MIMI NA MIMI
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Mvua ikaanza kuongezeka kiasi, Miryam bado akiwa amekaa chini huku wapendwa wake wakiendelea kumpa faraja, na ndiyo Tesha akawa ameenda hapo ili kuweza kumsaidia dada yake asimame. Nilikuwa nimesimama tu usawa wa kibaraza nikiwaangalia wote walipofanikiwa kumshawishi Miryam asimame ili waweze kwenda ndani kupanga mambo ya kufanya, naye Shadya akawa anashughulika na majirani waliokuwa wameingia ndani ya geti pia; akiwaomba waende makwao na kupumzika.
Bi Jamila na mama Chande wakawa wamemshikilia Miryam kumpa mkono alipoanza kutembea kuelekea ndani, na sasa alionekana kujikaza zaidi ili asiendelee kulia. Tesha akawa amekuja kwangu tena na kunishauri tuelekee kwenye bomba la hapo nje ili kujisafisha mikono, nami nikakubali na kwenda pamoja naye.
Mzee Hamadi, yule mwenyekiti, pamoja na wale wanawake wawili niliowakuta hapo wakawa wameondoka pia baada ya kuongea kwa ufupi na Bi Zawadi, na mwanamke huyo akaja pamoja na Shadya kufikia karibu na sehemu yenye bomba nilipokuwa nanawa.
Nilikuwa nimenawa usoni na kichwani, na sasa niliweka tu kiganja changu cha mkono wa kulia kipigwe na maji mengi kuiondoa damu, naye Tesha akachuchumaa karibu nacho na kuanza kukiangalia. Aliweza kuona kwamba kilikuwa kimevimba na sehemu nyingi ya damu iliyotoka ilikuwa yangu pia shauri ya kuchanwa na kipande cha kile chombo cha udongo nilichokipasulia kwenye mwili wa Joshua, hivyo akashauri twende ndani ili wanipake dawa tuitayo "spirit" na waufunge mkono kwa bendeji laini.
Niliposimama na kuwatazama Bi Zawadi na Shadya, nilikuta wakiniangalia kwa njia mpya iliyojaa huzuni nyingi sana, wakishindwa kunisemesha, na mimi nikishindwa kutoa neno lolote lile. Ni wazi kwamba hawakuwahi kutarajia kuja kuniona nikitenda kama vile nilivyokuwa nimemtendea Joshua, na mimi kwa wakati huu sikujihisi amani hata kuwatazama maana nilihofia labda hata wangeanza kuniogopa.
Lakini haikuwa hivyo. Bi Zawadi mwenyewe akaja na kunishika mkononi, na bila kusema lolote akaanza kuniongoza kwenda ndani ili wakanipatie msaada niliohitaji. Nikawa mtulivu tu, tukaingia sebuleni, nikaenda na Tesha mpaka chumbani kwake, na nafikiri Miryam na Bi Jamila walikuwa chumbani kwake kule ili kuchukua vitu alivyohitaji halafu ndiyo waelekee hospitali, kwa kuwa mama Chande alikuwa jikoni akionekana kuweka vifaa fulani kwenye mfuko, na Shadya akajiunga naye.
Nikiwa chumbani na Tesha, rafiki yangu huyu akawa ananiambia jinsi ambavyo kumpiga Joshua kama vile nilivyokuwa nimefanya ilikuwa kitu alichotamani mno kukifanya pia kwa muda mrefu sana, na akanipa sifa kuwa lilikuwa jambo sahihi kabisa.
Nilisimama tu huku nikimtazama jamaa bila kuhisi ahueni yoyote pamoja na yote, na ndiyo Bi Zawadi akawa amekuja na kisanduku chenye vifaa vya huduma ya kwanza na kutoa pamba, dawa, na bendeji, kisha tukakaa kitandani kwa Tesha naye akaanza kunichua kiganjani kwa spirit akitumia pamba. Iliuma, lakini sikujali.
Bi Zawadi alikuwa akiongea pamoja Tesha kwa hisia sana kuelekea suala zima la Joshua na Khadija, akisema alivunjika sana moyo, na aliumia mno kumwona Miryam akiteseka wakati dada wa watu alikuwa akijitahidi sana, sana, sana kuiunganisha hii familia. Tesha alionyesha kumwelewa dada yake pia, lakini akasema kwamba hilo ndiyo lingekuwa fundisho kwa Miryam kutokuwa na moyo mwepesi mno wa kuamini mtu kwa sababu tu ya kuwa ndugu, na alijua dada yake alijutia mno.
Nilikuwa nawasikiliza tu bila kusema lolote, naye Bi Zawadi akawa amemaliza kunifungia bendeji kiganjani na kisha kuishika mikono yangu kwa pamoja. Akanishukuru sana kwa kuwa msaada mkubwa kwao na kuniomba radhi pia kutokana na matatizo ya familia yake kusababisha na mimi niumie kama hivi nilivyokuwa nikiumia rohoni.
Akawa anasema ameona ni jinsi gani ambavyo nilimjali sana Mariam mpaka kukasirika namna ile na kukaribia hata kumng'oa kichwa Joshua, nami nikaendelea kumtazama tu kwa utulivu, nikiwa bado sijanena lolote lile kwa sababu ya kukosa amani moyoni.
Bi Zawadi alipokuwa amesimama ili arudishe kisanduku cha huduma ya kwanza chumbani kwake, Bi Jamila akawa ameingia pia, hivyo nami nikasimama na kumwangalia. Mwanamke huyo akaweka kiganja chake usawa wa mdomo huku akiniangalia kwa macho yenye huzuni sana, kisha akanisogelea na kunishika pande za mikononi.
"JC baba... uko sawa?" akaniuliza hivyo kwa kujali.
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Ehh! Pole sana mwanangu, kwa kila kitu. Naelewa kwa nini ulikuwa umekasirika sana baba, na kwa hilo nikuombe tu msamaha kwa kweli... hukustahili haya yote. Ila hayo nakuomba tuyaweke pembeni kwa wakati huu. Nashukuru sana kwa kuwasaidia watoto wetu. Wewe umekuwa baraka kubwa sana kwetu. Bila wewe yaani... sijui tu... nini kingewapata vijana wetu..." Bi Jamila akaongea kwa hisia.
Aliposema anaelewa kwa nini nilikuwa nimekasirika sana, nikawa nimetambua kuwa alijua sababu iliyofanya mpaka siku ile nikakorofishana na Miryam na mwanamke huyo kunipiga kibao, ikionyesha kwamba huenda Miryam alikuwa ameshamwambia yeye na labda hata Bi Zawadi pia, hivyo kwa njia fulani hapa ni kama alikuwa anaomba radhi kwa niaba ya Miryam.
"Hapana mama... usiseme hivyo, hamjanikosea kwa lolote kwa hiyo ondoa maneno ya kuomba msamaha. Na ni Mungu tu ndiyo mkubwa, amesaidi..." nikawa nimeanza kuongea hatimaye, lakini nikakatisha maneno yangu baada ya Miryam kuingia ndani humo upesi.
"Tesha, iko wapi...." Miryam alikuwa anataka kuuliza swali, lakini akaishia hapo na kubaki akinitazama baada ya kuniona.
Mama wakubwa wakanitazama pia na kisha kumwangalia yeye tena, na ndiyo Shadya akawa ameingia ndani hapo pia kwa kumpita Miryam.
"Naam dada... unasema?" Tesha akamsemesha Miryam.
Lakini Miryam akawa kama ameishiwa pozi, na macho yake yaliyojaa simanzi yakashuka na kukitazama kiganja changu kilichofungwa kwa bendeji.
"Mamu yuko hospitali gani? Inabidi tuwahi kabla mvua haijawa kubwa mno," Shadya akamwambia hivyo Tesha.
"Aaa... sijui hiyo hospitali jina lake... ni pale hivi, hii barabara ya kwenda Kongowe, ukilipita kanisa tu kwa pale mbele," Tesha akawaambia.
"Na wa hapo huwa wanatoa huduma mpaka mida kama hii?" Bi Zawadi akamuuliza.
"Ee, ni masaa 24," Tesha akasema.
"Mlimwachaje Mamu? Kuna sehemu ameumia sana?" Bi Jamila akauliza.
Tesha na mimi tukaangaliana kwa ufupi, kisha akasema, "Tumemwacha anaangaliwa na daktari. Alizimia shauri ya kuishiwa nguvu... alikuwa anaogopa sana. Ila... haja-hajaumia."
"Eh Mungu! Afadhali jamani," Bi Zawadi akasema hivyo.
Nikawa mtulivu tu, vile vile, huku Miryam akiushikilia mlango na uso wake ukielekea chini kwa huzuni.
"Mola ni mwema, Mamu atakuwa sawa. Basi twendeni. Shangazi... nyie mtabaki, si ndiyo?" Shadya akasema hivyo.
"Hapana, na sisi tunataka kuja kumwona Mamu," akasema hivyo Bi Zawadi.
Wakamwangalia Miryam, naye akasema, "Mtamwona tu mama. Ila... sasa hivi saa tisa... mnahitaji kupumzika angalau... mpate nguvu."
"Lakini Mimi..." Bi Zawadi akawa anataka kusisitiza.
"Usijali mama, nyie pumzikeni. Nitakuwa na mama Chande pia. Mkilala mtapata nguvu ili asubuhi mje... hasa wewe mama mkubwa, bado unatumia dawa na unahitaji kulala," Miryam akasema hivyo na kuelekeza maneno hayo ya mwisho kwa Bi Jamila.
Mama zake wakubwa wakaonekana kuridhia.
Shadya akamuuliza Tesha, "Na wewe si unakuja? Au macho yanauma sana bado ubaki?"
"Eeh... nimeambiwa natakiwa kulala... yapumzike ili hizi dawa zifanye kazi. Me nitabaki na mama hapa, nyie wahini... maana tuliwaacha wanamhudumia Mamu na hatujalipia pia... wasije wakaghairi kumsaidia," Tesha akasema hivyo.
"Sawa," Shadya akasema hivyo na kumsogelea Miryam.
"JC baba... unaenda kupumzika, si ndiyo?" Bi Jamila akaniuliza hivyo huku akinishika begani.
Kabla sijatoa jibu, Tesha akasema, "Kaka, si ulikuwa unarudi tena kwa Mamu? Kwa ajili... ya yale mambo muhimu uliyokuwa umeongea na daktari eeh?"
Nikatulia kidogo nikitafakari maneno yake, nami nikatikisa kichwa kukubali.
"Eeh. JC ataenda na nyie," Tesha akamwambia hivyo Miryam.
Nilikuwa simwangalii Miryam moja kwa moja, lakini ningeweza kuona akitikisa kichwa kidogo kuonyesha uelewa na kisha kutazama chini. Hatukutaka kupeana za uso bado.
"Ni sawa JC? Kama unaweza ukawa umechoka sana, au... labda na we' ukapumzike halafu utakuja hospitali asubuhi?" Shadya akanisemesha kwa upole.
Nikamwangalia na kusema, "Hamna. Nitaenda nanyi. Nahitaji kuongea na huyo daktari."
"Sawa," Shadya akasema hivyo.
Kwa sekunde chache, macho yangu na ya Miryam yakawa yamekutana tena, na aliniangalia kama vile anataka kunikwepa lakini kukawa kuna kitu kinamfanya ashindwe, nami nikamkazia macho kwa umakini.
Kisha ndiyo akayashusha yake na kusema, "Twendeni," naye akatangulia kutoka.
Wanawake wengine wakafuata baada yake, nami ndiyo nikamwambia Tesha kuwa nisingeweza kurudi hospitali nikiwa na T-shirt hili lililolowana, kwa hiyo kwa akili yake mwenyewe akawa amenitolea ile jezi yake ya Simba ili kubadili, kisha ningekuja kumrudishia.
Ilikuwa ni kuhisi uzito tu wa kwenda tena kwa Ankia kubadili mavazi kisha ndiyo nije kuwasindikiza wanawake wale, na ijapokuwa nilihisi uchovu, usingizi ulikuwa umenipaa, yaani sikudhani hata kama ingewezekana kuja kulala kabisa. Kwa hiyo nikavaa jezi, kisha ndiyo nikakausha maji yaliyokuwa nyweleni na kuzidhana kiasi, halafu tukatoka pamoja na Tesha kuelekea nje.
Aisee yaani hii sehemu kwa vioja ilikuwa ni hatari, toka nimefika kwa ajili ya likizo, nyumba ya Miryam haikuishiwa mikasa iliyokuwa inalemea sana hisia; si kwangu tu, ila kwa wote waliohusika, na hasa zaidi mwanamke huyo.
Walikuwa wameshafungua geti, naye Miryam akalitoa gari lake mpaka nje, kisha ni mama Chande ndiye ambaye akalifunga geti na kuelekea nje pia. Inaonekana alikuwa hapo kutoa support kubwa sana kwa hii familia maana naye alienda kuingia kwenye gari, kwa hiyo nikawa nasubiriwa mimi pekee.
Nikagonga tu kiganja changu kwenye kiganja chake Tesha kama kumuaga, nami nikawapita mama wakubwa pia na kuwatikisia kichwa kwa kuaga pia. Yaani raha kwa pande zote haikuwepo. Nikatoka na kwenda kwenye gari, nikitarajia kukaa siti za nyuma, lakini nikakuta Shadya na mama Chande wameketi humo, na siti ya mbele pembeni ya dereva ilikuwa wazi; ikiachwa kwa ajili yangu. Dah!
Kulikuwa na unoma fulani hivi wa wazo tu la kukaa pembeni yake Miryam, lakini hakukuwa na namna. Nikaingia, hii ikiwa ni mara ya pili niko ndani ya gari hilo na bibie mwenyewe, sijahesabu kuwa ya tatu maana nimeondoa ile yangu na Tesha wakati wa msiba wa Joy; hii ni kwa mimi na Miryam mwenyewe. Kwa utulivu wa kiume tu nikakaa na kutazama mbele, naye Miryam akaanza kuliendesha gari.
★★
Ulikuwa mwendo uliojaa ukimya mwingi sana, hakuna muziki, hakuna mtu kukohoa wala kuchafya, yaani ni huzuni tele iliyokuwa imelijaza gari hilo. Ningeshusha uso wangu kiasi na kumtazama Miryam kwa macho ya chini, na mwanamke huyo alikuwa makini tu kuendesha gari vizuri bila kuniangalia hata kidogo, lakini macho yake yalijaa hali ya wasiwasi mwingi.
Hakutaka kunitazama kwa sababu alihisi hatia, na kwa sababu ya kuwaza zaidi juu ya hali ya Mariam, niliona kwamba alikuwa akiogopa mno, lakini mbele yetu sote alionyesha kwamba yuko imara.
Nilimwonea huruma. Alikuwa mwanamke mwenye moyo mzuri sana. Moyo wake mzuri uliomsukuma mpaka amsamehe Joshua kwa mabaya yote aliyotenda kwa muda mrefu ili tu aiunganishe familia yake ndiyo kitu kilichokuwa kinamfanya awe imara, kwa hiyo sasa hivi baada ya haya yote kutokea ni wazi kwamba huo uimara ulikuwa umevunjika, na huenda hata hakujua afanye nini tena kwa sababu angehisi ni kama ameshindwa, kwamba hawezi.
Kile kitu ambacho Joshua aliwahi kumwambia kwamba hawezi kwa sababu ya yeye kuwa mwanamke, ndiyo hisia ambayo nadhani Miryam alikuwa akiipitia kwa sasa. Kulikuwa na mambo mengi, kuzungukia suala hilo lote mpaka kufikia kwa Mariam. Angehitaji kuwa imara zaidi kutokea hapo maana ikiwa kama angekata tamaa, hawa ndugu zake wengine wangeumia sana.
Alikuwa mpambanaji mzuri sana huyu mwanamke, lakini kama vile tu nilivyokuwa nimemwambia siku ile kanizabua usoni, si kila kitu alitakiwa kubeba mwenyewe. Kuna wakati angehitaji wengine pia wamsaidie, maana maisha ni kusaidiana hata kama mtu unahisi kwamba utaweza kubeba yote peke yako, bado zipo sehemu tu hata na wewe utahitaji msaada. Miryam alihitaji kufungua moyo wake juu ya hilo na kuacha kuhisi kwamba wengine wakitaka kumsaidia basi atakuwa kama mzigo kwao. Sijui ni kwa nini tu alikuwa anafikiria hivyo.
Yote hayo nilikuwa nayawaza kivyangu tu mpaka tukawa tumefika kwenye ile hospitali tena. Tukashuka, nami nikaona kwamba sasa gari moja la maaskari tuliloliacha hapo muda fulani nyuma halikuwepo, kumaanisha yule Yohana angekuwa ameshatolewa hapo hospitali baada ya kuondolewa kwa risasi yake mguuni. Nikawaongoza wanawake mpaka kufikia kwenye chumba alichokuwa amelazwa Mariam, kukuta binti akiwa amelala, na yule yule muuguzi aliyesema angemwangalia akiwa hapo kweli kutimiza wajibu wake.
Miryam, Shadya, na mama Chande wakakielekea kitanda cha binti na kuanza kumwangalia kwa simanzi, huku mimi nikiwa nawaangalia tu kutokea kwenye mwingilio, naye muuguzi akawafata na kuanza kuongea nao; dada mtu akijitambulisha na wenzake pia na kuuliza hali ya mgonjwa.
Muuguzi akawaambia kwamba aliendelea vizuri sasa na alikuwa ametulia zaidi, ila kwa maelezo mengine ingebidi daktari aje kuwapatia. Akawaacha kwa kusema anaenda kumwita daktari, na ile amefika usawa wangu, nikamwomba twende pamoja, naye akakubali na kunitangulia.
Mdogo mdogo tu tukavuka vyumba kadhaa na kufikia mlango wa ofisi ya daktari, na muuguzi huyu akaomba kuingia ndani humo na kuruhusiwa. Nikafuata nyuma yake, naye ndiyo alikuwa ameanza kumwambia daktari kuwa familia ya yule binti "mweupe" ndiyo ilikuwa imefika pamoja nami kwa hiyo aende ili aongee hasa na dada ya msichana huyo, naye daktari akakubali kwa kutikisa kichwa.
Alikuwa amekaa kitini kwenye meza pana kiasi ya mbao nzito iliyopakwa rangi nyeupe, kukiwa na makablasha kama yote pamoja na laptop, huku mwamba akiandika ripoti fulani bila shaka ya mgonjwa mwingine wa hapo.
Muuguzi akatupisha na kutoka ndani humo kabisa, ndiyo daktari akasimama na kusema, "Amekuja dada yake pamoja na nani?"
"Ndugu zake wengine wawili," nikamwambia hivyo.
"Sawa," akasema hivyo na kuja mpaka niliposimama.
"Vipi, umem... umempima Mariam?" nikamuuliza hivyo.
"Yeah, ilikuwa bahati tu adrenaline iliposhuka akawa amekojoa. Nurse akauwahi mkojo kwa hiyo tukaupima. Sijawahi kuona kiwango cha juu cha adrenaline namna hiyo kama kwa huyo msichana. Yaani ilikuwa kama imesimama sehemu moja tu," akasema hivyo.
"Ila sa'hivi si damu imetulia?"
"Ndiyo. Amelala tu usingizi wa kawaida."
"Okay, kwa hiyo... vipi lile suala?"
"Majibu yanaonyesha yuko safi kabisa," akasema hivyo.
Nikatulia kidogo, kisha nikauliza, "Nini?"
"Sidhani kama huyu msichana amebakwa," akaniambia hivyo.
Nikafuta mdomo jasho lisilokuwepo hata kidogo!
"Hakuna shida yaani. Hana infection wala ugonjwa wowote ambao tunaweza kusema ulikuwepo tayari, maana tumepima mpaka mimba na kuangalia kama anaweza akawa na hepatitis B, lakini hana," akaeleza.
Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Kwa hiyo... ngoja, vipi kuhusu secretion? Umempima?"
"Yeah, hilo pia," akanijibu hivyo.
"Na penyewe?"
"Yuko clean," akasema.
"Kabisa? Yaani... hakuna sign yoyote ya trichomonal vaginitis, au... labda bacterial...."
"Hamna... hana. Yuko safi kaka," akasema hivyo.
Ah! Kuna kaahueni fulani hivi kalipita moyoni baada ya kujua hayo, lakini nilielewa kwamba ilikuwa mapema bado kufikiri kila kitu kiko sawa.
Nikasema, "Aisee! Yaani doctor nilikuwa nimechoka... hali tuliyomkuta nayo, yaani... huyo jamaa aliyepigwa risasi alikuwa ameshamtolea nguo zote, kamweka kitandani, yaani Mariam alikuwa ndani ya horrific moment, nikadhani..."
"Basi inawezekana huyo jamaa alikuwa kwenye harakati ya kutaka kumbaka huyo binti ndiyo nyie mkawa mmefika na kumwokoa, sidhani sana kama alikuwa ameshamwingia. Sema... kama mtataka kuwa sure zaidi, basi akiamka vizuri mmpeleke kwenye hospital yenye vifaa bora zaidi. Mpeleke hata Muhimbili ukamwangalie. Ila sidhani sana kama mtakuta tatizo lolote, labda tu...."
"Yale ambayo yatafuata. Ndiyo, najua. Ah... natumaini tu kusiwe na tatizo lolote kabisa, yaani hakuna binti yeyote anayastahili mambo kama haya hata kidogo. Asante sana kwa kila kitu kaka," nikamwambia hivyo.
Akanishika begani kirafiki na kusema, "Usijali. Twende huko nikawaondolee hofu na hao wengine."
Nikamwambia, "Ona... nakuomba jambo moja. Usi... yaani waelezee tu kwamba hali ya Mariam iko sawa kwa sasa, lakini ishu ya rape uiongelee na dada yake tu. Haitokuwa vizuri sana ikisikika na kwa wengine maana..."
"Porojo zisizo kweli zinaweza kusambaa kuhusu huyo binti, eh?" akauliza hivyo.
"Ndiyo. Sitaki hiyo itokee. Nailinda dignity yake," nikamwambia kwa sauti tulivu.
"Usijali, naelewa. Unafanya vizuri. Twende," akasema hivyo.
Basi, baada ya hapo tukaondoka ofisini kwake na kwenda mpaka kwa Mariam tena, nikiwa nimemuuliza daktari kuhusiana na gharama za matibabu ya binti Mariam toka amefika hapo, naye alikuwa ameniambia kwamba kila kitu kiliorodheshwa ndani ya faili dogo maalumu kwa ajili ya Mariam, na ni yule muuguzi ndiye aliyekuwa nalo.
Kwa hiyo daktari alipokuwa amewafikia wakina Miryam na kuanza kuongea nao, mimi nikamwita muuguzi huyo na kumwomba aambatane nami mpaka sehemu ambayo ningeweza kutoa malipo kwa ajili ya binti, naye akaongozana nami.
Sijui ni kwa nini tu, lakini wakati huu sikujihisi amani hata ya kusogea kidogo karibu na kitanda cha Mariam na kumwangalia huyo binti. Sababu ya karibu zaidi kuifikiria ilikuwa tu kwamba labda yale niliyoyaona yakimpata msichana huyo ndiyo yalisababisha hali hii, lakini zaidi ni kuwa bado nilikuwa nikihisi hatia moyoni. Hivyo nilipokuwa tu nimemaliza kulipia gharama yote kwa kutumia kadi yangu ya benki, nikamwambia muuguzi awaambie wanawake wale kwamba niliondoka, naye akakubali.
Niliamua kujiondokea tu kutoka hospitalini hapo, mwenyewe, ili hatimaye niweze kwenda na kutulia nikiwa peke yangu baada ya yote yaliyokuwa yametokea. Tena nikisema kutulia namaanisha nilitaka tu kwenda kwa Ankia na kujitupia kitandani, nifumbe macho, nilale, basi. Nilikuwa nimechoka. Sana. Nikaita tu bodaboda aliyekuwa karibu na hapo, wale wasiolala wale wachapakazi kweli, mpaka saa kumi! Nikapanda, huyoo nikaanza kurudi pande zetu za mapumziko, nikiwa na karaha tele rohoni mwangu.
★★★
Nimekuja kuamka asubuhi ikiwa bado mapema kweli, na kilichoniamsha ilikuwa ni mwito wa simu yangu iliyokuwa inapiga kelele bila kukoma. Agh! Nilikuwa nahisi kichwa kinavutwa shauri ya macho kuwa mazito mno, wenge la usingizi likiwa kali sana, na hiyo hali iliniambia kuwa sikuwa nimelala kwa masaa hata kupita matatu.
Nikaichukua simu na kukuta mpigaji ni madam Bertha, nami nikalegea kitandani hapo na kufumba macho kwanza; nikiwa nashusha pumzi mbili tatu kwanza. Nikawa nakumbukia tu namna ambavyo nilifika hapa ile usiku na moja kwa moja kuja kitandani na kulala, na sikujali mbu wala joto, yaani nilifika tu na kufumba macho, na sasa hivi tena nikawa nimekatishiwa pumziko langu na huyo mwanamke.
Simu ikaacha kuita, kisha ikaanza tena. Najua jana madam alikuwa amenitafuta lakini kutokana na jinsi hali zilivyokuwa, sikuweza kumjibu. Sasa hapa bila shaka alikuwa anataka kuniwashia moto. Nikafumbua macho yangu yaliyojaa ukungu na kuipokea, kisha nikaweka sikioni.
"Madam..." nikasema hivyo kivivu.
"Wewe... unataka kunifanya me mtoto mdogo, eti?" Bertha akasikika upande wa pili.
"Hamnaa... nimetingwa... kuna ishu ilitoke...."
"Sitaki uniambie upuuzi! Ni hivi, nataka ufike hotelini upesi! Mimi napanga mambo ya maana halafu wewe unaleta mchezo, unajua gharama nayotoa?" akafoka.
"Siyo hivyo... ona, nakuja. Kulikuwa na dharura tu ndiyo maana nikawa..."
"Sijali. Fika hotelini haraka. Ikipita saa sita haujafika hapa..."
"Haitapita madam. Nakuja sasa hivi," nikamwambia hivyo kwa uhakika.
Nikasikia akisonya kwa hasira, kisha ndiyo akakata simu.
Nikaitoa yangu sikioni na kuangalia muda. Saa mbili. Uchovu wa usingizi niliokuwa nahisi, kujumuisha na maneno ya ukali ya huyo mwanamke, vikawa vimeiamsha tena hasira fulani ndani yangu hasa kutokana na kumbukumbu za mambo ya usiku uliotangulia kunirudia.
Sikutaka kuendelea kukumbukia yale ambayo macho yangu yaliona kwa sababu ubongo wangu ndiyo ulikuwa unayaleta hayo hayo, kwa hiyo nikaona bora nijilazimishe kunyanyuka dakika hii hii ili niende tu huko Royal Village kupokea mabango zaidi kutoka kwa madam, na ili anipe mambo mengine ya kushughulikia ili akili yangu iwe kwingine. Ndiyo jambo nililotaka zaidi kwa wakati huu.
Kwa hiyo nikaufungua mkono wangu ile bendeji, nikaivua jezi ya Tesha na suruali, kisha nikaenda kupiga usafi wa mwili na kurudi kuvaa nguo safi; T-shirt langu jeupe la mikono mifupi na suruali ya jeans ya samawati, pamoja na zile ndala mpya miguuni, na nikajifunga kwa bendeji tena kiganjani mpaka sehemu ya mwanzo ya mkono. Ningekuja kumrudishia Tesha jezi yake baadaye endapo kama singekwenda kutafunwa na madam huko hotelini.
Sikutaka akili yangu ichanganywe kwa lolote lile yaani, sikutaka hata kuanza kutafuta mtu yeyote sijui niulize Mariam anaendelea vizuri au la, hapana. Nilitaka tu hii siku iwe ya mambo mengine kwanza, hayo mengine najua ningeyakuta tu.
Nikatoka na kufunga, huyoo mdogo mdogo nikaanza kutembea kuelekea upande wa Masai na kupapita kwa kufata njia ambayo ingenifikisha lami; ikiwa ni saa tatu sasa. Ardhi ilikuwa na hali mbichi shauri ya mvua iliyonyesha usiku, lakini jua liliwaka kwa ukali wa kadiri ya asubuhi.
Watu wenye shughuli za asubuhi ndiyo walioonekana hapa na pale wakiendelea na biashara zao, nami nikaendelea na mwendo tu mpaka nilipofikia eneo la ile shule ya nursery ambalo ndiyo likafanya nikumbuke tena kwamba Tesha aliniambia yeye na mdogo wake walitekwa wakiwa hapo.
Kwa hiyo nikataka kupapita haraka tu, huku bado kichwa kikiwa kinavuta kwa mbali, na ndipo kukawa na muungurumo wa gari kutokea nyuma yangu. Sikugeuka kuliangalia kwa sababu nilitembea pembeni kwa kuacha nafasi katikati ya barabara iliyotosha kuliruhusu lipite bila shida, lakini nilipohisi limenikaribia tu, honi ikapigwa kidogo. Nikageuka na kuliangalia.
Ilikuwa ni gari aina ya Toyota Prado, kubwa na nyeupe, ikija taratibu kiasi kuonyesha kwamba honi hiyo ilipigwa ili nisimame. Kwa hiyo nikasimama, na ile limefika karibu nami mpaka usawa wa mlango wake wa mbele, nikawa sasa nimemwona aliyeendesha, na nilimtambua. Ilikuwa ni yule mwanamke "sugar mommy" niliyekutana naye Masai na kuunganishwa kwake kupitia Bobo, yaani Rukia.
Alionekana kuwa makini kweli kwa asubuhi hii, akiwa amevalia kiofisi zaidi. Alivaa shati la kike la satini nyekundu pamoja na sketi yenye kubana ya rangi ya maziwa, ikionekana kufikia tumboni kiasi kwa kulichomekea shati hilo kwa ndani. Alivaa miwani pana kiasi yenye kuonyesha macho yake, na wigi la nywele fupi lililoshonewa kwenye nywele zake kichwani, lipstick nyekundu midomoni, saa ya rangi ya dhahabu mkononi, na mkufu mwembamba shingoni ulioonekana kupitia uwazi mdogo wa kifungo cha juu kilichokuwa wazi.
Nikawa namtazama kwa umakini.
Akasema, "Za asubuhi?"
"Safi," nikamjibu hivyo.
"Unaenda wapi?"
"Naingia Makumbusho mara moja," nikamwambia hivyo.
"Ooh... unaenda kuchukua daladala?" akauliza.
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Panda basi nikusogeze hapo mbele," akasema hivyo.
Sikutaka kuzunguka. Nikafungua mlango wa hilo gari na kupanda, nikikaa pembeni yake sugar mommy, kisha ndiyo akaendelea kuendesha taratibu kuielekea lami.
"Umeumia mkononi, au?" Rukia akauliza hivyo.
"Ee, kidogo. Nilijikata na chupa," nikamwambia tu hivyo.
"Pole. Makumbusho kuna nini sasa?" akaniuliza.
Nikiwa nimeegamiza tu kichwa kwenye siti, nikamwambia, "Nimeitwa na boss wangu."
"Kazi gani unafanya?"
"Madawa," nikamjibu.
"Ahaa... pharmacy?" akauliza.
"Yeah," nikajibu hivyo.
Yaani pharmacy ya madawa ya kulevya!
Akauliza, "Mbona mbali sana? Ina maana unatoka kila siku Mbagala mpaka Makumbusho kwa ajili ya kazi na kurudi?"
"Mbagala siyo makazi ya jumla. Nimekuja tu kutembelea... ila me siyo wa huku."
"Unaonekana kama umechoka. Ulichelewa kulala nini?"
"Yeah. Mambo mengi."
"Mambo mengi eh? Ndiyo maana hadi ukani-ditch ule usiku?" akauliza hivyo.
Nikabaki kimya tu nikitazama mbele.
"Mbona haujibu? Ile siku ulienda wapi? Nikakutafuta lakini hata simu zangu hupokei..."
"Nilipatwa na dharura. Sikutarajia. Ndiyo maana nikakwambia mambo yalikuwa mengi, yaani sijapata hata muda kuijali simu," nikasema hivyo.
"Mmm... sawa."
Nikamtazama usoni kivivu, nikiona alivyokuwa na kautulivu fulani hivi kazuri, nami nikamwambia, "Najua ulijisikia vibaya, lakini sikufanya makusudi. Ilikuwa nje ya uwezo wangu."
"Sawa, haina shida. Una mambo mengi. Imeeleweka," akasema hivyo.
Nikarudi kutazama pembeni.
"Mke wako upo naye huku au... umemwacha huko ulikotoka?" akaniuliza.
"Sina mke. Na... nakuomba tusiongelee hayo. Niambie. Unaenda wapi sa'hivi?" nikamuuliza.
"Kazini," akajibu.
"Umependeza. Una uhakika hutaki tupite sehemu fulani kwanza tupige quickie halafu ndiyo uingie kazini?" nikamuuliza hivyo kiutani.
Akacheka kidogo na kusema, "Nitachelewa."
Nikatazama pembeni tena na kumwambia, "Haina shida, nakutania tu. Tutapangana hata baadaye... ukiwa free, nikiwa free, nitafute."
Nikawa namwona kwa jicho pana namna ambavyo aliniangalia mara kwa mara kama vile anatafakari kitu fulani, hivyo nami nikamtazama.
"Vipi?" nikamuuliza.
Akaibana midomo yake kwanza, kisha akasema, "Nilikuwa nafikiria sehemu nzuri ya kwenda... pamoja nawe."
"Sasa hivi?"
Akatikisa kichwa kukubali.
"Si umesema utachelewa?"
"Sijachelewa sana. Hata hivyo, me ndiyo boss," akaniambia.
Nikaangalia mbele, tukiwa lami sasa na mwendoni kuifikia Rangi Tatu. Niliposema kuhusu kwenda kupiga mechi fupi pamoja naye nilikuwa najaribu kumtania tu ili ile hisia ya kujisikia vibaya imwondoke, lakini nadhani akawa ameyachukulia maneno yangu kwa ufikirio halisi. Labda nilikuwa nimemfanya atamani jambo hilo haraka, kwa kuwa ndiyo kitu alichokuwa analilia tokea mara ya kwanza tumekutana.
"Ama we' ndiyo utachelewa?" akaniuliza hivyo kwa sauti yenye matumaini.
Nikamwangalia na kusema, "Sawa. Twende sehemu nzuri tucheze kidogo. Tutapanga mengine baadaye."
Akaonekana kufurahi kwa jinsi alivyotabasamu kiasi, nami nikalishika shavu lake na kulisugua kidogo kwa kidole changu ili aone fahari, kisha akaendelea kuweka umakini kwenye uendeshaji. Hisia zangu zilikuwa kwenye hali ya kukosa raha bado, hivyo nilitaka kufanya jambo hilo na huyu mwanamke ili niulazimishe tu mwili wangu upate raha hata kama roho yangu isingepata furaha.
★★
Kwa hiyo Rukia akaendelea kuendesha mpaka pande za Mbagala Complex, na huko akawa ametufikisha kwenye hoteli moja pana yenye ghorofa sita, na mimi bila kujali ni wapi ama panaitwaje, nikaambatana na mwanamke huyu mpaka ndani na kufanikiwa kupata chumba kwenye ghorofa ya pili. Alilipia yeye mwenyewe.
Kilikuwa safi, kitanda kipana cha sita/sita chenye mashuka meupe, kabati la nguo pembeni, bafu na choo humo humo ndani, na hata TV iliyokuwemo ilikuwa kubwa. Yaani ile tumeingia tu, sikutaka kukaa kupiga story kwanza, nikamshika mwanamke huyo mtu mzima kutokea nyuma kwa njia fulani kama nimeikaba shingo yake, naye akaudondosha mkoba aliokuwa ameushikilia.
Kuna kitu alichokuwa anataka kunisemesha lakini sikujali, nikaanza tu kulitandika makofi kalio lake nene na yeye akawa anaguna kwa sauti ya chini. Alikuwa amevaa viatu vya kuchuchumia vyenye rangi nyeupe, kwa hiyo ilikuwa kama vile tumelingana urefu, nami nikaanza kuivuta sketi yake kwa pande za mapaja mpaka kufikia kiunoni, na hapo nikalifichua tako lake nene lililofunikwa kwa kiasi na nguo ya ndani nyekundu aliyokuwa amevaa.
Nikaivuta kuelekea juu, nayo ikajiingiza katikati ya mstari uliotenganisha mashavu makubwa ya mlima wake. Alikuwa na ule weupe uliofifia, na kalio lake lilikuwa na mikunjo iliyolifanya liwe laini na zito, nami nikaendelea kulitembezea makofi kushoto na kulia huku nikilifinya kwa nguvu na viganja vyangu.
Sasa alikuwa ameinama na kuweka mikono yake kitandani baada ya mimi kuiachia shingo yake, hivyo nikafungua suruali yangu na kuutoa msuli uliokuwa umeshawamba wima tayari. Hii ndiyo maana ya "quickie," hakuna cha tomasa wala nini, yaani mtu unakuwa unaenda na muda.
Kwa hiyo nikaisogeza nguo yake ya ndani pembeni ya kalio lake na kuanza kujaribu kuiingiza mtambo yangu kwenye chombo cha mawasiliano, lakini kukawa na ugumu kiasi. Nilitarajia ingeingia tu kwa urahisi lakini pamoja na kuwa na umri mkubwa, kito cha Rukia kilikuwa kimebana sana. Mpaka nikashangaa. Nikatia bidii kumwingizia, wapi, akawa anasogea tu mbele kama kuonyesha anaumia, kisha ndiyo akaamua kugeuka na kukaa kitandani. Akaishika mashine yangu, nami nikamsogelea karibu zaidi, kisha akaiingiza mdomoni na kuanza kuinyonya. Ah!
Alikuwa na midomo minene, kwa hiyo ilitunika vizuri aliponinyonya namna hiyo na kujaribu kuizamisha mpaka kooni kabisa. Nikamuuliza ikiwa labda alikuwa anatumia dawa kuubana sana uke wake, naye ndiyo akaacha kuninyonya na kusema ndiyo, ila pia hakuwa amekutana na mwanaume kwa muda mrefu sasa.
Nikamwambia sawa, kisha nikamsaidia kumtolea shati lake ili lisije kujikunja sana, akibaki na sidiria nyekundu pia iliyoyafunika matiti yake makubwa. Akavua saa na cheni yake pia. Usawa wa kiuno chake baada ya kuilegeza zipu ya sketi aliyokuwa amevaa, niliweza kuona shanga kama nne za urembo kukizungukia, ikionyesha alikuwa mwanamke aliyependa sana mitindo mbalimbali ya kupagawisha mwanaume kimahaba, ndiyo nikainyanyua miguu yake juu na yeye akaegamia viwiko vyake na mgongo kitandani hapo.
(.........).
(.........).
(.........).
Nilipochoka mkao huo, nikamgeuza, naye akalalia tumbo huku miguu yake ikikanyaga chini, ndiyo zamu hii nikamwingia bila kuhangaika. Aisee! Nililitandika hilo kalio! Piga haswa, haraka-haraka yaani, nalo likawa linarukaruka tu huku mwanamke huyu akiguna kwa raha. Alikuwa na tabia ya kutaka sana kugeuka nyuma ili aniangalie, kwa hiyo nikakikandamiza kichwa chake kitandani huku nikiendelea kumpa vyake tu.
Alikuwa ameshanifanya nitamani tu kuendelea, kwa hiyo nikampandisha kitandani kwa usawa huo huo na kumlaza kwa ubavu, miguu yake ikibanana pamoja, kisha nikamwingia tena na kuendelea na show. Miwani yake ilikuwa imepinda usoni, akiniangalia kwa macho mazito huku akitoa miguno kwa kukaza meno yake, nami ndiyo nikawa nimehisi kuchoka zaidi na kusitisha kumkuna, kisha nikajilaza pembeni yake kuitafuta pumzi kwanza.
Yeye alipoona hivyo, akaishika mashine yangu iliyokuwa imesimama bado na kuanza kuinyonya kwa bidii, kwa ufundi, nami nikahisi nguvu mpya iliyofanya nisimame kwa unamba moja. Alikuwa amejaa mate mdomoni, akionekana kutaka raha zaidi, naye akaitoa miwani yake machoni na kujivuta kuja kwa juu yangu.
Nilihofia uzito wake maana alikuwa na mwili, siyo kama wa Shishi baby au Wellu Sengo lakini, ila hakukuwa na noma sana baada ya yeye kuukalia msumari na kuanza kupigiza kalio lake hapo kwa mwendo wa taratibu. Akaweka mikono yake kitandani pande za mabega yangu, uso wake ukiwa juu ya wangu, naye akaendelea kujisugua huku akitoa miguno kwa pumzi.
(..........).
(..........).
(..........).
(..........).
Nikaendelea kumtandika tu bila kuacha, ndipo akaanza kuvuta shuka kwa mikono huku akitaka kutoka juu yangu, lakini nikamkaza hivyo hivyo ili asikimbie. Kiuno chake kikapanda juu kwa mshtuko mpaka mashine yangu ikamtoka, nami nikawa nahisi maji yenye moto yakinimwagikia kama vile yanapulizwa, na Rukia akawa anatoa miguno huku akishtuka-shtuka mwilini, kisha akatulia hatimaye.
Mimi pia nikawa nimetulia, nikihisi kabisa kwamba nilikuwa karibu kumwaga raha zangu pia lakini zikawa zimekomea kibofuni. Rukia alikuwa amelaza kichwa chake pembeni na shingo yangu, akipumua kwa uchovu, nami nikamwambia, "Tunyanyuke. Nahisi saa limekata."
Akanyanyua uso wake na kunitazama, naye akasema, "Una haraka, eti?"
"Ndiyo. Hata wewe najua unahitajika huko mapema... nimesikia simu yako inaita mara tatu hapo," nikamwambia hivyo.
Akaweka kiganja chake kwenye nywele zangu na kusema, "Leo Jumamosi, siko tight kivile. Naweza kuahirisha kwenda kama ukitaka tubaki."
"Hapana, ni muhimu niondoke. Na nahisi nitachelewa na usafiri ila... leo ni lazima. Tutakutana tu hata baadaye," nikamwambia hivyo.
Bado nilionyesha kutokuwa na raha sana ijapokuwa nilikuwa nimemfurahisha yeye kupita maelezo, nami nikaashiria kutaka kunyanyuka, hivyo akasogea pembeni kuniruhusu nitoke chini yake
"Una maji mengi," nikamwambia hivyo.
Akatabasamu kiasi na kusema, "Umenipagawisha sana. We' ni mzuri... halafu unajua."
"Hata wewe. Ngoja nikajimwagie faster," nikamwambia hivyo na kutoka kitandani.
Fyuu bafuni, fyaa chumbani tena.
Nilikuwa najitahidi kukimbizana na muda maana tayari ilikuwa imeshafika saa nne na nusu, na kutoka huku mpaka huko kwa madam Bertha kwa misukosuko ya barabarani, niliomba tu isiwe kuchelewa sana. Nikawa nimejikausha maji, nikachana nywele vizuri, kisha nikaanza kuvaa nguo zangu tena, huku Rukia akiwa bado kitandani na sasa akiongea na simu yake.
Nilipokuwa nimemaliza kuvaa T-shirt langu, akawa ameachana na simu yake na kuniuliza, "Si tungeondoka wote?"
"Ingekuwa fresh, ila nimechelewa sana. Kuna ishu ya muhimu leo. Boss ata-mind hata kama nikisema kuna jam, kwa hiyo acha tu niwahi," nikamwambia hivyo.
"Unapanda daladala na mwendokasi, au?"
"Kutokea huku? Napanda boda mpaka pa kuchukulia daladala ndo' nielekee huko. Mwendokasi mpaka Kariakoo huko... sifiki."
"Kama utaweza, chukua boda au Bajaj ikupeleke huko moja kwa moja, usishindane na mikwaruzo ya daladala," akaniambia hivyo.
Nikamwangalia tu usoni baada ya yeye kuniambia hivyo, naye akasogea upande wangu na kuuokota mkoba wake, kisha akatoa pesa kutoka humo. Noti za elfu kumi kumi, akahesabu kidogo, kisha akanipatia. Nikazipokea huku nikizitazama kimaswali kiasi. Ni kwamba alikuwa ananilipa, au?
"Hii ya nini?" nikamuuliza hivyo, akiwa amesimama mbele yangu huku kavaa taulo iliyoufunika mwili wake kutokea kifuani mpaka usawa wa mapaja.
"Nauli. Utaenda, halafu baadaye nikiwa free nitakuita uje sehemu nyingine," akaniambia hivyo kwa sauti tulivu.
"Nauli? Elfu themanini? Kumbe una hela chafu eh?"
"Ahahah... hiyo ni ndogo mbona?"
"Wacha!" nikasema hivyo huku nikimwangalia kwa umakini.
Akatabasamu huku ameibana midomo yake.
"Sikia. Nahitaji kuongea hili ili tuelewane mapema, sawa? Usije kufikiri labda me ni... escort, au mdoli wa kulipwa kwa huduma. Siko hivyo Rukia," nikamwambia.
"Kweli eh? Basi ni vizuri. Me sina shida. Nimekuelewa sana toka muda... hata kama una videmu vingi tayari, me shida yangu ni penzi lako tu," akaongea kwa uhakika.
"Umeona nini kwangu kwani ambacho mumeo hana?" nikamuuliza hivyo.
"Ni hivyo tu. Nimekuelewa wewe. Mume wangu ni mtu wa safari mno, na najua hata yeye ana vipoza roho huko anakoendaga. Me nimekupendea tu pigo zako. Una pigo nzuri sana... na nataka nikupe matunzo mazuri wasiyojua kukupa hao videmu wengine," akasema hivyo na kung'ata mdomo wake wa chini.
"Una maringo!" nikamwambia.
Akacheka kidogo kwa pumzi na kuendelea kunitazama huku ameachama na kuulambisha ulimi wake gegoni. Yaani mapenzi njoo utamu kolea! Dah!
Nikamuuliza, "Una miaka mingapi?"
Akajibu, "Arobaini na tano. Wewe?"
"Ishirini na nane," nikamwambia.
"Ndiyo maana una nguvu. Uko kwenye peak... unanifanya najisikia kama denti," akaniambia hivyo kwa madaha.
Nikiwa naendelea tu kumtazama, akasogea karibu zaidi na kupitisha mikono yake mabegani kwangu, akielekea usoni ili aweze kunibusu mdomoni, nami nikamruhusu aanze kufanya hivyo. Nilikuwa makini sana, nikizipokea busu zake huku nikilishikilia kalio lake lililokuwa wazi ndani ya taulo kwa viganja vyangu, naye akaacha kunibusu hivyo na kunitazama machoni.
"Baadaye tukutane, eti mpenzi?" akaniuliza hivyo kwa deko.
Mm?
Nikamwambia, "Usijali. Nikiwa free, sitakuangusha. Kikubwa mawasiliano."
"Sawa," akasema hivyo.
Nilipenda tu namna alivyokuwa na kautulivu fulani hivi kalikofanya hali nzima ijae amani, nami nikamwacha hapo hatimaye na kuondoka zangu ili niwahi kufika kwa "madam kipiri" kabla sijarushiwa sumu yake pakiwa bado mapema.
★★
Mwendo wa kufikia saa zima na dakika chache ukawa umenifikisha maeneo ya Makumbusho, na moja kwa moja nikamwelekeza dereva wa bajaji mpaka kufikia kwenye hoteli ya Royal Village. Ndiyo, niliamua kuchukua bajaji binafsi mpaka huku ili niweze kuwahi baada ya kuachana na sugar mommy Rukia, na tulikuwa tumewasiliana wakati niko mwendoni na yeye kunisifia kwa mahaba niliyompa, akisema ana hamu sana ya kuja kuniona tena maana hakutegemea kwenda kazini asubuhi hii akiwa amechangamka namna hiyo.
Pamoja na kuwa suala hilo la Rukia liliegamia kwenye upande fulani mzuri wenye kusisimua, bado tu sikuwa nimeipata amani ya rohoni, yaani furaha sikuwa nayo hata chembe. Lakini ili kumridhisha, nikamwambia tu nilifurahi sana pia kuwa naye asubuhi hiyo, na kumsifia kwamba alikuwa mtamu sana. Kuonana baadaye lingekuwa suala la kuangalia na hali kama zingeruhusu, na hapo ndiyo tukawa tumeagana mpaka baadaye.
Yaani ile nimefika tu hotelini, saa sita ilikuwa imebakiza dakika nane tu kuingia. Kwa hiyo nikawahi kule ndani upesi sana mpaka kufikia kwenye mlango wa chumba chake madam, kisha nikagonga hodi na kusubiri. Vuup, kikadi kikapitishwa, na mlango ukafunguka.
Hapo mbele yangu alikuwa amesimama madam Bertha mwenyewe, akiwa amevaa T-shirt laini la mikono mirefu na cheni ya dhahabu shingoni, suruali ya skinny jeans nyeusi miguuni na viatu vyeupe vya kijanja. Mwonekano wake uliniambia kwamba alikuwa anataka kutoka, kama siyo ndiyo alikuwa amerudi kutoka sehemu, na kichwani bado nywele zake zilikuwa fupi kwa kupakwa dawa, ila sasa alikuwa amezichanganya na rangi ya maziwa kiasi upande wa juu. Kwa ule usistaduu wa kishua yaani.
Alinitazama kwa njia fulani kama vile anataka kunimeza, nami nikiwa namtazama kwa macho yenye uchovu nikalazimisha tabasamu kiasi na kunyanyua simu yangu kumwonyesha muda kwenye kioo.
"Sita juu ya alama! Sijachelewa, nastahili tuzo," nikaanza kumsemesha kwa njia ya utani.
Akatulia kidogo akiiangalia simu yangu, kisha akasema, "Umechelewa. Ni saa sita na dakika moja."
"Ah... umesubiri iingie dakika moja hapa ndiyo useme 'umechelewa.' Acha ujanja madam," nikamwambia hivyo.
"Umeanza kunichukulia kama mtani wako, eti?" akaniuliza hivyo kwa sauti makini.
Niliona wazi kwamba hakuwa kwenye mood ya utani, kama mimi tu, hivyo nikaweka umakini wangu pia na kumwambia, "I'm sorry. Hizi siku mbili zimekuwa nzito madam... I... got distracted."
Akanitazama usoni kwa umakini, kisha akaachia uwazi zaidi mlangoni ili niingie.
Nikapita mpaka ndani ya chumba hicho na kusimama usawa wa sofa upande mwingine, naye akafunga mlango na kuja mpaka karibu nami.
"Acha kuchanganywa na habari za familia wakati ambao biashara zimeanza kutembea mdogo wangu. Utapoteza ulichokipambania," akaniambia hivyo kwa mkazo.
Nikatikisa kichwa kukubaliana na hilo.
"Usifikiri kila simu nitakayokupigia inamaanisha nataka sex tu. Kuna watu wengi sana wa kunipa hicho kitu na sina muda nao. Nikikuvutia waya, pokea. Next time ukizingua nikapigwa joto la kupoteza madili yangu, nakuapia eh... nitahakikisha wewe ndiyo linakuivisha mpaka unakauka. Ushanisoma?" akaongea kwa hisia kali.
"Mwanzo, mwisho," nikamwambia hivyo.
Akavuta ulimi mdomoni mwake kutoa kero, kisha akasema, "Unajua kuna watu nilikuwa nimewapanga, uje uwaonyeshe unavyotengeneza madini ili wanipe access ya mahala secure na vifaa bora ili ishu yetu ianze kazi, na hiyo ilikuwa ni jana, Festus alikuwepo pia... lakini ukapotea tu sijui ukaamua kwenda wapi, nakupigia hupokei, ukafikiri nini, nawashwa sana au?"
Nilielewa alikuwa amekasirika mno, kwa hiyo nikamsogelea karibu zaidi na kumwambia, "Madam... nisamehe. Haitatokea tena, nime... nimekuangusha zamu hii, lakini... nakuahidi haitatokea tena. Kuanzia sasa hivi nitafuata unachotaka, nitakuwa popote ulipo ukinihitaji, maana hili dili nalihitaji sana. Sitakuangusha... jana kulikuwa na dharura tu, lakini haijalishi tena. Haitajirudia. I'm sorry."
Nilimwongelesha kwa njia ya kubembeleza sana, kisha nikaishika shingo yake taratibu huku mkono mwingine nikiuweka kiunoni kwake.
Akawa ananiangalia kwa njia ya kuudhika bado, naye akatazama pembeni na kusema, "Ole wako ije kujirudia. Sitakuelewa tena."
"I promise," nikamwambia hivyo kiuhakika.
Akanitazama usoni kiudadisi na kuuliza, "Mbona macho yako mazito hivyo? Ulikuwa wapi jana?"
Nikarudi nyuma kiasi na kusema, "Unakumbuka juzi... nilipigiwa simu hapa nikakwambia..."
"Eeh, uliitwa na shangazi yako... Mamu kafanyaje huko sijui... ndiyo ikawaje?" akanikatisha kwa kuuliza hivyo.
"Huyo binti alikuwa ametekwa," nikamwambia hivyo.
Akakunja uso kimaswali kiasi.
"Walimteka, kwa hiyo tukaanza kumtafuta. Ndiyo tumempata jana usiku... alikuwa karibu kuuliwa... ila sasa hivi yuko hospitali anaendelea vizuri. Sijalala vya kutosha shauri ya hiyo ishu," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.
"Walikuwa wamemteka huyo msichana kwa nini? Ni wakina nani?"
"Ni kaka yake tu mjingammoja. Anataka mali aliyorithishwa huyo msichana, kwa hiyo ndiyo ulikuwa mpango wake... amuue ili aipate," nikamwambia.
"Yaani kaka yake... ndugu yenu kabisa? Yeye yuko wapi?" akauliza.
"Mapolisi wamemkamata," nikamwambia.
"Hiyo ni story ya kweli, au umeitunga tu?" akaniuliza hivyo.
"Kwa nini nikudanganye? Huyu binti ni kama mdogo wangu. Isingekuwa ya hivyo ningekuwa nimekuja kwako. Huku ni muhimu, ila... tunaowapenda ni muhimu pia unajua," nikamwambia hivyo kwa upole.
Akanisogelea na kunishika begani, kisha akasema, "Ndiyo, najua. Ila ukiendelea kuweka familia mbele, mbele, mbele tu... hizo distraction hazitapotea. Sasa hivi nataka twende tour, nikuonyeshe network yetu, halafu wewe una kichwa kizito shauri ya usingizi. Faida gani? Baadaye tukienda kwenye meeting na wenzetu kuongelea masuala muhimu ukasikia shangazi, sijui Mamu kapata presha huko, ukimbilie kwake tena? Tell me if I'm just wasting my time fucking with you boy..."
"Hapana madam. Nimekwambia kuanzia sasa hivi, hivi vitu havitanichanganya tena. I'm all yours. Popote unapotaka twende, twende. Kichwa changu kipo active... hakuna shida," nikamwambia hivyo.
"Well, me nataka kuanzia sasa kiwe active kwenye hili game kwa asilimia mia. No setbacks, sijui familia bullshit... sitaki. Nahitaji uwe sambamba na mimi," akaniambia hivyo kwa mkazo.
Nikamshika kiunoni na kusema, "Okay. Niambie cha kufanya."
"Uje ukae hapa," akasema hivyo.
Nikatulia kidogo nikitafakari maneno hayo.
"Njoo hapa tukae wote. Ndiyo utakuwa karibu nami, utafata chochote nitakachokuelekeza na kutimiza kwa uharaka, na hautavurugwa na maisha ya kuruka-ruka kama uliyonayo huko Mbagala. Umenielewa?" akasema hivyo kwa umakini.
Nikatazama chini kwa kutafakari zaidi. Alikuwa akinipa ofa ya kuja kuishi hapa hotelini pamoja naye, ili tufanye alichotaka nikiwa karibu zaidi. Hii ingekuwa njia nzuri sana ya kuweza kumharibu mwanamke huyu, yaani kuishi na adui kwa ukaribu kabisa ili kujua siri zake na kutoa taarifa muhimu za mambo yaliyoendelea kwa askari Ramadhan.
Lakini hii ingemaanisha kwamba nilipaswa kuondoka Mbagala na kumwacha Mariam akiwa bado hajapona vilivyo, tena hasa baada ya matatizo yaliyokuwa yamempata, huenda hata hali yake ndiyo ingenihitaji zaidi. Kulikuwa na kitu ambacho kilitokeza kama malaika wawili, mmoja mweupe, mwingine mweusi; huyo mweupe akinishauri nisifanye jambo ambalo madam Bertha alilitaka ili niweze kuendelea kumsaidia Mariam, na huyo mweusi akishauri 'agh, achana na Mariam bana!' Kwani nalipwa kumsaidia? Si nije tu kukaa kwa huyu kibibi ili nilipize kisasi changu kitamu?
Nikawa nimekwama katikati ya fikira tofauti za maamuzi ambayo kichwa changu na moyo wangu vilitaka niyachukue. Ningefanya nini?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Full Story WhatsApp or inbox
Whatsapp +255 678 017 280