Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 87


Leo Erick aliwahi kurudi nyumbani tofauti na siku zote ambazo huwa anarudi na Erica, basi akabadili sare zake na kwavile alijihisi kuchoka

aliamua kuchukua zile karata zilizoletwa na Erica ili acheze kidogo.
Basi alikaa kitandani na kuzichukua ambapo alizichanga ila kuna kikaratasi kilianguka ikabidi akiokote na kukisoma,
“Nakupenda sana Erica”
Erick alishtuka mno na kujiuliza,
“Inamaana Elly ndio kamuandikia Erica huu ujumbe? Mmmh nae ameanza huu ujinga kweli!”
Erick alishangaa sana ila alimngoja Erica arudi na aliposikia tu kuwa amerudi basi aliinuka na kwenda chumbani kwake, naye alifika

chumbani kwa Erica na kufungua tu mlango yani hakugonga wala nini na kumfanya Erica apige kelele maana kifuani alikuwa wazi, ila

alipoona ni Erick alinyamaza na kujifunga na khanga kisha akamsema,
“Erick tabia mbaya hiyo, unaingia chumbani kwangu bila hodi!”
“Mbona na wewe huwa unaingia chumbani kwangu bila hodi?”
“Kwahiyo ndio umenilipizia? Muone vile”
“Ila kifua chako kimekuwa kizuri”
“Sitaki ujinga Erick, muone vile haya sema kilichokuleta”
“Chukua ujumbe wako wa kwenye karata”
Basi akampa ile karatasi na kumuuliza,
“Inamaana Elly ndio kakuandikia hivyo!! Elly si huwa unasema ni kaka yako?”
“Mmmmh aaaah karata hajanipa Elly”
“Ila alikupa Abdi eeeh!”
“Ndio”
“Nilijua tu, yani Erica unataka kuruhusu ujinga wa huyu mapema ukuharibie masomo!! Bora nilihama hiyo shule, sitaki kujiumiza kichwa,

sasa endelea na ujinga wako halafu utaona nitakacho kifanya”
Halafu Erick aliondoka zake, huku Erica akisoma kile kiujumbe kifupi na kwenda kukitupia chooni.

Mama Angel alifika kwa wifi yake akiwa na hasira sana, aliingia sebleni na kuita kwa hasira,
“Angel, Angel, Angel”
Wifi yake alitoka na kumuuliza,
“Kuna nini kwani?”
Angel nae alitoka, basi mama yake alimvuta na kumzaba kofi mbili mbili huku akimsema,
“Hivi wewe mtoto unataka hadi usikie mamako amekufa ndio utafurahi”
Shangazi yake akauliza,
“Kafanyaje tena?”
“Yani huwezi amini wifi, leo nikasema ngoja nikamuangalie Angel shule na nimchukue mwenyewe hadi dereva nikamtumia ujumbe kuwa

asiende kumchukua Angel, nilichokikuta sasa? Eti Angel yupo na yule mjinga mwenzie Samir wakielekea kwenye kituo cha daladala, mjinga

huyu kafanya leo bado kidogo tu nipate ajali jamani”
“Kheee pole wifi yangu jamani”
Kisha Shangazi akamuangalia Angel na kumuuliza,
“Inamaana Samir nae anasoma hapo shuleni kwenu?”
“Ndio shangazi, hata mimi sikujua kumbe aliahamia pale”
“Haya niambie imekuwaje mpaka ukaongozana nae kurudi nyumbani”
“Shangazi ni hivi, mimi na Husna tulipanga leo kurudi pamoja tu, ila Husna akaumwa gafla na kurudi kwao basi wakati wa kutoka ikabidi tu

niondoke mwenyewe, ila dereva hahusiki kwa hili maana nilimdanganya kuwa asije kunichukua, ila wakati naondoka gafla alikuja Samir ila

kweli kabisa shangazi sikutaka kuongozana nae”
“Haya, nenda chumbani kaendelee na ratiba yako ya leo”
Mama Angel alimshangaa wifi yake kujibu kirahisi hivyo, pia alishangaa mwanae kwa mpangilio wa lile jibu na kumuuliza wifi yake,
“Una uhakika alichokujibu ni cha ukweli?”
“Mimi sitaki kumjengea mtoto mazingira ya uoga ila namjengea mazingira ya kuniheshimu, na nikisema nitakupiga basi ujue nishampiga

maana sina msemo wa nitakupiga, atazoea na kujua ni uongo tu. Halafu huwa nawafundisha kuwa wakweli maana mimi ni mchunguzi kupita

unavyoelewa, kwahiyo swala la Angel niachie mimi mwenyewe tu kwani huyu Angel nitamnyoosha, kama alikuwa akikudanganya ni wewe

maana mimi sidanganywi kirahisi namna hiyo”
“Kheee saa wifi tufanyeje? Tumuhamishe shule au?”
“Hapana wala usiingie gharama nyingine wifi yangu ila mimi nitakula nae sahani moja huyu hata usiwe na mashaka wifi yangu”
Mama Angel alikaa sasa akapumua kisha wifi yake aliamua kumletea juisi ili ashushie na zile hasira alizokuwa nazo.
Aliongea kidogo tu na kuaga maana dereva alimuacha ndani ya gari.


 
SEHEMU YA 88


Mama Angel alipofika na dereva nyumbani kwake aliamua kumwambia sharti lake kuu,
“Ni lazima kumpeleka Angel shule na kwenda kumchukua hata akisemaje ni lazima kufanya hivyo”
“Sawa mama nimekuelewa”
Basi mama Angel aliingia ndani na kumkuta Vaileth akipika, basi alimuuliza,
“Dada, unapika nini leo?”
“Wali dada, njegere na nyama. Si shemeji atakula?”
“Atakula ndio maana huwa anapenda”
Kisha mama Angel aliondoka ila Vaileth alimuita na kuongea nae kidogo,
“Mama samahani, kuna ndugu yangu anataka kuja kunitembelea?”
“Anataka kuja lini?”
“Jumapili mama”
“Sawa hakuna tatizo, anakaribishwa”
“Asante mama, ila ataondoka Jumatatu”
“Sawa hakuna tatizo”
Kisha mama Angel akaenda zake chumbani kupumzika kwani alikuwa na mawazo yake ya kutosha tu ukizingatia kilichotokea siku hiyo.
Baada ya muda kidogo tu mumewe alirudi na kugundua kuwa mke wake amechoka ila alimuamsha na kuanza kuongea nae ambapo mama

Angel alimueleza yaliyotokea siku hiyo,
“Duh mke wangu hadi nakuonea huruma jamani, huyu Angel atakutoa kizazi mweeeh!! Hebu nizalie mie wadogo zake, acha habari za

kumfatilia Angel”
“Ila una nini mume wangu jamani! Kwahiyo Angel akileta mimba hapa nyumbani itakuwaje?”
“Nitaelea”
“Kheeee!!”
Mama Angel alichukia na kuinuka kisha moja kwa moja alienda chumbani kwa Angel kwahiyo alimuacha mumewe chumbani akiwa

mwenyewe.
Ilibidi mume wake amfate kwani kitu ambacho huwa hapendi katika maisha yake ni kugombana na huyu mwanamke,
“Sasa mke wangu unataka kuweka picha gani kwa watoto jamani eeeh! Hebu turudi chumbani”
Basi mama Angel aliinuka na kurudi chumbani, kisha mumewe alianza kumuomba msamaha ambapo mama Angel alikuwa kajinunisha tu

kisha mumewe akamwambia,
“Mama Angel, nilishakwambia na bado nakwambia kuwa wanaume kama mimi katika dunia hii tupo wachache sana na labda nimebaki

mwenyewe, mwingine labda atakuwa na masalia yang utu, mke wangu sipendi kukukera, sipendi uchukie, sipendi unune kwani tabasamu

lako ndio afya kwangu. Nakupenda sana mke wangu, ila nilikuwa naongea tu ili hawa watoto tusiwafatilie kivile, tuwafatilie ndio ila sio kwa

stahili hiyo ambayo unaifanya, kwakweli itakutesa mwenyewe mke wangu, nakupenda sana. Naomba unisamehe”
Kisha baba Angel alimbusu mama Angel, naye mama Angel alitabasamu kuonyesha kwamba ule msamaha kaupokea vizuri kabisa, kisha

walianza kushirikiana kwenye mambo mbalimbali.


 
SEHEMU YA 89

Muda wa kula walitoka na kwenda kula pamoja na familia ila leo walikula chakula ambacho kiliandaliwa na Vaileth, kwakweli Vaileth nae

alifurahi sana kwani alipenda mno kumuona baba mwenye nyumba akila kile chakula chake huku akitabasamu.
Basi Erica na Erick nao walipomaliza kula waliinuka ili kuondoka zao ila mama Angel alimuita Erick na kumwambia,
“Mwanangu naomba kesho uamke mapema unioshee gari yangu, sawa baba eeeh!!”
“Sawa mama hakuna tatizo”
Basi waliawaaga wazazi wao pale na kila mmoja aliondoka zake na kuelekea vyumbani kwao ila Erick alivyofika chumbani kwake tu

alichukua zile karata ili ampelekee Erica.
Alivyofika tu akamwambia Erica,
“Chukua karata zako hizi urudishe kwa huyo kichaa wako”
“Jamani Erick, usiseme hivyo, njoo tucheze pamoja”
“Hapana, siwezi cheza karata za huyo mpuuzi”
“Basi tusicheze karata, ila njoo tusimuliane mambo mbalimbali”
Basi Erick alitulia na kwenda kukaa kitandani kwa Erica kisha walianza kuongea mambo mbalimbali yanayoendelea, ambapo Erica alianza

kwa kumuuliza Erick,
“Hivi mama na baba leo walienda kwa dada Angel kufanya nini?”
“Mmmmh jamani, mimi nitajuaje hayo? Niliwaona tu wakienda ila sijui walienda kufanya nini”
“Ila baba na mama wanapendana eeeh!!”
“Ndio wanapendana, hivi Erica unajaribu kuniambia nini? Hebu tucheze karata tu”
“Basi, twende tukacheze karata chumbani kwa dada Angel”
Erick alikubali na moja kwa moja waliondoka nakuelekea chumbani kwa Angel, walikaa kitandani na kuanza kucheza zile karata. Walicheza

sana hadi mwisho wa siku wakachoka na ilikuwa ni usiku sana yani kila mmoja alijikuta akilala palepale huku karata zipo pembeni yao,

kwahiyo kwa siku hiyo walilala chumbani kwa Angel.

Kulipokucha asubuhi na mapema, basi baba Angel alijiandaa na kuonoka zake kuelekea kwenye shughuli zake, mama Angel nae aliamka

na kutoka ambapo alimkuta Vaileth tayari kashafanya usafi wa ndani na moja kwa moja alienda nje kisha akarudi ndani na kuanza kuongea

nae,
“Hivi Erick bado hajaamka eeeh!”
“Bado mama”
“Nilimwambia jana kuwa leo aamke mapema na aoshe gari yangu halafu kumbe kalala mpaka muda huuj”
“Si unajua mama leo ni mapumziko, nadhani analipiza siku alizoenda shule”
“Wakati jana waliwahi kulala, na Erica nae!”
“Hajaamka pia”
“Mitoto mijinga sana hii”
Kisha mama Angel alienda zake moja kwa moja chumbani kwa Erick ila alishangaa kutokumuona wala nini, akashangaa kuwa kaenda wapi

na kujiuliza kuwa pengine kaamka, basi moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ila napo hakuwakuta yani akawaza na kujiuliza sana,
“Hawa watoto wameenda wapi jamani!!”
Hakupata jibu na kuamua kurudi tena kwa Vaileth na kumuuliza kama kawaona,
“Kwani hujawaona Erick na Erica?”
“Sijawaona mama, kwani vyumbani mwao hawapo?”
“Hawapo ujue, watoto wehu hawa jamani”
Ilibidi mama yao atoke na kwenda kumuuliza mlinzi wa getini kama amewaona labda wakitoka.



 
SEHEMU YA 90


Erica ndio aliyeanza kushtuka na kumshtua Erick ambapo alimwambia,
“Erick amka, Erick amka”
Erick akaamka na kushangaa na kugundua kuwa walilala chumbani kwa Angel, kisha alimwambia,
“Kheee kumbe tumelala chumbani kwa Angel? Hivi ni saa ngapi saa hizi?”
Erica aliangalia saa ya ukutani kwa pale chumbani na kumwambia Erick,
“Kheee ni saa tatu”
Basi Erick alikurupuka pale kitandani na moja kwa moja alitoka kuelekea chumbani kwake ambapo Erica nae alitoka kuelekea chumbani

kwake pia na kwenda kuoga moja kwa moja.
Erick alitoka chumbani na kumkuta mama yake sebleni akionekana kuwa na mawazo sana, akamsalimia kisha mama yake akamfokea na

kumuuliza,
“Mjinga wewe, mbona nimekuja chumbani kwako sijakukuta?”
“Mbona nilikuwa chooni mama”
“haya, nenda kaoshe gari yangu mjinga wewe”
Basi Erick alitoka na kwenda nje moja kwa moja kuosha gari ya mama yao ambayo aliambiwa kuwa aende kuiosha.
Ericanae alimkuta mama yake sebleni ambapo alijibu kamaErick utafikiri waliambizana kujibu vile, basi mama yao alikuwa amechukia sana

na kuwafokea,
“Mmeniudhi sana leo, huko chooni ni choo gani hiko kinachofanya niite na msinisikie? Haya nenda kaoshe vyombo maana nilimwambia

kuwa daa asioshe, leo ni zamu yako”
Basi Erica alienda zake kuosha vyombo ambapo mama yao sasa ndio aliweza kwenda kujiandaa kwaajili ya kutoka yani ambavyo

hakuwaona watoto wake alianza kujihisi vibaya katika moyo wake.
Basi alipomaliza kujiandaa naye Erick alikuwa amemaliza kusafisha gari ambapo mama yake alipanda na kuondoka nalo kwani kuna mahali

alikuwa anawahi kwa siku hiyo.
Basi pale nyumbani walibaki Erick na Erica pamoja na Vaileth kwahiyo siku hiyo wakaitumia kama siku yao ya kuangalia video mbalimbali

maana mama yao anayewakataza hakuwepo kwa siku hiyo.

Basi mama Angel alifika kwenye shughuli zake na kushughulikia vizuri tu ambapo kwa kipindi hiko kulikuwa na mazao ambayo aliyafatilia,

wakati anamaliza zile shughuli zake alishangaa mtu kumuita,
“Erica”
Basi alisimama na kumuangalia ila hakuwa na kumbukumbu kama amewahi kuonana na mtu huyu, basi alisalimiana nae na kuanza

kuulizana nae,
“Samahani sijui tulionana wapi?”
“Mmmh najua huwezi kunikumbuka, siku zote mala ndizi hakumbuki ila mtupa maganda ndio huwa anakumbuka.”
“Kwani nani wewe, samahani jamani?”
“Kuna kipindi zamani kabisa ulikuwa na matatizo, mwanaume wako alioa na ukaja mtaani hadi ukazimia, ni mimi niliyekupeleka na tukawa

tukikutana stendi ulipokuwa ukifanyia kazi”
“Ooooh nimekukumbuka sasa”
Mama Angel alimkumbuka mwanamke huyu kama aliwahi kuonana nae, basi yule mwanamke alianza kumueleza mambo ya kale ambayo

kwa mama Angel yalibaki kama historia.
“Basi yule mwanamke aliachwa, na Bahati akaoa mwanamke mwingine ila amezaa watoto wengi huyo balaa na wanawake tofauti tofauti”
“Mmmmh!”
“Ndio hivyo, yani Bahati ana watoto wengi tena wa kila rangi na asipokuwa makini basi watoto wake wanaoana”
Mama Angel alizidi tu kumshangaa mwanamke huyu ambapo aliendelea kuongea,
“Basi ana mtoto anaitwa Abdi, ni katoto kadogo ka kidato cha kwanza ila mtoto huyu ni hatari, yani mtoto mdogo ila anatembea na

wanawake wakubwa kwa wadogo”
Mama Angel akashtuka kidogo kwani jina la Abdi amewahi kulisikia kabla, kwahiyo alijikuta akiogopa kwakweli na muda huo huo aliagana

na yule mwanamke ambapo alihitaji mawasiliano nae na alimpatia basi akaondoka zake ila alijikuta akitafakari sana kuhusu Abdi.

ITAENDELEA

 
SEHEMU YA 91

Mama Angel alivyorudi nyumbani kwake ilikuwa tayari ni usiku kwahiyo alishindwa kuongea na watoto wake kwani aliwakuta tayari wamelala, ukizingatia walichoka sana na usiku wa jana walichelewa sana kulala.
Muda kidogo mumewe nae alirudi na kwenda nae chumbani ambapo alimuuliza,
“Mbona siku hizi Jumamosi unachelewa sana kurudi?”
“Hata wewe umechelewa leo mke wangu, kumbuka nilikupigia simu ukasema bado hujarudi nyumbani, sasa niwahi kurudi halafu niwe na nani?”
“Si unacheza hata na watoto”
“Ooooh umeniambia jambo jema sana, Jumatatu asubuhi kuna sehemu tutaenda”
“Sehemu gani tena?”
“Nitakwabia tu hata usijali mke wangu”
Kisha siku hiyo baba Angel alimtaka mkewe wajiandae tu na wakale nje na nyumbani kwao kwahiyo walifanya vile na kuondoka zao.
Vaileth alibaki nyumbani kama kawaida ila kiukweli alitamani sana maisha aliyoyaona kwa baba Angel na mama Angel basi alikaa na kuanza kukumbuka maisha yake ya nyumba,
“Hivi watu wengine tukoje jamani! Huwa tunakosa bahati kama hizi kwanini? Nakumbuka mimi mwanaume aliyenizalisha, yani siku niliyomwambia nina mimba yako basi ndio ukawa mwisho wa mawasiliano yetu, nimeishi kwa shida mwanzo mwisho, nikiomba kazi za ndani wananikatalia sababu ya kuwa na mtoto mdogo. Nikaamua kumuacha nyumbani ila bado nilikuwa sipati kazi za ndani, ila huyu mama Angel katokea kama bahati kwangu, ila kawezaje kupata familia yenye upendo kiasi hiki!! Hadi raha jamani, natamani na mimi ningekuwa na maisha haya. Ila nadhani mama Angel ni kati ya wanawake waliojitunza na mwisho wa siku wamekuja kufurahia maisha, ila na mimi mbona nilijitunza sana? Ila niliyempata ndio akaniharibia maisha mazima kabisa, sijui wengine tuna gundu jamani loh!!”
Alikuwa akiongea huku akiumia sana moyoni mwake, kwakweli aliyapenda sana maisha ambayo mama Angel na mumewe waliishi na jindi ambavyo walipendana na kusikilizana.

Mama Angel na baba Angel waliporudi tu ni moja kwa moja walienda kulala maana walishashiba tayari, basi asubuhi waliamka na kuamsha watoto wao kisha kujiandaa na kwenda nao Kanisani.
Vaileth alitulia huku akiwasiliana na ndugu yake namna ya kufika mahali hapo sababu ndugu yake huyo alihitaji kuja kumtembelea, na jinsi alivyomuelekeza haikuwa ngumu sana kwani yule ndugu wa Vaileth alifika pale vizuri kabisa na alimkuta Vaileth getini akimsubiri.
Basi Vaileth alimkaribisha vizuri kabisa, na yule ndugu alikuwa akishangaa tu uzuri wa ile nyumba,
“Kheee jamani Nyanda ndio unaishi kwenye nyumba nzuri kiasi hiki!!”
“Weee halafu nilisahau kukwambia, mwenzio mjini nimezoeleka kwa jina la Vaileth. Hilo jina lenye gundu nililiacha kijijini”
“Kheee nitazoea hilo jina lako jipya kweli?”
“Mbona rahisi tu, sema Vai”
“Oooh sawa, ila bora mimi nilipewa jina zuri toka zamani”
“Ndio jina lako ni zuri lakini umesahau bibi anavyokuitaga? Yani bibi haiwezi hiyo Prisca anaita Purisika”
Basi wote walianza kucheka na kuongea mawili matatu huku akimuuliza alipofikia,
“Si nimefikia kwa Shangazi, ndio nikasema nahitaji kumsalimia Nyanda ndio akanipa namba zako. Ulipataje bahati ya kupata kazi kwenye nyumba nzuri hivi ndugu yangu?”
“Yani hii bahati acha tu, halafu nyumba hii usifikiri ni uzuri wan je tu, jamani hadi watu wa humu ni wazuri na wana roho nzuri sana, yani kazi za humu unadhani nafanya peke yangu basi!! Mama akiwepo tunasaidiana, watoto wa humu ndani wanaweza kazi zote, si wa kiume, si wa kike yani hakuna kazi inayowashinda, tofauti na nyumba zingine za matajiri ila hii ni mwisho”
“Ooooh hongera sana, na mimi nahitaji kazi za ndani ila kwenye nyumba kama hii”
“Si mpaka upate hiyo bahati!! Ni mimi tu nimejaaliwa, yani nyumba hii kwakweli imebarikiwa na Mungu, hapa unavyoona ni wote wameenda kusali, wanapenda ibada hao balaa”
Basi Prisca nae alijikuta akiyapenda maisha yanayoendelea kwenye ile nyumba kwa kuhadithiwa tu na Vaileth.
 
SEHEMU YA 92

Siku hii Tumaini nae na familia yake, walienda Kanisani na kurudi kwa pamoja, ila kama ambavyo Angel aliomba kuwa abadilishiwe ratiba basi Tumaini alimwambia kuwa awapikie chakula siku hiyo maana Angel alionekana kuwa na hamu ya kupika. Angel aliwapikia chakula kile na kukiandaa mezani ila walifika wageni wawili ambao walikuwa ni rafiki wa mume wa Tumaini na kula kile chakula kwa hakika wote walikisifia kuwa ni kizuri sana, jambo lile lilimfanya Tumaini ampende Angel maradufu, basi wakati wameenda jikoni akamwambia Angel,
“Angel mwanangu ukiendelea hivi kwa hakika utaolewa na mwanaume mzuri kama baba yako Erick”
Angel alitabasamu tu, kisha shangazi yake akaendelea kumwambia,
“Ila mwanangu unatakiwa kuwa mpole na mtulivu ili kumpata mume mwema”
Angel akaitikia na kwenda kutoa vyombo ambavyo walikuwa wanatumia wale wageni, ila katika wale wageni kuna mmoja wapo alikuwa akimuangalia sana Angel yani alikuwa akimuangalia kila kitu alichokifanya.
Na baada ya muda waliaga kuwa wanaondoka sababu muhusika hawakumkuta, basi waliwapa mikono ambapo yule mgeni aliposhika mkono wa Angel alimtekenya huku akitabasamu, ila Angel alibaki tu kumshangaa, kisha Tumaini aliwasindikiza wale wageni

Walipotoka Kanisani, familia ya mama Angel waliamua kwenda kidogo ufukweni kupata upepo na badae kidogo walirudi nyumbani kwaajili ya maandalizi ya kesho yake, Vaileth aliwatambulisha kwa yule mgeni wake na wao walimkaribisha vizuri tu kwa upendo kisha wote kwenda kulala tu.
Kulipokucha kama walivyopanga basi waliamka tu kwenye saa mbili asubuhi na kujiandaa kisha kuondoka pamoja, ila gari ya baba Angel ilielekea hospitali moja kwa moja na kumfanya mkewe aulize,
“Mbona tunaenda hospitali sasa?’
“Ndio tunaenda hospitali, hapa kuna dokta mzuri sana wa wanawake, nahitaji akakuangalie wewe kama una tatizo lolote maana nilishaongea nae, na leo hiko kijiti chako akitoe ili unibebee mimba”
Basi mama Angel hakusema neno lingine lolote zaidi zaidi ya kukubali atakavyo mume wake.
Basi waliingia pale hospitali na moja kwa moja walienda kwa dokta, kwakweli mama Angel alishtuka sana kumuona huyu dokta kwani ni mtu aliyekuwa akimfahamu vizuri tu.


Basi mama Angel hakusema neno lingine lolote zaidi zaidi ya kukubali atakavyo mume wake.
Basi waliingia pale hospitali na moja kwa moja walienda kwa dokta, kwakweli mama Angel alishtuka sana kumuona huyu dokta kwani ni mtu aliyekuwa akimfahamu vizuri tu.
Basi yule dokta akampa mkono mama Angel ila mama Angel alisita kutoa mkono wake na kumtaka mumewe waondoke, mume wake alimshangaa pia,
“Kwani kuna nini mke wangu jamani!!”
“Siwezi kuongea chochote na huyu dokta maana atafanya nibebe mimba ya utosi”
“Kwani kuna nini? Mnafahamiana?”
“Ndio”
Kisha mama Angel akatoka nje, ikabidi baba Angel amuombe msamaha daktari halafu akamfata mkewe nje, kwakweli mama Angel wala hakutaka kubaki tena kwenye ile hospitali hivyobasi ilibidi mumewe nae aondoke nae, waende mahali ili akamueleze ni kwanini hataki kutibiwa na yule dokta.
Walivyofika tu, walikaa na muda huo huo baba angel akamuuliza mke wake,
“Kwani tatizo ni nini?”
“Nadhani wewe, umesahau ila nitakukumbusha. Yule dokta anaitwa dokta Doroth, katika maswahibu yangu ya kipindi kile cha ujana nilishawahi kuongopa kuwa tumbo linaniuma wakati ametokea Rahim, nakumbuka ulinikimbizia hospitali ila haikuwa hospitali ile nadhani kahamia pale. Basi nilimkuta yule dokta na kumuomba akuongopee na kusema ninavidonda vya tumbo ila alitaka hela nyingi sana kwa mimi kusema uongo, kwakweli aliniumiza mno, naweza sema kuwa yeye ndio chanzo hadi niliosha vyombo vya hoteli mimi”
Mumewe nae alionekana kuanza kukumbuka,
“Ooooh sasa nimekumbuka vizuri kabisa, pole mke wangu kwa kukukumbusha matukio ambayo yalipita”
“Asante”
“Basi nikupeleke kwa yule dokta rafiki yangu”
“Naona umenichoka sasa baba Angel jamani, mimi naomba jambo moja tu. Kesho nitaenda mwenyewe hospitali na kutoa hiki kijiti, naomba wala usihangaike kutafuta madokta mume wangu tafadhari”
Basi baba Angel alimuangalia tu bila ya kusema chochote kile.
 
SEHEMU YA 93

Basi leo Prisca alianza kuongea na Vaileth kuhusu ile nyumba ya mama Angel kwani kwa muda huo hakukuwa na mwingine kwenye ile nyumba zaidi yao tu,
“Ndugu yangu Nyanda usiwe mjinga, hebu angalia mjengo huu jamani!! Inafaa kabisa wewe kuwa mmiliki wa mahali hapa”
“Loh Prisca hebu niondolee dhambi hizo za lazima jamani! Yani unamaana nimpindue mama mwenye nyumba?”
“Ndio mpindue ili wewe ubaki kuwa mama mwenye nyumba”
“Jamani Prisca unaongelea vitu gani jamani, hebu achana na huo ujinga”
“Wewe ndio mjinga Nyanda, unaacha kujipatia mali hizi!! Umeweza kubadili jina ila kwanini huwezi kufanya vitu vya msingi kama hivi!!”
“Sikia nikwambie jambo Prisca, watu kama nyie ndio huwa mnafanya wenye nyumba waseme kuwa wadada wa kazi wana nia mbaya na nyumba zao kwa kuchukua waume zao. Sikia jambo, huwa mama mwenye nyumba namuheshimu sana na ninampenda, hata yeye ananiheshimu na kunipenda ndiomana ananiamini kuniacha na nyumba yake, kingine watoto wake wananiheshimu sana na kunipenda, ni kweli naonea wivu familia hii jinsi walivyo na upendo ila hiyo sio sababu ya mimi kumpindua mama mwenye nyumba. Nataka hizi mali, najua wamechumaje? Najua wameanzia wapi? Hata msingi wa nyumba najua ulivyowekwa? Sawa, tufanye mfano nilikuwepo au nilishiriki kwenye ujenzi, je hiyo inamaana kuwa nyumba ni yangu? Unajua mara nyingine utu ni bora kuliko mali, nawapenda hii familia ni kama familia yangu naamini na mimi ipo siku nitapata mume mwema atakayenijali na kunithamini”
Prisca akacheka sana na kumwambia,
“Huyo mume mwema utampata vipi na ushazalishwa? Hakuna mwanaume anayependa mwanamke mwenye mtoto, hakuna nikwambie, yani hayupo mwanaume anayeweza kulea damu isiyo yake, hapo ni kufanya ndumba tu ili umpate”
“Kama ni hivyo basi jamii nzima itakuwa imejaa ushirikina maana kwasasa ni asilimia kubwa ya wanawake wamezalishwa na wanaume wamewakimbia. Ila mimi siamini kuhusu hilo, naamini mtu akipenda boga basi anapenda na ua lake, najua akinipenda basi atampenda na mwanangu”
“Naona hilo jina la vaileth limekuharibu, unanikera mimi”
“Pole sana ila huo ujinga sahau, siwezi kufanya kabisa, humu ndani nawaheshimu na kuwathamini najua nami Mungu atanisaidia nitapata mume mwema na kuanzisha nae familia ila kwasasa nipo mafunzoni. Nipo kujifunza maisha ila sio kuiba waume za watu”
Basi Prisca alichukia sana, na Vaileth alienda kumalizia kazi zake ili aweze kumsindikiza.
 
SEHEMU YA 94

Erica alikaa darasani akiendelea na masomo yake, Abdi akasogea kumnong’oneza,
“Ujumbe wangu uliuona”
Erica alimwambia jambo moja tu,
“Sitaki huo ujinga Abdi, naomba niache na kesho nakuletea karata zako”
Maana alikumbuka jinsi kaka yake alivyochukia kuhusu ule ujumbe, basi Erica aliendelea na masomo kama kawaida, kuna muda alihisi haja ndogo basi akainuka na kwenda maliwatoni.
Alipomaliza kujisaidia alishangaa wakati akitoka akakumbana na Abdi mlangoni ni kama alikuwa akimaliza ajisaidie, basi alimuuliza,
“Unafanya nini kwenye vyoo vya kike?”
Abdi hakujibu bali aliingia na Erica kwenye kile choo na kufunga mlango huku akimwambia,
“Nakupenda sana Erica, niamini nakupenda sana”
“Kheee wewe una wazimu au? Niache bhana, nitapiga kelele”
“Piga tu hizo kelele, si hunitakii mema utakuwa, pengine hutaki kuniona hapa shuleni ila nakupenda sana”
Halafu Abdi akamsogelea Erica mdomoni na kuanza kumbusu, muda huo Erica alikuwa akipambana na Abdi mule chooni ilia toke na mtindo wa vyoo vya shule ile hata ukipiga kelele chooni ni sawa na bure tu yani hakuna aliye nje ambaye atasikia zaidi ya mtu ambaye yupo kwenye korido ya choo, na kwa muda huo wanafunzi wote walikuwa darasani.
Erica alianza kupiga kelele ili Abdi amuachie basi Abdi alicheka na kumwambia,
“Kumbe hujui eeeh!! Humu chooni hakuna sauti inayotoka nje, yani sauti zote zinaishia humu humu ndani, cha kufanya nikubalie tu, onyesha ushirikiano ili wote twende darasani”
“Sasa ushirikiano gani unaousemea Abdi jamani!”
“Naomba nione kifua chako tu nitaridhika”
Erica alikuwa akimshangaa sana Abdi ila bado hakuweza kufunua kifua chake, na kujaribu kuendelea kupiga kelele ingawa alijua hazifiki popote ila Abdi alikuwa na nguvu kidogo na kumshinda nguvu Erica kwani alifanikiwa kumfunua sketi yake ila gafla mlango wa kile choo uligongwa na pale Erica kuona kuwa usalama wake umefika, mlango uligongwa sana na Abdi akamziba mdomo Erica ila alishangaa kusikia sauti ya Elly,
“Fungua mlango Erica, nimesikia sauti yako”
Erica alipambana ili wafungue mlango ila Abdi alimshinda nguvu na kutokufungua mlango basi Elly akamwambia,
“Naenda kuita mwalimu ilia je avunje huu mlango”
Ila muda huo huo Elly alitumia nguvu zake za ziada na kusukuma ule mlango hadi kitasa kilijiachia na ulifungua, cha kwanza alimvuta Abdi na kumpiga ngumi ya pua ambayo ilipoteza mawasiliano kabisa kwenye pua ya Abdi na kumfanya Abdi aanze kutokwa na damu puani, ila hilo halikuwa tatizo kwa Elly kwani yeye cha muhimu kwake ilikuwa ni kumuokoa Erica tu.
Kulikuwa na mwalimu anapita karibu na kile choo cha wasichana kwahiyo alisikia ule ugomvi na kuingia ila alikuta Abdi akitokwa na damu mfululizo basi ilibidi awachukue wote kwenda ofisini ambapo alimpigisha Elly magoti na Erica nae alitakiw akujieleza huku Abdi akipewa huduma ya kwanza.
“Kwanza, wewe Elly choo cha wasichana ulikuwa unatafuta nini?”
“Sikia mwalimu, mimi toka siku ya kwanza nilimumwambia Erica kuwa nitakuwa nikimlinda na kumtetea kwani mimi ni kaka yake na tulikubaliana hivyo, ila leo sikuelewa huyu Abdi alikuwa ananyemelea nini kwa Erica, basi kuna muda Erica alitoka darasani nikahisi lazima ameenda chooni, muda kidogo Abdi nae akatoka nikawa nahisi kitu, basi nilivyoona Erica anakawia kurudi nikaamua kwenda chooni kwao kuangalia imekuwaje ndio nikakuta Erica akipiga kelele, niliwasihi wafungue mlango ila Abdi aligomea usifunguliwe basi nikaamua kuuvunja, nisamehewe kwa hilo tu naye Abdi alipotoka nilimpiga ngumi moja ya pua”
“Hivi una akili wewe? Umeshindwa kuja kushtaki? Kati yaw ewe na Abdi unadhani ni nani mwenye makosa? Kwanza umeingia choo cha kike, pili umevunja mlango, tatu umempiga mwenzio”
“Ila mwalimu Abdi alitaka kumbaka Erica”
“Una uhakika gani juu ya hilo? Hebu kuwa na huruma, unatakiwa uje na mzazi wako mjinga wewe”
Kisha mwalimu alimchapa Elly kwa fimbo za kutosha tu, na kumwambia kuwa aondoke nyumbani hadi aje na mzazi wake, muda huo Erica alikuwa akitetemeka sana na kusema kuwa hawezi pia kuendelea kubaki shuleni kwani hana amani, mwalimu yule naye akamfokea sana,
“Ujinga ujinga tu, huna amani kitu gani? Huyu Abdi angeota kuwa unaenda chooni? Na wewe ondoka zako na ukamuite mzazi wako, waje waseme ni malezi gani amekupa wewe mtoto wake”
Mwalimu mwingine akadakia pembeni,
“Uwiii mzazi wa Erica usimuite tafadhari kwa kesi za kijinga hivi, mama mtata yule, akifika hapa yani walimu wote tutaipata unajua Angel alimuahamisha kivungu pia”
Ndipo pale yule mwalimu alipoelewa kuwa mzazi wa Erica ndio mzazi wa Angel basi akamwambia tu aende akapumzike nyumbani siku hiyo.
 
SEHEMU YA 95

Erica aliondoka na Ellyna kutaka aende nae kwao ili akaongee na mamake Elly ila Elly akamwambia,
“Usijali Erica, kwanza mama yangu hayupo”
“Jamani, roho inaniuma sana. Pole Elly jamani, yani umepata matatizo sababu yangu”
“Usijali, labda nikusindikize tu kwenu”
“Hamna usijali, mimi nachukua bajaji inipeleke nyumbani halafu ataenda kulipwa kule kule, usijali”
Basi Elly alimsindikiza tu Erica hadi kwenye bajaji halafu yeye akaondoka zake kurudi nyumbani kwao.
Erica alienda na bajaji hadi kwao, basi alivyofika alimuuliza tu dereva ni kiasi gani cha pesa kisha akaingia ndani na kwenda kumwambia Vaileth ambapo alimpatia hiyo pesa na akaenda kulipa ile bajaji na kuingia ndani. Muda huu vaileth ndio alimuuliza,
“Kwani tatizo ni nini Erica?”
“Dada, nitakusimulia ila bado natetemeka yani sina amani kabisa, leo yangesikika mengine”
“Kivipi mdogo wangu?”
“Naomba nikapumzike dada”
Halafu alienda zake chumbani, basi Prisca akaanza tena kumuhoji Vaileth,
“Kwahiyo hadi unaweka hela za akiba?”
“Ndio”
“Sasa huyu mtoto katoka wapi na bajaji hadi kalipa elfu saba?”
“Katoka nayo shuleni kwao”
“Kheee kwahiyo ni kawaida hiyo?”
“Hapana ni dharula kama leo, huwa anarudi na gari la shule mbona”
“Kwahiyo huyo bosi wako akija utamwambiaje?”
“Huyu mama mwenye nyumba ni mwelewa sana, hujui tu unamuongelea mtu gani. Inuka nikusindikize sasa”
Basi Prisca aliinuka ila hadi anatoka nje ya ile nyumba alikuwa akiishangaa tu jinsi ilivyokuwa, kwakweli ilimvutia mno kwa uzuri wake kwani ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia.
Yani muda wote wanatembea barabarani bado aliendelea kuisifia ile nyumba na kumtaka Vaileth afanye jambo kwajili ya kumdaka baba mwenye nyumba,
“Yani Prisca naomba uachane na hizo habari”
“Nitaachana nazo ndio ila hata shangazi nitamwambia kuhusu hili, yani sisi tunakufa na umasikini wakati wewe unauwezo wa kuchota utajiri tu hapa”
“Ni bora niwe masikini maisha yote ila sio kuiba mume wa mtu, haswaaa mume wa mama Angel, kamwe sitafanya huo ujinga”
Basi aliachana na ndugu yake akipanda daladala la kurudi kwao huku yeye akirudi anapofanyia kazi.
 
SEHEMU YA 96

Angel leo alitulia darasani kwani hakutaka tena makubwa yamkute kwa siku hiyo ukizingatia shangazi yake kashampa onyo hadi basi, alikaa darasani na kuendelea na masomo ya hapa na pale, hata Samir nae aliendelea na masomo yake ila muda wa kutoka kuna ujumbe Samir alimuandikia Angel na kumuwekea Angel kwenye daftari.
Sababu walikuwa wakitoka basi Angel akaona kuwa ni vyema asome ule ujumbe akiwa nyumbani kwao, basi dereva alivyoenda kumchukua aliondoka nae tu na kurudi kwa shangazi yake.
Kufika kwa shangazi yake, aliingia sebleni na kumkuta shangazi yake basi akamsalimia na kutaka kwenda chumbani ila shangazi yake alimuita,
“Angel, naomba begi lako hilo”
Ilibidi Angel avue begi lake na kumpa shangazi yake ambaye alifungua na kutoa lile daftari ambalo Samir alimuwekea ujumbe Angel, akalifunua lile daftari na kutoa ule ujumbe kisha akarudisha lile daftari na kumwambia Angel aende chumbani tu.
Kwakweli Angel alienda chumbani huku akijiuliza mno inakuwaje shangazi yake kajua kuhusu hiyo barua? Au mtu aliyesema ameangaliana sana na Samir ndiye aliyemwambia kuhusu ile barua? Alijikuta akijiuliza bila jibu lolote, na je huyo mtu anayemfatilia ni nani? Hakuelewa kwakweli.
Muda kidogo shangazi yake alienda chumbani na kuanza kuongea nae,
“Angel mwanangu, wewe ni binti mzuri na unavutia sana unaweza sema wazazi wananifatilia sana hapana, tunataka kukutengenezea maisha bora binti yangu. Mwanaume anayekupenda kweli atasubiri umalize shule ndio aanze propaganda zake za kukupenda ila anayekusumbua wakati wa masomo ujue huyo hakupendi wala nini. Kuwa makini sana binti yangu, sipendi kuona ukiishia kati eti sababu ya mimba sijui sababu ya mapenzi, napenda usome kama sisi tulivyosoma. Angel upo vizuri mwanangu na tena umeanza kupendwa toka utotoni, yani wewe una akiba zako benki za kutosha tu ila bila akili ni sawa na bure mwanangu, vitu vyote hivi vinataka akili, jitahidi sana ujue jinsi ya kutunza maisha yako. Jitunze na maisha nayo yakutunze, usipokuwa na akili, huo uzuri wako ni sawa na bure, yani kila mtu atakuona kinyago. Tulia mwanangu, mapenzi yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, tuliza akili hizo na ukae mbali na Samir, jicho langu ni kali sana nilikwambia ukiwa tena karibu na Samir nitakufanyaje?”
“Ulisema utanifanya unachojua wewe”
“Eeeeh ndio, nitakufanya ninachojua mimi. Nataka uishi vizuri, uwe mtoto mzuri na uzuri wako wa asili usipotee. Haya endelea na ratiba ya leo”
Shangazi yake aliondoka, kwahiyo Angel hata hakujua kuwa ile barua ilisema vitu gani sababu hakuisoma wala nini.

Mama Angel alirudi mwenyewe kwani kuna mahali aliachana na mumewe, kwahiyo yeye moja kwa moja alienda zake nyumbani kwake, basi alimkuta Vaileth ambapo baada ya salamu Vaileth alimuelezea jinsi Erica alivyorudi siku hiyo, basi aliamua kumuita mwanaeili amueleze imekuwaje siku hiyo.
Alivyofika, moja kwa moja Erica alienda kumkumbatia mama yake na alimsimulia kila kitu ambacho kilitokea shuleni siku hiyo, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kukumbuka jinsi alivyokutana na yule mwanamke ambaye alimwelezea kuhusu mtoto wa Bahati aliyeitwa Abdi, moja kwa moja alitambua kuwa yule Abdi ndio huyo mtoto wa Bahati, alisikitika sana kusikia alitaka kumbaka mwanae, ila alimshukuru sana Elly kwa kumuokoa mwanae.
Erick aliingia ndani na alisikia kila kitu wakati Erica akielezea, basi akasema
“Nilijua tu, sikuwa na imani na yule Abdi toka siku ya kwanza jamani. Mama fanya kitu”
Kisha alienda kumkumbatia Erica na kumsema,
“Namshukuru Elly aliyekusaidia mdogo wangu”
Ila Erick alikuwa na kisasi na Abdi hatari, hata mama yake alimuona jinsi alivyokuwa akichukia anavyomtaja huyo Abdi basi mama yao akasema,
“Hivyo ndio inavyotakiwa, naona Erick umeumia sana mwanangu, pole baba”
Basi Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake.
Leo baba Angel alichelewa kurudi hivyo alivyofika ilikuwa tu ni maongezi mengine hata mama Angel alisahau kumueleza habari za Abdi, ila tu baba Angel alikumbuka jambo moja tu na kumwambia,
“Mke wangu naomba kesho usisahau kwenda kutoa hiko kijiti”
“Sawa mume wangu, hata usijali”
Na kulivyokucha, baba Angel aliondoka zake na mama Angel aliondoka pia ili kutimiza ahadi aliyomuahidi mumewe ya kwenda kutoa kijiti.
Kwahiyo moja kwa moja alienda hospitali.
 
SEHEMU YA 97

Basi mama Angel anafika kwenye hospitali aliyoichagua yeye, na kuonana na daktari wake ambaye alimfanyia tiba vizuri tu, alimpenda huyu daktari sababu mara kwa mara alikuwa akihudumiwa naye kwa kipindi hiko, alimfurahia sana, daktari huyu alijulikana kwa jina moja haswaaa la dokta Maimuna, basi leo aliongea nae mawili matatu na kuagana.
“Ila mama Angel mimi na wewe tumefahamiana muda ila hatujawahi kutembeleana, karibu kwangu siku moja jamani”
“Nitakaribia dokta Maimuna hata usijali wala nini”
“Au siku tupate mahali tuongee mawili matatu”
Mama Angel akaitikia tu huku akitabasamu na kuendelea kuagana na yule dokta halafu akaondoka zake, ila wakati anataka kuelekea kwenye gari yake alikutana na mtu aliyemfahamu ambaye nae alikuwa akielekea hospitali, yule ndio aliyemshtua mama Angel,
“Erica, Erica, wewe Erica”
Mama Angel alisimama na kumuangalia, mtu huyu alishawahi kuwa kwenye mahusiano nae ya kimapenzi, alikuwa ni mwanaume wake wa kwanza kabisa, ila kwa kipindi hiko walikuwa wakiheshimiana.
“Za siku nyingi Erica?”
“Nzuri tu Babuu, wewe na mkeo hamjambo?”
“Hatujambo kabisa, yani sisi ni wazima wa afya. Vipi wewe na familia yako?”
“Nasi ni wazima wa afya, naona umekuja hospitali”
“Ndio ila hapa kuna shemeji yangu”
“Shemeji yako! Kivipi!”
“Hapa kuna mke wa Rahim”
Mama Angel alishangaa kwani Rahim alimfahamu fika ila mke wa Rahim hakujua kama yuko hapo hospitali, sema siku nyingi tu huwa hataki kukutana na mwanamke huyo, hivyobasi aliamuwa kumuaga Babuu kuwa anaondoka, basi Babuu akamwambia,
“Kheee unamuogopa yule mwanamke? Yule alikuwa na wazimu ujue, hata hivyo Rahim ana mke mwingine”
“Kheeee jamani!! Kumbe alioa tena?”
“Aaah yule kaka yetu tunamjua wenyewe, unaishi wapi kwani siku hizi?”
Hili swali hakulitaka hivyobasi alijifanya ana haraka na kuagana nae halafu akaondoka zake.

Erica alivyofika shuleni, Elly nae alifika ila moja kwa moja alienda darasani na kumpa kifuko kidogo Erica na kumwambia,
“Erica, hivyo ni visheti mama yangu alivitengeneza, nikaona bora nikuletee. Mimi itakuwa ndio mara ya mwisho leo kuja hapa shuleni”
“Kwanini Elly? Umefukuzwa?”
“Hapana ila mama yangu kwasasa yupo busy sana, hawezi kuja huku shuleni, usijali Erica nilitamani kuendelea kuwa karibu nawe ili nikulinde ila ndio hivyo haitawezekana. Kwaheri Erica”
Kwakweli Erica alijihisi vibaya sana na kumfanya ashindwe hata kubaki darasani kwani nay eye alifatana tu na Elly kutoka nje ya shule kwani hakuona sababu ya kuendelea kuwepo mahali hapo ikiwa kuna mtu hawezi tena kuendelea na shule sababu yake.
Basi walivyofika nje ya shule alimwambia,
“Elly, nakuahidi kesho mama yangu atakuja nawe utarudi shuleni”
“Kwahiyo, kesho nije shule?”
“Ndio njoo, yani mama yangu ndio atakuja kusimamia swala hili. Najua sijaaga shuleni ni kesi pia ila mpaka pale watakapoonyesha kukuelewa wewe.”
“Asante Erica kwa kunijali”
“Asante na wewe”
Basi wakaagana ambapo Erica alipanda tena bajaji na kurudi kwao.
 
SEHEMU YA 98

Leo Angel alikaa mbali kabisa na Samir, yani hataki hata ukaribu nae ila kitendo kile kilimfanya Samir aone kamavile Angel kamdharau maana kuna ujumbe alimwambia kwenye barua ila Angel hajautelekeza, kumbe Angel hata barua yenyewe hakuisoma, ila kitendo kile kilimkosesha raha kabisa Samir, muda kidogo aliingia madam Hawa na kumuita Samir ambapo aliondoka nae na kuelekea nae ofisini kwake halafu alianza kuongea nae,
“Unajua nilitoka kufundisha darasa lingine, nikapita pale darasani kwenu na kuchungulia ila nikakuona umeshika tama na sura yako inaonyesha kuwa na mawazo sana, tatizo ni nini kijana wangu?”
“Hapana sina tatizo madam”
“Mimi najua saikolojia ya mwanafunzi ilivyo, najua kama una matatizo Samir, niambie. Mimi ni kama mlezi wako, kuwa huru niambie chochote kile”
Samir akaona bora amueleze tu huyu mwalimu jinsi anavyompenda Angel kuwa labda mwalimu anaweza kumsaidia kisaikolojia,
“Madam ipo hivi, sijui hata niseme imetokeaje ila shule niliyotoka nilipohamia tu nilikutana na mdada wa kuitwa Angel kwakweli madam nilijikuta nikimpenda sana na bado nampenda, halafu hapa shuleni nimemkuta pia yani nakosa raha nikimtazama sababu hataki kusema kuwa ananipenda pia. Naumia sana madam, sina raha jinsi ninavyompenda”
“Ooooh kumbe ni mapenzi yanakusumbua, sasa Samir hebu hayo mawazo ya mapenzi yatoe kabisa kwenye akili yako. Halafu Jumamosi njoo nyumbani kwangu ili tuongee vizuri, sawa Samir”
“Asante madam Hawa”
“Yani rudi darasani na umuone Angel kama dada yako wala usihisi kuwa wampenda kimapenzi, jitahidi kwa hilo halafu kesho nitakuuliza pia kuwa imekuwaje ila kesho kuna jambo nitalifanya ila nataka ujiandae kisaikolojia. Samir wewe ni mvulana mzuri, unatakiwa utulie na usome ili ufike mbali, usianze kuchanganywa na habari za wanawake mapema kiasi hiko”
“Nashukuru mwalimu, nimekuelewa”
Kisha Samir alitoka mule ofisini na kuelekea darasani ila alipofika darasani alimuona Angel akiongea na Husna tena akionyesha kuwa hana wasiwasi na jambo lolote lile, kitu hiko kilimuumiza moyo zaidi.

Erica anarudi nyumbani mapema na kumtaka tena Vaileth ampatie pesa ambayo anenda kuilipa bajaji, baada ya kulipa Vaileth anaamua kumuhoji,
“Erica, na leo imekuwaje tena?”
Erica anaelezea ilivyokuwa, basi Vaileth anamuuliza tena,
“Inamaana Elly akiacha shule na wewe utaacha?”
“Dada sio hivyo, hebu fikiria jana nimemueleza mama jambo hili nilijua atachukua hatua ya kwenda na mimi shuleni ili akamtetee Elly, cha kushangaza mama hajaenda shule wala nini sasa Elly atatetewa na nani? Wakati kaondolewa shule sababu yangu!”
“Hilo nalo neno”
“Sasa leo nangoja wote warudi hapa baba na mama ndio nianze kuongea nao”
“Mmmh nakuona Erica, unatumia nafasi yako kudeka vizuri”
“Ndio lazima nideke maana mimi ndio mtoto wa mwisho”
“Kheee kwa uzee gani aliokuwa nao mama yako!! Akiamua kuzaa mtoto mwingine je? Halafi kwani wa mwisho peke yako, na Erick je?”
“Erick ni Kulwa na mimi ni Doto kwahiyo mimi ni wa mwisho, na kuhusu mama kuzaa watoto wengine basi angekuwa kawazaa siku nyingi sana ila hadi leo hakuna basi mimi ndio wa mwisho. Mamangu kwao yeye ndio wa mwisho na anaitwa Erica yanbi jina langu ndiomana na mimi kaniita Erica, na baba nae kwao ndio wa mwisho na anaitwa Erick ndiomana kaka anaitwa Erick. Kwahiyo mimi ndio wa mwisho tu, na mama hupenda kuniita mziwanda”
“Haya bhana, kitoto cha mwisho, furahia maisha mwaya”
Erica alitabasamu kwani hii hali ya kuwa mtoto wa mwisho ilikuwa inamfurahisha sana kwani alikuwa akisikilizwa sana na wazazi wake.
 
SEHEMU YA 99

Leo mama Angel moja kwa moja alipitia ofisini kwa mume wake kwani alitaka kumpa habari ya kutoa vile kijiti, ila alipofika kuna mtu alitoka kwenye ofisi ya mume wake nakupishana malngoni ambapo walisalimiana tu ila hakutaka kumjali mtu huyo wala nini.
Aliingia ofisini kwa mumewe, kwakweli hata baba Angel alifurahi sana kumuona yani akawa na furaha na kusema,
“Kwa jinsi nilivyofurahi naomba nifunge ofisi twende nyumbani mke wangu”
Basi mama Angel alikubali na kumfanya wafunge ofisi na kuondoka kwa pamoja kuelekea nyumbani.
Walivyofika tu nyumbani walishangaa kumkuta Erica akiwa sebleni na sare zake na begi lake yani hata kwenda kuvua nguo hakwenda, basi aliwasalimia ilibidi wakae ili wamsikilize kuwa kwanini muda huo yupo nyumbani na sio shuleni, basi Erica akawaambia,
“Kabla ya yote naomba muonje hivi visheti ambavyo mama yake Elly kaviandaa”
Basi Erica akatoa na kuwapa wazazi wake, ambapo baba Angel hata bila kuuliza alimega kisheti na kuanza kukila, ila alishtuka sana na kufanya wote wamuangalie.


Basi Erica akatoa na kuwapa wazazi wake, ambapo baba Angel hata bila kuuliza alimega kisheti na kuanza kukila, ila alishtuka sana na kufanya wote wamuangalie.
Mama Angel alimuuliza mumewe kuwa imekuwaje,
“Mpenzi, nini tatizo tena?”
Baba Angel hakusema kitu ila alinyanyuka, na kufanya mama Angel amfate nyuma, kuelekea nae chumbani, ila walivyofika chumbani baba Angel alimwambia mama Angel,
“Naomba nipumzike kidogo”
Basi mama Angel ilibidi amuache apumzike kidogo kitandani, kisha akarudi sebleni kuongea na Erica, alimuuliza swali,
“Kwani visheti hivi kakupa nani?”
“Kanipa Elly, mama yake ndio amevipika”
“Nahitaji kumuona mamake Elly”
“Kheee mama unafikiri utamuonea wapi? Huyo mama hata mimi sijawahi kumuona, leo tu kagoma kuja shule kwaajili ya mwanao, yani yupo tayari afukuzwe shule kuliko yeye aje kumtetea, eti yupo busy sana”
“Kwani Elly kafanya nini?”
Ikabidi Erica amsimulie tena mama yake, yani mama yake ndio kama akakumbuka na kuuliza vizuri,
“Yani walimu wenu wana wazimu kweli, ngoja niwapigie simu”
Basi mama Angel alichukua simu yake na kupiga ambapo mwalimu Harun ndiye aliyepokea halafu alianza kuongea nae,
“Yani nyie, mtoto wangu atake kubakwa, halafu mtu aliyemsaidia mwanangu asibakwe ndio mnamfukuza shule, hivi nyie walimu mpoje? Mmeshindwa kumdhibiti huyo bakabaka!”
“Samahani mama, kwani imekuwaje?”
“Ngoja, Erica akueleze labda utaelewa”
Kisha mama Erica akampa Erica simu ambapo alianza kumueleza mwalimu jinsi ilivyokuwa, ndio mwalimu kidogo kuelewa na moja kwa moja alimuita mwalimu mwenye kesi hiyo aweze kuongea na mama Angel,
“Mama Angel jamani usipaniki kiasi hiko”
“Nisipaniki ndio nini? Yani mtoto aliyemuokoa mwanangu mmemfukuza shule halafu bakabaka mmemuacha”
“Hapana mama hatujafanya hivyo, ila tumemwambia Elly aite mzazi wake sababu kavunja kitasa cha mlango wa chooni”
“Na asingevunja hiko kitasa si ndio mwanangu angebakwa? Hivi hamjafikiria hilo? Kwanini huyo mzazi wa Abdi asiitwe mpaka mzazi wa Elly? Jamani hebu achene bangi walimu, muacheni Elly arudi kuendelea na masomo yake”
“Sawa mama Angel hakuna tatizo, samahani kwa hilo. Kesho Erica aje shuleni tu kama kawaida”
“Na Elly je?”
“Naye aje shuleni tu”
Basi mama Angel alikata ile simu kisha aliinuka zake na kurudi chumbani ila leo kwa mara ya kwanza alimuona mumewe akikoroma sana, kwakweli mama Angel aliogopa kiasi kwani haikuwa kawaida kwa mumewe kukoroma hata achoke vipi, basi akachukua simu yake tena na kumpigia mama yake, ambapo alimueleza toka walivyorudi na mumewe kula vile visheti,
“Na wewe mama Angel jamani, kila siku nasema ni vizuri kuombea chakula kabla ya kukila. Sio mara zote chakula kinakuwa na sumu, ila vyakula vingine vina manuizo mabaya, huwezi jua kuhusu hilo. Haya usichelewe, sasa hivi ingia kwenye maombi maana hiyo hali sio ya kawaida, ingia kwenye maombi sasa hivi”
Mama Angel alipata hofu kidogo ila akajitia ujasiri na kuchukua biblia ambapo alisoma na kisha kuanza maombi ya kumuombea mumewe.
Baada yay ale maombi baba Angel aliamka na kuanza kujinyoosha nyoosha, basi mkewe alifurahi sana kisha alikaa karibu na muemewe na kumsikiliza kuwa anajisikiaje,
“Vipi hali yako lakini mume wangu?”
“Yani sijui vipi, huwezi amini hapa nililala halafu nilikuwa nikiota ndoto za zamani kabisa, eti nilikuwa nikiota mambo ya zamani kuwa yalikuwaje jamani, yani jinsi nilivyokuwa zamani ndio nilichokiota”
“Pole sana mume wangu, nikakuandalie chakula gani?”
“Labda chapati tu”
Basi mama Angel alitoka na kwenda kumuandalia mumewe chapati.
 
SEHEMU YA 100

Angel aliporudi kwa shangazi yake leo, alimkuta yupo na kumsalimia ambapo shangazi nae alimuuliza habari za shule,
“Ni nzuri tu shangazi”
“Vipi leo hujaongea na Samir?”
“Sijaongea nae shangazi”
“Vizuri sana, zingatia masomo yako yani masomo ndio yawe kila kitu kwako”
Basi Angel alienda chumbani ila kwa upande mwingine wa moyo alikuwa akiumia sana kuishi maisha ya bila kuongea na Samir ingawa wanaonana.
Usiku wa siku hiyo wakati amelala, akaota kuwa Samir ana mahusiano ya kimapenzi na madam Hawa, akawaona wameongozana pamoja huku wakikumbatiana, kwakweli Angel alishtuka sana toka kwenye ule usingizi, alikaa kitandani huku akijiuliza,
“Inamaana Samir kweli anaweza kuwa na mahusiano na yule mama mtu mzima inawezekana kweli? Hapana jamani, halafu yule mwalimu si ana mume wake yule, hawezi nadhani ni ndoto tu hii”
Basi aliendelea kulala ila hii ndoto ilikuwa ikifanya kazi katika akili yake.
Kulipokucha alijiandaa na kwenda shuleni, basi akiwa amefika shule alimuona Samir akiwa kaongozana na madam Hawa, aliumia moyo na kuamua kwenda kukaa kisha akamuuliza Husna,
“Hivi mume wa madam Hawa yuko wapi?”
“Ooooh yule madam hana mume ujue ndiomana mkali vile, sijui wanaume walimfanya nini, kwa kifupi yule madam anawachukia zaidi wanaume.”
“Oooh, hapo nimekuelewa”
Muda kidogo Samir aliingia darasani, halafu baada ya muda kidogo madam Hawa alienda kumuita Samir na kuelekea nae ofisini, kwakweli ile kitu ilikuwa ikimuuma sana Angel ila alijifanya kuwa hajali kitu chochote wala nini.
 
SEHEMU YA 101

Mama Angel alibaki nyumbani siku ya leo ila alijikuta akitafakari sana kuhusu mama Elly, yani aliona kuwa ni kitu cha ajabu sana kisha alimuuliza Vaileth,
“Eti Vaileth, hivi jana umeona ni kitu cha kawaida kwa baba kula vile visheti na kushtuka halafu kwenda kulala?”
“Mmmmh sio kawaida mama, hata mimi nilishangaa tu. Ila mbona vile visheti nilikula mimi na Erica na hatukuona tatizo lolote”
“Yani mimi niliogopa hata kuvionja jamani, tatizo lilikuwa nini sijui”
“Sijui kwakweli ila ni vyema ukamfahamu mama wa Elly kwani itasaidia sana na umshirikishe jambo hilo”
“Eti eeeh! Basi ngoja nitafanya hivyo tena leo leo”
“Ni vizuri uende muda ule ambao wanatoka shuleni kisha umwambie huyo Elly akupeleke kwao”
“Oooh umesema jambo la maana sana Vaileth, ndiomana nakupenda jamani. Itabidi tu leo niende mwenyewe shuleni kwakina Erica”
“Sawa mama, fanya hivyo”
Basi mama Angel alijiandaa na kumuaga Vaileth,
“Kuna mahali nitapitia halafu ndio nitaenda huko shuleni kwakina Erica”
“Sawa mama, badae”
Basi mama Angel akaondoka zake kuelekea kwenye shughuli zake.
Muda kidogo simu ya Vaileth iliita, kuangalia mpigaji ni shangazi yake, basi akapokea na kuanza kuongea nae,
“Shikamoo shangazi”
“Shikamoo mwenyewe kama ni mali, shikamoo tena na tena. Yani wewe ni mjinga sana kumbe unaishi kwenye jumba la kifahari halafu ndugu zako tunapata shida jamani!! Unashindwaje kuwaonea huruma ndugu zako?”
“Jamani shangazi”
“Sio jamani, unatakiwa ufanye kitu na umiliki nyumba hiyo, Jumamosi ninakuhitaji huku kwangu, uje ili tuzungumze”
“Mmmh kuhusu hayo shangazi au kuna mengine?”
“Kama kuna mengine si utayajua huku huku, ila nahitaji kukuona Jumamosi’
“Sawa shangazi nitakuja”
Basi Vaileth alikata ile simu na kuanza kuwaza sana kuhusu ndugu zake,
“Kwani ndugu zangu wana nini jamani, yani mimi nikawe na mahusiano na baba Angel kweli? Nimsaliti mama Angel jamani! Kwa jinsi wanavyopendana halafu mimi nikavuruge upendo wao? Hapana kwakweli, nipo tayari kufa na umasikini wangu ila sio kuharibu furaha ya watu”
Kisha akaamua kuendelea na kufanya kwake usafi.

Mama Angel alifika sehemu ambayo alikuwa amepitia kwanza ili aweze kwenda huko shuleni alikopanga, ila mama yake alimpigia simu hivyobasi aliamua kwenda kwanza kwa mama yake na sio kwenda shuleni kwakina Erica tena.
Moja kwa moja alienda kwa mama yake, ambapo alimkuta na kumsalimia pale,
“Oooh mama nimeitikia wito”
“Mwanangu, yani leo nimekukumbuka sana, nimekaa hapa nimekuwaza hatari na hivi jana uliponipigia simu ndio kabisa”
Mama Angel alifurahi sana kusikia mama yake alimkumbuka, halafu mama yake alianza kumuuliza kuhusu jana yake,
“Eeeeh mwanangu jana uliomba eeeh!”
“Ndio mama, niliomba ila ninahitaji kuonana na yule mama Elly”
“Na itakuwa vizuri sana, ili umfahamu”
“Ndio, nilitaka kwenda leo. Ila ndio nimeshakuja huku tena”
“Oooh na hapa huondoki muda huu mwanangu, nina hamu yakula chakula chako, yani nahitaji leo unipikie n anile chakula chako. Nimekimiss sana mwanangu, nakumbuka kipindi ukiwa mdogo tukisumbuana tu akili hapa, leo nimekukumbuka sana jamani mwanangu”
“Haya mama, unataka nikupikie nini tena?”
“Nisongee ugali tu, ila nimekumbuka na samaki. Hivi yule mwanaume wako wa samaki aliishiaga wapi yule?”
Mama Angel alicheka sana na kumwambia mama yake,
“Kumbe hujui mama, yule alimuoa rafiki yangu Fetty”
“Kheee Fetty aliyaweza yale maradhi kweli? Nakumbuka kipindi kile akilala nje ya geti pale. Hahaha alikuwa na wazimu sana yule jamani”
“Ila mama nawe, loh ulimfunga kijana wa watu”
“Ndio nilimfunga, ila ni ujinga wake ndio ulisababisha yale, yule hakuwa na upendo ila ni uchizi ule. Ila si mimi niliyemfunga jamani, alikuwa ni marehemu James, kumbe na yeye anakunyemelea loh!”
“Ila maisha mama jamani, yapitage tu tuingie kwenye kipindi kingine. Yani kipindi kile, nilikuwa kama chizi, sikuwa na raha hata kidogo jamani. Basi ngoja nikakuandalie upendacho mama”
Kisha mama Angel alienda kumuandalia mama yake chakula akitakacho.
 
SEHEMU YA 102

Erica leo aliingia darasani akiwa na Elly kwahiyo kwa kiasi walifurahi, na Abdi nae alikuwa darasani ila hawakuongea nae chochote kile na walitulia tu kuendelea na masomo, kisha Abdi aliitwa na mwalimu ambapo aliambiwa akamuite mzazi wake, kutokana na mlango wa choo ambao ulivunjwa na Elly basi Abdi aliondoka moja kwa moja na kwenda kwao kwaajili ya kumuita mzazi wake.
Basi muda wa mapumziko, Elly alianza kuongea na Erica ambapo kitu cha kwanza alimuuliza,
“Vipi vile visheti mlikula?”
“Ndio, ila kwani mama yako aliweka nini kwenye vile visheti?”
“Kwanini?”
“Baba yangu alivyokula alishtuka halafu alienda kulala, yani mama alikuwa na mashaka sana”
“Jamani mbona mama yangu hajaweka kitu chochote, na alinipa kwa upendo tu, akasema kampe rafiki yako Erica awapelekee kwao nao waonje mapishi yangu, hajaweka kitu mama”
“Aaaah ila kuja shule ndio kagoma?”
“Yani mama yangu yupo busy sana, si nilikwambia kuwa baba alimkimbia mama wakati nipo mdogo kabisa kwahiyo mama ndio wa kuhudumia familia nzima, kwahiyo mama ndio wa kutafuta kila kitu”
“Kwani kwenu mpo wangapi?”
“Nimezaliwa peke yangu, ila kuna watoto wa mama mkubwa tunaishi nao, ni yatima kwahiyo wanahudumiwa kila kitu na mama, yani mama yangu hana muda kwakweli, ndiomana kaniambia nisifanye kitu kibaya kwani yeye hana muda wa kuja shule na nikifanya mabaya basi nitakaa nyumbani kumsaidia kusambaza visheti”
“Kheee kumbe!! Sasa na wewe ada unalipiwa na nani huku?”
“Yani mama yangu yupo radhi alale njaa kuliko mimi nisome shule mbaya, anataka nisome shule nzuri yani hadi majirani wanamshangaa kwakweli, kupanda basi la shule nilikataa mwenyewe ila ningekubali basi mama angetafuta hela kivyovyote viel nipande basi la shule, ila nilimuhurumia”
“Kwakweli mama yako anakupenda sana Elly”
“Ndio ananipenda sana, ndiomana na mimi nampenda”
Basi waliongea ongea pale na kisha kurudi darasani.
 
SEHEMU YA 103

Abdi alirudi kwao ili kumuita mzazi wake kama alivyokuwa ametumwa na mwalimu, ila Abdi alikuwa akiishi na mama yake wa kambo, sababu baba yake hakuishi na mama yake mzazi, basi alifika na kumsalimia mama yake huyu kisha mama yake alimuuliza,
“Vipi tena mbona mapema?”
“Wanakuita shuleni mama”
“Oooh huo ujinga sifanyi jamani, ulipokuwa shule ya msingi kila leo naenda mimi kwenye makosa yako ya shuleni, sasa leo ataenda baba yako, kwakweli mimi siwezi hiyo biashara jamani. Mbona mwenzio Bahati hayupo hivyo?? Kila siku wewe tu, likitoka hili linaingia lile, kwakweli siwezi jamani siwezi kabisa”
“Jamani mama”
“Msubiri baba yako hapo arudi ndio uende nae huko shuleni, tena mng’ang’anie uende nae leoleo maana kesho haitawezekana, babako anasafiri”
“Sawa mama”
Basi Abdi akatulia kwao ambapo alimsubiria baba yake ili aje na waondoke pamoja kwenda shuleni.
Baba yake alivyorudi basi alimuelezea kuwa anaitwa na mwalimu, baba yake alianza kufoka,
“Mambo gani tena hayo jamani!! Yani walimu hawa huwa wananikera mno jamani, sasa wananiitia nini?”
Mkewe akadakia na kumwambia,
“Usilalamikie tu walimu, uliza kwanza mwanao kafanya nini hadi uitwe”
“Kweli, haya Abdi umefanya nini mwanangu?”
“Twende tu ukashuhudie mwenyewe baba, kosa sio langu ila walimu wanataka kunisingizia tu. Twende baba”
Mama yake akadakia,
“Wakusingizie kwa lipi? Kwani walimu hawana akili hadi wakusingizie? Nendeni huko shule jamani”
Basi baba yake alijiandaa na kuondoka na mwanae kuelekea shuleni, huku baba yake akimuuliza Abdi kama amefanya kitu gani hadi aitwe shuleni ila Abdi hakumwambia baba yake wala nini kwani angemwambia swala la yeye kuvunja kitasa cha mlango wa chooni basi baba yake angegoma kwenda kabisa.
Ila walipofika njiani, baba yake alisimamisha gari na kushuka maana kuna mtoto alimuona njiani na kumfanya mwanae amuulize,
“Baba vipi?”
“Aaaah hapana, huyu mtoto kafanana sana na mama yangu”
Kisha alimfata yule mtoto aliyekuwa wa kike na rika kama la Abdi, alimuuliza maswali na kumuomba ampeleke kwa mama yake kwahiyo safari ya kwenda shuleni kwakina Abdi ilihairishwa na muda huo huo walielekea nyumbani kwa yule mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Rukia.
Walipofika kwa mama Rukia, ndipo baba Abdi alipogundua kuwa huyo Rukia pia ni mtoto wake, basi muda huo huo aliomba kuondoka na mwanae kuliko mwanae kuhangaika mitaani kama alivyomkuta,
“Naomba tu nikakae nae mwenyewe”
“Oooh afadhali, maana hata mimi nimechoka kulea mtoto peke yangu”
Basi Rukia aliandaliwa na moja kwa moja baba Abdi alipanda nae kwenye gari na kumrudisha nyumbani kwa mke wake, ambapo mkewe alichukia sana na kuanza kulalamika pale pale,
“Mtoto mwingine tena!! Kwakweli nimechoka jamani, yani wewe baba ipo siku isiyo na jina mimi nitaondoka mahali hapa, siwezi hii kitu kwakweli”
Hakuwa na la kufanya kwakweli basi aliongea na Abdi kuwa kesho yake hatosafiri tena, kwani atampeleka Rukia kwa mama yake na badae ndio ataenda nae shuleni kama alivyoitwa na walimu.
 
SEHEMU YA 104

Mpaka muda wa kutoka hakuonekana Abdi wala mzazi wake, kwahiyo walimu walijua kuwa ataenda kesho yake, basi wakina Erica nao walitoka na kama kawaida waliondoka na kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.
Erica alivyofika Vaileth alimuuliza kama mama yake hakufika shuleni kwao,
“Hakuja, labda kuna mahali ameenda”
“Anataka kuja kumuona mamake Elly”
“Sidhani kama ni rahisi, mama nimemwambia kuwa yule mama haonekani kirahisi ila mama mbishi, haya aje kumuona tu”
Kisha Erica akaenda zake chumbani kwake, ila alishangaa sana kukuta Erick yupo chumbani kwake eti kajilaza, alimshtua na kumuuliza,
“Kheee Erick, umerudi muda gani na mbona upo huku chumbani kwangu?”
“Nimerudi muda sio mrefu, ila leo nilikukumbuka sana, yani nilijikuta natamani sana kukuona jamani. Sasa nimekuona moyo wangu umeridhika”
Basi Erica alitabasamu na kufurahi sana, kisha alimsogelea kaka yake na kumkumbatia ambapo naye Erick alijihisi vyema na muda huo akaondoka kuelekea chumbani kwake.
Mama Angel alivyorudi jioni ya siku hiyo alimuita Angel na kumwambia kuwa kesho yake ataenda shuleni kwao.
“Nahitaji kuonana na mamake Elly”
“Ila mama ni ngumu nimekwambia”
“Ni ngumu ndio ila nahitaji sana kuonana nae, kwahiyo kesho nitakuja shuleni kwenu kukuchukua wewe na huyo Elly kwahiyo mimi ndio nitamrudisha nyumbani kwao”
“Mmmh labda itawezekana ukamuona”
“Sio labda, nitamuona tu. Nahitaji sana kumfahamu”
Kisha akaachana na mwanae na kuondoka zake kwenda kuongea na Vaileth ambapo Vaileth alimwambia kuhusu dhumuni lake la Jumamosi kwenda kumtembelea shangazi yake,
“Halafu mama, nilikuwa naomba Jumamosi unipe ruhusa ili niende kumtembelea shangazi”
“Hakuna tatizo, ila tu uwahi kurudi”
“Asante sana mama”
Basi mama Angel aliamua kwenda kuendelea na majukumu yake ya siku hiyo.
 
SEHEMU YA 105

Angel alirudi kwao ila alikuwa na mawazo sana, sema akakumbuka maneno ya shangazi yake kuwa ajiweke makini na masomo ili aweze kuyakwepa yale mawazo aliyokuwa nayo.
Siku hiyo hadi wakati analala usiku ni kama alikuwa akihisi kuwa madam Hawa ana mahusiano na Samir,ila alijiuliza sana,
“Sasa kama kweli, kwanini naumia?”
Aliwaza na kukosa jibu, basi aliamua kujilazimisha tu kulala.
Kulipokucha alienda shuleni kama kawaida, ila na siku hiyo pia alimuona madam Hawa akifika na Samir halafu muda kidogo baada ya Samir kuingia darasani yule madam alifika na kumuita Samir, basi alimuangalia na watu darasani walionekana kuguna kwa siku hiyo.
Basi Husna akaanza kumwambia Angel,
“Unajua kwasasa kila mtu kaanza kupatwa na mashaka yani sio ukaribu huu wa mwalimu na mwanafunzi, huyu madam Hawa anatushangaza kwakweli”
“Kumbe na nyie mmemuona eeeh!”
“Ndio, kwanini kila siku asubuhi afike nae? Na kwanini baada ya kufika tu aje kumuita? Huwa anaenda kuongea nae nini ofisini?”
“Ila huyu madam mbona ni mtu mzima?”
“Ni mtu mzima ndio, ila kumbuka kuwa hana mume halafu huyu ni madam anayeogopewa shule nzima hii, ni kwanini aweze kuwa karibu hivyo na Samir? Hivi hujajiuliza swali hilo Angel?”
“Nimejiuliza ila nikakosa jibu”
“Basi jibu ni kuwa anatoka nae”
Wakaongea ongea pale ila Husna hakujua tu ni kwa jinsi gani jambo lile lilimuuumiza Angel.

Ilikuwa ni karibu na muda wa kutoka, walimu wakiwa ofisini waliona kwa mbali Abdi akishuka na baba yake kwenye gari kuelekea ofisini, basi walianza wenyewe kuongea,
“Uwiii jamani huyu Abdi kaamua kuja na baba yake mweeeh!”
“Ila hukumwambia kuwa aje na mama yake?”
“Nilimwambia, hata sijui kwanini anakuja na baba yake jamani!”
“Yule mama ni muelewa ila huyu baba ni mtata balaa, yani sijui itakuwaje mweeeh!”
“Hivi na siku ile aliyotoka na damu puani ilikuwaje?”
“Tulimwambia asiseme, alivyopona basi, tulimpa huduma ya kwanza ila tulimwambia kuwa asiseme, yani ugomvi huu una wazazi wasumbusu jamani hadi kero”
Baba Abdi aliingia ofisini, huku Abdi akikaa nje ya ofisi kusubiria baba yake aongee na walimu.
“Eeeeh nimeitikia wito, niambieni tatizo”
“Samahani mzee, ni hivi huyu Abdi kuna kitu kafanya shuleni hapa. Tulisikia sauti chooni, kwenda ndio tukamkuta Abdi, pamoja na binti mmoja na mvulana mwingine, Abdi alitaka kumbaka yule binti, sasa….”
Baba Abdi akawakatisha kwanza na kuwauliza tena,
“Mnasema Abdi alitaka kubaka? Jamani mnataka kuchekesha wasionuna, sasa Abdi abake kitu gani wakati hata kubalehe hajabalehe jamani, hivi walimu mna akili nyie kweli eeeh! Sasa Abdi abake vipi?”
“Tusikilize mzee kwanza, halafu mlango wa chooni umevunjwa, kwahiyo inabidi ulipe gharama za kutengeneza kitasa”
“Kwahiyo Abdi ndio kavunja huo mlango katika harakati za kubaka?”
“Hapana, ila mlango alivunja kijana aliyeenda kumuokoa yule binti”
“Hivi mnajua siwaelewi kabisa, yani siwaelewi. Mlango avunje nani na alipe nani? Hebu niitieni kwanza huyo aliyetaka kubakwa na huyo muokoaji”
Ikabidi mwalimu akamuite Ellyn a Erica kwani ulikuwa ndio muda wa kutoka, kwahiyo moja kwa moja walienda ofisini na kumkuta baba Abdi, ambapo walitambulishwa na walimu pale, kisha mwalimu akamwambia baba Abdi,
“Binti huyo hapo ambaye mwanao alitaka kumbaka, anaitwa Erica”
Baba Abdi akashangaa sana na kusema tena,
“Erica!!!”
“Ndio, anaitwa Erica, halafu huyu mvulana anaitwa Elly ndio ambaye alienda kumsaidia Erica”
“Hebu muiteni Abdi kwanza”
Walimu walimuita Abdi ambaye alikuwa nje ya ile ofisi ambaye aliingia na baba yake alimuuliza,
“Eti mwanangu, ulitaka kumbaka Erica?”
“Hapana baba, sijataka kumbaka”
Kisha baba Abdi akamuangalia Erica na kumuuliza,
“Eti ni kweli Abdi alitaka kukubaka wewe?”
“Ndio”
“Ulijuaje kama anataka kukubaka? Ulishawahi kubakwa?”
Yani walimu walichukia sana, walitamani hata kumwambia huyu mzee amuhamishe mtoto wao ili waepuke ule usumbufu wake, wakati kabla Erica hajajibu alifika mwalimu wa taalumu na kusema kuwa mzazi wa Erica yupo nje anamsubiri mtoto wake, basi mwalimu mmoja akasema,
“Eeeeh vizuri sana, mwambie aje”
Basi yule mzazi wa Erica akaitwa, alipoingia tu ofisini, macho yake yaligongana na macho ya baba Abdi kwani ni watu waliofahamiana.
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom