Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Inashangaza kidogo, eh? Ndiyo. Huyu jamaa aliyekuwa kwenye dili la kununua shamba la Mariam kupitia wawakilishi wake waliompata Joshua kama dalali, alikuwa ni mzee wangu. Ni kitu ambacho sikuwa nimetarajia kabisa mpaka Joshua alipotaja jina lake muda mfupi nyuma kule kituoni, na ndiyo maana nilihisi labda kuna mambo mengi kwenye visa vyote vilivyokuwa vikitokea sasa yalionekana kuwa kama yamepangwa fulani hivi na majaaliwa.

Yaani kweli, ilipaswa tu kuwa mzee wangu akawa ndiyo mnunuzi wa hiyo mali mpaka kusababisha hayo mambo yote mabaya kutokea! Ila sidhani ikiwa alijua undani wa visa hivyo vyote, na ndiyo nilikuwa nimekuja kusahihisha mambo. Oh, na kuhusu JC kuwa kijana wa jamaa mwenye pesa namna hii ni suala ambalo tutaliongelea baadaye. Ikiwa baadaye itakuja!

Baada ya kuwa ameniambia nikaribie, nikakisogelea kiti kimoja karibu na meza yake na kisha kukaa.

"Imeshapita miezi miwili toka mara ya mwisho tumeonana, eti?" mzee akaniuliza hivyo.

"Ee, nafikiri," nikamjibu.

"Okay. Umenikuta niko bize, ila nambie. Kuna tatizo?" akauliza.

"Ee, naweza kusema ni tatizo. Kuna jambo nahitaji unisaidie kulisuluhisha," nikamwambia.

Akashusha pumzi kiasi kama kutoa uchovu wa kifikira, naye akasema, "Ni kuhusu ishu ya dada'ako?"

Sikutarajia hilo, hivyo nikasema, "Hapana. Kwa nini kwani? Jasmine ana tatizo lolote?"

"Hawajakwambia?"

Nikatikisa kichwa kukanusha.

"Labda hawajaona ni busara kukwambia, hata hivyo haikuwa..."

"No, mzee... niambie. Kilichonileta ni kitu tofauti, ila... niambie kwanza Jasmine ana tatizo gani. Amebakiza miezi michache ajifungue, si ndiyo?"

"Yeah, miezi miwili au mmoja na nusu."

"Shida ni nini?"

"Wameachana na mume wake," akaniambia hivyo.

Nikakunja uso kimaswali kiasi, nami nikaangalia pembeni.

"Wamekorofishana sana juzi hapo, ilikuwa ugomvi mkubwa over a petty misunderstanding, na unajua jinsi dada yako alivyo. Ilikuwa karibu apate miscarriage. Mimba ingetoka," akasema hivyo.

Nikawa nimeshangazwa na hili, nami nikauliza, "Ulikuwa ugomvi... yaani, huyo jamaa wake alifanyaje, alimpiga au?"

"Hamna, walirushiana maneno tu. Huyo Kevin akaondoka zake, ndo' dada'ako akapata mshtuko. Ila walimpeleka hospital, sa'hivi yuko vizuri tu."

"Yuko wapi sasa hivi?"

"Yupo nyumbani. Imebidi akae na mama yenu mpaka akijifungua."

"Dah! Siyo poa. Itabidi nije niende kumwona," nikamwambia.

"Labda waliona wasikwambie ili wasikuharibie likizo yako. Kwanza umeenda wapi kwenye hiyo fungate lonesome?" akaniuliza hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Niko Mbagala."

"Kule nyuma kwenye jalala?" akauliza kiutani.

"Ahahahah... pazuri siku hizi, siyo kama Mondi alivyopaacha," nikamwambia.

"Okay, sawa. Niambie sa' ishu ni nini kama siyo Jas," akasema hivyo huku akiangalia karatasi moja mezani.

"Yeah, aa... kuna kiwanja, au niseme shamba. Kuna shamba unalotaka kununua, si ndiyo?" nikamuuliza.

"Shamba?"

"Eee. Kuna shamba linamilikiwa na mwanamke fulani nje ya mkoa, najua unataka kulinunua mzee."

Akaniangalia, kisha akasema, "Kuna vitu vingi kampuni inanunua J. Kuna miradi inaendeshwa, na ndiyo... kuna viwanja au mashamba tunayo-target hapa au kule ili kujenga mambo yetu fasta. Be specific."

Sikuwa najua shamba la Mariam lilipokuwa kihususa, hivyo nikamwambia, "Hili shamba liko nje ya jiji. Mkoa mwingine. Kuna, mwakilishi wako... alimlipa mwanaume fulani pesa in advance ili akuhalalishie kulipata, lakini najua mpaka sasa hivi haujalipata na ulikuwa unataka kuangalia upande mwingine, ila... ndiyo unahitaji jamaa arudishe pesa zako kwanza maana kakucheleweshea. Si unaipata hiyo?"

Akaweka uso wa kutafakari kiasi, naye akasema, "Yeah. Unaongelea shamba la... lile lililo Morogoro la mwanamke fulani anaitwa... Mariam Constantine?"

Sikujua Constantine kuwa jina la pili la binti Mariam, lakini nikamwambia, "Yes! Huyo huyo."

"Ndiyo. Nimejaribu kulipata hilo shamba tokea wiki chache zilizopita ila napewa tu delay. Umejuaje kuhusu hilo?" akauliza.

"Mmiliki namfahamu, yupo huko huko Mbagala," nikamwambia.

"Ooh! Well that's good then. Sijui kwa nini hawa watu wangu wanakuwa slow kunikamilishia, ila aliyekuwa anawakilisha kunirasmishia hilo shamba ndiye anayetuzungusha. Kama utaweza kumleta huyo mtu tufanye makubaliano hapa hapa face to face tutaimaliza hii yote haraka...."

"A.. ha-hapana mzee. Yaani, mmiliki ni msichana mdogo, anayesimamia hiyo mali ni dada yake. Sasa...."

"Shida ni nini, J?" akanikatisha.

Nikatulia kidogo, kisha nikamwambia, "Nakuomba usifanye taratibu za kununua hilo shamba."

"Nini?"

"Ni kiwanja kwa ajili ya huyo msichana, ana... ana tatizo fulani ambalo... yaani dada yake ndiyo anamsimamia, na hakuwa... ameliweka market, ila... kaka yake ndiyo alifanya kama deceit kuliweka market, nyie mkafikiri..."

"J subiri, sikuelewi. Ongea ueleweke vizuri maana nachanganyikiwa," akanikatisha kwa kusema hivyo.

Nikashusha pumzi tu na kuangalia pembeni.

"Hautaki ninunue hilo shamba kwa sababu gani? Huo ni mradi wa kampuni, na nilikuwa nimeshatoa pesa nyingi. Watu ambao wanahusika ndiyo wanatakiwa kuniletea taarifa za ni nini kinaendelea, wewe... unahusika vipi, halafu uje useme nisilichukue?" akauliza hivyo.

Nikamwambia, "Iko hivi. Tuseme kwa mfano, wewe unataka kununua shamba ambalo ni la Jasmine, sawa? Unatuma mwakilishi akuletee huo mchongo. Huyo mwakilishi akimtafuta Jasmine, anakutana na mimi kaka yake, namwambia kwa sababu me ni wa familia moja na mmiliki, nitamrahisishia kulipata, kwa hiyo atoe tu hela halafu mimi nita-deliver. Wakati huo huo kumbe Jasmine hataki kuliuza shamba, halafu hajui kuhusu haya makubaliano ambayo me nimefanya na mwakilishi wako, afu' hizo hela nimekula. Sasa, nachokifanya ni kuamua kuunda mpango wa kumwondoa Jasmine, sawa? Yaani nimuue, halafu nihalalishe umiliki wa hiyo mali kwangu mimi mwenyewe, ili ndiyo niitoe kwa niliowauzia. Sijui umenielewa hapo?"

Mzee akawa ananiangalia kwa utulivu tu.

"Ndivyo ilivyo na hii hali mzee. Dada yake na huyo binti ndiyo msimamizi wa hilo shamba, hakuwa na habari kwamba kaka yake kakubali dili la kuliuza kwa mtu mwingine. Huyu jamaa alikuwa anajua dada yake asingekubali kuliuza, kwa hiyo akajaribu kumuua mdogo wao halafu ahamishe haki ya kulisimamia hilo shamba kwake yeye mwenyewe, ili ndiyo akupe wewe," nikamwambia hivyo.

"Are you serious?" akauliza kwa sauti makini.

"Kabisa. Ni juzi tu hapa ndiyo alikuwa amemteka huyo msichana ili amuue, lakini mapolisi wakamkamata mapema kabla hajafanikiwa. Tena hapa ndiyo nilikuwa nimetoka alikofungiwa, akaniambia sasa nyie ndiyo mnao... mnaolihitaji hilo shamba," nikaeleza.

Akashikanisha viganja vyake na kuegamiza mikono mezani, naye akasema, "Kwa hiyo unataka kusema kwamba wameniibia, si ndiyo?"

"A.. ah, siyo kihivyo, yaani... ni huyu jamaa. Familia yake, na huyu dada mwenye haki ya usimamizi wa hilo shamba hakujua lolote. Mpaka sasa navyoongea na wewe yaani hajui kama jitihada za kununua hilo shamba ni zako, kaka yake yuko rumande, kwa hiyo wanafikiri imeshaisha. Ila najua mwenye deni la pesa zako ni huyu jamaa, siyo familia yake, kwa hiyo ndiyo maana nikaona nije kukuambia ili kukuelewesha... namna mambo yalivyo," nikamwambia.

"Aisee! Kwa hiyo mwenye shamba haliuzi, aliyesema linauzwa yuko ndani, pesa kala na sijapata faida yoyote, ila ni hasara anayotakiwa alipie, lakini yuko jela kwa hiyo hataweza kulipa, si ndiyo?" akauliza hivyo.

Nikaangalia chini kiasi na kutikisa kichwa kukubali.

"Kwa hiyo huyo jamaa alikuwa amepanga kumuua mdogo wake ili alipate... halafu ndiyo atuuzie?" akauliza.

"Ndiyo. Na alikuwa karibu kufanikiwa," nikamjibu.

"Kwa nini afanye hivyo?"

"Ni mjinga tu. Alikuwa eti anaogopa kwamba mtamfanya kitu kibaya kwa sababu tayari alikuwa amekula hela mliyompa mwanzoni na kalenda ilikuwa imeisha."

"Aliyemwambia tutamfanya kitu kibaya hakukosea. Nimetoa pesa nyingi kama kianzio J, halafu aje tu kusema kala na dili limefeli? Asingekuwa ndani sasa hivi angenitambua," akaongea kwa kuudhika.

"Achana naye tu, hafai. Ingawa hivyo... sijui sasa kwa upande wa pesa zako ndo' inakuwaje," nikamwambia.

"Tutamtoa, auze hata figo zake zote, arudishe hizo pesa!" akaongea kwa mkazo.

"Mzee..."

"Usini-mzee mimi! J, tumetoa hela nyingi kama kianzio, sawa? Tena mimi personally ndiyo nilikuwa nahitaji hicho kiwanja, nataka nijenge ishu nzuri sana itakayoleta matokeo mazuri. Kampuni inapanuka vibaya mno sasa hivi, nasambaza upendo nchini kote kwa kujenga matawi, watu wanufaike na sisi tukue zaidi. Halafu uje tu useme niiachie hii ipite? Hela siyo ya kuchezea kiurahisi namna hiyo. You should know that," akaniambia hivyo kwa mkazo.

"Najua, ila usitoe mtu figo zake kurudisha hicho kilichopotea... siyo fresh. Lakini pia najua... ukiangalia na jinsi hali ilivyo... unahitaji alternative nyingine mzee," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Ipi sasa, J?"

"Lazima itakuwepo tu. We' ndo' boss."

"Ahah... sikia. Pesa siyo zangu tu, zinahusika kwenye kampuni pia. Me ni boss wa ma-boss sita, lakini jua nina ma-boss watatu juu zaidi yangu. I answer to somebody too. Hapa siyo sehemu ya kusema milioni 5 ime-slip tu, hatujui imeenda wapi, halafu ah... ma-boss wapuuzie. Every penny matters. Ikiwa pesa niliyotoa kwa masilahi ya kampuni haitarudi on the deadline, inamaanisha niirudishe kwa kutoa kwenye ya kwangu mwenyewe. Hiyo inamaanisha nini J?"

Nikaangalia chini na kusema, "Hasara."

"Exactly. Kwa hiyo usifikiri nitaliachia kiurahisi tu. Kinachotakiwa... si umesema unamjua huyo mwanamke?"

"Ndiyo, lakini...."

"Nipe contact zake, nitazungumza naye moja kwa moja..."

"Sikia mzee, siyo rahisi kama hivyo. Yaani... hawezi akakupa hilo shamba..."

"Kwa nini asiweze? Sawa, naelewa hakujua, lakini hata me nimepoteza kitu fulani. Tena kikubwa. Look... nitaongea naye. Hata ukitaka, sitagusia pesa iliyopotea, lakini naweza nikamshawishi vizuri sana hadi akanipatia hiyo ishu. Nimekwambia niliilenga hiyo tokea muda, so... pamoja na haya yote ila bado naweza nika-fix something," akaniambia hivyo.

"Naelewa. Sema... sababu inayomfanya asikitoe kama kiwanja, ni mdogo wake. Huyo mdogo wake ndiyo Mariam, ni mgonjwa. Ninawajua hawa watu vizuri kwa sababu... me ndiyo namsaidia huyu binti ili apone..."

"Unamsaidia? Huko huko Mbagala?"

"Ndiyo."

"Ni mgonjwa wa nini?"

"Ana kitu... kiko kama ASD. Equivalent ya PTSD. Aliipata baada ya wazazi wao kufa kwenye ajali, na sasa hivi inaweza ikawa mbaya zaidi shauri ya mambo ambayo kaka yake amemfanyia hiyo juzi... ni hatari endapo kama ataachwa bila msaada unaomfaa yeye," nikaelezea.

"Na wewe ndiyo unampa huo msaada? Wakati huu huu wa mapumziko yako?"

"Ndiyo, ndiyo nilikutana nao huko. Dada yake anampenda sana, anamtunzia hilo shamba kwa ajili ya future akiwa na matumaini kwamba mdogo wake atapona ili aje kukimiliki yeye kama yeye, na kisha ajenge maisha yake kwa njia yoyote atakayoamua kutumia mali aliyoachiwa. Isingekuwa ya tamaa ya kaka yao, wala hata usingeingia kwenye hilo dili mzee, yaani siyo fair kwako kama ilivyo siyo fair kwao pia. Ni watu wazuri, wame... wamelaghaiwa tu. Nakuomba uangalie njia nyingine mzee. Ukitaka... nitasaidia kukutafutia shamba, au kiwanja sehemu fulani nyingine, but... nakuomba uangalie utaratibu wa kuliacha shamba la huyu binti. Tafadhali sana," nikaongea kwa hisia za wazi.

Mzee mkubwa akawa ananiangalia kwa ufikirio sana, huku akipiga-piga kidole chake kimoja mezani, kisha akasema, "Nina mambo mengi ya kufikiria J. Sikuwa nimetarajia uje uniletee na hili, kwa hiyo... hhh... anyway, nitaangalia cha kufanya ili tuepuke kuzunguka kwingi. Nitaongea na niliyemweka kufatilia hiyo ishu halafu tutaona."

"Asante sana. Nashukuru," nikamwambia hivyo kwa heshima.

"Huyo binti ana miaka mingapi?" akauliza.

"19. Anaelekea 20," nikamwambia.

"Kwa hiyo kaka yake akamteka halafu... akataka kumchinja, au?"

"Mara ya kwanza alitaka kumgonga na gari, akashindwa. Juzi ndo' ametuma watu wakamteka, wakataka na kumbaka kabisa halafu ndiyo wamuue," nikamwambia kwa hisia za hasira ya mbali.

"Na ni mdogo wake tumbo moja?"

"Baba mmoja, mama mmoja."

"Aisee! Huyo jamaa ni fala, eti?"

"Sana!" nikasema hivyo na kuvuta ulimi mdomoni kwa hasira kiasi.

Mzee akacheka kidogo kwa pumzi, naye akasema, "Haya, sawa. We' nenda, me nakomaa na huu udambwi hapa."

Nikacheka kidogo kwa kupata ahueni, nami nikasimama huku nikisema, "Asante sana. Ukitaka kunijulisha au kuniuliza lolote, nishtue tu."

Akiwa ameshayarudia makaratasi yake tena, akasema, "Sawa, usijali. Tutawasiliana. Unaenda kupita nyumbani?"

"Ee, kuna sehemu naingia kwanza. Muda ukiruhusu nitapita kumwangalia Jas na mama, kama siyo... basi nitawapigia," nikamwambia hivyo.

"Haya, baadaye. Kuwa care huko," jamaa akaendelea na ubize wake.

Nikatoka sehemu hiyo ya ofisi na kuelekea nje hatimaye, nikiwa nahisi ahueni kidogo ndani ya moyo wangu. Najua ni mambo mengi ambayo JC sijaelezea kujihusu bado, lakini utapata nafasi nzuri tu ya kunijua kwa ubora zaidi. Huyo ndiyo alikuwa mdingi. Mdingi mwenye nazo, halafu alikuwa mshkaji sasa. Hadi neno fala alilijua!

Niliondoka kutoka jengoni hapo baada ya kuagana na secretary wake, mtoto Faima, nami nikaenda kutafuta daladala ambazo zingeelekea maeneo ya ile hoteli ya Royal Village ili nikamwone mamaa kibosile Bertha. Angalau nilikuwa na uhakika sasa kwenye suala la ishu ya shamba la Mariam, kwamba utatuzi ungefanywa bila kuwasumbua wanafamilia wale maana nilikuwa nimetafuta suluhisho kutoka kwenye meza kuu ya wahusika. Tena ni mhusika, na alikuwa ni mshua wangu.

Sikutaka tu Miryam asumbuliwe zaidi kwa makosa ambayo kaka yake alipaswa kuyalipia. Najua kama ingetokea mzee wangu akamwita yule mwanamke kumwambia kuhusu hasara yake, Miryam angeweza hata kujichanga kabisa ili ailipie wakati haikuwa yeye aliyeisababisha. Alikuwa na mambo mengi ya kuangalia hata hivyo, kwa hiyo niliona hili lingine lingekuwa la kumwongezea mzigo juu ya mizigo. Joshua alikuwa anamkosti sana yaani, basi tu.

Nimesema mzee wangu alikuwa mshkaji, ila kwenye masuala ya kampuni yake hakutakaga mchezo. Kiukweli, kama angetaka, hizo figo za Joshua zingeenda kunyofolewa na kuuzwa ili pesa yake irudi kweli, lakini hakuwa na ukatili wa aina hiyo, ni basi tu najua alikasirishwa na mambo kwenda kinyume na matarajio yake. Hivyo, ningepaswa kuwa tayari kwa lolote kutokea hapa ili likija niwe na njia ya kuliitikia kwa uharaka, na kufanya mambo yaendelee kuwa na amani kwa pande zote mbili.

Umakini wangu sasa ungetakiwa kuwa kwenye upande wa tatu; madam Bertha.

★★

Baada ya kuchukua daladala na kufika eneo lililo karibu na Royal Village Hotel, nikawa nimeshuka na kutambua kitu fulani ambacho sikuwahi kugundua. Yaani, kumbe mara zote nilipokuwa nakuja huku kutokea Mbagala, daladala ingepita usawa wa hoteli hiyo kabisa kabla ya kukunja kona kwenye eneo la Vunja Bei ili kuelekea stendi ya Makumbusho.

Ikiwa ningekuwa nimetambua hilo mapema basi kila mara nilipokuja huku ningekuwa tu nashukia hapo na kwenda hotelini kwa madam badala ya kupoteza gharama zile zote kulipia Uber. Dah! Ila sema tu haikuwahi kuniingia akilini maana sikuwaga natazama sana nje, lakini kwa wakati huu hilo lingebadilika.

Kwa hiyo nikaanza kutembea kuielekea hoteli, mida ikiwa ni saa sita mchana sasa kuelekea saba, jua likiwa kali mno, nami nikampigia madam Bertha. Akawa amepokea, ndiyo nikamwambia nilikuwa naelekea hapo hotelini kwake ili kukutana naye, na kumuuliza kama alikuwepo kwa muda huu. Kwa njia ya kistaarabu tu, akanijibu kuwa ndiyo alikuwepo, ila muda siyo mrefu angetoka hivyo niwahishe kufika la sivyo nisingemkuta. Nikamwambia niko nje ya jengo kabisa hivyo ni sasa hivi tu naingia huko kwake, ndipo nikakata simu.

Nilitaka kujua sasa ni yapi yaliyokuwa mapya kwa upande wa mwanamke huyu tokea mara ya mwisho tumeachana pale Uhasibu ile jana tukiwa tumeahidiana mimi kurudi kwake ili nianze kuishi naye. Haikuonekana kwamba alikasirika nilipomwambia kuwa kuna ishu iliyozuka na kufanya jambo hilo lishindikane, na ndiyo nilitaka kujua kwa nini. Sikujutia kuamua kubaki Mzinga ili niendelee kumsaidia Mariam, ila bado na upande wa Bertha nilitakiwa kuwa "active" sana kwa sababu nilitaka suala la kumkamatisha limalizike upesi.

Nikapanda mpaka huko ghorofani na kukifikia chumba chake, nami nikaugonga mlango na kusubiri. Kidogo tu ukafunguliwa, madam mwenyewe akiwa hapo mbele yangu huku ananiangalia kwa utulivu machoni. Mwonekano wake ulionyesha kwamba kweli alikuwa anaelekea kuondoka.

Alivalia T-shirt jeupe la mikono mirefu lenye kubana kama sweta, likiziba mpaka sehemu ya juu ya shingo yake, pamoja na suruali ya jeans ya blue iliyokoza yenye urembo wa kuchanika-chanika mbele ya mapaja yake, ikilibana vyema umbo lake kwa chini. Miguuni alivaa mabuti ya kike mekundu yenye muundo wenye vichuchumio virefu kwa nyuma, huku urembo wa hereni, mikufu, na pete za dhahabu ukimpendezesha hata zaidi.

"Umependeza," nikamwambia hivyo.

"And I'm just getting started. Ingia," akaniambia hivyo na kurudi ndani.

Nikatabasamu kiasi na kuingia pia, kisha nikaufunga mlango na kumfata. Alikuwa ameelekea upande wenye sofa na kuketi, nami nikaelekea hapo pia huku nikiona laptop ndogo kwenye kistuli cha manyoya karibu na sehemu aliyokaa, pamoja na mkoba sofani. Akaanza kubofya-bofya kompyuta hiyo.

"Umenunua laptop?" nikamuuliza nikiwa nimesimama.

"Ilikuwepo mbona? Hujawahi tu kuiona," akajibu bila kunitazama.

"Kuna mishe unaenda kupiga sa'hivi?" nikamuuliza.

"Yeah," akajibu tena, umakini wake ukiwa kwenye laptop.

Nikashusha pumzi kiasi, kisha nikasema, "Madam... najua... sijawa keen kwenye kutimiza ahadi niliyokupa, ila... ni kwamba tu nadili na mambo mengi sana yaani, sikuwa nimetarajia kabisa kwamba yangeongezeka kwa hiki kipindi ndiyo maana mishe zinakuwa zinaingiliana mno. Inabidi nikae kwa muda fulani kule kuangalia mahitaji ya yule msichana baada ya kilichompata ile juzi, so... kuja kukaa huku moja kwa moja itachukua muda..."

Akaendelea tu ku-type bila kunipa itikio lolote.

"Najua huelewi mengi ila ndiyo hali halisi ilivyo, yaani... inanihitaji. Hata huku ni muhimu pia, natamani sana niwe hapa muda wote na wewe, lakini kwa hilo itabidi tu unipe muda Bertha," nikamwambia hivyo.

Hakuniangalia hata mara moja, lakini akaweka kiganja chake sofani na kukipiga hapo mara mbili, ishara ya kuniambia kuwa nikae karibu yake. Nikatii na kusogea hapo, kisha nikakaa. Akawa akiendelea na jambo alilokuwa akilifanya kwenye laptop hiyo kwa sekunde chache, kisha akaifunga na kunigeukia. Yaani akapandisha mguu mmoja sofani kwa kuukunja na kulaza goti lake kwenye paja langu, naye akawa ananiangalia huku akitabasamu.

"Mambo yameiva! Tunaanza kazi muda siyo mrefu," akaniambia hivyo kwa shauku kiasi.

"Unamaanisha..."

"Nimeshapata spot tutakayotumia kuanzishia ile ishu yetu. Mahesabu tumeshafanya, watu wangu watakuwa tayari kuanza kazi pamoja nawe ukiwafundisha kuunda ile kitu, so business itakuwa underway baada ya muda mfupi tu. Njia tumeshasafishiwa so, let's get crackin'!" akaongea kwa njia ya furaha.

Bado sikuwa nimeelewa kwa asilimia zote, kwa hiyo nikamuuliza, "Umeshapata sehemu inayofaa tutakayotengenezea madawa?"

"Yeah. Wakati wewe ulipokuwa umeenda ku-solve hayo matatizo yako, me nikafanya hiyo ishu itiki fasta. Kila kitu kiko tayari. Kilichopo tu ni wewe kuanza kupika dawa, uwaelekeze na watu wangu, then... money," akasema hivyo.

Nikalazimisha tabasamu, kisha nikamwambia, "Well that was fast. Hongera."

"Usiseme hongera mpaka kazi ianze na ikamilike. Yaani HB hii kitu ikikubali haraka, nitauza sana! I can't wait. Najihisi kama bonge moja la mwekezaji wa shilingi mia tu kwenye business itakayozalisha milioni mia. This is going to be so lit!" akaongea kwa furaha.

"Kabisa. Ahah... ni vizuri mambo yameenda fresh, ila... bado ulikuwa hujanionyesha mtandao unavyokaa Bertha..."

"Ningekuonyesha vipi wakati unakaa tu kuzurura huko?"

Nikaangalia pembeni tu.

"Sikia. We' usiwaze kuhusu network yetu, utaijua tu. La muhimu sasa hivi ni hili. Nitakuweka hiyo sehemu ufanye miujiza yako, faida ije upesi. Hapa tutachoangalia ni nini vinahitajika kwa ajili ya miujiza yako ili uanze kupika, watu wangu wajifunze pia, mizigo ianze kujaza maghala. Tusichezee muda yaani," akasema hivyo.

Nikatikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Na usijali. Kila kitu kitakuwa kwa muda wake. Kama unakuwa unataka kwenda kumsaidia mdogo wako, sijui nani, unakuwa unaenda kwa muda fulani, lakini muda wa kazi unatakiwa uwe sehemu ya kazi. Ukizingua, umeharibu kila kitu... maana sasa hivi tunaenda kwa umakini sana," akasema hivyo.

Kiukweli, sikutegemea kabisa aseme maneno hayo, lakini nikamwambia, "Sawa. Ondoa shaka kabisa."

Akaniangalia kwa upendezi na kushusha pumzi kwa kuridhika.

"Ahah... madam, sikuwa nime... yaani, nilifikiri basi ningefika hapa nikakuta labda ume..."

"Nini? Nimenuna?" akanikatisha.

"Eeeh..."

"Kisa?"

"Si kama hivyo tulikuwa... nilikuwa nimeahidi kuja kukaa hapa, halafu...."

"Agh, wala hata usijali. Dili na mambo yako kwa muda ambao nitakupa, lakini mambo yangu pia utadili nayo kwa muda nitakaokupa. Nimeshaona siwezi kukuchukua kimoja, so... nimekubaliana na hilo tu," akasema hivyo.

"Mh? Kweli ni wewe madam?"

"Kwani me nikoje?"

"Siyo jinsi nilivyokuzoea. Kwa leo? Siyo jinsi nilivyokuzoea kabisa. Yaani nilifikiri ningefika hapa ukaanza kunirushia maneno na chupa ya chai au ndala kuuliza kwa nini nakuwa sieleweki..."

Bertha akacheka kidogo kwa furaha.

"Ni lazima niulize. Hii sudden change imetokana na nini?" nikamuuliza.

Akanishika sikioni na kuanza kulivuta-vuta kwa vidole vyake taratibu na kusema, "Basi tu. Nimejisikia kuwa generous kidogo. Au ni dhambi?"

"Siyo dhambi. Inafanya tu una... unapendeka zaidi," nikamwambia hivyo.

"Kumbe? Ndo' napendeka zaidi ya unavyonipenda?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini.

"Yeah. Hata zaidi," nikamsemesha kwa njia ya utongozi.

"Well, endelea kuonyesha kwamba uko serious na mimi. Labda huo upendo utarudi kwa asilimia zote siku moja," akaongea kama vile ananitongoza yaani.

Nikatabasamu na kuuliza, "Nini kimekufanya umekuwa generous namna hii madam wangu?"

"Mhm... nilikutana na Festus, akaniambia mlivyoonana na kuzungumza," akasema hivyo.

Kauli yake ikanifanya nimtazame kwa njia makini kiasi.

"Mbona hukuniambia ulienda kwake?" akauliza.

"Aa... sikudhani alitaka, yaani..."

"Ndiyo, najua mambo yenu wanaume. Siyo lazima mpaka uniambie. Ila... mpaka Festus kukupeleka huko inaonyesha amekukubali sana," akasema hivyo.

"Kwa hiyo alikwambiaje?" nikamuuliza.

"Siyo mengi. Zaidi tu, jinsi ambavyo unafanya haya yote kwa sababu unampenda sana madam Bertha," akasema hivyo na kutabasamu.

Ahaa! Hapo sasa nikawa nimeelewa kwa nini madam alikuwa kwenye mood nzuri sana. Bila shaka Festo alimwambia kwamba ninampenda sana, na kutokana na jinsi alivyoaminiana na yule jamaa, nadhani maneno yaliyohusika huko kwenye maongezi yao ndiyo yalitosha kumfanya mwanamke huyu alegee namna hii kunielekea. Hapa udhaifu wake ukawa umeanza kuonekana wazi. Alihitaji kupendwa, na sasa ndiyo akawa ameona kuwa angekipata hicho kitu kutoka kwangu. Mchezo ukawa unaenda vizuri.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Dah! Kumbe jamaa na ye' naye mbea."

"Hahah... haongeagi ovyo, nilimlazimisha tu mpaka akaropoka. Nilifurahi tu kujua kwamba ulimaanisha yote uliyoniambia siku ile tuko bed. Umeanza kujiweka sehemu nzuri HB wangu. Keep it up," akaniambia hivyo kwa sauti tulivu lakini iliyoonyesha hisia.

Nikamshika shingoni kwake na kumkaribia usoni, kisha nikasema, "Chochote kwa ajili yako madam wangu."

Akatabasamu na kusema, "Mmm, usiwe cozy kupita kiasi. Bado unatakiwa uni-impress. Nilikwambia hili tako la gharama, unatakiwa kuendelea kupanda madaraja."

"Naelewa. Maneno hayatoshi. Ndiyo maana niko hapa. Nitajitahidi nisikuangushe," nikamwambia hivyo.

"That's my boy," akasema hivyo na kunirushia busu kwa ishara ya mdomo wake.

Nikatabasamu kiasi.

Akakaa vizuri zaidi na kusema, "Naelekea location kukutana na mtu. Mtumishi."

"Wa kilokole?" nikamuuliza.

"Yeah. Na yeye anahusika kupitisha madini. Naenda kumpanga," akasema hivyo huku akivuta mkoba wake.

"Dah! Kweli, Mungu walishagamwona kama boya," nikamwambia hivyo.

"Ahahah... ni kwa sababu ye' ni boya. Watumishi wake ndiyo wanahalalisha tu hilo," akasema hivyo.

"Ahahahah... ila Bertha!"

Akawa ametoa miwani yake ya urembo na kusema, "Me natoka sa'. Nakuacha hapa, au?"

"Oh no, naingia kule kitaa sa'hivi, labda nitarudi baadaye," nikamwambia.

"Poa."

Akasimama na kuvaa miwani yake, nami nikasimama pia.

"Vipi kuhusu... ile ishu ya Chalii, madam? Umemwangalia?" nikamuuliza.

Akatabasamu na kunishika shavu, naye akasema, "Usijali kuhusu Chaz. Hawezi kutusumbua. Sasa hivi utakuwa kwenye focus ya kazi yetu, basi. Umeelewa?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Twende. Nitakupanga kuhusu spot yetu mpya ya kazi baadaye..."

Baada ya mwanamke huyu kuniambia hivyo, akanipita na kuelekea nje, huku nami nikifuata nyuma yake taratibu.

Mambo yalikuwa yanajijenga upesi sana, na hivyo nilielewa haingechukua muda mrefu kwa huu mchezo wangu na madam Bertha kufikia ukomo. Lakini kutokea hapa ningepaswa kuwa makini SANA, kwa sababu ni pande nyingi zilikuwa zikihusika. Kumwagusha Bertha kusingekuwa kwa ajili ya kumuumiza yeye tu, bali na watu wake wengi aliojihusisha nao. Naongelea na huyo Festo.

Jamaa alikuwa anajua yule, na nilihofia angeweza kuwa mvurugaji wa mpango wangu kwa muda wowote ule kwa sababu alikuwa makini sana, kwa hiyo mimi ningehitaji kuwa hatua mbili mbele zaidi yake badala ya kusubiri tu mambo yaje halafu ndiyo nitoe itikio. Ningetakiwa kuhakikisha kwamba Bertha akianguka, aende chini pamoja na Chalii Gonga na Festo pia, na wasiwe na njia ya kurudi juu tena. Muda ndiyo ungeongea.

★★

Nikawa nimepewa lifti na madam mpaka kufikia maeneo ya Uhasibu kama tu siku ya juzi, naye akaniachia hapo na kuendelea na safari yake ya kwenda kumwona "mtumishi" wa kupitisha madawa. Nilikuwa nataka kwenda nyumbani kwetu kule kwanza ili nikawasalimu mama yangu pamoja na dada yangu, lakini kutokana na Bertha kunishurutisha nipande gari lake ili anilete huku, nikaona nighairi kwa leo. Sikutaka aanze maswali ya naenda kwa nani na kuanza kufatilia mengine asiyojua kunihusu, na ambayo sikutaka ajue.

Kwa hiyo, nikapanda usafiri ili nielekee Rangi Tatu kisha Mzinga, na nikiwa njiani nikaamua kumpigia mama yangu. Tukasalimiana vizuri, akiwa anaendelea salama tu toka mara ya mwisho tumeongea kwa simu, ndiyo nikamuulizia na dada yangu pia, Jasmine. Akasema kwa sasa Jasmine alikuwa akiendelea vizuri tu na kusubiri muda wake wa kujifungua ufike, ila ndiyo hakuwa na raha sana kutokana na matatizo yaliyokuwa yamempata wiki chache zilizopita.

Hivyo, nikaamua kuagana na mama na kumwambia ningekuja kwenda kuwasalimia, lakini Jasmine ningempigia pia ili tuongee kwa kina. Akasema hamna shida. Nikatulia kwanza ili nimpigie dada yangu nikishafika pale kwa Ankia, maana sikuona busara yoyote kuongea naye kwa marefu nikiwa ndani ya daladala.

Nimekuja kufika Mzinga ikiwa ishaingia saa nane ya saa tisa huko, hapo njaa ikiwa imenikong'oli vibaya mno, na nilielewa kukosa mlo wa asubuhi mara kwa mara ingekuwa na madhara ikiwa ningeifanya kuwa zoea maana ndiyo mlo muhimu zaidi, kwa hiyo nikaelekea pale kwenye ule mgahawa niliokaa na Miryam jana ili kupata chakula kwanza, halafu ndiyo ningejitahidi kuiboresha upya ratiba yangu ya ulaji mzuri baadaye.

Ugali wa nguvu, nyama, marage, mchicha, na maziwa, aaah mzee nikala kama vile nimepikiwa na mke kabisa. Hali nzuri ya nguvu mwilini ikarudi mahala pake baada ya kuwa nimemaliza msosi, nami nikalipia na kuanza kuelekea majumbani kwa Ankia. Nilipopita usawa wa Masai nikawa nimemwona Bobo pia, nasi tukasimama na kupeana salamu na maongezi ya hapa na pale, kisha ndiyo nikaendelea na safari mpaka nilipokuwa naishi.

Nilipoingia ndani, sikumkuta Ankia, bila shaka akiwa ameondoka kama alivyoniambia asubuhi na kusema tungeonana jioni, kwa hiyo nikaingia chumbani na kuanza kubadili mavazi ili niingie kwenye nguo nyepesi kwanza, halafu nimpigie dada yangu, kisha niende kujimwagia na kujiweka fresh nikaonane na binti Mariam.

Nikavaa T-shirt nyepesi na bukta, halafu nikafungua droo moja niliyokuwa nimekiweka kile kifaa cha piano, kinanda, ambacho nilinunua wiki chache zilizopita kule Kariakoo kwa ajili ya Mariam. Niliona kuanzia wakati huu ndiyo ingekuwa muhimu kuanza kukitumia pamoja naye, nami nikakiweka kitandani kwanza, kisha nikavuta simu na kumpigia Jasmine.

Dada yangu huyu alikuwa mtu wa mambo mengi sana kama tu mimi kaka yake. Yaani hata wakati huu aliokuwa na mimba ya miezi saba huko bado alipenda kujishughulisha na mambo mengi sana kwa sababu alipenda kufanya kazi, lakini hata zaidi wakati huu ni ile tu kutaka maisha yaendelee baada ya tatizo lake na aliyekuwa mume wake kuwafanya waachane.

Alipopokea na kuanza kuongea nami, ikabidi nikae kitandani kabisa na kumsikiliza kwa umakini. Alikuwa mwanamke mwenye hisia kali na za karibu sana, kwa hiyo akaongea vitu na mambo mengi sana ili kunifanya nimwelewe kwa undani wa mambo yote aliyopitia. Nikampa pole na kumwambia kwamba ningekuja kuonana naye hapo hapo nyumbani ndani ya siku hizi hizi mbeleni, na kumshauri ale vyakula fulani kuilinda afya ya mtoto, na kujitahidi kupumzika vya kutosha.

Akawa hana neno, akisema tu alikuwa amenikosa sana, na nilipokuwa nataka kumwambia nimem-miss pia, nikasikia mlango wa kuingilia kule sebuleni ukigongwa kuashiria mgeni alikuwa amefika. Kwa hiyo nikaagana vizuri na Jasmine na kurudia kumwahidi kwenda kumwona, kisha ndiyo nikatoka kwenda kufungua mlango ili nimsikilize mja aliyefika.

Ile nafungua mlango nikiwa na uso makini tu, nikajikuta nauyeyusha umakini wote baada ya kuona ilikuwa ni bibie Miryam! Yaani huyu mwanamke alikuwa ananikamata nyakati ambazo sikumtarajia kabisa. Akaachia tabasamu hafifu la kirafiki, nami nikatabasamu pia.

"Za sa'hizi?"

Kasauti kake katamu kakanipa salamu hiyo laini, lakini sikutoa jibu na kubaki kumtazama tu machoni.

"Za sa'hizi kaka?" akarudia tena.

Nikavuta pumzi upesi na kusema, "Nzuri... ni nzuri. Karibu."

"Asante. Nimekuja tuongee mara moja, kama hauko na... kazi labda...."

"Oh, sina kazi yoyote, karibu. Ingia," nikamkaribisha.

Akavua ndala zake za kike na kunipita, nami nikaivuta harufu ya marashi iliyotoka mwilini mwake kwa umakusudi kabisa wa kuisikilizia. Alikuwa amevaa ile Punjabi yake ya zambarau, huku nywele zake ndefu akiwa amezibana juu ya kichwa. Zilikuwa lainiii, yaani dah! Kuziangalia nyuma ya shingo yake zilifanya nitamani hata kuzigusa na kuzilaza-laza kama manyoya ya mnyama kipenzi, lakini nikaachana na mawazo ya kishetani na kufunga mlango tu.

"Nimekuona wakati unaingia hapo nje, nikasema nije ili tuongee kidogo," akasema hivyo akiwa amesimama bado.

"Kumbe? Nimepita kama upepo yaani, hata sikukuona. Karibu ukae," nikamwambia hivyo.

Akakaa sofani huku akitabasamu kiasi, nami nikakaa pembeni yake pia. "Za mizunguko?" akauliza.

Huku nikiwa nasugua goti langu kwa kiganja, nikamwambia, "Nzuri tu. Nilienda Makumbusho hapo mara moja kuonana na rafiki, ndiyo nimeingia mida hii. Nilikuwa ndo' nataka nije kumwona Mamu. Yupo?"

Akatabasamu na kusema, "Yupo. Ndiyo amemaliza kula mida hii."

"Okay, itabidi nimwahi, maana najua anapendaga kulala mchana pia. Vipi dawa anazokunywa lakini?"

"Anaendelea kunywa. Hapendi sana dawa, inabidi kulazimisha... lakini zinaenda," akasema hivyo.

"Ahah... angalau. Na wewe... haujaenda kazini?"

"Nimeenda asubuhi, leo nimewahi tu kurudi. Nilikuwa nataka niwepo pia ukija, nilifikiri ningefika kukuta mmeshaanza, kwa hiyo... nafurahi nimewahi..."

"Sawa kabisa. Wote tukiwepo na kutoa support kama hivyo, itamzidishia hali ya uchangamfu na kujiamini zaidi. Mwishowe hiyo kitu itaondoka maishani mwake. Ni suala la muda tu," nikamwambia hivyo.

Akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Yeah."

Akawa ameingiza mkono wake kwenye mfuko wa nguo yake ya juu na kutoa bahasha fupi iliyokunjwa na kisha kuielekeza kwangu, nami nikamtazama machoni.

Akasema, "Ninataka kushukuru kwa kusaidia kulipia bili ya Mamu kwenye ile hospitali ya mwanzo. Na ilikuwa kubwa, ulilipia dawa na vipimo vyote yaani... nimeona nikurudishie tu kwa sababu unafanya mambo mengi sana kwa ajili yetu. Asante sana, ila pokea tu hii. Itakuwa kama tulisaidiana wote... kulipia."

Nikabaki namwangalia tu kwa umakini. Ule umakini kwa makusudi yaani.

Akasema, "Acha kuniangalia hivyo bwana. Usifikirie vibaya, ni... shukrani tu."

Nikaendelea kumkazia macho.

"Wewe, jamani..." akaongea kwa njia iliyoonyesha hakupenda nilivyokuwa namwangalia.

Nikacheka kwa pumzi na kuangalia pembeni, kisha nikasema, "Inaonekana mpaka leo bado hujanielewa tu."

Akashusha macho yake kwa njia ya kukwazika kiasi.

Nikamwangalia na kusema, "Acha kufikiria kwamba unahitaji kunilipa Miryam. Nakuelewa. Ila sihitaji malipo, nimeshakwambia. Mamu... Mamu atapona. Ninachotaka kuona zaidi kuliko mambo yote ni Mamu akipona. Hayo ndiyo malipo nayotarajia, na yatafanikiwa kwa sababu wote tutashirikiana ili kumsaidia. Yakitimia, nitaridhika."

Akawa ananiangalia kwa utulivu tu.

"So... hiyo weka pembeni. Ukitaka itumie, we' itumie kwa mambo mengine tu, ila siyo mimi. Kofi ulilonitandika siku ile lilinitosha," nikamwambia hivyo kiutani.

Midomo yake ikajikunja akijaribu kuzuia tabasamu, lakini akashindwa na kuangalia chini huku akicheka. Alipendeza sana kiasi kwamba mpaka nikajikuta namtazama tu huku nikitabasamu kwa hisia.

Akaniangalia na kusema, "Sa' si ndiyo uchukue hii iwe kama pole?"

"A-ah, lile kofi lilikuwa zawadi, hujui hilo?"

"Kivipi?"

"Ndiyo liliniongezea moto mpaka tukafanikiwa kum-nab kaka yako. Kwa hiyo silalamiki, ninakushukuru," nikamwambia kwa uhakikisho.

Akaonekana kutafakari kitu, kisha akasema, "Nikuombe jambo fulani tafadhali."

"Ndiyo. Niambie..."

"Kuanzia wakati huu... sitotaka... yaani, usimwongelee tena huyo mwanaume. Hata tu kumwita kaka yangu... sitaki tena," akasema hivyo.

Nikamwangalia usoni kwa uelewa mpana wa kile alichomaanisha, nami nikamwambia, "Sawa. Nimeelewa."

"Nataka kuanzia sasa... kila kitu kiwe ni focus ya kumfurahisha mdogo wangu ili akae sawa zaidi. I'll contribute on anything required to help you help her," akasema hivyo.

"Wow! Tesha hakukosea. Unaongea kiingereza vizuri," nikamwambia hivyo.

Akatabasamu huku akinitazama kwa utulivu.

"Uko sahihi. Kikubwa sasa hivi itakuwa ni furaha ya Mamu, so mambo yote yenye kuvunja moyo yatatakiwa kutupwa bin... iwe kama hayajawahi kutokea. Mariam... ana-progress haraka sana, haitachukua muda mrefu atakuwa sawa kabisa," nikamwambia.

"Sawa. Ubarikiwe sana."

"Amen."

"Mhm... sasa hivi ndiyo nataka kwenda sambamba na kila kitu mtakachofanya ili nihusike kwa lolote, na... nijue naweza...."

"Miryam... usijali. Nimeshakuelewa," nikamwambia hivyo kwa kumtuliza.

Akatabasamu kiasi na kuangalia chini, nami nikawa namwangalia kwa upendezi. Yaani haka kahali kote kalikuwa kanafanya damu yangu irukeruke tu sijui hata kwa nini!

"Unajua sina namba yako?" akasema hivyo.

"Ih, kweli? Ahh hata me sina ya kwako mpaka leo..." nikamwambia hivyo.

Akasema, "Jamani! Yaani, utafikiri tulikuwa maadui..."

"Eti! Yaani hata namba tu?" nikamwambia hivyo, nasi kwa pamoja tukacheka kidogo.

Akarudisha bahasha mfukoni na kutoa simu yake, naye akanipatia akiwa ameweka sehemu ya kuandikia namba huku akisema, "Sasa hivi mambo yatabadilika. Nataka tuwe marafiki."

Nilikuwa nimeshaanza kuandika namba yangu kwenye simu yake aliposema hivyo, nami nikawa natabasamu kiasi baada ya kusikia kauli yake ya kutaka tuwe marafiki. Nikamrudishia simu, naye akaipigia namba hiyo. Simu yangu ikaita, nikiwa napewa namba ya bibie Miryam rasmi kwa mara ya kwanza kabisa na yeye mwenyewe, nami nikaitunza kwa jina lake.

Nikamwangalia usoni kukuta ananitazama kwa utulivu, nami eti nikaingiwa na haya na kutazama pembeni kisha kutabasamu kidogo.

"Nini?" akauliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kuonyesha hakuna kitu, kisha nikamwangalia tena.

"Mbona unatabasamu sana? Nini kimekufurahisha?" akaniuliza na sauti yake tamu.

"Sikuwahi kudhani... yaani, ungetaka tuwe marafiki. Nilikuwa nakuona wa kivyako mno, au labda unanichukulia kuwa siko..."

"Usiwaze hivyo tena. Hayo yamepita. Sisi ni marafiki sasa, sawa?" akanikatisha kwa kusema hivyo.

"Sawa. Lakini unajua nini?"

"Niambie."

"Toka tumejuana... sijawahi kukusikia ukilitaja jina langu," nikamwambia hivyo.

Akatabasamu huku akitazama pembeni.

"Yeah. Sijawahi kabisa. Huwa unaniita tu kaka, kijana, we' kaka... wewe..."

Akacheka kidogo kwa furaha.

"Tukiwa washka... ah, namaanisha, marafiki... nitapenda kusikia ukiniita kwa jina langu," nikamwambia hivyo huku nikitabasamu.

Akasema, "Haina shida. Nisamehe kwa kukuita hayo majina wakati huo, ila... sijawahi kutaja jina lako kwa sababu silijui."

Ka!

Kauli yake ikanifanya nimtazame kimaswali kiasi, nami nikamuuliza, "Hulijui jina langu?"

"Yeah," akajibu.

"Yaani... unatania, au? Maana, nakuja hapo kwako... unawasikia kabisa warembo wangu wanasema 'JC karibu,' 'JC za nyumbani?' 'JC hivi, JC vile...' halafu unaniambia hujui naitwa nani? Kweli Miryam?" nikamuuliza kwa kusuta.

Akacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "Najua hilo siyo jina lako, hicho ni kifupi tu, ama nickname, kama wao wanavyoniita mimi 'Mimi!'"

Aliongea kwa njia ya masihara, lakini kauli yake ikanifanya nimtazame kwa njia makini kiasi.

"Nitapenda nikikuita kwa jina lako kabisa. Kama wewe unavyoniita 'Miryam,'" akasema hivyo.

Dah!

Nikaangalia tu chini kiasi nikiwa natabasamu. Bila kutambua, mwanamke huyu alikuwa amegusa sehemu fulani ya maisha yangu ambayo mpaka sasa bado sijaiweka wazi, na kauli yake ilifanya niikumbuke. Alinifanya nihisi raha ya kina sana, ile raha kama ya wimbo wa Bebe Rexha 'say my name.' Hehe! Hapa uhondo ndiyo ulikuwa umeanza.

Nikamwangalia usoni tena, naye akasema, "So... ukitaka nikuite kwa jina lako, niambie unaitwa nani."

Nikatabasamu kiasi, kisha nikamwambia, "Naitwa Jayden."

Akatabasamu pia, kisha akasema, "Jayden..."

Ah! Jina langu ndani ya hiyo sauti? Ilikuwa kama vile limeimbwa!

"Sawa. Me sitakuita JC. Nitakuita Jayden. Kama Jaden Smith," akasema hivyo.

"Ahahah... Tesha si amesema hauangaliagi movie, hilo jina umelijuaje?" nikamuuliza kiutani.

"Tesha anaongea mno, najua vitu vingi pia, siboi sana kama mnavyofikiria," akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kwa hisia.

Akaninyooshea kiganja chake na kusema, "So Jayden... friends?"

Dah! Sikufikiria huyu dada angekuwa na uzungu mwingi namna hii, lakini ulimfaa, na alipendezea sana. Nikakishika kiganja chake pia na kuviunganisha kwa pamoja ili kukubali mwaliko wake wa kuwa marafiki rasmi.

"Friends," nikamwambia hivyo.

Tukaendelea kuangaliana kwa upendezi mwingi sana, nikiwa najihisi vizuri mno kupata ukaribu na mwanamke huyu baada ya misukosuko yote aliyopitia na familia yake siku chache nyuma. Nilitazamia mengi mazuri yaje kutokana na uhusiano huu mpya niliokuwa nimejipatia kwa huyu mwanamke, ambayo yangesaidia kumweka huru mdogo wake kutokana na tatizo alilokuwa nalo. Na kilikuwa ndiyo kitu nilichokitamani sana tokea siku ya kwanza kabisa nilipokutana naye.

Sasa huu ndiyo ungekuwa mwanzo wa mambo mengi ambayo yangebadili maisha yangu mimi, na Mimi.

END OF SEASON ONE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★
 
Sawa mkuu ila sijui kwanini ?? Mimi kila kipande nisomacho najikuta tu natamani J.C ale mbususu ya miryam mapema ... Yani wanavyokawia kawia hivi nahisi madam bertha anaweza akaharibu jambo hili lisitokee ...
 
Acha matusi ww .. aah bwana JC ..ah ety jc sorry bwana Elton Tonny msamehe huyu bure bro kk..
 
Yani nimenunua na bia kabisa alafu naona hamna kitu
 
Elton Tonny

MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Nilikuwa ndani ya hisia nzito sana ya furaha na faraja iliyofanya nisitambue upesi kwamba chozi lilinitiririka mbele ya watu hawa wote, ndipo nikawatazama kwa ufupi na kukuta wote wanatuangalia mimi na Mariam kwa hisia sana. Ni Miryam ndiye aliyekuwa akidondosha machozi pia huku akijifunika mdomo kwa kiganja chake, nami nikawa nimemwona daktari akija upande wetu pamoja na muuguzi.

Nikajifuta chozi upesi na vizuri sana ili Mariam asione kwamba nilikuwa nimelia wakati nimemkumbatia, kisha nikamwachia taratibu na kumwangalia usoni. Alikuwa ametazama chini tu, huku bado nikiona shida yake ya kutetemeka kichwa kiasi ikiwepo kwa wakati huu shauri ya mishtuko aliyokuwa amepitia, lakini nilikuwa nimefarijika kwamba angalau maendeleo ya utimamu wake hayakuwa yamepotea. Alinisemesha vizuri sana.

Huyo daktari alikuwa ni mwanamke mtu mzima, mnene kiasi, mweusi na mrembo pia, akiwa amekuja ndani ya wodi hii kuangalia wagonjwa wote, na baada ya kufikia sehemu ambayo Miryam na Ankia walikuwa wamesimama, akatusalimu wote kwa njia nzuri na kuuliza hali ilikuwa vipi kumwelekea msichana huyo aliyekuwa ameletwa jana.

Bi Zawadi ndiyo akamwambia kwamba yaani siyo muda mrefu tu binti Mariam alikuwa ametoka kusema maneno fulani ya "kizungu" baada ya kuniona mimi, ambaye alikuwa amenizoea sana kutokana na kumsaidia kabla ya kuletwa hospitalini hapa hiyo jana.

Daktari huyu akaja karibu yangu na Mariam, nami nikampisha. Akajaribu kumsemesha binti, akimuuliza hiki na kile, na Mariam akawa anajibu aidha kwa kutikisa kichwa au kuchezesha mabega, lakini hakusema neno lolote kwa daktari huyo wala kuonyesha hisia. Kwa hiyo daktari akafanya kuangalia utendaji wake wa mapigo ya moyo kwa kumpima, kisha akasema itakuwa sawa tu kwa binti kuondoka hospitali leo leo jioni, kwa kuwa afya yake iliruhusu.

Lakini akasema kuna dawa atatakiwa kutumia ili kutuliza zaidi msukumo wake wa damu, maana ingawa alikuwa na umri mdogo lakini presha yake kupanda kwenye damu ilikuwa kali mno; hasa kutokana na hali yake yeye kama yeye na yale aliyokuwa amepitia. Kuna mambo ya kina zaidi akawa amesema atahitaji kuzungumza na Miryam, hivyo akasema tunaweza kupata mlo upesi kisha dada mtu aende kuonana naye.

Baada ya hapo daktari akasepa, akimwacha muuguzi anasaidiana na wanawake kumbadilishia binti mrija wa mkojo, na sisi wanaume tukasogea pembeni kwanza. Miryam akanifata mimi na Tesha, naye akaniambia kwamba, ukifika wakati wa kwenda kumwona daktari ili kuzungumza naye kwa kina, niende pamoja naye. Akaniweka wazi kuwa inaonekana mazungumzo hayo yalielekea ishu ya vipimo vya ndani zaidi mwilini mwa Mariam kuona ikiwa binti alikuwa ametendewa vibaya kimwili, nami nikawa nimekubali kuambatana naye muda huo ukifika.

★★

Basi, baada ya Mariam kusaidiwa kufanya usafi, sote tukajiunga pamoja naye na kuanza kupata mlo pamoja. Kulikuwa na vyakula mbalimbali, dada mtu akiwa amenunua kama vyote utafikiri aliviiba kwenye tafrija, lakini binti alikula zaidi nyama ya kuku na kitimoto kwa sababu alizipenda sana.

Kuwa naye kwa wakati huu, sisi wote yaani, ilimfanya Mariam ajihisi salama, anapendwa, na hivyo ikawa rahisi kwake kuonyesha hamu aliyokuwa nayo kwenye kula vyakula alivyofagilia. Miryam angemlisha na kumtendea kama vile ana miaka miwili yaani, nasi sote tukaendelea kupeana ushirika mzuri hadi saa za kutembelea wagonjwa zilipokata na baadhi ya wauguzi kuja kutufukuza. Kistaarabu lakini.

Najua Miryam alikuwa akitumia pesa nyingi sana kumweka mdogo wake katika haya mazingira, na najua asingeacha kufanya yote awezayo ili hali nzuri kwenye pande zote za familia yake irejee.

Mpango kwa hapo ikawa kwamba Shadya abaki kumpa binti uangalizi, halafu Miryam angewarudisha mama zake wakubwa pamoja na Ankia nyumbani, kisha baadaye ndiyo bibie angerudi na kumchukua mdogo wake ili wampeleke nyumbani. Hakukuwa na makolokolo mengi wala ya kubeba, na Shadya alikuwa mwenye utayari sana kubaki na kusaidia kwa lolote lile ili kuiunga mkono familia hii.

Lakini kwanza, mimi na bibie Miryam tulihitaji kwenda kuzungumza na yule daktari, kwa hiyo tulipotoka kwa pamoja tulienda na kumtafuta, na baada ya kumpata, tukakaribishwa ofisini kwake na kuzungumza. Alikuwa ameshafahamishwa kuwa mimi ni daktari pia nayemsaidia binti kupambana na tatizo lililofanana na ASD, lakini sasa akawa ametuongezea ishu nyingine.

Akatuambia kwamba shida yake inayofanana na ASD ilitokana na kitu kinachoitwa kwa ufupi PTSD, hali fulani ambayo husababishwa na mshtuko au msongo mkubwa kutokana na matukio mabaya yanayoweza kumpata mtu maishani mwake. Kwa Mariam, ilikuwa ni kitu kilichosababishwa na maumivu ya kuwapoteza wazazi wake, lakini baada ya kilichompata juzi, hicho kiwango cha PTSD kilikuwa kimepanda, na hivyo angehitaji kusahaulishwa mambo hayo haraka iwezekanavyo, kwa njia zozote zile yaani ingehitajika binti aishi kwa amani kuu na furaha tele kutokea hapa.

Tukiwa watu wake wa karibu bila shaka tulijua mambo yapi ambayo binti alifurahia, na daktari akasema ameona hata leo binti aliitikia upesi ujio wangu kwa njia chanya ingawa bado anaumia, kwa hiyo mtu kama mimi sikupaswa kabisa kuondoka kwenye maisha yake. Hilo lingemsaidia haraka maana alikuwa na umri mdogo bado, kwa hiyo kiwango chake cha kuwa imara kingeongezwa nguvu kupitia mambo mengi mazuri aliyopenda, na kumjengea kumbukumbu bora ili utimamu wake uimarike pia kadiri siku zilivyosonga. Somo likawa limeeleweka.

Kuhusu ishu ambayo baada ya kumpima binti Mariam kuthibitisha ikiwa alikuwa amebakwa, haikuonekana kwamba hilo lilitokea, alikuwa safi kabisa, isipokuwa tu tungepaswa kuendelea kumwangalia kwa ukaribu zaidi maana huwezi kujua sikuzote. Angeweza kuwa hajachubuka na nini, ila kuna uwezekano alikuwa ameingiwa kwa njia ambayo haikuonekana wazi.

Jambo hili lilimtatiza sana Miryam, ambaye hakujua hayo yote yanamaanisha nini, na ni nini kinahitajika kufanywa. Kutokana na daktari huyo kuhitajika haraka kwenda kwa mgonjwa, akawa ameniomba nimweleweshe tu bibie Miryam baadaye, ila akamtia moyo kuwa asihofu; kila kitu kingekuwa sawa. Akatutakia heri na kutuaga.

Tukiwa tunaenda kujiunga na wengine, nikamwambia Miryam kwamba tungekuja kulizungumzia suala hilo baadaye ili nimweleweshe vizuri juu ya mambo yaliyohitajika kufanywa kutokea hapo, na la muhimu lingekuwa kukazia fikira zetu zote kumsahaulisha binti mambo mengi mabaya yaliyotokea juzi, na nikamwomba awasihi watu wa familia yake na hata marafiki wa karibu wasije kukaa na kuzungumzia vitu kama hivyo huku na binti akiwa pamoja nao, naye akaridhia hayo yote. Yaani Mariam ndiyo alikuwa kama yai letu, ingekuwa ni "kum-handle with care!"

★★

Baada ya kuwa tumemwacha daktari, Miryam aliwapeleka wanawake wengine nyumbani, huku mimi na Tesha tukiamua kwenda sehemu nyingine kutulia mpaka muda ambao Mariam angerudishwa kwao. Hakukuwa na lolote la maana sana kufanya, ila kwa mida ya saa tisa mchana kulikuwa na mechi ya kimataifa kati ya Taifa Stars na nchi gani sijui ya wazungu huko, kwa hiyo tukaenda tu kwenye pub moja maeneo ya Zakhem na kukaa hapo kuitazama ili kuua muda.

Tesha alitaka kunywa kidogo kwa hiyo akanunua bia mbili tu, na alitaka kuninunulia pia ila nikakataa; nikipendekeza tu niletewe soda, basi. Tukawa tunaongea mawili matatu, akiniambia ni namna gani alivyokuwa amehuzunishwa sana na mambo yote yaliyokuwa yametokea kwenye familia yake, ila alifarijiwa sana na msaada wote niliokuwa nimeutoa kwao.

Aliona kwamba bila mimi kiukweli kwa sasa angekuwa ameshazikwa, hivyo alihisi ana deni kubwa mno la kunilipa ambalo hakudhani angewahi kufanikiwa kulipia. Lakini akasema kwa lolote lile kuanzia sasa na kuendelea, nijue tu kwamba kama ningemhitaji, asingesita kuniunga mkono kwa asilimia zote. Yaani lolote lile. Nikamshukuru tu na kumwambia asiwe na hofu, la muhimu kutokea hapa ni kufanya kila kitu ili kumweka Mariam sehemu nzuri tena, naye akasema hilo ni uhakika.

Imefika mida ya saa kumi na moja baada ya mechi kuisha, tukaondoka maeneo hayo na kutembea mpaka Rangi Tatu. Tesha akawa amemtafuta dada yake kuuliza yaliyoendelea, naye Miryam akamwambia kwamba alikuwa amesharudi hospitalini mida hii hii kumchukua mdogo wake. Tesha akasema sawa, yuko pamoja nami hivyo tungekutana wote nyumbani baada ya muda mfupi.

Alipoagana na dada yake, Tesha akapendekeza tutembee taratibu tu kutokea hapo mpaka Mzinga ikionekana kuwa njia nzuri ya kukata wakati mpaka kufika kwao. Sikuona shida yoyote kukubaliana na wazo hilo, kwa hiyo mdogo mdogo tukaendelea kushuka. Katika maongezi mawili matatu Tesha akawa amenikumbusha kuhusu yule mwanadada aitwaye Dina, ambaye tulienda kule Uhasibu siku kadhaa nyuma kumtembelea.

Akasema anawasiliana naye sana, na hata hii ishu ya kutekwa juzi alikuwa amemwambia na Dina akasema angekuja kuwasalimia. Lakini Tesha akagusia namna ambavyo kila mara alipowasiliana na Dina, mwanadada huyo alipenda sana kuniulizia, na mara nyingi Tesha alimtania kuhusu kunitaka ila akawa anajihami.

Ila ilikuwa wazi kwamba Dina alitaka Tesha aniunganishe kwake, na sasa ndiyo jamaa akaniambia nimfikirie huyo rafiki yake endapo nikihitaji poza roho kuondoa misongo kibao. Nikamwambia tu ningeangalia na jinsi ambavyo mambo yangekwenda maana kwa sasa, akili yangu yote ilikuwa kwa Mariam, Mariam, Mariam, na Bertha kama ketchup pembeni. Basi.

★★

Tumekuja kufika kwao Tesha imeshaingia saa kumi na mbili kuelekea giza la saa moja, nasi tukawakuta wapendwa wetu wote wakiwa hapo; kutia ndani na Ankia. Mariam alikuwa amekaa pamoja na Miryam kwenye sofa moja, na baada ya kuniona tu, binti akaonyesha wazi kwamba alifurahia ujio wangu hapo kwa kunigeukia vizuri zaidi na kunitazama kama vile anataka kunisemesha, naye Miryam akaniambia nikae karibu yake ili bila shaka binti ajisikie vizuri.

Nikakaa pamoja na Mariam na kuanza kumsemesha hiki na kile, huku Miryam pia akiniunga mkono kwa kuongea pamoja nasi ili kumfurahisha mdogo wake, na ingawa Mariam hakuzungumza lolote lile lakini alionekana kuwa na amani sana. Upendo mwingi ambao angeupata kutokea hapa ungemsaidia sana huyu binti, na kila mmoja alionyesha kutaka hilo lifanikiwe kwa asilimia kubwa.

Mambo yaliyoendelea baada ya hapo ikawa ni kupata mlo wa pamoja tena ambao uliandaliwa na Shadya, Ankia, na bibie Miryam mwenyewe, nasi tukamaliza na kuendelea kukaa pamoja hadi kufikia saa nne. Usingizi wa mtoto ukawa umemvuta Mariam mapema, hivyo Miryam akamwongoza kuelekea chumbani ili akanywe dawa kwanza kisha ndiyo alale. Kalikuwa hakataki kuniacha kutokana tu na jinsi kalivyoniangalia wakati dada yake alipokasimamisha ili waende chumbani, lakini hatimaye wakawa wametuacha.

Muda uliposogea mpaka kuingia saa tano, Ankia akaona aage ili mimi na yeye tuelekee pale kwake kwa ajili ya mapumziko. Kwa mara nyingine tena, Bi Jamila na Bi Zawadi wakatoa shukrani za dhati kunielekea kwa sababu ya kuamua kubaki Mzinga ili kumsaidia binti yao, nami nikazipokea baraka zao kwa uthamini.

Nikawaambia wote kuwa kesho ningejitahidi kuja pia ili nicheze na binti taratibu kama ilivyokuwa mwanzo, isipokuwa zamu hii ingekuwa kwa njia tofauti kiasi. Njia tata zaidi ya mwanzo. Hawakuwa na neno.

Baada tu ya Miryam kuja sebuleni tena, mi' na Ankia tukanyanyuka ili kuondoka sasa, na tukawa tumemuaga bibie pia. Miryam akasema sawa na kuashiria kutaka kutusindikiza nje, hivyo tukaelekea mpaka kibarazani tukiambatana na Tesha pia. Ardhi iliyopambiwa vitofali vidogo-vidogo ya hapo nje ilionekana kulowana kiasi, kitu kilichomaanisha mvua ilikuwa imeshuka kidogo muda ambao tulikuwa ndani, na sasa ilikuwa imekata.

"Kaka, nazisubiri hizi mvua kwa hamu sana. Zipige haswa yaani," Tesha akaniambia hivyo.

"We! Usiombe hivyo. Hatutaki mabalaa mapema sisi. Kama kunyesha zinyeshe, lakini kawaida," Ankia akamwambia huku akivaa ndala zake.

"Haupendagi mvua Ankia..." Miryam akamwambia huku anatabasamu.

"Kwa kweli me mvua a-ah. Yaani ingekuwa bora tu... anga... mawingu yatande, lakini maji yasishuke," Ankia akasema.

"Mmmmm, unajua kujishaua wewe!" Tesha akamwambia.

"Ish, hivi unafikiri?" Ankia akasema.

"Kinachofanya usipende mvua kubwa ni nini?" Tesha akamuuliza Ankia.

"Radi na matope," nikamwambia.

"He! JC umejuaje?" Ankia akauliza.

"Nimekisia tu," nikamwambia hivyo.

"Afu' radi siyo Ankia tu, hata da' Mimi. Ahahah, siku ipige mvua ya maana na radi, unamkuta dada chini ya uvungu!" Tesha akasema hivyo, nasi tukacheka kwa pamoja.

Miryam akampiga Tesha kidogo begani huku akitabasamu, naye akasema, "Me siyo mwoga kihivyo bwana."

"Tulia, nitakuja nichukue mkanda tu," Tesha akamwambia.

Ankia akapiga mhayo kidogo na kusema, "Haya jamani, sisi tuwaache sasa. Tutatembeleana na kesoow."

"Yeah, ila... nilikuwa nataka niongee kidogo na..." Miryam akasema hivyo na kunitazama.

"Ahaa, sawa. Me ngoja nitangulie sa' JC," Ankia akaniambia.

"Haya," nikamwambia.

"Twende nikusindikize wewe, usije ukabebwa hapo nje," Tesha akamwambia Ankia huku naye akivaa malapa yake.

Nikabaki hapo kibarazani pamoja na bibie Miryam tukiwaangalia wawili hao walipokuwa wakielekea geti, kisha ndiyo akasema, "Hatujaongea kuhusu ile ishu aliyoisema daktari muda ule."

Nikamwangalia na kusema, "Ee ndiyo, kuhusu Mariam..."

"Yeah."

Nikamwambia, "Okay. Yaani ni kwamba, unakuta sometimes... mwanamke kama hivyo anaweza akawa ameingiwa vibaya, lakini kusiweze kuonekana michubuko au chochote kinachoweza kuashiria kwamba force imetumika. Kuna hiki kipimo wanaita colposcopy, ndiyo wametumia kumpima nafikiri... maana huwa kinaangaza hadi sehemu za ndani zenye uwezekano wa kuumia... kama tu camera ndogo na safi..."

Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

"Yeah. Sasa, kwa maelezo ya daktari, inaonekana hicho kipimo hakija-detect tatizo lolote lile kabla ya... kabla ya huyu msichana kuingiwa vibaya, ila kwa Mariam ninaamini yuko safi. Ambacho tu tunatakiwa kuangalia ni ikiwa uwezekano, yaani... IKIWA TU uwezekano upo kwamba aliingiwa, na hicho kifaa hakija-detect, basi ndiyo atapaswa kufanya routine ya vipimo ili kuwa na uhakika zaidi," nikamwelezea.

Akaonekana kutafakari maneno yangu, naye akauliza, "Kwa hiyo ni kama kusema, vipimo vinaonyesha mdogo wangu yuko safi kwa asilimia 70, ila kwa kuwa hatuna uhakika wa hizo 30, ndo' anatakiwa kuendelea kupima?"

"Uko sahihi. Ila nina-bet asilimia 99 Mariam yuko safi. Hiyo moja tu ndiyo tunatakiwa kuihakikisha," nikamwambia hivyo kwa kufariji.

Akatabasamu kiasi na kutikisa kichwa kuonyesha uelewa, naye akasema, "Sawa. Kwa hiyo, hiyo routine itaendaje?"

"Mmmm... nafikiri tufanye hivi. Baada ya wiki moja, mpeleke akapime baadhi ya magonjwa ya STI. Si unaelewa?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Wiki ya pili, mpime mimba. Ya tatu, mpime vitu kama... Syphilis, hepatitis... na HIV. Yaani ndani ya huu mwezi mmoja mbeleni ndiyo tutakuwa na uhakika wa asilimia zote kwamba yuko sawa kabisa akishapimwa namna hiyo. Na... hatakiwi kuambiwa chochote kuhusu haya, yaani... asije kubaki anakumbukia tu... yaliyotokea," nikamwambia.

Miryam akashusha macho yake kwa njia iliyoonyesha huzuni.

"Miryam... uko sawa?" nikamuuliza kwa upole.

Akaniangalia na kusema, "Ee, niko poa. Ila haya yote... yaani sometimes nawaza tu kama ningekuwa nimekusikiliza na kuchukua hatua mapema, haya yote yasingetokea. Part kubwa ya maumivu ya Mamu nimeisababisha. Na ninaogopa..."

Nikamwangalia kwa uelewa, nami nikamwambia, "Haina faida kujilaumu Miryam. Sasa hivi la muhimu ni hali njema ya mdogo wako, na ninajua atakuwa sawa tu. Haya tunayafanya ili kuwa na uhakika... kuweka tahadhari tu, na ni ya muhimu. Huu mwezi ukishapita, yatabaki kuwa historia."

Akatikisa kichwa kukubaliana na hilo, naye akasema, "Asante."

Nikawa nimewaza kitu fulani, nami nikamuuliza, "Vipi kuhusu... Joshua, na Khadija? Umeshasikia lolote kuwahusu?"

Uso wake ukageuka na kuwa makini kiasi, naye akasema, "Sijasikia. Na sitaki kujua lolote kuwahusu."

Aliongea kwa sauti tulivu lakini ilisikika kwa njia iliyoonyesha uchungu wa aina yake, nami nikatikisa tu kichwa kuonyesha nimemwelewa.

"Kwa hiyo... kesho utakuwa na..." Miryam akawa anataka kuniuliza kitu fulani lakini akaacha baada ya Tesha kuwa amerejea tena.

"Kesho nitakuja ndiyo. Aa, kuna sehemu naenda asubuhi, kwa hiyo mida ya baadaye tutakuwa pamoja na Mamu," nikasema hivyo baada ya Tesha kufika karibu.

Miryam akasema, "Sawa."

"Ankia ashalala, eti?" nikamuuliza Tesha.

"Hamna, hajadondo bado. Anakusubiria," Tesha akasema hivyo na kunipandishia nyusi zake kimchezo.

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Sawa, tutaonana kesho. Usiku mwema."

"Usiku mwema mwanangu," Tesha akasema hivyo na kugonga tano pamoja nami.

Nikiwa nimeanza kuvaa viatu vyangu, Miryam akasema, "Usiku mwema."

Nikamwangalia usoni kwa sekunde mbili tatu hivi, ile kitu tunaita "ku-admire" sura ya mtu mwingine ikiwa ndiyo naifanya wakati huu, nami nikamwambia, "Na kwako pia."

Kisha baada ya hapo nikaondoka na kuelekea upande wetu ili kupumzika mapema, kwa sababu nilikuwa nimefikiria kufanya jambo fulani mapema ya kesho kabla sijarejea tena kwenye familia hii ili niendelee kumsaidia Mariam. Ingekuwa ni muhimu sana, kwa hiyo nilipoingia tu kwa Ankia sikujizungusha na mengi; ikawa ni kuvua, kwenda kujimwagia kwanza, kisha ndiyo nikaagana na mwenye nyumba wangu na kuingia kulala.

★★★

Asubuhi ya Jumatatu hii haikukawia kufika, mpaka nikahisi ni kama vile nilifumba macho na kufumbua papo hapo pakawa pamekucha. Ni kwamba tu inaonekana mwili ulikuwa umechoka mno, na usiku wa kuamkia sasa ndiyo uliokuwa mrefu zaidi kwangu kulala kwa amani, maana nilimaliza utaratibu mzuri wa kusinzia wa masaa nane kabisa mpaka kuja kuamka mida hii ya saa moja.

Nikajitoa kitandani, na leo nilikuwa nimewahi hadi kumkuta Ankia akiwa kwenye taratibu zake za usafi. Na kalipenda kweli kusafisha vitu hata kama hakukuwa na uchafu. Tukasalimiana vizuri, akiwa anauliza sababu iliyofanya leo niwahi mno kutoka chumbani, ndiyo nikamwambia kuna sehemu nataka kuelekea kwanza kabla ya kuja kutumia muda pamoja na Mariam wangu. Akasema hata yeye pia angetoka baada ya kunywa chai, kwa hiyo labda tungekuja kuonana jioni.

Baada ya hiyo kwenda, nikaelekea nje na kufanya usafi wa mwili kama kawaida yangu, kisha ndiyo nikaingia chumbani na kuanza kujiandaa. Nikavaa vizuri kwa mtindo wangu wa kwenda kwa Bertha kibosile kule, isipokuwa tu sikuwa na dhumuni la kwenda kwa huyo mwanamke muda huu. Nikavuta simu na kumpigia mtu wangu wa faida sana aliyenisaidia mpaka tukawapata Tesha na Mariam ile juzi, yaani askari Ramadhan.

Akapokea, na kama kawaida yake, tayari kwa asubuhi hii alikuwa ameshaingia kazini na kuanza kushughulika na mambo yao mengi, na hivyo akanitaka nimwambie upesi ikiwa kuna taarifa mpya nilitaka kumpa. Nikamwambia taarifa mpya kwa sasa bado, ila nilichokuwa nahitaji ni kujua mahali ambapo Joshua na mke wake walikuwa wamewekwa.

Akasema tu hawakuwa wamewekwa pamoja, huyo Joshua akiwa katika kituo kilichopo Mbagala Maturubai, na mke wake alikuwa ametolewa dhamana ya muda mfupi siku ya jana. Akadai kwamba ni ndugu zake na huyo mwanamke ndiyo waliokuwa wamemdhamini, na walitaka hadi kumtoa Joshua lakini wakakataliwa. Nikamshukuru kwa taarifa hiyo na kumwambia tungetafutana wakati mwingine tena ili nimjulishe yale ya upande wa Bertha na Chalii Gonga, ndiyo tukawa tumeagana.

Hapo nikawa nimepata nilichokihitaji, na sasa ingekuwa kwenda kuchukua nilichokitaka. Kutoka kwa huyo Joshua. Mpango ulikuwa kwenda kuitafuta hiyo Maturubai sasa hivi ili nikaonane na huyo jamaa, na hiyo tu ilikuwa ni sababu tosha iliyofanya nisiwaambie watu wa familia yake Miryam kuhusu hilo. Nilikuwa na lengo, na niliombea niwe sahihi juu ya kile nilichowaza, hivyo baada ya kukamilika kimtoko nikamwacha Ankia hatimaye na kuingia mwendoni.

★★

Haikuchukua muda mrefu sana nami nikawa nimefika huko kwenye kituo cha polisi cha Maturubai. Nilikuwa nimekitafuta kupitia ramani lakini kufika ilihitaji mwongozo wa konda kwenye usafiri na bodaboda mpaka kufikia eneo husika. Hii ikiwa ni mida ya saa tatu kasoro asubuhi, nikaelekea ndani ya kituo hicho, na aisee!

Kilikuwa kibaya!

Sikuwahi kufika kwenye kituo cha polisi kilichokuwa na matunzo duni kama hiki. Yaani palionekana kama vile palikuwa pamepigwa na bomu la nyuklia halafu baada ya miaka mia moja ndiyo hawa watu wakaja kuchukua mabaki ya hili jengo na kuamua kulifanya liwe kituo cha polisi. Sitanii. Lakini kiukweli kupaona sasa kukanifanya nielewe kwa nini askari Ramadhan aliamua kuwaleta wakina Joshua huku. Paliwafaa kabisa!

Baada kuingia hapo ndani, nikamkuta afande mmoja akiwa amekaa nyuma ya kitu kama kaunta, mbaba, mweusi kiasi mwenye sura iliyokomaa, nami nikampa salamu. Kisha nikawa nimemuulizia Joshua, naye aliponiuliza nina uhusiano gani naye, nikamwambia mimi ni daktari wa binti ambaye mwanaume huyo alikuwa amemfanyia uhalifu juzi hapo, na nilihitaji kuzungumza naye.

Afande akasema huu haukuwa muda wa kuwafungulia hao watu wala kuwatembelea, eti muda hususa ikiwa ni saa nne na kuendelea. Nikamwambia mi' nahitaji tu kuonana na Joshua kwa muda mfupi ili nimuulize jambo fulani muhimu sana, na nilikuwa nimeshazungumza na askari Ramadhan ambaye ndiye alinielekeza kuja hapa. Nikaona nimpe na jamaa elfu kumi tu kama pole ya usumbufu, naye akakubali. Mapopo kwa hela!

Akaniambia nisogee naye kuelekea upande uliokuwa na selo ya walioshikiliwa. Tulipoufikia huo mlango, mpaka nikashangaa, yaani ulikuwa mwembamba ingawa wa chuma nzito kiasi, na askari huyu akafungua kufuri kubwa kwa nje na kisha kuita kwa sauti ya juu, "Wewe! Njoo hapa."

Inaonekana alikuwa akimwita Joshua bila shaka, na ni ukimya tu ndiyo uliofuata baada ya hapo.

"Wewe ndiyo... njoo hapa. Nyanyuka," askari akarudia tena kusema hivyo.

Sauti za vuu na vuu zikasikika sakafuni, yaani ndani ya hiyo selo kutuelekea sisi, ndiyo hatimaye Joshua akawa ametoka. Ah, aisee! Kumwona tena kulinitia hasira sana kwa kukumbuka kile alichotaka kumfanyia Mariam, lakini kama ingekuwa ni kwa mtu mwingine kabisa ambaye ndiyo amekutana naye hapo, basi angemwonea huruma kutokana na jinsi alivyokuwa akifanana.

Wakati huu alikuwa ndani ya kaushi nyeupe na bukta nyeusi kwa chini. Mwili wake ulionekana kuchafuka, huku akitembea kwa kuchechema kiasi kwa sababu ya maumivu sehemu fulani ya mwili wake. Usoni, jicho lake la kulia lilikuwa limejaa kama puto dogo yaani kutokana na kuvimba mpaka kutoweza kufunguka, na pua yake ilikuwa imeumuka pia. Taya yake ya kushoto ilikuwa imetanuka zaidi kwa chini, kitu kilichoonyesha kwamba fizi zake zilivimba pia, kwa hiyo kiujumla ni kwamba alikuwa na maumivu mengi sana usoni na mwilini. Mkono wangu ulikuwa mbaya kweli!

Akiwa tu ndiyo ametoka na kuonekana haelewi somo, akawa ameangalia upande niliosimama na kuniona, naye akanitazama usoni na jicho lake moja kwa njia ya kushangaa. Nikaona anameza na mate kabisa, sijui alifikiri nimekuja kumwongezea kipondo kingine?

Yule afande, baada ya kufunga mlango wa selo tena, akamwambia Joshua, "Kaa hapo. Kaa hapo chini."

Lakini Joshua akaendelea tu kusimama na kuniangalia kama vile hakusikia alichoambiwa.

"Wewe, hujanisikia?" askari akamwambia hivyo kiukali na kumpiga begani kwa nguvu kiasi.

Joshua akatoa sauti kuonyesha maumivu, huku akijirudi-rudi kwa kuchechema. Hapo begani ndiyo nilipokuwa nimepasulia chombo kizito cha udongo usiku ule nimemkunyuga, kwa hiyo nilielewa aliumia kwelikweli.

Nikamwambia askari, "Haina shida mkuu. Mwache tu asimame."

Askari huyu akamwangalia Joshua, naye jamaa akaniangalia huku amejishika bega.

"Nasikia mke wako wamemdhamini," nikamwambia hivyo.

"Eee. Me wamekataa. Umewaambia wanikatalie, ili... uje kuniongezea maumivu, si ndiyo?" Joshua akaniuliza hivyo.

"Ningependa sana kufanya hivyo, lakini me siyo mjinga kama wewe," nikamwambia.

"Kwa hiyo nini... umekuja kunitoa?" akaniuliza tena.

"Ahah... unaota ndoto za mchana..."

Nikamwambia hivyo huku nikisogea karibu na aliposimama yeye na askari.

"Siwezi kufanya upuuzi kama huo. Hii ndiyo sehemu sahihi unayotakiwa kuwepo. Na tena ukitoka hapa, ndiyo utaenda kukaa kule papana zaidi. Utapaita nyumbani... ndiyo utakutana na wengi walio kama wewe, hata zaidi yako," nikamwambia hivyo.

Akaonyesha sura ya kukosa amani, naye akasema, "Tafadhali bro... nisaidie. Najua nimekosea ila... ninaweza kubadili... kubadilika yaani... ahh... hii sehemu ni mateso kaka... nisaidie..."

"Ulipata nafasi nyingi sana za kusaidika, lakini ukazitupia dampo. Zamu hii utapata unachokistahili," nikamwambia hivyo kwa mkazo.

Akabaki kunitazama na kupumua kwa kutetereka.

"Kijana, tumia muda wako vizuri. Huyu anahitaji kurudi ndani," askari akaniambia hivyo.

Nikamsogelea Joshua karibu zaidi na kusema, "Nataka kujua ukweli."

"Kuhusu nini?" akaniuliza kwa hofu.

"Nimekuangalia tokea mwanzo. Kufanya yote uliyoyafanya... sidhani kama ilikuwa kwa sababu tu ya kutaka mali upate pesa. Kuna sababu nyingine, si ndiyo?" nikamuuliza.

Akaanza kubabaika, akitazama huku na huko na jicho lake kama Nick Fury.

"Niambie sababu iliyokusuka kurudia makosa yale yale tena na tena... mpaka udiriki kutuma watu wambake mdogo wako ili tu kumharibu, na we' ndo' upate faida yako ya kishenzi," nikamwambia hivyo kwa sauti makini.

Akashusha pumzi na kusema, "Lile shamba bwana... kuna mtu analitaka. Sasa... ehh... mimi ndiyo... nilikuwa...."

"Ongea ueleweke! We' vipi?" askari akamfokea.

"Jamaa nilifanya makubaliano naye... a..alikuwa anataka kulinunua sasa... mimi... tukafanya makubaliano, nilimwambia mwenye shamba ni ndugu yangu na ningehakikisha analipata ila... nikamwomba malipo yaani... nimfanyie kama udalali maana, nilikuwa na uhakika kwamba Miryam angeliachia shamba, maana Mariam ni mgonjwa... ila ndo' kama vile sasa.... akaanza kuzungusha, na...."

"Na wewe ukawa umekula hela uliyopewa kabla jamaa hajakutana na mwenye shamba ili kulichukua, si ndiyo?" nikamuuliza hivyo kwa kumkatisha.

Akaangalia chini kwa kukosa la kusema.

Nikapiga ulimi mdomoni na kutikisa kichwa kwa kutoamini haya yote, nami nikamwambia askari, "Kaka, unajua huyu jamaa ni mpumbavu sana?"

"Hata mi naona. Wewe utauzaje mali isiyo yako?" askari akamwambia hivyo Joshua.

"Halafu unasema Miryam akaanza kuzungusha, ulikuwa umeongea naye?" na mimi nikamuuliza hivyo.

Likabunda tu namna hiyo hiyo.

"Kwa hiyo we' ukala hela ya watu, halafu ukafikiria nini, ah... 'nitamuua tu Mariam, Miryam atasaini paper, kikishahamishiwa jina langu nitakiuza,' easy money. Are you fucking crazy? Kuiba... sisi wote hapa tumeshaiba, hata kama ni kudokoa shilingi mia utotoni, ilikuwa ni kuiba, lakini.... kuua? Kumuua ndugu yako wa damu ili tu upate hiyo shilingi mia? Joshua we' ni mtu wa aina gani? Tena mpaka unatuma watu wakambake, hivi kweli... ah! Unajua watu kama nyie ndiyo mnaosababisha tusitembelewe na wageni kutoka sayari zingine!" nikaongea hayo kwa hisia.

Mpaka afande akacheka kidogo na kutikisa kichwa.

Joshua akanitazama na kusema, "Bro... me nikuombe msamaha tu kwa...."

"Whoa there! Ishia hapo hapo. Usiniombe mimi msamaha, haitakuwa na faida yoyote kwako. Niambie nini kinaendelea sasa hivi kwa huyo jamaa'ako... basi," nikamwambia hivyo kwa uthabiti.

"Alikuwa amenipa muda... ni..nikamilishe hilo zoezi..." Joshua akasema hivyo kinyonge.

"Zoezi la kumuua mdogo wako?" askari akamuuliza.

"Hapana... yeye hajui kuhusiana na hayo. Yeye alitaka tu... hilo shamba... ajengee mambo yake, na ndiyo anachosubiri mpaka sasa hivi. Ila... nilimcheleweshea... kwa hiyo akawa anataka nimrudishie hela yake la sivyo angenizingua... ni..ana... ana nguvu sana, ana pesa..." Joshua akaeleza kwa masikitiko.

"Itakuwa vizuri akija kukuchinja ili taifa lipunguze mbwa wengi kama wewe," askari akamwambia hivyo.

"Ni nani huyo jamaa? Wa wapi?" nikamuuliza Joshua.

"Huwezi kumjua..." Joshua akaniambia hivyo.

"We' ulimjuaje? Usilete ujuaji hapa, unapoteza muda, sema haraka!" askari akamwamrisha.

"Bro... nakuomba... nitakwambia ni nani, ila kwanza nisaidie kutoka hii sehemu," Joshua akaniomba.

"Usijali kuhusu kutoka hapa, utaondoka tu. Niambie jina la huyo mtu," nikasema hivyo.

"Halitasaidia kwa lolote... na ni mtu mkubwa..." Joshua akasema.

"We' unaogopa nini? Si uko sehemu salama, au? Unalindwa kabisa... niambie ni nani huyo, urudi ndani, afande aendelee na kazi zingine. Kama shida ni pesa unayodaiwa, sema ni kiasi gani, useme huyo mtu ni nani, tutamtafuta, tutamrudishia hela yake ili asije kumsumbua Miryam. Sijui unanielewa?" nikamwambia hivyo.

"Huwezi ukafanya chochote bro... me nakwambia..." Joshua akaendelea kusema tu upuuzi wake.

"Ish, hivi huyu...? Yaani najaribu kuku.... halafu we.... aisee! Mkuu, mrudishe tu chumbani kwake... asante," nikasema hivyo.

"Tembea!" askari akamwamrisha jamaa aingie selo.

"Kaka, please..." Joshua akawa ananiomba.

"Wewe, nimesema pita huku! Nitakugonga virungu usitembee kabisa?!" askari akamwambia kwa ukali.

Mimi sikutaka tena kujali kelele za huyo jamaa, nami nikaanza kuondoka hapo nikiwa nawaza kurudi tu nyumbani na mengine yangefuata baadaye. Inaonekana askari alikuwa anamsukuma Joshua arudi kupumzika chumbani kwake, na ile tu ndiyo nimeukaribia mlango...

"Manyanza.... Frank Manyanza..."

Joshua akawa amesema hivyo. Nilipigwa na kitu fulani mbele ya hatua zangu kilichofanya nisimame ghafla, nami nikageuka nyuma kumwangalia Joshua. Sasa wote yeye na askari walikuwa wamesimama usawa wa mlango wa kuingilia selo, huku Joshua akiniangalia kama anataka kulia.

"Nini?" nikauliza hivyo kwa sauti ya chini kiasi.

"Huyo jamaa... ndi..ndiyo jina lake. Frank Manyanza," Joshua akathibitisha.

Nikapiga hatua chache kuwasogelea tena, nikiwa makini sana, nami nikamuuliza Joshua, "Frank Manyanza? Ndiyo anayetaka shamba la Mamu?"

Akatikisa kichwa kukubali.

"Kwa nini?" nikamuuliza hivyo tena.

"Nimekwambia ana hela... ana.. anataka kujenga madude yake, sijawahi hata kukutana naye live, namjulia kwa mwakilishi wake tu... yeye nimemwona kwenye picha... basi. Ni... ana hela, anaweza kuwa hatari sana ndiyo maana nilifanya hayo yote... na sijui sasa hivi itakuwaje yaani..." akajibu hivyo kwa wasiwasi.

Nikaangalia chini nikiwa nahisi... kushangaa.

Afande akaniuliza, "Unamjua?"

Nikiwa nimebaki kutatizika kiasi, nikatikisa kichwa kukubali.

"Ih?! Umemjulia wapi?" Joshua akarusha swali kwa wasiwasi.

"Usiniulize mimi, niambie ukweli. Una uhakika wa asilimia zote kwamba ni huyo unayemsema ndiyo alikulipa?" nikamuuliza kwa mkazo.

Akasema, "Nn..diyo. Ni yeye. Sikudanganyi."

Nikatazama chini kwa kukosa amani kiasi.

"Unam... unamjuaje?" Joshua akaniuliza.

"Haikuhusu. Umepita huko kooote kwa faida gani sasa? Kuishia jela? Ngoja nikwambie kitu Joshua. Mungu huwa anatukutanisha na watu kwa makusudi yake. Usifikiri nilitua tu paap, na kuja kukutibulia mipango yako kimazingara... hapana. Mungu tu ndiye aliyenileta huku ili niweze kuisaidia ile familia... na ninakuhakikishia hili... nitaendelea kuwasaidia mpaka mwisho. Mungu ana maana yake, hata kama mimi bado sijaijua, lakini nitaiishi. Ila wewe ukishakaa jela... ndiyo utajua ulikuwa hujui," nikamwambia hivyo kwa mkazo sana.

Joshua akawa ananiangalia kwa uso uliojaa majuto mengi.

"Imeisha hiyo. Mweke ndani mkuu," nikamwambia hivyo afande.

Kisha nikageuka zangu na kujiondokea. Kweli yaani kuna mambo mengi yaliyokuwa yanatokea mpaka nikawa nawaza ikiwa yalipangwa, ama ilikuwa ni hatma tu. Subiri, hicho ni kitu kimoja, au siyo? Lakini hilo halikujalisha.

Hivi sasa kilichokuwa muhimu kufanya ilikuwa kusahihisha upuuzi wote wa Joshua uliosababisha maumivu mengi sana, na kwa jinsi mambo yalivyokuwa yameeleweka kwangu wakati huu, inaonekana ni kama Mungu alikuwa ananipa nguvu ya kuwa hilo suluhisho tena na tena na tena. Hata sasa, utata wote wa suala la shamba la binti Mariam ningekwenda kuutatua, ili nisaidie kuilinda haki yake haijalishi alikuwa chini ya hali ipi. Ilikuwa ni yake, na yake peke yake.

★★

Nikachukua usafiri, moja kwa moja kurudi Rangi Tatu, kisha nikapanda mwingine kuelekea Makumbusho. Nilikaa kwenye siti ya daladala hii nikiwa na mawazo sana juu ya kile ambacho Joshua alikuwa ametoka kuniambia muda mfupi uliopita. Moja kati ya mambo ambayo unakuwa hujatarajia kabisa, ile kwamba kumbe ni kitu ambacho unakijua ila tu hukuwa umekijua. Hata tu kukifikiria yaani.

Hii ishu ya kumpambania Mariam ilikuwa imeanza kupanda daraja kufikia sehemu ambazo sikudhani ningeweza kufikia kabisa, lakini angalau niliona ni kwa mwongozo wa Mungu tu nilikuwa hapa kuwa suluhisho. Maswali mengi ya ni kwa nini hali hii ilizidi kuwa yenye kuchanganya na kusisimua kwa wakati ule ule yalivamia kona zote za fikira zangu, lakini nilichokuwa naenda kupambania kwa sasa ni kuumaliza upande wa hayo mambo yote sasa hivi. Yakome kabisa.

Nimekuja kufika Makumbusho kwenye mida ya saa nne na nusu huko, asubuhi hii hii, nami kama kawaida nikatafuta Uber na kutoa agizo la kupelekwa sehemu niliyotaka kwenda. Haikuwa Royal Village kama nilivyokuwa nimezoea kwa hizi wiki chache zilizopita, zamu hii nilikuwa naenda sehemu ambayo, niliomba tu Mungu yaani ingemaliza huu utata wote wa suala la shamba la Mariam.

Haikuwa na umbali mrefu sana kwa usafiri huu, na baada ya kufika eneo husika, nikalipa nauli, kisha nikashuka na kusimama mbele ya jengo moja refu kishenzi. Kubwa vibaya mno kati ya majengo kadhaa yenye ubora wa hali ya juu ulioonyesha kwamba watu wa humo walikuwa ni wa kwenda na wakati, na pesa. Kwa anayejua maeneo haya vizuri akikwambia jengo la MWANGA HOTEL linafananaje, ndiyo utaelewa kwamba huo ni mfano bora kufananisha jengo hili lililokuwa mbele yangu. Vioo pande zote kuanzia chini mpaka juu!

Sikutaka kupoteza muda kuangalia hiki ama kile kwa sababu hii haikuwa mara ya kwanza kufika hapo, kwa hiyo nikaelekea tu ndani huko, nikipishana na watu mbalimbali ndani ya sehemu zenye vitu maridadi sana. Moja kwa moja nikaelekea mpaka kwenye lifti na kupandisha hadi ghorofa la nane huko, nami nikatoka na kwenda sehemu yenye meza ya msaidizi wa mkuu wa kitengo cha ghorofa hii ili nipate huduma.

Kufika hapo, nikamkuta mwanamke huyu mwislam, aliyevalia kwa unadhifu sana na hijab yake kichwani. Alikuwa mweupee kama Miryam tu, na mpaka nimefika mbele yake, alikuwa akiingiza vitu fulani kwenye kompyuta yake, kwa hiyo hakuniangalia upesi.

Nikasema, "Habari za asubuhi?"

Akasema, "Salama. Tafadhali, subiri pale niku...."

Akaishia hapo baada ya kuniangalia, akiwa na lengo la kunionyesha sehemu ya kukaa ili nisubirie. Lakini baada ya kuwa amenitazama, akaachia tabasamu pana la furaha lililofanya uso wake upendeze sana, nami nikatabasamu kiasi pia.

"Heey! Jamani, ni wewe?!" akauliza hivyo.

"Ni mimi," nikamwambia hivyo.

"Za siku? Huonekani..."

"Ahh, nilikuwa likizo. Ila niko hapa hapa Dar, so... leo nikaona nije kutembelea."

"Aisee! Naona una likizo nzuri maana unazidi kuwa handsome tu..."

"Ahahahah, umeanza!"

"Ahahaaa, kweli. Ila ni muda umepita jamani!"

"Sana."

"Karibu. Umekuja kuonana na Mr. Manyanza?" akaniuliza hivyo.

"Yeah. Nilikuwa maeneo ya karibu nikaona nipite kumsemesha kidogo. Yupo?" nikamuuliza.

"Yupo, ila yuko bize. Hana hata appointment yoyote, kazifuta nyingi maana kuna load kubwa ya kazi anashughulikia..."

"Ahaa, sawa. Sema, me nataka nizungumze naye kwa ufupi tu... ni muhimu sana. Sitammalizia boss muda wala."

"Mh? Ngoja nimpigie, kama ni wewe anaweza...."

"Oh no, usimpigie. We'... nipeleke tu ofisini kwake kwa hizi staarabu zenu, maana anaweza akakukatalia kwa phone. Twende tumshtukize," nikamwambia.

"Wewe! Unataka anichape?" akaongea kwa maringo.

"Ahahahah, anakuchapa vipi bwana? Labda tu kakibao kwa huko nyuma," nikamtania.

Akacheka kidogo na kusema, "Halafu wewe! Mhm, haya twende. Ila nilikuwa nimekumiss..."

Usishangae, nilikuwa mtu maarufu!

Akanyanyuka kutoka kitini na kujiunga nami, nasi tukaanza kuelekea upande wa ofisi ya huyo boss wake. Huyu mwanamke alikuwa na shepu! Kama vile wale midoli wanaovalishwaga nguo ili kuvutia wateja, namna hiyo. Alikuwa mrefu pia, mwenye uzungu kama wote, halafu hapa alikuwa ni secretary wa huyu jamaa lakini kimwana alitembelea gari la Prado utadhani yeye ndiyo alikuwa bosi. Hawa watu walikuwa wa maana!

Tukafikia milango mipana ya vioo ambayo ilituruhusu kuona vizuri undani wa ofisi ya bosi wake, naye akafungua tu na kwa pamoja tukaingia. Hapo mbele yetu ilikuwa ni sehemu pana na safi sana ambayo iliwekwa meza ya kioo kizito yenye muundo wa ukweli kama tu logo ya apple, ndefu na pana, kukiwa na viti viwili vikubwa vyeusi upande huu wa mwanzo, halafu kwenye mkunjo wa katikati upande mwingine ndiyo kulikuwa na kiti cha bosi.

Hapo alionekana mwanaume mtu mzima, akiwa ndani ya suti safi kabisa, umakini wake wote ukiwa kwenye mafaili kadhaa na makaratasi yaliyokuwa mezani kwake, huku akiandika mambo fulani na kwenye kompyuta yake pia.

Tukawa tunaikaribia meza yake, na bila kututazama, mwanaume huyo akasema, "Faima... nimekwambia sitaki disturbance yoyote ile hata kama ni Mama Samia ndo' amekuja!"

Secretary huyu, Faima, akacheka kidogo kwa pumzi, naye akasema, "Ni mtu muhimu zaidi ya huyo, boss."

Jamaa akapandisha macho yake, na baada ya kuniona, akaegamia kiti chake vizuri zaidi na kuendelea kunitazama tu. Mimi pia nikawa namwangalia kwa utulivu.

Huku akiwa anatabasamu, Faima akamwambia, "Samahani, ameomba kuongea na wewe kwa muda mfupi. Anasema ni muhimu. Dakika tano tu."

Mtu mkubwa akamtikisia secretary wake kichwa mara moja, naye Faima akaondoka na kuniachia uwanja hapo.

"Well, hii ni surprise. Sikutarajia," jamaa akasema hivyo huku akitabasamu kiasi.

"Yeah, sorry kuvamia namna hii, ila ni muhimu kuongea nawe ana kwa ana," nikamwambia.

"Ana kwa ana? Kweli itakuwa muhimu sana," akasema hivyo.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Za huko ulikokuwa?" akaniuliza.

"Safi tu. Shikamoo mzee?"

"Marahaba mwanangu. Karibu."

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★
,

Elton Tonny, Elton Tonny, Elton Tonny, nakuita mara tatu, isije kuwa umetuacha njiapanda kwa season one kama wengine, usitufanyie hivyo​

Back
Top Bottom