Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #281
SEHEMU YA 224
Gari lilifika na alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati anatoka akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani Erica alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa mgongoni amelala.
“Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?”
“Wa dada yangu”
“Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?”
“Kaenda kazini”
“Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba changa basi inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki”
Swala la kuambiwa Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica.
Muda huo ilikuwa kama Erica kapigwa na bumbuwazi maana alisimama tu bila kwenda mbele wala kurudi nyuma, ila Mrs.Peter alikuwa ametangulia mbele akijua Salma anamfata nyuma ila muda huo Salma alikuwa akisimama palepale na alionekana akimuangalia Erica kwa chuki ya waziwazi, kitu ambacho kilimshangaza hata Erica mwenyewe, na kumuuliza,
“Mbona unaniangalia hivyo?”
“Utaacha lini uongo wewe mwanamke? Eti mtoto wa dada yangu (Huku akibana pua, na kuendelea kusema). Mtoto wako mwenyewe unasingizia wa dada yako, kwani ni kipi unachohitaji kwa huyu mama?”
Erica alimuangalia huyu Salma na kutamani hata kumpa tusi ila tu swala la kutukana halikuwepo kwenye kinywa chake, muda kidogo mwanae akaamka na kuanza kulia, ikabidi Erica amfunue na kumgeuzia kwa mbele, muda huo Salma alikuwa akiondoka kumfata Mrs.Peter ila Erica akamshika vizuri mkono Salma na kumrudisha nyuma kisha akamwambia,
“Mwangalie vizuri huyu mtoto ndio utaelewa ni kwanini sikusema wa kwangu.”
Kisha Erica akaondoka ila alimuacha Salma akiwa na maswali mengi sana, aliendelea kumfata Mrs.Peter ila kiukweli alikosa raha.
Erica alipotoka pale hospitali hata hakutamani kuita gari ya kukodi, na moja kwa moja alielekea kupanda daladala maana alijiona kama ni kudhalilika tayari ameshadhalilika vya kutosha, aliamua kuacha tu jamii yake ijue kuwa ana mtoto, hakuwa na sababu tena ya kumficha mtoto wake.
Akiwa kwenye daladala, alikaa siti ya nyuma ambako kulikuwa na wamama wawili wamekaa kwa pembeni yake wakiongea, yale maongezi yao aliyasikia yote na yalionyesha kuvuta sana hisia zake,
“Yani mwenzangu, kipindi kile natoka na mume wa mtu halafu mkewe hata simjui ila cha kushangaza nilikutana nae njiani si nikagombana nae, yani jamani mapenzi bhana yana wivu ambao mwizi humjui ila unashangaa unagombana nae. Niligombana na Yule mkewe hadi mumewe akaja kutuamulia ndio hapo nikajua kumbe Yule ndiye mkewe, na ubaya hakuniambia kuwa ameoa weee balaa lilizuka ila nikaamua kuwa mpole na kujitoa”
“Ila mapenzi ndio yalivyo, yani mnaweza kuwa mnatoka na mtu mmoja hamjuani ila unashangaa kuna mambo gafla tu mnachukiana jamani, sijui wale wanaoishi wake wawili au watatu wanajisikiaje ndani”
“Washazoea wale, ila katika ujana wangu nimejifunza jambo. Hawa wanaume ni bora kuwachuna tu, ukijiendekeza kuwapenda utalia jamani, ni waongo balaa”
“Hahaha, ila wakweli wapo bhana, sio wote waongo kumbuka hata na wao wanalalamika kuwa wanawake ni waongo”
“Ndio, ila wao wamezidi”
Basi kituo kilichofata wale wanawake walishuka na kumuacha Erica akitamani hata kuwauliza baadhi ya maswali ila hakuweza maana hakuwazoea.
Ila waliposhuka tu kule nyuma alipanda mkaka na kukaa karibu na Erica, Yule mkaka alimtazama Erica na kumtazama mtoto wa Erica kisha akamwambia,
“Dada, hongera sana una mtoto mzuri. Halafu ana tabasamu vizuri”
“Asante”
“Mmmmh sijaanza hata kukusalimia maana nilivutiwa na uzuri wa huyu mtoto, hali yako lakini”
“Nzuri, ila usijali”
“Ngoja nijitambulishe kidogo, dada mimi naitwa Moses. Nina duka langu zuri sana la nguo za watoto wakike na wa kiume. Naomba uje dukani kwetu hata mara moja uone huduma zetu, business card yangu hii”
Akamkabidhi Erica, naye Erica akapokea huku akisikiliza maelekezo mengine toka kwa Yule kaka,
“Tafadhali dada, naomba ufike. Nimevutiwa sana na mwanao. Najua atapendeza sana akivaa nguo zetu zile. Ila unaitwa nani, na mwanao anaitwa nani?”
“Mimi naitwa Erica, na mwanangu anaitwa Angel”
“Wow, majina mazuri sana. Nakutegemea basi dada ufike dukani kwetu. Ila ungenipa na namba zako”
Basi Erica akataja na namba zake kwa Yule kaka, kisha alivyofika kwenye kituo chake alishuka na kuelekea nyumbani kwao.