Simulizi: Lisa

Simulizi: Lisa

Kwahiyo kwa sisi tulioonjeshwa humu...tunawezaje kuendelea na chapter zilizobaki za Lisa au kupata Hadithi nzima??
Kuwasiliana direct na mwandishi atakupa maelekezo au kusubiri Hadi afungulie ku-copy na kufoward meseji telegram tueze kutuma huku
 
Tafadhali tupe hayo mawasiliano mkuu...tuone vile tunaweza toboa hicho kikwazo
 
LISA KITABU CHA......... (11) SIMULIZI...........................LISA
KURASA....................546- 550
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 546
Kusikia Sarah akipoteza udhibiti, Pamela alicheka kwa kuridhika.
Miaka mitatu iliyopita, Sarah alikuwa amemtesa yeye na Lisa. Hatimaye, ikawa zamu yake kumtesa Sara. Alijisikia vizuri sana. Ilibidi amfahamishe haraka Lisa.
Nani alijua kuwa baada ya Lisa kusikia jambo hilo, alinyamaza kwa muda. Kisha, akakemea, “Ulitenda bila kufikiri! Sarah si rahisi kushughulika naye. Ikiwa ameirekodi simu na kuihariri kidogo, Rodney atafikiria kuwa wewe ni mwanamke mkorofi.
Moyo wa Pamela ulirukaruka. Baada ya muda, alisema, "Anaweza kufikiria vyovyote anavyotaka. Hata hivyo, si kama nataka kuwa na uhusiano wowote naye.” Lisa alifungua midomo yake na kusema. "Sawa, mradi umeelewa." Kwa kweli, bado

alikuwa na wasiwasi kidogo. Kwani, hakuna mtu aliyemjua vizuri zaidi jinsi Sara alivyokuwa mwovu.
Rodney aliishi peke yake kwenye jumba la kifahari katikati mwa jiji.
Alipofika nyumbani, ghafla aligundua kuwa aliiacha simu yake kwa Pamela. Alijisikia uvivu sana kuirudia.
Angepitia kwa Pamela wakati anaenda kazini kesho yake asubuhi na kuchukua simu yake.
Akiwa anajiandaa kuoga tu, kengele ya mlango ililia. Akafungua mlango. Sarah alisimama mlangoni na uso wenye michirizi ya machozi. "Rodney, nilikupigia sasa hivi na ni Pamela ndiye aliyepokea. Alisema ana mimba ya mtoto wako. Ni ukweli?"
Uso wa Rodney ulibadilika sana. Hakuwa amefikiria jinsi ya kumwambia
Sara jambo hili.
“Yeye... alikuambiaje kuhusu hilo?”

Sarah alisoma tu uso wake. Alijua ni kweli kutokana na kujiumauma kwake. Isingekuwa kweli, Rodney angepinga moja kwa moja. Alikunja ngumi. Hakutarajia kwamba Rodney, ambaye alimshikilia kwa nguvu mikononi mwake, angeweza kupata mtoto na Pamela.
Alitoka nje huku akilia. “Pamela alisema hutaki atoe mimba na tena umempikia. Anakupenda na anataka kuninyang'anya mwanamume mzuri kama wewe."
Rodney alipigwa na butwaa. Pamela alisema alikuwa akimpenda? Pamela alitaka kumpokonya? Ajabu ni kwamba akili yake ilikuwa imechanganyikiwa hadi kilio cha Sarah cha kukata tamaa kilipomzindua. Hapo ndipo alipokasirika. Pamela alikuwa akizidi sana!
“Rodney, kwa nini unanifanyia hivi? Ni jambo moja kwamba Alvin hunitaki, lakini

hata wewe umenisaliti sasa. Nitaishije? Ni nani aliyesema atanipenda milele na hatawahi kuniacha?"
Kila neno kutoka kwa Sarah lilikuwa kama kofi kwenye uso wa Rodney na kumchoma.
“Sarah, samahani... niligundua tu kwamba alikuwa mjamzito siku chache zilizopita.” Rodney aliinamisha kichwa chake na kueleza, “Simpendi, lakini... familia yangu haikubali kutoa mimba ya huyu mtoto.”
Macho ya Sarah yalimtoka. Machozi yalimtoka pia. “Unasema unataka mtoto huyu azaliwe. Unataka nifanye nini? Unataka nirudi nyuma katika hili?"
Rodney alikuwa anaumwa na kichwa. “Wazazi wangu watamlea mtoto huyo baada ya kuzaliwa. Nilimwambia Pamela kwamba sitamuoa...”
“Rodney, tumia akili. Anajua humpendi sasa na anamtumia mtoto kama kigezo cha kukuvuta karibu. Anatumia ujauzito ili

aweze kukusogelea na kukufanya umpende. Kisha ataharibu uhusiano wetu.” Sarah alimshawishi kwa uchungu.
Rodney alichanganyikiwa kabisa na maneno yake. Alifikiri kwamba Pamela hakuwa mtu wa aina hiyo.
“Huniamini?” Sarah alitabasamu kwa huzuni. “Nilijua huniamini sana, kwa hiyo nilirekodi simu. Sikiliza.”
Alicheza rekodi. Rodney alipomsikia Pamela akisema, 'Sitaki kukuruhusu uwe na mtu mzuri kama huyo' kwa sauti ya kiburi kama hii, uso wake uligeuka kuwa mbaya.
“Rodney, sitaki kukulazimisha, lakini kama bado unataka kuwa na mimi, lazima umfanye Pamela atoe mimba. Sitaki mtu ninayempenda awe na mtoto wa nje ya ndoa. Nataka mtoto wetu tu. Ninakujali, kwa hivyo sitakuwa mvumilivu au mkarimu kiasi hicho.” Sarah alirudi nyuma hatua kwa

hatua na kuondoka huku macho yakiwa mekundu.
Rodney alimtazama kwa nyuma. Moyo wake ulikuwa na maumivu makali.
Yote yalikuwa makosa ya Pamela. Mwanamke ambaye hakujua mipaka yake. Alimtendea vizuri kidogo tu kwa sababu ya mtoto, lakini alikuwa akijaribu kusukuma bahati yake.
Usiku huo, Rodney hakuweza kulala hata kidogo. Asubuhi ilipofika, aliendesha gari kumtafuta Pamela. Sophia alifungua mlango. Alitabasamu na kusema, “Bi. Pamela bado anavaa ghorofani."
Rodney alipanda juu kwa hatua ndefu. Kwa kuwa kawaida hakukuwa na wanaume ndani ya nyumba, Pamela hakufunga mlango alipokuwa anavaa.
Rodney aliingia ndani ya chumba. Pumzi yake ikamshika kasi alipomuona yule mwanamke asiyekuwa na nguo mwilini

mwake chumbani. Kiuno chembamba hicho, ngozi yake nzuri, na hata mikunjo yake! Ni kana kwamba kulikuwa na miali ya moto machoni pake. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona mwili wa mwanamke kwa uwazi.
“Sophia, upo...”
Pamela alipogeuza kichwa chake na kuona macho meusi ya Rodney, alipiga kelele kwa mshtuko. Alifunga mlango wa chumba cha kubadilishia nguo kwa kelele.
Koromeo la Rodney lilikaribia kutoboka jkwa uchu. Jamani! Mwili wake ulikuwa na majibu. Angewezaje kushuka chini katika hali hiyo? Harakaharaka akaelekea bafuni katika chumba cha Pamela.
Pamela alimaliza kuvaa na kutoka nje akiwa amekunja uso. Aligundua kuwa hakukuwa na mtu ndani ya chumba hicho, lakini kulikuwa na kivuli cha mtu katika bafu lake.

Rodney alikuwa anafanya nini bafuni kwake?
Pamela alikuwa kituko nadhifu. Mara akakimbia na kugonga mlango. “Rodney, kuna bafu chini pia! Kwanini unatumia bafu langu? Huwezi kukojoa huko chini?"
“Nyamaza...” kishindo kikubwa cha Rodney kilisikika.
“Mbona sauti yako ni ya ajabu? Je, una tatizo la kukosa choo?”
Pamela alihisi kuchukizwa zaidi alipokuwa akiwaza jambo hilo. “Nani alikuruhusu kujisaidia haja kubwa katika choo changu binafsi? Inanuka.”
Akiwa bafuni, Rodney alikasirishwa na Pamela hadi akakaribia kupata kiharusi.
Lakini, hakuweza kujibu maneno yake hata kidogo. Ilikuwa afadhali afikiri kuwa alikuwa anakunya kuliko kumjulisha

kwamba alifkuwa akipiga punyeto akiwa bafuni kwake.
Dakika chache baadaye, uso wake ulikuwa na haya wakati anatoka bafuni. Walipoonana, alimuona Pamela akiwa ameziba pua na kumtazama kwa dharau.
“Pamela, mbona una tabia mbaya sana?" Rodney hakuwahi kuona aibu kama alivyokuwa wakati huo. "Ulijua ninakuja ukaamua kuvua nguo makusudi ili kunitongoza?"
“Huna aibu?” Pamela karibu alikuwa kupatwa na shinikizo la damu kutokana na hasira. "Hiki ni chumba changu, nyumba yangu. Ulikimbia bila kubisha hodi na kuniona nikiwa uchi. Badala yake unanieleza upuuzi wako.”
"Usifikiri kuwa sijui nia yako." Rodney alidhihaki, “Ulimwambia nini Sarah jana usiku? Unanipenda. Unataka kunitongoza na

kuharibu uhusiano wangu na Sarah. Unajidanganya bure."
“Unasemaje wewe?” Macho ya Pamela karibu yatoke kwenye soketi zake.
"Hah, unajua kabisa. Hukumbuki ulimwambia nini Sarah jana usiku?”
Rodney alimkumbusha neno kwa neno. Pamela alishangaa. Sawa, Lisa alikuwa
sahihi.
“Nilifanya hivyo makusudi ili kumfadhaisha Sarah. Ninamchukia kwa kumuumiza Lisa hapo awali—”
“Inatosha! Sasa unataka Sarah awe mnyonge kwa sababu ya Lisa?” Rodney alifoka na kumkatisha.
“Sitaki kuongea upuuzi na wewe. Ondoka hapa.” Pamela aliogopa kuharibu siku yake kwa sababu ya hasira, kwa hivyo aligeuka na kuondoka.

“Simama hapo hapo.” Rodney alimfuata. "Lazima nikupeleke hospitalini."
“Kwa ajili ya nini?”
"Kutoa mimba." Rodney alidhamiria. Ikiwa Pamela angekuwa mtu mkarimu anayejua mipaka yake, angeweza kumruhusu azae mtoto. Hata hivyo, baada ya maneno ya jana yake usiku, alikuwa na ufahamu wazi wa tabia ya mwanamke huyu mjanja. Hakutaka kujihusisha tena naye tena.
"F*ck youl" Pamela hakuweza kupinga kutema maneno machafu.
Ni aibu iliyoje. Alifikiri alikuwa na hisia ya kuwajibika jana yake usiku na kwamba angekuwa baba mzuri. Asubuhi tu iliyoofuata, akawa mjinga sana.
"Haya, twende." Rodney akamshika mkono.

“Sitaki.” Pamela alianza kuhangaika. Sio kwa sababu alitaka sana kumbakiza mtoto. Ilikuwa hivyo tu kwanini aitoe mimba kwa sababu tu Rodney alisema hivyo?
“Hakika ulichosema kuhusu sisi kuwa na adui wa pamoja na kutaka kuishawishi familia yangu kutoa mimba ni uongo tu. Unataka tu kubaki na mtoto ili iwe rahisi kwako kuolewa na mimi.”
Sio tu kwamba Rodney hakumuachilia, lakini hata alifungua mkono wake mwingine ili kumshika kwa nguvu.
"Rodney, niache niende!" Pamela alimsukuma kwa nguvu. Kwa sababu hiyo, aliposimama kwenye ngazi, mguu wake uliteleza na akaanguka chini.
Sura ya: 547
“Pamela...” Lisa, aliyeingia tu mlangoni, alimwona Pamela akianguka chini ya ngazi

hadi ghorofa ya kwanza.
Alikimbia juu kwa haraka. Alimwona Pamela akiwa ameshika tumbo lake. Uso wake ulikuwa ukitetemeka kwa maumivu.
“Lisa... inauma sana...”
“Pigia gari la wagonjwa haraka,” Lisa alimuamuru Sophia.
Sophia alipata simu haraka na kupiga 000. Wakati huo Rodney alirudi kwenye fahamu zake. Hakutarajia kwamba angeweza kuanguka.
Hakumsukuma. Hakufanya makusudi.
Rodney alishuka haraka haraka na kutaka kumbeba Pamela. Lakini, Lisa alisukuma mikono yake mbali. Akamkazia macho huku macho yake yakiwa yamejaa hasira.
“Potelea mbali! Una hamu sana ya kumuua

mtoto wako. Nani anajua kama utamuua mtoto kimakusudi ukiwa umembeba Pamela?”
"Lisa Jones, angalia mdomo wako! Je, mimi ni mtu mbaya sana?... F*ck... Anavuja damu.” Akili ya Rodney ilimtoka.
Pamela aliinamisha kichwa chini na kutazama. Uso wake ulikuwa umepauka. "Lisa, inauma huko chini."
“Jikaze, Sophia, nisaidie. Tutambeba pamoja,” Lisa alimwambia Sophia kwa haraka.
Sophia pia alikuwa amemsikia Rodney akisema anataka Pamela atoe mimba alipoenda kufungua mlango.
Hakuthubutu kumruhusu Rodney kusaidia pia.
Yeye na Lisa walimbeba Pamela na

kushukua chini na kumpeleka Pamela hospitali mara moja. Njiani, kichwa cha Pamela kilikuwa kimejaa jasho kutokana na maumivu. Baada ya kufika hospitalini, alipelekwa kwenye chumba cha dharura mara moja.
Lisa mara moja aliwapigia familia ya Shangwe. " Uncle Jason, mwanao alimsukuma Pamela chini ya ngazi na Pamela kaumia vibaya. Tafadhali njoo sasa hivi. Familia ya Shangwe lazima itupe maelezo juu ya suala hili.”
Rodney aliogopa sana aliposikia hivyo. “Wewe, unasemaje? Sikumsukuma hata kidogo. Ilikuwa ni yeye...”
Lisa alimpiga kofi usoni bila kumruhusu amalizie sentensi yake.
"Lisa, unathubutuje kunipiga?!" Rodney alikasirika na kutaka kumpiga mgongoni.

Lakini, Lisa alimkwepa haraka na kubonyea chini. Ngumi yake ilipopita alijikuta mwili wake ukiwa kwenye bega la Lisa. Lisa alimnyanyua na kulitupa umbo lake refu kwenye sakafu ya hospitali.
“Lo... Inauma...” mgongo wa Rodney nusura uchomoke kutokana na maumivu.
“Unahisi maumivu pia? Lakini kile unachohisi sasa hakiwezi kulinganishwa na maumivu ya Pamela.” Lisa alimtazama kwa hasira. "Rodney Shangwe, wanasema hata simba hatakula watoto wake. Hata kama humpendi Pamela, bado ana mimba ya mtoto wako. Unaweza kumchukia Pamela, lakini huwezi kumchukia hadi mtoto aliye tumboni mwake.”
“Kwa kweli sikumsukuma. Aliteleza na kuanguka mwenyewe kwa bahati mbaya.” Rodney alichanganyikiwa kutokana na kukemewa.

Lisa alifoka, “Kwa hiyo bado hukubali kwamba una makosa? Ikiwa usingejaribu kumburuta ili akatoe mimba, angeteleza?”
Uso mzuri wa Rodney ulibadilika rangi kutokana na maneno yake. Hakuwa na la kusema.
Daktari akatoka. “Mfuko wa uterasi wa mgonjwa umeharibika. Mtoto yuko katika hali mbaya pia, lakini bado tunaweza kumudu kumwokoa mtoto—”
Rodney alisema kwa kupigwa na butwaa, “Hii... Hakuna haja ya kuiokoa.”
"Funga mdomo wako! ” Lisa alimkazia macho kwa nguvu.
"Mlinde mtoto." Ghafla, Jason na Wendy walikuja mbio.“Dokta, huyu ni mjukuu wangu. Lazima umwokoe mjukuu wangu hata iweje,” Wendy alisema kwa dharura.

Daktari alisema, “Kwa kweli, sijamaliza sentensi yangu. Ikiwa tutatoa mimba, mgonjwa lazima apate utaratibu wa kusafisha kizazi na madhara kwa mwili wake yanaweza kuwa makubwa sana na huenda asiweze kupata mimba tena siku zijazo.”
Lisa alishtuka. Ilionekana kama Pamela alikuwa amekusudiwa kumtunza mtoto huyu. "Basi muokoe mtoto ..." Alijua Pamela hakika hakutaka kupoteza haki ya kuwa mama.
“Sawa, tafadhali saini hapa.” Daktari akatoa kalamu nje. Lisa akaweka sahihi yake.
Rodney alichanganyikiwa. “Kwa nini imekuwa hivi? Inawezekana kwamba Pamela aliwahonga madaktari ndani?"
Mara tu baada ya kusema maneno hayo, Lisa alikasirika. Alitaka kumpiga, lakini Jason alikuwa mwepesi na mkatili kuliko

yeye.Kofi kutoka kwa mwanamume haliwezi kulinganishwa na la mwanamke hata kidogo.
Mdomo wa Rodney ulitoka damu mara moja. Akayatoa macho yake kwa kutoamini.
“Baba...”
“Potelea mbali.” Jason alielekeza nje. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika kabisa. “Ondoka hapa! Sisi, familia ya Shangwe, hatuna chochote cha kufanya na wewe kutoka sasa. Mtoto wa Pamela hatakuwa na uhusiano wowote na wewe pia. Sio lazima kuwajibika kwa mtoto pia. Unaweza kwenda na kuwa pamoja na Sarah. Hakuna mtu atakayewazuia tena."
“Hapana, Baba. Mimi...”
“Kwa nini nina mtoto mbaya kama wewe?” Wendy akatikisa kichwa kwa kukata tamaa. “Nilishakushauri hapo awali, lakini bado ulinikatisha tamaa. Ondoka. Hatutakuwa na

uhusiano na wewe hata kidogo katika siku zijazo."
Rodney alihisi uchungu. “Baba, mama, kwa kweli sikumsukuma. Hivi kweli unanikana kwa ajili ya mjukuu na Pamela?”
“Bado hujaelewa? Kama binadamu, unapaswa kuwa na dhamiri na kujua kutovuka mipaka. Lakini huna dhamiri hata kidogo. Mtu kama wewe hastahili kuwa mwanangu. Hustahili kubaki katika familia ya Shangwe.” Jason alipiga kelele huku akitetemeka, “Potelea mbali! Sitaki kukuona tena!”
Walikatishwa tamaa kabisa na yeye.
Rodney alifungua kinywa chake. Mwishowe, wakati anakabiliwa na macho ya dharau ya kila mtu, angeweza tu kugeuka na kuondoka.
Upweke ulitawala mwili wake wote. Alijua kwamba hakuna mtu ambaye angemzuia kuwa pamoja na Sara katika siku zijazo.

Hata hivyo, kwa nini hakuhisi furaha? Badala yake, alihisi kupotea?
"Uncle Jason ..." Lisa hakutarajia Jason kumfukuza Rodney kutoka kwa familia ya Shangwe. Hata hivyo, bado aliwaambia Jason na Wendy kuhusu kilichotokea.
"Hata hivyo, Rodney alihusika katika tukio hili. Ikiwa asingemlazimisha Pamela kwenda kutoa mimba, haya yote yasingetokea.”
Jason akahema. Alisema, “Tulikosea. Nilifikiri Rodney bado ana hisia fulani ya kuwajibika ndani yake. Fadhili zake zinakaribia kutoweka kwa sababu ya Sara.”
Lisa alikunja uso kwa nguvu. “Lakini mtoto...”
“Mtoto hana tatizo, tumuombee tu. Tuna deni la Pamela kwa hili. Tutamlipa fidia.” Wendy alisema, “Tukiwa njiani kuja hapa,

tulipata simu na Mzee Shangwe. Mzee Shangwe anakusudia kumruhusu Nathan kumchukua Pamela kama binti yake wa kike. Kwa utambulisho kama binti wa baadaye wa Rais, ninaamini kwamba Pamela anaweza kumpata ampendaye katika siku zijazo bila kuwa na wasiwasi kuhusu chochote. Hakuna mtu atakayethubutu kumsema vibaya katika siku zijazo.”
Moyo wa Lisa ulitetemeka. Kuwa ‘mtoto wa hiyari’ wa Nathani kwa hakika ilikuwa utambulisho wa ajabu. Mbali na hilo, Nathan alikuwa na mtoto wa kiume pekee na mtoto huyo alikuwa akifanya kazi katika wizara ya sheria Nani angethubutu kuleta shida na Pamela katika siku zijazo?
"Baada ya muda, tutafanya sherehe kubwa ya kumtambua Pamela kama binti wa Nathan. Tutafahamisha ulimwengu wote kwamba Pamela ni sehemu ya familia ya Shangwe. Wakati huo huo, bado asilimia kumi ya hisa za Shangwe Corporation

zitahamishiwa kwake. Lakini hisa hizo zinaweza tu kurithiwa na mtoto aliye tumboni mwake sasa. Ikiwa ataolewa na mwanamume mwingine na kupata watoto na mwanamume huyo katika siku zijazo, hisa hizi zitabaki kwa mtoto. Tutapanga seti nyingine ya mahari pia,” Wendy alisema kwa dhati. Kuhusu hili ... nitamjulisha Pamela kuhusu hili baadaye."
Lisa aliweza kuona kwamba familia ya Shangwe kweli walikuwa waaminifu. Kwanza, ilikuwa ni kwa sababu ya hatia yao juu ya matendo maovu ya Rodney. Pili, walikuwa na wasiwasi juu ya mtoto katika tumbo la Pamela.
Sura ya: 548
Saa moja baadaye.
Baada ya Pamela kukaa katika hali nzuri, alifahamishwa kuhusu mipango ya familia ya Shangwe. Angekuwa mtoto wa hiari wa

Nathan, mgombea urais katika siku zijazo? Hakujua kama alie au kucheka.
"Pamela, ukimtoa huyu mtoto, utapoteza haki ya kuwa mama, na mtoto wa Rais ajaye" Lisa alisema kwa husuda.
“Ha! Inaonekana mbingu tayari zimeniamulia.” Pamela hakutarajia maisha yake kufikia hatua hiyo.
Alifikiria kuwa katika uhusiano wa kawaida wa kimapenzi hapo awali. Mwanamume huyo hakuhitaji kuwa baba wa familia yake, hivyo alipanga kumzaa tu huyo mtoto. Baada ya hapo, angejenga familia na mwanamume mwingine na kupata watoto. Lakini sasa, maisha yake yalikuwa yamechukua sura mpya.
Wendy alimfariji, akisema, “Usijali, Pamela. Kwa utambulisho wako huu katika siku zijazo, wewe ndiwe utachagua wanaume. Bila shaka, unaweza kuwa na wasiwasi kwamba wanaume watajali kwamba

umejifungua mtoto hapo awali. Lakini wanawake wengi walioolewa wakiwa na watoto wa nje ya ndoa wanaishi vizuri na kwa furaha pia. Isitoshe, ikiwa mtu yeyote atathubutu kukuonea, familia ya Shangwe itasimama kwa ajili yako.”
Pamela aliweza kucheka kwa uchungu tu. Kwa kweli, hakupaswa kuwa na malalamiko mengi. “Lakini sitamruhusu mtoto wangu amtambue Rodney kama baba yake. Kwanza, yeye hamtaki hivyo hastahili. Pili, sitaki mtoto wangu amwite Sarah mama yake wa kambo siku za usoni.”
“Hilo hakika halitatokea. Hatuna uhusiano wowote na Rodney tena. Tayari nimepanga kampuni iandae hati ya kumvua umiliki kampuni. Tutaitangaza kwa umma hivi karibuni,” Jason alisema bila kusita.
Pamela alishtuka. Familia ya Shangwe ilikuwa nzuri sana katika kufanya maamuzi.

Alihisi kuridhika na kushangazwa. Rodney lazima alitaka kutapika damu alipopoteza familia yake. Pia, Sarah angemvumilia Rodney kwa muda gani? Alijawa na matarajio ghafla.
Siku hiyohiyo, ukurasa rasmi wa Facebook wa Shangwe Corporation ulitoa taarifa: [Mkurugenzi wa Shangwe Corporation, Jason Shangwe, anatangaza rasmi kwamba amefuta uhusiano wa baba na mtoto na Rodney Shangwe. Wakati huo huo, Rodney hatakuwa tena na chochote cha kufanya na familia ya Shangwe kuanzia sasa na kuendelea. Wanafamilia wa Shangwe pia hawatakuwa na mwingiliano wowote na Rodney. Haki ya Bw. Rodney Shangwe ya urithi kwa mali zote za familia ya Shangwe ni batili. Inatarajiwa kwamba kila upande utaenda kivyake kuanzia sasa na kuendelea na hawataingiliana tena.]
Kisha, Jessica alitoa taarifa pia. [Nimekata uhusiano wa kaka na dada na Rodney

Shangwe.]
Carson Shangwe: [Nimekata uhusiano wa ukaka na Rodney Shangwe.]
Nathan Shangwe: [Sina uhusiano wowote wa kindugu na Rodney Shangwe.]
Taarifa za familia ya Shangwe zilitolewa moja baada ya nyingine. Taifa zima likashtuka. Wanamtandao wakatiririsha maoni yao kama kawaida:
[Rodney alifanya nini hadi kufukuzwa kutoka kwa familia ya Shangwe? Kila mtu katika familia ya Shangwe hata alikata uhusiano naye?]
[Rodney lazima awe mpumbavu. Ana baba na ndugu ambao wana mali yenye thamani mabilioniya dola. Ana hata baba yake mdogo ambaye atakuwa Rais, lakini aliikasirisha familia yake.]

[Nilisikia kwamba ni kwa sababu Rodney anasisitiza kuwa pamoja na Sarah. Familia ya Shangwe haijaridhika naye. Wanampendelea zaidi mchumba wake, Pamela.]
[Hii ndiyo familia ya Rais mtarajiwa tunayoizungumzia. Je, hiyo ni familia ambamo mwanamke mwenye pupa ya mali kama Sara anaweza kujiunga?)
Baada ya nusu saa, Nathan alichapisha picha nzuri ya Pamela kwenye Facebook yake ikiwa na maelezo: [Mimi na mke wangu tumeoana kwa miaka mingi.
Tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia mtoto wa kiume. Kwa kuongezea, tumekuwa tukitamani kuwa na binti lakini majaaliwa hayo hatukuwa nayo. Kwa bahati nzuri, mke wangu na Pamela Masanja wamekuwa wakielewana vizuri sana. Tumeamua kumchukua kama binti yetu wa hiari. Ingawa hataweza kuwa binti-mkwe wa familia yetu, kuwa binti yetu ni nzuri pia.]

Wanamtandao walipigwa na butwaa tena: [Nimechanganyikiwa. Kwa hivyo Rodney
alifukuzwa kutoka kwa familia ya Shangwe kwa sababu alikataa kumuoa Pamela?]
[Nilimhurumia Pamela hapo awali, lakini sasa ninamuonea wivu. Binti wa Rais mtarajiwa? Kweli kila mtu na bahati yake duniani.]
[Kama anaweza kuwa binti wa Rais, kwanini ni lazima awe mchumba wa Rodney? Ahhh, si kuwa binti wa Rais ni bora zaidi?]
[Je, bado unakumbuka kwamba watu walikuwa wakimrushia mayai
yaliyooza Pamela alipokuwa akitembea mitaani miaka mitatu iliyopita? Habari hii inatuambia tusiwadharau wanawake. Nani anajua ni lini atakuwa na nguvu na kuinuka tena?]
Wakati huo, Rodney alipigwa na butwaa

akitazama mfululizo wa taarifa hizo. Hakufikiri kwamba baba yake alikuwa akizingatia jambo hilo kwa uzito. Kwa njia ya haraka, alikuwa amemkana hadharani na wanafamilia wengine wa Shangwe walifuata nyayo.
Zaidi ya hayo, Nathan alimchukua Pamela kama binti yake wa kike pia.
Huyo mwanamke amekuwa dada yake? Hapana, si dada yake. Hakuwa hata na damu ya familia ya Shangwe kwanza.
Alikuwa kwenye hatihati ya kulia. Ingawa tayari alikuwa amefikiria matokeo mabaya zaidi yanayoweza kutokea asubuhi yake alipoamua kumlazimisha Pamela akatoe mimba, bado alihuzunika sana wakati huo ulipofika.
Wakati huo, Rodney alihitaji sana mtu wa kumfariji. Aliweza tu kumwita Sarah. “Sarah, nimekataa kumuoa Pamela. Lakini...nimefukuzwa kutoka kwa familia

ya Shangwe. Hutajali, sawa?"
“Kwanini... Kwanini nijali? Umefanya mambo mengi kwa ajili yangu... nimeguswa sana.” Sarah alishikilia msukumo wa kumkaripia. Kisha akasema kwa sauti ya chini, “Laiti ningejua mapema kwamba familia yako hainipendi sana...”
“Sarah, usiseme zaidi. Tayari nimefanya uamuzi wangu. Mtoto wa Pamela hatakuwa na uhusiano wowote nami katika siku zijazo,” Rodney alimkatisha kwa kuudhika.
Akimzungumzia Pamela, Sarah alikaribia kutema damu. "Kwanini baba yako mdogo alimchukua kama binti yake wa kike?"
Kuwa binti wa Rais mtarajiwa kulimuuma sana Sarah Hakupata picha ikiwa ni yeye ndiye angepata cheo hicho. Ingawa hakuwa binti yake wa kumzaa, utambulisho huo ulikuwa na nguvu za kutosha hivi kwamba Pamela angeweza kufanya chochote

anachotaka nchini Kenya sasa. Pamela angeweza kuolewa na kuwa na familia bora katika siku zijazo pia.
"Labda familia yangu ilifanya hivyo ili kufidia hatia yao." Rodney pia alishuka moyo. "Sahau. Wacha tu. Mwanamke huyo ana mahesabu makali sana. Mwishowe, alifanikiwa kupata alichotaka.”
Asahau? Je, jambo hili lingewezaje kufutika hivi hivi kwenye kichwa cha Sarah? Sarah alikuwa na hamu ya kumtukana kwa sauti. Alimwonea wivu sana Pamela. Yule b*tch amewezaje kuwa binti wa Rais wa baadaye? Alitaka utambulisho huo pia. Afadhali kuachana na Rodney.
Japo Rodney kweli alirudi upande wake mwishoni, lakini, bila usaidizi wa familia ya Shangwe, angekuwa tu mtu wa kawaida sasa bila kujali kama kampuni yake ya Osher Corporation ingefanya vizuri au la. Isitoshe, familia ya Shangwe ilikuwa

imemkataa. Ingekuwa ngumu zaidi kwa Rodney kuendelea katika ulimwengu wa biashara.
Hakuna mtu ambaye angemjali tena hata kidogo. Rodney angekuwa maskini kuliko Sarah sasa.
“Rodney, nadhani lazima utakuwa umekasirika sasa. Pumzika vizuri kabla ya kuomba msamaha kwa familia ya Shangwe. Hakuna chuki zinazodumu usiku mmoja kati ya baba na mwana.” Sarah akakata simu na kumwacha hivyohivyo.
Rodney alipigwa na butwaa. Alikuwa akitaka kuzungumza naye zaidi ili kupunguza hisia zake za kukata tamaa.
Akawaza na kumpigia Chester. "Chester, niko katika hali mbaya. Twende tukanywe usiku huu...”
“Siendi.” Chester alimkataa mara moja.

“Bado wewe ni rafiki yangu?” Rodney alikasirika.
"Sitaki kunywa kwa sababu ya ujinga wako." Chester alimkemea kwa ukali, “Rodney, sikuwahi kufikiria ungekuwa mjinga kiasi hicho! Ulimlazimisha Pamela kutoa mimba na hata kumfanya aanguke kwenye ngazi? Ulikuwa unafikiria nini?”
“Mimi... nilitaka tu kumridhisha Sarah. Sitaki kupata mtoto wa nje ya ndoa. Sarah na mimi tutapata watoto siku zijazo,” Rodney alisema akijitetea.
"Mm, basi natamani nyinyi wawili mpate watoto katika siku zijazo. Kikumbusho tu, lazima uwe na adabu wakati wowote unapomwona Pamela katika siku zijazo. Yeye ni binti wa baadaye wa Rais. Sentensi moja tu kutoka kwake inaweza kukuangusha chini.” Chester alicheka kabla ya kukata simu.

Uso wa Rodney ulijawa na aibu na huzuni. Alikuwa akiufuata moyo wake tu, kwanini kila mtu alikuwa akimtenga?
Sura ya: 549
Jioni.
Lisa alipeleka chakula hospitali. Pamela alimpa macho ya kuomba msamaha. “Lisa, nakuonea huruma kwa kukusumbua unihudumie. Kwanini usirudi? Nitamwomba Sasha aje.”
“Ni sawa. Ningekuwa rafiki gani ikiwa ningekutekeleza nyakati hizi? Isitoshe, nilipokuwa mjamzito huko Marekani, hukunitunza vizuri pia?”
Lisa aligundua kuwa Pamela hakuwa na furaha sana. Hata hivyo, aliweza kuelewa. Kuzaa mtoto ambaye hakuwa na baba ni vita vya ujasiri kwa mwanamke yeyote.

“Hiyo ni sawa. Nilijisikia furaha sana kutumia wakati na Suzie na Lucas huko Marekani. Kwa kweli, watoto ni wazuri sana pia.” Pamela ghafla alijisikia faraja alipokuwa akiwaza jambo hilo. "Siku hizi, kuna wanaume suruali wengi sana. Ni bora kuzaa mtoto wako tu. Wengi wanaishia kuchumbiana tu na kutofunga ndoa.”
"Bado utakuwa na fursa nyingi, haswa baada ya kuwa binti wa Rais wa Kenya. Kutakuwa na wanaume bora tu wanaokufuatilia."
"Mm-hmm." Pamela alicheka. "Nani anajua? Labda baada ya miaka michache, nitakuwa nikitembea kwenye ukumbi mkubwa wa karamu nimevaa gauni refu. Nitakapowaona wale shetani wawili, Rodney na Patrick, wakiinamisha vichwa vyao kwa unyenyekevu na kusimama kando, nitapunga mkono wangu na kusema, 'Walinzi, toeni vipande hivi viwili vya takataka hapa. Hawastahili kuwa hapa na

kuchafua macho yangu matukufu kwenye hafla kama hii.”
Lisa alishusha pumzi baada ya kumuona Pamela hatimaye akitabasamu.
Baada ya kumaliza kula, alimpigia Kelvin simu. " Samahani. Siwezi kuhamia kwako usiku wa leo. Sikujua hili lingetokea kwa Pamela...”
“Ni sawa. Yeye ni rafiki yako. Unapaswa kuendelea kumhudumia zaidi."
Kelvin alisema kwa upole, “Mko wodi gani? Nitakuja kuwatembelea baadaye.”
"Ni sawa, hakuna haja. Watu wengi sana kutoka kwa familia ya Shangwe wanapishana hapa kila dakika. Pamela pia anahisi kizunguzungu Tunapaswa kumwacha apumzike.”
“Sawa, nitakuja kesho.” Kelvin alisitasita kwa muda kabla ya kuuliza ghafula, * Je, kweli Nathan anamchukua kama binti yake wa kike?”

“Bila shaka. Nathan mwenyewe hata alitoa taarifa binafsi. Pamela atakapokuwa sawa, familia ya Shangwe itafanya sherehe kubwa ya kumtambua Pamela.”
Kelvin alisema kwa kina, "Inaonekana kama ajali hii ilikuwa baraka kwa Pamela. Binti wa Rais, utambulisho huu kwa kweli ni wa ajabu."
'Ni sawa tu. Pamela sio mtu anayejali mambo haya.” Lisa alikunja uso aliposikia maneno yake.
Hakufikiria kuwa ajali ile kweli ilikuwa baraka kwa Pamela. Ilikuwa sawa ikiwa watu wengine wangesema hivyo, lakini Kelvin alikuwa mtu aliyewaelewa. Kwa kusema maneno hayo... Ilikuwa ni ajabu kidogo.
Muda si mrefu baada ya Lisa kurejea wodini, sauti ya mtu akigonga mlango ilitoka nje. Aligeuka nyuma na kumuona

Alvin akiingia ndani huku taa nyeupe za wodini zikimulika. Alikuwa amevaa shati jeupe lililochomekewa kwenye suruali nyeusi. Alionekana kama mwanafunzi
“Kwa nini uko hapa?” Lisa alikunja uso tena.
Pamela alimpa Alvin jicho la pembeni pia. "Alvin, hatuko karibu na wewe, sawa?"
“Nilisikia kutoka kwa Chester kwamba rafiki yako amelazwa na uko hapa ukimhudumia. Nilikuja kutembelea." Alvin aliweka vitu mkononi mwake kwenye meza. "Hii ndiyo juisi fresh ambayo hutengenezwa pekee kwenye hoteli ya nyota tano na imetengenezwa hivi punde, na—"
"Sijali kuhusu juisi hata kidogo," Pamela alinung'unika, "Unaona hii meza? Vitu hivi vyote ni — ”
“Basi kuna samaki kamba hapa. Nilinunua kwa ajili yako.” Alvin alimtazama ghafla

Lisa. Macho yake yalikuwa ndani sana hata mtu angeweza kuzama ndani yake.
Maneno ya Pamela yalimkaba kooni. Kamba? Walikuwa ni samaki aliowapenda sana, lakini angeweza hata kula?
Uso wa Lisa ulilegea kidogo. “Asante, lakini naweza kununua mwenyewe ikiwa nataka kula. Aidha, Pamela hawezi kula hii kutokana na hali yake. Utakuwa unamjaribu tu.”
“Lisa hata kama hunipendi, si lazimaunijibu kikatili hivi.”
Alvin aliumia sana kukataliwa na Lisa. Uso wake mzuri ulikuwa umelegea kwa kukata tamaa. Uso huo, ambao ulionekana kana kwamba ulikuwa umechongwa kwa ustadi na miungu, ulionekana mpweke sana hivi kwamba mwanamke yeyote asingeweza kuuvumilia. Hata Lisa alikuwa ameduwaa kwa muda. Ni kana kwamba alikuwa

amemuumiza. Lakini, baada ya muda, alisema bila hisia, "Yaliyopita ni ya zamani. Nilikupenda sana zamani, lakini sikupendi tena kwa sasa.”
Pamela hakuweza kupinga kushusha pumzi. Maneno hayo yalikuwa makali sana. Alipoona sura ya Alvin ikionekana kupauka na kuumia, akataka kupiga makofi.
Hata hivyo, Alvin hakutaka kukasirika. Aliweka vitu vyake kwenye meza.
Hali yake ya unyenyekevu na mvumilivu ilikaribia kumfanya Pamela kuwa kipofu.
Alvin alifungua bakuli lililokuwa na samaki. Samaki wakubwa wa kamba mle ndani na harufu yake kali iliyafanya tumbo la Lisa na Pamela kuunguruma.
"Alvin, ikiwa unataka kula, unaweza kwenda kula nje?" Lisa alisema huku akihisi kuchanganyikiwa.
"Ninawachamgua kwa ajili yako.

Nitaondoka nikimaliza.” Alvin alisema bila kuinua kichwa chake, “Hata sawa usipokula. Nitawaacha tu hapa baada ya kuwachambua hata hivyo.”
Wakati huo, mtu mwingine aliyekuja kutembelea Pamela alitokeza mlangoni. Alikuwa Jerome. Mikononi mwake kulikuwa na waridi na baadhi ya vyakula vya wagonjwa. Alikuwa na tabasamu la shauku kupita kiasi. "Halo, Lisa. Ni sadfa iliyoje! Tunakutana tena.”
"Jerome, kwanini uko hapa?" Uso wa Lisa ulizidi kukosa raha.
"Pamela, unafahamiana na Jerome?"
"Simjui." Pamela akatoa macho yake.
Jerome alijifanya kana kwamba hakusikia hivyo. Alitabasamu na kusema, “Nilikuja kumtembelea Bi. Pamela. Bi. Pamela ni binti wa Seneta Nathani Shangwe. Uncle wangu na Nathan Shangwe ni watu

wanaofahamiana, kwa hiyo akaniomba nikutembelee.”
Uncle wake aliyekuwa akimzungumzia alikuwa Mason. Lisa alidhani mara moja kuwa familia ya Campos ilikuwa ikichukua fursa hiyo kuanzisha uhusiano na Nathan. Pamela alikuwa ngazi ambayo walitaka kuitumia. Lisa alikosa la kusema. Familia ya Campos haikuwa na aibu kabisa.
Jerome aliendelea kuzungumza kwa uso wa kiungwana. “Sikutarajia ungekuwa mrembo zaidi ana kwa ana kulinganisha na picha, Bi.
Pamela. Ingawa wewe ni mgonjwa, uzuri wako bado unafanya moyo wa mtu kudunda...”
Alvin, ambaye alikuwa akichambua wale samaki wa kamba pembeni, ghafla alidhihaki kwa kusonya.
Jerome alimkazia macho kwa hasira. “Alvin, unafanya nini hapa? Nijuavyo, ulimsaidia Thomas kumuumiza Bi Pamela

hapo awali.
Mtu kama wewe ana haki gani ya kuwa
hapa?"
“Bado hawajanifukuza. Mbona una haraka sana? Tayari umekuwa mkwe wa Rais mtarajiwa?” Alvin aliinua uso wake mkali. KIM International ilikuwa tayari imeharibiwa, lakini umaridadi wake na macho yake ya kutoboa yalimfanya Jerome ahisi kufedheheshwa.
Pamela na Lisa walipigwa na butwaa. Lisa akasema mara moja, “Jerome, si wewe na Melanie tayari mmeoana?”
Jerome alipokuwa karibu kusema jambo, Alvin alimuwahi na kusema, “Ndoa inaweza kuvunjika kupitia talaka. Isitoshe, utambulisho wa sasa wa Melanie haulingani tena na wa Jerome, ambaye ni Bwana Mdogo wa familia tajiri kabisa ya Campos.
Je, haitakuwa bora kwake kama angeweza kuanzisha uhusiano na Rais wa baadaye?”

“Alvin, funga mdomo wako! ” Jerome alikasirika. Ingawa alikuwa na mawazo hayo, haukuwa wakati wa kuyajulisha. “Naupongeza tu zuri wa Bi Pamela, sijamtongoza. Je, unafikiri kila mtu ni kama wewe, kutoridhika na ulicho nacho na kutoa talaka kama mchezo wa kitoto?”
Alvin alimtazama kwa ukalii. “Huenda ikawa mara yangu ya kwanza kusikia mwanamume aliyefunga ndoa akisema maneno yenye utata kama vile ‘Uzuri wako hufanya moyo wa mtu udunde... ’ kwa mwanamke mwingine.”
Uso wa Jerome ulikuwa umetoka kwa aibu. Macho yake yalikuwa yakimtazama Alvin kwa ubaya. “Chunga mdomo wako, Alvin. Unahitaji nikukumbushe mimi ni nani hasa?"
“Unataka kunikumbusha vipi?” Alvin alitabasamu kwa kumkazia macho.

Jerome hakuwa na maneno ghafla. Hakuweza kusema kwamba angetafuta mtu wa kumfundisha Alvin somo. Kulikuwa na watu wengine wodini, kwa hivyo hakuthubutu kuwa mbabe sana.
Alipata wazo na kumtazama Pamela kwa shauku. “Bi. Pamela, unahitaji mimi kumfukuza mtu huyu?"
Pamela alipigwa na butwaa. Alimtazama Lisa kwa hisia. Mwishowe, alisafisha koo lake. "Lisa, unaonaje?"
Kila mtu alimkazia macho Lisa. Hata Alvin alimkazia macho. Lisa alikuwa na hamu ya kuwapiga teke Pamela na Jerome. Kwanini walimpkazia yeye aamue? Angeweza kumruhusu Jerome afanye. Hata hivyo, alipotazama sura ya Jerome ya kiburi na kisha akatazama macho ya Alvin ya huzuni... hakutaka kuegemea upande mmoja.
“Ningependa mwondoke wote wawili.

Mgonjwa anahitaji kupumzika. Tunaelewa nia yenu nzuri, lakini tafadhali ondokeni." Lisa aliwataka wageni kuondoka. Aliwapa wote wawili maagizo sawa.
Alvin alishusha pumzi kidogo. Alishukuru kwamba hakumruhusu Jerome kumfukuza. Lakini, Jerome alihisi aibu kabisa. Alikuwa bosi wa Campos Corporation, lakini alifukuzwa pamoja na Alvin.
Lakini hata hivyo alitii, Hadhi ya Pamela ilikuwa maalum sasa na Lisa alikuwa rafiki yake.
Jerome aliweza kuvumilia tu. Alilazimisha tabasamu na kusema, “Basi, hatutawasumbua tena. ”
Jerome alipoondoka, alimtazama Alvin kwa ukali. Alvin akasimama. Macho yake meusi na yenye kuvutia yalikuwa yakimtazama Lisa. “Nimemaliza kukuchambulia kamba, nitaondoka sasa.” Baada ya kuongea aligeuka na kuondoka.

Sura ya: 550
Lisa aliumwa na kichwa na kumshika paji la uso. Alvin alikuwa tayari hana uwezo wa kufanya mapenzi. Hakujua ni nini kingine alitaka kwake.
"Alvin amekuwaje?" Pamela akawa na hisia. "Yeye ni tofauti kabisa na Alvin niliyemjua zamani. Alikuwa na kiburi sana hapo awali, haswa sura aliyokuwa nayo wakati alipokunyakua wakati wa harusi. Nilifikiri hatawahi kukuacha maishani mwake.”
Asingeweza kumwacha? Hakuweza hata kufanya ngono tena.
"Je, inaweza kuwa kwa sababu alipata mshtuko mkubwa sana wakati KIM International ilipoanguka?" Pamela aliuliza.

"Sawa, acha kubahatisha majibu."
Lisa akaenda mezani. Kuangalia wale samaki kamba, alitaka kuwatupa mbali.
Lakini, bado aliishia kuonja mmoja wao mwishowe. Walikuwa watamu sana. Hatimaye, alimaliza kila kitu.
•••
Katika maegesho, Alvin alipofungua tu mlango wa gari, dharau ya Jerome ikasikika kwa nyuma. "Alvin, kwa kweli hukunionyesha heshima hata kidogo pale wodini sasa hivi."
“Kwanini nikuonyeshe heshima?” Alvin alijibu kwa ujeuri.
"Sawa, labda bado hauelewi ukweli kwamba unaweza kuweka mkia wako kati ya miguu yako wakati uko mbele yangu sasa." Jerome alitoa kicheko cha kichaa kabla ya kugeuka na kuingia kwenye gari lake.
Alvin alikunja uso. Muda si mrefu gari la

Alvin lilipotoka hospitalini, aligundua kuwa gari lake lilikuwa likifuatiliwa. Magari matatu yalikuwa yakimfunga kwa nyuma. Macho ya Alvin yalikaza. Akaongeza mwendo ghafla.
Magari hayo matatu pia haikuwa rahisi kukabiliana nayo. Waligonga gari lake kutoka kushoto na kulia.
Alvin akageuza usukani haraka. Alipita kwenye nafasi finyu sana kati ya yale magari kwa mwendo wa radi. Dereva wa moja ya gari alishtuka na kukanyaga mwendo wa kasi, akagonga gari lililokuwa mbele yake.
Alvin alitabasamu baada ya kuona hivyo. Haraka akabadili mkondo wake, akakanyaga mwendo wa kasi, na kuondoka kwa kasi. Yule jamaa aliyegonga gari lingine aligonga usukani kwa hasira. Akapiga namba ya Jerome. "Bwana Campos, tulishindwa."
“Hamna maana! ” Jerome alifoka.

Alvin alielekea kwenye kampuni. Alimkuta Master Ganja akiwa amesubiri hapo kwa muda mrefu akiwa na taarifa za kusikitisha. "Bwana Mkubwa, Joshua na Tobias wanaomba kuondoka ONA."
“Imekuwa watu wangapi wiki hii?” Alvin aliuliza kwa utulivu.
Ganja alikunja ngumi. Baada ya muda mrefu, alijipa ujasiri na kusema, “Bwana Kimaro, kwa kweli... ninapanga pia kutoa ombi la kuondoka ONA.”
Kidokezo cha kukata tamaa kiliangaza machoni mwa Alvin. "Kwanini, Ganja? Nilitumaini ulikuwa waaminifu na mimi. Kuna mtu anakuwinda?”
"Hapana." Ganja alisita kwa muda lakini aliamua kuwa mkweli mwishowe. “Maya ni mjamzito. ONA hairuhusu mapenzi kati ya

wanachama wake. Ndio maana napanga kujiuzulu. Zaidi ya hayo, nimechoka sana na aina hii ya maisha. Nitastaafu na kwenda kuishi na Maya katika siku zijazo."
Alvin alishangaa. Lakini, alielewa kuwa familia ya Kimaro ilikuwa na uhaba wa pesa kidogo. Kuihudumia ONA kulihitaji kiasi kikubwa cha pesa. Kwa kweli hakuwa na pesa nyingi wakati huo. Labda ingekuwa bora ikiwa wale watu ambao walitaka kuacha wangeondoka. Wale waliobaki nyuma ndio wangekuwa waaminifu kweli kwa familia ya Kimaro.
“Unaweza kuondoka,” Alvin alisema kwa utulivu, “nitapanga mtu mwingine kuchukua nafasi yako.”
"Asante." Ganja aligeuka kwa kuomba msamaha na kuondoka.
"By the way, Ganja..." Alvin alizungumza ghafla, "Jack alipotupwa kwenye

uchochoro, una uhakika kwamba hakuna mtu mwingine aliyejua kuhusu hilo?"
Ganja alishtuka, lakini bado akasema bila kuyumbayumba, "Hakuna mtu mwingine aliyejua."
“Sawa.”
Baada ya Ganja kuondoka, Hans hakuweza kujizuia kuuliza, “Bwana Mkubwa, ulimaanisha nini kwa swali hilo la mwisho?”
"Sikutarajia Maya kuwa na ujauzito wa mtoto wake.” Alvin aliinua uso wake. Kulikuwa na mwanga katika macho yake. "Siku zote nilifikiri Ganja alikuwa mtu mwaminifu na mtulivu hapo awali. Lakini leo, nimegundua kuwa nilikosea. Ikiwa mwanamume anaweza kuacha kazi kwa ajili ya mwanamke, ina maana kwamba mwanamke huyo ana nafasi muhimu katika moyo wake.

“Unamaanisha?”
"Umesahau kuwa Maya amekuwa akimlinda Sarah kwa karibu katika miaka hii mitatu?" Alvin alimkumbusha Hans, “Sarah ni mtu wa aina gani? Katika miaka hii mitatu, Maya kila mara alimtetea Sarah. Maya anaweza kutumiwa na Sarah kutuzunguka pia. Yeye si mtu rahisi. Nilimshuku hapo awali, lakini nilimwamini Ganja.”
Hans alielewa mara moja. “Lakini sasa Maya ana mimba ya mtoto wa Ganja. Ganja anaweza kuwa ameficha baadhi ya mambo kutoka kwako ili kumlinda Maya. Bwana Mkubwa, unataka tuweke mtu wa kumfuatilia Ganja?"
“Utampata nani sasa hivi?” Alvin alitabasamu kwa uchungu. “ONA ndiyo nguvu yangu ya mwisho. Lakini, mara tu Ganja akiondoka, kutakuwa na wanachama zaidi wa ONA ambao watataka kuondoka.

Ngoja tuone. Wale ambao wako tayari kubaki hadi mwisho ndio watakuwa waaminifu zaidi. Nitaomba mtu amchunguze Ganja na Maya wakati huo utakapofika.”
•••
Saa mbili usiku, baada ya Kelvin kutoka kwenye hafla ya kijamii, aliingia kwenye Sedan yake.
Ghafla, akagundua dereva aliyekuwa mbele hasogei hata kidogo. Alihisi kuwa kuna kitu kilikuwa kibaya. Alipotaka tu kugeuza kichwa chake, bunduki ilibanwa kwenye paji lake uso.
“Usisogee. ” Mwanaume mmoja alikuwa akicheka hatari.
“Nani... wewe ni nani?” Kelvin alimtazama mtu aliyekuwa kando yake kwa kona ya macho yake. Mtu huyo alikuwa amevaa kinyago cheupe. Alionekana wa kutisha sana.

Kulikuwa na mtu aliyevaa kinyago cheusi akiwa amekaa kwenye siti ya mbele ya abiria pia. Alikuwa anacheza na kiberiti cha gesi katika hali ya utulivu. Umbo lake kubwa lilifanya kila mtu ndani ya gari kuonekana mdogo ghafla.
"Mimi ni mtu ambaye anataka kukuambia kitu." Yule mtu aliyekuwa akicheza na kiberiti alisema, “Kelvin, usimguse Lisa.”
"Nyinyi ni watu wa Alvin?" Macho ya Kelvin yalipoa.
Kama angekuwa Alvin nyuma ya hili, Kelvin angemfanya akabiliane na matokeo mabaya. Alvin asingeweza kuinuka tena katika maisha haya. Kelvin alikuwa anataka kumfunza Alvin somo kwa muda mrefu.
"Hapana." Yule mtu akawasha kiberiti cha geti na kuchoma sigara. Katika gari lenye giza, moto ulionekana. "Unahitaji tu kukumbuka maneno yangu. Ukimgusa Lisa,

sitakaa hapa na kukupa nafasi nyingine tena. Mara moja nitakupiga risasi kichwani.”
Kelvin alikunja ngumi. Mwili wake ulitetemeka kwa hasira. Hata hivyo, ni kana kwamba mtu huyo hakuweza kuona hali yake. Sauti yake ilikuwa baridi. “Najua pia, mlimuua Hisan kwa kutumia wauaji kutoka Somalia.”
Kelvin alishtuka. Hakuna mtu aliyejua juu ya muuaji isipokuwa Mason, kwa hivyo mtu huyu angewezaje kujua hilo?
"Pia najua ... hisia zako kwa Lisa Jones hazijawahi kuwa za kweli tangu mwanzo." Mtu huyo alicheka ghafla kwa sauti ya chini. "Labda watu wengine wangekuwa na upendo usioyumba na usio na mwisho, lakini upendo wako kwa Lisa una hila na ni unafiki mtupu."

Mwili wa Kelvin ulitetemeka.
Mtu huyu alikuwa nani? Kwanini mtu huyu
alijua siri zake wakati hakuna mtu anayepaswa kujua?
“Usimguse Lisa Jones. Usimguse, au nitakapokuona tena, utakuwa maiti. Unaweza kujaribu..."
Yule aliyejifunika sura kwenye kiti cha abiria alifungua mlango wa gari. Kisha, gari jeusi lisilo na nambari ya leseni likapita. Yule mtu wa upande mwingine wa Kelvin pia alijiondoa. Wale watu wawili kwa haraka wakaingia kwenye gari na kuondoka.
Kelvin alipiga ngumi ngumu juu ya kiti cha ngozi cha gari, uso wake mzuri ulijaa hasira na hofu.
Mtu kama huyo alitokea wapi? Hata alijua kuhusu mauaji ya Hisan?

"Bwana Mushi." Dereva akageuka nyuma huku akitetemeka.
"Tambua mtu huyo ni nani," Kelvin alitoa amri kwa sauti mbaya.
“Sawa. Tunaenda nyumbani sasa?" dereva aliuliza.
"Hapana, nipeleke kwenye klabu."
Kelvin alikasirika. Hapo awali alitaka kurudi nyumbani, lakini alikuwa amepoteza hisia zake. Maneno ya mtu huyo yalikuwa yamemfanya awe makini. Baada ya yote, mtu huyo alijua mengi sana. Hakuthubutu kucheza kamari. Hakuwezi kuwa na makosa katika mpango wake.
INAENDELEA LISA KITABU CHA 12

ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully.
Hata kama niko nyuma sana....., huyu Mzee ndo Babaake Alvin Mzee wa mipango mingi.....

Namfananisha na Mzee mmoja kwenye Black List Mzee wa plan mingi Bwana Raymond[emoji3]
 
Back
Top Bottom