Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 53

Kesho yake kulipokucha kama kawaida waliondoka na kenda shuleni ila leo baba yao hakuwepo kwahiyo mama yao alibakia mwenyewe huku akiendelea kuwa na mawazo kuhusu Angel,baada ya watoto wake kuondoka sasa aliamua kuongea na Vaileth ili amwambie vile anavyojihisi kuhusu Angel,
“Unajua huyu mwanangu simuelewi kabisa kiasi kwamba hata cha kufanya sijui yani”
“Nakushauri dada uende shuleni kwakina Angel, muite huyo kijana na Angel na umuulize mbele ya mwalimu wao wa nidhamu”
“Eti eeeh! Ngoja nijiandae sasa hivi niende”
Basi mama Angel alienda kujiandaa huku akiwa na mawazo sana juu ya binti yake, baada ya hapo aliondoka na kuelekea shuleni kwakina Angel.
Alifika shuleni na kuongea na mwalimu wa taaluma maana wa nidhamu hakumkuta ambapo aliomba aitiwe Angel na Samir, naye mwalimu hakusita bali alifanya hivyo.
Angel na Samir walipofika, basi mama Angel alianza kumfokea Samir na kumuuliza,
“Hivi kwanini unamsumbua mwanangu wewe kijana?”
Samir alimjibu huyu mama kwa ujasiri kabisa tena bila hata na uoga,
“Nampenda sana Angel”
Huyu mama alimuangalia na kumnasa kibao kwa hasira.


Alifika shuleni na kuongea na mwalimu wa taaluma maana wa nidhamu hakumkuta ambapo aliomba aitiwe Angel na Samir, naye mwalimu hakusita bali alifanya hivyo.
Angel na Samir walipofika, basi mama Angel alianza kumfokea Samir na kumuuliza,
“Hivi kwanini unamsumbua mwanangu wewe kijana?”
Samir alimjibu huyu mama kwa ujasiri kabisa tena bila hata na uoga,
“Nampenda sana Angel”
Huyu mama alimuangalia na kumnasa kibao kwa hasira.
Muda ule mwalimu wa nidhamu nae akafika kwahiyo alimkuta mama Angel akiwa na Angel pamoja na Samir, kwahiyo na yeye alishuhudia kile kibao ambacho mama Angel alimnasa Samir ikabidi asogee karibu na kuuliza,
“Kulikoni mama?”
“Kulikoni nini? Yani mnashindwa kuthibiti wanafunzi wenu? Si mapenzi shule yamekatazwa? Mnawezaje kuruhusu mambo kama haya yatokee kwenye shule yenu? Yani mtoto huyu anajibu kwa ujasiri na kujiamini kabisa kuwa nampenda sana Angel, ujinga ujinga tu”
“Basi mama, tulia tuzungumze”
“Sina cha kutulia, wewe Angel nenda kabebe begi lako tunaenda nyumbani sasa”
Angel aliondoka na kwenda kuchukua begi lake, na mama yake alibaki pale akiwa na jazba sana yani hakutaka kusikia hili wala lile kwa wakati huo.
Angel aliporudi na begi lake alimshika mkono na kutoka nae hapo shuleni na moja kwa moja alielekea nae nyumbani kwao.
Walipofika akaanza kuongea na bintiyake,
“Angel tafadhali mwanangu, najua upo kwenye darasa baya ila naomba nikuhamishe shule, yule kijana hakutakii mema mwanangu, anataka kukuharibia masomo yako tu”
“Sawa mama”
“Haya,nenda chumbani”
Halafu muda huo huo mama Angel alijiandaa na kutoka kwani kuna shule tayari alishaifikiria kwenye akili yake akaona ndio itamfaa mwanae kwa kipindi hiko.
 
SEHEMU YA 54


Angel alitulia chumbani kwake kisha Vaileth alimfata na kuanza kuongea nae,
“Kwani Angel wewe unajihisi vipi kuhusu huyo mkaka?”
“Hata sijui dada, yani sijui kwakeli ila akinisogelea nasisimka sana”
“Ila Angel majuto ni mjukuu, mzazi huwa anaona mengi sana. Huwezi jua ni kwanini anakukataza kuwa karibu na huyo kijana. Je upo tayari kuhama shule? Yani upo tayari kwenda shule atakayokutafutia mama yako?”
“Nipo tayari dada, nahitaji kusoma kwakweli, ila huyu Samir anaichanganya akili yangu kweli yani, sema nahitaji kusoma kama mama. Halafu ile shule walinizoea sana, yani shule yetu kuna mambo yanayaachia mno, ikiwezekana hata Erica wamuhamishe pale, yani shule ile wanafunzi kuwa na mahusiano darasani ni kawaida, na wakaka wote wamekuwa wakinifatilia ila wamenikosa, sasa namshangaa huyu Samir jamani yani nashindwa hata kumwambia sitaki”
“Sasa hapo umepata picha kamili, itakuwa Samir anapata ushawishi toka kwa wanafunzi wengine wa darasani kwenu,kuwa makini sana, anapokutafutia mama yako ukasome na ukamilishe masomo yako vizuri, usimtese mama yako na kumfanya aimbe wimbo mmoja kila siku, hebu muhurumie jamani”
“Nimekuelewa dada”
“Nashukuru kwa kunielewa, nikupe chakula ule?”
“Hapana, kwasasa sina njaa”
Basi muda huo huo alifika mama yake mkubwa yani mama Junior na kumshangaa Angel kwa kutokuwa shule,
“Vipi wewe?Muda huu ulitakiwa kuwa shuleni!”
“Ni kweli mamkubwa ila kuna mambo machache tu yamekwamisha”
“Mambo gani?”
“Kwanzambona Junior toka Jumatatu haji shuleni?”
“Kwakweli Junior kawa donda sugu, jamani nyie watoto tunawazaa tu ili tusionekane wagumba ila mnachotufanya wazazi wenu, anajua Mungu tu”
“Vipi tena mamkubwa?”
“Yani junior atanitoa pumzi huyu mtoto, nilikuwa hapa nikaondoka juu juu eti Junior kapiga mtoto wa mtu na yupo polisi, yani nimechanganyikiwa, kufika nyumbani ili niulize vizuri hicho kituo cha polisi nikapigiwa simu kuwa nitume laki moja ili junior aachiwe halafu Junior nae anaongea kama yupo kwenye wakati mgumu, jamani angalia kulia kushoto nikatuma hiyo hela mbele ya mtoto yena. Khaaa leo ndio nakuja kujua ukweli kumbe Junior alimpachika mimba mtoto wa watu huko ndio alikuwa akihangaika kupata hela za kutoa hiyo mimba, yani nimechoka”
“Kheee pole mamkubwa, yani Junior ndio kafikia huko jamani!!”
“Ndio hivyo, kwa kifupi Junior hafai tena hafai kabisa, ni muongo hakuna mfano wake”
Kwa upande mwingine Angel alimuonea huruma mama yake mkubwa kwani alionekana kuongea kama mtu aliyechoka kabisa kwenye kumlea Junior.
 
SEHEMU YA 55


Mama Junior alisinzia pale pale, hata Angel alimsikitikia sana na kuona kweli mamake mkubwa ana matatizo, muda kidogo mama Angel alirudi na kumkuta dada yake pale nyumbani kwahiyo yeye ndio alimuamsha,
“Kheee dada,vipi tena?”
Dada yake akaamka huku akianza kulalamika,
“Jamani mtoto huyu atania mdogo wangu, mbona mimi sikumbuki katika kumsumbua mama yetu jamani?”
“Hivi dada nae watoto wake wanamsumbua kama wa kwetu?”
“Kheee hujui kwani? Yule mtoto wa kwanza wa dada, si aliolewa yule? Basi kaachika kisa kaenda kumzalia mumewe mtoto na mwanaume mwingine akiwa ndani ya ndoa”
“Kheee ile mimba kumbe haikuwa ya mumewe?”
“Ndio hivyo, hata sijui kuna laana gani kwetu jamani loh!”
“Eeeeh na wewe vipi Junior na huko polisi”
“Sina hamu na yule mtoto, kakomba laki moja yangu kumbe alienda kumtoa mdada wa watu mimba”
“Kheee kivipi dada?”
Basi dada yake akampa maelezo ambayo aliwapa wakina Angel, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kumpa pole dada yake,
“Kheee pole dada jamani!”
“Asante, kabinti kawatu kalizimia wakati kakitolewa mimba, yani jasho la meno limenitoka jamani! Sijalala jana yote,nimesema leo nije tu kwako nipumzishe mawazo kidogo”
“Kheee pole dada jamani, kwanini Junior anafanya hivi!! Na hako kabinti kanaendeleaje sasa?”
“Kanaendelea vizuri namshukuru Mungu, ila sina hamu kwakweli yani, sina hamu kabisa. Na wewe vipi huyu Angel? Naona leo hayupo shule?”
Basi alianza kumsimulia dadake mkasa mzima na jinsi alivyoenda shuleni kwao,
“Ila dada, nimepata bahati ya kupata shule karibu na kule unapoishi, nilishindwa tu kupita sababu akili yangu haikuwa sawa”
“Mmmmh umeogopa kuwakuta watoto wa wifi yako, ni wavivu hao hatari yani hadi kichefuchefu jamani. Yakila yanaacha vyombo hapo ila nimewanyoosha yani, nadhani hadi mama yao akirudi watakuwa wamenyooka”
“Ila vipi maadili yao?”
“Kheee watoto wana heshima wale sijapata kuona, unajua hawawezi kwenda popote bila kukwambia? Na hawawezi kuchelewa kurudi, hawana marafiki wa ajabu yani urafiki wao ni wenyewe na ndugu zao, wanasikitika sana tabia ya Junior na kumsihi asinitese, watoto nawapenda sababu ya heshima tu wale”
“Nilijua tu kwenye heshima hapo ni mia ya mia, maana mama yao ni mtu wa maadili sana. Unajua alipanga chumba chuo ila kwenye chumba chake huwezi kuta mwanaume waaina yoyote, kwkweli alikuwa akijiheshimu sana, na alikuwa akichagua marafiki wa kuwa nae karibu, nakumbuka ni yeye aliniambia kuhusu Dora kuwa hafai kuwa rafiki yangu, kwakweli Tumaini kwenye mambo ya maadili nampa mia ya mia”
“Sasa ndugu yangu kwanini tusimpe watoto wetu hawa atusaidie kidogo kuwalea”
Hapa mama Angel akapunguza sauti kidogo na kusema,
“Watoto wetu hata hawamuhusu hawa, tunampelekeaje? Kumbuka hatujazaa na kaka zake”
“Lakini anaishi na kaka yetu”
“Hata kama, ila ngoja akirudi nitajaribu kuongea nae, sijui yeye anawezaje kuwafundisha watoto maadili kiasi hiki halafu kashindwa kuwafundisha kazi jamani!!”
“Tatizo la yule anapenda sana kuwa na wasichana wa kazi ndiomana, hivi umesema shule uliyomtafutia Angel ipo karibu na kwangu?”
“Ndio, ile shule kubwa kule”
“Oooh sasa huyu Angel nimuone anafanya ujinga ajue ni halali yangu, yani nikimkuta hata kasimama na mwanaume, uwiiii atanikoma”
Mama Angel alicheka sana na kumwambia,
“Kakushinda Junior unayeishi nae ndani utamuweza Angel anayeenda kusoma tu”
Basi wakacheka tu na kuendelea kutiana moyo juu ya watoto wao.
 
SEHEMU YA 56


Leo Erica alitoka shule akiwa mwenyewe, basi Elly alimfata na kuona jinsi alivyopooza,
“Mbona upo hivyo?”
“Dada yangu nasikia kaondoka na mama kwa hasira sana nahisi anaenda kumuhamisha shule, na kaka yangu nae amehamishwa shule, mimi nabaki mpweke jamani kwenye shule hii”
“Usijali Erica, kuanzia sasa jua kuwa una kaka anayeitwa Elly maana nitakulinda, nitakusaidia na nitakuwa nawe bega kwa bega, usijali vchochote kile Erica, tuko pamoja dada yangu”
Erica akatabasamu na kufurahi sana kisha aliagana na Ellyn a kuelekea zake nyumbani.
Alipofika nyumbani alimkuta mama yake na mama yake mkubwa, aliwasalimia pale na akawaambia kuhusu Elly,
“Mama, nimepata kaka shuleni. Anaitwa Elly, kasema kuanzia sasa yeye ndio atakuwa kaka yangu na atanilinda na kunisaidia, kwahiyo mama usiwe na wasiwasi tena kuhusu mimi”
Halafu akaondoka na kuelekea chumbani kwake, ila mama yake mkubwa alicheka na kusema,
“Mmmh hawa watoto jamani, kitoto cha kidato cha kwanza hiki kinatuletea habari kuwa kimepata kaka shuleni, yasije kuwa mambo ya Samir badae”
“Dada jamani usimuongelee huyo kiumbe, kabisa maana hadi nahisi kichefuchefu nikimfikiria”
Basi dada yake alicheka tu na kuaga maana aliona kashapumzika vya kutosha sasa, kwahiyo mama Angel alitoka na kwenda kumsindikiza dada yake.

Wakati wapo kwenye kituo cha daladala, mama Angel alishangaa kushikwa bega na kugeuka ila akamuona mtu aliyehisi kumfahamu ambaye hakuonana nae kwa muda mrefu sana ila yule mtu alionekana kubadilika sana kiasi kwamba mama Angel hakukumbuka vizuri kuwa alionana wapi na huyo mtu, basi alianza kusalimiana na mtu huyo,
“Jamani za siku nyingi Erica? Naona unashangaa sana, unanikumbuka?”
“Nimekusahau ila sura yako sio ngeni kwenye macho yangu”
“Mimi John, ndugu wa Rahim”
Mama Angel alishtuka kidogo ila alijigeresha,
“Oooh John, za siku nyingi?”
“Salama tu, vipi mtoto wetu hajambo? Jamani ni siku nyingi sana, tunamuhitaji mtoto wetu ili atutambue baba zake”
“Oooh nipe mawasiliano yako, nitakutafuta tu”
Basi yule john alimpa namba zake ila mama Angel alijifanya amezishika kichwani huku akidai kuwa simu yake kaisahau nyumbani halafu namba zake hajazishika,
“Basi usijali nikifika nyumbani tu nitakupigia”
“Ila kama sio mbali na hapa, twende wote ili nipafahamu pia”
“Oooh ni mbali na hapa, tutawasiliana tu”
Kisha mama Angel akapanda daladala moja na dada yake ili yule mtu asielewe chochote.
Walipokuwa ndani ya daladala ikabidi dada yake amuulize vizuri,
“Vipi kwani kuhusu yule?”
“Ni historia ndefu ila yule ni ndugu wa Rahim, sitaki wamfahamu Angel kwasasa kwani akili ya mwanangu wataivuruga sana kama kaka yao alivyotaka kuvuruga ndoa yangu”
“Kheee pole sana”
Basi kufika mbele alishuka na kukodi bajaji ambayo ilimrudisha hadi nyumbani kwake, ila muda anashuka nyumbani kwake mumewe alimuona maana nae ndio alikuwa kafika na gari lake na kuingia nae ndani.
 
SEHEMU YA 57

Walivyofika ndani alimuuliza vizuri ili amueleze kuwa alitoka wapi na bajaji kwa muda huo, basi mama Angel alimueleza kila kitu na mtu waliyekutana nae hadi akapanda bajaji,
“Ila mke wangu, Angel ana haki ya kufahamu ndugu zake ujue? Maana kuna leo na kesho, je Angel akitembea na kaka yake itakuwaje? Maana huyo Rahim nadhani alikuwa na watoto kila kona”
“Nitakuwa makini kuhusu hilo, sitaruhusu Angel atembee na ndugu zake ila siwezi kuruhusu Angel awe karibu nao kwasasa, nasubiri afike chuo ndio nimwambie maana nitakuwa naichanganya akili yake kwasasa”
“Ila fikiria pia kuhusu hilo kuwa kuna muda ukweli utajulikana tu, ni kweli Angel namlea kama mwanangu na kamwe haitakuja kubadilika hilo, nitampenda Angel siku zote za maisha yangu, kabeba jina langu na ukooo wangu ila bado anahitaji kujua ukweli wa ndugu zake, hata kama walimtelekeza mwanzo ila kuna umuhimu way eye kutambua ukweli wote. Halafu itapendeza zaidi kama ukiamua kunizalia mtoto mwingine mke wangu”
“Mmmh jamani kwa umri huu kweli nianze kubeba mimba jamani? Wakina Erick wana miaka kumi na tatu ndio wapate mdogo wao kweli?”
“Ndio, kwani tatizo liko wapi, nizalie mtoto mwingine, nimetamani sana kuwa na mtoto mdogo ndani ya nyumba, nakumbuka kipindi kile wakati Angel mdogo nilikuwa nacheza nae na kufurahi nae, kipindi mapecha wangu wadogo nilikuwa nacheza nao na kufurahi nao ila kwasasa hata na wao wanaona aibu kuja kuongea nami mambo ya kijinga waliyokuwa wakiongea muda wote, nizalie mke wangu jamani”
“Kwa umri huu!”
“Kwani umri kitu gani jamani? Tutamlea mtoto wetu huyo, na uzuri wakina Angel wapo basi nao watatusaidia kumlea, ila natamani sana tuwe na katoto kadogo humu ndani”
“Ngoja, nitafikiria hilo swala. Nilijua nimemaliza kuzaa jamani, ila ngoja nitafikiria mume wangu”
“Sawa mke wangu fikiria kuhusu hilo, yani tambua nina uhitaji sana wa katoto kadogo mke wangu”
“Sawa, nimekuelewa”
Mama Angel aliona mumewe akimpa mawazo mengine sasa, akajifikiria jinsi atakavyokuwa na mimba tena, je ataweza kukimbizana na wakina Angel maana ndio kama masikio yao yaliwekwa pamba kwa kipindi hiko, ila kwa upande mwingine alifikiria na kuona ana haki ya kumfurahisha mume wake, ila akaona ni vyema akaongee na mama yake kwanza kuhusu hilo.
 
SEHEMU YA 58


Kesho yake watoto walijiandaa kwenda shule, na mama Angel alitoka na Angel na kumpeleka kwenye shule mpya aliyomtafutia, aliweza kupata nafasi kwa haraka maana alifahamiana na mwenye shule ambaye alikuwa ni rafiki wa mume wake, basi alimkabidhi Angel hapo huku yeye kuendelea na taratibu zingine, ambapo alirudi tena katika shule ya awali aliyokuwa akisoma Angel ili kufanya taratibu vizuri za uhamisho, nao walimu hawakukataa sababu hali halisi na wao waliiona kwa Angel pale shuleni.
Alipomaliza hayo, sasa aliamua kwenda kwa mama yake ili akamsalimie na akaongee nae kuhusu jambo aliloambiwa na mumewe. Alifika kwao na kumkuta mama yake na kumfurahia sana, mama yake hakuishi na yeyote kwa kipindi hiko zaidi ya msichana wa kazi tu ambaye alikuwa akimsaidia kazi za hapa na pale kwani yeye kidogo umri ulienda enda,basi alianza kuongea nae,
“Nilijua utaniletea wajukuu zangu jamani Erica, sasa mbona umekuja mwenyewe?”
“Nitawaleta tu mama, hata usijali”
“Juzi nilikuwa kwenye kile chumba ulichokuwa unalala, jamani miaka inaenda sana hii, nikajikuta namkumbuka Angel kipindi kile alipokuwa mtoto na vile vituko vyake, hivi Angel alikuwa anaongeaga nini na babake kwenye simu kipindi kile? Nimekumbuka na kucheka sana, maana alikuwa akianza mpaka utamtafuta ili aongee nae”
Mama Angel nae alicheka na kumwambia mama yake,
“Tena umenikumbusha, ngoja nitamuuliza mume wangu kuwa alikuwa anaongea nini na Angel wakati mdogo maana si kwa mtoto kung’ang’ania kule kuongea na babake kama anaelewa vile”
“Yani ila nimewakumbuka sana wanangu, tulikuwa tukiishi vizuri sana, kidogo tu ushanikorofisha na kuniumiza kichwa”
“Mmmh jamani mama unayo hadi leo hayo mambo jamani, itakuwa ndiomana Angel ameanza kunisumbua pia, yani hapa nimeshamuhamisha shule ndio nilikuwa nashughulikia hayo mambo, mtoto ananiumiza kichwa yule balaa”
“Kafanyaje tena?”
Mama Angel akacheka na kumwambia mama yake,
“Mambo yale yale ya mapenzi ambayo yalinifanya mama yake akili iniruke”
“Ooooh maji hufata mkondo, yani kuna mambo huwa tunayatenda katika maisha lakini yakitugeukia tunaanza kulaumu, ila mimi sikuwa hivyo kwahiyo usifikiri kuwa wewe ulirithi kwangu hapana, ila huyo Angel karithi kwako kuwa makini sana mwanangu, mambo ya kuletewa mimba mapema hivyo hapana jamani. Bora mimi nilishakuwa na ujukuu tayari, ila wewe wa kuwa na mtoto mdogo mwingine halafu mwanao akuletee ujukuu jamani! Pole mwanangu”
“Asante mama, eeeh tena umeongea jambo lingine nililotaka kukwambia, eti baba Angel anataka nizae mtoto mwingine”
“Ndio zaa, mtu kizazi unacho kwanini unakibania kwa mumeo? Zaa jamani, mumeo anakupa kila hitaji utakalo, kwanini usimzawadie watoto? Eeeh! Kumbuka Angel sio wake, yani watoto wake ndio wale mapacha tu kama jicho vile, hebu mpatie watoto wengine”
“Mama nawe”
“Sio mama nawe, usiwe kama dada yako, yani anaona Junior anamtosha, ukimwambia zaa na mumeo utasikia oooh yule mwanaume ana watoto watatu tayari, ndio ana watoto watatu ila ni vizuri akipata nae mtoto pia, mngekuwa hamna vizazi sawa, ila vizazi vipo sema kuzaa hamtaki, hebu mzalie mumeo nae afurahi jamani! Sasa anateseka na kazi kiasi hiko ili iweje? Mtafutie mtoto apate sababu ya kuendelea kuchakarika”
“Ila watoto si wapo wale mama?”
“Hawatoshi, muongezee mmoja mumeo afurahi”
“Kwa umri huu mama”
“Hebu nenda huko, una miaka mingapi ya kushindwa kuzaa? Hebu nenda kamzalie mumeo jamani”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Sio kunielewa tu ila fanyia kazi nilichosema hapa, maana kunielewa tu haitoshi”
“Sawa mama, nasikia mtoto wa dada kafukuzwa na mumewe kisa amemzaa na mwanaume mwingine?”
“Unadhani mume afanyeje sasa hapo? Mara nyingine tunaweza kulaumu bure tu, ila hakuna kitu kinauma kama kusalitiwa ndani ya ndoa, muache akae kwao labda akili imkae sawa”
“Mmmh sawa mama”
Basi aliongea pale na mama yake na mwisho wa siku akamuaga na kuondoka zake kwani alishakipata alichokuwa akikitaka, yani alitaka tu kusikia mama yake akimwambia kuwa ni sahihi kwa yeye kuzaa tena au si sahihi kwa yeye kufanya hivyo.
 
SEHEMU YA 59

Angel kwenye ile shule mpya, alijitahidi sana kuzoea yale mazingira na kweli alikuta wanafunzi wapo makini sana, na alitambulishwa na kukaribishwa vizuri sana darasani. Haikuwa kama shule aliyotoka maana ile ilikuwa muda wote walimu wanafundisha na wakitoka basi wanakuwa wameacha maswali ya kujadili darasani yani jioni kabisa ndio walitoka shuleni na mama yake ndio alipita kumchukua ili kurudi nae nyumbani.
Basi akiwa kwenye gari alimuuliza kuwa anaionaje shule mpya aliyoenda,
“Eeeh vipi shule, umependa mazingira yake, wanafunzi, walimu vipi unaionaje?”
“Hii shule inaonekana wapo makini sana mama, yani wanafunzi ni kujadiliana tu darasani, sijaona mambo mengine sijui kwa siku za usoni huko ila ipo vizuri”
“Hujakumbuka marafiki zako?”
“Marafiki wenyewe ndio wale wakina Hanifa, hata siwataki tena. Rafiki yangu ninayemkumbuka ni Yusra tu basi maana alikuwa akinipenda na akinielekeza yaliyo sahihi”
“Sawa mwanangu, nahitaji usome kwa bidii, kuanzia kesho utakuwa ukiletwa na yule dereva na ndio atakuwa akija kukuchukua. Angel mwanangu nahitaji usome na ufike mbali, unataka kuwa nani badae?”
“Nataka kuwa Mwanasheria”
“Basi zingatia masomo ili ndoto zako zitimie”
Walifika nyumbani na moja kwa moja Angel alienda chumbani kubadilisha nguo na kwenda kufanya maswali ambayo alipewa na mwalimu wake, ila muda huo Erica na Erick nao walikuwa wamesharudi.
Basi Erica alimfata mama yake na kuanza kumwambia kuhusu Elly,
“Jamani mama huyo Elly anachekesha huyo yani ana vituko”
“Kafanyeje kwani?”
“Kuna mwanafunzi mmoja huwa anapenda sana kuongea na mimi anaitwa Abdi, basi leo wakati akiongea na mimi akaja Ellyn a kumwambia Abdi, ole wako umtongoze dada yangu nitakuvimbisha makalio”
Basi Erica akaanza kucheka tena na kumwambia mama yake,
“Halafu akamchora mtu kwenye karatasi ana makalio makubwa na kusema eti ndio Adbi yule akijaribu kunitongoza”
Alicheka tena na kumpa ile karatasi mama yake, ambaye nae alicheka baada ya kuiona ile karatasi na kusema,
“Inaonyesha huyu Elly ana vituko sana”
“Yani ana vituko huyo balaa, ukimuona mama siku hiyo utacheka sana”
“Haya mwanangu, nitafurahi kumfahamu Elly”
Kisha Erica ndio akaondoka sasa, yani mama yake akacheka sana kwani mtoto wake huyo ilionyesha kuwa hawezi kufanya kitu bila kusema.

Siku hiyo usiku wakati wanajiandaa kulala, simu ya mama Angel ilianza kuita alipoangalia aliona kuwa ni wifi yake ndio anampigia basi alianza kuongea nae,
“Wifi za siku?”
“Nzuri tu, jamani kwani vibaya kwa watoto wangu kukaa kwa shangazi yao jamani! Mbona dadako ananifanyia hivi jamani!”
“Sio vibaya, ila na wewe umezidi yani tangu uondoke hadi leo hujarudi unategemea nini? Na tunasikia kuwa upo kula bata tu, ulikuwa wapi kula bata hapo nyuma jamani! Haya mambo ya kugundua stepu wakati mziki ushaisha ni mabaya sana”
“Umeanza maneno yako ya karaha, hivi kwani huwezi kuongea vizuri bila maneno ya karaha, kwahiyo ulitaka nami kaka yako anikute na mtoto kama ambavyo kaka yangu alikukuta wewe na mtoto?”
“Kheee nimeshindwa”
Kisha mama Angel akamkabidhi mumewe simu na kumwambia kuwa aongee na huyo wifi yake,
“Ongea mwenyewe na dada yako”
Mumewe akachukua ile simu na kuanza kuongea nayo,
“Na bora umepiga, yani nilitaka nikupigie mwenyewe, kwanini dada yangu unafanya mambo ya ajabu kiasi hiko? Kwanini lakini? Wale si watoto wako, wewe ndio unajua uchungu wake, kwanini kutaka kumsumbua mwenzio kisa ni shangazi yao”
“Ila yeye hana mtoto mdogo pale, kwahiyo nimempelekea ili wamchangamshe”
“Mjinga wewe, angewataka si angewaomba mwenyewe? Hana mtoto mdogo sababu hajaamua kuwa nae sio kwamba anataka watoto wako wakachangamshe nyumba yake, yani Tumaini nakwambia hivi dada yangu mpaka kuisha kwa wiki hii nikikuta hujaenda kuwachukua watoto wako basi nitawabeba na kuwapeleka kwa mama yako, huwa sipendi ujinga kabisa mimi. Huo ujinga usifanye”
“Jamani Erick”
“Hakuna cha jamani wala nini, jitahidi urudi ukachukue watoto wako, yani mimi nitauliza hadi Jumamosi nikiona hujaenda kuwachukua basi nawabeba wote na kuwapeleka kwa mama yako, huo ujinga sitaki kuusikia kabisa, wewe ni dada yangu ila wakati mwingine hebu jiongeze basi, unatesa wenzio kwakweli”
“Sawa nimekuelewa”
Kisha Tumaini akakata simu na kumfanya baba Angel kumkabidhi mkewe ile simu huku akisema,
“Yani huyu dada yangu asinitanie kwakweli, atashangaa tu nikipeleka watoto wake kwa mama yake”
Mama Angel hakuongeza neno kwani alitaka mumewe abaki na maamuzi anayoyataka.
 
SEHEMU YA 60

Siku hiyo kama kawaida watoto walijiandaa na kwenda kwenye shule ambazo walikuwa wanasoma, ilikuwa ni siku ya Ijumaa kwahiyo kila mmoja alijua wazi kuwa siku ile huwa ni fupi sana na Angel nae alikuwa shuleni kama siku ya kwanza kwa Ijumaa kuwepo katika shule ile.
Basi aliendelea na masomo yake kama kawaida, ila hawakuwahi kutoka na kupewa tena maswali na kazi mbalimbali za kufanya hapo shuleni.
Hadi jioni kama kawaida ndio walitoka na dereva wao alifika kumchukua na kuondoka nae.
Walipofika getini Angel alishtuka sana, kwani alimkuta Hanifa akiwa na Samir pale nje kwao inaonyesha Samir aliamua kumfata kwao.


Walipofika getini Angel alishtuka sana, kwani alimkuta Hanifa akiwa na Samir pale nje kwao inaonyesha Samir aliamua kumfata kwao.
Angel alimuomba dereva amshushe, basi yule dereva alimshusha Angel halafu Angel akawa anawafata Samir na Hanifa ili kuwaambia waondoke maana anaelewa kama mama yake akiwakuta hapo itakuwa balaa tupu, ila wakati anawasogelea, Samir alimuona na kuinuka pale nje ya geti na kumfata Angel kisha akamkumbatia kwa nguvu sana na kumwambia kuwa,
“Angel nakupenda, siwezi mimi kuishi bila ya wewe”
Huku akimbusu kila sehemu katika mwili wake, muda huo huo mamake Angel nae alikuwa akirudi kwahiyo aliona jinsi Angel alivyokumbatiwa na Samir pale nje ya geti, kwakweli alichukia sana na kushuka kwenye gari kwa hasira.
Akawafata karibu na kuwaachanisha kwa hasira kisha alimkunja Samir na kumwambia,
“Sasa wewe mtoto nadhani unataka kunitibua uzazi, haya naomba upambane na mimi!”
Samir nae akamjibu,
“Kwani mama nimekuja kupambana na mtu hapa!! Nimekuja kumuona Angel sababu nampenda sana”
Mama Angel alizidi kupata hasira na kumsukuma Samir ambaye alianguka chini, halafu alimsogelea Hanifa na kumnasa kibao, kisha akamshika mkono Angel na kuingia nae ndani yani gari yake alimtuma tu dereva aende kuiingiza, yani siku hiyo alikuwa na hasira sana alijikuta akimsukuma tu mwanae kuingia nae ndani, moja kwa moja alienda kujifungia nae chumbani na kuanza kumwambia,
“Siku zote huwa nakwambia nitakupiga nitakupiga ila huwa sikupigi, yani leo ndio nitakupiga Angel, unaniletea ufedhuli ndani ya nyumba yangu!!”
Mama Angel alichukua mkanda wa suruali wa mume wake na kuanza kumtandika nao Angel, yani Angel alikuwa akipiga makelele tu ya kuomba msaada.
“Mama nisamehe, mama utaniua”
Ila mama yake alikuwa akimpiga kwa hasira alizokuwa nazo maana yeye alihisi kuwa Angel ndio kawaita Hanifa na Samir, wala hakuwaza vingine zaidi ya hivyo, basi Vaileth alienda mlangoni huku akigongea mama Angel mlango na kumsihi amsamehe Angel,
“Mama nakuomba msamehe Angel, nakuomba mama”
Erick na Erica nao walienda mlangoni kwa mama yao huku wakionyesha kulia na kuomba mama yao amsamehe dada yao kutokana na makelele ambayo Angel alikuwa akiyapiga, kwa bahati Erick alikumbuka jambo na moja kwa moja alienda kwenye chumba ambacho baba yao huwa anahifadhi funguo za ziada, kisha alisogea pale mlangoni na kufungua mlango, moja kwa moja alimkimbilia dada yake chini ambapo alikuwa akipigwa na mama yao, kiasi kwamba zile fimbo za mikanda zilikuwa zikishuka katika mwili wake ila hakujali zaidi ya kumtoa Angel kutoka kwenye mikono ya mama yao, yani ilionyesha kuwa mama yao alikuwa na hasira sana kwani walipomtoa Angel nae alifunga mlango na komeo la ndani kabisa, alikaa chini na kuanza kulia sana yani alijikuta akilia mno huku akisema,
“Hivi kosa langu ni nini jamani! Kwanini mimi inanitokea hivi, tuseme siwezi kulea au ni kitu gani jamani! Mbona wazazi wengine wanatulia na watoto wao, haya maswala ya kuzaa na wababa wasiojielewa ndio yameenda kuibuka kwa mwanangu Angel, kwanini anisumbue hivi,? Nimeacha hela ngapi katika shule niliyomtoa? Nimetoa hela ngapi katika shule niliyomuhamisha? Kwanini jamani, kwanini mimi?”
Alilia sana hadi alizimia pale pale sababu ya kulia kwa hasira.
Hanifa akiwa bado nje na Samir, alimshika mkono Samir ili waondoke ambapo bado Samir alikuwa akigoma, basi Hanifa alimwambia,
“Samir, sitaki kesi ujue, babake Angel akitukuta hapa kuna mawili yatatokea, either tupelekwe monchwari au tupelekwe ICU, mimi sipo tayari kwa lolote kati ya hayo”
Basi alimshika mkono na kumlazimisha kuondoka, mwisho wa siku aliondoka ila kishingo upande kwani bado alikuwa akitamani kukaa hapo hapo kwakina Angel.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 61



Wakina Erick walimpeleka Angel chumbani kwake huku akilia na akiwa na alama za mikanda ambayo mama yake alikuwa akimtandika nayo,basi Vaileth ndio alibaki nae chumbani huku akijaribu kumuweka sawa kisaikolojia na kumpooza na vile viboko alivyochapwa na mama yake,
“Angel usimchukie mama yako, kafanya kwa hasira hakujua. Msamehe bure”
“Ila mimi hakuna kibaya nilichofanya jamani, mimi nimetoka shule na wale nimewakuta nje ya geti yani najilaumu kushuka kwenye gari kwani nilikuwa nawaambia waondoke wasije kutwa na mama, ona sasa kilichonipata mimi”
Angel alikuwa akilia na Vaileth alikuwa akimbembeleza huku akijaribu kumtia moyo kwa kile kilichotokea.
Wakina Erick walivyoona kimya chumbani kwa mama yao wakapatwa na wasiwasi, yani muda huo huo walienda kwenye simu yao ya mezani na kumpigia baba yao na kumueleza kilichotokea, ndani ya muda mfupi tu baba yao alikuwa nyumbani ila mlango haukufunguka maana mama Angel aliufunga ndani kwa komoe, ilibidi mumewe ajitwike ufundi na kuvunja ule mlango wao, kwakweli alimkuta mkewe chini amezimia, na yeye alihisi kiwewe, moja kwa moja alienda kumuamsha mkewe ambaye hakuamka wala nini,kwakweli alipatwa na mashaka pia ila alipomuangalia vizuri aligundua kuwa kazimia basi akamwagia maji na kumfanya azinduke, alikuwa akishangaa shangaa tu basi mumewe akawaambia wote watoke na kuongea na mkewe,
“Naomba ujiandae muda huu tunatoka”
“Tunaenda wapi mume wangu?”
“Jiandae tu utajua tunapoenda”
Basi mama Angel aliinuka ila alijaribu kukumbuka vizuri aliona hakumbuki zaidi ya kichwa kumuuma tu,aliamua kwenda kuoga na muda huo wakati anaoga mumewe alienda kuzungumza na Angel ili kujua kuwa ilikuwaje, ambapo Angel alimueleza huku akilia, basi alimkumbatia mwanae na kumwambia kuwa yataisha tu na kila kitu kitakuwa sawa,
“Mwanangu usijali, nakuomba umsamehe mama yako ana hasira sana. Unajua tumemkuta kazimia eeeh!”
Angel alishtuka kusikia kuwa mamake alizimia basi mamake akamtoa uoga,
“Ila usiogope wala usijali kwani anaendelea vizuri kwasasa, mimi na yeye tunatoka kwahiyo mtabaki na dada yenu hapa naomba mmuheshimu na mumsikilize. Pole mwanangu”
“Asante baba”
Basi baba yao alitoka mule chumbani kwa Angel na kurudi chumbani kwao huku akijaribu kurekebisha mlango ambao aliuvunja kidogo ila mama Angel alipotoka bafuni alimuuliza mumewe
“Vipi huo mlango umefanyaje?”
“Aaaah achana nao, nitamuita fundi aje aurekebishe, basi malizia kujiandaa mke wangu tutoke”
Na kweli alijiandaa na wakatoka huku akimuachia maagizo Vaileth kuwa awaangalie vizuri watoto wake.
Wakati gari ikitoka nje ya geti lao alijikuta akikumbuka kila kitu huku akiangalia mara mbili mbili, aliuliza.,
“Angel yuko wapi?”
“Tukirudi nyumbani utamkuta”
“Unajua huyu mtoto kanikera sana leo, hujui tu”
“Wewe ndio hujui tu, hivi mama yako angekuwa anakupiga kiasi ambacho umempiga Angel ingekuwaje? Mama yako alikuwa anakupiga ila kwa kiasi sio kwa stahili hii mke wangu, utaua mtoto nakwambia, hasira ni hasara, twende tu ukapunguze mawazo kwanza"
“Hivi nimempiga sana eeeh!”
“Tena sio ya kuongea maana hadi umemtoa alama mtoto, unataka kumuharibu sura halafu utamuoa wewe? Mbona sura yako haikuharibiwa jamani!”
“Kwahiyo wewe ulinipendea sura?”
“Mapenzi hayachagui kitu kikoje, huo upendo wa dhati unatoka moyoni, kama sura ni wanawake wangapi wenye sura nzuri ambao nilikutana nao ila sikuwataka nikakutaka wewe!”
“Kwahiyo mimi sio mzuri eeeh!”
Mama Angel alionekana kuchukia na mumewe akamwambia,
“Yani tatizo lenu ndio hilo wanawake, mtu akisema hivi basi wewe unasema vile, nimesemea uzuri umeanza kusema kwahiyo mimi umenipendea sura, nakwambia kupenda kunatoka moyoni unasema kwahiyo mimi sio mzuri, jamani mama Angel sisi ni watu wazima sasa, hebu tuachane na hayo mambo ya kijinga”
“Kumbe unaniona mimi mjinga!”
Muda huu ndio alinuna kabisa ikabidi mumewe aanze kumbembeleza,
“Sijasema wewe ni mjinga mke wangu, hivi ningeanzaje kuoa mwanamke mjinga jamani!! Mke wangu wewe ni mwanamke wa kipekee una akili sana ndiomana sikutaka kukuacha kwakweli, nimepigani penzi langu mno na wewe ni shahidi wa hilo, na kuhusu uzuri, kwakweli mke wangu wewe ni mzuri kuliko wote ulimwenguni, umerandisha hadi watoto wamekuwa visura wanavutia ndiomana wameanza kufatiliwa wakiwa wadogo, kwakweli kama kuchagua mimi ni namba moja maana nimeona kisura, mrembo, mzuri na mwenye akili yani sifa zote nzuri unazo mke wangu”
Kisha baba Angel alisimamisha gari kidogo na kumbusu mke wake, yani ile kitu ilimfanya mama Angel ajihisi ufahari sana, kwakweli alifurahi sana na alikuwa akitabasamu tu huku baba Angel alkiendelea na safari sasa.
 
SEHEMU YA 62

Basi walifika kwenye hoteli na kushuka kisha wakakaa na kuagiza chakula ambapo walikuwa wakila na kuongea mambo mbalimbali,
“Sasa mke wangu, nikuombe kitu kimoja”
“Kitu gani hiko?”
“Unaonaje Angel akimaliza kidato cha nne tumpeleke Africa kusini”
“Mmmh hapana jamani, inamaana hutaki kumuona Angel nyumbani eeh!”
“Sina maana hiyo mke wangu, ila nilitaka kumtenganisha na hawa wanaume wakware”
“Kwani huko Afrika kusini hakuna wakware? Ningekuwa naenda kuishi nae sawa, ila kwenda kuishi peke yake hapana jamani, nataka nione watoto wangu wote pamoja, ila ninapokosea kwenye malezi nijue mume wangu”
“Sawa, nimekuelewa mke wangu. Ila nilikuwa natoa wazo tu hilo”
“Huko tuendage sisi wenyewe, ila watoto wangu hapana jamani”
Mara mama Angel alishangaa kushikwa bega, kugeuka hivi ni mtu ambaye alikuwa akifahamiana nae vizuri sana, ambaye alimwambia kwa mshangao,
“Kheee Erica!”
“Jamani Fetty kumbe upo!”
Basi walikumbatiana kwa furaha kisha Fetty alikaa na kumsalimia baba Angel pia huku akisema,
“Kweli nimeamini katika dunia kuna mapenzi ya dhati, kwa hakika nyie mlipendana yani hadi leo mpo pamoja?”
Mama Angel na baba Angel walitabasamu huku baba Angel akimwambia,
“Ndio, penzi la kweli lipo ila cha muhimu ni kumpata mtu ambaye atakupenda kweli na utampenda kweli. Katika mapenzi si vizuri kukurupuka, yani ukikurupuka lazima ukutane na mauzauza na mbeleni yakakushinda”
“Kweli kabisa uyasemayo, kama mimi najuta kukurupuka kuolewa”
Mama Angel alimuuliza,
“Kivipi? Si uliolewa na Bahati wewe?”
“Ndio, nilijua atanipenda na kunijali vile alivyokuwa akikupenda wewe na kukusumbua kumbe hakuna kitu wala nini?”
“Kheee jamani, tena nimekumbuka kuhusu Bahati (Kisha akimuangalia mumewe na kumuuliza) Hivi yule Samir sio mtoto wa Bahati kweli? (Alimuangalia Fetty na kumuuliza) Bahati hana mtoto wa kuitwa Samir?”
“Kafanyeje huyo Samir?”
“Ni anamsumbua mwanangu balaa, yani hadi kichwa kinaniuma sababu ya huyo mtoto, haogopi kitu na haogopi mtu yeyote, yani anachojua yeye ni usumbufu tu basi”
“Duh! Pole, huyo Samir simfahamu labda kama alizaaga na kumficha ila kuna mambo ya Bahati yanatia hadi kichefuchefu”
“Mambo gani hayo?”
“Yani huwezi amini, Bahati alizaa na yule mkewe aliyemuacha na kunioa mimi, kumbe alizaa pia na mdogo wa mke wake, halafu kumbe Bahati alimbaka mama mkwe wake na yule mama akapata ujauzito na kwenda kuutoa ila kumbe iligoma kutoka, kwahiyo Bahati kazaa na familia nzima, yani ninavyokwambia hadi kichefuchefu kuanza kufikiria hayo”
“Mmmh mbona mtihani huo pole”
Baba Angel aliwaaga kidogo kuwa anakwenda maliwatoni kwani aliona hao wanawake hawakawii hata kuzungumzia na yeye, basi aliondoka na kuwaacha pale ambapo Fetty aliendelea kuongea,
“Asante shoga yangu, kikweli nimechoka yani nimechoka kabisa, maana hao watoto wote wamebwagwa pale nyumbani, halafu kumbuka mimi nina mtoto pia nilizaa na yule kichwa rungu, kwahiyo jumla wanne, halafu Bahati nimezaa nae watoto wawili jumla watoto sita, na sijui huko nje kama hana watoto wengine, umenipa habari zakina Samir tena kichwa kinanipasuka hapa”
“Kwahiyo wewe umekuja hapa hotelini mwenyewe?”
“Ndio, nimekuja kupumzisha mawazo jamani, ile sio ndoa bali ni ndoano, yani kukurupuka huku kubaya sana. Leo alikuja yule mama mkwe wake, uwiii katukana jamani, katukana mkoo wangu mzima, kiukweli najuta kumfahamu Bahati, najuta kuolewa nae”
“Ila wewe ulikuwa huyajui hayo wakati unaolewa nae?”
“Mimi nilijua tu kazaa na yule mke wake, na vile mkewe alikuwa mshirikina basi niliona ana sababu madhubuti kabisa ya kuachana na mkewe. Kuna kipindi alikuwa akinisumbua hatari wakati nina mimba ya huyu mtoto wa mwisho, si ndio wakanibwagia watoto wote, nimepata shida shoga yangu balaa. Ila wanaume hawa sio wa kuwaamini jamani, mwanaume sio mama yako wala sio baba yako”
“Ila mimi mume wangu namuamini”
“Usimuamini kivile, siku ukiletewa mtoto aliyezaa huko wapi sijui nadhani utapata ugonjwa wa kupooza, jamani usimuamini mwanaume, ni kweli anakupenda ila usimuamini kupitiliza. Hebu ona toka ameenda chooni hadi sasa hajarudi mmmh!”
“Mmmh na wewe Fetty jamani, hadi shemeji yako unamnanga mmmh!!”
“Hivi kwanza Bahati hajakusumbua? Kuna kipindi wimbo wake ulikuwa ni wewe, oooh mke wangu alikuwa ni Erica, sijui Erica ndio aliumbwa kwaajili yangu, jamani mwanaume ana wazimu yule sijapata kuona”
“Mmmh makubwa”
Muda huo huo baba Angel alitoka maliwatoni na kwenda pale kwenye meza ambapo alimtaka mkewe waondoke, kwahiyo mkewe na Fetty walibadilishana namba, kisha wakamuaga pale,
“Ila na mimi ndio narudi kwangu”
Basi wakaagana nae na kuondoka eneo lile.
 
SEHEMU YA 63



Fetty alirudi kwa mume wake ambaye alianza kumfokea kwa kitendo cha kuchelewa kurudi,
“Kweli kabisa mke wa mtu ndio unarudi nyumbani kwako muda huu!”
“Kumbe ulikuwa ukifurahia yale matusi ambayo mama mkwe wako alikuwa akinitukana mchana? Ulikuwa ukifurahia eeeh!”
“Kheee mke wangu jamani! Nina haki ya kukuhoji”
“Haya na mimi nina haki ya kukuhoji, niambie Samir umezaa na mwanamke gani?”
“Samir??”
“Ndio, usijifanye humjui mtoto wako, yani ningekujua toka mwanzo wewe mwanaume sidhani kama ningekubali kuolewa na wewe, sijui ndio unataka kuanzisha timu ya mpira jamani! Haya Samir umezaa na nani na yuko wapi?”
“Jamani, watoto wangu wote wapo hapa nyumbani, sina mtoto wa kuitwa Samir”
“Hivi wewe kumbuka siku watoto wameletwa hapa nyumbani ulisemaje? Ulisema kuwa ulipewa madawa na ukawa unatembea tu na wanawake, sasa unashangaa vipi kuhusu mtoto wako Samir? Yani najua kuolewa na wewe jamani, natamani nirudishe miaka nyuma ili nisikubali hata ndotoni kuolewa na wewe. Nakiri wazi sikupendi”
“Jamani mke wangu, toka nakuoa unaelewa kabisa hali halisi inayoendelea kwangu, ni wewe ndio ulikuwa ukinieleza mambo ya kufanya, na hata wakati nataka kuteleza tena ulikaa chini na kunionya huku ukinielekeza mambo sahihi ya kufanya, sasa ni nini cha kufanya mimi na wewe tugombane? Ni hao watoto? Kwani historia yake sijakwambia? Bora ningekuwa sijakwambia ila nimekueleza kila kitu mke wangu yani hakuna kitu katika maisha yangu ambacho hukifahamu mke wangu. Nakupenda na ninapenda tuishi kwa upendo, hivi ningekuwa na mtoto wa kuitwa Samir si ningekwambia mke wangu jamani! Kwanini nikufiche sasa kitu kama hiko!”
Fetty hakutaka kumsikiliza mumewe kwani alijua kuwa anaongopewa tu na mumewe ila huyo Samir ni mtoto wake, ingawa hakumuona ila aliamini kuwa Samir ni mtoto wa Bahati baada ya kuambiwa na mama Angel.

Kulipokucha, baba Angel alimwambia mke wake,
“Hivi leo si ndio Jumamosi?”
“Ndio leo ni Jumamosi, kwani kuna nini?”
Subiri, baba Angel alienda kujiandaa na baada ya hapo alimuaga mke wake kuwa anatoka ila alimwambia jambo moja,
“Jitahidi leo uzungumze vizuri na mtoto maana umemuweka katika mazingira ya uoga, mwambie ni jinsi gani unaumia kuona yeye akitaka kuharibikiwa, ila usimfanyie ukali tafadhali’
“Sawa nimekuelewa”
Basi baba Angel akaondoka ila hakumwambia mkewe anapoelekea kwani alijua fika lazima angemkatalia tu.
Basi mama Angel nae aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Angel ambaye alikuwa akilalamika kuwa viungo vinamuuma kutokana na zile fimbo alizochapwa na mama yake,
“Pole sana mwanangu, yani mama yako nilikuwa na hasira sana kwa muda ule. Fikiria ni hela ngapi nimepoteza kwaajili ya elimu yako, halafu nikukute katika hali ile kwakweli nilichukia”
“Lakini mama ungeniuliza kwanza ili nikuelezee”
“Sasa ningekuuliza nini pale? Ningekuuliza kama na wewe unampenda Samir au kitu gani?”
“Hapana mama sio hivyo, ila ungeniuliza kama nami nimekubaliana na wale kuja, kwani hata mimi pia nilishangaa kuwaona nyumbani kwetu mama, kwakweli sikutegemea”
“Labda nikuulize hivi, je na wewe unampenda Samir?”
“Mama jamani!”
“Sio mama jamani, nijibu”
“Hapana mama, mimi bado mwanafunzi. Nahitaji kutimaza malengo yangu na ndoto zangu”
“Sawa, ngoja nikuuliza kitu kingine. Je kuna chochote ambacho huwa unahitaji nakunyima?”
“Hapana mama, kila kitu unanipa”
“Unaweza sema mbona simu nimekunyang’anya ila nimekunyang’anya simu baada ya kukuta ukiwasiliana na hao wajinga wakina Samir na wakina Hanifa, mwanangu nakupenda sana jamani, yani sitaki nikupoteze kwa mambo ya kijinga, hebu thamini upendo wangu japo kidogo kwa kuniheshimu. Nakupenda mwanangu naomba ujithamini pia na ujiheshimu. Sina mengi ya kukwambia ila nakupenda sana mwanangu”
Angel alifurahia maneno ya mama yake na kumkumbatia kwa furaha.
 
SEHEMU YA 64


Baba Angel moja kwa moja alienda kwa mama Junior yani dada yake na mama Angel, basi alifika pale na kumkuta nyumbani kwake amekaa huku akionyana na mtoto wake, basi akawasalimia pale na kuuliza nini tatizo,
“Jamani shemeji, tatizo ni huyu Junior, ananiumiza kichwa kwakweli hata sijui nifanyeje nae. Maana mtoto ana mambo ya ajabu sijapata kuona, hapa mtaani hakuna mtu asiyemjua Junior jamani”
“Wewe Junior, kwanini unafanya mambo ya ajabu kiasi hiko?”
Junior aliangalia chini kwa aibu kwani kwa upande mwingine alikuwa akimuogopa baba yake mdogo huyu, kisha baba Angel alimwambia,
“Haya muombe msamaha mama yako kwa yote uliyomfanyia na useme mbele yangu hapa kuwa hutorudia tena kufanya ujinga wa namna hiyo”
Basi Junior alimwambia mama yake,
“Mama nisamehe, sitarudia tena”
Ila baba Angel alimwambia kwa ukali tena,
“Msamaha gani unaomba hivyo? Hebu piga magoti huko”
Basi Junior alipiga magoti kwa mama yake na kumuomba msamaha mama yake, yani mama yake alishukuru sana kwa ujio wa shemeji yake huyu. Junior hakuweza kufanya kiburi kwa bamdogo wake huyu kwani mara nyingi huwa anamfata akiwa na shida ya hela halafu huyu baba yake mdogo anamsaidia.
Basi mama yake alimwambia kuwa amemsamehe pale na kisha baba Angel alimtaka kwenda kujisomea, nae Junior alifanya hivyo basi mama yake alianza kuongea pale,
“Nashukuru sana umekuja yani huyu Junior ni wawili tu ndio huwa mnamuweza, wewe na mjomba wake Tony, kwakweli nashukuru sana”
“Aaah usijali dada yangu, shemeji yangu usijali tupo pamoja. Eeeeh hawa watoto wa Tumaini wako wapi?”
“Wapo, wamelala muda huu. Watoto wavivu hawa hatari”
“Naomba kaniitie”
Basi mama Junior alienda kuwaamsha na kuwaambia kuwa mjomba wao anawaita, ambapo walitoka wote na kwenda kumsalimia, kisha akawaambia,
“Naomba mjiandae na mbebe mabegi yenu maana tunaenda kwa bibi”
Wale watoto hawakubisha kwani muda huo huo walienda kujiandaa, kisha mama Junior alimuuliza baba Angel,
“Shemeji, unawapeleka kwa bibi? Kivipi?”
“Nawapeleka kwa bibi yao ndio, mama yake mzazi na mama yao”
“Kheee mwenyewe hataki watoto wake waende kule”
“Sikia shemeji nikwambie, yule ni bibi yao haijalishi chochote ila yule ni bibi yao. Halafu kama baba Junior kashindwa kuwapeleka hawa watoto kwao, ngoja mimi nifanye hilo jambo. Naomba usinikatalie maana hawa watoto ni watoto wa dada yangu, mimi ni mjomba wao. Kwahiyo acha tu nifanye hili shemeji”
“Mmmh sawa, mimi sina neno”
Basi baada ya muda watoto walikuwa wamejiandaa kisha baba Angel aliaga pale na wao wakaaga halafu akaondoka nao.
 
SEHEMU YA 66


Kulipokucha wakati wakijiandaa kwenda Kanisani, walishangaa asubuhi asubuhi mtu akiita kwa nguvu nje,
“Erica, wewe Erica weee”
Basi mama Angel alitoka ndani ili kuangalia anayeita, alishangaa kuona ni wifi yake, ambapo walipokutana tu, yule wifi yake alimsogelea mama Angel na kumnasa kibao cha nguvu ambacho kilimpeleka hadi chini.
Kwakweli mama Angel alisikitika sana, halafu akainuka na kumuuliza wifi yake,
“Kwani kosa langu nini Tumaini?”
“Hivi wewe una akili kweli? Utapelekaje watoto kwa mama yangu wakati unajua anaishi mwenyewe? Sawa ni bibi yao ila kwanini usiwapeleke kwa mama yako ambaye ni bibi yao pia”
“Jamani sio mimi niliyefanya hivyo, kwanza nashangaa tu maana unanipa lawama nisizozielewa”
“Najua ni wewe tu maana akili zako huwa unazijua mwenyewe, hivi unajua kwanini niliwaweka wale watoto kwa mama Junior? Mbona sikuwaleta kwako? Kwanini usijiulize hilo, na kwanini mama Junior asiniambie mwenyewe zaidi ya wewe kamavile ni watoto wako? Unajichukulia maamuzi tu kama kichaa”
Tumaini akanyua tena mkono wake ili amzabe kibao tena mama Angel, ila muda huu baba Angel alitoka ndani na kuudaka ule mkono wa dada yake kabla hata haujashuka tena kwenye shavu la mke wake, kisha yeye ndio akamzaba kibao dada yake na kumwambia
“Hivi ndio ustaarabu wa wapi huo? Yani unafika kwa watu huna hata salamu unaanza ubondia wako, hivi lini utaacha hayo mambo yako dada yangu! Haya nipige mimi sasa”
“Jamani Erick ndio unanipiga mimi dadako!”
“Nilishawahi kukwambia na sasa nakwambia tena, huyu mwanamke akiumia ni mimi nimeumia, kwahiyo ukimpiga huyu mwanamke jua kwamba umenipiga mimi. Na sasa nimekuruhusu upigane nami”
Basi Tumaini akawa mpole na kuanza kuomba msamaha,
“Nisamehe tafadhali ila ilikuwa ni hasira”
“Hasira gani hiyo? Huo ni ujinga na sio hasira, halafu unamuonea sana wifi yako, sijui una nini wewe lakini”
Kisha baba Angel alimsogelea mke wake na kuwa kama akimpukuta vile kutokana na alivyoanguka, basi yule wifi wa mama Angel aliendelea kuomba msamaha tu,
“Nisameheni tafadhari”
Basi baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza,
“Je tumsamehe!”
“Ndio, mimi sina tatizo nae lolote lile”
“Haya sasa, tuambie hiyo hasira yako uliyokuja nayo ilikuwa inahusu nini?”
“Samahani tena jamani, yani mimi nilichukia kuhusu watoto wangu, kwanini wapelekwe kwa mama”
“Sasa wewe umeuliza ni nani kafanya hivyo? Ila licha ya hivyo si nilikwambia jamani kuwa ukichelewa basi napeleka watoto kwa mamako, najua kule ndio unauchungu nako, hivi kweli wewe unakaa miezi miwili unakula bata huna hata habari na watoto jamani!”
“Ila kabla ya yote mngeniuliza kwanza kwanini nimewapeleka kwa mama Junior, mbona sikuwaleta hapa jamani! Haya yaishe maana nimesharudi”
“Ila cha muhimu kweli umerudi, na wewe dada yangu kuzamia Arusha kiasi hiko ndio nini jamani!”
“Yani mama alivyonipigia simu jana nilihisi kiwewe, ila Erick hufai jamani loh!”
Tumaini akawa anacheka mwenyewe, mara wakina Angel wakawa wanatoka ndani maana walishajiandaa kwa kwenda kazini, basi Tumaini alipomuona Angel akasema,
“Jamani huyu mtoto kadri anavyokua ndio anavyozidi kuwa mrembo jamani, mfuge mbwa sasa”
Baba Angel na mama Angel wakacheka na kumtaka waende nae tu kanisani,
“Sawa tutaenda ila tukitoka nahitaji kwenda na wifi yangu mahali”
“Kheee mshapatana tayari!”
Tumaini akamuangalia mama Angel na kusema,
“Eti wifi yangu kwani bado una kinyongo? Wifi yangu mzungu bhana wala hana mambo ya Kiswahili”
Mama Angel alitabasamu tu kisha wote wakaondoka na kuelekea Kanisani.
 
SEHEMU YA 67

Walipotoka kama ambavyo Tumaini alimtaka wifi yake waende pamoja basi alimsindikiza maana hakujua hata anaenda nae wapi, ila alishangaa tu wakienda nyumbani kwa wifi yake ambapo walipofika alimkaribisha vizuri sana kisha akamwambia,
“Karibu wifi yangu, kwanza kabisa naomba unisamehe kwa nilichofanya leo kwako sikutegemea kufanya vile yani hasira hizi kweli hazifai, nisamehe wifi yangu. Najua niliapa kutokupiga tena kibao hata sijui leo kimefanyika kitu gani kwangu”
“Hamna shida nimekusamehe nakumbuka kuna kipindi zamani uliwahi kuninasa kibao tena nikiwa kwetu”
Tumaini akacheka na kusema,
“Halafu sikomi tu sijui kwanini, kipindi kile nilidundwa na mama yako na leo Erick kanidunda, jamani hii tabia ya kunasa vibao naiacha rasmi yani wifi yangu hata usijali. Naomba unisamehe tu”
“Usijali pia nimekusamehe”
“Sasa nimekuita hapa kwangu unisaidie jambo moja tu, ndugu yangu leo kaka yao kuna wageni anakuja nao halafu wale watu wanataka chakula cha tofauti ambacho hawajawahi kula, nakumbuka kuna kipindi ulipika biryani pale nyumbani kwako, naomba na mie unipikie biryani leo yani kila kitu kipo ila ni pishi lako tu ndio ninalihitaji, mimi huwa napika ila najua kwako ndio mwisho, najua watajiramba humu. Nakuomba wifi yangu tafadhari”
“Hakuna shida, na watoto wako wapo wapi?”
“Oooh nadhani wamelala”
“Kwani uliwachukua muda gani?”
“Yani jana nilivyopigiwa simu, ni muda ule ule nilienda kukata tiketi ya ndege, kwahiyo nimeenda usiku kuwachukua kwa mama, sasa leo asubuhi ndio nimepigiwa simu na mume wangu kuambiwa hiyo kitu kwahiyo nikanunua mahitaji yote na kuja huko kwenu sasa”
“Mmmh ila wewe mshari sana”
“Tuachane na hayo bhana, twende ukakaangize mambo yako yanayomchanganya kaka yangu”
Basi Tumaini akamletea wifi yake nguo ya kubadilisha ili waanze mapishi kwanza nae mama Angel alifanya hivyo na kuanza yale mapishi aliyoombwa na wifi yake, muda huo Tumaini alikuwa akitengeneza juisi ya kunywa hao wageni.
Baada ya kumaliza, basi mama Angel alichukua ile juisi na kuionja kisha akamwambia wifi yake,
“Sasa kwenye hii juisi ongeza na passion kidogo kuleta ladha nzuri zaidi”
“Oooh ndiomana nakupenda wifi yangu, ngoja nikanunue pale gengeni”
Basi aliondoka na kwenda kununua passion kisha akarudi na kuzisaga vizuri na kuongeza kwenye ile juisi ambapo wifi yake alikunywa tena na kuisifia kuwa ni nzuri.
Kisha walikaa kidogo kuongea wakati wifi yake ameanza kujiandaa kuondoka, ila alimuuliza,
“Wifi unajua sijaelewa, watoto wako wapi?”
“Wapo kujisomea, halafu hawajajua kama umekuja, ngoja nikawaite”
Basi alienda kuwaita watoto wake ambao walifika na kumsalimia shangazi yao kisha kurudi zao chumbani,
“Unajua kuna kitu sijaelewa”
“Kitu gani?”
“Mwanzoni ulisema wamelala, na sasa ukasema wapo kujisomea yani nashindwa kuelewa kwakweli, hwakai kuangalia Tv? Au inakuwaje?”
“Humu ndani mimi na watoto wangu kuna ratiba kabisa, kwahiyo kuna masaa ya kufanya chochote kitakachofanyika, kuna muda wa kulala, kuna muda wa kusoma, kuna muda wa kucheza na kuna muda wa kuangalia Tv, huwezi kuwakuta muda wa kulala wanaangalia Tv au muda wa kusoma wanacheza, haipo hiyo kitu nyumbani kwangu”
“Umewezaje kufanya wawe hivo?”
“Ni mazoea tu, unajua nimewajengea mazoea toka wadogo, mimi wakati naishi na baba, kuna mdada wa kazi kwakweli huwa namsifu sana mdada yule kwakweli kanilea katika maadili yanayofaa, hata mama huwa anamsifu ila kitu kimoja tu ambacho hakunifundisha vizuri ni kufanya kazi na kujitegemea ila vingine vyote alikuwa vizuri”
“Kwahiyo na wewe watoto wako umeacha wawe wavivu au?”
“Hapana, ila watafanya kazi gani? Bado wadogo”
“Wadogo? Huyo wa kwanza ana miaka kumi na mbili jamani angekuwa anaosha hata vyombo”
“Kheee kwahiyo wakina Erica wanafanyaga kazi kwani?”
“Kheee wanangu wameanza kufanya kazi muda tu, hata nikiwaacha peke yao hawalali njaa wale, wanajua kupika, kuosha vyombo, kufua yani kazi zote wanafanya, nani awafanyie? Mimi nimewafundisha kila kazi”
“Khee hongera sana, basi nitaanza kumfundisha Leah kufanya kazi”
“Ila nakupa nawe hongera sana kwa kuwalea watoto wako katika maadili, jamani mimi ni mkali sana ila hao wakina Erica tu wananivizia na kukaa kuangalia Tv, halafu kitu kingine ni Angel ananiumiza kichwa jamani”
“Anafanyeje kwani?”
“Kuna kijana anaitwa Samir, uwiii ananiumiza kichwa balaa, sijui nifanyeje mimi”
“Kwani huyo kijana anafanyeje?”
“Anamtongoza Angel, yani anamfatilia balaa hadi sina raha”
“Oooh halafu Angel si ndio yupo kidato cha nne!!”
Ilibidi mama Angel amueleze kila kitu wifi yake kuhusu Angel na huyo Samir, basi Tumaini akamwambia,
“Naomba unipe Angel niishi nae kwa kipindi hiki tu, mimi sisafiri tena kwasasa”
“Oooh utakuwa umenisaidia kwakweli”
“Basi Jumatano nitakuja kumchukua, anatoka shule muda gani?”
“Jioni kabisa”
“Mmmh atakuwa kajiandaa kweli kuja huku jamani!! Sijui ila tutawasiliana basi, au nije Ijumaa?”
“Yani hadi Ijumaa nitakuwa nimetokwa na pumu kabisa”
“Basi Jumatano nitakuja”
Basi wakaongea ongea pale na kuagana kisha mama Angel akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 68


Mama Angel alipanda bajaji kuelekea nyumbani kwake kwani hakutaka kupelekwa na wifi yake, na alimwambia kuwa asubirie tu wageni.
Basi wakati anakatisha na ile bajaji akamuona Samir na kumwambia yule kijana wa bajaji asimamishe ambapo alisimamisha na mama Angel alimwambia Samir,
“Wewe kijana!”
Samir akasogea alipo mama Angel na kumsalimia ila mama Angel alimnasa kibao Samir na kumwambia,
“Nadhani siku ile sikukwambia ila ukome kumfatilia binti yangu”
“Ila mama unanionea bure tu, sio kosa langu wala sio kosa la mwili wangu”
“Sasa ni kosa la nani?”
“Ni kosa la moyo wangu”
Kisha Samir alikimbia baada ya kusema vile, basi mama Angel alirudi kwenye bajaji huku akisonya tu, basi yule dereva wa bajaji akamwambia,
“Inaonekana huyu kijana anampenda sana binti yako”
“Kwanini umesema hivyo?”
“Macho yake yanaonyesha tu wakati akisema sio kosa lake, yani nadhani alitamani hata kulia mbele yako kuwa anampenda sana mwanao”
Mama Angel hakumjibu kitu huyu kijana, basi alifika nyumbani kwake na kushuka ila alipoangalia kwenye mkoba hakuwa na hela ya kutosha, ilibidi apige simu ndani na simu yake ilipokelewa na Angel,
“Angel naomba niletee elfu kumi na tano hapo kabatini”
Basi akakata simu na muda kidogo Angel alitoka na kumkabidhi mama yake ile hela, yani yule kijana alikuwa akichukua ile hela huku macho yote yakimuangalia Angel huku akisema,
“Naitwa Ally”
Mama Angel alichukia na kusema,
“Mjinga wewe, sasa mwenye haja ya kufahamu jina lako hapa ni nani? Muone vile, chukua hela yako na uondoke. Halafu wewe Angel hebu rudi ndani huko”
Basi yule kijana alichukua zile hela na kusema,
“Ila mama kwakweli umezaa jamani, naomba nikuite mama mkwe”
“Una kichaa nini wewe! Nani mama mkwe wako? Hebu ondoka huko”
Mama Angel akaingia getini na kumkuta Angel akiwa kasimama tu ndani ya geti na kumuuliza nay eye kilichomsimamisha hapo ni kitu gani,
“Na wewe nini kimekusimamisha hapo?”
“Hamna kitu mama ila nilitaka kukuuliza”
“Haya niulize”
“Siku zote huwa unasema tusitumie hela vibaya ila mbona leo umetoa elfu kumi na tano na kumlipa yule dereva wa bajaji?”
“Kheee na wewe mtoto kwani kumlipa dereva wa bajaji ni kutumia hela vibaya? Yule kanifanyia huduma kwahiyo lazima nimlipe. Haya twende ndani”
Basi wakaingia ndani ambapo Erick na Erica walikuwa sebleni wakiangalia video tena walikuwa hawana hata habari, basi alivyoingia wakamsalimia, ndipo alipowauliza
“Mmeshajisomea?”
Walikaa kimya tu wakimuangalia, basi akawaambia tena
“Hebu nendeni mkajisomee huko”
Akatokea Vaileth na kumwambia,
“Mmmh mama jamani, watoto hawafanywi hivyo, saivi jioni ni muda wao wa kupumzika na kujifunza mambo mbalimbali si kama unavyowaona hapo wanajifunza kipindi cha mapishi, halafu twende jikoni nikakuonyeshe”
Basi mama Angel alienda na Vaileth jikoni halafu Vaileth akamuonjesha kitu mama Angel, ambaye alikula na kusifia sana huku akimwambia Vaileth,
“Aiseee, unajua sana kupika”
“Unadhani ni mimi nimepika basi!!”
“Ni nani sasa?”
“Ni Erica huyo, yani yeye mwenyewe kaja jikoni leo nakusema dada kuna kitu nataka nijaribu kupika, basi nikamuacha akachukua unga wa ngano na kukanda na mwisho akapika hivi, hadi nimemuuliza vinaitwaje hivi kasema visheti, yani Erica ni mtaalamu haswaaa”
“Oooh huyu mtoto nahisi nimejizaaa mweeeh! Yani kapika vizuri hivi!”
Basi alisahau hata kama alikuwa akiwafukuza wakajisomee, zaidi zaidi wakati anaelekea chumbani kwake akamuita Erica ili amsifie vizuri zaidi,
“Kwakweli mwanangu hongera, kumbe upo vizuri eeeh!”
“Asante mama”
“Ila umejifunza wapi kupika visheti? Nani kakufundisha?”
“Ni Elly ndio kanifundisha mama”
“Elly? Jamani Elly si mtoto wa kiume?”
“Ndio ila mama yake ni mtaalamu mzuri sana wa kupika visheti, sasa Elly aliniletea shuleni na nikapenda ladha yake basi nikamwambia anielekeze namna ya kuvipika ndio akanielekeza”
“Oooh vizuri sana mwanangu, nadhani huyo Elly ni rafiki mwema, ipo siku nitamfahamu”
Basi mama yake aliingia chumbani halafu Erica akarudi sebleni na kumkuta Erick akila vile visheti huku akisema,
“Yani leo sitaki kula chakula chochote kingine, nadhani hivi visheti vinanitosha”
Erica alitabasamu na kumwambia Erick,
“Nimejitahidi eeeh!”
“Sio umejitahidi, ni umeweza kabisa mdogo wangu. Yani ladha ya hivi vidude nimeipenda sana”
Angel nae alikuwa amekaa pale sebleni ila aliinuka na kuelekea chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 69

Usiku wa siku hiyo Angel alijikuta akiwa na mawazo sana juu ya Samir hata alihisi usingizi hamchukui, yani alikuwa akikumbuka matukio yote ambayo Samir amemtendea na jinsi Samir alivyokuwa akimueleza kuwa anampenda sana, basi alikuwa akikumbuka kila kitu na kujisemea,
“Natamani hata ningekuwa na simu basi ningempigia Samir”
Sasa aliamua kujisomea ili aweze kuacha mawazo juu ya Samir, akachukua madaftari yake na kuanza kujisomea, wakati anapekua vizuri alishangaa kuona karatasi imeandikwa namba na akakumbuka kuwa hiyo ni namba ya Samir ambayo alipewa kwa mara ya kwanza kabisa ila hakutilia maanani siku aliyopewa, basi akashika kile kikaratasi huku akitamani sana kuwasiliana na Samir kwa muda huo, alipoona ndani ni kimya sana yani wote wamelala, akaangalia muda kwenye saa ya ukutani na kubaini kuwa ilikuwa saa nane usiku, basi akatoka chumbani kwake kwa kutembea taratibu hadi sebleni ambapo kulikuwa na simu ya mezani halafu akapiga ile namba ambayo kwa muda mfupi iliita na muda huo huo ilipokelewa na Samir, na alivyopokea tu alisema,
“Kipenzi changu Angel, kumbe unanifikiria kama mimi ninavyokufikiria!”
Angel akashtuka na kumuuliza,
“Umejuaje?”
“Yani huwezi amini nilikuwa na mawazo sana juu yako, basi nikamuomba Mungu hata muujiza utokee ili angalau nisikie sauti yako na kweli Mungu kajibu maombi yangu, ulipopiga tu nikajua lazima utakuwa wewe. Nakupenda sana Angel, nadhani hii ndio kauli yangu pekee utakayoisikia hadi siku naingia kaburini, sitoacha kukwambia ni jinsi gani nakupenda, kwakweli Angel wewe nakuona ndio kila kitu katika maisha yangu, nakupenda sana”
Angel akapumua kiasi na kushindwa hata kujibu kwani midomo yake ilikuwa ikitetemeka, basi Samir aliaendelea kuongea,
“Angel, huongei jamani kipenzi changu! Najua hata wewe unanipenda pia, kwakweli Angel katika maisha yako jua kuwa wanaume wote wanaokwambia wanakupenda basi hawakupendi kweli kasoro mimi tu, yani wewe umeumbwa kwaajili yangu na mimi nimeumbwa kwaajili yako. Nakupenda sana Angel”
Angel akajikaza na kusema jambo moja tu kwani alihofia kuja kubambwa hapo akiongea na ile simu,
“Usiku mwema Samir”
“Oooh unataka kulala kipenzi, lala ukijua kuwa nakupenda sana, mawazo yangu ni juu yako. Mimi na wewe tutajenga familia moja yenye nguvu iliyofunikwa na mapenzi ya dhati”
Kisha Samir akambusu Angel kwa njia ya simu yani Angel alifumba hadi maco kwa kupatwa na hisia na lile busu kisha akakata ile simu na kurudi chumbani kwake.
Alilala huku akitabasamu tu kwani aliona ni ufahari sana kwa yeye kupendwa na Samir.
 
SEHEMU YA 70

Kulipokucha kama kawaida walijiandaa wote na kwenda shuleni, basi Erica akiwa darasani kwao kama kawaida alikaa dawati moja na Ellyn a kuanza kumuhadithia kuhusu mapishi ya jana aliyoyafanya nyumbani kwao,
“Jamani Erica, sasa mbona hujaniletea nami nionje?”
“Aaah nimesahau jamani, yani nimesahau kabisa, nisamehe”
“Sawa nimekusamehe ila siku nyingine ukipika basi niletee nami nionje”
“Sawa, halafu mama yangu anataka kukufahamu”
“Hata mama yangu pia anataka kukufahamu, huwa namueleza kuhusu wewe basi anasema nahitaji kumfahamu huyo Erica”
“Hakuna tatizo, ipo siku atanifahamu tu”
Akasogea Abdi na kumnong’oneza kitu Erica ambapo Erica alionekana kuduwaa kwa muda basi Elly akauliza,
“Nini tena? Halafu wewe Abdi si nimekukataza maswala ya kumfata fata dada yangu!”
“Ameshindwa Erick ndio utaweza wewe!!”
“Sasa Erick ni Erick na mimi ni Elly, nione tu hivi hivi ila sitaki masikhara”
Elly alikuwa akiongea kama mtu aliyechukia sana, ilibidi Abdi aondoke tu hapo na masomo yakaendelea kama kawaida.
Wakati wa kutoka, Erica alishangaa akitafutwa na mtu ambaye alipofika alimgundua kwani ni mara kadhaa alimuona na dada yake, mtu huyo alikuwa ni Samir basi alimwambia Erica,
“Natumai unanifahamu?”
“Ndio nakufahamu, wewe ni Samir”
“Sio Samir tu bali mimi ni shemeji yako”
Erica akawa kimya basi Samir akamwambia,
“Naomba chukua huu ujumbe wangu na ukampe dada yako, tafadhali umpe dada yako tu wala asione mwingine”
Kisha Samir alimpa Erica karatasi ambayo ilibanwa na pini za kubania karatasi na kumuaga pale ambapo Erica alipanda kwenye basi la shule kurudi nyumbani kwao huku akijiuliza kuwa ile barua imeandikwa vitu gani.

Erica alifika nyumbani kwao na moja kwa moja alienda chumbani kwake kuvua sare zake za shule kisha alifungua ule ujumbe aliopewa na Samir kuwa ni wa dada yake, basi alianza kuusoma yeye, muda anamaliza kuusoma nae Erick aliingia chumbani kwa Erica na kumkuta yuko makini sana kwahiyo kama alimshtua na kumfanya Erica afiche lile karatasi, basi Erick alimuuliza,
“Unaficha nini sasa?”
Erica hakusema kitu, basi Erick akasema tena,
“Umeanza kunificha na mimi Erica?”
“Hapana kaka, ila kuna ujumbe nimesoma”
“Ujumbe gani?”
Basi Erica akamuelezea alivyokutana na Samir na jinsi alivyompa ujumbe wa kupeleka kwa dada yao, kisha alimpa Erick ausome huku akimwambia,
“Jamani dada Angel anapendwa, yani nimesoma hadi nimetamani niwe mimi ndio naambiwa hayo maneno”
“Mmmh Erica na wewe, umeanza mambo”
“Hamna, hebu soma huo ujumbe loh! Samir anampenda sana dada”
Erick nae aliusoma ule ujumbe na kuguna sababu kweli ulikuwa unamaneno mazito sana, basi Erick alimtazama Erica na kumuuliza,
“Je unaweza kupenda kama huyu anavyopenda?”
“Kwanini nisiweze? Ila nasubiri nikue maana kwa umri huu siwezi kufanya chochote kinyume na mama ila dada anapendwa jamani”
“Ila kwa kumuokoa dada yetu tafadhali tusimpelee huu ujumbe”
Kisha Erick akaondoka na ule ujumbe na kwenda nao chumbani kwake.
 
Back
Top Bottom