Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

utata.JPG

392

Saa 11:25 jioni…

Muda wa saa kumi na moja alasiri ulinikuta nikiwa ndani ya ukumbi maalumu wa mikutano katika majengo ya Ikulu jijini Dodoma nikimsubiri Rais Albert Masinde.

Pamoja nami ndani ya ukumbi ule alikuwemo Daniella, maofisa wa usalama kutoka SOG na Taasisi ya SPACE, viongozi waandamizi wa taasisi za ulinzi na usalama, Baraza la Usalama la Taifa, na wanausalama wastaafu ambao baadhi yao walikuwa wamechangia kufanikisha harakati za kumkomboa Rais Masinde.

Wastaafu niliowaona hapo ni pamoja na mkurugenzi mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rajabu Kaunda; Askofu Jerome Masinde; Daktari Chitemo; na Othman Mwambe.

Hadi muda huo tulikuwa tukimsubiri Rais Masinde ambaye alisubiriwa kulihutubia taifa.

Rais Masinde alipaswa kulihutubia taifa tangu saa kumi kamili za jioni lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizobainisha kuwa jumuia wa siri ya Triangle walikwisha weka mizizi yao kila sehemu na wangeweza wakafanya jambo lolote na muda wowote wautakao, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa alitoa maelekezo kwa mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya kuhakiki upya usalama katika ukumbi ule wa habari Ikulu.

Kufuatia agizo hilo waandishi wote wa habari na wageni waalikwa walitolewa nje, ukumbi ukakaguliwa upya na wanausalama huku taarifa za kila mmoja aliyefika hapo zikihakikiwa, na ndipo wakaruhusiwa kuingia mmoja mmoja huku wakikaguliwa. Baada ya kuhakikisha ukumbi uko salama, tukaendelea kumsubiri Rais ili sasa aweze kulihutubia taifa.

Ndani ya ukumbi ule kulikuwa na runinga kubwa mbili zilizotundikwa ukutani, ambazo zilirusha habari mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Muda wote macho na masikio yangu yalikuwa makini kutazama na kusikiliza kila habari iliyotangazwa. Kwa siku kadhaa sikuwa zimesoma magazeti wala kufuatilia taarifa mitandaoni na hivyo sikujua nini kilikuwa topic kubwa mtaani.

Habari zote nilizozisikia kwenye runinga sikuzifurahia. Ilikuwepo habari niliyoitaraji. Niliisubiri kwa hamu, si kwa ajili ya kuihitaji bali kwa ajili ya kuona ingewasilishwa vipi, na wananchi wangeipokeaje!

Macho katika kioo cha runinga, uso ukiwa umechoshwa kwa matangazo yote yaliyokuwa yakiendelea. Kadiri muda ulivyozidi kwenda nilianza kushangazwa na ukimya wa ajabu pasipo kuambiwa kwa nini Rais alikuwa hajatokea hadi muda huo licha ya kwamba uhakiki wa usalama katika ukumbi ule wa Ikulu ulikuwa umefanyika upya na wahusika kuridhishwa na hali ya usalama.

Saa yangu ya mkononi ilisema kuwa dakika sabini na tano zilikwisha vuka tangu itimie saa kumi kamili za jioni, yaani ilikuwa imeshatimia saa kumi na moja na dakika ishirini na tano.

Nilishachoshwa kusubiri na nilianza kutamani kuondoka ndipo tulipopewa taarifa kuwa Rais Masinde alikuwa anaingia, mara mlango maalumu wa kuingilia Rais katika ukumbi ule wa habari pale Ikulu ukafunguliwa huku ulinzi mkali ukiwekwa wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Albert Masinde akijitokea na kwenda kusimama katika kiti alichoandaliwa.

Halafu matangazo yaliyokuwa yakiendelea kwenye vituo mbalimbali vya runinga yalikatizwa ghafla na wimbo wa Taifa ukapigwa. Baada ya wimbo huo, sauti nzito, yenye majonzi na msiba mkubwa, ya Rais Albert Masinde ilisema: “Habari za jioni Watanzania wenzangu?”

Kisha, tofauti na ilivyozoeleka kuwa hotuba ya Rais ilikuwa ikiandaliwa, safari hii hakuwa na karatasi yoyote ya hotuba iliyoandaliwa na wala Rais hakuwa akisoma popote, maneno yote aliyatoa kichwani na alizungumza kwa hisia kali sana…

“Awali ya yote ninapenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwa hai hadi leo hii na kuja mbele yenu niongee nanyi machache kuhusiana na maswala kadhaa muhimu kwa taifa letu, ikiwa ni pamoja na mambo yaliyojitokeza kwa siku tatu hizi ambayo wengi wenu hamyajui. Kwa kweli kuna mambo kadhaa makubwa kwa taifa letu ambayo yamenilazimu nije mbele yenu leo…” kufika hapo Rais alinyamaza, akameza mate halafu akaendelea.

“Kwa muda sasa tumekuwa katika mchakato wa kuandaa muswada wa sheria ya haki za binadamu. Muswada ambao umekuwa na changamoto nyingi kwani ndani yake kuna vipengele ambavyo vinatambua haki za makundi ya watu wanaojihusisha na mapenzi na ndoa za jinsia moja, haki ya kutoa mimba, biashara ya mihadarati pamoja na mambo mengine kadhaa ambayo yanakwenda kinyume kabisa na tamaduni zetu na hata mafundisho ya dini zetu…

“Kumekuwa na shinikizo kubwa toka kwa nchi tajiri na jumuia za siri zenye nguvu kiuchumi, wakizitaka nchi zetu za Afrika zihakikishe zinapitisha sheria za kutambua haki za makundi niliyoyaeleza. Nchi nyingi za Afrika, kwa uoga na unafiki, tayari zimekwisha pitisha sheria hii na chache ikiwemo Tanzania bado hatujafanya hivyo…” Rais alinyamaza kidogo kabla ya kuendelea.

“Binafsi, nilijaribu kulitafakari swala hili kwa kina na kusikiliza maoni ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na nikaona kuwa siko tayari kuona taifa likiangamia kwa kupitia mikono yangu. I must stand up and fight. Sitaki kuona watoto wetu wakija kuishi katika taifa ambalo nimeshiriki katika kuiharibu misingi yake…

“Niliweka bayana ndani ya kikao cha Baraza la Mawaziri na sasa naweka bayana kwenu wananchi kwa kutangaza kuufuta muswada huo wa sheria za kijinga, jambo hili limeonekana kutowafurahisha wakubwa na hivyo likakaribia kuyagharimu maisha yangu… kama isingekuwa jitihada za Idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa, iliyopambana usiku na mchana kuhakikisha wanazuia hujuma mbaya iliyoandaliwa dhidi yangu na taifa langu, niseme tu ukweli hivi sasa Watanzania mngekuwa katika maombolezo ya kitaifa…

“Ninafahamu kwamba kuna baadhi ya Nchi, vikundi na watu binafsi ambao hawalitakii mema taifa hili, hawa ndio walioandaa mpango wa hujuma kuhakikisha natekwa nyara na kulazimishwa kusaini makubaliano ya kuisaliti misingi ya taifa hili iliyowekwa na waasisi wetu, wakati nikiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mtwara…

“Huenda baadhi yenu mlishangaa kukatishwa ghafla kwa ziara yangu mkoani Mtwara na mimi kutoonekana hadharani, jambo lililoambatana na matukio kadhaa ya kigaidi yaliyoanzia hapa jijini Dodoma na baadaye kule Mtwara… matukio haya yamesababisha vifo vya Watanzania wenzetu huku wengine wakijeruhiwa…

“Niwe mkweli, ndani ya nchi hii zipo chembechembe za usaliti. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wote waliohusika katika hujuma hii ni watu wakubwa tu au waliopitia nyadhifa kubwa serikalini. Baadhi yao kwa sasa tunawashikilia na pindi uchunguzi ukikamilika tutawafikisha mahakamani. Wengine akiwemo mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais, na hata mke wangu Mama Juliana Masinde wamekufa katika sakata hili… pia wamo baadhi ya wanajeshi wetu waliotusaliti na wengine waliokodiwa kama mamluki toka nchi kadhaa kuja kusaidia kuihujumu nchi hii…

“Sasa, kuna baadhi ya Nchi za Jumuia ya Madola, tunazifahamu kwa majina, zipo mbioni kutangaza kususia mkutano wa Nchi za Jumuia ya Madola unaotakiwa kufanyika Ijumaa wiki hii hapa Jijini Dodoma kwa kisingizio kuwa hakuna usalama nchini Tanzania, yote hii kutaka kuihujumu nchi hii…

“Kwa kuwa wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kwenye hujuma hii wameonesha hawaitakii mema nchi ya Tanzania, sasa ninatangaza rasmi kuwa kikundi ama Nchi yoyote iliyoshiriki kwa namna moja ama nyingine ihesabike kuwa adui wa Tanzania, tuwaeleze ukweli kuwa hatuogopi na hatuyumbi. Tupo tayari kulinda mipaka na rasilimali zetu kwa gharama yoyote…

“Shime Watanzania, tushikamane na tuliombee taifa letu lizidi kuwa imara na salama… Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. Ahsanteni sana kwa kunisikiliza…” Rais Masinde alimaliza hotuba yake halafu akainuka na mara moja akazungukwa na walinzi wake, kisha huyo akaondoka zake kupitia mlango ule ule alioingilia.

_____

Endelea...
 
utata.JPG

393

Saa moja baadaye, mnamo saa kumi na mbili na dakika ishirini, mimi na Daniella tulikuwa ndani ya chumba maalumu cha mikutano cha Rais Masinde katika Ikulu ya Dodoma. Rais Masinde alikuwa ameomba kuongea nasi wawili tu ofisini kwake.

Wakati wa maongezi yetu, Rais Masinde aliwaagiza wasaidizi wake kutuandalia vinywaji ambavyo tungevihitaji. Hata hivyo tuliamua kuwa wazalendo kwa kunywa Konyagi. Kila mmoja wetu alikuwa na bilauri ya Konyagi, mvinyo unaozalishwa nchini Tanzania kwa kutumia zabibu za Dodoma. Rais alikuwa anakunywa sharubati ya mchanganyiko wa embe na pasheni.

“Hakika ninyi ni mashujaa ambao nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwapata. Nchi hii inapaswa kujivunia watu kama ninyi,” Rais Masinde alisema kwa furaha baada ya wasaidizi wake kutoka na kutuacha peke yetu. “Nimepewa taarifa zenu zote jinsi mlivyohangaika usiku kucha mkikumbana na misukosuko mingi, ninathubutu kusema kuwa ninyi wawili ndiyo mlikuwa mmeushikilia moyo wa nchi hii.”

Hatukumjibu bali tuliinamisha vichwa vyetu kwa heshima kukubali sifa alizotumwagia. Mara Rais Masinde akaonekana kukumbuka jambo.

“Hivi mmepata mahitaji yote?” Rais Masinde alituuliza huku akitutazama kwa umakini.

“Usijali, mhesimiwa Rais, tumepata kila kitu,” niliwahi kusema.

Good!” alisema Rais Masinde na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. kisha akaongeza, “Natumai mmefuatilia hotuba niliyoitoa jioni hii?”

“Ndiyo mheshimiwa Rais!” mimi na Daniella tulijikuta tukiitikia kwa wakati mmoja na kutazamana.

Halafu nikaongeza, “Hongera sana, mheshimiwa Rais. Hakika umeingia katika historia ya dunia kama Rais shujaa asiyeyumba. Kitendo hiki ulichokifanya leo naamini kila mwananchi huko aliko anakupongeza kwa ushujaa huu. Hakuna aliyetegemea kama ungekuwa na ujasiri mkubwa wa namna hii. Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa kuyazingatia maadili ya nchi.”

Rais Masinde alinyanyua bilauri yake ya sharubati na kupiga funda kubwa kisha akafumba macho kwa sekunde kadhaa akiusiklizia ubaridi wa ile sharubati wakati ikishuka kooni kwake. Kisha akasema, “But… it wasn’t that easy, young man!

I know!” nami nilimjibu pasipo shaka yoyote.

Imagine, unatoka kwenye situation kama yangu halafu unatakiwa utoe hotuba kama ile…” Rais Masinde alisema na kuongeza, “…leo nina furaha kubwa kwani nimefanya jambo ambalo sikutegemea kulifanya. Kwa muda mrefu nilikwisha choshwa kuwa kibaraka wa mataifa makubwa lakini sikuwa na ujasiri wa kuweza kupambana nayo. Nimekuwa Rais kivuli kwa muda mrefu na sitaki kuendelea kuwa kivuli kwa kuwaachia watu wengine wafanye uamuzi juu ya nchi hii…

“Wananchi waliponichagua walikuwa na uhakika mkubwa wa maisha yao kuboreka lakini mpaka leo bado sijaitimiza ahadi hiyo. Nilifanywa kibaraka lakini sasa nimeamua kutoka kuwa kibaraka wa mashetani hawa na kuwa Rais wa Watanzania. Nataka niisafishe nchi. Nataka niondoke madarakani taifa likiwa safi kama lilivyoachwa na waasisi wetu.”

Kufika hapo Rais Masinde alinyamaza na kuigugumia sharubati yote iliyokuwemo katika bilauri yake.

“Mheshimiwa Rais, niseme tu hiki ulichokifanya umedhihirisha wazi kuwa wewe si mtu wa kutaka kutumiwa. Sisi tutakuwa nawe bega kwa bega kuhakikisha unafanikiwa kwenye misheni yako,” Daniella alisema baada ya kupiga funda la Konyagi na kuikita bilauri yake juu ya meza ndogo iliyokuwa mbele yake.

“Ahsante sana, binti… Ninaamini kwa uongozi wa Mungu tutapambana na kulishinda genge hili lenye kutaka kuiharibu dunia. Niseme tu, karibu sehemu kubwa ya watu wanaonizunguka si wazuri kwa kuwa nilipewa maelekezo ya kuwateua, kwa hiyo utaona ni namna gani tulivyo na vita ngumu. Kinachoniumiza moyo ni kuwa wananchi hawajui kuhusu genge hili bali wananifahamu mimi. Nchi ikiyumba lawama zote zitaniangukia…” Rais Masinde alisema kwa huzuni.

Kisha kikakotokea kitambo kifupi cha ukimya kabla Rais Masinde hajavunja ukimya huo. Alikuwa anazungumza kwa huzuni kubwa. “Kingine kibaya zaidi, hata mke wangu Juliana alikuwa upande wao!”

Hatukushangaa sana maana tayari tulikwisha ambiwa kuhusu jambo hili na Askofu Masinde. Ndipo sasa ukafuata wakati ambao Rais Masinde aliamua kutusimulia mambo ambayo, kwa kauli yake mwenyewe, watu wachache sana waliyafahamu.

Alitusimulia jinsi alivyokutana na mwanadada Juliana Isidory Magupa ambaye baba yake alikuwa Mtanzania mwenyeji wa Mwanza lakini mama yake akiwa na asili ya Rwanda.

Wawili hawa walikutana masomoni katika Jimbo la Texas nchini Marekani, wakati yeye Masinde akichukua Shahada ya Pili ya Mawasiliano kwa Umma. Juliana yeye alikuwa anachukua Shahada ya Kwanza ya Sheria.

Huko ndiko uhusiano wao ulipoanzia na baadaye walikuja kufunga ndoa baada ya Albert Masinde kuamua kubakia pale chuoni kufundisha.

Jambo ambalo hakulijua ni kwamba tayari Juliana alikuwa mwanachama wa jamii ya siri ya Triangle na alikuwa ameshapata mafunzo mbalimbali ya kijasusi, na mojawapo ya masharti aliyokuwa akiyafuata ni kutozaa, ndiyo maana katika ndoa yao hawakubahatika kupata mtoto, ila Albert alikuwa na watoto mapacha aliowapata kabla hajakutana na Juliana.

Wakati Albert Masinde akifundisha chuoni, Juliana alikuwa akizunguka sehemu mbalimbali duniani kama mwanaharakati wa kupagania haki za binadamu na kuna wakati alianza kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa wanaharakati duniani.

Baada ya miaka kadhaa ya kufundisha huko Marekani, Juliana alimshawishi Masinde kuingia kwenye siasa na kuahidi kumsaidia kwa kila hali hadi afikie nafasi ya juu ikiwemo kuwa mkuu wa nchi. Jambo hili lilikuwa gumu sana kwa Albert Masinde kwani hakuwahi kufikiria kuwa mwanasiasa na hakujua angeanzaje.

Ndipo Juliana alipoanza kumkutanisha na watu mbalimbali mashuhuri pasipo kumwambia ukweli kuwa walikuwa wakitoka katika jamii ya siri ya Triangle, na watu hao waliahidi kumsaidia Masinde kufikia ndoto hiyo.

Akaacha kazi na kurudi Tanzania ambako aligombea ubunge na kushinda kwa kishindo, kisha Rais wa wakati huo, Kingoba Mgaya, akamteua kuwa Waziri wa Tamisemi na baadaye alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje. Hapo ndipo nyota yake ilipong’ara. Akajulikana kila kona ya nchi.

Miaka mitano baadaye wakati Rais Mgaya akijiandaa kustaafu, katika mchakato wa kumtafuta mrithi wake ndipo jina la Dk. Albert Masinde lilipopenya kimiujiza na hatimaye kuwa mgombea Urais wa Chama tawala.

Sasa wakati akitusimulia, Rais Masinde alikuwa anadhani kuwa huenda zilitumika nguvu za ziada zikiwemo zile za giza katika kumfanya akubali kila kitu alichoambiwa na Juliana na hata kwenye mchakato ndani ya chama.

“Natambua kuna mambo mengi machafu mke wangu aliyafanya ikiwemo kujiingiza katika imani za kishetani. Alikuwa na nguvu za ajabu akifanya mambo ambayo wengine hawawezi kuyafanya, na ilifikia hatua ya kunieleza kuwa hata mimi ningeweza kuwa na uwezo kama ule endapo ningehitaji. Uwezo wa kufanya mambo makubwa kushinda uwezo wa mwanadamu,” Rais Masinde aliongea kwa huzuni.

So sorry for that, Mr president. Sikujua kama umepitia mambo magumu namna hiyo,” nilisema kwa huzuni huku nikimtazama Rais Masinde usoni. Niliyahisi maumivu aliyokuwa akiyapitia wakati huo.

“Ni kweli, Jason, nimepitia mambo mengi magumu sana katika kipindi hiki cha urais wangu. Mambo mengine siwezi kuwasimulia… kwa muda mrefu nilitafuta upenyo wa kuniwezesha kuachana na watu hawa lakini nilishindwa. Hili si jambo jepesi. Ni jambo la hatari kubwa kwani hawa jamaa ni watu hatari kama nilivyoeleza lakini pamoja na hatari hiyo sasa nimeamua kupambana nao,” Rais Masinde alisema.

Kisha aliitazama saa iliyotundikwa ukutani mle ofisini kwake na kugutuka kwa mshtuko. Nami niliyapeleka macho yangu kuitazama saa ile, nikagundua kuwa ilishatimia saa moja kamili za jioni. Muda huo Rais alitarajiwa kupumzika.

Mara wasaidizi wake waliingia na kumpa taarifa kuwa muda wa kupumzika ulikwisha fika na kwamba tulipaswa kuondoka na kumwacha rais apumzike. Rais Masinde akainuka na kutupa mkono. Tukaagana na kutoka.

* * *

Endelea...
 
utata.JPG

394

Binti shushushu…




Saa 1:15 jioni…

WAKATI tukiwa pale nje ya viunga vya Ikulu ya Chamwino, Dodoma, tukijiandaa kuondoka ili kuingia kwenye gari aina ya Mercedes Benz la rangi nyeusi ambali lilikuwa litupeleke maeneo tuliyofikia, nilishtuka kusikia nikiitwa jina langu. “Jason!”

Kilichonishtua si kusikia jina langu likiitwa bali kusikia ile sauti iliyoliita jina hilo. ilikuwa sauti nyororo ya kike, sauti ambayo nilihisi kuifahamu. Naam! Nilishapata kuisikia kwa ukaribu zaidi ikininong’oneza jambo sikioni. Nikahisi moyo ukinilipuka.

Sauti ile wakati ikiniita iliambatana na mchakato hafifu wa hatua za mtu aliyekuwa akija upande wangu kwa mwendo wa haraka na nilipogeuka nikashangaa sana kumwona Amanda, dada wa Sofia akinijia kwa mwendo wa haraka.

Amanda alikuwa amevaa suti nadhifu ya kike ya rangi ya kijivu na alikuwa amevaa kifaa maalumu cha mawasiliano kwenye sikio lake. Uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu pana. Hakuonekana kushangaa kuniona pale Ikulu.

“Jason, unatakiwa ofisini kwa mkuu wa itifaki, mara moja,” Amanda alinipa ujumbe huku akinitazama usoni kwa umakini, kisha alimweleza dereva ambaye alitakiwa kutupeleka kwenye maeneo yetu kuendelea na safari ya kumpeleka Daniella kule alikofikia.

Niliagana na Daniella nikimweleza kuwa ningempigia simu baada ya kutoka pale Ikulu kumjulisha, maana tulipanga kwenda sehemu kwa ajili ya kujipongeza baada ya kazi ngumu ya kumkomboa Rais. Na nilimpania kweli kweli!

Nikiwa bado katika mshangao, Amanda aliniongoza hadi kwenye ofisi niliyoitwa, tulitembea kimya kimya bila kuongea hadi tulipofika kwenye mlango wa ofisi hiyo. Akagonga mlango mara moja na kuufungua kuniruhusu niingie.

Niliingia mle ofisini na kumwacha Amanda akiwa amesimama nje, na hapo nikajikuta nikiwa katika ofisi pana na nadhifu sana, ofisi ya mkuu wa itifaki. Mle ofisini nilimkuta Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, David Mshana; Mkuu wa Itifaki Ofisi ya Rais, Hassan Mambo; na Mkuu wa SOG Kanali Othman Mjaka, wakiwa wameketi kwa kikao cha faragha.

Nilisimama kwa ukakamavu na kupiga mguu chini kutoa heshima ya kiaskari. Wale wakuu wakaitikia salamu yangu.

“Nimeitika wito, mkuu,” niliongea huku nikiwa bado nimesimama kikakamavu. Sikujua has ani nani kati yao aliyekuwa ameniita pale.

“Jason Sizya!” mkurugenzi mkuu David Mshana aliita jina langu kisha akinielekeza kwa mkono sehemu ya kuketi.

“Naam, mkuu!” nilijibu kwa heshima huku nikiketi juu ya kiti nilichoelekezwa nikiwa tayari kusikiliza nilichoitiwa.

“Najua umejiuliza kwa nini umeitwa hapa na pengine hukutarajia kutukuta mimi na mkuu wako wa kikosi…” mkurugenzi mkuu David Mshana alisema huku akinitazama usoni. “Usijali, japokuwa habari ninayokwenda kukupa ilitakiwa ifuate utaratibu husika lakini nimeona si vibaya kukwambia leo, ukajua mapema…”

Moyo wangu ulipiga kite kwa nguvu na mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio isivyo kawaida, hata hivyo milango yangu ya fahamu ilikuwa makini zaidi huku nikijaribu kuishirikisha akili yangu kikamilifu katika kunifikishia taarifa.

“Kwanza kabisa Idara ya Usalama wa Taifa imekutazama kwa jicho la pekee sana, kama ofisa usalama mwaminifu, mkakamavu, mpiganaji, mvumilivu na asiyekubali kushindwa, hivyo umependekezwa kuendelea na mafunzo zaidi. Hapa tunavyoongea, wiki mbili zijazo unatakiwa kuondoka kuelekea nchini China kwa mafunzo zaidi katika medani za kijasusi kwa ngazi kubwa zaidi. Taratibu zote zitafanyika kikosini kwako wiki ijayo. Nakutakia mapumziko mema na unaweza kwenda,” mkurugenzi mkuu David Mshana alimaliza.

Nilirudi nyuma hatua moja na kutoa heshima ile ile halafu nikageuka na kutoka, pale nje kwenye ukumbi nikutana tena na Amanda aliyeonekana kunisubiri. Safari hii alikuwa amevua kile kifaa cha mawasiliano na alikuwa ameshabeba mkoba wake tayari kuondoka.

Amanda aliniongoza tena, kimya kimya, tukakatiza viunga vya Ikulu hadi kwenye maegesho ya magari ya wafanyakazi wa Ikulu. Nilitamani kumuuliza jambo lakini nikachagua kubaki kimya kwanza maana kulikuwa na jambo ambalo sikuwa ninalifahamu na ilinilazimu kuendelea kusubiri, niliamini ningelifahamu tu.

“Ingia twende,” Amanda alisema huku akinifungulia mlango wa mbele upande wa abiria. Lilikuwa gari zuri jeusi aina ya BMW.

Niliingia na kuketi kwa utulivu. Halafu yeye akazunguka upande wa pili na kufungua mlango wa dereva, akaingia na kuwasha gari. Kisha akaliondoa taratibu.

“Leo sikuachi, utaondoka nami,” Amanda aliniambia huku akinitazama kwa tabasamu usoni. Macho yake yalikuwa makini kunitazama usoni.

“Wewe ni shushushu?” hatimaye nilimuuliza Amanda huku nikimtazama kwa mshangao.

“Unaweza kuniita hivyo kama utapenda,” Amanda aliniambia huku akitabasamu.

“Labda ungegombea urembo au ungecheza filamu ungekuwa na mafanikio zaidi, you look gorgeous. Kwa nini ukaamua kuwa shushushu?” nilimuuliza Amanda na kumfanya aangue kicheko.

Kisha akayakaza macho yake kutazama mbele wakati tukilivuka geti la Ikulu, na alipoyarudisha macho yake kwangu akaniambia, “Uzuri wangu hauna maana yoyote kwangu mbali na ile ya kuwaghilibu na kuwafikia walengwa wangu kwa urahisi.”

Nilijikuta nikiangua kicheko hafifu baada ya kukumbuka jinsi nilivyokutana naye kwa mara ya kwanza nyumbani kwa Almasi na kujikuta nikimtamani ghafla kutokana na urembo wake, halafu siku hiyo hiyo tukaenda Maisha Club na baadaye tukawa kule Capital Social Club ambako kulitokea sekeseke.

Kumbukumbu ya tukio la kigaidi pale Capital Social Club usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili ikarudi tena kichwani mwangu na kukumbuka kila kitu. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nikiokolewa na mtu ambaye sikumfahamu na hadi sasa nilijiuliza ni nani aliyekuwa akiniokoa na adui zangu?

Muda wote Amanda alikuwa akinipiga jicho huku akiendesha gari lake kisha akaachia tabasamu. Ni kama alikuwa ameyasoma mawazo yangu kwani aliongea kwa sauti laini iliyojaa upendo ndani yake. “Pole sana, Jason, kwa yote yaliyotokea siku ile.”

“Natambua sana kuwa sote tumechongwa toka kwenye mti mmoja na tofauti yetu ipo katika namna tulivyochongwa tu,” niliongea kwa sauti tulivu. Kisha nilimuuliza Amanda huku nikimtazama kwa umakini. “Akina Sofia wanajua?”

“Hapana. Hawajui na wala hawatakiwi kujua,” Amanda alisema huku akiachia kicheko hafifu.

Endelea...
 
utata.JPG

395

“Uliingiaje kitengo?” nilimuuliza huku nikiendelea kumtazama kwa umakini.

“Baba yangu ndo aliyeniingiza, yeye pia yupo kitengo,” Amanda alijibu.

“Anaitwa nani?” nilimuuliza. Akacheka.

“We unamtakiani baba’angu?” Amanda aliniuliza huku akiendelea kucheka.

“Kwani kuna ubaya kama nitamfahamu?” nilimuuliza.

“Hakuna, ila habari za baba yangu naomba tuachane nazo,” Amanda alisema, kisha akaongeza, “Nimefurahi sana kukuona tena.”

“Sawa, sasa unaweza kunieleza, ni lini ulitambua kuwa mimi ni ofisa wa usalama?”

“Kabla hata sijakutana na wewe, nilisikia habari zako hasa kuhusu operesheni zako mbili, ile ya Ufukweni Mombasa na ile nyingine iliyopewa jina la Taharuki!” Amanda alisema na kushusha pumzi. Kisha akaendelea.

“Wiki iliyopita nilifanikiwa kunasa mawasiliano ya watu fulani waliopanga kukumaliza mara tu ukiingia hapa Dodoma, maana waliamini ungeweza kuharibu mipango yao. Hapo ndipo nilipoanza kukufuatilia zaidi kwa siri kabla hata hujatua Dodoma na nilipata faraja kubwa nilipogundua kuwa unafahamiana na shemeji Almasi, sasa kazi ya kukulinda ikawa rahisi kwangu.”

“Kwa hiyo ni wewe…?” nilitaka kumuuliza Amanda lakini akanikatisha.

“Ndiyo. Ni mimi niliyekuwa nikikulinda. Nilifahamu kila kilichokuwa kimepangwa kifanyike siku hiyo, hadi tunaingia pale ukumbini nilijua nini kingetokea na tayari nilikwisha jiandaa kukabiliana na hali hiyo. Tukiwa pale ukumbini niliwaona watu wawili niliowatilia shaka, nikajua tayari kazi imeanza. Ulipoelekea chooni mmoja akakufuata, nami nikachukua jukumu kukulinda,” Amanda alisema na kunifanya nibaki mdomo wazi kwa mshangao.

Halafu Amanda alinisimulia jinsi alivyonifuatilia hadi kule nje kwenye maegesho ya magari ambako aliwaona watu wawili wakishuka toka ndani ya gari moja dogo lililoegeshwa eneo lile. Wakapewa ishara ya kunizunguka na mwenzao aliyetokea ndani ya ukumbi wakati akinifuata kule nje.

Na hapo akili ya Amanda ikafanya kazi haraka haraka na kuanza kuua kimya kimya kila aliyeonekana kunisogelea kwa bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Akanieleza mengi yaliyoendelea kutokea hadi ile milipuko ya mabomu…

Dah! Sasa nilikubaliana na maneno ya Amanda kuwa uzuri wake haukuwa na maana yoyote kwake mbali na ile ya kuwaghilibu na kuwafikia walengwa wake kwa urahisi! Hadi hapo nilikuwa nimekosa kabisa neno la kusema.

Nilipokuja kushtuka tayari tulikuwa tumeshafika kwenye makazi yake, kisha aliniongoza kuelekea ndani, halafu tukaingia chumbani kwake.

Chumba kilikuwa kikubwa na kisafi sana kilichokuwa kikinukia utuli na kitanda kikubwa cha samadari kilichokuwa katikati ya chumba, kitanda kile kilikuwa cha futi sita kwa sita, kikiwa na droo mbili kila upande, na juu ya zile droo kulikuwa na taa mbili za rangi nyekundu zilizokuwa zinatoa mwanga hafifu wenye mg’ao baada ya kuwashwa na kufanya nusu ya chumba kile kuwa kizani.

Halafu kitanda kile kilikuwa kimetandikwa mashuka mazuri yenye maua ya kupendeza ya rose na jasmine huku yakiwa na michoro ya makopa kopa kumaanisha upendo. Ni kama vile Amanda alikiweka kitanda chake tayari kwa ajili ya ugeni maalumu.

Mbele ya kile kitanda kulikuwa na seti nzuri ya runinga pana aina ya LG iliyotundikwa ukutani na chini yake kulikuwa na meza nzuri nyeusi ya kioo.

Upande wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na jokofu la vinywaji lililokuwa kwenye kona, na hatua chache kutoka kwenye lile jokofu kulikuwa na dirisha pana la kioo lililokuwa limefunikwa kwa pazia zito na refu lenye nakshi za michoro ya maua yaliyodariziwa vizuri na kuyafanya yapendeze.

Upande wa kulia kulikuwa na kabati la nguo la ukutani na pembeni ya lile kabati na pembeni yake kidogo kulikuwa na meza ya vipodozi, na kwenye kona ya chumba kile upande huo huo kulikuwa na mlango wa kuelekea bafuni.

Nikiwa bado nashangaa Amanda aliufunga mlango wa chumbani kwa ufunguo na alipogeuka kunitazama akanikuta nikiwa bado nimesimama nikishangaa. Akakiendea kitanda chake na kujilaza kitandani. Macho yetu yakakutana, nikapumua kwa nguvu.

Dah! Sikuwa nimetarajia jambo lile maana akili na mawazo yangu yalikuwa kwa Daniella, lakini ujio wa Amanda ulionesha kuanza kunivuruga akili yangu.

Kwa mara nyingine tena niliushuhudia uzuri wa binti huyu. Moyo ulianza kunienda mbio baada ya kumwona akiinuka toka pale kitandani na kuanza kutoa nguo zake, moja baada ya nyingine.

“Nadhani tunahitaji kuoga kwanza ili kuondoa uchovu wa usiku huu kabla ya chochote,” Amanda aliniambia na hakuonesha kuwa na aibu ile ya kike mbele ya mwanamume.

Nilizishuhudia chuchu changa kifuani kwake na hapo nikahisi damu ikinichemka na kuanza kwenda mbio kwenye mishipa yangu ya damu. Amanda alimaliza kuvua nguo zote mbele yangu na kujifunga taulo. Akageuka na kunikuta nikiwa bado nimesimama nikimtolea macho. Sikuamini kama nilikuwa ndani ya chumba kimoja na Amanda.

Amanda aliliendea kabati lake la nguo na kufungua mlango mmoja, akatoa taulo lingine jipya kabisa, akanirushia. Nikalidaka.

“Jason, mi natangulia bafuni. Utanikuta,” Amanda aliniambia na kufungua mlango na kuingia bafuni.

Sasa nikawa kama niliyezinduka toka kwenye bumbuwazi, hata hivyo sikutaka kuitumia vibaya nafasi hii adimu niliyoipata japokuwa tayari nilikuwa na hisia juu yake toka tulipokutana siku ya kwanza. Amanda alikuwa na mvuto wa ajabu mno.

Nilivua nguo haraka haraka na kujifunga kiunoni lile taulo nililopewa na Amanda halafu nikaingia bafuni. Nilijikuta nikiwa ndani ya chumba kipana cha bafu, mle bafuni kulikuwa na beseni kubwa la kuogea lililojazwa maji yenye mapovu, na wakati huo Amanda alikuwa ndani ya maji hayo.

Kitendo cha kuingia tu bafuni nikashtukia nikirushiwa maji ya baridi tumboni. Nikashtuka na kuruka. Amanda akacheka kisha akainuka na kunikaribia taratibu, akanitoa lile taulo nililokuwa nimejifunga kiunoni, halafu akaniongoza ndani ya lile beseni kubwa la kuogea huku akinipiga busu moja zito lililonifanya damu ichemke zaidi.

Nami nilimvuta karibu na kumpiga busu maridadi la mdomoni halafu nikauzamisha ulimi wangu kinywani mwake na kuanza kunyonya sharubati, na hapo nikamshuhudia Amanda akinivuta kwake zaidi na kunikumbatia kwa nguvu.

Kilichofuata baada ya hapo kilituhamisha kabisa toka katika dunia hii na kutupeleka katika ulimwengu wa mahaba mazito. Katika muda huo mfupi tulijikuta tukiweka kando mambo yote yaliyotokea na kujivinjari katika sayari ya mahaba. Hatukusikia la mwadhini wala mnadi swala!

Hakika Amanda alikuwa mjuvi wa mambo. Aliyafahamu mambo. Nilipagawa kwa mambo aliyonifanyia. Sikutaka kuachwa nyuma kwani hata mimi mambo haya niliyaweza mno, hivyo nami nilimdhihirishia kwamba nilikuwa na kiwango cha juu, si katika mambo ya ujasusi tu bali hata katika mambo ya mahaba.

Huu ni mwisho wa Msimu wa Saba kwenye mfululizo wa Harakati za Jason Sizya. Usikose Msimu wa Nane katika mkasa uitwao “Kifo Ughaibuni?”.
 
Pamoja na matatizo ya kukatika katika kwa umeme lakini nimetimiza ahadi yangu leo. Nawatakia wote mapumziko mema ya Week end. Tutakutana tena panapo majaaliwa katika harakati zingine za mwamba baharia Jason Sizya...

🙏🙏 ahsanteni wote kwa uvumilivu wenu, ingawa wapo baadhi yenu wamesusa kabisa pasipo kujali changamoto zilizokuwa zikinikabili...
 
Daaah asante sana Bishop na hongera kwa kumaliza huu mzigo hakika ulikuwa bomba sana. Tumejifunza, tumeburudika na kuelimika. Barikiwa sana...Bishop aka Jason Sizya...
 
Mkuu Asante sana! Kuna kasehemu umenikosha, eti Jason na Daniela wakaamua kuwa wazalendo kwa kunywa konyagi. Mbele ya Rais wakala makali [emoji1][emoji1]. Ila naambiwa pia MAMA ANAPIGA KONYAGI!

Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
 
Hatimae tumeumaliza utata! Shukrani sana mkuu nakuombea afya njema uendelee kukonga nyoyo zetu! 🤩🤩🤩
 
Pamoja na matatizo ya kukatika katika kwa umeme lakini nimetimiza ahadi yangu leo. Nawatakia wote mapumziko mema ya Week end. Tutakutana tena panapo majaaliwa katika harakati zingine za mwamba baharia Jason Sizya...

[emoji120][emoji120] ahsanteni wote kwa uvumilivu wenu, ingawa wapo baadhi yenu wamesusa kabisa pasipo kujali changamoto zilizokuwa zikinikabili...
Shukran bishop,tutasubiri kwa hamu msimu wa nane
 
Unajua mi najiuliza sana sipati jibu huyu kaka anampenda kweli mkewe? Kama anampenda mbona anamfanyia hivi? Kama hampendi mbona alikaribia kuchizi kipindi anaumwa na hakufanya hivi alitulia wushing her apone? Kwakweli hastahili kuwa na huyu dada sema wanawake nasie kwa kujifanya mabingwa wa kusamehe sjui tunatakaga sifa au kama Rey alishaona uchafu woote bado kendaolewa nae inafikirisha inaudhi inakera na utakuja kushangaa zainabu wa kilosa ana mimba nyingine na mke anasamehe sjui tunakuaga tumelewa mda wote au
Anampenda mno! Jitahidi kutofautisha NGONO na MAPENZI.. Jason anampenda RAY wake. Kwa mwanaume ham ya ngono ni kama ham ya chakula, wengine huvumilia kuikatili miili yao. Ila JASON hajivungi, anatimiza haja yake.
 
Back
Top Bottom