Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

utata.JPG

349

Dakika chache zilizofuata eneo lote la hospitali lilijaa Polisi na wanausalama wengine wakiwemo JWTZ, na kulikuwa na gari moja la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na walifanikiwa kuuzima moto kwenye lile gari jeusi aina ya Mark X lililolipuka. Polisi na maofisa wa usalama waliokuwa na silaha walishika doria kulinda eneo lile kuhakikisha hakuna uhalifu mwingine unaotokea. Maofisa wale walikuwa makini sana wakizungusha macho yao pembe zote.

Utepe maalumu wa njano maarufu kama ‘Barricade tape’ wenye maandishi ya “Police Line Do Not Cross” ukizuia watu kuvuka eneo lile la tukio ulikuwa umezungushwa na barabara ya kuingia na kutoka katika hospitali ile ya Ligula iliwekwa kizuizi cha askari. Kila mtu aliyetaka kupita eneo lile alisimamishwa, akahojiwa na kama alionekana hahusiki basi alizuiwa kupita.

Taarifa za tukio lile la kihalifu zilikuwa zimesambaa haraka sana mjini kama moto wa nyikani, makundi mbalimbali ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Mtwara yalizidi kukusanyika katika eneo lile la hospitali, watu wakubwa kwa wadogo, na walikuwa wanashangaa na wengine wakisimuliana jinsi walivyoshuhudia.

Nilitamani sana kujipenyeza katikati ya makundi hayo ya watu ili kutafuta lolote jambo ambalo lingetusaidia kwenye ung’amuzi wetu juu ya kile kilichokuwa kinaendelea pale Mtwara lakini muda haukuturuhusu kufanya hivyo. Bado tulikuwa na safari ndefu ya kuutafuta ukweli wa sakata lile lenye utata, na tulijua kuwa iwapo tungezubaa hata sekunde moja tu basi tungeweza kuwapa nafasi maadui wa taifa kuharibu ushahidi nyumbani kwa Samson Dadi ambako tulitakiwa kwenda, na pia tulihitaji kwenda kumhifadhi sehemu fulani salama mmoja wa wale watu tuliopambana nao ili apatiwe matibabu stahiki na kisha tumuhoji.

Tulijipakia kwenye gari letu na kuondoka tukiliacha eneo lile likiwa chini ya uangalizi wa wanausalama walioongozwa na RSO Mama Komba na Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), SACP Deus Kashani, ambaye sura yake ilionekana kusawajika sana kwa mawazo na kujawa mikunjo ya hasira na uchungu.

Suala la kutoa maelezo kwa viongozi wale wa usalama mkoani Mtwara, yaani SAPC Kashani na Mama Komba tuliliacha kwa wale askari wawili tuliowakuta wodini wakimlinda Samson Dadi ambaye sasa alikuwa marehemu, kwa kuwa walikuwa wameshuhudia kila kitu tangu mwanzo.

Wakati tukiondoka toka eneo lile SAPC Kashani alikuwa akiangaza macho yake pembe zote kama aliyekuwa anachunguza kitu. Alikuwa mwanausalama makini sana na mkakamavu asiyeruhusu makosa ya kipumbavu yaliyoashiria uzembe yatokee awapo kazini.

Nilimfahamu vizuri SACP Kashani, alikuwa mmoja kati ya askari waadilifu na waliofanya kazi kwa bidii kuhakikisha nchi inakuwa katika hali ya utulivu na amani. Kabla ya kupandishwa kuwa RPC wa Mtwara, SACP Kashani alikuwa Mkuu wa Upepelezi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni. Hakuwa na mzaha kabisa awapo kazini, angeweza kumfuatilia hata shetani katika harakati zake za kuharibu amani au maadili mema ya wana wa Mungu na akamtia mbaroni kisha akamburuza mahakamani, tena peke yake.

Wakati gari letu linaondoka pia niliwaona waandishi wa habari waliokuwepo eneo lile wakianza kumzonga wakitaka kupatiwa maelezo ya tukio zima, lakini SACP Kashani, kutokana na kuchanganyikiwa na mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkoa wake hakupenda kuongea hata na mmoja wao. Aliwaomba wawe wavumilivu, wasubiri kwanza ripoti ya wataalamu wa upelelezi.

Tukiwa barabarani tulikuwa makini sana kuhakikisha hakuna gari lolote lililokuwa likitufungia mkia. Tulikuwa tumejiandaa kwa mapambano endapo tungegundua kulikuwa na watu waliokuwa wakitufuatilia. Mateka wetu alikuwa amezirai na alikuwa amepatiwa huduma ya kwanza ili kuzuia damu isiendelee kutoka. Sasa Daniella akaanza kunielezea kuwa baada ya mimi kutoka mle wodini yeye alifanya uchunguzi mle wodini na kumpekua marehemu lakini hakupata chochote ambacho kingeweza kumsaidia.

Na alipotoka mle ndani ndipo akashuhudia wale jamaa wakiruka toka ndani ya gari, mmoja akaanza kupambana na mimi wakati yule mwingine akipotelea nyuma ya majengo ya damu salama.

Alichofanya ni kumfuata yule mwingine na kupambana naye, akammaliza na kuchukua ile bunduki yake aina ya US Barrett M82 kisha akaelekea kwenye lile gari lao na kuingia ndani ya gari ambapo almikuta dereva amekufa na kulikuwa na bunduki nyingine moja aina ya ile ile ya US Barrett M82 pamoja na maguruneti mawili ya kurusha kwa mkono. Akayachukua na kutoka haraka ndani ya lile gari huku akishangaa namna hawa jamaa walivyokuwa wamejipanga kisawa sawa na kwamba ndani ya gari lao kulikuwa na vifaa vya mawasilano muda wote. Alipotoka tu akaniona bado nikiendelea kupambana na yule jamaa.

Wakati akijiandaa kuja kunisaidia ghafla likaingia lile gari jeusi aina ya Mark X toka nje lililokuwa likielekea kule mahala nilikokuwa. Akaingiwa na wasiwasi kwamba gari lile nalo lilikuwa ni la wale jamaa tuliokuwa tukipambana nao kwa sababu alimwona mwanamume mmoja akiruka kininja toka ndani ya ile gari akiwa ameshika bunduki aina ya US Barrett M82, ndipo alipolitupia bomu la mkono gari lile na kulilipua.

“Dah, kweli hawa jamaa wamejipanga vilivyo!” nilisema huku nikitupa macho yangu kuangalia kwenye vioo vya pembeni kuona kama kulikuwa na gari lolote lililotufungia mkia. Halikuwepo. “Hata hivyo bado najiuliza na sipati jibu; watu hawa ni akina nani?”

“Ni vigumu kusema ni akina nani lakini ninaweza kusema kwamba watu hawa ni wapiganaji hasa wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu. Ni makomando hatari wanaotumia vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano. They are professionals…” Daniella alisema kwa msisitizo.

“Tukimbana vizuri huyu mwenzao basi tutaweza kuwafahamu watu hawa ni akina nani na ipi ajenda yao hadi kumteka Rais!” nilisema huku nikimtupia jicho yule mateka wetu aliyekuwa amepoteza fahamu. Daniella alikubaliana nami.

Hata hivyo akili yangu iliendelea kusumbuka nikijiuliza ingekuwaje endapo huyu mateka wetu asingetoa ushirikiano, je, tungefanyaje kuwajua hawa watu na kujua wapo nyuma ya nani? Nani alikuwa anawatuma na kwa ajili ya malengo gani?

Ndiyo maana tuliona pia kuwa kulikuwa na haja ya kupata majibu kwa kukutana na mjane wa Samson Dadi, na kama tungefanikiwa kuongea naye na kufanya uchunguzi ndani ya nyumba yake basi tungepata ngazi ya kutupeleka hatua nyingine.

Baada ya kuzunguka barabara kadhaa tukijaribu kumpoteza yeyote ambaye angejaribu kutufuatilia ili asijue tulipanga kuelekea wapi, hatimaye gari letu lilisimama kwenye nyumba moja kubwa iliyokuwa eneo tulivu kabisa la ufukweni la Chuno. Na hapo nikapiga honi mara mbili mbele ya geti la nyumba ile.

Mara tukaona lile geti likifunguka lenyewe pasipo kufunguliwa na mtu, nikaliingiza gari ndani ya uzio wa nyumba ile pasipo kusita na kwenda kuliegesha sehemu maalumu ndani ya uzio wa ile nyumba kubwa ya ghorofa moja iliyochukua eneo kubwa.

Ilikuwa moja ya nyumba salama na ya kifahari iliyo sehemu tulivu mno. Mimi na Daniella tukashuka na na hapo tukamwona mzee mmoja mrefu na mtanashati mwenye mwili wa kimazoezi akitutazama kwa makini na kisha akaachia tabasamu. mara moja tukatambua kuwa huyo ndiye mzee tuliyekuwa tumefahamishwa kuwa alikuwa Daktari Athuman Chitemo.

Tulimfuata pale alipokuwa amesimama tukamsalimia kwa heshima na tulipotaka kujitambulisha yule mzee akatukata kauli akisema kuwa tayari alikuwa anatufahamu.

“Msijali vijana wangu, Mama Komba amenipigia simu na kuniarifu juu ya kilichotokea hospitali. Ameniambia niwape msaada. Karibuni ndani,” Daktari Chitemo alisema huku akituangalia kwa makini.

“Tushukuru sana, mzee…" Daniella alisema kisha akaongeza, “Kuna mtu ndani ya gari anahitaji kwanza huduma.”

Tulimtoa yule mateka wetu na Daktari Chitemo akatuelekeza chumba fulani hivi cha kumwingiza yule jamaa, kilikuwa chumba kilichokuwa chini ya ardhi na kilionekana kuwa chumba maalumu cha matibabu kilichokuwa na mitambo na vifaa vyote muhimu vya tiba, kama ambavyo ungevikuta katika hospitali yoyote kubwa.

Daktari Chitemo aliifahamu vyema kazi yake kwamba ilikuwa imezungukwa na hatari muda wote, japokuwa alikuwa ameshastaafu kazi katika Idara ya Ujasusi alikokuwa akifanya kazi kama daktari, lakini hadi wakati huo bado aliendelea kutumiwa na Idara kwa kazi za dharura kama ile. Ndiyo maana nyumba yake ilikuwa imejengwa kwa namna ambayo usalama ulikuwa wa uhakika na alitenga chumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya maofisa na watu maalumu waliopaswa kutibiwa mahali salama pale wanapokuwa wameumia.

Alikuwa akiishi peke yake ndani ya jumba lile huku mke, watoto na wajukuu zake wakiishi Marekani na ndugu wengine wakiwa wamesahauliwa vijijini. Watu wengi waliolifahamu jumba hilo hawakupata kumfahamu mmiliki wake zaidi ya kumwona mzee mmoja ambaye alifahamika eneo lile kama mlinzi tu wa jumba hilo. Na mzee huyu alipoulizwa kuhusu mmiliki alidai kuwa aliishi nje ya nchi na hakujua ni nchi gani ila ilitokea mara kadhaa alikuja na hakukaa sana.

Hakuna kati yao aliyegundua kuwa mzee ambaye walimdhania kuwa ni mlinzi ndiye mmiliki wa jumba hilo, na ndiye huyu Daktari Chitemo. Jumba lake lilikuwa ndani ya eneo la ekari tatu hivi lililolimwa likapandwa miti na matunda na kuzungushiwa seng’enge na ukuta wenye mfumo maalumu wa ulinzi huku likifungwa umeme kwa namna yake. Lilikuwa na vyumba vya siri na milango ya siri ambayo mtu yeyote asingebaini bila matakwa ya mmiliki wake.

Wakati tukiwa ndani ya kile chumba maalumu tulichomwwingiza yule mateka, sikuacha kustaajabu jinsi mzee Chitemo alivyojiandaa sana. Alikuwa na kila kitu kilichohitajika ndani ya nyumba yake. Hii ilikuwa kama hospitali. Daktari Chitemo alituelekeza sehemu ya kumlaza yule mateka wetu, kwenye kitanda cheupe cha chuma na tulipomlaza vizuri tukamfunga pingu.

“Sasa sijui niwapatie kinywaji gani, vijana?" mzee Chitemo alituuliza baada ya zoezi zima kukamilika.

Nikasema haraka, “Hapana, Hapana, mzee Chitemo. Tunashukuru sana.” Mzee Chitemo akainua mikono juu kumaanisha kuwa, ‘kama mpendavyo.’

Hatukuwa na muda kabisa wa kupoteza, bado tulikuwa na safari ya kwenda nyumbani kwa Samson Dadi na baadaye tungerudi tena pale ili kumhoji yule mateka na lazima aeleze ni wapi walipompeleka Rais na nani aliyekuwa kiongozi wa genge lile. Whoever did this to our President must be in our hands by dusk tomorrow. Niliweka kiapo.

Lakini kama binadamu wengine, sikuumbwa kwa chuma wala mfupa. Nilitumia damu mwilini na ubongo kichwani mwangu. Kama binadamu wengine, mwili wangu ulijua kuchoka na ubongo wangu ulihitaji mapumziko. Kwa takribani siku mbili sasa si mwili wala akili yangu iliyokuwa imepata fursa ya mapumziko.

Muda wote nilikuwa mashakani, nikiwafuatilia watu hatari waliomteka Rais huku mimi pia nikifuatiliwa na watu hao hao, nikijua kuwa nawafuatilia watu hatari na vile vile kuwa nilikuwa nafuatiliwa na watu hatari. Kila dakika ilinikuta macho kimwili na kiakili, kuzisaka roho za watu hao huku nikiilinda roho yangu mwenyewe.

Kwa hali niliyokuwa nayo nilihitaji kuoga. Nilikuwa mchovu na mwenye njaa. Hali kadhalika, sikuwa nimechafuka tu bali kuchakaa. Mchanganyiko wa damu, jasho na vumbi mwilini mwangu ulinifanya nijihisi kunuka. Nilitamani sana nimwambie Daktari Chitemo anielekeze lilipo bafu niingine nijimwagie maji ya baridi na kisha nipumzike kidogo. Lakini sikuwa na muda huo. Tulikuwa na mengi ya kufanya. Awali ya yote, tulihitaji kwenda nyumbani kwa Samson Dadi… halafu tungeenda kuonana na mke wa Rais aliyekuwa amehifadhiwa kwenye nyumba salama mahala fulani akipatia huduma… kisha…

Daniella alinishtua na kuniambia kuwa tulipaswa kuondoka, akamuaga Daktari Chitemo tukimweleza kuwa tungerudi hapo baada ya saa mbili, mnamo saa moja ya jioni. Tukatoka na kuelekea kwenye gari letu tukimwacha Daktari Chitemo akianza kumshughulikia yule jamaa.

* * *

Endelea...
 
utata.JPG

350

Kizaazaa!




Saa 11:05 jioni…

MWILI wangu ulikuwa umechoka na tumbo langu lilinguruma kutokana na njaa lakini hiyo haikunizuia kuendelea na safari ya Majengo. Muda huu Daniella ndiye aliyekuwa kwenye usukani. Pamoja na uchovu wa mwili wangu lakini nilikuwa makini sana kutazama nyuma ili kujaribu kubaini kama kulikuwa na gari lililotufungia mkia. Nilifurahi kuwa hadi tukiwa katika Barabara ya Makonde sikuwa nimeona gari lolote nililolitilia shaka kuwa lilitufungia mkia nyuma yetu wakati tulipokuwa tukiendelea na safari yetu.

Wakati tukikaribia Tiffany Diamond Hotel, katika barabara ile ya Makonde, ghafla bodaboda moja ikakatiza upesi mbele yetu! Daniella alijitahidi kuikwepa bodaboda ile kwa kupeleka gari kando ambapo napo huko kulikuwa kuna gari aina ya Toyota Spacio lililokuwa linakuja nyuma kwa kasi, hivyo tukaishia kubamizwa ubavuni na kusababisha tafrani barabarani!

Daniella alifanikiwa kulimudu gari akiliegesha pembezoni mwa barabara ile huku akishuka haraka. Nami nikashuka.

Shit!” nilimsikia Daniella akilaani huku akisaga meno. Ile bodaboda iliyosababisha ajali hiyo ilitokomea isionekane wapi ilipoelekea. Hakuna hata aliyekumbuka kunakili namba zake.

Gari letu lilikuwa limebonyea kiasi upande ule liliobamizwa. Punde alitokea dereva wa gari lile aina ya Spacio lililotuparamia wakati Daniella akijaribu kuikwepa bodaboda. Alisimama akilitazama gari lake pasipo kuongea chochote, alibaki ameshika tamaa. Nilimtazama nikagundua kuwa alikuwa akifikiria kuhusu taa za gari lake zilizovunjika na kuharibu ile sehemu ya mbele ya gari lake upande wa kushoto.

Hey!” nilimwita yule dereva wa Spacio, akanitazama kwa sekunde kadhaa bila kusema neno.

“Dah, taa zangu na shoo ya mbele,” hatimaye yule dereva wa Spacio aliongea huku akionekana kama aliyetaka kulia. “Sijui nitamwambiaje bosi? Ndiyo kwanza leo siku ya pili tangu bosi anikabidhi gari hili!”

“Nipe namba yako ya simu nikurushie fedha ukarekebishe gari lako,” nilimwambia yule dereva.

“Hivi unajua thamani ya hizi taa wewe?” yule dereva aliniuliza kwa mshangao huku akionekana wazi kuanza kuchanganyikiwa.

“Najua, taa na kurekebisha hiyo sehemu ya mbele haizidi laki tatu na nusu,” nilimwambia. Akanitazama kwa mshangao. “Nitajie namba upesi.”

Yule dereva alishusha pumzi, akataja namba zake za simu, nikamtumia shilingi laki nne papo hapo kupitia huduma ya SimBanking. Ujumbe mfupi wa kumtaarifu kuwa ameingiziwa shilingi laki nne kwenye simu yake ulimfanya anitazame kwa namna ya kutoamini, uso wake ulichanua kwa tabasamu.

Hatukuwa na muda wa kupoteza wala kuwasubiri askari wa usalama barabarani kama walivyoshauri mashuhuda wa tukio lile. Tuliingia ndani ya gari letu, tukaondoka fasta. Dakika kumi baadaye tulikuwa katika Barabara ya Zambia tukiutafuta Mtaa wa Saadani.

“Hii ndiyo Saadani Street, sasa anza kuitazama hiyo nyumba namba M-16,” Daniella aliniambia baada ya kuiacha Barabara ya Zambia na kuingia katika mtaa mmoja ambao mwanzo sikuwa nimejua kama ndiyo ulikuwa Mtaa wa Saadani. Na hapo nikageuka na kuanza kuzitazama vizuri nyumba za mta ule. Ulikuwa ni mtaa wenye nyumba zilizojengwa katika mpangilio unaovutia.

“Ile pale,” Daniella alikuwa wa kwanza kuiona nyumba tuliyokuwa tukiitafuta lakini hakusimama, akaendelea mbele hadi mwisho wa barabara ya mtaa huo, nia ilikuwa kutafuta hakika kwanza kuwa hakukuwa na mtu aliyekuwa akitufuatilia.

Gari lilipofika mwisho wa mtaa nikafungua mlango wa gari na kushuka na hapo nikaanza kurudi kule nyuma kwenye ile nyumba tuliyoipita, nikimwacha Daniella akitafuta mahali pa kwenda kuliegesha gari kisha abaki nje akichunga usalama wangu. Wakati natembea nilipishana na watu wachache katika mtaa ule.

Saa yangu ya mkononi ilionesha kuwa ilikuwa imetimia saa kumi na moja na dakikia ishirini za jioni. Ilikuwa ni rahisi sana kuitambua nyumba namba M-16 katika mtaa ule kwani ilikuwa nyumba ya kisasa sana ikijitofautisha na nyumba nyingine zote za jirani, ikiwa imezungukwa na ukuta mrefu na mbele kulikuwa na geti kubwa jeusi.

Nilipofika pale nikagonga getini, sekunde chache baadaye mlinzi akafungua mlango mdogo wa geti na kunitazama. Alikuwa ni mwanamume mrefu mweusi mwenye umri kama wangu aliyekuwa amevalia sare zenye rangi nyeupe na nyeusi, pamoja na kofia ya bareti nyeusi iliyochoka, mkononi akibebelea bunduki aina ya shotgun.

“Naweza nikakusaidia?” yule mlinzi aliniuliza kwa sauti ya amri huku akinikazia macho.

“Naomba kuonana na mama mwenye nyumba,” nilimwambia kwa sauti tulivu huku nikimtazama katika namna ya kumkagua kuona kama alikuwa mlinzi mwenye maadili au pandikizi.

“Una miadi naye?” yule mlinzi aliniuliza huku akizidi kunikazia macho ya udadisi.

“Hapana. Ni dharura tu, kuna jambo muhimu nataka kuongea naye,” nilisema nikijitahidi kuwa mtulivu.

“Kama hauna miadi naye siwezi kukuruhusu kumwona,” yule mlinzi alisema kwa msisitizo huku akitaka kulifunga lile geti. Nikamzuia.

“Nimekwambia ni dharu…” nilisema lakini akanikata kauli kwa sauti iliyojaa hasira na dharau.

“Nimekusikia, na bila shaka nawe umenisikia. Siwezi nikakuruhusu kama hauna miadi!” yule mlinzi alisema huku macho yake yakianza kubadilika rangi na kuwa mekundu.

Nikasonya. Sasa nililazimishwa kufanya kitu ambacho hakikuwapo kwenye mipango yangu kwa kuwa sikutaka kujitambulisha kwake mimi ni nani na pia sikuwa tayari kuona muda wangu nilioutumia kuja hapo unakwenda bure.

Kufumba na kufumbua niliusukuma ule mlango mdogo wa geti ambao sasa alikuwa anaanza kuufunga, nikaingia ndani huku nikikidaka kichwa cha mlinzi huyo kwa kutumia mkono wangu wa kuume, nikakizungusha kidogo na kukikita kwa namna ya kumfanya apoteze fahamu, sikukusudia kumuua. Kisha nikamlaza kwenye maua na kufunga ule mlango mdogo wa geti.

Nikauendea mlango mkubwa wa barazani ambao niliamini ndiyo wa kuingilia sebuleni, nikagonga taratibu na kusubiria majibu.

“Karibu!” sauti ya kiume ilifoka tokea ndani, punde mlango ukafunguliwa na kichwa cha mtu kikachomoza kutazama nje.

Alikuwa mwanamume ambaye kwa kumtazama tu nilitambua kuwa alikuwa ndugu wa Samson Dadi kwa jinsi walivyofanana, alikuwa na weupe fulani na nywele nyingi. Alivalia shati la rangi ya bluu la mikono mirefu na suruali nyeusi ya kitambaa, miguuni akiwa amevaa soksi tu.

Alivyotazama nje akakutana na macho yangu akaonekana kushtuka kidogo, akanikazia macho kama aliyekuwa akinifananisha.

“Naweza nikakusaidia?” hatimaye aliniuliza huku akinikazia macho yaliyojaa udadisi. Nikagundua kuwa alishangaa kuona nikiwa nimevaa suti maridadi lakini iliyokuwa imechafuka kwa vumbi.

Endelea...
 
utata.JPG

351

“Ndiyo, bila shaka hapa ni kwa Samson Dadi, na wewe ni mdogo wake!” nilimwambia yule jamaa, akasita kidogo kisha akatikisa kichwa kukubali.

“Ndiyo, ila mimi ni kaka, si mdogo wake,” yule jamaa alisema.

“Mimi ni ofisa usalama,” nilijitambulisha huku nikimwonesha kitambulisho changu. “Nimekuja hapa kuonana na mkewe Samson.”

“Kuna tatizo gani ofisa?” yule mwanamume mlangoni aliniuliza upesi huku akionekana kushtuka sana. Macho yake yalibeba hofu.

“Hakuna tatizo kubwa,” nilisema nikimshusha presha. “Ila nahitaji tu kufanya naye maongezi.”

“Kuhusu sakata la Samson au kuna jipya?” yule mwanamume aliniuliza huku uso wake ukiwa bado umebeba hofu.

Sikuona sababu ya kujibu swali lake, nikamkazia macho mwanaume huyo huku nikikunja sura yangu. Na hapo nikamwona akinywea na kulazimisha tabasamu.

“Karibu, unaweza ukaingia tu,” yule mwanamume alisema huku akisogea kando kunipisha niingie.

Bila kusita nilizama ndani na kutokea sebuleni. Ilikuwa sebule kubwa iliyosheheni samani za kisasa zilizokuwa katika mpangilio mzuri. Katika sofa moja alikuwa ameketi mwanamke mmoja ambaye kwa kumtazama tu jinsi alivyo nilibaini kuwa ndiye aliyekuwa mke wa marehemu Samson Dadi.

Alikuwa mwanamke mnene, mfupi na mweupe kwa rangi ya ngozi yake. Muda huo alikuwa amevalia dera la bluu lenye naksi za rangi nyekundu na njano. Macho yake yalikuwa madogo, mashavu yake makubwa na kidevu kisichoonekana. Nilimsalimia kisha nikajikaribisha mwenyewe kwenye sofa mojawapo. Yule kaka wa Samson pia aliketi kwenye sofa lingine.

Japo niliweza kutambua kuwa alikuwa na hofu lakini alijitahidi kunikarimu kwa sauti nyembamba ya chini. “Karibu sana, kaka… sijui unatumia kinywaji gani?”

“Hapana, dada’angu, nashukuru wala usijichoshe. Nipo sawa,” nilimwambia kwa sauti tulivu huku nikimtazama kwa umakini.

“Hata juisi?” yule mwanamke aliniuliza huku akinitazama kwa makini.

“Basi nipatie juisi kama hutojali,” nilisema. Yule mwanamke akainuka na kwenda kwenye jokofu, akatoa jagi moja la juisi na bilauri, akamimina juisi kwenye bilauri na kunipatia. Nilipiga funda moja kisha nikajitambulisha.

“Karibu, sijui unataka nikusaidie nini?” yule mwanamke aliniuliza kwa sauti ya chini kama ambaye hakutaka mtu fulani aliyekuwa nje ya sebuleni ile asikie maongezi yetu.

Niliweza kuhisi kuwa alikuwa mwingi wa wasiwasi na alikuwa akiongea kwa woga. Pia nilibaini kuwa alikuwa bado hajapata taarifa juu ya kile kilichomtokea mumewe. Hali hiyo ikanishtua ingawaje nilijitahidi sana kuuzuia mshtuko wangu.

“Nahitaji kujua taarifa kuhusiana na mumeo, kujua kama ulifahamu chochote kuhusu mawasiliano yake na watu ambao uliwatilia shaka, natafuta namna ya kusaidia jambo hili,” nilisema. “Naomba ushirikiano wako kamilifu.”

“Bahati mbaya sina taarifa yoyote mpya. Zote nimeshatoa kwenu polisi,” yule mwanamke alisema kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa.

“Utaniambia tu hizo hizo ambazo ulizitoa. Kama nilivyosema hapo awali, nia yangu ni kuhakikisha haki inapatikana. Kama mumeo kaonewa basi ijulikane,” nilimwambia kwa sauti tulivu.

Hata hivyo niligundua kuwa mwanamke huyu hakuonekana mtu mwenye matumaini. Si bure, huenda askari waliomhoji walimtisha na njia walizotumia kumhoji hazikuwa rafiki au kulikuwa na jambo alilifahamu kuhusu mumewe lililomfanya asiwe na matumaini, au alikuwa hana imani kama mimi ningeweza kumsaidia, na hivyo alikuwa anatimiza tu wajibu kunijibu maswali yangu.

“Dada’angu, nipo hapa kwa ajili ya kuhakikisha haki inapatikana. Najua huna imani na mimi na pengine wenzangu wametumia njia za vitisho katika kukuhoji na sasa umechoshwa na mahojiano… na pengine waona yanakupotezea muda,” nilisema kwa sauti tulivu kisha nikaitazama saa yangu ya mkononi.

“Sura yako inanifanya nijisikie kukuamini ingawa roho hainiruhusu. Nadhani hujui, tangu niliposikia mume wangu amekamatwa leo saa tano na nusu asubuhi na baadaye mchana nikafuatwa mara mbili na maofisa wa usalama tofauti tofauti na kuulizwa maswali mazito mazito, na wakati mwingine kutishwa kwa sababu nisizozielewa… sasa nimeshindwa kufahamu ni ofisa gani hasa anahusika na kesi hii!” yule mwanamke alisema kwa kukata tamaa.

Muda wote yule kaka wa Samson alikuwa kimya akinitazama kwa namna ya kunisaili. Huenda yeye pia hakuwa na imani na mimi.

“Kwa sasa mimi ndiye nahusika na kesi hii, nimetoka Dar es Salaam kwa ajili ya jambo hili… hivyo tafadhali sana, naomba unipe ushirikiano wako," nilisema kwa sauti tulivu huku nikimtazama yule mwanamke machoni. Muda mfupi macho ya yule mwanamke yakawa mekundu.

Yule mwanamke alikuwa kimya kwa kitambo fulani. Ni kama vile alikuwa anavuta kumbukumbu, ila iliyokuwa inamchoma, uso wake ulijieleza kwa ndita za majonzi.

“Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita, alikuwa kuwa maisha yake yapo mashakani. Nilimuuliza kwa nini haendi polisi, akanijibu kuwa haitosaidia. Sikuelewa anamaanisha nini mpaka wiki iliyopita…” yule mwanamke alisema na kusita, akamtupia jicho shemeji yake.

“Alikwambia nini kinaweka maisha yake rehani?” nilimuuliza nikiendelea kuwa mtulivu.

“Hakuniweka wazi, aliniambia kifupi tu kuwa amelazimishwa na maofisa fulani wakubwa wa usalama kuidhinisha mzigo fulani toka kwenye meli moja ya nje uingizwe nchini, alisema kuwa mzigo huo ni hatari na ana wasiwasi unaweza kuleta taharuki. Aliambiwa jambo hilo libaki kuwa siri kubwa na endapo akitoa siri hii sehemu yoyote basi watamuua yeye na ukoo mzima,” yule mwanamke alisema huku akifuta machozi.

“Alikutajia majina ya maofisa hao?” nilimuuliza kwa sauti tulivu. Yule mama alisita kidogo, akainamisha uso wake na kupangusa machozi.

“Tiger na Chameleon… ila sina hakika kama ni majina yao halisi…” yule mwanamke alisema baada ya kufikiria kidogo.

“Umeshawahi kuwaona maofisa hao, namaanisha wameshawahi kuja hapa nyumbani?” nilimuuliza kwa shauku.

“Wao kama wao hawakuwahi kuja hapa ila siku moja tu waliwatuma wawakilishi wao kuteta na mume wangu. Mimi sikuruhusiwa kuwepo sebuleni wakati wanaongea mambo yao,” yule mwanamke alisema na kushusha pumzi.

“Kwa hiyo… ina maana mumeo aligoma kuidhinisha mzigo huo kuingia nchini?” nilimuuliza huku nikijaribu kuyapima maelezo yake iwapo yalikuwa na ukweli wowote.

“Ndiyo. Lakini alisema kama angekuwa hajaoa wala kuwa na watoto angesimamia msimamo wake lakini hakutaka kabisa familia yake na watu wake wa karibu waguswe na hivyo hakuwa na namna ya kufanya isipokuwa kuruhusu meli hiyo itie nanga bandarini. Hata hivyo nimekwamini ndiyo maana nakwambia lakini mwenyewe amenitaka sana nifunge mdomo wangu,” yule mwanamke alisema na kuanza kulia. Ikanibidi nipoteze kama dakika tatu kumbembeleza ili aweze kurudia kwenye hali ya kuongea.

“Kwani mna watoto wangapi na wapo wapi kwa sasa?” nilimuuliza yule mwanamke.

“Tuna watoto wawili, kwa sasa wapo shule boarding,” yule mwanamke alisema baada ya kusita kidogo.

Nilipomuuliza ni shule gani watoto wao wapo akanitajia. Kisha, nikawataka yeye na shemeji yake, kaka wa Samson wawe na ujasiri wa kupokea kile nilichotaka kuwaambia. Nikawapa taarifa za kifo cha Samson Dadi.

“Masikini mume wangu we-e-e!” yule mwanamke aliangusha kilio cha kuomboleza, akajitupa tupa juu ya lile sofa. “Mume wangu w-e-e-e, mume wangu umeniacha peke yangu. Umekwenda wapi, mume wangu?”

Huzuni pia ilimfika yule kaka wa Samson, akalia ingawa yeye hakulia kwa sauti. alilia kimya kimya. Ni michirizi ya machozi tu ilionekana kupasuka machoni mwake. Nikawasiliana na Daniella, kupitia kifaa maalumu cha mawasiliano, na kumtaka aje.

* * *

Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua ili kuujua utata uliogubika sakata zima la Harakati za Jason Sizya...
 
Mtanisamehe wakuu, sipo poa kabisa lakini nimeona nisiwaache hivi hivi Jumamosi ya leo, bora niwamegee kidogo. Tuombe Mungu atuweke hai, kesho nayo ni siku...
Bishop kama Bishop leo jumapili utakuwa uko madhabahuni...unaongoza ibada. Uko sawa tunaendelea ku enjoy na kujigunza, asante sana hatujapungukiwa kitu jmos njrma imekuwa kabisa na kipande ulichotuachia cha taharuki.
 
Baba Askofu pole sana na changamoto za afya, natumai utakuwa vema mapema iwezekanavo ili kuweza kuendelea na simulizi yetu pendwa. Nakutakia uponyaji mapema
 
Nawashukuru sana wakuu kwa kunitakia afya njema, ukweli hali yangu haikuwa nzuri kabisa ila kwa sasa nipo fit kiaina. Baadaye nitajitahidi kutupia simulizi ili tuianze weekend yetu vizuri...

Ahsanteni sana kwa kunivumilia[emoji120][emoji120]...
 
Habari Bishop mimi ni miongoni mwa wasomaji wakubwa wa riwaya humu Jf kwa kweli umeitendea haki hii Jamii forums umeingia kwenye rekodi ya wandishi ninao wakubali humu kama vile singanojr UMUGHAKA Patrick kifuku Kelvin Mponda na wengine wazuri wote
Rai yangu kwako ukipata nafas weka story ukiwa huna nafas endelea na majukumu mengine Asante
 
utata.JPG

352

Saa 11:55 jioni…

Sasa hali ndani ya sebule ya nyumba ya Samson Dadi ilikuwa imetulia kidogo, mke wa Samson alikuwa amenyamaza. Daniella akiwa amesimama alinitazama na kunipa ishara fulani kisha alimgeukia yule mwanamke na kusema, “Dada, kama nilivyokwambia mahali hapa kwa sasa si salama kwa sasa, umefika muda wa kukupeleka sehemu salama zaidi wakati mipango mingine ikifanywa.”

Yule mwanamke hakusema neno, alishusha pumzi ndefu huku akifuta machozi na kuinamisha uso wake chini. Kwa hali ilivyokuwa tulikuwa tumekubaliana kumhamisha yule mwanamke na kumpelekea nyumba salama kwa ajili ya usalama wake, na ile nyumba ya Samson Dadi ingebaki chini ya uangalizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, hasa baada ya kuwasiliana na RSO Mama Komba, na kutuahidi kuleta wanausalama wawili ili kuiweka ile nyumba chini ya uangalizi wao.

Pia Mama Komba alitueleza kuwa alikuwa kwenye mchakato wa kutuma mwanausalama kwenda shuleni kuwachukua watoto wa Samson Dadi na kuwapelekwa mahali alipo mama yao, hadi mambo yakae sawa.

Kwa hivyo, Daniella alikuwa na jukumu la kumpeleka mke wa Samson kwenye nyumba salama kwa kutumia gari letu na kisha kwenda kuzungumza na mke wa Rais, Mama Juliana Masinde. Na mimi nilitakiwa nitafute usafiri wa kunifikisha nyumbani kwa Daktari Chitemo kwenda kumhoji yule mateka wetu.

“Mama, naomba nenda chumbani kajiandae haraka, hatuna muda,” Daniella alimwambia mke wa Samson ambaye muda huo alikuwa akiinuka kwa kujizoazoa pole pole akisaidiwa na shemeji yake, yule kaka wa Samson ambaye aliitwa Jackson Dadi.

“Una uhakika utaweza kumfikisha huko peke yako?” nilimuuliza Daniella huku nikimtazama kwa umakini.

“Kama unadhani nilipewa ukomando kwa sababu ya sura na umbo langu, umekosea sana,” Daniella aliniambia kwa sauti kakamavu iliyojaa jeuri na kujiamini. Nilimtazama usoni nikaona macho yake yakimaanisha hivyo.

Yalikuwa ni macho ambayo yalifanana kabisa yale ya nyoka aina ya Koboko aliyeghadhabika. Yalikuwa makini mno kuliko macho ya simba jike mwenye watoto na yalikuwa kama yanayosema, “Laiti ungekuwa upande wa adui zangu ningekuonesha kilichomnyoa kanga manyoya ya shingoni.”

Nilitambua kuwa Daniella alikuwa jasusi mwenye mbinu na ujuzi wa hali ya juu akiwa amepata mafunzo ya ukomando nchini China na kufuzu, mafunzo ambayo hutolewa hatua kwa hatua. Kambi zote za mafunzo ya msingi huwa msituni, kwa nchi zenye misitu, na kwa baadhi ya nchi zisizo na misitu huwa hata mapangoni.

Katika kambi za ukomando wanajeshi hujifunza mambo mbalimbali kama vile ukakamavu, ujasiri, uvumilivu, kutumia silaha mbalimbali, kupigana, kujificha na kufichua, kukimbiza na kukimbia masafa marefu usiku na mchana kwa kutumia ramani, dira, jua, mwezi hata nyota. Na wakati wote hujifunza kuua bila kusita wala kuona kinyaa au kuchafukwa matumbo. Kuua kwa kutumia chochote kile.

Daniella alikuwa amepitia hatua zote na alikuwa ni komando aliyefuzu kwa kila idara japo kwa mtazamo wa nje alionekana ni mwanamke wa kawaida, mwanamke mzuri, tena ni zaidi ya uzuri wa haja. Mrembo kwa sura na umbo matata sana lenye kuweza kuitaabisha vibaya nafsi ya mwanaume yeyote.

Wakati mawazo hayo yakipita akilini kwangu Daniella alikuwa akinitazama kwa umakini kisha alinitoa kwenye mawazo hayo wakati alipoanza kunieleza wasiwasi wake kuhusu nyumba namba M-14 iliyokuwa mkabala na ile nyumba ya Samson Dadi. Alisema kwamba wakati akiwa nje aliwaona wanaume watatu wenye sura za kazi, wakiwa wamevalia nguo nyeusi, wakiingia humo. Hakujua waliingia humo kufanya nini, na hakujua kwa nini aliwatilia shaka. Lakini kwa maelezo yake alihisi tu si watu wema na hivyo alinitaka niwe makini na nyumba ile wakati tunatoka.

Kisha alitoka kwenda kusogeza gari na kuliingiza ndani ya uzio wa nyumba ya Samson Dadi, na wakati huo mke wa Samson Dadi alikuwa ameshajiandaa, shemeji yake akamsaidia kubeba begi lake hadi kwenye gari letu, wakaingia na gari likaondoka likituacha mimi na Jackson Dadi tukilisindikiza kwa macho hadi lilipopotea mbele ya macho yetu. Kisha Jackson aliondoka wakati mimi nikiwa bado nimesimama pale pale getini.

Yule mlinzi wa nyumba hiyo ambaye nilikuwa nimemzimisha sasa alikuwa ameamka na kuketi, kichwa kikimvangavanga. Nikashusha pumzi huku nikiitupia jicho nyumba namba M-14 iliyokuwa ikitazamana na ile nyumba ya Samson Dadi. Sikuona jambo.

Niliendelea kusimama pale nje ya geti la nyumba ya Samson Dadi nikijifanya kusubiri usafiri, nikarusha tena macho yangu kwenda kwenye ile nyumba iliyokuwa mkabala na pale niliposimama, nyumba ambayo Daniella alikuwa ameitilia mashaka. Bado sikuona mtu, lakini kabla sijageuza shingo yangu nikamwona mtu dirishani akichungulia. Kisha mtu huyo alitoka upesi pale dirishani na kupotea! Kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwangu.

“Hawa watu ni akina nani?” nilijiuliza kisha nikawaona watu wawili wakipita pale mtaani kwa mwendo wa taratibu, jirani kabisa na pale nilipokuwa nimesimama.

“Kwema, kaka?” walinisalimia kwa pamoja.

“Nyie mnaonaje?” niliwajibu huku nikiwatazama kwa umakini.

“Kama ilivyo!” wakanijibu kwa pamoja.

“Na iwe hivyo!” niliwajibu. Na hapo tukawa tumetambuana. Walikuwa ni maofisa wa usalama waliotumwa na RSO Mama Komba kuja kuweka uangalizi kwenye ile nyumba ya samson Dadi.

Hata hivyo hawakusimama, walipitiliza kwa mwendo wa taratibu kama waliokuwa wanaelekea mbele zaidi. Nami nikaondoka na kuwapita huku nikiwataka kuwa makini na ile nyumba namba M-14 iliyokuwa mkabala na nyumba ya Samson Dadi, kisha nikaongeza mwendo kuelekea sehemu ambayo ningepata usafiri.

Sasa nilikuwa nimeuacha mtaa ule wa Saadani na kuingia mtaa mwingine, nia yangu ilikuwa niende nikatokee Barabara ya Zambia, nikahisi nilikuwa nafuatiliwa! Kwa mahesabu yangu ambayo yalikuwa sahihi, kulikuwa na gari lililokuwa linakuja nyuma yangu, tena kwa kasi!

Basi nilichofanya ni kuongeza kasi ya mwendo wangu na nilipoifikia kona ya kwanza nikaikata na kuanza kutimua mbio. Na kabla gari hilo nililohisi kuwa lilinifuatilia halijachomoza, nikawa nimejibanza nyuma ya kibanda fulani cha duka kilichokuwa mbele ya nyumba moja kubwa!

Halafu nikachungulia kuangaza kule lilikokuwa likitokea lile gari. Punde nikaliona lile gari likipita hapo likiwa katika mwendo wa taratibu. Lilikuwa gari jekundu aina ya Mazda lenye vioo vyeusi visivyoonesha waliokuwemo ndani. Hata hivyo kioo cha nyuma cha dirisha kilikuwa kimeshushwa na hapo nikawaona wanaume wawili wakiwa wanachungulia na kurusha macho yao kutafuta kitu. Nyuso zao hazikuwa za amani.

Gari likapita! Na kama sekunde tatu tu baada ya gari lile kupita, nikasikia sauti kavu ya mtu ikifoka nyuma yangu kwa Kiswahili chenye lafudhi ya Kimakonde, “Unafanya nini hapo, bwana wewe!”

Nikageuka haraka kutazama kule ilikotokea ile sauti na hapo macho yangu yakakutana na macho ya mzee mmoja mfupi mwembamba ambaye kwa mwonekano wake tu nilibaini kuwa alikuwa Mmakonde. Mzee yule alikuwa amevalia kanzu na koti jeusi juu ya kanzu. Kichwani alivaa baraghashia ya kufumwa kwa mkono.

Sauti yake ilikuwa kali sana, na majibu yake niliyaona punde tu maana baada ya swali lake nikasikia sauti ya gari ikivuma na mara ikaja kutuama mbele ya ile nyumba! Nikagundua kuwa lile gari lilikuwa limerudi nyuma na kuja kusimama mbele ya kile kibanda cha duka. Nilipotazama kule kwenye gari nikawaona wanaume wawili wakishuka na mkononi walikuwa na bastola.

Endelea...
 
utata.JPG

353

Mmoja wa wale watu akaniona na kufyatua risasi mfululizo kunielekea! Nilikuwa mwepesi kuchupa na kujibanza kwenye ile nyumba kubwa nyuma ya mti mkubwa wa kivuli. Yule mzee wa Kimakonde aliyekuwa akinifokea muda mfupi uliokuwa umepita alikimbilia ndani!

Sikusubiri zaidi, nilitazama nyuma yangu yaani nyuma ya nyumba ile kubwa nikauona ukuta wa matofali, haraka nikaukwea kama nyani na kutua upande wa pili, nikaanza kutimua mbio kuufuata uzio mwingine wa matofali wa nyumba ile niliyoingia. Muda huo huo nikasikia vishindo vya watu wengine nao wakitua ndani ya uzio ule. Walikuwa ni wale wanaume wawili wakinifukuzia! Wakaanza kurusha risasi kwa pupa!

Haraka nikachupa kuuvuka ule uzio mwingine pasipo hata kuushika. Niliruka kama Samaki mkizi, nikatua kwa ustadi upande wa pili na kisha nikakimbia upesi kwa nguvu zote kuufuata uzio fulani wa makuti, na wakati nikiukaribia nikagundua wale waliokuwa wakinikimbiza walikuwa wametua ndani ya uzio ule. Wakaendelea kufyatua risasi kwa pupa na kusababisha taharuki kubwa katika mtaa ule ambao sikujua uliitwaje!

Katika kurusha risasi ovyo, risasi moja ilinipunyua sehemu ya begani na kunisababishia jeraha dogo. Hata hivyo sikusimama, niliendelea kukimbia kuokoa nafsi yangu. Nikafika mahala palipokuwa na ua wa mabati nikajificha. Wale jamaa walikuja hadi eneo lile, wakasimama wakiwa wameduwaa wasijue nimeelekea wapi.

Walitazama kushoto na kulia mimi nikiwa nawachora tu toka pale mafichoni. Hawakuweza kuniona. Kisha niliwaona wakitaka kuondoka ila mmoja akaonekana kama aliyehisi jambo, nikamwona akimshtua mwenzake huku akimwashiria kwa macho kutazama eneo nililokuwa nimejibana.

Sikuwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kupambana. Haraka nikachomoka toka mafichoni huku nikitua upande mwingine na kuwafyatulia risasi, kitendo ambacho hawakuwa wamekitarajia. Mimi sikuwa mkurupukaji kama wao, nilikuwa bingwa wa shabaha. Kila risasi niliyoachia ilitua mahali palipokusudiwa na hivyo ndani ya sekunde chache wote wawili walilala chini wakiwa hawana uhai na hivyo kunipa amani ya muda. Ndiyo… amani ya muda kwa kuwa nilijua kazi ilikuwa ndiyo kwanza inaanza.

Niliwapekua haraka haraka na kupata vitambulisho, kadi moja ya kibiashara na noti kadhaa. Niliichukua ile kadi ya kibiashara na kutoka hapo nyuma, nikakimbia na kwenda kutokea katika barabara ya mtaa mwingine. Nilipogeuka kutazama nyuma yangu sikuona mtu, nilikuwa mwenyewe sasa.

Mara nikaiona bodaboda moja ikija mbele yangu, nikaisimamisha na kumwamuru dereva wake ashuke, bastola yangu ikiwa imetuama vyema mkononi. Yule kijana akatii mara moja, nikaiparamia na kutimka.

Ila sikwenda nayo mbali sana, nikaiacha sehemu fulani kwenye kijiwe cha bodaboda, na hapo nikadaka bodaboda nyingine. Nayo iliponisogeza hadi sehemu fulani ambayo iliniridhisha, nikaiacha na kupanda teksi ambayo nayo ilinifikisha sehemu fulani nikashuka na kuchukua bodaboda nyingine…

* * *



Saa 1:05 jioni…

Muda huu ulinikuta nikiingia ndani ya nyumba ya Daktari Chitemo, ilikuwa ni baada ya mizunguko ya hapa na pale ili kuwapoteza maboya watu waliotaka kufuatilia nyendo zangu.

“Anaendeleaje?” nilimuuliza Daktari Chitemo huku nikiwa nimesimama kando ya kitanda nikimtazama yule mateka wetu. Muda huo alikuwa amerudiwa na fahamu zake.

“Kwa sasa hali yake si mbaya, kama unavyoona, amerejewa na fahamu na tayari nimemfunga Plaster Of Paris,” Daktari Chitemo aliniambia. Neno Plaster Of Paris lilimaanisha bandeji ngumu ambayo tumezoea kuita P.O.P.

“Kwa hiyo ninaweza kwenda kumfanyia mahojiano?” nilimuuliza Daktari Chitemo huku nikimtazama yule mateka kwa umakini. Uso wangu nikiwa nimeukunja.

“Nadhani ungesubiri japo siku mbili hivi kabla ya kumfanyia mahojiano ili hali yake iwe nzuri kidogo,” Daktari Chitemo alinishauri.

“Siku mbili? Hatuna muda kabisa…” nilisema. “We’ll take it from here.”

What!” Daktari Chitemo aliniuliza kwa mshangao.

Your job here is done, you can leave it to me now!” nilimwambia Daktari Chitemo kuwa kazi yake ilikuwa imeishia hapo na sasa angeniacha nifanye na kazi yangu. Daktari Chitemo alinitazama usoni na kuona kuwa nilikuwa namaanisha.

You are kidding, Jason… Huyu mtu bado anahitaji usimamizi na hawezi kuhojiwa kwa sasa,” Daktari Chitemo alisema kwa huzuni huku akimtazama yule mateka ambaye muda huo alikuwa ananitazama kwa namna ya kutia huruma.

“Nakushukuru sana daktari kwa yote uliyofanya kuhakikisha mtu huyu anazinduka lakini nasikitika kukwambia kuwa kazi yako imeshakwisha. Nioneshe chumba cha mahojiano ili kazi yangu ianze na kama kutakuwa na tatizo lolote nitakutaarifu,” nilimwambia Daktari Chitemo huku nikijitahidi kuweka huruma kando. Daktari Chitemo akaonekana kukerwa sana na kauli yangu, akanitazama kwa hasira.

“Jason, can we talk for a minute?” aliniuliza kwa sauti tulivu huku akijitahidi kuificha hasira yake. Tukatoka ndani ya kile chumba na kuelekea sebuleni.

What are you doing, Jason?” Daktari Chitemo aliniuliza kwa sauti tulivu huku akinitazama kwa makini usoni.

I’m doing my job, Doctor,” nilimjibu Daktari Chitemo kwa sauti tulivu.

“Jason, mbona unajiweka katika hatari kubwa! Huyu bwana bado anaumwa sana na afya yake imetetereka kutokana na kupoteza damu nyingi, anatakiwa uangalizi wa daktari. Kwa nini unakuwa mbishi?” Daktari Chitemo aliniuliza kwa mshangao, sauti yake ilikuwa tulivu lakini iliyobeba hasira na uchungu.

Doctor, this is my job and I’m going to do it the way I want. Huyu jamaa ana taarifa za muhimu sana ambazo ni lazima tuzipate leo hii hii. We don’t have that time to wait, so if you don’t mind, nioneshe chumba cha mahojiano nikafanye kazi yangu,” nilimwambia yule mzee kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa sikuwa na masihara hata kidogo na nilipanga kumfanyia mahojiano yule jamaa muda huo.

Daktari Chitemo alinitazama kwa kitambo fulani pasipo kusema neno kisha aliinuka kwa unyonge pasipo kusema neno na kuniashiria nimfuate. Nikainuka na kumfuata, tukaelekea kwenye ngazi za kushuka kule chini hadi kwenye chumba kimoja kilichokuwa na mlango wa chuma. Kilikuwa chumba cha siri cha mateso na kwa kukitazama tu usingeshindwa kutambua kuwa kilidhihirisha kila aina ya mateso.

Chumba kile kilikuwa na kioo kipana ukutani kilichomfanya mtu aliyekuwemo mle ndani ya chumba asiweze kumwona mtu aliyekuwa nje ya chumba, lakini mtu wa nje aliweza kumwona vizuri aliyekuwa mle ndani. Katikati ya kile chumba kulikuwa na viti viwili vya chuma na meza kubwa ya chuma, na kulikuwa na bomba refu la chuma lililokatiza katikati ya chumba kutoka upande mmoja wa chumba hadi mwingine ukutani.

Juu ya ile meza ya chuma kulikuwa na balbu ya umeme ya mwanga usiokuwa mkali sana kutoka katika dari ya chumba ikiwa imening’inizwa kwa waya mwembamba na mrefu. Na juu ya dari kulining’inizwa vyuma vifupi vilivyokunjwa na kuchongwa mbele yake mfano wa vyuma vya kuning’inizia nyama buchani.

Upande mmoja wa chumba kulikuwa na kitanda chembamba cha chuma chenye mikanda imara, mnyororo mfupi na pingu za miguuni na mikononi za chuma, na kando yake kulikuwa na meza ya kioo iliyowekwa vifaa mbalimbali vya mateso likiwemo sinia kubwa lenye gundi maalumu, kisu, mikasi, waya mwembamba lakini imara, koleo, nyundo na misumali, bomba la sindano na chupa kadhaa za dawa tofauti, dawa moja ni ile ambayo mtu akichomwa huufanya ubongo na akili yake iwaze kusema ukweli tu.

Endelea...
 
utata.JPG

354

Nililiridhika na kile chumba, nikarudi kwenye chumba cha tiba alimolazwa yule mateka na kusimama kando ya kitanda, nikamtazama kwa sekunde kadhaa na kushusha pumzi.

Now it’s just me and you. Today I’m your angel of death,” nilimwambia yule jamaa kuwa siku hiyo nilikuwa malaika wake wa kifo endapo asingesema ukweli, nikamwona akinitazama kwa macho yaliyotia huruma.

Nikamweka kwenye kitanda cha kusukuma kilichokuwa na magurudumu, pasipo kujali malalamiko yake kuwa alikuwa anaumia, kisha nikakisukuma kile kitanda hadi kwenye kile chumba cha mahojiano, nikamlaza yule jamaa juu ya kile kitanda chembamba cha chuma chenye mikanda imara, mnyororo mfupi na pingu za miguuni na mikononi za chuma, halafu miguu na mikono yake nikaifunga kwa mikanda imara pasipo kujali kama alikuwa anaumia.

Nilifanya vile kwa sababu nilifundishwa kutomwamini mtu yeyote hata marehemu, hivyo nilipohakikisha mateka wangu hawezi kuleta tabu yoyote nikavuta kiti kimoja na kukiweka mbele ya mateka huyo, nikaketi juu yake na kumtazama.

Now tell me, where is the President…?” nilianza kumuuliza yule jamaa nikitaka anieleze mahali walipomficha Rais lakini akanikatisha.

Go to hell!” yule mateka aliniambia kwa dharau huku akijaribu kunitemea mate usoni, lakini alikuwa dhaifu na hivyo yale mate hayakufika kwenye uso wangu. Nikamtazama na kuachia tabasamu.

“Ninakukumbusha kuwa hapa ulipo ni nusu ya jehanamu kwa hiyo nataka unijibu kiufasaha kila nitakachokuuliza na kitakachokuokoa utoke humu ndani ukiwa hai ni ukweli tu… Tell me the truth and you’ll get out of here alive,” nilimwambia yule mateka kwa sauti tulivu.

You go to hell. Huna hadhi ya kunihoji, kwanza nakuhurumia sana kijana sijui kwa nini unakubali kutumiwa kirahisi namna hii? Tafadhali achana na huu upuuzi unaoufanya na umwambie aliyekutuma kwamba hawezi kupambana na sisi,” yule jamaa alisema kwa dharau

“Ninyi ni akina nani? Na mmempeleka wapi Rais?” nilimuuliza kwa sauti tulivu pasipo kujali dharau zake.

“Unajisumbua sana asee!” yule jamaa alijibu kijeuri. “Sijui kwa nini unakuwa mgumu kunielewa? Kwa nini unaendelea kuhatarisha maisha yako na kuiweka familia yako katika matatizo makubwa? Tambua kwamba ndani ya muda mfupi ujao utajutia hiki unachokifanya.”

“Kuhatarisha maisha yangu ndiyo jambo ninalolipenda zaidi, na pia huwa napenda kukutana na watu wenye dharau na wanaojiamini kama wewe,” nilimwambia yule mtu huku nikichukua kitu kama mkasi chenye ncha kali sana.

“Sasa unataka kuni-kunifanya ni-ni-nini wewe?” yule jamaa aliuliza kwa woga.

“Usijali, we si jeuri na hutaki kujibu maswali yangu kwa upole, sasa utajibu kwa njia hii!” nilimwambia yule jamaa na wakati huo huo nikashusha kwa nguvu ule mkasi na kuuzamisha kwenye nyama ya paja lake la mguu wa kulia.

"Aaarrrggghhh!” yule jamaa alipiga kelele kubwa. Nikatulia kidogo na kumtazama usoni halafu nikarudia tena zoezi lile kwa mguu ule ule wa kulia. Akaendelea kupiga kelele kubwa.

“Ninyi ni akina nani na Rais mmempeleka wapi?” nilimuuliza kwa sauti ya ukali. Halafu nikatulia. “Niambie, ninyi ni nani na Rais mmemficha wapi?”

“Sijui!” yule jamaa alisema huku akigugumia kwa maumivu. Nikainua tena ule mkasi ili nikite juu ya mguu wake, akapiga kelele.

Please, stop that!” yule jamaa alilia. Nikamtazama nikiwa nimekunja sura yangu.

“Haya niambie, Rais yupo wapi na nani mkuu wenu?” nilimuuliza.

“Kweli mimi sijui chochote,” yule jamaa alisema huku akigugumia kwa maumivu makali aliyoyapata.

I think this is not working,” nilisema huku nikikirudisha kile kifaa chenye ncha kali, nikachukua bomba la sindano, nikavuta dawa fulani nyeupe toka katika kichupa kidogo. Yule jamaa alinitazama kwa hofu.

“Nilikuonya toka mwanzo lakini umepuuza. Utanieleza kila kitu leo vinginevyo kifo chako kitakuwa cha taratibu na cha mateso sana,” nilimwambia halafu nikadondoshea matone kadhaa pale kwenye nyama ya paja nilipozamisha kile kitu chenye ncha kali, sehemu ambayo ilikuwa inatoa damu.

Yule jamaa alijitingisha kwa nguvu pale kwenye kitanda kutokana na maumivu makali aliyoyapata huku akipiga kelele kubwa. Sikujali, nikachukua gundi na kumfunga mdomo ili asiweze kupiga kelele halafu nikadondoshea tena matone kadhaa pale kwenye paja nilipopachoma na kitu chenye ncha kali. Yule jamaa aliendelea kugugumia kwa maumivu makali. Kisha nikamfungua ile gundi niliyomfunga nayo mdomoni.

“Uko tayari kuniambia ninachokihitaji?” nilimuuliza wakati akiwa ndani ya maumivu makali sana.

You go to hell, you devil!” yule jamaa alisema kwa hasira, nikamfunga tena mdomo kwa ile gundi na kuchukua kisu, nikamkata kidogo shingoni halafu nikadondoshea matone kadhaa mahala nilipokata.

Yule jamaa alikukuruka pale kitandani kana kwamba alikuwa katika hatua ya kukata roho. Nilimwangalia kwa sekunde chache halafu nikamfungua ile gundi mdomoni.

“Uko tayari kujibu nilichokuuliza?” nilimuuliza yule jamaa lakini hakujibu kitu, alibaki akilia kwa maumivu makali.

C’mon, guy… tell me what I need to know!” nilisema kwa ukali nikimtaka aniambie kile nilichohitaji kukijua. Yule jamaa aliendelea kulia kwa maumivu makali sana aliyoyasikia.

Dah! Jamaa alikuwa na roho ngumu sana! Hata hivyo nilijua tu kuwa mwishoni lazima atapike kila kitu alichokuwa akikijua. Nilimwacha nikaelekea mezani na kuchukua kifaa kidogo cha kukatia, nikakiwasha na kukijaribu. Yule jamaa akanitazama kwa hofu usoni.

“Utanisamehe, umetaka mwenyewe tufike hapa tulipofika na nilikuonya toka mapema. I’m a monster na ninachokwenda kukufanyia kitabaki katika kumbukumbu za uzao wako daima. Nitakukata kidole kimoja kimoja nikianzia na vidole vya miguu na halafu nitakuja mikononi na halafu nitanyunyiza dawa hii inayouma. Ila ukitaka nisifanye hivyo nijibu haraka kile nilichokuuliza,” nilisema kwa sauti kavu.

Yule jamaa hakujibu kitu bado aliendelea kulia kwa maumivu makali. Nikakiwasha kile kifaa halafu nikakishika kidole cha mwisho cha mguu wake wa kulia na kukikata. Yule jamaa alipiga kelele kubwa sana.

C’mon, guy, usilazimishe tufike huku. Niambie kile ninachokitaka,” nilisema kwa ukali. Bado yule jamaa aliendelea kugaagaa huku akilia kwa maumivu makali mno.

“Bado unaendelea kuwa jeuri?” nilimuuliza huku nikiwaza kumbadilisha sura yake. Nikakishika kidole kinachofuata na kukikata. Yule jamaa akapiga kelele kubwa hadi sauti ikaanza kumkauka.

Please stop!” yule jamaa aliomba huku akilia kwa uchungu.

Are you ready to tell me what I want?” nilimuuliza.

I will tell you… I will tell you everything. Please stop hurting me…” yule jamaa alisema huku bado akiendelea kulia kwa maumivu makali.

Now tell me everything,” nilisema huku nikiwa nimevaa sura ya kazi iliyokuwa mbali na utani. “Sema, Rais yuko wapi na nani kawatuma kwenda kumuua Samson Dadi?”

“Sijui aliko Rais, mi nimekodiwa tu kumuua Dadi… kwa kweli sijui hasa kazi ni ya na-na-nani, aaarrgghh please don’t hurt me,” yule jamaa alilalama.

“Nani aliyekukodi na amekulipa nini?” nilimuuliza.

“Chameleon, Chameleon… ni-me-ko-diwa na Chameleon, oh!” yule jamaa aliongea kwa tabu huku akigugumia kwa maumivu, “ame-ni-ni-lipa vizu-ri…”

“Chameleon ndiye nani na yupo wapi?” nilimuuliza kwa shauku.

“Ni m-m-mku-u wa…” yule jamaa alikuwa akinieleza kwa tabu, muda huo nikahisi uwepo wa mtu mwingine sehemu fulani mle ndani. bila kusubiri nikachupa na kuanguka kando huku risasi zikipita na kumwingia yule jamaa pale kitandani.

Halafu nikasimama haraka na kujibana nyuma ya mlango wa kuingilia kwenye kile chumba, mlango ambao ulikuwa umefunguliwa nusu. Risasi za kutosha ziliendelea kumiminika toka pale mlangoni na kusambaratisha vitu vilivyokuwemo mle chumbani. Kisha ukimya ukatawala huku pande zote mbili, mimi niliyekuwa ndani na mtu aliyekuwa nje, kila mmoja akimtegea mwingine. Sote tulisubiri nani awe wa kwanza kujitokeza.

Niliendelea kubana kimya kabisa pale nyuma ya mlango. Baada ya takriban dakika tatu nikasikia sauti hafifu ya nyayo za mtu ikisonga kuingia ndani. Kwanza ulitangulia mtutu wa bunduki aina ya US Barrett M82 kisha mikono yenye misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu, halafu mtu kiwiliwili cha mmoja mrefu aliyezidi futi sita akiwa na mwili wa kimazoezi kikaingia. Yule mtu alikuwa kama kivuli.

Alikuwa ndani ya mavazi meusi na raba nyeusi miguuni na alivalia soksi nyeusi usoni. Wakati akivuta hatua fupi fupi kuingia ndani ya chumba kile huku akipokelewa na ukimya wa hali ya juu, nami nikaamua kujitokeza na kuweka mtutu wa bastola yangu kwenye kisogo chake.

“Tulia kama unanyolewa na weka bunduki yako chini,” nilimwamuru kwa sauti kavu.

Yule jamaa hakuwa mbishi, alifanya hivyo kwa kuinama ili aiweke ile bunduki chini, lakini alipokaribia kuiweka chini akafanya hila dhidi yangu kwa kunipiga kwa miguu yake akifanya kama anaruka sarakasi, kumbe hakujua kuwa alikuwa anapambana na mtu makini zaidi anayeongozwa na hisia ya sita. Nilikuwa nimeshamsoma kitambo tangu alipokuwa akiinama, na hivyo alipojaribu hila hiyo nilimkwepa na kumshushia pigo moja la teke kali la kuzunguka lililotua katika uti wake wa mgongo, yule jamaa akaanguka sakafuni akiwa hana uhai.

Mara nikahisi tena kuwa kulikuwa na mtu mwingine akiingia kimya kimya ndani ya kile chumba, nikageuka haraka huku nikiruka kando, bastola yangu nikiielekeza upande huo, na kwa kufanya vile macho yangu yakakutana na macho ya Daniella akiwa amesimama mlangoni bila wasiwasi wowote, alikuwa akinitazama kwa tabasamu.

“Dah! Naona jamaa amekutana na pigo la mauti!” Daniella alisema huku akitabasamu.

Yeah… pigo la kifo,” nilijibu huku nikigeuza shingo yangu kumtazama yule jamaa pale chini. Kisha nikamuuliza Daniella kwa mshangao uliochanganyika na wasiwasi, “Na imekuwaje huyu jamaa akafanikiwa kuingia hadi huku? Mzee Chitemo yuko wapi?”

“Yupo kule chumba cha tiba. Jamaa walimuwahi wakamdhibiti,” Daniella aliniambia huku akiusogelea ule mwili wa yule mtu na kuanza kuupekua.

“Walikuwa wangapi?” nilimuuliza Daniella kwa wasiwasi.

“Wawili… mmoja alibaki nyuma, nikawahi kumzimisha ndiyo nikaja huku,” Daniella alisema huku akitoa bastola moja aina ya Barretta, kete kadhaa za bangi na kitambulisho, toka kwenye mifuko ya yule mtu. Kisha alikitazama kwa makini kile kitambulisho kabla hajamaka kwa mshangao. “Kapteni Kaike!”

Nikakichukua kile kitambulisho na kukisoma. Yule mtu aliitwa Steven Kaike na alikuwa mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwenye cheo cha Kapteni.

* * *

Usichoke kuifuatilia simulizi hii hadi mwisho...
 
Back
Top Bottom