Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa akiachia ni full packageUsiikatishe nadhani tunasoma wengi kingine napenda style yako mzigo full bila makelele
Twende mwamba wee ucjali watu wanasoma kimya kimya!Dah! Ila inakatisha tamaa sana kutokana na mwitikio wa wasomaji humu, wanawaona wawili tu kama si watatu. Kuna wakati nafikiria kuikatisha...
Huyo Jason Sizya ni kiboko aisee.Hongera mkuu kwa kutuburudisha wasomaji wako.View attachment 2200867
110
“Usiseme hivyo Asia, nakupenda na nitakupenda hadi kifo kitakapotutenganisha,” niliongea kwa utulivu huku nikiruhusu tabasamu langu kuchanua usoni.
“Unanidanganya Jason, unachofanya ni kunifariji kama mtoto. Kwa kweli nafsi yangu inajuta kukufahamu. Umeuteka moyo wangu na sasa nashindwa kabisa kukuacha.”
“Nakuhakikishia kuwa nipo tayari kwa lolote mpenzi. Wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu,” niliongea huku nikizichezea nywele zake na hapo nikaona tabasamu hafifu likichanua usoni mwake.
“Kweli mpenzi?” Asia aliniuliza huku akiniangalia machoni. Sasa tabasamu liliupamba uso wake.
“Kweli kabisa nakuhakikishia,” nilimhakikishia.
“Lakini tuna tofauti kubwa, mimi ni Muislamu na wewe ni Mkristo, sasa tutaoana vipi?” Asia alisema. Nikafikiria kidogo.
“Vyovyote utakavyopenda wewe, ikiwa Kiserikali, Kikristo na hata Kiislamu pia… niko tayari kubadili dini kwa ajili yako!” nilisema kwa kumaanisha. Hata hivyo bado kauli yake kuwa alikuwa na kasoro kubwa iliyomfanya asiwe tayari kulala na mimi ilizidi kuniumiza kichwa, nikaona nimalize utata.
“Asia, sasa naomba uniambie ukweli… kwa nini hauko tayari kulala na mimi?”
Asia alionesha kushituka na uso wake ulionesha maumivu kiasi fulani. Tabasamu lililokuwa limetawala likayeyuka ghafla. Alibaki akiniangalia kwa kitambo kirefu akionekana kujishauri. akijaribu kutabasamu, alitaka kuendelea lakini hakufanya hivyo. Ilimchukua muda kujikusanya pamoja ili aweze kunieleza yaliyomsibu.
“Kwa kweli hata sijui nianzie wapi kukueleza… lakini kwa kifupi ni kwamba, nimekuwa nikiishi na Virusi vya Ukimwi kwa muda mrefu baada ya kuambukizwa na wazazi wangu…” Asia alisema sauti ya unyonge.
Habari ile ilikuwa kama pigo la kisu ambalo lilipenya mwilini na kuujeruhi moyo wangu. Nilishtuka sana na moyo wangu ulipiga mshindo mkubwa kama uliotaka kupasuka kwa mshtuko. Masikio yangu hayakuamini kile ambacho yalikuwa yakikisikia na ubongo wangu uligoma kabisa kukubaliana na kile nilichokisikia toka katika kinywa na Asia.
Jambo hilo lilikuwa kubwa mno na nilishindwa kulibeba kabisa. Nililiona jahazi la mapenzi yetu likienda mrama na mimi kama nahodha nilikuwa sina uwezo wa kulinusuru toka katika gharika lile kubwa.
“Jason, Wazazi wangu walishindwa kufuata taratibu za kiafya hasa ukizingatia kuwa kipindi kile bado wanasayansi walikuwa hawajagundua mbinu mbadala za kumfanya mtoto asipate maambuikizi ya ukimwi. Nilizaliwa nikiwa na virus vya ukimwi, na mama yangu kabla ya kufa alinikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia ndiyo maana pamoja na kuwa nakupenda sana lakini nimekuwa nikisita kulala na wewe…” Asia alisema huku akiniangalia usoni.
Nilivuta pumzi ndefu kisha nikazishusha taratibu. Jasho jepesi lilikuwa likinitoka mwilini na mapigo yangu ya moyo yalikwenda kasi sana. Hata hivyo nilijikuta nikimhurumia sana Asia.
“Nakupenda sana Asia, nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu japo umeniambia unaishi na virusi vya ukimwi, lakini tambua si mwisho wa maisha yako. Bado kuna mambo mengi ambayo tunaweza kufanya bila kuathiri maisha yetu,” nilimwambia Asia kwa sauti tulivu lakini iliyobeba huzuni kubwa ndani yake. Machozi yalikuwa yananilengalenga machoni.
“Lakini kwa tatizo langu sina hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…” Asia alisema kwa huzuni, nikamkatisha.
“Hapana, usiseme hivyo. Ungekuwa huna thamani kwangu nisingekuwa na wewe muda huu. Ni kwa sababu una thamani ndiyo maana unaona niko na wewe…” nilimwambia Asia kwa sauti tulivu.
“Unachokifanya sasa ni kunipa moyo tu. Hilo tu basi! Si zaidi ya hivyo,” Asia alisema kwa huzuni.
“Nikuombe kitu?” nilimuuliza huku nikimtazama moja kwa moja machoni.
“Ndiyo.”
“Naomba uniruhusu nikuoe, najua kuwa tukifuata ushauri wa kitaalamu tutaishi vizuri kama…”
“Jason!” nilikatishwa na sauti kali ya Jamila iliyotushtua sote, mimi na Asia, wakati tukiwa bado tumekumbatiana pale kwenye sofa tukipeana faraja.
Nikainua kichwa na ghafla nikakutana na kitu ambacho sikukitarajia kabisa. Jamila alikuwa amesimama mlangoni na alikuwa akitusogelea taratibu na kisha akasimama hatua kadhaa toka mahala tulipokuwa tumeketi kwenye sofa. Mkononi kwake alikuwa ameshika bastola. Sikujua aliitoa wapi na alikuwa amefika hapo muda gani.
“Jamila!” niliita kwa mshangao.
Asia naye alimwona na kunitazama, tukatazamana pasipo kusema chochote. Muda huo Jamila alikuwa anatetemeka kwa hasira.
“Jamila please… huhitaji kufanya hivyo tunaweza kuzungumza…” Asia alisema kwa sauti ya kutetemeka.
“Shut up! Nakuheshimu sana Asia na usitake nikufanyie kitu ambacho hutakisahau… tena usinieleze upumbavu wako wowote la sivyo nitaanza na wewe,” Jamila alisema kwa ukali kisha akaikoki bastola yake na kuielekeza kwa Asia.
“Jamila hebu acha utani na silaha za moto,” nilisema kwa sauti tulivu katika namna ya kumsihi Jamila. Hata hivyo macho yake hayakuonesha masihara hata kidogo.
“Nakujua vizuri Jamila, najua wewe si muuaji na huwezi kuniua, tafadhali weka bastola chini,” niliendelea kumsihi Jamila.
“Unanijua vizuri eh? Kwa taarifa yako huujui upande wangu wa pili… sasa leo nitakuonesha mimi ni nani!” Jamila alisema kwa hasira huku akiihamishia bastola yake kwangu, midomo ilikuwa inamtetemeka kwa hasira.
“Jamila tafadhali naomba upunguze hasira unaweza kufanya kitendo ambacho utakijutia maishani mwako. Tafadhali punguza hasira na uiweke chini bastola yako tuongee…” nilijitahidi kumsihi Jamila.
“Hakuna tena kitu cha kuongea mimi na wewe Jason. Umekwisha nionesha wazi kwamba mimi na wewe tumefikia mwisho bila hata kujali kama nimebeba mtoto wako tumboni. Hakuna kitu tunachoweza tukaongea tena. It’s over Jason… it’s over!” Jamila aliongea huku machozi yakimtoka, ni wazi alikuwa ameumia sana moyoni.
“Una roho ya kikatili sana Jason, pamoja na kujiweka wazi kwako bado umeamua kunigeuka na kunitupa kama takataka! Nimeumia sana kiasi ambacho sikutegemea. Maisha yangu yote niliyakabidhi kwako na sioni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi hapa duniani bila ya kuwa na wewe…” Jamila alisema huku machozi yakiendelea kumtiririka.
Sasa aliishika vyema bastola yake na kuielekeza kwenye kichwa changu huku kidole cha shahada kikielekea kwenye triga tayari kufyatua risasi.
“Jamila tafadhali acha utani, hiyo ni silaha za moto,” Asia alimwambia Jamila huku akipiga hatua za taratibu kumkaribia.
“Stop! Unaona nafanya utani we malaya? Unaona kama nawatania eh?” Jamila alisema kwa ukali na mara akaielekeza bastola kwa Asia na mlipuko mkubwa ukasikika. Wote tukaanguka na kulala sakafuni. Baada ya nukta kadhaa nikafumbua macho yangu taratibu, pembeni yangu alilala Asia na damu nyingi zikimtoka.
“Shetani mkubwa wewe! How could you do this?” nilijikuta nikifoka kwa ghadhabu.
“Usihofu Jason. Hata wewe utamfuata malaya wako muda si mrefu,” Jamila alisema huku akiachia tabasamu la kifedhuli. Ni wazi alikuwa amechanganyikiwa maana alianza kucheka pasipo sababu. Kisha akanyamaza na kunitazama kwa macho makali yaliyojaa chuki huku akiukaza mkono wake kuielekeza bastola yake kwangu.
Hapo akili yangu ilianza kufanya kazi haraka. Nilimtazama kwa umakini machoni nikijaribu kuyasoma mawazo yake. Kufumba na kufumbua nikajinyanyua toka pale sakafuni na kumrukia lakini kabla sijamfikia nikashtukia kitu fulani cha moto mkali kikipenya kifuani kwangu na kunitupa sakafuni kwa kishindo kikubwa.
Nikajikuta nikiwa katikati ya maumivu makali sana yasiyoelezeka, nilianza kutetemeka kama niliyekumbwa na ugonjwa mbaya wa degedege. Maumivu makali yalinitawala katika kifua changu, nikajishika kwenye kifua na kugundua kulikuwa na damu zikinitoka, ikanibidi niukaze mkono wangu ili kuzuia damu nyingi isiendelea kuvuja katika sehemu ambayo risasi ilipita.
Jamila alinitazama kwa hofu, akawa kama aliyerudiwa na fahamu zake, akaanza kuweweseka huku akiwa haamini kwa tukio alilolifanya. Aliitupa bastola yake sakafuni na kunisogelea, akapiga magoti na kunikumbatia huku akiangalia kifuani kwangu kisha akaanza kulia kwa uchungu.
“Jason, nilikuwa nakutania! Tafadhali usiniache…” Jamila alisema huku akilia kwa uchungu, alionekana kuchanganyikiwa sana kwa kitendo alichokifanya. “I’m sorry Jason! Please forgive me!”
Mara mlango wa sebuleni kwangu ukapigwa kumbo na hapo nikasikia sauti ya vishindo vya watu waliokuwa wakija mbio pale sebuleni, niliinua uso wangu kuangalia nikaona watu watatu, wanaume wawili na mwanamke mmoja aliyewafuata kwa nyuma. Niliweza kumtambua yule mwanamke, alikuwa mchumba wangu Rehema na alivaa gauni zuri la kitenge na kilemba kichwani.
“Oh My God! We binti umemuua Jason? Kwa nini umemuua Jason?” niliisika kwa mbali sauti ya Rehema akipiga ukelele.
Muda huo huo nikamwona Jamila akiniachia haraka na kuinuka huku akiwa ametahayari.
Taratibu nikahisi nguvu zikiniishia huku mwili ukizizima kwa kukosa uwezo wa kufumbua macho na hapo nikajikuta nikiwa katika hali nzito ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu ikiutawala moyo wangu. Na mara giza zito likaanza kutanda kwenye mboni zangu za macho na mwili wangu ukilegea, mapigo yangu ya moyo nayo yakaanza kudorora, mwishowe nikahisi roho yangu ikifika njia panda.
“Wewe simama na usijaribu kupiga hata hatua moja! Wewee, hebu mkamate!” kwa mbali nikasikia sauti ya mwanamume ikisema kwa ukali.
“Jason! Jasoon! Jasoooon amkaaa!” kwa mbali sana niliisikia sauti ya Rehema akiniita huku akilia.
Nilitaka kuinuka lakini badala yake nikaanza kujiona nikitumbukia kwenye shimo refu sana lilikokuwa na kiza. Nilijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini nilihisi sauti yangu haikuweza kutoka bali niliisikia akilini mwangu…
* * *
Mambo yanazidi kunoga. Endelea kuufuatilia mkasa huu wa kusisimua...
Nipo mpendwa, asante kwa kuniita japo kitambo kidogo nilikuwa sijaingi JF....Pamoja sana Mkuu[emoji1666]Karibuni wadau kwa stori nyingine ya kusisimua: the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tate Mkuu Bigjahman moneytalk marybaby nipo2 ram kisukari Smart911 Madame S carbamazepine Astelia culture gal [USER=448001]Prisoner of hope Mine eyes kuku mweus @Thad hearly Shunie Tumosa Mine eyes Kudo @swahiba92 @ludist Toyota escudo Clkey macson3 boga la kiangazi LEGE Smart911 Richard irakunda skfull popie @Krizy Beat hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie @Bughy Harry Mlenge Kacheda mjasiliamali Laki Si Pesa cocochanel big jambo mludego Shupavu Kacheda mjasiliamali Mweweso Songa Heri esiankiki mnadhimu mkuu wa jf red apple the-sniper MR KUO dan oseko Jackal kuku mweus mtugani wa wapi huyo chiqutitta ndukulusudicho ADK aggyd BAHARI J Litro [emoji68]
Duh! Belinda akafa kirahisi tu maskini🥲[emoji25]View attachment 2163558
10
Hata hivyo, kuna nyakati ambazo nilikuwa najiuliza kama hawa wanawake ni viumbe dhaifu kupita vyote duniani ama walikuwa viumbe majasiri kulikoni vyote? Kila nilivyofikiria uchungu wanaoupitia katika kutubeba kwenye matumbo yao na kisha kutuzaa katika hali ya uchungu mkubwa, basi nilipiga goti na kuwavulia kofia ya heshima ingawa kulikuwa na mengine lukuki ambayo kila nilipoyafikiria nilijikuta kichwa kikiniuma sana.
Pamoja na kufikiria hivyo bado tabia ya kuwabadili wasichana kama nguo sikuiacha na ilinifanya nigombane na kaka yangu Eddy mara kwa mara, kwani yeye aliamini kuwa mwanamke alistahili kupewa heshima yake kama ilivyokuwa kwa mwanamume.
Mara nyingi Eddy aliniasa kwa kuniambia kuwa “mwanamke unayemchezea leo, ndiye atakayeolewa na mwanamume mwenzako kesho! Je, unajua mke utakayemuoa anafanywa nini leo na mwanamume mwenzako?”
Neno ambalo halikukauka mdomoni mwa Eddy kila mara aliposikia nina uhusiano na mwanamke mwingine lilikuwa ni “Jason, tafadhali usipende kuchezea hisia za mwanamke.” Alipenda kunikumbusha kuhusu tukio la kuhuzunisha la kifo cha mwanadada Belinda Mwikongi, aliyekuwa binti wa Diwani wa Kata ya Gongoni katika Manispaa ya Tabora, mzee Albert Mwikongi.
Belinda alikuwa msichana aliyetokea kunipenda sana na siku zote aliamini kuwa ningemuoa baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kama ambavyo nilikuwa nimemuahidi, kumbe moyoni kwangu sikuwa na mpango wowote wa kumuoa bali nilipanga kumchezea tu.
Kilichomfanya Belinda anipende sana na kuniamini zaidi ni kwa sababu mimi ndiye ‘nilimwondolea utoto’ wake baada ya kumlaghai sana na kisha kumwingiza katika dunia ya wakubwa. Hiyo ilikuwa ni baada ya kufanya mtihani wake wa mwisho wa kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Uyui hapo Tabora.
Wakati nakutana na Belinda alikuwa na umri wa miaka 18 na alikuwa bado hajamjua mwanamume. Nilipomuuliza kwa nini alikuwa amejitunza hadi wakati huo aliniambia kuwa mtu pekee ambaye alipaswa kuchukua zawadi hiyo ni mume wake pekee na asingeweza kumwamini mtu mwingine yeyote hata mimi japo alikuwa ametokea kunipenda.
Kiukweli nilitumia kila njia hadi kumnasa Belinda na kumwingiza kwenye himaya yangu. Belinda hakuwa mtu wa wanaume kabisa na hakujua chochote kuhusu ulimwengu wa mapenzi. Kilichonisaidia kumnasa ni kwamba nilikuwa mchezaji mzuri sana wa mpira wa kikapu, mchezo ambao Belinda alikuwa anapenda sana kuuangalia.
Hapo ndipo ukawa mwanzo wa uhusiano kati yetu, uhusiano ambao mwanzoni ulianza kwa sharti kwamba tusingekuwa tunakutana faragha mpaka pale ambapo tungeingia kwenye ndoa, hasa kwa kuwa nilikuwa nimeahidi kumuoa pindi tu akishamaliza masomo yake.
Hata hivyo, kutokutana faragha lilikuwa sharti gumu sana kwangu lakini nililipokea kwa shingo upande kwa sababu nilijua tu kuwa ingetokea siku angefanya kosa kwa kuingia kwenye kumi na nane zangu. Siku moja tu alipojisahau nami nikautumia mwanya huo huo kumfunga goli la kiufundi, na hapo ndipo pazia la mapenzi yetu lilipofunguka rasmi.
Wakati matokeo ya mtihani wake yakiwa ndiyo kwanza yametoka ndipo alipogundua uwepo wa mabadiliko mengi katika mwili wake ikiwemo kutapika na kutoona siku zake za kila mwezi. Aligundua hilo baada ya kuona imepita miezi miwili na hali yake ya kimwili ikianza kubadilika.
Baada ya kugundua jambo hilo alinitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu ya mkononi kunieleza kuhusu mabadiliko katika mwili wake na kwamba mama yake alikuwa ameanza kumshtukia na hivyo alikuwa ana mpango wa kumpeleka hospitali kupimwa ujauzito. Kiukweli jambo lile lilinishtua sana, na hivyo nikawa natafuta namna ya kujinasua kwa kuwa sikuwa tayari kuingia kwenye majukumu ya kutunza familia.
Kesho yake alinipigia simu lakini sikupokea akaamua kunifuata nyumbani na kunikuta nikiwa na msichana mwingine aliyeitwa Rahma, na hapo nikaamua kumkana jambo lililomuumiza sana. alilia sana lakini bado nilishikilia msimamo wangu ule ule ya kwamba simjui, na wala sikujali. Hata hivyo, japokuwa sikuamini kuwa duniani kulikuwa na mapenzi ya kweli lakini ukweli ulibaki kuwa Belinda alikuwa ananipenda kikweli kweli!
Pamoja na kumkana kwamba sikumjua lakini chozi lake liliniumiza sana na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi hatia ikinikaba moyoni mwangu. Hata hivyo, sikutaka kuonesha kama nilikuwa nimeumizwa wakati nilipokuwa mbele ya Rahma, msichana ambaye siku hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana naye.
Siku iliyofuata kaka yangu Eddy alinipigia simu na nilipopokea tu nikashtushwa na sauti yake ya huzuni, akanipa taarifa za kuhuzunisha kwamba Belinda alikuwa amekufa baada ya kunywa sumu. Na kwamba alikuwa ameacha barua fupi iliyokutwa kando ya maiti yake, chumbani kwake ikielezea kuwa “aliamua kujiua kwa sababu asingeweza kuishi huku akimshuhudia mwanamume ampendaye akimsaliti na wanawake wengine…” hata hivyo, katika barua hiyo hakuwa ametaja jina la mwanamume huyo.
Taarifa ile ilinichanganya sana na kifo cha Belinda kiliniumiza sana nikiamini kuwa mimi ndiye niliyesababisha mauti yake. Hata hivyo, sikuwa na namna nyingine yoyote ya kufanya kwani maji yalikwisha mwagika na yasingeweza tena kuzoleka. Ilibidi nimsahau na maisha mengine yaendelee.
Eddy alitarajia kuwa kifo cha Belinda kingekuwa funzo kwangu lakini haikuwa hivyo, ni kama niliyekuwa na pepo la ngono, niliendelea na maisha ya ‘kula ujana’ na walimbwende wa kila rika, kila umbo, kila rangi na kadhalika kila nilipopata nafasi ya kufanya hivyo. Niliamini kuwa maisha yangu yasingeweza kuwa ya furaha kama nisingeiridhisha nafsi yangu ilivyotaka.
Nilikula ujana kwa kubanjuka na warembo mbalimbali nikiamini kuwa huo ndiyo ulikuwa muda wangu sahihi wa kuyafurahia maisha yangu maana kuna wakati ungefika nisingeweza tena kubanjuka nao, hata mwanamuziki Samba Mapangala aliwahi kuimba kuwa “Vunja mifupa kama bado una meno…”
______
Itaendelea...
Pamoja sana aseeeee daaaaaaaaaaahView attachment 2205708
114
Saa 11:30 jioni…
Siku hiyo hiyo ya Jumapili nilifika nyumbani kwa Dk. Camilla Mpogoro, dada wa Rehema, nikiwa nimeongozana na Eddy na Swedi. Safari hii Mama hakutaka kuongozana nasi bali alibaki nyumbani. Tulimkuta Dk. Mpogoro na mumewe na walitupokea vizuri ingawa Dk. Camilla hakuonesha ule uchangamfu aliokuwa nao siku zote, na baada ya kuniona alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi.
Ni hapo nilipopata taarifa zilizozidi kuninyong’onyesha kabisa, nilitamani nami ninywe sumu nijiue kwani sikuona kama nilistahili kuendelea kuvuta pumzi huku nikiwa mwenye hatia.
Taarifa nilizopata pale ni kwamba hali ya Rehema ilikuwa mbaya sana kwani alikuwa amepooza kabisa na mwili wake haukuweza hata kutikisika, macho yake yalifumba na hakuweza hata kufumbua jicho, na ilibidi baba yao mzee Benard Mpogoro aje kwa ndege ndogo ya kukodi na kumchukua, akapelekwa Muhimbili ambako haikusaidia na hivyo akapelekwa nchini India kwa matibabu na huduma zaidi.
Nilishindwa kujizuia kutokana na taarifa ile, nikajikuta nikitokwa na machozi muda wote. Sikupata neno ambalo lingeweza kuelezea uchungu niliokuwa nao kwa wakati ule. Ilikuwa ni kama filamu ya kusikitisha na ilikuwa vigumu sana kuamini kilichotokea.
Baada ya taarifa ile Dk. Mpogoro alinipa barua ambayo ilikuwa imeandikwa na baba yao akiagiza kwamba nipewe. Niliipokea huku nikiitazama ile bahasha kwa wasiwasi, sikutaka kuifungua pale. Na baada ya maongezi mafupi tuliaga na kuondoka, na tulipofika tu nyumbani niliharakisha nikaifungua ile barua, iliandikwa:
Ndugu Jason,
Pamoja na yote yaliyotokea, nakuombea kwa Mungu upone haraka na uendelee na majukumu yako. Nakuomba samahani kwa kuwa nimeshindwa kuja hospitali kukujulia hali kwa sababu nimekuta hali ya binti yangu Rehema ni mbaya sana, amepooza mwili baada ya kushuhudia kile kilichotokea nyumbani kwako, na inaonesha wazi kuna mambo yaliyokuwa yanaendelea chini kwa chini yanayonifanya nisifahamu lengo lako kwa binti yangu ni nini hasa!
Japokuwa hatujui mlikutana vipi na wapi na ni kwa kiasi gani mnapendana lakini kuna maamuzi ambayo sisi wazazi wake tumeamua kuyachukua, kwanza tumeamua kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi. Jambo la pili ambalo najua linaweza kuwa gumu kwako lakini hatunabudi kulifanya, nakuomba achana kabisa na binti yangu Rehema. Tumegundua kwamba umekuwa ukimuumiza sana kihisia na hutaki kubadilika, kumbuka wewe ndiye chanzo cha binti yetu kupatwa na matatizo haya.
Sitaki tena kusikia masuala ya mahusiano kati yako na Rehema na kama unataka kuendelea na uhusiano na binti yangu itabidi usubiri kwanza nife lakini kama bado nipo hai sitaruhusu kamwe. Naomba usinielewe vibaya Jason, nakupenda kwa sababu wewe ni kijana mchapakazi, jasiri, msomi makini na mwenye nidhamu lakini hufai kuwa na binti yangu.
Najua hili ni jambo ambalo hukulitegemea na linaweza kukuumiza sana lakini kuna nyakati katika maisha lazima tufanye maamuzi magumu. Sisi wazazi tumefanya maamuzi hayo kwa faida yako na ya binti yetu.
Nasisitiza tena: kaa mbali na binti yangu.
Meja Jenerali Benard Mpogolo…
_____
Nilipomaliza kuisoma barua hiyo nilihisi kama mwili wangu ulikuwa umepigwa na shoti kali ya umeme. Nilihisi ubaridi mkali ukinitambaa mwilini na mwili ukifa ganzi. Barua ile ilikuwa na maneno mazito sana na ambayo katu sikutegemea kuyasikia katika wakati ule ambao nilihitaji sana kupata faraja. Nilihisi kuadhibiwa na dunia.
Kulikuwa na maumivu makali sana ndani ya moyo wangu, maumivu ambayo hayakuelezeka. Ilikuwa ni zaidi ya maumivu. Niliwaza sana kuhusiana na mustakabali mzima wa maisha yangu bila Rehema; niliwaza nilikotoka, niliko na kule nilikokuwa nikienda, nikajiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa au laana. Nilijikuta nikilia sana. Eddy na Swedi walijitahidi sana kuniliwaza.
“Eddy, najua nimekosea sana lakini sistahili kuadhibiwa na dunia kiasi hiki! Kwa nini?” nilisema kwa uchungu huku nikitokwa na machozi.
“Jason, jikaze wewe ni mwanamume… kumbuka kila jambo hutokea kwa sababu maalumu, hivyo mtegemee Mungu pekee, yeye atakushindia. Be strong my brother,” Eddy aliniambia huku akinipiga piga taratibu mgongoni.
“I’m hurt, brother. Kwa nini yule mzee anifanyie hivi?” nilisema kwa uchungu mkubwa.
“Calm down. Huna sababu ya kuumia sana, kumbuka akipangacho Mungu binadamu hawezi kukipangua… kama Rehema ndiye mwanamke uliyeandikiwa kuwa naye basi siku moja utakuwa naye. Kumbuka mlikotoka, kumbuka kakuvumilia kwa mengi! Mapenzi yana nguvu kuliko kitu chochote kile, mapenzi yana uwezo hata wa kuusambaratisha mlima. Kama ni kweli wewe na Rehema mnapendana siku moja mtakuwa pamoja, niamini ndugu yangu,” Eddy aliniambia na kauli yake ikaungwa mkono na Swedi.
Sikwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kukubaliana na matokeo, kwani hata kama ningefanya nini tayari ilikwisha tokea, nisingeweza kuurudisha wakati nyuma. Sasa nilikuwa nimekosa mwana na maji ya moto. Asia na Jamila walikuwa wamekufa, na sasa Rehema alikuwa kitandani akipigania uhai wake huku baba yake akinitaka nikae mbali na binti yake!
Sikuwa na mtu wa kumtupia lawama kwani yote hayo yalisababishwa na tamaa yangu, tamaa ya kutamani kila kilichofichwa ndani ya andawea ya kila msichana mrembo aliyepita mbele yangu.
Nilihisi kuchanganyikiwa sana nikiwaza kuwa kila sehemu ambako ningepita macho ya watu yangekuwa yakinitazama kwa kunisuta; wapo ambao wangekuwa na hasira juu yangu, wapo ambao wangenitazama kwa dharau na baadhi wangenitazama kwa huzuni. Kwa kweli sikujua nifanye nini!
Sasa nilianza kutamani ardhi ipasuke ili nijifiche ndani yake kukwepa macho ya jamii. Nikajikuta nikipata wazo la kunywa sumu ili nami niondoke hapa duniani.
Huu ni mwisho wa Msimu wa Pili kwenye mfululizo wa Harakati za Jason Sizya. Usikose Msimu wa Tatu hapa hapa katika mkasa uitwao “Fungate”.
Ndugu mwandishi bishop,nakukubali sana brother,tunasoma bure bila kulipia,watu kama hawa wasikukatishe tamaa,nimesoma simulizi zako zote brother,hii ndio staili yako,na ninzuri,shukran sana brotherStori nzuri ila kusifia mavitu ndio inaboa.... screen kubwa mara handsome...nikisoma stori ya mhusika huwa natengeneza muonekano wake mimi mwenyewe bila kusaidiwa na muandishi.....yote kwa yote tunashukuru kwa stori.