Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 224

Gari lilifika na alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati anatoka akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani Erica alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa mgongoni amelala.
“Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?”
“Wa dada yangu”
“Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?”
“Kaenda kazini”
“Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba changa basi inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki”
Swala la kuambiwa Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica.
Muda huo ilikuwa kama Erica kapigwa na bumbuwazi maana alisimama tu bila kwenda mbele wala kurudi nyuma, ila Mrs.Peter alikuwa ametangulia mbele akijua Salma anamfata nyuma ila muda huo Salma alikuwa akisimama palepale na alionekana akimuangalia Erica kwa chuki ya waziwazi, kitu ambacho kilimshangaza hata Erica mwenyewe, na kumuuliza,
“Mbona unaniangalia hivyo?”
“Utaacha lini uongo wewe mwanamke? Eti mtoto wa dada yangu (Huku akibana pua, na kuendelea kusema). Mtoto wako mwenyewe unasingizia wa dada yako, kwani ni kipi unachohitaji kwa huyu mama?”
Erica alimuangalia huyu Salma na kutamani hata kumpa tusi ila tu swala la kutukana halikuwepo kwenye kinywa chake, muda kidogo mwanae akaamka na kuanza kulia, ikabidi Erica amfunue na kumgeuzia kwa mbele, muda huo Salma alikuwa akiondoka kumfata Mrs.Peter ila Erica akamshika vizuri mkono Salma na kumrudisha nyuma kisha akamwambia,
“Mwangalie vizuri huyu mtoto ndio utaelewa ni kwanini sikusema wa kwangu.”
Kisha Erica akaondoka ila alimuacha Salma akiwa na maswali mengi sana, aliendelea kumfata Mrs.Peter ila kiukweli alikosa raha.

Erica alipotoka pale hospitali hata hakutamani kuita gari ya kukodi, na moja kwa moja alielekea kupanda daladala maana alijiona kama ni kudhalilika tayari ameshadhalilika vya kutosha, aliamua kuacha tu jamii yake ijue kuwa ana mtoto, hakuwa na sababu tena ya kumficha mtoto wake.
Akiwa kwenye daladala, alikaa siti ya nyuma ambako kulikuwa na wamama wawili wamekaa kwa pembeni yake wakiongea, yale maongezi yao aliyasikia yote na yalionyesha kuvuta sana hisia zake,
“Yani mwenzangu, kipindi kile natoka na mume wa mtu halafu mkewe hata simjui ila cha kushangaza nilikutana nae njiani si nikagombana nae, yani jamani mapenzi bhana yana wivu ambao mwizi humjui ila unashangaa unagombana nae. Niligombana na Yule mkewe hadi mumewe akaja kutuamulia ndio hapo nikajua kumbe Yule ndiye mkewe, na ubaya hakuniambia kuwa ameoa weee balaa lilizuka ila nikaamua kuwa mpole na kujitoa”
“Ila mapenzi ndio yalivyo, yani mnaweza kuwa mnatoka na mtu mmoja hamjuani ila unashangaa kuna mambo gafla tu mnachukiana jamani, sijui wale wanaoishi wake wawili au watatu wanajisikiaje ndani”
“Washazoea wale, ila katika ujana wangu nimejifunza jambo. Hawa wanaume ni bora kuwachuna tu, ukijiendekeza kuwapenda utalia jamani, ni waongo balaa”
“Hahaha, ila wakweli wapo bhana, sio wote waongo kumbuka hata na wao wanalalamika kuwa wanawake ni waongo”
“Ndio, ila wao wamezidi”
Basi kituo kilichofata wale wanawake walishuka na kumuacha Erica akitamani hata kuwauliza baadhi ya maswali ila hakuweza maana hakuwazoea.
Ila waliposhuka tu kule nyuma alipanda mkaka na kukaa karibu na Erica, Yule mkaka alimtazama Erica na kumtazama mtoto wa Erica kisha akamwambia,
“Dada, hongera sana una mtoto mzuri. Halafu ana tabasamu vizuri”
“Asante”
“Mmmmh sijaanza hata kukusalimia maana nilivutiwa na uzuri wa huyu mtoto, hali yako lakini”
“Nzuri, ila usijali”
“Ngoja nijitambulishe kidogo, dada mimi naitwa Moses. Nina duka langu zuri sana la nguo za watoto wakike na wa kiume. Naomba uje dukani kwetu hata mara moja uone huduma zetu, business card yangu hii”
Akamkabidhi Erica, naye Erica akapokea huku akisikiliza maelekezo mengine toka kwa Yule kaka,
“Tafadhali dada, naomba ufike. Nimevutiwa sana na mwanao. Najua atapendeza sana akivaa nguo zetu zile. Ila unaitwa nani, na mwanao anaitwa nani?”
“Mimi naitwa Erica, na mwanangu anaitwa Angel”
“Wow, majina mazuri sana. Nakutegemea basi dada ufike dukani kwetu. Ila ungenipa na namba zako”
Basi Erica akataja na namba zake kwa Yule kaka, kisha alivyofika kwenye kituo chake alishuka na kuelekea nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 225

Alifika kwao na kukutana na mama yake ametoka dukani kwahiyo waliingia wote getini, mama yake alimuuliza kwa mshangao,
“Kheee Erica, leo umekuja kwa mguu bila gari? Yani mtoto wako umemuacha wazi kabisa”
“Nimechoka mama, nitamficha mtoto huyu hadi lini?”
“Ukiwaza hayo, wazo na kuwa utawezaje kueleza watu kuwa mtoto hana baba?”
“Jamani mama, kwani kuna watoto wangapi baba zao wamekufa na wanaishi?”
“Weeee usitake kufananisha watoto ambao baba zao wamekufa na mwanao, kumbuka wale baba zao wapo ila wamekufa ila mwanao hana baba kabisa yani hiyo ndio tofauti yao”
“Mama, kwakweli humu ndani mnanichanganya jamani. Mimi nishajiamulia kuishi na aibu yangu, kama huyu mtoto simtaki basi nikamuuze huko ila sio kumficha”
“Yani Erica, unamjibu mamako majibu ya shombo kiasi hiko jamani. Wewe mtoto loh! Utajibu mwenyewe wajomba zako wakija, na Yule mjomba wako aliyekuwa akikulipia ada utamuonyesha shahada uliyoipata chuo ulipomaliza walikutunuku mtoto”
Erica akaona si vyema ajibishane na mama yake, kwahiyo aliamua kwenda ndani tu.
Alicheza cheza na mwanae na kumlisha, kiukweli mwanae hakuwa mtoto msumbufu na alikuwa na afya nzuri tu kwahiyo haikumpa shida sana kwenye kumlea.
Usiku wake akawaza jambo moja, akakumbuka jinsi Rahim alivyomwambia kuwa anaomba hela za matumizi badala aombe hela za biashara, akafikiria kumuomba Rahim hela ya biashara ila akafikiria ni biashara gani sasa atafanya,
“Mmmh nitaenda kwa yule kaka kuangalia biashara ya hivyo vitu vya watoto halafu niianze hiyo biashara”
Akamsikia dada yake amerudi maana dada yake alianza tena kwenda kazini, kwahiyo alimfata kuongea nae ili kumuuliza kama ameshawahi kusikia biashara ya vitu vya watoto, alimsalimia pale na kumpa pole ya kazi kisha akamuuliza kuhusu hiyo biashara,
“Ni biashara nzuri sana umewaza mdogo wangu, ila hiyo biashara ukitaka ufanye vizuri na uheshimike, unatakiwa uwe na mtaji wa kutosha”
“Kama kiasi gani dada?”
“Kwa kuanzia sio mbaya ukiwa na milioni kumi na tano”
“Mmmh dada, mbona hela nyingi hivyo?”
“Hahaha Erica, bado hujaijua hela wewe yani milioni kumi na tani ni nyingi? Ukiwa na hela hata sio nyingi, sema ni kwavile hela hamna ndiomana”
“Nataka nimuombe baba wa mwanangu”
“Ila kama huyo mwanaume alikuwa nankupa hadi milioni tatu, nne sidhani kama milioni kumi na tano itamshinda. Tena atafurahi sana ukiwa na wazo la kufanya hivyo”
“Sawa dada, kwahiyo nimuombe milioni kumi na tano eeeh! Si utanisaidia dada kwenye hiyo biashara?”
“Nitakusaidia ndio, mimi nina rafiki zangu wengi tu wanajishughulisha na maswala ya bishara. Hata usijali nitakusaidia maana kusubiri kazi ni ngumu kwa kipindi hiki”
Erica alimshukuru pale dada yake, kisha muda wa kwenda kulala alimtafuta Rahimhewani na alimkuta ila leo hakutaka kabisa kumuanzishia mada sijui amekutana na mama yake pamoja na Salma, sijui swala la kumdanganya kumbe Salma ni mjamzito. Hakutaka kuzungumza nae swala hilo, na moja kwa moja alimueleza swala lake la kutaka biashara,
“Biashara gani utaiweza wewe?”
“Nataka biashara ya kuuza nguo za watoto na vitu vyao vya kuchezea”
“Kwahiyo unataka mzigo ukachukue China na Dubai?”
“Aaah ikiwezekana kufanya hivyo nitafanya, ila kwasasa nahitaji kuanza hiyo biashara”
“Haya, mtaji kiasi gani?”
“Milioni kumi na tano”
“Na wewe una kiasi gani?”
“Mimi sina hela ndiomana nimekwambia wewe Rahim, si unajua nimemaliza chuo nikawa kwenye uzazi, sasa hela nitatoa wapi mimi?”
“Usinitanie Erica, hela zote nilizokuwa nakupa ulizipeleka wapi?”
“Rahim jamani, hakuna hela uliyonipa bila sababu. Hel azote zilikuwa na sababu na zilienda kwenye matumizi ya hizo sababu, sasa ningekuwa nazo ningekuomba kweli?”
“Erica, kuna wanawake wangapi wanauza maandazi, vitumbua, kachori, visheti? Kuna wanawake wangapi?”
“Wengi sana”
“Na wewe kwanini usiwe katikati ya hao wanawake?”
“Jamani Rahim, kwanini lakini unanifanyia hivyo? Sijazoea kuuza vitumbua, sijui visheti, hizo biashara zinataka mazoea”
“Aliyekwambia wale wamezoea nani? Yani Erica unataka mimi nitoe milioni moja, mbili, tatu, nne hadi kumi na tano kweli? Wewe msichana una akili kichwani mwako? Kichwa chako kizima hiko? Yani nitoe milioni kumi na tano kweli? Yani unaitamka kama sijui ni hela ndogo. Erica, kweli kabisa milioni kumi na tano?”
“Jamani Rahim, unajua mimi nikifanya biashara sitakusumbua wewe kuhusu swala la mtoto maana nitakuwa najitosheleza kuliko hivi. Kumbuka ni wewe ulinishauri nifanye biashara, kweli saizi unanishangaa jamani?”
“Kama unataka kusaidia kwenye malezi ya mtoto, kwanini usitafute kazi? Au basi ungeniambia naomba hela nianze biashara ya sambusa, najua mtaji wake hata elfu hamsini haifiki, unaniambia kitu cha mtaji wa mamilioni ya pesa jamani Erica? Unahisi sina majukumu mengine ila nina majukumu ya wewe tu?”
“Rahim, sikuelewi yani sikuelewi kabisa. Kwani ni kitu gani unachotaka mimi niwe? Kwakweli Rahim hapana jamani, mtandaoni kwenyewe nikutafute mimi, kila kitu nikubembeleze kama mtoto mchanga. Na kutwa kunitoa akili yani kama duniani nipo peke yangu nisiyekuwa na akili. Nashukuru Rahim kwa hayo unayoniambia”
“Ila kwani nakwambia uongo? Erica kiukweli akili huna, hata mwanaume atakaye kuoa atajuta, wewe sio mwanamke wa kuolewa maana huna akili hata kidogo. Huwezi kuja kuniomba hela yote hiyo mimi, kwa kazi gani ninayofanya?”
“Kweli nimeamini, mwanaume akishakutumia anakuona huna thamani tena. Siku zote hukujua kama sina akili hadi umenizalisha? Na ulianzaje kuzaa na mwanamke asiye na akili? Rahim, kwasasa nimefika mwisho maana nishajibembeleza kwako hadi nimechoka”
“Kwahiyo unamaanisha nini?”
“Rahim, kuanzia leo sitakutafuta tena hewani, sitakuomba tena hela yoyote ya matumizi ya mtoto yani sitakusumbua kwa chochote kile. Mimi ni mwanamke ndio ila nitapambana na nitaishinda hii hali, nimepata aibu, nimedhalilika ila bado sijafika mwisho. Kwaheri”
Alituma ujumbe ule akitegemea kujibiwa kwa kuombwa msamaha na Rahim ila ule ujumbe haukujibiwa na ilipita saa nzima bila ujumbe kujibiwa huku Rahim akionekana hewani tu, kitendo hiko kilimuumiza sana Erica, alijikuta akimwaga machozi.
Alilia sana hadi alisikia jogoo zikiwika na kugundua kuwa kumekucha, akachukua simu yake kuangalia mida akakuta ni saa kumi alfajiri, alihisi kichwa kikimuuma kwa kulia sana ila muda huu alijifuta machozi na kusema,
“Leo ndio mwisho wa kulia, sitalia tena. Kwasasa natakiwa kuinuka na kuonyesha kuwa naweza, mtoto wangu nitamlea mwenyewe”
Erica alilala kwa muda huo huku kichwa kikimuuma sana.
 
SEHEMU YA 226

Kesho yake aliamka na kujiandaa kisha akamuacha mwanae na mama yake na kwavile nyumbani kwao kulikuwa na mdada wa kazi wa dada yake Bite, ikawa rahisi zaidi.
Erica akaenda mjingi akizunguka kwenye maofisi kadhaa kuulizia kazi, alizunguka sana siku hiyo hadi jioni alirudi kwao akiwa amechoka sana bila mafanikio yoyote.
Alichoka sana, dada yake alimuita na kumuuliza kuwa alienda wapi siku hiyo, Erica alimueleza kuwa alienda kutafuta kazi,
“Kwani huyo mwanaume alikwambiaje kuhusu hela ya biashara?”
Erica alimueleza dada yake kila kitu alichojibiwa na Rahim,
“Kwahiyo mdogo wangu umechukia sababu hajakupatia hiyo milioni kumi na tano?”
“Hapana dada, sijachukia sababu hiyo. Ila nimechukizwa na majibu anayonipa, kwani kutoa hela ni lazima? Si unasema tu sina, sasa majibu aliyonipa dada ndio yaliyoniumiza sana”
Erica aliamua kumuonyesha dada yake jumbe zote alizokuwa akijibiwa na Rahim, kiukweli hata Bite alianza kujiwa na huruma na mdogo wake, alijaribu kuhisi ni wapi anakopitia ndiomana kakosa hata uelekeo na kuamka tu kuanza kutafuta kazi kwa kuulizia tu maana alikuwa hana muelekeo.
“Sikia Erica, umeshawahi kufanya field kwa shemeji yako James, kwanini usiende tena huko”
“Mmmh dada, kwa shemeji tena!”
“Usiogope Erica, tumeshajua kila kitu kwahiyo hakuna tatizo lolote. Mwanzoni tulikuwa hatujui, najua James hawezi kukataa wewe usifanye kazi kwenye ofisi yake ila vilevile hawezi kukufanyia tena vitendo vya ajabu wakati ukweli tunaujua kama kukulazimisha kuwa akurudishe nyumbani, hawezi tena maana kipindi kile ni mimi nilikuwa namtetea. Ila sasa swala la kuongea nae akuweke kazini mimi silifanyi kwakweli maana huyo James ananitia kichefuchefu tu”
Erica aliongea ongea na dada yake na kwenda kulala, ila alishafikiria jambo kuwa shemeji yake akifika kumuomba msamaha dada yake basi ndio siku hiyo aongee nae kuhusu swala la yeye kwenda kazini kwake.
 
SEHEMU YA 227

Siku hiyo alikuwa nyumbani kwao hana hata habari, alishangaa kumuona shemeji yake James akifika, na kujua lazima atakuwa anataka kuomba msamaha vizuri, na ni kweli kabisa James alikuwa amekuja kwa lengo la kumuomba mkewe msamaha, James akamwambia Erica,
“Nenda nje kaone gari niliyomnunulia dada yako, sijui ataipenda? Hebu kaiangalie kwanza”
Erica alitoka nje na kuiangalia ile gari, kwa hakika ilikuwa nzuri sana,
“Mmmh jamani, dada alikuwa akitamani sana kupata gari ya mtindo huu. Sasa kaipata, mmmh kweli shemeji ana pesa, dada yangu amsamehe tu”
Muda kidogo Bite naye alifika nyumbani kwao, na kupaki gari yake, akashuka na kumuangalia mdogo wake akishangaa ile gari kisha akamuuliza,
“Gari mpya nzuri hii ya nani?”
“Umeipenda dada?”
“Nimeipenda ndio, ila hata nikiipenda kazi bure. Kwasasa natakiwa kuwa mpole tu, hizi gari nzuri nitabaki kuziangalia kwa macho”
Basi Erica akampokea dada yake mkoba na kwenda nae ndani, ila Bite alipomuona James alionyesha kuchukizwa na hata hakumsalimia na kupitiliza ndani ila Erica aliongea na shemeji yake kwa ishara kuwa dada yake amelipenda sana lile gari.
James akainuka na kumwambia Erica asubiri kisha aliporudi alikuwa na boksi mkononi, akalishusha chini, ilikuwa ni keki.
Erica akamuita dada yake kwa furaha, Bite alienda tu pale sababu mdogo wake kamuita, kisha Erica alifungua lile boksi, akashangaa kuona keki imeandika ‘Happy birthday Angel’ kwakweli Erica alijihisi kutokwa na machozi maana kweli ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mwanae ila hakutaka kuikumbuka kwavile hakuwa na chochote cha kufanya kwaajili ya mtoto wake ila shemeji yake alimpa mshtukizo wa hali ya juu, Erica alimuangalia na kumuuliza,
“Umejuaje shemeji?”
“Nilimuuliza dada mkubwa Mage kubwa ulijifungua lini na mwanao anaitwa nani, nikaona leo siku ya kuzaliwa ya mtoto huyu iwe ni siku ya furaha kwetu. Ndiomana nikamletea na mke wangu zawadi ya gari alilokuwa analitamani kwa siku nyingi sana, (Akamuangalia mkewe na kumwambia) Najua mke wangu huwezi kukataa zawadi yangu kwenye siku muhimu kama hii ya kuzaliwa kwa malaika kwenye familia yenu. Naomba nikiri wazi nakupenda mke wangu Bite na familia yako ni familia yangu. (Kisha akatoa kadi ya gari na funguo kimkabidhi Bite)”
Bite alijikuta akimsogelea mume wake na kumkumbatia huku akitoa machozi maana hakutegemea kama kitu kile kingempa furaha kiasi kile mdogo wake ukizingatia kwa siku za karibuni tu alionekana akiwa na masononeko mkubwa.
Walikata keki na kufurahi kwa pamoja, kisha James akawaomba kuwa waende mahali wakapate chakula cha usiku, ila Erica alikataa kwavile alitaka shemeji yake na dada yake wapate muda wa kuzungumza.
Kisha Bite akajiandaa na kutoka na mumewe na walitumia gari lile jipya ambalo mumewe alifika nalo kama zawadi ya Bite.
 
SEHEMU YA 228

Erica alitulia mwenyewe na watoto sebleni maana mama yake hakuwepo ila baada ya muda mfupi alirudi na kuulizia kuwa Bite yuko wapi,
“Ametoka”
“Ametoka muda huu? Mbona gari yake ipo nje?”
Erica alimueleza mama yake kuhusu kilichotokea kuwa Bite kapatana na mume wake,
“Nilijua tu, yani mambo ya mapenzi sio ya kuingilia kabisa. Unaweza kusema hadi koo likukauke ila unashangaa hao washarudiana”
“Ila mama kwani hukupenda warudiane?”
“Nisipende kwa lipi? Unafikiri nafurahi kuona watoto wangu ndoa zinawashinda? Ila nilitaka ampe adabu kidogo Yule mwanaume maana hanta adabu jamani, ningekuwa mimi hata nisingekubali kirahisi hivyo. Ila mapenzi mmmh!”
Baada ya usiku kuingia vizuri Bite na James walirudi na kujiandaa kwaajili ya kurudi kwao, mama yao akamuuliza Bite,
“Usiku huu?”
“Ndio mama, kesho si kazini”
“Mmmh haya bhana, mapenzi siyaingilii”
Basi Bite alijiandaa kisha kumuaga mama yao na kuanza safari, na waliondoka na ile gari mpya, kwahiyo gari ya mwanzo ya Bite iliachwa pale pale nyumbani.
Erica alikuwa chumbani kwake kwa lengo la kulala, ila akafikiria sana, akatamani apate mwanaume ambaye hata akifanya makosa anajua jinsi ya kuomba msamaha ila sio aina ya Rahim ambaye hata hajali chochote.
Akawaza kuhusu Bahati kuwa ndiye mwanaume pekee aliyeonekana kumpenda sana, ila alishangazwa na hali ya Bahati ya kutokumtafuta toka siku ile wakati sio kawaida ya Bahati, lazima angeenda kuendelea kumuomba msamaha au angempigia simu ila ni kimya kabisa.
Aliamua yeye kumpigia simu ila hakuipata namba ya Bahati hewani, jmbo lile lilimfanya ajihisi vibaya sana kwani kwa muda huo alihisi kuhitaji sana uwepo wa Bahati.
Basi wiki nzima alikuwa akifanya kazi ya kumtafuta Bahati hewani ila hakumpata na kumfanya azidi kukosa amani, akaona ni vyema aende anapoishi Bahati ili ajue nini kimempata Bahati maana sio kawaida kabisa.
 
SEHEMU YA 229

Siku hiyo akajiandaa vizuri kabisa, kisha kumuaga mama yake kuwa kuna mahali anaenda ila hakumwambia ukweli kama anaenda nyumbani kwa Bahati, alimuacha mtoto wake pale na kuondoka.
Alifika hadi mahali ambako Bahati alikuwa amepanga, alikuta baadhi ya majirani, akawasalimia na kwenda kwenye chumba cha Bahati ila alikuta kufuri kwahiyo Bahati hakuwepo. Aliamua kumuuliza jirani mmoja wa Bahati, huyo jirani alikuwa ni mdada.
“Dada, samahani eti Bahati yuko wapi?”
“Kheee Bahati, yupo kuoa. Ana shughuli leo”
“Kuoa!”
Erica alishtuka sana na kuuliza kwa umakini ila Yule jirani alimuhakikishia Erica kuwa Bahati yupo kuoa,
“Kwani hujui?”
“Sijui”
“Ngoja nikupeleke anapofungia ndoa”
Basi Erica akaanza kuongozana na Yule mwanamke kuelekea mahali ambako Bahati alikuwa anaoa, walifika kwenye nyumba ambako kulikuwa na watu wengi na shamra shamra, kitu kilichodhihirisha kuwa kuna shughuli.
Muda kidogo maharusi walikuwa wanatoka ndani yani ndoa ilishafungwa, bado Erica alikuwa haamini na kuangalia kwa makini hao maharusi wanaotoka ndani.
Alishangaa kuona Bahati akiwa ndiyo bwana harusi, akiwa ameambatana na binti mmoja ambaye ndio bibi harusi, yani Erica alihisi kizunguzungu muda huo.


Basi Erica akaanza kuongozana na Yule mwanamke kuelekea mahali ambako Bahati alikuwa anaoa, walifika kwenye nyumba ambako kulikuwa na watu wengi na shamra shamra, kitu kilichodhihirisha kuwa kuna shughuli.
Muda kidogo maharusi walikuwa wanatoka ndani yani ndoa ilishafungwa, bado Erica alikuwa haamini na kuangalia kwa makini hao maharusi wanaotoka ndani.
Alishangaa kuona Bahati akiwa ndiyo bwana harusi, akiwa ameambatana na binti mmoja ambaye ndio bibi harusi, yani Erica alihisi kizunguzungu muda huo.
Yule mwanamke aliyempeleka Erica pale alimuona alivyokuwa anapepesuka, ikabidi amdake na kwenda nae mahali chini ya mti na kumkalisha, kisha kumuuliza
“Nini tatizo dada, umechanganyikiwa gafla”
“Acha tu dada yangu”
“Pole, au Bahati alikuwa ni mwanaume wako?”
“Hapana, ila sijapenda vile hajanipa taarifa”
“Ila usimlaumu dada, hii ndoa yenyewe imekuwa haraka haraka sana hata sisi tumeshangaa ila kwavile hatukumjua msichana wake labda pengine alikuwa nae kitambo ila ndoa ya gafla sana hii”
Erica aliomba asaidiwe kuinuka aondoke, kisha Yule mwanamke akamsaidia na kumuitia bodaboda ambayo Erica alipanda na kuondoka.
Yule mwanamke alionekana kusikitika sana ni kweli Erica alimdanganya ila yeye alihisi jambo kuwa pengine Bahati alikuwa na mahusiano na msichana Yule, alikuja jirani mwingine na kumuelezea jinsi Yule msichana alivyoondoka pale,
“Kheee kwani wewe humjui Yule?”
“Simjui, ni nani kwani?”
“Yule msichana amewahi kuja mara moja au mbili pale nyumbani, na ukiongea na Bahati mar azote alisema ni jinsi gani alimpenda Yule msichana hata nashangaa imekuwaje kuoa msichana mwingine. Mmmh mapenzi haya!”
“Mmmh kwa mtindo huo hata usiyalaumu mapenzi, sidhani kama Bahati alikuwa akimuongopea Yule msichana ila baba yake Nasma huyu binti anayeolewa na Bahati jamani baba ni mchawi Yule hakuna mfano”
Walijikuta wakiongelea tukio lile lile la Erica kutaka kuzimia na jinsi ndoa ya Bahati ilivyofanywa kwa haraka sana.
 
SEHEMU YA 230

Erica alirudi nyumbani kwao, na hata hakuongea na mtu kwani mwanae muda huo alikuwa chumbani na bibi yake, basi Erica aliingia chumbani kwake na kujifungia mlango kisha kulia sana, yani alilia ila alikumbuka maneno yake kuwa hatolia tena ila bado machozi yalimtoka,
“Hivi Bahati kweli ndio ulikuwa unasema unanipenda sana na hakuna mwanamke unayemuona zaidi yangu kweli? Umeamua kuoa Bahati, ama kweli mimi ni fungu la kukosa jamani. Inamaana Yule msichana kaanza nae muda mrefu sana, huwezi kuniambia ndani ya wiki mbili tu umfahamu mtu mpaka mfikie kuoana, yani lazima Yule msichana anajuana nae kwa siku nyingi sana. Siamini kama Bahati kanisaliti jamani”
Erica aliumia sana moyo wake na kukosa raha kabisa ila hakuwa na la kufanya kwa wakati huo, akakumbuka jinsi alivyokuwa akipewa hela na Rahim na jinsi alivyokuwa akimpa hela Bahati ila leo hii Rahim kamkosa na Bahati kamkosa pia, alikosa raha kabisa na kujiona hana thamani.
Mama yake alimuhisi kuwa Erica amerudi na kumuita, ilibidi Erica ajifute machozi yote na kwenda kumsikiliza mama yake,
“Kheee yani unarudi kimya kimya husemi jamani, na utafute msichana wa kazi sasa maana mtoto utakuwa unamuachia nani? Utafute msichana wa kazi”
“Sawa mama”
“Na mbona macho yamekuvimba? Ulipotoka huko umepigwa au nini?”
“Hamna kitu mama”
“Unajua wewe mtoto utachanganyikiwa jamani, siku hizi huendi kanisani yani upo upo tu. Huwa kuna mahubiri kwenye redio, basi mara moja moja hata uwe unawasha na kusikiliza mahubiri”
“Sina redio mimi”
“Hata simu zina redio, ila ngoja nitakupa maana mimi nina redio mbili. Uwe unasikiliza na mahubiri uweze kukaa vizuri na moyo wako”
Yale maneno ya mama yake hayakumuingia wala nini, badala yake alimchukua mwanae na kuingia nae chumbani ila muda huu hakuweza kuendelea kulia maana mtoto wake alipomuona akilia alilia pia, kwahiyo alijizuia asilia mbele ya mtoto wake badala yake alicheza nae tu.
Usiku ulipofika alijaribu kutafuta usingizi ila kiukweli usingizi aliukosa kabisa huku akijihisi ni msichana mwenye mkosi katika maisha yake, kwa muda ule alitamani sana kupata hata mtu wa kumbembeleza kwenye simu, akawaza sana kuwa afanye nini, akafikiria watu aliokuwa kwenye mahusiano nao, Rahim ndio huyo kageuka mbogo, Bahati ndio huyo kaoa, kusema Babuu asingeweza tena kuweka ukaribu nae kwani kiukweli ni shemeji ingawa hajamuweka wazi, hapo wazo likamjia kumtafuta Erick tu maana kwa muda huo hakuona mwingine wa kumliwaza kwa kumwambia maneno matamu.
Akainuka na kuchukua ile barua ya Erick kisha kuangalia namba zake na kumpigia, ila simu iliita na kukata, akapiga tena simu iliita na kukata, akahisi kuwa huenda Erick amelala kwa muda huo.
Akaiweka simu pembeni huku akijaribu kutafuta usingizi ila aligalagala kitandani kwa muda wote na wala hakupata usingizi kwani kiukweli alikuwa na mawazo sana na ndiyo yalimfanya asiweze kupata usingizi.
Kwenye mida ya saa kumi alfajiri, alisikia simu yake ikiita, aliichukua na kuangalia mpigaji akaona ni Erick, alitabasamu sana akaipokea na kuanza kuongea nae, ila akagundua Erick alikuwa amelewa na kufanya awe na maneno mengi sana,
“Erick, mbona umelewa hivyo?”
“Wewe ni Erica?”
“Ndio, mimi ni Erica”
“Wewe ndio unayenipa sababu za kulewa Erica, hivi unajua ni jinsi gani nakupenda? Kweli Erica siku zote hizo ndio umenitafuta leo? Nimeona namba hata sijajua ni wewe nimepiga tu kumbe ni wewe kipenzi change, nakupenda sana Erica”
“Ila umelewa Erick”
“Ndio nimelewa ila nimelewa kwaajili yako”
Na ikawa kimya ilionyesha kama mtu anakoroma kwamaana hiyo Erick alilala na simu kwavile alikuwa amelewa, ilibidi Erica akate ile simu, ila alitabasamu kuona kumbe Erick bado anamkumbuka, na muda huo akalala na tabasamu usoni huku akisahau yote ambayo yametokea mbele yake.
itaendelea
 
SEHEMU YA 224

Gari lilifika na alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati anatoka akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani Erica alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa mgongoni amelala.
“Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?”
“Wa dada yangu”
“Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?”
“Kaenda kazini”
“Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba changa basi inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki”
Swala la kuambiwa Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica.
Muda huo ilikuwa kama Erica kapigwa na bumbuwazi maana alisimama tu bila kwenda mbele wala kurudi nyuma, ila Mrs.Peter alikuwa ametangulia mbele akijua Salma anamfata nyuma ila muda huo Salma alikuwa akisimama palepale na alionekana akimuangalia Erica kwa chuki ya waziwazi, kitu ambacho kilimshangaza hata Erica mwenyewe, na kumuuliza,
“Mbona unaniangalia hivyo?”
“Utaacha lini uongo wewe mwanamke? Eti mtoto wa dada yangu (Huku akibana pua, na kuendelea kusema). Mtoto wako mwenyewe unasingizia wa dada yako, kwani ni kipi unachohitaji kwa huyu mama?”
Erica alimuangalia huyu Salma na kutamani hata kumpa tusi ila tu swala la kutukana halikuwepo kwenye kinywa chake, muda kidogo mwanae akaamka na kuanza kulia, ikabidi Erica amfunue na kumgeuzia kwa mbele, muda huo Salma alikuwa akiondoka kumfata Mrs.Peter ila Erica akamshika vizuri mkono Salma na kumrudisha nyuma kisha akamwambia,
“Mwangalie vizuri huyu mtoto ndio utaelewa ni kwanini sikusema wa kwangu.”
Kisha Erica akaondoka ila alimuacha Salma akiwa na maswali mengi sana, aliendelea kumfata Mrs.Peter ila kiukweli alikosa raha.

Erica alipotoka pale hospitali hata hakutamani kuita gari ya kukodi, na moja kwa moja alielekea kupanda daladala maana alijiona kama ni kudhalilika tayari ameshadhalilika vya kutosha, aliamua kuacha tu jamii yake ijue kuwa ana mtoto, hakuwa na sababu tena ya kumficha mtoto wake.
Akiwa kwenye daladala, alikaa siti ya nyuma ambako kulikuwa na wamama wawili wamekaa kwa pembeni yake wakiongea, yale maongezi yao aliyasikia yote na yalionyesha kuvuta sana hisia zake,
“Yani mwenzangu, kipindi kile natoka na mume wa mtu halafu mkewe hata simjui ila cha kushangaza nilikutana nae njiani si nikagombana nae, yani jamani mapenzi bhana yana wivu ambao mwizi humjui ila unashangaa unagombana nae. Niligombana na Yule mkewe hadi mumewe akaja kutuamulia ndio hapo nikajua kumbe Yule ndiye mkewe, na ubaya hakuniambia kuwa ameoa weee balaa lilizuka ila nikaamua kuwa mpole na kujitoa”
“Ila mapenzi ndio yalivyo, yani mnaweza kuwa mnatoka na mtu mmoja hamjuani ila unashangaa kuna mambo gafla tu mnachukiana jamani, sijui wale wanaoishi wake wawili au watatu wanajisikiaje ndani”
“Washazoea wale, ila katika ujana wangu nimejifunza jambo. Hawa wanaume ni bora kuwachuna tu, ukijiendekeza kuwapenda utalia jamani, ni waongo balaa”
“Hahaha, ila wakweli wapo bhana, sio wote waongo kumbuka hata na wao wanalalamika kuwa wanawake ni waongo”
“Ndio, ila wao wamezidi”
Basi kituo kilichofata wale wanawake walishuka na kumuacha Erica akitamani hata kuwauliza baadhi ya maswali ila hakuweza maana hakuwazoea.
Ila waliposhuka tu kule nyuma alipanda mkaka na kukaa karibu na Erica, Yule mkaka alimtazama Erica na kumtazama mtoto wa Erica kisha akamwambia,
“Dada, hongera sana una mtoto mzuri. Halafu ana tabasamu vizuri”
“Asante”
“Mmmmh sijaanza hata kukusalimia maana nilivutiwa na uzuri wa huyu mtoto, hali yako lakini”
“Nzuri, ila usijali”
“Ngoja nijitambulishe kidogo, dada mimi naitwa Moses. Nina duka langu zuri sana la nguo za watoto wakike na wa kiume. Naomba uje dukani kwetu hata mara moja uone huduma zetu, business card yangu hii”
Akamkabidhi Erica, naye Erica akapokea huku akisikiliza maelekezo mengine toka kwa Yule kaka,
“Tafadhali dada, naomba ufike. Nimevutiwa sana na mwanao. Najua atapendeza sana akivaa nguo zetu zile. Ila unaitwa nani, na mwanao anaitwa nani?”
“Mimi naitwa Erica, na mwanangu anaitwa Angel”
“Wow, majina mazuri sana. Nakutegemea basi dada ufike dukani kwetu. Ila ungenipa na namba zako”
Basi Erica akataja na namba zake kwa Yule kaka, kisha alivyofika kwenye kituo chake alishuka na kuelekea nyumbani kwao.

Ericaaaaaaaa hata hazugagi [emoji1438]‍♀️[emoji1438]‍♀️[emoji1438]‍♀️[emoji1438]‍♀️
 
SEHEMU YA 231



Palipokucha aliamka na kufanya shughuli zake zingine ila kwenye mchana hivi akapigiwa simu, kuangalia ni Erick alikuwa akimpigia, Erica alipokea ile simu huku akitabasamu,
“Hivi jana nilikuwa naongea na wewe kweli Erica au mtu gani?”
“Ni mimi mwenyewe, umenisahau?”
“Siwezi kukusahau Erica, ila umejua kuniumiza wewe mwanamke kwanini lakini? Umepata ujumbe wangu muda mrefu tu ila umenikaushia, kwanini ulinichunia Erica?”
“Nisamehe Erick?”
“Hunipendi tena?”
“Hapana, bado nakupenda”
“Kama wanipenda, kwanini unafanya niumie moyo Erica? Nilirudi nchini ila sikuweza kukaa sana na kuamua kuja tena Kusini maana nilihisi hutaki hata kuniona”
Erica alijaribu kuongea na Erick na walionekana kupatana sana ila katika maongezi yale Erica hakuthubutu kumwambia Erick kuwa ana mtoto maana hakujua angechukulia vipi swala hilo ukizingatia hakutaka kuumia kabisa.
Kwahiyo siku ya leo ilikuwa ni siku ya tabasamu zito kwa Erica hata mama yake aliweza kugundua ni jinsi gani binti yake anavyoonyesha furaha.
Jioni ilipofika alipigiwa simu na shemeji yake James,
“Erica, nimeambiwa na dada yako kuwa unahitaji kazi. NImelifanyia kazi swala hilo, hivyobasi naomba ujiandae na wiki ijayo uje kuanza kazi”
“Shemeji unasema kweli?”
“Ndio Erica, kuna muda nimetaniana na wewe? Njoo kazini na utafurahi na moyo wako, ni mengi kanieleza dada yako nimeingiwa na huruma sana ila najua utakapokuwa kazini itakuwa rahisi kuendesha maisha yako. Naomba wiki ijayo uje kuanza”
Erica alimshukuru sana shemeji yake kwa uamuzi ule maana kwake ilikuwa ni faraja sana ukizingatia katika maisha yake hiko kilikuwa ni kipindi kigumu sana.
Alipomaliza alienda kumueleza mama yake kuwa amepata kazi kwenye ofisi ya shemeji yake, alijua mama yake angefurahi sana ila ilikuwa kinyuma.
“Kheee mama, mbona hujafurahi?”
“Erica, unaweza ukahisi labda mama yako sikupendi au nini na nini ila nakupenda sana, unajua nakupenda. Na yote ninayokwambia huwa nakwambia kwa upendo, najua kwasasa una shida sana na kazi ila kazi ya kufanya kwa shemeji yako sijaipenda”
“Jamani mama, ila shemeji kabadilika”
“Wewe wasema hivyo, ila wanaume nawajua vizuri sana kushinda hata wewe na ndugu zako mnavyowajua. Ulinipa habari kuwa James alimletea mwanao keki, nilitabasamu tu eti anaonyesha kujali familia ya mke wake. Wapo wa kujali familia ya mke ila sio kwa James, yani haaminiki hata kidogo. Gari ya mwanzo ya dada yako imeachwa hapa nje, nina uhakika shemeji yako atakupa wewe. Na kazi ndio hivyo kakupa, yani James ana akili kupita tunavyofikiria yani lazima atakusumbua tu halafu sitaki ugombane na dada yako”
“Jamani mama, haiwezi kuwa hivyo”
“Haya, ila mimi ni mkubwa nimetangulia kuliona jua. Kwavile umeamua sawa, mimi nakutakia kila la kheri ila uwe makini sana”
“Usijali mama kuhusu umakini”
“Uliniambia hivyo hivyo mwanzo ila ukamaliza degree na degree ya mtoto, kuwa makini. Mwanaume sio ndugu yako, yani muone kama samba na usipende kuwa nae karibu, sijui shemeji itakutokea puani”
Erica alimsikiliza mama yake ila alimuona mara nyingine mama yake anaongea ongea tu ukizingatia ni yeye mwenyewe ndiye kafanya hata atafute kazi sababu ya kumsema sana kuwa anakaa nyumbani hana shughuli yoyote.
Mama yake Erica aliinuka na kumletea Erica redio ambapo alimwambia awe anasikiliza mara moja moja hata mahubiri maana akili yake ilionekana kulala sana.
 
SEHEMU YA 232


Kiukweli Erica toka apewe na mama yake redio hakuwahi kusikiliza mahubiri wala nini na mara nyingi alikuwa akiongea na Erick tu.
Siku ilifika ya Erica kwenda kazini kwahiyo akaenda kazini, siku hizo alikuwa na tabasamu usoni ukizingatia mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Erick, na mara nyingi aliwasiliana nae mtoto akiwa amelala kwahiyo hakumweka wazi kuwa ana mtoto kwani hakujua Erick angechukulia vipi swala la yeye kuwa na mtoto.
Alifika ofisini na shemeji yake alimpokea na kumuonyesha kazi ya kufanya ambapo alimuweka kwenye mapokezi ya kuingia kwenye ofisi yake,
“Yani mtu yeyote asije kuniona bila kupitia kwako Erica, utafanya kazi zingine ila utahakikisha hilo. Sitaki watu wafanye mazoea ya kuingia ofisini kwangu kama chooni”
“Sawa bosi nimeelewa”
“Aaah usiniite bosi bhana”
“Sasa nitakuita shemeji wakati tupo kazini? Lazima nikupe heshima yako, wewe ni bosi wangu”
“Niite James itapendeza zaidi”
Kisha James akaelekea ofisini kwake na kumuacha Erica pale azoee mazingira. Alifanya kazi zake na muda ulipofika tu alibeba mkoba wake na kuondoka kwani hakutaka ile tabia ya kuagana na shemeji yake ukizingatia matendo ya shemeji yake tayari alishayajua.
Erica alienda kupanda daladala moja kwa moja, ila kabla hajapanda alishikwa bega, kugeuka alikutana na Dora na alionyesha kuwa mpole sana,
“Erica, mambo”
“Safi”
“Erica, nihurumie mwenzio angalia ninavyopata shida. Sikupenda iwe hivi ndiomana nakuomba msamaha, kwanza kabisa napenda tuwe marafiki kama zamani hata kama sitaolewa tena na kaka yako ila nahitaji tuwe marafiki.”
“Dora, sitaki tena urafiki na wewe”
“Sikia Erica, hakuna binadamu aliyemkamilifu duniani, kila mtu hajakamilika na kila mtu ana mapungufu sake. Nakubali kuwa nilikuwa malaya, nishatoa mimba nyingi, ila nimebadilika sasa, hivi unadhani wewe ukihukumiwa kwa makosa ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma utajisikiaje? Erica, kuna mahali nafanya kazi ili siku ziende tu ila kiukweli sina raha, toka lile songombingo la nyumbani kwenu. Kakako kaniambia kuwa yeye hana matatizo ila anasema kwamba uhuru wake umeubeba wewe yani wewe ndiye mwenye maamuzi ya mimi kuendelea na kaka yako au la. Erica hata kama hutaki mimi niwe na kaka yako ila naomba basi tuwe karibu, tuwe marafiki, nimejirekebisha Erica na ninakiri shoga yangu”
Erica alimuangalia Dora ambaye aliongea kama mtu kweli ila kwavile Erica alishajiwekea kutokupatana tena na Dora, ikabidi aachane nae kisha yeye kuondoka zake. Akaend kupanda daladala na kuondoka.
 
SEHEMU YA 233


Alifika nyumbani kwao akiwa na uchovu sana ambapo mama yake alimuuliza kuwa hiyo siku ya kwanza kazini aliionaje,
“Aaah mama ipo vizuri kabisa, yani pale ofisini wamenipokea vizuri ukizingatia niliwahi kuwa pale kabla”
“Hivi na mahubiri unasikiliza kweli?”
“Nasikiliza mama”
“Haya kama unasikiliza”
Erica alimuitikia mama yake ili kiukweli hakuwahi kusikiliza toka mama yake ampe redio, alienda kuoga na kula chakula cha usiku.
Muda anaenda kulala siku hiyo akaona ni vyema asikilize hayo mahubiri anayoyasema mama yake, akafungua kituo alichoambiwa na mama yake na kukuta muhubiri akiendelea na mahubiri,
“Unajua mara nyingine ufanikiwi kumbe sababu ya kufanya mambo mabaya kwa wenzio, hakuna kitu chema kama kusamehe ndiomana maandiko yanasema samehe saba mara sabini, tunatakiwa kuwa watu wa misamaha. Tusamehe ili kuachilia baraka zetu, swala la kukaa na kinyongo sio zuri”
Erica alihisi usingizi na kuzima redio ila yale mahubiri yalimuingia vilivyo,
“Kwa maana hiyo sina baraka sababu sijamsamehe Dora, labda sababu namuwekea vikwazo Dora kuolewa na kaka yangu ndiomana na kwangu kumetokea vikwazo. Inabidi nimsamehe tu, potelea mbali aliyonifanyia ila natakiwa kumsamehe”
Alijiambia na moyo wake kuwa atakapokutana tena na Dora atamsamehe.

Kesho yake alienda kazini, ila James alimuigta kuzungumza naye,
“Erica, kwanini jana hujaja kuniaga?”
“Sikujua kama napaswa kukuaga, nilipoona wengine wameondoka basi na mimi nikaunganisha nao”
“Erica, mimi ni shemeji yako na wakati huo huo mimi ni bosi wako. Nimekuweka katika kitengo cha karibu na mimi kwa makusudi kabisa, kwanza nakuamini halafu sitaki wafanyakazi wengine wakusumbue sumbue. Kitengo ulichokuwepo hutakiwi kuondoka bila ya kuniaga, kwani kuna umuhimu mkubwa wa kufanya hivyo ili hata muda huo najua kuwa umeondoka na nitakabiliana vipi na watakaokuja kuniona. Usifanye tena hivyo Erica”
“Sawa bosi nimesikia”
“Usiniite bosi Erica, niite tu James. Na vipi ulitumia usafiri gani?”
“Nimetumia daladala”
“Sasa kwanini utumie daladala wakati gari ya dada yako ipo tu pale kwenu imekaa, ngoja kesho nikuletee funguo na uanze kuiendesha”
Erica alimshukuru shemeji yake pale kisha kuendelea na kazi zake za pale ofisini, kwenye mida ya mchana walifika watu wawili wakiomba ruhusa ya kuongea na bosi wake,
“Mnahitaji kuongea nae nini?”
“Kampuni yetu kuna bidhaa inajihusisha nazo, kwahiyo tulihitaji kuongea nae ili atupe ruhusa tuweze kuzungumza na wafanyakazi wake”
Erica aliinuka na kwenda kuwaombea ruhusa kwa bosi wake ambapo aliruhusu aingie mmoja wapo, kwahiyo Yule mwingine alibaki pale na Erica, mara kidogo alifika na mwenzao mwingine, Yule akamsalimia Erica, Erica alimtazama na kumuona ni Dora, kumbe alikuwa miongoni mwa wale watu kwenye ile kampuni, Dora alipomuona Erica tu akaona sasa hapa itakuwa shida kupata nafasi maana alijua ni jinsi gani Erica alimchukia.
Dora kabla ya salamu alimfata Erica na kumwambia,
“Erica nakuomba jusitukatalie hili sababu na mimi nipo, Erica ni kazi hii wenzio yani hapa ndio pananifanya niendelee kuishi, nakuomba Erica”
Dora akapiga na magoti na kumfanya Yule mwenzie aliyeambatana nae amshangae, Erica alisimama na kumshika mkono Dora akimsimamisha kisha akamkumbatia na kumwambia,
“Nishakusamehe, huna sababu ya kupiga magoti kwangu”
Dora alionekana kufurahi sana, hata Yule mwenzao alipotoa kwa bosi alishangaa kumuona Dora akifurahi sana ingawa yeye akutoka na furaha, Erica akamuuliza imekuwaje,
“Bosi kasema hakuna nafasi ya kuongea na watu wake”
“Aaah msijali, nitaongea nae na nitawapigia simu”
Kwahiyo wakamuachia Erica namba za simu na kuagana nae pale.
Muda wa kuondoka, Erica alienda kumuaga shemeji yake na kumwambia kuhusu wale watu kuja kuzungumza nao,
“Sasa Erica mimi nimeshindwa kupanga ratiba, labda upange wewe”
“Nitapanga basi bosi”
“Aaah Erica jamani, sitaki unite bosi. Acha hilo jina tafadhali”
“Sawa”
Kisha James akampa Erica alfu ishirini kwaajili ya nauli ya siku hiyo, Erica alikataa ila James alimsisitiza achukue kwahiyo alichukua na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 234


Alirudi nyumbani kwao, akamkuta mama yake na kumsalimia,
“Ila leo umewahi kurudi?”
“Nimerudi na bodaboda mama”
“Yani kuanza kazi tu ushaanza kukodi pikipiki za kukurudisha nyumbani!”
“Hapana mama, shemeji alinipa nauli ndio nikapanda pikipiki”
“Mmmh ameanza kukupa nauli? Sisemi kwa ubaya Erica, ila kuwa makini sana na shemeji yako”
“Nimekuelewa mama”
Erica aliingia chumbani kwake ila hakudhania kama kuna tatizo litatokea baina yake na shemeji yake kwani kwa kipindi hiko hakutaka kujihusisha na maswala ya mapenzi kabisa, aliona kuzungumza na Erick pekee inatosha, na siku hiyo kabla ya kulala alimtafuta hewani na kuzungumza nae,
“Tena Erica, kuna kitu nilikuwa nawaza. Kwakweli natamani sana kuwa na mtoto, usingetoa ile mimba yangu saivi mtoto wetu angekuwa mkubwa sana. Basi Erica naomba nitakaporudi tuzae, usitoe tena mimba yangu”
“Mmmh kabla ya ndoa hapana kwakweli”
“Nitakuoa Erica, nakupenda ujue ila tuzae kwanza. Nakuomba tafadhali”
“Tutajadiliana hilo, usijali”
Walijadiliana mambo mbalimbali kisha kuagana usiku mwema na Erica kulala, hakutaka kumwambia ukweli Erick kuwa yeye tayari ana mtoto, swala hilo lilimuuma ila hakujua ni jinsi gani angemwambia Erick.
Kesho yake alienda kazini kama kawaida, na shemeji yake kumkabidhi funguo za lile gari la dada yake kuwa awe anaenda na gari lile ofisini, ila Erica alikuwa akienda bila gari kwani alijua angezua maswali mengi sana kwa mama yake. Ile wiki yote aliimaliza kwa kutokwenda na gari kabisa, na kila siku alimpa visingizio shemeji yake vya kwanini hakwenda na gari.

Ilikuwa ni Jumamosi asubuhi, Erica akapigiwa simu na namba ngeni akapokea, Yule mpigaji alijitambulisha kuwa ni Moses na kuanza kumkumbusha Erica walipokutana hadi Erica akakumbuka.
“Naomba leo uje ofisini kwetu”
“Ila bado sina pesa ya kuja kununulia nguo au vifaa vya kuchezea mtoto”
“Hapana, sikuiti kwaajili ya kununua nguo au vifaa ila kuna jambo lingine la muhimu sana nakuitia, naomba uje na mtoto wako”
Erica aliongea na Yule mtu na kukubaliana nae kuwa atakwenda, baada ya kukata simu aliwaza kuwa atatokaje pale kwao na mtoto wake? Wakati anawaza hayo, mama yake alimuita,
“Erica, wiki nzima umefanya nishinde nyumbani hapa na mtoto, ni wakati sasa wa kutafuta mdada wa kazi. Leo natoka, naenda kukutana na wamama wenzangu maana wiki yote sijaonana nao”
Erica alimuitikia haraka mama yake kwani alijua akitoka tu, itakuwa rahisi kwake kutoka pia.
Na kweli mama yake alivyotoka tu, alijiandaa na kumuandaa mtoto wake kisha akaita gari ya kukodi na kuondoka zake, alitamani aondoke na gari ya dada yake ila aliwaza mtoto atamuwekaje kwenye gari ukizingatia hakuwa na kiti cha kupanda na mtoto kwenye gari, halafu mtoto mwenyewe alikuwa na utundu wa kimya kimya.
Erica alifika kwenye duka la kina Moses na kushangaa duka lilikuwa kubwa sana, na alipofika tu Moses alimsalimia na kumdaka mtoto wa Erica huku akiita wenzie,
“Njooni mmuone sasa mtoto huyu alivyo mzuri”
Wenzie wote walifika na kumbeba beba Angel huku wakimbusu na kusifia kuwa ni mzuri sana, Moses alianza kuongea na Erica,
“Kwanza kabisa hongera kwa kupata mtoto mzuri hivi, yani ndoto zetu tulihitaji kupata mtoto awe balozi wa bidhaa zetu na siku niliyokuona na mtoto wako nilivutiwa nae sana, nimekuja kuwasilisha swala hilo kwa wenzangu waliafikiana na mimi na ndio leo naona kila mmoja hana la kusema kwa uzuri wa mtoto huyu. Sasa upo tayari tusaini mikataba mtoto wako awe balozi wetu?”
Erica alikaa tu kimya kwani kama alipigwa na bumbuwazi hivi kwa mwanae kupata ubalozi ikiwa si mtoto wa mtu maarufu wala nini ila alipendwa tu, wakati amekaa kimya kwa muda akasikia sauti ya mdada,
“Kheee mtoto mzuri hivi, mamake yuko wapi?”
Erica akageuka kumuangalia mdada huyo, macho yake yakagongana na Tumaini, ambaye ni dada wa Erick.
 
SEHEMU YA 235

Erica alikaa tu kimya kwani kama alipigwa na bumbuwazi hivi kwa mwanae kupata ubalozi ikiwa si mtoto wa mtu maarufu wala nini ila alipendwa tu, wakati amekaa kimya kwa muda akasikia sauti ya mdada,
“Kheee mtoto mzuri hivi, mamake yuko wapi?”
Erica akageuka kumuangalia mdada huyo, macho yake yakagongana na Tumaini, ambaye ni dada wa Erick.
Tumaini alipomuona Erica alimsogelea kwa tabasamu zito na kumkumbatia,
“Jamani Erica, za siku”
Kabla Erica hajajibu, Yule Moses akamwambia Tumaini,
“Huyu sasa ndio mama wa Yule Malaika mzuri unayemuona pale”
Tumaini alimuangalia mara mbili mbili Erica bila ya kummaliza maana alikuwa akishangaa na kupigwa na bumbuwazi kidogo, ila Moses alikatisha ule mshangao wao na kumwambia Erica atoe maamuzi ya kusaini mkataba kwao ili mtoto wake awe balozi, Tumaini akasema
“Kabla ya yote, naomba kwanza niongee na huyu mdada halafu atakuja kumalizana nanyi”
Tumaini akatoka nje na Erica, ambapo mtoto wa Erica aling’ang’ania kubembwa kwahiyo ikabidi Erica amnyanyue mtoto wake na kuongozana na Tumaini na kwenda kusimama mahali ili waongee. Tumaini alianza kumuuliza Erica,
“Umempata lini huyu mtoto Erica? Ina maana siku ile nilipokuja kwenu ulikuwa tayari na mtoto?”
“Ndio”
“Mbona ni msiri kiasi hiko Erica? Ndiomana hukutaka kunitafuta hewani kabisa, siku zote ukafanya nipate lawama kwa Erick sababu yako kumbe tayari una mtoto!”
Erica alikaa kimya tu kwani alijihisi aibu na hata hakujua aseme kitu gani, Tumaini aliendelea kuongea,
“Je Erick anajua kuwa una mtoto?”
“Hapana”
“Erica, unajua wewe ni muuwaji eeh! Hivi unajua ni kiasi gani Erick anakupenda? Unashindwa kumwambia swala kama hili ili mwenzio asonge mbele maana anakaa kukufikiria wewe kumbe tayari ulishazaa na mwanaume mwingine”
“Ni bahati mbaya Tumaini”
“Bahati mbaya? Kwahiyo ulibakwa? Kuna mapenzi huwa yanafanywa kwa bahati mbaya Erica? Ama kweli unamuumiza kaka yangu, sasa Erica naomba swala hili la wewe kuwa na mtoto umwambie mwenyewe, mimi sitasema ila umwambie mwenyewe”
“Naogopa nitamuumiza”
“Kama unaogopa kumuumiza basi mwambie, maana unavyokaa hivyo bila kumwambia ndio unamuumiza maradufu. Mwambie mapema ili ajue anajipangaje, mimi sitasema huu ujinga wako ila wewe useme mwenyewe”
“Tumaini jamani nisamehe”
“Nikusamehe nini sasa mimi? Kuna ulichonikosea? Hakuna, ila umemkosea Erick, naomba umweleze ukweli wa mambo ili mdogo wangu awe na maamuzi kama kusuka au kunyoa”
“Sawa, basi nitamwambia”
“Nakujua vizuri Erica, binti cha uongo. Umesema hivyo kuniridhisha tu, sasa naomba usikubali kusaini mkataba wa mwanao kuwa balozi hadi pale utakapokuwa umemueleza ukweli Erick”
“Sasa mimi nitaondokaje hapa bila kusaini? Si itaonyesha nimekataa jamani?”
“Erica, waambie kuwa unaenda kufikiria kwanza. Sitaki usaini na ukiwa mbishi hata huo ubalozi mwanao ataukosa kabisa, sijapendezewa na ulichofanya, sijapendezewa kabisa. Jitahidi umwambie ukweli Erick”
Erica alikubali kuwa atamwambia ukweli Erick, kwahiyo aliingia tena dukani na kuwaomba mkataba asaini siku nyingine kisha akaondoka zake.
Hakuna aliyeelewa kuwa Tumaini alikuwa akiongea nini na Erica ila walishangaa tu Erica akiwaambia kuwa mkataba atasaini siku nyingine, mpaka akajifikirie kwanza wakati kiukweli kwa Erica wala halikuwa swala la kujifikiria.
 
SEHEMU YA 236


Erica alirudi nyumbani na mwanae, tena kwa bahati alikuta mama yake bado hajarudi maana angemkuta amerudi sijui angemueleza nini amuelewe. Alitulia akitafakari kuwa ni namna gani atamueleza Eick, alitamani sana ubalozi kwa mwanae ila je atatumia njia gani kumueleza Erick kuwa ana mtoto? Alijikuta akiwaza sana bila ya jibu, hata hakujua aanzie wapi na aishie wapi, aliwaza sana hadi kujikuta usingizi ukimpitia akiwa pale sebleni na mwanae.
Mama yake alifika na kumshtua,
“Wewe Erica vipi? Kazi ndio kwanza wiki ya kwanza, ndio unashikwa na uchovu kiasi hiko!”
“Hamna mama”
“Halafu mbona inaonyesha kama mlitoka hivi!!”
“Hamna mama, tulikuwa hapa hapa nyumbani”
“Haya, ila swala la kutafuta mdada wa kazi ulifikirie na kulipa kipaumbele”
Erica aliinuka muda huu na kwenda chumbani kwake kumlaza mwanae nay eye kupumzika vizuri, aliwaza kuhusu maneno ya mama yake,
“Mama anaona sifai kufanya kazi kwa shemeji wakati huo huo anahitaji nitafute msichana wa kazi, jamani nitamlipa nini sasa nisipokazana na kazi?”
Aliwaza ila alijua wazi kwa wakati huo hakuwa na uchaguzi wa aina yoyot, aliamua tu kulala na mwanae.
Aliamshwa na simu ya Erick na kupokea kwa kuanza kumsalimia,
“Erica, nimekumiss sana mpenzi wangu:”
“Hata mimi nimekumiss”
“Sijui lini nirudi ili tufanikishe swala letu la kuwa na mtoto”
Hapo kidogo moyo wa Erica ulisizi kwani alihisi kama akishindwa kuendelea kuongea zaidi na Erick kwani hakujisikia kabisa kumueleza ukweli, aliamua kukatisha maongezi na kusema anaenda kuoga atampigia akitoka.
Alipokata alijitafakari sana,
“Hivi nitawezaje kumwambia Erick kuwa nina mtoto? Na je Erick atalichukuliaje hilo swala? Sitaumiza moyo wa Erick kweli? Sitaki aumie kama mimi nilivyoumia”
Alishindwa kuongea nae kabisa na hakuweza tena kumpigia simu.

Siku ya kwenda kazini tena alijiandaa na kuondoka ila aliogopa kuchukua lile gari la dada yake, alipofika tu ofisini kwenye mida ya saa nne bosi wake alimuita,
“Erica, unajua sikuelewi yani gari nimekupa ila bado unakuja kwa daladala na kila siku unanipa visingizio nisivyovielewa kabisa, mara leo nimechelewa nikaona nisije na gari sijui leo imefanyaje. Kwani tatizo ni nini Erica?”
“Ngoja nikwambie ukweli, sijui kuendesha”
“Kumbe ni hivyo tu jamani! Si ungeniambia mapema, basi nitakupa pesa uende kusomea udereva. Kwahiyo utakuwa unawahi kutoka ukasome”
Erica aliitikia tu, kiukweli kuendesha alijua sema hakuwa na leseni tu na hiyo haikuwa sababu sana ya yeye kutokwenda kazini na gari ila alimuogopa mama yake, kwahiyo akaendelea na kazi zake zingine.
Jioni ilipofika, shemeji yake alimuita tena na kumkabidhi laki tatu kuwa akasomee udereva,
“Hapana shemeji usinipe pesa, nitasoma nikipata mshahara”
“Hapana Erica, nishakwambia usiniite shemeji. Naomba upokee hii pesa na ukasome udereva, sikupangii pa kwenda kusoma ila wewe tafuta sehemu yoyote ukasome, na pesa isipotosha njoo uchukue nyingine”
Erica alijijkuta yupo mtegoni tu, na kuchukua ile pesa kisha kuondoka zake.
“Kwahiyo nikatafute mahali pa kusomea udereva”
“Kesho usije ofisini, nenda katafute mahali kisha utakuwa unaenda ukitoka kazini. Nitakuwa nakuruhusu mapema tu, najua ndani ya wiki mbili utakuwa tayari umemaliza, na swala la leseni, kesho kutwa nitamuita mwenzangu wa TRA hapa na atakupa mlolongo wote kisha ataenda kukutengenezea leseni”
Erica hakuwa na jibu la kumpa shemeji yake zaidi ya kukubaliana na kile alichokuwa akisema, kisha James akaendelea kuongea,
“Sina nia yoyote mbaya na wewe Erica, nadhani bado huamini kama nimeachana nay ale mambo. Nafanya hivi kwa upendo kwa mdogo wa mke wangu ambaye ni mdogo wangu pia, sitaki uteseke. Hujui tu ni jinsi gani nimeumia alivyonieleza dadako kuhusu baba wa mtoto wako, nakuhurumia sana Erica na sitaki ujione kama ni mwenye makosa sana duniani kwahiyo sifanyi vitu kukuweka kwenye mitego yangu au nini, nafanya kwa upendo tu ndiomana nimekwambia utafute mwenyewe sehemu ya kusomea udereva, hata usiniambie ni wapi ila nitakuwa nakupa ruhusa uende kusoma”
“Sawa nimekuelewa shemeji”
“Jamani Erica kila siku nakwambia usiniite shemeji”
“Unadhani nitakuitaje? Nakuheshimu na siwezi kukuita jina lako”
“Hata kama ila hakuna tatizo, usinifikirie vibaya Erica, hata sina nia mbaya na wewe”
James aliongea kama mtu aliyekuwa akijutia sana makosa yake, hivyo Erica alikubaliana nae na kwenda kuendelea na kazi.
 
Back
Top Bottom