Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Abdallahking

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2018
Posts
3,985
Reaction score
10,840
Simulizi: NGUVU YA MAPENZI
Mwandishi: ATUGANILE MWAKALILE
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES


SEHEMU YA 1

Mdada mmoja mrembo sana aliyeitwa Angel alionekana siku hii akiwapeleka wadogo zake kuripoti katika shule mpya maana wadogo zake hao walikuwa ndio wanaanza kidato cha kwanza na yeye alikuwa yupo kidato cha nne, basi alifika nao shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu ambaye alimzoea sana sababu alikuwa ni mwalimu wake pia maana ni shule hiyo hiyo ambayo nay eye alikuwa akisoma kwa kipindi hiko, basi aliwakabidhi pale na mwalimu alianza kuongea na Angel,
“Halafu Angel unajua wenzio wa kidato cha nne walianza kuja shule toka wiki iliyopita halafu wewe leo umeleta wadogo zako tu na kutaka kuondoka”
“Sir Harun, sipo vizuri mimi ndiomana sijaja shule”
“Na wazazi wako wako wapi?”
“Wamesafiri ndiomana hata wadogo zangu imebidi niwalete mimi”
“Hata hivyo, bado unatakiwa uje kwenye masomo Angel, upo kwenye level ngumu sana hiyo”
“Sawa, basi kesho nitakuja mwalimu”
Kisha Angel akamuaga pale mwalimu wake na kuondoka zake, siku hiyo Angel hakumwambia dereva wao maana kuna matendo yule dereva alikuwa akiyafanya kwake na kufanya Angel asimuamini kuwa nae karibu kwahiyo aliamua kujiondokea mwenyewe.
Akiwa njiani wakati wa kurudi kwao akapigiwa simu na rafiki yake Hanifa,
“Uko wapi Angel?”
“Nipo karibia na maeneo ya shule ila narudi nyumbani”
“Kheee nilivyosikia shule si nikajua umeenda shule”
“Niende wapi, kwanza nahisi uvivu hatari ila nimekuja kuwakabidhi wadogo zangu wanaanza kidato cha kwanza, kwahiyo ilinilazimu niwalete maana wale watoto wamedekezwa sana na mama”
“Sawa, basi naomba upitie hapa dukani kwetu kuna jambo nataka tuongee”
“Sawa, hakuna tatizo”
Moja kwa moja Angel alielekea dukani kwakina Hanifa ili kuweza kuzungumza nae mawili matatu.
 
SEHEMU YA 2


Angel alifika dukani kwakina Hanifa na kuanza kuongea nae maana hakujua ni kitu gani ambacho aliitiwa na Hanifa siku hiyo,
“Sikia Angel nimekuita hapa maana kuna jambo zuri nataka kuongea na wewe”
“Jambo gani hilo?”
“Kwanza una mpango wa kurudi lini shule?”
“Wiki ijayo”
“Basi naomba Ijumaa uje hapa”
“Mmmh Ijumaa kufanya nini tena? Yani Ijumaa ndio baba na mama wanarudi, sasa itakuwa balaa si unajua mama yangu akiwepo yani hakuna kutoka ni ananichunga hadi nywele yule mwanamke”
“Yani jambo lenyewe kwa Ijumaa itakuwa ni vizuri sana likifanyika”
“Mmmh ngoja nitaangalia basi, niambie ulichoniitia leo”
“Hamna ni hiko hiko”
“Jamani hiko si ungeweza kuniambia hata kwenye simu tu!!”
“Kwani wewe hukupenda kuniona jamani Angel!!”
Muda kidogo alikuja ndugu wa Hanifa ambapo Hanifa alimtambulisha kwa Angel sababu hakumfahamu,
“Angel, huyu ni ndugu yangu anaitwa James”
“Oooh James, nafurahi kumfahamu”
“James, na huyu ni rafiki yangu anaitwa Angel”
“Oooh nafurahi kukufahamu Angel”
Kisha James akampa mkono wake Angel, ila moja kwa moja James alijikuta akimpenda Angel yani alijikuta akimpenda gafla tena kimapenzi, basi mpaka muda Hanifa anamsindikiza Angel basi James alikuwa akimuangalia tu Angel hadi alipoishia yani alishindwa kutoa jicho lake kwa Angel.
 
SEHEMU YA 3


Hanifa alivyorudi dukani, James alianza kumuuliza vizuri kuhusu Angel,
“Samahani dada, yule Angel ana mpenzi?”
“Mmmh unataka nini? Binti mrembo vile utamuweza? Yani yule Angel kwao hawana dhiki ujue, sasa utaweza kumuhudumia unamuulizia, basi ushamtamani hivyo”
“Yani sio kumtamani, nampenda sana, jamani nimempenda haswaaa nadhani usiku nikilala nitaota Angel tu”
“Sasa unadhani Angel anaweza kukukubali mtu kama wewe? Aaanze tu, ila Angel hana mchumba yani huyu binti licha ya urembo wake na uzuri wake, hana mchumba wala mpenzi halafu mama yake ni mtu wa dini sana, halafu ni mkali sana yani anambana binti yake kiasi sidhani kama anaweza kuwa na mwanaume mama yake asigundue”
“Aaaah usinifanyie hivyo bhana Anifa, mimi nampenda Angel yani nimempenda sana hapa naona kama yeye ndio pumzi yangu”
Hanifa akacheka sana na kumwambia James sasa,
“Kwa taaarifa yako huyu Angel nimemuita leo hapa sio kwasababu yako ila ni kwasababu ya mjomba, yani mjomba ni anampenda Angel kufa kabisa, sasa tuone kama una uwezo wa kushindana na mjomba anayekulisha, kukuvisha na kukusaidia uende chooni mjinga wewe, yani mimi Angel ni rafiki yangu haswaaa ila nimemuita sababu ya mnjomba, sema tu mjomba mwenyewe katingwa leo, kwahiyo ndugu yangu tafuta lingine, kuhusu Angel umekosea namba”
“Sawa nakubaliana na wewe ila nipe hata namba yake tu yani utakuwa umefanya kitu kikubwa sana kwangu”
“Hahaha, namba utamuomba mwenyewe ukimkuta mahali ila sikupi namba yake kabisa, andika maumivu tu”
“Ila roho mbaya hiyo Hanifa”
“Roho mbaya unayo wewe unayetamani mwanamke ambaye ameshatamaniwa na mjomba wako”
Basi James aliumia tu kwani alijiona wazi kuwa amempenda Angel tena amempenda sana.


 
SEHEMU YA 4

Angel alirudi nyumbani kwao na moja kwa moja alienda kupika kwani alijua wadogo zake karibu watarudi, nyumba yao ilikuwa kubwa na nzuri lakini mama yao hakuweza msaidizi wa kazi pale nyumbani kwahiyo kazi zote walikuwa wakizifanha wenyewe kasoro za nje tu ambazo zilikuwa zikifanywa na mlinzi wa nyumba ile.
Wakati Angel anapika, simu yake ikaita alipoichukua na kuangalia alikuwa ni mama yake basi alipokea kwa shauku sana na kuanza kuongea nayo,
“Kwanini hujaenda shule leo?”
“Jamani mama, si nimewapeleka wadogo zangu”
“Hivi Angel mwanangu kwanini lakini eeeh! Nahitaji usome na ufike mbali, ndoto yangu ni kuwa wewe utakuwa daktari mkubwa sana na mashuhuri hapa nchini, ila kwanini unakuwa mzembe hivyo!”
“Jamani mama, shule tunafungua wiki ijayo”
“Mjinga wewe, wiki ijayo ya wapi? Mwalimu wako Harun katoka kunipigia simu muda sio mrefu kuwa kidato cha nne wenzio walianza kwenda toka wiki iliyopita, sitaki ujinga Angel, kesho shule, sio kwavile sipo basi ndio utegee, kesho nimesema shule”
“Sawa mama, nimekusikia”
Angel alikata simu ya mama yake ila alichukia sana kwani alijua ni mwalimu wake Haruni ndio kamsemea kwa mama yake,
“Yani mwalimu mbea yule, mwanaume mzima mbea, sijui anamtaka mama yangu!! Ngoja, nitamwambia baba halafu atakoma”
Basi akamalizia kupika na kwenda kuangalia tv tu maana aliona mama yake kashamletea habari za shule ambapo alitaka kutegea mpaka wiki nyingine, baada ya muda kidogo wadogo zake nao walirudi kutoka shule basi alianza kuongea nao kuhusu siku ya kwanza shuleni,
“Haya wadogo zangu wapendwa, shule ile mmeionaje? Mazingira yakoje? Mmeipenda au?”
“Kama hatujaipenda mtatuhamisha?”
“Ushaanza Erick na ujinga wako, muhamishwe muende wapi? Pale mpende msipende mtasoma pale pale”
“Sasa ulikuwa unatuuliza ili iweje? Kwanza njaa inaniuma?”
“Kheee yani hili toto, sijui mama kaliokota wapi. Nenda jikoni huko ukajipakulie, niambie Erica, umeionaje shule mdogo wangu”
“Shule ni nzuri sana na nimeipenda ila dada leo Erick kapigana”
“Kheee siku ya kwanza shuleni na kupigana jamani! Picha gani mmeonyesha? Amepelekwa kwa mwalimu?”
“Hapana, ila kampiga mtoto wa watu ngumi”
“Ndiomana umerudi tu na kulalamika njaa, ngoja nimpigie simu mama yako nimwambie ujinga wako wa kupigana”
Hakuna mtu ambaye huwa wanamuogopa kama mama yao basi Erick alirudi kumuomba msamaha dada yake ili asipige simu kwa mama yao,
“Dada nisamehe tafadhari, naomba nisamehe dada. Usimwambie mama”
“Ukipigana tena je!”
“Sirudii tena kupigana dada yangu, naomba unisamehe”
“Msamaha wangu kwako, nakuletea sare zangu za shule uzipige pasi maana na mimi kesho naenda”
“Sawa dada nitafanya hivyo”
Basi Angel alicheka na kwenda kuchukua sare zake ili mdogo wake ampigie pasi halafu yeye alirudi kukaa huku akiangalia vizuri vipindi vya kwenye Tv.
Muda kidogo Angel aliona uvivu na kuinuka kwenda chumbani kulala, basi Erica alipomuona kaka yake akihangaika na zile nguo za Angel kuzipiga pasi tena kabla ya kula wakati alilalamika kuwa njaa inamsumbua, basi akamsogelea na kuhitaji kumsaidia,
“Erick, acha nizipige mimi. Nenda kale tu”
“Oooh ndiomana Mungu alifanya uwe pacha wangu, muda mwingi unanihurumia, asante Erica”
Basi Erica alinyoosha zile nguo vizuri kabisa kisha kumpelekea dada yake kuchumbani na kuziweka vizuri ila Angel hakuwa amelala kabisa maana alikuwa akichezea tu simu basi zile nguo zilivyoletwa na Erica akauliza,
“Mbona umeleta wewe na sio Erick ambaye nimempa hiyo adhabu”
“Erick anakula dada”
“Kwa kuteteana nyie mapecha siwawezi, haya niwekee vizuri hapo”
Erica aliweka na kutoka mule chumbani.



 
SEHEMU YA 5


Kesho yake asubuhi na mapema walijiandaa wote na kwenda shuleni, na walipofika Angel aliwaacha wadogo zake kwenda kwenye madarasa yao halafu yeye kwenda kwenye madarasa ya wenzie wa kidato cha nne, ila alipoingia tu darasani kuna mkaka aligongana nae macho na kugundua kuwa yule mkaka alikuwa ni mgeni katika darasa lao, yani Angel alikuwa akimuangalia huyu mkaka na huyu mkaka pia alionekana akimuangalia Angel hadi alipokaa walikuwa wakiangaliana na kila mmoja alionekana kuogopa kumfata mwenzie labda kumsalimia, kwani huyu mkaka alijiona kuwa ni mgeni kufanya hivyo haipendezi, naye Angel aliona kuwa akimfata yule mkaka itakuwa kama anajipendekeza kwa mgeni.
Basi yule mkaka akameza mate tu mpaka mwenzie wa pembeni akamstua na kumwambia,
“Wewe naona unamuangalia mrembo wa darasa kiasi hiko utamuweza!! Yule binti ni matawi ya juu, kwanza umeona alivyo mrembo?”
“Nimeona yani ni mrembo haswaaa”
“Basi fata masomo yako, usimuone hivyo, walimu wenyewe ofisini wanagongana vikumbo kwaajili yake, wanafunzi hapa shuleni ndio balaa yani, kwakweli mtoto kaumbika yule”
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa Angel au Malaika, yani yule ni Angel kweli, hata ukimuangalia lazima uvutiwe nae, pole sana ila najua kumpata huwezi”
“Siwezi kweli, ila nitajaribu”
“Ila kwenu mna uwezo nyie”
“Ni kweli ila mimi kutongoza sijui kabisa, sema nimempenda sana”
Mwenzie akacheka na kumwambia,
“Wengi wanampenda ila kumpata hawawezi, kwanza mama yake ni mkali huyo balaa. Akiongozana nae huwezi hata kumsalimia”
Yule mkaka akaguna tu na kuendelea na mambo mengine wakati huo Angel nae akiendelea na mambo mengine ila rafiki yake aligundua kitu toka kwa Angel sababu alimuona akimuangalia sana yule mkaka,
“Mmmh Angel mbona umemuangalia sana yule mkaka?”
“Naona sura yake ni ngeni, ndiomana nimemuangalia sana ulihisi nini?”
“Nilihisi unampenda eti? Nikawaza huyu Angel si huwa anajifanya hapendi wanaume, imekuwaje tena kwa huyu?”
Angel akacheka tu na rafiki yake akaendelea kuongea,
“Yule mkaka anaitwa Samir”
“Aaaah Samir!! Yani ushaenda kudaka jina la mgeni jamani Yusra”
“Sasa mgeni anapendeza vile nisidake jina lake kweli jamani, inawezekana hiyo eeeh!”
“Umempenda?”
“Sijasema hivyo jamani Angel”
Basi wakaongea na kuendelea na mambo ya masomo maana muda huo na mwalimu aliingia kufundisha.




 
SEHEMU YA 6


Muda wa kutoka shule ulipofika, Angel alitoka na alikuwa akisubiriwa na wadogo zake na kuwauliza kwa makini,
“Erica, vipi leo Erick hajapigana?”
“Jamani dada, sijapigana”
“Haya sasa, tunarudi nyumbani kwa amani”
Walirudi nyumbani wakiwa wamechoka na njaa ziliwasumbua, wakaanza kulalamika,
“Jamani kuna umuhimu wa kuwa na mdada wa kazi, hivi kwanini mama anatufanyia hivi jamani!”
“Ila siku zote baba huwa anasema kuwa mdada wa kazi ni wa muhimu sana ila mama hataki hata kusikia, hebu ona tulivyochoka, hivi nani anaweza kupika kwasasa? Hebu kamuagizeni huyo mlinzi mkate, tule mkate na chai tupumzike”
Basi wakamuagiza mlinzi mkate ambapo baada ya muda mfupi aliwaletea na wakanywa chai baada ya hapo Angel aliwaambia wadogo zake,
“Haya leo ofa, nendeni kavueni sare zenu za shule nikazifue”
Basi waliharakisha na kumpatia dada yao kisha kila mmoja kwenda kuoga wakati dada yao ameenda kufua zile nguo na kuoga.
Muda huu Erick na Erica walikaa sebleni ila Erick alikuwa akipiga miayo sana ikabidi Erica amuulize,
“Ulishiba kweli Erick?”
“Nitashiba wapi? Mkate wenyewe mdogo ule, mimi ni mtoto wa kiume yani kula vitu vyepesi vile nateseka”
“Pole jamani, nikakusongee ugali?”
“Kheee Erica ndio unajitoa kiasi hiko!! Asante sana kwa kunijali, wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu”
Basi Erica aliinuka na kwenda kumsongea ugali kaka yake ambapo ulipokuwa tayari, Erick alikula ule ugali kwa maziwa mtindi, basi Angel alikuja ndani na kushangaa,
“Kheee Erick umesonga ugali?”
“Angel huyo kanisongea”
“Kumbe Angel unajua kusonga ugali? Ndiomana mama hataki kuweka msaidizi wa kazi maana anajua kazi zote wanae tunaweza”
Basi Angel akasogea na kuubonya bonya ule ugali na kuona kuwa umeiva kisha alienda chumbani kwake.




 
SEHEMU YA 7


Angel akiwa chumbani kwake alishangaa sana kwani kila muda alikuwa akikumbuka tukio la kukutanisha macho na Samir, halafu kwenye akili yake alihisi kama jina la Samir limeanza kutawala, kiasi kwamba Erica alienda chumbani kwake na kumshtua naye akageuka na kusema,
“Samir”
Erica alicheka na kumuuliza dada yake,
“Mmmh dada, Samir ndio nani?”
“Mmmh umbea huo, haya ulikuwa unasemaje?”
“Mama amepiga simu ya mezani pale, kasema Ijumaa wanarudi”
“Jamani hadi Ijumaa dah! Mimi nitakuwa nimeshachoka na kazi za nyumbani kwakweli, arudi aje afanye mwenyewe”
Erica alicheka na kuondoka chumbani kwa dada yake maana hata yeye alikuwa na chumba chake.
Basi Angel akakumbuka alichoongea na Hanifa kuhusu Ijumaa ikabidi ampigie simu kwani hakujua atafanyaje wakati wazazi wake ndio wanarudi,
“Hanifa mwenzangu nitashindwa kuja hiyo Ijumaa”
“Jamani Angel ni kitu cha muhimu sana tafadhali, nakuomba usikose na wala haitochukua muda mrefu”
“Ni kitu gani jamani eeeh!”
“Sikia rafiki yangu, kwani unaogopa nini kuja?”
“Mama na baba wanarudi Ijumaa, sasa mimi nitakuja vipi?”
“Sikia Angel, Ijumaa huwa watu wanawahi kutoka shule kwahiyo wewe ukitoka pitia hapa dukani mara moja tu halafu unaondoka”
“Halafu wewe unanichuza ujue maana hata shule huji ila umekazana tu kuuza duka halafu mimi unataka kunichuza”
“Hapana, nadhani unanielewa Angel, naanzaje kufanya kitu kinyume sasa jamani eeeh!”
“Haya nitaangalia uwezekano”
Basi akakata ile simu na kuendelea na mambo mengine ila usingizi ukampata pale pale.


 
SEHEMU YA 8

Angel aliamka kwenye mida ya saa tatu na alikuta wadogo zake ndio wanakula, basi na yeye alikaa na kuanza kula, ila aliguna,
“Mmmh hiki chakula kapika nani tena?”
“Erick huyo kapika”
Angel akacheka na kusema,
“Kweli nyumba inavituko hii jamani, yani Erick ndio kapika leo dah! Sio kwa michumvi hii uliyoitia kwenye hizi tambi mdogo wangu jamani! Ngoja kesho nitapika tambi za sukari na mtajiramba haswaaa, haya hebu nipeni hiyo juisi nionje nayo”
Basi wakammiminia ile juisi na kuinywa huku akisema,
“Hii lazima imetengenezwa na Erica”
Basi Erica akatabasamu na kuitikia kuwa ni yeye ameitengeneza, basi Angel akasifia na kusema,
“Kwa hakika mume atakayekuoa mdogo wangu atafaidi sana”
Erick alionekana kuchukia, akadhira chakula na kuinuka,
“Kuleni wenyewe sasa”
Angel alicheka na kusema,
“Kheee ulitaka na wewe nikusifia na michumvi hii! Susa baba, wenzio tunakula kama kawa, umetujazia michumvi hadi tuumwe safura halafu unataka nikusifie”
Basi Angel alikula kula pale ila aliona ambavyo Erica hakuwa na raha na kumwambia,
“Wewe achana na yule aliyesusa, sisi tujilie zetu tukalale, achana na wehu wa kususa”
“Ila dada ungembembeleza kidogo”
“Biashara hiyo sifanyi, mama yake angekuwepo labda ndio angeenda kumbembeleza, sikia inuka kambembeleza pacha wako huko maana naona nawe umeishiwa na amani, ndio shida ya kuzaliwa mapacha hii”
Basi Erica aliinuka na kwenda chumbani kwa Erick, na Angel aliendelea kula huku akilalamika kuhusu chumvi na hatimaye kuinuka kwenda kulala tena.
Basi Erica akaanza kuongea na Erick,
“Jamani twende ukale ndio uje kulala Erick”
“Kwakweli wewe Erica una moyo wa mama kabisa na roho ya baba, ila dada Angel jamani dah! Yani anajijua mwenyewe na anajijali mwenyewe tu”
Basi akainuka na kwenda mezani na kuendelea kula ambapo Erica alimuuliza kaka yake,
“Ila wewe ni kitu gani kilikukera kwa alivyoongea Angel hadi ukagoma kula?”
“Tuachane na habari hizo Erica, ngoja ninywe juisi nikalale. Ni kweli hii juisi uliyoitengeneza ni tamu sana”
“Kwahiyo ni kweli mume atakayenioa atapata raha”
“Hivi Erica wewe na udogo huo unaanza kuongelea habari za mume wa kukuoa? Ngoja mama aje nimwambie”
“Hapana jamani, mimi nilikuwa nafata maneno ya dada tu”
Basi walimaliza kula na kila mmoja alienda kwenye chumba chake kulala.



 
SEHEMU YA 9


Siku hiyo walichelewa kuamka na kufanya wajiandae haraka sana, na kugundua kuwa hata gari la shule limewaacha,
“Sasa dada tutafanyaje?”
“Ngoja nimpigie dereva simu aje atupeleke shuleni”
Basi Angel akampigia dereva wao ambaye baada ya muda mfupi tu alifika kuwachukua ili waende shule, basi pale mbele alikaa na Angel na kuanza kuongea nae,
“Ila mbona siku hizi Angel hutaki niwapeleke safari zenu?”
“Aaaah wewe unakera bhana”
Yule dereva aliendelea kuongea ila hakuna jambo ambalo Angel alimjibu, basi walifika shuleni na kushuka ambapo dereva alimuuliza Angel,
“Vipi wakati wa kutoka nije kuwachukua?”
“Aaaah tutarudi na gari la shule”
Basi wakaachana nae halafu wao wakaelekea kwenye madarasa yao.
Leo wakati Angel anaingia darasani akagongana kikumbo na Samir na kujikuta wakitazamana sana, na wote kusema kwa pamoja,
“Samahani”
Basi wakajikuta tena wakiangaliana, Samir akampa mkono Angel na kumwambia,
“Naitwa Samir, sijui nawe waitwa nani?”
Naye Angel alimpa mkono na kumwambia,
“Naitwa Angel”
Cha kushangaza walisikia kelele darasani na kugeuka darasani ili kuangalia kuna nini, wakagundua kuwa wanafunzi kwenye darasa lao wanawashangilia huku wakipiga na makofi, yani kwa mara ya kwanza Angel alijihisi aibu sana kiasi kwamba hakuweza kuingia darasani na kutoka nje kabisa ambapo Samir nae alitoka na kuelekea alikokuwa akienda.
Baada ya muda kidogo ndio Angel akaingia darasani, alipokaa tu rafiki yake Yusra alianza kumcheka na kumwambia,
“Naona shoga yangu umepatikana, sio kutazamana kule na Samir jamani mmmh!! Unampenda eeeh!”
“Aaaah mambo gani hayo Yusra?”
“Sio mambo gani, unajua saivi sisi ni wakibwa, kidato cha nne sio mchezo yani, unamtaka?”
“Mimi nataka kusoma”
“Huna lolote, unamuogopa mama yako tu ila unamtaka”
Angel alitabasamu tu bila ya kusema chochote kile.


 
SEHEMU YA 10


Muda wa kutoka ulipofika, Samir alijikaza na kumsogelea Angel ambapo alimuomba namba yake ya simu nae Angel hakusita kwani muda huo huo alimpa Samir namba yake huku akiagana nae na kwenda kuwafuata wadogo zake ambapo aliondoka nao hadi nyumbani kwao.
Walipofika nyumbani basi Angel akafanya kama kawaida kwani aliwaambia wadogo zake kuwa wapike chai na wale tena mkate ila Erick aligoma,
“Jamani dada kwanini lakini unafanya hivi? Tupikie chakula tule, kumbuka ahadi yako ya jana”
“Kheee nyie watoto jamani, basi ngoja niende chumbani kubadili nguo ndio nianze kupika”
Basi Angel akaelekea chumbani kwake, ila alichukua simu yake na kuiwasha, muda huo huo ukaingia ujumbe ukisema,
“Angel, ni Samir hapa. Vipi ushafika kwenu? Nimekumiss teyari”
Angel akatabasamu na kumjibu Samir, muda huo akajikuta ameanza kuwasiliana na Samir na kusahau ahadi yake kwa wadogo zake kuwa anaenda kuwapikia chakula.
Alikaa chumbani hadi wadogo zake wakamfata dada yao,
“Jamani dada Angel mbona unatufanyia hivi!! Njaa zinauma”
“Ila na nyie mmezidi jamani, kumbukeni mimi sio msichana wa kazi humu ndani eeeh! Ngoja nimpigie mama”
Basi Angel alimpigia mama yao ambapo muda huo huo alipokea, basi Angel alimsalimia na kuanza kuongea nae,
“Kwakweli mama kuna umuhimu wa kuwa na mdada wa kazi humu ndani, wanao tunateseka sana, hebu ona tumetoka shuleni tumechoka na chakula hamna”
“Ushaanza uvivu wako Angel”
“Sio uvivu mama ila nimesema ukweli, tunachoka sana na masomo”
“Haya, hilo swala la mdada wa kazi nalifanyia kazi. Nipe Erica niongee nae kwanza”
Basi Angel alimpa Erica simu ambapo aliongea na mama yake ila Angel alimyang’anya simu na kusema imeisha chaji, basi akakata ile simu. Si kweli kwamba iliisha chaji ila alitaka kuwasiliana na Samir tu kwa njia ya ujumbe, hadi wadogo zake wakaamua tena kwenda kujipikia wenyewe.
Yani Angel kwa muda huo alikuwa na simu tu basi Samir akamuuliza,
“Simu huwa unaiweka wapi ukija shule?”
“Huwa naiacha nyumbani”
“Naomba njoo nayo?”
“Mmmh, nitaitumiaje shule sasa?”
“Njoo nayo ili tuwe tunawasiliana hata darasani, kesho njoo nayo”
Yani Angel alijikuta akishindwa kukataa kabisa, kwani alihisi asilimia kubwa ya mawazo kwa muda huo yalikuwa juu ya Samir tu.


 
SEHEMU YA 11


Hata kuamka kula hakujishughulisha kula chakula kilichopikwa na wadogo zake, bali alikunywa chai na mkate na kwenda kulala ila aliwasiliana na Samir hadi analala.
Kulipokucha walijiandaa na kwenda shule, ila siku hiyo darasani alikuwa na simu tu chini ya dawati na alikuwa akijibu jumbe za Samir halafu waliangaliana na kutabasamu.
Kuna muda mwalimu alikuwepo darasani ila Angel aliinama na kutuma ujumbe kwa Samir, mwalimu akamsogelea Angel na kumuuliza,
“Nini unafanya chini ya dawati huko?”
“Hamna kitu mwalimu”
Basi mwalimu akapenyeza mkono wake chini ya dawati la Angel na kukuta ile simu ambayo Angel aliitumia kutuma jumbe kwa Samir.


Kuna muda mwalimu alikuwepo darasani ila Angel aliinama na kutuma ujumbe kwa Samir, mwalimu akamsogelea Angel na kumuuliza,
“Nini unafanya chini ya dawati huko?”
“Hamna kitu mwalimu”
Basi mwalimu akapenyeza mkono wake chini ya dawati la Angel na kukuta ile simu ambayo Angel aliitumia kutuma jumbe kwa Samir.
Mwalimu aliichukua ile simu na kumwambia Angel,
“Baada ya kipindi uje ofisini kwangu”
Kwakweli Angel hakuwa na raha kabisa kiasi kwamba alichofundish mwalimu kwa muda huo hakukielewa kabisa, basi mwalimu alifundisha na kumaliza kisha alimuangalia Angel na kumwambia kuwa afatane nae, yani Angel aliinuka huku akiwa hana amani katika moyo wake.
Moja kwa moja walienda kwa yule mwalimu, alikuwa ni mwalimu Harun ambaye alihusika pia na mambo ya nidhamu pale shuleni, walivyofika ofisini alimwambia Angel apige magoti ambapo Angel alifanya hivyo kisha akamwambia,
“Umeanza lini tabia ya kuja na simu shuleni Angel? Mama yako anatambua hili?”
“Nisamehe mwalimu”
“Hivi unatambua kuwa hii ni kesi kubwa sana? Nikiipeleka kwenye uongozi wa shule, jua kabisa huna shule na upo kidato cha nne sasa utakimbilia wapi? Na nikipeleka kwa mama yako, nadhani siku hiyo utataja jina lako la kuzaliwa, kwanini umefanya hivi Angel? Kwanza ulikuwa ukiwasiliana na nani muda wa kipindi?”
“Nisamehe mwalimu”
“Msamaha wangu ni wewe kumtaja uliyekuwa ukiwasiliana nae darasani muda wa kipindi”
“Hakuna mtu mwalimu”
“Kwahiyo unadhani nimegundua vipi kama ulikuwa na simu? Wewe mtoto ni mjinga sana, yani unafanya ujinga kama huu shuleni halafu unasemaje? Hivi hujihurumii Angel, upo kidato cha nne na unatakiwa kuwa makini sana, kuzingatia masomo yako ili ufanye vizuri kwenye mtihani wa taifa, ila wewe bila aibu unawasiliana na watu darasani. Ila kwavile umekataa kumtaja uliyekuwa ukiwasiliana nae, basi utapiga magoti hapo hadi kesho”
Angel hakuona tatizo la yeye kupiga magoti ila hakuona vyema kumtaja Samir ambaye alikuwa ni mgeni katika shule hiyo, alimuhurumia iwapo angefukuzwa shule, ingekuwaje? Alijikuta akipiga magoti kwa muda mrefu sana hadi akaanza kulia ili mwalimu amsamehe ila mwalimu alikataa na kumtaka ataje aliyekuwa akiwasiliana nae, mara alishangaa kuona mlango wa ofisi ile ukifunguliwa na aliyeingia alikuwa Samir, kwakweli Angel alishtuka na kumuangalia Samir kuwa alitaka kufanya nini, ila alimuona Samir akimfata mwalimu na kumwambia,
“Ni mimi ndiye nilikuwa nikiwasiliana na Angel muda wa kipindi darasani”
“Hivi una akili wewe kijana? Nadhani ndiomana huna shule unayodumu wewe mjinga, haya Angel inuka hapo na uondoke, mimi nitashughulika na huyu mjinga”
Angel akawa akishangaa shangaa tu, yule mwalimu akasema kwa ukali,
“Inuka Angel, toka hapa ofisini ila hii simu nitabaki nayo, mimi nitashughulika na huyu kidume sasa”
Angel aliinuka na kutoka ila alijihisi vibaya sana, nje ya ofisi kulikuwa na wadogo zake, ndio akagundua kuwa muda wa kutoka ulifika na wadogo zake walienda kumuulizia na kuambiwa kuwa yupo huko kwahiyo walimfata basi alitoka nao na kuondoka nao.


 
SEHEMU YA 12


Walivyofika nyumbani cha kwanza kabisa walimuuliza,
“Kwani dada ilikuwaje leo?”
“Aaaah achaneni na habari hizo”
“Halafu mbona macho yako yamevimba?”
“Nimewaambia achaneni na hizo habari, ngoja nikapumzike”
Erick na Erica walitazamana maana dada yao alionekana kuwa alilia na ilionyesha kuwa hana raha maana hata habari ya kupika ili wale hakuwa nayo, ikabidi tu wenyewe wajipangie majukumu na kwenda kubadilisha nguo kwanza halafu kuanza kupika,
“Kwahiyo Erick tupike kwanza ndio tukafue nguo, eti eeeh!!”
“Tutafua hata kesho bhana, kumbuka kesho ndio Ijumaa”
Sawa hakuna tatizo”
Basi wakaenda kupika pamoja huku wakielekezana cha kupika na kufurahi tu wakati wanapika, mara simu ya mezani ilikuwa ikiita, moja kwa moja Erica alihisi ni mama yao tu kwahiyo aliikimbilia ile simu na kuipokea kisha akaanza kuongea nayo,
“Mama shikamoo, tumekumiss”
“Marahaba mwanangu kipenzi, nimewamiss pia. Mnaendeleaje hapo nyumbani lakini?”
“Salama kabisa mama, ila dada Angel hayupo salama maana leo tulivyotoka darasani tukaenda kumuangalia kwenye darasa lao ili tuondoke pamoja ila hatukumkuta wala nini, na ndio mkaka mmoja akatuambia kuwa dada yupo ofisini kwa mwalimu wa nidhamu, basi tuliongozana nae na yeye aliingia baada ya muda dada alitoka ila macho yake yalikuwa mekundu sana”
“Jamani Angel, kafanyaje tena? Mmemuuliza dada yenu?”
“Tumemuuliza ila kakataa kutujibu na kasema anaenda kulala, hapa tunahangaika na kupika, kwakweli mama kuna kila sababu ya kupata msaidizi hapa nyumbani”
“Mmmh Erica unaongea sana wewe, kama redio jamani! Huyo msichana wa kazi nitakuja nae, ila nahitaji kuongea na Angel, nimejaribu kupiga simu yake haipatikanbi, hebu kaniitie”
“Sawa mama”
Erica aliweka simu pembeni na kwenda chumbani kwa Angel kumuita,
“Dada Angel, mama amepiga simu anataka kuongea na wewe”
“Basi ushamwambia hivyo!!”
“Ndio, nimemwambia kuwa hatukukukuta darasani bali ofisini na macho yako yanaonyesha kuwa umelia sana”
“Kione vile, umbea tu”
Angel aliinuka na kumsukuma mdogo wake kichwa, kisha akatoka nje kuelekea kwenye simu ambayo mama yake alipiga, akamsalimia na kuanza kuongea nae,
“Kwanini hupatikani hewani?”
“Sijawasha simu mama”
“Kwanini wamekukuta ofisini? Na kwanini macho yako yalionyesha kama ulilia?”
“Mama, macho yananiuma leo na nilienda ofisini kuchukua dawa, yani mama unamsikiliza Erica? Huyu mtoto ni muongo”
“Nitajua tu ukweli wote, bado nasisitiza kuwa kesho narudi. Sasa amka ule chakula, kama mnaona uvivu kupika, basi muagize dereva akawanunulie chakula ila sio kuwaacha wadogo zako na njaa”
“Sawa mama”
Angel alimaliza kuongea na mama yake na kukata simu kisha akamuita Erica na kuanza kumsema,
“Hivi wewe katoto ukoje? Mbona mmbea hivyo? Haya umepata faida gani sasa kumwambia mama? Ipo siku nitakupiga hadi ushangae”
Erick akatokea mbele yao na kusema,
“Kwenye swala la kumpiga Erica hapo usahau dada, sababu siwezi kuacha umpige Erica nakuangalia”
Basi Angel akawasonya na kuondoka zake, maana Angel hakupenda kubishana sana na Erick maana alikuwa ni mrefu kushinda wao kwahiyo mtu pekee aliyemuweza ni Erica tu sababu hakuwa mrefu sana.
Basi Erick na Erica walienda kuendelea na kupika.


 
SEHEMU YA 13

Ijumaa hiyo waliamka asubuhi na kujiandaa kwenda shuleni ila Angel alikuwa na mawazo sana kwani hakujua ni adhabu gani ambayo Samir amepewa baada ya kusema ukweli kuwa ni yeye ndio aliongea nae.
Basi walifika shuleni na moja kwa moja Angel alienda darasani, ila alishangaa muda mfupi badae Samir nae aliingia darasani na kwenda kukaa tu akiendelea na masomo kanakwamba hakuna kitu kilichotokea, kwakweli Angel alitamani sana kujua kuwa imekuwaje ila hakujua wala nini.
Basi masomo yaliendelea hadi muda wa kutoka darasani wala Samir hakuonekana kujali kitu chochote, basi Angel alitoka ila muda huu aliitwa na mwalimu yule wa nidhamu na kwenda nae ofisini kisha mwalimu akamwambia,
“Angel, hili ni onyo la mwisho kwako, kwakweli hii kitu ikijirudia utaona shule ni chungu hii, najua na mama yako angejua basi hata nyumbani kwenu ungepaona pachungu, nakurudishia hii simu ila sitaki kusikia ukiwasiliana tena na Samir, zingatia masomo yako. Tumeelewana?”
“Ndio nimekuelewa mwalimu, asante kwa kunisamehe”
Kisha mwalimu yule alimkabidhi Angel ile simu ambapo Angel alitoka na kuwafuata wadogo zake ambao walikuwa wakimsubiri na kurudi nao nyumbani.
Walipofika kwao siku hii ilikuwa ni ya tofauti sana kwani walikuta mama yao na baba yao wamerudi, walifurahi sana na kuna mdada walitambulishwa pale kuwa ndio atakuwa msaidizi wao wa kazi pale nyumbani,
“Wanangu wapenzi, huyu dada anaitwa Vaileth, atakuwa akitusaidia kazi za hapa na pale hapa ndani, naamini atawalea katika maadili niyatakayo”
Angel alifurahi sana kusikia hili kwani ndio jambo ambalo alikuwa akililia kwa muda mrefu sana,basi alimwambia mama yake,
“Asante sana mama”
“Ndio nimeamua kuwafurahisha wanangu”
Basi wakainuka ili waende kubadilisha sare zao za shule, ila mama yao alimuita Angel na kumwambia
“Angel, lete simu yako”
Angel akaitikia na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, kisha akaitoa ile simu toka kwenye begi lake la shule na alijua moja kwa moja mama yake anataka akaikague, basi akafuta kila kitu ambacho kiliendelea kwenye simu yake halafu akampelekea mama yake ile simu akitumai baada ya muda mchache angemrudishia ila mama yake hakufanya hivyo wala nini.



 
SEHEMU YA 14


Muda wa kula chakula cha jioni ulipofika, wote walikaa pamoja na kula huku wakifurahi ila baba yao alisema amechoka sana hivyo akawahi kwenda kulala kwahiyo sebleni alibaki mama na watoto wake akaanza kuongea nao,
“Eeeeh niambieni kwanza maisha ya kuishi wenyewe? Najua haijawahi kutokea ila kipindi hiki ilibidi tu wanangu kutokana na majukumu ya hapa na pale, eeeh niambieni”
Walikaa kimya kidogo basi mama yao akaanza,
“Niambie mwanangu Erica, maisha ya kuishi wenyewe uliyaonaje?”
“Mmmh yalikuwa magumu mama”
Erick nae akadakia,
“Yani mama, usiku tunalala kwa kunywa chai na mikate jamani!”
“Kheee Angel, kweli ulikuwa unawalaza wadogo zako kwa chai na mikate!”
“Mmmh mama jamani, mimi ni dada yao ndio ila sio kusema kuwa kila jukumu nitaweza maana mimi pia bado mdogo, hebu angalia niende shule, nirudi kupika, niwafulie, nilikuwa nachoka mama”
“Mmmh dada jamani, umetufulia mara moja tu”
“Na wewe Erick, kwani kufua hamjui hadi mummpe hilo jukumu dada yenu?”
“Hapana mama, alisema mwenyewe”
Mara simu ya Angel ilianza kuita pale, basi mama yake akaangalia na kukuta jina la mpigaji limetokea Hanifa, akampa Angel na kumwambia aongee nayo, basi Angel akaipokea na kutaka kuondoka pale ili akaongee nayo ila mama yake alimshika mkono na kumwambia,
“Kaa hapo uongee nayo”
Basi Angel hakuwa na namna zaidi ya kuongea na ile simu mbele ya mama yake,
“Jamani Angel, nimekusubiri leo hujatokea kwanini jamani!”
“Tulichelewa kutoka shule”
“Basi naomba kesho uje, nipo chini ya miguu yako”
“Sawa”
Angel akakata ile simu kisha mama yake akamuuliza,
“Ulikuwa ukiongea nae nini?”
“Hanifa hakuja shule leo, alikuwa anauliza tu kama tuliwahi kutoka au la!”
“Mbona mwishoni umemjibu sawa!”
“Kaniambia Jumatatu nisisahau madaftari nyumbani ili apitie tulichosoma”
“Kwahiyo kuna kipindi huwa unasahau daftari au kitu gani?”
“Hapana mama, ila kuna masomo huwa sitembei na daftari zake mara kwa mara”
“Angel, utaona mama yako nakufatilia sana ila nina maana kubwa sana, badae utashukuru na kuona ni vyema nilikuwa nakufatilia, naielewa dunia hii ilivyoharibika, yani wanaume wakiona mtoto mzuri kama wewe lazima mate yawadondoke, sitaki mjinga yoyote aharibu maisha yako”
Angel akawa anamuangalia tu mama yake ingawa kiukweli hakupenda vile ambavyo mama yake alikuwa akimchunga, basi mama yao aliwaangalia Erick na Erica na kuwaambia,
“Ninavyomchunga dada yanu ni sawa na nyie, kwanza nadhani sharia za nyumbani kwangu mnazifahamu, sitaki marafiki wa ajabu hapa nyumbani kwangu, yani kabla hujawa na rafiki ni lazima apitie kwangu nimkague kwanza na nimuhoji maswali, kama nitaridhika nae basi atakuwa rafiki yako, vinginevyo sitaki marafiki hapa kwangu. Nahitaji nyie ndio muwe marafiki, jambo likikutaziza, mwambie mwanafamilia hapa akusaidie, mpo watatu mnatosha kabisa”
Erica akauliza,
“Kwahiyo mama na wakina Junior je?”
“Sasa wale ni marafiki? Hebu kuweni na akili, wale ni ndugu zenu, yani hapa ni ndugu tu ujinga ujinga wa kuharibu wanangu siutaki, Erica sitaki marafiki wa ajabu ajabu, halafu sitaki kusikia kuna wanaume huko wanakuchanganya akili, Erick uwe mlinzi wa dada yako, nawe Erick sitaki marafiki wa ajabu, na maswala ya wanawake sitaki kuyasikia, kwahiyo Erica utakuwa mlinzi wa kaka yako. Halafu nyie wawili mtamlinda dada yenu Angel, yani sitaki kusikia ujinga wa aina yoyote ile. Nadhani mnanielewa!”
“Tumekuelewa mama”
Walijibu kwa pamoja kisha mama yao akawaruhusu kwenda kulala.


 
SEHEMU YA 15

Kiukweli Angel alienda kulala akiwa na mawazo sana, alijikuta akimfikiria sana Samir na akijiuliza maswali mengi sana,
“Hivi mfano Samir akapiga na simu yupo nayo mama itakuwaje? Mmmh hivi mama nae alikuwa anafanywa hivi kama anavyotufanyia sisi jamani!”
Basi akajibembeleza pale kitandani na kulala, ila siku hiyo aliota yupo na Samir na wapo sehemu nzuri sana wakifurahi huku Samir akimwambia kuwa anampenda sana, yani ile ilikuwa ni ndoto ya furaha sana kwa Angel na kumfanya akiamka huku akitabasamu na kujiuliza,
“Hivi ni kweli Samir ananipenda? Mbona nimewasiliana nae siku zote hajaniambia kuwa ananipenda? Au alitaka tu kuwa rafiki yangu! Na mbona toka lile sekeseke la mimi kukamatwa na simu hajaniongelesha tena? Mmmh hebu mawazo ya kupendwa na Samir yatoke kwenye kichwa change”
Kisha akaendelea kulala mpaka kulipokucha.

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, na siku hii baba yao aliwaambia wajiandae ili waende kwenye matembezi kwani alitamani sana kwenda kwenye matembezi na watoto wake ukizingatia yeye na mkewe walikuwa safarini, kwahiyo walijiandaa na kutoka pale kwao, mtu pekee waliyemuacha nyumbani alikuwa ni Vaileth, na walimuacha sababu hakuonekana kupenda kutembea.
Basi wakiwa kwenye gari, Angel akauliza,
“Baba, unatupeleka wapi kwani?”
“Tunaenda ufukweni, yani huku mama yenu huwa anapapenda sana ila ni muda mrefu sijawahi kuja nae”
Mama yao akauliza,
“Kheee kumbe tunaenda ufukweni?”
“Ndio, tena ufukwe ule ambao wewe huwa unaupenda sana”
Mama yao alionekana kutabasamu kiasi, halafu gari lilienda hadi ufukweni ambapo walishuka na kuchagua sehemu moja na kukaa kama familia, basi Angel akawaomba wazazi wake,
“Naomba niende nikachezee chezee maji baba”
Na wadogo zake nao wakaomba hivyo hivyo basi baba yao akawaruhusu ila mama yao alitaka kukataa swala lile mpaka baba yao akamwambia,
“Acha bhana mke wangu watoto wafurahi leo, ujue tumetaka kuwafurahisha”
“Sawa, hakuna shida”
Basi Angel na wadogo zake wakainuka na kwenda kuanza kucheza cheza karibu na maji, mule kwenye maji aliona watu walioonyesha wapo karibu yani ni wapenzi wakimwagiana maji na kutoka nje mara wakirushiana mchanga, basi Angel alijikuta akiwaangalia kwa muda mrefu sana hadi mdogo wake Erick alimshtua,
“Mmmh dada, mbona unawaangalia sana wale?”
“Nawaangalia wanavyopendana, inaonekana wanapendana sana”
“Kama baba na mama”
Basi Erica akasema,
“Weee baba na mama wanapendana zaidi jamani, sijui enzi za ujana wao walikuwaje, na mimi nikija kuolewa basi natamani nimpate mume mwenye upendo kama baba”
Basi Erick akamuuliza,
“Kwahiyo unataka mumeo aitwe Erick? Maana Erick ni jina la baba!”
“Mmmh wewe nawe, sina maana hiyo ila nimesema mwenye upendo”
“Na mimi nikioa nataka nipate mke mwenye upendo kama mama”
“Sasa ulinipinga nini mimi mwanzoni? Kwahiyo unataka mkeo aitwe Erica? Maana Erica ni jina la mama”
Basi Angel akacheka na kusema,
“Nyie watoto msinichekeshe jamani, ila twendeni tuwaulize baba na mama kwanini mimi waliniita Angel halafu nyie mkawa Erick na Erica ambayo ni majina yao? Kwanini?”
Basi wakatoka eneo lile na kurudi tena kwa wazazi wao ambapo Angel ndio alianza maswali kwa wazazi wao,
“Eti mama kwanini mimi mliniita Angel halafu hawa mkawapa majina yenu?”
Mama yao alicheka na kumuuliza,
“Kwahiyo nawe ulitaka majina yetu?”
“Ndio, maana mimi ndio mtoto wa kwanza, nilitakiwa niitwe Erica”
Baba yao akacheka sana na kuanza kumjibu Angel.
“Wewe umeitwa Angel sababu ulikuja kwenye maisha yetu na kubadili kabisa mfumo mzima wa maisha yetu yani ulikuwa kama malaika kwetu ndiomana tukakuita Angel, sawa mama yangu eeeh!”
Angel alitabasamu kusikia vile na alifurahi sana kwani aliona kuwa kapewa heshima kubwa sana, kisha Erica nae akamuuliza baba yao,
“Na sisi je baba?”
“Kwani na nyie hamjihisi furaha kupata majina ya wazazi wenu? Kipindi tunakuwa watu wengi walidhani mimi na mama yenu ni mapacha, ndiomana tulipowapata ninyi tukaona tuwaite majina yetu, kwahiyo na nyie mnathamani kubwa sana kwetu ndiomana tumewapa majina yetu”
Erick na Erica walitazamana huku wakitabasamu na kumuangalia dada yao ambapo nae alitabasamu tu ila kwa muda huo mama yao hata hakuongea chochote kile, kisha baba yao akawaambia warudi kwenye gari ili waende mahali kula chakula cha jioni, nao walifanya hivyo ambapo waliingia kwenye gari na moja kwa moja baba yao alienda hadi hotelini na kila mmoja kuagiza chakula anachokitaka na kuanza kula ila muda kidogo Angel akaomba aende maliwatoni ambapo mama yake alimruhusu.



 
loviesundy jonta FrankMakeps Jogoo wa Shamba II dluv mwakiri Tysher 100miles bubblymolly Nuhu39 subadesubking sherberry mireille ukhty khadija jKingSenior kukumsela Mtende Litro bioto yona raphael mkulima2 kaswiza90 kisukari uhaale benybeny fred tarimo Empiree Atropine bugza msokela Tieli Baba Moh Secret Man aretasludovick MR KUO Loveleads Bigjahman Mine eyes Depal lameckkawawa Don Clericuzio nipo2 Lengutee Shupavu nyakisese song 16 femalepilot APOSTLE Babu la Bara Mr no kizeze seeker of knowledge mbongopopo Lewis18 Smart911 G.T.L ndyagulu katui helment Gonangaga Mr Cu MWANAKA havanna Fernandes Rodri tumebarikiwa The Hurricane Mdex MADAXWEYNE ASA 1 Loi Ter gwankaja pwiro Kalicharan Ferruccio Lamborghini pocknut mpasta Behaviourist jonoma paul samky assey binti mapozi Sangomwile cutepie daqway kilyabanu mkono Mogan Mogan bombei_safaya red apple Interlacustrine Region financial services Duduvwili chiqutitta Gobole Mkulima Jr kalisheshe msengho kathago dumjeuri yna2 Yabwalate Makiseo kawoli mmbaga lambago iddhassan Kilongawima uniq Sweta LA Tanzania goroko77 aggyd Robert saimon moshi mawazo haba mahondaw nestorymange ADK LWENYI Smt016 Queen M Zeeyonce Poor Brain Active Qa people dokta lu TheOneNation makedonia dan oseko mjery Tee Mammie spleen Usher raymond Black hermit qinglong Captain Stressor kuchikubwa Bayser17 samua angetege cute nee Secret genius ntera Restless MastaKiraka Kigera Kwetu dronedrake dudus unque bin unuq kibambrasi adri Kilawo Jovet izzo mangonifera indica Umaskinikerosana njiroo ze future Econometrician zacha mrsleo Dreadnought adden becknature sophiere Rural Swagga Chumchang Changchum Authority Macrean jr lulu za uru mludego Tanayzer pokemon Mweweso Mhariri Abuu Dharr
 
SEHEMU YA 16

Angel akiwa anataka kuingia maliwatoni akashangaa akishikwa bega, kugeuka akashangaa kumuona James yule ndugu wa Hanifa na kuanza kusalimiana nae,
“Umenikumbuka Angel?”
“Mmmh nakukumbuka ndio ila jina lako limenitoka”
“Mimi ni James, yule ndugu wa Hanifa, nimefurahi sana kukuona. Tafadhari naomba namba yako ya simu”
Angel akafikiria kidogo na kushindwa kujibu kwani simu ilishachukuliwa na mama yake, basi akamwambia,
“Mimi sina simu”
“Mmmh mbona Hanifa uliwasiliana nae kwenye simu?”
“Ndio ila imeharibika”
“Usinifanyie hivyo Angel”
Basi James akamshika Angel mkono, kwakweli Angel alishtuka kidogo kwani hakuwa na mazoea ya kushikana mikono na mwanaume ambaye si ndugu yake kama hivyo, mara mama yake akatokea na Angel kuutoa mkono wake kwa James huku akiwa na wasiwasi, kisha mama yake akamuuliza,
“Wewe Angel, ndio chooni hapo?”
Basi James akataka kuondoka ila mama Angel alimzuia na kumuuliza Angel,
“Niambie huyu ni nani?”
“Huyu ni ndugu wa Hanifa”
“Aaaah kumbe mnapigiana simu na Hanifa sababu ya huyu!!”
“Hapana mama”
Kisha mama Angel alimuangalia James na kumuuliza,
“Unaitwa nani na ulikuwa na agenda gani na Angel?”
“Naitwa James, nilikuwa namsalimia tu”
Huyu mama alitema mate pembeni na kumwambia James,
“Ondoka mbele ya macho yangu, unanichefua. Hivi wewe Angel akili yako ikoje hiyo, mbona kuwaza ujinga kiasi hiko! Huyu James atakupa nini ambacho mimi na baba yako tumeshindwa kukupatia? Kwakweli sijapenda, haya nenda chooni nakungoja mlangoni”
Basi Angel akaingia chooni na baada ya muda alitoka na kuondoka na mama yake ambapo mama yake alikuwa akimlalamikia njia yote,
“Sasa nisikilize kwa makini, sitaki kusikia habari za James, sitaki kusikia kuhusu Hanifa sitaki kitu chochote. Mbona unataka kunitia aibu jamani Angel loh!”
Walirudi mezani na mama yao aliwataka kufunga chakula na kwenda kula nyumbani, sema sababu mumewe alikuwa akimsikiliza sana kwahiyo alikubali na muda huo huo kuamua kuondoka pale hotelini.
 
Back
Top Bottom