Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Baada ya Miryam kuondoka, Ankia akawa amekuja chumbani kwangu. Aliweza kuhisi kwamba kuna jambo halikuwa sawa maana akaniambia kwamba Miryam aliondoka tu bila kumwambia lolote, au kuaga, na alionekana kama ana huzuni. Akaniuliza ikiwa kulitokea tatizo, nami nikamwambia hakuna shida kubwa, bali kuna jambo dogo tu lilituchanganya mimi na bibie lakini tungelishughulikia tu. Mambo yangekuwa sawa.

Akasema haya, ningejua la kufanya tu kudili na mpenzi wangu, na kama nilikuwa nimemuudhi basi nijitahidi kumbembeleza kwa njia yoyote ile mpaka alegee. Nikamshukuru kwa kunisaidia kumleta bibie hapa, na sikusahau kuhusu kumpa zawadi hivyo nikamwambia ningempatia kesho tena nikitoka. Ilikuwa imeshaingia saa kumi na mbili jioni, na Ankia akawa na mpango wa kutoka kwenda kuzurura wapi-wapi sijui na Bobo wake, hivyo hapa alikuwa amekuja kuniambia kwamba kuna msosi umebaki; nikihisi njaa, najua jinsi ya kupakua.

Nikamshukuru, naye ndiyo akaenda kuanza kujiandaa. Nikaendelea kukaa hapo kwa zaidi ya nusu saa nikitafakari tu. Bado ishu aliyoileta Miryam hapa kuhusiana na mdogo wake ilikuwa inazunguka kichwani, na kwa kuwa nilimwahidi Bi Jamila ile asubuhi kwamba ningeenda kuwasalimia tena, nikaona ninyanyuke na kwenda kujimwagia ili nikaitimize hiyo ahadi. Lakini pia nilihitaji kwenda ili nianze kuangalia kama kile ambacho Miryam aliniambia kilikuwa na ukweli.

Yaani, nilitaka kumwona Mariam, nimwangalie, nimtathmini, nimwelewe. Halafu baada ya hapo ndiyo ningejua namna sahihi ya kuja kuzungumza naye ili kuweza kumsaidia kuyaondoa mawazo yake ya kimapenzi aliyokuwa amejenga kunielekea. Bado niliamini huyu binti alikuwa kwenye mwanzo tu wa kuzielewa hisia zake mwenyewe, na labda kweli alivutiwa na mimi, lakini ndiyo angepaswa kuelewa kwamba asingeweza kuwa nami. Ah, ingeeleweka tu, alikuwa mgonjwa wangu hata hivyo, na mimi nilimjua.

Kwa hiyo nikaenda kujiogesha, mpaka namaliza kuvaa vizuri tayari saa moja ilikuwa imeshaingia, na Ankia alikuwa ndiyo anakaribia kuondoka pia. Nikaenda mpaka kwa jirani zetu na kuwakuta mama wakubwa pamoja na Miryam wakiwa wamekaa kwa kutulia sebuleni, Bi Zawadi akifurahi sana kuniona. Nikawasilimu wakubwa na kuketi, story zikianza kwa Bi Zawadi kuniambia kuhusiana na ajali fulani waliyosikia imetokea huko Kongowe, na Miryam alikuwa ametulia tu sofani akionekana kuwa bize na simu yake.

Baada ya dakika chache Mariam akawa amekuja sebuleni pia, akitokea huko chumbani kwao. Alikuwa amevalia T-shirt nyepesi ya pink, suruali nyeupe ya jeans laini iliyombana, na nywele zake zilikuwa kwa msuko ule ule wa mafundo mawili manene ya rasta ndefu yaliyokaa kama mapembe ya ng'ombe yaliyolala. Alikuja moja kwa moja mpaka sofani nilipokaa na kuketi karibu nami, naye akanisalimia vizuri huku akinilalia begani kiasi kuonyesha furaha yake. Alinukia vizuri, harufu kama ya dada yake, na inaonekana alikuwa ametoka kuoga.

Mariam aliendelea kunishikilia mkono huku akinitaka niongee naye kuhusu mambo haya na yale, akiuliza vimaswali vyovyote tu ili umakini wangu wote uwe kwake pekee. Mama wakubwa nao walikuwa wanachangia maongezi yetu na nini, na kila mara nilipomwangalia Miryam, niliona namna ambavyo alijitahidi kuficha hisia zake kila wakati Mariam alipoonyesha uchangamfu wake kwangu kwa ukaribu sana, na najua hilo lilimkosesha amani sana bibie.

Siyo kwamba ni wivu, yaani Miryam aliumia kuona kwamba kilichompa furaha zaidi mdogo wake ni kitu ambacho hangeweza kukipata kwa sababu ni yeye Miryam ndiye aliyekuwa anakimiliki, na nilimwelewa. Alikuwa anaogopa Mariam kuumia sana, lakini hakukuwa na namna. Mwisho wa siku huyu binti angepaswa tu kujua ukweli, kama ndugu zake wote, na ningejitahidi kufanya hivyo kwa busara ili asije kupata mshtuko mwingine. Ndiyo alikuwa yai lao hapa, hawakutaka kabisa avunjike.

Basi, muda ukatembea mpaka kufikia saa mbili, na Tesha akawa amefika pamoja na Shadya. Jamaa alikuwa mizunguko na nini, na hapo alikuwa amekuja pamoja na mifuko iliyobeba vyakula kwa ajili ya familia nzima, ndiyo sababu hakuna mtu aliyekuwa ameingia jikoni leo. Bila kuchelewa maandalizi ya ulaji yakaanza, Mariam akisaidiana na Shadya kuviweka vyakula vizuri huko jikoni ili kuja kuipamba meza, nami nikawa nimepata nafasi ya kumsemesha Miryam kupitia simu.

Nikamtumia ujumbe, nikimwambia asiwe na shaka, suala la mdogo wake nitalishughulikia vizuri kabisa, tena kesho, ili muda mrefu usije kupita zaidi na jambo hilo kuja kuzua utata baadaye sana ikiwa wazi kwa mdogo wake kwamba siwezi kuwa naye. Miryam akanijibu kwa kusema ni kweli ana mashaka, na hofu, lakini ana imani kwamba mambo yatakaa sawa. Kama niliweza kumsaidia mdogo wake akaushinda ule ugonjwa, basi alijua ningeweza kumsaidia asivunjike mno moyo mpaka madhara kutokea. Imani alikuwa nayo, kwa hiyo angesubiri kuona matokeo, na akaomba samahani kwa kuondoka namna ile saa zile tulipokuwa pamoja.

Nikamwambia asiwe na hofu kabisa. Tena nikamwambia kwamba Mariam angefurahi mno siku ambayo dada yake angekuja kunitambulisha kwao kama mume mtarajiwa, nami nikamwona Miryam anatabasamu kiasi kwa kufarijika, naye akanitazama kwa hisia. Nikiwa nimegusia hilo suala la kutambulishwa, ndiyo nikamuuliza tu ikiwa alikuwa na mpango wa kuwaambia ndugu zake kuhusu mahusiano yetu mapema, lakini akanijibu kwamba anataka nitulize hali kwanza kwa upande wa mdogo wake, kisha ndiyo hayo mengine yangefuata.

Aliona nina haraka sana, na kweli, nilitamani mno iwe wazi kwa wote kuhusu uhusiano wetu ikiwa bado mapema, hata kama mwanzoni ingewashangaza lakini najua mwishowe wangepaswa kukubali tu kuwa tulipendana. Na ndiyo baada ya hapo, ningepeleka mahusiano yetu kwenye hatua ya juu zaidi. Sikuwa nikimtania nilipomwambia nataka kumwoa haraka, ilikuwa ni kusubiria tu awaambie mama zake kuhusu sisi, kisha ndoa ingefata bila kuchelewa.

Shadya na Mariam wakaandaa meza vizuri, nasi kwa pamoja tukaenda hapo kushiriki mlo. Zilikuwa zimenunuliwa ndizi za kukaangwa, nyama ya kitimoto kilo tano, vipande vya kuku, chips, na juice. Ah, hii ilikuwa ni kazi ya Tesha bwana, ambaye inaonekana aliangukia bahati nzuri sana leo na kupata mchongo uliomwezesha kuipendezesha meza yao kwa ajili ya familia yake nzima, na hakutaka kutuambia ni mchongo gani ila nahisi ni Happy ndiyo alikuwa amemsababishia. Huyo dada alifanya kazi ya upishi kwenye hoteli kubwa, kwa hiyo uwezekano kwamba jamaa alipewa mavyakula na mpenzi wake ulikuwa wa juu.

Hayo hayakujalisha sana, la muhimu ni kwamba familia yake ilithamini mno, na mimi mwenyewe nikala pia kwa raha zote, huku nikielewa msosi wa Ankia ungegeuka kiporo cha kesho. Tulikula huku tunapiga story zenye kufurahisha, Mariam akiwa ameketi pembeni yangu na amechangamka, yaani ule utu wake wenyewe wa "kidada" ukionekana wazi. Akaanza hadi kutaniwa na mama zake kwamba sasa hivi halishwi kama alivyokuwa amezoea kulishwa, kwamba amekua, naye akasema ndiyo, anakula mwenyewe sasa hivi na anaweza kumlisha yeyote kati yetu kama tukitaka.

Akafanya kuthibitisha hilo kwa kuniwekea nyama karibu na mdomo wangu ili nile, nami nikaipokea na kula. Mama zake na Shadya wakacheka kweli, wakisema sasa hivi Mariam amepona ndiyo atanigeuza mimi mtoto, naye Tesha akamwambia aendelee kunilisha maana nilistahili hilo eti kama zawadi yangu kutokana na msaada wote niliompa binti. Niliona hilo kuwa kama utani, lakini Mariam akalichukulia kikweli. Bila kusita, akaanza kunilisha, yaani akawa anachukua chakula na kuniwekea mdomoni, na sikuwa na jinsi ila kula ili vibe lisiondoke, lakini niliona kwamba jambo hili lilizua utata kiasi kwa upande wa dada yake.

Miryam alikuwa ametulia tu, akiniangalia kila mara nilipolishwa na Mariam na wengine walipocheka kwa furaha, lakini yeye hakutabasamu wala nini, bali akaendeleza utulivu wake tu na kula chake taratibu. Ikanibidi nimwambie Mariam imetosha, kwa upole, aendelee tu kula cha kwake, lakini akaweka ule uso wa kitoto kwamba hataki kuacha, yaani angenilisha mpaka mwisho. Hee, Tesha akasema haya sasa, ndiyo ningetakiwa kula la sivyo ningeliza mtu hapo. Dah!

Ili tu taswira isitoke mbaya, nikaendelea kupokea chakula alichonilisha binti na kuigiza kwamba nimestareheka, lakini nilijisikia vibaya sana kuacha hilo litendeke mbele ya Miryam. Lingekuwa jambo la kawaida tu ikiwa nisingejua kwamba Mariam alikuwa na hisia kwangu, kama tu wengine walivyoliona, lakini mimi na Miryam tulijua halikuwa la kawaida kwa sababu lingefanya binti aendelee kuongeza vitu vingi ndani ya hisia zake kunielekea. Kama leo kaweza kunilisha mbele ya familia yake, kesho angeweza kufanya kitu kingine tena bila hofu. Hii ingepaswa ikome upesi.

Miryam akawa wa kwanza kushiba, na tena hata hakumaliza chakula chake, naye huyo akaelekea jikoni kujisafisha na kisha akaenda chumbani mazima. Inaonekana hali nzima ya hapo ilimboa tu, na kiuhalali kabisa. Sisi wengine tulipomaliza kula pia tukajisafisha na kurudi sebuleni tena kutulia, na Mariam hakutaka kutoka pembeni yangu. Alikuwa na amani kweli mwenyewe, akitulia zaidi wakati huu kuangalia tamthilia pamoja na mama zake na Shadya, na ilipofika mida ya saa tano kasoro ndiyo nikaona niwaage.

Wao pia wakaniaga vizuri, Mariam akinifanya niahidi kuja na kesho asubuhi kumwona, nami nikakubali na kutolewa nje na Tesha ili aende kufunga geti. Akilini mwangu alikuwa anacheza Miryam tu, nikiwa nawaza kufika chumbani kwangu halafu nianze kuchat naye, na tulipokuwa tumelifikia geti, Tesha akanisemesha kidogo.

"Oya, nataka kukuuliza kitu..." Tesha akasema hivyo.

"Ropoka," nikamwambia.

"Aa, bangi za nini sasa?" akaniuliza hivyo.

Nikacheka kidogo kwa pumzi.

"Vipi ishu yako na Miryam bro, inaendeleaje?" akaniuliza.

Nikatabasamu kiasi na kumuuliza, "Kwa nini umeniuliza hivyo?"

"Ahah, we' sema. Nimeona... kakitu-kitu..."

"Kanini?"

"Niliona kama mlikuwa mnachat hivi... kijanja yaani..." akasema hivyo na kuninyanyulia nyusi kidadisi.

Nikatabasamu tu na kuangalia chini.

"Mlikuwa mnajishaua, mnachat kama vile siyo nyie, nimeona. Au nimekosea?" akauliza.

Nikamwangalia na kutikisa kichwa kukanusha.

"Kwa hiyo? Mko pamoja tayari?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini.

Nikatikisa nyusi kukubali.

"Ah..."

Akasema hivyo na kunyanyua kiganja chake, nami nikakikutanisha na changu kwa kuviunganisha pamoja, kisha tukavutana na kukumbatiana kishkaji.

"Safi sana bro. Umejitahidi!" Tesha akasema hivyo baada ya sisi kuachiana.

Nikasema, "Yeah, ila... bado bado dada yako anataka tu-lay low, so...."

Akafanya ishara ya kufunga mdomo wake kwa zipu na kuniambia, "Me mtu wako, usijali, sitamropokea yeyote."

"Asante," nikasema hivyo.

"Nilikuwa nimeshaanza kuhisi umesogea close nilipowaona jana mnaingia kwenye send-off. Mwamba uko vizuri, hadi Mimi ameyeyuka!" akasema hivyo.

"Kawaida tu rafiki yangu. Tulikuwa tumeshapendana... nilihitaji tu kumfanya aone hilo, sa'hivi tuko pamoja," nikamwambia.

"Aminia. Fanya mambo sasa, uoe hapa," akasema hivyo.

"Ili?" nikamuuliza.

Akanionyeshea ishara ya kuendesha gari kwa mkono wake.

"Ahahahah... mjinga wewe! Ndo' unachowaza tu," nikasema hivyo.

Tukagonganisha viganja vyetu huku tukicheka kidogo, naye akasema, "Mwana itakuwa poa sana. Ukianza we' na da' Mimi mkafanikisha, nafata me na Happy."

"Uko tayari kumwoa?"

"Anataka tuishi wote. Kwa hiyo hapa mambo yakiwa good kabisa, nitaenda kuishi naye. Ndoa itafata tu. Nimekaribia kupata kazi," akaniambia hivyo.

"Ahaa... safi kaka. Mungu mkubwa, tutafanikiwa tu," nikamwambia.

"Uhakika. Haya mwanangu, usiku mwema. Ila najua huendi kulala sa'hivi wewe, unataka tu ukachat na dada eti?"

Nikaweka kidole mdomoni na kumfanyia, "Shhh..."

Akanisukuma kutoka getini kwao na kusema, "Nenda huko!"

Nikatoka hapo kwao nikiwa nahisi furaha, nami ndiyo nikaenda zangu mpaka chumbani na kujitia wepesi ili nipande kitandani na kweli nimcheki bibie tuweze kuchat kidogo. Lakini ile nimeangalia simu, nikakuta ujumbe kutoka kwake, akiwa ameniambia kwamba anaingia kulala mapema, kwa hiyo akawa amenitumia na 'goodnight' kabisa. Dah! Mambo gani tena haya?

Nikajaribu kumpigia, lakini ikaita tu mpaka ikakata. Labda kweli alikuwa anahitaji kulala ama labda tu hakujihisi amani sana bado, kwa hiyo nikaamua kumtumia ujumbe mzuri wa upendo wangu kwake na kumtakia usiku mwema, bila kusahau kumwakikishia kwamba Mariam angekuwa sawa. Ni hicho tu ndiyo najua kilimnyima raha Miryam kwa leo.

Yaani, katika kumsoma binti Mariam muda ule niko pale kwao, niliona wazi sasa kwamba furaha yake yote alikuwa ameielekeza kwangu, mimi nikiwa kama kitovu cha hiyo furaha, na ndiyo sababu akanipenda pia. Miryam kweli aliogopa kwamba mdogo wake angevunjika moyo sana ikiwa ningemkataa, lakini ningefanya nini? Nisingeweza kutoka nao wote, bibie mwenyewe alilijua hilo.

Hapa ambacho kingetakiwa ilikuwa ni mimi tu kumwelewesha binti vizuri, nihakikishe namwacha mahali salama kihisia, halafu ndiyo tungesonga mbele kwa mengine. Bado alikuwa kijana mdogo, angekuja kuendelea na shule, na najua angepata tu mtu mwingine ambaye angempenda namna ilivyostahili. Kwa hiyo hili suala ningetakiwa kuliua upesi sana ili lisiendelee kumkosesha Miryam wangu amani, na ndiyo hadithi ya mapenzi yetu ingeendelea kusonga vizuri hatua kwa hatua.


★★★


Asubuhi ya siku ya Jumatatu ikafika. Nililala kwenye saa saba jana baada ya kufanya utafiti kidogo juu ya suala la jina kamili la Festo. Haikuwa rahisi, ila nikafanikiwa kulipata, na nikamtumia Adelina kupitia WhatsApp na kumwomba aniangalizie safari ya huyo jamaa, kisha angenipatia jibu. Ndiyo leo kuamka kwenye mida ya saa tatu nikakuta ujumbe kutoka kwa Adelina akisema angenitumia jibu hakika akifanikiwa kujua. Nikamshukuru kwa hilo. Nikaangalia na upande wake Miryam wa jumbe na nini, lakini hakuwa amenitumia chochote. Nikaamua tu kumpigia, na bibie akapokea.

Tayari alikuwa ameelekea kazini kwake, nami nikamwambia kwamba mida ya baadaye ningekwenda huko kumwona. Akasema haikuwa na shida na nikianza kwenda nimjulishe maana angeweza kutoka, nami nikakubali hilo. Lakini nilikuwa nimeshamwelewa huyu. Huenda alitaka nimjulishe muda ambao ningeanza kwenda ili anipige swaga ooh nimetoka, njia yake ya kunikwepa tu ili tusionane mpaka awe na uhakika kwamba suala la Mariam nimedili nalo. Kwa hiyo muda ambao ningeenda huko nisingemwambia, ili nimbambe tu hivyo hivyo bila yeye kutarajia. Akili mtu wangu!

Tulipomaliza kuongea ndiyo nikapiga push-up zangu na nini, kisha nikaelekea kujisafisha. Ankia alirudi hiyo hiyo jana kwenye saa sita, Bobo akiwa amemleta, na walikuwa wamepondeka kiasi kwa kunywa bia na kula vyakula vitamu huko walipokuwa. Bobo alimpenda kweli Ankia, akahakikisha ameingia kulala vizuri, kisha ndiyo tukaagana na yeye kuondoka. Sasa hivi nikiwa nimetoka kwenda kuoga tayari saa nne ilikuwa imeshaingia, na Ankia tayari alikuwa ameamka. Alikuwa kwenye ile hali ya kivivu, hakufanya usafi ila chai alikuwa ameshaandaa, nami nikamtania kwa kumwambia inaonekana alitembezewa kipigo cha maana na Bobo hiyo jana.

Nikaenda kuoga akiwa amenitandika kofi begani, eti hataki nimtanie hivyo, na baada ya kusafisha kinywa na kuoga nikarudi ndani kuvaa vizuri kabla ya kwenda kunywa chai. Na ingenyweka na kiporo, huwa vinakuwa vitamu kweli kuliwa na chai asubuhi, kwa hiyo ningekula. Ankia alikuwa kwenye maandalizi ya kutoka ili akafungue duka lake, na wakati nikiwa chumbani bado nikitengeneza nywele zangu vizuri, akaja mpaka humu na kunisemesha.

"JC..."

"Ankia, me mume wa mtu sa'hivi, uwe unapiga hodi," nikamwambia hivyo kiutani huku nikizipiga-piga nywele zangu kwa chanuo.

Akasonya kidogo na kusema, "Kwa kipi ambacho sijakiona?"

Nikamfanyia kejeli kwa mdomo kama wanawake wanavyofanyiana, 'ng'oo!'

Akasema, "Mamu amekuja."

Nikaacha kutengeneza nywele na kumtazama usoni.

"Yupo hapo anakusubiria. Me ndo' naenda. Harakisha," akaniambia hivyo.

Hakujua ni jinsi gani kauli yake ilinifanya nihisi kuishiwa pozi, siyo kwa njia mbaya, yaani ile tu kwa kutotegemea. Mariam alikuwa amekuja hapa? Ahee... mbona majanga!

Ankia akasema 'baadaye,' nami nikamtikisia kichwa kukubali. Nikasogea mpaka hapo mlangoni na kuchungulia pale sebuleni, na kiuhakika, Mariam alikuwa amekaa sofani, Ankia akimpita na kumuaga vizuri sana, kisha binti akabaki peke yake. Alikuwa amevaa vile vile alivyokuwa amevaa jana nilipokwenda kwao, akikaa kwa kuegamia sofa huku akikumbatia mto mdogo mkononi, na kidole kimoja kikiwa mdomoni mwake huku akitazama TV. Dah!

Aliona nachelewa kwenda kwao, kwa hiyo akawa amenifata. Mhm, haya. Nikaweka chanuo pembeni, maana naona nafasi ya kuyamaliza haya yote ilikuwa imejileta kiulaini mbele yangu. Hakungekuwa na muda mwingine bora zaidi wa kuzungumza vizuri na binti kama siyo sasa, kwa hiyo nikaweka simu mfukoni na kwenda hapo sebuleni, nikiwa ndani ya T-shirt nyepesi na pensi yangu ya kijani. Mariam aliponiona namwelekea, akaachia tabasamu la furaha na kujisawazisha kwa jinsi alivyokuwa ameketi, nami nikaivuka miguu yake na kukaa pembeni yake hapo sofani.

"Good morning," akaniambia hivyo huku akitabasamu.

Nikatabasamu pia na kusema, "Morning. How are you?"

"Very much fine," kakajibu.

"I can see that. Umeshaanza hadi kunizidi kiingereza na mimi, umekuwa mzungu," nikamtania.

"Ahh... unadanganya. We' ndiyo umenifundisha..."

Mariam akasema hivyo huku akianza kuchezea kimkia cha rasta zake taratibu, na aliniangalja kwa njia fulani yenye hisia sana.

Nikaacha kumtazama na kusema, "Leo naona umewahi kuamka sana."

"Eeh, nimeamka saa moja, nikadeki ndani, nikamsaidia mama mkubwa kupika chai... ndiyo nikaja," akasema hivyo.

"Ahaa, safi sana. Unajitahidi. Warembo wangu hawajambo?" nikamuuliza.

"Eeeh. Wapo. Tesha ameondoka, na dada. Wapo wenyewe tu," akaniambia.

"Ndo' ukaona uje unisalimie?"

Mariam akabana midomo huku akiniangalia kwa macho yenye... raha yaani, naye akatikisa kichwa kukubali hilo.

"Sawa. Umeshakunywa chai?" nikamuuliza.

"Eeeh. Na wewe?" akauliza.

"Bado, ila nitakunywa tu. Ndo' nilikuwa nataka ninywe nije niwaone, halafu...."

Akanikatisha kwa kusema, "Ih, kumbe bado? Ona... weka... a-ah, ngoja nikuwekee chai, unywe hapa hapa, halafu ndiyo twende..."

Aliongea hivyo na kuashiria kutaka kunyanyuka, nami nikamshika mkono na kusema, "Hapana, Mamu... nitakunywa baadaye. Usijali."

"A-aaa... acha nikakuwekee..." akaongea kwa sauti ya kudeka kabisa.

Nikafumba macho na kuinamisha uso kiasi, kisha nikatazama pembeni nikiwa nahisi kutatizika yaani.

Akauliza, "Au hautaki nikuwekee?"

Nikamwangalia. Alionyesha hisia sana, yaani kwa alichotaka kufanya, alitaka kukifanya kwa moyo wote na haikumpa raha kuwaza kwamba nisingetaka akifanye kwa ajili yangu. Sikutakiwa kuzunguka sana hapa, yaani nilihitaji nimwambie nilichowaza haraka, maana kumwachia mno afanye hivi vitu kungemfanya adhani navipenda mno. Alikuwa amenilisha jana, leo aniwekee chai tena ili aanze kuninywesha? Hapana. Ningehitaji kuwa thabiti, ila nimfikie kwa upole.

Nikiwa bado nimeushika mkono wake nikamwambia, "Hapana, wala usijali Mamu. Sihisi njaa. Halafu... nataka niongee na wewe kwanza."

Mariam akajilegeza na kukaa vizuri zaidi, huku akiwa ananiangalia kwa macho makini na tabasamu lililojengeka taratibu.

Nikamwachia mkono na kusema, "Mamu... ninafurahi sana kuona kwamba unaendelea vizuri mno sa'hivi. Mwanzoni ulikuwa unaumwa sana, lakini sasa hivi...."

"Nimepona kwa sababu yako," akanikatisha kwa kusema hivyo.

Nikatulia na kuendelea kumwangalia usoni kwa utulivu.

Akajisogeza karibu yangu kidogo na kusema "Mimi ndiyo ninafurahi zaidi JC, maana... umenisaidia mno. Naongea vizuri tena kwa sababu yako, nafikiri vizuri tena kwa sababu yako, yaani...."

"Mamu, sijafanya kila kitu me mwenyewe. Dada yako, Tesha, mama zako, wamekusaidia pia. Jitihada zetu wote ndiyo zimekusaidia," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Ni sawa, ila... wewe ndiyo umechangia zaidi. Bila ya wewe, nisingekuwa hivi," akaniambia hivyo.

Aliongea vizuri! Yaani nilimtazama na kuanza kuona mtu mwingine kabisa.

Nikashusha pumzi kiasi, nami nikamwambia, "Mamu... kuna jambo muhimu nahitaji kukuelewesha. Sawa? Ni... najua kwamba we' ni msichana mkubwa sasa, na ni binti mzuri sana..."

Akatabasamu kwa njia ya shau huku akinitazama kwa hisia.

"Nimeshaona maendeleo yako, na ni mazuri. Uko tayari kwa ajili ya mengi, ku... kutoka tena nje, kurudi tena shule, kuwa na marafiki wakubwa kama wewe, na... ukiwa tayari zaidi, zaidi ya sasa namaanisha, unaweza hata kuanzisha mahusiano na mtu ambaye...."

Mariam akanikatisha kwa kucheka kidogo kwa pumzi huku akifunika uso wake.

Nilikuwa najaribu kwenda taratibu ili anielewe vizuri, kwa hiyo nikaendelea kusema, "Nisikie sasa. Yaani, wewe uko sehemu nzuri sana kwa sasa kuanza tena kuishi kawaida, kama vijana wenzako. Utatakiwa kurudi shule, labda chuo... usome, ukutane na vijana wenzako, ujue mambo mengi zaidi yatayokusaidia u...."

Kabla sijamaliza kuongea, nikashtukia Mariam ananisogelea na kunipiga busu kwenye shavu upesi sana, kisha akakaa vizuri tena!

Nikamwangalia usoni, na yeye alikuwa akiniangalia kwa macho yenye matumaini mazuri kweli, halafu akaanza kutoa tabasamu lile la kujirudia-rudia kama vile anajaribu kulizuia. Kuangalia kiganja chake kimoja, nikakuta amejishika sehemu ya paja lake na kulifinya-finya kwa njia iliyoniambia kwamba alikuwa amepandisha hamu, hamu kunielekea. Ha, huu ungekuwa mtihani!

Nikamwangalia machoni tena na kusema, "Mamu... sikia. Nachotaka kukwambia ni kwamba...."

Mariam akanifata tena ghafla na kunipiga busu mdomoni, mpaka nikashangaa! Zamu hii, baada ya kunibusu tu hivyo mara moja, akaweka mto pembeni na kuendelea kuinamishia uso wake karibu kabisa na wangu, akiniangalia kwa njia ya mapenzi yenye dhati yaani, na kwa kweli hali hii nzima ilifanya mwili wangu upandwe na msisimko wa ajabu mpaka nikaanza kuvimba dude. Sikuelewa kwa kweli. Huu ujasiri binti alikuwa anautoa wapi?

Nikiwa nimezubaa kiasi, Mariam akafanya kitu ambacho sikutarajia kabisa, kabisa, kabisa! Akafanya kujinyanyua na kuipitisha mikono yake mabegani kwangu, yaani katikati ya uso wangu hadi kulishika sofa nilipoegamia, halafu akapitisha mguu wake mmoja hapa chini na kupanda juu yangu, akinikalia mapajani na kunitazama usoni kwa macho yenye hisia. Nilishindwa kujua namna ya kuitikia jambo hilo na kubaki nimeganda huku nikimtazama kwa umakini, mapigo ya moyo yakianza kwenda kasi, damu ikichemka, na hisia zangu kuvurugika.

Yaani akawa ameniweka kati, eti kutaka kunionyesha mapenzi. Nilihisi kuchoka! Bila kupenda, mashine yangu ndiyo ikazidi kuvimba, na kwa kuwa nilivaa pensi tu, ilikuwa rahisi sana kuhisi namna ambavyo binti aliikandamiza kwa jinsi alivyokuwa amenikalia, naye akawa ananiangalia kwa macho yaliyojaa... ashiki! Eeh, yaani hilo ndiyo neno. Hakutaka kusikia nini wala nini, Mariam alitaka vitendo.

"Mamu..."

Nikajikuta nanena tu jina lake kwa upole, nikijaribu kumshika sehemu za ubavu wake nimtoe kwangu kwa wepesi ili kuzuia jambo hili, lakini nilipomgusa tu, Mariam akatazamisha uso wake juu na kufumba macho kwa kilichoonekana kuwa kusisimka, halafu akaanza kujivuta-vuta taratibu katikati ya mapaja yangu na kuishika mikono yangu kwa pamoja. Eh!

Nikamwambia, "Mariam, nisikilize. Nisikilize mdogo wangu..."

Akaniangalia na kutabasamu kivivu fulani hivi, halafu akasema, "Nimetamani kwa muda mrefu sana kufanya hivi..."

Nini?! Nikabaki nikimtazama machoni kwa umakini.

Akanishika shingoni na kusema, "Unanisisimua sana..."

"Oh God!" nikanena hivyo kwa sauti ya pumzi.

Yaani hakuwa "binti Mariam" niliyemzoea, hapa alikuwa Mariam mwenyewe sasa, akili yake ikielewa vizuri kile ambacho alitaka. Maneno ya Miryam yalikuwa kweli, na mimi nilikuwa na makosa kudhani ingekuwa rahisi tu kumsemesha shauri ya mazoea, ila hapa ndiyo nikatambua kuwa hii ishu ilikuwa ya daraja lingine. Ningepaswa nimtoe huyu dada juu yangu upesi, lakini kwa uangalifu sana. Bado nilimwona kama mgonjwa wangu hata kama alikuwa amepona-pona.

"Mamu, sikia. Hapa ni kwa... ni kwa watu. Shuka, usinikalie hivi. Kaa hapo nikwambie kitu kwanza..."

Nikamsemesha namna hiyo huku nikiishika mikono yake na kujaribu kujivuta ili nimtoe juu yangu, lakini akaigeuza nguvu yangu kiasi kwa kuirudisha mikono yake mgongoni, yaani iwe kama nimeibana mgongoni kwake, halafu ndiyo akanilalia zaidi kifuani na kukaa mapajani kwangu akiwa amejibinua. Yaani mpaka nikashangaa. Hivi vitu alikuwaga anavijua au?!

Ikabidi niiachie mikono yake ili huo mtazamo umwondoke, na kabla sijaongea, akasema, "Ankia hayupo. Mpaka jioni."

Alikuwa ananiongelesha kwa sauti laini, tamu yaani, mdomo wake ukiwa karibu na wangu, na macho yake yakiwa na mlegeo hafifu huku pumzi zake zikiupa joto mdomo wangu. Nilikuwa nimekaza huko chini, yaani nilihisi kabisa dhambi inaenda kutendeka muda siyo mrefu! Kwa nini alinisisimua namna hii? Sikuelewa kwa kweli.

Akaweka mkono wake mmoja usawa wa kiuno changu na kusema, "Ni muda mrefu sana... sijafanya hivi."

Nikamuuliza, "Unaikumbuka mara ya mwisho?"

Akaangalia pembeni kwa ufikirio, kisha akatikisa kichwa kukanusha. "Nahisi... vitu vingi. Vina... vinapanda kila... nikikuona. Tokea siku ile..." akasema hivyo.

Nikaweka uso makini zaidi, nami nikauliza, "Siku gani?"

Akaniangalia usoni vizuri na kusema, "Ulipokuwa nyuma... na Dina."

Ohohooo!

Aisee! Kumbe siku ile kweli binti alikuwa ameniona nilipofanya na yule Dina pale kwao, na huenda hilo ndiyo jambo lililozidisha mtazamo huu aliokuwa nao sasa kunielekea, ikiwa kama siyo kitu kilichofanya uanzishwe.

"Kumbe ulituona?" nikamuuliza hivyo kwa sauti ya chini.

"Ndiyo. Tokea hapo... nilikuwa natamani... niku... niku...."

Akawa anababaika kiasi. Hadi nikawa namwonea huruma.

Akajitahidi kusema, "Nikuambie nakupenda... ila nikawa naogopa."

"Kwa nini?" nikajikuta namuuliza hivyo.

"Sijawahi.... au... sikumbuki kama nimewahi kupenda mwanaume. Labda... nimeshapendwa, lakini... kwa jinsi navokupenda wewe sasa hivi... sijawahi kuhisi hivyo," akaniambia hivyo kwa njia pole sana.

Unajua hii ndiyo pindi ambayo mpaka mtu unakuwa unatamani kuwa na uwezo wa kuzigawa hisia zako mara mbili, lakini unajua huwezi. Ipo ile kwamba mwanamke anaweza akanifata na kutaka tupige mambo tu, hapo naweza hata nikajifikiria mara mbili mbili na kusema ngoja ninywe pombe kisha nipige tu, halafu nitatubu kwa Mungu, niisingizie na pombe kidogo, Miryam asijue. Si mara moja tu? Ila kwa hii hali, Mariam alikuwa ananiomba nimpende kama yeye alivyonipenda, kitu ambacho hakingewezekana.

Na tena siyo kwa sababu tu ya dada yake, ila kwa sababu yake yeye mwenyewe Mariam. Nisingemuumiza hisia kwa kukubali jambo hilo hata kama ningekuwa na uwezo upi wa kuficha mambo, kiukweli alikuwa ni mwanadada mwenye kuvutia sana; kisura, kiutu, kiumbo, sikuwahi kumchukulia hivyo, ila sasa ndiyo nikawa nimeona hilo. Lakini hiyo haingenipa ruhusa ya kuamua kuzichezea hisia zake hata kama uanaume wangu ungetaka vipi kuvunja amri ya sita. Ila bado nilikuwa nimebanwa kwenye kona kali mno hapa.

Akawa kama anasubiri nimwambie kitu fulani baada ya kuwa ameniambia hayo, lakini mimi nikakosa la kusema zaidi na kubaki kuangalia chini tu. Akili ilikuwa inapingana na hisia. Yaani akili ikawa inanifanya nitamani mambo kuwa tofauti, labda iwe kama kipindi kile ambacho nilikuwa natembeza tu kwa mwanamke yeyote mzuri aliyenikubali, lakini hisia zilikataa. Haikufaa. Hasa kwa huyu mwanadada. Lakini ningetumia njia gani kumwondolea huo mtazamo ambao ni wazi ulikuwa umeshakita mizizi?

Kwa kuona nimetulia kutafakari tu, Mariam akaifinya nyonga yangu kwa kiganja chake, nami nikamwangalia usoni. Hapo hapo mwanadada huyu akanifata mdomoni na kunipiga denda laini, siyo busu, denda! Nikarudisha kichwa changu nyuma, lakini akanifata na kuendelea kulazimisha denda pamoja nami. Ai! Midomo yake ilijaa mate, naye akaona anishike kichwani kabisa na kuendelea kuinyonya midomo yangu kwa hamu kubwa kuliko!

Hisia za kimahaba zikanipanda kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Nilikuwa siamini haya yaliyokuwa yanatokea. Mariam alikuwa ananyonya mdomo wangu kwa njia yenye ustadi, yaani ile 'experience' nzuri ya hii kitu alionekana kuwa nayo, na mimi huku mzee nguvu zikaendelea kukimbilia sehemu moja tu. Nilikaza, yaani nilikaza haswa. Nilinyanyua viganja vyangu hewani kiasi, nikivifunga na kuvifungua kwa kutaka kumtoa huyu dada karibu nami, lakini nikawa nashindwa. Na kilichofanya nishindwe, ndiyo kikawa kitu kilichofanya nianze kuanguka.

Viganja vyangu vilikuwa vinatakiwa kumwondoa huyu dada mwilini kwangu, lakini badala yake, nikajikuta namshika nyuma ya kichwa chake kwa mikono yote na kuanza kurudisha denda hiyo kwa hamu kubwa! Ah, siyo poa. Yaani pamoja na yote niliyokuwa nimetoka kuwaza kupingana na hii ishu, JC nikajikuta naanguka. Tena kwenye penzi la mdogo wa mpenzi wangu. Acha kabisa! Hii kitu huwa inatutafuna wanaume vibaya, usiombe. Yaani huwa tukifika hapa, tunasahau kila kitu, na mimi haikuwa rahisi sana kusahau, ila sijui tu kwa Mariam ikawa vipi.

Eh bwana eh, denda ikaendelea. Nilimdendesha huyu binti kwa ufundi, yaani ile denda yenyewe, mpaka nikahisi nafurahia kufanya hivyo. Najua ile hali ya upya, yaani msisimko unaotokana na ishu za mambo yote yaliyopelekea mpaka sisi wote kufika hapa, na ndiyo nikawa nimetambua kwamba nilikuwa dhaifu sana mbele ya huyu binti. Kwa mambo mengi, toka nimeanza kumsaidia mpaka sasa, nilikuwa na udhaifu mkubwa sana kwake. Hisia zangu za kumjali mno ndiyo zikapelekea nimruhusu afike huku pamoja nami, yaani msimamo wangu wote ukalegea mbele yake ndani ya dakika mbili tu. Mambo ikawa kwisha!

Mariam akaonekana kupandwa na hamu zaidi, akajitoa mdomoni mwangu na kuanza kupumua kimahaba sana, na mimi pasipo kuongozwa na akili, nikawa naendelea kubusu kidevu chake hadi kuifikia shingo, na yeye hakuacha kupeleka kiuno chake mbele na nyuma kwa njia ya kusugua mtambo wangu uliokuwa umevimba na kukandamizwa kwa kalio lake. Joto lilinipanda, yaani... sikufikiria la kufanya, nikawa naendelea kubusu tu shingo yake taratibu. Kulikuwa na zile fikira za 'Mungu wangu, nafanya nini?' lakini nikaendelea tu kufanya hiyo nini. Siyo poa!

Mariam alikuwa amelegea kweli, akiushika mkono wangu kwa nguvu na kupumua kwa njia yenye deko, yaani kama anataka kulia vile, nami kwa sekunde chache, nikaacha kumbusu na kumwangalia kwanza. Nilimtazama kwa umakini, bado nikiwa najishangaa yaani, kujiruhusu mpaka nianze kufanya hivyo, naye akaniangalia usoni kwa macho legevu na kunyonya kiasi mdomo wake wa chini. Nilikuwa kwenye fikira iliyotatizika, nikaanza kumfikiria dada yake tena, naye Mariam akafanya kitu kilichonihamishia mawazo hayo upesi.

Akashika T-shirt lake kutokea kiunoni na kuanza kulipandisha juu, mpaka akalifikisha usawa wa vikwapa, halafu ndiyo likajivuta juu lenyewe sehemu ya kifua na kukifichua chote kabisa. Aisss! Moto ukazidi kukolea. Binti hakuwa amevaa sidiria, kwa hiyo kwa mara ya kwanza kabisa nikawa nimekiona kifua chake waziwazi mbele yangu.

Alikuwa amebeba matiti yasiyo na ujazo mwingi, zaidi, kilichofanya yaonekane kuwa makubwa kiasi ni namna ambavyo chuchu zake zilikuwa zimevimba. Yaani alikuwa na chuchu nene zilizonyanyuka kuelekea mbele na hivyo kufanya matiti yazifate, na yalikuwa meupeeh, huku chuchu zikiwa na weusi-kahawia uliozipendezesha mno. Ilikuwa kama naangalia matunda mawili matamu sana ambayo hakuna mtu aliwahi kuyala, na msisimko wa hapo ukafanya nihisi mashine yangu ikikaza mpaka kuanza kuuma.

Sikudhani angekuwa na akili ya kupeleka mambo moja kwa moja hapo, ila hayo yalikuwa ni makosa yangu kwa kumchukulia kuwa kama mtoto mdogo bado. Haya mambo aliyajua, na mimi JC hapo ndiyo akawa amenipatia. Ah, hamu ilikuwa inanitesa kinoma halafu dada yake bado alikuwa ananibania, sikumbuki hata mara ya mwisho kupata huu msosi ilikuwa lini, kwa hiyo yule Shetani ndani yangu alikuwa anailazimu njaa ipande zaidi ili nianze kukamua hiki chakula kitamu sana mbele yangu. Sijui ingekuwaje kwa kweli!

Baada ya Mariam kunifunulia kifua chake, akanishika shingoni taratibu na kufanya kama kunivuta, na bila woga wowote ule, akaniambia kwa hisia, "Come on..."

Ei!

Nilikuwa napewa ninyonye, Mungu wangu, ninyonye matiti ya mdogo wake na mpenzi wangu! Ilikuwa kama ndoto vile, na najua isingekata kwa kufumba na kufumbua macho. Mate yalinijaa, nikiyaangalia matiti yake kwa hamu sana, naye alipoona najishauri bado akaamua kujisogeza kwangu zaidi na kuligusisha titi lake la kushoto midomoni mwangu. Nikafumba macho na kujitoa akili, nami nikalamba chuchu yake kidogo sana, na itikio lake likawa kuikaza zaidi shingo yangu kwa vidole vyake.

Kulikuwa na kautamu ka chumvi-chumvi kwenye ngozi ya chuchu yake, nami nikaanza kuilamba kwa uendelevu. Alinukia vizuri, harufu kama ya dada yake, na nadhani jambo hilo likaongezea hamu yangu ukali kwa kuhisi uvutano wa karibu zaidi kwake ulionifanya niendelee tu kuilamba chuchu yake. Nilikuwa nimefumba macho bado, nami nikaiingiza yote mdomoni na kuinyonya taratibu. Mariam akalegea zaidi, nikihisi kama anataka kuanguka sijui, nami nikamshika kiunoni na kumwangalia usoni.

Akarudisha mhimili wake vizuri, na kwa sauti ya kunong'oneza akasema, "Nhh.. naishiwa nguvu..."

Nikabaki nikimtazama machoni tu kiwasiwasi hivi.

Akanishika shingoni tena na kusema, "Usiache. Nasikia raha sana."

Duh!

Mariam akanisogezea kifua chake usoni kwa mara nyingine tena, nami nikaachama tu bila kupenda na kulipokea titi lake. Zamu hii, nilianza kulinyonya kwa kulivuta ndani ya mdomo kabisa, naye akanishika kichwani kwa mikono yote kwa njia ya kukumbatia na kunikandamizia kwake zaidi. Utamu ambao wanaume huwa tunahisi kunyonya hivi vitu huwa tunaujua siye tu, na kiukweli Mariam alikuwa na utamu wake mtamu.

Nikawa namnyonya huku nikiangalia jinsi alivyoonyesha raha ya hali ya juu, akiyabana mabega yake na kujikunja kiasi, na akilifinya-finya titi lake lingine shauri ya raha hiyo kumkolea, na hata mwili wangu ulisisimka vya kutosha kuonyesha ulifurahia tendo hili kufanyika. Lakini kihalisi, hili jambo lilinitatiza sana. Kumwangalia Mariam usoni ilinifanya nimuwaze dada yake, sana, siyo tu kwa sababu walifanana, ila kwa sababu jambo hili lisingekuwa sahihi kufanya.

Naelewa furaha ya Mariam ilikuwa ni suala muhimu katika kuendeleza hali yake njema, ila nisingeweza kumpa hii furaha aliyokuwa akiitaka. Nilimpenda Miryam, hilo nilihitaji kumweleza Mariam wazi, iwe leo, ama lini, angetakiwa kuelewa. Haingekuwa na maana kuruhusu jambo hili litokee halafu nirudi kwa dada yake tena, hiyo ingenifanya niwe nani? Nisingemfanyia Miryam hivyo. Na sikutaka kumfanyia huyu mwanadada kitendo hiki hata kama ingemuumiza moyoni. Na sijui kwa nini tu hilo dude langu likaamua kunyanyuka, huu haukuwa wakati mzuri hata kidogo!

Nikajitahidi kuzipinga tamaa za kimwili na kuacha kumnyonya namna hiyo, naye akaanza kulivuta-vuta titi hilo kwa kuonekana kuwashwa zaidi. Aisee! Nilikuwa nimefanya nini? Sikupaswa kabisa kumfikisha huyu binti sehemu hiyo. Nikashindwa hata kumwangalia usoni kwa sababu ya kuhisi hatia sana, nikitazama pembeni tu huku moyo wangu ukiingiwa na hofu kutokana na kutambua kosa langu, naye akawa ametulia tu juu yangu, bila shaka akinitazama kwa subira.

Nikasema, "Mamu nisamehe. Nisamehe sana mdogo wangu..."

Mariam akanishika shingoni na kusema, "Umefanyaje kwani? Mbona unaomba msamaha?"

Nikamwangalia usoni kwa huzuni.

Akatabasamu kiasi na kusema, "Usijali. Hujaniumiza. Ninapenda sana unavyonifanya."

Aliongea taratibu, kwa hisia ya dhati, yaani dah! Kwa hiki nilichokifanya mpaka nikajiona Shetani sasa hivi, wakati sekunde chache nyuma nilikuwa nahisi kukifurahia kweli. Sijui nilikuwaje!

Mariam akasema, "Tuendelee..."

"Hapana, Mamu... ime-imetosha," nikamwambia hivyo huku nikijifuta mdomo.

Hapo hapo nikaishika T-shirt yake na kuishusha upesi, naye akawa ananiangalia kwa kutoelewa.

"Mamu, hatuwezi kuendelea. Sawa? Tunaishia hapa... sikupaswa kufanya hivi... nisamehe. Nimekukosea sana," nikamwambia hivyo kwa hisia.

"Kwa nini?"

Aliuliza hivyo kwa sauti yake ya upole sana, akiwa hajanielewa vizuri najua maana hadi tayari nilikuwa nimeshaanza kumpandishia hamu hata zaidi, nami nikabaki nikimtazama machoni kwa hisia sana.

"Au haujapenda? Nimewahisha sana?" akauliza.

"No, siyo hivyo... sijamaanisha hivyo Mamu. Ni kwamba... we' ni rafiki yangu. Sawa? Napenda tukiendelea tu kuwa marafiki..." nikamwambia hivyo kwa upole.

Bado alikuwa amenikalia, naye akasema, "Marafiki. Kwa nini usi... hauja.... haujanipenda JC?"

"Siyo hivyo Mamu, we' ni msichana mzuri sana. Sawa? Mzuri, mrembo, yaani... unawafunika hadi wakina Beyonce kabisa. Hamna mtu asiyeweza kukupenda. Hayupo..." nikamwambia hivyo.

Akaendelea kuniangalia machoni kwa hisia.

"Ila... mimi ni kama kaka yako, sawa? Nakuona we' kama Nuru. We' na Nuru mnafanana sana, wote nawaona kama wadog...."

"JC... acha kuniongelesha hivyo. Me siyo mtoto," akaniambia hivyo kwa hisia.

Nikatatizika kiasi moyoni, maana ni kweli bado nilikuwa namtendea kama mtoto mdogo.

Akasema, "Niambie tu ukweli. Haujanipenda?"

Nikashindwa kumtazama usoni na kutulia tu nikitazama pembeni, maana nilikuwa nimefanya iwe ngumu kupata namna ya kumwambia kwamba nilimpenda mtu mwingine, na alikuwa ni dada yake. Nilipomtazama usoni hatimaye, nikakuta machozi yakiwa yameanza kumlenga kwa kasi, nami nikashtushwa kidogo na jambo hilo. Nikamshika shingoni kwa viganja vyangu vyote huku nikimtazama kwa hisia sana, na yeye akawa ananiangalia kwa macho yenye huzuni.

"Mamu... Mamu usilie. Nisikie. Nakupenda. Sawa? Nakupenda sana. Wewe ni mtu wa muhimu mno kwangu, hilo sikudanganyi. Lakini... ukweli ni kwamba... nakupenda kama mdogo wangu, Mariam. Nakupenda kama Tesha anavyokupenda, kama mdogo wangu. Nime... nimeshakuzoea kwa jinsi hiyo Mamu... kama mdogo wangu. Unaelewa?" nikamwambia hivyo kwa upole.

Machozi yakaanza kumtiririka, naye akasema, "Lakini me nakupenda JC. Nataka tuwe.... wapenzi. Usinione kama mtoto. Naweza kukufurahisha. Nitakufurahisha..."

Alinitia simanzi kali sana, mpaka chozi likanitoka.

Akapindisha shingo yake kidogo na kusema, "Niambie unataka nini... nitakupa..."

Masikini!

Nikajifuta chozi haraka na kuanza kumpangusa yake pia, nami nikamwambia, "Hauhitaji kunipa chochote mama. Wewe ni msichana mzuri, unatosha. Tunaweza kufurahishana kwa kuwa marafiki tu, kama sikuzote tum... tumekuwa tukifanya. Ila hatuwezi kuwa wapenzi Mariam..."

Akaangalia chini huku machozi yakiendelea kumtoka.

Nikamtazamisha usoni kwangu na kumwambia, "Ona... sikwambii hivyo kwa sababu haujanivutia. Kama nilivyokwambia, wewe ni msichana... mzuri sana. Lakini mimi sikufai Mariam. Siyo mimi nayestahili kuwa mpenzi wako. Mimi... unanijua kwa mengi mazuri, lakini... nimefanya mengi yasiyo mazuri pia... nimeumiza watu na kujichukia kwa sababu hiyo, na... ni mengi nayojutia. Sitaki nikuweke kwenye hiyo orodha mdogo wangu... sitaki nikukukubalie, nicheze na hisia zako halafu ifikie sehemu nikuumize.... sitaki kukuumiza Mariam. Wewe ni muhimu SANA kwangu, sitopenda kukudanganya..."

Mariam akaniangalia na kuuliza, "Nani anakusaidia sasa?"

Nikamwangalia usoni kwa umakini kiasi.

"Najua lazima awepo mtu anayekusaidia... usitekwe sana na mapito... uwe mtu bora. Ni nani?" akauliza hivyo.

Aliongea kama mtu-mzima mzima yaani, kwa kweli alikuwa anaelewa vizuri sana mambo haya kuliko nilivyodhani.

"Niambie JC. Una mpenzi?" akaniuliza hivyo.

Nikiwa nimeshauachia uso wake, nikaangalia chini tu na kutikisa kichwa kukubali kwa unyoofu.

Mariam akavuta pumzi ndefu kiasi na kuishusha, akisafisha pua mara kwa mara, naye akaangalia chini na kusema, "Sawa. Nimeelewa."

Mh?

Nikaendelea kutazama chini kwa huzuni na kwa umakini pia, kwa sababu sikujua bado hali ya akili yake ingekuwa vipi baada ya hapo.

Akaniangalia kwa chini huku akidondosha machozi na kusema, "Asante. Kwa kuniambia ukweli."

Nikatikisa tu kichwa kuonyesha uelewa.

Akanishika kiganja kimoja na kusema, "Usijali JC. Nitakuwa sawa. Usiwaze kabisa. Hiki kidogo ulichonipa leo kimefurahisha sana... hujui tu..."

Nikamwangalia usoni kwa hisia.

"Ila wewe kuwa honest na mimi ni... ni kitu nimependa zaidi. Asante. Ndiyo moja ya mambo yanayofanya nikupende sana..." akasema hivyo kwa sauti yenye uchungu fulani hivi.

Nikaingiwa na simanzi zaidi na kushindwa kujizuia kudondosha machozi, nami nikasema, "Nisamehe Mariam..."

"Nisamehe pia JC..." akaniambia hivyo kwa hisia sana.

Nilishindwa hata kumwangalia usoni tena, na akiwa bado amenikalia, Mariam akakishika kichwa changu na kunikumbatia, akikiweka kifuani kwake na yeye kulaza kichwa chake juu ya changu kwa nguvu kiasi. Nikakaza macho huku machozi yakizidi kunitoka tu, nami nikaukumbatia mgongo wake pia huku nikihisi huzuni, hatia, na maumivu mengi sana moyoni mwangu.

Sijui ni kwa nini niliumia kiasi hiki, yaani ih! Roho iliniuma! Na binti kuwa mwelewa namna hiyo ndiyo kitu kilichonizidishia simanzi hata zaidi, yaani kwa huu muda wote wa likizo hakuna mtu mwingine aliyekuwa amenitoa machozi zaidi ya jinsi yeye alivyofanya. Nilikuwa na udhaifu mkubwa mno kwa huyu mwanadada, yaani wa hali ya juu. Sikuweza kuzuia hisia zangu mbele yake kabisa.

Mariam alilia kwa kwikwi na kwa pumzi, hakutoa sauti yaani, naye akaniachia baada ya sekunde chache na kujitoa mapajani kwangu. Akasimama kabisa mbele yangu, mimi nikimwangalia kwa hisia nyingi sana, naye akanionyesha tabasamu hafifu na kisha kuondoka kabisa hapo kwa Ankia.

Nikafunika jicho moja tu kwa kiganja na kujikaza nisilie, lakini ndiyo kile kilio cha uchungu kikaja kwa kasi zaidi. Kile cha ndani sana, kikitaka kitoke kwa nguvu zote, lakini nikajitahidi kuzuia hilo na kubaki sofani hapo nikiwa na huzuni kuu mno. Labda njia yangu ya kumfikia binti kwa asilimia zote haikuwa nzuri, nilikosea kwa vingi, lakini nilishukuru tu kwamba sikupitilizisha hayo makosa, na nikafanikiwa kumwambia ukweli. Alionekana kuumia, lakini alielewa. Ambacho kingebaki sasa ingekuwa kuona ni wapi jambo hilo lingeishia, kwa sababu nisingeacha kuhakikisha kwamba Mariam alikuwa sawa.








★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★


Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana
 
Wangapi walikua wanasoma huku wanamwambia jamaa aache asiendelee
Hahah mwanangu Elton unajua tukupe maua yako
Sema Mamu alishasema anapenda simu km ya Da Nuru huu ndo muda wa kumzawaidia ss ili atutolee jamu kwa Mimi
Siku analiwa Mimi nitakaa na Vaseline pembeni
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Rukia akaja mpaka karibu nami na kunishika mgongoni, naye akasema, "Acha kudengua bwana... I know you want it."

Nikaingiwa na hasira kali na kuushika mkono wake kwa nguvu, halafu nikamgeukia huku nikiupindishia pembeni. Akatoa sauti ya maumivu na kuinamia upande mmoja, ndiyo nikamwachia huku nikimsukuma kidogo.

"Iwe mwanzo na mwisho! Usije kunisogelea tena. Ukiniona, pita huko. Sitaki mazoea, umenisikia?" nikamwambia hivyo kiukali.

Akawa ananitazama kwa njia yenye hasira pia.

Wakaja wanaume wengine watu wazima hapo na kukuta hali haiko poa, na mmoja wao akauliza tatizo lilikuwa nini. Nikiwa namtazama Rukia kwa hisia kali, nikavuta ulimi kwa nguvu na kuondoka tu hapo, nikiwa nawaza mengi kweli. Tendo dogo la kipuuzi alilofanya huyo mwanamke lingeweza kunigharimu vikubwa, yaani sijui Miryam angenifikiriaje. Dah, yaani madhambi yangu ya nyuma yalikuwa yameanza kunirudia kwenye wakati ambao nilitaka yasahaulike kabisa, na matokeo ni kwamba yangeweza kuniharibia maisha mazuri ya mbele niliyotaka kujenga.

Nikashuka ngazi na kwenda kusimama sehemu ambayo nilijua lazima Miryam akitoka kule vyooni ni lazima angepita hapo, kama wanaume na wanawake wengine tu. Nilikuwa nimeingiwa na wasiwasi yaani, lakini najua nilitakiwa kuongea naye upesi. Nilitaka kufuta wazo lolote baya ambalo lingekuwa limemwingia baada ya kuona ile ishu. Sijui kwa nini tu alipaswa kuwa sehemu hiyo wakati huo huo Rukia aliponivamia, yaani!

Kumwongelea Rukia, mwanamke huyo akawa amepita hapo hapo nilipokuwa nimesimama, nami nikaendelea kutulia tu nikitazama pembeni kama vile simwoni. Akaendelea kushuka ngazi mpaka kurudi kule ndani ya ukumbi, na baada ya sekunde chache, Miryam akawa amefika hapo pia. Nilipomwona tu, nikamsogelea karibu na kutaka kumshika mikononi, lakini akajiweka katika hali ya kujihami na kurudi nyuma kidogo.

"Miryam..." nikamwita kwa sauti ya chini.

Akaangalia juu na huko chini, naye akasema, "Unafanya nini? Kuna mtu anaweza akatuona..."

"Miryam, sikia... ulichoona muda ule..."

Akatikisa kichwa huku akifumba macho na kusema, "Jayden, tutaongea baadaye. Nahitajika ndani."

"Miryam usinifikirie vibaya. Huyo mwanamke amenifata tu, halafu amelewa, me hata...."

"Najua, Jayden. Najua," akanikatisha kwa kusema hivyo.

Nikatulia.

Akanishika mkono na kusema, "Usihofu. Nakuamini. Najua huyo amekufata mwenyewe, na nimeona ulipomsukuma. Sijachukulia vibaya."

Nikahisi ahueni kidogo, maana hapo nilikuwa nimeshapandisha mzuka wa kufikiri angenitema.

Akasema, "Najua wanawake wengi watakuangalia kwa njia hiyo, hata mimi wanaume wengine hunitazama hivyo, kwa hiyo ninakuelewa. La muhimu ni kwamba nakujua, unanijua... nakuamini, unaniamini... kwa hiyo usihofu. Sijakufikiria vibaya, tuko vizuri."

Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Asante. Ila I'm sorry... haikuwa poa we' ku... kuona hiyo kitu."

Akapita mtu mwingine hapo, naye Miryam akaniachia mkononi na kuanza kushuka ngazi huku akiwa amenionyesha ishara ya mdomo kusema 'baadaye.'

Raa!

Ilinipa faraja kujua kwamba Miryam aliniamini, hata kama asingekuwa amenikuta kwenye hiyo hali aliyonikuta muda mfupi nyuma, alijua kwamba ninampenda. Nikatuliza tu makeke, na najua alichosema ni kweli, wanawake wengi walionyesha kuvutiwa na mimi na najua wanaume wengine walimtaka yeye pia. Kikubwa ndani ya uhusiano wangu na bibie kama kwenye mahusiano yote kilipaswa kuwa uaminifu. Haijalishi tulitoka wapi na tulifanya nini, jambo kuu kwenye mapenzi yangu na Miryam lingetakiwa kuwa uaminifu mpaka mwisho.

Kwa hiyo ingenibidi niwe mwangalifu zaidi kutokuja kumpa Miryam sababu yoyote ile ya kunishuku kabisa, maana mimi nilimwamini yeye kwa asilimia zote, hivyo na yeye ningetakiwa kumpa sababu za kuniamini sikuzote. Na alikuwa na akili tulivu yenye utambuzi mkubwa sana, yaani kama pale ingekuwa mwanamke mwingine mpenzi wangu ndiyo ameniona vile na Rukia, ningechuniwa mwezi mzima kabisa kama siyo kutemwa.

Hivyo hilo likiwa limewekwa pembeni, nikarudisha hali yangu ya kujiamini zaidi na kurudi pale ukumbini kumalizia sherehe ya Doris mpendwa wetu, ambayo ikaendelea kutupa wakati mzuri wa kuwa pamoja na familia na marafiki. Na huyo Rukia hakunisogelea tena, yaani alionekana mtulivu kabisa na kunipotezea, na hilo lilikuwa jambo zuri. Sikutaka tena ije izuke ishu kama hiyo aliyonifanyia huyo mwanamke, na kwa njia hiyo ningeendelea kufanya mapenzi yangu na bibie Miryam yastawi zaidi.


★★★


Basi, Jumapili ikawa imeingia. Namaanisha yaani, tulikaa kwenye hiyo sherehe ya Doris mpaka saa sita usiku, ndiyo tukaitafuta njia ya kurudi nyumbani na kufanikiwa kufika ikiwa ni saa saba inayoikimbilia saa nane kabisa. Mama wakubwa walikuwa wamechoka, hata Miryam na Mariam pia, na walifika kwao na moja kwa moja kwenda vyumbani. Sisi wengine tuliendelea kukaa kuongea kidogo mpaka saa nane yenyewe na ndiyo tukaagana sasa; Tesha na mpenzi wake, Happy, wakilala pamoja hapo kwao. Alikuwa ameshamtambulisha rasmi kwa dada yake.

Mambo baina yangu na Miryam yalikuwa mazuri tu. Hatukuwaonyesha wengine ukaribu wetu, ila hatukukosa kuonyeshana namna tulivyokuwa na uvutano mkubwa baina yetu. Ningemtumia jumbe kadhaa za utani na yeye kunijibu vizuri, akiwa amepotezea kabisa lile suala la Rukia kule ukumbini, kwa hiyo nilikuwa na amani. Niliingia kulala pale kwa Ankia ikiwa ni saa tisa kasoro, na mwanamke huyo vilevile akapumzika mida hiyo baada ya kuagana na Bobo.

Kwa hiyo nimekuja kuamka kwenye mida ya saa tatu asubuhi, na bado nilihisi usingizi lakini nikajitahidi tu kuamka. Umeme ulikuwa umekatika lakini ni vizuri kwamba niliilaza simu ikiwa chaji, hivyo nikanyanyuka, piga push-up sabini kunyoosha mikono, kisha nikatoka na kwenda kuoga.

Ankia alikuwa bado amelala, shauri ya kwamba yeye na Bobo walikunywa bia jana kwenye sherehe, kwa hiyo hapo alikuwa bado amepondeka maana tulirudi wakiwa wamechangamka. Ni mimi tu na Miryam, mama zake wakubwa na Shadya ndiyo ambao hatukunywa pombe jana, na nimseme Mariam pia ingawa ni wazi pombe haikuwa kitu yake kabisa. Lakini kalirudi kwao kakiwa kamebeba majuisi na makuku!

Hivyo, nilipomaliza kuoga nikavaa vizuri kabisa, mtoko wangu tu wa kawaida siyo kama nilivyokuwa nimevaa jana kwenye sherehe. Kuna sehemu nilitaka kwenda, lakini kwanza kabisa ningepita hapo kwake Miryam ili niwasalimie walio macho, halafu ndiyo ningekwenda huko nilikodhamiria. Nikamtumia bibie ujumbe wa salamu kuuliza kama alikuwa ameshaamka, lakini hakujibu. Sijui sana ikiwa angekuwa amekwishaamka lakini kwenda ilikuwa lazima ili kujua. Kwa hiyo nikatoka hapo, T-shirt nyeusi, jeans, raba nyeupe, huyoo nikaenda nje Ankia akiwa bado anakoroma.

Nilipofikia hapo getini kwake Miryam, nikakuta mlango mdogo wa geti uko wazi kiasi, nami nikaingia tu na kukuta gari la bibie likiwepo. Inaonekana kulikuwa na mtu ametoka, kwa hiyo nikaelekea mpaka hapo varandani na kuvua viatu kwanza, na mlango wa kuingilia ndani ulikuwa wazi, wazi kabisa yaani nadhani kuruhusu upepo na mwanga uingie ndani vyema. Kwa ukaribu huo, niliweza kusikia sauti ya Bi Jamila hapo sebuleni akiongea maneno yaliyohusiana na ndoa, nami nikatambua kuwa alikuwa akiongea na Miryam.

"... hadi raha jamani! Kila mtu alikusifia, kuna wengine, yule mama yake Shamte kwa mfano... akawa anasema umependeza mno kumzidi hadi bi harusi, kwamba unafaa kabisa kufanya harusi yako maana... hee... watasema tu!" Bi Jamila akasema hivyo.

Miryam akasikia akicheka kidogo na
kumwambia, "Na wewe unapenda kusikiliza maneno-maneno mama..."

"Ni ukweli! Ulimzidi Doris, sikwambii hivyo kumpakazia mwenzio ubaya, ila hadi mama yake aliona wivu. Sisi tunajua. Ona... najua tumeshaongea, ila... nilikuwa nimepigia picha jinsi send-off yako na wewe itakavyokuwa. Itapendeza sana, sana, sana! Mola ajalie niweze kuiona, yaani Mimi... naisubiri hiyo siku kwa hamu..." Bi Jamila akasema hivyo.

Nikaingia ndani hapo huku nikisema, "Na haitachelewa, mrembo wangu!"

Nilikuta wanawake hawa wawili pekee wakiwa wamekaa hapo sebuleni, Bi Jamila akiketi sofani huku anashona nguo fulani iliyoonekana kuwa ya Mariam, na Miryam akiketi chini kabisa ambapo meza ilisogezwa pembeni, huku kukiwa na beseni dogo lililokuwa na unga wa ngano uliokandwa, na ungo wenye vipande vidogo vilivyokandwa kwa kutenganishwa na bibie mwenyewe; nadhani akiviandaa kwa ajili ya kutengeneza chapati. Kuingia kwangu na kusema hivyo kukafanya wote waniangalie, nami nikakaa pembeni sofani huku nikitabasamu.

"Yaani mama, na Miryam atakuja kufanya bonge la send-off asikwambie mtu! Anatutulizia tu. Au uwongo Miryam?" nikasema hivyo na kumwangalia bibie.

Alikuwa ameshikilia kampira ka unga alikozungusha huku akinitazama kwa utulivu.

"Ahahah... kweli, yaani sipati picha. Ndiyo nachotamani zaidi kuona kwa ajili ya huyu mwanangu," Bi Jamila akaniambia hivyo.

Miryam akaendelea na kazi yake kwa utulivu tu.

"Na imeshasomeka, mrembo wangu. Mungu kashaiandika, inakuja, ni siye kungoja tu. Ahah... shikamoo?" nikamwambia hivyo Bi Jamila.

"Marahaba baba. Umeamkaje?" Bi Jamila akaniuliza.

"Vizuri. Naona nyie ndiyo wa kwanza kuamka. Wengine bado wanavuta mashuka?" nikamuuliza hivyo.

"Aa... ni Zawadi na Mamu tu. Shadya na yeye ameondoka mapema. Tesha ndiyo amemsindikiza mchumba wake huko barabarani, anarudi kwao," Bi Jamila akasema hivyo.

"Dah, na Tesha anaenda kuoa hivyo..."

"Nakwambia! Ahah... kameamka mapema hako kadada, kakapiga deki hapa, kakaosha na vyombo, halafu kamemsalimia Miryam kwa heshima kweli, yaani! Nimekapenda," Bi Jamila akasema hivyo.

"Ahahahah... mmekuza..." nikasema hivyo.

"Eeh, Tesha kawa kidume. Miryam ndiyo... bado bado anajivuta," Bi Jamila akaongea hivyo kwa njia fulani kama amekwazika.

Miryam akamtazama kwa yale macho ya 'aaaa jamani,' naye Bi Jamila akatabasamu.

Nikamwangalia bibie na kusema, "Ila ni kweli. Kuna kale kamsemo sijui 'chelewa chelewa utapitwa,' ndiyo kanamvizia Miryam naona..."

Miryam akanitazama usoni kiumakini, nami nikabana tabasamu langu.

Bi Jamila akasema, "Umeona JC? Me huwa namwambia. Ushauri tu. Afanye upesi, eh? Aolewe, tucheze na wajukuu..."

Miryam akasema, "Mama...."

"Mrembo wangu yuko sahihi kabisa. Ndoa itakupendezea sana Miryam, yaani vile Doris alivyokuwa jana, wewe itakuwa mara mia!" nikamwambia hivyo.

Akakaza midomo yake huku akiniangalia kwa ile njia ya kiukali, kama kuniuliza nafanya nini.

"Kabisa! Atapendeza mno. Sema unajua nini, sasa hivi nimeshaelewa kwamba ni uamuzi wake, na... atapaswa apate mtu wa kumpenda na yeye ampende. Hatuwezi kulazimisha tunayotamani na yeye ayatamani, maisha ya siku hizi siyo kama ya zamani. Uwongo JC?" Bi Jamila akasema hivyo.

"Ni kweli. Mama yaani unasema kweli kabisa. Kwenye suala la uchaguzi ndiyo moyo unahusika, siyo kitu cha kuwahisha tu maana Miryam akisema awahishe anaweza akapata limtu litakalomtendea vibaya baadaye, anakuwa na busara kuangalia kwa umakini ni nani atakayemfaa, na akimpata akaridhika, ndiyo anabebwa naye sasa..." nikasema hivyo na kumkata Miryam jicho la pembeni.

Alikuwa anafinya tu ngano huku akiniangalia kama vile hataki, na mimi hapo nilikuwa nakoleza tu uchokozi.

Bi Jamila akasema, "Ni kweli kabisa. Sisi tulikuwaga tunachaguliwa waume nakwambia. Yaani unakaguliwa, halafu unapelekwa kwa mwanaume anakuoa. Sasa hivi mambo yamebadilika, lazima kuacha mtu achague mtu anayemfaa. Kabisa yaani, nimejifunza hilo."

Nikatabasamu kwa hisia na kumwambia, "Ndiyo hali halisi. Na siyo kwa wanawake tu, hata sisi. Mimi kwa mfano, kama nilivyokwambia siku ile, yaani nahakikisha kwamba nimepata mwanamke ambaye najua nitatulia naye kabisa ndiyo tunafunga ndoa. Lakini hiyo ni mpaka na mimi niwe na uhakika wa kwamba nitatulia. Hakuna kurukaruka kama nyani, no. Ndiyo ndoa itadumu."

Bi Jamila akatikisa kichwa kukubali hilo.

Nikamwangalia bibie na kumtikisia nyusi kidogo, naye akatikisa kichwa kama kuonyesha anakerwa sana na haya maongezi ya kimafumbo kutoka kwangu na mama yake mkubwa, wakati mada iliyemhusu alikuwa yeye, na alikuwa hapo hapo akiongelewa kama vile hayupo.

Bi Jamila akasema, "Kwa hiyo JC, ngoja nikuulize kitu. Hivi... kwa mwanamke kama Miryam, unadhani ni mwanaume wa aina gani anafaa kuwa naye ili ndoa itulie na azae vizuri?"

"Mama!" Miryam akamwita kimshangao.

Mimi mwenyewe nilimshangaa, sikuelewa aliuliza hivyo katika maana ipi, naye Bi Jamila akasema, "Namaanisha kwamba, yaani katika haya masuala ya uzazi, nimeangalia umri wako Mimi. JC ni daktari, yaani nataka kujua anaonaje... usalama uliopo kwako wewe kuzaa umri ukiwa umeshafi...."

"Mama, hilo siyo suala la kuzungumzia tukiwa na...."

"Haina shida, naweza kujibu," nikamkatisha bibie.

Miryam akaniangalia usoni kimkazo.

"Katika njia ya kidaktari zaidi, si eti?" nikasema hivyo kumwelekea Bi Jamila.

Bi Jamila akasema, "Eeeh, yaani nataka tu kujua. Umri wake Miryam ni mkubwa, na hajawahi kupata ujauzito..."

Miryam akafumba macho na kuinamisha uso wake, nami nikabana tabasamu langu kiasi.

"Kwa nyakati hizi tuseme akaolewa, akapata ujauzito, usalama upo mzuri wa yeye kujifungua?" Bi Jamila akamalizia swali lake.

"Naweza kusema ndiyo. Ana afya nzuri..." nikasema hivyo na kumtazama Miryam usoni.

Yeye akawa ananiangalia kwa mkazo.

Nikasema kizembe, "Na ana mwili mzuri pia..."

Miryam akaangalia pembeni huku akizungusha macho kiasi, akiendelea kuikata ngano.

Nikamtazama Bi Jamila na kumalizia kwa kusema, "Na hata kama tuseme kukitokea tatizo linaloweza kufanya iwe ngumu, siku hizi kuna njia za kitaalamu za kuwasaidia wanawake wanaojifungua wapitishe mtoto salama. Kwa hiyo anaweza kujenga familia vizuri tu."

"Eti eh?" Bi Jamila akauliza.

"Kabisa. Yaani kiulaini..." nikasema hivyo.

Niliposema kiulaini, nilikuwa nafikicha viganja vyangu kuonyesha huo ulaini, nami nikamtazama Miryam kukuta amenikazia jicho, kitu ambacho kikafanya nijikaze kutotabasamu.

Bi Zawadi akauliza, "Kwa hiyo hata akifikisha miaka arobaini, bado anaweza kupata watoto bila changamoto?"

"Ih! Tena miaka arobaini tu? Yaani anajifungua mapacha watatu bila tatizo kabisa," nikamwambia hivyo kwa uhakika.

"Kweli?" Bi Jamila akauliza.

"Eeh..." nikasema hivyo.

Miryam akaendelea kuniangalia usoni kwa njia ya kukerwa.

"Tena yaani Miryam, mpe mazingira mazuri sana, mwanaume anayemfaa kabisa, anazaa watoto wazuri bila shida hata chembe," nikamwambia hivyo Bi Jamila.

"Kumbe? Basi ni mwanaume yupi unayefikiri anamfaa? Yaani... apate mume wa aina gani ili amwandilie mazingira ya hivyo?" Bi Jamila akaniuliza.

Nikamwangalia bibie usoni, yeye pia akiwa ananiangalia kwa macho makini, nami kwa makusudi nikasema, "Mwanaume kama... mimi kwa mfanoo...."

Miryam akakaza midomo yake huku akitikisa kichwa chake kwa ukakamavu kunizuia nisiropoke upuuzi.

Nikajitahidi kuzuia tabasamu na kumalizia maneno yangu kwa kusema, "Mimi kwa mfano siwezi kusema kwa uhakika. Hapo ndiyo tutarudi tena kwenye ishu ya yeye kuamua. Maamuzi yote ni yake, maana tunaweza kuorodhesha sifa zote hapa, ila... mwisho wa siku unaelewa kwamba hakuna mtu mkamilifu. Si unajua?"

Bi Jamila akasema, "Hmm... ni kweli."

Miryam akaendelea kusugua ngano mkononi na kunitolea ishara kwa mdomo wake kama kusema 'hivi we ukoje?' nami nikatabasamu kiasi.

Bi Jamila akasema, "Basi me naendelea tu kumwombea binti yangu aolewe, na ajifungue mapema na salama. Ndiyo kitu nachotamani zaidi kuona kabla...."

"Mama..." Miryam akamkatisha kwa kumwita hivyo.

"Ahah, nisamehe mwaya. Naongea mno," Bi Jamila akamwambia hivyo na kumpiga kidogo begani kishosti eti.

Miryam akaendelea na kazi yake. Kwa sababu fulani, niliona ni kama vile hakuwa sawa kabisa kihisia, siyo kwa sababu tu ya hizi mada, ila ni kama kulikuwa na jambo lingine akilini mwake lililomsumbua.

Bi Jamila akasema, "Umeshakunywa chai baba? Nikuwekee japo kavu, bado chapati hazija...."

"Oh mrembo wangu, usijali. Niko poa. Nilikuja kuwacheki kwanza kabla sijatoka. Kuna sehemu naenda," nikasema hivyo na kumwangalia Miryam.

Bibie hakuniangalia machoni, lakini nikaona macho yake yakipanda kiasi baada ya kusikia kauli hiyo.

"Wapi, kanisani?" Bi Jamila akauliza.

"A-ah, naenda tu kufatilia mishe fulani hivi, halafu nageuka," nikamwambia.

"Haya sawa. Siku hizi Mamu ametulia zaidi, hamchezi kama vile mwanzoni, yaani naona anapona kabisa JC," Bi Jamila akaniambia hivyo.

"Yeah, anaendelea vizuri sana. Mungu anasaidia. Nitakuja kumcheki na yeye baadaye pia," nikasema hivyo.

"Sawa baba, uwe na safari njema," Bi Jamila akaniaga namna hiyo.

Nikasema, "Amen. Miryam, me naenda..."

Nilimwongelesha kwa sauti ya chini, naye akapandisha macho yake mazuri kuniangalia huku akiwa kama amevimba yaani, nami nikatabasamu tu na kunyanyuka kutoka sofani, na moja kwa moja nikaelekea nje. Hisia zangu za bibie kusumbuliwa na jambo fulani bado zilikuwepo, hivyo ningetakiwa kujua ikiwa zilikuwa za kweli nikija kukutana ama kuwasiliana naye baadaye, lakini kwa sasa nikaamua kwenda kuchukua usafiri ili nielekee huko Kawe. Ndiyo, Kawe.

Nilitaka kwenda kuhakikisha ishu ya Festo kuondoka, na cha kwanza ingekuwa kujua alikuwa ameiacha nyumba yake katika msimamo upi, ndiyo ningetafuta njia ya kujua pia ikiwa kweli aliondoka nchini ama zilikuwa swaga tu.

★★

Safari ya kuelekea huko Kawe ilichukua muda wa saa kama moja na nusu, nami nikaenda kule ambako nyumba maridadi ya Festo ilikuwepo. Hali ya nyumba hii ilikuwa vile vile tu kwa namna nilivyoikumbuka, hivyo nikasogea mpaka getini na kubonyeza tufe la kengele. Ikanibidi nibonyeze kwa mara nyingine tena baada ya dakika kama mbili kupita bila ya geti kufunguliwa, ndiyo likawa limefunguliwa hatimaye.

Aliyefungua hakuwa mwingine ila yule yule mlinzi wa nyumba hii, na alinikumbuka, hivyo tukasalimiana vizuri kabisa, halafu nikaulizia ikiwa bosi mkubwa alikuwepo. Mwanzoni hakutaka kutoa jibu la moja kwa moja na kunihoji kwa nini nilimuuliza hivyo, nami nikampiga za kijanja kwa kusema nilihitaji tu kuonana naye ana kwa ana maana zilikuwa zimepita siku kadhaa hatujaonana, na kwenye mawasiliano sikuwa nikimpata. Ndiyo akawa ameniambia kwamba jamaa hayupo, amesafiri. Hivyo tu.

Katika ile njia ya kuendeleza maigizo, nikamuuliza ikiwa alijua jamaa angerudi lini maana inaonekana alikuwa akijilinda kutokana na hali fulani ndiyo sababu akawa hapatikani, na ilikuwa muhimu sana niongee naye maana alikuwa bosi wangu pia. Ndiyo huyu mlinzi akasema kwamba Festo alikuwa ameondoka nchini. Yaani hakutakiwa kumwambia yeyote, ila aliniambia kwa sababu tu alielewa hizo mishe zetu na nini, kwa hiyo akasema jamaa ameondoka nchini na hajui atarudi lini.

Ila kama ni kitu ambacho mlinzi alielewa, ni kwamba hii nyumba ingeuzwa, na yeye hapo asingechukua muda mrefu kuondoka. Akasema inawezekana kulikuwa na matatizo na bosi wetu ndiyo alikuwa anayakimbia, kwa hiyo akanishauri niwe makini na mwangalifu sana nisije nikajikuta nakuwa kama yule shefu Saidi. Alijiongelea na yeye pia katika hiyo maana, kwa hiyo nikamwambia alikuwa akisema kweli kabisa. Nikatega pia kwa kuuliza ikiwa Festo aliondoka kwa kutumia ndege, naye mlinzi akasema ndiyo, tena alimsindikiza jamaa mpaka airport na kuhakikisha analirudisha gari lake huku.

Ahaa? Hapo nikawa nimepata nilichohitaji, lakini bado nilitaka kuwa na uhakika ZAIDI. Mlinzi alikuwa msaada tosha, lakini niliona uwezekano wa mambo aliyoniambia kuwa uwongo tu uliopikwa na Festo mwenyewe ili ajilinde zaidi, ningejuaje? Kama nyumba ingeuzwa, ina maana na magari yangeuzwa pamoja nayo? Nikataka kupata uthibitisho mwingine tena.

Kwa hiyo nikampa tu mlinzi heri nzuri na kumwomba samahani ya usumbufu, huku nikielewa wazi kwamba angeweza hata kumwambia Festo kuwa nilikuja kumtafuta. Ila hakungekuwa na shida sana maana niliigiza kutojua kwamba jamaa aliondoka, na kwa upande wake Festo wa mambo hilo lilikuwa kweli.

Baada ya kuondoka eneo hilo, nikavuta simu yangu na kumpigia Adelina. Zilikuwa zimepita siku chache bila ya sisi kuwasiliana tokea ile siku amepewa taarifa kuwa nilikufa, baada ya kuwa nimeibiwa simu na kuirejesha, kwa hiyo alipopokea kukawa na hisia nzuri ya mwanzo baina yetu.

"JC, mambo?" akasikika upande wa pili.

"Safi Adelina. Za kwako?" nikamsalimu pia.

"Nzuri, Mungu anasaidia. Wazima Mbagala?"

"Tunaendelea poa tu. Vipi, uko bize?"

"Hapana, leo nimetulia tu ndani. Jumatatu mpaka Jumamosi ndiyo nakuwa kazini," akasema hivyo.

"Ahaa... kumbe umeshaanza kazi?"

"Yeah, sikukwambia?" akauliza.

Nikakunja ngumi na kufanya 'yes' kimya-kimya, halafu nikasema, "Hapana, ulikuwa hujaniambia kama umeanza tayari, ila ulisema tu unakaribia kuanza. Lazima mambo yawe mengi."

"Eeeh bwana, ndiyo nimeanza hii wiki. Mambo ni mengi ndiyo, si unajua international airport?"

"Wacha we,'" nikasema hivyo.

Akacheka kidogo.

"Unadili na mambo gani?" nikamuuliza hivyo.

"Ninafanya service ya kutoa tiketi na kukagua passport, ama vitambulisho maalumu. Yeah," akaniambia hivyo.

"Umeridhika eeh?"

"Sana. Napenda sana kuwa hapo, ingawa masaa ni mengi ya kazi, ila shift tunabadilishiwa. Najihisi nimefika nyumbani."

"Hongera mwaya. Uko pazuri," nikamwambia hivyo.

"Ahah... asante. Ila siyo pazuri kama kwako wewe daktari..."

"Aa wapi, kwangu ndiyo pagumu, yaani! Asikwambie mtu," nikasema hivyo.

"Ila angalau tukiwa hivi na kazi, maisha yanasonga vizuri. Tunapata chance kuyaboresha, na kuwasaidia wengine. Kama tu wewe unavyofanya," akasema.

Nikatabasamu na kumwambia, "Ni kweli kabisa. Hivi... Adelina, kwa mfano tuseme nataka kujua ikiwa mtu amepaa na ndege kwenda labda nchi jirani, au wapi... ndani ya hizi siku chache... inawezekana?"

"Yaani kama amesafiri kwa ndege jana au juzi?"

"Eeh..."

"Yeah, inawezekana. Rekodi zinakuwepo, ni kutafuta tu jina la mtu unayetaka kujua amesafiri lini, tunaangalia, then...."

"Ooh, sawa," nikawa nimeelewa.

"Kuna mtu unataka kujua kama amepanda ndege?" akauliza.

"Eeh, na nitaomba unisaidie ili kujua kama kweli alipanda ndege. Ni rafiki yangu, nasikia ameenda Nairobi hapo juzi ila sijui lini. Nitakupa jina lake ujaribu kuniangalizia, eti? Ikiwa itakuwa sawa..." nikamwambia hivyo.

"Itakuwa sawa ndiyo, usijali. Si amesafiri hizi siku chache za mwisho?" akaniuliza.

"Eeh, yaani wiki hii hii kutokea Jumamosi iliyopita..."

"Mhm... JC bwana! Usiniambie haya ndiyo yale masuala ya kufatiliana mpaka Nairobi... wivu na nini..." Adelina akasema hivyo huku akicheka.

Nikacheka kidogo pia na kusema, "Hamna, siyo hivyo."

"Mmm, haya. Nitakuangalizia. Usijali. Utanitumia jina la mwenzako, kesho nikiweza nitaangalia," akaniambia hivyo.

"Asante sana. Nitakupa na zawadi," nikasema hivyo.

"Ahahah... kutafuta jina tu?"

"Eeeh, utastahili zawadi. Au hupendi zawadi?"

"Napenda. Utanipa Zawadi gani sasa?"

"We' ungependa ipi?"

"Mmmm... ni wewe tu uchague. Utakayopenda, nitaipenda," akasema hivyo.

"Au siyo?"

"Eeeh. Na uje kututembelea huku kwetu Kinyerezi. Itakuwa zawadi nzuri sana."

"Usihofu. Siku siyo nyingi nitakutembelea. Na si unatulia hasa kwenye Jumapili?"

"Eeh, Jumapili ndiyo nakuwa home. Karibu sana, hata ijayo uje basi," akanisihi.

"Sawa. Nitafanya hivyo. Ndiyo naelekea kupanda gari kurudi home pia, nilikuwa nimetoka," nikamwambia.

"Ahaa, basi sawa, tutawasiliana eh? Ndiyo na me nataka kupika," akaniambia.

"Haya dear, baadaye," nikamuaga.

"Poa."

Baada ya mazungumzo hayo, sasa nikawa nimejipatia uhakika wa kuthibitisha zaidi ikiwa kweli Festo alikuwa ameondoka, na nikawa natumaini kwamba jambo hilo lingekuwa kweli kwa asilimia zote. Ikiwa aliondoka nchini, basi amani yangu na bibie Miryam ilikuwa ya uhakika, hasa kwa wakati huu, hivyo ningetakiwa kulipata jina kamili la jamaa na kumtumia Adelina ili hatimaye niupate uhakika huo.

Nikaamua kwanza kwenda kwenye mgahawa mmoja mzuri ili kupata mlo, maana sikuwa nimekula tokea asubuhi hadi mida hii ya saa saba mchana, na baada ya hapo safari ya kurejea Mbagala ikaanza.

★★

Nimekuja kufika Mzinga kwenye mida ya saa tisa kuelekea kumi, nami nikaelekea kwa Ankia moja kwa moja na kumkuta mwanamke huyo akiwa zake ndani anamalizia kutengeneza mahanjumati. Alikuwa amechelewa kupika cha mchana maana aliamka muda umeenda halafu akanywa supu kwenye saa sita, kwa hiyo wakati huu alikuwa akiunga mboga ili ajilie na wali wake mwenyewe kupata nguvu zaidi. Mimi nikiwa nimeshiba bado, nikamwambia ningeingia tu kupumzika maana nilijihisi uchovu, ule uchovu wa uvivu tu, naye akasema haya, angeendelea kuwepo tu hapo.

Kwa hiyo nikaingia zangu chumbani na kubadili mavazi, nikivaa nguo nyepesi, kisha nikajitupia kitandani na kuwasha simu. Moja kwa moja nikamtafuta bibie wangu, nimchatishe wee maana najua alikuwepo nyumbani kwake tu leo. Wakati natoka huko Kawe nilikuwa nimemtumia jumbe kadhaa, tuka-chat kidogo WhatsApp na yeye kusema yupo tu nyumbani na kuna vitu alikuwa akishughulika navyo, kwa hiyo nilimwacha kwa kumwambia narejea Mzinga na ningemtafuta nikifika. Ndiyo nikawa natimiza ahadi sasa.

Katika suala la kuchat, Miryam alipendelea tutumie zaidi WhatsApp na siyo sms kawaida, kwa hiyo alinipatia pazuri maana mimi pia nilipenda kuwa 'online' muda wote, ikiwa sikuwa tu na mambo mengi yaliyoninyima muda wa kuchat na watu. Hivyo nikamcheki, akajibu, nasi tukaanza kuchat sasa. Nilikuwa nauliza kiutani kama chapati zimebaki ili niende kula, kama Mariam yuko poa, nikaingiza utani na utani mwingi yaani, lakini Miryam hakuwa amezama sana kivile katika mawasiliano haya pamoja nami. Yaani hata tu kwenye kuchat ningeweza kuhisi kwamba hakuwa ndani ya hali ya kawaida kihisia.

Kwa hiyo nikamwambia nataka kumwona. Akasema niende kwake nimwone kama nataka, lakini nikasema nataka yeye ndiyo aje hapa. Akaonyesha kutotaka hilo maana hakupenda kujichoresha kwa kuanza mazoea ya kuja kwa Ankia mara kwa mara, nami nikamwambia asiwe na hofu. Kwa leo tu, muda huu hasa kwa sababu alikuwa huru, ingefaa aje ili tuongee mawili matatu, tukiwa chumbani kwangu, yaani ukaribu wetu ukue zaidi, na nikamwambia nina njia ya kumleta bila kuzua michoro mingi.

Akawa amekubaliana na hilo hatimaye, naye alipouliza ni njia gani, nikamwambia atulie, inakuja muda siyo mrefu. Akaelewa haraka kwamba nilitaka kumtumia Ankia, naye akasema nisimsumbue rafiki yake bwana. Nikamwambia tulia wewe, sikubali kushindwa mpaka nihakikishe anakuja, na ndiyo kweli nikamfata Ankia kumwomba aende hapo kwa bibie kuzuga-zuga na nini, halafu amtoroshe kijanja aje kunipa company kidogo ya ana kwa ana. Ankia alikuwa hataki eti, nami nikamshawishi kwa kumwambia ningempa zawadi nzuri kabisa, nalo ndiyo likanyanyuka na kwenda hatimaye.

Nikajawa na furaha kweli moyoni, nami nikarudi zangu kitandani na kuendelea kuchat na bibie. Nikamjulisha kuwa mpitiaji ameshatumwa, hivyo ningemsubiria yeye mletwaji afike. Nimetulia hapo kwa dakika kama ishirini hivi, ndiyo nikasikia Ankia akiwa amerejea tena huko sebuleni, na alikuwa ameurefusha kweli huo upitiaji. Nilisikia anaongea na mtu, najua ikiwa ni bibie, nami nikaendelea tu kujilaza kitandani kwa utulivu huku nikiegamja mto.

Mlango wa chumba changu ulipofunguliwa, nikatazama hapo na kuachia tabasamu hafifu huku nikimwangalia mwingiaji, malkia wa moyo wangu, Miryam mwenyewe. Alikuwa amevaa T-shirt jeusi wakati huu, la mikono mifupi, pamoja na khanga nzuri nyeupe iliyofunika umbo lake la chini kuficha alivyovaa kwa ndani. Mwonekano wa kawaida tu huku akiwa amezibana nywele zake kwa nyuma, lakini uzuri wake uliufanya hata huo mwonekano uonekane kuwa wa hali ya juu. Hizo nguo zilikuwa na raha sana kuvaliwa naye!

Akiwa ameshika simu yake kiganjani, akarudishia mlango tena mpaka kuufunga, kisha akaanza kuja hadi karibu kabisa na sehemu niliyojilaza na kusimama huku akinitazama kwa utulivu tu. Kulikuwa na nafasi ya wazi usawa wa sehemu niliyojilaza, nami nikakishika kiganja chake na kumvuta kwangu ili akae. Akashuka taratibu na kukaa hapo kitandani, nami nikalalia ubavu na kupitisha mkono wangu kwenye kiuno chake, nikimvuta-vuta kichokozi.

"Mpenzi wangu kafika. Nilikuwa nimem-miss huyo!" nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Akaniangalia tu machoni, na kwa sababu fulani, bado niliona kwamba alikuwa makini sana, kama vile kuna jambo lilikuwa linamsumbua.

"Vipi? Mbona kama umenuna?" nikamuuliza kwa sauti ya kudekeza.

Akiwa ananiangalia tu usoni, akatikisa kichwa kuonyesha hakuna kitu.

"Ama ndo' unanipa silent treatment shauri ya yale maongezi yangu na mama mkubwa wako saa zile?" nikamuuliza hivyo huku nikitabasamu.

Akasema kwa sauti ya chini, "Halafu hayo masihara yako wewe! Ulikuwa unamwingizia ma' mkubwa vitu vya ajabu kichwani, sijui ukoje..."

"Ahahahah... natamani useme 'ntakuchhapaa,'" nikamwambia hivyo kiutani.

"Na ipo siku nitakutandika kweli," akasema hivyo na kuangalia pembeni, akiwa makini yaani.

"Ahahahah... basi nisamehe... ikiwa hiyo ndo' imekufanya uwe grumpy namna hii," nikamwambia hivyo kwa sauti ya kudekeza.

Akasema, "Hamna, wala siyo hivyo."

"Sa' mbona umeweka hilo pozi? Kuna mtu amekulazimisha umeze chura hapo ulipotoka?" nikajaribu kumtania.

Akawa ananiangalia tu usoni kwa njia ya kuonyesha utani haujamwingia.

Nikaendelea kwa kusema, "Niambie. Ni nani? Au umemmeza chura kwa kupenda mwenyewe?"

Akaendelea tu kuniangalia kama vile hataki.

Nikamwambia, "Sema kama umekula chura, Miryam. Na me nina kitabu changu cha sheria, nataka nikupige busu, sasa... utapaswa uondoe hilo gaga la chura mdomoni kwanza, siwezi me kupita na huo ulimi aisee. Kuna mswaki hapo.... ila hamna, tumia brashi kabisa la kusugulia jeans liko hapo, afu' finya dawa yote ya mswaki mpaka iishe ndo' u...."

Akaangalia pembeni taratibu na kutabasamu kiasi kwa kukunja midomo yake.

Nikacheka kidogo na kumtikisa kiasi, nami nikaegamia kiwiko changu ili nijinyanyue, halafu nikambusu begani na kisha kusema, "Unaonekana kuchoka. Nilikuwa tayari kwa mechi, ila kama unataka tuiahirishe siyo mbaya, kwanza... hata tiketi za mashabiki hatukuwa tume...."

Akacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "Acha ujinga!"

Nikacheka pia na kuishika shingo yake taratibu, naye akanigeukia.

Nilikuwa nimeshapandwa na hisia nzuri sana kwa kuwa karibu naye namna hii. Nikawa naisugua shingo yake taratibu kwa kidole gumba huku nikiashiria kumfata mdomoni, naye akasogea zaidi na kuufata mdomo wangu pia. Hii ndiyo ikawa mara ya tatu midomo yetu kukutana na kupeana denda tamu kabisa. Tukaziunganisha ndimi zetu na kisha kuanza kupiga busu laini za taratibu, kama wazungu vile, naye ndiyo akaikatisha na kuibana midomo yake kiasi. Alikuwa ameshafanya niamshe balaa, lakini nilipomwangalia tena nikaona kwamba hakuwa sawa kabisa. Kuna kitu 'serious' kilikuwa kinaitafuna akili yake.

Akawa ameinamisha tu uso wake kiasi huku naye sasa akiwa amenishika pajani, nami nikamwambia, "Naona kuna kitu kinakusumbua."

Akaniangalia machoni kwa utulivu.

"Niambie. Kuna nini?" nikamuuliza kwa umakini zaidi.

Akashusha pumzi kiasi na kusema, "Sijui ninakuwa paranoid tu, au... yaani sielewi akili yangu imekuwaje."

"Paranoid? Shida ni nini kwani?" nikamuuliza kwa upole.

Akaniangalia na kusema, "Mamu."

Nikawa makini zaidi na kuuliza, "Amefanyaje?"

"Jana usiku, tulipofika ndani tukaongea kidogo kabla ya kulala. Alikuwa ananiuliza vitu, namwelekeza, sasa... mada ikawa imegeukia kwa wanaume. Alitaka kujua mengi... yaani nimfundishe vitu kwa sababu anafikiri mimi nina experience zaidi. Sikutarajia, ila hiyo sudden interest yake ikanifanya nimchimbe zaidi. Ndiyo akawa ameniambia kwamba... kuna mtu anampenda," Miryam akasema hivyo.

Nikakunja uso kimaswali kiasi, kisha nikajikuta naanza kucheka. Nikalalia mto tena na kuendelea kucheka tu, lakini Miryam alikuwa ameangalia pembeni kwa njia fulani kama vile amevunjika sana moyo, kwa hiyo nikajituliza na kukaa vile vile nilivyokuwa nimekaa karibu naye.

"Mariam amekwambia hivyo?" nikamuuliza hivyo huku nikitabasamu.

Akabaki kimya na kuendelea kutazama pembeni tu.

"Miryam... kumbe ni hivyo tu? Me nikafikiri unataka kusema kweli umemeza chura halafu mwenzio hapa nimeshakubusu! Umeniokoa kupata presha," nikamwambia hivyo kiutani.

Akaniangalia machoni kwa njia ile ile ya umakini.

Nikamwambia, "Usiogope Miryam. Najua unachowaza. Sawa... haya mapenzi ya siku hizi huwa yanaleta matatizo tu hasa kwa vijana wadogo, ila... hata ufanye nini... Mariam atayapitia pia. Amekaa ndani muda mrefu, kwa muda huo kuna watu walimwona kama mtoto tu, ila kwa kuwa sasa hivi afya yake inarudi mahala pake, ni lazima mvuto wake utaanza kuonekana tu kwa wengi... na yeye atakuwa na choice zake."

Miryam akaendelea kuniangalia tu kwa umakini.

"Ahah... nafikiri sherehe jana inaweza ikawa ime-trigger something... atakuwa ameona mengi, na ameona wengi. Sikia... naelewa. Najua ni muhimu kumlinda bado, ila huwezi sikuzote kumchunga. Ameshakua, na ameanza kujitambua tena. Kwa hiyo... the best way to protect her ni kumpa mwanga zaidi... mwongozo mzuri sana... akili yake ipo, najua atakuelewa..." nikamwambia hivyo kistaarabu.

Miryam akaendelea tu kuniangalia machoni baada ya mie kusema hayo.

Nikawa naisugua shingo yake taratibu, na nilipenda sana kufanya hivyo maana ilikuwa lainiii, kisha nikamwambia, "Usijali. Bila shaka... hata alipokuwa ameanza kuzinguliwa na lile suala la kichwa mpaka kipindi hiki, haya mambo ya... uanamke... si ulikuwa unamsaidia?"

Akatikisa kichwa mara moja kukubali.

"Basi, najua yuko poa, anajielewa... maana we' dada yake najua unamtunza vizuri," nikasema hivyo na kumbonyeza mbavuni kwa kiganja changu kingine.

Akashtuka kidogo na kupiga ulimi mdomoni kiasi, naye akautoa mkono wangu hapo kama vile hataki yaani, ndiyo akasema, "Tatizo siyo hilo."

"Sasa shida ni nini? Unahofia atapata mtu halafu atatoroka home, au? Asingekuwa ameongea na wewe, anafunguka kwako kwa sababu anajiamini, na anakuamini. Halafu... hebu kwanza niambie huyo jamaa aliyesema anampenda ni nani? Unamjua?" nikamuuliza hivyo.

Akaniangalia machoni kwa njia ya kutatizika.

Nikasema, "Asije akawa muhuni wa hiki kitaa ila, hapo ndiyo itakuwa shida. Au alimwona jana kwenye send-off? Inawezekana ikawa amekumbuka amewahi kwe...."

"Ni wewe," Miryam akanikatisha kwa kusema hivyo.

"Naam? Nini?" nikaitikia kauli yake kwa kutoelewa.

"Mamu anakupenda wewe, Jayden," akaniambia hivyo kwa sauti isiyosikika kuwa na raha.

Eh!

Kwa sekunde chache nikabaki kumwangalia usoni utadhani sikuwa nimesikia alichotoka kusema, naye akawa amenikazia macho yake tu.

"Ahah... Miryam acha masihara basi..." nikamwambia hivyo.

Akaendelea tu kuniangalia machoni kwa njia ya kuonyesha utani haukuwepo hapo.

Nikajivuta na kukaa kitako kabisa, na kwa sauti ya chini nikamuuliza, "Mariam amekwambia ananipenda mimi?"

Akasema, "Ndiyo. Sana."

Nikabaki kumtazama kwa utulivu.

"Hisia zake ziko in check sasa hivi. Anajua anachokitaka, na wewe ndiyo hiyo choice yake. Tena... ameniambia ni tokea muda mrefu tu, sema anakuonea aibu, anasema hajui jinsi ya kuongea na wewe. Leo tena akakuulizia, mida fulani hapo akanisemesha tena, ameniambia nije nimsaidie kumuunganishia kwako... kwa sababu hajawahi kutongoza mwanaume," Miryam akasema hivyo huku akiniangalia kwa ile njia ya ukakasi yaani.

Ohohoo! Tatizo hilo!

Yaani nilikuwa sijategemea kabisa hiki kitu. Nikawa nimetambua sasa kwamba hili suala lilikuwa limemkosesha amani sana Miryam, kwa sababu alikuwa katikati ya uchaguzi wa kuugawanyisha upendo aliokuwa nao kwa mdogo wake, na upendo aliokuwa nao kwangu. Ni wazi kwamba hakutaka kuziumiza hisia za mdogo wake kabisa, lakini hakujua afanye nini ili kutimiza hilo.

Ingekuwa ni juu yangu, na sote tulijua kwamba kwa njia yoyote ile, ningetakiwa kumweka wazi yule binti kuwa nisingeweza kufanya mahusiano naye, sema tu ndiyo hicho ambacho Miryam alikuwa akikiogopa; kujua kwamba kwa vyovyote vile mdogo wake angeumia tu. Nilitakiwa kutafuta njia ya kumwambia yule binti ukweli wa hisia zangu bila kuchukua kisoda na kuukwangua moyo wake mchanga, yaani nimuumize bila kumuumiza sana.

Hali ya ukimya ikakijaza chumba hiki kutokana na sisi wawili kuzama kwenye kina kirefu cha fikira, nami nikamwangalia Miryam na kuona ametazama tu pembeni kwa mawazo. Nikakishika kiganja chake kwenye kitanda taratibu, lakini hakugeuza shingo yake kunitazama.

Kwa upole, nikamwambia, "Miryam... sidhani kama... yaani... itakuwa tu ni suala la kuongea naye. Namwelewa vizuri, kwa hiyo... nitamwelewesha kwamba...."

"Kwamba dada yake ndiyo sababu hawezi kuwa na wewe?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini bila kuniangalia.

Nikamwambia, "Miryam, mimi ni mkubwa sana kwake, namwona kuwa kama mdogo wangu kabisa, ananiamkiaga...."

"Kwani mimi siyo mkubwa kwako? Hilo ni tatizo?" akauliza hivyo huku akiniangalia.

"Sina maana hiyo, nasema tu kwamba nimeshamzoea kama mdogo wangu. Sidhani ikiwa atachukulia vibaya nikimwambia ukweli. Na... anachokifikiria nimeshakielewa, hiyo ndiyo kitu tunaita Stockholm Syndrome, mtu anaweza akafikiri anampenda mtu kwa sababu tu amemsaidia, lakini unakuta bado anakuwa hajazielewa hisia zake yeye mwenyewe vizuri... ndiyo inaweza ikawa hivyo kwa Mariam pia. Bado ni mdogo, hajapitia mengi kwenye maisha ya mapenzi, kwa hiyo sidhani...."

Miryam akawa anatikisa kichwa taratibu kama kukataa, naye akasema, "Jayden namjua mdogo wangu. Ninajua anapotaka kitu, anakuwa amekitaka kweli. Amekupenda. Usifikiri hii itakuwa easy, hebu imagine... unamwambia uko na mtu mwingine, anaumia. Mbaya zaidi aje kujua ni dada yake. Vipi kama bila sisi kujua... hicho kitu kikawa kimemsababishia apate hata mshtuko mwingine kwenye ubongo...."

"Miryam..."

"... yale ma-ASD... na PTSD yamrudie... tena vibaya? Tatizo lake la kichwani linaweza kurudi kwa njia tusizotarajia... anaweza hata avunjike moyo, ajiumize... labda hata ajiue!" akaongea kwa hisia.

"Miryam, usiwaze huko bwana. Acha kufikiria hivyo," nikamsihi kwa kubembeleza.

Akashusha pumzi na kufumba macho yake.

"Sikia, usi... usi-panic. Najua unatupenda sisi wote ndiyo maana unawaza sana, lakini niamini... hii ishu itakaa sawa. Usi-stress hivyo. We' tulia tu mama. Haitafika huko kote," nikamwambia hivyo kwa upole.

Akaangalia juu kiasi na kushusha pumzi kama kujipa utulivu, naye akakitoa kiganja changu mkononi kwake na kusimama kabisa, akiashiria kutaka kuondoka.

"Miryam, una...."

"Naenda kujimwagia maji, nahisi joto sana," akanikatisha kwa kusema hivyo, bila hata kuniangalia.

Kwa kumwelewa, nikamwambia tu, "Sawa. Nicheki ukitulia."

Akatikisa kichwa kukubali, kisha akaanza kuondoka hapo.

Alipoufungua tu mlango ili ndiyo atoke, nikamwambia, "Nakupenda."

Miryam akasimama kwanza, akiwa ameushikilia mlango, lakini hakugeuka wala kutoa neno lolote, kisha akaendelea tu kutembea na mlango ukajirudishia mpaka kufunga. Doh!

Kazi nilikuwa nayo. Nilifikiri angekuja hapa na mimi kumpetipeti kidogo aondoke na furaha, lakini ya kuzuka yakawa yamezuka tena. Kwa hiyo kumbe Mariam alikuwa ananipenda. Sijui yaani ila, sikushangaa sana, lakini sikuwa tu nimetarajia kabisa kupatwa na jambo hilo kwa wakati huu, achilia mbali taarifa hiyo kuletwa na mtu ambaye mimi ndiyo nilimpenda; dada yake huyo huyo aliyenipenda. Aisee!

Ningetakiwa kushughulika na hili suala kwa busara sana maana sikatai, kile ambacho Miryam alihofia hata mimi nilihofia pia. Nikawaza sijui nimtafutie tu huyo dogo ka-boyfriend kengine kazurizuri ili anipotezee mimi? Ila hapana, hiyo ndiyo isingekuwa busara. Ningepaswa kumpanga Mariam kwa njia ambayo ingemwelewesha kuwa si kila kitu ambacho mtu hutaka sikuzote huwa anakipata, hasa kama tayari kimeshamilikiwa na mwingine. Lakini katika hilo, ningetakiwa niwe mwangalifu sana ili nisije kuwa sababu ya kumvunja vibaya mno huyo binti.







★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★


Pata Full Story WhatsApp au inbox

Whatsapp +255 678 017 280

Karibuni sana
dah Pole sana damu yangu JC lakini ndo mitihani ya Mapenzi hiyo
 
Safi sana JC kwa kuweza kuzishinda hisia zako kwa Mamu,ungenihuzunisha sana kama ungefanya naye tendo
 
Wangapi walikua wanasoma huku wanamwambia jamaa aache asiendelee
Hahah mwanangu Elton unajua tukupe maua yako
Sema Mamu alishasema anapenda simu km ya Da Nuru huu ndo muda wa kumzawaidia ss ili atutolee jamu kwa Mimi
Siku analiwa Mimi nitakaa na Vaseline pembeni
🤪🤪🤪🤪
 
Ndugu yetu Elton Tonny tupe muendelezo, wala hujawahi kutuangusha
 
Njia ya pekee ya kukomesha michezo ya hatari ni kusamehe na kuyaacha yapite,

Ukiamua kulipiza kisasi, ujue na wengine watakuja kulipiza dhidi yako. Na hiyo itakua ni endless chain
 
Kazi ndo kwanza inaanza, JC kuwa makini ila tu usije ukamua huyo black mamba maana utajiongezea uhatari kwa watu wanaokuzunguka na wewe mwenyew
 
Back
Top Bottom