Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 312

Kisha Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake, na giza lilishaanza kuingia, akaona simu yake inaita kuangalia akakuta Erick anapiga, kwakweli akaogopa kupokea maana alikumbuka maneno yale aliyoambiwa kwenye ndoto na Yule mganga, ndipo akakumbuka hata ile leso ambayo ipo nusu kwahiyo alitoka tena ili kumueleza mama yake.
Akamwambia alivyozungumza na Fetty na jinsi alivyoenda kuangalia pochi yake na kukuta leso nusu,
“Mmmh mwanangu, hatujamaliza hili linazuka lingine jamani tutapona kweli?”
“Sijui mama”
“Hebu mpigie Yule mwanamaombi umueleze hayo na mimi ngoja niwapigie watumishi wengien niwaeleze maana sio kitu cha kawaida hiko”
Basi Erica alichukua simu yake na kumpigia Yule mwanamaombi, kisha baada ya salamu alimueleza Yule mganga alivyomtokea usiku na akamueleza jinsi alivyoongea na rafiki yake na jinsi alivyoona leso yake,
“Erica, kwanza tunatakiwa kumshukuru Mungu sana kwa hilo. Kwakweli Mungu wetu ni muaminifu sana, tulihitaji kujua ni kwanini bado anakufatilia? Ila Mungu katuonyesha kwa wazi kabisa kumbe Yule mganga ana kipande cha leso yako, sasa naomba niingie kwenye maombi ili nijue cha kufanya na hiyo leso. Na wewe uombe tafadhali”
“Sawa, na mimi naomba”
Erica alivyokata simu akamueleza mama yake aliyokuwa akiongea na Yule mwanamaombi,
“Hata mimi watumishiwamesema waombee kwanza swala hilo na kunitaka na mimi kuingia kwenye maombi. Njoo tuombe kwa pamoja mwanangu”
Basi Erica alisogea kwa mama yake na kushikana mikono kisha kuanza maombi ya kwa pamoja ambapo yalifanyika kwa muda kama wa nusu saa, kwakweli Erica alijihisi kuchoka maana hakuyaweza maombi ya vile ila ni mama yake tu ndio alikuwa akiomba.
Basi baada ya maombi wakati wametulia tulia, simu ya Erica iliita tena na alikuwa ni mwanamaombi anapiga, basi Erica alipokea na kuanza kuongea nae,
“Sasa Erica, chukua hicho kitambaa na mtoke nje kabisa ya nyumba yenu kimwagie mafuta ya taa na ukichome moto huku ukiendelea kuomba, maana huyo tayari ni adui kwako hafai”
Basi Erica alipokata simu alimfahamisha mama yake kisha walibeba kile kitambaa mpaka nje na kukitupa kisha kumwaga mafuta ya taa na kukichoma yani kilikuwa kinatoa harufi kama kuna damu inaungulia, hadi mama Erica akasema,
“Mmmmh mara nyingine tunakaa ndani kiajabu jamani, sasa kukaa na kitambaa kinachomwa kinakuna kama damu mmmh! Makubwa haya”
Walihakikisha kitambaa chote kimeungua kisha walirudi ndani na kujiandaa kwaajili ya kulala kwani ilikuwa ni usiku tayari, walifanya tu maombi ya kulala na kwenda kulala.
Kwakweli kwa siku ya leo Erica alilala tu kwani hakutaka hata kuongea na Erick kwenye simu kwani bado alikuwa na uoga nay ale maneno ya Yule mganga.
 
SEHEMU YA 313


Kulipokucha, Erica aliamka na kuanza kufanya mambo yake mengine kisha alienda kumsalimia mama yake ambapo alimuuliza kuhusu usiku wa jana kuwa ulikuwaje kwake,
“Vipi lile shetani lilikujia tena ndotoni?”
“Hapana mama, sikumuona ndotoni”
“Basi itakuwa ni kile kitambaa ndio kilikuwa kinamfanya aje kwa urahisi kwenye ndoto zako, mwanangu hilo liwe fundisho sasa mambo ya waganga hapana, yani utahisi una nia njema ya kwenda kwa mganga ila atakachokufanya utajuta maisha yote. Waganga hawana tiba yoyote zaidi ya kukuongezea majini tu ambayo yakicharuka yatafanya ufanye vitu vya ajabu”
“Ila mama nilienda ili kujua ukweli kuhusu Bahati”
“Eeeh ukishajua ukweli?”
“Nijue tu basi”
“Yani wewe nae una mambo ujue, yani Yule Bahati kafanyiwa michezo na ndugu zake, acha kama ilivyo, kwani wewe ndio una uchungu zaidi na Bahati kushinda ndugu zake? Kwanini kujitakia matatizo yasiyo na lazima? Ukiujua ukweli ufanye nini sasa? Kama kachezewa na ndugu zake acha, Yule sio mumeo kusema uhangaike nae mpaka utake kuingia matatizoni, angekuwa mumeo sawa ila sio mumeo Yule, usitake kujiletea tena matatizo. Maana utaambiwa kuna mganga wa kumrudisha Bahati kwako utaenda, huku mtoto ushamuuza kwahiyo atakuwa na baba watatu au?”
Erica alikaa kimya tu na mama yake aliendelea kumuasa kuwa aachane na hayo mambo ya kwenda kwa mganga wa kienyeji maana hayatamsaidia chochote.
Basi akaendelea kufanya mambo mengine, muda kidogo akapigiwa simu alipoangalia ni ile namba ya Yule bosi wake ambaye ni mama yake Erick, kwa hakika alishindwa kupokea kwani aliogopa na kuacha iite hadi ikatike hata ilipopigwa tena napo hakupokea wala nini.
Jioni ya siku hiyo, akapigiwa simu na namba ngeni, alikuwa na mashaka nayo ila aliamua kuipokea, sauti ilikuwa ni ya Yule bosi wake ambaye ni mama yake Erick, alimsalimia kwa uoga kisha Yule mama akamuuliza,
“Mbona hujaonekana kazini kwa siku ya tatu sasa?”
Alikuwa akijiuma uma tu kwani hakuwa na cha kujieleza, kisha Yule mama aliendelea kuongea,
“Hata kama ulihitaji kuacha kazi, hukujua kama kuna utaratibu wa kuacha kazi? Ungekuja na kuniuliza, kwani kuna siku nimegombana na wewe Erica hadi uache kazi gafla hivyo?”
“Hapana sijaacha kazi”
“Sasa kwanini huji kazini?”
“Aaah naumwa”
“Hujui taratibu za kazi? Huwa watu wakiumwa hawaji tu kazini? Kuna taratibu zake,na hata kuacha kazi kuna taratibu zake”
“Naomba nisamehe”
“Sawa, Jumatatu nakuhitaji hapa kazini na ulete na uthibitisho wa daktari kuwa ulikuwa unaumwa, nimekupa siku nyingi za kushghulikia swala hilo. Kuumwa au kuacha kazi kuna taratibu zake, sio kujiamulia tu, hii kazi sio ya baba yako au ya mama yako. Nakuhitaji kazini Jumatatu, kwaheri”
Yule mama akakata simu, kwakweli Erica alibaki na mawazo kwani hakuelewa kuwa ataanzaje kwenda kazini ikiwa Yule mama anaujua ukweli wote ila akasema atajua hiyo hiyo Jumatatu kuwa ataenda au la.
 
SEHEMU YA 314

Usiku uliingia na alifanya mambo yake kama kawaida ila akapigiwa tena simu na Erick, bado alikuwa anaogopa kupokea kutokana na maneno ya Yule mganga, kwahiyo hakupokea ingawa iliita na kuita ila hakupokea. Alijua kama anafanya makosa na anaumiza moyo wa Erick ila hakutaka kupokea kwani alijua kama Erick angepata matatizo basi kwake ndio ingekuwa kuzidi.
Aliiacha tu ile simu kuita hadi kukatika, muda wa kulala ulifika na akalala.
Saa kumi alfajiri akapigiwa na dada yake Mage na kupokea,
“Amka Erica ujiandae, saa kumi na moja utoke hapo uje stendi”
“Dada jamani, mama ushamwambia?”
“Ukiwa unajiandaa, ukimaliza kujiandaa nibipu halafu mimi nitapiga kumwambia mama ni wapi tunaenda?”
“Sawa dada”
Basi simu ikakatika na Erica akaanza kujiandaa hadi alipomaliza kupakia na nguo zake kwenye begi la mgongoni akambipu dada yake kisha ilionyesha kama mama yao kapigiwa maana alimsikia akiongea na simu huku akitoka chumbani kwake inaonyesha alikuwa anakuja kwenye chumba cha Erica.
Alimuangalia mwanae sana aliona atamkumbuka sana kwa hizo siku mbili atakazokuwa huko mkoani.
Kisha mama yake alifika chumbani kwake na kumwambia,
“Kumbe Erica una safari na dada yako? Kwanini hukuniambia?”
“Nilisahau mama, yani dada ndio kanikumbusha asubuhi hii. Nisamehe mama”
“Haya mfanye haraka, leo uwahi kurudi sitaki ujinga wa kuchelewa”
“Sawa mama”
Hakujua ni wapi ambapo mama yake ameambiwa na dada yake, ila alimshika mwanae na kumbusu kisha kumuaga mama yake na kuondoka, kitu pekee ambacho mama yake hakukielewa ni kumuona akibeba begi la mgongoni na pochi ila hakuuliza sana kutokana nay ale aliyoelezwa na Mage, Erica hakuelewa ni kitu gani mamake alichoambiwa na dada yake ila yeye alishukur tu kupata ruhusa na kuondoka.
 
SEHEMU YA 315


Alifika stendi na kukutana na dada yake kisha wakaingia kwenye basi, na muda kidogo safari ilianza na alikuwa kimya tu safari nzima, ila walipokaribia kufika alimuuliza dada yake,
“Dada, umemuaga vipi mama?”
“Nimemwambia kuna kuna project nafanya, kwahiyo namuhitaji Erica maana zinatakiwa zipigwe picha alfajiri, akakubali ndiomana hata umetoka na begi mgongoni hajakuuliza maana nimemwambia kuwa utabeba nguo kadhaa”
“Kheee na tusiporudi leo?”
“Wewe tulia tu, jioni nitampigia simu mama. Najua jinsi ya kumpanga na atanielewa tu”
Erica alimuitikia dada yake, na hatimaye karibia na jioni ya siku hiyo walifika kwenye kijiji cha baba zao wadogo na kupokelewa vizuri sana.
Baada ya muda kidogo Derick nae alifika, na kwenda kupokelewa ambapo nae alifikia hapo kwa baba zao wadogo., na walikaa nyumbani kwa baba yao mdogo ambaye ndio mkubwa kwenye eneo hilo
Baba zao wadogo watatu walifika na walikaa nao ili kuzungumza nao, ambapo kwanza waliambiwa kuwa kesho asubuhi wataenda kwenye kaburi la baba yao na kuweza kuanza kufanya hayo matambiko, Erica alitulia kimya akisikiliza.
“Kwakweli mimi kama baba yenu mdogo ambaye ndio mkubwa kwasasa nimesikitishwa sana na haya mambo nilipoyasikia. Unajua baba yenu ndio alikuwa wa kwanza kwenye familia yetu, kwahiyo kitendo kama hiki ni laana kubwa sana na hakitakiwi kabisa kwa jamii. Ni bora mmeamua kukiri ili tuvunje laana hii, kwanza kabisa Erica na Derick mshikane mikono na kukubaliana kuwa nyie ni ndugu maana mmetenda vitendo vya aibu sana”
Erica alifanya hivyo ila hakuwa na tatizo kabisa, kwani hakuwahi kuwa na matamanio na Derick hata kulala nae ni Derick ndio alifanya njama ila kwa yeye mwenye hakutaka kitu cha namna hiyo kitokee.
Kisha baba zao wadogo walitaka kujua chanzo cha wao kujikuta wakifanya laanza hiyo, ila walijitetea kuwa walikuwa hawafahamiani kama ni ndugu, basi baba zao walisema kuwa wamewasamehe na kuwa tayari kufanya tambiko la kuvunja hiyo laana kwao.
Walipomaliza pale, baba yao mdogo aliwapeleka mtoni ili wapate kuona mandhari ya mto hata wakipenda kuoga waoge huko, kwakweli mandhari ile ilikuwa nzuri sana ila hapakuwa na watu kabisa, Erica akauliza,
“Mbona mandhari inavutia lakini hakuna watu baba?”
“Unajua siku hizi, asilimia kubwa wana mabomba nyumbani kwahiyo huku mtoni watu huja mara moja moja kutembea tu. Ila panavutia sana na maji yake ni mazuri kushinda hata yanayotoka nyumbani, mara nyingine huwa tunakuja kuoga huku kama kuondoa mikosi katika maisha yetu”
Erica alipenda wazo la maji kutoa mikosi, hivyo akaamua kuchota ili akaoge nyumbani maana walienda nan doo, na baba yao mdogo aliwaambia wabebe ndoo kwavile maji yale hupendwa na watu wengi sana, kwahiyo alijua watayapenda tu.
Usiku walikula na kuonyeshwa sehemu za kulala, kweli Mage alimpigia mama yao simu na kutafuta namna ya kumdanganya kuwa siku hiyo haitawezekana kurudi,
“Hivi Mage unajua kuwa Erica ana mtoto mdogo nab ado ananyonya?”
“Mama nawe jamani! Huu ndio wasaa mzuri kwa huyo mtoto kuacha ziwa”
“Ila bado hajafikisha miaka miwili”
“Mama, siku hizi nani ananyonyesha mtoto miaka miwili? Hiyo ilikuwa zamani bhana, ila tusamehe mama mambo yameingiliana”
Basi alikubali tu ili kishingo upande.
 
SEHEMU YA 316

Kesho yake waliamka na kwenda mtoni kuchota maji kwani tayari Erica aliyapenda maji yale, kisha walirudi na kuoga na kujaribu kujishughulisha kidogo pale, wakisaidiana na mama yao mdogo huku wakisubiri muda wa tambiko, ila Yule baba yao mdogo alikuja na kusema,
“Jamani, mzee wa mila kaniambia kuwa hii sio siku nzuri kwa tambiko kwahiyo itabidi tufanye kesho”
Erica akashtuka kidogo,
“Jamani hadi kesho!”
“Ndio, hadi kesho nadhani hamjui vizuri mambo ya tambiko. Mambo mengine sio ya kulazimisha, siku nzuri kwa tambiko ni Jumanne na Alhamisi yani hata kesho Jumatatu tutafanya tu ila Jumanne ilikuwa nzuri zaidi. Ila leo Jumapili ni mbaya haifai”
Ilibidi tu wakubali kwani wao hawakujua mambo ya tambiko, kisha wakaendelea na mambo mengine ya pale nyumbani kwa baba yao mdogo huku wakitembelea mashamba mbalimbali na kuangalia vitu mbalimbali.
Mchana wa siku hiyo, Erica alipigiwa simu na mama yake, akapokea na kumsalimia, ila mama yake alianza kwa kumpa lawama,
“Wewe mtoto una nini lakini? Umeondoka hata mwenzio hujamuaga ni haki hiyo Erica? Halafu simu zake hupokei kwanini? Unajua una mambo ya ajabu wewe, hebu pokea simu ya mwenzio sio vizuri ujue”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Tena kijana wa watu anaonekana ana upendo sana ila namuhurumia kwakweli maana wewe huwa hueleweki kabisa, kwanza huko ulipoenda na dada yako sipaelewi kabisa. Vipi mnarudi saa ngapi leo?”
Erica hakuwa na jibu bali alimkimbizia dada yake simu ili aongee na mama yao, kama kawaida Mage alitafuta Kiswahili cha kumlainisha mama yao kisha akakata simu, muda huo Erica alikuwa nje, kisha dada yake aliweka simu kabatini.
Erica akiwa hana habari nje, simu yake ilianza kuita na ni Derick ndio aliiona na kuifata kuiangalia, akaona mpigaji ameandikwa ‘My love Erick’
Kiukweli alijihisi kutokuwa na furaha gafla na kupokea ile simu, hata Erica hakujua kuwa ni kitu gani Derick aliongea na Erick.

Jioni ya siku hiyo Erica alitaka tena kwenda mtoni kuteka maji kwavile alijikuta akipenda sana maji ya kutoka mtoni, akamuomba dada yake amsindikize,
“Dada, nisindikize nikachote maji”
“Aaah jamani Erica, asubuhi si tumeenda jamani, unataka maji yam to kila muda loh! Hata hivyo sio mbali sana unaweza kwenda tu”
“Ila naogopa mwenyewe, sijazoea halafu bamdogo alisema watu hawaendi endi kule”
Akatokea Derick na kusema kuwa yeye atamsindikiza maana hana cha kufanya na alitaka kuendelea kuangalia mto, na Mage akadakia,
“Bora umsindikize maana Erica kwa uoga ni balaa”
Kwahiyo Erica aliondoka na Derick kuelekea mtoni kuchota maji.
Kufika mtoni Derick alianza kumchombeza Erica,
“Hivi Erica, huwa ukikaa hunikumbuki?”
“Nikukumbuke kivipi?”
“Yani huwa hukumbuki kabisa kama umewahi kuwa na mahusiano na mimi?”
“Aaah hayo yashapita Derick, sisi ni ndugu ujue”
“Ndugu wa kweli Erica ni Yule uliyezaliwa naye mama mmoja kwani mama ndio anajua ukweli wa mtoto kuwa baba yake nani”
“Kwahiyo una maana mimi si ndugu yako?”
“Hapana, ila mwenzio nakukumbuka sana Erica”
“Hebu acha habari hizo Derick, sisi ni ndugu nione dada yako kama mimi ninavyokuona kuwa u kaka yangu”
“Ila Erica, yani kesho laana itakuwa imevunjwa ila leo tumeachiwa kwa makusudi kabisa”
“Sikuelewi”
“Tumeachiwa siku ya leo kufunga ukurasa wetu, tafadhali Erica, nipe mara moja tu”
“Hivi una akili wewe, huko kichwani ni mzima? Yani huna hata aibu kweli kabisa mimi nikatembee tena na wewe? Kwanza wewe si mpenzi wangu, ninaye wangu tayari, pili wewe ni ndugu yangu yani wewe ndiye umefanya tufike huku kuvunja laana halafu bila aibu unaniambia ushetani huo”
“Erica sio ushetani, kiukweli nakutamani sana yani kadri tunavyoenda mie nazidi kupatwa na hisia, sina raha kabisa Erica, naomba mara moja tu. Nimeamua kukwambia ukweli, sina raha tangu nimekuona Erica, naomba mara moja tu”
“Nitolee ujinga wako mie”
Erica alichota maji na kubeba ndoo yake kisha kuanza safari ya kurudi kwani alijua kuendelea kuongea na Derick hapo ni kutafuta matatizo tu.
Erica aliongoza mbele sana, ila akasikia kishindo kuwa Derick kaanguka kwakweli hapo alishikwa na huruma ukizingatia ni ndugu yake, akatua ndoo yake na kurudi nyuma kumuangalia, wakati anamuangalia Derick alimvutia kwa chini ambapo Erica alianguka chali sababu hakujipanga, kisha Derick akaenda juu ya Erica ilionyesha wazi alikuwa na lengo la kumbaka.
 
SEHEMU YA 318

Walipofika, Erica alienda kuoga, kisha akaenda chumba walichotengewa, akapokea ujumbe tu toka kwa Derick,
“Naenda kuulizia vyumba Erica, nikishapata tu nakuja kukuchukua ili twende pamoja, kwahiyo nitakushtua nje hapo utoke”
Erica alisoma ule ujumbe huku akitafuta namna tu ya kumkatalia, alitamani dadake awe karibu nae zaidi ili wazo la Derick lisiwepo tena maana Derick alimsumbua ilihali akijua ni nduguye.
Kwenye mida ya saa moja moja, Derick alionekana kurudi ila alipiga simu ya Erica ambayo haikupokelewa kwahiyo ilibidi amuagize dada yao Mage kuwa anamuita Erica, dada yao alivyofika ndani alimwambia Erica,
“Wewe, kakako anakutafuta huko nje”
“Dada, naomba nikwambie kitu”
“Kitu gani? Unataka kuanza tena habari za mama, nilishakwambia niachie kuhusu mama najua jinsi ya kuongea nae.”
“Hapana dada, sio kuhusu mama”
“Ila kuhusu nini?”
“Ni kuhusu huyu Derick”
Mara simu ya Erica ilikuwa inaita na mpigaji alikuwa Derick, dadako akamkazania kuwa apokee simu au atoke akaongee na Derick kisha wao wataongea badae,
“Hapana dada sio badae, ni muda huu inabidi tuongee”
“Ni kuhusu nini?”
“Dada, huyu Derick ananitaka”
“Aaaah Erica hebu acha zako mdogo wangu, Derick mwenyewe ndio kaniomba tuivunje hii laana halafu mwenyewe akutake inawezekana kweli hiyo?”
“Ila Dada, mimi ni mdogo wako nisikilize”
“Hata Derick nae ni mdogo wangu”
“Dada, siendi kuongea na Derick hadi kesho kwenye tambiko, na hata hapo nje sitoki leo”
“Erica, sikuelewi”
“Nielewe tu”
Basi dada yake alitoka, na Derick alipiga tena ikabidi Erica apokee ili amkatalie ajue msimamo wake,
“Derick, sitaki tena sitaki ujinga wako huo”
“Unajua nataka kukwambia nini lakini?”
“Nini?”
“Toka nje”
“Sitoki”
“Ni hivi vyumba nimekosa Erica, kwahiyo nilikuwa nakwambia basi twendo bafuni kama tulivyopanga”
“Nikome Derick, mimi ni dada yako. Kwaheri”
Erica akakata simu ila kiukweli alikuwa na hofu hata ya kwenda nje kwa siku hiyo kwani alihisi pengine Derick anaweza kumvizia hata chooni, kitendo hiko kilimfanya Erica asitoke nje kabisa, hata chakula cha usiku hakula na kusema kuwa ameshiba ila si kweli kwamba alishiba ila hakutaka kula sababu hakutaka kutoka nje kwenda uwani kujisaidia hata haja ndogo maana alihisi vibaya kuhusu Derick kuwa huenda akamvizia uwani na kumbaka sababu Derick alionekana hana hata habari ya undugu wao.
Wakati anataka kulala, akapigiwa simu na mama yake, ikabidi apokee na kumsalimia,
“Hivi Erica una akili gani wewe? Yani huna uchungu hata na mwanao? Hupati wasiwasi hivyo hujamuona mwanao hadi leo?”
“Nisamehe mama”
“Nikusamehe kitu gani na umemfanyia roho mbaya mwanao, siku ya pili hii inakatika ukiwa mbali na mtoto, unamsononesha mtoto kwakweli. Halafu kitu kingine ni kwanini unamtesa kijana wa watu?”
“Nani mama?”
“Wewe mwenyewe uliniambia ooh mama nampenda sana Erick, hivi mtu unayempenda sana unaweza kumfanyia huo ujinga? Yani unaenda mahali hata humuagi? Kuwa mbali sio kigezo ila swala la kumuaga lipo palepale, ulitakiwa kumpigia simu mpenzi wako na umuage, ushauza mtoto halafu unafanya ujinga kweli? Kijana wa watu anakupigia simu unampa mwanaume apokee kweli Erica?”
Hapo Erica alishangaa kuwa ni mwanaume gani kampa aongee na Erick, ila akashindwa namna ya kumuuliza mama yake vizuri na kuishia tu kumuomba msamaha,
“Sasa kesho uwe hapa nyumbani, sitaki kusikia hizo habari sijui tunaenda kupiga picha, sijui ujinga ujinga gani sitaki kusikia. Mmekazana kupiga piga picha mmekuwa waigizaji nyie, mnatengeneza filamu? Hebu tuwekane wazi basi, huo ujinga sitaki, kesho muwe hapa nyumbani. Sawa!”
“Sawa mama nimekuelewa”
Basi Erica akakata simu ya mama yake ila alijiuliza maswali mengi sana kuhusu na aliyepokea simu ya Erick, muda huo huo akapokea ujumbe toka kwa Erick,
“Erica, nakupigia simu mpenzi wangu hupokei ila leo ukaamua kumpa mwanaume apokee simu kweli Erica jamani! Mbona mimi nakupenda sana, kwanini unifanyie hivyo? Halafu mwanangu umemuacha wakati bado alikuwa ananyonya, mmemkosesha haki mwanangu, nimeumia sana”
Yani Erick aliandika kamavile ni baba mzazi wa Yule mtoto kiasi kwamba yale maneno Erica yalimuingia, akatamani kumpigia simu Erick ili ajaribu kumuelewesha ila simu yake haikuwa na salio, na muda huo huo dada yake na watoto wengine wa baba yake mdogo waliingia kulala kiasi kwamba hakuweza tena kumsimulia vizuri dada yake kuhusu sakata la Derick.
 
SEHEMU YA 319

Kulivyokucha, waliamka na kufanya shughuli ndogo ndogo kisha baba yao mdogo ambaye ndio alikuwa mkubwa alifika na wale wengine watatu na kuwataka Erica, Derick na Mage waongozane nao kwenda makaburini.
Waliondoka na walivyofika kwenye kaburi la mzee wao alifika mzee wa kimila na kuanza kusema mambo ya kimila wanayotakiwa kufanya, kwanza kuna mashuka walitakiwa wavae kisha wakae kwenye lile kaburi sababu baba yao alikufa, kwa maana hiyo angekuwa hai basi angewapakata wakati Yule mzee anawasomea mila.
Basi kimya kilitanda wakati Yule mzee akifanya mambo yake ya mila za kuvunja laana ya kutembeleana ndugu, alipokaribia kumaliza aliweka mikono yake juu ya vichwa vya wale watoto yani Derick na Erica na kusema,
“Hawa watoto nawaleta kwenu mizimu muwaangalie, watoleeni laana iliyokuwa mbele yao. Huyu wa kike apate mume wa kuolewa nae na huyu wa kiume apate mke wa kumuoa. Laana yote juu yao imevunjika muda huu.Hawakutambua makosa yao, wahurumieni”
Kisha aliendelea na maneno ya kilugha kwa muda na kuwataka wainuke kisha kuna mahali walitakiwa wakanyage na kulikuwa na kitu kama mbao laini ambapo kila alipokanyaga mmoja ile mbao ilivunjika kisha Yule mzee akachukua vile vipande na kuchimba pembeni ya kaburi la baba yao na kuvifukia, hapo wakaambiwa ndio mwisho wa tambiko lao ila wanatakiwa waende kwanza mtoni wakaoge.
Kwahiyo walianza safari ya kwenda mtoni muda ule, kisha wakaoga kwa maelekezo ya Yule mzee na walioga na nguo, kisha walitakiwa kukaa pembeni kukauka yani wanakauka na nguo zao huku Yule mzee akiendelea na mambo mengine ya mila zao.
Baada ya hapo waliambiwa ni muda wa kurudi kule walipofikia ila ilikuwa mchana tayari na jua lilikuwa ni kali sana, kiasi kwamba walikuwa wakitembea na kupumzika yani hadi wanafika nyumbani walikuwa wamechoka choka kwa mizunguko ya siku hiyo na mambo yaliyokuwa yakifanywa.

Kufika nyumbani, Erica alimwambia dada yake kuwa wajiandae na waondoke siku hiyo hiyo, baba yao mdogo alikuwa akiwapinga kuondoka siku hiyo,
“Jamani si bora mngeondoka asubuhi!”
“Natakiwa kazini bamdogo, kwahiyo bora tuondoke leo na tutaingia usiku wa manane nyumbani”
“Jamani Erica, ila wewe mtoto mbishi sana na ukiamua lako huwa hutaki kupingwa haya, ila sidhani kama ni vyema kufanya hivyo”
Mage hakumbishia sana mdogo wake kwani tayari alishamdanganya sana mama yao kwahiyo hata yeye aliona ni vyema waondoke tu wafike kwao usiku, ila kabla ya kwenda kujiandaa Yule mzee wa kimila alisema kuna kitu kimoja alikisahau na anatakiwa kukifanya juu yao, walimsikiliza vizuri na kuwaambia kuwa inatakiwa wachanjwe, kwakweli Erica alishtuka na kuuliza,
“Kuchanjwa tena!”
“Ndio, hii itawasaidia kuwapa kinga kwani hata watu wabaya hawataweza kuwapata”
Erica hakuweza kukataa kwani dada yake alimkazia macho kwahiyo akakubali kisha mzee wa mila akaanza na mmoja mmoja na kuwachanja, ila zamu ya Erica ilipofika ilikuwa kazi sana maana Erica alikuwa muoga kiasi kwamba hakumchanja vizuri inavyotakiwa, ila akampaka dawa hivyo hivyo.
Baada ya hapo aliwaambia kuwa wanatakiwa wasioge hadi kesho, baba yao mdogo akasema,
“Basi inabidi waondoke kesho maana huyu mtoto mbishi leo anaweza kwenda kuoga huko kwao”
Baba yao mdogo alisema kuhusu Erica, na baba zao wadogo wote wakaafiki kuwa waondoke kesho yake, kwahiyo hawakuwa na namna zaidi ya kukubali kuondoka kesho yake tu.
Wakati bado wamesimama pale wakiongea ongea, alifika mzee mmoja na kusalimiana na Yule mzee wa kimila kisha na wale baba zao wadogo, ambapo baba yao mdogo mmoja alianza kumtambulisha Yule mzee kwa wale watoto wa ndugu yake, Yule mzee alihamaki huku akiwaonyeshea kidole Erica na Derick,
“Kwahiyo hawa watoto ni ndugu?”
Baba yao mdogo akamjibu,
“Ndio ni ndugu, watoto wa kaka”
“Kwakweli kuna tatizo kubwa hapa, tena tatizo kubwa”
“Tatizo lipi hilo?”
“Hawa watoto nimewakuta jana kule kichakani karibu na mtoni wakifanya mapenzi”
Kila mmoja alishangaa na kuwaangalia Erica na Derick, huku baba yao mdogo akiuliza kwa hamaki,
“Eti nini?”
“Nimewakuta hawa wakifanya mapenzi, nimewaona kwa macho yangu haya mawili, mliposema ni ndugu nimeshangaa sana amakweli dunia imeisha”
Baba yao mdogo aliwauliza, ila Erica akakaa kimya maana hakujua kama mada ya jana ingeibuka hapo kwa namna hiyo, baba yao alipoona Erica kanyamaza alijua ni kiburi tu kinamsumbu, ikabidi amuulize Derick, ambaye aliamua kujibu,
“Tusameheni baba wadogo, naomba mtusamehe sana. Kwavile tuliona tunaenda kuvunja laana, Erica aliniomba tufanye mapenzi mara ya mwisho, jamani mimi ni mwanaume sikuweza kukataa, naomba mtusamehe”
Wale baba wadogo walimuangalia Erica kwa ukali sana, na kumuamuru kuwa apige magoti chini kwa hasira huku baba mdogo wake akiongea kwa gadhabu,
“Wewe mtoto una matatizo gani eeeh! Kumbuka wewe mezaliwa na mama halali wa ndoa yani mke halali wa baba yenu, yani leo mnakuja kusuluhishwa kwa ujinga mlioufanya halafu unaenda kumshawishi ndugu yako kufanya tena kile kitendo kweli!”
Ikabidi Mage aingilie kati,
“Ila wewe Derick hebu kuwa mkweli, unajua jana Erica aliniambia kuwa unamtaka nikamwambia haiwezekani, hebu kuwa mkweli Erica amekushawishi wewe kufanya hivyo jamani! Ni kweli Erica ana kiburi, mbishi lakini hawezi kufanya hivyo, hana tamaa ya mapenzi kiasi hiko”
Erica nae alijaribu kujitetea na kuonyesha ule ujumbe wa Derick kuwa hata alitaka kutafuta chumba ili wakalale, ila Derick alijitetea,
“Erica, hebu kuwa mkweli si ni wewe mwenyewe ndio uliniambia hujaridhika pale polini, unataka nikatafute chumba twende huko tukamalizane kabla ya leo, na jana nilienda tu kujigelesha ili kukuridhisha na muda ule nimekuita nje nilitaka kukwambia kuwa chumba sijapata ili wewe uweze kuachana na wazo hilo”
“Jamani Derick unanisingizia hivyo kweli!”
Alikuwepo na mama yao mdogo, mke wa baba yao mdogo akasema,
“Lakini hapa kuna namna, kwanini Erica alikuwa anang’ang’ania jana kwenda mtoni, hata dada yake alimkatalia ila aling’ang’ania, lazima maneno ya Derick yaaminike maana kwanini ulitaka kwenda mtoni jioni ile?”
Yule mzee nae akaongezea na kusema,
“Kwa mimi naweza kumuamini huyu kijana kwani kwa macho yangu nilimshuhudia huyu binti akimshika huyu kijana na kumbusu”
Lile swala lilifanya wote wazidi kumuangalia kwa mshangao Erica, kiasi kwamba Erica alijilaumu kwa kutokurekodi mazungumzo ya yeye na Derick maana ingemsaidia kwa kiasi Fulani kulalamika, hakuweza kujitetea zaidi kwani huwa hawezagi kujitetea kwahiyo alijikuta akiinama na kuanza kulia.
Ikabidi dada yake ainame akimbembeleza mdogo wake maana alimfahamu vizuri sana, kwakweli hadi wazee walijikuta wakikosa maamuzi kwa muda huo, wakasema wasubiri kesho wafanye maamuzi ila Erica aligoma, alilia sana akimwambia dada yake kuwa anataka aende nyumbani tu. Dada yake akamwambia,
“Erica kulia hakusaidii kitu, simamia ukweli wako ila ukilia utajiumiza bure tu”
Kisha Mage aliinua macho yake na kumtazama Derick kisha akamwambia,
“Yani sikujua kama wewe ni mbaya kiasi hiki, huna vitu vingine vya kufanya zaidi ya kumsingizia Erica eeh!”
“Sasa mimi nimsingizie kwa lipi jamani, muulize kama hakuwahi kutoa mimba yangu, muulize hapo”
Wale baba wadogo walimuangalia Erica kwa masikitiko sana, mmoja akamuuliza,
“Kumbe hadi mimba ulipata na kutoa? Kheee jamani mbona makubwa haya!”
“Tena huyu Erica asitake kuniweka mimi ubaya, hapo alipo ana mtoto ambaye hata hajui baba wa mtoto ni nani sababu alitembea na familia nzima”
Baba wadogo wakashangaa zaidi kwani habari za mtoto walifichwa kwahiyo kubumbuluka huko kuliwashangaza sana, ilibidi wamuangalie Mage ili awaambie ukweli,
“Yani hadi wewe Mage wakutuficha sie kweli!!”
“Tusameheni jamani, tulitaka kutafuta siku maalumu ndio tuwashirikishe kuhusu hili, hata mashangazi wanajua”
“Kwahiyo nao wametuficha? Kweli wanawake mnajuana, ila mficha maradhi kifo humuumbua. Kumbe Erica una tabia chafu kiasi hiki kweli”
Kwakweli Erica alichoka kusikia yale maneno na akaamua kutoa ya kwake ingawa huwa akiongea kama ana hasira hivyo ndio huwa anaonekana hana adabu kabisa,
“Nashukuru sana, mimi ni mwanamke ndiomana nimeonekana malaya sababu nimezaa, sijui unasema nimetoa mimba nashukuru sana. Ila huyo Derick kama wanaume wangekuwa wanapata mimba basi angekuwa na mimba hadi ya pua, sitaki kuongea sana kwaherini”
Erica aliinuka pale alipopigishwa magoti na kuingia ndani kuchukua begi lake, kwakweli baba zake walisikitika sana maana waliona kama kawadharau kitendo cha kuinuka walikompigisha magoti.
Ila Erica alitoka ndani na begi lake tayari kwa kuondoka, ilibidi Mage nae akachukue begi ili waondoke, kisha wakaenda pale kwa baba zao kuwaaga maana Mage asingeweza kumuacha mdogo wake aondoke mwenyewe ikiwa ni yeye aliyemshawishi mdogo wake kwenda kule, ila Yule mzee wa mila aliwaomba wasiondoke kwanza,
“Erica, naomba nikufanyie dawa kwanza. Unaonekana una matatizo sana wewe binti”
“Hapana, sitaki tena dawa yoyote”
Erica aligoma ila dada yake alimbembeleza akubali kufanyiwa hiyo dawa waondoke, kwavile Erica alitaka kuondoka, akakubali kufanyiwa hiyo dawa ambapo Yule mzee wa mila alimpaka paka madawa usoni na shingoni na kumsomea somea maneno pale kisha kuwaruhusu waondoke.
Muda ulikuwa umeenda sana, kwahiyo ilibidi wakapande zile gari zinazofanya safari za usiku kwa usiku yani Erica alitaka afike kwao tu.
 
SEHEMU YA 320

Wakawasindikiza hivyo hivyo kishingo upande, wakafika stendi na kupata basi, kisha Erica na dada yake wakapanda, kwakweli Erica alijihisi gasia sana na zile dawa alizopakwa kiasi kwamba hakutaka kukutana na yeyote anayemfahamu hadi aingie kwao, maana alijihisi kunuka midawa ya kienyeji mwili mzima, ile hali ilikuwa inamkera sana,
“Dada, tukishuka tu itabidi nichukue tax hadi nyumbani”
“Ndio tutachukua gari ila hiyo hali mama akikuona nayo itakuwa balaa, me nadhani tuchukue gari twende kwangu kwanza ukaoge halafu ndio uende nyumbani”
“Ila bora ningepata sehemu hata huku huku ningeoga”
“Haitakiwi kuoga Erica, maana kuna dawa umepakwa kwahiyo hadi kesho”
Kwakweli Erica alikuwa amekereka sana ila kwavile alihitaji kufika nyumbani tu aliona ni afadhali.
Basi gari ile ilitembea usiku kwa usiku, ilivyofika saa saba usiku kuna mahali ilibidi isimame kwa muda kisha kwenye mida ya saa kumi iliendelea na safari mpaka wakafika stendi kuu, ilikuwa pamekucha kabisa tayari maana ilikuwa kwenye mida ya saa moja asubuhi.
Walishuka na moja kwa moja walisogea kwa dereza wa gari za kukodi ili kuongea nae awapeleke wanapohitaji kwenda, wakati wanaongea nae alifika mama kwa Yule dereva akimwambia,
“Kijana nimekuja kukushukuru, umenipa ushauri mzuri sana wa kumpeleka ndugu yangu apande bodaboda awahi basi, na kweli ameliwahi kashanipigia simu kuwa kapanda tayari”
“Aaah usijali mama”
Kisha Yule mama alionekana kama anatoa hela ya kumpa Yule dereva kama asante, wakati huo Yule mama alimuangalia Erica na kusema maana Erica alimpa mgongo kwahiyo hakumuona usoni,
“Mbona umbo la huyu binti kama nalifahamu”
Yule mama akazunguka kwa mbele kumuangalia, akashtuka na kusema,
“Kheee Erica!”
Erica naye alimuangalia huyu mama, alimtambua kwa sauti ila alipomuangalia ndio akamtambua vizuri, alikuwa ni Yule bosi wake yani mama yake na Erick.


Yule mama alimuangalia Erica na kusema maana Erica alimpa mgongo kwahiyo hakumuona usoni,
“Mbona umbo la huyu binti kama nalifahamu”
Yule mama akazunguka kwa mbele kumuangalia, akashtuka na kusema,
“Kheee Erica!”
Erica naye alimuangalia huyu mama, alimtambua kwa sauti ila alipomuangalia ndio akamtambua vizuri, alikuwa ni Yule bosi wake yani mama yake na Erick.
Erica alikaa kimya tu, kisha Yule mama aliendelea kuongea,
“Unanuka madawa ya kienyeji mwili mzima, mmh mtoto mshirikina wewe. Nilijishangaa kukuingiza kazini bila hata usahili kumbe mtoto mshirikina loh!”
Erica akaona ni tatizo pale, akaanza kumwambia dada yake kuwa wafate gari nyingine, ila wakati wanaondoka Yule mama alimvuta Erica,
“Umeshindwa hata kunisalimia kweli!”
“Shikamoo”
“Mpaka niombe Erica! Au mganga wako kakwambia kuwa usiongee na mimi? Ila namshukuru sana Mungu kwa kunionyesha rangi yako halisi, hata nilitaka nikufikirie kidogo ila siwezi kukufikiria tena Erica, wewe ni mchafu sana”
Erica akaona hata akijitetea kwa hali ile hawezi kusikilizwa na Yule mama, hivyo aliondoka tu na kuingia kwenye gari nyingine kisha Mage alipanda pia na kumtaka dereva awapeleke waendapo.
Safari ilikuwa moja kwa moja kwa Mage, ila ambacho hawakujua ni kuwa Mama Erick alikuwa akiwafatilia nyuma na walipofika ndipo aliondoka kwani alijia pale ndio kwakina Erica, basi waliingia ndani na moja kwa moja Erica akajiandaa ili akaoge, dada yake akamwambia kuwa akimaliza kuoga anywe chai kwanza ndipo aende kwao maana hata usiku wa jana hakula, alikubaliana nae na alienda kuoga kwanza ili kwenda kwao akiwa safi na hata mama yake asimshtukie, alipomaliza kuoga, alikwenda kuvaa, wakati anatoa nguo zake kwenye begi aliona kuna kitu kama dawa imeviringishwa kwenye karatasi, alishtuka sana ila hakuelewa imefika fika vipi kwenye begi lake na hakuelewa ni kwanini imewekwa kwenye begi lake ila alivaa na kurudisha vitu kwenye begi lake kisha akataka kwenda kumuuliza dada yake kuhusu hiyo dawa, muda huo aliweka mizigo yake sebleni. Sasa wakati anatoka nje alimsikia dada yake akiongea na shemeji yake na kugundua kuwa shemeji yake ameambiwa kuwa yeye yupo hapo kwake, akamsikia akimwambia mkewe,
“Huyo mdogo wako unadhani namuamini tena! Hata kuja kwangu hapa sitaki, yani mtoto kamuumbua James Yule balaa, ndiomana kazaa mtoto asiye na baba”
“Usiseme hivyo jamani mume wangu, Yule ni mdogo wangu”
“Hata kama, hafai kabisa, hafai kuigwa na jamii. Sasa dada yake akiachana na mume wake yeye atapata faida gani? Na usikute ni yeye katengeneza kila kitu ili James aonekane mbaya, nilikutana na James dah aliongea kwa masikitiko sana, na kilichomuumiza zaidi ni kuambiwa aombe msamaha kwa Yule mdogo wako eti ampigie magoti, kwakweli mimi simtaki hapa kwangu”
Kwakwele Erica akajihisi vibaya sana, kisha akatoka mule ndani na kumsalimia shemeji yake ambaye alionekana kumuitikia ilimradi tu, kisha akamwambia dada yake kuwa anahitaji kuondoka,
“Aaaah subiria mdogo wangu unywe chai”
“Nitaenda kunywa nyumbani, kwaheri dada”
Aliingia sebleni na kuchukua begi lake kisha kuanza kuondoka, hata dada yake alipomsimamisha ili amsindikize hakusimama na muda huo alipofika njiani akasimamisha pikipiki na kupanda kisha akamuelekeza Yule bodaboda ampeleke hadi kwao maana alitaka tu kuwahi nyumbani, sababu moyo wake alihisi kama una fundo vile.
Kwakweli dada yake hakumuelewa kabisa kuwa kwanini kafanya vile, hakujua kama maongezi aliyokuwa akiongea na mumewe yote Erica kayasikia.
 
SEHEMU YA 321



Erica alifika nyumbani kwao akiwa na hasira sana, kwanza sehemu aliyoenda na dada yake na maneno aliyoyasikia toka kwa shemeji yake, aliingia ndani na kumkuta mama yake ambaye alisikitika sana baada ya kumuona, akamsalimia kisha akataka kwenda chumbani ila mama yake alimrudisha nyuma,
“Weee weee rudi hapa, rudi hapa upesi yani huna hata aibu unataka kwenda chumbani? Leta hilo begi lako hapa”
“Kwanini mama?”
“Nimekwambia lete”
Ikabidi Erica ashushe lile begi la mgongoni ampe mama yake, kisha mama yake akamwaga nguo zote za kwenye lile begi, kisha na kile kifurushi cha dawa kilianguka na kumshtua zaidi mama yake ambapo alianza kukishika kile kifurushi, Erica alijaribu kumsihi mama yake aachane nacho ila mama yake hakukubali, alikifungua kile kifurushi na kukuta dawa mbali mbali za kienyeji zikiwa zimeandikwa vitu mbali mbali, nyingine iliandikwa ‘dawa ya mvuto kazini - ya kuweka kwenye mkoba’ ‘dawa ya kumvuta mpenzi aliye mbali - ya kuchoma na kunuiza’ ‘dawa ya mapenzi – ya kujifukiza’
Kwakweli mama yake alimuangalia kwa mshangao Erica,
“Kheee Erica mwanangu kumbe ulienda tena kwa mganga?”
“Hapana mama”
“Hapana kitu gani na uthibitisho huu hapa? Yani umeenda kutafuta dawa ya mvuto kazini? Dawa ya kuvuta mpenzi aliye mbali? Unataka nini wewe ikiwa kijana wa watu anakupenda jamani Erica? Umeenda kutafuta dawa ya mapenzi? Nani amekudanganya kuwa mapenzi yana dawa jamani Erica!”
Mama yake alimpa lawama zote, na kisha kumtaka akae ili aongee nae vizuri,
“Kwanza niambie vizuri ulipoenda na dada yako hadi kupata kilanga cha kumuachisha mtoto ziwa, kupata kilanga cha kulala mbali na mtoto wako, kupata kilanga kushindwa kupokea simu ya mwanaume unayeimba wimbo kuwa unampenda sana, kupata kilanga cha kutafuta dawa zisizoeleweka. Kwanza kabla ya yote ni kwanini ulikuwa hupokei simu ya kijana wa watu?”
“Mama, kuhusu simu niliogopa kutokana na yale maneno niliyoambiwa na Yule mganga kwenye simu, kwahiyo niliogopa asije kupatwa na madhara kweli”
“Akili mbovu kabisa wewe, sasa apatwe na madhara gani?”
“Mama, uliniambia lisemwalo lipo na kama halipo linakuja kwahiyo mimi nikaogopa kitu kibaya kumpata Erick”
“Ila kwanini Erica unapenda kuharibu maana ya maneno, hivi iku ile tumeingia kwenye maombi hadi kuchoma ile leso chanzo ni nini? Chanzo ni maneno mabaya na jinsi alivyokuwa akikufatilia Yule mganga ila tulivunja maneno yake kwa kuchoma kile kitambaa na kukemea, halafu wewe hupokei simu ya kijana wa watu sababu ya ujinga?”
“Nisamehe mama”
“Haya niambie ukweli ulienda wapi na dada yako? Sitaki ujiume ume nataka uniambie ukweli na ukweli mtupu ndio nauhitaji”
“Mama nisamehe ila kiukweli tulienda kwakina baba wadogo”
“Hivi una akili wewe? Kwanini mnifiche mimi na kwanini muende kule? Ni miaka mingapi sijaenda kwa hao baba zenu wadogo? Hivi Erica una akili kweli?”
“Dada alisema twende”
“Aaaah yani huyu Mage huyu. Ya kwake hajamaliza halafu anaanza na mengine, kwahiyo hao baba zenu wadogo ndio wamekupa na hii dawa eeeh!”
“Hapana mama, hata mimi sielewi hiyo dawa imetokea wapi?”
“Punguani wewe, nenda ukaoge huko na hili begi niachie mwenyewe, umeniudhi sana mimi”
Erica alimuitikia mama yake maana alishamuona kuwa kacharuka, kisha akainuka na kwenda chumbani kwake ambapo alienda kuoga tena kama ambavyo mama yake alimwambia, kisha akabadilisha nguo, na kwenda tena sebleni kumuuliza mama yake kuwa mwanae yuko wapi,
“Sasa unadani yuko wapi?”
“Sijui mama”
“Amelala chumbani kwangu”
Basi akaenda kuchukua chakula na kula, gafla mama yake akapigiwa simu na kuanza kuongea nayo, kwa jinsi mama yake alivyokuwa akiongea alihisi tu aliyempigia ni baba yake mdogo na ilionyesha alikuwa akilalamika swala la Erica kuwa na mtoto na wenyewe kutokuambiwa, mama yake alivyomaliza kuongea na simu tu akasema,
“Ujinga mlioufanya na dada yako kwakweli sijaupenda kabisa, ngoja nimpigie simu huyo dada yako”
Mama yake alionekana kumpigia simu Mage na kumwambia kuwa aende nyumbani kwao, ilibidi Mage nae akubali maana alijua tayari ana mashtaka kwa mama yake.
 
SEHEMU YA 322

Baada ya kumaliza kula, Erica alienda chumbani kwake kupumzika na kuamua kulala kidogo kwani alikuwa na uchovu sana, ingawa alijua wazi kuwa mama yao kanpigia simu dada yake ila alitaka dada yake akifika ndio aamke na hadi akiitwa ndio ataenda kusikiliza mamake anachoongea na dada yake, wakati usingizi umempitia vizuri leo akapigiwa simu, akashtuka na kuangalia akaona ni namba ngeni, kupokea ni Mzee Jimmy,
“Kweli kabisa Erica wa kunidanganya mimi mtu mzima na ndevu zangu?”
“Nimekudanganya nini tena?”
“Ulinidanganya kuwa mwanao anaumwa kumbe unanikimbia, sikia Erica sijawahi kupenda mwanamke hivi katika maisha yangu. Ingawa huyo mwanamke ni mama yako kiasi cha kutotaka mimi niwe na wewe ila Erica nakupenda sana, sitaki kukuchezea nahitaji kukuoa. Yani wewe kubali tu nitangaze ndoa na utachagua tufungie wapi”
“Nashukuru sana kwa wazo lako la kutaka kunioa ila mimi nina mchumba wangu nampenda sana, hata bila ya mama na wewe kujuana ila nampenda sana mchumba wangu, ni yeye ndio atakuwa mume wangu, hujui tu siku ile ilikuwaje ila mimi nishamuomba Mungu kuwa mwili wangu huu uwe ni mali ya mume wangu tu, sitaki mwingine wa kuchezea mwili wangu, samahani sana sikutaki, sikuhitaji, nisamehe bure. Nampenda sana mume wangu mtarajiwa”
“Mmmh wewe binti wewe labda nisijue kama unaolewa maana nitahakikisha huolewi”
Erica akaamua kukata ile simu kwani hakutaka kusikia mtu yeyote akimpa vitisho tena kuhusu Erick, kwa muda huo alikuwa akisubiri usiku aongee vizuri na Erick kwenye utulivu maana alijua lazima Erick amechukia kwahiyo alitaka aongee nae vizuri zaidi ili Erick apunguze hasira zake, akaangalia simu yake na kukumbuka kuwa hakuwa na vocha kwahiyo akaamua kwenda dukani kununua vocha.
Aliponunua vocha tu, akashikwa began a mtu akashtuka na kugeuka, akashangaa kumuona Sia, alishangaa sana kwani hakutegemea kumuona mtaani kwao,
“Mbona unashtuka sana, umeona mzimu au nini?”
“Hapana, nashangaa mitaa ya kwetu huku umefuata nini?”
“Kumbe unaishi mitaa ya huku eeh! Huku ni kwetu pia, ila nimefurahi kukuona kuna kitu nataka nikuulize”
“Kitu gani?”
“Hujaongea na Erick kwa siku ngapi?”
“Kwanini?”
“Nilimpigia simu, anaonyesha ana jazba sana. Nikamuuliza tatizo nini anasema ni kwavile hajaongea na wewe, Erica umempa nini Erick na mimi nimpe?”
“Sijampa chochote”
“Erica, nilishakwambia kuwa erick ndio moyo wangu, erick ndio maisha yangu, umempa nini Erick mpaka kuchanganya akili yake kiasi hiki! Mama yangu ni mgonjwa, alihitaji kuongea na Erick ila Erick ananijibu kuwa hawezi kuongea na mama yangu sababu akili yake imevurugika hajaongea na wewe. Limbwata gani Erica umempa Erick?”
“Sijampa chochote ila mimi na erick tunapendana sana”
“Humpendi Erick wewe, ungempenda usingezaa na mwanaume mwingine. Erica kwanini usiende kuwa na mwanaume uliyezaa nae jamani hadi kuwa na Erick kweli? Unanikosesha raha Erica, unaikosesha familia yangu raha, unadhani mama yangu akifa leo lawama nitampa nani kama sio wewe?”
“Utakuwa unanionea Sia, mwenye maamuzi ni Erick sio mimi. Najua nampenda Erick ila bado Erick ana maamuzi kama awe na mimi au la, najua Erick kawa na mimi sababu ananipenda, kwahiyo usinifikirie vibaya”
“Erica, tafadhari naomba uachane na Erick kwa usalama wa maisha ya mama yangu, nakuomba uachane na Erick kabisa, sitaki shida mimi. Nahangaika na mama yangu, hataki kula toka juzi sababu ya kutokuongea na Erick, nadhani unaelewa jinsi gani mama anauma, naomba uachane na Erick”
Erica akaona akiendelea kuongea na Sia hapo wanaweza kugombana bure maana aliona sura ya Sia inavyobadilika na kuwa na gadhabu zaidi, basi aliamua kuondoka tu ila hakujua kuwa alipokuwa akirudi kwao Sia nae alikuwa akimfata nyuma nyuma, hadi anaingia nyumbani kwao hakujua kama Sia alimfatilia hadi kwao ila Erica aliingia tu kwao.
 
SEHEMU YA 323


Alipoingia tu ndani akasikia dada yake akizungumza na mama yake na kujua kuwa dada yake alifika, tena dada yake alionyesha kumwambia habari yote mama yao na hapo alijihisi aibu sana, alipoingia tu mama yake alimuita na kumwambia akae ili asikilize ile habari.
Kwakweli dada yake alikuwa akiongea hadi Erica alikuwa akijihisi aibu, alipomaliza dada yake kueleza akamwambia mama yao,
“Muulize mwanao huyo kama kuna uongo hapo?”
“Eeeh Erica, kuna uongo hapo?”
“Hakuna”
“Ila nilikwambia uniambie ukweli wote wewe mtoto jamani, jioni hii umeumbuka ona sasa!”
“Nisamehe mama”
“Ulivyohodari kuomba msamaha sasa huwa hukumbuki hata ujinga unaoufanya”
Kisha mama yao akamgeukia Mage na kuanza kuongea nae kwa kumfokea,
“Ila na wewe Mage huna akili yani huna akili kabisa, sikutegemea kama unaweza kufanya ujinga wa aina hii. Haya mdogo wako angebakwa na huyo Derick ungepata faida gani? Halafu una uhakika gani Derick ni mtoto wa baba yenu? Mtoto gani haendani tabia na baba yenu hata kidogo eeeh! Huyo Derick ndio alimfanya mdogo wako kuona chuo kichungu halafu mnakaa na kumsikiliza, na wewe unasikiliza na kufanya maamuzi yako. Erica ni mwanangu, kafanya makosa mlete kwangu niambie sijui katembea na kaka yake, ulishawahi kusikia katembea na Tony? Huyo hamjui ndiomana imekuwa hivyo, na hiyo laana ndio ya kuvunja kwa matambiko jamani! Yani na wewe Mage kama sijakulea kwenye dini vile, ulishindwa kuja kuniambia mama hivi na hivi ili niombe halafu unampeleka mdogo wako kwenye matambiko kweli! Sijapenda yani sijapenda kabisa”
“Mama unanilaumu bure, badala umkanye huyo Erica unanilaumu mimi mama jamani. Na huyo mtoto wako wakina bamdogo wamenipigia simu kuwa jana alivyoondoka kwa kisirani vile wamechukizwa sana”
“Kheee usinitibue, wewe na hao baba zenu wadogo kwanza wamenipigia simu hapa nimekorofishana nao tu na wewe usinitibue, ulitaka aendelee kukandamizwa kuwa amemtaka Derick kimapenzi au! Hata kama Derick sio ndugu yake bado sana Erica kumtaka kijana kama Derick, aisee umenitibua leo Mage, ondoka tu nenda kwa mume wako”
Ilibidi Mage ainuke na umuaga mama yake ila mama yake alionyesha kuchukizwa sana, muda huo Erica hakuamini macho yake kuwa mama yake ameamua kuwa upande wake na kumtetea kwakweli alijihisi furaha kiasi.

Basi wakati dada yake ameondoka na yeye akainuka ili kwenda chumbani, ila mama yake aliongea kwa ukali,
“Wewe mjinga, hebu kuja ukae hapa”
Erica alirudi kukaa na kumuangalia mama yake aliyeonyesha kubadilika kabisa sura, kisha akaanza kusema,
“Wewe mjina ulianzaje kutembea na mjinga kama Derick? Kuwa muwazi kwangu, niambie ukweli nikusaidie, usinifiche chochote”
Sababu dada yake alishaelezea mambo mengi ikabidi Erica awe mkweli tu akaanza kumueleza mama yake toka siku aliyotaka kubakwa na wakina George na jinsi Derick alivyomsaidia, akaeleza pia jinsi Derick alivyomuwekea kilevi na kujikuta akilala nae, alimueleza kila kitu hadi walivyokutwa na Mage, yani alimueleza mama yake kila kitu kasoro swala la kutoa mimba tu kwani alihisi lingemchukiza zaidi mama yake.
“Kheee Erica mwanangu kumbe huko chuo ndio ulifikia hali hiyo ya kwenda hadi disco mwanangu kweli!! Ila mimi nilijua siku nyingi sana kuwa huyu Derick ni shetani, ila mwanangu kwanini hupendi kusema unakaa na siri moyoni? Hebu ona vitu walivyoenda kukufanya nab ado amekusingizia ujinga, naomba uniruhusu nikachome zile dawa na zile nguo zako zote zinazonuka madawa”
“Jamani mama”
“Usitake kunifanya nipate kichaa, tena unyamaze kimya, ungetaka kusema jamani mama basi ungeniambia kabla ya kwenda huko kwenye tambiko. Haya njoo unionyeshe nguo zote walizokuwa wakifanya tambiko”
Basi walitoka na lile begin je huku giza likiwa limeingia tayari, Erica alimuonyesha mamake nguo ambazo alimwagia mafuta ya taa na kuzichoma pamoja na ile dawa huku akimtaka Erica amsimulie kilichokuwa kikifanywa kwenye tambiko,
“Ila tuliambiwa ni siri”
“Wewe hakuna siri kwa mama yako, tena uniambie kila kitu usinifiche chochote”
Ilibidi Erica aanze kumsimulia mama yake kutoka mwanzo hadi mwisho, hadi muda aliposikia mwanae anaita bibi kuwa kaamka, basi Erica alienda ili kumpokea mwanae maana ni siku nyingi sana, ila mwanae akampita na kwenda kwa bibi yake ambaye alimnyanyua na kuingia ndani,
“Jamani mama, Angel hanitaki”
“Atakutaka vipi ulimkimbia, hata simu ya uongo na ukweli kuwa nimpigie mwanangu hakuna, atakutaka vipi?”
Erica alijiona kweli ana makosa, hivyo akaamua kuanza kumbembeleza mwanae hadi badae akamkubalia na kukaa nae kwa muda.
Muda wa kulala ulipofika alienda nae chumbani kulala, ila aligoma na kutaka kulala na bibi yake kwahiyo Erica hakuwa na jinsi zaidi ya kumruhusu mtoto wake akalale na bibi yake, kisha yeye kurudi chumbani kwake ambapo aliweka ile vocha na kumpigia Erick na baada ya muda tu Erick alipokea ile simu, kwahiyo Erica alianza kwa kumuomba msamaha kwa kuondoka bila kumuaga huku akimbembeleza na kuongea nae vitu vingi,
“Ila Erica sijapenda kwa simu yako kupokelewa na mwanaume, kwakweli sijapend kabisa, Erica hujawahi piga simu yangu ikapokelewa na mwanamke na kwanini mimi unifanyie hivi?”
“Nisamehe Erick”
“Na mwanaume anajitapa kabisa kuwa ni mtu wako, Erica kwanini unifanyie hivi? Au ni sababu nimekwambia swala la ndoa mimi na wewe mpaka niweke mambo sawa”
“Hapana Erick sio hivyo, nakupenda sana hata sielewi huyo mtu aliyepokea simu alikuwa na maana gani.”
Erica alitumia njia ya kumbembeleza sana Erick na mwisho wa siku Erick alimuelewa kisha akamuuliza jambo lingine,
“Je kuna siku ambayo dada yangu amekusumbua tena? Au kipi kingine kilichokusumbua?”
“Kinachonisumbua ni mwanamke wako Sia, kila akikutana na mimi ananitaka mimi niachane na wewe na kusema kuwa yeye hawezi kuachana nawe, nahisi utatuoa wawili yani moyo unaniuma sana ila huwa siwezi kubishana nae. Erick, wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho, nakumbuka ulisema kuwa unaachana na wanawake zako wote, hivi kama huyu Sia ungekuwa umeachana nae, hivi angewezaje kunitishia mimi niachane na wewe”
“Erica, huyo mwanamke hana akili tu yani anajua ukweli kuwa nakupenda wewe ila yeye anajifanya ni king’ang’anizi, ila simtaki”
“Kama humtaki mbona huwa unawasiliana nae?”
“Huwa ananitafuta mwenyewe sasa”
“Mwambie huwezi kuwasiliana nae tena, sitaki anipe vitisho najua mimi na wewe tunapendana”
“Sawa malkia wangu”
Basi Erica aliongea kwa furaha sana na Erick na kisha kuagana na kulala.
 
SEHEMU YA 324


Kesho yake Erica aliamka na kufanya mambo yake ya hapa na pale, kisha kwenda kumchukua mwanae, ila muda huo wa asubuhi akapigiwa simu na Erick tena, kwahiyo akapokea na kuongea nae,
“Erica, Yule mtu wa kazi alikutafuta ila ndio ulikuwa hupokei, alitaka akutafute leo ila nimemuomba akutafute Jumamosi ili Jumatatu ukaanze kazi, sawa”
“Ila hata leo angenitafuta kusingekuwa na tatizo, niko tayari kuanza kazi”
“Aaah pumzika kwanza, kaa kidogo na mtoto na utaenda tu kufanya kazi, usiwe na haraka”
Basi akaongea nae na kukata simu, kisha muda huo huo akaona ujumbe toka kwa Rahim akaufungua na kuusoma,
“Erica, hutaki kuingia kwenye mtandao, hutaki kuongea na mimi ila unachokifanya kitakutokea puani. Mwezi ujao narudi nakuja kumchukua mtoto wangu”
Kwakweli bado kidogo akili imruke baada ya kusoma ujumbe huo ila kwavile alikumbuka mama yake alimwambia kila kitu awe anasema ikabidi aende kwa mama yake kumueleza kuhusu ujumbe aliopokea kutoka kwa Rahim, akamsikiliza mama yake atakachosema,
“Erica mwanangu usiwe na mashaka, ila lazima uwaze maana mtoto ushamuuza kwa mwanaume mwingine, yani hayo ndio makosa uliyoyafanya bila kunishirikisha. Ni kweli wanaume huwa wanakera sana ila si vizuri kuuza mtoto kwa baba mwingine, labda kama baba wa mtoto alimkataa”
“Ila mama hata Rahim alimkataa Angel”
“Ila alikuwa akimuhudumia mwanzoni, kuna wanawake huko amebeba mimba tu anamwambia mwanaume ila mwanaume anasema sitaki uniambie habari hizo, hiyo mimba siijui, kwahiyo wewe ulipata bahati sana. Hata alibadilika labda kuna kitu alifanyiwa maana wanaume ni wahuni sana na uhuni wao wakikutana na wanawake waliojichokea akili huwa wanawakorogea dawa basi hapo ndio anakuwa mbogo na wala haelewi kitu. Kosa lako wewe ni kuuza mtoto tu”
“Sasa mama nitafanyaje?”
“Hebu tulia kwanza, yani usiwe na presha wala nini, anaanzaje kufika tu na kuchukua mtoto? Kuna taratibu, na hata hivyo mtoto hachukuliwi kwa mama hadi afike miaka saba, ila una uwezo wa kukataa, wanasema mtoto ni wa baba ila kiukweli mtoto ni wa mama yani mama anaouwezo wa kufanya chochote kwa mtoto, usiwe na mashaka mwanangu. Kesho nitakwambia cha kufanya ila kwasasa kuwa na amani kwanza”
Basi Erica alisikiliza ushauri wa mama yake na kuendelea na mambo mengine kwa siku hiyo.

Usiku kama kawaida aliwasiliana na Erick, ila leo alimpa habari iliyomfurahisha kidogo,
“Erica, Yule Sia hatokusumbua tena, nishamalizana nae, nahitaji kuwa nawe Erica”
“Nimefurahi sana kusikia hivyo”
“Halafu mwezi ujao narudi, Erica lazima nikuoe kwahiyo usijali kitu yani lazima tuishi wote”
Kwakweli Erica alifurahi sana kwani jambo hili lilimpa raha vilivyo.
Akalala huku akitabasamu, kulipokucha alisikia kelele nje ya nyumba yao na kumfanya ashtuke na kutaka kutoka, akakutana na mama yake ambaye pia alikuwa akitoka maana zile kelele alizisikia, walishangaa kuona kuna binti akijigalagaza na kulala kwenye uwanja wao, ikabidi mama Erica na Erica wamsogelee binti Yule ili kumuuliza kuna nini, walipomsogelea na kumuinua na kumuuliza, binti aliinua kichwa na Erica alishtuka sana kwani alikuwa ni Sia halafu alisema kwa uchungu,
“Erica umeniulia mama yangu”
Hata mama Erica alishangaa kusikia vile.
 
SEHEMU YA 325



kulipokucha alisikia kelele nje ya nyumba yao na kumfanya ashtuke na kutaka kutoka, akakutana na mama yake ambaye pia alikuwa akitoka maana zile kelele alizisikia, walishangaa kuona kuna binti akijigalagaza na kulala kwenye uwanja wao, ikabidi mama Erica na Erica wamsogelee binti Yule ili kumuuliza kuna nini, walipomsogelea na kumuinua na kumuuliza, binti aliinua kichwa na Erica alishtuka sana kwani alikuwa ni Sia halafu alisema kwa uchungu,
“Erica umeniulia mama yangu”
Hata mama Erica alishangaa kusikia vile.
Ilibidi mama Erica amuinamie vizuri Sian a kuongea nae,
“Hebu ongea taratibu binti nikuelewe”
“Erica kaniulia mama yangu”
“Sasa usipayuke hivyo nyumbani kwangu, utanijazia watu, Erica kamnyonga huyo mama yangu, kamtilia sumu au kamfanya kitu gani hadi useme kamuua?”
Sia alikuwa akilia tu, ilibidi mama Erica amuinue na kumuingiza ndani maana pale aliona angemjazia watu, na angemjazia watu kweli jinsi alivyokuwa akilia kwa kisirani, alipomuingiza ndani ndipo alipoanza kumuuliza tena,
“Hebu ongea taratibu binti nikuelewe, mimi ndio mama wa huyu Erica unayesema kakuulia mama yako, nataka kujua kamuua vipi? Maana nipo na Erica usiku wote, sasa katoka muda gani kuja kumuua mama yako?”
Sia alikuwa akilia tu, kisha mama Erica akamwambia tena,
“Lia, ukimaliza utanieleza vizuri maana sikuelewi (Halafu akamuangalia Erica na kumuuliza) Au wewe unamuelewa?”
“Simuelewi pia mama”
Hapo ndipo Sia alipoibuka na hasira, akasogea karibu na Erica na kumzaba kofi, mamz Erica akamrudisha nyuma na kumpa onyo,
“Wewe binti usitake kunipandisha kichaa change, na mimi ni kichaa kama wewe. Nishakwambia mimi ndio mama wa Erica, huyo Erica kakuulia mama yako vipi? Unainuka na kumpiga mwanangu kofi, sasa mimi sitajali umefiwa wala nini, nitakusambulia hapa uione dunia chungu, haya sema sasa Erica kamuua vipi mama yako”
“Anajua mwenyewe, ila Mungu atanilipia nashukuru sana”
Akainuka na kutaka kutoka pale kwakina Erica, ila mama Erica akamzuia na kusema,
“Wewe ungekuwa na haja ya kuacha Mungu akulipie sidhani kama ungefika hapa kwangu na kupiga yowe, nahitaji kujua tatizo ni nini? Nahitaji kujua mwanangu huyu kaanza lini uuwaji? Huondoki hapa bila ya kunieleza kwakweli”
“Unanionea tu wakati mimi nina uchungu, ni hivi mama yangu ni mgonjwa sana na Erica anajua hilo, mama yangu huwa nafuu yake ni kuongea na Erick, nampenda sana Erick ni mpenzi wangu na tumekubaliana kuoana, mama anatambua hilo hata marehemu baba yangu anatambua hilo na kabla ya kifo chake alinipa baraka zote za kuolewa na Erica, sasa huyu Erica kamwambia Erick asiongee na mimi wala mama yangu wakati anajua ni mgonjwa sana, hivi tunavyoongea mama yangu yupo kwenye hali mbaya sana, toka jana Erick amegoma kuongea na mama, na mama yangu anakufa ila chanzo ni Erica”
“Kwahiyo huyo mama yako bado hajafa ila yupo kwenye hali mbaya?”
“Ndio mama yangu yupo kwenye hali mbaya sana, hakuna matumaini ya kupona”
“Kwahiyo mamako akiongea na Erick ndio atapona?”
“Ndio”
Huku akiendelea kulia, ila mama Erica alimtuliza na kumwambia,
“Sasa hukutakiwa kuja na kupiga kelele mlangoni kwangu, mambo kama hayo ulitakiwa kuongea kuwa ni hivi na hivi na hivi unaeleweka sio kupiga kelele sijui Erica kaniulia mama yangu sijui nini na nini haipendezi, hivi watu wangejaa unadhani ingekuwaje na wangemfikiriaje Erica? Haya nenda kwa mamako na Erick atampigia simu muda sio mrefu, kwaheri”
basi Sia alitoka na kuondoka zake, mama Erica hakuongea chochote na Erica ila alienda humbani kwake na kuchukua simu yake kisha kumpigia simu Erick, kwakweli hata Erick alishangaa siku hiyo kupigiwa simu na mama yake Erica, basi alipokea na kumsalimia ila kabla Yule mama hajaitikia salamu akamwambia Erick,
“Wewe kijana fanya majukumu yako, unajua kuna mama anayetegemea simu yako kwa maisha yake, mpigie simu mama huyo, usimtafutie mwanangu matatizo, kwaheri”
Mama Erica akakata simu kisha akarudi sebleni.
 
SEHEMU YA 326

Muda amerudi sebleni Erica alikuwa ameenda chumbani, akamuita kwa ukali sana, ikabidi Erica aende kumsikiliza mama yake,
“Hivi Erica, hukuona wanaume wengine au nini? Ni raha gani ya kugombea mwanaume? Sipendi kitu kinaitwa kugombea mapenzi jamani, sipendi kabisa. Kwanini mapenzi yapo hivi lakini? Erica umeshindwa kabisa kupata mpenzi wako peke yako hadi mpenzi wa kugombea hadi uambiwe umeua mama wa watu sababu ya kugombea mapenzi Erica?”
“Mama, kiukweli nampenda Erick, nampenda sana”
“Hivi unajua kupenda wewe, nakuuliza unajua kupenda? Huyu Erica sio ndio Yule kijana aliyekusababishia matatizo wakati upo shuleni kweli?”
“Ndio yeye mama”
Mama yake akamnasa kibao pia na kumwambia,
“Nimekupiga kwa uzembe, yani mwanaume aliyekusababishia matatizo shuleni umeamua kumkubali hadi mtoto kumuuzia, hivi wewe Erica ni mjinga kiasi gani? Huyo Erick ana nini cha zaidi huyo hadi mtu afike na kugalagala hapa ooh Erica ananiulia mama yangu, sijui nishaahidiwa Erick ndio mume wangu, haya na wewe uliahidiwa na majengo ya shule yenu ile kuwa Erick ndio mume wako?”
“Hapana mama”
“Kuanzia leo sitaki kusikia habari za huo uchafu wa kuitwa Erick, tulia wewe mtoto upate wako, mbona mwanangu wewe ni mzuri tu unahangaika na nini jamani? Erick, Erick ndio nani yeye, ni mwanaume pekee duniani? Mbona kuna wanaume wengi sana”
“Ila mama nampenda Erick”
“Unampenda ila yeye hakupendi, kashamuahidi msichana wa watu atamuoa, sasa wewe atakuweka wapi? Mbona hujiongezi jamani!”
“Ila mama Erick ananipenda pia”
“Nimekwambia sitaki kusikia habari za Erick kwenye nyumba yangu, sijui habari za Bahati sitaki kusikia, maana kasikia raha kuendeshwa na madawa huko, sitaki kusikia habari zake”
“Sasa mama niwe na nani?”
“Usiniulize mie, unataka nikufanyie chaguo la wa kuwa nae? Kwanza tushughulike swala la Angel maana tayari ushamuuza kwa huyo Erick kumbe ana mwanamke kashaahidiana nae huko hadi kuoana, sitaki kumsikia huyo Erick, maana kashanitibua tayari”
Kwakweli leo ilikuwa siku mbaya kwa Erica, yani hakuamini kama mama yake mwishoni angefikia maamuzi ya kutokumtaka Erick, aliinuka na kwenda chumbani kwake, akawaza sana na kufikiria kuhusu Erick, hakika alimpenda sana yani moyo wake aliona ukijaa kuhusu Erick tu kwahiyo swala la kuambiwa kuwa Erick asisikike mule ndani kwao lilimpa ukakasi sana.
Aliingia ndani na kulala tena yani hata kuoga hakwenda kuoga, ilimbidi mamake ndio amuogeshe mtoto amlishe na abaki akicheza cheza nae.
 
SEHEMU YA 327


Jioni ya siku hiyo, mama yake Erica aliamua kumuita mwanae maana hakumuelewa kwani hakula kabisa siku hiyo na alipomuita alijibu kuwa hajisikii kula, mama yake akasema,
“Yani sababu ya Erick ndio hadi kula umesamehe, masikini mwanangu, huyo Erick kakupa nini eeeh! Huyo Erick ana nini ambacho wanaume wengine hawana”
“Mama hujui tu, nampenda Erick, nampenda sana”
“Katika maisha yako hujawahi kupenda mwingine zaidi ya Erick?”
“Sijawahi mama”
“Kwahiyo ulikuwa unatembea nao tu, ukamaliza familia nzima kutembea nayo bila kuwapenda, ukatembea na mtu hadi ukazaa nae bila kumpenda, hivi inaingia akilini hiyo? Erica eeeh! Hebu niambie labda mimi sijui, Erick ana nini ambacho wanaume wenzie hawana?”
“Mama, nampenda tu naomba niruhusu niwe na Erick”
“Haya kuwa nae ila baada ya wiki mbili unijibu kuwa Erick ana nini ambacho wenzie hawana”
Kitendo tu cha mama yake kumruhusu kuwa na Erick kilikuwa ni kitendo cha furaha sana kwake maana alihisi kama kadhulumiwa nafsi kwa kuambiwa kuwa aachane na Erick wakati anampenda sana.
Kwahiyo muda huo alifanya shughuli zake zingine na kula, hadi muda wa kulala ulipofika. Leo mwanae alikubali kwenda kulala nae, kumbe alikuwa na nia zake, alitaka kuongea na Erick, kwahiyo ikabidi Erica apige simu na kumpa Angel aongee nae, alipomaliza akaichukua yeye sasa na kuanza kuongea nae,
“Erica, niambie ni nini kimetokea leo?”
Ikabidi Erica amsimulie jinsi Sia alivyofika nyumbani kwao na jinsi alivyokuwa akilia lia,
“Poleni Erica, najua ni kosa langu ila naomba mnisamehe sana. Erica, kipindi umeniacha sikujielewa yani sikujielewa kabisa, nimeanza kunywa pombe sababu yako Erica, nikawa na wanawake wengi sababu yako ndio mwisho wa siku hadi nikaangukia kwa Sia, ila yote nilikuwa natafuta penzi la dhati kuwa labda kuan mahali nitapenda kama ninavyokupenda wewe, ila sijaweza Erica, na watu hawa wamekuwa wagumu kuelewa kama siwapendi maana zamani nilikuwa nawaigizia kuwa nawapenda, Erica nilifanya yote haya kupata unafuu wa moyo, Erica nimeanza kukupenda muda mrefu sana, siku ya kwanza kukuona tu nilikupenda na wala sio kwamba nilikutamani, hapana ila nilikupenda. Erica, nakuomba vumilia tu kwa yote yanayotendeka ila upendo wetu ubakie vilevile, tuendelee kupendana siku zote za maisha yetu”
“Erick nakupenda, sitamani chochote kitenganishe mapenzi yetu, ni kweli naumia sana kuhusu wanawake zako wa nyuma ila ongea nao vizuri wasinifanyie fujo, Sia anadai uhai wa mama yake unategemea simu yako wewe”
“Yule nae aniondolee wazimu mie, nitashika uhai wa mama yake mimi nimekuwa Mungu? Wale wajinga sana, badala wampeleke mama yao hospitali eti wanasema akiongea na mimi ndio atapoan, balaa likiwashika ndio atakumbuka maneno yangu niliyokuwwa nikimwambia kuwa tatizo sio mimi ila mpelekeni hospitali huyo mama, oooh ukiongea nae ndio anapona, jamani mimi nimekuwa malaika hadi nisaidie watu kupona? Nimekuwa dakari? Huwa siwaelewi kabisa”
Basi Erica alikuwa akifarijiana tu na Erick na kujisikia amani sana kwa kufanya hivyo kwani aliona kupata amani ya moyo, hadi wanaagana alikuwa na furaha sana.
 
SEHEMU YA 328

Zilipita siku tatu, ilikuwa ni jioni wakati mama Erica akifagia uwanja wake, akashangaa kumuona tena Sia, na leo alivalia nguo nyeusi huku macho yakiwa mekundu kweli kweli, kwakweli mama Erica alihisi kuna jipya linazuka tena muda sio mrefu, ikabidi amuulize kulikoni, ila Sia alimsogelea mama Erica akamkumbatia na kulia sana, Yule mama akamuuliza kuwa imekuwaje,
“Mama yangu amekufa kweli, sina mama mimi. Liwazo langu kaondoka”
Akaendelea tena kumkumbatia mama Erica akilia, ikabidi mama Erica amuulize,
“Tatizo ndio lile lile la Erick kutokuongea na mama yako ndio kasababisha kifo au nini?”
“Hapana mama, Erick alikuwa akiongea vizuri kabisa na mama yangu hata leo asubuhi kaongea nae ila hali ya mama imebadilika jioni hii wakati tunatafuta usafiri tumuwaishe hospitali mama alikuwa ameshakufa”
Akaendelea kulia, ikabidi mama Erica aanze biashara ya kumbembeleza, kisha akaenda ndani kwake na kujivika kanga vizuri na kumuaga Erica,
“kuna msiba wa gafla umetokea ndio naenda”
Hakumpa Erica maelezo ya kutosha ila aliyoka nje na kuongozana na Sia kwenda msibani.
Alifika pale msibani kisha sia kwenda kuungana na ndugu zake wengine wakiendeleza vilio, Mama Erica aliingia nae ndani na kutoa pole kisha akatoka nje ili kuungana na wanawake wengine katika shughuli za pale kama kuandaa chakula na kuweka sawa mazingira ya msiba maana msiba hauna ugeni, aliwakuta wanapika chakula cha watu kwa usiku wa siku hiyo, sema hapakuwa na wamama wengi sana sababu msiba ndio umetokea siku hiyo hiyo, hadi mama Erica akaauliza,
“Mbona watu si wengi?”
“Aaah kwani na wenyewe walikuwa na tabia ya kushtuka msiba ukitokea basi? Baba yao ndio alikuwa hodari na alipokufa basi tena ila wat wengi watakuja siku ya mazishi”
wakati wanapika pika na wanawake wa pale wakaanza kuongea wakiongea,
“Yani hawa watoto akili zao jamani ni mbovu tu, mama yao anaumwa siku nyingi badala wampeleke hospitali eti atapona tu”
Mwingine akadakia,
“Mimi nilikuwa nikimkuta kazidiwa, nikiwaambia habari za hospiatali wanasema wana dawa zao”
“Kwanza cahanzo cha ugonjwa wa mama yao ni nini?”
“Huyu mama tangu mumewe amekufa basi na yeye akaanza kuumwa, ila kipindi hiki ndio vikachachamaa ila watoto wanadai wana dawa zao”
“Dawa gani hizo? Mbona mama yao kafa sasa kama wana dawa zao?”
“Yani watoto wajinga wale, sijui dawa gani wenyewe. Nakumbuka miaka miwili iliyopita kulikuwa na kijana mmoja anabadilishaga magari Yule mvulana, kazuri zuri hivi, ndio alikuwa anakuja na kumpeleka Yule mama hospitali hadi akawa anaendelea vizuri ila nimeshangaa mwaka huu toka uanze ukimkuta kazidiwa unajibiwa kuwa kuna dawa zake”
“Unajua hospitali ni muhimu sana, hata kama unatumia dawa za kienyeji ila nenda hospitali kwanza ujue unaumwa na nini, hata waombeaji wenyewe huwa wanasema kapime kwanza, maana ugonjwa ukijulikana ni rahisi zaidi tofauti na ugonjwa usipojulikana”
Mama Erica alisikiliza kwa makini sana na kugundua kuwa pale kulikuwa na tatizo licha ya Yule mama kuugua hadi kufa ila kulikuwa na tatizo.
Basi mama Erica alishughulika pale kisha alipoona usiku umeingia sana akaamua kuondoka kidogo kurudi nyumbani kwake maana asingeweza kulala hapo msibani kwani hata kwake hakutoa maelezo ya kutosha.

Alimkuta Erica akiwa sebleni tu maana ilikuwa ni usiku tayari. Erica alimsalimia mama yake kisha kumuuliza kuwa alikuwa akiwahi kwenye msiba wa nani maana alimwambia tu kuwa anaenda msibani,
“Nilienda kwenye msiba wa mama wa mke mwenzio”
“Mama wa mke wmenzangu? Kivipi?”
“Mama yake na Sia amekufa”
“Kheee mamake amekufa, masikini jamani”
“Hiyo kusikitika ya leo mbona haikuwepo siku ile Erica eeeh!!”
“Jamani mama! Lazima nisikitike maana si kitu nilichokitarajia, mbona niliongea vizuri na Erick kuwa awe anampigia simu mara kwa mara mama yake Sia, jamani mama wa watu amekufa! Inamaana Erick alikuwa apigi simu?”
“Hebu wewe nawe nitolee ujinga mie, huyo Erick ni daktari kusema akipiga simu anasema watumie dawa Fulani au nini? Erick ndio malaika mtoa roho kusema huyu nimchukue sasa au nini, hebu nitoleeni balaa, sema uzuri hujawa chanzo tena cha kifo cha huyu mama. Nadhani kifo chake kilifika ila kama kawaida wanadamu hutafuta sababu tu, mwishowe wakuchukie bure.”
Erica alibaki kusikitika tu, kisha akaenda chumbani kwake na kumpigia simu Erick ila simu yake haikuwa na salio, yani pale alipata mawazo sana kwani alihitaji haswa kuongea na Erick, akawaza akaona ni vyema akanunue vocha ili ampigie na kuongea nae, akatoka chumbani kwake na kujifunika kanga, ila mama yake alikuwa sebleni na kumuuliza,
“Haya saa hizi unataka kwenda wapi?”
“Nataka kwenda dukani mama kununua vocha”
“Hapana, siwezi kukuruhusu uende dukani muda huu, Erica mwanangu kumekuwa na matukio kwako yasiyoeleweka kabisa, hivi naanzaje kukuruhusu kwenda dukani eeeh! Ngoja kesho utaenda”
“Jamani mama”
“Nimesema leo hutoki, umenisikia? Wewe jione ni mtu mzima ila mimi nakuona bado ni mdogo sana, leo hutoki kwenda popote muda huu”
kisha mamake akaenda kufunga mlango na kwenda na funguo chumbani kwake, kwahiyo Erica hakuwa na namna yoyote ile zaidi ya kurudi chumbani kwake, ila alikuwa na mawazo sana hadi hakuwa na raha sababu alitamani sana muda huo aongee na Erick na hakujua ni kwanini Erick hakumpigia simu siku hiyo.
Alipokuwa amekaa na mawazo chambani kwake muda kidogo akapigiwa simu na namba ngeni, Erica alipokea simu hiyo kwani alikuwa na mawazo sana na Erick, kwani alikuwa akidhani mtu akimpigia simu ni Erick ingawa alikuwa akiona kabisa ile namba si namba ya nchi aliyokuwepo Erick, alipokea na kuongea nayo na kugunduwa kuwa mpigaji ni mzee Jimmy,
“Kheee bado unanifatilia wee mzee?”
“Naachaje kukufatilia Erica eeeeh! Katika maisha yangu sijawahi kumpenda mwanamke yoyote kama ninavyokupenda wewe, usisikilize maneno ya mama yako, nikubali mimi na huyo mwanao ataishi maisha mazuri kama jina lake”
“Asante kwa hayo maisha mazuri ila mimi nimeridhika”
“Erica, nishaiambia familia yangu yote kuwa nataka kuoa na wote wamenikubalia, niruhusu nikuoe Erica”
“Unajua unanichosha yani unanichosha sana, huwa sipendi hata kukusikia ukiongea kwenye simu unanichosha balaa”
“Erica, pole kwa kukuchosha. Naomba unisamehe, nifanye nini ili unisamehe?”
Erica akakumbuka kuwa anahitaji vocha, alijikuta tu akimuambia,
“Nitumia vocha”
“Hilo tu Erica? Niambie kitu gani tena?”
“Nitumie vocha nina shida nayo”
“Nikutumie ya shilingi ngapi?”
“Ya elfu tatu”
“Sawa nakutumia Erica, nakupenda sana umechanganya akili za mtu mzima mimi”
Basi Erica akakata ile simu na baada ya muda mfupi vocha iliingia kwenye simu yake, kuangalia ilikuwa ni vocha ya elfu hamsini, akatabasamu kisha akabonyeza namba za Erick na kumpigia, ambapo simu iliita bila kupokelewa, alipiga kama mara tatu na sim haikupokelewa, alikuwa na mawazo sana maana sio kawaida kabisa, hakuwa na ugomvi mkubwa na Erick wa kusema ashindwe kupokea simu, akashangaa sana, alikaa kama lisaa lizima, yupo macho tu akajaribu tena kupiga simu muda huu Erick alipokea simu ya Erica, ila Erick aliongea katika hali ya ulevi sana, mpaka Erica akamshangaa,
“Erick umeanza tena kunywa pombe kiasi hiko kweli? Si ulisema ulevi ulianza sababu yangu, leo vipi upo na mimi na unakuwa mlevi?”
“Erica huelewi tu”
“Sielewi nini sasa”
Erick alikuwa hata kujibu hajibu vizuri sababu ya kulewa hadi Erica aliamua kukata simu kwa hasira, huku akichukia sana moyoni, alihisi Erick kuna mwanamke mwingine anamsumbua ndiomana kaamua kunywa pombe, alijikuta akiumia sana yani siku hiyo hakuweza kulala kabisa.
Kwa kukosa usingizi hadi aliamua kuingia tena kwenye mtandao wa kijamii baada ya kipindi kirefu sana tangu alipogombana na Rahim, na alivyoingia tu alikutana na jumbe kadhaa za Rahim zikimpa lawama tu, kisha muda huo huo Rahim alituma tena ujumbe,
“Erica, leo umeingia mtandaoni siamini”
“Nipo”
“Habari Erica, mtoto anaendeleaje?”
“Leo ndio umejua kuwa una mtoto na mimi? Wewe si ulijifanya kunijibu shombo wewe?”
“Erica, una matatizo wewe sio bure, kwani hujui kosa lako la mimi kuwa vile? Hivi unawezaje kumuomba mwanaume milioni kumi na tano? Kuna mwanaume kichaa anayeweza kufanya hivyo? Hakuna mwanaume wa kukupa hela hiyo hata awe na hela kiasi gani”
“Si kweli Rahim, ungekuwa na malengo na mimi ungenipa. Najua hiyo hela uwezo nayo unao, na hata kama ungekuwa huna ungeniambia kiustaarabu ila sio kwa majibu yal uliyonipa, sikufurahishwa nayo kwakweli”
“Sawa, hukufurahishwa nayo ila namtaka mwanangu Erica”
“Usinichanganye, unamtaka mwanao kivipi? Mama yako mwenyewe alikuja hapa na hata kurudi tena hajataka, na mtoto mwenyewe alikuwa na mashaka nae kuwa si wa kwako halafu wewe unamuhijtaji mwanao kwa kigezo kipi haswa?”
“Unajua fika Yule ni mwanangu, yani hata uongee vipi ila ukweli unaujua kuwa Yule ni mwanangu, sikukutuma uje kwangu ila umalaya wako ndio uliokuleta kwangu, hadi ukadanganya kwenu kuwa unasafiri wakati unakuja kulala na mimi sababu ya umalaya wako na mimba ukabeba ukijua nitakuoa, ulibugi kwakweli kwani siwezi kuoa mwanamke kama wewe”
“Yani leo hii Rahim ndio unaniita malaya? Kwahiyo mtoto umezaa na malaya?”
“Erica, unajua sipendi kuongea sana, namtaka mwanangu. Ndio wewe ni malaya, kwani nani hajui hilo? Wewe mwanamke hufai ndiomana hata wazo la kukuoa halikuwepo katika akili yangu”
“Ulivyokuwa unaniambia unanipenda?”
“Nilikuwa nawe ili kupoteza muda tu, nilikwambia vile ili uniamini ila kiukweli wala sikukupenda. Mwanamke gani wewe, nasikia ulitembea na familia yangu nzima, na atakayekuoa wewe atakuwa chizi, hakuna mwenye akili timamu atakayemuoa mwanamke wa dizaini yako, na hata huyo mtoto namtaka tu ila sijui kama naye hajanitia aibu maana mtoto wa nyoka ni nyoka”
“Kwahiyo ndicho ulichotaka kuongea na mimi hicho mtandaoni kuwa kila siku ingia mtandaoni kumbe ndio ujinga huo unataka kuniambia?”
“Sio ujinga ila nakwambia ukweli, kawaida wanaume kuwa na wanawake wengi ila mwanamke kuwa na wanaume wengi kwa hakika huyo mwanamke hafai kwenye jamii, Erica huwezi kuolewa wewe kamwe, maana mtu akijua tu tabia yako atakuacha”
Erica alichukia sana na kutoka kwenye mtandao wa kijamii huku akianza kutokwa na machozi na kuitathmini tabia yake, ila alihangaika kote kutafuta penzi la kweli, alijiona mjinga sana kuhangaika na wanaume waliomwambia kuwa wanampenda kwa kumsanifu tu.
“Hivi mtu unawezaje kujifanya unampenda mtu wakati humpendi? Kweli kabisa leo hii huyu Rahim ndio ananiambia maneno haya jamani? Kuna uwezekano mkubwa sana wa wote waliosema wananipenda kumbe hawanipendi wala nini? Ni nani anayenipenda kweli? Hivoi Erick ananipenda kweli au na yeye atanigeuka siku moja kama leo alivyolewa? Lakini hapana Erick ananipenda bhana, nayachukia mapenzi, sijui kwanini yapo.”
Kiukweli siku hiyo hakulala kabisa kwani alijikuta akiwa na mawazo mengi sana mpaka asubuhi.
 
SEHEMU YA 329


Mama yake alijiandaa mapema kwenda msibani na kumuaga Erica pale kwani kulikuwa na hati hati kuwa wanaweza kuzika siku hiyo, basi akaondoka zake na Erica kurudi chumbani kwake.
Alifika msibani na kweli alikuta kuna mipango ya mazishi siku hiyo wakashugulika na kazi za pale kisha kwenye mida ya saa sita walienda kuzika na kurudi tena pale nyumbani, alimuona Sia ameongozana na binti mwingine ambaye sura ilimjia jia kuwa anamfahamu, walipofika karibu yake ndio akagundua kuwa Yule binti ni Tumaini ambaye alikuwa akijua ni rafiki wa Erica, muda huu Sia alimsogelea tena mama yake Erica na kumkumbatia kwa kilio,
“Mama yangu hayupo tena, nimebakiwa na Erick tu”
Basi mama Erica alikuwa akimbembeleza lakini hakuelewa ni kwanini alikuwa akiyasema yale aliyokuwa akiyasema, basi Tumaini nae akasogea karibu na Yule mama ili kumsalimia, na alipomaliza kumsalimia tu akamwambia,
“Familia tunamtambua Sia, familia tunamtaka Sia kuwa mke wa Erick, nakuomba mama mwambie Erica akae mbali na Erick maana hatumtambui”
Kwakweli mama Erica alikuwa akiwashangaa sana wale mabinti, hakufikiria kama wangeleta habari hizo msibani, muda huo huo Tumaini akamwambia mama Erica kuwa anaenda kumuita na mama Erick ili amwambie jinsi Erica wasivyomtaka kwenye familia yao, ila muda ule ule Sia alifatwa na mama yake mdogo ila alipofika pale alianza kumshangaa mama yake Erica na kusema,
“Kumbe ni wewe!”
Walitazamana kwa muda na kujikuta wakikumbatiana kwa furaha.


Kwakweli mama Erica alikuwa akiwashangaa sana wale mabinti, hakufikiria kama wangeleta habari hizo msibani, muda huo huo Tumaini akamwambia mama Erica kuwa anaenda kumuita na mama Erick ili amwambie jinsi Erica wasivyomtaka kwenye familia yao, ila muda ule ule Sia alifatwa na mama yake mdogo ila alipofika pale alianza kumshangaa mama yake Erica na kusema,
“Kumbe ni wewe!”
Walitazamana kwa muda na kujikuta wakikumbatiana kwa furaha.
Kisha wakaenda pembeni kuzungumza, kwahiyo Sia alibaki mwenyewe pale akishangaa tu kuwa watu wale wamejuana vipi, wakati huo Tumaini nae alifika na mama yake Erick ila hawakumkuta mama Erica, Tumaini akamuuliza Sia kuwa mama Erica ameenda wapi,
“Muda ule ule alifika mama yangu mdogo, sasa sijui wanafahamiana vipi, wakachukuzana na kuondoka”
Ikabidi Tumaini aombe radhi kidogo kwa kumsumbua mama Erick, kisha akamwambia,
“Ila mama usijali, napafahamu kwakina Erica, au nikupeleke muda huu?”
“Hapana, saivi kuna mahali nataka kwenda, nilikuja kuzika tu”
Basi akaondoka na kumuacha Tumaini na Sia pale huku Tumaini akimpa mpa moyo Sia kuwa aijali yeye ndio mke halali wa Erick.

Sababu ya kutokulala usiku, basi muda huo Erica alikuwa hoi na usingizi hadi maam yake anarudi na kugonga mlango kwakweli Erica alikuwa amelala sana hadi ilibidi akamgongee dirishani ndipo Erica alipotoka na kuwafungulia kisha mama yake akaingia na Yule mgeni huku akimkaribisha sana,
“Karibu, karibu. Hapa ndio nyumbani kwangu”
“Jamani ni siku nyingi sana”
“Ten asana”
Basi Erica akawasalimia na kurudi kulala chumbani kwake kwani kiukweli alikuwa na usingizi sana, basi mama yake na Yule mwenzio walijikuta wakiongelea mambo mbalimbali ya zamani hadi kuanza kuongelea na msiba uliotokea,
“Hivi aliyekufa pale ni nani yako?”
“Ni dada yangu”
“Aaah pole sana, dada yako tumbo moja?”
“Ni dada wa bamkubwa na bamdogo yani tumbo moja”
“Kwani alikuwa akisumbuliwa na nini?”
“Mwenzangu hata hatuelewi maana ugonjwa aliokuwa akiumwa nadhani ni siri ya watoto wake, nilikuwa naenda kumuona yani kuna kipindi unakuta kazidiwa haswaa naanza kufokea wale watoto kuwa kwanini hawampeleki dada yangu hospitali, basi wanasema Sia ndio anajua dawa ya mama yao, Sia ndio Yule binti nilikukuta nae. Ni mtoto wa dada yangu Yule, ndio mwanae wa mwisho. Nikimuuliza Sia dawa ya dada ni nini, ananiambia subiri basi sijui anapiga simu wapi na kumpa mama yake aongee nayo baada ya hapo utakuta dada kaamka na kuanza kula tena, nilikuwa nashangaa sana, na sijui kwanini walikuwa hawampeleki hospitali”
“Ila ndugu mnatakiwa kujua sababu, sio watoto kuwaficha ficha”
“Na hakika wanatuficha ficha sana, ila Yule Sia ndio huwa simuelewi kabisa, msiba umetokea muda kidogo na yeye akapndoka, ila asilimia kubwa ya watu waliofika msibani wanasema habari wamepewa na Sia, nadhani alienda kusambaa habari si mbaya ila yule mtoto wa dada yani hata sijui kapagawa na nini? Wewe umemfahamia wapi maana ndio nilikukuta nae”
Ikabidi mama Erica amwambie kwa kifupi tu jinsi alivyo mfahamu Sia,
“Kheee mtoto ana wazimu Yule, yani aje kulia mlangoni kwake jamani! Mtoto mjinga Yule, ila kiukweli nimefurahi sana kuonana na wewe, tuachane na hizo habari za huyo mtu ila nataka kujua kwani huyo kijana na mwano wana mpango gani?”
“Wamepanga kuoana, wana mtoto tayari”
“Oooh hongera sana, jamani binti yangu kazaa na mwanaume huyo hajielewi wala nini, mtoto anaenda miaka minne sasa ila baba haeleweki na hajawahi kuja kumuona mtoto wake”
“Pole ndugu, ndio uzazi huo”
Basi wakawa wanaongea mambo mbali mbali na kukumbushana vitu vingi ila Yule mama aliaga na kusema kuwa angerudi siku nyingine ili waongee vizuri,
“Ngoja nikamalize mambo ya msiba kwanza, nitakuja kukuaga na tutaongea vizuri, ila habari za watoto zisikuumize kichwa hizi, nitaenda kuongea na Sia tu nijue muafaka ni nini. Sawa ndugu yangu!”
“Sawa, utakuwa umenisaidia sana”
Basi akamsindikiza na kuagana nae, alivyorudi ndani sasa alimkuta Erica ametoka sebleni na mtoto wake,
“Yani wewe pindi mgeni yupo ndani hapa ndio ukajifanya hutoki chumbani, umeona kaondoka ndio umetoka”
“Nisamehe mama, kwani ni nani Yule?”
“Ungekuja kumsalimia ningekutambulisha, ni rafiki yangu wa siku nyingi sana. Nilikuwa nasoma nae. Ila una tabia mbaya, umesubiri kaondoka ndio umetoka”
“Hapana mama, nilikuwa na usingizi”
“Kwahiyo saivi umeisha?”
“Angel ananisumbua mama”
“Mpe chakula, mtoto njaa huyo”
Basi Erica akamuacha pale mtoto na mama yake na yeye kwenda jikoni kumuandalia mwanae chakula.
Muda huo huo simu yake ilianza kuita, ila ilikuwa na mtetemeko tu maana alitoa sauti ila muda huo simu ilikuwa kwenye kochi basi Angel akashuka kwa bibi yake na kwenda kuichukua, bibi yake akaidaka ili kuangalia mpigaji, akakuta ni Erick, akacheka na kumuita Erica aliyekuwa jikoni,
“Haya mpenzi wako anapiga simu maana hadi kaandikwa my love mmmh!! Wewe mtoto wewe mapenzi yanaumiza sana, sijui hujawahi kuumia na mapenzi?”
“Nimewahi mama na nimeumia mara nyingi tu”
“Ungekuwa umewahi usingethubutu kuandika hata mpenzi, yani ungeweka jina lake tu bila vikorombwezo vingine, mtu pekee wa kujidai nae na kumpa majina uyatakayo ni mume wako ila hawa wasioeleweka utajiumiza moyo bure”
“Jamani mama!”
“Sio cha jamani, pokea simu hiyo, ona ishakatika”
Na kweli simu ilikatika muda ule wakati Erica akiongea na mama yake, ila Erica alikaa chini na kuongea na mama yake,
“Mama, mapenzi ni nini? Sielewi yani sielewi kabisa, kichwa changu kinavurugika kila kukicha”
“Maliza kuandaa chakula cha mtoto, mlishe kisha njoo ukae sasa uniulize nikuelekeze kidogo”
Basi Erica alienda kumalizia kuandaa chakula cha mtoto na alipomaliza alimlisha kama mama yake alivyomwambia.
 
Back
Top Bottom