Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 168


Leo Junior aliondoka na Vaileth kuelekea kwa mama yake, na walifika na kumkuta mama yao akiendelea na mambo yake ya siku hiyo, mama Junior aliwakaribisha na kusema,
“Eeeeh leo na wewe Vaileth umetaka kupafahamu kwangu!”
Vaileth akatabasamu tu kisha mama Junior alimwambia mwanae,
“Kwanza hongera sana kwa kumaliza kidato cha nne mwanangu, halafu pili bora umekuja kwani nataka wiki ijayo twende pamoja kwa bibi yako”
“Aaaah mama, nitaenda mwenyewe tu”
“Kheee kwanini wakati mimi nipo?”
“Usijali mama, nitaenda mwenyewe kwa bibi”
Mama Junior hakutaka kuongea zaidi ila pia hakujua ni kwanini mtoto wake ameenda na Vaileth kwa siku hiyo kwani hakujua kazi ya Vaileth ni kitu gani.
Jioni ilipofika, Junior aliaga kuwa anaondoka na Vaileth kuelekea kwa mamake mdogo, mama yake alimsihi sana alale ila Junior alikataa kabisa na hivyobasi akaondoka akiwa ameongozana na Vaileth.
Wakiwa njiani, Junior alimwambia Vaileth,
“Nitakutambulisha kwa ndugu zangu wote, nataka wote wajue ni jinsi gani nakupenda”
“Mmmh Junior, unajua ni tatizo kubwa hilo?”
“Tatizo lipi sasa? Kwani kupenda ni dhambi? Kupenda sio dhambi wala nini, ni kweli nakupenda kweli kwahiyo sioni kama kuna sababu ya kunizuia mimi kufanya kile nitakacho, siwezi kwenda kuishi tena nyumbani kwani nahitaji muda mwingi niwe nakuona wewe”
Vaileth hakuongeza neno lolote zaidi ya kutabasamu tu, kwa upande mwingine alijiona kuwa yupo sawa ila kwa upande mwingine aliona kuwa anafanya makosa makubwa sana.

Mama Angel, leo alirudi mapema tu nyumbani kwake, ila baada ya muda mfupi tu Junior na Vaileth nao walirudi na kumpa salamu za kule walipotoka, basi aliongea nao kidogo na moja kwa moja akainuka na kuelekea chumbani kwake.
Ila alipofika tu chumbani kwake, alipigiwa simu na mama Junior na kuanza kuongea nae,
“Weee mama Angel, hivi huyo Junior na Vaileth nini kinaendelea kati yao?”
“Kwanini dada?”
“Mmmh nahisi kama kuna mahusiano ya kimapenzi kati yao!”
“Mmmh sidhani dada, Vaileth anatambua wazi tabia za Junior, kweli kabisa aanze tu kuwa na mahusiano na Junior jamani! Basi atakuwa hana akili kabisa, ila naona wakiishi tu kama kaka na dada”
“Hebu kuwa makini mdogo wangu, kwa siku hii moja tu nimeweza kuelewa kuwa kuna kitu hakipo sawa kati yao, unajua kama mzazi basi jambo kama hilo lazima liniumize, halafu huyu Vaileth ni mkubwa, halafu si ana mtoto huyu!”
“Ndio ana mtoto, tena mkubwa tu, nadhani kwasasa mwanae ana miaka mitano”
“Haya sasa, mwanamke mwenye mtoto mkubwa wa miaka mitano ndio akawe na mahusiano na mwanangu kweli!! Hapana jamani, sijapenda, hebu fatilia hilo swala kwakweli, unajua sio kawaida eeeh! Ni kweli Junior ana mapungufu yake, ila haijawahi kutokea kwa Junior kugoma kulala hapa nyumbani kwangu na vile vile kugoma kuongozana na mimi kwenda kwa bibi yake na badala yake anadai kuwa ataenda mwenyewe, nahisi kuna kitu kipo juu ya huyu msichana”
“Sawa nimekusikia dada, nakuahidi kuwa nitafanyia kazi hilo swala na nitajua imekuwaje, yani nitaelewa tu mbivu na mbichi”
Mama Angel aliongea na dada yake na kumpa moyo pale, ila baada ya kukata ile simu alijiona wazi kuanza kuhangaika na kazi mpya sasa ya kumfatilia Junior na Vaileth wakati amepumzika kumfatilia Angel.
Ila wakati akiongea na simu ile kumbe mwanae Erica alikuwepo mlangoni, na kwavile alikuwa akiongea kwa nguvu basi mwanae Erica alisikia kila kitu ambacho mama yake alizungumzia kwenye ile simu.
 
SEHEMU YA 169

Usiku wakati wa kulala, Erica alimfata Vaileth chumbani na kuanza kuongea nae,
“Basi leo nimemsikia mama akiongea na simu na mama mkubwa, na walikuwa wakiongelea kuhusu wewe na Junior”
Vaileth akashtuka kidogo na kuuliza kuwa alikuwa akiwaongelea kitu gani,
“Inasemekana wewe na Junior mna mahusiano ya kimapenzi, sasa mama kasema kuwa atawachunguza”
“Mmmmh ila Erica, kuna muda huwa unakera ila kuna muda huwa unafaaa sana kwa matumizi mbalimbali. Asante sana kwa ujumbe wako”
“Ila je ni kweli kuna mahusiano yanaendelea kati yako na Junior?”
“Mmmh jamani Erica, kama ni kweli kuna siku nitakwambia mwenyewe”
“Kwahiyo sio kweli?”
“Naomba tuachane na habari hizo, kwani nahitaji kupata muda wa kupumzika kwasasa”
Erica aliagana nae na moja kwa moja alienda chumbani kwa kaka yake ili kumpa huo ujumbe, ila muda ameingia chumbani kwa kaka yake basi kaka yake nae alikuwa ametoka bafuni kuoga, kwahiyo Erick alimkuta moja kwa moja Erica yupo chumbani kwake na kumuuliza,
“Vipi una mpya gani?”
“Ni hivi, nimemkuta mama akiongea na mamkubwa na walikuwa wakiongelea swala la Vaileth na Junior. Je wewe unahisi kuwa Vaileth na Junior wana mahusiano?”
“Kwani wakiwa na mahusiano tatizo ni nini? Vaileth na mwanamke na Junior ni mwanaume”
“Mmmh jamani, ila kumbuka Vaileth ni dada yetu. Kwahiyo Junior ana mahusiano na dada!”
“Kwani wewe unatakaje? Unataka Abdi aletwe hapa ili nae uishi nae nyumba moja”
Erica aliinuka huku akicheka kicheko cha kimbea na kusema,
“Sio Abdi bhana, saivi ni mambo ya Bahati”
Halafu Erica akaondoka zake, ile kitu ilimfanya Erick ajiulize maswali mengi sana, kuwa huyo Bahati ni nani? Anajua tu kuwa Erica alipewa viatu na mwanaume ila hakumjua huyo Bahati, kwahiyo alijikuta akitamani sana kumfahamu huyo Bahati ambaye kwa muda huo ametajwa na Erica, basi alitafakari kwa muda kidogo ila hakupata jibu wala nini.
Moja kwa moja aliamua zake kulala tu.
Kulipokucha, walijiandaa kwaajili ya kwenda shuleni kama kawaida, basi Erick alienda shuleni ila siku hiyo gari lao la shule lilipata hitilafu kidogo kwahiyo dereva alisimamisha na kuanza kutengeneza gari lile, wakati dereva akitengeneza gari lile, baadhi ya wanafunzi walikuwa wameshuka na wapo pembeni ya gari wakiangalia kinachoendelea ndipo alifika binti mmoja ambaye walikuwa wakisoma nae ila Erick hakuwa na mazoea na binti huyo kwani yeye hakuwa na ukaribu kabisa na watoto wa kike, basi yule binti alimfata Erick karibu na kuanza kuongea nae,
“Naitwa sarah! Nipo kidato cha pili”
“Oooh, mimi nipo kidato cha kwanza”
“Unajua nimekuangalia sana, mbona unaonekana umekaa peke yako peke yako kwani una tatizo gani?”
“Hapana, sina tatizo lolote”
“Hupendi kuongea na watu? Ila unaonekana unatokea kwenye familia nzuri sana, unajua katika maisha niliwahi kusikia stori moja hivi kuwa mahusiano mazuri ya kimapenzi huanzia shuleni”
“Unazungumzia nini kwani?”
Lile gari lilitengemaa na wanafunzi wote walirudi kwenye gari halafu safari ya kwenda shuleni ikaendelea.
Ila walipofika shuleni, yule binti alimpa Erick ujumbe halafu yeye aliondoka zake na kuelekea darasani kwao, kwakweli Erick alimshangaa sana na hakuelewa kuwa yule binti alikuwa na maana gani.

Nyumbani siku hii walibaki Junior na Vaileth tu, ambapo Vaileth alimueleza Junior kile ambacho aliambiwa na Erica,
“Nilijua tu, yani mama yangu huwa anaacha kufatilia mambo ya maana ila yeye huwa anakazana na kufatilia ujinga tu ambao huwa haumsaidii chochote kile.”
“Ujinga upi?”
“Sasa aanze kunifatilia mimi kweli ataweza? Mbona kipindi kile hakuweza, kiukweli Vaileth umebadilisha sana maisha yangu, tena umeyabadilisha kwa kiasi kikubwa sana kwahiyo hata waseme kitu gani kwangu ni sawa ma bure tu”
“Ila tunatakiwa kuwa makini sana, kwani tukigundulika kuwa tupo pamoja ni hatari kubwa sana. Ni hatari kwangu na ni hatari kwako pia”
Muda kidogo alifika mgeni, na mgeni huyo alikuwa ni mama Junior, hakwenda kwa taarifa kwavile alitaka ajaribu kuona kuwa ni kitu gani kinaendelea.
Basi Junior alikaa na mama yake na kuanza kuzungumza nae,
“Mama, hivi bamdogo alikueleza kuwa ni mazingira gani ambayo alinikuta nayo mimi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuja kuishi nae hapa kwake?”
“Kivipi?”
“Bamdogo alinikuta mimi nikiwa guest, na nilikuwa na mwanamke mkubwa sana. Kiukweli maisha yangu yaliharibika sana na kila kitu mlichokuwa mnanisema niliona kama ni kumpigia mbuzi gitaaa. Ila nakuuliza sasa, je maisha yale na haya ninayoishi sasa yapi ni bora?”
“Sikuelewi Junior, kwani unazungumza kuhusu nini?”
“Mama, jana nimekuja kwako kukuona nikiwa nimeongozana na Vaileth ila umeanza kunihisi vibaya, hata kitendo chako cha kufika leo hapa ni kwamba unataka kunichunguza. Hivi mama umeshindwa kunichunguza siku zote hizo ndio unichunguze leo kweli? Unajua wazi kuwa sipendagi unafki, niambie mimi wazi ni kitu gani unanihisi sio kuanza kunichunguza chunguza. Haya nikiwa na mahusiano na Vaileth, je wewe nakupunguzia kitu gani mama yangu? Kwani Vaileth sio mwanamke wa kufaaa kuwa na mimi? Watoto wa kike ndio huwa wanachungwa kwani wanaweza leta mimba nyumbani, ila mtoto wa kiume sio wa kuchungwa, nikileta watoto kwako ni baraka kuwa mtoto wako ni rijali”
Mama Junior alimuangalia mwanae na kutikisa kichwa, kwakweli hakuona kabisa umuhimu wa yeye kuendelea kuwepo kwenye eneo lile, kwani muda huo huo aliamua kuondoka tu.
Kwakweli mama Junior alitembea njiani huku akitafakari mambo mengi sana na kusema,
“Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka, yani huyu Junior ni tabia za baba yake mtupu, kupenda wanawake, na muda wote kuona kuwa anachofanya yeye sio kosa yani anaona kuwa anachofanya yeye kipo sahihi. Yani hapa kwakweli sijazaa kabisa bali nimeingia kwenye matatizo”
Wakati akitembea mara akashikwa bega, kugeuka alimuona mtu ambaye alimfahamu vizuri sana, na kumshangaa,
“Kheee wewe kumbe upo?”
“Nipo dada, kwanza kabisa naomba unisamehe kabisa kwa yote ambayo nilikukosea”
“Kumbe bado unayo hayo?”
“Unajua, kuna muda huwa nafikiria sana kuhusu wewe na kuona kuwa kiburi nilichokufanyia basi leo kimekuja katika maisha yangu”
“Kivipi?”
“Mimi nilikuwa msichana wako wa kazi na ulinilea vizuri kabisa, ulinifanya kama mdogo wako ila sikuwa na huruma kwani niliamua kutembea na mume wako hadi kupata ujauzito, mumeo alinipangishia nyumba na kuanza kuishi na mimi kwa siri siri hadi siku ambayo wewe na mdogo wako mlikuja na kufanya fujo katika nyumba ile. Dada nikianza kukuelezea niliyopitia kwa hakika utanihurumia sana, ila kwa kifupi na mimi nilipata bahati ya kuolewa, ila unajua kilichotokea kwangu? Mume wangu pia alienda kuzaa na msichana wa kazi, yani dada huwa nalia mno kwani maisha kumbe ni duara, yanazunguka pale pale”
“Usijali, kwangu yalishaisha kitambo sana. Hajambo mwanao?”
“Hajambo, ila ninao na wengine. Mwanangu yule nilimuita James, jina moja na baba yake, yule mtoto alikataa shule, yani kanisumbua sana, kwasasa anaishi na mjomba wake, ila ana matukio mengi ambayo hayafurahishi hata kidogo. Kuna muda huwa najutia sana, na kujilaumu sana, ila ndio hivyo maji yakimwagika hayazoleki wala nini. Nimefurahi kukuona tena, kama hutojali basi naomba mawasiliano yako”
Mama Junior hakuwa na pingamizi la aina yoyote ile zaidi zaidi ya kubadilishana namba na yule mwanamke, wala hakutaka kumfikiria sana kwani kwa muda huo hata yeye alikuwa na mawazo yake ya kutosha tu.
 
SEHEMU YA 170

Muda wa kutoka shule ulipofika, Erick alitoka na kwenda kupanda kwenye gari ili kurudi nyumbani kwao, ila siti aliyokaa basi pembeni yake alienda kukaa binti ambaye walionana asubuhi ya siku hiyo, binti aliyeitwa Sarah.
Basi yule binti alianza kumuongelesha,
“Unajua muda huu wa kutoka nimefurahi sana kukaa na wewe. Sikia usinifikirie vibaya wala nini, wakaka wengi huwa wanafikiria kuwa mwanaume ndio anayetakiwa kumtongoza mwanamke, ila kuna muda mwingine inatokea tu kwa mwanamke kumtongoza mwanaume”
“Kwahiyo wewe unanitongoza?”
“Na unajua kuwa haipendezi kwa mwanaume kumkatalia mwanamke, yani siku zote hizi huwezi amini huwa nakuangalia sana na leo nimeamua kujitoa muhanga tu na kukwambia ukweli, nadhani ni kusudi la Mungu kwa gari letu la shule kuharibika siku ya leo. Kwa kifupi, Erick nakupenda sana, katika maisha yangu nimetamani sana nianze mahusiano nikiwa shuleni, na nilipokuona wewe niliona kuwa hii ndio nafasi yangu ya pekee kabisa. Nakupenda sana, nahitaji uwe wangu”
Yani Erick alimuangalia sana huyu Sarah kwani hakuwahi kufikiria kama kuna binti mdogo kamaSarah mwenye ujasiri wa kusema yale aliyoyasema, kwahiyo alibaki akimuangalia tu huku akimshangaa, kisha Sarah akamwambia tena,
“Sio lazima uniambie kwa muda huu, hata Jumatatu hakuna tatizo, nitasubiri jibu langu”
Erick alifika nyumbani kwao na kushuka, moja kwa moja aliingia ndani ila leo alimkuta Junior akiangalia video ya ngumi, basi alipobadilisha nguo nae alirudi pale sebleni na kuungana na Junior kuangalia ile video, kisha Junior alimuuliza,
“Hivi mikanda mizuri hii ya ngumi kaileta nani? Najua mamdogo hawezi kufanya kitu cha namna hii”
“Kuna yule rafiki yake na Erick, wa kuitwa Samia, basi ndio mletaji wa mikanda hii”
“Oooh halafu yule Samia anaonekana anakupenda”
Erick alicheka tu halafu Junior alimuuliza tena,
“Hivi Erick, huwa huna mwanamke eeeh! Hata siku moja hujawahi kuja kuniuliza chochote kile”
Mara mlango ulifunguliwa na Erica aliingia ndani na kujibu lile swali,
“Yani wewe Junior, tabia zako basi unataka kila mtu awe nazo, hivi huoni kama Erick ni kijana mdogo! Sasa awe na wanawake wa kazi gani?”
“Ila wewe nawe, wanaume ndio tunaongea hapa. Sijakuuliza wewe, yani wewe tukisikia hata kuna mwanaume anakunyemelea basi huyo mwanaume ataipata, maana nyie watoto wakike mnatakiwa kulindwa, ila Erick ni mtoto wa kiume kwahiyo ni haki yake kuwa na wanawake”
Erica alichukia na moja kwa moja kuelekea chumbani kwake.

Mama yao aliporudi siku hiyo, moja kwa moja Erica alienda kumueleza mama yao kile ambacho Junior alikuwa akiongea na Erick, kwakweli mama Angel alichukia sana na kumfanya ahisi kuwa Junior anataka kuanza kumfundisha mtoto wake tabia mbaya.
“Haya mwanangu, asante kwa taarifa”
Basi Erica aliondoka zake, na baba Angel aliporudi mama Angel alimueleza lile jambo zima kwa vile alivyoelezewa na Erica,
“Aaaah mke wangu jamani, hebu wasikuchanganye kitu hao watoto jamani, yani wasikuchanganye mke wangu. Saivi tulee mtoto wetu huyo, tukianza kufikiria mara Junior hivi, mara Erick vile kwakweli tutashindwa kufanya mambo ya maana”
“Kwahiyo umeanza kutetea ujinga eeeh!”
“Mimi sitetei chochote kile ila naongea ukweli mke wangu, hebu tufikirie mambo ya maana basi. Mwanetu huyo tutamuita nani? Na vitu kama hivyo”
“Kheeee yani wewe, haya umewasiliana na Angel?”
“Oooh sijawasiliana nae, ngoja nimpigie simu mama”
Basi baba Angel alimpigia simu mama yake na kuomba kuongea na Angel ambapo waliongea nae Angel huku wakimuulizia kuwa maisha ya kule anayaonaje,
“Ni kuzuri baba, nishazoea tayari”
“Ni vizuri kusikia hivyo, ongea na mama yako”
Basi alimpa simu mama Angel ambaye aliongea na mwanae na kisha kuagana nae, kikweli mama Angel alikuwa ameridhika sana kuongea na mtoto wake kwahiyo kwa muda huo aliweza kulala tu kwa amani na kusahau yote aliyokuwa akiyasema.
 
SEHEMU YA 171

Angel na bibi yake walianza kuongea, ambapo bibi yake alimuuliza,
“Mbona hujawaambia wazazi wako kuwa na wewe una simu yako ili wawe wanakupigia humo?”
“Mmmmh bibi, usiwaambie, yani mama hataki kabisa nimiliki simu ujue”
“Kwanini sasa jamani?”
“Hata sijui, ila mama hapendi niwe na simu”
“Aaaah na mama yako nae ana mambo ya kizamani utafikiri ni mmama wa enzi zetu jamani, wakati ni mmama wa kipindi hiki, anatakiwa kulea watoto wake kisasa, kwani mkimiliki simu ndio nini sasa? Hebu anitolee ushamba mie. Mjukuu wangu, kesho tutaenda mahali, ni pa muhimu sana maana kuna wafanyabiashara wa maana naenda kuonana nao”
“Sawa bibi”
“Basi mapema kabisa ujiandae, sawa”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi Angel alienda zake kulala, kwakweli Angel alipenda sana maisha ya kuishi na bibi yake huyo kwani alikuwa akimfanya ajiachie sana na kumfanya ajihisi vizuri sana kuishi na bibi yake.
Wakati analala alipigiwa simu na Mussa na kuanza kuongea nae,
“Kesho nitakuja tena kwenu Angel, nina shida sana ya kuonana na wewe”
“Aaaah ni ngumi maana kesho kuna mahali naenda na bibi yangu, kwahiyo sitaweza kuonana na wewe”
“Sawa, hakuna tatizo lolote. Itabidi tuonane kw awakati mwingine”
Basi Angel alikubaliana na Mussa kuonana na wakati mwingine na moja kwa moja kwa muda huo aliamua kulala tu.
Kulipokucha, ni kama ambavyo alipanga na wifi yake, kwani alijiandaa halafu bibi yake alimuita na kuondoka nae pamoja mpaka kwenye kikao cha wafanyabiashara ambapo bibi yake alikuwa ameenda kuonana nao.
Basi bibi yake alikuwa akimtambulisha Angel karibu kwa kila mtu aliyekuwepo eneo hilo, kuna rafiki yake mmoja alimuita pembeni na kuongea nae,
“Huyu mtoto unayemtambulisha hivi ni nani yako?”
“Mjukuu wangu huyu, mtoto wa Erick”
“Oooh, ndio wamekupa wewe umlee?”
“Ndio, mimi si bibi yake”
“Mmmh! Hao wazazi nao wamechoka kulea mtoto au? Yani wamekuletea wewe, hivi unakuwaga na muda kweli wa kuangalia watoto wewe! Yule wako mwenyewe umshukuru mdogo wako, hivi wewe ni wa kulea mtoto kweli!”
“Wewe nawe umetumwa au kitu gani? Hebu achana na mimi na mjukuu wangu”
Kisha bibi Angel akaenda kumfata mjukuu wake na moja kwa moja alienda kukaa nae kwenye meza ambapo wageni mbalimbali walikuwa wakifika kwenye kikao kile.
 
SEHEMU YA 172


Siku ya leo Samia alipeleka tena mikanda mingine nyumbani kwakina Erica, na alivyofika baada ya kuwakabidhi ile mikanda aliwaambia jambo ambalo Erick lilimchanganya kidogo,
“Basi leo kabla sijaja huku, nilipitia pale kwenye duka lenu, nikakutana na yule mama ambaye alisema kuwa niende pale nikachukue ninachokitaka, ila nimemkuta yule mama akigombana na yule mkaka wa kwenye lile duka”
“Mmmmh! Akigombana nae kivipi?”
“Yule mama alikuwa akimwambia yule kaka kuwa lile duka ni la mtoto wake”
Erick alishangaa sana kwani ugomvi wa duka lile hakuwahi kuushuhudia wala hakujua kama kuna kitu cha namna hiyo, basi hakutaka hata kupoteza muda kwani muda huo akatoka zake nje na kupanda kwenye gari lao kwahiyo hakuondoka na Samia wala na mtu mwingine yoyote yule.
Erick alifika dukani, na kweli alimkuta Steve akibishana na mwanamke mmoja ambaye yeye hakumfahamu, basi alisogea karibu na kuuliza,
“Kwani tatizo ni nini hapa?”
“Tatizo la hapa ni huyu mama, yani huyu mama binafsi huwa simuelewi kabisa”
Basi Erick alimuangalia yule mama na kumuuliza,
“Kwani tatizo ni nini dada?”
“Usiniite dada mie, niite mama, hebu kuwa na heshima kwa wakubwa wako”
“Haya mama, unalalamika kitu gani hapa dukani?”
“Nenda kamuulize baba yako vizuri, kuwa lile duka ni la nani na yeye atakueleza vizuri”
“Una kichaa wewe mama au? Nimuulize vizuri wakati duka ni la kwangu”
“Kwani wewe ni nani?”
“Kumbe hata unayeongea nae humjui! Mimi ndio mmiliki halali wa hili duka”
“Hili duka ni la mtoto wangu”
Erick alimuangalia huyu mama na kumwambia,
“Huwa sipendi kubishana katika maisha yangu, naomba uondoke sasa hivi”
“Kheee inawezekanaje mtoto kama wewe kunitishia maisha mimi? Hivi unanijua vizuri mimi? Yani laiti ungejua mimi ni nani basi usingethubutu kufungua mdomo wako na kusema chochote kile”
Erick hakuwa muongeaji sana, hivyobasi hakutaka kubishana zaidi na huyu mama zaidi zaidi aliamua kumsukuma ila kitendo kile kilimfanya yule mama atoe kilio cha ajabu utafikiri kafanywa kitu gani,.
Kilio kile kilifanya watu wengi sana wajae katika duka lile, halafu yule mama alianza kusema,
“Yani mtoto niliyemzaa mwenyewe, leo hii ananisukuma kama mwizi”
Steve na Erick walibaki wakishangaa tu.

Erick hakuwa muongeaji sana, hivyobasi hakutaka kubishana zaidi na huyu mama zaidi zaidi aliamua kumsukuma ila kitendo kile kilimfanya yule mama atoe kilio cha ajabu utafikiri kafanywa kitu gani,.
Kilio kile kilifanya watu wengi sana wajae katika duka lile, halafu yule mama alianza kusema,
“Yani mtoto niliyemzaa mwenyewe, leo hii ananisukuma kama mwizi”
Steve na Erick walibaki wakishangaa tu.
Erick alimuuliza Steve,
“Kwani huyu mwanamke anazungumzia kitu gani?”
kwakweli hata Steve hakumuelewa yule mwanamke, na sababu alizidi kufanya watu wajae pale dukani ikabidi Steve apige simu moja kwa moja kwa baba Angel ili afike mahali pale kwani alihisi labda baba Angel ndio anaweza kuelewana na yule mwanamke.
Watu walijaa pale huku wakimsikiliza ambapo alikuwa akiwaambiwa stori ambayo walikuwa wakishangaa tu,
“Kwahiyo mtoto wako mwenyewe aliyekusukuma ni yupi?”
Alikuwa akimnyooshea Erick ila Erick alisema,
“Sio mama yangu huyo jamani!”
Steve nae alikuwa akisema pale,
“Jamani jamani, msimsikilize huyu mwanamke ana wazimu tena wazimu uliopitiliza, huyu sio mwanae”
Kisha Steve alimfata karibu yule mwanamke na kumwambia,
“Nimemuita baba mwenyewe mwenye hili duka, endeleza uchizi wako nadhani utajuana nae vizuri tu”
Wakati akiongea nae hayo, mara gari la baba Angel nao liliwasili eneo lile, ila baada ya yule mwanamke kuona lile gari tu aliinuka haraka na kukimbia toka eneo lile.
Kwakweli baba Angel hakupenda kabisa jinsi watu walivyojaa nje ya duka lake na kuanza kuwatimua ambapo wengi walisambaratika, halafu aliingia dukani na kumuuliza Steve kuwa kuna nini huku akimuangalia Erick aliyekuwa kainama chini tu,
“Kwakweli sijui nikwambiaje bosi, ila nisamehe kwakweli. Toka nianze kazi hapa amekuwa akifika Sia, nadhani unamfahamu vizuri sana hata mama alishawahi kumkuta”
Basi baba Angel alimchukua Steve pembeni na kuanza kuongea nae kwa undani zaidi,
“Huyo Sia huwa anakuja kufanya nini na huwa anafanya kitu gani na leo kafanya nini hadi kujaza watu namna ambayo nimekuta? Yani haya ndio matatizo ya kuweka duka uswahilini jamani, hadi najuta hapa. Niambie kwanza imekuwaje?”
Steve alianza kumueleza kuanzia mara ya kwanza ambapo Sia aliasema kuwa duka lile ni mali ya mtoto wake na jinsi alivyosema wazo la kujenga duka hapo amelitoa wapi, na jinsi leo alichokifanya hadi kujaza watu kiasi kile, baba Angel aliweza kuelewa ni kwanini hata Erick amepooza basi alimfata na kuanza kuongea nae,
“Mwanangu, kwanza kabisa na wewe niambie leo kitu gani kimekuleta huku?”
“Baba, ulisema kuwa niwe nakuja kuangalia hili duka mara kwa mara, sasa leo alikuja rafiki yake na Erica na amesema kuwa kuna mwanamke yupo dukani akigombana na huyu anko basi ndio nikaamua kuja”
“Sawa, kwa kifupi nimeelewa mwanangu”
Kisha baba Angel alimuangalia Steve na kumwambia,
“Nahitaji kupata muda wa kutosha niweze kuongea na huyo Sia, najua kuwa ipo siku au kuna muda atarudi tu. Na usimwambie chochote kile ila kuna askari watakuwepo na akija tu basi watamkamata na kunipigia simu”
Kisha baba Angel alimtaka Erick waweze kuondoka, na moja kwa moja alienda nae hotelini kwani mwanae huyu alimuona kuwa ni mkubwa na anapaswa kufahamu vitu vingi sana.
 
SEHEMU YA 173

Basi baba Angel alifika na Erick hotelini na kuanza kuongea nae,
“Kwanza kabisa Erick nakupongeza sana kwa kuwa kijana mzuri kwa kipindi chote hiki, inaonyesha mtoto wangu wewe hupendi makuu. Mimi baba yako nilianza mahusiano ya kimapenzi nikiwa mdogo sana, yani wakati nipo darasa la nne tayari kuna wanawake nilianza kuwatamani na kuna wengine waliokuwa wakinitaka kimapenzi, ila nilipofika kidato cha pili ndio nilimuona yule mama yenu kwa hakika nilijikuta nikimpenda sana ila sikuweza kumpata sababu tulikuwa tunasoma. Kwanini nimekwambia yote haya? Sababu nahitaji mwanangu uwe makini sana, haya maisha bila umakini hakuna utakachoweza kufanya, kama ukipenda kitu basi kishikilie hiko hiko, mimi nilipomkosa mama yenu ndio nikazidi kuwa muhuni kiasi kwamba nilikuwa na kila aina ya mwanamke na mwishowe nikaangukia kwa yule chizi ambaye umemuona amefanya vurugu dukani, unajua kuna watu mbalimbali unaweza kukutana nao katika maisha na wengine wakapita tu bila ya tatizo lolote katika maisha yako ila kuna watu ni ruba yani wenyewe huwa hawapiti bila kukusababishia matatizo katika maisha yako. Yule mwanamke hana lengo jema katika maisha yangu, naona bado ana kinyongo kikubwa sana na mimi sababu tu sikumuoa yeye ila nikamuoa mama yenu, mengine nitakusimulia zaidi mwanangu. Ila kwasasa, nakuomba kitu kimoja, usimsimulie mama yako chochote kile kilichotokea pale dukani halafu yale yote ambayo yule mwanamke kaongea kwako ona kama hakuna cha maana alichozungumza yani wewe achana nayo tu hata usiyajali wala nini. Mimi naelewa ni kwanini kasema vile, kwahiyo mwanangu hata usichukulie maneno ya yule mwanamke kuwa na maana, mimi ni baba yako na mama yako ndiye mama yako yani sisi ni wazazi pekee ambao tupo katika maisha yako. Achana na maneno ya yule mwanamke mwanangu. Natumaini umenielewa, mimi najua ni kwanini yule mwanamke kakwambia vile ila wewe achana na maneno yake”
“Nimekuelewa baba, hakuna tatizo”
Halafu mwanangu, nitaenda kukuonyesha duka lingine. Sipendi ukae kwenye duka ambalo lina migogoro, kwanza lile duka nitalifunga tu, dah yule mwanamke kanikera sana”
Erick alimuitikia baba yake ila maswali aliyokuwa akijiuliza kichwani ni mengi mno, kwanza kwanini asimueleze mama yao kuhusu lile swala, halafu kwanini baba yake anaonekana kuona lile jambo kuwa la kawaida kabisa, ila hakusema chochote kile zaidi zaidi walimaliza maongezi yao na kurudi tu nyumbani kwao.

Angel akiwa na bibi yake kwenye kile kikao, muda huu Angel aliomba ruhusa kwa bibi yake kuwa anaenda uwani mara moja, ila wakati ameondoka kuna mbaba mmoja ambaye alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana alimfata Angel kwa nyuma na kuwa kama akimvizia atoke chooni, na kweli Angel alipotoka alianza kuongea nae,
“Binti, sijafanya vibaya kuja kukusubiri huku ila ningefurahi zaidi kama ningepata mawasiliano yako”
Kwavile bibi yake alishamtambulisha kwa mfanyabiashara huyo basi yeye hakuona tatizo kabisa basi akatoa simu yake ili aangalie namba na amtajie ila simu ile alivyoishika tu ilizimika, ni simu ambayo alikuwa akiwasiliana nayo ila ilikuwa ikimsumbua sana katika swala la chaji, basi Angel alimuangalia yule mbabu na kumwambia kuwa simu imezimika, halafu akarudi nae kwenye kikao ambapo kikao kile walikuwa wakimaliza kwa muda ule, ila yule baba alimfata bibi yake Angel na kumwambia,
“Julieth, kweli simu gani hiyo ya kumpa mjukuu wako atumie jamani!”
“Aaaah unajua hiko kimeo kilikuwa ndani, sasa mjukuu wangu hakuwa na simu kwahiyo nikaona ni vyema atumie tumie tu”
“Aaaah sijapenda kabisa, yani mfanyabiashara mkubwa kama wewe mjukuu wako anaanza kutumia vimeo kweli jamani!”
“Oooh wewe nawe, ushaanza mambo yako, haya mnunulie mjukuu wangu simu”
Bibi yake Angel aliongea kwa lengo la kujifurahisha tu, ila yule babu aliahidi kuwa kesho yake angemletea simu Angel, basi wakaongea pale na kuagana na wale wafanya biashara wengine halafu kila mmoja kuondoka ambapo Angel aliondoka na yule bibi yake.
Njiani, Angel alimuuliza bibi yake,
“Sasa, bibi yule ataniletea simu gani?”
“Ngoja tu utaiona kesho, halafu yule hanaga masikhara jamani mimi nilikuwa namtania tu. Ila sio kosa langu kwa wewe kutumia kimeo, ni kosa la wazazi wako. Yani wanafanya mambo kama hawana hela vile, hivi kweli kabisa baba yako na mama yako wameshindwa kukununulia simu jamani! Ila sio mbaya, yule babu atakununulia”
“Kwani anafanya biashara gani yule?”
“Ilimradi nimeanza kuja nawe kwenye vikao vua biashara basin i wengi utawafahamu ila yule babu ni mfanyabiashara mkubwa sana, yani ana biashara nyingi nyingi halafu zote ni kubwa, anatambulika kwa jina moja kubwa la Mr.Peter”
“Oooh sawa bibi”
Basi walifika hadi nyumbani ambapo kwa siku hiyo Angel aliamua kulala tu kutokana na uchovu na mizunguko ya hapa na pale na bibi yake.
 
SEHEMU YA 174

Muda ambao Erick na baba yake walirudi nyumbani, walimkuta mama Angel alisharudi nyumbani muda mrefu tu, basi mama Angel aliwauliza,
“Kheee wenzetu mmetoka wapi muda huu?”
Baba Angel alicheka tu na moja kwa moja kutangulia chumbani ambapo mama Angel nae alimfata nyuma na kuanza kuongea nae,
“Leo hata kunifata umeona ni shida halafu saizi ndio mmeingia nyumbani, umetoka wapi na mwanao?”
“Ila na wewe mke wangu mara nyungine jamani, unajua kuna vitu vingine ni lazima kwa baba kuzungumza na mtoto wake wa kiume kama ilivyokuwa mama kuzungumza na mtoto wake wa kike”
“Sasa unadhani mimi nitazungumza nini na Erica jamani! Bora hata Angel, maana huyu Erica ni kitu gani mtu unaweza kuzungumza nae akakuelewa”
“Kwanini sasa?”
“Mtoto ni mbea na hakuna anachokuelewa hata umwambie nini!”
“Sasa unadhani Erica katoa wapi tabia ya umbea? Ukiona hivyo ujue wazi kuwa hata wewe ulikuwa mbea ndiomana Erica nae yupo hivyo”
“Hapana jamani, mimi sikuwa na tabia hiyo kabisa, yani siwezi kuongea chochote na Erica sababu ya tabia yake ya umbea”
“Subiri akikua ataacha”
“Ila katika yote, huyu Erick ndio huwa ananishangaza sana. Kwa jinsi tabia yako ilivyokuwa nilijua nitapata shida sana kwa Erick kama angefata tabia yako, yani hakuna pa kupona kwake, wewe tabia moto, baba yako alikuwa moto yani kwakweli nafurahi sana kuona Erick yupo na tabia tofauti kabisa. Na hivi tuna pesa si ndio ingekuwa balaa, maana mtoto wetu ni mzuri jamani, yani angekuwa muhuni basi kwa hakika ingekuwa balaa yani tabia yake ingekuwa ya Junior ikasome”
“Erick hawezi kufanya ujinga, halafu katika watu wenye tabia mbaya, naomba usiniweke mimi kabisa. Inamaana basi hata Angel unamuonea tu maana kachukua tabia yako”
Hilo lilimkera mama Angel kwani binafsi yake hakuipenda tabia ya Angel haswaa kuhusu Samir, ila alichukia kwa muda na kusema,
“Natumaini mwanangu alipo atarudi akiwa amenyooka vya kutosha”
“Ndio, atarudi kanyooka”
Baba Angel hakutaka kuongea mengi kwa muda huo kwani hakutaka hata kuelezea yale ambayo yalitokea kwa siku hiyo kuhusu Sia.
 
SEHEMU YA 175

Angel leo akiwa ametulia na bibi yake, walipata ugeni ambapo mgeni alikuwa ni yule baba Mr. Peter, basi walimkaribisha vizuri sana ambapo alikuwa katimiza ile ahadi yake ya kumletea Angel simu ambapo alimkabidhi pale, bibi yake alishangaa kidogo na kusema,
“Kheee mbona umemchukulia simu ya gharama sana jamani! Yani simu ambayo hata bibi yake tu situmii!”
“Na wewe Julieth hebu acha mambo yako, kwani hiyo simu ina ugharama gani jamani! Simu ya milioni mbili tu ndio inakutoa roho kiasi hiko jamani! Mwache mtoto atumie simu inayoendana na hadhi yake”
“Haya, Angel chukua hiyo simu babu yako kakuletea”
Angel aliichukua pale na kumshukuru yule mzee ambaye alimsaidia pale kuweka laini kwenye ile simu huku akimwambia,
“Mjukuu wangu, tena wewe sababu ni kijana basi utajua matumizi mengi sana kwenye hiyo simu yani sio kupiga na kutuma ujumbe tu ila hiyo simu ina mambo mbalimbali, kuna mitandao ya kijamii humo yani mambo mengi mengi, utajifunza na kujiunga”
“Sawa, nashukuru sana”
Angel alimuacha bibi yake pale na yule mzee kisha yeye alienda zake chumbani ambapo alianza kutumia ile simu.
Muda ule ule alipigiwa simu na Mussa, kwahiyo alipokea na kuanza kuongea nayo,
“Jana nilitaka kuja Angel, ila umenikatili ujue”
“Aaaah pole”
“Unatumia simu ya aina gani?”
“Ni mpya, kwani unatakaje?”
“Aaaah, nilikuwa nataka kukununulia simu nyingine, kesho nakuja Angel”
“Haya, karibu”
Angel alimaliza maongezi na Mussa na kukata ile simu, kisha aliamua kuanza kuibonyeza bonyeza ile simu na kuingia katika mtandao wa facebook ambao alijiunga kwa siku hiyo hiyo, ila alishangaa kwa muda ule ule kutumiwa ombi la urafiki na mtu ambaye alikuwa akimfahamu kwa jina ila mtu huyo hakuweka picha yoyote kwenye mtandao, aliona jina Samir, kwanza alipoona moyo wake ulishtuka halafu alijiuliza,
“Je huyu ni Samir yule niliyekuwa nasoma nae au ni kitu gani?”
Ila alikubali ombi la urafiki wa Samir ambapo muda huo huo Samir alianza kuwasiliana nae,
“Hivi ni wewe Angel tuliyosoma wote au?”
“Hata mimi najiuliza, hivi ni wewe Samir au?”
“Kama ndio hivyo basi tumekutana kweli, dah nimefurahi sana. Kuna mambo yanaweza kutokea katika maisha ila hujui maana yake wala nini?”
“Kwanini? Na umejuaje kuwa ni mimi? Maana ndio kwanza nimejiunga leo kwenye huu mtandao”
“Ni hivi Angel, mimi nipo na mama yangu kwaajili ya kazi Fulani huku. Sasa leo, aliniambia kuwa nijiunge na facebook kwani kuna kundi sijui anataka awe anaangalia picha za mishono ya nguo, kwahiyo nilijiunga kwasababu ya mama. Yani nikashangaa nimemaliza tu kujiunga, naona jina lako kuwa naweza tuma ombi la urafiki kwako basi ndio nikatuma”
“Mmmh Samir, kuna nini kati yetu?”
“Sidhani kama kuna kingine zaidi ya upendo, yani upendo baina yangu na yako ni mkubwa sana kiasi kwamba hauwezi kuzuiwa na chochote kile, ndiomana kila kinachofanyika baina yetu basi lazima tujikute tukiwa pamoja, halafu nitumie na namba yako ya simu”
Angel aliitwa na bibi yake, kwahiyo aliacha ile simu na moja kwa moja kwenda kuongea na bibi yake,
“Kheee Angel umejifungia chumbani, mgeni anataka kuondoka. Ndio nimekuita akuage”
“Oooh, karibu sana”
“Asante mjukuu wangu, nashukuru”
Kisha mr.Peter alimuangalia bibi yake Angel na kumwambia,
“Julieth, nadhani nitatafuta siku ili twende kufurahi na mjukuu wetu. Unajua nimempenda sana huyu mtoto, anaonekana yupo vizuri, kwanza hana kiburi na hana majivuno yani ni maringo tu kidogo”
“Aaaah mtoto wa kike huyu kwahiyo kuringa ni lazima, ila ukimzoea utamuona kawaida tu”
Basi Angel alimuaga yule babu na moja kwa moja kutaka kurudi chumbani kwake ila bibi yake alimwambia,
“Angel, nilipenda sana chakula ulichokipika juzi, pika tena kama kile mjukuu wangu ili tule”
Basi Angel alipitiliza jikoni na kuanza kupika chakula ambacho bibi yake naye alikihitaji.
 
SEHEMU YA 176

Usiku wa siku hiyo, Angel aliingia tena kwenye mtandao na kuanza kumtafuta Samir, yani kwenye ule mtandao alikuwa akiwasiliana na Samir tu na hata marafiki alikuwa na rafiki mmoja tu ambaye ni Samir halikadharika na kwa Samir pia, alikuwa na rafiki mmoja tu na muda ule Samir nae alikuwa hewani akisubiri ujumbe toka kwa Angel, basi Angel alimtumia Samir namba yake ya simu halafu akamuuliza,
“Halafu Samir, ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kati yako wewe na madam Hawa?”
“Hakuna chochote, yule madam alinichukulia kama mwanae, na aliataka nisome basi. Unajua yule madam nilimueleza ukweli kuhusu wewe”
“Mmmh kwahiyo ulimwambia nini?”
“Nilimwambia kuwa nakupenda sana, yani katika vitu vyote sikuweza kumficha kuhusu wewe, ni kweli nakupenda sana Angel. Mimi sina nia sijui ya kukuharibia masomo yako, sijui kukuharibia usichana wako hapana, ila mimi nakupenda, yani wazazi wako hawakuelewa tu kuhusu mimi, yani mimi ile ukaribu tu na wewe nasikia kuridhika katika moyo wangu yani hakuna kingine zaidi ya hiki”
“Mmmh! Kwahiyo mimi na wewe tuwe wapenzi?”
“Jamani Angel unauliza majibu kweli! Mimi na wewe tuwe wapenzi ndio, wala tusitumie papara wala nini kwani ni wazi kuwa mimi na wewe tunapendana sana, ila pia tusikubali kutenganishwa mapenzi yetu. Siku moja nitakuhadithia historia ya mama yangu katika mlolongo wa mapenzi maana mimi huwa naongea na mama kiurafiki kabisa. Kwahiyo Angel, mimi nina maana kubwa sana kukufata wewe sababu nakupenda kweli na sitaki kutengwa na wewe, siwachukii wazazi wako kwani najua walikuwa wakifanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa huwi na mimi ila tu hawakujua nguvu ya mapenzi ambayo ipo kwangu juu yako”
Yani Angel alikuwa akisoma huu ujumbe mara mbili mbhili huku akitabasamu, yani aliwaza vitu vingi sana vya tangia anafahamiana na Samir, na jinsi walivyokuwa wakitenganishwa basi alikuwa akitabasamu tu na kuaendelea kuwasiliana nae.
Mwisho wa siku walijikuta wakilala usiku sana, yani kwenye saa tisa usiku ndio walilala sababu ya kuwasiliana sana.

Leo mama Angel aliamua kwenda kumtembelea mama yake mzazi kwani na tumbo lake lilikuwa kubwa sana kwa kipindi hiko ila aliona ni vyema kama akienda kumsalimia mama yake,
“Oooh mama kijacho, karibu sana. Ila katika mimba zako zote basi hii mimba umeibeba kwa uhuru sana”
Mama Angel alicheka kidogo, kisha akamwambia mama yake,
“Ila hata mimba zingine nazo sikupata shida, kama mimba ya Angel ndio kabisa”
“Usitake kujisifia hapa. Mimba ya Angel si ndio ulikuwa ukijificha nayo mwanzo mwisho, hata mtoto ulikuwa ukimficha asionekane na watu. Halafu leo hii unasemaje? Eeeeh na Angel yuko wapi? Maana ajiandae kupokea mdogo wake huyo”
“Mmmh mama, mbona Angel yupo kwa bibi yake yani mama yake na Erick”
“Kheee kweli Erica umechoka mwanangu, kwa wingi gani wa watoto hadi umempeleka Angel huko?”
“Mama jamani, Angel alikuwa hajatulia kwahiyo niliona ni vyema kama nikimpeleka kwa bibi yake huko”
“Yani Erica, kila kitu unaelewa yani hakuna usichoelewa, yule mama toka lini akalea watoto? Huyo Angel unamtakia nini? Kwahiyo umemkimbiza Angel ili asikimbizane na wanaume, unafikiri huko ndio umemuokoa? Yani yule Julieth namfahamu vizuri sana, jamani hajui kulea watoto yule ni hajui kabisa, tabia atakazorudi nazo Angel huko kwa hakika utaimba haleluya na hutoweza kumrekebisha tena yani kila ukitaka kumrekebisha ndio utakuwa unamuharibu zaidi”
“Jamani mama unanitisha”
“Sikutishi ila nakwambia ukweli mtupu, yani huko mwanangu umemtumbukiza mwanao nakwambia. Yule mama hajui kulea watoto kabisa, na hivi huwa anajifanya anaishi kizungu sababu kaishi sana nchi za nje, subiri tu picha kamili ya ulichokipeleka huko”
“Jamani mama, unajua hadi umenikosesha raha”
“Na ukose vizuri tu hiyo raha, hivi raha iko wapi kwa kulelewa mtoto? Tumaini ndio alikuwa yupo vizuri kwani hata watoto wake unaona jinsi anavyowalea, ila yule mama uliyempelekea mtoto kuna mtoto gani hata wa ndugu yake aliyemlea vizuri? Unataka nikupe historia ya yule mwanamke katika kulea watoto? Huyo mumeo aliharibika wakati anaishi na mama yake, na ikawa kidogo afadhari alivyoishi na mamake mdogo yani hata ukikutana na Julieth mwenyewe anakuelezea. Yani yeye huwa naangalii kama hiki ni kizuri kwa mtoto na hiki ni kibaya, yule huwa anahisi watoto wote ni kama watoto wa kizungu, kuna tofauti kubwa sana ya kulea watoto wa Kiswahili na watoto wa kizungu, haijalishi una pesa kiasi gani ila mtoto wa Kiswahili ni wa Kiswahili tu. Akili kichwani mwako, sikujua huo ujinga ambao umeufanya jamani, bora hata mngeniletea mimi mjukuu wangu nikae nae mwenyewe”
“Basi mama, nitaenda kumchukua”
“Yani katika siku ambazo umeongea na mimi, leo umeongea na mimi kitu cha kunichefua Erica. Yule mtoto kweli!!! Jamani utaniambia mimi, yani wewe huwa unamsifia kila leo ooh mwanangu mzuri mzuri basi kwa yule bibi yake hizo sifa zako ni mara mia yani Angel atakuwa anajiona kama malaika katika ulimwengu huu. Fanya kitu mapema kabla mtoto hajaharibika zaidi”
“Sawa mama, nimekuelewa mama yangu”
Basi siku hiyo mama Angel hakuwa na amani tena kiasi kwamba hadi muda anaondoka kwa mama yake bado alikuwa na wazo moja tu juu ya Angel.
Usiku wa siku hiyo mama Angel aliamua kuongea na mume wake kuhusu kwenda kumchukua Angel,
“Naona umemkumbuka mtoto wako tayari!”
“Ndio nimemkumbuka, tena sana tu”
“Je huogopi kuwa wakina Samir watamfata tena?”
“Aaaah hata wakimfata, nitajua jinsi ya kuwathibiti ila kiukweli nimemkumbuka sana”
“Sawa basi tutaenda wote kumfata, siwezi kukuacha umfate peke yako katika hali hiyo uliyokuwa nayo mke wangu”
Mama Angel alikubaliana na mume wake kuwa kesho yake ataenda nae pamoja kwenda kumfata Angel.
 
SEHEMU YA 177


Leo usiku Angel nae alikuwa akiwasiliana vizuri sana na Samir, yani kwa siku hizi chache, mawasiliano yake na Samir yalikuwa ya hali ya juu.
Muda anawasiliana na Samir, basi Mussa alimpigia simu na kuanza kuongea nae,
“Mbona siku hizi Angel hupokei simu zangu?”
“Jamani, mbona nimepokea, unataka nipokeaje?”
“Unanipotezea siku hizi, sijui hata kwanini. Ila kesho nitakuja”
“Hakuna shida karibu”
Kwa upande wa Angel, hakumuona Mussa kama mtu baki bali alikuwa akimuona kama ndugu yake, tofauti na Mussa ambaye alikuwa akimuhitaji Angel kimapenzi. Yani Angel na hivi aliona kuwa kafanana na Mussa ndio kabisa yani, alimuona kama ndugu yake kwahiyo alikuwa akiongea nae kawaida tu.
Baada ya hapo aliendelea kuongea na Samir, na kama kawaida hadi alichelewa kulala kwa siku hiyo pia sababu ya kuongea na Samir.
Kilipokucha, Angel aliitwa na bibi yake ambapo siku hiyo mapema kabisa, yule bibi alimuaga Angel kuwa anatoka kidogo maana kuna biashara alikuwa akiishughulikia.
Jioni ya siku hiyo, Angel alipigiwa simu na Mr.Peter ambaye alimwambia Angel,
“Toka hapa nje ya geti nina shida na wewe”
Basi Angel moja kwa moja alitoka nje, ila alipofika tu yule Mr.Peter alimsogelea Angel na kumkumbatia, muda huu mama Angel na baba Angel nao walikuwa wamewasili pale kwa bibi yake Angel, ila mama Angel alishtuka sana kwa kumuona huyu mzee na kusema,
“Mr.Peter!!!”
Huyu mzee nae alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi kwani alikuwa akimshangaa pia mama Angel.


Jioni ya siku hiyo, Angel alipigiwa simu na Mr.Peter ambaye alimwambia Angel,
“Toka hapa nje ya geti nina shida na wewe”
Basi Angel moja kwa moja alitoka nje, ila alipofika tu yule Mr.Peter alimsogelea Angel na kumkumbatia, muda huu mama Angel na baba Angel nao walikuwa wamewasili pale kwa bibi yake Angel, ila mama Angel alishtuka sana kwa kumuona huyu mzee na kusema,
“Mr.Peter!!!”
Huyu mzee nae alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi kwani alikuwa akimshangaa pia mama Angel.
Baba Angel nae alikuwa akishangaa na kumuuliza mke wake,
“Mnafahamiana kumbe!”
Angel aliwakimbilia wazazi wake, kanakwamba hakuna kitu ambacho kimetokea pale, kwakweli mama Angel hakuongea jambo lolote zaidi ya kumtaka Angel aingie ndani tu halafu yeye alimfata kwa nyuma yani hakuna kingine cha zaidi alichozungumza kwa muda ule.
Alifatana na Angel hadi ndani na kumwambia,
“Haya fungasha kila kilicho chako tuondoke”
“Jamani mama, ujue bibi hayupo”
“Sitaki kusikia, awepo au asiwepo ila leo tunaenda nyumbani”
Kwakweli Angel hakumuelewa mama yake wala nini na muda huo mama yake alienda kukaa sebleni huku akiwa na mawazo sana haswaa kitendo cha kumkuta Mr.Peter akimkumbatia mwanae.
Muda kidogo, baba Angel nae aliingia sebleni na kukaa karibu na mke wake ila alijifikiria kidogo kumuongelesha kwani huwa anamfahamu mkewe kama ni mkali sana, na muda ule mama Angel alimuita Angel,
“Wewe Angel bado tu!”
Ikabidi mumewe amuulize,
“Kwani bado nini?”
“Kwani hapa tumekuja kufanya nini? Si tumekuja kumchukua Angel?”
“Ushamuulizia mama yuko wapi?”
“Mimi hayanihusu, nimemfata mwanangu”
“Yani mke wangu unajua mambo mengine unayoyafanya kwa hasira huendi kwa utaratibu maana huo sio utaratibu ujue”
“Sitaki habari za kusikia ni utaratibu au sio utaratibu, huyu Angel ni mwanangu. Ni damu yangu mimi yani mimi ndiye mwenye uchungu na mtoto huyu”
“Aiseeee ningekuwa ni aina nyingine ya mwanaume sijui yani”
Baba Angel aliinuka na kutoka nje kwani hakutaka hata kubishana na mke wake.
 
SEHEMU YA 178

Moja kwa moja baba Angel aliamua kumpigia simu mama yake ili kumpa taarifa tu kuwa wanaondoka na Angel kwa muda huo,
“Mama samahani, mama Angel kamkumbuka sana mwanae kwahiyo tumekuja kumchukua”
“Kheee mbona gafla hivyo!! Hebu nisubirini kwanza nifike”
“Mama, kwakweli hapa itashindikana kukusubiri”
“Kwanini sasa? Nimesema nisubirini”
Yule bibi Angel alikata ile simu ila wakati baba Angel akirudi ndani ili kumpa mkewe ile taarifa alishangaa kukuta mke wake tayari kashainuka na kuanza kutoka na Angel kwaajili ya kuondoka, basi akamwambia mke wake,
“Mama Angel, tumsubirie kwanza mama basi”
Mama Angel hakusikiliza swala hilo hata kidogo kwani muda huo huo alimvuta mtoto wake mkono na kutoka nje, kwahiyo baba Angel hakuwa na namna ya kufanya jambo lolote lile zaidi zaidi ya kufatana na mke wake tu.
Basi walienda kupanda kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani kwao iliwadia, yani mama Angel alionekana kuwa na hasira sana.
Walifika nyumbani usiku sana kwani kidogo kule kwa bibi yake Angel kulikuwa na mwendo, moja kwa moja Angel alienda chumbani kwake na wazazi nao walienda chumbani kwao.
Ila baba Angel alikuwa amechukia sana siku hiyo kwa kile kilichofanywa na mkewe, kiasi kwamba hakuweza kusema chochote kile na moja kwa moja alienda kulala tu.
Mama Angel alitulia tuli akifikiria jambo, kwanza alianza kuwaza,
“Hivi yule mr.Peter ni kitu gani alikuwa akifanya na mwanangu? Ndiomana mama aliniambia kuwa yule mama hajui kulea mtoto wala nini hata sijui nilianzaje kumwambia mume wangu apelike mtoto kule jamani!”
Ingawa walirudi na Angel ila alikuwa na mawazo sana.

Usiku wa leo Angel alikuwa akifikiria vitu vingi sana pale kwao, kwanza aliwaza ni kwanini mama yake alichukia sana baada ya kukuta kakumbatiwa na yule mzee,
“Ila mama nae jamani sijui ana matatizo gani, yule mzee si sawa na babu yangu tu!! Sasa yeye kachukia nini yani kitu gani kilichomchukiza kwa yule mzee kunikumbatia jamani wakati alikuwa akinisalimia tu! Na hii simu itabidi niwe naificha maana akigundua basin i balaa, lazima atanipokonya tu”
Kwahiyo Angel aliona ni vyema kwa simu yake kufanya nayo mawasiliano ndani tu na kweli alipoiwasha tu muda huo alikutana na ujumbe toka kwa Samir,
“Yani nilikukumbuka sana Angel mpenzi wangu?”
“Mmmh wewe nawe jamani! Hata mimi nimekukumbuka”
“Kwasasa upo wapi?”
“Nilikuwa kwa bibi ila mama yangu kaja leo na tumeondoka nae hai hai kwahiyo nipo nyumbani kwasasa”
“Kheee mama yako nae naona huwa hana kazi za kufanya yani kazi yake ni kukufatilia wewe tu, hebu mwambie baba yako afanye kazi ya ziada”
“Kazi gani?”
“Ampe mimba, hahaha”
“Tayari anayo, yani yupo kuhangaika na mimba yake”
Basi Samir alikuwa akicheka sana huku akiendelea kuwasiliana na Angel, na siku hiyo pia waliwasiliana sana kiasi kwamba Angel alilala saa nane za usiku.
Kulipokucha, Angel aliamka na kutoka sebleni kisha kuanza kuongea na Vaileth ambaye alimkuta yupo karibu sana na Junior,
“Mmmh makubwa, kwahiyo siku hizi Junior ndio unapika pamoja na Vaileth?”
“Kwani kuna ubaya gani? Maisha kusaidiana”
“Mmmmh! Mama anayajua haya kuwa mnasaidiana?”
“Achana na habari za mama, maana yeye huwa anajielewa mwenyewe tu. Yani mama huwa anapinga kila kitu, kiwe kibaya au kizuri basi yeye anapinga tu”
“Kheee kumbe na nyie mmeshamjua?”
“Ndio, yani yeye kazi yake ni kupinga jamani! Yani hana jambo lolote zuri hata mara moja”
Basi walicheka pale kisha Junior akasema tena,
“Hapa cha msingi kila mtu kufanya jambo analoliona yeye ni zuri maana ukifatilia anayoyataka mama basi utachina maana huyu mama anajijua mwenyewe, tunatakiwa kufanya kitu ambacho roho inapenda”
Angel nae alicheka kisha alirudi chumbani kwake kujaribu kumtafuta Samir kwani kwa muda huo alihisi kuwa ameshamkumbuka.
Ila alipochukua simu yake tu, alishangaa kukutana na ujumbe toka kwa Mussa,
“Ulichonifanyia Angel sio kizuri, nimekuja hapa kwenu ila sijakukuta, ujue nakupenda sana”
Angel alishtuka kidogo kwani hakufikiria kama kuna muda ambao Mussa atamueleza habari za kumpenda sana ila hakumjibu wala nini na kuendelea na mambo yake.
 
SEHEMU YA 179

Baba Angel leo akiwa kazini alipigiwa simu na mama yake ambaye alianza kumlaumu moja kwa moja kwa kitendo chake cha kuondoka na Angel,
“Hivi wewe Erick una akili kweli? Kwanini sasa umefanya ulichokifanya? Mimi nilikwambia kuwa kuhusu Angel nisubirini nirudi ila mmemchukua mtoto bila kunishirikisha, halafu kilichowafanya mumjibu vizuri yule baba wa watu ni kitu gani?”
“Tumemjibu vibaya nani jamani mama?”
Yule mr.Peter, hivi mnaelewa yule ni nani? Yule baba ni mfanyabiashara mkubwa sana, mmeanza kumuwazia vibaya kuhusu Angel, jamani yule baba aanze kumtamani Angel kwa lipi? Yule baba ana familia yake, ana mke, watoto na wajukuu tena wakubwa kushinda Angel halafu kweli mmmeanza kumdhania mabaya kwa Angel jamani!”
“Mama jamani sijui hata kama naweza kukueleza jambo lolote lile ukanielewa, ila nitakuja tuzungumze vizuri. Unajua mke wangu alivyo na kisirani”
“Yule mwanamke jamani! Yani asingekuwa mtoto wa mtu niliyemfahamu kwa hakika nisingeruhusu uoane nae, maana mambo yake anajijua mwenyewe yule mwanamke. Nipeni jibu linaloeleweka kuwa kwanini mmemchukua mtoto bila ridhaa yangu”
Bibi Angel alikata ile simu, kwakweli baba Angel aliona mke wake kamsababishia matatizo tu sababu ya tatizo lake la kuchunga mtoto. Basi siku hiyo alipomaliza shughuli zake, moja kwa moja alienda ofisini kwa mke wake ili kuongea nae kwa ufupi.
Alimkuta akiwa anaendelea na kazi zake, basi alikaa nae na kuanza kuongea nae,
“Hivi mke wangu kile kitendo cha jana unaona ni sawa?”
“Ngoja na wewe nikuuliza, hivi yule mbabu kumkumbatia mtoto wetu unaona ni sawa?”
“Hivi unamjua yule mbaba kwani? Nasikia ni mfanyabiashara maarufu sana”
“Dah! Sijui kama unaweza kunielewa, mama mzazi wa Rahim anajulikana kwa jina la Mrs.Peter na yule Mr.Peter ndio mume wake, najua umenielewa sasa kwanini nilipaniki jana”
“Ila sio tatizo mke wangu, kumbe ni babu yake!!”
“Hivi unaongelea kitu gani Erick? Hebu niambie agenda yako ni nini?”
“basi yameisha, hata hivyo kilichonileta hapa sio hiko ila tu nahitaji kwenda na wewe mahali tukapumzike kidogo kwa siku ya leo”
Yani baba Angel wala hakumueleza tena malalamiko ya mama yake, kwani hakupenda pia kwa swala zima la kumkera mke wake hata kidogo.
 
SEHEMU YA 180

Leo, wakati Erick akitoka shuleni akiwa hana wazo lolote lile ingawa kwenye gari alisumbuliwa na Sarah ambaye alikuwa na kawaida hiyo ya kumsumbua Erick, kwanza kabisa alimwambia jambo,
“Erick, unatakiwa kuwa na simu ili mimi na wewe tuwe tunawasiliana”
“Sijafikiria kabisa swala la kumiliki simu”
“Kheee mtoto wa kiume huna wazo la kumiliki simu kwanini? Erick nakuomba uwe na simu ili tuwe tunawasiliana maana nina mambo mengi sana ya kuzungumza na wewe”
Kuna muda Erick hakumjibu huyu binti kwani alimuona ni kama mtu aliyetrumwa vile.
Ila leo aliposhuka tu kwenye gari, alishangaa akiitwa jina,
“Erick!!”
Basi alisimama na kuangalia kuwa ni nani aliyekuwa akimuita kwa muda huo, basi aliposimama pale ndipo aliposogea mwanamke mmoja hivi ambaye alimkumbuka sura yake kuwa ni mwanamke wa dukani ambaye alidai kuwa ni mwanae na kujaza watu wengi, basi Erick alimuangalia huyu mwanamke kwa muda ila yule mwanamke alimsogelea Erick na kumwambia,
“Erick mwanangu, hujambo?”
“Kwani wewe mwanamke una matatizo gani lakini? Mimi sio mtoto wako”
“Hebu acha kujiongopea huko, mimi ni mama yako na hilo haliwezi kubadilika kamwe, mimi ndiye ambaye nilikubeba miezi tisa”
“Unazungumzia kitu gani?”
“Kuna siku utanielewa tu vizuri sana ila kwasasa utaona kama mwanamke kichaa ndio anaongea mbele yako, iko hivi. Erick wewe ni mtoto wangu na hilo wala halibadiliki, kwanza jiangalie jinsi ilivyokuwa kati yako wewe na huyo mama unayeishi nae humo ndani, je huyo mama anakupenda kweli? Huyo mama anakujali kama mtoto wake wa kumzaa? Hebu fikiria swala la baba yako kukupatia lile duka, hebu fatilia, ni hivi huyo mama yako ni anapinga vikali sana swala hilo yani hataki kabisa wewe umiliki chochote katika nyumba hii. Usifikiri hajui kama wewe sio mwanae! Anajua wazi kuwa wewe sio mtoto wake na hana uchungu wowote ule na wewe, nakwambia ukweli wewe ni mwanangu, wewe ni damu yangu, unatakiwa kuwa karibu na mimi ili ufahamiane na ndugu yako”
“Sikuelewi”
“Huwezi kunielewa, ila wewe ni mwanangu. Baba yako analijua hilo na mama yako analijua hilo, hii familia itaendelea kukutenga hadi mwisho na siku zote hutokuwa na amani wala raha, ila ukishirikiana na mimi basi utairudisha furaha yako kwani umepata bahati sana kumpata mama mwenye akili kama mimi. Katika maisha yangu niliomba sana Mungu anipatie mtoto wa kiume, na kweli akanipatia wewe yani wewe una kazi kubwa sana kwangu, wewe ndio wa kubadilisha maisha yangu na ndiye pekee wa kubadilisha historia yangu na kunifanya nionekane mtu mpya yani hiyo kazi ipo juu yako wewe. Sikukuzaa kwa bahati mbaya ila nilikuzaa kwa lengo maalumu kabisa. Nimejionyesha kwako ili utambue kuwa mimi ndiye mama yako mzazi, fanya yote ila mimi ndiye mama yako mzazi na sasa naenda tena kupigania mali yako”
Halafu yule mwanamke akaondoka zake, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la ajabu sana machoni na masikioni mwa Erick, hakuelewa na alizidi kuona akili yake ikichanganyika na kumfanya azidi kukosa raha.
Basi aliingia ndani na kuwaza vitu vingi na moja kwa moja alianza kujiona tofauti na watu wengine kwenye familia hiyo, kwanza alikumbuka jinsi baba yake alivyomwambia kuhusu dukani kuwa asimueleze mama yake, na pia aliwaza jinsi ukaribu wa mama yao na Angel pamoja na Erica halafu ukaribu wake na mama yake, aliona kweli kuna kasoro, kwakweli lile jambo lilimfanya aumie sana moyo wake na moja kwa moja alikaa chumbani tu akiwa na mawazo sana kwa siku hiyo.

Baba Angel na mama Angel walitoka pale ofisini na moja kwa moja walienda hotelini ambapo huko waliagiza chakula na vinywaji, kwahiyo wakaanza kula huku wakiambizana mambo mbalimbali yanayoendelea,
“Hivi ushaenda kuangalia mtoto wetu huyu ni jinsia gani?”
“Mmmmh yani kwasasa nadhani huyu mtoto anataka kutushtukiza tu, maana kila nikienda kupima basi Napata jibu kuwa mtoto kajificha, kwahiyo jinsia yake haijulikani”
“Ila nadhani atakuwa wa kiume”
“Kwanini sasa awe wa kiume?”
“Ili mke wangu upumzike kidogo maana naona Angel na Erica wanafanya akili yako iruke kabisa”
Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga ni Steve, basi aliipokea na kuanza kuongea nayo,
“Bosi, yule mwanamke kaja na leo, na uzuri ni kuwa huyu askari kamshikilia kwahiyo unaweza kuja kuonana nae”
“Sawa”
Baba Angel alimuangalia mke wake kwa muda pale kwani aliona si vizuri kama akienda kule na mke wake, kwahiyo aliona ni vyema kama atatumia njia nyingine ili tu asiende na mke wake kule, basi akamwambia,
“Mama Angel, unajua kwa hali yako ilivyo kwasasa sio vizuri kukaa hotelini kwa muda mrefu!! Inatakiwa upate muda wa kutosha ili upumzike mke wangu”
“Oooh nashukuru sana kwani inaonekana kuwa unanijali sana”
Basi baba Angel alimuomba muhudumu kumfungia kumfungia kile chakula chao kilichobaki halafu ni moja kwa moja walirudi nyumbani tu.
 
SEHEMU YA 181


Muda huu familia ilikuwa imejiachia kabisa, yani waliendelea na vipindi vyao kwenye Tv bila ya tatizo lolote, sababu tu waliamini kuwa wazazi wao hawapo ila katika watu wote ni Erick pekee ndio hakuwa na raha kabisa na kwa muda huo alikuwa amekaa tu chumbani kwake. Erica kama kawaida alienda kwa kaka yake ila alimuona pia kuwa hakuwa na furaha kabisa, ila hata yeye aliumia kwani hakumzoea kumuona Erick katika hali kama hiyo.
Basi muda kidogo mama Angel na baba Angel walirudi ila muda ule ule baba Angel alitoka tena, ila kwa muda huo huo Erica alienda chumbani kwa mama yao kuongea nae kuhusu Erick kama ilivyokawaida yake kwa jambo lolote linalotokea ndani ya nyumba yao basi kulisema kwa mama yao,
“Mama, yani leo toka Erick atoke shuleni sijui ana matatizo gani, yani hana furaha hata kidogo hata chakula amekataa”
“Jamani, mwanangu kapatwa na nini tena?”
“Sijui mama, ila leo hata mimi hataki kuongea nami vizuri kwani kila nilichokuwa namuongelesha hakunijibu halafu inaonekana ana majonzi sana mama.”
“Mmmh! Ngoja nikaonhee nae basi”
Muda huo huo mama Angel aliinuka na moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ila hata yeye alimuona mwanae kuwa hana raha kabisa halafu alionekana kila alipojaribu kujiweka katika furaha hakuwa na furaha kabisa, basi mama Angel alianza kuongea na mwanae,
“Mwanangu Erick, tatizo ni nini baba? Mbona unaonekana huna furaha kabisa?”
“Samahani mama, kuna jambo nataka nikuulize”
“Jambo gani hilo? Niulize tu”
“Kwanza mama, ni kwanini hunipendi?”
Mama Angel alishtuka sana kwa swali lile maana hakutegemea kama swali kama lile lingetoka kwenye kinywa cha mtoto wake, basi nae alimuuliza,
“Sikupendi? Kivipi Erick? Yani mimi niache kumpenda mtoto pekee wa kiume niliyenaye?”
“Sikia mama, kuna mambo huwa nafanya na baba na mara nyingi huwa anasema nisikushirikishe, kama swala la mimi kupelekwa kwenye lile duka jipya la baba. Swali langu mama ni kuwa, ni kweli mimi ni mtoto wako?”
“Jamani jamani Erick, mbona unataka kuniumiza tumbo la uzazi wewe mtoto jamani! Katika uzao wangu, nimezaa mapacha kwa mara moja tu yani wewe na Erica na ndiomana tuliwapa majina yani tukimaanisha kuwa ni mimi na baba yenu. Erica kachukua badala yangu na wewe umechukua badili ya baba yenu. Sasa kama wewe sio mwanangu basi na Erica sio mwanangu pia maana ni watoto ambao niliwazaa pamoja. Halafu dhana ya kusema kuwa mimi nakuchukia unaitoa wapi Erick?”
“Sijui mama, ila kuna mama nimekutana nae na ameniambia kuwa yeye ndio mama yangu mzazi, na wewe na baba mnalitambua hilo. Mama niambie ukweli, kama mimi ni mtoto wa kuokotwa nijue moja halafu ni vyema kama nikiwajua wazazi wangu halisi, hata kama ni masikini hakuna tatizo mimi nitaishi nao tu”
“Jamani Erick mbona unataka kuniliza wewe mtoto eeeh! Nani kasema kuwa wewe sio mtoto wangu? Nikubebe mwenyewe tumboni, nikusae kwa uchungu, nikunyonyeshe kwa matiti yangu haya, leo hii anaibuka mtu na kusema kuwa wewe sio mtoto wangu kweli! Erick hayo maneno yametokea wapi jamani! Umeyatoa wapi hayo maneno Erick mwanangu!”
Mama Angel pia machozi yalimtoka kwani maneno ya mtoto wake yalikuwa yakimuumiza sana, kiukweli alikosa raha gafla pia na hakuelewa kuwa mwanae hayo maneno kayatoa wapi, basi alimsogelea mwanae na kumkumbatia huku akilia na kusema,
“Mwanangu hebu niambie ni wapi umeyatoa hayo maneno jamani, yani nani amekueleza vitu vya namna hiyo? Mimi sikukatazi dukani sijui sababu sio mwanangu hapana jamani, hata baba yako anajua ni kwanini nakukataza, mimi mwanangu nataka usome na ufike mbali, ukianza kuwaza biashara kwasasa ni wazi kuwa utaona elimu haina maana yoyote katika maisha yako ila hiko sio kigezo kuwa sikupendi mwanangu. Kwanza nani kakwambia hayo maneno jamani! Mtoto nimzae mwenyewe halafu leo asiwe mwanangu! Toka nizaliwe sijawahi fikiria jambo la namna hiyo. Nani kakwambia mwanangu?”
“Mama kuna mwanamke ambaye huwa anagombana na yule anko pale dukani, na yule mwanamke ameyasema maneho hayo siku nimeenda pale dukani na watu wengi walijaa ila baba alikuja na kusema kuwa nipuuzie maneno ya yule mwanamke. Leo wakati nimetoka shule, nimekutana na yule mwanamke nje ya geti letu na ameniambia tena kuwa mimi sio mtoto wa familia hii bali ni mtoto wake na nyie mnalitambua hilo ndiomana hamnipendi”
“Oooh jamani kuna watu wanaweza kukukumbusha hadi siku uliyoingia leba, kwakweli sijawahi kufikiria kitu cha namna hii kwa mtoto wangu pekee wa kiume, hivi mimi nisikupende Erick jamani, nimpende nani sasa? Subiri kwanza”
Mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake ambapo alibadilisha nguo kisha akamfata Erick na kumtaka waondoke ili waende dukani kwani lengo lake lilikuwa ni kuongea na Steve kwani alihisi lazima Steve anafahamu vizuri kuhusu huyo mwanamke, kwahiyo mama Angel na Erick waliondoka muda huo.
 
SEHEMU YA 182

Mama angel alipoondoka tena, huku nyuma familia ilifurahi kidogo ila kama kawaida ya Erica, muda mama yake anaongea na Erick basi alikuwa mlangoni akisikiliza kila kitu.
Kwahiyo walipoondoka, moja kwa moja alienda chumbani kwa Angel ili akamuelezee mambo yake, alipoingia chumbani kwa Angel alimkuta na ile simu ila Angel alishtuka sana yani ilibakia bado kidogo tu aangushe ile simu na kuanza kumsema mdogo wake,
“Jamani wewe Erica, hebu jifunze kuheshimu vyumba vya watu wengine, ukiwa unaingia basi ujue jinsi ya kugonga hodi”
“Kheee samahani dada, ila nimeona hiyo simu nzuri sana. Ndio haya mambo anayoyalalamikia Erick, humu ndani kuna upendeleo, hebu ona wewe una miliki simu kubwa na nzuri halafu inaonekana ya gharama wakati sisi hata kupiga ile simu ya mezani ukigundulika ni balaa”
“Halafu wewe nawe mambo mengine yatakushinda, hebu uachage vitu vingine vikupite. Halafu nikusikie fyokofyoko kwa mama kuwa nimemuona Angel na simu ndio utanielewa vizuri. Mimi ni mkubwa na sio kila ninachokuwa nacho mimi basi na nyie muwe nacho, hebu kuwa mpole tu. Haya kilichokuleta muda huu”
Erica akaanza kumuelezea toka Erick alivyorudi amepooza hadi jinsi alivyokuwa akiongea na mama yao na jinsi mama yao alivyoondoka nae,
“Kheee mambo mengine yanachekesha, sasa Erick nae anafatiliza maneno ya watu mbona atapata shida sana? Sasa bora hata yeye, mie mwenzie nasemwa kila leo kuwa nafanana na waarabu na wala sina tatizo lolote lile kwani najua huyu ndio mama yangu na baba ndio baba yangu, hata mtu atokee wapi na kusema hawa sio wazazi wangu basi nitambishia. Yani mtu akisema sifanani na wazazi wangu basi nitasema nimefanana nao hata kucha, unajua maisha haya ni kawaida kabisa kutokufanana na wazazi hata mama amewahi kuniambia hivyo. Sasa Erick anataka nini lakini jamani!!”
Simu ya Angel ilianza kuita na muda huo huo Angel alimwambia Erica,
“Haya chaumbea nipishe niongee na simu maana wewe najua nitakayoongea nayo kwenye simu basi utayabeba kama yalivyo na kwenda kutabwaga unapopajua wewe”
Basi Erica aliinuka ila hakupenda vile dada yake alivyomuita chaumbea.

Mama Angel na mwanae walifika dukani, na moja kwa moja walipoingia ofisini walimkuta baba Angel, Steve na yule mwanamke ambaye ni Sia, na yule mwanamke alipomuona mama Angel alipiga makofi na kusema,
“Sasa ukweli utajulikana, nimefurahi sana wote mmekuja”
Mama Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu sana, na kujikuta akipatwa na hasira juu yake na kwenda moja kwa moja kumzaba kibao ila cha kushangaza mama Angel alianguka chini na kuanza kugalagala.

Mama Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu sana, na kujikuta akipatwa na hasira juu yake na kwenda moja kwa moja kumzaba kibao ila cha kushangaza mama Angel alianguka chini na kuanza kugalagala.
Kitendo kile kilifanya wote waanze kumshughulikia mama Angel ambapo walimbeba na kumtoa nje na kumpakiza kwenye gari, halafu baba Angel pamoja na Erick wakaondoka nae kuelekea hospitali.
Kwahiyo pale dukani alibaki Steve na Sia, ila kiukweli Steve pia alichukizwa na ile tabia ya Sia, nay eye mwenyewe kuamua kumsogelea Sia huku akitaka kumzaba kibao ila Sia alikamata ule mkono wa Steve na kumuuliza,
“Kinachokufanya utake kinipiga ni kitu gani?”
“Hivi unajua wewe mwanamke huna akili!”
“Ni kweli mimi sina akili tena sina akili kabisa, nadhani akili zangu hujawahi kuzijua ila mimi ni chizi kushinda unavyofikiria wewe. Halafu wewe unawezaje kutaka kunipiga mimi kibao? Mwanamke niliyekufundisha mapenzi, niliyekuonyesha mapenzi ni kitu gani wewe halafu unajitia ushujaa kutaka kunipiga mimi! Hebu jiheshimu dogo”
Halafu Sia alitoka na kuondoka zake, yani Steve alimuangalia yule mwanamke bila ya kummaliza, alikaa chini na kutafakari baadhi ya mambo. Alianza kukumbuka mambo ya zamani ambayo yaliwahi kutokea katika maisha yake, kwanza kabisa alimkumbuka mwanamke ambaye aliwahi kumpenda katika maisha yake ila kwa kipindi hiko hakujua kuwa yule mwanamke yuko wapi, akakumbuka pia jinsi alivyoanza mahusiano na Sian a kusema,
“Isingekuwa lile tunda lake lenye dawa basi mimi nisingekuwa nae, ila kitu kingine isingekuwa uroho wangu basi nisingekuwa na huyu mwanamke, ni aina gani ya mwanamke hii jamani! Eeeh Mungu ninusuru”
Alibaki tu analalamika, ila aliona ni vyema kufunga duka tu kwa muda huo kwani tayari ilikuwa ni usiku.
 
SEHEMU YA 183


Basi wakati mama Angel amepelekwa hospitali ni moja kwa moja daktari alimchukua na kwenda kumuhudumia, muda huu Erick alikuwa nje na baba yake kwahiyo hawakuweza kuongelea chochote kile maana mawazo muda huo yalikuwa ni juu ya mama Angel tu. Basi Erick alimwambia baba yake,
“Baba, huwa mnasema kila kitu tunapaswa kuomba. Kwanini tusimuombee mama!”
“Oooh umenikumbusha jambo jema sana, kuna mama mmoja hivi tulikuwa tukimtumia sana kwenye maswala ya maombi, ngoja leo nimpigie simu”
Basi baba Angel alimpigia simu huyo mama na kuongea nae kwa muda kidogo kisha kufanya nae maombi na kukaa pale na mtoto wake huku wakisubiri majibu kuwa ni kitu gani kilimsibu mama Angel muda kidogo Daktari alifika na kumwambia baba Angel,
“Hongera sana, mkeo kajifungua”
“Oooh! Mungu ni mwema kwakweli, huyo mwanangu ataitwa Ester”
“Kheee umejuaje kama ni wa kike au mlipima?”
“Halafu nimejikuta tu nikiropoka hilo jina sababu muda sio mrefu nilikuwa nikiongea na mama mmoja wa maombi anayeitwa Ester”
“Basi hongera sana, mkeo kakupatia huyo Ester”
Baada ya muda kidogo ndipo baba Angel pamoja na Erick waliruhusiwa kwendfa kumuona mama Angel pamoja na mtoto, kwakweli walifurahi sana, hata mama Angel alifurahi yani kwa muda huo walisahau kila kitu kilichotokea mwanzo sababu ya ile furaha.
Ingawa ilikuwa ni usiku ila walikuwa na furaha sana kiasi kwamba waliona kuwa ni mapema kabisa kabisa.
Basi walikazana kuongea nae pale, huku baba Angel akipigia simu baadhi ya ndugu zao na kuwapa ile taarifa ya kuhusu kujifungua kwa mama Angel, na kila alipopiga simu alisema kuwa mwanangu Ester amezaliwa.

Baba Angel na Erick waliporudi nyumbani walitoa taarifa kwa wote kuwa mama yao kajifungua mtoto wa kike, basin a wao walifurahi sana.
Muda Erick akiwa chumbani kujiandaa kulala kutokana na uchovu wa siku hiyo, akafatwa na Erica ambaye alianza kuongea nae,
“Haya sasa Erick, mama kaongeza jinsia yetu tena. Kwahiyo wewe unabaki kuwa mtoto wake wa pekee”
“Mmmh sisi wote ni watoto wake wa pekee, haijalishi ni jinsia gani?”
“Shauri yako, mimi nakwambia ukweli yani mama atazidi kukupenda wewe maana umebaki kuwa mtoto wake wa pekee wa kiume maana wote sisi ni wanawake. Dada Angel, mimi na sasa tuna Ester, mmmh sijui atakuwa mbea kama mimi!”
“Kheee kumbe unajijua! Niache nipumzike kwanza Erica kwa muda huu maana najua ukianza kuongea hapo hata hutomaliza wakati wewe ulishalala, mwenzio sijalala hata kidogo halafu kesho tunaenda tena shuleni”
Basi Erica alimuacha kaka yake na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kulala.
Kulipokucha kama kawaida, walijiandaa na kwenda shuleni, ila leo Erick alipokaa kwenye kiti cha basi la shule, basi Sarah nae alifika na kukaa hapo halafu akaanza kumuuliza,
“Mbona unaonekana umechoka hivyo Erick?”
“Aaaah jana nimechelewa sana kulala, kwani tulikuwa hospitali na mama”
“Kheee kafanyaje tena?”
“Amejifungua mtoto wa kike, kumbe ilikuwa ni uchungu”
“Oooh jamani, wifi yangu mwingine kazaliwa jamani! Nitakuja kumuona Erick”
Basi Erick alimuangalia tu Sarah, kwani huyu binti alikuwa na vituko ambavyo ilikuwa ngumu sana kwa Erick kuvielewa.
 
SEHEMU YA 184


Leo mama Angel aliruhusiwa kurudi nyumbani, kwahiyo alirudi nyumbani na mtoto akiwa ameambatana na mumewe pamoja na mama yake ambaye kwa kipindi hiko ilibidi aje akae hapo ili kumsaidia mwanae kwaajili ya uzazi ule.
Kwahiyo walirudi pale nyumbani na kuanza kufanya mambo mengine ya familia ikiwa ni pamoja na yule mama kuelekeza chakula cha kupika kinachomfaa mama mzazi, ilibidi wakina Angel wawe wapole sana kwani Angel alimtambua bibi yake huyo.
Basi muda huu Angel na Junior walitoka nje na kwenda kukaa kwenye bustani huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Angel, swala la huyu bibi kuwepo hapa unalionaje?”
“Mmmh majanga ujue, yani huyu bibi nahisi atatufatilia hadi muda wa kulala, na usipokula utaulizwa kwanini hujala, na ukichelewa kulala basi ujiandae maswali kwanini umechelewa kulala”
“Kumbe unamjua eeeh!”
“Namjua ndio, niliishi kwake siku tatu tu ila nilijiona kama naishi miaka, jamani bibi anafatilia huyu balaa, hapa nawaza akianza mambo yake ni balaa”
“Ila usijali Angel, kwasasa tumekuwa wakubwa, huyu bibi tutamnyoosha”
Yani wakajikuta wakipanga mambo mbalimbali kuhusu bibi yao ambaye kwa kipindi hiko ndio alifika kwaajili ya uzazi wa mama Angel.

Muda wa kutoka shule siku hiyo, Erick na Erica waliingia pamoja nyumbani kwao, kwahiyo walipofika tu moja kwa moja walienda kumuangalia mtoto mpya ambaye mama yao alikuwa kamleta nyumbani.
Ila mama Angel alimuuliza Erick,
“Mwanangu unaendeleaje?”
“Salama mama”
Mama Angel aliona bora aanze hiyo tabia ili Erick asijisikie vibaya tena kama ambavyo alijisikia mwanzoni.
Baada ya hapo, Erick aliondoka kuelekea chumbani kwake naye Erica alienda chumbani kwake pia.
Baada ya muda kidogo, Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Erick, nikwambie kitu”
“Niambie”
“Yani leo, nilipoenda jikoni nimemkuta dada Vaileth na Junior wanabusiana”
“Mmmmh Erica na wewe jamani! Eeeeh walifanyaje?”
Basi Erica akainuka na kwenda kumuonyesha kaka yake ambavyo amewakuta Vaileth na Junior ndani ila kile kitendo kilijenga hisia kali sana kwa Erick, hata Erica mwenyewe alijishtukia na kuondoka mule chumbani kwa kaka yake, basi Erick alikaa chini na kuanza kujiuliza,
“Kwanini nimejihisi hivi baada ya Erica kunibusu? Au ndiomana yule mama anasema kuwa mimi sio mtoto wa familia hii? Hapana haiwezekani, mimi ni mtoto wa familia hii na Erica ni pacha wangu ila tu sijui inakuwaje, nayeErica ananifanyia kama makusudi hivi!”
Basi aliamua kufanya mambo mengine tu kwa muda huo.

Siku hii ilikuwa ni siku ya Jumamosi, kwahiyo hawakwenda shuleni walikaa tu nyumbani huku wakiendelea na kazi mbalimbali za nyumbani.
Kwenye mida ya mchana, Junior alikuwa amekaa bustanini yani kwa siku hizo Junior alijikuta akipenda sana kukaa bustanini zaidi kuliko kukaa ndani, basi Erick alimfata Junior na kuanza kuongea nae, ambapo Junior alimwambia,
“Eeeh sasa huo ndio uanaume, sio muda wote kukaa karibu na wanawake tu. Yani wewe sababu pacha wako ni mwanamke basi huna rafiki mwingine zaidi ya Erica tu, hivi kuna hata rafiki zako ambao unabadilisha nao mawazo Erick!”
“Hapana, hata marafiki kiukweli kabisa sina. Kwanza mama anawatunza sana watoto wake wa kike, na alishawahi kuniambia kuwa hataki marafiki wa kiume kwani wataharibu watoto wake, kwahiyo mimi sinaga marafiki kabisa, ndiomana hapa utaona wanakuja rafiki wa Erica kw asana maana hata Angel alikatazwa kuhusu swala zima la marafiki”
“Ila mamdogo jamani, hata sijui alizaliwa kipindi gani yani ana mambo ya kishamba sijapata kuona. Na hivyo kazaliwa mjini na kukulia mjini, hivi angezaliwa kijijini hata sijui ingekuwaje? Sasa anawakataza msiwe na marafiki ili muishi maisha gani? Maisha bila marafiki hayaendi kabisa, mimi muda mwingi utanikuta nipo na simu kwani rafiki zangu wengi sana nawasiliana nao na licha ya kuwasiliana nao huwa natoka kwenda kuwatembelea na kuongea nao mambo mbali mbali. Sasa wewe Erick ukijifungia muda wote, ni lini utachangamsha hiyo akili yako? Lini utatambua jambo la kutenda kwa muda huu au ule? Unajua kuna mambo tukiyakwepa maishani basi tutakuja kuyafanya kwenye utu uzima na kuonekana ni kituko, binafsi huwa sipendi kufatiliwa kwenye mambo yangu. Nilishawahi kukuuliza, hivi una rafiki wa kike ila hukuwahi kunijibu”
“Dah! Unaongea sana Junior. Ngoja nikuulize kitu, hivi ukimpenda mwanamke unajisikiaje katika moyo wako?”
“Kwanza unajihisi kutamani kumuona mwanamke huyo muda wote, ila kuna siri moja katika mwili wa mwanaume mdogo wangu, yani mwanamke unamtamani kwanza halafu unampenda, yani cha kwanza unachoona kwa mwanamke uliyevutiwa nae basin i wazo kuwa upo nae kitandani yani ukivunja nae amri”
“Unasemaje!”
“Ona unavyoshangaa jamani! Hivi wewe ni mzima kweli? Hivi umekamilika wewe! Katika maisha ya mwanaume hiko ndio kitu kikubwa sana, hebu acha uzoba. Basi kwa akili zako nadhani unawaza yale maneno kuwa tendo lile ni mpaka uoe, hivi utaoa lini ili ufaidi? Hizo ni akili za kimama, ndiomana nakwambia jichanganye na wanaume wenzio ili upanue akili hiyo”
“Kumbuka nipo kidato cha kwanza”
“Kwani kidato cha kwanza ndio nini? Watu walianza toka darasa la kwanza huko, sembuse kidato cha kwanza! Yani wakati unaanza unajaribu jaribu hadi mwishowe unakuwa mtaalamu kabisa”
“Mmmmh! Haya, na kama umempenda mwanamke ila huyo mwanamke hakutaki ni kitu gani unaweza kufanya ili kumsahau?”
“Jamani wewe jamani hadi unatia huruma, hivi mwanamke umpende asikutake kwasababu gani? Akikutaa dawa ni moja tu, unatakiwa kuwa na mwanamke mwingine wa kuweza kumtia wivu yule mwanamke umpendaye.”
“Kwahiyo wewe una wanawake wangapi?”
Muda huo Vaileth alikuwa akienda kuwaita kwaajili ya chakula, kwahiyo alijikuta maongezi yao mengi sana ameyasikia, ila kiukweli aliumia sana moyo wake kwa yale maneno ya Junior ila hakusema chochote zaidi ya kuwaita tu kwaajili ya chakula basi nao waliinuka na kwenda kupata chakula tu kama kawaida.
 
SEHEMU YA 185


Maneno ya Junior yalianza kukaa kwenye kichwa cha Erick, aliona ni vyema kwake kama atakubali kuwa na Sarah, alihisi huenda akikubali kuwa na Sarah basi wazo la hisia juu ya dada yake litapotea kabisa,
“Mmmh ila mama akigundua itakuwa balaa. Ila mimi ni mtoto wa kiume niogope nini sasa? Wapo watoto wa darasa la kwanza na wameanza hayo mambo sembuse mimi wa kidato cha kwanza!”
Aliona kuwa ni sahihi kwa yeye kufikiria hivyo, ila muda huo Erica alienda tena chumbani kwake kama kawaida kumpelekea habari ambazo alizichota huko.
“Erick basi nikwambie leo jamani, nilienda tena jikoni yani nimetoka jikoni muda sio mrefu. Vaileth alikuwa akipika, halafu Junior akaenda nyuma ya Vaileth na kumkumbatia halafu alitaka kumbusu kama ile jana, kheee maaajabu ya leo sasa, dada Vaileth akamtoa Junior halafu akamnyooshea kidole na kumwambia kuwa usinizoee”
“Kheee una uhakika na unachokisema Erica?”
“Ndio, yani nimeshuhudia mwenyewe, itakuwa wamegombana tu. Ila yule dada nilikuwa namuhurumia sana, jamani Junior hafai kabisa, Junior sio mwanaume wa maana”
“Sasa mwanaume wa maana kwako ni yupi?”
“Mwanaume wa maana kwangu awe kama baba, yani anipende mimi tu. Katika maisha yake kusiwe na aina yoyote nyingine ya mwanamke zaidi yangu mimi. Anijali, aniheshimu na anithamini. Mwanaume wa hivyo basi nipo radhi kumpa nusu na robo ya maisha yangu”
“Mmmh kumbe! Wanawake mnapenda kupendwa eeeh!”
“Nenda kamuulize mama, yani muulize hitaji kubwa la mwanamke ni kitu gani? Basi mama atakujibu kuwa hitaji la kwanza la mwanamke ni kupendwa, ila nahisi katika dunia hii mama yetu ana rah asana jamani! Unajua baba haendi popote toka mama ajifungue, akitoka basi muda mfupi tu anarudi kumuona mama na Ester, kwakweli baba ana upendo sana”
“Kama mimi, nina uhakika watoto wangu watasema kama wewe unavyosema sasa”
“Mmmh kujisifia tu, huna lolote na wewe”
Halafu Erica aliondoka zake, ila kaka yake alimuangalia tu bila ya kusema kitu chochote kile.

Muda wa kulala ulipofika, Vaileth alienda chumbani kwake ila kiukweli maneno ambayo Junior alikuwa akiongea na Erick kwa siku hiyo hayakumfurahisha hata kidogo,
“Jamani, yani mimi Vaileth nimejidumbukiza kabisa. Mara nyingine ni heri tu kuwa na mtu mzima maana ana mawazo ya kikubwa ila kuwa na mtoto kama Junior ni kazi kubwa, yeye anawaza kubadili wanawake tu, yani hanifai kabisa. Najuta hata kwanini nilimkubali”
Junior alienda kugonga mlango wa Vaileth ambapo alienda kumfungulia, ila Junior alivyoingia akafanya kama kawaida ambapo alimfata karibu Vaileth na kumkumbatia ila leo Vaileth alimsukuma kwa pembeni na kumfanya Junior amuulize kuwa tatizo ni kitu gani,
“Kwani una shida gani Vaileth? Tumekuwa wote vizuri sana kwa kipindi chote hiki au huyu bibi kakusema vibaya?”
“Hivi wewe Junior unaona mimi ni mtoto mwenzio eeeh! Kiasi cha kunifanya utakavyo?”
“Sikia nikwambie, mapenzi hayana ukubwa wala udogo. Kwani mimi na wewe tumepishana miaka mingapi? Si miaka mitano tu! Siku zote huwa nakwambia katika miaka hiyo ona kuwa mimi ndio nimekupita wewe na wala usifikirie kuwa wewe umenipita mimi, tatizo lako ni nini sasa? Umri au kitu gani? Unaweza kunizidi ila kwenye swala la mapenzi nimekuzidi na mengine nakufundisha”
“Unajua usinizoee wewe, tena usinizoee kabisa, wewe mtu gani wewe. Upo na mimi kumbe unawaza wanawake wengine?”
“Jamani jamani, aliyesema nawaza wanawake wengine ni nani? Mbona unataka kunizulia tum engine Vaileth wangu jamani!”
“Hivi unafikiri sikukusikia wakati unazungumza na Erick leo? Nimesikia kila kitu”
“Kheee kumbe kwasababu hiyo tu! Yale mimi nilikuwa naongea tu kufurahisha mdomo, kwanza Vaileth umebadilisha sehemu kubwa sana ya maisha yangu. Ujinga niliokuwa namwambia Erick, mimi siwezi kuufanya kabisa. Nakupenda sana, usinifikirie vibaya”
Junior akamsogelea karibu tena Vaileth ila kwa muda huu Vaileth alijikuta akiwa mpole kabisa, yani kwa Vaileth ilikuwa kamavile Junior anamfata na sumaku maana hata malalamiko yake aliyakuta yanayeyuka kwa muda mfupi, kisha wakaamua kulala pamoja kwa muda huo.
 
Back
Top Bottom