia akatoa tabasamu bandia na kusema, "Ndiyo."

"Njoo nikupe lifti basi naelekea nyumbani pia."

Ni wakati huu bodaboda yule akawa amefika mbele ya Baraka.

"Ah... haina shida dada. Asante sana kwa wema wako. Nilikuwa nimeshaita boda hapa," Baraka akamwambia.

"Lakini hapa hautalipia... we kaka nenda tu, nitampeleka huyu ni rafiki yangu," Beatrice akamwambia na bodaboda.

"Asa' s'kashaniita sista... niondoke vipi tena?" boda huyo wa usiku akasema.

Baraka akaamua kupanda tu nyuma ya pikipiki.

"Usijali, wacha tu niende kwa boda. Usiku mwema dada, asante sana," Baraka akasema.

Kisha bodaboda akaondoa pikipiki hapo na kuanza kuelekea upande alioelekezwa. Beatrice akafunga kioo na kupiga kelele nyingi za hasira ndani ya gari lake. Akipumua kwa jazba kubwa, akawa anatikisa kichwa kwa njia ya kukataa kwamba haingewezekana Baraka kumtoroka namna hiyo. Lakini angefanyaje sasa kwa kuwa mwanaume huyo tayari alikuwa amemwacha?

Safari ya bodaboda kurudi hotelini iliendelea, huku Baraka akishukuru Mungu kwamba aliweza kumwepuka mwanamke yule. Alielewa vizuri kabisa akilini kwamba kama angekubali kupanda lile gari, basi ndiyo ingekuwa mwisho wake kwa sababu mwanamke yule ndiye ambaye alijaribu kumuuua Dylan, kwa hiyo asingeshindwa kumfanyia hivyo hivyo na yeye pia. Alifikishwa kwenye hoteli ile, akashuka, akamlipa bodaboda, kisha akaanza kuielekea ili kurudi kwa familia yake.

Lakini ghafla, pale pale gari moja likafika kwa kasi sana mbele yake na kusimama kwa mshtukizo mpaka matairi yakatoa kelele!

Baraka alishtuka sana kwa kuwa hakutarajia jambo hilo, naye akarudi nyuma kidogo akishangazwa na jambo hilo. Huu ulikuwa ni usiku wa saa 7, hivyo hakukuwa na watu eneo hili isipokuwa labda walinzi wa majengo tofauti tofauti ya eneo hilo; ikiwemo na hoteli ile. Baraka aliweza kutambua kwamba gari hili halikuwa geni sana machoni pake, na akili yake ikamwambia kwa haraka lilikuwa ni la....

Kioo cha mlango wa mbele wa gari hilo kikafunguka na hapo hapo mkono ulioshika bastola ukatoka na kumwelekea Baraka. Hakuwa hata na muda wa kushtushwa na jambo hilo kwa sababu risasi mbili zilifyatuliwa na kumpiga kifuani mwake! Hazikuwa risasi zenye msukumo mkubwa kwa sababu hazikumwangusha chini mara moja, naye akawa amebaki kasimama na kuachama mdomo wake akihisi maumivu makali sana. Kwa kuwa bado macho yake yalitazama kuelekea gari hilo, aliweza kuona kioo kikipanda juu tena, na sura ya aliyekuwa ndani haikuwa ya mwingine, ila Beatrice mwenyewe.

Gari liliondoka kwa kasi sana, na milio ya risasi hizo ilishtua watu wengi waliokuwa kwenye majengo ya hapo karibu. Baraka akadondoka chini baada ya kuishiwa nguvu, naye akawa anaita majina ya watu aliowapenda sana kwa sauti dhaifu.

"Shhanni...eh...e...Emmiliaah...kkh...Steve...Leihhlaaa...aahh...Ethan...Ehhthan...Ethhh..!"

Na baada ya hapo, pumzi yake ikakata.


β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

WhatsApp +255 787 604 893
 
Baraka has gone so soon, he paid the big and major sacrifice towards the Dylan's observation. Missed calls na sms aliyomtumia Dylan ni alert na information nzuri na za wazi kabisa
Beatrice aliact vizuri ndani ya ukumbi baada ya kugundua ulinzi wa mule ndani na mejiexpose kijinga kabisa kupiga simu ya madhara katika eneo la wazi.
 
Baraka has gone so soon, he paid the big and major sacrifice towards the Dylan's observation. Missed calls na sms aliyomtumia Dylan ni alert na information nzuri na za wazi kabisa
Beatrice aliact vizuri ndani ya ukumbi baada ya kugundua ulinzi wa mule ndani na mejiexpose kijinga kabisa kupiga simu ya madhara katika eneo la wazi.
Oyaaa nawe unaunga mkono akufe? [emoji23][emoji23] asife, azinduke aseme halafu apalaraizi atunzwe kwa wema wake

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom