feisal firdaus
JF-Expert Member
- Apr 6, 2022
- 424
- 675
Yes tupo pamojaSEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
Tulifika nyumbani huku nikitambua wife kachukia kiasi lakini nilipanga kutomwambia chochote hata akilazimisha .lakini muda ule hakuongea chochote.
Usiku wa saa tisa mke wangu aliniamsha , akinambia anahisi kuna mtu anatembea nje,
Nikatoka kwa tahadhari huku nikichukua manati yangu ili kama Kuna hatari yeyote nijihami huku nikiwaza huyo mtu atakuwa karukaje uzio, na kama kafanikiwa basi ni mtu hatari, nilichukua tahadhari nikizunguka nyumba yote lakini sikuona wala kushitukia jambo baya. nikawasha tochi kujiridhisha hasa sehemu ambazo mwanga haukufika vizuri. Lakini hakukuwa na jambo lolote nililoona nikahakiki mageti yote yakawa salama .
Nilirudi ndani na kumkuta mke wangu sebuleni akiwa kashika tama , kama mwenye jambo kubwa moyoni,
Mwenzetu vipi mbona umekuja huku si ulale, eeh muda bado wa kuamka.
Nilimwambia.
Nilale Nina raha gani hata usingizi sipati, Kila nikijaribu kujilazimisha , wapi nashindwa Nina mawazo sana, ni kwamba baba Jack utaniua kwa presha , na hii aibu unayonitia hakika unaenda kupotea mume wangu, kama siyo jela basi utakufa vibaya .
Mume wangu kumbe ni jambazi? Tena ni tapeli mkubwa nasikia , mwanzo nilikuwa nakataa ,napinga , naona ni majungu na fitina za walimwengu lakini kwasasa taarifa zimeenea mtaani hapa kote nasemwa mimi, kwani unataka Nini haswa kwenye maisha yako.
Mbona una kazi nzuri tu japo huwezi kukidhi mambo yote lakini angalau upo kwenye level ambayo ni ya kawaida.
Sisi ni masikini sawa, lakini hatuna umasikini wa kushindwa kumudu mambo madogo madogo.
Halafuuuu kama ni kweli unadhulumu pesa za watu, mbona sioni jambo jipya? Kama ni projects zako, najua unaendesha kwa namna gani kwani mambo yako mengi unanishirikisha. Lakini kwa hili hapana.
aliweka kituo.
Umeongea sana,
Umeuliza maswali umejijibu mwenyewe,
Unasema kama ni projects zangu unazijua kwani huwa nakushirikisha, hivyo tambua kuwa unayoyasikia ni uongo na fitina za walimwengu tu, tena ni vyema ukaniambia ni nani kasema Mimi ni jambazi na umemsikia lini.
niliuliza.
Usinitishe kwahiyo unataka ukamfanye Nini huyo mtu, kumbe ndiyo maana unarudi saa tano za usiku mara nyingi,
mara boss kasema niende huku mara nani kanituma, kumbe hutumwi Wala Nini ni habari zako za kitapeli tu na plani za kijambazi Sasa mwisho wako nauona, na nadhani ni muda wa Kila mmoja kuangalia ustaarabu wake siwezi tena kuendelea kudhalilika, ni kweli tulifunga ndoa,yenye mashahidi pale altareni na mbele ya yule padre lakini sidhani kama ni vigumu kuachana na wewe nitaenda hukohuko kwenye baraza la mapadre niwaelekeze hizi habari , siwezi kuishi na wewe tena.nitapeleka cheti ili kama vipi ndoa ivunjwe
Umeacha kwenda kanisani nikikukumbusha unaleta visingizio visivyo na maana, unalewa sana unakunywa sana pombe ,
Hivi hujihurumii, hutuwazii sisi kama familia, huwazi kuhusu wanao maana urithi wa watoto ni Elimu Sasa bado tuna safari ndefu ya kuwatengenezea
Njia watoto wetu,
Sasa leo na kesho unaingia jela, au unaviziwa unauawa, eeenhee niambie itakuwaje.
Mimi sina Elimu yeyote, na Kila ninachofanya leo ni kutokana na sapoti yako, hata biashara zangu ni za kwako kwani Kila ninapoyumba huwa unaniinua.Daniel (akinitaja jina)
tafuta polepole , nakuamini na nakukubali sana una Kila sifa ya kuitwa mume,baba wa watoto wangu na mlezi
Sasa kwa njia uliyochagua na unayoenda nayo siyo sahihi Daniel utakufa.yule mwenzako Jastini ni mkongwe na ameshakata tamaa wewe je,na nashangaa wewe umeponaje pale central ukashindwa kukaa mahabusu?
aliweka kituo huku nikimwacha aongee, ajimalize atoe dukuduku lake lote sikutaka nimkatishe kwani anadai hizi taarifa kazisikia kwa watu wengi hivyo napaswa kutumia busara kuzungumza naye ili anielewe na si vinginevyo.
Mke wangu tumechelewa kulala , halafu tena unaniamsha mara nani anatembea huko nje, Ina maana uliniamsha ili uniambie hizi habari,
Si ungesema tu. nilimwambia kwa mshangao.
Nilitaka usingizi ukutoke kwanza kwa kutembea tembea huko nje nikijua utanisikiliza ninachosema,lakini pia Kwa taarifa za wewe kusikia ni jambazi nilitaka nikupime una uoga gani.alinijibu kuwa alinisumbua tu.
Haya umegundua Nini baada ya Mimi kutoka nje.
niliuliza huku nikiwa nimeshakasirika.
Ni Siri yangu , ila tambua unanitisha sana tena mengi nayasikia ni mengi sana wewe endelea tu muda wako utafika tu ipo siku yako isiyo na jina.
aliendelea kulalamika lakini Mimi niliamua kurudi ndani chumbani nikimuacha sebuleni Kisha nikajiinamia nikiwa mwenye mawazo kiasi.
Kwanini nahusishwa na skendo za utapeli na ujambazi, ni dhahiri kuna roho ya kishetani inanifuatilia na nisipochukua hatua mapema nitaangamia mke wangu kashalishwa maneno, kule kazini ndiyo hivyo tena, hata da Vero sikupokea simu yake sijui hata alitaka kusema nini, pia ni mtu ambaye ameshaanza kunidharau. au niende kwa sangoma nikapandishwe nyota?
Au nianze kushiriki kanisani,nitapokelewa kwa heshima kama zamani?maana hata kwenye jumuiya yangu nina miaka kadhaa sijashiriki.
Mimi sijawahi kuiba na sina hizo sifa licha ya kupitia magumu mengi kipindi cha nyuma lakini sijawahi kuwaza kuiba kitu cha mtu , haya ya sasa yanatoka wapi?
Ee MUNGU nisaidie maana naona kama anayosema mke wangu yanaenda kunitokea masaa machache yajayo.
Nikiwa nimejiinamia huku nje kukiwa kunapambazuka, mke wangu aliniita.
Mume wangu nakuona unavyowaza na kutafakari naona ni muda sahihi wa kuweza kuacha mara Moja tabia zako hujachelewa bado....... Kabla hajamalizia sentensi yake
Niliinuka na kumkaba shingoni nikimkaba kama napigana na mwanaume mwenzangu , Kisha nikamtupia kitandani huku nikihema hata yeye aliishia kujishika shingoni huku akiugulia maumivu.
Wewe ni mpuuzi hukai chini na Mimi ukaniuliza kwa adabu, unaanza kuropoka Ukiwa hujui hata kinachoendelea , halafu bila hata kufikiri unaniambia eti umesikia watu wanasema, kwahiyo hao watu wanaujua ukweli kuliko Mimi muhusika, kiasi cha wewe kuchukua maneno kama yalivyo na kuniambia mimi. nilifoka kwa sauti
Mume wangu unataka kuniua, wewe niue tu nimalizie, alilalamika mke wangu.
Sikujali nilimnasa vibao kadhaa ,nikavaa nguo zangu sikutaka hata kuoga then, nikachukua wallet yangu na kujiridhisha kuwa ipo vema nikatoka ,kufika sebuleni namuona dada wa kazi akiwa na wasiwasi akiwa kasimama tu.
Huenda alitamani kuniuliza lakini angeanzaje .jamani hakuna anayepanga kumpiga mkewe ila ni mambo hutokea unajikuta umeshafanya maamuzi Kuna vitu vinakera sana.
Nilipanda pickup yangu huku nikiwa naelekea njia ya shamba lengo niende kwa mtaalamu ambaye nasikia yupo vizuri maana mazingira na upepo niliopitia ilikuwa ni hatari mno kwangu. Kwakuwa boss alinipa permission ya siku kadhaa hivyo nikaona ni muda wa kuweza kufanya ukarabati wa vitu kadhaa.
Saa mbili ya asubuhi ilinikuta nikiwa nimeshauacha Mkoa wa
Dar es salaam , nikichanja mbuga kwenda uzaramoni .
Nikiwa nimekaribia kwenye Kijiji mahali ambako nasikia mtaalamu anapatikana, huku nikipunguza mwendo na kuuliza uliza wenyeji sehemu anayopatikana yule mtaalamu.Nikaelekezwa.
Kabla sijafika simu iliita namba ikiwa ngeni, moyo ulienda mbio huku nikipokea kishingo upande maana ni kipindi nikiona namba ngeni nawaza polisi tu.
Mimi ni Mzee wako mjumbe wa huu mtaa, vipi mwanangu uko wapi?
aliuliza yule Mzee mara tu baada ya kusalimiana.
Nipo mbali sana Mzee vipi una shida gani? niliuliza.
Sawa, mkeo kaniletea malalamiko hapa si muda mrefu,na kwanini umparueparue mtoto wa kike vile shingoni,
Jamani Daniel hata wewe?
Si kwamba nashangaa wanandoa kuumizana ila sikutegemea namna ulivyo ukapige mwanamke, tafadhali huko ulikoenda ukirudi nipigie simu, na mtoto wa watu hajataka kwenda polisi , unadhani akienda na makovu uliyomsababishia utakuwa kwenye wakati gani kijana . aliweka kituo yule mjumbe.
Dah Mzee wangu nikirudi tutaongea,nilijibu kwa kifupi Kisha nikakata simu.
Huku nikisimama katikati ya barabara nikiwa na mawazo kadhaa,
Kwanza nilianza kujuta kwa niliyoyafanya kwa mke wangu, nilimuhurumia sana, nilijiona mjinga kwa kitendo cha kumpiga ni ukatili nimefanya.
Mke wangu si Malaya jamani, na hata kama anafanya huenda ni kwa Siri sana maana uchunguzi wangu wote sijawahi kumuhisi, na hizi ndiyo kesi kubwa kwa wanandoa
Nilijiwazia.
Nilishtuliwa na honi ya gari Canter moja iliyojaza mihogo ikiwa imepangwa kiustadi.Nikawapisha huku nikiwaomba msamaha.
Wewe Nini bro, unawaza nini au tukupe msuba uvute? Unakaa kiboya boya barabarani. nilitukanwa lakini sikujibu chochote. Huku taratibu nikielekea nilipokusudia.
Itaendelea.................. .
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app