Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

Bora umekuja JC,episode kadhaa basi luch time hii tumuibie bosi muda wake
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nilikuwa najaribu kusoma hali hiyo mbele yangu kwa usahihi ijapokuwa pombe ilikuwa kichwani, na jamaa hakuonekana kutania kwa kile alichotaka nifanye upesi. Nitoke hapo na kwenda nje. Huko nje kulikuwa na nini?

Nikamuuliza, "We' ni nani?"

"Nimesema toka nje. Usiulize maswali," akasema hivyo.

"Bro, sikia. Sijalipia nilivyokuwa nimeagiza huko mbele... kwa hiyo..."

"Aaacha kujifanya unajua kuzungusha. Masai huchukui chochote kabla hujalipia, aisee pita hapa, sekunde tatu tu, la sivyo utaumia," akaniambia hivyo.

Kukasikika sauti ya watu wakitoka kule VIP na kuja upande wetu, na huyu jamaa akanisogelea karibu zaidi na kuigusisha chuma yake kwenye ubavu wangu huku akiniwekea mkono begani kwa njia ya kirafiki eti. Nilikuwa nimepatwa na hisia mbaya hapo! Ile kutazamia kwamba risasi ingeweza kuniingia tu hapo hapo, aisee! Ilifanya nijikaze tu na kuangalia pembeni.

Hao watu walikuwa ni wawili, mmoja akiwa mhudumu wa vyumba vya wageni kwa sehemu hii, nao wakatufikia na kutupita huku wanatuangalia tulivyosimama kama vile tunapendana sana. Jamaa akawapa tabasamu hafifu na kujifanya anataka kunong'oneza kitu sikioni mwangu kwa njia fulani kama vile amelewa, kwa hiyo wawili hao wakatupita tu na kuelekea nje kabisa wakidhani labda walevi tuna ishu zetu hapa.

Jamaa akawa ananitazama kwa ukaribu na kuigiza tabasamu la kirafiki huku akisema, "Twende nje, sitarudia tena kukwambia hiyo kauli."

"Kwa hiyo nikikataa utaniua? Itakuwa imekupa faida gani?" nikamuuliza hivyo kwa ujasiri.

"Haijalishi, ila itakuwa ni hasara kwako. Na siyo wewe tu. Nikikuua hapa... na hao marafiki zako wal'okaa huko wananyukwa... kuna watu wangu wanawaangalia," akasema hivyo.

Nikamtazama kwa mshangao makini usoni. Sikuwa nimetegemea kabisa hilo!

Akauliza, "Kwa hiyo?"

Nikajipa utulivu tu rohoni, nami nikamwambia, "Twende."

Akaniachia taratibu na kusema, "Tangulia."

Dah!

Nikaanza kuelekea getini taratibu huku jamaa akiwa kwa nyuma, na siwezi kudanganya, hofu ilikuwepo kiasi. Yaani, hii kitu ndiyo ikanifanya nitambue kwamba bado sikuwa salama kama nilivyodhani, mpaka nikawa nawaza ingekuwa bora endapo kama ningekuwa najua judo na makaratee ili nimchangamkie huyu jamaa kama tu "mastelingi" wa kwenye filamu.

Ila hii ilikuwa ni kitu halisi, nyendo moja ya kipuuzi tu kutoka kwangu ingeweza kunisababishia madhara, na pia hata marafiki zangu ambao hawakuhusika kwa lolote na hizi ishu nilizokuwa nimejiweka ndani yake.

Tulipofika upande wa nje, nikaona gari aina ya Noah ya silver likiwa limeegeshwa umbali mfupi wa nyuma kutoka hapo kwenye geti la jengo la Masai, si mbali sana na sehemu ya kulaza magari ya eneo hilo. Nikamwangalia jamaa usoni, naye akaninyooshea kiganja chake kuelekea hilo gari, kwamba nilifate.

Mdogo mdogo tu nikaenda, mpaka nilipofikia mlango wa kuingilia upande wa siti za abiria, nao ukafunguka wenyewe kwa kuvutwa kutokea ndani. Kulikuwa na jamaa mwingine humo, baunsa kichizi, na nafikiri ndiyo sababu wakamwagiza huyu mwingine mdogo mdogo ndiyo anifate la sivyo kama angekuja huyu jamaa ningetimua kwa kudhani labda amekuja kunidunda!

Akaniambia niingie, nami dah... nikaingia. Alikuwa mwenyewe tu humo, naye akasema nikae siti za nyuma kutokea hapo alipokaa yeye, nami nikatii. Yaani walikuwa wanatoa zile vibe za ujambazi, na ingawa nilikuwa nimekunywa lakini nikajitahidi kuonyesha kwamba kichwa kiko makini.

Yule mwingine aliyekuwa amenifata ndiyo akaingia kwenye usukani, gari likawashwa, kisha likaanza kutembea kuelekea upande wa mbele zaidi wa Masai kulikokuwa na mwanga na watu zaidi. Hii ilikuwa ni saa tano tayari, yaani saa tano tu, eti nikawa nimetekwa, tena kwa upole kabisa bila kufungwa kamba wala nini. Nikatulia tu.

Gari limefika usawa wa lango la kuingia hapo Masai, likasimama, nami nikawa najaribu kuchungulia kule ndani ili niwaangalie marafiki zangu, ila kwa upande tuliokuwa tumekaa, kwa hapo nisingeweza kuwaona. Lakini akaanza kuja jamaa mwingine tena kutokea huko ndani, na moja kwa moja akaja na kuingia ndani humu kwenye gari.

Alikuwa na mwili imara pia, akivaa kwa njia fulani makini iliyoniambia kwamba bila shaka angekuwa na silaha huyu; labda kiunoni. Dah! Walikuwa hawatanii. Yaani kama ningezingua tu, basi inawezekana huyu jamaa aliyeingia sasa hivi ndiyo alikuwa na kazi ya kuhakikisha anawaumiza na marafiki zangu kule ndani. Sijui hawa watu walikuwa wanatoka wapi!

Nikawa nimetulia tu, hivyo hivyo nikiwapa ushirikiano yaani, ndiyo ile gari limeanza kuondoka hapo, simu yangu ikaita. Mabaunsa wote wakanitazama usoni, na yule niliyemkuta humu mwanzoni akaninyooshea kiganja chake kama kusema nimpe simu yangu, nami nikaitoa mfukoni kukuta mpigaji ni Tesha.

Nikamwambia jamaa, rafiki yangu anapiga ili kujua niko wapi maana sikuwa nimewaaga, nikiomba aniruhusu nipokee ili tu nimwambie nimeondoka na asinisubirie, lakini huyu mwanaume akaikwapua simu yangu upesi na kisha kutoa ishara kwa kidole chake kwamba nikae kimya, na wote kwa pamoja walikuwa wamekaa kwa mtindo wa kunigeukia ili wanione vizuri nisije kuleta mchezo-mchezo.

Akaizima simu yangu na kuiweka pembeni, halafu ile sasa ndiyo tumeingia lami na kuanza kushuka na barabara iliyoelekea Rangi Tatu, mwenzake akanisogelea kwa kuvusha mikono yake kwenye siti huku akiwa ameshika kitambaa chekundu kilichokunjwa, akikielekeza machoni mwangu. Nilikuwa nahisi hasira sasa, lakini sikuwa na ujanja. Mtu hata angeweza kuniambia haya nimejitakia mwenyewe, uongo? Maana hata ingawa sikujua kwa nini hii imetokea sasa, nilielewa kwamba ni kitu ambacho kingeweza kutokea.

Kwa hiyo nikamwacha jamaa ayafunike macho yangu kwa kitambaa, nami nikahisi aliporudi kukaa pamoja na mwenziye. Hawakuzungumza hata mara moja, ikinifanya nione kwamba walipenda kuwa watu wa vitendo zaidi. Nilihisi kuchoka kiakili. Sasa hivi si ningetakiwa kuwa sehemu fulani namrukia na yule Rukia? Tena na ka raha ka pombe kakiwa kichwani? Hii noma ikatokea wapi tena? Ilikera sana.

Ila huu haukupaswa kuwa wakati wa kuanza kujuta, ulitakiwa kuwa wakati wa kufikiria ni nini kilikuwa kimenikuta, na nifanye nini kukifuta. Ni wazi kwamba huyu bwege aliyetishia maisha yangu na ya rafiki zangu akiwa pamoja na wenzake walikuwa wametumwa kunichukua na kunipeleka sehemu fulani, na niliombea tu isiwe kwenye kambi ya mateso lakini ni wazi walinihitaji nikiwa hai; ila labda kwa sasa tu.

Wa kwanza kabisa kuingia ndani ya akili yangu kuhusika na hili alikuwa ni Chalii Gonga, maana inawezekana taarifa ya mimi kwenda Masai alikuwa ameipata na hivyo kuwatuma mbuzi wake waje kunisomba. Ikiwa ilikuwa ni yeye, basi najua alichotaka ilikuwa kunitisha, maana sasa hivi nilielewa vyema kwamba hakuwa na kifua cha kutunisha mbele ya Bertha, na mwanamke huyo alikuwa ameshamwonya kuhusu kunigusa la sivyo angekipata kutoka kwake.

Au labda usikute hii ilikuwa ishu inayohusiana na huyo Rukia? Ile ya mke wa mtu sumu? Je kama ni bwana wake ndiyo alikuwa ameagiza hawa watu wakanitupe baharini huko? Hamna, sidhani sana kama hili suala lingekuwa limeegamia upande huo, maana maandalizi yote tu ya kunikamata hivi yalikuwa ya mpangilio ulionyooka vyema, na huyo Rukia ndiyo kwanza nilikuwa nimekutana naye leo.

Kwa hiyo nikawa nimefikiria na upande mwingine wa mambo. Vipi ikiwa aliyekuwa anafanya hivi ni Bertha mwenyewe? Usikute madam alikuwa amekasirishwa mno na kitendo cha mimi kuamua kutokwenda kwake tena, na kujua namna ambavyo mwanamke huyo hakupenda masuala ya kwenda kinyume naye ilinifanya niwaze labda hapa ndiyo nilikuwa nimefatwa ili nipelekwe kwake anionyeshe yeye nani. Dah, hizi drama hizi! Mpaka nikawa nawaza bora tu kama nisingekuja Mbagala kwa ajili ya likizo!

Mwanzoni nilidhani vitu vingekwenda kwa mstari ila sasa ndiyo nilikuwa naona jinsi gani mambo mengi yalivyokuwa yanazidi kuwa magumu tu. Safari hii ikiwa inaendelea, nikaamua kutulia tu ili ikifika ukomo wake nijionee ni nini kilikuwa kinanisubiri, na kuomba Mungu aniepushe na janga lolote baya zaidi kabla hata sijamaliza mengi niliyokuwa nakusudia kutimiza.

★★

Ilichukua muda wa kama saa zima kabisa kutokea wakati ambao nilitekwa mpaka muda ambao gari hilo likawa limesimama sehemu fulani iliyoonekana kuwa ndiyo kituo cha mwisho. Sikuwa nimeona tulikopita shauri ya kufunikwa macho, lakini huku palikuwa mbali. Yaani ni kama nilikuwa nimepelekwa machinjioni na mimi kuamua kuja kwa hiari, ila sikuwa na jinsi.

Nikaanza kusikia sauti ya geti kutokea nje, ikionekana lilikuwa likifunguliwa, kisha gari likatembea tena kwa mwendo mfupi na kusimama, kisha likazima kabisa. Nikawa nasikia sauti ya mbwa aliyekuwa akibweka kwa hasira, nami nikatambua kwamba hii sehemu haikuwa miliki ya watu hawa walioniteka, bali ya aliyewatuma. Oh, hiyo ilikuwa ni bila shaka. Kidogo tu sauti ya huyo mbwa kubweka ikaanza kufifia mpaka ilipokoma kabisa, nami nikaelewa "dogi" alikuwa amepelekwa kufungiwa.

Milango ya gari ikaanza kufunguliwa, nami nikashikwa mkono na kuambiwa nitoke. Nikawaambia si waniruhusu tu nitoe kitambaa, lakini hawakunijibu na kunishusha tu kutoka ndani ya hilo gari huku bado wakiendelea kunishika mikononi. Wakaanza kunitembeza kwenda mbele zaidi, kisha tukaanza kupanda ngazi. Hawakuwa na papara, yaani hata sikujikwaa, ikionekana utume wao ulikuwa kunifikisha hapo nisipopajua nikiwa salama. Ila labda ndiyo nikamalizwe vizuri sasa!

Hatua kwa hatua, tukamaliza kupanda ngazi, kisha ikafata tambarare ya vigae bila shaka, na hatua zikaendelea tu mpaka kufikia sehemu ambayo ningeweza kuhisi ilikuwa ni sebule pana sana. Ile hali tu ya unafasi niliihisi vyema, kisha jamaa waliokuwa wamenishikilia wakaniachia.

Nikawa nimesimama tu huku nikiinamisha uso wangu kiasi kusikilizia sauti fulani, nazo zilikuwa ni za hatua zilizoelekea kwangu taratibu kutoka kwa mtu mwingine tofauti na hawa watatu waliokuwa wamenikamata, kisha zikakoma baada ya huyo mtu kufika mbele yangu.

Bila shaka ilikuwa ndiyo aliyewaagiza, na siwezi kukataa kwamba hapa hisia za wasiwasi zikazidi kupanda zaidi, nisijue lipi sahihi kufanya; nitulie tu namna hiyo hiyo ama nikitoe kitambaa mimi mwenyewe. Hadi nilihisi pombe imeniisha kichwani.

"Kalikuwa kametulia kweli..." sauti ya mmoja wa wale wanaume walioniteka ikasema hivyo.

"Mtolee kitambaa," sauti nyingine ikatoa hilo agizo.

Nikakaza uangalifu kuielekea, ikiwa ndiyo ya huyo mtu mwingine aliyekuja hapo, mwanaume, na niliifahamu. Sijui kwa nini tu, lakini sikuwa nimeitegemea kabisa. Kitambaa kikavutwa kutoka usoni kwangu, nami nikatazama hapo mbele na kuthibitisha zaidi sasa kwamba ilikuwa ni Festo!

Jamaa akawa ananitazama kwa umakini sana, wanaume wake wakiwa wamesimama pembeni huku wakiniangalia pia, nami nikaangalia chini na kucheka kidogo kwa pumzi. Mwamba alikuwa na bonge moja la mtindo, siyo poa!

Hii sehemu tu tuliyokuwepo kwa sasa iliongea mengi kuhusu namna ambavyo alikuwa na maisha ghali, maana sebule ilikuwa pana vibaya mno, kila kitu kilichokuwemo kikiwa cha gharama na kupangwa vyema, kusiwe na utofauti wowote na mpangilio wa vyumba vya mahoteli makubwa zaidi jijini ambayo ni watu wenye pesa chafu tu ndiyo wanaweza kumudu kulala hata kwa usiku mmoja.

Lakini hii haikuwa hoteli. Ilikuwa nyumba kabisa, pana kinoma yaani... sijui nielezeeje. Huenda ilikuwa ya kununua, ama aliijenga mahala fulani, na inaonekana ni sehemu ambayo hakutaka wengine waijue ndiyo maana mpaka nikaletwa macho yakiwa yamefunikwa. Nikamwangalia tena.

Alikuwa amevaa T-shirt laini la mikono mirefu, zile za kuvutika kama ya michezo tu, pamoja na suruali ya aina hiyo hiyo kuonyesha alikuwa katika hali ya kupumzika tu hapa kwake. Mikono ikiwa mifukoni, aliendelea kuniangalia kwa umakini wa kawaida tu kama vile anasubiria niseme kitu fulani, lakini mimi nikatulia tu na kuendelea kumtazama pia.

"Vipi?" hatimaye akanisemesha kwa kuuliza hivyo na sauti yake kuu.

"Fresh," nikajibu hivyo.

"Natumaini sijakushtua sana," Festo akasema hivyo kwa utulivu.

"Hamna, kushtuka siyo neno naloweza kutumia. Labda tu niseme... sikutegemea," nikamwambia hivyo.

Yule jamaa ambaye ndiyo alinitoa kule Masai kwa kunitishia kuniua akaanza kusema, "Cheki hayo macho ya pombe! Nimemkuta na jimama Masai alikuwa ndo' yupo kwenye zone...."

"Sijakuuliza," Festo akamkatisha kwa kusema hivyo.

Jamaa akatulia.

"Kwa nini hivi?" nikamuuliza hivyo Festo.

"Nini?" na yeye akaniuliza.

"Una namba yangu. Kama ulitaka tukutane, si ungenishtua tu? Haja ilikuwa wapi mpaka uwatume warembo zako waje kunibeba?" nikamuuliza tena.

Festo akatabasamu kiasi.

Baunsa mwenye mwili mkubwa zaidi akaninyooshea kidole na kusema, "Chunga hilo shimo lako dogo, acha usenge! Unamwita nani mrembo? Umeshajiangalia kwenye kioo?"

"Okay, basi, nitaimaliza mimi mwenyewe. Nendeni mkalale," Festo akawaambia hivyo.

Hao wanaume wakaanza kuondoka hapo, huku huyo baunsa akinitazama kwa chuki kama vile anataka kunimeza, na mimi mwenyewe nikimwangalia kwa ujasiri.

Alipokuwa tu amenipita, nikakumbuka kitu fulani, nami nikamgeukia na kusema, "Oya... simu yangu."

Jamaa akasimama na kunigeukia pia, kisha akaitoa simu yangu kutoka mfukoni mwa suruali yake na kuninyooshea, nami nikaichukua huku bado tukiangaliana kiuadui. Eti alikuwa anataka kuondoka nayo!

Akajiunga tena na wenzake kuondoka hapo. Waliondoka kabisa kutoka kwenye hii sebule kuelekea nje, siyo kwamba walielekea vyumbani kulala hapo hapo, kwa hiyo tukawa tumebaki sisi wawili. Nikawa nasikia sauti ya mbwa akibweka tena kutokea pale nje. Hakupenda wageni wa usiku huyo.

Festo akasema, "Kumbe na wewe unalo la beberu?"

Alikuwa anamaaisha mimi ni jasiri, nami nikamwambia, "Ndiyo, lipo. Wanaoniangalia kwa wepesi huwa wanafikiri mimi mzembe, ila langu ni zito sana tu."

"Kwa hiyo walipokuchukua hukuogopa kabisa?"

"Sikuwaogopa wao, ila nilihofia kile ambacho aliyewatuma alikuwa amewapanga kufanya. Wasingecheza na karata ya kitisho cha kuwaumiza marafiki zangu, nisingekuwa hapa sasa hivi."

"Kwa hiyo ungefanyaje, ungepigana nao? Unajua usingeshinda."

"Ndiyo, ila ningepoteza nikiwa nimejaribu. Huwa siendi chini bila kupambana," nikamwambia hivyo.

Akanisogelea karibu zaidi, naye akasema, "Huoni kwamba bado uko chini? I mean... aliyewatuma hao katumia udhaifu wako kukuleta mpaka huku, na umekuja kwa sababu ya huo udhaifu. Utatokaje chini kama utaendelea kujiruhusu kuwa na udhaifu?"

Nikabaki kimya tu. Alikuwa anawaongelea marafiki zangu, au watu wowote ambao niliwapenda, na alikuwa sahihi kabisa. Sema, hakujua kwamba sikuzote kile ambacho kinaonekana kuwa udhaifu kwa mtu ndiyo kinaweza kuwa kinachompa nguvu, na mimi bado sikuwa nimeonyesha nguvu yangu iko wapi. Angekuja tu kuiona.

Akasema, "Ikiwa utaruhusu udhaifu wako uonekane kila sehemu, itakuwa rahisi kwa maadui zako kukuangamiza. Kwa hiyo ukitaka kutoka chini, utapaswa kuuangamiza huo udhaifu wewe mwenyewe. Sijui unanipata?"

Nikatikisa kichwa kukubali, nami nikamwambia, "Uko sahihi. Sikutaka wale watu waguswe, ila... hiyo siyo sababu pekee. Nilikuwa nimeshaelewa kwamba aliyewatuma hao viazi alikuwa wa kidiplomasia zaidi, kwa hiyo kumpa attention ilikuwa lazima. Kama angewaambia tu waje na kuniua... ningekuwa nimeshakufa."

Akaendelea tu kuniangalia kwa umakini, naye akauliza, "Kwa nini unafikiria naweza kutaka kukuua?"

"Sijui sana kuhusu hilo... ila najua hauniamini bado," nikamwambia hivyo.

"Kwa sababu umefunikwa macho wakati wa kuja huku?"

"Hilo... na pia kwa sababu ulifikiri ningeogopa sana kitu kama hiki. Mimi siogopi... najua mwisho wangu utafika tu. Lakini naelewa kwamba anayefikiri ninaogopa, yeye ndiyo anaweza akawa anaogopa kitu fulani kutoka kwangu mimi," nikamwambia hivyo.

Akacheka kidogo na kurudi nyuma kiasi, naye akasema, "Unafurahisha. Unayemwongelea yuko mbele yako... na hauko sahihi kwa sababu hana lolote la kukuogopea wewe, ila kwenye suala la kuua haupingwi. Nikitaka kukuua, nitafanya hivyo ndani ya muda mfupi sana. Lakini kukuua wewe itanipa mimi faida gani?"

"Sijui. Labda... ili nisije kukuharibia CV kwa Miryam," nikamwambia hivyo.

"Oh, kwa hiyo unafikiri mimi ndiyo naogopea hicho kutoka kwako?" akauliza hivyo

Nikatulia kidogo, kisha nikasema, "Ndiyo."

Akanitazama kwa macho yenye umakini.

Nikaangalia chini kwa ufupi, kisha nikamtazama na kumwambia, "Najua hatuko level moja... ila me ni mwanaume mwenzako. Nimeshaona wazi kwamba umempenda yule mwanamke... na kama wengi wetu tulivyo yaani, hautaki lolote likuharibie pale. Ndiyo maana najua unafikiri mie kuwa pale inaweza ikakutibulia, lakini... me siyo wa hivyo kaka. Umenileta hapa kunionya, najua, lakini... nakuhakikishia mimi sitakuwa shida kwako. Pale huwa naenda kwa biashara zingine kabisa na... hakuna yeyote anayejua kama nina mishe zangu pembeni... mishe zetu. Nikikutibulia wewe, si nitakuwa najiharibia tu mwenyewe? Halafu kwanza... nani ataniamini hata kama ningesema nini?"

"Kwa hiyo natakiwa tu kukuamini kwa sababu... Bertha kakuleta kwetu?" akaniuliza hivyo.

"Hapana. Kwa sababu najijua. Wewe ndiyo una nguvu zaidi yangu, hata ukiamua kunizingua kama ulivyosema... mapema tu. Halafu... me mwenyewe nina watu wangu wasiojua kuhusu unyama naofanya, naishi nao maisha... tofauti kabisa. Lazima nijilinde. Wewe uko juu yangu, ukiwa salama, na mimi nakuwa salama. Kwa nini nikusnichie kwa mtu unayemkubali? Halafu kwanza yule dada hata sina mazoea naye kabisa... nacheka tu na familia yake, yeye ananionaga kama mtoto. Afu' nije kumwambia sijui nini kuhusu wewe, unafikiri ataamini... tena kwa jinsi mlivyo tight? Haipo..." nikaongea kwa ushawishi.

Akawa ananiangalia kama vile ananisoma tu, naye akasema, "Sawa. Nilifikiri umelewa sana, kumbe bado uko active."

"Hata gari naweza kuendesha," nikamwambia hivyo.

Akacheka kwa mguno na kutikisa kichwa kidogo, kisha akaanza kuelekea upande uliokuwa na bar ya vinywaji. Bar ile ya ndani, yenye muundo wa ukweli yaani, nami nikawa nimemwona akivuta chupa nzito yenye pombe, iliyoonekana kuwa kali, na glasi mbili fupi, kisha akaanza kuzimiminia.

Najua kuna vitu ambavyo huyu mwanaume alikuwa anataka kushiriki pamoja nami kwa sehemu hii, na nilikuwa nimejitahidi kumwonyesha kwamba nina akili nzuri ya kusoma nia za watu pia, ila kutokea hapo ingenibidi kuwa chonjo zaidi kwa sababu nilikuwa namwambia masuala ya mimi kutokuwa "snitch" huku nikijua nafanya kazi na askari kuzitibua ishu zao. Angalau niliweza kufanya mkutano huu uegamie kwenye suala la Miryam tu, ila kwa mengine ambayo yangefuata, ningehitaji kuwa makini sana.

Ikanibidi nitume ujumbe mfupi kwa Tesha na Ankia upesi kuwaambia kwamba nilipatwa na dharura ndiyo maana niliondoka, maana baada ya kuiwasha simu jumbe zao za kuuliza nilikuwa wapi ziliingia, sambamba na za yule mwanamke aliyeitwa Rukia, ila huyo nikampuuzia kwanza. Ilikuwa inaingia saa saba usiku sasa.

Festo akawa amerejea niliposimama akiwa ameshikilia glasi zenye vileo, naye akanipa moja huku akisema, "Whiskey. Ushatumia?"

Nikapokea glasi hiyo na kumwambia, "Nimeshatumia pombe nyingi sana."

"Mhm... naona. Unapenda kulewa," akasema hivyo na kunywa yake kidogo.

"Ndiyo, kama unavyojua... kilevi ndo' biashara inayonyanyua taifa, kwa hiyo lazima kujua kila ladha yake ili ukiiendesha... uwe unaelewa nini maana yake," nikamwambia hivyo.

"Ahahahah... eti maneno ya msomi. Uko vizuri, lakini umelewa wewe. Kaa," akasema hivyo huku akiketi kwenye sofa pana nyuma yake.

Nikakaa pia na kuendelea kumtazama.

Alikuwa amekaa kwa kuegamia na kuitandaza mikono yake, huku glasi ikiwa kiganjani na miguu ikikunja nne kwa mridhiko. "Kwa hiyo niambie. Mbali tu na impressive feat ya kuweza kutengeneza cocaine kwa mikono, kwa nini daktari anayefanya kazi Muhimbili aanze kujihusisha na madawa ya kulevya?" akaniuliza hivyo.

Nikatabasamu kidogo na kusema, "Naona ushafanya research kunihusu. Au... ni story tu mlizokuwa mnapiga na mama zake Miryam?"

"Tayari nilikuwa nimeshakuchunguza kabla hata hawajaropoka, ndiyo maana bado sikuwa nimekutafuta kwa simu cause nilitaka nikuelewe kwanza. Ila kuna kitu ambacho kinatia akili yangu duduwasha. Inaonekana tu kuwa out of the blue kwamba... umeenda likizo Mbagala, siku chache tu ukampata Bertha na kuamua... 'yeah, nitatengeneza coke, nitajiunga na huyu drug queenpin, tutapanua business,' halafu nini... happily ever after? No. Nimeshaona. Una nia nyingine. Niambie. Unachotaka hasa ni nini kutoka kwa Bertha?" akauliza hivyo.

Umeona? Hapa nilikuwa kwenye jaribio kweli, na ningehitaji kutumia akili ili kile ambacho ningemwambia kipatane na AKILI YAKE kuweza kumshawishi kwamba nampa ukweli.

Nikaweka uso makini na kushusha whiskey kidogo kooni, kisha kwa utulivu nikasema, "Nia yangu ni ile ile kama uliyonayo kwa Miryam. Nampenda Bertha."

Akaendelea kunitazama kwa umakini.

"See... uko sahihi. Haya siyo maisha niliyokuwa nayo... na sikufichi... sikufikiria ningekuja kujiweka upande huu hata kidogo. Lakini hisia zangu kwa yule mwanamke ndiyo zikanilazimu nitumie njia yoyote ile ili niweze kumvuta kwangu... hata kama ni kubadili aina ya maisha yangu kwa ajili yake. Ni kama wewe tu. Ni lazima mbele ya Miryam uwe mtu mwingine kabisa ili umvute kwako kwa kutegemea na jinsi yeye alivyo hasa, na una potential kubwa ya kufanikiwa kwenye hilo kwa sababu umeshaielewa akili yake, kwa hiyo unajua ufanye nini ili uufikie moyo wake. Hata mie nimefanikiwa kucheza na akili ya Bertha, lakini bado ananitumia kama dildo tu, na ni sawa kwa sababu bado nahitaji kuufikia moyo wake kabisa, kwa hiyo lazima nifanye mambo ambayo yatamfanya anikariri mimi tu... eventually yaani," nikamwambia hayo.

Nikamwona akiwa anayafikiria maneno hayo kwa kina. Sidhani kama alikuwa anaona, lakini nilikuwa natumia udhaifu wake ili kujipa nguvu, lile lile somo la mwanzoni. Na nilikuwa naigiza vizuri, we acha tu!

Nikamalizia kwa kusema, "Kwa hiyo iko hivyo. Ahah... unaweza ukafikiri nazingua tu, 'ah wapi, huyu dogo amekutwa na jimama huko Masai kwa hiyo anatema upuuzi tu hapa,' ila no. Huo ndiyo ukweli naoujua mimi. Nikikukuta unapewa lap dance na kahaba hiyo haimaanishi umeacha kumpenda unayempenda kabisa, uongo? Ni starehe tu. Kuna vitu tu ni lazima mwanaume ufanye ili kupata unachotaka. Kama wewe utakuwa malaika mbele ya Miryam, hata mimi nitakuwa Shetani mbele ya Bertha, kwa sababu ndiyo vitu wanavyotaka tuwe ili wafurahi. Simple."

Akawa anatikisa kichwa taratibu kama kuonyesha hayo yamemwingia fresh, kisha akauliza, "Na kama asipokuja kuthamini upendo wako?"

"Basi... kitakachofuata kitakuwa kwa wakati huo huo. Kwa sasa naangalia tu kilichopo, na jinsi ya kukiboresha ili nifanikiwe," nikamwambia hivyo.

"Mbona naona kama umeshafanikiwa? Kwani hauli Bertha?"

"Ahah... ndo' kitu nilichosema kuhusu dildo. Sitaki iwe hivyo tu. Ndiyo maana nikapambana mpaka akaniona kuwa wa maana kiasi kwenye mipango yake... na ndo' nataka ibaki kuwa hivyo kwa wakati huu ili niendelee kutafuta njia zaidi za kumfanya aje kuniweka hapa," nikasema hivyo huku nikionyesha moyo.

"Yule mwanamke ni kichaa. Utajipa kazi," akasema hivyo huku akinywa.

"Ahahah... najua. Ndiyo maana nimempenda, kwa hiyo hata kama hiyo kazi itakuwa ngumu najua tu nitaenjoy. The crazy things we do for love," nikasema hivyo.

Akatulia kidogo, kisha akasema, "Well... itabidi tu kukubali kwamba sababu yako ni legit... na hiyo 'lover boy bullshit' inakufaa kwa sababu we' bado mdogo."

"Ahahah... na wewe tutasemaje? Hata we ni lover boy kwa Miryam..."

"Okay, kwanza... ishu yangu na Miryam ni biashara yangu mimi na yeye tu. Nisije kamwe kusikia, ama kujua Bertha na wengine kati ya walio kwenye business na sisi wanamfahamu. Tutakosana," akasema hivyo kwa sauti makini.

"Ondoa shaka. Mimi siyo domo kaya. I got you," nikamwambia hivyo.

"Vizuri. Pili... Bertha anaonyesha kukuamini, ndo' maana nikamruhusu akuweke pamoja nasi, masuala ya kupendana naye utajua mwenyewe. Nachotaka ni kila kitu kwenda swiftly ukianza kushiriki kwenye "market" yetu. Unaonekana kuwa mjanja, lakini ukiwa na sisi inabidi ujue jinsi ya kuwa makini. Hautatakiwa kuwa mtu wa kukutwa umelewa tu na kusondekwa kwenye gari bila kuwa na njia za tahadhari na kujilinda, umenisoma?"

"Kitabu chote nimekielewa kabisa," nikamwambia hivyo.

"Safi. Sina mengi, najua Bertha ndo' atakuwa mwalimu wako mzuri zaidi wa mambo yetu... ikiwa bado hajaanza kukufundisha. Kwa hiyo... piga whiskey, ukitaka kupumzika panda ngazi, ingia chumba cha pili pande la kushoto. Uangalie usikojolee mashuka, bado mapya," akasema hivyo na kumalizia kileo chake.

Nikasema tu, "Aaaa... kumbe nalala leo hapa?"

"Inaingia saa nane, kesho mapema napaswa kuondoka, na tako lako litanyofolewa na mbwa ukitoka nje sasa hivi... sina mpango wa kukusindikiza," akasema hivyo.

Nikatabasamu kidogo huku macho yakiwa mazito sasa, nami kwa kujifanya nimegongwa sana na pombe nikamuuliza, "Kwa hiyo... Miryam... ushaanza kula?"

Akaweka glasi pembeni na kujisawazisha vizuri, kisha akasema, "Bado."

Nikajitabasamisha na kusema, "Yule dada ni mtata. Hapendagi michezo ya kitoto... ana-like vitu 'serious' na maisha. Komaa," kisha ndiyo nikamalizia whiskey yangu.

Akasema, "Najua. Yule ndiyo mwanamke wa kuoa, siyo wa michezo tu. Anajali, mrembo, msafi, mkarimu, siyo mbinafsi... yaani yuko tayari kuweka wanaume pembeni kwanza ili tu ajitoe kwa ajili ya familia yake. Hataki distraction za mapenzi. Ni mzuri sana. Ndiyo anafaa kuweka ndani ili ndoa itulie."

Nikaendelea kumwangalia kwa utulivu.

"Umeongea point nyingi kujaribu kunifananisha na wewe kwa kumtumia Miryam, lakini mimi na wewe ni tofauti sana. Me siyo mtu wa... "kitakachofuata kitakuwa kwa wakati huo huo..." no. Mimi nitafanya lolote lile ili awe wangu kwa muda unaonifaa, maana sitaki kuendelea kujifanya rafiki mwema tu mpaka mwisho... hata kama ikinibidi niiondoe familia yake yote baadaye ili abaki peke yake ndiyo nimchukue... nitafanya hivyo."

Maneno hayo ya mwisho kutoka kwa Festo yakanifanya nimwangalie mwanaume huyu kwa umakini sana, yakiwa yameingiza taarifa mbaya sana akilini mwangu ambayo kiukweli iliogopesha.

Akasimama na kusema, "Usisahau maelekezo ya kukifikia chumba, lover boy. Tutaonana baadaye."

Kisha akanipita na kuelekea upande uliokuwa na ngazi, akielekea chumbani nafikiri. Dah!

Kwa muda mfupi nikaendelea kukaa hapo sofani nikiwa nawaza jinsi ambavyo hatma hazikutaka kuionyesha huruma familia yake bibie Miryam hata kidogo. Yaani, bila yeye kujua, wengi wa watu aliokuwa akiwaona wazuri kwake ndiyo ambao walikuwa tayari kumuumiza ili tu wapate faida za kibinafsi. Mbaya zaidi aliyekuwa anayaona haya yote ni mimi hapa, mtu ambaye mwanamke huyo hakumwamini.

Angalau kwa yule Joshua ningeweza hata kuungwa mkono na Tesha kidogo ikiwa ningemwambia kuhusu hila za kaka yake, lakini Festo, nilikuwa na nini dhidi yake ambacho ningeweza kutumia ili kuishawishi ile familia kwamba hakuwa mzuri kwao? Tena na mimi ningeonekana kuwa wale wale tu maana katika mambo mabaya aliyojihusisha nayo na mimi nilikuwa nimejiweka kwa sasa, kwa hiyo nisingeweza kuwa na njia za kuwalinda wale watu kutokana na mambo yoyote ambayo mwanaume huyo angepanga kuwafanya endapo kama Miryam angeendelea kumkatalia kufanya mahusiano.

Hivi, ni kwa nini ilipaswa kuwa mimi niliyetakiwa kuyajua haya mambo yote lakini iwe kama nimefungwa mikono kuweza kufanya chochote kuyatatua? Unajua yaani nilikuwa nimeanza kuchoka kwa kweli, lakini, bado tu kulikuwa na hisia zilizonisukuma kutaka kuleta suluhisho kwa sababu sikuweza kujizuia kujali. Nilitakiwa nishughulike na Bertha, nimwondoe Joshua, na sasa tena Festo akawa juu zaidi ya hii orodha. Raa!

Nikajikuta tu naangukia hapo hapo sofani kwa sababu ya kichwa kuwa na mvurugo wa hali ya juu, nami nikabebwa na usingizi kutokana na uchovu mwingi wa kimwili na kiakili niliohisi.



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nimekuja kuamka pakiwa pameshakucha zamani, lakini kwa hapa ingeknekana labda bado ni muda ule ule tu kutokana na jinsi ambavyo taa zilimulika sana humo ndani yaani muda wote, na kwa sababu fulani, mapazia hayakufunguliwa kuruhusu hewa na mwanga wa nje upenye ndani, ila viyoyozi maalumu vilitengeneza "fresh air."

Nikajitazama kuthibitisha, na ndiyo, bado nilikuwa kwenye sofa. Macho yalichomachoma kiasi, nami nikaanza kuyafikicha huku najinyanyua ili nikae. Mgeni nililala kwenye sofa ndani ya nyumba yenye vyumba kama vyote. Nilikuwa nahisi fukuto la ajabu mwilini, nikiwa nimetokwa jasho lenye kuchukiza, na nilihisi kichefuchefu ambacho kilikuwa kinavuruga kabisa kifua changu na kunitaka nitapike. Shauri ya kunywa bia nyingi jana halafu nikaja kuchanganya na ile whisky baadaye, asante sana Festo.

Ile tu ndiyo nimemwaza Festo, nikaanza kuangalia mazingira kwenye nyumba hiyo kutokea hapo nilipokuwa nimekaa, na macho yangu yakatulia sehemu ambayo ilikuwa ndiyo jikoni; jiko la wazi na pana lenye makolokolo kama yote ya kisasa na yaliyopangiliwa vizuri, kukiwa na mwanaume mfupi kiasi aliyekuwa amevalia kwa njia iliyoonyesha kwamba alikuwa mpishi. Tena wale "mashefu" wa kuajiriwa waliosomea upishi.

Jamaa alikuwa bize kwenye kaunta-sinki pana akiwa anakatakata nyama na maviungo-viungo mengine, akiwa anatengeneza vyakula fulani vilivyotoa aroma nzuri sana, nami nikaamua kuvuta simu yangu ili nitazame muda. Nilishangaa kukuta ni saa sita mchana, siku ya Ijumaa, na watu kama wote walikuwa wamenitafuta aidha kwa kunipigia ama kutuma ujumbe. Sikuamini kama nilikuwa nimepitisha usingizi mrefu namna hiyo, ila nadhani ni shauri ya kunywa sana jana huku nikiwa na uchovu mwilini.

Nikaona niweke simu pembeni ili kwanza nikashughulike na hiki kichefuchefu nilichokuwa nahisi, nami nikasimama na kuanza kwenda pale kwa Shefu. Alikuwa mweusi, mwenye sura makini sana ya mtu anayejua kubucha, nami nikamsalimia kistaarabu. Akaitikia vizuri, na kabla hata sijamuuliza, akasema kwamba "boss" alikuwa ameshaenda kazini, na alimwambia kwamba nikiamka nipate msosi mzuri kisha nikae kusubiri mtu ambaye angekuja kunichukua kutoka hapa ili ndiyo niondoke. Mh?

Nikamwambia asante, ila nilichokuwa nahitaji kwa sasa ni maji ya kunywa ya baridi sana, ndiyo akanionyesha friji ilipokuwa. Nikaenda hapo na kuchukua maji, nikibeba jagi kabisa, kisha nikarudi kwenye sofa kuchukua simu na kuanza kuelekea ngazini. Nikaenda mpaka kwenye chumba ambacho Festo alinielekeza ile usiku, kikiwa kipana na kisafi, cha wageni, na inaonekana hata kitanda hakikuwahi kuguswa na mtu yeyote yule.

Nikaweka simu pembeni na kuanza kunywa maji sasa. Shusha, shusha, shusha, kudadeki ikawa kama nimekiumua kichefuchefu maana ndiyo kikaongezeka sasa. Nikaliwahi bafu, nami nimeifikia tu ile siti ya choo cha kukaa nikainama kiasi na kuanza kuuondoa uchafu.

Nilijisikia vibaya sana, lakini nikaona niongeze maji tena kwenye mfumo wangu na kujitapisha kwa mara nyingine, kisha ndiyo nikapata ahueni. Uzuri kichwa hakikuuma, kwa hiyo nikavua nguo zangu na kuanza kujisafisha kabisa kimwili kwa kuoga na kuswaki. Nilitumia mswaki wa wageni humo ndani nikiombea Shefu asiwe amewahi kuutumia!

Baada ya hiyo pindi iliyoonekana kuwa nzito vibaya mno, nikakifata kitanda na kujitupia hapo ili nijisikilizie vizuri. Nikaona kuna kiyoyozi cha kielektroni juu ukutani, nami nikaamua kunyanyuka ili kwenda kukiwasha. Nikarudi kitandani tena nikiwa nimeichukua simu, na kaupepo kakiwa kananiliwaza ndiyo nikaamua kuzipitia sms sasa.

Kwanza waliokuwa wamenipigia walikuwa wengi yaani, lakini kwenye upande wa jumbe walinitumia wale waliokuwa na uvutano nami zaidi; wanawake. Ankia, Latifah, Soraya, Khadija, Ibtisam, Rukia, na wengine niliokuwa nafahamiana nao kitambo, wote walikuwa wameniachia sms, lakini baada ya kuona yule dada yake Joy aliyeitwa Adelina ametuma ujumbe pia, nikawa nimekumbuka kitu fulani. Leo ilikuwa Ijumaa. Aisee!

Nilimwahidi mwanamke huyo kwamba ningemsindikiza siku hii ikifika kwenda kule Nachingwea kuiunga mkono familia yake kwa ajili ya ujenzi wa kaburi la mdogo wake, na jumbe zake zilikuwa kadhaa kutokea asubuhi akiniuliza kama nitaenda, ikiwa niko bize au nimetingwa sana, mpaka kufikia saa tano ambayo akawa ametuma ujumbe kwamba yeye ameshakwenda na Mungu akipenda tungeonana. Dah, nilijisikia vibaya! Na alivyokuwa mstaarabu sasa!

Nikawa hadi nashindwa yaani, sijui nimtumie maneno gani, nami nikaangalia jumbe za Ankia kukuta naye ameniambia kuhusu hilo suala. Yeye mwenyewe alikuwa ameshasahau maana hakuwa amewasiliana na Adelina tena tokea ile siku ameenda pale kwake kumtembelea, ila ndiyo alipopigiwa simu asubuhi akajitahidi tu kujiandaa na kuondoa harufu za pombe, kwa hiyo sasa walikuwa pamoja kuelekea huko na rafiki yake. Alikuwa amenitafuta sana pia asubuhi kwa kupiga, lakini mimi ndiyo hivyo, sikuwa na habari.

Kwa hiyo nikaamua tu kumtumia ujumbe Adelina wa kumwomba samahani kwa kusema nilipatwa na hitilafu iliyosababisha nikashindwa kuijali hata simu, nami nikamwahidi kwamba tutayajenga zaidi wakishafika huko ama wakirudi.

Baada ya hapo, nikawapitia wengine pia, nikiona wazi namna ambavyo yule Khadija ndiyo alikuwa amenipigia mara nyingi zaidi, lakini hakukuwa na simu wala ujumbe wowote ule kutoka kwa madam Bertha. Sijui alikuwa amejichimbia wapi! Au alikuwa amenichunia? Nikaamua kumpigia. Mara mbili, kimya, ya tatu ndiyo akapokea. Akauliza nasemaje, nami nikamwambia nimemmiss. Nikasikia akisonya kidogo na kusema angenitafuta baadaye maana sasa hivi yuko bize, nami nikamwambia sawa.

Nikajikuta nacheka kidogo, kupata ile ahueni kwamba hakukuwa na noma kwa upande huo, nami nikaona sasa ndiyo ungekuwa muda mzuri kwenda kula maana kifua kilikuwa kimeanza kutulia na njaa ilikuwa inanikong'oli. Sikuwa nimekula tena tokea asubuhi ya jana nilipokula chapati mbili kwa Ankia. Sikusahau! Na labda ndiyo maana uchovu ulipita ule wa kawaida jana, na sasa nikawa nahisi mwili unarusha-rusha tu damu kwa ndani.

Nikavaa nguo zangu tena, na nilikuwa na uhitaji wa kubadili haya mavazi, hayakunukia ile "mimi" nzuri tena. Nikaenda pale sebuleni na kukuta Shefu akiwa amekaa kwenye kiti kirefu cha plastiki usawa wa ile bar ya vinywaji huku akitumia simu yake, na aliponiona akashuka na kusimama kwa 'attention,' ile ya mstalini. Nikamkaribia na kumwambia ajiachie tu, mimi sikuwa bosi wake, ila nilikuwa na njaa kali sana. Akasema nielekee upande wa meza ya chakula, kila kitu kilikuwa pale na yeye angenihudumia, nami nikafikicha viganja vyangu na kwenda upande huo.

Nikakaa kitini, meza ikiwa na vyombo kama hotpot, masahani, vijiko, chupa za chai, bakuli lenye matunda, naye Shefu akaja na kuanza kuniambia kuna hiki na kile, nichague nataka nini halafu anipakulie. Dah! Maisha hayo, tena kwa msoto wa kuuza madawa ya kulevya!

Mimi nilitaka kula kila kitu, kasoro maini tu, kwa hiyo nikamwambia aniwekee kila kitu kimoja kimoja, naye akafanya hivyo. Kwa hiyo ikawa ni hivi, half cake moja, kipande kimoja cha mkate msito, soseji moja, kipande cha nyama ya kuku, supu ya ngombe, na kipande kimoja kimoja cha matunda. Nilikula!

Shefu alikuwa amesimama pembeni, eti akitakiwa kusimama tu mpaka nimalize kula, nami nikamwambia aache ujinga na akae ili tule wote. Alikuwa anafata kile kitu wanaita protocol, utaratibu eti. Nikamwonyesha urafiki na kumfanya ajiachie pia, nasi tukawa tunakula huku tunapiga story.

Nikamweleza kwamba mimi ni rafiki ya bosi wake, na ndiyo nilikuwa nimekuja kumtembelea hiyo jana. Akasema aliambiwa hivyo pia na bosi wake, kwamba mimi ni mgeni wa muhimu sana kwa hiyo anitengenezee chakula kizuri na kunionyesha heshima, hivyo hakutegemea kwamba ningekuwa na ukarimu wa kumkaribisha ale pamoja nami maana alijua mimi mtu wa hadhi ya juu sana.

Akawa ananiambia kwamba yeye hakuishi hapo, bali alikuwa kikazi kwa ratiba, na kila baada ya kumaliza kazi yake angeondoka kabla ya saa moja kuingia. Ni mara chache angeonana na bosi wake, yaani hasa kama angekuwa ameshinda tu nyumbani ama kama akileta watu fulani kwa ajili ya party. Na akasema hajui kwa nini lakini alikuwa anamwogopa kweli bosi wake.

Nikaona kwamba mwanaume huyu alikuwa mtu mzuri, nami nikamwambia ajitahidi tu kufanya kazi yake bila kujiingiza kwenye mambo yasiyomhusu, na hangekuja kamwe kuona kwamba bosi wake ni mbaya. Kuhusu kulifanyia jengo hili usafi, akasema walikuwa wanakuja wafanyakazi wengine pia kwa ratiba kama yeye tu. Kulikuwa na mlinzi maalumu hapo nje ambaye ndiye alishughulika na yule mbwa mkali pia, kwa hiyo kabla ya hawa watu kuingia au kuondoka hapa, walitakiwa kumjulisha ili amfungie kwanza kuepuka ajali zozote za kung'atwa.

Sasa ndiyo nikawa nimetambua kutoka kwa mwanaume huyu kwamba jengo hili lilikuwa kwenye eneo lijulikanalo kama Mbezi Beach. Shefu hakujua kama sikufahamu kuhusu hilo, kwa hiyo nikawa nimemwambia iwe siri yetu tu kwamba tulikula pamoja na kuzungumza pia endapo kama bosi wake angekuja kumuuliza. Shefu akakubali. Alinikubali.

Tukiwa tunaenda kumaliza mlo, yule Khadija akawa amenipigia kwa mara nyingine. Mwanamke alikuwa na mchecheto huyo! Yaani hata Ibtisam sikuwa nimetoka naye bado ingawa alikuwa mzuri kweli, lakini yeye hakuwa king'ang'anizi kama huyu Khadija. Ila nikaona nimtolee uvivu kwa kuwa sasa mwili ulikuwa unarudisha nguvu. Nikapokea na kumsikiliza.

Alikuwa anataka tukutane leo, kwa sababu siku ya leo hakuwa amebanwa kwa lolote lile, na mume wake alikuwa na mambo mengine mpaka usiku mno. Alienda mbali mpaka kusema alikuwa ameniota kabisa, na alijisikia vibaya sana kutonipata kuanzia wakati niliompa namba mpaka sasa. Nikamwambia nilitingwa tu lakini sikuwa nimemsahau.

Sasa alikuwa anataka tukutane leo leo yaani kwa udi na uvumba, maana eti Joshua alikuwa anamwonea sana. Nilikuwa namsikiliza huyu mwanamke, yaani alikuwa mwongeaji aliyejua kupamba maneno yake ili tu apate alichokitaka, na ili kuondoa kero nikamwambia sawa; kama anakitaka sana basi atafute sehemu nzuri, siyo ya kizushi, ndiyo tukutane hapo ili tufanye alichotaka.

Akasema haina shida, yaani muda wowote kutokea sasa hivi ndiyo angekuwa amefika Mbagala kutokea Uhasibu alipokuwa na biashara zake, kwa hiyo mimi nijiandae tu kukutana naye sehemu atakayonielekeza. Alikuwa mwongo! Dakika mbili tu nyuma alikuwa amesema hajabanwa kwa lolote, eti sasa hivi tena akawa ameshafika na Uhasibu.

Nikasema poa tu na kumkatia simu, kisha ndiyo nikaenda zangu kusafisha mikono na mdomo. Sikuwa hata nikimaanisha kile ambacho nilimwambia huyo mwanamke, yaani basi tu. Kama mambo mengi ya upande wangu yasingeeleweka yaani hata kama angefanya nini baadaye, nisingeenda kukutana naye. Nilikuwa nahitaji muda wa kutuliza na haka ka mashine siyo kila siku kulima tu wanawake!

Shefu akasafisha meza, mimi hapo nikiwa nimeshamaliza usafi na kwenda kukaa sofani, kisha nikaingia mitandaoni kuangalia nini kipya. Shefu akaja mpaka sofani na kukaa, akiniuliza ikiwa ningependa kuitiwa usafiri sasa, nami nikaona niulize amemaanisha nini. Ndiyo akawa ameniambia kwamba bosi wake alimpa maagizo kuwa nikimaliza tu kula ndiyo amtumie taarifa kuwa mgeni kaishakula ili Festo atume sasa majambazi wake waje kunifata.

Nikawaza kwa ufupi, kisha nikamwambia atulie kwanza tupumzike kidogo. Nikamwomba anisimulie kuhusu maisha yake na familia kama alikuwa nayo, naye akafurahia kufanya hivyo. Nilikuwa tu nataka nile muda zaidi hapa maana hii nyumba ilikuwa nzuri balaa, na baada ya kuona kuna "console" ya kucheza game iliyokuwa imeunganishwa kwenye flat screen kubwa upande mwingine wa sebule hiyo, nikapata wazo la kucheza game pia.

Nikamuuliza Shefu, niliyekuwa nimejua sasa kwamba aliitwa Saidi, ikiwa alijua kucheza, naye akasema aliwahi kucheza PS zamani lakini hajui sana ikiwa angeweza sasa hivi. Nikamshawishi kwenda upande huo na kuwasha hilo TV kubwa kama dirisha, kisha tukawasha na hiyo deki ya game na kushika pad. Nilikuwa nimemiss hii kitu, na nilijua hii ingekuwa sehemu ya kuutafuta uchangamfu zaidi ili ule utulivu wa kiakili niliouhitaji niweze kuupata pia.

Tukaanza kucheza mpira, hao katuni wakiwafanana kweli wakina Messi na Ronaldo, hadi Siuuu waliweza kufanya! Shefu Saidi alipata shida kucheza mwanzoni lakini nikaendelea kumfundisha mpaka na yeye akaanza kujitahidi kunifunga. Nilijikuta nafurahia sana wakati huu mzuri pamoja na huyu baba, na masaa yakazidi kwenda nikiwa hapo hapo kwa Festo.

★★

Tuliendelea kucheza game mpaka kufikia saa kumi na moja, yaani Shefu Saidi alipenda sana hii kitu mpaka akawa amejisahau. Si ndiyo akapigiwa na bosi Festo sasa kuulizwa nini kilikuwa kinaendelea! Akaanza kupaniki, lakini
nikamtuliza.

Nikamwambia aseme mimi nilitaka kupumzika zaidi kwa hiyo bado nilikuwa hapa, naye shefu akamwambia hivyo Festo. Jamaa alikuwa na mambo mengi huko inaonekana, kwa hiyo akawa amemwambia shefu aniambie kwamba ameshawatuma watu wake waje na kunipeleka nilipoishi, naye shefu akakubali kufanya hivyo.

Baada ya bosi kukata simu, Saidi akaeleza namna ambavyo kweli alikuwa amefurahia uwepo wangu hapa mpaka akawa amesahau protocol. Nikamwambia asiwaze, na endapo kama akipenda tuwe marafiki nje ya kazi yake, basi tuachiane namba ili ikiwezekana tuje kufurahia pindi nyingine yenye kuburusisha kama hivi.

Nilipendezwa naye kwa sababu alikuwa mnyenyekevu sana huyu baba. Kwa hiyo akanipatia namba yake, kisha akaanza kuhakikisha kila kitu kinarudia mpangilio wake mzuri sehemu hiyo.

Haikuchukua muda mrefu sana na shefu Saidi akawa amepigiwa simu na mlinzi pale nje kuambiwa kwamba gari lilikuwa nje likinisubiria mgeni. Sijui kwa nini ingawa huyo Festo alikuwa na namba yangu hakuwa akinitumia jumbe za kunijulisha chochote kile, lakini na mimi niliona niendelee kukausha tu. Nisingejihangaisha hata kumtumia salamu yaani.

Kwa hiyo baada ya Saidi kuniambia kuhusu kusubiriwa na gari huko nje na yule mbwa kufungiwa, nikawa nimeenda kule chumbani kuvaa viatu vyangu na kuhakikisha nimejiweka sawa kimwonekano, kisha ndiyo nikatoka hapo na kumuaga mpishi huyo mwenye heshima. Lakini akaona anisindikize kabisa kuelekea nje, nasi tukaenda huku nikiangalia uzuri wa nyumba hii.

Zamu hii nisingefunikwa macho kwa kitambaa wala nini kwa hiyo labda Festo alikuwa ameanza kuniamini. Na ilikuwa ni bonge moja la jumba, ikionekana kuwa ya kununua, uwanja hapo nje ukiwa na mazingira safi pamoja na magari mawili ya kifahari tofauti kabisa na lile la Kluger ambalo Festo ndiyo alipenda kutumia alipotembelea sehemu kadha kama pale kwa kina Miryam.

Hiyo ilionyesha kwamba jamaa alificha kiasi upande huu wa maisha yake kwa watu wengi ambao hakutaka waujue, na inawezekana alikuwa na sehemu nyingine ya kukaa ambayo ingemfanya aonekane kuwa wa maisha ya kawaida tu. Kila mtu mwenye figisu ana njia zake za kujilinda, na huyu Festo alionekana kuwa makini kweli.

Kwa hiyo nikawa nimetolewa mpaka nje ya geti na kukuta Subaru Forester nyeusi ikiwa hapo, sijui ikiwa ni Uber, nami ndiyo nikampungia mkono wa kuaga Shefu Saidi na kuingia siti za nyuma. Alipenda sana kuonekana kuwa rafiki yangu.

Nikiwa ndani ya gari sasa, nikamtazama dereva na kuona alikuwa mwanaume mgeni kabisa kwangu, nami nikamsalimu kwa utulivu. Akaitikia vizuri na kuniambia amepewa maagizo ya kunipeleka Mbagala, ila tukifika huko nianze kumwelekeza mpaka kufikia mahala ambapo nilitaka kushukia. Nikakubali, nikiwa nimetambua kwamba huyu hakuwa kama wale majambazi ambao walinifata mpaka Masai kabisa, lakini huwezi kuwa na uhakika sikuzote.

Gari likaanza kutembea.

★★

Tulipita maeneo nisiyofahamu, ila kutokea Kawe pale kuelekea Mbagala sikuwa mgeni sana. Khadija sasa! Alianza kupiga simu, yaani kutokea Morocco mpaka tumefika Rangi Tatu, mwanamke alikuwa amepiga mara kumi na saba, na zote sikupokea!

Nilikuwa nahisi kero tu, yaani niliona wazi kwamba alikuwa ameanza kuniganda mno, mpaka nikawaza sijui nimpige block? Angalau hakuendelea kupiga tena mpaka nilipofika Mzinga, nami nikamwambia dereva anishushe hapo hapo; sikutaka anipeleke mpaka pale kwa Ankia kabisa.

Nikashuka, giza la saa moja likiwa limeanza kuingia, nami mdogo mdogo nikatembea mpaka kufika kwenye maskani yangu ya hii likizo. Sikuwa naziacha funguo za ziada alizonipa Ankia, na hapa nilikuwa nazo kwa hiyo nilipofika tu nikafungua geti na kuelekea ndani.

Nilikuwa nimeona gari la Miryam likiwa hapo kwake kwa nje kumaanisha mwanamke huyo alikuwepo, kwa hiyo hata wazo la kusema niwapigie mama wakubwa kuuliza hali ya Mariam nikaona nilitulize kwanza. Kwa muda huu, sikuhitaji misongo, lakini kuwa tu karibu na kwao hakungeiondoa. Yaani kwa mambo mengi akili yangu ilikuwa kwao tu. Ningefanyaje?

Nikabadili mavazi na kwenda tu sebuleni kukaa, ikiwa ni saa moja yenyewe sasa, na ile tu nataka kumtafuta Adelina ili kutuma salamu tena, simu ikaanza kuita. Khadija. Dah! Najua asingeacha kupiga kabisa huyu mwanamke, hivyo nikapokea ili nimwambie mambo yamenibana kwa hiyo sitoweza kwenda.

Kabla sijaongea, kutokea upande wa pili akasema, "Jamani wewe... nakupigia hupokei kweeli? Unajua nimeshapangilia kila kitu hapa? Kwa nini unanifanyia hivyoo?"

Nikatulia kidogo, kisha nikauliza, "Umepangilia nini?"

"Nimetafuta sehemu nzuri kama ulivyotaka, tokea saa kumi jamani... nakupigia hupokei, kweli?"

"Ndiyo, ni kweli. Nilikuwa bize..."

"Sa' si ungeniambia? Mbona kama unajisikia sana?"

"Aa wee... kama imeanza kufika huko, kata hii simu sasa hivi!"

"Me sijaongea vibaya, namaanisha tu... nimefanya kama ulivyoniambia, sasa nimekupigia kweli hata ukawa hupokei jamani! Hata kama ingekuwa ni wewe usingejisikia vizuri, lakini... nisamehe. Me... nakuomba uje," akanibembeleza.

"Uko wapi?"

"Sa'hivi niko hapa... nimesogea hapa Rangi Tatu, nimeingia hapa Highway, nakusubiri. Si unapajua?"

"Sipajui bana," nikaendelea kumwonea.

"We' njoo tu hata na bodaboda, mwambie akulete Highway... atakuleta..."

"Khadija nisikilize. Mimi sina hela, sawa? Kama unatarajia kupata hela, nakwambia mapema... mimi sina hela," nikamwambia kwa msisitizo.

"Kwani me nilikwambia nataka hela? Me nataka uje... nakutaka wewe kaka jamani, acha hizo basi. Hela ninayo, nalipia kila kitu... wewe njoo," akaendelea kubembeleza.

"Kwa hiyo nikitaka bia arobaini, utaninunulia?"

"Hata themanini, wewe njoo! Jamani, eh!" akasema hivyo.

"Umeshaanza kunywa wewe, eti? Maana naona unaongea tu..."

"Me nataka uje... kama bia utakunywa, na kama unaumwa nitakuponya. Usinifanyie uzushi jamani... uliniahidi. Njoo bwana. Kwani kuna kazi gani unayofanya sa'hivi?"

Nikatulia kidogo nikitafakari maneno hayo, nami nikamwambia, "Hamna. Hamna kazi yoyote."

"Sa' si uje? Niko free sana leo. Njoo tupeane love baby... nitakupa vyote," akasema hivyo.

Akanifanya nitabasamu kiasi, nami nikamuuliza, "Nimeshakuwa na baby?"

"Ndiyoo... we' ni mpenzi wangu. Njoo nikufurahishe bwana," akasema hivyo.

Nikafumba macho na kutikisa kichwa kidogo, nami nikamwambia, "Haya nakuja."

"Sawa. Si uko hii hii Mbagala sa'hivi?"

"Niko home kabisa."

"Sawa, we' njoo. Chukua boda kutokea hapo Mzinga ikulete mpaka hapa, nitalipia..."

"Mbona unaniwahisha sana?"

"Si unajua kuna suala la muda, my?"

"Si umesema uko free?"

"Eeh, ila ndo' mpaka saa sita tu. Nitatakiwa kurudi nyumbani. Nijali tu wangu," akaongea kwa ushawishi.

"Haya, nipe dakika kumi, nimefika," nikasema hivyo, na simu ndiyo ikakatwa.

Nilikuwa nimefikiria kumzingua huyu mwanamke, lakini sasa nikawa nimeamua kwenda ili tu kujiridhisha kidogo. Na sikumwamini. Ikiwa alitaka tuingiliane kimwili, ningefanya kitu ambacho sikupendelea kabisa kufanya pamoja na kuwa daktari na mengine mengi, yaani kutumia mpira wa kinga.

Nilitaka tu kumtumia huyu mwanamke kwa ajili ya jambo lingine, na kama ningekuwa kwenye mstari sahihi kufanya hivi, basi haya yote yalikuwa na faida kuyafanya hata kama sikuyaridhia sana. Na hata hivyo nilikuwa tu na uhitaji wa kuondoka tena ili kuyaweka pembeni kwanza haya mazingira yaliyokuwa yananilazimu kumwaza tu Mariam na dada yake.

Nikatoka hapo sebuleni na kwenda chumbani kuvaa kimtoko zaidi, pulizia manukato yangu, kisha nikaondoka kwa mara nyingine tena. Sikugeuka nyuma yaani.

★★

Nikawa nimefika hapo Highway baada ya dakika chache kutokea Mzinga, bodaboda go, na sikuwa nimesahau kuhusu kuchukua kinga; nilinunua chache dukani kabla ya kuja huku. Hii Highway ilikuwa ni kumbi ya starehe na vinywaji kama Masai tu, lakini yenyewe ilikuwa pana zaidi na yenye mtindo maalumu kikazi.

Namaanisha yaani hata wahudumu walivaa kwa sare za black and white kabisa, kitu ambacho Chalii Gonga alikuwa amefeli kuwafanyia waliopendezesha baa yake huko nilikotoka. Angalau hapa kulikuwa na kale kamvuto zaidi yaani watu walioingia wangejiona labda hata wako Kitambaa Cheupe, ila siyo kwamba ilikuwa nzuri kivile.

Kwa hiyo nilipokuwa nimefika tu, ikiwa ndiyo inaelekea kuingia saa mbili, nilimpigia huyo Khadija, naye akaja mpaka upande uliokuwa na sheli si mbali sana na hiyo sehemu, ikiwa ndiyo nilishukia hapo. Alikuwa amevaa kigauni kifupi cheusi kilichoyaacha mapaja yake wazi kiasi, yaani si mbali kutokea magotini, na kiliubana mwili wake kuchoresha umbo matata alilokuwa nalo na kufanya awe kivutio cha macho.

Tayari tu mimi mwenyewe nilikuwa natazamwa sana hapo nilipokuwa nimesimama, kwa hiyo huyu mwanamke alipofika karibu nami ndiyo karibia kila mtu aliyepita ama kusimama hapo nje akawa anatuangalia.

Khadija alikuwa amevaa kwa kujiachia sana wakati huu, yaani nilitambua kuwa hakuvaa sidiria kabisa, na chupi aliyokuwa amevaa kwa ndani ilikuwa ya aina ya kandambili ili sehemu kubwa ya makalio yake iwe nje kugusana na nguo yake iliyombana, kwa hiyo alipotembea yaani huko nyuma palitikisika kwa fujo sana. Na alionekana kupenda zile fujo fujo huyu, ndiyo maana nikawa najiuliza ni kwa kipi ambacho mume wake angekuwa anakikosa hapa mpaka kumwonea, na mwanamke naye aamue kuchepuka.

Ila sikujali sana kuhusu hayo. Nilichojali zaidi sasa ikawa kwamba baada ya kumwona namna hiyo, hamu tu hata ya kutaka kutembea naye ikawa ile ya sitaki-nataka. Alijichoresha mno, siyo kwamba kulikuwa na uajabu sana kutokana na jinsi alivyojiweka wakati huu, ila tu kwa sababu ilikuwa ni yeye yaani, sikupenda. Na hata zaidi alipokuwa amenifikia karibu, akanikumbatia ili eti tuchorwe vizuri sasa na watu wote, harufu ya pombe ikimtoka vyema mdomoni.

Nikamtoa kwangu taratibu na kumtazama kwa umakini, huku jicho lake lege kiasi likinitazama kimapenzi kabisa, ndiyo nikamwambia amependeza. Akacheka kidogo na kuuliza bodaboda aliyenileta yuko wapi ili amlipe, nami nikamwambia tayari alikuwa ameshaondoka kwa kuwa nilijilipia mwenyewe. Akasema yaani najua kweli kuzungusha, ila tutumie muda vizuri maana saa mbili inaingia, kwa hiyo akanishika mkononi na kuanza kuelekea kule kwenye Bar akitembea nami kwa ukaribu sana.

Aliona jinsi ambavyo sikuwa mtu wa kucheka-cheka sana na watu maana tulipokuwa tumeingia kule ndani, kuna wale waliokuwa wakishoboka kiasi na yeye kusimama kuwasemesha, ila mimi hata sikusimama kumsubiri. Mpaka akanifata na kuniuliza mbona namwacha kama vile niko kivyangu, ndiyo nikamwambia mimi sishobokagi na watu, akitaka kuongea na mtu hakatazwi, ila siyo lazima mpaka na mimi nijiunge naye.

Kwa kuelewa agenda yangu vizuri sasa, akawa mpole na kuniongoza mpaka alipokuwa amekaa; meza pana ya plastiki sehemu ya kona iliyojificha kiasi, na hapo walikuwa wamekaa wanawake wengine wawili rika kama la Khadija tu pamoja na mwanaume mtu mzima, mkubwa kabisa yaani kutosha kuwa mzazi kwangu, nasi ndiyo tukakaa hapo.

Tukasalimiana vizuri tu, huku nikiona jinsi ambavyo walinitazama kwa hamu, yaani labda nianze kushoboka nao sasa, lakini nikatulia tu na kuweka ubize kwenye simu yangu. Kulikuwa na bia hapo mezani, naye Khadija akawa ananinong'oneza kimakusudi tu yaani ili kujionyesha, akiniuliza nataka bia gani. Nikamwambia aagize Serengeti Lite, nikiwa makini yaani, naye akatii.

Hawa watu tuliokaa nao walikuwa ni washkaji zake Khadija eti, akiniambia hasa wale wanawake wawili alijuana nao na ile alipokuwa amekuja hapa kunisubiria, akawa amekutana nao. Ila nilijua alikuwa anadanganya tu, hao walikuwa ni mashoga zake wakipewa bia za ofa na huyo mwanaume mwingine, na hapa alikuwa amenileta ili kunioshea kwao, kwamba yuko na mtu mkali sana, si kingine. Hizi akili nazielewa sana.

Kwa hiyo nikaletewa bia tatu, nami nikamwambia Khadija nataka kuona bia themanini hapo mezani. Akacheka kwa furaha sana na kuanza kunisemesha kwa ukaribu ili tuonekane wapenzi wa dhati, na kweli, macho ya wengi hayakujizuia kutuangalia. Kulikuwa na sehemu zenye wanawake wakali kupita huyu mwanamke, na wengi waliniangalia sana. Hawa marafiki zake Khadija wakawa wanamtania eti awe mwangalifu asije kuibiwa mtu wake, naye akawa anajinadi kwa kusema haiwezi tokea maana tunapendana sana.

Nilianza kuona kwamba Khadija alikuwa amelewa zaidi, kwa sababu alikuwa ameshaanza kunywa pombe ile jioni kufikia wakati ambao nilikuja hapa, kwa hiyo mpaka namaliza bia zangu tatu yeye pia alikuwa ameongeza na kushusha zingine kooni. Aliongea na marafiki zake kwa kujiachia sana, kufikia hapo akiwa ameupandisha mguu wake mmoja juu ya paja langu, nami nikawa naona hapa siyo.

Highway ilikuwa imechangamka, lakini kwa hii kitu niliyokuwa nafanya nilikuwa napata vibe zenye kuboa tu. Khadija akataka kuniongezea bia, lakini nikamzuia. Nikamwambia imeshaingia saa tatu, tuondoke, naye akakubali. Alifikiri nina hamu sana ya kuondoka hapo pamoja naye ili tukafanye yetu, ila mimi nilikuwa nataka tu nitoke sehemu hii.

Moja, mbili, tatu, tukawa nje, Khadija akitembea nami huku ameshika kiwiko changu na pochi yake, na akionekana wazi kwa yeyote yule kwamba bia imemgonga, lakini hakuyumba. Nikamuuliza ni wapi kabisa alipokuwa amepanga twende kwa ajili ya jambo letu, naye akasema angenipeleka, ila tungepaswa kuchukua bodaboda mpaka kufika huko. Alikuwa anataka tupande kwenye boda moja eti, lakini nikamwambia hapana; tupande mbili maana sikupenda kubanana.

Kwa sababu fulani alionekana kupenda sana ujeuri niliokuwa namwonyesha maana alikuwa akicheka tu kwa kufurahia chochote nilichosema, nasi tukawa tumepata bodaboda mbili na kupanda; aliyopanda Khadija ndiyo ikiongoza kuelekea alipotuwekea makazi ya muda.

Tukiwa ndiyo tumeingia barabarani, nikawa nimepigiwa simu na askari Ramadhan, nami nikakumbuka kwamba nilikuwa na miadi ya kukutana naye leo ili tupange mikakati, lakini na hilo nikawa nimesahau. Nikapokea, naye alitaka tu kunijulisha kuwa kuna vitu vilimbana sana leo kikazi ndiyo maana akakosa muda wa kunitafuta, ila kama ni sawa basi kesho tutakutana mapema, kwa kuwa ingekuwa ni Jumamosi.

Nikamwambia haikuwa na shida kabisa, na ile amekata simu ndiyo bodaboda zikawa zimesimama. Haikuwa mbali sana kama nilivyodhani ingekuwa, tena hayo hayo maeneo ya Rangi Tatu kupita Zakhem kuelekea sehemu ya kushusha abiria usawa wa tawi la benki ya KCB, kisha kukunja kona kuiacha barabara ya lami na mbele kidogo ndiyo tukafikia jengo pana lenye ghorofa mbili. Lingefaa hata kuitwa hoteli, lakini wamiliki wakaona ni bora zaidi kuliita Lodge.

Eneo hilo lilikuwa na hali ya ugiza, kusiwe na watu wengi sana kuachana na wapita njia, mafundi wachache wa gereji walioonekana kwa mbele, na daladala kadhaa zilizotulia. Kwa hiyo tuliposhuka, Khadija akalipia usafiri, kisha ndiyo tukaelekea ndani ya hiyo lodge. Alikuwa amepitisha mkono wake kiunoni kwangu na kutembea nami akilalia bega langu, nami nikawa nimemshikilia begani pia kumwonyesha 'support.'

Tukaingia mpaka mapokezi, na mhudumu aliyekuwepo hapo, mwanamke mtu mzima pia, akawa amempa Khadija funguo ya chumba ambacho tayari mwanamke huyu alikuwa amelipia, nasi tukaanza kuelekea sehemu yenye ngazi. Tulipanda ngazi na kufika ghorofa la pili, na ilikuwa kama vile hamna watu wengi sana hapa, ila bila shaka kwa waliokuwepo walikuwa vyumbani wakifanya yao. Na ilikuwa sehemu nzuri, Khadija alijitahidi.

Akanifikisha kwenye mlango wa chumba chake, naye akatangulia kuingia huku nikifata kwa ukaribu nyuma yake; macho yangu yakitembea na mdundiko wa kalio lake. Kama ni kuondoa stress angekuwa amenisaidia sana kwa leo pia kama tu kucheza game na Shefu Saidi kulivyokuwa kumenituliza.

Chumba kilikuwa kizuri, kisafi, kitanda kipana, hadi kulikuwa na TV ndogo ya flat screen ukutani, naye Khadija akaenda kitandani na kukaa kwa kujiachia, mikono yake ikiupa mwili egemio huku ananiangalia kwa macho yenye uvutio. Ilikuwa ule mtindo kama vile anakaribia kulala chali, nami nikawa nimesimama tu huku nimeshasimamisha msuli kwa ndani tayari. Fikira tu za jambo lote.

Akaniambia, "Nimegharamika kweli kwa ajili yako leo."

"Umelipia shi'ngapi hapa?" nikamuuliza.

"Elfu hamsini," akanijibu hivyo.

"Na pombe ulikuwa unanunua. Umetoa wapi hela?"

"Ish... nina kazi, kwani unanionaje?"

"Naona kama mume wako ndiyo anakugharamia, ila hii... unaweza ukawa umemchomolea laki ama umedanga kwingine ili tuwe hapa..."

"Ahahaaa... nayedanga naye ni wewe. Na sijawahi mimi... kutoa hela kwa ajili ya mwanaume... wewe ndiyo wa kwanza," akasema hivyo kilevi.

"Kumbe?"

"Eeeh. Njoo hapa..."

Akaniambia hivyo huku akiupandisha mguu wake kwenye wakwangu akiwa ameunyoosha, mpaka kiatu f
chake kikagusa sehemu yangu ya siri na kuikandamiza kiasi. Nikaushika na kumsogelea karibu zaidi kwa kuingia katikati ya miguu yake, akiipanua sasa na kujilaza zaidi kitandani huku ananiangalia kwa hamu. Kwa hiyo sasa nikawa kama nimelala juu yake, uso wangu ukiwa karibu na wake, naye akaanza kupitisha vidole vyake kichwani kwangu taratibu.

"Yaani una sura nzuri we' kaka..." akaniambia hivyo.

"Kumbe? Mbona sikujua?" nikamsemesha kizembe.

"Ahah... nimekuelewa sana..." akaniambia hivyo.

"Na mume wako je?"

"Mzinguaji tu..."

"Kwenye kipi?"

"Mambo mengi. Tunaelewana, sema yeye tatizo lake ana gubu sana. Yeye atoke nje na mahawala, sawa tu... halafu mimi hataki nifanye jambo kama hilo. Wanaume wengi wananitaka, nawapotezea... lakini wewe hapana. Nimeshindwa kujizuia..." akaongea kwa njia fulani ya madaha sana.

Akataka kunivuta ili tuanze kupiga busu, lakini mimi nikataka nimchimbe zaidi kwanza, kwa hiyo nikaweka mgomo kiasi na kusema, "Ngoja kwanza. Hivi siku ile nimekushika nyonyo, si alituona?"

"Ahhh... eeh alituona," akanijibu hivyo.

"Mbona akawa mpole?"

"Ah... pale alikuwa anaigiza tu, we' ile familia si unaijua?"

Kauli yake ikanifanya nitambue kwamba huyu mwanamke alielewa mambo mengi sana kuhusiana na familia ya Miryam na mume wake, nami nikaona nitikise kichwa kukubali hiyo hoja.

"Alituona. Hiyo siku tumerudi nyumbani nilisemwa!" akasema hivyo.

"Wewee..."

"Acha kabisa. Alinitukana kweli. Ila huwa nikija chini tu baadaye mambo yananyooka. Mwenzako nikafikiri sitakuja kukuona tena, ila Mungu akiwa na mipango yake bwana... haipingwi..." akasema hivyo.

Nikatoa tabasamu hafifu, kisha nikaona nikoleze mambo.

Nikafunua upande wa kushoto wa gauni lake kifuani, na titi lake moja likafichuka. Nikaanza kulinyonya, nene kweli, nikinyonya chuchu yake taratibu huku navuta lile la kulia, naye akawa anapumua kwa raha na kugeukia upande kwa upande huku akichezea nywele zangu kichwani.

Nikaacha kulinyonya na kuanza tu kulivuta-vuta, kisha nikamuuliza, "Kwa hiyo mume wako bado anawa-mind sana ndugu zake, eti?"

"Ahh... eeh... wakuda tu. Wewe mwenyewe... sijui unawasaidia lakini si Miryam am
ekufukuza juzi? akasema hivyo.

Nikamtazama kwa umakini, nami nikamuuliza, "Umejuaje? Ni kweli kabisa alinifukuza."

"Mama mkwe mdogo aliniambia jana nilipoenda pale. Hadi na yeye alikuwa haelewi. Ulimfanya huyo Miryam lolote baya?"

Nikawa namwangalia kwa umakini, nami nikamwambia, "Hamna hata. Ila ni kweli kabisa... ni wakuda sana. Nilikuwa namshauri tu halafu akanifukuza. Alinikera!"

"Huyo mwanamke ndiyo alivyo, huwa hasikilizi, anajionaga anajua sana. Wote tu ni wajinga-wajinga... hata usijipendekeze kwao..."

"Kweli kabisa. Hawanipi faida yoyote, na watakuja kuishia pabaya maana wana viburi mno. Natamani kitu chochote tu kiwapate ili wajifunze," nikaendelea tu kutia chumvi.

"Si ndiyo maana Joshua yuko hapo? Atawanyoosha tu!" akasema hivyo.

"Kumbe? Basi hiyo itakuwa vizuri. Ningekuwa najua hata nisingempinga jamaa kipindi kile... basi tu," nikaongea kama vile namuunga kabisa mkono.

"Eee... alinihadithiaga... alikuwa karibu kweli kuchukua mali ila ukamvurugia. Lakini nikwambie kitu? Sasa hivi hawatoki. Yaani kipute extra kinawakuta. Utakuja kusikia," akaniambia hivyo.

"Joshua anakuja kivingine, au siyo?"

"Haswaa! Mimi hapo tu ndiyo huwaga namkubali... hakatagi tamaa. Na hivi anajua kuigiza, alinipanga fresh kweli kwa ajili ya hii show... we' subiri tu... imeshaanza kazi. Huyo mwanamke ataelewa haelewi," akaongea kwa nyodo za wazi.

Mh?

Nikajikuta naangalia tu pembeni nikiwa nawaza kuhusu taarifa hii, nikifikiria kuhusu ni nini ambacho kingekuwa kimeanza kufanywa na Joshua dhidi ya familia ile. Umeona? Nilikuwa sahihi kufikiri huyu mwanamke alijua vitu fulani kuhusu mipango ya mume wake, na hii ingekuwa nafasi nzuri ya kujua yote yaliyokuwa yamepangwa ili nitafute njia ya kuyazuia bila kujali kingine.

Khadija alikuwa amenishika mgongoni, nikiwa nimelala juu yake lakini kwa ubavu, kwa hiyo akapitisha mkono wake kwa chini mpaka kuigusa mashine yangu na kusema, "Jamani... ni(.....) basi!"

"Eh! Maneno makali dear," nikamwambia hivyo.

"Ninawashwa mwenzako..." akasema hivyo kwa deko.

Nikaingiza kiganja changu kwenye mapaja yake na kushika sehemu ya kati, naye akanyanyua mguu wake na kuutandaza vizuri ili niweze ku....

Kabla sijaanza kufanya mitekenyo yoyote ile kwa huko chini, simu yangu ikaanza kuita. Ilikuwa mfukoni, kwa hiyo nikatoa kiganja changu kwenye mapaja ya huyu mwanamke na kuanza kuivuta. Khadija akawa ananiambia niachane nayo, nami nikasema kama isingekuwa mwito kutoka kwa mtu muhimu basi ningeitolea sauti ili tuendelee na mambo yetu.

Nilipofanikiwa kuitoa nikakuta mpigaji akiwa ni Bi Zawadi, nami nikatulia na kuangalia muda hapo hapo kwenye simu. Ilikuwa ni saa tatu na nusu sasa, nami nikaona niachane na Khadija kwanza ili nimsikilize mama mkubwa. Nilihisi lingekuwa suala lililomhusu binti Mariam kama siyo tu kwamba alitaka kunisalimia. Khadija akawa ameendelea kujilaza niliposema simu ni muhimu kupokea, kisha ndiyo nikapokea na kuweka sikioni.

"Haloo... JC..." Bi Zawadi akasikika.

"Naam mrembo wangu... za jioni?" nikaitikia.

"Si salama sana baba," akasema hivyo.

Sauti yake ilijengeka kiwasiwasi yaani, nami nikamuuliza, "Kuna tatizo gani mama?"

"Tafadhali niambie umemwona Tesha..." akasema hivyo

"Tesha? Leo hapana, sijaonana naye," nikamjibu.

Khadija akajinyanyua na kukaa, akiniangalia kwa ukaribu na macho yake lege.

"Eh Mungu!" Bi Zawadi akasema hivyo kwenye simu.

"Shida ni nini?" nikauliza kwa kujali.

"Tesha ameondoka na Mamu... alitakiwa kuja muda siyo mrefu ila mpaka sasa hivi hawajarudi..."

Kauli hiyo ikanifanya nishtuke kiasi moyoni.

"Jamani tumechanganyikiwa huku JC... tumemtafuta hapatikani mpaka sasa hivi... atakuwa amempeleka wapi Mamu?" Bi Zawadi akaongea kwa hisia.

"Tesha alikuwa ameondoka naye kwenda wapi?" nikamuuliza.

"Walitoka... Tesha alikuwa ameenda kufata kitimoto... Mamu akamsindikiza, walitakiwa kurudi mapema, ila wakakawia. Tulikuwa tunampigia simu kumuuliza mbona anachelewa na usiku unaingia, akawa anasema mboga bado ni ya kusubiri sana. Imefika mpaka saa tatu tukaanza kumpigia ndiyo akawa hapatikani kabisa! Eh... mpaka Miryam na Joshu wametoka kwenda kuwatafuta... pale walipoenda kuchukua nyama hawapo tena, na Mimi bado hajarudi. Wanawatafuta..." akaeleza hayo.

Nikakaza ngumi baada ya kusikia hivyo, nami nikamuuliza, "Joshua alikuwa hapo na nyie?"

"Ndiyo, alikuja kututembelea... JC, nakuomba utusaidie kumpata Tesha. Tuna wasiwasi sana, yuko na mtoto na sasa hivi usiku baba..." akaniomba.

"Sawa, usijali. Nitaangalia cha kufanya. Nikipata lolote nitakujulisha," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Asante sana baba," akashukuru.

Simu ikakatwa, nami nikaangalia pembeni kwa umakini.

Khadija akanitikisa begani kiasi na kuuliza, "Vipi? Ilikuwa mama mkwe wangu kama sikosei?"

Nikatazama chini na kusema, "Eeh. Ananiambia Tesha ameondoka na mdogo wake ila mpaka sasa hivi hawajarudi. Hapatikani... kwa hiyo wanawatafuta."

Khadija akacheka kidogo, kisha akasema, "Si nilikwambia?"

Maneno hayo yakanifanya nimtazame usoni, naye alikuwa anatabasamu kwa njia iliyoonyesha kwamba hilo ni jambo alilokuwa analielewa vizuri. "Unamaanisha nini?" nikamuuliza.

"Kipute extra kinawakuta! Joshu ashafanya yake, huyo msichana kabebwa," akasema hivyo.

Nikajitahidi kuonyesha kwamba hicho alichokisema hakikunishtua, na kwa kumpa kichwa ili afunguke zaidi nikasema, "Ahaa... kumbe ni Joshua! Dah, mwamba yuko vizuri... ndo' ile ishu uliyoniambia, eti?"

"Sasa je!"

"Wewe... lakini, huyu ameniambia kwamba Joshua yupo nao, sasa... kafanyaje hivyo?"

"Aah... nisikilize. Joshua ana akili. Katuma watu wake, halafu yeye yuko nao pale kwao kwa hiyo hawawezi kujua kama ni yeye. Nimekwambia Joshua anajua kuigiza wewe! Hadi anajifanya kwenda kuwatafuta ahahaaa... haki ya Mungu..."

"Ahah... heh... kwa hiyo... wamembeba Mariam... ili iweje sa'?"

"Si hako kataahira ndiyo kanasababisha Joshua asipewe mali yake? Akikaondoa ndiyo money zitaanza kuingia tena... na zamu hii nitakuwa namnyonya ka...."

"Subiri. Kwo'... unawajua waliotumwa?" nikamkatisha.

"Agh, ni huyo tu Yohana... rafiki yake. Wengine me siwajui. Ndiyo maana nilikwambia leo niko free sssana... Joshua alikuwa ameshanipanga mapemaaa. Kwa hiyo yupo huko anawa-teach, na mimi niko hapa nam-cheat... ahahahahh..." akasema hivyo na pombe yake kichwani.

"Kwa hiyo Mariam wamempeleka wapi? Wanaenda kumfanya nini?" nikamuuliza nikiwa nimeingiwa na wasiwasi.

"Watajua wenyewe! Wamtupe, wamfukie, wamchinje, sawa tu. Hakana faida yoyote hako kajinga. Ila kwa jinsi ambavyo namjua Yohana, lazima watakabaka kwanza mpaka watosheke ndiyo miamala ianze kuingia..." akasema hivyo na kuanza kucheka.

Fikira za mambo aliyoyasema huyu mwanamke zilifanya nihisi kama vile nimepigwa na kitu kizito yaani, nami nikatazama pembeni nikiwa nahofia sana. Nilichoka aisee!

Yaani niliwaza namna ambavyo hizi hali ziliendelea kuniweka katikati ya kila jambo lililohitaji suluhisho kwa njia ambayo ilikuwa kama vile imepangwa, mpaka kwa mara nyingine tena nikawa najiuliza kwa nini mimi. Lakini kwa wakati huu, nilitakiwa kukazia fikira zaidi juu ya njia ya kuweza kuwa suluhisho hilo kikweli, ili Mariam asipatwe na masaibu ambayo watu hawa walimpangia. Angekuwa kwenye hali ipi kwa sasa yule binti?



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Ngoma inogile hiyo, mwamba maswali yametosha we mpe mkuyenge huyo mwanamke faster utoke ukamsake Tesha
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Khadija akawa ananipapasa kwa njia ya kuamsha hisia, naye akaanza kunilamba shingoni na kusema, "Tuachane nao. Watauana wenyewe huko, sisi aaah... tunajilia bata zetu. Njoo baby..."

Akataka kunivuta uso ili tupige denda, lakini nikajitoa kwake na kusimama kabisa kutoka kitandani, kisha nikaanza kutafuta namba fulani ya simu.

"Vipi tena my?" Khadija akaniuliza hivyo.

Nikapata namba hii na kupiga, kisha nikaweka simu sikioni.

"Unampigia nani?" Khadija akauliza tena.

Baada ya mlengwa kupokea, nikasema, "Hello... bwana Ramadhan..."

Ilikuwa ni askari Ramadhan ndiyo, naye akasema, "Ee hallo. Vipi, kuna jipya?"

"Ni baya sana mkuu. Nahitaji msaada wako," nikamwambia hivyo.

"Ni kuhusiana na huyo mwanamke?" akauliza.

"Hapana, ni... ni mdogo wangu. Ametekwa," nikamwambia hivyo.

Nikaona sura yake Khadija ikionyesha mshangao mkuu baada ya mimi kusema hivyo, naye akasema, "Wewe..."

"Mdogo wako ametekwa? Lini? Na nani?" askari Ramadhan akauliza.

"Hii hii jioni. Kaka... nakuomba utume tu hata watu waje nilipo, nimemshikilia mtu anayefahamu walipo hao wapumbavu," nikamwambia.

Khadija akasimama na kuanza kunisogelea huku akisema, "Wewe, unafanya nini? Unaogea na nani?"

Askari Ramadhan akaniuliza, "Ndo' aliyeongea hapo?"

"Ndiyo," nikamjibu hivyo.

Khadija akanishika mkononi na kusema, "Wewe... unafanya nini? Unataka kunigeuka? Mbona..."

Nikamsukuma kwa nguvu mpaka alipoangukia kitandani tena, nami kwa hasira nikamwambia, "Tulia hapo hapo... nitakuwasha!"

"Mbona sikuelewi?" Khadija akaniuliza kwa hofu.

"Uko wapi?" askari Ramadhan akauliza hivyo kwenye simu.

"Tuko hapa Mbagala Rangi Tatu... lile eneo lenye tawi la benki ya KCB sijui kama unalifahamu..."

"Haina shida, tutalipata. Endelea kumshika huyo asikuponyoke," askari Ramadhan akaniambia.

"Sawa. Tafadhali waambie vijana wako wawahi kaka... mdogo wangu anaweza akawa kwenye shida kubwa," nikamwambia kwa msisitizo.

"Usijali, nakuja mimi mwenyewe hapo. Sipo mbali," akaniambia hivyo.

"Sawa," nikasema hivyo na kukata simu.

Nikamwangalia Khadija, akiwa kitandani bado na akiniangalia kwa macho yenye mshangao, naye akasema, "Kumbe we' ni snitch!"

"Ndo' breaking news!" nikamwambia hivyo kwa hasira.

Akasimama na kutaka kunipita ili aukimbilie mlango, lakini nikamshika kiunoni kwa nguvu na kumvuta tena akirudie kitanda.

"Niachie!" akapiga kelele.

Nikamwachia kweli, nami nikaifata pochi yake na kuchukua simu yake pia, kisha nikauwahi mlango na kutoka. Nikaufunga mlango kwa funguo kabisa, na kutokea humo ndani nikawa namsikia jinsi alivyoupiga-piga mlango na kuita kwa sauti ya juu, akitaka nimfungulie. Kelele zake zikawa zimewatoa baadhi ya watu waliokuwa kwenye vyumba vyao hapo juu na kutokea chini pia, na yule mwanamke wa mapokezi pamoja na mlinzi wakawa wamekuja pia kujua nini kiliendelea.

Nikiwa nimesimama hapo hapo usawa wa mlango, nikawaelezea kwamba mwanamke huyo pamoja na watu aliokuwa akishirikiana nao walimteka mdogo wangu wa kike na kumpeleka sehemu isiyojulikana kwa madhumuni mabaya, na huyu mwanamke angekuwa anajua ni wapi kwa hiyo nilikuwa nimewasiliana na mapolisi ili waje kunisaidia kumshurutisha aseme kila kitu na kwenda kumsaidia mdogo wangu huko alikokuwa.

Mwanamke yule wa mapokezi, akiwa ni msimamizi wa hiyo lodge pia, pamoja na mlinzi walikuwa wakihofia labda mapolisi kuja hapo haingekuwa nzuri, lakini nikawahakikishia kwamba lengo lao kuja ilikuwa ni huyu mwanamke tu, wasingewazingua kwa lolote.

Nikawaomba uvumilivu watu wengine ambao walisumbuliwa na kelele za huyo Khadija, nao wakaonyesha uelewa na kusema nimefanya jambo sahihi ili kuweza kumsaidia mdogo wangu. Hadi baadhi yao wakaanza kuongelea suala hilo kwa undani zaidi kwa kufananisha na visa walivyofahamu, nami nikaendelea kusubiri huku nikiomba isiwe kuchelewa sana kumsaidia binti Mariam.

★★

Hazijapita dakika arobaini, naye askari Ramadhan akawa amenipigia kuniambia ndiyo alikuwa amefika kwenye eneo nililokuwa nimemwelekeza, ila ningepaswa kumsogeza mpaka sehemu niliyokuwepo kabisa.

Kufikia sasa nilikuwa nimekaa kwenye sofa ile sehemu ya mapokezi pamoja na yule mwanamke msimamizi, huku mlinzi akija mara kwa mara kutuangalia, na hata kelele za Khadija zilikuwa zimetulia, kwa hiyo nikamwambia Ramadhan kwamba ninatoka hapo nje ili kumleta. Nikamwambia msimamizi asije kumfungulia Khadija mpaka nirudi maana maaskari ndiyo walikuwa wameshafika, naye akaniambia nisijali.

Nikatoka, mpaka nje ya geti, nami nikawa naielekea lami nilikodhani ningeona gari lolote la kipolisi, lakini sikuwa hata nimeifikia na tayari nikaona Land Cruiser ya samawati iliyolowana, ambayo kwa nyuma ilikuwa wazi kwa ajili ya kukalisha wahalifu bila shaka, na kwenye ubavu/mlango ilikuwa imeandikwa "POLISI." Ilisimama usawa wa mlingoti wenye bendera kwenye jiwe la msingi la CHADEMA, nami nikajua lazima tu askari Ramadhan angekuwa humo.

Nikiwa umbali mfupi tu kutoka hapo, nikampigia simu huku nikilipungia mkono gari hilo kuvuta uangalifu wa waliokuwemo, nazo taa za mbele za hilo gari zikashtua mara mbili kunielekea kuonyesha kwamba walikuwa wameniona. Gari likaanza kunifata, kwa hiyo nikakata simu na kuirudia Lodge tena.

Watu waliokuwa kwenye eneo la hapo nje wakati huu walitutazama sana, si unajua mapopo wakiwa wameingia maeneo sikuzote huwa kuna presha? Kwa hiyo niliposimama usawa wa geti, gari likawa limesimama pia pembeni ya barabara, kisha akashuka askari Ramadhan pamoja na askari mwingine; mwandamani wake.

Ramadhan alikuwa na mwili wenye nguvu, mkubwa na mrefu kunipita, na wakati huu alikuwa amenyoa kipara kichwani, akivaa T-shirt jeusi la mikono mifupi pamoja na suruali jeans, viatu vigumu kama mabuti, na kwenye bega alininginiza bunduki ndefu, zile AK-47 zenye kiwiko cha mbao nzito mwishoni.

Mwenzake alikuwa ni mwanaume mtu mzima pia, mweusi na mwenye ndevu kiasi kidevuni, akiwa amevaa T-shirt jeusi pia na suruali ya kardet ya kiaskari, na mabuti ya kiaskari. Kwenye mkanda wake kiunoni zilining'inizwa pingu mbili za chuma (wengine wanabebaga za kamba), nao kwa pamoja wakanifikia karibu zaidi.

"Asante sana kwa kuja kaka..." nikamwambia hivyo askari Ramadhan.

"Ndiyo humo?" Ramadhan akauliza hivyo.

"Ee, yuko ndani," nikamjibu.

"Twende," akasema hivyo.

Nikatangulia. Moja kwa moja mpaka kule juu, na hata yule mlinzi wa hapo pamoja na msimamizi yule mwanamke wakawa wamefuata nyuma yetu mpaka tulipofika chumbani na kuingia. Sikuwa nimesahau kubeba simu na pochi yake Khadija.

Tulimkuta akiwa amejilaza kitandani, sijui usingizi wa pombe ulikuwa umeshaanza kumbeba, nami nikaupiga-piga mguu wake ili kumwamsha. Akajigeuza taratibu na kututazama, na nafikiri baada ya kumwona Ramadhan vizuri ndiyo akawa ameelewa mchezo sasa. Akavuta miguu yake vizuri zaidi na kujikalisha hapo kitandani huku akitutazama kwa wasiwasi.

"Niliyekwambia ametekwa ni binti anayekaribia miaka 20... anaitwa Mariam... ni mgonjwa wangu huwa namsaidia, kwa hiyo namwona kama mdogo wangu. Mume wa huyu mwanamke ndiye aliyetuma watu wamteke kwa ajili ya masilahi fulani ya kibinafsi... na ametoka kuniambia wanapanga kumbaka kisha wamuue. Inabidi atupeleke walikompeleka Mariam... ni muda mrefu umepita, nina hofu sana," nikamwambia hivyo askari Ramadhan kwa huzuni.

Akamwangalia Khadija na kusema, "Wewe, hayo yote ni kweli? Mmemteka mtoto mdogo mkamuue?"

Khadija akawa anatikisa kichwa kukataa huku akifinya-finya vidole vyake kwa woga, naye akasema, "Me... siyo mimi... me... nimeambiwa tu... me sihusiki..."

"Wamempeleka wapi?" Ramadhan akauliza kwa sauti ya amri.

"Me... sijui... si..." Khadija akawa anajing'ata-ng'ata.

"Ahaa? Nikutekenye ili ujue?" askari Ramadhan akamsemesha hivyo huku akitishia kumfata.

Khadija akarudi nyuma kwa woga huku akionekana kutaka kulia, naye akasema, "Hamna, hamna... me sijui sana... yote anayajua Joshuua... me huwa ananiambia tu... ila me sijahusika... haki ya Mungu sijahusika..."

"Joshua ndiyo nani?" akauliza yule askari mwingine.

"Mume wake. Kaka sikia. Kaniambia mmoja wao ni rafiki yake huyo Joshua... anaitwa Yohana. Huyo ndiyo kamteka Mariam... na inawezekana wawili, maana shabaha yao kuu ni huyo msichana lakini wakati wanamchukua alikuwa na mtu mwingine... kaka yake, na yeye ni kijana mdogo. Huyu mwanamke anajuana na huyo Yohana. Tukimpata, tumempata Mariam," nikamwambia hivyo askari Ramadhan.

Akamwangalia Khadija, ambaye alikuwa amejibana mwishoni mwa kitanda huku akitutazama kwa hofu, naye akamuuliza, "Una namba za huyo Yohana?"

Khadija akatikisa kichwa kukubali.

"Jibu kwa mdomo ukiulizwa maswali," askari mwingine akamwambia hivyo.

"N.. ndiyo.. ipo kwenye simu yangu.. a-ameidhukua huyu..." Khadija akasema hivyo huku akininyooshea kidole chake.

"Ushawahi kukaa jela?" Ramadhan akamuuliza.

"Hamna, jamani... me sija... sihusiki, sihusiki, ni wenyewe tu... me nilikuwa namwambia tu huuyo... wamemchukuua... siyo mimi! Me siwezi kuteka mtu... haki ya Mungu..." Khadija akawa anaongea huku machozi yakimlenga.

"Ila si ulikuwa unafurahia mume wako kufanya hivyo? Kiwapate chochote kibaya hao ndugu wawili... cha moto utakiona," Ramadhan akamwambia hivyo.

Khadija akaanza kulia huku akitikisa-tikisa viganja vyake eti kwa mideko. Aliniudhi!

"Sasa nisikilize... acha ujinga kujiliza... nisikilize. Kama hautaki tufikishane pabaya, utafanya kila kitu nitakachokuelekeza, sijui umenielewa?" Ramadhan akamwambia hivyo.

Khadija akatikisa kichwa haraka-haraka kuonyesha yuko tayari.

Ndipo askari Ramadhan akaomba nimpatie simu ya mwanamke huyo, naye akaanza kumpanga sasa juu ya kile alichotaka afanye. Khadija hakuwa na namna ila kukubali tu kila kitu, naye akapewa simu yake ili kutekeleza amri za askari. Yule msimamizi alikuwa hapo pia pamoja na wapangaji wengine wa vyumba waliokuja kushuhudia, nami nikawa tu natazama muda kwa wasiwasi mwingi sana. Ilikuwa ni saa tano kasoro sasa. Ambayo yangekuwa yametokea!

"Haya. Mpigie..." askari Ramadhan akamsemesha Khadija.

Mwanamke akatii na kupiga simu, kisha akaweka mfumo wa kipaza sauti ili maongezi ambayo yangeendeshwa yasikike kwetu sote. Ikapokelewa.

"Vipi sugar? Umenimiss tayari?" sauti ya mwanaume ikasikika kutokea upande wa pili.

Sote tukaelewa kwamba huyo alikuwa ndiyo Yohana.

Khadija akasema, "Eeh... baby, nimekumiss. Uko'api?"

"Tss, kwani hujui mishe tul'ofanya leo? Halafu huyo mume wako zamu hii akizingua yeye ndiyo tutambanika. Kazi zote tunafanya sisi, yeye ka-relax tu na kupiga domo 'ooh hela zitakuja tu mkishamteka na kumfukia'... anafikiri kuteka na kuua mtu kazi rahisi eti?" Yohana akasema hivyo.

Ramadhan akamwonyesha Khadija kwa ishara ya kidole kuwa awahishe mambo.

Khadija akasema, "Yohza... huyo msichana yuko wapi? Ume.. umempeleka wapi?"

"Hahah... nilijua tu wivu ungekuingia. Unawaza nimeshafinyia ndani huku, eti?" Yohana akasema hivyo.

"Ni.. siyo kwamba... yaani... ni muhimu nijue. Joshu ameniambia kwamba... usi-usimfanye chochote kwanza... yaani usimguse mpaka akwambie..." Khadija akasema hivyo.

"Joshua kakwambia wewe uniambie hayo? Hana namba yangu?"

"Hap-hapana... siyo kama hivyo. Sikia. Yeye yuko na hao watu sasa hivi... wanamtafuta huyo msichana. Ameniambia nikufikishie hiyo taarifa... kwa sababu hataki mwasiliane mpaka pakae fresh kabisa... ila ana maana yake kuto..kutotaka... umuumize mdogo wake..."

"Kageuka kuwa mdogo wake sasa hivi wakati ameshanituma mara mbili kumuua? We' vipi?" Yohana akasema hivyo.

Khadija akatulia kidogo, kisha akauliza, "Kwa hiyo... umemuua?"

Nikang'ata meno nikisubiri jibu kwa kujikaza, na huyo Yohana akasema, "Bado. Kamelala bado, huyu mjingammoja alitumia midawa mingi kweli kukalewesha. Ila kanaonekana katamu. Kakiamka tu nakala... nataka niirekodi miguno."

Nikakunja ngumi kwa kuhisi hasira.

Khadija akasema, "Hamna Yohana, usifanye hivyo kwanza... nisikilize..."

"Hahahah... nilijua ni wivu tu unakusumbua. Kichululu cha mume wako si kama mkonga wangu, ndo' maana hutaki niuingize kwingine zaidi yako, eti? Na siku akijua unachepukia kwangu sijui ndiyo na me nitatumiwa watu waniue? Ila hamnaaa... hupendwi kama hivyo. Hahahah..." Yohana akasema hivyo kizembe.

Khadija akaonekana kukosa amani, lakini akasema, "Kwa hiyo... umempeleka pale pale kwako tunakutanaga?"

"Yyyeah... kwenye kichali chetu cha mapenzi. Kule maficho palikuwa mbali... na hilo jam Mbagala, eh! Tukaona tuwalete hapa kwanza. Unataka kuja nini? Ulilete hilo sambwanda!" Yohana akasema.

"Wote yeye na kaka yake?" Khadija akauliza tena.

"Mbona maswali mengi sana? Umekuwaje wewe?" Yohana akauliza hivyo.

"Hamna... nilikuwa tu... naangalia kama mazingira yanaruhusu ili labda nije... nimekumiss kweli..." Khadija akapamba maneno.

"Ih, kumbe kweli unataka kuja? Sasa hivi? Mume wako si atazingua, au? Kwani analala huko huko? Ama me ndo' nije... maana hawa madogo wote tumewafungia hapa, sasa we' ukija wakakuona ama kusikia miguno yako, si watashtukia dili? Hehehe... shangazi katuteka..." Yohana akasema hivyo.

Khadija akawa anatutazama kwa wasiwasi tu, naye askari Ramadhan na mimi tukaangaliana kwa umakini.

Huyo Yohana akaendelea kusema, "Tumehangaika kuwaingiza hapa kwa siri, siyo salama kutoka na kuingia mpaka huu mchongo ukate. Hata me nimekumiss, ila kwa leo vunga... pamebana. Hapa tunangoja ifike saa nane nane ndo' tuwachinje hawa kuku huko nje, tuwafukie, mengine yaje. Mume wako anapaniki mno, anafikiri sisi hatujui kazi yetu, au? We' si ndiyo mjumbe wake? Mwambie atulize mshono... kazi itakamilika kama tulivyopanga, asianze kuingiza biashara zingine sasa hivi..."

"S..sawa... basi..." Khadija akawa anatafuta la kusema.

"Sisi ndo' wakali. Sisi ndiyo Kleptomaniax. Zamu hii asiwe ametuzushia lakini, na yeye tutamzingua maana hata magari bado tunatumia ya mkopo... mwambie..." Yohana akasema.

Ramadhan akamwonyesha Khadija ishara kuwa akatishe mazungumzo, na mwanamke huyo akasema, "Haya... basi baadaye baby, eh? Bye..."

"Mbona hamna hata..."

Askari Ramadhan akakata simu kabla maneno ya huyo mpuuzi hayajamalizika, naye akasema kumwelekea Khadija, "Vizuri. Haya... nyanyuka. Unatupeleka kwenye hicho kichali cha mapenzi sasa hivi."

Khadija akawa ananiangalia kwa huzuni sana, lakini sikumwonea huruma hata kidogo. Kwa kipi labda? Akajitoa kitandani na kusimama pembeni ya msimamizi wa hiyo lodge.

Askari mwandamani akamfata na kumfunga kwa pingu mikononi huku akisema, "Watu wengine sijui wakoje! Mtu anaongelea kumchinja mwanadamu mwenzake kama kuku na anacheka kabisa!"

"Leo ndiyo wamepatikana," akasema hivyo yule mwanamke msimamizi.

"Hiyo sehemu ni mbali sana?" Ramadhan akamuuliza Khadija.

Akatikisa kichwa kukanusha, naye akasema, "Ni hapo Mzinga... eneo fulani la ndani ndani..."

Eh! Kumbe walikuwa Mzinga tu hapo hapo?

Nikamwambia askari Ramadhan, "Kaka... nawasihi tuwahi. Hawa watu wanaonekana kuwa vichaa."

"Kweli, na ndo' watu wa kuweka mbali kabisa na jamii. Wewe... pita..." Ramadhan akasema hivyo na kumwamrisha Khadija namna hiyo.

Mwanamke huyo akatangulia kutoka huku akifuatwa kwa ukaribu na askari mwandamani, nasi wengine tukawa nyuma yao. Nilijihisi vibaya sana moyoni, yaani ile hisia kwamba kuna jambo baya lilikuwa limetokea na hapa ndiyo tulikuwa tunaenda kulishuhudia. Niliomba Mungu tu hisia zangu zisiwe sahihi.

Tukaenda mpaka kwenye gari, Khadija akiketishwa siti ya mbele pamoja na mwandamani wa askari Ramadhan, ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha, ili atoe mwongozo mpaka kufikia huko kwenye "kichali cha mapenzi." Mimi na askari Ramadhan tukakaa huku nyuma palikokuwa wazi lakini kukiwa na siti za mtindo wa mabenchi, na safari ikaanza.

★★

Ilikuwa kama Mungu tu kwamba hakukuwa na msongamano wa magari kwa sasa. Mwandamani wake askari Ramadhan alijitahidi kuendesha kwa kasi lakini kwa umakini sana mpaka tukalifikia daraja la Mzinga ndani ya dakika tano tu.

Tukiwa tunaendelea na mwendo, askari Ramadhan alikuwa amenijulisha kwamba muda ule nimempigia kumjulisha kuhusu kisa hiki yaani ndiyo alikuwa ametoka tu kuwatia mbaroni wahalifu fulani wawili akiwa na waandamani wenzake, kwa hiyo alijitahidi kuiwahi na hii ishu pamoja na mwenziye mmoja kwa sababu maaskari wengine walianza kushughulika na mambo mengi pale kituoni. Inaonekana alipenda sana kazi yake, na ndiyo maana alikuwa na hamu sana ya kuja kuwatia mbaroni
wakina Bertha na Chalii Gonga pia, akisema hiyo ingekuwa ni keki kubwa.

Yaani ile kalandinga imelipita tu daraja, mwendo mfupi kabla ya kufikia pale ambapo ukisema ushushiwe Mzinga ndiyo daladala itasimamia, gari likakata kona kuingia kwenye barabara ya vumbi. Likaanza kushuka kwenye njia nyembamba sana kuvuka maduka ya mafundi wa mageti ambayo yalikuwa yamefungwa sasa, taratibu kabisa mpaka kufikia njia ambayo ilianza kupanuka zaidi kuelekea eneo lenye hali ya ugiza, miti na vichaka vingi, na nyumba zilizoachana-achana.

Askari Ramadhan akawasiliana na askari mwenziye kuuliza ikiwa huyo mwanamke alitoa uelekeo sahihi kabisa, naye akajibu ndiyo; pombe ilionekana kuwa kichwani kwa Khadija bado lakini woga wake ulimpa umakini kuwaongoza vyema.

Walikuwa wakiongeleshana kupitia zile simu/redio zao maalumu, a.k.a walkie talkie, naye Ramadhan akamwambia mwenzake ahakikishe kwamba mwanamke huyo anampa hadhari ya mapema kwamba tumekaribia kuifikia nyumba aliyopo huyo Yohana mpuuzi, ili tuweze kuingia pale bila kutarajiwa. Jamaa akakubali.

Sikuwa nimemtafuta Bi Zawadi ama yeyote wa familia yake tena kuwajulisha kuhusu maendeleo haya kwa sababu hiyo hiyo. Sikutaka kumpa tahadhari Joshua, kwa sababu kama ningewaambia huko tunamkaribIa Mariam, wangemwambia Joshua, na jamaa angeweza kukimbia.

Kwa hiyo nikaona nitulie tu, na ilikuwa ni ule utulivu wa nje kama vile hali ya hewa inavyokuwa imetulia kabla ya dhoruba kali kuanza, na mimi ndivyo ilivyokuwa kwa ndani. Nilikuwa nina hasira! Sikujua kipimo chake.

Mwendo wa kuyumba-yumba wa hili gari ukakoma baada ya muda mfupi, nalo likatulia na kuzima taa za mbele kabisa. Askari Ramadhan akasimama, mimi pia, nasi tukawa tukaangalia eneo hilo mbele yetu. Kulionekana kuwa na nyumba ya matofali ya block isiyokuwa na umeme sijui, kubwa kiasi, ikiwa upande wa mbele zaidi kujitenga na barabara. Tuliweza tu kuiona kutokana na mwanga usiokuwa na nguvu sana wa taa iliyokuwa kwa ndani, labda tochi ama solar.

Askari aliyekuwa kwenye usukani akamjulisha askari Ramadhan kwamba mwanamke huyo alisema nyumba ya huyo jamaa ndiyo hiyo, kwamba anakaa hapo na ndugu zake wahuni tu kama yeye wanaojihusisha na mambo mengi mabaya. Hawa niliwaona kuwa wadogo sana kufikia nyenzo za watu kama Festo na Bertha, lakini kwa huu upuuzi waliokuwa wamefanya? Walikuwa kule juu yaani kwenye orodha ya wabaya wangu.

Tukashuka, wote, Khadija na pingu zake mikononi, naye Ramadhan akaanza kumpanga. Jamaa alikuwa makini kweli, akimwambia tunakwenda pale kwa pamoja kimya kimya, na yeye Khadija tunamtumia kama chambo ili huyo bwege anaswe kiurahisi. Ilikuwa kama mission impossible yaani, Ramadhan akiniamini kuwa pale pia kama nyongeza ya msaada ili lolote lile lisilotazamiwa likitokea basi nihusike upesi, nami nikakubali.

Tukaziondolea simu sauti, kisha tukaanza kwenda. Ilikuwa na faida kwamba hakukuwa na watu waliopita sehemu hiyo kwa wakati huo, nami pamoja na mwandamani tukawa tumefika usawa wa sinki pana la choo ardhini kuwatangulia Ramadhan na Khadija, ambako pembezoni niliweza sasa kuona gari aina ya Toyota Corolla.

Lilifahamika kwangu upesi kuwa ndiyo lile lile ambalo lilitumiwa kipindi cha nyuma kujaribu kumgonga Mariam, kwa hiyo ikawa wazi zaidi kuwa tulifika sehemu sahihi.

Nikapitiliza mpaka kufikia kuta za nyumba hiyo na kujibanza kwa umakini. Nikawa karibu kabisa na dirisha moja, na kutokea hapo ningeweza kusikia sauti za wanaume wakiongea mule ndani, lakini zaidi ikawa ni sauti za kukuru-kakara kutoka kwenye kitu kama kitanda, na miguno iliyozibwa. Dah!

Wasiwasi ukanipanda, nikajaribu hata kuchungulia hapo kidogo lakini nisingeweza kuona lolote kutokana na dirisha kufunikwa na magunia kutokea ndani, nami nikasikia sauti ya chini ya kicheko niliyotambua kuwa ya yule Yohana. Huyo mpumbavu mmoja aliyekuwa ametumwa kuharibu maisha ya binti Mariam!

Sasa askari Ramadhan pamoja na Khadija walikuwa wameufikia mlango, nami nikatoka hapo nilipokuwa na kusogea mpaka sehemu ambayo ilikuwa na nguzo nene ya hiyo hiyo nyumba ili Ramadhan anione, naye akaniangalia. Nikamwonyesha kwa ishara za mikono kwamba mambo yanaharibika, afanye haraka, ndiyo akampa ishara Khadija kwamba apige hodi.

Khadija akasema, "Hodii... Yohza..."

Wanaume waliokuwa wanaongea huko ndani wakaacha, naye askari mwandamani akawa amejibanza pembeni ya mlango sasa huku Ramadhan yeye akielekeza bunduki yake hapo mbele.

"Yohana... Yohza baby... ni mimi... najua haujalala, nimewasikia mnaongea. Njoo bwana..." Khadija akasema hivyo.

Na alikuwa anajitahidi kuigiza.

Sauti kule ndani ikasikika ikisema, "Oya... demu wako kaja... achana na hiyo show..."

Kisha mlango ukafunguliwa hapo na sauti ikasema, "Ndiyo umekuja sa...."

Maneno hayo yakakatishwa na sauti ya kishindo huku askari Ramadhan akisikika kusema, "Rudi ndani, nyani wewe! Tulia! Wote... njoo hapa! Sogea!"

"Lala chini, lala chini!" sauti ya askari mwandamani ikasikika pia.

Nikajipa ujasiri na kupanda hiyo sehemu ili nami niende hapo ndani. Nilitakiwa kutulia nje, lakini kwa wasiwasi niliokuwa nao? Hamna.

Nikafika hapo ndani na kukuta wanaume watatu wakiwa wamelala chini huku wamefunika vichwa vyao kwa mikono, na Khadija akiwa amepigishwa magoti na askari mwandamani huku Ramadhan akielekea usawa wa korido lililoelekea vyumbani.

Hapo walipokuwa wamelala hao jamaa palikuwa na mkeka chini, stuli mbili pembeni na viti vya plastiki vilivyokuwa vimeangushwa huku na kule. Sakafu ilikuwa ya kokoto, ikionekana hii nyumba bado haikuwa imekamilishwa kiujenzi, na ni harufu za sigara ndiyo zilizotawala hewani.

Nikamwangalia askari Ramadhan akiwa anaelekea huko mbele, nami nikamwahi na kumwonyesha mlango wa chumba kilichokuwa kwenye kona aliyoipita huku nyuma. Nikamwonyesha kwa ishara kwamba humo ndiyo kuna tatizo, naye akageuka pamoja nami na kukifata hicho chumba.

"Wewe uliye humo ndani? Yohana wa Kleptomaniax... toka haraka sana," askari Ramadhan akaamrisha.

Ningeweza kusikia sauti za kilio kilichozibwa kutokea humo, na aliyekuwa ndani hakutoa jibu kwa amri ya Ramadhan.

Askari huyu akajaribu kuusukuma mlango kwa nguvu, lakini haukufunguka. Nikaupiga pamoja naye kwa bega pia, wapi. Kisha ndiyo jamaa akarudi nyuma kidogo na kuupiga kwa teke zito, nao ukafunguka kwa kubamiza kabisa. Askari Ramadhan akaingia taratibu huku akinyoosha bunduki yake mbele, nami pia nikafata nyuma yake. Nilichokikuta kilifanya niishiwe nguvu kiasi.

Kwenye chumba hicho kulikuwa na kitanda cha double decker, na kwenye godoro la chaga ya chini ndiyo alikuwepo Mariam, akiwa amelala bila kuwa na nguo hata moja mwilini! Pembeni yake alisimama mwanaume mtu mzima kama tu askari Ramadhan, akiwa anamalizia kufungua kamba zilizoonekana kuwa zilimfunga binti Mariam mikono na miguu kwa kuutandaza mwili wake hapo ili amwingie kinguvu.

Huyo jamaa alikuwa na mwili mnene kiasi na kitambi cha pombe, mweusi mwenye ndevu kiasi kidevuni, na sasa alikuwa kifua wazi na vinyweleo vyake huku akijisitiri kwa bukta chini, na ndiyo akawa amemaliza tu kuifungua kamba ya mwisho mguuni kwa Mariam na kumvuta binti huyo kwa nguvu sana.

Aisee! Mariam alikuwa amefungwa kwa kitambaa mdomoni, macho yake yakitiririsha machozi mengi sana huku akitetemeka, na mwanaume huyo alikuwa ameushika mwili wake usiokuwa na nguo kutokea nyuma yake huku mkono mwingine ukiwa umeshika kisu na kukiweka karibu na shingo ya binti.

Ah, nilihofishwa sana na hicho nilichokiona mbele yangu aisee! Moja kati ya taswira mbaya sana tunazoonyeshwaga kwenye filamu za wazungu ndiyo ikawa mbele yangu. Nilihofia sana usalama wa huyu binti.

Ilikuwa imembidi askari Ramadhan asitishe kwenda mbele zaidi, lakini hakuishusha bunduki yake. Huyo jamaa, ikiwa ni Yohana nadhani, akawa anatuangalia kibabe huku akionyesha kutotaka mchezo la sivyo angemkata Mariam kwelikweli.

"Unajua nini kitaku-save matatizo makubwa mdogo wangu? Shusha hicho kisu, mwachie huyo mtoto, halafu ujisalimishe," askari Ramadhan akamwambia hivyo jamaa.

"Unafikiri mimi ni fala? Wewe ndiyo utupe bunduki yako... la sivyo nitamchinja huyu... sitanii. Mimi ni mkatili vibaya sana," jamaa akaongea kwa besi nzito.

"Eti eeh? Kwa hiyo ukimuua unafikiri nitakuacha?" Ramadhan akamuuliza.

"Ndiyo nakwambia hivi... itupe hiyo bunduki, la sivyo namuua. Tena itupie huku kwangu..." jamaa akaamuru.

Nilikuwa nahisi adrenaline inapanda mwilini, lakini nisijue la kufanya kutokea hapo.

Ramadhan akasema, "Unafikiri tuko kwenye movie, eti? Acha ujinga. Mwachie huyo mtoto..."

"We' ndiyo mjinga kama hautairusha hiyo bun..."

Kabla ya Yohana kumaliza maneno hayo, askari Ramadhan akafyatua risasi moja iliyotoa sauti kali sana!Nilishtuka kwa kutotarajia hilo na kuziba masikio yangu huku nikiinamia pembeni, kisha ndiyo nikatazama hapo mbele tena.

Sasa huyo Yohana alikuwa anapiga kelele za maumivu, 'waaaaah...' huku akiwa ameanguka chini na mguu wake ukionekana kuvuja damu nyingi. Askari Ramadhan alikuwa ameshawahi hapo, naye akamshika Mariam mkono kutokea chini ambapo binti alikuwa ameangukia pia na kumnyanyua ili asimame, kisha akamtolea kitambaa mdomoni.

Nikasimama vizuri zaidi, mapigo yangu ya moyo yakidunda kama ngoma, nami nikaingia ndani hapo zaidi mpaka kufikia aliposimama Mariam. Askari Ramadhan akamwachia binti na kumsogelea huyo Yohana karibu, kisha akaweka bunduki yake begani na kumshika mkono, akianza kumburuza kwenda nje na makelele yake. Dah!

Nikamwangalia Mariam kwa huruma na kumshika mabegani, naye akawa ananiangalia kwa hofu kama vile hanijui, yaani macho yake yalionyesha kuniogopa, huku viganja vyake vikitetemeka usawa wa kifua chake cheupe. Nilijihisi vibaya sana moyoni, mpaka nikakosa neno lolote la kumwambia. Ningesema nini? Eh?

Sikujua, na nisingeweza kuelewa ni hali ipi ambayo huyu binti alikuwa amepitia, ila hii haikuwa sehemu ya kuendelea kukaa. Wazo la kwanza katika kichwa changu lilikuwa kumwahisha Mariam hospitali baada ya kumpata Tesha pia, na bado sikuwa na uhakika ikiwa kaka yake alikuwa hapo.

Sikuona nguo yoyote ya kike humo ndani, hivyo kwa haraka nikalitoa shuka lililokuwa limefunika godoro la chaga ya juu kwenye kile kitanda, nami nikaufunika mwili wake kuanzia shingoni mpaka miguuni. Alikuwa ametazama chini, jasho lilimtoka kwa wingi, mapigo yake ya moyo yakidunda kwa nguvu sana, macho yake yakionekana kuchoka, huku pumzi zake za kilio zikimtoka kwa kutetemeka. Yaani!

Nilijua huyu asingekuwa wa kuambiwa 'twende' na yeye kuanza kutembea. Nilipaswa kumbeba. Ile tu ndiyo nataka kupitisha mkono wangu kwenye miguu yake kwa chini ili nimnyanyue, Mariam akalegea na moja kwa moja kudondokea mikononi kwangu kwa ughafla uliofanya niende chini pamoja na uzito wake.

Nikajitahidi kumshika shingoni na mgongoni vizuri na kumtazama kwa kujali, naye sasa alikuwa amefumba macho kabisa.

"Mamu.. Mamu..."

Nikajaribu kumwamsha, wapi! Nguvu zilikuwa zimemwisha masikini!



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Jumapili leo mwamba JC wengine sio wanywaji kwahiyo tunachil home tu tubless basi tusukumie weekend
 
Ukimtaka single mother wewe deal na mtoto wake ,, muoneshe upendo kadrii uwezavyo

JC .. katambua upendo wa miryamu upo kwa mariam ..kivyovyote ukiweza
Kumfanya mariam akupenda basi na miryamu atakupenda pia. Jc ni lover boy ajuaye anachokifanya..
 
Ukimtaka single mother wewe deal na mtoto wake ,, muoneshe upendo kadrii uwezavyo

JC .. katambua upendo wa miryamu upo kwa mariam ..kivyovyote ukiweza
Kumfanya mariam akupenda basi na miryamu atakupenda pia. Jc ni love boy ajuaye anachokifanya..
Anachakata for purpose
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Mvua ikaanza kuongezeka kiasi, Miryam bado akiwa amekaa chini huku wapendwa wake wakiendelea kumpa faraja, na ndiyo Tesha akawa ameenda hapo ili kuweza kumsaidia dada yake asimame. Nilikuwa nimesimama tu usawa wa kibaraza nikiwaangalia wote walipofanikiwa kumshawishi Miryam asimame ili waweze kwenda ndani kupanga mambo ya kufanya, naye Shadya akawa anashughulika na majirani waliokuwa wameingia ndani ya geti pia; akiwaomba waende makwao na kupumzika.

Bi Jamila na mama Chande wakawa wamemshikilia Miryam kumpa mkono alipoanza kutembea kuelekea ndani, na sasa alionekana kujikaza zaidi ili asiendelee kulia. Tesha akawa amekuja kwangu tena na kunishauri tuelekee kwenye bomba la hapo nje ili kujisafisha mikono, nami nikakubali na kwenda pamoja naye.

Mzee Hamadi, yule mwenyekiti, pamoja na wale wanawake wawili niliowakuta hapo wakawa wameondoka pia baada ya kuongea kwa ufupi na Bi Zawadi, na mwanamke huyo akaja pamoja na Shadya kufikia karibu na sehemu yenye bomba nilipokuwa nanawa.

Nilikuwa nimenawa usoni na kichwani, na sasa niliweka tu kiganja changu cha mkono wa kulia kipigwe na maji mengi kuiondoa damu, naye Tesha akachuchumaa karibu nacho na kuanza kukiangalia. Aliweza kuona kwamba kilikuwa kimevimba na sehemu nyingi ya damu iliyotoka ilikuwa yangu pia shauri ya kuchanwa na kipande cha kile chombo cha udongo nilichokipasulia kwenye mwili wa Joshua, hivyo akashauri twende ndani ili wanipake dawa tuitayo "spirit" na waufunge mkono kwa bendeji laini.

Niliposimama na kuwatazama Bi Zawadi na Shadya, nilikuta wakiniangalia kwa njia mpya iliyojaa huzuni nyingi sana, wakishindwa kunisemesha, na mimi nikishindwa kutoa neno lolote lile. Ni wazi kwamba hawakuwahi kutarajia kuja kuniona nikitenda kama vile nilivyokuwa nimemtendea Joshua, na mimi kwa wakati huu sikujihisi amani hata kuwatazama maana nilihofia labda hata wangeanza kuniogopa.

Lakini haikuwa hivyo. Bi Zawadi mwenyewe akaja na kunishika mkononi, na bila kusema lolote akaanza kuniongoza kwenda ndani ili wakanipatie msaada niliohitaji. Nikawa mtulivu tu, tukaingia sebuleni, nikaenda na Tesha mpaka chumbani kwake, na nafikiri Miryam na Bi Jamila walikuwa chumbani kwake kule ili kuchukua vitu alivyohitaji halafu ndiyo waelekee hospitali, kwa kuwa mama Chande alikuwa jikoni akionekana kuweka vifaa fulani kwenye mfuko, na Shadya akajiunga naye.

Nikiwa chumbani na Tesha, rafiki yangu huyu akawa ananiambia jinsi ambavyo kumpiga Joshua kama vile nilivyokuwa nimefanya ilikuwa kitu alichotamani mno kukifanya pia kwa muda mrefu sana, na akanipa sifa kuwa lilikuwa jambo sahihi kabisa.

Nilisimama tu huku nikimtazama jamaa bila kuhisi ahueni yoyote pamoja na yote, na ndiyo Bi Zawadi akawa amekuja na kisanduku chenye vifaa vya huduma ya kwanza na kutoa pamba, dawa, na bendeji, kisha tukakaa kitandani kwa Tesha naye akaanza kunichua kiganjani kwa spirit akitumia pamba. Iliuma, lakini sikujali.

Bi Zawadi alikuwa akiongea pamoja Tesha kwa hisia sana kuelekea suala zima la Joshua na Khadija, akisema alivunjika sana moyo, na aliumia mno kumwona Miryam akiteseka wakati dada wa watu alikuwa akijitahidi sana, sana, sana kuiunganisha hii familia. Tesha alionyesha kumwelewa dada yake pia, lakini akasema kwamba hilo ndiyo lingekuwa fundisho kwa Miryam kutokuwa na moyo mwepesi mno wa kuamini mtu kwa sababu tu ya kuwa ndugu, na alijua dada yake alijutia mno.

Nilikuwa nawasikiliza tu bila kusema lolote, naye Bi Zawadi akawa amemaliza kunifungia bendeji kiganjani na kisha kuishika mikono yangu kwa pamoja. Akanishukuru sana kwa kuwa msaada mkubwa kwao na kuniomba radhi pia kutokana na matatizo ya familia yake kusababisha na mimi niumie kama hivi nilivyokuwa nikiumia rohoni.

Akawa anasema ameona ni jinsi gani ambavyo nilimjali sana Mariam mpaka kukasirika namna ile na kukaribia hata kumng'oa kichwa Joshua, nami nikaendelea kumtazama tu kwa utulivu, nikiwa bado sijanena lolote lile kwa sababu ya kukosa amani moyoni.

Bi Zawadi alipokuwa amesimama ili arudishe kisanduku cha huduma ya kwanza chumbani kwake, Bi Jamila akawa ameingia pia, hivyo nami nikasimama na kumwangalia. Mwanamke huyo akaweka kiganja chake usawa wa mdomo huku akiniangalia kwa macho yenye huzuni sana, kisha akanisogelea na kunishika pande za mikononi.

"JC baba... uko sawa?" akaniuliza hivyo kwa kujali.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Ehh! Pole sana mwanangu, kwa kila kitu. Naelewa kwa nini ulikuwa umekasirika sana baba, na kwa hilo nikuombe tu msamaha kwa kweli... hukustahili haya yote. Ila hayo nakuomba tuyaweke pembeni kwa wakati huu. Nashukuru sana kwa kuwasaidia watoto wetu. Wewe umekuwa baraka kubwa sana kwetu. Bila wewe yaani... sijui tu... nini kingewapata vijana wetu..." Bi Jamila akaongea kwa hisia.

Aliposema anaelewa kwa nini nilikuwa nimekasirika sana, nikawa nimetambua kuwa alijua sababu iliyofanya mpaka siku ile nikakorofishana na Miryam na mwanamke huyo kunipiga kibao, ikionyesha kwamba huenda Miryam alikuwa ameshamwambia yeye na labda hata Bi Zawadi pia, hivyo kwa njia fulani hapa ni kama alikuwa anaomba radhi kwa niaba ya Miryam.

"Hapana mama... usiseme hivyo, hamjanikosea kwa lolote kwa hiyo ondoa maneno ya kuomba msamaha. Na ni Mungu tu ndiyo mkubwa, amesaidi..." nikawa nimeanza kuongea hatimaye, lakini nikakatisha maneno yangu baada ya Miryam kuingia ndani humo upesi.

"Tesha, iko wapi...." Miryam alikuwa anataka kuuliza swali, lakini akaishia hapo na kubaki akinitazama baada ya kuniona.

Mama wakubwa wakanitazama pia na kisha kumwangalia yeye tena, na ndiyo Shadya akawa ameingia ndani hapo pia kwa kumpita Miryam.

"Naam dada... unasema?" Tesha akamsemesha Miryam.

Lakini Miryam akawa kama ameishiwa pozi, na macho yake yaliyojaa simanzi yakashuka na kukitazama kiganja changu kilichofungwa kwa bendeji.

"Mamu yuko hospitali gani? Inabidi tuwahi kabla mvua haijawa kubwa mno," Shadya akamwambia hivyo Tesha.

"Aaa... sijui hiyo hospitali jina lake... ni pale hivi, hii barabara ya kwenda Kongowe, ukilipita kanisa tu kwa pale mbele," Tesha akawaambia.

"Na wa hapo huwa wanatoa huduma mpaka mida kama hii?" Bi Zawadi akamuuliza.

"Ee, ni masaa 24," Tesha akasema.

"Mlimwachaje Mamu? Kuna sehemu ameumia sana?" Bi Jamila akauliza.

Tesha na mimi tukaangaliana kwa ufupi, kisha akasema, "Tumemwacha anaangaliwa na daktari. Alizimia shauri ya kuishiwa nguvu... alikuwa anaogopa sana. Ila... haja-hajaumia."

"Eh Mungu! Afadhali jamani," Bi Zawadi akasema hivyo.

Nikawa mtulivu tu, vile vile, huku Miryam akiushikilia mlango na uso wake ukielekea chini kwa huzuni.

"Mola ni mwema, Mamu atakuwa sawa. Basi twendeni. Shangazi... nyie mtabaki, si ndiyo?" Shadya akasema hivyo.

"Hapana, na sisi tunataka kuja kumwona Mamu," akasema hivyo Bi Zawadi.

Wakamwangalia Miryam, naye akasema, "Mtamwona tu mama. Ila... sasa hivi saa tisa... mnahitaji kupumzika angalau... mpate nguvu."

"Lakini Mimi..." Bi Zawadi akawa anataka kusisitiza.

"Usijali mama, nyie pumzikeni. Nitakuwa na mama Chande pia. Mkilala mtapata nguvu ili asubuhi mje... hasa wewe mama mkubwa, bado unatumia dawa na unahitaji kulala," Miryam akasema hivyo na kuelekeza maneno hayo ya mwisho kwa Bi Jamila.

Mama zake wakubwa wakaonekana kuridhia.

Shadya akamuuliza Tesha, "Na wewe si unakuja? Au macho yanauma sana bado ubaki?"

"Eeh... nimeambiwa natakiwa kulala... yapumzike ili hizi dawa zifanye kazi. Me nitabaki na mama hapa, nyie wahini... maana tuliwaacha wanamhudumia Mamu na hatujalipia pia... wasije wakaghairi kumsaidia," Tesha akasema hivyo.

"Sawa," Shadya akasema hivyo na kumsogelea Miryam.

"JC baba... unaenda kupumzika, si ndiyo?" Bi Jamila akaniuliza hivyo huku akinishika begani.

Kabla sijatoa jibu, Tesha akasema, "Kaka, si ulikuwa unarudi tena kwa Mamu? Kwa ajili... ya yale mambo muhimu uliyokuwa umeongea na daktari eeh?"

Nikatulia kidogo nikitafakari maneno yake, nami nikatikisa kichwa kukubali.

"Eeh. JC ataenda na nyie," Tesha akamwambia hivyo Miryam.

Nilikuwa simwangalii Miryam moja kwa moja, lakini ningeweza kuona akitikisa kichwa kidogo kuonyesha uelewa na kisha kutazama chini. Hatukutaka kupeana za uso bado.

"Ni sawa JC? Kama unaweza ukawa umechoka sana, au... labda na we' ukapumzike halafu utakuja hospitali asubuhi?" Shadya akanisemesha kwa upole.

Nikamwangalia na kusema, "Hamna. Nitaenda nanyi. Nahitaji kuongea na huyo daktari."

"Sawa," Shadya akasema hivyo.

Kwa sekunde chache, macho yangu na ya Miryam yakawa yamekutana tena, na aliniangalia kama vile anataka kunikwepa lakini kukawa kuna kitu kinamfanya ashindwe, nami nikamkazia macho kwa umakini.

Kisha ndiyo akayashusha yake na kusema, "Twendeni," naye akatangulia kutoka.

Wanawake wengine wakafuata baada yake, nami ndiyo nikamwambia Tesha kuwa nisingeweza kurudi hospitali nikiwa na T-shirt hili lililolowana, kwa hiyo kwa akili yake mwenyewe akawa amenitolea ile jezi yake ya Simba ili kubadili, kisha ningekuja kumrudishia.

Ilikuwa ni kuhisi uzito tu wa kwenda tena kwa Ankia kubadili mavazi kisha ndiyo nije kuwasindikiza wanawake wale, na ijapokuwa nilihisi uchovu, usingizi ulikuwa umenipaa, yaani sikudhani hata kama ingewezekana kuja kulala kabisa. Kwa hiyo nikavaa jezi, kisha ndiyo nikakausha maji yaliyokuwa nyweleni na kuzidhana kiasi, halafu tukatoka pamoja na Tesha kuelekea nje.

Aisee yaani hii sehemu kwa vioja ilikuwa ni hatari, toka nimefika kwa ajili ya likizo, nyumba ya Miryam haikuishiwa mikasa iliyokuwa inalemea sana hisia; si kwangu tu, ila kwa wote waliohusika, na hasa zaidi mwanamke huyo.

Walikuwa wameshafungua geti, naye Miryam akalitoa gari lake mpaka nje, kisha ni mama Chande ndiye ambaye akalifunga geti na kuelekea nje pia. Inaonekana alikuwa hapo kutoa support kubwa sana kwa hii familia maana naye alienda kuingia kwenye gari, kwa hiyo nikawa nasubiriwa mimi pekee.

Nikagonga tu kiganja changu kwenye kiganja chake Tesha kama kumuaga, nami nikawapita mama wakubwa pia na kuwatikisia kichwa kwa kuaga pia. Yaani raha kwa pande zote haikuwepo. Nikatoka na kwenda kwenye gari, nikitarajia kukaa siti za nyuma, lakini nikakuta Shadya na mama Chande wameketi humo, na siti ya mbele pembeni ya dereva ilikuwa wazi; ikiachwa kwa ajili yangu. Dah!

Kulikuwa na unoma fulani hivi wa wazo tu la kukaa pembeni yake Miryam, lakini hakukuwa na namna. Nikaingia, hii ikiwa ni mara ya pili niko ndani ya gari hilo na bibie mwenyewe, sijahesabu kuwa ya tatu maana nimeondoa ile yangu na Tesha wakati wa msiba wa Joy; hii ni kwa mimi na Miryam mwenyewe. Kwa utulivu wa kiume tu nikakaa na kutazama mbele, naye Miryam akaanza kuliendesha gari.

★★

Ulikuwa mwendo uliojaa ukimya mwingi sana, hakuna muziki, hakuna mtu kukohoa wala kuchafya, yaani ni huzuni tele iliyokuwa imelijaza gari hilo. Ningeshusha uso wangu kiasi na kumtazama Miryam kwa macho ya chini, na mwanamke huyo alikuwa makini tu kuendesha gari vizuri bila kuniangalia hata kidogo, lakini macho yake yalijaa hali ya wasiwasi mwingi.

Hakutaka kunitazama kwa sababu alihisi hatia, na kwa sababu ya kuwaza zaidi juu ya hali ya Mariam, niliona kwamba alikuwa akiogopa mno, lakini mbele yetu sote alionyesha kwamba yuko imara.

Nilimwonea huruma. Alikuwa mwanamke mwenye moyo mzuri sana. Moyo wake mzuri uliomsukuma mpaka amsamehe Joshua kwa mabaya yote aliyotenda kwa muda mrefu ili tu aiunganishe familia yake ndiyo kitu kilichokuwa kinamfanya awe imara, kwa hiyo sasa hivi baada ya haya yote kutokea ni wazi kwamba huo uimara ulikuwa umevunjika, na huenda hata hakujua afanye nini tena kwa sababu angehisi ni kama ameshindwa, kwamba hawezi.

Kile kitu ambacho Joshua aliwahi kumwambia kwamba hawezi kwa sababu ya yeye kuwa mwanamke, ndiyo hisia ambayo nadhani Miryam alikuwa akiipitia kwa sasa. Kulikuwa na mambo mengi, kuzungukia suala hilo lote mpaka kufikia kwa Mariam. Angehitaji kuwa imara zaidi kutokea hapo maana ikiwa kama angekata tamaa, hawa ndugu zake wengine wangeumia sana.

Alikuwa mpambanaji mzuri sana huyu mwanamke, lakini kama vile tu nilivyokuwa nimemwambia siku ile kanizabua usoni, si kila kitu alitakiwa kubeba mwenyewe. Kuna wakati angehitaji wengine pia wamsaidie, maana maisha ni kusaidiana hata kama mtu unahisi kwamba utaweza kubeba yote peke yako, bado zipo sehemu tu hata na wewe utahitaji msaada. Miryam alihitaji kufungua moyo wake juu ya hilo na kuacha kuhisi kwamba wengine wakitaka kumsaidia basi atakuwa kama mzigo kwao. Sijui ni kwa nini tu alikuwa anafikiria hivyo.

Yote hayo nilikuwa nayawaza kivyangu tu mpaka tukawa tumefika kwenye ile hospitali tena. Tukashuka, nami nikaona kwamba sasa gari moja la maaskari tuliloliacha hapo muda fulani nyuma halikuwepo, kumaanisha yule Yohana angekuwa ameshatolewa hapo hospitali baada ya kuondolewa kwa risasi yake mguuni. Nikawaongoza wanawake mpaka kufikia kwenye chumba alichokuwa amelazwa Mariam, kukuta binti akiwa amelala, na yule yule muuguzi aliyesema angemwangalia akiwa hapo kweli kutimiza wajibu wake.

Miryam, Shadya, na mama Chande wakakielekea kitanda cha binti na kuanza kumwangalia kwa simanzi, huku mimi nikiwa nawaangalia tu kutokea kwenye mwingilio, naye muuguzi akawafata na kuanza kuongea nao; dada mtu akijitambulisha na wenzake pia na kuuliza hali ya mgonjwa.

Muuguzi akawaambia kwamba aliendelea vizuri sasa na alikuwa ametulia zaidi, ila kwa maelezo mengine ingebidi daktari aje kuwapatia. Akawaacha kwa kusema anaenda kumwita daktari, na ile amefika usawa wangu, nikamwomba twende pamoja, naye akakubali na kunitangulia.

Mdogo mdogo tu tukavuka vyumba kadhaa na kufikia mlango wa ofisi ya daktari, na muuguzi huyu akaomba kuingia ndani humo na kuruhusiwa. Nikafuata nyuma yake, naye ndiyo alikuwa ameanza kumwambia daktari kuwa familia ya yule binti "mweupe" ndiyo ilikuwa imefika pamoja nami kwa hiyo aende ili aongee hasa na dada ya msichana huyo, naye daktari akakubali kwa kutikisa kichwa.

Alikuwa amekaa kitini kwenye meza pana kiasi ya mbao nzito iliyopakwa rangi nyeupe, kukiwa na makablasha kama yote pamoja na laptop, huku mwamba akiandika ripoti fulani bila shaka ya mgonjwa mwingine wa hapo.

Muuguzi akatupisha na kutoka ndani humo kabisa, ndiyo daktari akasimama na kusema, "Amekuja dada yake pamoja na nani?"

"Ndugu zake wengine wawili," nikamwambia hivyo.

"Sawa," akasema hivyo na kuja mpaka niliposimama.

"Vipi, umem... umempima Mariam?" nikamuuliza hivyo.

"Yeah, ilikuwa bahati tu adrenaline iliposhuka akawa amekojoa. Nurse akauwahi mkojo kwa hiyo tukaupima. Sijawahi kuona kiwango cha juu cha adrenaline namna hiyo kama kwa huyo msichana. Yaani ilikuwa kama imesimama sehemu moja tu," akasema hivyo.

"Ila sa'hivi si damu imetulia?"

"Ndiyo. Amelala tu usingizi wa kawaida."

"Okay, kwa hiyo... vipi lile suala?"

"Majibu yanaonyesha yuko safi kabisa," akasema hivyo.

Nikatulia kidogo, kisha nikauliza, "Nini?"

"Sidhani kama huyu msichana amebakwa," akaniambia hivyo.

Nikafuta mdomo jasho lisilokuwepo hata kidogo!

"Hakuna shida yaani. Hana infection wala ugonjwa wowote ambao tunaweza kusema ulikuwepo tayari, maana tumepima mpaka mimba na kuangalia kama anaweza akawa na hepatitis B, lakini hana," akaeleza.

Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Kwa hiyo... ngoja, vipi kuhusu secretion? Umempima?"

"Yeah, hilo pia," akanijibu hivyo.

"Na penyewe?"

"Yuko clean," akasema.

"Kabisa? Yaani... hakuna sign yoyote ya trichomonal vaginitis, au... labda bacterial...."

"Hamna... hana. Yuko safi kaka," akasema hivyo.

Ah! Kuna kaahueni fulani hivi kalipita moyoni baada ya kujua hayo, lakini nilielewa kwamba ilikuwa mapema bado kufikiri kila kitu kiko sawa.

Nikasema, "Aisee! Yaani doctor nilikuwa nimechoka... hali tuliyomkuta nayo, yaani... huyo jamaa aliyepigwa risasi alikuwa ameshamtolea nguo zote, kamweka kitandani, yaani Mariam alikuwa ndani ya horrific moment, nikadhani..."

"Basi inawezekana huyo jamaa alikuwa kwenye harakati ya kutaka kumbaka huyo binti ndiyo nyie mkawa mmefika na kumwokoa, sidhani sana kama alikuwa ameshamwingia. Sema... kama mtataka kuwa sure zaidi, basi akiamka vizuri mmpeleke kwenye hospital yenye vifaa bora zaidi. Mpeleke hata Muhimbili ukamwangalie. Ila sidhani sana kama mtakuta tatizo lolote, labda tu...."

"Yale ambayo yatafuata. Ndiyo, najua. Ah... natumaini tu kusiwe na tatizo lolote kabisa, yaani hakuna binti yeyote anayastahili mambo kama haya hata kidogo. Asante sana kwa kila kitu kaka," nikamwambia hivyo.

Akanishika begani kirafiki na kusema, "Usijali. Twende huko nikawaondolee hofu na hao wengine."

Nikamwambia, "Ona... nakuomba jambo moja. Usi... yaani waelezee tu kwamba hali ya Mariam iko sawa kwa sasa, lakini ishu ya rape uiongelee na dada yake tu. Haitokuwa vizuri sana ikisikika na kwa wengine maana..."

"Porojo zisizo kweli zinaweza kusambaa kuhusu huyo binti, eh?" akauliza hivyo.

"Ndiyo. Sitaki hiyo itokee. Nailinda dignity yake," nikamwambia kwa sauti tulivu.

"Usijali, naelewa. Unafanya vizuri. Twende," akasema hivyo.

Basi, baada ya hapo tukaondoka ofisini kwake na kwenda mpaka kwa Mariam tena, nikiwa nimemuuliza daktari kuhusiana na gharama za matibabu ya binti Mariam toka amefika hapo, naye alikuwa ameniambia kwamba kila kitu kiliorodheshwa ndani ya faili dogo maalumu kwa ajili ya Mariam, na ni yule muuguzi ndiye aliyekuwa nalo.

Kwa hiyo daktari alipokuwa amewafikia wakina Miryam na kuanza kuongea nao, mimi nikamwita muuguzi huyo na kumwomba aambatane nami mpaka sehemu ambayo ningeweza kutoa malipo kwa ajili ya binti, naye akaongozana nami.

Sijui ni kwa nini tu, lakini wakati huu sikujihisi amani hata ya kusogea kidogo karibu na kitanda cha Mariam na kumwangalia huyo binti. Sababu ya karibu zaidi kuifikiria ilikuwa tu kwamba labda yale niliyoyaona yakimpata msichana huyo ndiyo yalisababisha hali hii, lakini zaidi ni kuwa bado nilikuwa nikihisi hatia moyoni. Hivyo nilipokuwa tu nimemaliza kulipia gharama yote kwa kutumia kadi yangu ya benki, nikamwambia muuguzi awaambie wanawake wale kwamba niliondoka, naye akakubali.

Niliamua kujiondokea tu kutoka hospitalini hapo, mwenyewe, ili hatimaye niweze kwenda na kutulia nikiwa peke yangu baada ya yote yaliyokuwa yametokea. Tena nikisema kutulia namaanisha nilitaka tu kwenda kwa Ankia na kujitupia kitandani, nifumbe macho, nilale, basi. Nilikuwa nimechoka. Sana. Nikaita tu bodaboda aliyekuwa karibu na hapo, wale wasiolala wale wachapakazi kweli, mpaka saa kumi! Nikapanda, huyoo nikaanza kurudi pande zetu za mapumziko, nikiwa na karaha tele rohoni mwangu.


★★★


Nimekuja kuamka asubuhi ikiwa bado mapema kweli, na kilichoniamsha ilikuwa ni mwito wa simu yangu iliyokuwa inapiga kelele bila kukoma. Agh! Nilikuwa nahisi kichwa kinavutwa shauri ya macho kuwa mazito mno, wenge la usingizi likiwa kali sana, na hiyo hali iliniambia kuwa sikuwa nimelala kwa masaa hata kupita matatu.

Nikaichukua simu na kukuta mpigaji ni madam Bertha, nami nikalegea kitandani hapo na kufumba macho kwanza; nikiwa nashusha pumzi mbili tatu kwanza. Nikawa nakumbukia tu namna ambavyo nilifika hapa ile usiku na moja kwa moja kuja kitandani na kulala, na sikujali mbu wala joto, yaani nilifika tu na kufumba macho, na sasa hivi tena nikawa nimekatishiwa pumziko langu na huyo mwanamke.

Simu ikaacha kuita, kisha ikaanza tena. Najua jana madam alikuwa amenitafuta lakini kutokana na jinsi hali zilivyokuwa, sikuweza kumjibu. Sasa hapa bila shaka alikuwa anataka kuniwashia moto. Nikafumbua macho yangu yaliyojaa ukungu na kuipokea, kisha nikaweka sikioni.

"Madam..." nikasema hivyo kivivu.

"Wewe... unataka kunifanya me mtoto mdogo, eti?" Bertha akasikika upande wa pili.

"Hamnaa... nimetingwa... kuna ishu ilitoke...."

"Sitaki uniambie upuuzi! Ni hivi, nataka ufike hotelini upesi! Mimi napanga mambo ya maana halafu wewe unaleta mchezo, unajua gharama nayotoa?" akafoka.

"Siyo hivyo... ona, nakuja. Kulikuwa na dharura tu ndiyo maana nikawa..."

"Sijali. Fika hotelini haraka. Ikipita saa sita haujafika hapa..."

"Haitapita madam. Nakuja sasa hivi," nikamwambia hivyo kwa uhakika.

Nikasikia akisonya kwa hasira, kisha ndiyo akakata simu.

Nikaitoa yangu sikioni na kuangalia muda. Saa mbili. Uchovu wa usingizi niliokuwa nahisi, kujumuisha na maneno ya ukali ya huyo mwanamke, vikawa vimeiamsha tena hasira fulani ndani yangu hasa kutokana na kumbukumbu za mambo ya usiku uliotangulia kunirudia.

Sikutaka kuendelea kukumbukia yale ambayo macho yangu yaliona kwa sababu ubongo wangu ndiyo ulikuwa unayaleta hayo hayo, kwa hiyo nikaona bora nijilazimishe kunyanyuka dakika hii hii ili niende tu huko Royal Village kupokea mabango zaidi kutoka kwa madam, na ili anipe mambo mengine ya kushughulikia ili akili yangu iwe kwingine. Ndiyo jambo nililotaka zaidi kwa wakati huu.

Kwa hiyo nikaufungua mkono wangu ile bendeji, nikaivua jezi ya Tesha na suruali, kisha nikaenda kupiga usafi wa mwili na kurudi kuvaa nguo safi; T-shirt langu jeupe la mikono mifupi na suruali ya jeans ya samawati, pamoja na zile ndala mpya miguuni, na nikajifunga kwa bendeji tena kiganjani mpaka sehemu ya mwanzo ya mkono. Ningekuja kumrudishia Tesha jezi yake baadaye endapo kama singekwenda kutafunwa na madam huko hotelini.

Sikutaka akili yangu ichanganywe kwa lolote lile yaani, sikutaka hata kuanza kutafuta mtu yeyote sijui niulize Mariam anaendelea vizuri au la, hapana. Nilitaka tu hii siku iwe ya mambo mengine kwanza, hayo mengine najua ningeyakuta tu.

Nikatoka na kufunga, huyoo mdogo mdogo nikaanza kutembea kuelekea upande wa Masai na kupapita kwa kufata njia ambayo ingenifikisha lami; ikiwa ni saa tatu sasa. Ardhi ilikuwa na hali mbichi shauri ya mvua iliyonyesha usiku, lakini jua liliwaka kwa ukali wa kadiri ya asubuhi.

Watu wenye shughuli za asubuhi ndiyo walioonekana hapa na pale wakiendelea na biashara zao, nami nikaendelea na mwendo tu mpaka nilipofikia eneo la ile shule ya nursery ambalo ndiyo likafanya nikumbuke tena kwamba Tesha aliniambia yeye na mdogo wake walitekwa wakiwa hapo.

Kwa hiyo nikataka kupapita haraka tu, huku bado kichwa kikiwa kinavuta kwa mbali, na ndipo kukawa na muungurumo wa gari kutokea nyuma yangu. Sikugeuka kuliangalia kwa sababu nilitembea pembeni kwa kuacha nafasi katikati ya barabara iliyotosha kuliruhusu lipite bila shida, lakini nilipohisi limenikaribia tu, honi ikapigwa kidogo. Nikageuka na kuliangalia.

Ilikuwa ni gari aina ya Toyota Prado, kubwa na nyeupe, ikija taratibu kiasi kuonyesha kwamba honi hiyo ilipigwa ili nisimame. Kwa hiyo nikasimama, na ile limefika karibu nami mpaka usawa wa mlango wake wa mbele, nikawa sasa nimemwona aliyeendesha, na nilimtambua. Ilikuwa ni yule mwanamke "sugar mommy" niliyekutana naye Masai na kuunganishwa kwake kupitia Bobo, yaani Rukia.

Alionekana kuwa makini kweli kwa asubuhi hii, akiwa amevalia kiofisi zaidi. Alivaa shati la kike la satini nyekundu pamoja na sketi yenye kubana ya rangi ya maziwa, ikionekana kufikia tumboni kiasi kwa kulichomekea shati hilo kwa ndani. Alivaa miwani pana kiasi yenye kuonyesha macho yake, na wigi la nywele fupi lililoshonewa kwenye nywele zake kichwani, lipstick nyekundu midomoni, saa ya rangi ya dhahabu mkononi, na mkufu mwembamba shingoni ulioonekana kupitia uwazi mdogo wa kifungo cha juu kilichokuwa wazi.

Nikawa namtazama kwa umakini.

Akasema, "Za asubuhi?"

"Safi," nikamjibu hivyo.

"Unaenda wapi?"

"Naingia Makumbusho mara moja," nikamwambia hivyo.

"Ooh... unaenda kuchukua daladala?" akauliza.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Panda basi nikusogeze hapo mbele," akasema hivyo.

Sikutaka kuzunguka. Nikafungua mlango wa hilo gari na kupanda, nikikaa pembeni yake sugar mommy, kisha ndiyo akaendelea kuendesha taratibu kuielekea lami.

"Umeumia mkononi, au?" Rukia akauliza hivyo.

"Ee, kidogo. Nilijikata na chupa," nikamwambia tu hivyo.

"Pole. Makumbusho kuna nini sasa?" akaniuliza.

Nikiwa nimeegamiza tu kichwa kwenye siti, nikamwambia, "Nimeitwa na boss wangu."

"Kazi gani unafanya?"

"Madawa," nikamjibu.

"Ahaa... pharmacy?" akauliza.

"Yeah," nikajibu hivyo.

Yaani pharmacy ya madawa ya kulevya!

Akauliza, "Mbona mbali sana? Ina maana unatoka kila siku Mbagala mpaka Makumbusho kwa ajili ya kazi na kurudi?"

"Mbagala siyo makazi ya jumla. Nimekuja tu kutembelea... ila me siyo wa huku."

"Unaonekana kama umechoka. Ulichelewa kulala nini?"

"Yeah. Mambo mengi."

"Mambo mengi eh? Ndiyo maana hadi ukani-ditch ule usiku?" akauliza hivyo.

Nikabaki kimya tu nikitazama mbele.

"Mbona haujibu? Ile siku ulienda wapi? Nikakutafuta lakini hata simu zangu hupokei..."

"Nilipatwa na dharura. Sikutarajia. Ndiyo maana nikakwambia mambo yalikuwa mengi, yaani sijapata hata muda kuijali simu," nikasema hivyo.

"Mmm... sawa."

Nikamtazama usoni kivivu, nikiona alivyokuwa na kautulivu fulani hivi kazuri, nami nikamwambia, "Najua ulijisikia vibaya, lakini sikufanya makusudi. Ilikuwa nje ya uwezo wangu."

"Sawa, haina shida. Una mambo mengi. Imeeleweka," akasema hivyo.

Nikarudi kutazama pembeni.

"Mke wako upo naye huku au... umemwacha huko ulikotoka?" akaniuliza.

"Sina mke. Na... nakuomba tusiongelee hayo. Niambie. Unaenda wapi sa'hivi?" nikamuuliza.

"Kazini," akajibu.

"Umependeza. Una uhakika hutaki tupite sehemu fulani kwanza tupige quickie halafu ndiyo uingie kazini?" nikamuuliza hivyo kiutani.

Akacheka kidogo na kusema, "Nitachelewa."

Nikatazama pembeni tena na kumwambia, "Haina shida, nakutania tu. Tutapangana hata baadaye... ukiwa free, nikiwa free, nitafute."

Nikawa namwona kwa jicho pana namna ambavyo aliniangalia mara kwa mara kama vile anatafakari kitu fulani, hivyo nami nikamtazama.

"Vipi?" nikamuuliza.

Akaibana midomo yake kwanza, kisha akasema, "Nilikuwa nafikiria sehemu nzuri ya kwenda... pamoja nawe."

"Sasa hivi?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Si umesema utachelewa?"

"Sijachelewa sana. Hata hivyo, me ndiyo boss," akaniambia.

Nikaangalia mbele, tukiwa lami sasa na mwendoni kuifikia Rangi Tatu. Niliposema kuhusu kwenda kupiga mechi fupi pamoja naye nilikuwa najaribu kumtania tu ili ile hisia ya kujisikia vibaya imwondoke, lakini nadhani akawa ameyachukulia maneno yangu kwa ufikirio halisi. Labda nilikuwa nimemfanya atamani jambo hilo haraka, kwa kuwa ndiyo kitu alichokuwa analilia tokea mara ya kwanza tumekutana.

"Ama we' ndiyo utachelewa?" akaniuliza hivyo kwa sauti yenye matumaini.

Nikamwangalia na kusema, "Sawa. Twende sehemu nzuri tucheze kidogo. Tutapanga mengine baadaye."

Akaonekana kufurahi kwa jinsi alivyotabasamu kiasi, nami nikalishika shavu lake na kulisugua kidogo kwa kidole changu ili aone fahari, kisha akaendelea kuweka umakini kwenye uendeshaji. Hisia zangu zilikuwa kwenye hali ya kukosa raha bado, hivyo nilitaka kufanya jambo hilo na huyu mwanamke ili niulazimishe tu mwili wangu upate raha hata kama roho yangu isingepata furaha.

★★

Kwa hiyo Rukia akaendelea kuendesha mpaka pande za Mbagala Complex, na huko akawa ametufikisha kwenye hoteli moja pana yenye ghorofa sita, na mimi bila kujali ni wapi ama panaitwaje, nikaambatana na mwanamke huyu mpaka ndani na kufanikiwa kupata chumba kwenye ghorofa ya pili. Alilipia yeye mwenyewe.

Kilikuwa safi, kitanda kipana cha sita/sita chenye mashuka meupe, kabati la nguo pembeni, bafu na choo humo humo ndani, na hata TV iliyokuwemo ilikuwa kubwa. Yaani ile tumeingia tu, sikutaka kukaa kupiga story kwanza, nikamshika mwanamke huyo mtu mzima kutokea nyuma kwa njia fulani kama nimeikaba shingo yake, naye akaudondosha mkoba aliokuwa ameushikilia.

Kuna kitu alichokuwa anataka kunisemesha lakini sikujali, nikaanza tu kulitandika makofi kalio lake nene na yeye akawa anaguna kwa sauti ya chini. Alikuwa amevaa viatu vya kuchuchumia vyenye rangi nyeupe, kwa hiyo ilikuwa kama vile tumelingana urefu, nami nikaanza kuivuta sketi yake kwa pande za mapaja mpaka kufikia kiunoni, na hapo nikalifichua tako lake nene lililofunikwa kwa kiasi na nguo ya ndani nyekundu aliyokuwa amevaa.

Nikaivuta kuelekea juu, nayo ikajiingiza katikati ya mstari uliotenganisha mashavu makubwa ya mlima wake. Alikuwa na ule weupe uliofifia, na kalio lake lilikuwa na mikunjo iliyolifanya liwe laini na zito, nami nikaendelea kulitembezea makofi kushoto na kulia huku nikilifinya kwa nguvu na viganja vyangu.

Sasa alikuwa ameinama na kuweka mikono yake kitandani baada ya mimi kuiachia shingo yake, hivyo nikafungua suruali yangu na kuutoa msuli uliokuwa umeshawamba wima tayari. Hii ndiyo maana ya "quickie," hakuna cha tomasa wala nini, yaani mtu unakuwa unaenda na muda.

Kwa hiyo nikaisogeza nguo yake ya ndani pembeni ya kalio lake na kuanza kujaribu kuiingiza mtambo yangu kwenye chombo cha mawasiliano, lakini kukawa na ugumu kiasi. Nilitarajia ingeingia tu kwa urahisi lakini pamoja na kuwa na umri mkubwa, kito cha Rukia kilikuwa kimebana sana. Mpaka nikashangaa. Nikatia bidii kumwingizia, wapi, akawa anasogea tu mbele kama kuonyesha anaumia, kisha ndiyo akaamua kugeuka na kukaa kitandani. Akaishika mashine yangu, nami nikamsogelea karibu zaidi, kisha akaiingiza mdomoni na kuanza kuinyonya. Ah!

Alikuwa na midomo minene, kwa hiyo ilitunika vizuri aliponinyonya namna hiyo na kujaribu kuizamisha mpaka kooni kabisa. Nikamuuliza ikiwa labda alikuwa anatumia dawa kuubana sana uke wake, naye ndiyo akaacha kuninyonya na kusema ndiyo, ila pia hakuwa amekutana na mwanaume kwa muda mrefu sasa.

Nikamwambia sawa, kisha nikamsaidia kumtolea shati lake ili lisije kujikunja sana, akibaki na sidiria nyekundu pia iliyoyafunika matiti yake makubwa. Akavua saa na cheni yake pia. Usawa wa kiuno chake baada ya kuilegeza zipu ya sketi aliyokuwa amevaa, niliweza kuona shanga kama nne za urembo kukizungukia, ikionyesha alikuwa mwanamke aliyependa sana mitindo mbalimbali ya kupagawisha mwanaume kimahaba, ndiyo nikainyanyua miguu yake juu na yeye akaegamia viwiko vyake na mgongo kitandani hapo.

(.........).

(.........).

(.........).

Nilipochoka mkao huo, nikamgeuza, naye akalalia tumbo huku miguu yake ikikanyaga chini, ndiyo zamu hii nikamwingia bila kuhangaika. Aisee! Nililitandika hilo kalio! Piga haswa, haraka-haraka yaani, nalo likawa linarukaruka tu huku mwanamke huyu akiguna kwa raha. Alikuwa na tabia ya kutaka sana kugeuka nyuma ili aniangalie, kwa hiyo nikakikandamiza kichwa chake kitandani huku nikiendelea kumpa vyake tu.

Alikuwa ameshanifanya nitamani tu kuendelea, kwa hiyo nikampandisha kitandani kwa usawa huo huo na kumlaza kwa ubavu, miguu yake ikibanana pamoja, kisha nikamwingia tena na kuendelea na show. Miwani yake ilikuwa imepinda usoni, akiniangalia kwa macho mazito huku akitoa miguno kwa kukaza meno yake, nami ndiyo nikawa nimehisi kuchoka zaidi na kusitisha kumkuna, kisha nikajilaza pembeni yake kuitafuta pumzi kwanza.

Yeye alipoona hivyo, akaishika mashine yangu iliyokuwa imesimama bado na kuanza kuinyonya kwa bidii, kwa ufundi, nami nikahisi nguvu mpya iliyofanya nisimame kwa unamba moja. Alikuwa amejaa mate mdomoni, akionekana kutaka raha zaidi, naye akaitoa miwani yake machoni na kujivuta kuja kwa juu yangu.

Nilihofia uzito wake maana alikuwa na mwili, siyo kama wa Shishi baby au Wellu Sengo lakini, ila hakukuwa na noma sana baada ya yeye kuukalia msumari na kuanza kupigiza kalio lake hapo kwa mwendo wa taratibu. Akaweka mikono yake kitandani pande za mabega yangu, uso wake ukiwa juu ya wangu, naye akaendelea kujisugua huku akitoa miguno kwa pumzi.

(..........).

(..........).

(..........).

(..........).

Nikaendelea kumtandika tu bila kuacha, ndipo akaanza kuvuta shuka kwa mikono huku akitaka kutoka juu yangu, lakini nikamkaza hivyo hivyo ili asikimbie. Kiuno chake kikapanda juu kwa mshtuko mpaka mashine yangu ikamtoka, nami nikawa nahisi maji yenye moto yakinimwagikia kama vile yanapulizwa, na Rukia akawa anatoa miguno huku akishtuka-shtuka mwilini, kisha akatulia hatimaye.

Mimi pia nikawa nimetulia, nikihisi kabisa kwamba nilikuwa karibu kumwaga raha zangu pia lakini zikawa zimekomea kibofuni. Rukia alikuwa amelaza kichwa chake pembeni na shingo yangu, akipumua kwa uchovu, nami nikamwambia, "Tunyanyuke. Nahisi saa limekata."

Akanyanyua uso wake na kunitazama, naye akasema, "Una haraka, eti?"

"Ndiyo. Hata wewe najua unahitajika huko mapema... nimesikia simu yako inaita mara tatu hapo," nikamwambia hivyo.

Akaweka kiganja chake kwenye nywele zangu na kusema, "Leo Jumamosi, siko tight kivile. Naweza kuahirisha kwenda kama ukitaka tubaki."

"Hapana, ni muhimu niondoke. Na nahisi nitachelewa na usafiri ila... leo ni lazima. Tutakutana tu hata baadaye," nikamwambia hivyo.

Bado nilionyesha kutokuwa na raha sana ijapokuwa nilikuwa nimemfurahisha yeye kupita maelezo, nami nikaashiria kutaka kunyanyuka, hivyo akasogea pembeni kuniruhusu nitoke chini yake

"Una maji mengi," nikamwambia hivyo.

Akatabasamu kiasi na kusema, "Umenipagawisha sana. We' ni mzuri... halafu unajua."

"Hata wewe. Ngoja nikajimwagie faster," nikamwambia hivyo na kutoka kitandani.

Fyuu bafuni, fyaa chumbani tena.

Nilikuwa najitahidi kukimbizana na muda maana tayari ilikuwa imeshafika saa nne na nusu, na kutoka huku mpaka huko kwa madam Bertha kwa misukosuko ya barabarani, niliomba tu isiwe kuchelewa sana. Nikawa nimejikausha maji, nikachana nywele vizuri, kisha nikaanza kuvaa nguo zangu tena, huku Rukia akiwa bado kitandani na sasa akiongea na simu yake.

Nilipokuwa nimemaliza kuvaa T-shirt langu, akawa ameachana na simu yake na kuniuliza, "Si tungeondoka wote?"

"Ingekuwa fresh, ila nimechelewa sana. Kuna ishu ya muhimu leo. Boss ata-mind hata kama nikisema kuna jam, kwa hiyo acha tu niwahi," nikamwambia hivyo.

"Unapanda daladala na mwendokasi, au?"

"Kutokea huku? Napanda boda mpaka pa kuchukulia daladala ndo' nielekee huko. Mwendokasi mpaka Kariakoo huko... sifiki."

"Kama utaweza, chukua boda au Bajaj ikupeleke huko moja kwa moja, usishindane na mikwaruzo ya daladala," akaniambia hivyo.

Nikamwangalia tu usoni baada ya yeye kuniambia hivyo, naye akasogea upande wangu na kuuokota mkoba wake, kisha akatoa pesa kutoka humo. Noti za elfu kumi kumi, akahesabu kidogo, kisha akanipatia. Nikazipokea huku nikizitazama kimaswali kiasi. Ni kwamba alikuwa ananilipa, au?

"Hii ya nini?" nikamuuliza hivyo, akiwa amesimama mbele yangu huku kavaa taulo iliyoufunika mwili wake kutokea kifuani mpaka usawa wa mapaja.

"Nauli. Utaenda, halafu baadaye nikiwa free nitakuita uje sehemu nyingine," akaniambia hivyo kwa sauti tulivu.

"Nauli? Elfu themanini? Kumbe una hela chafu eh?"

"Ahahah... hiyo ni ndogo mbona?"

"Wacha!" nikasema hivyo huku nikimwangalia kwa umakini.

Akatabasamu huku ameibana midomo yake.

"Sikia. Nahitaji kuongea hili ili tuelewane mapema, sawa? Usije kufikiri labda me ni... escort, au mdoli wa kulipwa kwa huduma. Siko hivyo Rukia," nikamwambia.

"Kweli eh? Basi ni vizuri. Me sina shida. Nimekuelewa sana toka muda... hata kama una videmu vingi tayari, me shida yangu ni penzi lako tu," akaongea kwa uhakika.

"Umeona nini kwangu kwani ambacho mumeo hana?" nikamuuliza hivyo.

"Ni hivyo tu. Nimekuelewa wewe. Mume wangu ni mtu wa safari mno, na najua hata yeye ana vipoza roho huko anakoendaga. Me nimekupendea tu pigo zako. Una pigo nzuri sana... na nataka nikupe matunzo mazuri wasiyojua kukupa hao videmu wengine," akasema hivyo na kung'ata mdomo wake wa chini.

"Una maringo!" nikamwambia.

Akacheka kidogo kwa pumzi na kuendelea kunitazama huku ameachama na kuulambisha ulimi wake gegoni. Yaani mapenzi njoo utamu kolea! Dah!

Nikamuuliza, "Una miaka mingapi?"

Akajibu, "Arobaini na tano. Wewe?"

"Ishirini na nane," nikamwambia.

"Ndiyo maana una nguvu. Uko kwenye peak... unanifanya najisikia kama denti," akaniambia hivyo kwa madaha.

Nikiwa naendelea tu kumtazama, akasogea karibu zaidi na kupitisha mikono yake mabegani kwangu, akielekea usoni ili aweze kunibusu mdomoni, nami nikamruhusu aanze kufanya hivyo. Nilikuwa makini sana, nikizipokea busu zake huku nikilishikilia kalio lake lililokuwa wazi ndani ya taulo kwa viganja vyangu, naye akaacha kunibusu hivyo na kunitazama machoni.

"Baadaye tukutane, eti mpenzi?" akaniuliza hivyo kwa deko.

Mm?

Nikamwambia, "Usijali. Nikiwa free, sitakuangusha. Kikubwa mawasiliano."

"Sawa," akasema hivyo.

Nilipenda tu namna alivyokuwa na kautulivu fulani hivi kalikofanya hali nzima ijae amani, nami nikamwacha hapo hatimaye na kuondoka zangu ili niwahi kufika kwa "madam kipiri" kabla sijarushiwa sumu yake pakiwa bado mapema.

★★

Mwendo wa kufikia saa zima na dakika chache ukawa umenifikisha maeneo ya Makumbusho, na moja kwa moja nikamwelekeza dereva wa bajaji mpaka kufikia kwenye hoteli ya Royal Village. Ndiyo, niliamua kuchukua bajaji binafsi mpaka huku ili niweze kuwahi baada ya kuachana na sugar mommy Rukia, na tulikuwa tumewasiliana wakati niko mwendoni na yeye kunisifia kwa mahaba niliyompa, akisema ana hamu sana ya kuja kuniona tena maana hakutegemea kwenda kazini asubuhi hii akiwa amechangamka namna hiyo.

Pamoja na kuwa suala hilo la Rukia liliegamia kwenye upande fulani mzuri wenye kusisimua, bado tu sikuwa nimeipata amani ya rohoni, yaani furaha sikuwa nayo hata chembe. Lakini ili kumridhisha, nikamwambia tu nilifurahi sana pia kuwa naye asubuhi hiyo, na kumsifia kwamba alikuwa mtamu sana. Kuonana baadaye lingekuwa suala la kuangalia na hali kama zingeruhusu, na hapo ndiyo tukawa tumeagana mpaka baadaye.

Yaani ile nimefika tu hotelini, saa sita ilikuwa imebakiza dakika nane tu kuingia. Kwa hiyo nikawahi kule ndani upesi sana mpaka kufikia kwenye mlango wa chumba chake madam, kisha nikagonga hodi na kusubiri. Vuup, kikadi kikapitishwa, na mlango ukafunguka.

Hapo mbele yangu alikuwa amesimama madam Bertha mwenyewe, akiwa amevaa T-shirt laini la mikono mirefu na cheni ya dhahabu shingoni, suruali ya skinny jeans nyeusi miguuni na viatu vyeupe vya kijanja. Mwonekano wake uliniambia kwamba alikuwa anataka kutoka, kama siyo ndiyo alikuwa amerudi kutoka sehemu, na kichwani bado nywele zake zilikuwa fupi kwa kupakwa dawa, ila sasa alikuwa amezichanganya na rangi ya maziwa kiasi upande wa juu. Kwa ule usistaduu wa kishua yaani.

Alinitazama kwa njia fulani kama vile anataka kunimeza, nami nikiwa namtazama kwa macho yenye uchovu nikalazimisha tabasamu kiasi na kunyanyua simu yangu kumwonyesha muda kwenye kioo.

"Sita juu ya alama! Sijachelewa, nastahili tuzo," nikaanza kumsemesha kwa njia ya utani.

Akatulia kidogo akiiangalia simu yangu, kisha akasema, "Umechelewa. Ni saa sita na dakika moja."

"Ah... umesubiri iingie dakika moja hapa ndiyo useme 'umechelewa.' Acha ujanja madam," nikamwambia hivyo.

"Umeanza kunichukulia kama mtani wako, eti?" akaniuliza hivyo kwa sauti makini.

Niliona wazi kwamba hakuwa kwenye mood ya utani, kama mimi tu, hivyo nikaweka umakini wangu pia na kumwambia, "I'm sorry. Hizi siku mbili zimekuwa nzito madam... I... got distracted."

Akanitazama usoni kwa umakini, kisha akaachia uwazi zaidi mlangoni ili niingie.

Nikapita mpaka ndani ya chumba hicho na kusimama usawa wa sofa upande mwingine, naye akafunga mlango na kuja mpaka karibu nami.

"Acha kuchanganywa na habari za familia wakati ambao biashara zimeanza kutembea mdogo wangu. Utapoteza ulichokipambania," akaniambia hivyo kwa mkazo.

Nikatikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Usifikiri kila simu nitakayokupigia inamaanisha nataka sex tu. Kuna watu wengi sana wa kunipa hicho kitu na sina muda nao. Nikikuvutia waya, pokea. Next time ukizingua nikapigwa joto la kupoteza madili yangu, nakuapia eh... nitahakikisha wewe ndiyo linakuivisha mpaka unakauka. Ushanisoma?" akaongea kwa hisia kali.

"Mwanzo, mwisho," nikamwambia hivyo.

Akavuta ulimi mdomoni mwake kutoa kero, kisha akasema, "Unajua kuna watu nilikuwa nimewapanga, uje uwaonyeshe unavyotengeneza madini ili wanipe access ya mahala secure na vifaa bora ili ishu yetu ianze kazi, na hiyo ilikuwa ni jana, Festus alikuwepo pia... lakini ukapotea tu sijui ukaamua kwenda wapi, nakupigia hupokei, ukafikiri nini, nawashwa sana au?"

Nilielewa alikuwa amekasirika mno, kwa hiyo nikamsogelea karibu zaidi na kumwambia, "Madam... nisamehe. Haitatokea tena, nime... nimekuangusha zamu hii, lakini... nakuahidi haitatokea tena. Kuanzia sasa hivi nitafuata unachotaka, nitakuwa popote ulipo ukinihitaji, maana hili dili nalihitaji sana. Sitakuangusha... jana kulikuwa na dharura tu, lakini haijalishi tena. Haitajirudia. I'm sorry."

Nilimwongelesha kwa njia ya kubembeleza sana, kisha nikaishika shingo yake taratibu huku mkono mwingine nikiuweka kiunoni kwake.

Akawa ananiangalia kwa njia ya kuudhika bado, naye akatazama pembeni na kusema, "Ole wako ije kujirudia. Sitakuelewa tena."

"I promise," nikamwambia hivyo kiuhakika.

Akanitazama usoni kiudadisi na kuuliza, "Mbona macho yako mazito hivyo? Ulikuwa wapi jana?"

Nikarudi nyuma kiasi na kusema, "Unakumbuka juzi... nilipigiwa simu hapa nikakwambia..."

"Eeh, uliitwa na shangazi yako... Mamu kafanyaje huko sijui... ndiyo ikawaje?" akanikatisha kwa kuuliza hivyo.

"Huyo binti alikuwa ametekwa," nikamwambia hivyo.

Akakunja uso kimaswali kiasi.

"Walimteka, kwa hiyo tukaanza kumtafuta. Ndiyo tumempata jana usiku... alikuwa karibu kuuliwa... ila sasa hivi yuko hospitali anaendelea vizuri. Sijalala vya kutosha shauri ya hiyo ishu," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

"Walikuwa wamemteka huyo msichana kwa nini? Ni wakina nani?"

"Ni kaka yake tu mjingammoja. Anataka mali aliyorithishwa huyo msichana, kwa hiyo ndiyo ulikuwa mpango wake... amuue ili aipate," nikamwambia.

"Yaani kaka yake... ndugu yenu kabisa? Yeye yuko wapi?" akauliza.

"Mapolisi wamemkamata," nikamwambia.

"Hiyo ni story ya kweli, au umeitunga tu?" akaniuliza hivyo.

"Kwa nini nikudanganye? Huyu binti ni kama mdogo wangu. Isingekuwa ya hivyo ningekuwa nimekuja kwako. Huku ni muhimu, ila... tunaowapenda ni muhimu pia unajua," nikamwambia hivyo kwa upole.

Akanisogelea na kunishika begani, kisha akasema, "Ndiyo, najua. Ila ukiendelea kuweka familia mbele, mbele, mbele tu... hizo distraction hazitapotea. Sasa hivi nataka twende tour, nikuonyeshe network yetu, halafu wewe una kichwa kizito shauri ya usingizi. Faida gani? Baadaye tukienda kwenye meeting na wenzetu kuongelea masuala muhimu ukasikia shangazi, sijui Mamu kapata presha huko, ukimbilie kwake tena? Tell me if I'm just wasting my time fucking with you boy..."

"Hapana madam. Nimekwambia kuanzia sasa hivi, hivi vitu havitanichanganya tena. I'm all yours. Popote unapotaka twende, twende. Kichwa changu kipo active... hakuna shida," nikamwambia hivyo.

"Well, me nataka kuanzia sasa kiwe active kwenye hili game kwa asilimia mia. No setbacks, sijui familia bullshit... sitaki. Nahitaji uwe sambamba na mimi," akaniambia hivyo kwa mkazo.

Nikamshika kiunoni na kusema, "Okay. Niambie cha kufanya."

"Uje ukae hapa," akasema hivyo.

Nikatulia kidogo nikitafakari maneno hayo.

"Njoo hapa tukae wote. Ndiyo utakuwa karibu nami, utafata chochote nitakachokuelekeza na kutimiza kwa uharaka, na hautavurugwa na maisha ya kuruka-ruka kama uliyonayo huko Mbagala. Umenielewa?" akasema hivyo kwa umakini.

Nikatazama chini kwa kutafakari zaidi. Alikuwa akinipa ofa ya kuja kuishi hapa hotelini pamoja naye, ili tufanye alichotaka nikiwa karibu zaidi. Hii ingekuwa njia nzuri sana ya kuweza kumharibu mwanamke huyu, yaani kuishi na adui kwa ukaribu kabisa ili kujua siri zake na kutoa taarifa muhimu za mambo yaliyoendelea kwa askari Ramadhan.

Lakini hii ingemaanisha kwamba nilipaswa kuondoka Mbagala na kumwacha Mariam akiwa bado hajapona vilivyo, tena hasa baada ya matatizo yaliyokuwa yamempata, huenda hata hali yake ndiyo ingenihitaji zaidi. Kulikuwa na kitu ambacho kilitokeza kama malaika wawili, mmoja mweupe, mwingine mweusi; huyo mweupe akinishauri nisifanye jambo ambalo madam Bertha alilitaka ili niweze kuendelea kumsaidia Mariam, na huyo mweusi akishauri 'agh, achana na Mariam bana!' Kwani nalipwa kumsaidia? Si nije tu kukaa kwa huyu kibibi ili nilipize kisasi changu kitamu?

Nikawa nimekwama katikati ya fikira tofauti za maamuzi ambayo kichwa changu na moyo wangu vilitaka niyachukue. Ningefanya nini?




★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Back
Top Bottom