Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 119

Kulipokucha kama kawaida walijiandaa kwenda shuleni huku baba Angel na mama Angel wakitoka pamoja pia kwani nao waliaenda kwenye kazi zao.
Vaileth alibaki nyumbani ila alikuwa na mawazo sana na kujisemea,
“Ona sasa hata siaminiki tena kama zamani, kwakweli shangazi na Prisca wameniponza. Ningejua bora hata Prisca asingefika hapa au bora nisingeenda”
Mara simu yake ilianza kuita, alipoangalia aliona ni namba ya shangazi yake basi ilibidi aipokee na kuanza kuongea nayo,
“Shangazi shikamoo”
“Haina haja, ushafanya hiyo dawa?”
“Mmmh shangazi, kwanza nimepata aibu sana yani kwasasa naishi kwa fedheha kubwa”
“Khaaa unasemaje wewe”
Ilibidi Vaileth amueleze shangazi yake kuhusu yote yaliyotokea, jinsi yeye alivyobambwa na zile dawa, yani shangazi yake alichukia sana,
“Mjinga sana wewe, yani kumbe zile dawa uliweka kwenye mkoba?”
“Ndio shangazi, ningeweka wapi sasa?”
“Si nilikwambia uweke kwenye maziwa mjinga wewe? Kwani hujui ni wapi ambapo wanawake huwa wanaficha vitu vyao muhimu? Yani umenikera sana, kwahiyo umechukua uamuzi gani?”
“Wale watoto walienda kumwaga zile dawa, kwakweli nimelia sana kwa kuwasihi wasinisemee kwa wazazi wao, yani nina mawazo hatari”
“Hebu niondolee ujinga ujue, kesho nitamuagiza Prisca aje huko na atakuletea dawa yani atakuja mara moja na kuondoka na ole wako ufanye ujinga tena”
“Jamani shangazi, sitaki hayo mambo”
“Mjinga wewe, hutaki nini? Yani jua kuwa usipofanya hivyo undugu na wewe umeisha, na katika maisha usiombee kabisa kutengwa na shangazi maana ukoo mzima utakutenga, yani wewe unataka kuniletea ujinga muda wote? Umenikera sana mjinga wewe. Sasa Priscaatakuletea kesho hizo dawa”
“Mmmmh shangazi”
“Sitaki miguno wala nini, nimemaliza. Kesho Prisca atakuja na lazima uifanye hiyo dawa, utake au usitake”
Halafu shangazi yake alikata simu ile na kumfanya Vaileth apate maswali zaidi.

Erica kama kawaida mda wa mapumziko alikaa na Elly na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, basi Erica aliamua kumueleza kuhusu yaliyotokea Jumamosi nyumbani kwao, yani kuhusu yule mdada wao wa kazi, kwakweli Elly alishangaa sana na kusema,
“Kheee huyo mdada hawafai ujue, kumbe ni mshirikina”
“Ndio, nimechukia sana kwakweli”
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa Vaileth, jamani kwakweli nimebaki tu kumshangaa kuwa mchawi halafu anajifanya kutuchekea chekea”
“Muwe nae makini sana huyo jamani. Kwenu sipajui ila nahisi huyo kawaonea wivu tu”
“Halafu Erick anasema eti tusiwaambie wazazi”
“Mmmh sijui, ila nitamuhadithia na mama yangu najua atanipa ushauri uliobora”
“Sawa sawa Elly”
Basi walirudi darasani na kuendelea na masomo.
Muda wa kutoka ulipowadia, Erica moja kwa moja alielekea kwenye gari ya kurudi kwao ila Abdi alimsogelea na kumwambia kwa sauti ndogo,
“Kuna jambo kati ya mama yako na baba yangu”
Halafu Abdi akaondoka, kwakweli Erica hakumuelewa ila alimuangalia tu.
 
SEHEMU YA 120

Erica alivyofika kwao, moja kwa moja alienda jikoni ambapo Vaileth alikuwa akipika na kuanza kumwambia aonje, yani Vaileth alifanya tu vile sababu Erica alionekana kutokuwa na masikhara ila alipomaliza kuonja alimuuliza Erica,
“Kwanini unanifanyia hivi?”
“Sikuamini kwakweli, yani sikuamini kabisa. Imani yangu kwako imekufa”
“Duh! Haya bhana”
Basi Erica alienda chumbani na muda wa kula ulivyofika alirudia kile kile alichokifanya jana kuwa kile chakula aanze kukionja, kwakweli wazazi wao hawakuelewa kwahiyo walibaki tu wakishangaa ila hawakuhoji sana ambapo Vaileth alifanya vile na kisha waliendelea kula kama kawaida na kuongea kidogo na kwenda kulala.
Leo baba Angel aliamua kumwambia mama Angel,
“Hivi kwanini tusimuulize mtoto kuwa kwanini anafanya hivi?”
“Mmmh mimi naona anafanya kwa kujifurahisha”
“Kweli kujifurahisha ndio kila siku? Kesho tumuulize mtoto mama Angel wala tusichukulie kawaida hili swala mke wangu”
“Sawa mume wangu nimekuelewa, basi kesho tutamuuliza maana hata mimi nimeanza kujiuliza maswali kadhaa kuwa kwanini afanye hivi anavyofanya? Unajua imekuwa tofauti kabisa”
Basi wakaongea na kuamua kulala.
Kulipokucha kama kawaida walienda kwenye shughuli zao tu.

Leo Vaileth alikuwa na mawazo zaidi kwani kadri Erica alivyokuwa akimfatilia ndio ambavyo alizidi kukosa raha kabisa mule ndani, basi wakati akiendelea na kazi za hapa na pale muda ule ule alifika Prisca, kwahiyo alimkaribisha huku akiwa na mawazo sana, basi Prisca alianza kumwambia,
“Acha ujinga shoga yangu, hii nyumba ni mali yako lazima tuimiliki sisi kwasasa. Hivi huoni raha kuishi kwenye nyumba kubwa kama hii! Nyumba ambayo imejaa kila kitu, yani ina mali na utajiri, hebu angalia kwanza hiyo Tv ilivyokubwa, angalia Friji jamani, halafu ukifungua friji unakuta kuna kila kitu hivi mtu utakuwa mjinga hadi lini eti uteseke wakati kuna maisha mazuri unayachezea tu. Hebu acha ujinga huo Nyanda, hii nyumba tunatakiwa tuiweke kwenye kumi na nane zetu na huyu baba mwenye nyumba aporomoshe magorofa na kwetu pia, na sisi tupate magari ya kutembelea, tumechoka kutembea kwa miguu ujue, yani mimi nimechoka kabisa kila siku kupuyanga na miguu, hakikisha huyu baba hapindui”
“Jamani, mimi sitaki hayo mambo”
“Utake au usitake ni lazima ufanye”
Basi Prisca alimshika mkono Vaileth mpaka kile chumba alichokuwa akilala Vaileth na kisha kutoa zile dawa na kuziweka mezani kisha akamwambia,
“Hii dawa unatakiwa uifanye leo, yani tunapotoka pale getini umwage kidogo ila nyingine uende ukamwage kidogo kwenye mlango wa chumba cha mabosi zako. Ni kikuwapi chumba chao?”
Vaileth alikaa kimya, basi Prisca alimtishia kumsemea kwa shangazi yao, ikabidi amuonyeshe ambapo Prisca aliimwaga ile dawa kidogo na kusema watakapopita asubuhi ndio itaanza kufanya kazi vizuri, kisha akamgeukia Vaileth na kumwambia,
“Yani ujue ndio kazi imeanza hivi yani lazima huyu baba aingie kwetu”
Kisha akamshika tena mkono Vaileth na kurudi nae chumbani halafu akamwambia,
“Sasa hii dawa utaiweka kwenye chakula usiku wa leo, yani usiache”
“Je hiko chakula hakitanidhuru mimi?”
“Yani iko hivi, hii dawa ni kwaajili ya muhusika tu sema muhusika anatakiwa ale zaidi ya wote kwahiyo unapoweka kwenye chakula hakikisha upande ule anaochukua baba ndio unaweka nyingi zaidi, yani utaona matokeo yake kwakweli ni kesho tu huyu baba mwenye nyumba atakutaka, halafu kuna hii unanawia chini yani akikutaka tu hata usirembeshe yani unampa muda huo huo wakati ushanawia hii dawa basi kwisha habari yao”
“Mmmmh naogopa”
“Acha ujinga wewe”
Basi Prisca alimpa Vaileth zile dawa ambazo aliziweka mezani kwake huku Prisca akimwambia kuwa asisahau kumwaga getini maana Vaileth alishindwa kumsindikiza kwa kusema kuwa ana kazi nyingi, kiukweli hakupenda kabisa mpango wa ile dawa na kwa haraka haraka alitamani kwenda hata kuimwaga ila alipigiwa simu na shangazi yake muda huo huo na kupewa onyo kali.
 
SEHEMU YA 121

Erica akiwa shuleni na Elly, leo Elly ndio aliyeanza kumwambia Erica kutokana na ushauri aliopewa na mama yake,
“Erica, mama yangu kaniambia kuwa huyo dada yenu wa kazi itakuwa anamtaka baba yenu yani anataka baba yenu amuache mama yenu na awe na yeye”
“Kheee kwahiyo yeye ndio achukue nafasi ya mama?”
“Ndio hivyo”
“Kheee, lazima nimwambie mama kwa mtindo huo yani amtoe mama yetu halafu akae yeye jamani? Kwakweli huo ni ujinga kabisa, yani mimi naenda kumwambia mama leo siwezi kukubaliana na hiyo hali”
Yani Erica muda wote siku hiyo alikuwa na wazo la dawa aliloambiwa na Elly, basi muda wa kutoka shule ulipofika waliondoka kama kawaida kwenda nyumbani.
Siku hiyo Erica alivyofika nyumbani alikutana na Erick nae ndio amefika na hata wazazi wao nao waliwahi sana siku hiyo.
Basi walivyoingia tu pale pale sebleni, Erica hakutaka hata kupoteza muda kwa wakati huo kwani alianza kuongea pale pale wakati wazazi wake hata hawajaenda chumbani,
“Baba na mama jamani nimekaa na hili swala ila nimeshindwa kuvumilia kabisa, naomba twendeni tukamchunguze dada Vaileth”
“Kivipi Erica”
“Nifateni”
Erica aliongoza hadi chumbani kwa Vaileth wakati huo Vaileth akiwa jikoni, basi walipofungua mlango tu hata hapakuwa na haja ya kupekua kwani walikuta dawa zile zipo mezani.


Basi walivyoingia tu pale pale sebleni, Erica hakutaka hata kupoteza muda kwa wakati huo kwani alianza kuongea pale pale wakati wazazi wake hata hawajaenda chumbani,
“Baba na mama jamani nimekaa na hili swala ila nimeshindwa kuvumilia kabisa, naomba twendeni tukamchunguze dada Vaileth”
“Kivipi Erica”
“Nifateni”
Erica aliongoza hadi chumbani kwa Vaileth wakati huo Vaileth akiwa jikoni, basi walipofungua mlango tu hata hapakuwa na haja ya kupekua kwani walikuta dawa zile zipo mezani.
Kwakweli walishangaa sana na aliyeshangaa zaidi alikuwa ni mama Angel na kufanya amuite Vaileth kwa nguvu sana,
“Wewe Vaileth weee, hebu njoo upesi”
Basi Vaileth alienda hadi mule chumbani kwake huku akitetemeka, kisha mama Angel alimuuliza kwa ukali,
“Unamaana gani na hizi dawa?”
Vaileth alianza kulia huku akiomba msamaha, yani mama Angel alizidi tu kuchukizwa na kumuulia vizuri,
“Kuwa wazi mjinga wewe, una mpango gani na hizi dawa? Yani lengo lako ni kitu gani?”
“Sijui mama kama mtanielewa”
Kwakweli walisikitika sana, kisha mama Angel alimuangalia mume wake na kumwambia,
“Haya ndio mambo niliyokuwa nayachukia kuhusu wasichana wa kazi, yani nimekuwa nikiwachukia sababu ya mambo kama haya”
Kisha akamuangalia tena Vaileth na kumuuliza,
“Haya niambie, ulikuwa na maana gani na hizo dawa?”
Bado Vaileth alikuwa akilia, basi Erica akasema vile ambavyo aliambiwa na Elly,
“Mama, leo shuleni nilivyomuhadithia Elly kaniambia kuwa dada atakuwa anamtaka baba yetu kwahiyo anataka akupindue wewe, ndio ambavyo kaambiwa na mama yake”
Mama Angel alichukia zaidi na kutaka kujua kuwa yale mambo yemeanzia lini, ilibidi Erica aeleze mlolongo mzima na aseme kuwa ni kwanini hawakusema mapema,
“Ila Elly alivyoniambia hivi nimeogopa sana, na ile sinema tuliyoangalia Jumamosi yani nimeogopa zaidi na kuamua kuwa tuje tumchunguze dada”
Kwakweli mama Angel alimuangalia Vaileth kwa hasira sana, na muda ule ule hata hakutaka maelewano nae kwani alimwambia kuwa afungashe kila kitu na aondoke zake, basi wakatoka mule chumbani na kumuacha Vaileth akiwa analia.
Baba Angel na mama Angel wakaelekea chumbani kwao ila kabla hawajaingia ndani, gafla walisikia sauti kutoka kwa Vaileth ikisema,
“Msiingie kwanza”
Wakageuka na kumuangalia ambapo Vaileth alienda na tambala bichi na kuanza kufuta pale mlangoni huku machozi yakimtoka kwani alikuwa akiifuta ile dawa ambayo ilimwagwa na Prisca, basi mama Angel alimuangalia kwa ukali sana mpaka alipomaliza kupadeki pale mlangoni kisha waliingia ndani ila hawakuongea nae chochote kile na Vaileth aliondoka kuendelea kujiandaa kuondoka kwenye nyumba hiyo.
 
SEHEMU YA 122


Baba Angel na mama Angel walikuwa chumbani ila walikuwa wakiongelea lile tukio ambalo limetokea kwa siku hiyo, yani mama Angel bado alikuwa na malalamiko yako ya kuhusu wasichana wa kazi,
“Ndiomana sipendi wasichana wa kazi mimi”
“Ila mke wangu mbona huyu binti alionekana kuwa mastaarabu sana”
“Kwahiyo unataka tumuache ili akuibe wewe!!”
“Sina maana hiyo, ila nahitaji ukae nae na uongee nae nap engine ukaelewa kuwa tatizo hilo chanzo chake ni nini, yani mimi sidhani tu kama aliamua kujichukulia hayo maamuzi lazima kuna chanzo. Hebu kaa nae uzungumze nae, unajua hawa wadada wa kazi hatuwahitaji ila kuna muda wana umuhimu wao katika maisha yetu mfano tuna watoto wanasma, huoni kama ni kuwachosha yani watoke shule na waanze kupambana na kazi za nyumbani! Mimi nakuomba mke wangu uongee nae kwanza kabla ya kuondoka hata pindi tutakapotafuta mdada mwingine tujue tumchunguze wapi na kitu gani tufanye ili kuishi nae na kama haeleweki pia basi tumfukuze”
“Nimekuelewa mume wangu ila kusema ukweli yani huyu Vaileth amunikera sana, hapa nilipo simtamani hata kidogo. Kweli kutaka kuniibia mume wangu jamani!! Anajua ni wapi mimi na wewe tumetoka? Anajua ni njia gani tumepita hadi sasa tuko pamoja? Kwakweli nimechukia sana”
“Naelewa mke wangu, ila fanya hivyo. Nakupenda sana mke wangu”
Basi mama Angel alikubali kwenda kumuuliza kwanza Vaileth kabla ya kumtimua kabisa aondoke.

Vaileth alikuwa akipanga vitu vyake huku machozi yakimbubujika na kujiona kuwa ni mjinga sana kati ya wajinga na wala hakuelewa kuwa kwa muda huo ataenda wapi,
“Hivi mimi Vai kwanini nimekuwa mjinga kiasi hiki!! Kwanini niliogopa vitisho vya shangazi, kwani wao ndio maisha yangu? Kwakweli nimekuwa mjinga sana”
Alijilaumua mno kwa jambo lile lililotokea, kwani angekataa mapema basi lile jambo hata lisingemkuta.
Muda kidogo mama Angel aliingia chumbani kwa Vaileth na kumkuta akimalizia kujiandaa basi alimkalisha chini na kuanza kuongea nae,
“Hivi Vai unajua kuwa nilikuamini sana, kiasi cha kukuachia nyumba yangu, watoto wangu na pesa zangu, yani huoni ni imani gani niliyokuwa nayo juu yako! Hivi kwanini ukataka kunifanyia hivi! Ni kwanini umtake mume wangu? Je unajua ni wapi tulipotokea, unajua ni kwanini tuko pamoja hadi leo?”
“Nisamehe sana mama, kwakweli halikuwa lengo langu kufanya hivi na hata sikutaka na wala nisingefanya hivi”
“Kwahiyo ulikuwa na lengo gani? Na kwanini kutuletea dawa ndani?”
“Mama, nitakueleza kila kitu cha kweli kabisa wala sitakuficha chochote kile, na sijui kama utanielewa”
“Haya nieleze”
Basi Vaileth ni kweli aliamua kumueleza kila kitu tangu siku ambayo Prisca alifika pale na alivyomwambia na jinsi alivyoitwa na shangazi yake na kupelekwa kwa mganga wa kienyeji na jinsi alivyofika na dawa na kukamatwa na wakina Erica, na jinsi Prisca alivyofika tena na kuleta hizo dawa nyingine na dawa nyingine kumwaga kwenye mlango wao wa kuingilia chumbani huku akimsisitiza kuwa nyingine akamwage kwenye geti lao la kuingilia,
“Kiukweli mama sikuzitaka hizi dawa, na niliweka mezani ili niweze kwenda kuzimwaga, ila sijui nimejisahau na nini. Nisamehe sana mama yangu, naomba msamaha, sitorudia mimi. Naomba msamaha”
Mama Angel alipumua kwanza wala hakuwa na jibu kwa muda huo kisha alimwambia Vaileth,
“Subiri basi, tutaongea badae”
Ila kabla mama Angel hajainuka, simu ya Vaileth iliita na aliamua kupokea basi mama Angel aliamua kukaa ili asikilizie vizuri, na vaileth alipokea ile simu na aliweka sauti kubwa kabisa kwani mpigaji alikuwa ni shangazi yake,
“Wewe mjinga, vipi ushafanya hizo dawa?”
“Hapana shangazi, nilishakataa kwa Prisca haya mambo sitaki”
“Hebu mtoto acha ujinga wewe, hivi akili zako zikoje kwani? Unafikiria kwa kutumia makalio au nini? Mara ya kwanza umetupa hizo dawa kwa makusudi kabisa, na sasa Prisca kakuletea unasema hutaki kuzifanya, hivi mtoto una laana gani wewe?”
“Shangazi, mimi ni heri nife na umasikini wangu ila kama nilivyokwambia siwezi kufanya haya mambo na hizo dawa zenu nimeenda kuzimwaga. Sitaki kabisa hayo mambo yenu”
“Wewe mtoto wewe loh! Nilikwambia usipofanya hizo dawa sahau kuhusu undugu wetu yani hata ukiumwa usitushirikishe”
“Sawa shangazi ila mimi siwezi kufanya hizo dawa”
“Hivi una nini lakini wewe mtoto? Hivi unaona raha kwa ndugu zako kua na umasikini eeeh! Naomba uje huku Jumamosi”
“Kwa jambo kama hilo shangazi siji”
“Wewe mtoto usinitanie ujue, kesho nakuja huko na Prisca”
Kisha shangazi akakata simu kwa hasira yani ilionekana amechukizwa sana na majibu ya Vaileth, basi mama Angel alimuangalia kwa muda Vaileth kisha akamuomba simu yake ambapo Vaileth alimpatia halafu mama Angel aliondoka nayo.
 
SEHEMU YA 123

Basi Erica alimfata Erick na kuongea nae kuhusu jambo lile ambalo limetokea siku ile, basi alianza kuongea nae,
“Kaka, je nimefanya vibaya nilivyofanya vile?”
“Hapana hujafanya vibaya”
“Kwahiyo umenielewa? Sipendi kukukera kaka yangu ujue”
“Naelewa hilo dada yangu, kwahiyo hata usijali”
Basi Erica alifurahi na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake, ila alipokuwa chumbani kwake akakumbuka jambo toka kwa kaka yake hivyo basi akaenda tena na kufungua mlango wa chumbani kwa kaka yake, kwakweli alipofungua mlango alikuta kaka yake akiwa kajilaza kitandani yani alikuwa mtupu kabisa kwamaana hiyo Erick alivua nguo zote na kujilaza, kwakweli Erica alishtuka sana na leo alitoka nje kwa uoga kabisa kwani hata aliogopa tena kuingia chumbani kwa kaka yake, kisha akarudi zake haraka haraka chumbani kwake huku akijiuliza kwanini alienda kwa kaka yake bila hodi, basi baada ya muda mfupi Erick nae alienda chumbani kwa Erica huku akicheka na kumwambia Erica,
“Usijali dada yangu, usijali kitu. Fanya kama hujaona chochote kile”
“Mmmh nimeogopa”
“Sasa umeogopa nini jamani!!”
“Aaaah hamna kitu”
“Fanya kama hujaona chochote dada yangu, usiku mwema”
Halafu Erick alitoka mule chumbani na kurudi zake chumbani kwake.
Yani Erica alikuwa akiwaza sana na kujiuliza kuwa kwanini aliingia kwa kaka yake siku hiyo bila hodi kwani maumbile ya kaka yake yalianza kutembea kichwani mwake, wakati alishawahi kumuona akitoka kuoga ila siku hiyo ikawa tofauti sana kwani aliona maumbile ya kaka yake yakitembea tu muda wote kwenye akili yake.

Yani siku ile mama Angel alilala akiwa na mawazo sana, yani hakuelewa kuwa ni kitu gani afanye kwa Vaileth yani hakuelewa kabisa.
Basi palivyokucha, baba Angel aliongea kidogo na mke wake kabla ya kuondoka ambapo mkewe alimuuliza,
“Sasa mume wangu tutafanya nini na hili swala la Vaileth? Je tumfukuze au?”
“Mke wangu kwakweli nakuachia wewe mwenyewe, yani wewe ndio utaamua kuwa ni kitu gani kifanyike”
“Sawa mume wangu”
“Najua una busara sana mke wangu na utajua ni kitu gani kifanyike”
Basi baba Angel alijiandaa vizuri kabisa kisha alimuaga mke wake na kuondoka maana mama Angel siku hiyo alisema kuwa atabaki nyumbani tu.
Basi kabla mama Angel hjaenda kufanya shughuli nyingine au kuongea na Vaileth alisikia kuna ujumbe umeingia kwenye simu ya Vaileth basi aliichukua na kusoma ule ujumbe aliona jina ni Prisca, kwahiyo ulitoka kwa Prisca,
“Yani Nyanda umefanya shangazi apatwe na presha kabisa sababu ya ujinga wako, na badae nakuja na shangazi hapo nyumbani kwenu. Tutafanya dawa kwa nusu saa tu, halafu tutaondoka. Kwahiyo wewe usishughulike tena na chochote kile, mambo yote tutayanya wenyewe”
Basi mama Angel aliandika ujumbe kumjibu Prisca,
“Haya karibuni”
Halafu aliondoka kwenda kuongea na Vaileth ambapo alipofika tu kule alimwambia Vaileth ajiandae ili aende nae sehemu basi Vaileth hakukataa kufanya vile kwani muda ule ule alienda kujiandaa na baada ya hapo aliondoka akiwa ameongozana na mama Angel.
 
SEHEMU YA 124

Angel akiwa shuleni, kwasasa aliweza kwa kiasi kikubwa sana kuzuia hisia zake kwa Samir kwani muda mwingi aliutumia kwaajili ya masomo yake na alikuwa wala hahangaiki kumsalimia Samir ukizingatia alihisi kuwa Samir ana mahusiano na madam Hawa kutokana na ile tabia ya madam Hawa aliyokuwa akiifanya ya kumuita Samir kila muda.
Basi alikaa akijisomea siku hiyo ila alishangaa sana alipoitwa na madam Hawa, kwakweli aliinuka kwa uoga flani ila alienda na kumfata yule madam mpaka ofisini ambapo yule madam alimuuliza,
“Angel, unayaonaje maisha ya hii shule?”
“Yapo vizuri tu, nishazoea kwasasa”
“Na vipi wanafunzi unawaonaje?”
“Nawaona wapo vizuri tu madam”
“Na vipi kuhusu Samir?”
Angel alishtuka kidogo na kukaa kimya bila ya kujibu hilo swali ambapo madam Hawa alimuuliza tena,
“Mbona hunijibu Angel? Vipi kuhusu Samir?”
“Sijakuelewa madam, kuhusu Samir kivipi?”
“Aaaah yani unamuonaje Samir darasani?”
“Namuona kama mwanafunzi mwenzangu na kama kaka yangu”
“Vizuri sana, hivyo ndio maisha ya shule yanavyotakiwa yawe, unatakiwa kumuona hivyo Samir na si vinginevyo ila nikisikia kuwa kuna hata chembe za mapenzi kati yako na Samir yani nitakushulikia mwenyewe yani sitasubiri mzazi wako wala nini, umenielewa”
“Nimekuelewa madam”
“Nahitaji usome kwa bidii na mwisho wa siku ufaulu vizuri, si unajua mnakaribia kufanya mitihani ya taifa?”
“Naelewa hilo madam”
“Sawa, na usome kwa bidii sasa”
Angel alimuitikia madam kisha aliruhusiwa kurudi darasani na kuendelea na masomo yake.
 
SEHEMU YA 125

Mama Angel na Vaileth walikuwa mahali ambapo hata Vaileth hakuelewa ni kwanini wapo mahali hapo na wala hapakuwa mbali na nyumbani kwao, baada ya muda ujumbe uliingia kwenye simu ya Vaileth,
“Tumeshafika, tupo hapa getini”
Basi nae akajibu,
“Nisubirini hapohapo”
Na muda kidogo akamwambia Vaileth kuwa warudi nyumbani, kiukweli Vaileth hakuwa akielewa chochote kila, na muda ule ule waliondoka hadi pale kwake ambapo nje ya geti waliwakuta shangazi wa Vaileth pamoja na Prisca, basi mama Angel pamoja na vaileth walisogea pale ambapo mama Angel aliwasalimia kwanza ila Vaileth alikaa kimya tu kwani hakuelewa kuwa ni kitu gani ambacho mama Angel alitaka kukitenda kisha mama Angel alimwambia mlinzi afungue geti halafu waliingia ambapo aliwakaribisha wale wageni yani nao walikuwa wakiingia kwa uoga uoga sana, alifika nao kwenye kibaraza na kukaa nao kisha alianza kuwauliza,
“Samahanini jamani, kwani mimi nina kasoro gani kukaa ndani ya nyumba hii?”
Walikaa kimya tu kwani hata hawakuelewa, halafu akawauliza tena,
“Kwani Vai akishampata mume wangu basi nyie mtafaidika na nini? Mnajua mimi na mume wangu tumetoka wapi? Mnajua hii nyumba tumeijenga vipi? Unajua kuna kipindi nilikuwa nawaona wasichana wa kazi ni wabaya sana ila nimegundua kuwa kuna wengine sio wabaya ila wanapata ushawishi toka kwa ndugu zao, hivi mkishavunja undugu na Vaileth ndio mnapata faida gani?”
Walikaa kimya na kuona aibu sana, basi Prisca aliona jambo jema ni kuomba msamaha tu kwa wakati huo kwani alihisi kuwa wameshaumbuka,
“Naomba dada utusamehe”
Ila shangazi alidakia na kujifanya hajui kosa lao,
“Kwani msamaha Prisca unaomba kwa kosa gani?”
Prisca alikaa kimya kisha mama Angel alisema tena,
“Yani wewe shangazi mtu ndio huna hata aibu wakati wewe ndio kuongoza wenzio kiguu na njia kwenda kwa waganga wa kienyeji, kama ulikosea maisha ni wewe ujue! Yani kama ulikosea na kuolewa na mwanaume asiyejielewa ni wewe, usitake kwenye maisha wote tufanane, ndiomana kuna wasichana wa kazi, kuna wakulima, kuna manesi, kuna madereva, kuna makonda, kuna wabeba zage yani kila mtu na karama zake katika haya maisha yani unatakiwa kuwa makini sana kwa unayoyafikiria kuyafanya. Je ulidhani utapata faida gani ikiwa mimi nimemkamata Vaileth akiweka dawa? Na nikimfukuza huyu Vaileth utakuwa umeupata huo utajiri? Yani ni mtu mzima lakini huna akili hata moja”
Kiukweli shangazi aliona aibu sana kiasi kwamba aliinuka na kuanza kuondoka ila mama Angel alimvuta kwa nyuma na kumwambia,
“Mbona una kiburi sana wewe shangazi, hivi unajua kama hapa ni nyumbani kwangu?”
Basi yule shangazi kwa aibu kubwa alisema,
“Naomba nisamehe, naomba pia uniruhusu niende”
Basi mama Angel alimuangalia ambapo yule shangazi alitoka halafu Prisca alimfata nyumba, kisha yeye na Vaileth walirudi ndani kwao.

Erica leo shuleni alimuhadithia Elly kuhusu kila kitu kilichotokea jana yake nyumbani kwao kuhusu yule dada yao wa kazi, basi Elly akamuuliza,
“Kwahiyo wazazi wako wamechukua uamuzi gani?”
“Mmmh hata sijui kuwa wameamuaje ila chochote watakachoamua ni sawa tu kwani mimi nishawaambia ukweli wa mambo yote ulivyo”
“Sawa, umefanya vizuri sana, ila leo mama yangu kaniuliza kuhusu dada yako Angel na kaka yako Erick, eti wanaendeleaje?”
“Wanaendelea vizuri tu, kwani mama yako anamfahamu dada Angel na Erick?”
“Sijui ila aliniuliza hivyo ila nadhani anawafahamu”
“Sasa anawafahamu vipi?”
“Mbona hata wewe anakufahamu!”
Yani Erica alishangaa sana na kusema,
“Mimi atakuwa ananifahamu kwa jina”
“Hadi kwa sura, mama yangu anakufahamu”
“Kwakweli Erica alishangaa mno kusikia mama yake Elly anamfahamu vizuri sana yeye, ila aliacha kuendelea kuuliza maswali zaidi na moja kwa moja walirudi darasani.
Muda wa kutoka ulipofika, kila mmoja aliondoka zake ila na laeo Abdi alimfata Erica na kumwambia,
“Jana nimeongea kidogo na baba na kaniambia kuwa katika maisha yake hakuna mwanamke aliyewahi kumpenda kama mama yako, hebu mwambie mama yako amuhurumie baba yangu hata aongee nae kidogo kwani atakuwa amemfariji”
“Hivi Abdi huwa unaongelea vitu gani?”
“Naongelea kuhusu mapenzi, baba yangu hajawahi kupenda kama alivyompenda mama yako kwa maana hiyo hata mama yetu wa sasa baba hampendi wala nini kwani upendo wake wote upo kwa mama yako”
Kwakweli Erica alimuangalia tu na kuondoka zake, kwani alienda kupanda gari na walielekea nyumbani kama kawaida.
 
SEHEMU YA 126

Ila leo Erica alivyofika nyumbani kwao tu moja kwa moja aliamua kwenda chumbani kwa mama yake, aligonga na kumkuta ndani ambapo mama yake alimkaribisha yani hakuvua hata sare za shule, baada ya kumsalimia mama yake alianza kumuuliza,
“Eti mama, wewe na baba Abdi kuna nini kiliendelea kati yenu?”
“Unauliza nini wewe? Umeanza kukosa adabu eeeh!”
Basi Erica alimuomba msamaha mama yake na kuanza kumuelezea vile alivyokuwa akiambiwa na Abdi,
“Kheee na wewe unakosa adabu kama huyo Abdi? Mtu alitaka kukubaka, unawezaje tena kukaa chini na kuongea nae?”
“Huwa sikai nae mama, ila huwa ananifata muda wa kutoka”
“Hebu niondolee ujinga wako, na siku nyingine ukija kuniuliza maswali ya kijinga namna hiyo basi nitachukua jukumu la kukutandika, mjinga wewe. Si bora uongee na Elly tu ingawa mama yake hataki kufahamika nasi”
Basi Erica alimuomba msamaha mama yake na kuanza kumueleza habari za Elly yani jinsi mama yake alivyowasalimia Angel na Erick,
“Kheee amewajuaje?”
“Hata mimi nashangaa, tena Elly anasema sio kwa majina tu bali anawafahamu hadi kwa sura”
“Kheee jamani, inamaana huyo mamake Elly anatufahamu vizuri sana?”
“Nasikia hadi mimi ananifahamu vizuri mama na sijawahi kumuona kwakweli”
“Mmmh mbona Napata mshangao hapa”
“Ndio hivyo mama, hata mimi nimeshangaa pia”
“Haya, nenda kavue hizo sare za shule ule chakula na ukajisomee”
Basi Erica alitoka mule chumbani kwa mama yake ila mama yake alibaki na maswali mengi sana akijiuliza kuhusu mama Elly maana inaonyesha ni mtu ambaye anaifahamu familia yake vilivyo, akajiuliza sana kuwa je mama Elly ni nani? Hakupata jibu kwakweli.

Baba Angel aliporudi leo usiku aliamua kwanza kumueleza kile kilichotokea siku hiyo kuhusu ndugu wa Vaileth na kile alichokifanya, mumewe akamuuliza,
“Kwahiyo Vaileth humfukuzi tena?”
“Simfukuzi kwanza ila nipo kwenye kumchunguza kwa karibu sana, kuna mambo nahitaji kujifunza”
“Sasa, utamchunguzaje?”
“Mume wangu, wewe usijali niachie kuhusu hili”
Kisha alianza kumueleza jinsi Erica alivyomsimulia kuhusu mama yake Elly, kwakweli baba Angel alishangaa pia ila mkewe alimuuliza,
“Au mama Elly aliwahi kuwa mwanamke wako? Elly sio mwanao kweli?”
“Jamani mke wangu umeanzaje kunihisi hivyo jamani! Yule Elly si rika moja na wakina Erica, mimi sikuwa tena na mambo ya wanawake toka kipindi nimeanza kumlea Angel jamani, kwahiyo Elly hawezi kuwa mwanangu”
“Sasa kwanini inakuwa hivi! Kumbuka mamake Elly hataki nimfahamu halafu familia yangu yote anaifahamu si ndio mwanzo wa kuripuliwa njiani bila kujua maana bora adui ujue kuliko adui akujue wewe halafu wewe humjui”
“Unamaanisha kuwa mamake Elly ni adui yetu?”
“Ndio, kwanza hebu kumbuka vile visheti. Kwanini ulipokula ilikuwa vile ni mpaka nilipoingia kwenye maombi! Kwakweli sina imani na mama yake Elly, nahisi ni adui yangu na familia yangu”
“Basi mke wangu ngoja tuukate mzizi wa fitina, ile shule tulimuhamisha Erick, tukamuhamisha Angel na kwanini tusimuhamishe Erica? Ukizingatia kwanza kuna wanafunzi wabaya ambao walitaka kumbaka Erica wetu halafu sisi kama wazazi tumetulia tu yani hatujachukua hatua yoyote ile, hivi mfano Erica angebakwa ingekuwaje? Pili kuna mwanafunzi ambaye mzazi wake anafatilia maisha yetu na kama unavyomjua Erica ni mropokaji, basi mambo ya nyumba yetu yote anayamwaga kwa Elly, kwahiyo inakuwa rahisi kwa huyo mamake Elly kutufahamu kiundani zaidi. Naona ni vyema tukimuhamisha shule Erica”
“Sasa tutampeleka shule gani?”
“Ngoja, nitaongea na Erick na tutajua shule ya kumpeleka Erica, wala usiumie kichwa mke wangu sababu ya mambo madogo kama hayo, hapo ni kumuhamisha mtoto shule tu”
“Sawa mume wangu nimekuelewa”
Basi mama Angel alikubaliana na mume wake kuhusu kumuhamisha Angel shule aliyokuwa akisoma ili kumuepuka huyo Elly.
 
SEHEMU YA 127

Leo Samir akiwa nyumbani alimuona mama yake akiwa nyumbani pia basi alimuuliza,
“Vipi mama, leo huendi kazini?”
“Zamu yangu ni kesho asubuhi”
“Mmmmh!”
“Sasa mbona umeguna?”
“Na baba nae yuko wapi?”
“Hivi wewe mtoto kwani maisha yangu mimi na ya baba yako yanakuhusu nini? Mbona unakilanga wewe?”
“Mmmh msms, leo wakati nimetoka shule nilikutana na mtu njiani alikuwa akiongea ongea na kusema anamtafuta sana baba yake, baada ya kumpeleleza niligundua kuwa baba yake ndio huyu huyu baba yetu wa hapa nyumbani. Jamani mama kwa huyu baba tupo wengi sana yani ingekuwa ni uwezo wangu basi ningejibadilishia baba”
“Una laana wewe, unakula bure, unalala bure, unaenda chooni bure, hulipii maji wala umeme nab ado unafanya madudu shuleni ila tunatumia gharama zetu kukuhamisha shule, sasa badala ukazanie masomo umebaki tu kusema humtaki baba huyu. Yani umtake au usimtake ndio tayari mume wangu mimi, ndio tayari ni baba yenu hata awe na watoto kila mtaa ila ndio baba yenu, umeona watoto wake wanaishi hapa? Ukimkuta tena mtoto wake mwambie aende kwa bibi yao maana bibi yao bado mzima na mwenye afya na nguvu kwahiyo analeaga tu wajukuu. Ujinga sitaki Samir”
Mama yake alionekana kachukia sanakwani muda huo huo aliondoka zake na kwenda kulala na kumuacha Samir akiendelea kuongea swala lake la kubadilishiwa baba.

Siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda hospitali ili kuangalia kama tayari amenasa au bado na kama bado ajue kuwa atumie chakula gani kwani alitamani amfurahishe mume wake kwa kupata mimba tena na kumzalia watoto.
Basi alifika hospitali na kwenda moja kwa moja kwa dokta Maimuna ambaye alimuandikia vipimo na kwenda kupima kisha alifika na kusomewa majibu,
“Oooh hongera sana mama Angel, tayari wewe ni mjamzito”
Mama Angel alifurahi sana na kujua mumewe lazima atafurahi zaidi, kisha akamwambia daktari,
“Basi niandikie vyakula vya kula kuanzia kipindi hiki, nataka mimba yangu hii niwe nayo katika hali salama kabisa”
daktari alitabasamu na mara simu ya daktari iliita basi aliomba samahani kidogo kwa mama Angel na kuanza kuongea na ile simu, alipomaliza alimwambia mama Angel,
“Oooh leo mume wangu kaamua kunitembelea hospitali, ni vyema sana ukamfahamu”
“Sawa, itakuwa ni vizuri sana”
Basi dokta Maimuna akampigia simu mumewe na kumtaka moja kwa moja aingie ofisini kwake ili amtambulishe pia kwa rafiki yake mama Angel.
Baada ya muda kidogo mlango wa ofisi ya dokta Maimuna ulifunguliwa na aliingia mume wa dokta Maimuna, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kutoa macho kwa yule mume wa dokta Maimuna kwani ni mtu aliyemfahamu sana.
 
SEHEMU YA 128

Baada ya muda kidogo mlango wa ofisi ya dokta Maimuna ulifunguliwa na aliingia mume wa dokta Maimuna, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kutoa macho kwa yule mume wa dokta Maimuna kwani ni mtu aliyemfahamu sana.
Ila dokta Maimuna wala hakuangalia mshangao wa mama Angel zaidi zaidi alimtambulisha mumewe kwa mama Angel,
“Oooh mama Angel, huyu ni mume wangu anaitwa Rahim. Mume wangu, huyu ni mteja wangu nan i rafiki yangu anaitwa mama Angel”
Kwakweli mume wa dokta Maimuna alitumia kama dakika tano kujibu na vile vile kwa mama Angel alishindwa hata kusema neno, basi yule mume wa dokta Maimuna akanyoosha mkono wake ili kumsalimia mama Angel huku akisema,
“Nafurahi kukufahamu”
Ila mama Angel hakunyoosha mkono wake wala nini, badala yake aliinuka na kutoka pale ofisini na kuondoka, kwakweli dokta maimuna alikuwa akishangaa tu ile hali maana hakuielewa.
Basi mama Angel moja kwa moja alienda kwenye gari yake na kuondoa gari huku akiwaza vitu vingi sana, akakumbuka kuwa hapo hospitali alishawahi kukutana na mtu mwingine aliyefahamiana nae, na mtu huyo alisema kuwa kuna shemeji yake pale hospitali kwahiyo alipata picha kamili, basi alianza kujiuliza,
“Inamaana dokta Maimuna kaolewa na Rahim? Vipi kuhusu mke wa Rahim imekuwaje? Mmmh mwanaume msumbufu yule, sidhani kama nitarudi tena kwenye hii hospitali hata kama dokta Maimuna amekuwa dokta wangu wa kipindi kirefu sana”
Basi mama Angel aliamua muda huo kurudi nyumbani kwake tu huku akiwa na mawazo mengi sana.

Ilikuwa ni jioni wakati baba Angel ametoka kazini ila alimchukua mwanae Erick na kutoka nae, kuna duka lake alihitaji kumuonyesha, yani hakuingia hata ndani ila alivyomuona Erick tu aliondoka nae.
Walifika mpaka kwenye hilo duka na kumuonyesha mwanae,
“Eeeeh mwanangu, unasemaje kuhusu hili duka?”
“Lipo vizuri sana baba”
“Nataka Jumatatu lianze kufanya kazi, si unajua maisha yangu mimi ni biashara yani sina maisha mengine zaidi ya biashara”
“Naelewa baba”
“Naamini biashara zangu utazifanya vyema, Angel anafahamu biashara zangu nyingi sana”
“Ila baba, naomba nikuulize swali?”
“Niulize”
“Mbona dada Angel ana nywele kama za kiarabu?”
“Mmmh wewe mtoto wewe, yule Angel kafata nywele za marehemu bibi yangu”
“Aaaah sawa”
Kisha baba Angel alienda mahali na Erick kisha alimuuliza,
“Nataka kumuhamisha Erica shule, nimuhamishie shule gani?”
“Oooh baba, mimi naona ni vyema ukimpeleka shule ya wasichana tupu”
“Ooooh kwanini?”
“Sababu huko hatokutana tena na wakina Abdi”
Yani mtu pekee ambaye Erick hakumpenda katika maisha ya dada yake ni Abdi tu, basi baba yake aliafiki swala la kumpeleka Erica shule ya wasichana, kisha baada ya maongezi hayo waliamua kuondoka pale na ilikuwa ni usiku tayari.
Wakati wanaondoka, wakiwa njiani baba Angel alimuona mtu ambaye alikuwa akimfahamu basi alimpigia honi na mtu huyo akageuka, basi baba Angel alishusha kioo ila yule mtu baada ya kumuona baba Angel alikimbia sana hata yeye mwenyewe hakuelewa ni kwanini alikimbia basi ilibidi tu arudi nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 129

Walipokuwa nyumbani, mama Angel aliamua kumuuliza mumewe kuwa alienda wapi na Erick,
“Ulienda wapi na Erick?”
“Nilienda kumuonyesha duka letu jipya”
“Umeanza ubaguzi eeeh!”
“Kivipi jamani mke wangu?”
“Kumbuka ahadi yako, kila biashara utaanza kumuonyesha kwanza Angel? Na kwanini uende na Erick tu na kumuacha Erica?”
“Unajua mke wangu kuna muda huwa sikuelewa kabisa kuwa unataka kitu gani, yani huwa sikuelewi mke wangu, sasa hapo kosa langu ni nini? Yani kipi nimekosea, kuonyesha biashara kwa Erick? Kwani Erick sio mtoto wetu? Hebu niambie kwanza maana wewe ndio mama”
“Sasa ndio maneno gani hayo? Unamaana mimi nilichepuka?”
“Sina maana hiyo mke wangu, hebu jaribu kunielewesha, kuwa katika nyumba hii na katika watoto wetu natakiwa kufanya nini na nini? Na kitu gani sitakiwi kufanya kwa watoto wetu? Au nikifanya kitu gani kwa mtoto huyu basi kwa mtoto huyu nisifanye?”
“Hapana sijasema hivyo ila umeanza kumpendelea Erick sababu ndio mwanaume mwenzio”
“Sasa nilivyokuwa nampendelea Angel kuna sababu gani katikati? Unajua mama Angel mara nyingine uwe unafikiria kabla ya kuongea”
“Kwahiyo mimi ni mjinga eeeh!”
“Oooh usikuze mambo mama, nakupenda sana”
Basi mama Angel alitabasamu kwani alipoambiwa nakupenda sana na mumewe alikuwa akijihisi rah asana kwenye moyo wake, na hapo alianza kumwelize swala la kwamba yeye ni mjamzito, kwakweli baba Angel alifurahi sana baada ya kusikia mkewe ni mjamzito kwani kitu kile alikuwa akikitamani kwa muda mrefu sana, basi alimwambia,
“Najua na hapo utanipatia mapacha tu”
Mama Angel alitabasamu na kusema,
“Eeeeh tutawaita wakina nani?”
“Mke wangu, tutatoa tu majina hakuna wasiwasi wowote ule, ila hao ni mapacha lazima”
Basi mama Angel muda huo alikuwa na furaha sana.

Erick moja kwa moja alienda kwa Erica na alimueleza sehemu ambayo walienda na baba yao, kiukweli Erica hakuwa hata na haja ya kuzungukia biashara za baba yake kiasi cha kumfanya asione wivu wanapomwambia kuwa walienda kwenye biashara ndiomana hata baba yake alikuwa hamchukui mara nyingi kumpeleka kwenye biashara zake, basi Erica alibaki tu kumpongeza kaka yake,
“Hongera sana kaka, naamini biashara za baba utazisimamia vizuri”
“Ila leo nimemuuliza baba, kuwa mbona dada Angel ana nywele za kiarabu wakati mimi na wewe tuna nywele za kawaida?”
“Eeeeh akasemaje?”
“Akasema kuwa dada Angel kafanana na marehemu bibi yake”
“Jamani huyo bibi na mimi si angenirithisha zile nywele, nazitamani ujue, ona nywele zangu zilivyo kama nywele za mama”
Basi Erick alicheka na kumwambia,
“Ila hivyo hivyo na nywele zako unapendeza, unajua wewe unafanana sana na mama. Yani nahisi mama kakulandisha kila kitu”
“Hapana sio kila kitu maana mimi sina kisirani kama mama”
Walianza kucheka ila mama yao aliingia kule chumbani na kuwafokea,
“Mnasemaje nyie, mimi nina kisirani?”
Erica na Erick walikaa kimya tu, kisha mama yao akawaambia,
“Haya, twendeni mkale nyie wajinga, waone vile”
Basi wakainuka na kufatana na mama yao kwenda kula kwanza.
 
SEHEMU YA 130

Angel leo baada ya kula chakula cha usiku, alimfata shangazi yake na kuanza kuongea nae,
“Asante sana shangazi, nakupenda sana”
“Nakupenda pia mwanangu, ila hiyo asante ya nini?”
“Umenisaidia sana shangazi, yani kwasasa nimejikuta napenda kusoma kuliko kitu chochote”
“Ooooh hiko ndio nilichokuwa nakitaka, haya mwanangu nenda ukapumzike eeh!”
Basi Angel aliondoka zke, leo na mjombawake alikuwepo yani mume wa Tumaini ambaye alifurahi sana kuona vile basi alimfata mke wake na kumkumbatia kisha akambusu na kumwambia,
“Nakupenda sana, kwa hakika watu wangekuwa na moyo kama wako basi kusingekuwa na unyanyasaji”
“Kwanini?”
“Unajua siku narudi na kukuta Angel yuko hapa nilijiuliza sana kuwa anaishije na wewe, ila kila siku naangalia maisha ambayo Angel anaishi na wewe, kwakweli mke wangu unastahili pongezi na unastahili sifa”
“Sasa jamani mimi nimchukie Angel nipate faida gani?”
“Najua unaelewa kuwa ni kitu gani ninachoongelea mke wangu, basi twende tukalale tu”
Tumaini akatabasamu na moja kwa moja kwenda na mume wake kulala.

Leo ilikuwa ni siku ya Jumamosi, mume wa Tumaini alimwambia mke wake kuwa anahitaji kwenda nae katika matembezi, basi Tumaini alijiandaa kisha jioni ya siku hiyo alitoka na mume wake.
Ambapo mume wake moja kwa moja alimpeleka ufukweni, kwakweli katika maisha yao ya ndoa basi hawakuwa na harakati hata mara moja za kwenda ufukweni kwahiyo ilikuwa ni mara ya kwanza, basi Tumaini akamuuliza mumewe,
“Umenileta huku kufanya nini?”
“Kwahiyo ulivyosikia tunaenda kutembea ulijua ni wapi?”
“Yani mimi nilijua kuwa labda tutaenda hotelini sijui wapi wapi yani sikuwa na wazo kuwa tutakuja huku”
“Kwahiyo huku hujapapenda mke wangu?”
Kabla Tumaini hajajibu swali hilo, alikuja mtu na kumziba macho huku akimwambia,
“Otea mimi ni nani?”
Mume wa Tumaini alikuwa akicheka tu kwani alijua itakuwa huyo mtu anafahamiana na mke wake, na hakuwa na mashaka nae kwani alikuwa ni mwanamke, basi Tumaini akajaribu kufikiria na kukosajibu kabisa, kisha akamwambia,
“Dah! Nimeshindwa kuotea”
basi yule mtu alimuachilia Tumaini mikono huku akicheka sana, kwakweli Tumaini alifurahi kumuona kwani alikuwa ni rafiki yake wa muda mreu ila alitengana nae kwa kipindi sababu walikuwa na matatizo nae kidogo,
“Oooh jamani Sia, hata siamini kuwa ni wewe!”
“Ni mimi Tumaini, umeanza kupenda lini kuja ufukweni?”
“Aaaah ni shemeji yak oleo ndio kaamua anitoe ushamba kidogo”
Basi Sia alimuangalia mume wa Tumaini na kumsalimia pale kisha akamwambia,
“Unajua toka kipindi cha harusi yenu sijaonana nanyi tena!”
“Eeeeh vipi na wewe upo ufukweni na nani?”
“Niwe na nani mwenzangu? Nipo mwenyewe”
“Kheee mumeo yule yuko wapi?”
“Mmmmh yule mwenzangu aliota mapembe, yani nilijuta kumfahamu kitu alichonifanyia yule ni Mungu pekee anajua, sitaki hata kumuona”
“Na kipindi kile ulikuwa una mimba, mtoto je upo nae au yupo nae?”
“Oooh mtoto ninae mwenyewe, ila tuachane na habari za mtoto ila tuongelee mambo ya maana. Vipi kaka yako na mkewe?”
“Mmmh sijui, sijawasiliana nao muda sana”
“Basi naomba mawasiliano yako”
Kisha Tumaini akabadilishana mawasiliano na Sia halafu Sia alimuaga Tumaini na kuondoka zake, basi mume wa Tumaini akasema,
“Hivi huyu si ndio alikuwa akimtaka mdogo wako huyu kipindi kile? Hadi alitaka kuharibu ndoa yao si ndio huyu!”
“Ndio ni yeye, ila alibadilika”
“Mmmmh sijui mke wangu, ila ukweli anaujua yeye mwenyewe”
Basi walikaa kaa kidogo ambapo Tumaini alidai kuwa warudi nyumbani tu, basi wakarudi nyumbani.
 
SEHEMU YA 131


Leo baba Angel alikuwa nyumbani kwake, muda huo alikuwa kwenye kile chumba cha kujisomea huku akisoma magazeti yake, mara akapigiwa simu na dada yake,
“Mmmh otea leo nimeonana na nani?”
“Jamani mimi nitajuaje sasa mtu uliyeonana nae wewe?”
“Aaaah na wewe hata hutaki kujaribu kuotea, nimeonana na Sia”
“Kheee Sia?”
“Ndio, na nimeongea nae mengi sana”
“Ooooh alikuwa anasemaje sasa? Unajua jana pia nikiwa njiani nilimuona mtu kama yeye, halafu nina uhakika alikuwa ni yeye ila nilipompigia honi akageuka nami nikashusha kioo cha gari jamani toka hapo alitembea haraka na kunipotea, sijui bado ana kisirani na mimi?”
“Hapana bhana, sidhani kasema tu nikusalimie wewe na mkeo”
“Oooh sawa”
Basi wakaongea pia kuhusu maendelea ya Angel na kuagana, ambapo baba Angel alikata ile simu na muda huo huo mama Angel aliingia mule kwenye kile chumba na kumuuliza mumewe,
“Ulikuwa unaongea na nani?”
“Na Tumaini, alikuwa akinipa habari za Angel”
“Oooh nishamkumbuka mwanangu, sijui lini niende nikamuone jamani?”
“Unaonaje tukienda kesho baada ya kutoka Kanisani?”
“Oooh jambo zuri sana hilo, sawa mume wangu basi tutaenda kesho”
Basi wakakubaliana kufanya hivyo.

Muda wa kulala ulifika na wote walienda kulala ila Erica alienda chumbani kwa kaka yake na kumtaka wacheze karata, basi Erick alikubali kwani anamtindo wa kukubali kila kitu anachoambiwa na Erica, walianza kucheza zile karata huku wakicheka na kufurahi basi erica akamuuliza kaka yake,
“Hivi inamaana ukioa ndio mwisho wa mimi na wewe kucheza pamoja?”
“Jamani Erica mbona unakuwa huelewi, mimi nilikwambia sitokuja kuoa maishani mwangu”
“Kwanini sasa?”
“Sababu ninayempenda siwezi kumuoa kamwe”
“Nani huyo?”
“Unataka kumjua?”
“Ndio, nataka sana nimfahamu?”
“Basi kesho nitakuonyesha picha yake”
“Duh! Hadi picha yake unayo? Kweli unampenda jamani, sikufikiria hilo. Ila kama wewe hutooa basi na mimi sitoolewa wala nini?”
“Kwanini sasa?”
“Sijui ila nadhani sitaolewa sababu na wewe hutaki kuoa, siku ukioa basi na mimi nitaolewa siku hiyo”
Erick alicheka na kumtaka dada yake waendelee kucheza karata na kama kawaida yao walicheza karata sana na kujikuta wamelala hapo hapo.
 
SEHEMU YA 132



Kulipokucha mama Angel aliamka na kujiandaa yeye pamoja na mumewe kwaajili ya kwenda kanisani ila alishangaa kuona watoto wake bado hawajaamka, basi aliamua kwanza kwenda chumbani kwa Erick ili akamuamshe halafu aende chumbani kwa Erica.
Basi alishangaa sana alipoingia chumbani kwa Erick kukuta wamelala pamoja na Erica yani hawana hata habari na zile karata zipo pembeni, kwakweli alisikitika sana na kujisemea,
“Ooooh karata tena jamani!”
Basi alisogea karibu na kuwashtua ili kuwaamsha,
“Nyie wajinga hebu amkeni huko”
Erick na Erica walishtuka huku wakijinyoosha na kuwa kama wakishangaa, basi mama yao akaanza kuwasema,
“Hivi nyie mmeanza lini ujinga wa kulala pamoja? Hivi unajua kuwa mshakuwa wakubwa nyie?”
Baba tyao alisikia mama Angel akiwasema watoto wake na kuamua kwenda ili kuwatetea, ambapo aliuliza kwanza na mkewe alikuwa akimueleza kwa jazba sana basi akamwambia,
“Mke wangu, hebu punguza presha, hao ni ndugu sasa ubaya uko wapi wakilala pamoja? Mbona huku uswahili utakuta wazazi wanachumba na sebule tu na watoto wa kutosha na watoto wao wote wanalala chumba kimoja bila kujali jinsia, sembuse hawa? Hebu acha kuwatisha watoto, wamekuwa wakubwa ndio ila acha kuwawekea sababu ya kufanya mengine. Watoto hawa toka wana miaka mitano umekuwa ukiwatenga, je mke wangu unataka kuwajengea nini hawa watoto?”
“Baba Angel tafadhali, usinifundishe kulea”
“Sikufundishi, ila hata mimi na dada yangu Tumaini mbona tunaishi kawaida tu sababu tumeshazoeana na tunajuana kama ni ndugu”
“Usinifundishe kulea tafadhali”
“Haya yameisha, haya nyie jiandaeni twende kanisani na leo tukitoka Kanisani basi tunaenda kumuona dada yenu Angel”
Erick na Erica walifurahi sana na moja kwa moja walianza kujiandaa kisha wazazi wao nao wakatoka mule chumbani kwa Erick.

Wakati Erica akimalizia kujiandaa alishangaa Erick akienda chumbani kwake, basi Erica alimwambia,
“Eeeeh Erick, umekuja kuniangalia kama nimemaliza?”
“Ndio, maana wewe nawe ukianza hata humalizi. Halafu nimekuletea picha yako”
“Picha yangu?”
“Ndio”
Basi Erick alitoa picha na kumkabidhi Erica, kwakweli Erica alishangaa sana kwani ile picha yake ya muda kidogo, walipiga kwenye mahafali ya darasa la saba, basi akamwambia Erick,
“Kumbe picha yangu hii ulikuwa nayo eeeh! Tabia mbaya hiyo, kila siku naitafuta”
“Aaaah na mimi nimeiona leo wakati natoa nguo hizi kabatini”
“Ila asante sana”
Basi Erick aliondoka zake, naye Erica aliendelea kujiandaa na badae alitoka pamoja na wazazi wake kuelekea Kanisani kama ambavyo walikuwa wamepanga.
 
SEHEMU YA 133

Leo Vaileth akiwa mwenyewe nyumbani, alishangaa tu kumuona Prisca akiwa amefika pale nyumbani kwa mama Angel,
“Jamani Prisca, umekuja kufanya nini tena? Mbona hamnitakii mema na kazi yangu hii jamani!”
“Sio kwamba hatukutakii mema, ungejua ni muda gani nimekaa hapo nje ya geti lenu nikkisubiri hao mabosi wako waondoke hujui tu, yani walivyoondoka tu na mimi nimekuja, kwakweli Nyanda hatuhitaji kufa kwa umasikini wakati utajiri tunauona”
“Mimi nipo tayari kufa masikini ila kuharibu kazi yangu sipo tayari, yani kwa dawa yoyote unayotaka kuifanya sipo tayari. Na leo ningeenda pia Kanisani ila sijisikii vizuri ndiomana wameniacha, kwakweli Prisca naomba uende”
“Hapana, mimi siondoki hadi tufanye hizi dawa”
“Prisca, nitamuita mlinzi akuondoe yani sina masikhara kabisa kuhusu hilo ndugu yangu. Usinitanie ujue”
“Kheee yamekuwa hayo Nyanda?”
“Ndio, sitaki ujinga. Nawe katafute kazi halafu ufanye huo ujinga wako”
“Yani Nyanda unanijibu hivyo, ujue naweza nikakuharibia hata hii kazi ukaiona chungu!”
“Niharibie tu hakuna tatizo”
Kisha Vaileth akaenda kumuita mlinzi ili amuondoe Prisca, yani kile kitendo kilimuuma moyo sana Prisca na alisema kuwa ni lazima atalipiza kisasi.

Leo wakati Tumaini na familia yake wametoka kanisani wakapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Derrick, basi Tumaini akamwambia,
“Kwanini umekuja bila taarifa?”
“Hapa ni kwa ndugu yangu ujue, sasa unataka nitoe taarifa, taarifa gani?”
Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.


Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.
Kiukweli mama Angel hakuipenda ile kitu hata kidogo na kujikuta tu akijitoa mikononi mwa Derrick ila Derrick alionekana kutaka kuendelea kumkumbatia ndipo baba Angel alipoamua kumuachanisha Derrick na mkewe huku akisema,
“Inatosha sasa”
Ila Derrick akasema,
“Dah shemeji, una wivu hadi kwa ndugu? Au umesahau kama huyu Erica ni ndugu yangu? Ni dada yangu huyu, baba yetu ni mmoja”
Baba Angel hakujibu kitu, basi mama Angel alisogea moja kwa moja kwa wifi yake Tumaini na kumuuliza,
“Umeanzaje kumkaribisha huyu?”
“Aaah mimi sikuelewa, ila ninachojua ni kuwa ni ndugu yako na sijui kama kuna mengine kati yenu na hata hivyo sijamkaribisha bali amekuja mwenyewe”
Muda huo Angel nae alikuja na kuwakumbatia ndugu zake kwa furaha sana kwani ni muda mrefu hajaonana nao.
Basi alimfata baba yake sasa na kuanza kuongea nae kwani Angel alimpenda sana baba yake, ni mara nyingi aliongea na baba yake na alijionea vizuri sana kwani baba yake pia alimpenda sana,
“Baba nafurahi sana kwani shangazi anakaa vizuri sana na mimi”
“Oooh nafurahi kusikia hivyo, ukimaliza shule utaniambia ni wapi unataka kwenda kutembea”
“Asante sana baba, nakupenda sana”
Basi Angel alikuwa akimkumbatia baba yake kwa furaha hadi Tumaini akasema,
“Haya sasa wapendanao wamekutana, maana nahisi Angel ndio roho ya mdogo wangu jamani”
Wote walikuwa wakicheka kasoro Derrick aliyeonekana yupo kimya toka muda ule baba Angel amtoe toka mikononi mwa mke wake.
Ila alikaa kimya kidogo na kuanza kumwambia Tumaini,
“Hey, Tumaini ulimuuliza Erica kuhusu lile swala”
“Swala gani?”
“Swala la mimba yangu”
Mama Angel akaona huyu anataka kumuharibia siku basi akainuka na kumshika mkono halafu akaenda nae nje na kuanza kuongea nae,
“Hivi Derrick una nini lakini? Hivi unajua kama ni muda mrefu sana umepita jamani, kwanini upo hivyo hadi leo eeeh!”
“Nisamehe ila najua mtoto wangu angekuwa ni mkubwa kushinda huyo Angel”
“Hivi wewe umesahau yote yaliyotokea kati yangu na yako? Kwani tulienda kufanya tambiko ili iweje jamani eeeh! Hivi wewe si kaka yangu jamani! Yani natamani marehemu baba angekuwepo na angerekebisha makosa yake, nina uhakika asingeruhusu uzaliwe mjinga wewe, hivi unaacha kufatilia maisha mengine ila unawaza ujinga tu muda wote jamani!!”
“Sikia Erica, kipindi naanza na wewe si kwamba nilitaka kukujaribu hapana bali nilikupenda kwa dhati sema ilitokea tu mimi na wewe tukawa ndugu, kweli huwa naumia hadi leo kwani leo hii ni mimi ambaye ningekuwa naishi na wewe na sio huyo kichaa Erick”
Mara mume wa mama Angel alitoka nje na kumwambia Derrick na mama Angel,
“Jamani, hivi kwanini sieleweki Kiswahili!! Derrick nakuomba umuache mke wangu tafadhali, ni ndugu yako ndio ila sikuamini ndiomana nakwambia uwe mbali na mke wangu”
Tumaini nae alitoka na kumshika mkono Derrick ambapo moja kwa moja alitoka nae nje ya geti na kumwambia,
“Derrick kwaheri, siwezi Kurusu uharibu amani ya nyumba yangu”
Kisha akaingia ndani na kufunga geti halafu akamfata mama Angel na baba Angel na kuwataka warudi tu ndani na waendelee na maongezi kama kawaida.
 
SEHEMU YA 134



Nyumbani kwa dokta Maimuna, leo alimuuliza mumewe kwa makini kuwa ni kwanini mama Angel alishtuka baada ya kumuona na aliamua kuondoka,
“Aaaah yule mwanamke ana kichaa ujue, nafahamiana nae yule”
“Unafahamiana nae kivipi?”
“Enzi hizo za ujana, niliteleza na kuwa na mahusiano nae, na nikabahatika kuzaa nae mtoto mmoja, yani huyo Angel ni mwanangu mimi”
“Kheee kumbe!! Una mtoto mwingine wa kuitwa Angel!! Sasa yeye yuko wapi?”
“Yuko nae huko, unajua yule mwanamke ni kichaa yani yeye na mumewe wamejimilikisha mwanangu na kufanya ni mtoto wao, hawataki hata mwanangu anifahamu yani sijui hata wanapoishi”
“Kheee hukuwafatilia?”
“Sikuwafatilia wapi? Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu, na walipokuwa wakiishi mwanzo nilikuwa napafahamu vizuri tu hata nilikuwa naenda kumuangalia mwanangu tena kafanana na mimi balaa, ila sijui vipi wakaamua kuhama pale na kuuza nyumba kabisa ili mimi tu nisijue wanapoishi”
“Kwao kabisa na huyo mama Angel unapafahamu? Toka walipohama uliwahi kwenda kwao?”
“Kiukweli, kwao kabisa nilikuwa napafahamu ila kwasasa nimepasahau kabisa. Ila naamini kuwa kuna siku yule mtoto atahitaji kunifahamu baba yake wa ukweli na mama yake hatokuwa na jinsi zaidi ya kumleta tu kwangu”
“Yani hiyo ndio shida yenu wanaume, huwa mnakimbia majukumu yenu kwa kuamini kuwa mtoto akikua atakutafuta baba yake, unajua mtoto kwa kadri anavyolelewa na mama ndivyo anavyozidi kupandikizwa chuki kuhusu baba yake aliyemtelekeza? Kiasi kwamba hata kukuona tena hatamani! Hivi unajua hilo?”
“Aaaah najua mwanangu atanitafuta tu, unajua nimefanana nae!”
“Ila kumbuka ni mtoto wa kike, ambavyo amekuwa na kuanza urembo huko kufanana nae kutatokea wapi? Hebu kuwa makini bhana mfatilie mwanao”
“Kheee una nini leo Maimuna? Katika maisha ya kufahamu watoto wangu hata mara moja hujawahi kuniambia kuwa nimfatilie mwanangu, na siku zote nikikwambia kuwa akikuwa atanitafuta huwa unakubalianana kauli yangu, mpaka wenyewe wanapelekwaga tu kwa mama yangu kule. Ila huyu Angel imekuwaje? Unamfahamu kwani?”
“Simfahamu ila nahitaji umfatilie”
“Haya, nimekuelewa mke wangu”
Kwakweli dokta Maimuna alishangaa mno akihitaji kufahamu zaidi kuhusu Angel, yani alitamani sana kumuona huyo Angel na kujua kuwa kwa kipindi hiko anafanya nini na anafanana vipi.
 
SEHEMU YA 135


Leo mama Junior alimkumbuka sana mdogo wake na alihitaji kwenda kumuona ila hakutaka kumtaarifu wala nini, hivyobasi moja kwa moja aliondoka kwake na kuelekea kwa mama Angel bila kujua kuwa mama Angel hayupo wala nini.
Basi alivyofika karibu na getini kwa mama Angel alishangaa kumuona mtu kama akimwaga kitu halafu alianza kusota yani kama mtu anayefanya uchawi, kwakweli mama Junior alichukia sana na kumfata yule mtu pale getini kisha alimuinua na kumkunja halafu alimnasa vibao vya kutosha huku akimuuliza,
“Nani kakutuma wewe mbwa? Unafanya nini hapa? Unafanya uchawi kwenye nyumba ya mdogo wangu? Haya mambo huwa nayasikia tu, kumbe ni kweli!”
Basi mama Junior alimuita mlinzi wa nyumba ile ambapo alitoka nje na yeye alishangaa sana baada ya kuambiwa kile ambacho huyo msichana alichokuwa akifanya, basi akasema,
“Hivi wewe si nimetoka kukutimua ndani!! Kumbe umekuja kufanya maovu yako huku nje”
Mama Junior nae alishangaa sana na kuuliza,
“Kumbe alianzia ndani?”
“Ndio, ni ndugu yake na Vaileth huyu”
“Khaaa kumbe!! Vaileth, wee Vaileth”
Basi Vaileth alienda haraka haraka na kushangaa kukuta Prisca ameshikwa na mama Junior kisha mama Junior alimwambia alichokuwa akifanya ndugu yake huyo, kwakweli Vaileth alishindwa kabisa cha kusema, na muda huo huo mama Junior alimuamuru mlinzi kuwa amfunge kamba yule Prisca mpaka muda ambao wakina mama Angel watakaporudi ili na wao wajionee hayo.

Ilipofika jioni,familia ya baba Angel waliaga pale kwa shangazi wa Angel na kuondoka zao, wakiwa kwenye gari Erica aliwauliza wazazi wake,
“Mama, kwani yule mbaba tuliyomkuta kwa shangazi ni nani?”
“Aaaah yule ni mjomba wenu”
“Aaaah sasa mbona inaonekana kama hamumtaki kabisa, maana naona mlikuwa kama mkimfukuza hivi”
“Mmmh na wewe, hebu mara nyingine uwe una nyamaza kimya maana kuna mambo hata huwa hayakuhusu”
Basi ilibidi Erica akae kimya tu.
Walipofika nyumbani walishangaa sana kumkuta Prisca akiwa kibarazani huku kafungwa mikono na miguu, kwakweli mama Angel alishangaa sana na mara dada yake alitoka na kuanza kumueleza mlolongo mzima, kwakweli muda huu baba Angel alichukia pia, na moja kwa moja alienda kumshika Prisca na kuanza kumzaba makofi,
“Kwanini unanifanyia ujinga hivi kwenye nyumba yangu? Nadhani hunijui vuzuri wewe”
Na muda huo huo baba Angel alipiga simu polisi na muda kidogo walifika maaskari na kumkamata Prisca halafu wakampeleka rumande, yani muda huo Vaileth alikuwa ndani tu, yani pale ndio mtu unaelewa kuwa damu ni nzito, yani alikuwa akimuhurumia sana ndugu yake.
Basi mama Junior akasema,
“Tena huko rumande wamuweke mwezi mzima, yani nilichomkuta anafanya kwakweli huyu msichana hafai kabisa”
“Aaaah wiki tu inamtosha dada”
“Kheee unamuonea huruma wakati alitaka kuharibu nyumba yako mwenyewe? Na hata sijajua ni dawa gani ameweka mlangoni jamani!”
“Hamna shida, inabidi ndugu yake akafagie”
Kisha mama Angel alimuita Vaileth ambaye alitoka chumbani na kumwambia kuwa akafagie eneo lile, basi Vaileth alienda kufagia ila huku akiwa na mawazo sana yani alikuwa akifagia huku machozi yakimtoka.
 
SEHEMU YA 136


Muda wa kulala, siku hiyo Vaileth alikaa kitandani kwa muda kwanza akitafakari na kujiuliza,
“Hivi kwanini umasikini unafanya tudhalilike kiasi hiki!! Yani tunadhalilika sababu ya umasikini, tunahitaji utajiri wa lazima, ndugu yangu Prisca hajataka kabisa kukubaliana na hali halisi kuwa hata mimi nilibambwa, na hata tulibambwa wote pamoja na shangazi ila leo bado kapata ujasiri wa kuja tena kufanya dawa? Hivi kwanini mambo haya lakini, ndugu yangu anateseka rumande jamani sababu ya umasikini”
Alijikuta akiinama huku akitokwa na machozi, yani hakuwa na raha kabisa, alijihisi kuumia moyo sana, akakumbuka kipindi wapo kijijini akiwa ameongozana na Prisca huku wakiongea mambo mbalimbali, akakumbuka jinsi walivyoahidiana kufanya kazi kwa bidii ili kupata pesa na kufanya maendeleo ikiwa na kuwasaidia wazazi wao. Kwakweli aliumia sana, ila atafanyaje sasa ikiwa na yeye ile kazi anaihitaji sana kwani hakuwa na msaada wowote ukizingatia hata mwanaume aliyezaa nae alimkimbia kwahiyo alikuwa na uchungu sana moyoni huku akilaumu umasikini wao.
Basi siku hiyo alilala kwa mbinde sana kwani alihisi pia yeye ataishia vibaya sana kwani yakiisha mambo ya Prisca aliona pia kuwa yeye hawatamuacha salama kwani nae ataonekana kuwa ni mtu mbaya na asiyefaa.

Kulipokucha, Vaileth alishangaa akiitwa na leo aliyemuita alikuwa ni baba Angel basi alitoka moja kwa moja na kwenda sebleni na kuanza kuongea nae,
“Najua una uchungu sana kwa kile tulichofanya kwa ndugu yako, ila hata wewe ungekuwa ni sisi basi ungefanya kitu hiko hiko, unajua haiwezekani kabisa mtu tumeongea nae swala moja mar azote ila anajifanya kama hasikii zaidi zaidi anaenda kuleta dawa zingine na kuanza kuzisambaza getini kwetu, kwakweli nimechukia sana. Tusamehe bure kwa hilo, ila nduguyo tumempeleka polisi ili tu kumshikisha adabu”
“Naelewa shemeji, hakuna tatizo”
“Ila muda huu nimekuita ili nikuulize jambo moja, ni kitu gani wewe kama wewe ulitamani kukifanya baadaa ya kupata hela?”
“Kitu pekee nilichokuwa natamani ni kuboresha nyumba wanayoishi wazazi wangu kani bati lake limeoza na huwa wanaingiliwa na mvua kipindi cha masika. Kwahiyo nikipata pesa basi kitu cha kwanza nitakachofanya ni hiko”
“Oooh sawa, hakuna tatizo. Basi tutaongea vizuri, ila acha kuwa na mawazo Vaileth”
Kisha baba Angel alienda chumbani na kumuaga mke wake maana siku hiyo mke wake alisema kuwa hatoenda popote halafu yeye aliondoka zake kwani shida yake ilikuwa ni kwenda kumtafutia Erica shule nyingine ukizingatia ile shule aliyokuwa akisoma Erica walishaikataa kabisa.
 
SEHEMU YA 137


Leo Erica alikaa na Abdi na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, ambapo Elly alianza kumwambia Erica,
“Basi mama yangu anasema kuwa anamfahamu hadi shangazi yenu”
“Shangazi yetu? Anamfahamu kivipi?”
“Nyie shangazi yenu si anaitwa Tumaini? Halafu nasikia ukoo wenu umeingiliana sana, mamangu anasema lazima mtakuwa na laana”
“Kivipi? Unajua sikuelewi?”
“Ni hivi, mama yako na baba yako, halafu shangazi yenu Tumaini na mjomba wenu Tony yani baba yenu ni ndugu wa shangazi yenu yani kaka na dada hafu mama yenu na mjombaTony ni ndugu pia yani kaka na dada, halafu kuna mama yenu mkubwa na mumewe wote kuna undugu katikati, basi mama yangu anasema hiyo ni laana maana hairuhusiwi”
“Jamani, mbona sisi tunaishi kawaida tu!”
“Ndio ila kuna laana katikati yenu, maana ukoo wenu umeingiliana ingiliana”
“Kheee makubwa, sikujua kama ni hivi ila mama huwa nikimuuliza hata hanijibu vizuri. Jana tulienda kwa shangazi na kukutana na mbaba mmoja anaitwa Derrick, kiukweli huyu sijamwelewa kabisa yani na mama hataki kusema ukweli”
“Basi usijali, sababu mama yangu anafahamu mengi sana ya ukoo wenu, nitamuuliza kuhusu hilo pia halafu kesho nitakuletea majibu”
“Oooh asante sana Elly, nashukuru kwa kuniambia mambo ambayo hata mimi binafsi nilikuwa siyafahamu kama yanahusu familia yetu”
Basi baada ya maongezi hayo walirudi tena darasani.
Muda wa kutoka ulipofika, kila mmoja aliondoka zake na kwenda kwao.
Ila Erica alivyofika kwao alijihisi kuwashwa sana na ile habari aliyoipata basi moja kwa moja alienda chumbani kwa kaka yake na kuanza kumsimulia ila muda huo bila kujua kumbe mama yao alikuwa mlangoni akiwasikiliza maana nay eye kuna kitu alikuwa anaenda kufata chumbani kwa Erick, basi akamsikia Erica akimwambia Erick,
“Yani Elly kaniambia kuwa kesho atanieleza kila kitu kuhusu huyo mjomba Derrick maana mama yake anajua kila mtu kwenye ukoo wetu”
“Duh! Huyo mamake Ellyn i noma, ila ni nani jamani! Kwanini anajificha sasa? Kama ni mtu mwenye lengo zuri ni kwanini ajifiche jamani!”
“Hata mimi namshangaa ila nahisi ni mtu ambaye mama na baba wanamfahamu vizuri sana”
“Ila mimi simuamini maana lazima atakuwa ni adui wa familia yetu ndiomana anafahamu mambo mengi yanayoendelea kwenye familia hii”
“Aaaah sio kweli, sio adui yetu wala nini. Mimi nina uhakika tukija kumfahamu tutamfurahia”
“Binafsi sitaki hata kumfahamu huyo mama maana naona hana lengo jema na familia yetu”
“basi kesho ataniambia kila kitu kuhusu huyo mjomba Derrick, mama si amenificha? Ngoja kesho nije nikueleze”
Kwakweli mama Angel alichukia sana na kujikuta akimchukia Elly na mama yake kwani alijua kuwa hana lengo jema na familia yake, kwa upande mwingine aliona mwanae Erick ana akili zaidi ya Erica kwani ameweza kutambua kwa haraka kuwa huyo mama hafai ila Erica anaona huyo mama ni mtu mzuri tu kwake.

Basi usiku wa siku hiyo mama Angel alimsimulia mumewe kila kitu kuhusu kile ambacho Erica na Erick walikuwa wakiongea, kwakweli hata baba Angel alishangaa sana na kujiuliza,
“Huyo mwanamke ni nani sasa?”
“Yani hapo ndio pabaya, adui usipomjua utapata shida sana”
“Ni kweli mke wangu, yani tungemjua huyo mwanamke ingekuwa rahisi sana kwetu, ila kuna shule tayari nimeshamtafutia Erica”
“Bora, sitaki tena kesho Erica aende kwenye ile shule”
“Kesho, nitaenda nae kwenye shule mpya ili akafanye usahili kwanza maana hizi shule zingine wana sharia sana”
“Shule yenye sheria ni nzuri mume wangu, yani ni kumpeleka tu huko huko maana huyu mtoto naye anataka kuanza vituko tu”
Basi mama Angel na baba Angel walikubaliana kuhusu swala la Erica kuhamishwa shule ile anayosoma.
Kulipokucha baba Angel alijiandaa na kutoka ambapo alimkuta Erica nae amejiandaa basi alimuita na kuongea nae,
“Mwanangu, leo kuna shule nakupeleka ukafanye usahili maana nataka kukuhamisha ile shule”
Erica alinyong’onyea sana na kulalamika kwa baba yake,
“Jamani baba, kwanini unihamishe shule jamani! Mimi nimeizoea ile shule”
“Ila shule ninayotaka kukuhamishia ni bora zaidi”
kwakweli Erica alichukia sana ila hakuwa na namna zaidi ya kupanda kwenye gari na baba yake huku wakianza safari ya kuelekea huko shuleni.
Baba Angel alimuona mwanae jinsi alivyochukia kutokana na lile swala la kutaka kumuhamisha shule, basi aliona njia ya pekee ili mwanae afanye usahili vizuri ni kumwambia maneno mazuri ili aweze kufanya usahili vizuri zaidi, basi alimwambia,
“Mwanangu sikia, leo ukifanya usahili vizuri basi ukimaliza nakupeleka shuleni kwenu ili ukaongee na wanafunzi wenzio na upate kuwaaga ila ukifanya usahili vibaya sahau kabisa kama utarudi tena kule shuleni kwenu maana nipo radhi niwaombe walimu wakuchukue hivyo hivyo”
“Baba nakuahidi kuwa nitafanya usahili vizuri sana, yani baba yangu hata usiwe na mashaka na mimi maana nitafanya usahili kwa umakini wote”
Basi baba yake alitabasamu na kuendelea na safari.
 
Back
Top Bottom