Simulizi: Harakati za Jason Sizya


333

Mpambano mwingine…




Saa 7:00 usiku…

MVUA kubwa ilianza kunyesha sambamba na upepo wa wastani na hivyo kuifanya sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kwa wakati huo wa usiku kutawaliwa na hali ya baridi. Hii ilitokea muda mfupi tu tangu tulipofika kwenye nyumba za maofisa wa Usalama wa Taifa eneo la Makumbusho, nyumbani Pamela.

Tulipofika hapo Pamela hakutaka niondoke kama alivyoniambia hapo awali kuwa nimpitishe kisha ndiyo nielekee nyumbani kwangu Upanga, na badala yake kupitia ushawishi wake kama mwanamke tukajikuta tukitumbukia tena kwenye mtego mwingine wa mapenzi mazito.

Yalikuwa mapenzi motomoto yaliyonifanya nitamani kuitangazia dunia kuhusu utamu wa mwanamke huyo. Pamela alikuwa mwanamke mtundu sana aliyejua jinsi ya kucheza vizuri na hisia za mwanaume na kwa kweli aliniwezea sana na kunifanya nisahau mikasa yote niliyokuwa nimekumbana nayo katika harakati za kumsaka Bosco Gahizi na wenzake.

Mara tu tulipoingia nyumbani kwake tukaanzia bafuni tulikokwenda kuoga ili kutoa uchovu na kuipoza miili yetu na tukiwa huko bafuni Pamela akaanza vitimbi vyake vya hapa na pale. Wakati tukioga kwenye bomba la mvua alinivuta na kunikumbatia huku akiipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu na kufanya joto kali la mwili wake linipe faraja kubwa.

Nilishindwa kuvumilia, nami nikazungusha mikono yangu kumshika kiunoni kisha nikawa nakiminya minya kiuno chake. Tukatazama machoni kisha tabasamu maridhawa likachomoza kwenye nyuso zetu. Kisha Pamela akapeleka mkono wake kwenye malighafi zangu na kuanza kuzitomasa kwa namna ya kunipandisha mdadi halafu akaanza kunichua taratibu mshumaa wangu katika namna ya kuamsha vilivyolala, kwa kweli sikuweza kukivumilia kitendo kile, nikaamua kumpelekea moto huko huko bafuni.

Na tulipomaliza ngwe moja tukaoga na kisha tukaelekea chumbani ambako sasa kila mmoja alikuwa amempania mwenzake, maana tulipoingia tu chumbani Pamela akaanza uchokozi, nikambeba na kumtupia kitandani huku wote tukiangua vicheko hafifu vya mahaba. Kisha kama watu tuliopandwa na wazimu wa mapenzi tukaingia mchezoni na muda mfupi uliofuata tulijikuta tukimezwa na ulimwengu wa huba. Ilikuwa ni kama sinema ya kusisimua yenye kila aina ya vionjo vya kumtoa nyoka pangoni.

Tulikuwa kwenye ulimwengu mzito wa mapenzi na dunia ilikuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yetu. Tukizisahau shida zote. Pamela alikuwa amezitendea vyema hisia zangu na raha tuliyoipata macho yetu hayakuweza kutazama. Muda huo hatukukumbuka kitu kingine chochote isipokuwa kuivunja amri ya sita, huku mapenzi yakionekana kunoga kwa namna yake na miguno ya mahaba ikihanikiza kila mahali mle chumbani.

Tulivingirishana kwa sarakasi za aina yake pale kwenye uwanja wa sita kwa sita huku mechi yetu ikitawaliwa na rafu za kila aina kwa kuwa mchezo wetu haukuwa na refa wala kamisaa, na kila mtu alijaribu kuonesha ufundi wake pasipo kujali kama alikuwa anafuata sheria za mchezo au la.

Nilicheza sana rafu kwa kuwa nilikuwa nimegundua hila ya Pamela kuwa aliamua kutumia utundu wa hali ya juu ili kunifanya niongee lugha aliyoitaka, kwani Waswahili husema kuwa “kichwa cha chini kikisimama cha juu huwa hakifanyi kazi sawa sawa.”

Tulipambana kwa takriban saa nzima na hatimaye mchezo wetu ulifika tamati huku wote wawili tukiwa hoi kabisa, kila mmoja wetu akionekana kutosheka na mwenzake.

_____



Saa 3:30 asubuhi…

Nilishtuka toka katika usingizi wa fofofo na kuyafumbua macho yangu taratibu kisha nikayatembeza mle chumbani kuangalia huku na kule nikijaribu kusikiliza kwa umakini. Sikujua kitu gani kilikuwa kimenishtua na kuukatisha ghafla usingizi wangu uliokuwa umenichukua ghafla! Ilikuwa ni siku nyingine na muda huo tulikuwa bado tumelala.

Nilipotupa macho yangu kando nikagundua kuwa hata Pamela pia alikuwa bado amelala fofofo. Kwa mbali nilisikia sauti hafifu ya mkoromo wake wa uchovu. Nikaitupia jicho saa yangu ya mkononi na kushtuka. Muda huo miale ya jua la asubuhi ilikuwa inapenya dirishani na kutuama pale kitandani tulipolala.

Kwa mara kwa kwanza tangu nianze harakati za upelelezi kuhusu tukio la kigaidi lililosababisha kuteketea kwa jengo la Alpha Mall nilikuwa nimelala usingizi mtamu sana wa kueleweka kiasi cha kuchelewa kuamka.

Hakika penzi zito la Pamela lilikuwa limeamsha ari mpya nafsini mwangu na kupitia ukaribu ule kitu fulani kilikuwa kimeanza kujengeka moyoni mwangu. Hata hivyo tumbo langu lilikuwa dhaifu sana kwa njaa. Njaa ilikuwa inauma sana utadhani nilikuwa na vidonda tumboni na kichwa changu kilinivangavanga sana.

Kichwa kilikuwa kizito sana mithili ya mtu aliyekuwa ametwishwa kiroba cha mchanga na nilihisi kuchoka mno, kichwani nilikuwa na mawenge ya usingizi yaliyonipa hali ya kutaka kuendelea kulala. Pilika pilika za siku iliyotangulia, pombe kali na ukichanganya na mahaba mazito basi hali ikawa si hali.

Hata hivyo, akilini mwangu niliutaka utulivu kwa gharama yoyote ile japo nipate kupumzisha mwili na kupata japo lepe la usingizi. Nilichotamani ni kulala tu mpaka pale ambapo mwili wangu ungeniruhusu kuamka. Niliuhisi uzito wa kichwa changu na mawenge ya usingizi yakinitesa na hivyo hali hiyo ilikuwa inanipa hali ya kutaka kuendelea kuuchapa usingizi. Lakini sasa nilijikuta nimeamka na sikujua nini kilikuwa kimeniamsha.

Nikayatega masikio yangu kwa umakini kusikiliza na hapo nikagundua kuwa sauti ya simu yangu ya mkononi iliyokuwa ikiita kwa fujo ndiyo iliyonishtua kutoka usingizini. Nikaitazama na kuiona namba ngeni, nikataka niipuuzie lakini hisia zangu zikaniambia kuwa ilikuwa simu muhimu sana. Nikaipokea na kuipeleka sikioni.

“Hallo!” nilisema kivivu vivu na kushusha pumzi ndefu.

“Jason!” sauti ya mkurugenzi mkuu iliita kutoka upande wa pili wa simu. Nikashtuka sana na kujikuta nikiinuka toka pale kitandani na kuketi kitako.

“Naam. Shikamoo, mkuu!” nilisalimia kwa unyenyekevu mara tu nilipogundua kuwa nilikuwa naongea na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa aliyeamua kunipigia simu moja kwa moja.

“Marahaba, Jason, habari za tangu usiku?” mkurugenzi mkuu aliniuliza kwa upole kama mzazi anayeongea na mwanawe wa kwanza, mara tu baada ya kumuoza mke.

“Salama, mkuu,” nilimjibu mkurugenzi mkuu kwa unyenyekevu.

“Sasa ni hivi… Mheshimiwa Rais anakupongeza sana kwa kazi uliyoifanya ambayo imetusaidia kuubaini mtandao hatari wa kihalifu, yeye pia anakubali sana uwepo wako katika idara nyeti kama hii… nimetoka kuzungumza naye sasa hivi na kuna jambo ameniambia…” mkurugenzi mkuu alisema na kunyamaza kidogo kuruhusu mate yapite kohoni mwake.

Muda huo huo nikamwona Pamela akishtuka na kunitazama usoni kwa aibu, alipogundua kuwa nilikuwa naongea na simu akajiinua na kusogea karibu yangu ili asikie.

“…Waswahili wanasema ‘mcheza kwao hutunzwa’. Hivyo wewe na wenzako Luteni Lister na Pamela mnatakiwa leo saa saba mchana muwepo Ikulu kuonana na Mheshimiwa Rais, ana mambo mazuri ya kuongea nanyi. Naomba mwambie na Pamela, najua uko naye,” mkurugenzi mkuu alisema.

Pamela ambaye muda huo alikuwa ameweka sikio lake kwenye simu yangu kusikiliza akashtuka sana na kuweka kiganja cha mkono wake mdomoni kuziba mdomo kwa woga, huku akinikodolea macho.

“Sawa mkuu. Nashukuru sana kwa taarifa hii, nashukuru sana sana…” nilisema kwa unyenyekevu. Haha…! niligundua kuwa mkurugenzi mkuu alishakata simu wakati nikiendelea kushukuru. Kisha mimi na Pamela tukatazama na kucheka.

Huu ni mwisho wa Msimu wa Sita kwenye mfululizo wa Harakati za Jason Sizya. Usikose Msimu wa Saba katika mkasa uitwao “Utata”.
 
Kweli hii ilikuwa taharuki big up bishop.kwa mtazamo wangu huko tuondako ni harakati kwelikweli za kijasus
 
Asante sana askofu kwakweli una namna unasimulia ambayo haielezeki nlikua natamani kuuliza khs mkuu Koba na yule secretary wa Jason lakini acha nikae kwa kutulia pengine yatajibika utatani...asante sana mkuu
 
Asante sana askofu kwakweli una namna unasimulia ambayo haielezeki nlikua natamani kuuliza khs mkuu Koba na yule secretary wa Jason lakini acha nikae kwa kutulia pengine yatajibika utatani...asante sana mkuu
Haha! Ni kweli bado kuna "Utata". Endelea kufuatilia...
 
Nilianza na SAFARI YA BUZWAGI iliyonihakikishia ajira ndipo nikasema kuwa NARUDI BUZWAGI kujiandaa na FUNGATE ambalo lilikuja kumleta MGENI MWEMA ambaye hatimaye akafunga safari nyingine kwenda kupumzika UFUKWENI MOMBASA na aliporudi ikazuka TAHARUKI kubwa inayokwenda kuishia kwenye UTATA...

Dah, sijui itakuwaje. Tusubirie...
 
Pamoja sn mkuu[emoji120]
 
Tuko
Na bado utata utaibua kisa kingine. Hii straight forward umeitendea haki .big up bishop
 
Shukran sana bishop,naamini washabiki wako kindakindaki tuna maswali lakini naamini yatajijibu mbeleni,afande koba,secretary wake Jason nafikiri utatuondolea huu utata!
 
Kongole kwako Bishop huwa na furahia Sana kazi zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran sana bishop,naamini washabiki wako kindakindaki tuna maswali lakini naamini yatajijibu mbeleni,afande koba,secretary wake Jason nafikiri utatuondolea huu utata!
Kubaki na maswali ndo kunakoleta mshawasha na raha ya stori. Hata hivyo mtakachokutana nacho ni UTATA mtupu...
 
Dah, Kiukweli imekua ni muendekezo wenye kuburudisha sana. Ubarikiwe sana mkuu
 
Kubaki na maswali ndo kunakoleta mshawasha na raha ya stori. Hata hivyo mtakachokutana nacho ni UTATA mtupu...
Kwa kweli ndio raha ya story zako,na mume wa muheshimiwa waziri sijui atabinjukiwa hukohuko south?wacha tukusubirie mtaalamu wetu utujibie haya maswali!
 
Haha! Naona umeamua kutangulia mbele, mkuu. Leo nina nafuu kidogo. Baadaye kidogo nitashusha vitu..
Naam shida ya hawa watu unapewa kazi alafu nyuma unapewa mtu wa kujufutilia kushindwa kwako na kushinda...na unichi wako!! Unafekishaje kazi ya 100% kuwin? Lazima upotee
 
Haha! Naona umeamua kutangulia mbele, mkuu. Leo nina nafuu kidogo. Baadaye kidogo nitashusha vitu..
Pole sana mkuu, Mungu akuponye chaaap kwa haraka hakika unatupa burudani na mafundisi...somo la kunusa hatari ni muhimu sana hata kwa maisha ya kawaida sio lazima uwe kipenyo.
 
Shukrani saaana! Umalaya wa Jason jamani! Ananikera mimi huyu!
 
Ungetuacha na utata ata kidogo mkuu na sio hili fukuto arosto unalotuachia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…