THE JAGGERS
JF-Expert Member
- Apr 3, 2023
- 545
- 410
hahahaha.Oyaa amka bhanaa ni ndoto hiyoo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahahaha.Oyaa amka bhanaa ni ndoto hiyoo
Duuu kutiana genye tu kundomba aaahMIMI NA MIMI 2
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI
★★★★★★★★★★★★★★★★
Niliendelea kumkumbatia Miryam kwa sekunde chache nikiwa nahisi furaha sana, kisha nikamwachia na kumtazama usoni kwa hisia sana. Yeye pia alikuwa akiniangalia kwa macho yenye hisia kwelikweli, nami nikatikisa kichwa kidogo nikiwa yaani bado siamini-amini.
"Aisee! Yaani sijui hata niseme nini..." nikaongea hivyo kwa hisia.
Akatabasamu tu na kuendelea kuniangalia kwa upendo.
Nikasema, "Wee... ume... umefikaje hapa haraka hivi? Yaani... usiniambie umekimbia kutokea Kijichi..."
Akacheka kidogo kwa pumzi, naye akasema, "Kwani hujui kwamba nina gari?"
"Ahahah... this is amazing..." nikamwambia hivyo kwa sauti yenye hisia sana.
Akabaki akinitazama usoni kwa macho yenye upendo mwingi, nami nikalishika shavu lake kidogo huku nikimwangalia kama vile nataka kumtafuna, siyo kwa ubaya, ila kwa hamu nzuri na kubwa sana niliyokuwa nayo kumwelekea. Ndipo sauti ya koo kusafishwa ikatokea pale sebuleni, nami nikaangalia hapo na kuona Ankia alikuwepo bado. Miryam akageukia huko pia.
Nikasema kwa kujishaua, "Ankia? Kumbe bado upo?"
"Ulifikiri me jini nimepotea, au?" Ankia akaniuliza hivyo.
Miryam akatabasamu kiasi.
"Kwanza unatakiwa uwe umeshapotea, unafanya nini hapa? Hebu... go away..." nikamwambia hivyo Ankia kiutani.
"Mm? Yaani ndiyo umeshaanza na kuringa..." Ankia akaniambia hivyo kwa njia ya nyodo.
"Siyo kuringa, we' si ulikuwa unaenda dukani? Nenda..." nikamwambia hivyo.
Ankia akaniangalia kwa njia yenye nyodo na kuikunja midomo yake, na Miryam akacheka kidogo tu na kujishika shingoni.
Nikamfanyia Ankia ishara ya kumfukuza kwa kiganja na kumwambia, "Shoo!"
Ankia akacheka kwa mguno, naye akamwambia Miryam, "Baadaye mpenzi."
Miryam akatikisa kichwa kukubali heri hiyo, naye Ankia akawa ameondoka hatimaye. Raa!
Miryam akanigeukia na kunitazama usoni tena, nami nikamwangalia na kujichekesha kidogo kwa haya eti. Nikawa nahisi hali ya utete kidogo, nikiangalia pembeni huku napiga-piga kiganja changu kimoja mguuni, kisha namwangalia tena na kukuta amenikazia jicho tu, halafu sote tukajikuta tunacheka kidogo kwa kupatwa na hisia nzuri sana.
Ndipo nikamwambia, "Karibu. Njoo ukae... aa... namaanisha... siyo humu chumba... yaani... kama... utapenda tukae humu... chumbani.... au, pale... sofani... simaanishi ukiingia chumbani nita... siyo kwamba nafikiria hivyo... ila we' ndo' unaweza ukawa unafikiria... siyo kwamba... namaanisha... sikuoni unawaza... dah, naharibu aisee..."
Miryam akacheka kidogo na kutikisa kichwa chake, naye akasema, "Wasiwasi wa nini sasa tena?"
Nikafumba jicho moja na kumwangalia kwa kujihami eti.
"Ahah... me ndiyo ningetakiwa niwe na wasiwasi, maana...."
Kabla hajamaliza kuongea, nikamkumbatia kwa mara nyingine tena ili kumpa kitulizo, ambacho na mimi kwa upande wangu nilikihitaji sana. Nilihisi amani kubwa sana moyoni, na nilihitaji aihisi pia. Nikawa nimemshikilia huku nikiyumbisha miili yetu taratibu kama vile nambembeleza yaani, naye alikuwa ameiweka mikono yake mgongoni kwangu na kuitembeza taratibu huku amenilalia begani kwa raha zote. Yaani!
Nikiwa bado nimemkumbatia, nikasema kwa sauti ya chini, "Vipi tukikaa?"
Akajibu kwa sauti yake tamu, "Wazo zuri."
Nikamwachia taratibu kabisa, halafu tukatazamana machoni kwa hisia sana, kisha nikakishika kiganja chake na kwenda naye mpaka pale sebuleni na kuketi sofani. Akakaa pembeni yangu pia, huku nikiwa nimekishika kiganja chake bado, naye akakiweka kingine juu ya mkono wangu, na chenyewe nikakishika.
"Umeni-surprise sana Miryam..." nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.
Akatabasamu kiasi na kusema, "Najua. Samahani kwa hilo."
"Samahani ya nini sasa? Haujui kwamba umenipa furaha sana?"
"Wakati tayari nilikuwa nimeshakuvunja moyo?" akasema hivyo huku akiniangalia usoni kwa umakini.
Nikatulia tu na kuendelea kumwangalia.
Akasema, "Jayden... I'm sorry. Nimekutesa sana... I know..."
"Usijali. Nilikuwa nakuelewa."
"Still, yaani... nimekufanyia vibaya mno. Pamoja na yote, umefanya vingi sana kwa ajili yangu kunithibitishia unanipenda, lakini nikawa nakupiga mateke tu. Najua nilikuwa nakuonea sana, na naomba tu unisamehe kwa leo... yaani bado nilikuwa nimechanganyikiwa..."
"Ulichanganywa na nini?"
"Kila kitu. Nilikuwa najiuliza... kwa nini niko hivi. Nimekupenda pia, lakini bado tu nikawa najipofusha kwa kiburi changu...."
"Miryam..."
"... ambacho kinanifanya nijione kuwa sahihi kwa kila kitu. Umenifundisha sana, umeshanionyesha kwamba kuwa hivyo haifai, lakini bado nikawa sielewi. Ni kweli," akasema hivyo kwa hisia.
Nikaanza kusugua kiganja chake taratibu.
"Leo... nimeshindwa Jayden. Nimeshindwa kuendelea kujifanya mgumu tena. Nakupenda. Na ninakuhitaji. Sijui kingine tena," akasema hivyo.
Nikatabasamu kiasi kwa hisia.
"Lakini... bado naogopa. Na baada ya ulichoniambia leo, nimetambua kuwa nakuhitaji zaidi sasa ili niache kuogopa tena. Umesema unaniona me kuwa kama msaada kwako..."
"Yeah, kabisa."
"Well, na mimi nakuona kuwa msaada wa moyo wangu. Nimetambua pia kwamba wewe ndiyo kipande cha pili cha moyo wangu kinachokosekana ili kuufanya uwe kamili, na ninakuhitaji uwe karibu nami ili uunganike pia na kuwa kitu kimoja," akaongea kwa hisia sana.
Dah! Alikuwa na maneno matamu!
"Kwa hiyo wakati huu mimi ndiyo nimekuja kukuomba nafasi Jayden. Uko tayari kunibeba?" akaniuliza hivyo.
Nikamkazia macho kiasi, nami nikamuuliza, "Hilo ni swali au jibu?"
Akatabasamu na kuangalia chini.
Nikamshika shavuni taratibu, naye akaniangalia. "Kwa asilimia zote, Miryam. Niko tayari. Unalijua hilo."
Akasema, "Mambo yatakuwa mengi, na magumu sa...."
"Usijali Miryam. Niko nawe. We are two parts of the same whole now, and I intend to keep it together no matter what..." nikatia na kimombo kidogo kumfariji.
Akakishika kiganja changu usoni kwake, naye akasema, "Asante."
Nikampa tabasamu hafifu kwa hisia.
Akashusha pumzi na kuangalia chini kwa utafakari, naye akasema, "Nina hamu kubwa... na matarajio mengi kuona ni wapi hii itanifikisha."
Nikamwachia taratibu usoni na kusema, "Hata mimi. Na ninaiona kuwa sehemu nzuri sana, sema ndiyo nataka niifikie nikiwa pamoja nawe."
Akatabasamu na kuendelea kuniangalia kwa hisia sana machoni.
Nikajikuta nimetulia zaidi, nikimtazama kwa njia hiyo hiyo yenye hisia kama yeye tu, na mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakienda mbio kwa sababu ya hisia zangu kunitaka nifanye jambo fulani. Niliiangalia midomo yake na kuona jinsi ambavyo iliachia uwazi kidogo uliofanya mpaka nikahisi kusisimka yaani, na nilipomtazama machoni, akawa bado ameniangalia tu kwa njia yenye subira.
Nikataka kupiga hatua kumwelekea kwa kuusogeza uso wangu karibu zaidi na wake, lakini akaacha kuniangalia na kusema, "Inabidi niingie nyumbani Jayden."
Nikainamisha uso wangu kiasi na kubana midomo, kisha nikatikisa kichwa kukubali hilo. Nilipomtazama usoni, nikakuta ananiangalia huku akitabasamu kiasi, nami nikajirudisha nyuma na kuangalia pembeni kwa njia ya kujishaua. Alikuwa amenisoma huyo!
Nikasema, "Sawa... najua umechoka. Nenda tu... ukapumzike."
Akatikisa kichwa kukubaliana na hilo, halafu akasema, "Na wewe ndiyo ulikuwa unaingia kupumzika bila shaka..."
"Eeh... nilikuwa nahisi uchovu... sijui hata wa nini, ila... sa'hivi umeisha. Nimepata nguvu mpya," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu na kusema, "Vizuri."
Kulikuwa na kale kahali kenye kusisimua fulani hivi, yaani, mpaka raha. Nilimtazama kwa upendo mwingi sana, naye akawa ananiangalia tu kama vile anasubiri nimuage vizuri.
Ndiyo akaniambia, "Narudi hapo Masai kwanza."
"Masai? Kwa nini? Yaani... hauendi nyumbani? Si umesema...."
"Nililiacha gari pale, ndiyo nikaja hapa," akanikatisha kwa kusema hivyo.
"Oooh, sawa. Ngoja. Kwa nini uliliacha gari Masai?" nikamuuliza.
"Nilipokuwa nakuja... sikutaka kuja mpaka huku na gari, hapo nyumbani wangeona maana... nilikuwa nataka kwanza..." akaishia hapo.
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Uje kwangu."
Akatabasamu pia na kutikisa kichwa kukubali.
Nikamwambia, "Okay, nimeelewa. Umetumia akili, maana wambea wengi."
"Hapa penyewe nikitoka wakaniona, inaweza kuzua utata..."
"Oh no, haina shida. Sidhani kama ina shida. Hata hivyo we' siyo mgeni hapa, hao wakina Fatuma watajua umekuja tu kumsalimia Ankia labda..."
"Labda..." akasema hivyo na kuangalia pembeni.
"Ahah... naitamani ifike siku ambayo tutatembea pamoja... proud... kila mtu ajue kwamba wewe ni wangu," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu na kusema, "I hope for that day to come too. Ila kwa sasa... tuweke mambo yetu chini kwanza..."
"Yeah, yeah, najua. Chochote kile unachotaka tufanye, nitafata..." nikamwambia hivyo.
Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
Nikiwa namwangalia kwa hisia, nikamwambia, "Asante Miryam. Kwa kunipa hii nafasi. Nitajitahidi kuwa mume mzuri kwako."
Akatabasamu zaidi na kuuliza, "Mume eeh?"
"Ahahah... kidume wako," nikamwambia hivyo na kupandisha nyusi kichokozi.
"Ahah... sawa. Mimi pia. Nitajitahidi kukupa furaha Jayden," akaongea kwa sauti yake tamu sana.
Nilimwangalia huyu mwanamke kwa mapenzi ya dhati yote niliyohisi moyoni, yaani nilipenda sana hii hali aliyokuwa ananifanya niihisi wakati huu. Akiwa ananitazama kwa hisia pia, akanishika shavuni kwa kiganja chake laini, halafu akausogelea uso wangu karibu zaidi na kunipa busu moja, moja tu, ambayo ilinipa msisimko wa hali ya juu zaidi ya msisimko wa busu mia moja ambazo mwanamke mwingine yeyote angenipa!
Midomo yake laini iliikandamiza ya kwangu na kuvutana nayo mara moja tu na taratibu kabisa, naye akaiachia ikiwa imetoa sauti tamu kama vile ametoka kufyonza pipi tamu sana, kisha akajirudisha nyuma tena na kuniangalia kwa hisia. Sasa hapo mimi! Huo msisimko ulikuwa umeniamshia bonge moja la balaa, damu ilianza kunyanyua mdude fulani kwa nguvu isiyopimika, yaani nilihisi mwili wote unaitikia kitendo chake kidogo tu kwa hamu nzito sana. Nikabaki nikimtazama machoni kwa utulivu, huku hisia zangu zikiwa zinafurukuta huku na huko ndani yangu.
Akiwa anasugua shavu langu kwa kidole chake taratibu, akasema, "Nakupenda."
Yaani aliisema hiyo 'nakupenda' katika ile njia ya kiutu-uzima, uhakika yaani, hakuona aibu wala kuhofia kuniambia hivyo. Alijivunia kabisa.
Nikatabasamu tu na kumwambia, "Nakupenda pia."
Nilikuwa nimeweka mkono wangu usawa wa sehemu ya kati kwenye suruali ili kuficha saibu lililokuwa limenyanyuka baada ya yeye kunipiga busu kwa mara ya kwanza kabisa, na mwanamke wangu akanyanyuka kutoka hapo sofani na kuanza kuelekea mlangoni. Ikanibidi niendelee kutulia tu hapo hapo sofani maana sikutaka aone hili dubwana mapema namna hii, bado hayo mazoea sikuwa nimemwanzishia kwa hiyo kujibana ilikuwa lazima. Akafungua mlango na kuniangalia kwa ufupi, nasi tukapeana tabasamu la furaha kwa pamoja, kisha ndiyo akatoka hatimaye. We!
Yaani ile ametoka tu, nikanyanyuka na kuanza kurukaruka hapo ndani, nikapanda na kwenye sofa na kuanza kuruka kwa furaha tele. Nilihisi furaha isiyo na kifani. Nilikuwa kama nimechanganyikiwa. Nikafata na simu yangu chumbani na kuweka muziki wa Jux na Dayamondi "bora kuenjoiiiiii... maisha mafupi ni simpoo," nami naikaanzisha miuno na dansi za kipuuzi ili tu niitoe furaha yangu. Nilicheza wimbo mpaka mwisho, nami nikajitupia sofani na kubaki najichekea mwenyewe tu kwa kuhisi raha kuu mno moyoni mwangu.
Hatimaye Miryam akawa wangu. Dah! Ingebidi kutokea hapa sasa nimwonyeshe namna gani ambavyo alikuwa akiukosa uhondo wa mapenzi kwa huo muda wote alioukosa. Yaani ningemfurahisha, angenipenda mpaka milele. Sikufikiria kuhusu changamoto, sijui matatizo na vikwazo, yaani nilichowazia juu yake ilikuwa ni furaha tu. Ya nini niteseke roho wakati Miryam alikuwa wangu? Hiyo kitu haingekuwa na nafasi tena!
Na ningehakikisha nampa furaha aliyoistahili kwelikweli, ili nami nitulie kwa furaha na amani tele moyoni mwangu. Siku ile nimemwambia ukweli kuhusu hisia zangu nilijipiga mara mbili kifuani ili kujipa moyo katika mbio za kuhakikisha namkamata, na sasa akawa amekamatika, hivyo ningetakiwa kujipiga mara nyingi zaidi kifuani wakati huu kwa kiburi changu chote kuwa ndiyo, nilimpata! Piga kifua kwa masifa kama King Kong yaani! Araa? Hatimaye Miryam alikuwa bibie wangu!
★★
Haukupita muda mrefu sana na Ankia akawa amerejea tena kutoka kazini kwake, ikiwa imeshaingia saa moja, na alinikuta ndani nikiwa najiandaa kutoka. Nilitaka kwenda gym kwanza kuchangamsha mwili kabla ya kuja kwenda kwa Miryam kuwasalimia wapendwa wangu, na muda ule ambao Miryam aliniacha hapa, tuliwasiliana kupitia sms, nikimuuliza ikiwa alifika kwake bila vilongolongo vingi, naye akawa amekubali. Kwa wakati huu akawa akishughulika na mambo fulani ya hapo kwao.
Ankia alikuwa na hamu ya kutaka kusikia mengi yaliyojiri baada ya kuniacha hapa na Miryam muda ule, nami nilikuwa na furaha sana bado lakini kwa wakati huu nilitulia zaidi. Nikamwambia ningekuja kumpa ukweli wote nikitoka gym, ila kiufupi tu ni kwamba ilikuwa siku iliyogeuka kuwa yenye amani kubwa sana kwangu. Sikutarajia yaani. Kwa hiyo ningetakiwa kwenda kuchangamsha mwili kwanza kisha ndiyo nije kumpa ubuyu aliotaka, na yeye nikamwambia atanipa ubuyu niliotaka kama malipo. Hakuelewa namaanisha nini, ila nilikuwa namwongelea Bobo, hivyo ingekuja kuelezeka baadaye.
Nikatoka hapo na kwenda hadi gym ya pale Mzinga, na tayari nilikuwa nimeshaanza kujuana na baadhi ya mangangali waliokuja hapo lakini sikupitilizisha sana mazoea, nami nikanyanyua na kushusha chuma kwa muda wa kama saa moja na nusu, kisha ndiyo nikarudi tena kwa Ankia. Sasa nilikuwa nimechangamka kwelikweli yaani, nikaoga na kuvaa vizuri, kisha ndiyo nikakaa pamoja na mwanamke huyo sebuleni kupiga story kidogo.
Ikiwa imeshaingia saa tatu, Ankia ndiyo alikuwa anaelekea kuivisha wali huko, nami nilikuwa nimemsimulia namna ambavyo Miryam alinifunulia hisia zake na kukubali tuanze mahusiano rasmi kabisa. Akanipongeza nakwambia, yaani utafikiri hatukuwahi kufanya mineng'emuo kabisa, na ndiyo nikawa nimemuuliza kuhusu Bobo sasa. Ankia alikuwa anajifanya kama vile hajui naongelea nini, lakini mwishowe akakiri kuwa ni kweli alianza kutoka kimahusiano pamoja na yule kaka, ingawa aliyapeleka taratibu ili kuhakikisha haumizwi. Na yeye nikampongeza pia.
Muda huu wote tangia nirudi kutoka gym, nilikuwa nasubiri tu Miryam anitumie ujumbe au nini, lakini hakufanya hivyo. Nikawa nimejaribu kumtumia ujumbe wa salamu, lakini hakujibu, hivyo nadhani alikuwa na shughuli bado. Nilikuwa nimemcheki na Tesha pia, ambaye bado hakuwa amerudi hapo kwao, hivyo nikaona nimuage tu Ankia kwa ufupi ili nikawasalimie wakina Bi Zawadi, kisha ningerudi kula. Kilikuwa kisingizio tu maana niliwashwa kweli kutaka kumwona bibie, kwa hiyo nikavaa malapa na moja kwa moja kwenda hapo kwake.
Nilipoingia tu getini, gari lake Miryam lilikuwa hapo nje, na pale varandani alikuwepo Shadya pamoja na bibie mwenyewe. Miryam aliketi mkekani huku akiwa anakwangua nazi kwenye mbuzi, na Shadya aliketi pembeni yake tu akiwa kama anampa umbeya mpwa wake. Miryam alivalia lile dera lake la kijani huku nywele zake zikiwa zimefunikwa kwa kilemba, na baada tu ya kuniona, akaacha kukwangua nazi na kuachia tabasamu hafifu kunielekea.
Nikaanza kuelekea hapo huku nikijitahidi kubana la kwangu, na Shadya akaita jina langu kama njia fulani ya kuniambia 'karibu.' Hii bado ilikuwa saa tatu, na ilinishangaza kidogo kukuta Miryam anakwangua nazi wakati huu. Alifika mapema nafikiri ile saa kumi na mbili, kwa hiyo sikujua kwa nini upishi ulikuwa umechelewa namna hiyo. Miryam akaendelea kukuna nazi, nami nikasogea mpaka hapo varandani nikiwa natabasamu kumwelekea Shadya.
"Habari za hapa wapendwa?" nikawasalimu.
"Safi tu," Shadya akasema hivyo.
"Salama," Miryam akaitikia pia.
"Ndo' umerudi?" Shadya akaniuliza.
"Ah, hamna, nilikuwepo tu toka kitambo. Kuna mishe nilikuwa nafanya kidogo... nilienda tu na gym kupasha kidogo, nikarudi tena," nikasema hivyo na kumwangalia Miryam usoni.
Miryam yeye akawa amejikausha kama vile hana muda na mimi na kuinamisha uso wake tu. Sikuiona simu yake hapo alipokuwa, hivyo ni wazi aliiacha ndani.
"Ahaa... ulikuwa umeenda kuongeza misuli kidogo," Shadya akasema hivyo.
"Eeeh..." nikakubali.
"Angalia usije ukakonda mashavu," Shadya akaniambia hivyo.
"Hahah... hamna, sizidishi. Halafu kidogo nisahau... jamani, Shadya shikamoo yako mkubwa," nikamwambia hivyo.
"Marahaba mwanangu. Na hili joto, angalau umekuja tununuliwe na soda," Shadya akasema hivyo.
"Ah, hapo usiwaze. Mnyama nmefika," nikamwambia hivyo.
Miryam akanyanyua uso na kunitazama usoni kwa mkazo.
"Hahaaa... eti mnyama! Tutoe jero jero basi tununue Afiya hapo kwa Fatuma," Shadya akasema hivyo.
"Aaaa... jero! Yaani badala uombe elfu kumi, unaomba jero? Jero na we' wapi na wapi?" nikamwambia hivyo.
"Hahaaa... usinifurahishe mie! Mbona itakuwa poa sana!" Shadya akasema hivyo huku akimtazama Miryam.
Miryam akawa ananiangalia kwa macho yenye kuhukumu, kimasihara yaani.
Shadya akasimama kabisa na kuninyooshea kiganja huku akisema, "Nitoe jembe langu la faida. Nachukua hapo sasa hivi."
"We' mwenyewe ndo' unaenda?" nikamuuliza hivyo.
"Eeh, nafata mwenyewe. Nipe," akasema hivyo.
Nikaingiza mkono mfukoni na kujifanya natafuta hela kwa bidii kweli, huku nikiona jinsi Miryam alivyokuwa akinitazama kwa macho makini, nami nikatoa sarafu mbili za mia tano na kumpa Shadya.
"Ih! Sa' ndo' nini JC?" Shadya akauliza.
"Inabidi tu upokee. Elfu kumi imegoma kutoka," nikamtania namna hiyo.
Akacheka kidogo na kusema, "Kumbe na we' mzushi tu..."
"Ahahahah... siyo sana. Maisha magumu..."
"Magumu wapi, mwone! Kama siyo uchoyo... wakati juzi umempa shangazi malaki kabisa..." Shadya akasema hivyo huku akianza kuvaa ndala.
"Ahahah... basi nisamehe. Ila na yako itakuja tu," nikamwambia hivyo.
"Siyo mbaya mwaya. Mimi, ngoja nifate Afiya tupoze koo..." Shadya akasema hivyo.
Akaelekea nje, nami nikamwangalia Miryam na kukuta anaendelea na kazi yake tu. Nikamfanyia 'pss, psss,' naye akaniangalia na kuninyooshea kidole chake kama kunionya nisimfanyie hivyo, nami nikacheka kidogo kwa pumzi.
"Mbona unakuna nazi muda umeenda?" nikamuuliza.
Akaacha kuniangalia na kusema, "Niliyemwagiza alete vitu alichelewa."
"Mmmm... na tokea muda ule hauku...."
Kabla sijamaliza kuongea, mlango wa kuingilia ndani hapo ukafunguka, na binti Mariam akawa ametoka. Nikatabasamu kiasi, na moja kwa moja binti akawa amenifata na kunisalimia, kisha kwa lazima nikavutwa ili twende ndani. Sikuwa nataka kumwacha bibie, yaani nilitamani nikae tu hapo niendelee kuongea naye kuhusu chochote, ila sikuwa na jinsi. Yeye mwenyewe alikuwa amekaza tu, ile kuvunga kwamba hatuna uvutano wowote bado ni kitu tulichohitaji kufanya kwa sasa na ndiyo alikuwa makini nacho.
Hivyo nikachoma ndani, nikakutana na mama wakubwa tena tokea ule mchana nilipowaacha, nasi tukakaa kupiga story mbili tatu. Shadya alirejea na kumletea Mariam juice ambayo ilipaswa kuwa ya Miryam, kwa kuwa bibie alimwambia ampe mdogo wake kama mbadala. Miryam akawa anapita na vyombo kuelekea jikoni, akishughulika na mapishi, na Mariam alikuwa akimsaidia. Sikupata nafasi ya kutazamana naye tena, wala kumtumia tu ujumbe kwa sababu simu yake ilikuwa chaji, na ile imefika mida ya saa nne, Ankia akanipigia simu kuniambia kwamba alikuwa amenipakulia; niende. Dah!
Ikanibidi niwaage tu hawa, huku moyoni nikiwa nimeumia kutoweza kutoa wonyesho wowote ule wa uvutano baina yangu na bibie, maana aliigiza vyema kama vile hatuna dili. Mariam alikuwa anataka nibaki mpaka chakula kiive hapa kwao, lakini nikamwelewesha tu kuwa Ankia alikuwa ameshapakua kabisa, kwa hiyo ningeenda kula ili asijisikie vibaya. Mama wakubwa wakanipa sapoti pia, na hatimaye binti akaniachia. Nilipotoka tu, nikamtumia Miryam ujumbe mfupi nikimwambia kuwa asiache kunicheki akitulia, nami ndiyo nikaelekea kwa Ankia.
★★
Msosi wa Ankia ulikuwa mzuri, wali na samaki, nasi tukala pamoja huku story zikiwa juu ya suala la Bobo kutoka na Ankia. Mchecheto wangu bado ulikuwepo, yaani nilikuwa nakula huku naongea na Ankia, lakini akili yangu yote ilikuwa kwenye simu. Nilikuwa nimeiweka pembeni nikisubiri iwake, na kila mara ilipowaka kuingiza ujumbe ningeichukua upesi kuangalia kama ni Miryam, lakini matarajio yangu yakawa yanapigwa chini maana ni watu wengine ndiyo waliokuwa wananicheki. Ilikera!
Ankia akawa ameona hilo, naye akaniambia si nimtumie tu ujumbe Miryam badala ya kusubiri yeye ndiyo anitumie, lakini nikazira, nikiiweka simu pembeni na kusema nisingejisumbua mpaka yeye mwenyewe ndiyo anitafute. Ilikuwa ya shingo upande tu hiyo, naye Ankia akasema haya, ila akagusia namna ambavyo aliona nilikuwa situlii kweli. Tulipomaliza kula, nikatulia tu na kuendelea kusubiri lolote kutoka kwa bibie, nikiwa nimeamua kuwa sitamtafuta kweli mpaka yeye ndiyo ashtuke.
Nikakaa na Ankia hapo sebuleni, tukiwaangalia wakina Efendi na nini kwenye TV, hadi inafika saa tano, bibie akawa kimya tu. Mh? Nikawaza labda alikuwa ananisikilizia ili mimi ndiyo nimcheki kwanza, lakini si nilikuwa nimeshatuma sms kadhaa? Kujibu hata mojawapo tu alishindwa? Nikafikiria kuwa inawezekana Miryam angekuwa na shughuli fulani tu iliyomweka bize, hivyo nikaona nikiondoe hiki kimuwasho cha kutaka tuwasiliane muda wote. Sikupaswa kusahau kuwa huyu alikuwa mwanamke mtu mzima mwenye mambo mengi, hakuwa kama pisi nilizopitia.
Ndani ya muda huo huo, Ankia akasema anaenda hapo Masai, Bobo kamwita. Nikampa ile "mhm" kikejeli, naye akanicheka kwa njia ya kejeli na kwenda chumbani kujiandaa. Haya bwana, mimi ndiyo ningebaki na kaupweke wakati ulipaswa kuwa muda wangu wa kuondoa upweke, angalau hata kwa simu tu. Mwenye nyumba wangu akatoka akiwa amevaa T-shirt la mikono mifupi, jeupe, pamoja na kikaptura-skinny kilichofikia mwanzo wa mapaja yake; juu kidogo ya magoti yaani. Alikuwa amejipiga na makunato mwenyewe, naye akaniaga huku akinitania kwa kusema kama vipi nimwite Miryam aje ili nisibaki kununa tu hapo.
Kejeli zote nikazipokea, sawa bwana, naye akawa ameniacha na kwenda huko ikiwa inaingia saa sita. Kwa watu wa aina yake, palikuwa ndiyo pamekucha. Hapo alikuwa ameitwa na bwana wake, wakanywe na kujifurahisha bila shaka, na kama ni kitu ambacho sikuwa nimesema awali, ni kwamba kwa kipindi hiki Bobo ndiye aliyekuwa ameachiwa usimamizi wa Masai YOTE, yaani awe kama mmiliki, lakini kwa muda tu. Kuna madili na madili inaonekana yalikuwa yamefanywa baada ya Bertha kukamatwa na Chalii kuuawa. Hivyo Ankia alikuwa analishwa bata haswa.
Mzee nikabaki sofani tu huku naitazama TV utadhani nina ugomvi nayo, nikiwa nimeshaghairi kuishika tena simu maana saa sita ilikuwa inatembea tu bila ya Miryam kuwa amenicheki. Nikawaza labda hata angekuwa ameshalala, si unajua labda uchovu na nini, kwa hiyo nikaona ni bora nichukue simu tu ili nimtumie ujumbe wa kumtakia njozi njema. Nikaishika simu, na ile nataka kumtumia ujumbe, ikaanza kuita hapo hapo. Tabasamu hafifu likajengeka usoni kwangu, maana ilikuwa ni bibie mwenyewe ndiye aliyepiga, nami nikapokea na kuweka sikioni.
"Hello..." sauti yake tamu ikasikika.
"Ndiyo ukaona unichunie mpaka sa'hivi, eti?" nikamuuliza hivyo nikijifanya nimeudhika.
"Ooh, I'm sorry... yaani, nilikuwa nimetingwa na kazi, yaani.... ah..." akaongea kama vile amechoka mno.
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Usijali, naelewa."
"Yaani nisamehe tu. Kuna jambo nafix hapa, kila mara linakua tu... nikashindwa hata kushika simu..."
"Ishu gani unadili nayo?"
"Ni ishu ya Mamu tu, hamna kwere. Nimemaliza kuandika, nilikuwa naandika barua fulani hapa..." akasema hivyo.
"Okay sawa. Nilidhani labda ungekuwa umeshalala..." nikamwambia.
"Hamna, bado niko macho. Yaani ndiyo nimeziona text zako za muda ule sa'hivi. Pole nimekuonea mno, eti?" akaongea kama ananibembeleza yaani.
"Ah, wala usijali. Me niko poa..." nikajibu kwa unyoofu.
"Mbona nahisi kama umenuna?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini.
"Mh? Ninune nini sasa?" nikauliza hivyo huku nikitabasamu.
"Si nimekufanya umenisubiri mno?"
"Wala hata, akusubiri nani? Ndo' kwanza hapa nasinzia," nikamwambia hivyo kiutani.
Akacheka kidogo, naye akaniambia, "Haya, usiku mwema basi..."
"Ih, we' unaenda wapi? Em' tulia hapa," nikamwambia hivyo.
Akacheka tena, kisha akasema, "Sawa. Niambie."
"Ulikuwa umeshapanda bed?" nikamuuliza hivyo.
"Ndiyo nimetoka kujimwagia, nataka kupanda ndiyo," akasema hivyo.
"Nataka kukuona," nikaongea kwa sauti ya chini.
"Tuongee kwa video call?" akauliza.
"Hamna. Nataka nikuone kabisa," nikasema hivyo.
Akatulia kidogo, kisha akasema, "Kivipi, yaani... hapo nje?"
"Mmm," nikakubali.
"Jayden... sa'hivi usiku..."
"Siyo sana bwana..."
"Mh... ahah... umeshaniona leo, mara nyingi tu. Tutaonana kesho, ama tuongee kidogo kwa video call," akasema hivyo.
"Mm-mm... Nataka kuonana nawe live... kidogo tu. Nimeshaku-miss," nikaongea kwa sauti yenye kubembeleza.
"Lakini... wengine washalala...."
"Please... kidogo tu. Natoka hapo nje, nakuona tu ukutani, then unarudi ndani chap," nikamshawishi zaidi.
Nilikuwa napigia picha sura yake nzuri akijishauri na kujishauri, naye akasema, "Sawa. Natoka upesi."
"Me nishafika," nikamwambia hivyo.
Hapo hapo nikaruka kutoka sofani na kuukimbilia mlango, moja moja mpaka nje na kusogea hadi kwenye ukuta wa uzio. Sasa je! Ankia alidhani ningeboeka eti, si niko hapa sasa? Araa!
Sikuwa nimekata simu, nami nilipokuwa nimesimama, matobo ukutani yaliniruhusu kuuona mlango wa kuingilia ndani kwao bibie, na hapo nikauona ukifunguka na Miryam mwenyewe akisimama sehemu hiyo. Akatabasamu, mimi pia nikampa tabasamu, naye akaiweka simu sikioni na kuongea kwa sauti ya chini sana, akisema amefurahi kuniona tena. Lakini mimi nikamwambia nilitaka aje mpaka hapa, hata nimguse tu, naye akawa anaona kama namsumbua.
Nikaendelea kumbembeleza aje, kwa ile sauti ya Alikiba 'ooooh aje...' naye akayeyusha chuma. Akarudi ndani zaidi na kurejea na funguo, kisha akalifungua geti la mlangoni kwa uangalifu na kutoka, akiwa hajasahau kuvaa ndala zake miguuni. Nikakata simu hatimaye na kuendelea kumwangalia hadi alipokaribia sehemu niliyosimama, na alikuwa amevalia ile nguo yake ya kulalia, huku nywele zake akizivalisha kikofia laini kichwani.
Akasogea hadi hapo ukutani, nyuso zetu zikitenganishwa na hilo uzio, na kwa sauti ya chini akasema, "Ila Jayden! Mbona we' msumbufu sana?"
"Yaani kama vile haunijui! Umeshasahau nilivyokuwa nakusumbua mpaka ukakubali muziki wangu? Na bado..." nikamwambia hivyo kiutani.
Akaniangalia kimkazo eti, halafu akasema, "Umeridhika sasa? Nenda ukalale."
"Tesha amerudi?" nikamuuliza.
"Hamna. Amelala huko kwa rafiki yake," akasema hivyo.
"Haya, njoo..." nikamwambia hivyo.
"Wapi?" akauliza hivyo kimshangao.
Nikamwita kwa kiganja huku nikirudi nyuma zaidi usawa wa huo huo uzio na kusimama, ambao kwa upande wake ungekuwa ni ule usawa wa bomba lao la maji hapo nje. Bado palikuwa na ugiza maana taa haikuwa imebadilishwa.
Miryam akatembea kwa uangalifu ili asitoe sauti kubwa ardhini, na alipokaribia hiyo sehemu, akauliza kwa sauti ya chini, "Unataka kufanya nini wewe?"
Nikampitishia simu yangu hapo hapo kwenye tobo moja ukutani, nikimwambia kwa ishara kuwa aichukue, naye akaipokea huku akiniangalia kwa kutoelewa. Hapo hapo nikaanza kupanda huo ukuta, mpaka juu, nikajitahidi kuwa mwangalifu sana ili nisikanyage vyupa na nondo zenye kuchongoka zilizokuwa kwa hapo juu. Miryam alishangaa! Akafunika mdomo wake kwa viganja huku akiniangalia kama vile haamini, nami nikafanikiwa kuvuka upande wetu na kushuka mpaka sehemu aliyokuwa amesimama yeye. Ukuta wa uzio haukuwa mrefu sana.
Baada ya kufika chini na kumgeukia, nikaona namna ambavyo alikuwa ananiangalia kimaswali sana, nami nikajitabasamisha kimchezo tu na kumtikisia nyusi kiuchokozi.
Akasema, "Jayden una... una matatizo gani?"
Nikaichukua simu yangu na kuiweka mfukoni, halafu nikakishika kiuno chake na kumvuta karibu zaidi na mwili wangu kwa makusudi.
"Wewe!" akasema hivyo kwa kunong'oneza huku akiangalia pembeni kwa njia ya tahadhari.
"Niliposema nataka kukuona, nilimaanisha hivi," nikamwambia hivyo kwa sauti tulivu.
"Ja.... hii siyo akili. Una... unawaonyesha wezi kwamba hapa ni rahisi kuingia..."
"Wezi gani, Miryam? Mwizi pekee aliyepo hapa ni mimi... na tayari nimeshauiba moyo wako," nikamwambia hivyo kizembe.
Akalibana tabasamu lake la haya, kisha akaangalia pembeni na kusema, "We' ni kichaa."
"Umeona eh? Yaani sina akili ikija juu yako..."
Akapiga ulimi kidogo na kusema, "Niachie bwana... hebu nenda. Saa saba inakaribia, halafu... natakiwa niamke mapema."
"Mbona bado mapema?" nikamuuliza hivyo bila kumwachia kiuno.
"Ahh... sitanii Jayden. Natakiwa nilale usingizi wa kutosha hata masaa machache. Nina safari kesho," akasema hivyo.
Kauli yake ikanifanya nimwachie kiuno taratibu, naye akatulia hapo hapo tu akiniangalia kwa hisia. Aliona imevuta umakini wangu.
Nikamuuliza, "Safari ya wapi tena?"
Akainamisha uso wake kwa ufupi, kisha akanitazama na kuniambia, "Nitaenda Morogoro."
"Moro? Unaenda kufanyaje?"
"Naenda tu kucheki haya masuala ya shamba la Mamu. Watunzaji kule wana... malalamiko fulani... so naenda kuweka mambo sawa,"
"Ahaa, ndo' ulichokuwa unafanyia kazi?"
Akatikisa kichwa kukubali.
"Okay. Lakini... kesho si ni send-off ya Doris? Utaikosa?" nikamuuliza.
"No. Nachukua treni ya mwendokasi..." akajibu hivyo.
"Ooh, kwa hiyo unaenda fasta tu na kugeuka..."
"Eeeh... na natakiwa niondoke mapema kabisa. Nataka nifike huko kwenye saa mbili, nishughulike na hayo mambo, halafu niwahi kurudi. Yaani kama ni kuchelewa, kumi na mbili jioni niwe huku tayari..."
"Okay. Na siku hizi Dar na Moro ishakuwa kama Mbagala na Kariakoo..."
"Ahah... teknolojia. Ila ndo' maana nimekwambia nataka kuwahi kulala, saa kumi na moja niwe nimeshaamka... halafu we' kichwa umenibana tu hapa..." akasema hivyo.
"Ahahah... utanilaumu? I'm so addicted to you..."
"Kwani hiyo ni makosa yangu?"
"Ya nani sasa?"
"Ni yako. Jifunze kujizuia. Siyo lazima mpaka unione kila mara..." akaniambia hivyo kwa uhakika.
Nikamkazia macho kiasi.
"Eeeh... si tungeweza hata kuongea kwa video call? Ya nini hadi unaruka ukuta ili eti uniguse? Yaani wewe!" akaongea hivyo huku akiniangalia kama amekerwa.
"Ah, basi tu, sa' nitafanyaje? Sijisikii fresh kutokukuona live kwa muda mrefu. Unakumbuka kama kuna siku yoyote imepita sijakuona tokea nilipokwambia nakupenda?" nikamuuliza.
"Mhm... hapana..."
"Ndiyo hivyo. Yaani we' ni dawa ya kila kitu kwangu, nikikuona napona..."
"Na kesho je? Tuseme nikaenda, nikachelewa kurudi, halafu nikapitilizia kwenye sherehe na tusionane kabisa mpaka kesho-kutwa... itakuwaje?" akauliza hivyo.
Nikatulia kidogo nikimtazama machoni kwa hisia sana, nami nikamwambia, "Tutaenda wote."
Akakunja uso wake kimaswali na kuuliza, "Wapi? Moro?"
Nikatikisa nyusi kukubali.
"Wewe! Acha masihara yako basi... ahahah..." akashangaa kidogo.
"Sitanii. Nataka niende nawe," nikamwambia hivyo kwa uhakika.
"Ahah... Jayden, hii ni safari ya kikazi, siendi kuzurura...."
"Hata kama. Nataka tu niwe pamoja nawe," nikamwambia hivyo.
"Kwa hiyo... kweli kabisa unataka tuondoke pamoja?"
"Yeah. Nitakusindikiza, na me nina muda sijaondoka jijini... itakuwa kama tour ndogo. Whatcha say?" nikamuuliza hivyo.
"Eh... mhm... yaani naona unataka kukaba kila kitu sasa..."
"Kabisa. Sitaki yaani... sitaki nihisi uko mbali nami kabisa Miryam. Yaani kila mara nataka tu nikuone, niwe karibu yako, nihisi uwepo wako... inanipa amani sana," nikamwambia hivyo kwa hisia.
Akaniangalia kwa ufikirio kiasi, kisha akaniambia, "Unavyoongea hivyo... inavutia. Lakini sijui kwa nini, nakuwa nahisi ni maneno rahisi sana kwako kusema kwa sababu labda umeshayatumia kwa wengi..."
Nikatikisa kichwa kiasi kukataa na kumshika mkono, nami nikamwambia, "Najua Miryam, najua ndiyo tumeanza, na ninaelewa kwamba hatujatoka pazuri mno. Sitarajii moyo wako uwe umeshafunguka kwa kila kitu, yaani... najua bado unataka kuwa mwangalifu. Sitakuhakikishia kwamba nakupenda kwa maneno tu, nitakuhakikishia na kwa matendo pia. Ndiyo itakuwa sehemu ya kukufanya uache kuogopa."
"Ahah... okay, ni sawa. Nisamehe tu lakini, maana sometimes nakuwa...."
"Usijali. Nakuelewa," nikamwambia hivyo na kumshika shavuni taratibu.
Akabaki akinitazama usoni kwa macho yenye imani sana.
Nikamwambia, "Najua sitaenda na wewe kila sehemu utakayoenda, lakini popote ambapo naweza kuwepo kwa ajili yako... nitakuwa hapo Miryam. Ndiyo nachotaka kufanya hasa kwa wakati huu. Natamani kama... ningeweza ku-rewind muda yaani... ningeurudisha muda nyuma na kukupata kipindi hichoo..."
"Ahah... si ungekuwa mdogo wangu sana?" akauliza hivyo kwa hisia.
"Yeah, lakini haingejalisha. Ningekupata tu na kukupenda, na ningekuonyesha huo upendo kwa muda mrefu zaidi mpaka kufikia huu wakati ambao tumesimama hapa... na kuendelea," nikamwambia hivyo kwa sauti yenye kubembeleza.
Akakishika kiganja changu huku akiniangalia machoni kwa hisia sana.
"Sikudhani ingewezekana tena Jayden kuja kupenda kutoka moyoni. Yaani sikufikiria ningekuja kupenda tena namna hii, na sikujua kama ningekuja kupenda kila kitu kuhusu mtu hadi nilipokutana na wewe Miryam. Yaani ninakupenda zaidi ya ninavyokupenda sana," nikamsemesha kwa hisia.
Akatabasamu zaidi huku akisugua kiganja changu taratibu kwa vidole vyake laini, naye akauliza, "Huwa unayatoa wapi hayo maneno Jayden?"
Nikatabasamu tu na kumwambia, "Nayasomaga tu kwenye mitandao, ndo' nakuja kuyamwaga hapa..."
"Oooh... kwa hiyo kumbe nafikishiwa tu mawazo ya mtu mwingine hapa, eh?" akauliza hivyo kiutani.
"Oops! Nimekamatika..." nikaongea kikejeli.
"You fool!" akaniambia huku akitabasamu.
Sote tukacheka kidogo kwa pumzi.
Akatikisa kichwa kuonyesha uthamini, naye akasema, "Asante sana kwa kunipenda. Ninakupenda sana pia."
"Yaani tulivyo... kama Romeo na Juliet," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu zaidi kwa furaha.
Nikauachia uso wake na kuuliza, "So... kesho nitakusindikiza Moro, eh?"
"Sawa. Tutaenda pamoja. Aa... nafikri hapo stendi zinakuwepo gari zinazoenda Stesheni... sijajua sana, ila tuta...."
"Tutapanga tu pa kukutana, afu' tutaenda pamoja, tutajua," nikamwambia hivyo.
Akatikisa kichwa kukubaliana na hilo.
Nikavishika viganja vyake vyote kwa chini na kusema, "Okay. Basi ngoja nikuache ukalale sasa. Me huwa nina usingizi mzito kwa hiyo nitaweka alarm."
"Kumi na moja, sharp," akaniambia hivyo.
"Mm-hmm," nikakubali.
"Haya, usiku mwema, nenda sasa. Uruke ukuta kwa uangalifu... na iwe mwanzo na mwisho," akasema hivyo.
Nikacheka kidogo kwa pumzi.
"Go!" akaniambia hivyo kwa msisitizo.
Nikaangalia juu, kisha nikaanza kuimba kwa sauti ya chini, "Basi nichumu, ni-kiss mwah.. ai nichumu, ni-kiss mwah..."
Nikamwangalia tena na kukuta anatabasamu kwa ile njia ya kuhukumu, akinishusha na kunipandisha eti, nami nikatabasamu kwa furaha.
Akanicheka kidogo kwa pumzi, kisha akasema, "Una hakika ulikuwa umeshasugua kinywa?"
Nikakunja uso kimaswali.
"Kama huoshagi mdomo kabla ya kulala, hiyo chum ndo' huipati," akasema hivyo kiutani.
"Ih! Kumbe umeshatoa na kitabu cha masharti afu' bado hujaniuzia?" nikamuuliza hivyo kiutani pia.
Akacheka kidogo huku ameziba mdomo.
"Na sasa hivi ndiyo unaniambia sharti la kwanza wakati hata nilikuwa sijaliandaa hili domo? Basi usiku mwema..." nikamwambia hivyo nikijifanya nimeudhika.
Bado alikuwa anacheka, nami nikaigiza kutaka kupanda ukuta, lakini akaishika T-shirt yangu na kuivuta huku akisema, "Hebu njoo hapa..."
Nikageuka na moja kwa moja kukutana na mdomo wake ulionifuata bila kusita. Ah!
Miryam alipatia aisee. Alijua. Zamu hii hakunipiga busu, alinila denda! Denda ya maana! Aliufinya mdomo wangu kwa midomo yake taratibu sana, akiepuka kutumia ulimi mwanzoni na kuacha midomo yetu pekee ndiyo ivutane, kisha ndiyo akaingiza ulimi wake ndani yangu na kutoa penzi la mdomo kwa ufundi ambao sikuwa nimeutegemea kabisa! Alikuwa na midomo mitamu, akipenda nimwachie tu yeye ndiyo aonje kila alichotaka kula, na katika hali ya kunogewa zaidi, akakishika kichwa changu kwa mikono yake yote na kuanza kukipapasa taratibu kama vile hataki tuache. Sijui hata aliweka wapi simu yake. Nilisisimka nyie!
Nikakishika kiuno chake kwa njia ya kukumbatia, kwa nguvu, bibie akiwa amenogewa tu kunipa denda hii tamu sana, miguno laini ya pumzi ikimtoka kadiri alivyoendelea kunipatia utamu wa ulimi wake, na nilikuwa nimeshasimama dede kwa nguvu kubwa sana. Yaani hapo nikasahau yote, nikiwa tayari kwa lolote lile ambalo angefanya lifuate, maana hisia zilikuwa huko juu juu yaani. Ndoto ilikuwa inatimia hapa!
Ilionekana ni kama dakika nzima ilipita akiwa ananipandishia moto kwa denda hii, ndipo akaikatisha taratibu na kuweka paji lake la uso usawa wa shavu langu. Nikafumbua macho na kuona yeye akiwa amefumba ya kwake bado, akiwa anazungusha kichwa chake taratibu na nyuso zetu zikiwa kwa ukaribu mno, nami nikatabasamu na kubana ubavu wake kwa kiganja changu, katika njia ya kumtekenya, naye akapandisha nyonga kidogo na kufumbua macho yake kuniangalia.
Aliniangalia kwa njia yenye hamu, kisha akaweka kiganja chake kifuani kwangu na kusema, "I really like this, Jayden. But I don't want us to go too fast..."
Aliongea kwa sauti tamu mno yenye kunong'oneza kiasi, yaani hata kama hakuwa akitaka tupeleke mambo mengi haraka sana, hapa tu tayari alikuwa ameshanipeleka mawinguni huko.
Nikiwa namwelewa, nikamwambia, "Usijali. I got you."
Akarudisha uso wake nyuma na kunitazama kwa hisia, naye akasema, "Tutaonana baadaye."
Nikatikisa kichwa kukubali hilo, ndiyo nikakiachia kiuno chake na kuusogelea ukuta. Nikapanda taratibu na kwa uangalifu sana, yeye bado akiwa amesimama hapo hapo, nami nikashukia upande wa kwa Ankia na kumtazama tena. Akanipungia mkono wa kwa heri ya sasa, nami nikaunda kopa kwa viganja vyangu na kumwonyeshea kwa kuiweka usawa wa moyo. Akatabasamu kwa hisia sana, kisha huyoo akaelekea ndani kwake.
Nikageuka tu na kuelekea ndani kwetu pia, nami nikafunga mlango na kutulia hapo sebuleni kwanza. Nikajikuta najishika mdomo wangu, nikitabasamu kama zezeta yaani kwa kukumbukia hiyo "chumu" niliyopewa hapo nje, na bado hapa chini palikuwa pamevimba eti! Nilikuwa na hisia nzuri sana, sana, sana, kwa wakati huu, na najua zingeendelea kupanda juu zaidi kadiri ambavyo siku zingeendelea.
Na huyu mwanamke alionekana kuyajua mapenzi kwelikweli, siyo mchezo, yaani nilikuwa nina hamu ya kuyatalii naye mengi sana kutokea hapa. Kwa kuwa siku ya kesho ningekwenda naye Morogoro, ningetakiwa kujiweka katika uimara wa kiume ndani ya akili, ili kama utalii wa kwanza ungefanywa hiyo hiyo kesho, uwe wa maana. Ona, nilikuwa hadi nimeanza kuwaza upuuzi mapema namna hii!
Lakini najua hilo lingekuwa jambo hakika kufanyika baina yangu mimi na yeye, haijalishi lini, kwa hiyo kweli utayari ulihitajika maana nilikuwa nimeshamhamu kwa muda mrefu sana sasa huyu mwanamke. Nikaona nizime taa na kwenda kulala, yaani nikajitupia kitandani huku natabasamu tu na kufurukuta-furukuta huku na huko kwa kuhisi mihemko ya hatari, nikiingoja alfajiri ifike ili niondoke na mwanamke wangu.
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Pata Full Story WhatsApp au inbox
Whatsapp +255 678 017 280
Karibuni sana
hata marefa wana timu zao MIMI apange Matokeo ili JC afunge goliMIMI NA MIMI 2