Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 61


James alimuita Bahati na kumsimamisha, kisha akamnasa kofi,
“Ila kaka unanionea”
“Nakuonea nini mshenzi mkubwa wewe, unataka kuharibu maisha ya Erica nikuangalie tu”
“Nampenda kweli na sina haja ya kuahribu maisha yake”
Akamnasa tena kibao,
“Na ole wako nisikie umetembea nae, nitakuchinja na utanijua vizuri mimi ni nani. Kuanzia sasa, Yule muone kama kituo cha polisi, nitakufunga mimi. Potea mbele yangu”
James alikuwa na hasira sana maana kila akikumbuka jinsi Erica alivyomlaghai halafu anakutana na kijana wa ajabu ajabu alikuwa na Erica roho ilimuuma sana kamavile Erica ni mke wake.
Alirudi nyumbani na kumkuta mkewe sebleni,
“Kheee ulienda wapi na wewe?”
“Yani Yule mjinga nilienda kumpa onyo sababu sikuridhika kabisa”
“Asante mume wangu kwa kumjali mdogo wangu”
“Kwanza yuko wapi? Anatakiwa nae tumpe onyo asituletee tena watu wa kijinga jinga hapa nyumbani”
“Yupo chumbani kwake, ila nishaongea nae”
“Haitoshi, mimi ndio baba mwenye nyumba. Aibu ikija hapa tutadhalilika wote”
“Kweli mume wangu, yupo chumbani kwake kule”
James akaenda kwenye chumba cha Erica na kufungua mlango ila ulikuwa mgumu na kuonyesha kuwa umefungwa kwa ndani, James akasema kwa hasira,
“Wewe Erica fungua mlango”
Erica nae akajibu kwa kwa kujiamini,
“Sifungui mlango, dada ameshanisema inatosha”
“Una kiburi eeh!”
Erica akawa kimya na kumfanya James achukie zaidi, akarudi sebleni alipo mkewe na kumwambia,
“Dogo lako lina kiburi sana, unajua limegoma nisiongee nalo!”
Bite akachukia pia na kuinuka, akafungua mlango wa Erica ukawa haufunguki na kumwambia,
“Wewe Erica nifungulie mlango kichaa wewe”
Erica akafungua mlango, dada yake akamzaba kibao,
“Unajifungia milango nyumba yako hii? Nyumba ni yangu na mume wangu halafu bila aibu unajifungia milango na kugoma kutufungulia. Na kwanini umegoma shemeji yako asikuseme?”
“Dada ulishanisema nimesikia jamani, nianze kusemwa tena kwanini?”
“Hivi unajua kama Yule ndio baba mwenye nyumba?”
“Najua dada”
“Sasa unabishaje kusemwa na shemeji yako?”
“Dada, ngoja nikuulize swali. Hivi ni tamaduni za wapi eti shemeji aje chumbani kwangu kunisema? Hata kama hii ni nyumba yenu, ila hiki chumba nalala mimi na sidhani kama ni jambo linalofaa eti shemeji aingie chumbani kwangu? Hiki ni chumba cha msichana, naweka vitu vya kike, yani shemeji akutane na chupi zangu kweli? Au akutane na pedi zangu? Labda kama nimezidiwa sijiwezi kabisa na hakuna msaada anaweza kuja kunisaidia ila sio nikiwa mzima hivi, ni tamaduni za wapi hizo? Kama mnahitaji kunishambulia kwa kunisema si mniite sebleni hapo, mnisemeee weee hadi yaniingie ila sio kwa shemeji kunifata chumbani kwangu”
Kwa kiasi Fulani haya maneno yalimuingia Bite ila ilibidi ajitete kidogo,
“Sasa kwani wewe unahisi nini kama angeingia na kukusema humu? Yule si kama kaka yako tu?”
“Ni kweli kama kaka yangu ila kumbuka si kaka yangu ni shemeji yangu”
“Usimfikirie vibaya mume wangu, hawezi kufanya ujinga kwako hata mara moja, kwanza anakuona kama mwanae hata sijui umeanzaje kumfikiria vibaya hivyo shemeji yako Erica! Huyu ni mume wangu, hajawahi kuwa na mwanamke mwingine yeyote nje zaidi yangu, iwe kumtamani mdogo wangu kweli?”
“Sijasema hivyo dada labda kama umefikiria vibaya na wewe pia ila nimekwambia sio tamaduni zetu”
Bite kwa kiasi maneno ya mdogo wake yalimuingia na kwa kiasi yalimchukiza na kuamua kutoka zake mule chumbani kwa Erica.

 
SEHEMU YA 62


Siku hiyo Erica hata kula hakwenda sababu muda wa kula dada yake alimuita hakutoka, sasa aliwaza akitoka muda ambao shemeji yake amebaki mwenyewe sebleni itakuwaje, kwahiyo aliamua kukaa chumbani tu huku akijisemea,
“Sitaki kuharibu ndoa ya dada yangu, siwezi kumwambia ukweli wowote ila mimi nitajiepusha na hapa. Huyu shemeji si mzuri tena kwangu. Hivi ndio dada anasema mwanaume akikukuta bikra hakusaliti kweli mmh!! Mimi tu mdogo wa mke wake alinitamani, je wa huko nje inakuwaje? Hakuna cha kuolewa na bikra wala nini, asinibabaishe na yeye, kwanza nishaharibu siwezi kurudisha siku nyuma”
Aliwaza na kupanga vizuri vitabu vyake kwaajili ya kujiandaa kesho kwenda chuo.
Asubuhi alikuwa ashajiandaa na kutaka kutoka na dada yake, ila Bite alidai kuwa siku hiyo alichelewa sana kazini, basi James akasema sababu na yeye anatoka basi atampitisha chuoni, mmh Erica akaona hiyo sio sawa kwake ilibidi amuombe dada yake amshushe hata stendi maana alikuwa na haraka sana asingeweza kumsubiria shemeji yake, dada yake alivyopanda tu kwenye gari yake, Erica nae alikuwa amepanda na kumuomba amuache tu kituoni, ilibidi dadake afanye hivyo.
Erica alienda moja kwa moja hosteli, ila hakuwa na kipindi chochote siku hiyo kwahiyo alikuwa na lengo tu la kurudi chuo na si kukaa pale nyumbani na shemeji yake.
Akawa amekaa tu akiwasiliana na Bahati kwa njia ya ujumbe, Bahati alimuomba Erica aende kumuona maana anajisikia vibaya, ukizingatia hakuwa na kitu chochote cha kufanya kwa siku hiyo akaona ni vyema tu kwenda kumuona Bahati na kupafahamu anapoishi.

 
SEHEMU YA 63


Alifika anapoishi Bahati na kumkuta, walikuwa wawili tu ndani, Bahati akamuuliza Erica,
“Unajua ninachoumwa?”
“Unaumwa nini?”
“Naumwa mapenzi Erica”
“Unaumwa mapenzi? Kivipi?”
“Erica, wewe ndiye tiba yangu, wewe ndiye wa kunifanya nipone”
“Sikuelewi”
Bahati alimuangalia Erica kwa macho ya huruma sana huku akiongea kwa sauti ya huruma,
“Kheee kwahiyo umeniita ili ufanye mapenzi na mimi?”
“Usinifikirie hivyo Erica, nakupenda”
“Hapana, sipo tayari Bahati. Sipo tayari kabisa”
Erica akainuka ili aondoke, Bahati akashika kisu na kumwambia Erica,
“Ukiondoka najiua, ni heri nife kuliko kukukosa wewe”
Huruma ikamshika Erica ila hakutaka kulala na mwanaume kwakweli huo ulikuwa mtihani mgumu sana kwake, ila hakuwa na jinsi kwani hata taswira ya kawaida ya Bahati ilibadilika kabisa, ikabidi Erica akubali.
Baada ya lile tendo, Bahati alimuangalia Erica na kumwambia,
“Pole Erica”
“Pole ya nini?”
“Najua nimekuumiza Erica, ila nashukuru kwa kunipokea”
Erica alimuangalia tu huyu Bahati ambaye aliendelea kuongea,
“Asante Erica, asante kwa kunitunzia”
“Sikuelewi”
Hunielewi Erica? Nakushukuru sana, yani siamini kuwa mimi ni mwanaume wa kwanza kwako, asante sana Erica kwa kunitunzia bikra yako”
Erica alimshangaa sana huyu Bahati.
 
SEHEMU YA 64


Erica alimuangalia tu huyu Bahati ambaye aliendelea kuongea,
“Asante Erica, asante kwa kunitunzia”
“Sikuelewi”
Hunielewi Erica? Nakushukuru sana, yani siamini kuwa mimi ni mwanaume wa kwanza kwako, asante sana Erica kwa kunitunzia bikra yako”
Erica alimshangaa sana huyu Bahati.
Ila Bahati aliendelea tu kumsifia Erica kuwa ni msichana wa pekee sana, Erica aliamua kumuaga Bahati kuwa anarudi hosteli. Bahati aliinuka na kutaka kumsindikiza Erica,
“Kheee si ulisema unaumwa wewe?”
“Ndio nilikuwa naumwa ila nilikuwa naumwa mapenzi”
Erica alimuangalia Bahati kisha kuanza kuondoka na Bahati alikuwa akimsindikiza, na alimpeleka hadi hosteli.
Muda wote Bahati alikuwa akimsifia Erica kwa uzuri aliokuwa nao,
“Erica mpenzi wangu, wewe ni msichana mrembo sana najua kuna vijana wengi watakufata na kukudanganya kuwa wanakupenda huku wakikusifia kuwa wewe ni mzuri, wakikwambia kuwa wewe ni mzuri na mrembo waambie unajua utaweza kwa kiasi Fulani kuwakata makali yao. Wakikutaka kimapenzi waambie kuwa una mpenzi, Erica sikudanganyi wala sikutanii nakupenda sana”
Erica alikuwa anamsikiliza tu anavyoongea hadi alivyofika hosteli na kuagana nae.

 
SEHEMU YA 65


Kufika hosteli alipoenda kuoga alijilaumu sana kwa kujiingiza kwenye mapenzi na Bahati,
“Uuuh Mungu wangu, kwahiyo sasa nimetembea na wanaume watatu. Si ndio nimekuwa Malaya jamani? Na kati yao hakuna wa kuwa mume wangu, ila mimi nina kilanga, kilichonifanya nitembee na Bahati ni nini? Nadhani ni mawazo niliyonayo sababu ya George, ila Yule mwanaume ni mpuuzi sana, wa kuniacha mimi kweli? Mbona Yule Bahati amejisifia kuwa yeye ndio wa kwanza kwangu? Au wanaume wapo tofauti? Ila Mungu anisaidie nisije kutembea na mwanaume mwingine tena, kama nimeamua kuwa na Bahati basi niwe naye yeye tu”
Aliwaza sana, na kumaliza kuoga kisha kwenda ndani kuvaa nguo, alipomaliza alifika mtu na kumwambia
“Erica kuna kijana anakuita nje”
Erica hakuelewa kuhusu huyo mtu anayemuita, kwahiyo alitoka kwenda kumuangalia na ilikuwa tayari saa mbili usiku.
Alishangaa kumuona kuwa ni Adam, Yule kijana aliyemwambia kuwa anaelewa kuhusu George na Dora.
“Adam, umejuaje kama nakaa hosteli hii?”
“Nimejua tu, nilikuwa nikiulizia unapokaa”
“Haya karibu”
“Asante, ila ni vyema tukitafuta mahali tuongee”
“Usiku huu? Ungeongea tu hapa hapa au tuongee kesho’
“Hapana tusingoje kesho”
Erica akashangaa sana kuwa wasingoje kesho, ni ujumbe gani anataka kumwambia ila bado hakujua ni wapi angekaa nae na kuzungumza nae. Adam akamuomba wakakae kwenye vimbweta vya bustanini ili azungumze nae, Erica alikubali.
 
SEHEMU YA 66


Walifika kwenye vimbweta vya eneo hilo na kujikuta wakiwa wawili tu maana lile eneo taa zake ziliharibika kwahiyo palikuwa na giza na kufanya hata watu kujisomea eneo hilo iwe ni vigumu sababu ya giza, basi Adam alikaa pale na Erica kwaajili ya maongezi yao.
“Eeeh nakusikiliza Adam”
“Unajua Erica wewe ni msichana mrembo sana?”
“Najua, sema lingine”
“Mmmh ngoja tuachane na hiyo mada kwanza. Nilitaka kukueleza kuhusu George na Dora”
“Eeeh”
“Yani George ni mwanaume muongo sana, kashawadanganya wasichana wengi sana, na kuharibu maisha ya wasichana wengi sana. Tena alishwahi kuwa na mahusiano na Yule Dora ila badae wakawa marafiki. Dora aliwahi kuwa mpenzi wangu, kwahiyo George alimpora Dora kwangu iliniuma sana”
“Kumbe! Dora si rafiki mwema na sitaki tena urafiki naye”
“Ila mimi nina Wazo”
“Wazo gani?”
“Najua wewe ulikuwa na mahusiano na George na umeumizwa na George na Dora, mimi nimewahi kuwa na mahusiano na Dora na rafiki yangu alikuwa George, wameniumiza pia watu hawa. Naomba tuwafanyie revenge”
“Kivipi?”
“Mimi na wewe tuwe pamoja”
“Pole, ila umechelewa Adam”
“Kivipi?”
“Mimi nina mahusiano na mtu mwingine kwasasa”
“Mmmh Erica jamani, najua unasema hayo sababu hunijui kwa undani vizuri. Ila ungenijua usingesema hayo”
Adam akawa anamsogelea Erica ili ambusu mdomoni, ila Erica alimrudisha nyuma na kumwambia,
“Adam, nina mpenzi tayari hata hapa unaponiona nimetoka kufanya nae mapenzi”
“Unasemaje?”
“Ndio hivyo, siwezi kuwa na mpenzi mwingine tena”
Adam akaona kuendelea kumuomba Erica kuwa wapenzi ni kujisumbua tu kwa hivyo aliamua kuagana nae, kisha Erica akarudi hosteli.
Na alipofika tu uliingia ujumbe kutoka kwa Bahati,
“Nakupenda sana Erica, wewe ni mwanamke muhimu sana katika maisha yangu”
Alisoma ujumbe huu na kutabasamu alijiuliza kuwa inakuwaje wakati kwa kawaida wanaume wanapokutana kimwili na mwanamke ndio wakati wa mwanaume huyo kutokumtaka tena huyo mwanamke ila ilikuwa tofauti sana kwa Bahati.
Kwnye mida ya saa tano usiku akapokea simu kutoka kwa dada yake Bite,
“Wewe mbona hujarudi nyumbani?”
“Dada, nimeamua kurudi hosteli”
“Hivi una akili wewe, yani unafanya jambo bila hata ya kunishirikisha kweli?”
“Dada nisamehe ila sikuwa na la kufanya zaidi ya kurudi hosteli”
“Ili iwe rahisi kufanya madudu yako?”
“Hapana dada usinifikirie hivyo”
“Kesho shemeji yako atakuja kukuchukua na utarudi nyumbani sawa”
“Lakini dada”
“Sitaki cha lakini, nimemaliza”
Bite akakata simu na kumuacha Erica akiwa na mawazo sana kwani alifikiria cha kufanya sababu hakutaka tena kurudi nyumbani kwa dada yake na hakutaka kumwambia dada yake ukweli kwa kuhofia atavunja mahusiano ya dada yake na shemeji yake.
Yani usiku wa siku hiyo alikuwa akiwaza tu kesho anamkwepaje shemeji yake.
 
SEHEMU YA 67


Kulipokucha mapema kabisa, aliamshwa na simu ya Bahati na alikuwa akimsalimia na kumtakia masomo mema.
“Mmmh huyu mwanaume nae ana kibarua loh!”
Akainuka na kujiandaa kwaajili ya kwenda chuo maana siku hiyo alikuwa na kipindi cha asubuhi.
Wakati anaingia kwenye bwalo la kusomea, akapishana na George ambaye alionekana kumuangalia sana Erica ila Erica alipita kamavile hamuoni, akaingia zake darasani.
Wakati anatoka, Dora alimfata nyuma na kumsalimia,
“Erica mambo”
“Safi ila sitaki mazoea na wewe Dora”
“Erica jamani, kumbuka tunasoma wote”
“Tunasoma wote? Kwani na wewe ni mwaka wa kwanza kama mimi? Wewe si mwaka wa pili, umecarry hili somo ndiomana tunaonana”
“Hata kama Erica, ila sio vizuri unavyonifanyia”
“Ila ni vizuri kwako kwa mwanaume uliyetembea nae wewe kumlengesha atembee na mimi! Hivi mkoje watu jamani? Yani hata huoni kinyaa kwa mwanaume uliyekuwa na mahusiano nae kuja kuwa na mahusiano na rafiki yako? Usiniambie ndio usomi au uzungu, huo ni uchafu? Na kwa taarifa yako, hutoniona tena nikimfatilia huyo George wala nikiumia kwaajili yake, kwangu mimi ni kama mtu ambaye hajawahi kuwepo katika maisha yangu”
Erica akaondoka zake, ila mbele kidogo kuna mdada alimsimamisha Erica na kumwambia kuwa amesikia alichokuwa anaongea na Dora.
“Pole sana, unajua sisi wasichana mara nyingine ni sisi wenyewe ndio tunaharibiana ndiomana wanasema adui wa mwanamke ni mwanamke”
“Kweli kabisa, yani Yule Dora kanifanya nisiwe na hamu na marafiki kabisa”
“Ila si wote wenye tabia zisizofaa”
“Sijawahi kuwa na rafiki mwenye tabia njema, yani napataga vimeo tu”
“Hapana usiseme hivyo, By the way naitwa Tumaini sijui mwenzangu unaitwa nani.”
“Naitwa Erica”
“Ningependa tuwe marafiki, hata kwa kawaida tu yani tuwe tunaongea na kubadilishana mawazo”
“Hakuna shida”
“Unajua Yule Dora uongo ndio uliomfanya hadi akafeli na kurudia lile somo”
“Kumbe unamjua”
“Ndio namjua”
Basi Erica aliongozana na huyu mdada hadi hosteli na kugundua kuwa anaishi nae hosteli moja kasoro vyumba tu. Akaagana nae na kuelekea kwenye vyumba vyao.

 
SEHEMU YA 68


Erica alitulia na kupigiwa simu na namba ngeni akapokea,
“Erica, mimi ni shemeji yako James. Nakuuliza nije saa ngapi kukuchukua?”
“Hapana shemeji, mimi hosteli pananitosha”
“Ila dada yako kasema nije nikuchukue”
“Hapana shemeji”
“Nakuja Erica”
James akakata simu, kwakweli Erica alijiona yupo kwenye mtihani mzito sana kwake kwani hakutegemea kabisa kama shemeji yake huyo anaweza kuwa king’ang’anizi kiasi hiko, akawaza sana, akataka kuondoka hapo hosteli.
Ila wakati anatoka tu akakutana na Tumaini,
“Khaa kumbe ulitaka kuondoka Erica, mi nilikuwa nakufata. Unataka kwenda wapi kwani?”
“Kutembea tembea tu”
“Basi twende pamoja, mimi nilikuwa nakufata ili nikuonyeshe chumba ninachoishi”
“Si ushanionyesha ni pale”
“Hapana, pale nakaa kihosteli ila kipo chumba mtaani nimepanga. Twende Erica”
Kwasababu Erica alitaka kuondoka hapo hosteli na hakuwa na mahali pa kuelekea kwa muda huo akaamua kukubali tu kwenda na Tumaini.
Walifika nyumbani kwa Tumaini na kumkaribisha ndani, alishangaa sana kuona Tumaini ana kila kitu kwenye chumba chake,
“Kheee hongera, umewezaje kumiliki vyote hivi?”
“Boom, yani boom ninalopata ndio nanunulia vitu ninavyotaka. Unajua kwetu wananipa hela ya kila kitu na hawajui kama Napata mkopo, kwahiyo ule mkopo ndio nafanyia mambo yangu”
“Kwahiyo ada”
“Mimi Napata mkopo asilimia mia, na kwetu huwa wananipa ada yote, sasa nitafanya nini hapo zaidi ya kujipendezesha”
“Mmmh hongera sana”
Mara simu ya Tumaini ikaita na akaongea nayo kwa muda, alipokata akamuangalia Erica na kumwambia,
“Ni mdogo wangu nilikuwa nawasiliana nae, kasema anakuja kunitembelea.”
“Aaah sawa basi, ila kwenu wewe una deka sana?”
“Hahaha hapana bhana, halafu kwa baba tupo wawili tu mimi na huyo mdogo wangu anayekuja ila mama tofauti.”
“Wazazi wako wanaishi pamoja?”
“Hapana, baba na mama yangu hawajaoana, ila baba ana hela sana kwahiyo huwa anatuhudumia kwa kila kitu. Sijui kuishiwa mimi, Yule mdogo wangu anayekuja ndio balaa maana baba anamuhudumia na mama yake nae anamuhudumia yani baba na mama yake wanashindana kumuhudumia, hajaanza kazi ila ana hela uchafu.”
Erica alijikuta akitamani sana maisha ya Tumaini na kutamani hata yeye ndio angekuwa Tumaini. Muda kidogo mdogo wa Tumaini alifika na kugonga mlango, Tumaini akamfungulia na kuingia ndani.
Erica alibaki anamshangaa tu kwani alikuwa ni Erick, Yule aliyesoma nae.

 
SEHEMU YA 69


Erica alijikuta akitamani sana maisha ya Tumaini na kutamani hata yeye ndio angekuwa Tumaini. Muda kidogo mdogo wa Tumaini alifika na kugonga mlango, Tumaini akamfungulia na kuingia ndani.
Erica alibaki anamshangaa tu kwani alikuwa ni Erick, Yule aliyesoma nae.
Tumaini ndiye aliyemshtua Erica na kumtoa kwenye mshangao,
“Erica mbona unashangaa hivyo? Huyu ni mdogo wangu anaitwa Erick. Karibu Erick, huyu ni rafiki yangu na ni mdogo wangu pia anaitwa Erica.”
Erick alimuangalia sana Erica, ila Erica nae alimuangalia sana Erick kisha Erick akampa mkono Erica na kumwambia,
“Nashukuru kukufahamu”
Hii hali kidogo ilimchanganya Erica maana Erick ni mtu anayemjua fika ila leo anaishia kumpa mkono tu na kumwambia kuwa anashukuru kumfahamu, alishindwa hata kujibu na kujikuta akikaa kimya na kutikisa kichwa tu.
Kisha Tumaini akaanza kuongea na mdogo wake,
“Naona uenifanyia surprise leo”
“Aaah nilikuwa napita mitaa ya huku ndio nikaamua kuja kukutembelea dada”
“Nimefurahi sana”
“Dada kaninunulie kinywaji basi”
“Aaah kwa mara ya kwanza leo umetaka kinywaji, basi sawa ngoja nikakununulie kinywaji chako unachopendaga”
Tumaini akatoka na kuwaacha Erica na Erick ndani, kisha Erica alimuita Erica,
“Erica”
“Abeee”
“Mbona umetulia sana?”
“Nifanyeje sasa na umejifanya hunijui”
“Mmmh sio hivyo nakukumbuka vizuri Erica ila nakumbuka pia ulivyofanya nidhalilike shuleni, sikutaka dada ajue kuwa wewe ni msichana uliyefanya mdogo wake nipate aibu shuleni ndiomana nikajifanya sikufahamu. Ila ni vyema tukipeana mawasiliano halafu tutaongea vizuri zaidi”
Erica alimpa Erick namba zake, muda kidogo Tumaini alirudi na vinywaji mkononi. Kisha akawafungulia na kuwakaribisha,
“Hapana mimi situmii kilevi”
“Kwanini Erica?”
“Situmii tu”
“Mmmh unakosa uhondo basi”
Ikabidi achukue ile bia kisha amuwekee juisi Erica maana yeye hajalelewa katika mazingira ya kunywa kilevi.

 
SEHEMU YA 70


Waliongea ongea pale kisha Erick alimtumia ujumbe Erica kuwa aage na amsubirie mahali ili waongee, kwahiyo Erica akamuaga Tumaini,
“Dada, mi naona niende”
“Jamani kwani una kipindi jioni hii? Mbona mapema?”
“Hapana, ila kuna mahali natakiwa kwenda”
“Subiri basi, mdogo wangu akiondoka nikusindikize”
Erick akadakia kwa dadake,
“Unajua mimi naondoka muda gani?”
Ikabidi wacheke tu kisha Tumaini akamruhusu Erica kuondoka huku akimsindikiza kidogo.
Wakiwa njiani, Erica alitumiwa ujumbe na Erick,
“Jitahidi umkwepe huyo dada maana huwa akiamua kumng’ang’ania mtu anamng’ang’ania huyo balaa. Hashindwi kukupeleka na ukarudi nae”
Kisha Tumaini nae akamuuliza tena,
“Kwani Erica unawahi wapi jamani?”
Mara Erica akapigiwa simu na shemeji yake,
“Nakuja kukuchukua Erica”
“Sawa shemeji”
“Ushajiandaa?”
“Ndio nishajiandaa”
James alishangaa pia muda huu yani Erica kaongea nae bila kubisha chochote kile kumbe Erica alikuwa anaongea vile ili kumuaminisha Tumaini kuwa kuna mahali anawahi,
“Natakiwa kuwahi hosteli maana shemeji anakuja kunichukua”
“Unaenda nae wapi”
“Naenda nae nyumbani, alisema dada jana aje anichukue”
“Aaah sawa, basi usije ukachelewa kujiandaa”
Basi Tumaini akaita bodaboda na kumlipa kisha akamwambia amfikishe Erica hosteli, kwahiyo Erica alipanda ile bodaboda.

 
SEHEMU YA 71


Baada ya Tumaini kurudi tu Erick nae akamuaga,
“Jamani Erick kumbe unaondoka muda huu huu si ungeniambia tu mi nimpeleke Erica?”
“Mmmh dada nawe yani unaanza kuthamini wageni kupita mimi jamani?”
“Basi yaishe”
Basi Erick alitoka pale na kuondoka, kisha akawasiliana na Erica, sababu alikuwa na gari ilikuwa rahisi kumfata Erica hosteli kwao.
Alipofika maeneo ya karibu na pale hosteli alimshtua Erica naye alitoka kisha Erick akamuomba apande kwenye gari yake na kuanza kuondoka,
“Mmmh tunaenda wapi Erick?”
“Nahitaji kuongea na wewe Erica, hujui tu ni furaha gani ipo moyoni mwangu baada ya kukuona na wewe”
Basi Erick alipeleka gari hadi hotelini na kukodi chumba, kisha akaingia na Erica huku akimwambia kuwa lengo lake anahitaji tu kuongea nae.
Walifika chumbani na kukaa kwaajili ya maongezi,
“Erica nilikutafuta sana ila sikujua ni wapi pa kukupata, nashukuru nimekupata sasa. Vipi bado unanipenda?”
“Mmmh!”
Erica aliguna maana alifikiria kuhusu Bahati, na vipi amkubali Erick itakuwaje kwa Bahati wakati anaonyesha akimpenda sana,
“Mbona unaguna Erica, hunipendi?”
“Hapana”
“Nini sasa Erica?”
“Sijui”
“Hujui nini?”
“Sielewi”
Erick alimsogelea karibu Erica na kumbusu, kwakweli Erica hakuweza kukataa chochote kwa Erick sababu ni mwanaume aliyekuwa katika moyo wake kwa kitambo sana, na ile hali ilimpa urahisi Erick wa kufanya chochote kwa Erica.



 
SEHEMU YA 72


Erica alijikuta akifanya mapenzi na Erica na walipomaliza katika siku zote ile siku alijawa na aibu kupita maelezo ya kawaida, alishikwa na aibu sana baada ya kumaliza lile tendo na Erick kiasi kwamba hakuweza hata kumuangalia tena usoni, hadi Erick aliamua kumuuliza
“Erica vipi mbona umejawa na aibu kiasi hiko?”
“Hapana”
“Usijali Erica, nakupenda ujue. Usijali kwa yote yaliyopita kati yetu, najua una maisha yako na mimi nina maisha yangu kwasasa ila upendo ni kitu cha ajabu sana, bado utaendelea kuishi moyoni mwangu kama mimi ninavyoishi moyoni mwako. Usinionee aibu Erica”
Bado Erica aliona aibu sana, basi Erick aliinuka na kwenda kuagiza chakula.
Erica alioga na kuvaa kisha kuchukua simu yake, akakuta kuna simu ambazo hazikupokelewa za shemeji yake pamoja na Bahati, kisha akakuta ujumbe kutoka kwa Bahati,
“Kumbuka nakupenda sana Erica, tafadhali usinisaliti”
Alisoma ule ujumbe huku moyo wake ukimsuta sana kwani tayari alishamsaliti Bahati kwa kulala na Erick, alijiuliza cha kufanya lakini hakuwa na jibu,
“Erick nampenda tena nampenda sana, naye ananipenda ila sijui maisha yake kwasasa na sijui anafikiria nini kuhusu mimi. Bahati ananipenda sana, hata sijui nifanyeje”
Aliwaza sana na kukosa jibu, Erick alikuja na chakula ambapo alimbembeleza Erica wale kile chakula.
Walipomaliza alimbembeleza kuwa alale pale na ampeleke hosteli kesho yake,
“Hapana Erick, inabidi nirudi leo”
Wakati anabishana na Erick pale kuna ujumbe kwenye simu yake ukaingia kutoka kwa shemeji yake,
“Erica uko wapi? Nimekuja kukuuliza kwenye hosteli yenu hapa wamesema hawajui ulipoenda? Uko wapi na nilikwambia nakuja kukuchukua? Nakungoja hapa nje ya hosteli yenu nipo kwenye gari yangu”
Erica alisoma ule ujumbe na kumuangalia Erick ambaye alimuuliza kuwa tatizo ni nini ila akajikuta ameropoka tu kuwa amekubali kulala nae hapo hotelini hadi asubuhi, jambo hilo lilikuwa ni furaha sana kwa Erick huku akimpa Erica ahadi za kila aina.
Erica aliamua kuzima simu ili shemeji yake asimpate tena hewani ila hakujua kama kile kitendo chake cha kuzima simu kilimuumiza sana Bahati.

 
SEHEMU YA 73


Bahati alipoona kuwa hampati hewani Erica akaamua kwenda hosteli kwa Erica, alipofika moja kwa moja alienda kumuulizia akaambiwa kuwa Erica hayupo na kumfanya azidi kupatwa na mashaka kuwa huenda Erica kapatwa na matatizo, wakati anatoka ndipo alipokutana na shemeji wa Erica ambaye alikuwa anataka kuondoka sababu alishamsubiri sana Erica bila ya matokeo yoyote.
Bahati alishtukia tu akikamatwa na kuingizwa kwenye gari kisha akapuliziwa kitu machoni na kumfanya apoteze fahamu.
Kuja kushtuka alikuwa baharini anapigwa tena inaonyesha alipigwa sana,
“Kaka nisamehe”
“Nikusamehe nini mbwa wewe, yani mimi naenda kumchukua Erica halafu wewe ulimfungia!”
“Si kweli kaka”
Ila James hakutaka kumsikiliza zaidi ya kumuongezea kipigo na kumuacha pale pembezoni mwa bahari.
James aliondoka hadi hosteli kwakina Erica tena, alimuulizia Erica ila bado hakuwepo alichukia sana na kurudi nyumbani kwake. Bite alimuuliza mume wake,
“Vipi Erica yuko wapi?”
“Mdogo wako ni mjinga sana kati ya wajinga, unajua alikuwa na Yule jamaa hadi simu kanizimia”
“Jamaa gani?”
“Si Yule wa siku ile, ila nimempiga sana yani mimi vijana wa kuharibu mabinti siwapendi kabisa”
“Jamani huyu Erica mbona anataka kututia aibu jamani! Itabidi kesho niende kwa dada yetu Yule mkubwa nikamueleze habari za huyu Erica maana atatutia aibu kwakweli”
Bite alichukia sana kwa mwenendo huo wa mdogo wake maana aliona sasa amekuwa mtu wa ajabu.



 
SEHEMU YA 74


Palipokucha, Erica alijiandaa vizuri kabisa kisha Erick alimrudisha hosteli. Alikuwa amechoka sana kwahiyo alifikia kulala kwanza mpaka jioni ndio akajiandaa kwaajili ya kwenda chuo maana alikuwa na kipindi muda huo.
Alirudi jioni kabisa na kuwasha simu yake, alikutana na jumbe mbali mbali zilizoongozana ila ujumbe uliomshtua zaidi ni ujumbe wa Bahati,
“Jana nilikuja hosteli kwenu maana sikukupata hewani, ila nilikamatwa na Yule ndugu yako wa kiume wa siku ile na amenipiga sana akidai kuwa nimekufungia”
Erica aliamua kumpigia simu Bahati, hata ongea yake ilionyesha wazi kuwa ni mtu mwenye maumivu sana, ila aliongea nae na akamueleza ilivyokuwa ila yeye hakuweza kumueleza kuwa ni kwanini alizima simu yake maana hakujua ni jinsi gani amwambia ukizingatia kapigwa kwaajili yake.
Wakati anawasiliana na Bahati, Erick nae akamtumia ujumbe kuwa amemkumbuka sana,
“Erica kipenzi cha moyo wangu nishakukumbuka tayari”
Akatabasamu na kusahau kabisa kama kuna mtu alikuwa anawasiliana nae aliyekuwa na maumivu ya kupigwa.
“Nakukumbuka pia Erick”
“Naomba nikuulize swali Erica”
“Niulize tu”
“Je una mpenzi?”
Erica alifikiria na kuona kama atamwambia ukweli Erick basi atamkosa kwahiyo hakuwa na budi zaidi ya kumdanganya kuwa hana mpenzi,
“Hapana sina, vipi wewe?”
“Upande wangu ni historia ndefu, ila tuachane na hayo. Unajua nakupenda Erica”
Lile swala la kwa upande wangu ni historia ndefu lilimpa changamoto kubwa sana Erica kwani alihisi huenda kuna mwanamke ana mahusiano na Erick, alijikuta akimuonea wivu kupindukia, ila hakuweza kumwambia Erick amueleze huo mlolongo wa stori ndefu.
Basi Erick akamuomba Erica kuwa aonane nae keshokutwa.
“Nitakuja hosteli kwenu kukufata”
“Sawa Erick”
Akakubaliana nae kuwa atafika kuonana nae, moyoni mwake kwa muda huo alikuwepo Erick tu tena hakukumbuka wengine wote zaidi ya kumuwaza Erick.
Swala hilo lilimfanya apotezee kabisa simu za Bahati kwani aliona akimpotezea ndipo Bahati ataacha kumfatilia ukizingatia kashamwambia Erick kuwa hana mahusiano mengine yoyote yale.

Ilifika siku aliyopanga kuonana tena na Erick, na kweli Erick kama alivyopanga alienda hosteli anapokaa Erica na kumsubiria kwa nje, Erica alipofika nje alikutana na Bahati akiwa na alama alama za kupigwa kumbe Bahati alipoona tena kimya aliamua kuja kumuona Erica, kwahiyo wakati Erica akimshangaa Bahati kuwa kafata nini tena, muda ule ule Bahati alisogea alipo Erica na kumkumbatia kisha akambusu, wakati huo Erick alikuwa mbele yake akiwaangalia kwa mshangao.



 
SEHEMU YA 75




Ilifika siku aliyopanga kuonana tena na Erick, na kweli Erick kama alivyopanga alienda hosteli anapokaa Erica na kumsubiria kwa nje, Erica alipofika nje alikutana na Bahati akiwa na alama alama za kupigwa kumbe Bahati alipoona tena kimya aliamua kuja kumuona Erica, kwahiyo wakati Erica akimshangaa Bahati kuwa kafata nini tena, muda ule ule Bahati alisogea alipo Erica na kumkumbatia kisha akambusu, wakati huo Erick alikuwa mbele yake akiwaangalia kwa mshangao.
Erica akona sasa picha yake itavurugika, akajitoa kwenye mikono ya Bahati, kisha Bahati akamuuliza,
“Vipi tena Erica?”
Erica akawa anaondoka akielekea alipo Erick, ila Erick aliingia kwenye gari yake akapanda na kuondoka zake. Ila Bahati nae alikuwa akimfata kwa nyuma, na ilionyesha jinsi gani Erica amechukia kwa Erick kuondoka kwahiyo mbaya wake kwa muda huo alikuwa Bahati, akageuka nyuma kwa gadhabu ili amseme Bahati, ila kabla hajamsema Bahati akamwambia,
“Yani Erica hukutaka kukumbatiwa na mimi sababu ya kijana mwenye gari? Sina gari ndio ila nina mapenzi ya dhati kwako Erica, nakupenda sana”
“Sitaki kuusikia huo wimbo tena”
“Erica jamani, kosa langu ni nini kwako? Kosa langu ni kukupenda? Angalia nilivyoumia kwa kipigo sababu ya kukupenda wewe”
“Usinibabaishe, umeyataka mwenyewe. Bahati sitaki tena unifatilie”
“Siwezi Erica, siwezi kamwe nakupenda sana”
“Lakini mimi sikupendi”
“Hunipendi sababu ya Yule kijana mwenye gari Erica? Muda ukifika, Mungu akipenda na mimi nitamiliki gari yangu”
“Sitaki kusikia hizo ngonjera, kwaheri”
Erica alirudi zake ndani mule hosteli kwani aliona kashaharibu na hakujua ni kwa jinsi gani anaweza kufanya aweze kuelewa na Erick.
 
SEHEMU YA 76


Alipokuwa ndani alipigiwa sana simu na Bahati ila hakupokea hata moja, akapata wazo kuwa inabidi aende kwa Tumaini ili ajaribu kumdadisi kuhusu Erick, ila akawaza kuwa lazima Bahati atakuwa chini akaimsubiri maana huwa hakati tamaa kwahiyo ikabidi atumie njia ya kumkwepa ili aende kiurahisi.
Alijiandaa na kutoka, ni kweli wakati anatoka alimuona Bahati amejikalia chini ya mti akimsubiria,
“Yani huyu mkaka wa ajabu hakati tamaa loh!”
Akamsogelea, kisha Bahati akainuka ili amsikilize,
“Bahati mpenzi wangu yani bado unanisubiri hapa nje?”
“Nitafanyaje sasa na wewe umechukia Erica?”
“Mimi sikuchukia ila nilikuwa napima tu upendo wako, nimegundua una upendo wa hali ya juu Bahati. Ila ukapumzike kwasasa mpenzi wangu, pole sana umeumia kwaajili yangu. Yani moyo umeniuma kweli”
Bahati alitabasamu kusikia maneno haya kutoka kwa Erica maana hakutegemea kabisa kama Erica angemwambia maneno yale ya kumbembeleza, alimuahidi kuwasiliana nae muda wote na kupokea simu zake huku akimbembeleza kuwa aondoke, hadi Bahati akakubali kuondoka.
“Mimi nina kipindi, kwahiyo ukiona sijapokea simu zako ujue nipo kwenye kipindi kwasasa. Tutakuwa tunawasiliana mpenzi wangu, hata usijali”
Basi wakaagana pale kisha Bahati akaondoka halafu Erica akaenda kwa Tumaini.

Ilikuwa Bahati kwani ni muda ule ule Tumaini alikuwa ndio amerudi toka kwenye matembezi yake,
“Karibu Erica, jamani si ungesema nikupitie”
“Nilikukumbuka tu dada yangu”
“Karibu, za tangu siku ile”
Wakaanza kuongea huku wakifurahi sana ilikuwa kama watu ambao wamefahamiana kwa muda mrefu sana kumbe sio siku nyingi tangu wawe marafiki, ilionyesha wanapatana sana.
Erica alianza kumuuliza kwa kumtega,
“Vipi Yule mdogo wako Erick ana mchumba?”
“Mmmh Erica usiniambie kuwa umempenda mdogo wangu Yule?”
“Aaah jamani dada nimeuliza tu”
“Erica nakupenda sana mdogo wangu ten asana, siwezi kukushauri uwe na Erick kwakweli”
“Kwanini?”
“Nimejua tu ushampenda, Erick huwa anapendwa na wadada wengi sana sababu ana sura ya mama yake na mwili wa baba. Ni mzuri kwakweli wa kuvutia na wengi wanampenda”
“Kwasababu watu wengi wanampenda ndio hafai kuwa na mimi?”
“Aaah hiyo sio sababu ila Erick nahisi kuna kipindi aliathirika kisaikolojia”
“Kwanini?”
“Ni anabadilisha wasichana Yule kama nguo, yani kila siku nafanya kazi ya kumpa ushauri maana magonjwa mengi ila anajidai wanamfata wenyewe. Erick amekuwa na msichana mmoja anaitwa Sia, ni mvumilivu sana yani Yule Sia hata amfumanie hapo Erick hakubali kumuacha, yani atanipigia simu na kujiliza sana ila hamuachi Erick, yani Yule dada anampenda Erick balaa ila mdogo wangu Yule ni pasua kichwa”
“Aaah mfano mimi ananifaa kijana wa aina gani?”
“Wewe anakufaa kijana mpole, mtulivu na mwenye upendo wa dhati. Erica nakupenda sana na hakika ningependa urafiki wetu ukuwe na ningefurahi uwe wifi yangu ila sio kwa Erick, hapana kabisa Erick hafai, ni mdogo wangu ila hafai”
Tumaini alimwambia Erica ila hakujua alivyoumiza moyo wa Erica kila alipomwambia kuwa Erick hamfai ukizingatia nanampenda sana. Basi akaongea ongea nae pale na kumuaga, kama kawaida Tumaini alimkodia bodaboda Erica imfikishe hosteli.
 
SEHEMU YA 77


Erica alikuwa na mawazo sana siku hiyo, akikumbuka kuwa Erick alimuona na Bahati wakikumbatiana ila Erick aliondoka kwa hasira na mpaka muda huo hakumtafuta, Erica akiwaza kuwa amtafute yeye na kujaribu kumuelewesha ila kila alipokumbuka aliyoambiwa na Tumaini hakutaka tena kuwasiliana na Erick,
“Sijui kwanini nimetembea nae, itabidi kesho nikapime ukimwi. Kumbe Erick kawa muhuni vile, najuta mimi Erica”
Aliwaza sana na kumfanya aumie sana moyoni mwake, ila jumbe alizozipata toka kwa Bahati zilimpa faraja sana.
Kesho yake hakuweza kufanikisha lile swala lake la kwenda kupima maana masomo yalikuwa mengi sana, kwahiyo akajikuta akiwa yupo makinisana na masomo yake, na alishtukia kuwa mwezi huo ni mwezi wa mitihani kwahiyo alijishughulisha sana na masomo hata hakutaka kuwasiliana sana, hata dadake alipompigia simu na kumwambia kuhusu kuongea nae alimwambia kuwa kipindi hiko ana mitihani kwahiyo aongee nae kwa kipindi kingine.
Kwahiyo karibia mwezi mzima alikuwa busy sana na masomo yake hadi pale walipomaliza mitihani na kufunga chuo kwaajili ya kuingia mwaka mwingine, mtu pekee aliyekuwa akiwasiliana nae mara moja moja kwa kipindi hiko alikuwa ni Bahati tu.

Erica alirudi kwao likizo ila alijiona kuwa yupo tofauti sana na siku zote, kwanza alikuwa akichoka sana na muda mwingi alijisikia usingizi na kujiuliza kuwa atakuwa na tatizo gani, akawaza kuwa kesho yake aende hospitali ili akaangalie hali yake vizuri.
Kesho yake ilivyofika, kabla hajajiandaa kuondoka, walifika nyumbani dada zake wawili, dada yake Bite akiwa ameongozana na dada yake Mage, aliwasalimia na kuwakaribisha.
“Mama yupo?”
“Ametoka ameenda kwenye kikoba”
“Haya, kilichotuleta sio mama ila tuna shida na wewe”
“Shida gani?”
“Erica, inabidi tukakupime ujauzito”
“Mkanipime ujauzito kwanini?”
“Erica usije ukatutia aibu, hebu nenda kajiandae huko twende hospitali, tulikuwa tunangoja tu ufunge chuo mjinga wewe”
Erica aliwashangaa sana dada zake hawa ila hakuweza kuwabishia maana walikuwa wakimfatilia vilivyo, basi akajiandaa ili aende nao huko hospitali, ila Mage akawakatisha
“Bite, kwanini tujisumbue kwenda mpaka hospitali wakati kuna vile vipimo vya mimba!”
“Vinapatikana wapi sasa”
“Maduka yote ya madawa, nenda kanunue basi”
Mage akamuelekeza Bite kisha Bite akaondoka na kwenda kununua, kwahiyo Erica alibaki na dada yao mkubwa Mage ambaye alimuita Erica karibu,
“Mdogo wangu kwanini umekuwa na tabia za ajabu?”
“Hapana dada sina tabia za ajabu”
“Yani kweli wanaume wanakufata hadi nyumbani unasema huna tabia za ajabu kweli?”
“Sasa dada mnavyonifanyia hivi mnaona ni sahihi? Mimi ni msichana mkubwa sasa”
“Hatukatai ni mkubwa ila bado hujaolewa, upo kwenye uangalizi wetu. Unafikiri leo na kesho ukileta matatizo hapa aibu kwa nani? Sisi ndio tutaaibika Erica. Katika watoto wote wa mama sikufikiria kama wewe unaweza kuwa na tabia za ajabu kiasi nilichoambiwa”
“Hapana dada, sina tabia za ajabu mimi”
“Sasa mdogo wangu huwa unahangaika na nini, si utulie tu ukimaliza chuo utaolewa”
“Dada, aliyewaambia mimi nahangaika nani? Mbona mimi ni mpole tu”
Mage alitumia muda mwingi sana kumshauri mdogo wake huyu na kumwambia kuwa kwanini wameamua kuja kumpima ujauzito maana wamekuwa na mashaka nae halafu habari zake wamezisikia.
“Mmezisikia wapi dada?”
“Jua kwamba habari zako tunazijua”
Erica alijiuliza sana kuwa wanajua habari zake zipi na wanazijua jua vipi ila hakupata jibu.
Bite alirudi na kipima mimba, kisha wakamtaka Erica kukinga mkojo wake ambapo alifanya hivyo na wakapima pale nay eye akiwa anaangalia,
“Mungu wangu Erica una mimba? Aibu gani hii umetupa jamani Erica?”
“Nilijua tu dada, ndiomana nikakuzania tuje tumpime ujauzito, aliyeniambia anamjua sana huyu mdogo wetu, kipindi hiki alikuwa na mitihani ila alikuwa analala sana badala ya kujisomea, kumbe ana mimba loh!”
Erica alikuwa kimya tu akiwaza maana ni swala la aibu kweli ila hakujua afanye nini, dada zake nao waliongea kwa ukali sana na gadhabu kubwa.
“Bite mdogo wangu twende kwanza tukajadiliane cha kufanya, tukikaa hapa na huyu mtoto tutampasua bure”
Wakaondoka na kumuacha Erica pale, muda kidogo mama yao alirudi ila Erica hakumwambia ukweli mama yake kuwa dada zake walifika maana aliona ni swala la aibu sana na hakujua hata ataanzia wapi kumwambia mama yao, kwani hata yeye swala lile lilimchanganya vilivyo.
 
SEHEMU YA 78


Aliingia chumbani kwake na kuwaza sana, aliwaza kuwa kama hiyo mimba itakuwa ya nani,
“Mungu wangu, mdada wa chuo kweli na sijui mimba ya nani? Si akili mbovu hii! Je ya Erick au ya Bahati? Mungu wangu”
Aliwaza sana na kukumbuka kuwa alilala na Bahati halafu kesho yake akalala na Erick,
“Mmmh nimefanya umalaya na sasa nina mimba, hata sijui ni ya nani. Sijui nitafanyaje?”
Aliwaza sana, kisha akachukua simu yake na kumtumia ujumbe Erick,
“Nina mimba yako”
Kisha akamtumia ujumbe huo huo Bahati halafu akatulia kusikilizia kuwa yupi kati yao atakayejibu.
Muda kidogo simu yake ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni Bahati, hakutaka kupokea kwani hakutaka kusikika akiongelea habari za mimba

kwa mama yake, kisha Bahati aliamua kumtumia ujumbe.
“Erica kweli uyasemayo? Kama ni kweli basi nimefurahi sana, maana ndoto yangu ni wewe kuwa mke wangu na kuwa mama wa watoto

wangu, nakupenda sana Erica”
Alingoja ujumbe kutoka kwa Erick ila hakutumiwa ujumbe wa aina yoyote ule na kumfanya aumie sana moyoni mwake kuwa kwanini Erick

amemfanyia vile ilihali amemwambia kuwa ana mimba.
Muda kidogo simu yake ilianza kuita na namba ilikuwa mpya akaipokea,
“Habari, naitwa Sia. Nimeona ujumbe wako kwenye simu ya mpenzi wangu, tafadhari achana na Erick, habari za mimba utajijua mwenyewe

ila naomba uachane na Erick. Tuache kwa amani tunapendana sana”
“Kheeee”
“Usishangae, habari ndio hiyo. Erick ni mpenzi wangu. Kama ulikuwa hujui basi ujue, Erick ana mpenzi ambaye ndio mimi. Sitaki tena uwe

karibu na Erick achana nae”
Erica alikata ile simu kisha alijikuta akilia sana, tena alilia mno kama siku ambayo alisingiziwa shuleni kuwa amekutwa na Erick wakibusiana

yani alilia sana, hakuamini kuwa angeambiwa yale maneno na msichana wa Erick.
“Kumbe Erick ana mwanamke kweli? Alikuwa ananidanganya tu jamani! Mapenzi ni mabaya sana”
Alilia mno kwani moyoni mwake alimpenda Erick vilivyo na hata wangesema kuhusu ile mimba kama ingekuwa ya Erick wala asingejali kitu

ila kwanza hana uhakika na mimba ya nani halafu alichoambiwa na msichana wa Erick kilimuumiza sana, alijikuta siku hiyo akishindwa

kulala kabisa na kuwa macho siku nzima.
 
SEHEMU YA 79


Kesho yake walifika dada zake Erica na kumwambia mama yao kuwa wanataka kutoka na Erica, walimwambia kuwa ajiandae kisha

alipomaliza wakaondoka nae.
Erica hakuelewa ila dada zake walikuwa wakienda nae hospitali, walipofika Bite alibaki nje kisha mage akaenda nae kwa daktari,
“Huyu hapa ndiyo tuliongea habari zake umtoe mimba”
Erica akahamaki,
“Kutoa mimba!”
“Ndio, tena ufunge bakuli lako hilo hakuna kupiga makelele, ulibeba mwenyewe mimba kwenye starehe zako, hakuna atakayekubali umletee

aibu nyumbani”
Basi daktari akawaelekeza chumba cha kumpeleka Yule mgonjwa, yani Erica hakuweza kubisha chochote kwa dada zake maana akifikiria

kuwa mama yake ataambiwa ukweli ndio pale aliona uchizi kabisa.
Aliingia kwenye chumba na daktari aliingia na kumuandaa kwaajili ya kumfanyia zoezi la kumtoa mimba, muda kidogo Yule daktari

akapigiwa simu na kupokea. Erica alisikia tu daktari alichokuwa akijibu,
“Usiondoke bhana, nisubirie nje ya chumba cha mwishoni, kuna kazi nafanya naimaliza sasa hivi usijali…….. Nitakwambia nikitoka, ni muda

mfupi tu hata nusu saa haifiki……. Mimi na wewe tena, sisi ni kama ndugu rafiki yangu, nitakwambia bhana”
Kisha daktari akakata ile simu na kuanza kumshughulikia Erica, kwakweli maumivu aliyoyapata Erica alijikuta akiapa kutokufanya mapenzi

tena katika maisha yake, yalikuwa ni maumivu ya muda mfupi ila yalikuwa ya hali ya juu.
Daktari alivyomaliza alimpa pole, kisha akamwambia,
“Pumzika kidogo, nitamuandikia dadako dawa za wewe kwenda kutumia pole sana”
Daktari alitoka, kwakweli Erica hakuwa na furaha kabisa kwani kile kitendo hakukitegemea na kilikuwa ni kitendo cha ajabu kwake,

akajifikiria kuwa Erick na Bahati watamfikiriaje maana ataonekana kuwa muuwaji, akajiambia kuwa atamwambia Bahati kwamba

alimdanganya kuhusu mimba, ukweli ni hakuwa na mimba wala nini kwahiyo swala la Bahati kwake halikuwa tatizo kabisa, akafikiria pia

kuhusu Erick kwanza hata kuhusu mimba Erick alikuwa hajui sababu ujumbe ulijibiwa na mwanamke wake kwa maana hiyo mwanamke

wake ndio alisoma ule ujumbe na lazima atakuwa ameufuta, kwahiyo hakuna tena wa kumuhofia kati yao.
Hakutaka kuendelea kupumzika zaidi mahali hapo kwani palimfanya awaze vitu vingi sana, kwa muda huo alitaka tu kwenda nyumbani, na

kama kupumzika basi akapumzike nyumbani kwao. kwahiyo aliinuka na kujiandaa kutoka ili awafate dada zake waondoke.
Erica alitoka kwenye kile chumba, kupiga jicho mbele yake aligongana macho na Erick akiwa amesimama na Yule daktari, kumbe ni Erick

ndiye alikuwa akiwasiliana na daktari muda ule ndani.
 
SEHEMU YA 80


Erica alitoka kwenye kile chumba, kupiga jicho mbele yake aligongana macho na Erick akiwa amesimama na Yule daktari, kumbe ni Erick

ndiye alikuwa akiwasiliana na daktari muda ule ndani.
Erica alitamani hata kurudi ndani ila hata kama akirudi Erick alishamuona, kwahiyo akajifanya anaondoka kamavile hajamuona Erick ila

aliitwa,
“Erica, Erica”
Alisimama na Erick akamsogelea na kumuuliza,
“Kumbe ni wewe Erica uliyekuwa unafanya yale yasiyofaa kwenye kile chumba?”
Erica alimuangalia, na pale pale akamgeuzia kibao maana hakutaka apewe lawama kwa muda huo, alimwambia,
“Sasa kinachokushangaza ni nini?”
“Umeanza lini mchezo huo?”
“Leo”
“Kwanini Erica? Hujihurumiii, hujui kama watu huwa wanakufa kwa kufanya hivyo?”
“Usitake kunitibua Erick, nilikutumia ujumbe kuwa nina mimba yako ukampa simu mwanamke wako anitukane. Halafu leo ulitegemea

nifanyeje? Huyo mtoto ningezaa nilee peke yangu? Tena achana na mimi kabisa”
Erica akaondoka na kumuacha Erick akimshangaa sana maana alivyokuwa anaongea kana kwamba kitu alichokifanya ni sahihi wakati

hakiruhusiwi kabisa ila yeye aliongea bila hata ya mashaka.
Erick alirudi kwa Yule daktari na kuagana nae, ila muda anatoka ndio aliwaona Erica pamoja na ndugu zake wakiondoka pia ikabidi awafate

nyuma ili apajue anapoishi Erica.

Ilikuwa tofauti maana Bite alienda nao mpaka nyumbani kwake, alitaka mdogo wake augulie hapo kwanza, kwahiyo Erick alijua pale ndio

nyumbani kwakina Erica, kisha akaondoka zake.
Erica alionekana kutokupakubali kabisa kwa dada yake,
“Hapana dada, mngenirudisha nyumbani tu”
“Hapana, nyumbani nitakupeleka kesho kutwa, uugulie hapa kwangu”
“Hapana dada, nawaomba nirudi nyumbani”
“Erica usiwe mbishi, unajua haupo sawa na mama hajui ni sisi tu tunaojua, keshokutwa nitakupeleka nyumbani ubaya uko wapi?”
Erica alikubali kukaa kwa dada yake kwa muda ila kwa shingo upande kwani hakupenda kabisa kukaa hapo kutokana na vile alivyotaka

kufanyiwa na shemeji yake, yani aliamua kukaa kwa machale sana.

 
Back
Top Bottom