Simulizi: Harakati za maisha

Yes tupo pamoja

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mkeo anaongea sana Aisee hampi mtu nafasi ya kumuuliza yeye lawama tu kha!
 
Hata ningekuwa ni mimi kwa uongeaji wa mkeo angelamba vibao mtu unakaa unashangaa hali inavyokwenda yeye anaongea Kama vile ana uhakika kibaya zaidi anataka muachane!
 
Nimetoka kwa "mr the dragon" holaa, Nimekuja apa amna kitu,nkaenda kwa 'insider man' napo patupu, nikaona haitoshi nkasema ngoja niende kwa 'singano jr" napo pia patupu,,wakuu nielekezeni chimbo lingine tafadhar...
 
Nimetoka kwa "mr the dragon" holaa, Nimekuja apa amna kitu,nkaenda kwa 'insider man' napo patupu, nikaona haitoshi nkasema ngoja niende kwa 'singano jr" napo pia patupu,,wakuu nielekezeni chimbo lingine tafadhar...
nipe link ya mr the dragon nikapoze arosto
 
Nimetoka kwa "mr the dragon" holaa, Nimekuja apa amna kitu,nkaenda kwa 'insider man' napo patupu, nikaona haitoshi nkasema ngoja niende kwa 'singano jr" napo pia patupu,,wakuu nielekezeni chimbo lingine tafadhar...
Singano jr tayari keshapost
 
Nimetoka kwa "mr the dragon" holaa, Nimekuja apa amna kitu,nkaenda kwa 'insider man' napo patupu, nikaona haitoshi nkasema ngoja niende kwa 'singano jr" napo pia patupu,,wakuu nielekezeni chimbo lingine tafadhar...
Nenda kwa JBourne59 ana msegemnege 😁
 
SEHEMU YA THELATHINI

Niliulizia ulizia hadi nikafika pale kwa mganga ambaye niliambiwa huku nikijiuliza mbona sioni hata hekaheka. Nilitafuta sehemu nzuri nikapaki Samaki wangu Kisha taratibu nikajisogeza karibu na sehemu husika huku nikikaribishwa na akina mama wa pale Kisha tukasalimiana.

Karibu sana baba
karibu . Nilikaribishwa karibu na mti fulani wa mfenesi ambako kulikuwa na mbaombao fulani ikionesha ni sehemu ya fundi selemala kwani kulikuwa na milango na vitanda kadhaa local iliyotengenezwa kienyeji.

Hapa ni kwa Mzee (Nikitaja jina)
Niliuliza.

Ni kweli baba, ningependa kuuliza kwani una shida gani baba. aliniuliza yule mama aliyeonekana ni mpole lakini pia Dini ilimkaa vyema sana.

Nasikia hapa Kuna mtaalamu wa zile tiba zetu. Hivyo Kwa kuuliza majirani nimeambiwa ni hapa, vipi mama au nimekosea siyo penyewe. Niliongea huku nikijichekesha yaani ile ugenini.

Ni sahihi wala hujakosea ni hapa hapa ila Mzee katoka kidogo Wala hayupo mbali sana, ngoja tumtume kijana akamuite. aliongea yule mama aliyeonekana ni mwenye adabu ile ya kijijini, ile ya asili yaani nilifurahi sana namna anavyoongea huku nikiletewa maboga yaliyochemshwa kwa kukatwa vipande na chai iliyopo kwenye kikombe Cha plastic, nilipokea kwa mikono miwili. Huku nikikumbuka mbaaaaaaaaali. Nikaanza kula taratibu.

Baada ya kumtuma mwanaye na yeye akaingia ndani nadhani alitaka niwe huru.
Nilitulia huku nikitoa simu mfukoni ili nizugezuge nayo wakati nikimngoja mwenye nyumba. Missed calls zilikuwa nyingi huku wakiwa ni wapuuzi tu wakiwemo wale jamaa wanaotaka nishiriki kwenye mambo ya mpira.nikawapuuza tu.
Mtu pekee ambaye niliona simu yake ni ya muhimu ni Saidi, nikampigia maana yule ni dereva wetu hivyo simu yake ilikuwa ya maana muda ule nikaipiga.

Hello bro vipi kwema, uko wapi leo sijakuona job vipi kaka, nadhani ni siku ya pili . aliniuliza

Nipo mdogo wangu Nina dharula hivyo nadhani kuanzia keshokutwa nitakuwepo . Nilimjibu.

Sawa kaka Mimi ilikuwa niende mkoani Mwanza nimfuate rafiki yako , ila Leo nafika hapa asubuhi naambiwa safari imeahirishwa kwani jamaa kachukua ndege tayari, yaani nimeboreka kinoma kaka. aliongea yule dogo akionesha hakulala akiiwaza ile safari.

Basi sawa mdogo wangu Mimi naona imekuwa nafuu kwako pia maana safari hatua. niliongeza

Nafuu wapi kaka Mimi nilitaka leo niburuze chombo hadi Rock City mwisho wa siku wenye mamlaka wameghairi, baadaye basi bro.akakata simu.

Kwanza nilicheka kimoyomoyo huku nikiwaza namna dogo alivyo na wenge yaani safari ambazo watu hatuzitaki yeye ndiyo kwanza anazifurahia , Sasa ngoja wewe muache GM akijua huwa anapenda safari ndiyo kwanza atatumwa Hadi akome , unatoka Mbeya ukifika Dar es salaam unaambiwa uende Mtwara umpeleke mtu fulani, ukifika tu Mtwara unapigiwa simu urudi haraka , uende wapi sijui ndani ya wiki moja ushamaliza mikoa kibao. Halafu hupewi siku za kupumzika , huku hupati bakhishishi yeyote zaidi ya pongezi za mdomo.

Utasikia, wewe ndiye mwenye nidhamu namba moja kwenye hii taasisi hii hivyo ongeza bidii utafika mbali, huku siku zikikatika bila majibu. yaani upande cheo au daraja kwa nidhamu na heshima yako?
Huku CV yako ikiwa ni kilomita mbili?
Thubutuuuu. Nilijiwazia.

Lakini nilifurahi kwa ujio wa jamaa yangu maana tangu wamsukumie Mwanza huwa anarudi lakini huwa sipati muda wa kuongea naye ila kwasasa nitahakikisha nafanya mpango nipige naye stori ni agemate, mnywaji kama Mimi, halafu ni bonge la mjanja yaani mishe anazijua kubwa zaidi ni msomi Mimi mwenyewe simkaribii, na sijui ana mkosi gani miaka yote hapandishwi daraja

Dakika zilikatika huku kukiwa hakuna mtu anayekuja licha ya kuambiwa amefuatwa, nikaamua kumpigia mke wangu lakini simu iliita bila kupokelewa, nilijua tu hakuwa mbali na simu bali aliamua tu kunikalia kimya.

Baada ya muda kidogo alikuja Mzee fulani mwenye kanzu kuukuu , akanisalimia huku akiwa kama na kauoga fulani.

Karibu sana ndugu yangu, vipi labda nikusaidie nini . aliuliza yule Mzee.

Siku nyingi sana nilisikia wewe ni mtaalamu wa mambo yetu hivyo kama ujuavyo kwenye maisha Kuna mambo mengi hivyo nimekuja uniangalie . niliongea kwa sauti ya chini huku nikiwa makini.

Mmmh pole sana, ni kweli nilikuwa nafanya kazi hiyo zaidi ya miaka kumi na tano lakini kufikia mwaka jana nikaamua kuachana nayo, nimemrudia mola wangu , kiufupi naswali kwasasa.
Iko hivi matatizo na mitihani ipo kwa mtu yeyote yule huwezi ikwepa ni namna MUNGU alivyotuumba huwezi kunyoooka muda wote. na hupaswi
Kuona unanyanyaswa ukipatwa na mitihani hivyo ni kiasi cha wewe kukabiliana nayo tu kwani Kuna muda MUNGU hutoa mitihani ili tumkumbuke

Pia unatakiwa kuwa makini kwenye maisha yako kwasababu yapo mambo yanatokea kwa bahati mbaya, lakini mengine ni uzembe wetu wenyewe, Ukiwa mstaarabu na mwenye kiasi basi mwenyezi MUNGU atakusaidia. aliweka kituo yule Mzee huku akinikatisha tamaa sana kwani lengo langu halikutimia .

Nilitamani nimuulize kama Kuna mtaalamu mwingine tofauti na yeye lakini nikaona hawezi kuniambia kwasababu inaonesha Imani Imani imemkolea. Na hata ndiyo madhara ya kujulia kitu ukubwani . Ulimbukeni tu, nilijiwazia.

Karibu sana ndugu yangu huyu ni mke wangu mdogo, na hapa ndipo hata shughuli zangu nilikuwa nafanyia baada ya kuwa mke wangu mkubwa kuwa hataki , nadhani ndiyo maana umeelekezwa hapa , lakini kwanini wakusumbue, hakuna asiyejua kuwa Mimi nilishaachana na habari hizo .

alinitembeza kwenye mashamba yake ya mihogo huku nikienjoy sana , matunda kama mafenesi nilibeba ya kutosha na vitu vingine vingi. Huku nikipuuza hata yaliyonipeleka kule.

Unajua watu wengi wa mjini Wana dharau sana na majivuno , lakini wewe upo tofauti licha ya muonekano wako kuonesha kama nilivyofikiria.alivunja ukimya yule Mzee

Hapana Mzee,dharau ni namna ya mtu alivyo tu hakuna uhusiano wowote na kuishi mjini. nilimjibu.

Wewe Mimi nimefanya kazi ya uganga wa kienyeji kwa muda wa miaka zaidi ya kumi nimepokea wateja wa Kila aina , Kuna watu wanakuja kwaajili ya huduma tu hawataki story Wala nini, hata wewe nilitegemea baada ya kukukatalia kuwa nimeacha hiyo kazi ungeinuka na kuondoka muda huohuo. Lakini nimepokea moja ya mtu wa tofauti sana. aliongea yule Mzee huku mkewe akichuma ndimu na kuniletea Zikiwa nyingi sana..

Yaani mume wangu huyu ni mtu wa pekee sana alivyokuja nilimchukulia tofauti sana lakini mmmmh kweli umdhaniaye siye, aliongea yule mwanamke akimwambia mumewe.

Weweee Mimi nimezaliwa kijijini tena ndani ndani hivyo haya ni Moja ya maisha niliyokulia. Nilifafanua kwani huwa sipendi kujikweza hata kama ni ..............

Jamani msalimie sana mke mwenzangu natamani angekuwepo maana ulivyo naamini hata yeye yupo kama wewe . aliongea mke wa yule Mzee Kisha tukacheka tukifurahi.

Pickup yangu ilijaa zawadi kibao, hakika nilifurahi sana, ndimu, mihogo na mafenesi yaani kama naenda kufungua genge, hakika nilitamani kulima maana Nina ekari kibao za mashamba na nisiite shamba maana huwa hayalimwi labda nikistaafu nitalima. nilijiwazia huku wenyeji wangu wakiingia ndani Kisha wakatoka huku nikipewa karanga
ambazo zipo kwenye maganda yake, zikiwa kwenye mfuko fulani.
Ilikuwa ni siku ya aina yake haswa ukizingatia ni jana tu nilikuwa kwenye korido za central nikiponea kwenye tundu la sindano kuwekwa ndani.

Tuliagana na wale wenyeji wangu nikaondoka huku nikiwa njiani nikifikiria namna ambavyo mke wangu angefurahi kuona zile zawadi Lakini tulikuwa tumeshatofautiana.
Nikaamua kumpigia simu, baada ya kumsumbua mara nyingi akapokea .

Enhee kwahiyo umeshamalizana na wanawake zako, uko vizuri ndiyo unampigia mama Jack si ndiyo, Mimi nakuruhusu lala huko huko. Saa nane hii mchana si bado masaa tu tuimalize siku , hebu achana na mimi Kisha akakata simu.

Itaendelea.............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…