Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 155

Mama Angel na baba Angel kama ambavyo walikuwa wamepanga, basi leo walienda moja kwa moja kwa Tumaini ili kumuona mtoto wao na kumtakia mtihani mwema, na walipofika tu kweli walimkuta yupo ndani anajisomea, basi walimuita na kumsalimia kisha wakamtaka kuendelea na masomo yake kama kawaida, basi na wao walikaa wakiongea pale na Tumaini kuhusu mambo mbalimbali, na muda kidogo mume wa Tumaini nae aliwasili na kusalimiana nao pale halafu alianza kuongea nao,
“Jamani eeeh! Leo niliamua kufatilia lile tukio mjue, yani nimefatilia nijue yule mdada ofisini kwangu alikuja kufanya ninina kwanini ikawa vile”
“Mmmh kaka, kwahiyo umemgundua sasa?”
“Yani ni hivi, yule binti alikuwa ni mgeni machoni mwa wote pale ofisini, ila nilivyouliza kwa watu wengine walidai kuwa wanamfahamu yule dada, kuwa yule dada ni mpiga madili, watu wakasema kwamaana hiyo kuna mtu atakuwa kampa kazi ya kuja ofisini kwangu ila mpaka muda huu sijajua ni mtu gani na alikuwa na lengo gani”
Pale ndio maneno ya Dora yalianza kufanya kazi vizuri katika akili ya mama Angel na moja kwa moja, na kumfanya azidi kumchukia Sia kwani jibu alilokuwa nalo kwenye akili yake ni kuwa Sia hakuwa mtu mzuri tena, basi alimuuliza tena kaka yake,
“Kaka Tony, hivi hakuna hata mtu mmoja aliyesema kuwa huyo dada huwa anatumiwa na nani?”
“Nasikia huwa anatumiwa na watu mbalimbali, kwa maana hiyo hata kuanguka hakuanguka wala nini, yule alikuwa kwenye maigizo tu”
“Ooooh sema kwa mtindo huo basi inatakiwa kuwa makini sana”
“Ni kweli, haswaaa kwasisi wafanyabiashara maana utakuta mara nyingine unafatiliwa na mtu bila hata kujua kuwa unafatiliwa, ila inatakiwa kuwa makini sana. Nataka kufunga kamera kwenye ofisi yangu”
“Oooh utakuwa umefanya jambo la maana sana”
Kisha mama Angel alimuuliza baba Angel,
“Hivi na ile ofisi mpya mume wangu umefunga kamera kweli!”
“Mmmmh bado sijafunga kule”
“Mi naona ni vyema nako ufunge kamera”
“Sawa sawa, nitafanya hivyo tu”
Basi wakaongea pale na kuamua kuaga, ambapo baba Angel na mama Angel waliondoka kwani waliona muda wao umeisha wa kuendelea kukaa mahali hapo.

Mama Angel na baba Angel walipofika nyumbani waliwakuta watoto wao wakiwa makini sana na kuangalia Tv, kama kawaida mama Angel aliwatimua maana hakupenda wakae pale sebleni kwa muda mrefu ila kitendo cha kuwatimua wale watoto wake muda huo walienda tu chumba kimoja ambapo walienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea mambo mbalimbali, Erica alimuuliza kaka yake,
“Sasa hizo muvi za ngumi Samia akizileta tutakuwa tunaangalia wapi ikiwa mama anatufukuza sebleni?”
“Ooooh mbona jambo dogo hilo, sikia nikwambie mimi na wewe inatakiwa letu liwe moja. Mbona kwenye ile sebule ya juu ina Tv pia, si huwa wanasema hadi wageni waje? Mimi ndio ninafungua za vyumba vyote humu ndani kwahiyo hata usijali tutakuwa tunaenda na kuangalia kule”
“Jamani, ndiomana nakupenda Erick, ila mimi picha za ngumi naogopa sana”
“Sasa unaogopa nini wakati utakuwa unaangalia na mimi? Usiogope maana tutaangalia wote”
“Sawa kaka yangu, basi tucheze karata na leo”
Erick alikubali na kuanza kucheza karata ambapo kama kawaida walicheza sana hadi usiku na wakajikuta wameshikwa na usingizi mule mule chumbani kwa Erick.
Kulipokucha, Erick alikuwa wa kwanza kuamka leo na kumshtua dada yake ambaye nae alikurupuka, kwahiyo ile tabia ilikuwa kawaida kabisa kwao maana haikuwa mara ya kwanza ukizingatia mara nyingi walijikuta wakiwa pamoja.
Basi asubuhi ile nyumba nzima leo walienda kwenye ibada hadi Junior, ingawa huwa ni mbishi kwenda ibadani ila leo alienda, kwahiyo nyumba nzima waliondoka.
Wakiwa ibadani, Erica alitoka mara moja maana kuna kitu alikiona nje ya Kanisa wakati wanataka kuingia, kwahiyo walipokuwa Ibadani tu aliwavizia na kutoka zake nje ili kuangalia kile alichokiona, basi aliondoka hadi lile eneo ila kuna kijana aligongana nae kikumbo na kuanza kuombana nae msamaha,
“Nisamehe tafadhari”
“Nisamehe mimi kwa kutoangalia mbele”
“Aaaah usijali chochote, by the way naitwa Bahati, vipi wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Erica”
“Ooooh jina zuri sana, hongera”
“Asante”
Erica macho yote yalikuwa pale alipoona alichokuwa anakitaka ila kuangalia vizuri alikuta kimeshanunuliwa, na kujikuta akisema,
“Aaaargh washachukua tayari”
Yule Bahati alimuuliza,
“Wamechukua kitu gani?”
“Kuna kiatu nilikiona pale, nikakipenda sana, yani nilitaka kukinunua jamani, wamekichukua tayari”
Basi Bahati alisogea pale na Erica na kujua ambaye alichukua kile kiatu kisha kwenda kumuomba ili waweze kununua kile kiatu, yule mtu aliwaambia labda wampe hela mara mbili ya bei ya kawaida ya kile kiatu. Kilikuwa ni kiatu cha kawaida kabisa ila Erica alionekana kukipenda sana, kiliuzwa elfu tano kwahiyo yule mtu alisema labda apewe elfu kumi, Bahati akamuangalia Erica na kumuuliza,
“Je utakinunua kwa bei hiyo?”
Erica aliitikia tu na kufanya Bahati amuulize tena ila Erica alikaa kimya, kwani kiukweli hakuwa na hela yoyote pale ila alikuwa akijitutumua tu kuwa anataka kununua kile kiatu, badae akamwambia Bahati,
“Mwache tu aende, nilikuwa nakiangalia tu”
“Mmmh jamani, hadi tumemrudisha ujue!”
“Aaaaah kumbe hela yenyewe sina”
Basi Bahati alitoa hela yake na kununua kile kiatu kwa yule mtu kisha alimkabidhi Erica kile kiatu, kwakweli Erica alitabasamu na kufurahi sana huku akimwambia,
“Asante sana”
“Usijali, natumaini tutaonana tena”
Basi Erica moja kwa moja alirudi tena kanisani lakini hakuna mwanafamilia wa Erica aliyegundua kuwa Erica alitoka nje ya kanisa ule muda wa ibada.
 
SEHEMU YA 156

Ibada ilipoisha wote wanarudi nyumbani na moja kwa moja Erica anaenda kuweka vile viatu chumbani kwake, kwakweli alivipenda sana vile viatu ingawa vilikuwa ni vya kawaida sana ila alijikuta akivipenda sana, basi alikuwa akiviangalia na kukumbuka tukio lote la kugongana na yule mtu wa kuitwa Bahati, pia alikumbuka sura ya mtu yule ilivyoonekana kwani yule mtu alikuwa na sura ya upole sana, basi alikuwa akitabasamu tu na kusema,
“Anaitwa Bahati, kweli nimepata bahati ya kukutana nae, mvulana mwenye sura ya upole kiasi kile”
Basi siku hiyo alikuwa na furaha sana kupita maelezo ya kawaida.
Mambo mengine yaliendelea pale nyumbani kama kawaida, walipomaliza kula chakula cha usiku kwa siku hiyo, mama Angel alimuuliza mwanae,
“Vipi leo ndio upako umekushukia au?”
Erica alicheka na kusema,
“Ndio mama”
“Naona maana sio kwa tabasamu hilo ulilokuwa nalo, nimebaki najiuliza hapa, kuwa mwanangu umefurahishwa na kitu gani. Ila kama upako umekushukia basi nafurahi kusikia hivyo ila leo jamnai muwahi kulala maana kesho shule”
“Sawa mama”
Na muda huo huo waliondoka na kila mmoja kwenda chumbani kwake kulala kama kawaida.
Ila leo mama Angel alimwambia mumewe kuwa kesho yake angeenda tena kutembelea lile duka ambalo walimuweka Steve asimamie, na mumewe hakuona kama ni tatizo kufanya hivyo kwani aliona ni jambo jema.

Kesho yake wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wameshaanza mtihani wao wa mwisho, kwahiyo kulikuwa na ukimya sana mashuleni, na madarasa ya vidato vingine walikuwa kimya pia kwani hawakutakiwa kuonekana hata kukatisha maeneo ambayo kidato cha nne walikuwa wakifanya mtihani.
Sehemu ambayo alikaa Angel ilikuwa ni kiti cha kwanza kabisa, ila mtihani wa kwanza ulipoisha na kukusanya ile mitihani, wakati wamesimama aligundua kuwa alipokaa ilikuwa ni sehemu ambayo moja kwa moja alionana na Samir ambaye alikaa mwishoni kabisa.
Ila walipotazamana walijikuta wakitabasamu tu, kisha kutoka kwenye chumba cha mtihani na moja kwa moja kwenda kujipanga kwaajili ya mtihani mwingine ulikuwa ukifatia kwa siku hiyo.

Leo Sia aliamua kwenda tena sehemu ambako Steve anafanya kazi, basi alifika na kuingia ingawa Steve alimkatalia, basi alivyoingia akacheka na kusema,
“Hivi wewe unaweza kunikatalia mimi kweli? Wewe ni nani? Hivi unajua mimi ni nani kwa huyo Erick?”
Steve alikaa kimya tu kwani alikuwa na hasira sana ila muda kidogo mara mama Angel nae aliingia mule ofisini na wakagongana macho na Sia, kiukweli mama Angel alichukia sana.


Steve alikaa kimya tu kwani alikuwa na hasira sana ila muda kidogo mara mama Angel nae aliingia mule ofisini na wakagongana macho na Sia, kiukweli mama Angel alichukia sana.
Akajikuta akianza kumfokea Steve,
“Nilikwambia nini wewe lakini? Kufanya hii kazi hutaki au”
Sia alikuwa pembeni akicheka tu utadhani aliyoyafanya yalikuwa ni mazuri, il kitendo kile cha kucheka ndio kilizidi kumchukiza mama Angel, na kujikuta akimuuliza kwa hasira,
“Na wewe ni kitugani kinachokuchekesha?”
“Unayenichekesha ni wewe, badala ya kuniuliza mimi kuwa imekuwaje nipo hapa unafanya kazi ya kumfokea huyo Steve, kwanza unajua kama Steve ni mume wangu? Je wewe unaweza kumtimua mume wako? Kama ilivyokuwa vigumu kwako ujue hata kwa Steve kunitimua mimi mke wake ni vigumu sana, na ukumbuke kuwa mimi na Steve tuna mtoto kwahiyo nina haki ya kujua kuwa mtoto wetu atalelewaje na ataishije”
“Hivi unaongea au unaropoka?”
“Kwani wewe unahisi kitu gani? Unahisi naongea au naropoka? Wewe Erica, usijifanye kuwa unajua kila kitu, kuna mengine huyajui na huwezi kuyajua maana kuna werevu na wajuaji zaidi yako”
Halafu Sia aliondoka zake na kumuacha pale mama Angel akiwa na Steve.
Basi mama Angel alimuangalia tena Steve kwa muda kidogo ila hakuongea jambo lolote kwa muda huu zaidi zaidi alitoka nje pia na kupanda gari lake ambapo moja kwa moja alienda ofisini kwa mume wake.
 
SEHEMU YA 157


Mama Angel alifika ofisini kwa mume wake,ila pale pale mapokezi alimuona binti mmoja naye akionekana kutaka kwenda kumuona mume wake ofisini, muda huo kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, akamsogelea yule binti na kumuuliza,
“Una shida gani binti?”
“Nahitaji kuonana na bosi”
“Karibu basi”
Mama Angel alimshika mkono na kwenda nae hadi ofisini kwa mume wake kisha akamwambia akae kwenye kiti, halafu yeye akakaa kwenye kiti kingine na kuanza kumsikiliza shida yake, kwakweli yule binti inaonyesha hakujua kama mama Angel ndio angekuwepo kumsikiliza, muda huo baba Angel hakuwepo ofisini wala nini alikuwa ametoka, kwahiyo mama Angel alimuangalia tena yule msichana na kumwambia,
“Nielezee shida yako”
“Samahani, nilikuwa naomba kazi”
“Mbona unajiuma uma hivyo? Kazi gani unataka kwa kujing’atang’ata hivyo?”
“Nisamehe ila kilichonileta hapa ni kuomba kazi tu”
“Una shida ya kazi wewe? Umekuja kutafuta kazi kwa hivyo ulivyo? Umevaa kope za bandia, kucha za bandia, yani upo kama jini hivi kuna kazi gani utafanya wewe? Au kuna mwenye ofisi yake ya kumkaribisha mtu kama wewe! Kwanza huna maadili hata kidogo, umevaa nguo fupi hivyo, ndio walivyokudanganya kuwa ukienda kuomba kazi uende umevaa nguo fupi ili kumvutia bosi wa kiume? Haya umenikuta bosi mwanamke ambaye vyombe ulivyoviweka sina haja navyo na hakuna hata kimoja kilichonivutia juu yako, kwasasa inuka tu, jikung’ute na utoke nje”
Na kweli yule binti aliinuka pale kwenye kiti na kutoka nje kwa aibu kubwa sana ambapo nje alikutana na baba Angel ambaye kwa muda huo alikuwa akielekea ofisini kwake, basi alimuangalia na kutikisa kichwa, na moja kwa moja alipoingia ofisini alimkuta mkewe ambaye alianza kumsimulia kuhusu yule mwanamke.
“Kwakweli mume wangu pole sana, yani kumbe huwa mnakutana na vituko vya kiasi hiki!! Pole sana, ila mimi naomba nikuombe kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Nitaenda kuongea na mtu wa mapokezi ili watu wa ajabu ajabu wote wasiweze kuingia humu ofisini kwako, kama mtu anakuja ofisini kwako ajiheshimu basi! Sio kukaa kama shetani sijui la wapi, mtu kajibandika mikucha mirefu kama jini, kope nazo hadi zinataka kugusa nywele, halafu bila aibu anakuja kuomba kazi, tafadhari watu wa namna hii sitowataka katika ofisi yako”
“Sawa mke wangu”
Ni muda huo huo mama Angel alienda kuongea na yule mtu wa mapokezi na kumueleza kuwa ni aina gani ya watu ambao hawataki kwenye ofisi ya mume wake wala nini.
Na baada ya hapo alirudi ofisini ambapo na mume wake walijiandaa kwaajili ya kutoka tu.
 
SEHEMU YA 158


Iliuwa ni nyumbani kwa baba Abdi, ambapo kwa siku hii hakwenda kwenye shughuli zake kwani aliamua kupumzika tu kwa muda huo, mara alikuja mama wa mwanae na mwanae, huyo mwanamke kipindi cha nyumba aliwahi kuwa mke wake na aliitwa Nasma ila kwa kipindi hiki alijulikana kwa jina la mama Bahati kutokana na jina la mtoto wake.
Basi alifika hapo tena bila hata salamu alianza kuongea,
“Jamani, hivi hawa watoto wengine wakoje eeeh! Najua ni kwa kipindi kifupi tu nikasema basi na mimi nikae kidogo na mtoto wangu huyu, ila mnajua alichonitenda?”
Fetty aliuliza,
“Kwani kakufanyeje tena? Yani katika watoto wote humu ndani kidogo huyu Bahati ana afadhari, kwanza ni mtoto muelewa na asiye na makuu yoyote”
“Kheee mtoto muelewa! Jamani, huyu mtoto kuna mahali nilimtuma jana nikampa elfu kumi ila cha kushangaza, karudi nyumbani hana shilingi kumi kwa kifupi hakuwa na hela yoyote, halafu namuuliza ananijibu kirahisi tu kuwa kapoteza, jamani hiyo ni sahihi?”
Bahati akaangalia na baba yake ambaye alimuuliza,
“Eti Bahati, hiyo hela umeipeleka wapi?”
“Imepotea baba”
Basi huyu baba alitoa elfu kumi nyingine mfukoni mwake na kumkabidhi mama Bahati ambaye kwa kiasi flani alichukia zaidi na kusema,
“Sijapata kuona mwanaume anayeharibu watoto kama wewe, sasa ndio nini hivi! Yani huwezi kumsema mtoto jamani, hivi unajua kuwa elefu kumi ni kubwa sana yani kirahisi rahisi tu kama hivi unatoa nyingine”
“Kwani ulikuwa unataka nini mama Bahati?”
“Unatakiwa kumuadhubu huyu mtoto, hayo sio malezi nikwambie”
Fetty nae akachangia,
“Bora useme wewe, yani mimi humu ndani nishaongea hadi basi, hawa watoto hakuna kosa wanalofanya wakaadhibiwa yani hakuna kabisa, huyu baba muone tu hivi hivi ila yeye ndio anawahonga hawa watoto yani hawa watoto wanafanya wakitakacho kwani baba yao ana wachekea sana”
Basi baba Bahati akawaambia,
“Jamani mnajua mara nyingine hata mnacholalamika sikijui jamani, kwani hawa watoto tatizo ni nini? Kama leo huyo Bahati tatizo ni nini, kasema kuwa kapoteza hiyo hela, nianze kumuhadhibu kweli nitakuwa sijatumia utu kabisa. Halafu Nasma si nishakurudishia hiyo hela yako! Chukua nah ii ya usumbufu”
Alitoa elfu kumi nyingine na kumkabidhi, yani mama Bahati aliinuka na kusonya halafu kuondoka zake, yani hakuondoka na mtoto wala nini ilibidi Bahati amfate nyuma mama yake ili ajue kama bado ataendelea kuishi nae au ataanza tena kuishi pale kwa baba yake.
Fetty alimuangalia mume wake na kumwambia,
“Tena umenikumbusha, nilienda kwa mama yake Erica, kaniambia kuwa anaomba kuongea na wewe, kwahiyo tupange siku twende tukaongee”
“Basi huko ulienda kumuelezea kuwa mume wangu ana watoto kumi nje ya ndoa, tena utakuwa umeeleza kamavile hujui chanzo cha mimi kuwa na watoto wote hawa. Je niwatupe? Niwakatae au niwatenge? Wewe ni mwanamke wa pekee sana kwangu, huwa siwezi kusahau upendo wako kwangu, kunijali kwako kote huko huwa sisahau maana bila wewe sijui mpaka leo ningekuwaje Fetty, sema tatizo lako hutaki kuijua nafasi yako kwangu. Hebu fikiria ni kiasi gani umeweza kubadilisha maisha yangu na umeweza kubadilisha fikra zangu, fikiria kuwa ni kiasi gani huwa unasimama kunitukana na kuniambia maneno machafu, je kuna siku yoyote nimewabhi kusema kuwa nimechoka kwa matusi yako na kejeli zako kuwa kila mmoja aishi maisha yake? Kuna siku yoyote nimefungua mdomo wangu kusema hivyo! Unapataga hasira na kuaondoka nyumbani, kuna siku hurudi hata saa saba za usiku, je nimewahi kukulalamikia? Yote sababu nakujali sana na kukupenda ila sijui kwanini hutambui hilo mke wangu”
“Hujanijibu nilichokwambia, je tutaenda?”
“Hakuna tatizo tutaenda ila nilikuwa najaribu tu kukuelewa kuwa ni kwa jinsi gani ninavyokuthamini na kukujali katika maisha yangu, wewe ni mtu wa maana sana kwangu Fetty”
Fetty alimuangalia tu mume wake ila kwa kiasi Fulani alikuwa akiyafurahia yale maneno ambayo mume wake alikuwa akimwambia.
 
SEHEMU YA 159

Wakati wakina Erica wanatoka darasani, ilibidi Samia ampe Erica mikanda ambayo aliamuahidi kuwa atampelekea,
“Ile mikanda ya ngumi nimekuja nayo”
“Basi Erick atafurahi sana”
“Ila hongera sana Erica, una kaka mpole huyo, halafu mzuri mwenyewe”
“Mmmmh na wewe Samia jamani! Ila ni kweli kaka yangu ni mzuri”
“Yani hilo nakupa hongera sana, yani ana mwili wa kiume kaka yako ujue, kwanza mrefu yani anapendeza”
Erica alicheka ila kwa kiasi Fulani alimshangaa sana Samia kwa kumsifia kaka yake wakati alikuwa akimuona Samia kuwa ni mdogo pia, kwahiyo kitendo cha kumsifia kaka yake kilimshangaza kidogo.
Basi Erica alifika na nyumbani kwao na kuingia muda mmoja alioingia Erick na moja kwa moja alimuonyesha ule mkanda ambapo aliletewa na Samia, na baada tu ya kubadilisha nguo kwa muda huo walienda sebleni na kuuweka na kuanza kuangalia, muda huu walikaa sebleni pamoja na Vaileth.
Ilivyofika jioni, Junior nae alitoka shuleni, ni alikuwa ametoka kwenye mtihani, basi alivyoingia ndani wote walimpa pole kwa mitihani ambayo alikuwa ameifanya siku hiyo ambayo ndio ilikuwa inaishia.
Basi Vaileth aliinuka na kuelekea jikoni ili kumuandalia chakula Junior ambaye alitoka kufanya mitihani, ila Junior nae alienda jikoni na kumkumbatia Vaileth, ambapo Vaileth leo alimuuliza kuwa ni kwanini anapenda kufanya vile,
“Nilkimaliza mitihani kabisa nitakwambia sababu ya mimi kufanya hivi!”
Basi Vaileth aliandaa chakula na wote walifika na kukaa na kula kile chakula ila baada ya kula hata wakina Erica waliondoka kwamaana hiyo hata wazazi wao waliporudi siku hiyo hawakujua kuwa watoto wao walikaa kuangalia video kwa siku hiyo.

Steve, siku ya leo alivyoondoka pale kazini alifatwa tena na Sian a kuanza kuongea nae,
“Kwani wewe Sia una nini?”
“Sina tatizo lolote, ila kesho nitamleta mtoto wetu hapo dukani”
“Kivipi na anakuja kufanya nini?”
“Yule ndio mrithi wa hilo duka kama hujui, kama una ujasiri basi muulize huyo Erick hilo duka amelitengeneza kwasababu gani? Na ilikuwaje hadi akalianzisha? Nani aliyempa wazo la yeye kuwa na duka kama hilo? Ukiweza kumuuliza hayo na akakujibu kwa hakika utaelewa ni kwanini nafanya hivi mimi kwahiyo kesho nitamleta mwanangu hapo dukani, yeye ndiye mrithi wa halali wa hilo duka”
Yani Steve bado alikuwa akimshangaa sana Sia, yani alimtafakari bila kumpatia jibu la moja kwa moja, basi aliachana nae pale na kuondoka huku akitafakari sana yale maneno ya Sia huku akisubiri kwa hamu siku ya kseho yake ambayo Sia atamleta mtoto wake.
Siku hiyo moja kwa moja alirudi tu nyumbani kwao na kuamua kupumzika huku akitafakari mambo mbalimbali.
Kesho yake Steve alifika dukani na kuanza kufanya mambo mbali mbali huku akijua kuwa ujio wa Sian a mtoto itakuwa muda sio mrefu, ila haikuwa hivyo kwani pale dukani kwa muda huo alifika baba Angel na mafundi wa kufunga kamera kwenye lile duka kale, basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, ila baba Angel hakumuuliza chochote cha kuhusu ujio wa Sia wala nini, basi Steve aliamua kumuuliza kwa utani tu,
“Eti kaka samahani, hivi ni nani aliyekupa hii idea ya kuanzisha duka hili au eneo hili?”
“Unajua kuna siku moja nilikuwa mahali kwenye hili eneo, nakumbuka nilikutana na mvulana mmoja hivi ila sijawahi kumuona hadi leo mtoto yule, basi yule mvulana nilijikuta nikiongea nae mambo mengi sana, moja wapo la jambo ambalo nilikuwa nimeongea nae ni kuwa watu wa eneo hili wana uhitaji sana na huduma hizi ambazo nimeweka kwenye hii biashara yangu, yule mtoto aliniambia kuwa angekuwa na uwezo basi angefanya yeye hicho kitu, kwakweli niliumia kumsikiliza na pale niliamua kumpa pesa kidogo na tangia hapo ndio nikaanza kupafanyia kazi eneo hili. Na ndiomana hili duka nilipolimaliza basi mtu wa kwanza kumleta hapa ni mtoto wangu wa kiume aitwaye Erick, kwani hili ni duka lake yani ni mali ya mtoto wangu Erick”
“Ooooh! Hapo nimekuelewa tayari bosi wangu”
Basin a yule mtu aliyekuwa akifunga kamera, alizifunga kwenye duka lile na baada ya hapo baba Angel alimuaga Steve kwa kumwambia,
“Nitamleta tena mwanangu Erick ili umfahamu nan a nimfahamishe pia kuwa hili duka ni lake”
“Sawa, hakuna tatizo”
Mwisho wa siku baba Angel akaondoka zake, ila Steve alikuwa na maswali mengi sana akijiuliza bila majibu ya aina yoyote ile ila pia Sia hakufika kabisa siku hiyo hadi siku ikaisha wala hakuonekana Sia kabisa.
 
SEHEMU YA 160

Siku hiyo Erick akiwa shuleni wala karibia na muda wa kutoka, alishangaa tu kuona baba yake akiwa ameenda kumfata pale shuleni, kwa upande mwingine alifurahi sana kwa kitendo cha kufatwa na baba yake kwani aliweza kuona ni kwa jinsi gani baba yake alimpenda sana.
Basi baba yake aliongea nae kuwa anataka apitie nae kwanza kwenye ile biashara yake, waliingia kwenye gari huku wakiongea mawili matatu,
“Najua wewe ni mtoto wa kiume, sio mropokaji kama dada yako Erica, sasa nataka twende tena huku kwenye duka maana hili ni duka lako”
Erick alitabasamu, kisha baba yake akaendelea kuongea,
“Nitakuonyesha vitu vyote vya muhimu kwenye duka hilo mwanangu, nataka hata muda mwingine kama zile siku za mwisho wa wiki uwe unaenda dukani kuangalia maendeleo ya duka”
“Mama atakubali kweli niwe natoka?”
“Nitaongea nae, lazima mama yenu aelewe kuwa wewe ni mtoto wa kiume, tunavyomlea Angel na Erica ni tofauti kabisa na tunavyotakiwa kukulea wewe, leo na kesho mimi nisipokuwepo ni nani atasimama kwaajili ya dada zake? Yani wewe kaka mtu ukishindwa kusimama unajua nini kitatokea? Ndiomana nataka kufanya haya mapema sana, hii ni biashara ya kwanza, hata biashara ya Erica nitakupeleka wewe kwanza ili ukaone vizuri ilivyo nataka mwisho wa siku niwe nimewafundisha watoto wangu kuwa wafanyabiashara wazuri zaidi yangu, sio mimi ni mfanyabiashara mzuri halafu watoto wangu hawajui chochote kuhusu biashara, yani hii kitu inaniumiza sana kichwa mjue. Kwahiyo mwanangu ujue nina maana kubwa sana kufanya hiki ninachofanya”
“Sawa baba, nimekuelewa na ninakuahidi kuwa sitakuangusha kabisa, yani usiwe na mashaka yoyote juu yangu”
Basi walifika hadi dukani ambapo Baba Angel alimtambulisha Erick kwa Steve pale, na pia kumuonyesha mambo yote ya muhimu Erick, kisha akamwambia Steve,
“Naomba huyu mtoto anapokuja umpe ushirikiano unaotakiwa maana huyu ndio wa kuwaongoza dada zake, kwahiyo hakuna chochote kwasasa kitakachofanywa kwenye duka hili bila kumshirikisha huyu. Kwa kifupi huyu ndio bosi wako”
“Sawa sawa nimekuelewa”
Erick alifurahi sana kwani aliona baba yake kampa heshima kubwa sana na aliona kuwa ile kazi ndio iliyokuwa inamfaa yeye kwani siku zote alitamani sana kukaa dukani na kufanya biashara ya duka kuliko kukaa darasani muda wote.
Walipomaliza pale, walimuaga Steve na moja kwa moja baba Angel na mtoto wake waliondoka na kuelekea nyumbani, yani siku hiyo walionekana tu wamerudi pamoja ila hawakuwaelewa tu kuwa wamepitia sehemu gani hadi kufika pale wakiwa pamoja kama vile.

Ilikuwa siku ya kumaliza mtihani wa mwisho na siku hiyo walimaliza mapema sana, na ilikuwa ni furaha kubwa kwa wanafunzi wote wa kidato cha nne, basi kwa shule ya wakina Angel walipanga kesho yake ndio iwe siku ya mahafali kwa wanafunzi wale waliomaliza kidato cha nne.
Kwanza kabisa wote walikutanika sehemu moja ambapo walimu waliwapa soda kila mmoja na vitu vya kutafuna tafuna kama kujipongeza kwanza kwa kumaliza mtihani, basi kila mmoja alikuwa na furaha sana, basin i siku hiyo ambayo Husna alimkumbusha Angel kwa kumuuliza,
“Hivi Angel, siku ile wakati wote tumeitwa pale kuungumza ni kitu gani kilitokea hadi wewe na Samir mlichelewa kuja?”
“Sijui, ila bora umenikumbusha, tabia mbaya hiyo Husna yani uliniacha darasani ukitegemea nini?”
“Hivi unajua kuwa mimi sikuwepo darasani wala nini? Hata mimi mwenyewe nilishanga tulipoenda pale wakati mwalimu akizungumza mara watu wakageuka nyuma, kuangalia ni wewe na Samir mlikuwa mkitokea, hata sijui ni kitu gani kilitokea katikati”
Mara Samir akawafata katika maongei yao na hapo akasema mbele ya Husna,
“Husna, naomba wewe uwe shahidi wa haya maneno yangu nitakayotamka leo. Angel, sijasema unikubali au usinikubali ila mimi nasema kile kilichopo moyoni mwangu, kiukweli nakupenda sana Angel, yani hilo haliwezi kubadilika na kitu chochote kile, hata iweje ni siku zote nitaimba wimbo huu mmoja kuwa nakupenda sana”
Husna alicheka na kuguna ila Angel alishindwa kujibu kabisa. Muda kidogo alifika mwalimu na kumuita Angel kwaaana aliitwa na mzazi wake, kwahiyo Angel ilibidi aachane nao na moja kwa moja kwenda alipoitwa na mama yake.
Mama yake alimkumbatia kwa furaha sana huku akimpongeza kwa kumaliza mitihani yao, na kumwambia,
“Haya panda kwenye gari tukamchukue na Junior, yani leo nimefurahi sana jamani. Twendeni mahali kwanza mkale mnachotaka halafu ndio tutarudi nyumbani kwaajili ya maandalizi ya hayo mahafali yenu”
Angel hakuwa na sababu ya kukataa kwani moja kwa moja alipanda kwenye gari ya mama yake na kuondoka eneo lile la shule yao na moja kwa moja walienda shuleni kwakina Junior ambapo walimchukua naye Junior na kuondoka nae, kisha mama Angel aliwapeleka wanae kwenye duka lao kubwa la nguo na kuwataka wachague nguo ya kuvaa kwa muda huo ambapo walichagua na kubadilisha zile sare za shule halafu moja kwa moja alienda nao mahali ambapo alisema kuwa wataenda kupata chakula wakitakacho kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 161

Wakati wametulia wakila chakula hoteli yani mama Angel, Angel pamoja na Junior, mara muda huo alionekana Husna akiwa ameongozana na James ambao walienda pale kuwasalimia.
Ila leo mama Angel aliamua kumuuliza swali huyu James,
“Samahani, kwani wewe baba yako ni nani na yuko wapi?”
Junior alimuuliza mamake mdogo,
“Mbona umemuuliza hivyo mamdogo?”
“Aaaah Junior, unajua huyu kafanana sana na baba yako”
“Mmmh tuseme huyu ni ndugu yangu!!”
James akajibu,
“Kwakweli mimi sijui baba yangu alipo, nimeishi na mama kwa kipindi chote hiki na kwasasa tunaishi na mjomba wetu na ndiye anayetulea. Hata hapa tulikuja nae ila alipoona tu meza hii basi mjomba aliondoka”
Mama Angel akatingisha kichwa kidogo na kusema,
“Mjomba wenu ndio huyo George?”
“Eeeeh ndio”
Basi mama Angel akatoa kadi yake yenye namba na kumkabidhi James kisha akamwambia,
“Mpe huyo mjomba wako, mwambie kuwa nahitaji kuzungumza na yeye maana nahitaji sana kufahamu kuhusu wewe, ni vyema kwa ndugu kufahamiana. Unaitwa James, na kiukweli ni kuwa unafanana sana na James, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa sana kwa James kuwa baba yako halafu huyu Junior ni ndugu yako”
Basi kwavile walimaliza kula, hivyobasi waliinuka na kuwaaaga Husna na James pale na kuondoka zao kurudi nyumbani.

Kesho yake walijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye mahafali ya siku hiyo ambayo shule ya wakina Angel ilikuwa imepanga kufanya vile, basi ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wazazi wa wanafunzi wale walikuwa wamekutanika pale shuleni ili kufatilia shughuli nzima ya mahafali inavyoenda.
Wakati wameshakabidhiwa vyeti vyao vya kawaida pale shuleni ilikuwa ni furaha ambapo walipiga picha na mambo mengine yaliendelea, basi wakati wa kula chakula, Angel alishangaa akivutwa mkono na Samir nae alijikuta akimfata tu Samir alipompeleka ambapo Samir alimpeleka hadi eneo ambalo hapakuwa na watu kwa wakati ule na kuanza kumwambia tena,
“Angel, nakupenda sana ten asana. Wewe ni mwanamke wa maisha yangu, bila wewe siwezi kitu”
Angel alikuwa akimuangalia tu Samir kwani alijikuta kuwa Samir akimuongelesha kitu na yeye kushindwa kumjibu kabisa zaidi zaidi kuishia akimuangalia tu.
Basi Samir alimvuta karibu yake na muda huo huo alianza kumbusu Angel mdomoni, ila muda huo mama Angel nae aliinuka kuongea na simu ila kutokana na makelele ya pale aliamua kuzunguka kidogo ili aweze kusikilizana na aliyempigia, kwahiyo kitendo cha kumkuta Samir na Angel kilimshtua sana kwa wakati huo.
 
SEHEMU YA 162


Basi Samir alimvuta karibu yake na muda huo huo alianza kumbusu Angel mdomoni, ila muda huo mama Angel nae aliinuka kuongea na simu ila kutokana na makelele ya pale aliamua kuzunguka kidogo ili aweze kusikilizana na aliyempigia, kwahiyo kitendo cha kumkuta Samir na Angel kilimshtua sana kwa wakati huo.
Yani hadi simu aliiweka pembeni na kwa hasira alisogea na kumchukua Angel, na muda huo huo alienda kuwaita ndugu baadhi waliokuwa pale shuleni na kuondoka nao, kwahiyo aliondoka na Angel akiwa wala hajamaliza mambo ya mahafali wala nini.
Moja kwa moja walienda nyumbani yani mama Angel alikuwa na hasira sana kwa wakati huo, basi baba Angel ne muda huo alirudi nyumbani kwani alikuwa akitaka kupumzika kidogo halafu aunganishe shuleni kwa mwanae ambako ndio kulikuwa na mahafali, ila alishangaa kumkuta mkewe nyumbani tena akiwa na hasira sana, basi moja kwa moja alienda nae chumbani kuzungumza nae,
“Kwani vipi? Mbona unaonekana ukiwa umejawa na jazba kiasi hiko mke wangu? Na je mahafali yameisha kweli?”
“Yaishe wapi? Huyu mtoto ni punbguani sijapata kuona jamani, yani Angel ni punguani, punguani namba moja. Kweli wa kumkuta kasimama na huyo Samir wake kweli wamekumbatiana!”
Ila mke wangu jamani, unajua kuna kitu nafikiria hapa kuhusu huyo Angel na Samir inaonyesha wanapendana sana yani mimi na wewe tutajitahidi kwa kila hali ila bado itashindikana kuwatenganisha”
“Inamaana umeshindwa tena kumlinda Angel?”
“Sijasema kuwa nimeshindwa”
“Sasa unawezaje kumuachia huyo Samir kuwa na Angel? Huyo sio mwanaume bora katika maisha ya mtoto wetu, ila leo nimeona ule uamuzi wako wa kumpeleka Angel Africa kusini basi ufanye kazi, maana nadhani akiishi mbali ndio itakuwa vizuri zaidi”
“Hakuna tatizo juu ya hilo, ila tu nilikuwa nakwambia mke wangu tunatakiwa kuwa makini sana. Unajua huyo Angel na Samir bado hawajawa pamoja kwahiyo wanaona kila tunachofanya ni kuwazuia tu, ila tungejaribu kuwaacha pamoja japo kwa mwezi mmoja tu, watachokana wenyewe nakwambia na kila mmoja ataona bora aendelee na mambo yake kuliko kuendekeza mambo ya mapenzi”
“Hapana mume wangu, sipo tayari kwa hilo. Ni heri Angel aende sehemu ya mbali”
“Sawa, ila mimi naona basin i vyema kama akienda kuishi na mama yangu maana nae anaishi peke yake halafu yupo mbali kule na anatamani sana kuishi na mtoto”
“Ooooh napo ni wazo zuri tu”
Mama Angel hakuwa na tatizo juu ya Angel kwenda kuishi na mamake na baba Angel maana mama huyo mara nyingi alikuwa yupo na mambo yake tu kwahiyo hakuweza kumnyanyasa au kumtesa mtoto.
Basi wakakubaliana kuwa Angel watampeleka huko sababu ni mbali pia kwahiyo waliona itasaidia sana, ila baba Angel aliona ni vyema kwa swala hilo kulifanya mapema, hivyo siku hiyo hiyo aliwasiliana na mama yake na kukubaliana kuwa kesho yake aweze kumpeleka Angel huko kwani mama yao nae alisema kuwa kwa siku ya kesho ndio atakuwa na muda mzuri zaidi wa kupokea wageni.
 
SEHEMU YA 163

Usiku wa siku hiyo, Samir alikuwa nyumbani kwao baada ya uchovu wa siku nzima hiyo, kwahiyo alitulia kwao kwa muda huo akiwa amechoka haswaaa ila alishukuru sana kwa ile siku kuisha.
Mdogo wake Samia alimfata kaka yake na kuongea nae kidogo,
“Hivi umejisikiaje kuwepo kwenye mahafali bila ya wazazi? Yani mama hayupo wala baba hayupo?”
“Nilikuwa kawaida tu, kwani wazazi wetu ni kawaida kwa wao kutokuwepo katika matukio muhimu hivi kwahiyo hakuna kitu ambacho nimeshangaa wala nini”
“Ila kaka, hivi unamuelewaga baba?”
“Mimi sijawahi kumuelewa huyu baba hata mara moja, yani hakuna hata siku moja ambayo nimewahi kumuelewa huyu baba, kwanza sina uhakika kama ni baba yetu mzazi”
“Kwahiyo sisi tuna baba mwingine eeeh!”
“Ndio, hebu wewe jiulize kitu kimoja. Watoto wengi wa huyu baba huwa wanapelekwa kwa bibi yani kwa mama yake, ila sisi tukitaka kwenda kwa bibi tunapelekwa kwa bibi mzaa mama, yani hakuna siku hata moja tumeenda kwa mzaa baba, na yote tisa kumi ni kuwa hajawahi kuja hapa hata mara moja.hivi bado unaamini kuwa huyu ni baba yetu?”
“kweli kabisa kaka, huyu sio baba yetu ila baba yetu ni nani sasa?”
“Hilo swali, jibu lake analo mama tu. Ila ipo siku ambayo mama itabidi tu atueleze ukweli halisi kuhusu baba yetu mzazi”
Samia alikubaliana na maneno ya kaka yake, na baada ya hayo walienda kufanya tu mambo mengine na moja kwa moja kwenda kulala.
Ila usiku wa siku ile Samir alipigiwa simu na mama yake na kuanza kuongea nae,
“Mwanangu Samir, wakati unasubiri majibu kuna kazi nimekutafutia huku. Kwahiyo kesho au keshokutwa utatakiwa kusafiri kuja huku, nadhani tunaelewana”
Hakuna tatizo mama, ila je ni kazi gani?”
Utaijua huku huku”
Samir hakutaka kubishana chochote na mama yake zaidi ya kukubaliana nae tu kuwa ataenda kufanya kazi ambayo mama yake alikuwa amemtafutia kwa kipindi hiko.
Kulipokucha ilibidi Samir ajiandae maana mama yake alimtafuta tena na kumtaka aweze kusafiri kwa lengo la kwenda hiyo sehemu, kwahiyo Samir alijiandaa na kuondoka kwahiyo alimuaga tu mdogo wake na kuondoka zake yani alisafiri kwa muda huo.

Leo Baba Angel alifika na Angel kwa bibi yake yani kwa mama yake mzazi, yule mama aliwakaribisha vizuri kabisa na kuongea mawili matatu na mtoto wake,
“Kwahiyo mmeona ni vyema aje apumzike kidogo huku kwangu?”
“Ndio mama, ukizingatia huna mtoto mwingine yoyote yule hapa nyumbani!”
“Ni kweli, hata mimi nimefurahi kwa kumleta hapa”
Basi Angel alionyeshwa tu chumba ambacho atakuwa analala kwa kipindi hiko kisha baba Angel aliaga kwa mama yake kuwa anaondoka, basi walipotoka nje mama yake alimuuliza tena,
“Hivi kuhusu swala la kumleta huyu mtoto kwangu umekubaliana vizuri na mama yake kweli?”
“Ndio mama, na mama yake ndio kaona kuwa ni vyema kama akija huku kupumzika kidogo maana ndio kashamaliza mitihani”
“Yani sina tatizo, ila mwanangu. Hivi na mke wako mlizungumza vizuri kuhusu huyu mtoto kweli?”
“Kivipi mama?”
“Usinifikirie kwa ubaya, ila toka huyu mtoto akiwa mdogo kabisa nilikwambia mwanangu kuwa mtoto hafanani na sisi huyu ila nakumbuka ulinijibu kuwa kitanda hakizai haramu, siwezi kukataa kwani mimi na mama wa mkeo ni marafiki wakubwa sana, ila kuna ulazima wa kufatilia uhalisia wa huyu mtoto ingawa najua unapingana na ukweli kwani vitu vingi sana ushawekeza kwa kutumia huyu mtoto. Usichukie mwanangu, ni kawaida tu hii, nilikuwa nakupa changamoto tu”
Baba Angel alimuangalia mama yake kisha alimuaga na kuondoka zake, ila pia aliona kuwa ile sio sehemu sahihi kwa mwanae, sema kwa kipindi hiko hakutaka mtoto huyo aende Afika kusini kwani alitaka kama akimpeleka huko basi mtoto asiwe peke yake, ndiomana kwa kipindi hiko aliona ni vyema kumleta Angel huku alipomleta.
Baba Angel alipotoka tu kwa mama yake, moja kwa moja alienda kwa dada yake, na alimkuta na kuanza kuongea nae, ambapo dada yake alimuulizia kuhusu habari za Angel nae alimuelezea,
“Ila nyie ni mna vilanga sijapata kuona katika maisha haya jamani, mbona mmekuwa na vilanga hivyo na mke wako. Angel nimeishi nae vizuri kabisa hapa hadi kamaliza mitihani, ila huyo mkeo kumkuta kidogo tu Angel sijui na mwanaume basi mshipa wa fahamu ushamtoka kabisa, jamani Angel ni mtoto wa kike hivi mnaweza kumbana hadi lini? Halafu malezi mnayompa Angel sio malezi wala nini, mfundishe mtoto atambue baya na jema yani atambue yote na ikitokea amefanya kitu yani ajue kama hiki ni kibaya au hiki ni kizuri, hivi kwa staili hii inayofanyika mtaweza kweli kumuweka Angel katika mstali unaotakiwa jamani!! Anazidi kukua yule, utamshikilia hadi atakapoolewa utaweza?”
“Sio kosa langu lakini”
“Sio kosa lako nini, halafu mmekubaliana kumpeleka mtoto kwa mama yako, hivi yule mama toka lini kalea mtoto? Wewe mwenyewe hakukulea wala nini, sema tu ukweli si umelelewa na mamako mdogo wewe! Je alikulea mama yako? Aaache kuwaza mambo yake akaanze kumuwaza Angel jamani, yani mara nyingine hadi mnakera, huyo Erica kabeba mtoto bila hata ya kunishirikisha halafu saivi unaniambia kuwa mmempeleka kwa mama yenu, jamani na msinishirikishe kwa lolote lingine lile. Mtu unaweza ukawa na pesa ila usiweze kulea watoto katika misingi inayotakiwa, sasa unachofanya kwa huyo Angel sio kujenga bali kubomoa”
Tumaini alionekana kuchukia haswaa kwa kitendo cha kumuondoa mtoto bila ya kushirikishwa kitu chochote kile.
Baba Angel hakutaka kumaliza maneno pale kwani muda ule ule aliaga na kuondoka zake tu.
 
SEHEMU YA 164

Kesho yake Steve akiwa dukani siku hiyo, ndipo Sia alipoenda na binti mmoja na kumtambusha pale kwa Steve, kwakweli Steve alimshangaa na kumuuliza,
“Ni nani huyu mtoto?”
“Huyu ndio mwanetu”
“Hebu acha masikhara, kwani sijui kama mtoto alikuwa ni wa kiume au? Huyu mtoto ni nani?”
“Huyu mtoto anaitwa Samia”
“Kheeee Samia! Ni mtoto wa nani na umemtoa wapi?”
Sia alimuangalia Samia na kumwambia,
“Chagua chochote unachokitaka kwenye duka hili kama ambavyo nilikuahidi”
Basi Samia alianza kuchagua ila Steve alimzuia na kufoka pale, kwanza alimfokea Sia,
“Unamaanisha nini lakini? Kwani wewe mwanamke una nini eeeh! Sia sijawahi kukupiga ila ukiendelea na huu upuuzi kwakweli nitakupiga”
“Thubutu, mimi ndiye niliyekufundisha maisha wewe, unipige thubutu”
“Unajua huna akili wewe, unawezaje kwenda kuchukua watoto wa watu huko na kuwaambia sijui waje wachague wanachokitaka jamani kutoka kwenye hili duka? Hili duka ni lako”
“Kumbe hujui eeeh! Hili duka ni langu ndio, maana hili duka ni la mtoto wangu”
Steve alitikisa kichwa na kucheka,
“Unajua mara nyingine, hebu tuwe na akili basi, usifanye umasikini ukakudhalilisha kiasi hiko unachotaka, hiyo ni aibu unayofanya. Kila siku kubadili watoto, hata kama mwanao ndio ametoa wazo hili la kuwa na duka eneo hili ila bado huwezi sema kuwa duka hili ni la mtoto wako. Kwakweli hii sasa umezidisha”
Steve akaona bora tu atumie uanaume wake, kwani alimvuta Sian a kumtoa nje ya duka lile kisha aliongea na mlinzi kuwa mwanamke yule asimruhusu tena kusogelea duka lile, halafu alirudi dukani na kumwambia Samia,
“Wewe mtoto ondoka na huyo mama yako sijui nani yako”
“Hapana sio mama yangu halafu mimi na yeye hata hatufahamiani”
“Duh! Kwahiyo kakutoa wapi?”
“Aliniuliza kama namfahamu Erica na Erick nami nilimjibu kuwa nawafahamu, basi akasema ananipeleka kwenye duka lao na nikachague kitu chochote ninachokitaka kwenye hili duka ila mimi sifahamiani na huyu mama wala nini”
Steve alimuangalia huyu mtoto na kumtaka tu na yeye aondoke ila kiukweli hakuelewa ni kwanini Sia anafanya vitu vya namna ile.
 
SEHEMU YA 165

Muda wa kutoka Steve alijiandaa kwaajili ya kwenda nyumbani kwao, kwahiyo alifunga vizuri duka ila wakati anaondoka aliona kuna kijana mdogo ambaye alikuwepo karibu na lile duka, basi alijikuta akipatwa na shauku ya kuongea na yule kijana,
“Habari yako kijana”
“Salama, shikamoo”
“Marahaba, samahani unaitwa nani?”
“Naitwa Elly”
“Mbona upo hapa kwa muda huu?”
“Ni hivi, leo kuna jambo nimeambiw ana mama yangu kuhusu hili duka”
“Jambo gani?”
“Mama yangu kaniambia kuwa hili duka ni mali yangu, kwahiyo kwa siku ya leo nikae hapa kumsubiria mmiliki ili anikabidhi duka langu”
Steve alimuangalia sana huyu kijana kisha akamwambia,
“Huyo mama yako anaitwa Sia eeeh!”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Naomba ongozana na mimi”
Kisha Steve alisimamisha bajaji na kupanda na yule kijana halafu akaondoka nae hadi nyumbani kwao.
Moja kwa moja alienda nae chumbani kwake na kuanza kuongea nae,
“Hivi unajua ya kuwa huyo mama yako Sia ni mtu ambaye hana akili timamu? Iko hivi, unionaye hapa, nimewahi kuwa mume wa mama yako”
“Kheee inamaana wewe ndiye baba yangu!”
“Inawezekana ikawa hivyo ila mama yako si mkweli katika maisha yake, na ndiomana anakufanya uwe unatangatanga tu bila kujua uelekeo wako wa aina yoyote ile. Kwasasa naomba ukae hapa na mimi, najua ni kitu gani kitafanya ili kuweza kukusaidia maana yale unayoishi sio maisha hata kidogo”
Basi kwa siku hiyo Elly alilala hapo nyumbani kwao na wakina Steve, yani hata Steve hakutaka kujua kama huyu ni mtoto wake au la sema alichoona yeye kuwa ni sawa kwa wakati huo ni kumuokoa huyu mtoto toka mikononi mwa Sia kwani alimuona kama mtu asiyekuwa na akili timamu.

Kulipokucha, Steve alijiandaa na kwenda kazini na aliondoka na yule mtoto ila walipofika tu pale nje ya duka, walimkuta Sia yupo pia, kiuweli Sia alipomuona Steve na yule mtoto alimfata na kumzaba vibao viwili vya nguvu kisha alimchukua yule mtoto na kuondoka nae, yani Steve hakumuelewa kabisa ni kwanini anafanya kile alichokuwa anakifanya, zaidi zaidi aliamua tu kwenda dukani na kuanza biashara kama kawaida ya siku zote.
Leo kwenye duka alifika Erick kama ambavyo aliambiwa na baba yake kuwa awe anakuja kutembelea duka hilo mara kwa mara, ila leo Steve aliweza kuongea mambo mengi sana na huyu Erick,
“Unajisikiaje kuwa mmiliki wa hili duka?”
“Ila sidhani kama hilo ni swali maana baba yangu ana miliki maduka mengi sana, kaniweka hapa ili niweze kuzoea biashara na si vinginevyo kwahiyo hii kwangu sio ajabu wala sio miujiza wala nini”
Steve aliamua tu kuongea nae mambo mengine huyu Erick kwani alionekana kuwa na majibu sana, basi Erick alitembelea tembelea lile duka kiasi kisha aliondoka zake na kurudi kwao.
Erick alipofika kwao tu, alifatwa na dada yake ambaye alimuuliza,
“Haya, leo ni mwisho wa wiki ila uliondoka ukaenda wapi?”
“Nilienda kuangalia biashara ya baba, je unataka siku twende wote?”
“Ndio, tena itakuwa vizuri sana”
Wakati wanaongea pale nje alifika Samia na kuanza kusalimiana nao kisha aliwaeleza yaliyotokea yote kwa yeye kupelekwa kwenye duka lao na kuambiwa kuwa achague anachokitaka,
“Unamfahamu huyo mama?”
“Hata simfahamu jamani, yani yule baba wa dukani nae aliniuliza swali kama hilo”
“Haya, ulikuwa ukifanya nini muda huo hadi kuchukuliwa na huyo mama?”
“Mimi nyumbani kwetu naishi kwa uhuru sana kwanza huwa nafanya ninachotaka mimi kwa muda ninaotaka mii, kwasasa mama na kaka yangu wote hawapo kwahiyo nyumbani huwa nabaki mimi na msichana wa kazi tu, nilitoka kidogo na kukutana na yule mama”
“Kwahiyo unapoishi sio mbali na lile duka?”
“Ni kweli sio mbali, leo twendeni kwetu mkapafahamu”
Waliona kuwa ni jambo zuri tu, hivyo moja kwa moja walienda ndani na kumuaga Vaileth halafu wote watatu yani Erick, Erica na Samia waliondoka, wakati huo Erick ndio alikuwa akiendesha lile gari.
 
SEHEMU YA 166


Nyumbani Alibaki Vaileth akiwa na Junior maana kwa kipindi hiko Junior aligoma kabisa kurudi nyumbani kwao, kwahiyo yeye aliona kuwa ni vyema kuendelea kuishi kule kule kwa mamake mdogo kuliko nyumbani kwao, basi Vaileth alienda jikoni kuandaa chakula, ila Junior pia alienda jikoni, ila leo Vaileth aliamua kumuuliza Junior ni kwanini anapenda kumfata fata vile,
“Junior, kwanini lakini? Unajua kipindi kile unasoma hadi unaingia kwenye mitihani nilikuwa najiuliza sana kuwa ni kitu gani kinachopelekea wewe kuwa karibu na mimi kiasi hiki!”
“Unataka kukijua Vaileth?”
“Ndio, niambie ni kitu gani?”
“Usiwe na haraka sababu nitakwambia kitu kinachonipelekea mimi kuwa hivi kwako”
“Mmmmh!”
“Usigune, ila nitakwambia tu”
Basin a siku hiyo Junior alimsaidia Vaileth katika mapishi yote na walipomaliza walitulia na wote waliporudi pale nyumbani walikula na kwenda kupumzika, yani wazazi wakina Erica hata hawakujua kama siku hiyo watoto wao walitoka nyumbani wala nini yani hawakujua chochote kile.
Wakati wa kulala, Vaileth alishangaa muda huo Junior akiingia chumbani kwake, basi alimuuliza kwa mshangao,
“Junior, unafanya nini chumbani kwangu?”
“Nyamaza Vaileth, kuna kitu nataka kukwambia”
“Kitu gani?”
Junior alimsogelea Vaileth na kuanza kumbusu, yani Vaileth hakuweza kumsukuma Junior wala hakuweza kumfukuza, zaidi zaidi alijikuta akishirikiana nae na mwisho wa siku walilala pamoja chumbani kwa Vaileth.

Siku hiyo asubuhi, mama Angel aliongea na baba Angel kuhusu Junior,
“Unajua nini, mama Junior jana kanipigia simu kuwa anamtaka mtoto wake”
“Na yeye aache kutusumbua akili, kwanza huyu mtoto sio mtoto mdogo, tumuache Junior aamue mwenyewe ni lini ataenda kwa mama yake ila sio mtu ambaye tutampeleka kama mzigo au kitu gani?”
“Unayoyasema ni kweli, ila pia tunaweza kumshauri Junior aende tu akamsalimie mama yake”
Basi wakaona kuwa jambo hilo lipo sawa, na moja kwa moja walipotoka waliamua kumshauri Junior jambo hilo ila na yeye aliwaomba jambo moja,
“Mnajua siku hizi nimebadilika sana kiasi kwamba sipendi kutembea mwenywe, kwahiyo mimi nawaomba kama hamtojali basi niende kumsalimia mama nikiwa nimeongozana na Vaileth”
“Ooooh, hilo sio tatizo hata kidogo, unataka kwenda lini ili tumwambie Vaileth afanye kazi zake mapema siku hiyo?”
“Nadhani kesho au kesho kutwa”
“Basi tutaongea nae, hakuna tatizo”
Mama Angel alikubaliana na Junior ila hakujua kuwa ni kitu gani kilichopo baina ya Junior na Vaileth.
Basi siku hii ya leo walijiandaa na kwenda Kanisani kama kawaida, na walienda wote kwa pamoja na walipomaliza ibada walirudi nyumbani wote kwa pamoja.
Muda huu Erick alienda moja kwa moja chumbani kwa Erica na kumuuliza,
“Nasikia kuna viatu ulinunuliwa na mwanaume, viko wapi?”
“Viatu nilinunuliwa na mwanaume? Nani amekwambia?”
“Nionyeshe kwanza viko wapi?”
“Jamani, ni siku nyingi mambo hayo, nani kakwambia Erick?”
“Mimi ni kaka yako na ninapaswa kujua mambo yote yanayoendelea juu yako. Viko wapi hivyo viatu Erica?”
Ilibidi Erica atoe hivyo viatu na kumuonyesha kaka yake ambaye aliviangalia na kusema,
“Kuanzia leo Erica nakuomba, unapohitaji jambo lolote lile niambie mimi, nakuomba sana isije ikatokea tena ukanunuliwa kitu na mwanaume”
“Ila mbona hakuna ubaya!”
“Erica, elewa kaka yako naongelea kitu gani. Nimesema sitaki hiki kitu kijirudie kabisa”
Kisha Erick alionekana kutoka kwa hasira, ila Erica hakuelewa kuwa kaka yake alipewa ile habari na nani mpaka kachukia kiasi kile.
 
SEHEMU YA 167


Angel akiwa nyumbani kwa bibi yake huyu, ilionekana kuwa huyu bibi hakuwa na muda kabisa wa kufatilia mtoto sijui kafanya nini au atafanya nini, zaidi zaidi alimpatia simu ili aweze kuwasiliana na marafiki zake na kutokujisikia mpweke.
Angel kule aliweza kupata marafiki mbalimbali kiasi kwamba aliona kuwa yale ndio maisha ambayo alikuwa ameyakosa kwa kipindi kirefu sana tangia anaishi kwa mama yake.
Siku hiyo akiwa ametulia nyumbani kwa bibi yake, alipigiwa simu na namba ngeni ila akagundua kuwa mpigaji amekosea namba nakumwambia,
“Utakuwa umekosea namba maana unayemuulizia sio mimi”
“Samahani,kwani wewe unaitwa nani?”
“Mimi naitwa Angel”
“Basi itakuwa ni jambo la busara kama tukifahamiana, mimi naitwa Mussa”
“Oooh sawa, kwaheri”
“Aaaah usikate simu Angel, nitafurahi sana kama nikikuona”
Angel alimkubalia huyo Mussa kuonana nae, na alichokifanya ni kumuelekeza nyumbani kwa bibi yake ili huyo Mussa afike hapo kwa bibi yake waonane.
“Basi nitakuja kesho”
“Sawa, karibu”
Angel hakuwa na tatizo lolote kwani bibi yake huyo alikuwa akiishi nae kama marafiki na walijikuta wakiongea vitu vingi sana.

Siku hiyo ndio ambayo Angel alipanga kukutana na Mussa, na huyo Mussa alipanga kufika hapo nyumbani kwakina Angel yani kwa bibi yake Angel, basi muda ulifika na Mussa alifika na moja kwa moja alimpigia Angel simu kuwa yupo nje ya pale kwao, basi Angel aliinuka na kumwambia bibi yake kuwa kuna mgeni wake,
“Mwambie akaribie tu ndani”
Basi Angel akatoka nje ili kumkaribisha Mussa, ila alipoonana na Mussa alishangaa sana yani yeye alikuwa akimshangaa Mussa na Mussa nae alikuwa akimshangaa Angel.



Basi Angel akatoka nje ili kumkaribisha Mussa, ila alipoonana na Mussa alishangaa sana yani yeye alikuwa akimshangaa Mussa na Mussa nae alikuwa akimshangaa Angel.
Baada ya muda kupita wakishangaana, yule Mussa alimuuliza Angel,
“Kwani wewe unaitwa Angel nani?”
“Mimi naitwa Angel Erick, na hapa nilipo ni nyumbani kwa bibi yangu mzaa baba”
“Aaaah sawa, basi duniani wawili wawili, ila dah tunafanana sana kama ndugu vile”
“Hata mimi ndio nakushangaa, mbona tumefanana hivi jamani!! Tena sio ndugu tu ila ni kama mapacha vile”
“Ila cha muhimu, mimi na wewe sio ndugu hilo ndio la msingi. Duniani wawili wawili, kwanza nisingefurahi tuwe ndugu, dah wewe ni mrembo sana Angel”
Angel alimuangalia tu huku akitabasamu na kumkaribisha ndani ila muda huo huo simu ya Mussa iliita na kufanya amuage Angel huku akimwambia kuwa,
Ilimradi nimepafahamu hakuna tatizo, nitakuja tena kukuona”
Basi Mussa aliondoka, halafu Angel alirudi ndani alipo bibi yake ambaye alimuuliza,
“Huyo mgeni yuko wapi?”
“Aaaah kapata dharula bibi, kwahiyo kaondoka ila imechukua kama dakika tano mimi na huyo mgeni tukiangaliana”
“Kwanini?”
“Jamani bibi, ninafanana nae balaa. Yani kama ndugu yangu vile ila ukoo wetu ni tofauti”
Bibi alimuangalia Angel kwa muda kidogo, kwani alipatwa na hisia moja kwa moja kuwa huyo mtu ni ndugu wa Angel ila Angel anaona ukoo tofauti sababu hafahamu ukweli wa ukoo wake, sema bibi yake hakuongeza neno lolote lile kuhusu ukoo wa Angel.
 
Back
Top Bottom