Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 81


Kesho yake Erica aliwasiliana na Bahati na kumuomba amtumie hela kwenye simu yake,
“Nitakutumia shilingi ngapi Erica? Simu yangu haina hela ya kutosha”
“Nitumie yoyote tu”
“Kwani uko wapi kwasasa”
“Nipo huku kwa dada na nina shida na hela”
Basi akatumiwa shilingi elfu tano na Bahati, kisha akatoka nje na kumuaga dada yake kuwa anaenda dukani kununua vocha,
“Niagize mdogo wangu nitaenda kukununulia”
“Hapana dada, dukani hapo tu acha niende mwenyewe”
Basi Erica aliondoka, na moja kwa moja alienda kutoa ile elfu tano na kufanya nauli ya kurudi kwao.
Mama yake alishangaa sana alipomuona,
“Vipi mbona hujarudi na dada yako wakati yeye kasema utarudi naye?”
“Mama, sitaki kukaa kwa dada. Nimemtoroka tu”
“Kwanini umefanya hivyo?”
“Mama, nimekumiss sana mama yangu hata sitaki kukaa mbali na wewe ndiomana nimemtoroka maana ningemuaga aisngekubali niondoke”
Muda kidogo mama yake alipigiwa simu na Bite akimwambia kuwa Erica haonekani,
“Yani ndio kafika huku muda huu huu”
Kisha mama akampa simu Erica aongee na dada yake,
“Hivi wewe Erica una matatizo gani? Mfano ungeniaga ungepungukiwa na nini? Kwanini unapenda kufanya mambo ya kijinga lakini”
“Nisamehe dada”
“Kiukweli unakera yani unakera sana”
Dada yake akakata simu, kisha Erica akaelekea chumbani, alikaa na kulia kwanza maana tayari alifanya kitendo ambacho hakutarajia kukifanya katika maisha yake, tayari alikuwa ametoa mimba, roho ilimuuma sana.
“Labda mtoto wangu ndio alikuwa huyo huyo, Mungu wangu jamani. Hivi familia zingine zikoje hizi? Eti nitawatia aibu, hivi ni aibu yangu au aibu zao? Yani mdada mkubwa wa chuo bado nachungwa kiasi hiki kweli?”
Alilia sana, hakuwa na raha hata kidogo, aliamua kulala tu.
 
SEHEMU YA 82


Erica hakuwa na hamu hata na simu yake kwani hakutaka kuwasiliana na yeyote Yule, akaiweka mbali naye kabisa akajikuta akipiga mahesabu tu ya wanaume aliotembea nao,
“Nilimpata Babuu, tulipendana sana tena sana ila Babuu kaishia kidato cha nne na kazi zake ni za kubangaiza, nikaachana nae na kuangukia kwa George, kweli kabisa kwa sifa za George ni msichana gani ambaye mahusiano yake hayaeleweki atamkataa George? Aliahidi kunioa na alionyesha kunipenda sana kumbe nae hamna kitu, sasa huyu niliyekutana nae ufukweni ndio balaa, anajitia hadi kulia kwasababu yangu ila hali yake ya maisha ni ngumu sana. Nikaamua kumkubali Erick ambaye ni mwanaume wa maisha yangu ila kumbe ana wanawake kibao. Hivi mapenzi ni nini? Mbona yananitenda hivi jamani? Sitaki kuwasiliana na yeyote kati yao, bora hata Babuu ila sidhani kama atanipenda tena”
Alikuwa na mawazo sana na kuamua kulala tena hadi kunakucha.
Siku hiyo siku nzima alijishughulisha na kazi za nyumbani hata simu hakutaka kushika tena ingawa alijua atakapoichukua atakutana na simu za kutosha toka kwa Bahati ila hakujali kwa muda huo .

Kwenye mida ya saa mbili usiku ndipo alichukua simu yake kuona waliompigia, ila alikuta waliompigia sana ni wawili tu yani Bahati na Erick, kwa mara ya kwanza alikuta Erick amempigia simu zaidi ya mara tatu ingawa sio kawaida yake, anayepigaga simu hovyo ni Bahati.
Akakutana na ujumbe wa Bahati kwanza,
“Erica ulichonifanyia sikutegemea kabisa, nimekuja kukuona kwa dada yako kumbe alikuja na Yule bwanako mwenye gari! Erica umefanya nipigane sana na Yule jamaa, na kasema kuwa umetoa mimba, Erica umetoa mimba yangu kweli? Nalia tu mimi, jamani mwanangu wa kwanza umemuua Erica”
Ni pale alipogundua kuwa Bahati kakutana uso kwa uso na Erick nyumbani kwa dadake ila alijiuliza kuwa Erick alipafahamu vipi pale hakuwa na jibu, akashuka chini na kukutana na ujumbe wa Erick,
“Erica unajua wazi ni kwajinsi gani nakupenda, wewe msichana umekuwa fimbo kwangu ya kuumiza moyo wangu kila kukicha. Uliniumiza kipindi kile nikajua sababu ya utoto, umefanya niwe na tabia za ajabu sana kwa kukukosa, na muda nakupata kumbe ndio umekuwa hufai kabisa, Erica wa kunidanganya mimi huna mwanaume kumbe unaye? Wa kwenda kutoa mimba yangu Erica kweli? Na mimba yenyewe umemdanganya na jamaa kuwa ni yake. Kwakweli Erica umeniumiza sana, sikutegemea kama kuna mwanamke wa kuniumiza kiasi ambacho umeniumiza Erica. Niliwahi kukwambia kuwa sitoacha kukupenda, na kweli sitoacha kukupenda Erica. Kwaheri”
Ule ujumbe ulipasua moyo wa Erica, na ulionekana kutumwa jana yake, yani kwa muda huo hata hakuelewa kuwa ni kitu gani afanye, alichukua simu yake na kuanza kumpigia Erick ila ile simu haikupokelewa, akaamua kuandika ujumbe,
“Tafadhali pokea simu yangu Erick”
Ujumbe haukujibiwa pia, na kumfanya Erica kupatwa na mawazo yasiyokuwa na mwisho.
Siku hiyo hakuweza kulala kabisa na aliona kuwa usiku ni mrefu sana, alijitoa muhanga kuwa kesho akamtafute Tumaini ili amuelekeze alipo Erick akaongee nae,
“Kumbe Erick ananipenda kweli? Mungu wangu jamani, nitafanyaje mimi Erica jamani”
Muda huo Bahati nae alikuwa akimpigia simu ila zile simu za Bahati alihisi zikimpigia kelele tu kwani kwa muda huo alitaka kuona simu ya Erick tu.
Saa kumi na mbili asubuhi akaanza tena kumpigia simu Erick ila haikupokelewa simu yake, akaamua kumtumia tena ujumbe,
“Erick nakuomba pokea simu yangu usikie ninachotaka kusema”
Baada kama ya lisaa limoja ujumbe ule ulijibiwa,
“Useme nini kwangu? Ni kipi cha kuniambia Erica ambacho sikijui? Leo saa nne asubuhi naondoka na baba kwenda Afrika kusini, haikuwa safari ya kwenda mimi ila nimemuomba baba kwenda nae, nahitaji kutuliza akili yangu kwanza. Kama unataka kuongea na mimi njoo uwanja wa ndege kabla ya hiyo saa nne uniage, kwaheri”
Erica alihisi kuchanganyikiwa kabisa, akaenda bafuni kuoga kisha akajiandaa kwaajili ya kuondoka ili akamuwahi Erick.
Wakati anatoka, mama yake akamuuliza,
“Unaenda wapi asubuhi asubuhi hii Erica?”
Akawa anajiuma uma maana hakufikiria kama kuna maneno ya kumdanganya mama yake kwa muda huo,
“Mbona unajiuma uma, hebu kaa pale tuzungumze kwanza”
Yani Erica alitamani hata kumtukana mama yake maana hiyo ilikuwa saa mbili asubuhi nay eye alikuwa anataka awahi, ila atafanyaje sasa lazima amsikilize mama yake,
“Erica mwanangu ni siku nyingi sijakaa kuzungumza na wewe? Unaendeleaje kwanza?”
“Naendelea vizuri, ila mama si tuzungumze wakati nikirudi”
“Erica utanipangiaje muda wa kuzungumza na wewe lakini? Ujue mimi ni mama yako!”
Ilibidi Erica awe mpole na kumsikiliza mama yake ila kiukweli alikuwa akikereka tu na mabayo mama yake alimwambia kuhusu maisha maana alitaka kuondoka na mama yake alimkawiza hadi saa tatu na robo ndio akampa ruhusa ya kuondoka.
Erica alikata tamaa ya kuonana na Erick ila bado alienda uwanja wa ndege.
 
SEHEMU YA 83


Alifika uwanja wa ndege kwenye saa nne na nusu, yani hakuwa na furaha kabisa, wakati anasonga pale uwanjani akiwa na mawazo akagongana na mtu, alimuangalia na kumuomba msamaha,
“Uwe makini binti, mtoto mdogo hivyo unawaza nini?”
Erica alimuangalia vizuri sasa huyu mtu alikuwa ni mkaka wa kishombeshombe, Erica alikuwa kama akimshangaa hivi, Yule mkaka aliamua kujitambulisha,
“Naitwa Rahim, sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“Naitwa Erica”
“Mbona unaonekana kuwa na mawazo sana?”
Erica alikuwa kimya tu akimtazama, Yule mkaka alimwambia Erica,
“Anyway, chukua kadi yangu hii tutawasiliana”
Erica akachukua ile kadi na kuiweka kwenye pochi yake, kisha akaendelea na safari yake halafu Yule mkaka nae akaondoka zake.
Aliposogea mbele alishikwa bega, alipogeuka tu alikutana na Tumaini,
“Kheee Erica unafanya nini tena huku?”
Erica alijiuma uma, alitamani kumwambia ukweli ila alihofia ikabidi amrudishie swali yeye,
“Na wewe unafanya nini huku dada?”
“Mimi nimekuja kumsindikiza mdogo wangu Erick na baba wanaenda South”
“Kumbe mdogo wako kasafiri?”
“Ndio, yani mdogo wangu hadi namuhurumia”
“Kwanini?”
“Ngoja tukae mahali nikusimulie”
Wakaondoka mahali hapo na kutafuta sehemu yenye mgahawa na kukaa kisha kuagiza vinywaji na kuendelea na maongezi, ila kabla hawajaongea kitu chochote simu ya Tumaini iliita na Tumaini aliipokea,
“Tutaongea badae, saivi kuna sehemu nipo mara moja”
Alivyokata akamuangalia Erica na kumwambia,
“Yani huyu msichana king’ang’anizi huyo?”
“Msichana gani?”
“Si Yule Sia nilikwambiaga kuwa ni mchumba wa Erick”
“Kafanyaje tena?”
“Huyu msichana hajielewi hata sijui kwanini anamng’ang’ania hivyo mdogo wangu wakati mdogo wangu mwenyewe yupo kama kachanganyikiwa. Bora aende zake huko labda ajipatie hata mzungu”
Erica akatabasamu kidogo ila kiukweli alikuwa anaumia moyo, akamwambia tena Tumaini,
“Eeeh nieleze sasa”
“Sikia nikwambia, mdogo wangu Yule Erick kuna kipindi alikuwa akiishi na mamake mdogo na kuna shule moja alipelekwa mgeni tu halafu akafanya madudu na kufukuzwa, nilimuuliza mdogo wangu kwanini alifukuzwa shule akasema ni sababu ya msichana Fulani hajawahi kunitajia jina la huyo msichana ila alisema kuwa alimtongoza huyo msichana halafu huyo msichana akamsemea kwa walimu, kitendo kilichofanya Erick achukiwe na kufukuzwa shule ingawa mamake mdogo aliomba sana Erick asamehewe. Nilimuuliza kuwa ni kweli alimpenda huyo msichana huwa ananijibu hadi leo anampenda sana. Unajua sisi wanawake mara nyingine tunasababisha wanaume kuwa na tabia za ajabu ajabu, yani mdogo wangu Erick kawa mlevi, unajua anakunywa Yule balaa, kawa mtu wa wanawake lakini chanzo chote ni huyo dada”
“Kheee jamani masikini yake, je unatamani kumjua huyo mdada?”
“Sitaki hata kumjua maana nitamuumiza nikimjua, kaumiza sana maisha ya mdogo wangu, hili nililosikia sasa ndio balaa”
“Lipi hilo?”
“Nasikia Erick alikutana tena na huyo mdada na mdada akadai kuwa ana mimba yake, ila Erick kamshuhudia kwa macho yake Yule mdada akitoka kwa dokta kutoa mimba yake, yani katoa mimba ya mdogo wangu kumbe Yule mdada ana mwanaume mwingine. Juzi mdogo wangu kapigana na huyo mwanaume balaa, jamani mdogo wangu hajawahi kupigania mapenzi ndio mara yake ya kwanza. Huyo dada ni shetani kwakweli”
“Inasikitisha lakini”
“Kwakweli inasikitisha sana, yani mimi sipendi mwanamke anayetoa mimba simpendi kabisa. Unajua kutoa mimba ni uuwaji! Hivi sisi tungetolewa na wazazi wetu, tungekuwepo leo? Ila mwanamke muuwaji hana hata huruma anatoa mimba kwakweli, nawachukia watoa mimba. Huyo msichana nikimjua nitamraruwa kwakweli”
Erica hakuwa hata na usemi kwani muhusika alikuwa ni yeye tena ilionyesha Tumaini akiongea kwa uchungu sana jinsi gani alivyo na hasira na huyo msichana ambaye ndio yeye,
“Nimemwambia mdogo wangu, huyo msichana hakupendi labda anapenda pesa ulizonazo tu lakini upendo hana. Hivi Yule msichana anajiona kutoa mimba ndio kashinda, anadhani anabaki kuwa binti loh! Hapana hajui tu, anakuwa mama wa marehemu na sio binti tena”
Erica alinyamaza kwani yale maneno yalimgusa vilivyo, na kuuliza tena
“Kwahiyo mdogo wako atarudi lini?”
“Si oleo wala kesho, kwanza hakutakiwa kusafiri ila kwa hali aliyokuwa nayo, baba ameona bora aende nae. Halafu sasa mpaka tupo nae airport bado anajipa imani kuwa huyo msichana atakuja kuongea nae, cha kushangaza hadi wameingia ndani hakuna huyo msichana kuja wala nini. Mdogo wangu anatia huruma kwakweli, ila Erica huku airport ulifata nini?”
“Aaah dada alinipa mzigo kuna mfanyakazi wa hapa nilikuwa nimempelekea, na nimefika muda sana sema nimechelewa tu kuondoka, ningejua mpo hapa hata ningewatafuta. Namuonea huruma mdogo wako, mpe pole sana”
“Yani kuna wakati natamani kumjua huyo mama marehemu na atanitambua kwakweli, atanieleza sababu za kumuumiza moyo kaka yangu na sababu za kumuua aunt yangu”
Erica aliamua kuagana na Tumaini huku akidai kuwa anatakiwa kurudi kwao mapema ila ukweli ni kwamba maneno ya Tumaini yalimuingia vilivyo na moyo kumuuma sana.
Ila Tumaini alimwambia kuwa anahitaji waende wote nyumbani kwao ili akapafahamu anapoishi Erica, hakubisha juu ya hilo na kuamua kuondoka nae.

Walifika nyumbani kwao, kupiga jicho getini alimuona kuna kijana amekaa chini, aliposogea akagundua kuwa ni Bahati, kwakweli Erica alitamani kurudi na Tumaini walipotoka ila kabla hajafanya chochote Bahati aliinua kichwa chake na alipomuona kuwa ni Erica aliinuka na kwenda kumkumbatia huku akilia, ikabidi Erica amuulize,
“Sasa unalilia nini?”
“Nalilia kiumbe changu Erica, namlilia mwanangu”
Erica aligeuka na kumtazama Tumaini kama naye anayasikia yale maneno anayoyasema Bahati.
 
SEHEMU YA 84




Walifika nyumbani kwao, kupiga jicho getini alimuona kuna kijana amekaa chini, aliposogea akagundua kuwa ni Bahati, kwakweli Erica alitamani kurudi na Tumaini walipotoka ila kabla hajafanya chochote Bahati aliinua kichwa chake na alipomuona kuwa ni Erica aliinuka na kwenda kumkumbatia huku akilia, ikabidi Erica amuulize,
“Sasa unalilia nini?”
“Nalilia kiumbe changu Erica, namlilia mwanangu”
Erica aligeuka na kumtazama Tumaini kama naye anayasikia yale maneno anayoyasema Bahati.
Akamuona Tumaini akimuangalia pia, kwahiyo alijua moja kwa moja Tumaini amesikia kile kilichokuwa kikiongelewa na Bahati, kwahiyo alijishauri pale pale na halmashauri ya kichwa chake na kumsukuma Bahati pembeni,
“Erica unanifanyia hivi Erica?”
“Una matatizo gani wewe? Nishakwambia usinizoee”
Kisha akamuangalia Tumaini na kumshika mkono,
“Dada twende ndani”
Aliingia getini na Tumaini na kumuacha Bahati pale nje, Tumaini alikuwa na maswali mengi sana juu ya Erica kwanini kamfanyia kaka wa watu vile, kwahiyo akamuuliza,
“Erica, kwanini lakini umemfanyia vile”
“Nitakuhadithia ndani, ni chizi Yule”
Basi waliingia sebleni, kisha Erica akaenda chumbani kwa madai kuwa anaenda kuweka mkoba ila kiukweli alienda kumpigia simu Bahati maana kwa vyovyote vile Bahati asingeondoka pale kwao na angezidi kumsababishia matatizo, alipiga simu na Bahati alipokea,
“Samahani mpenzi wangu kwa nilichokufanyia nisamehe bure”
“Ila kwanini umenifanyia hivi Erica?”
“Nitakusimulia vizuri ila kwasasa naomba uondoke, unajua yule ni dada yangu na sikutaka ajue mahusiano yetu. Wakati ukifika watajua tu ila sio kwasasa, nakuomba mpenzi wangu niokoe mwenzio maana na mama nae akikukuta hapo ni balaa”
“Sawa, basi badae nitakupigia tuongee. Nakupenda Erica”
“Usijali, nakupenda pia”
Ilibidi ampe maneno ya kumlainisha ili iwe rahisi kumuondoa pale kwao maana angemuharibia sifa yake kwa Tumaini.

 
SEHEMU YA 85


Kisha akarudi kwa Tumaini, ambapo Tumaini alitaka haswaa kujua kuhusu Yule mkaka pale nje,
“Iko hivi, Yule mkaka alikuwa na mke wake anayeitwa Erica. Sasa inasemekana mkewe alikimbia na watoto kwahiyo Yule mkaka kama kaathirika kisaikolojia, yani yeye kila mdada anayeitwa Erica anadhani kuwa ni Yule mkewe basi ndio shida yake mara ukutane nae aanze kulia sijui leta mwanangu sijui nini na nini, ananikera balaa”
“Duh! Pole, sasa kama ndio hivyo atakuharibia sana ukija kupata mchumba”
“Kweli ataniharibia”
“Erica, sijawahi kukuuliza. Hivi una mchumba mdogo wangu?”
“Hapana dada”
“Kwanini?”
“Nayaogopa mapenzi, wanaume hawaaminiki”
“Ila wapo wenye mapenzi ya kweli, sema ni vigumu kuwatambua. Ila unaweza kwa mara ya kwanza usimpende mwanaume ila ukimkubali unaanza kumpenda taratibu, wenye mapenzi ya kweli wapo Erica”
“Basi nasubiria hao wenye mapenzi ya kweli, mmoja wapo anipende mimi”
Tumaini akatabasamu tu na kuanza kumuuliza Erica kuwa pale anaishi na nani,
“Hapa naishi na mama tu, hizo nyumba mbili hapo nje wanaishi wapangaji wetu. Mimi na mama tuna funguo kwahiyo asiponikuta atafungua na nisipomkuta nitafungua na kuingia ndani”
“Aaah sawa”
Simu ya Tumaini ikaanza kuita, akaichukua na kuingalia kisha akasema,
“Aaah ni Sia tena, huyu nae loh”
Akapokea na kuanza kuongea nae, Erica alitulia kimya akisubiri amalize kuongea halafu amuulize kuwa kuna nini tena kwa huyo Sia. Tumaini alipomaliza tu kuongea Erica alimuuliza,
“Kwani huyo Sia anataka nini?”
“Yani huyu Sia ananichekesha tu hadi nakereka na mashtaka yake, mwanaume mwenyewe kashaondoka sijui anafikiri huo msamaha nitamuombea wapi”
“Kafanyaje kwani?”
“Nasikia Yule mama marehemu wa Erick alituma sms kuwa ana mimba ya Erick halafu Sia akaifuta ile sms sijui na kuongea nae huyo mama marehemu, nasikia huyo mdada alishtaki kwa Erick basi ndio Erick kamchukia Sia na hata hii kuondoka hajamuaga”
“Kheeee!!”
“Ndio hivyo, wasichana wengine jamani. Ila mimi ningekuwa Erick ningempenda sana Sia, ana mapenzi ya dhati Yule dada ila sio huyo mama marehemu wake yani na nikimjua huyo mama marehemu jamani atanikoma”
“Inaonyesha Erick alimpenda sana huyo mdada”
“Ndio alimpenda sana ila msichana mwenyewe hapendeki, kwanza sio msichana ni mama marehemu. Yani simfahamu huyo mdada ila namchukia balaa, maisha yangu yote nitamchukia ni kivuruge Yule kaivuruga akili ya mdogo wangu”
Erica alipumua kwanza sababu laiti kama Tumaini angejua kuwa anayemsimulia ndio muhusika mwenyewe sijui angefanyaje ila hakuelewa.
Mama yake alirudi na alimtambulisha Tumaini kwa mama yake kisha Tumaini akaaga na kuondoka zake.

 
Wakuu ningependa kuomba radhi kwa kuchelewa kuituma. Huku kwetu Transformer ilileta shida, so hatuna umeme. Hapa nipo internet cafe.
Ratiba itabadilika kidogo lakini, umeme ukirudishwa mambo yataenda sawa.
 
SEHEMU YA 86


Erica alienda chumbani kwake ila alihisi akili yake yote ikivurugika kwani alijikuta akifikiria sana kuhusu Erick, akakumbuka toka siku ya kwanza ambayo Erick alifika shuleni kwao, akakumbuka jinsi Erick alivyomtongoza na jinsi walivyofukuzwa shule, akakumbuka jinsi alivyokutana nae tena na vile ilivyokuwa, aliumia sana moyoni,
“Kumbe ilikuwa ni kweli Erick ananipenda, nimempoteza Erick wangu mimi. Hivi na Tumaini akija kujua kuwa mwanamke mwenyewe ndio mimi? Mungu wangu, ila sijatoa mimba kwa kupenda, ni nani atakayeniamini kuwa sikutoa mimba kwa kupenda? Erick ndio anafaa kuwa na mimi na si mwingine yoyote, roho inaniuma mimi, nitampata wapi tena Erick jamani?”
Aliwaza sana na kumwambia ukweli Tumaini hakuweza kuwa labda aombe namba za Erick atakazokuwa anatumia kule alipo , hakuweza chochote alibaki akilia tu na moyo wake na kuzidi kutokuwa na raha wala furaha, kwa wakati huo hakuna aliyekuwa anaumiza akili yake zaidi ya Erick tu.
Aliamua kulala tu maana akili yake ilikuwa imevurugwa haswaaa.
Kesho yake akiwa anapangapanga vitu kwenye mkoba wake, akaona kadi alipo iangalia ilikuwa ya Rahim,
“Aaah Yule mkaka wa jana uwanja wa ndege, mmmh sijui nimpigie? Hapana kwakweli nitaingia kwenye majaribu mengine bure, mkaka mwenyewe mzuri vile na hivi nina mawazo ya Erick nisije kujikuta majaribuni bora niache tu”
Akaichukua ile kadi na kwenda kuitupa nje kwani hakutaka kujiingiza kwenye majaribu mengine maana aliona aliyo nayo yana mtosha.
Baada ya kuitupa alijishangaa akikaa hivi sura ya Yule mkaka ikimjia akilini,
“Shindwa shetani, sitaki mawazo ya kijinga mie, niliyo nayo yananitosha”
Akatoka tena nje na kuitafuta ile kadi kwenye matakataka kisha akaenda kuichoma moto kabisa ili asishawishike kumtafuta Rahim kabisa maana aliona kama ipo kwenye matakataka kuna muda atajisahau na kuichukua tena kwahiyo akaona ni vyema kuichoma moto kabisa, kisha akarudi ndani na kuendelea na kazi zake zingine.
 
SEHEMU YA 87


Zilipita kama siku mbili huku Bahati akimuomba muda wa kuzungumza nae, alimuomba sana ikabidi Erica akubali kwenda kuongea na Bahti, walienda ufukweni kwaajili ya maongezi kwani Bahati alitaka kujua kuhusu mimba. Alivyofika alimkuta Bahati ameshafika muda tu kwahiyo alikaa na kuanza maongezi nae,
“Niambie ukweli Erica, ulitoa mimba yangu”
“Bahati, hivi ni nani aliyekupa hizo habari unajua unanishangaza”
“Nilikutana na Yule mwanaume wako mwenye gari, nikaanza kugombana nae ndio akasema umetoa mimba yake, nikamwambia ni yangu basi ndio ugomvi wetu ulikuwa hapo”
“Una uthibitisho gani kuwa mimi nilikuwa na mimba na una uthibitisho gani kuwa mimi nilitoa mimba”
“Sina uthibitisho zaidi ya ujumbe ulionitumia kuwa nina mimba”
“Nikikwambia kuwa ule ujumbe nilituma kukupima imani yako utaniamini?”
“Kunipima imani?”
“Ndio, nilitaka kujua kama unanipenda kweli. Wanaume wengi wanaposikia wanawake zao wana mimba huwakimbia ndiomana nilitaka kujua na wewe utafanyaje”
“Kwahiyo si kweli kwamba ulikuwa na mimba?”
“Sijawahi kuwa na mimba Bahati”
“Na si kweli kama umetoa?”
“Nitatoaje mimba ambayo sijawahi kuwa nayo, hata nakushangaa kwakweli. Huyo mkaka atakuwa na yake tu, sijawahi kuwa ni mimba mimi na sijawahi kutoa mimba mimi”
“Erica unaniambia ukweli?”
“Ndio, kwanini nikudanganye sasa?”
Bahati alimuangalia Erica ila kwavile alikuwa anampenda sana ikabidi amkubalie kwa chochote alichokisema wala hakuweza kumpinga.
“Kaninunulie juisi basi, kweli unanikalisha hapa tunaongea tu bila hata kinywaji?”
Bahati akaona ni kweli, kwahiyo akainuka ili akamnunulie juisi, muda huo Erica nae akainuka na kuanza kutembea tembea pembezoni mwa maji, alijisemea mwenyewe,
“Mwanaume kununua juisi tu anapata mawazo, je kulea mtoto ataweza huyo! Yani hapa nimebugi, nimebugi kabisa sijui nifanyeje kumuepuka mtu huyu na kaniganda kama ruba”
Wakati anajisemesha aligongana na mtu mbele yake, kumuangalia ni Yule mkaka aliyekutana nae uwanja wa ndege Rahim, na huyu mkaka alimkumbuka vizuri sana Erica, kwani alimuita kwa taratibu,
“Erica”
“Samahani”
“Usijali, inaonyesha mar azote unakuwa na mawazo sana. Na mbona haukunitafuta?”
Erica alikuwa akijiuma uma tu kwa maelezo, Yule mkaka akatoa kadi yake nyingine ya namba na kumpa Erica,
“Naomba unitafute, nina kitu muhimu sana cha kukwambia wewe. Au huna vocha?”
“Hapana ninayo”
Yule kaka alitoa elfu ishirini mfukoni mwake na kumkabidhi Erica,
“Tafadhali pokea, weka vocha unipigie”
Erica alichukua ile hela na kuiweka mfukoni, kisha akaondoka zake na kurudi alipokaa, akamkuta Bahati amechukia sana,
“Mbona umechukia hivyo?”
“Yule ulikuwa unaongea nae pale ni nani?”
“Mmmh jamani Bahati ndio uchukie hivyo kweli?”
“Ndio, ni nani Yule?”
“Alikuwa ananiuliza tu mazingira ya huku hayajui vizuri”
“Anakuuliza hajui kama wewe ni mke wa mtu”
“Mmmh ushaanza na wivu wako, hebu tuondoke”
Bahati alionekana wazi kuchukizwa na kile kitendo cha Erica kuzungumza na Yule mkaka, kwahiyo Erica aling’ang’ania kuondoka na ikawa bora kwao kuondoka tu kwa muda huo.
Erica alifika tena nyumbani kwao na kuchukua kile kikadi chenye namba ya Rahim, akataka ampigie ila moyo wake ukasita akaamua kwenda tena nje kukichoma moto akiogopa kuingia mtegoni.
Erica alijaribu kumuweka Bahati moyoni ila ilikuwa ngumu sana kwake kwani upendo wake ulikuwa kwa Erick tu na kitu hiko kilisumbua sana akili yake, akajikuta akitamani sana kuwasiliana na Erick.
 
SEHEMU YA 88


Siku hiyo aliamua kwenda kumtembelea Tumaini ila lengo lake lilikuwa ni kuweza kuongea nae apate namba ya Erick yani alitaka ajaribu kutumia maneno ya ujanja apewe namba ya Erick kwani hakutaka Tumaini ajue ukweli kuwa kivuruge ndio yeye.
Alifika kwa Tumaini na kusalimiana nae, ila kabla hajaanza nae maongezi mengine Tumaini alipata ugeni, na mgeni huyo alikuwa mdada ambapo Tumaini akamtambulisha Erica,
“Erica, huyu ni wifi yangu mchumba wa Erick anaitwa Sia. Sia, huyu ni mdogo wangu pia anaitwa Erica”
Basi Erica akasalimiana na Yule Sia ila alishangaa sana kwani yeye alihisi kuwa labda Sian i mdada asiyevutia, alishangaa kumuona Sian i msichana mrembo sana tena anavutia hata akashangaa inakuwaje na yeye anasumbulkiwa na penzi la Erick wakati anaweza akamuacha na kupendwa na mkaka mwingine.
Sia alionekana kuwa na maongezi binafsi na Tumaini ila Tumaini aligoma kwenda pembeni,
“Sia, ongea tu hapa hapa nakusikiliza”
“Mmmh wifi jamani!”
“Ndio, mi nina mambo yangu hapa, wewe ongea tu”
“Umewasiliana na Erick?”
“Hapana, vipi wewe umewasiliana nae?”
“Ndio, nilimpigia simu ila inaonyesha alikuwa amelewa sana”
“Ila kulewa si ndio kawaida yake”
“Dada nisaidie, nampenda Erick ujue, yani nampenda sana. Kiukweli hataki hata kuongea na mimi, nimembahatisha tu na anasema alijua ni mtu mwingine hakujua ni mimi. Akaanza kulalamika kuwa namba nimepewa na nani, na kusema hapokei tena simu yangu. Dada nampenda sana Erick”
“Sasa Sia, mimi nitakusaidiaje hapo wifi yangu? Maana hata mimi mwenyewe namuonea huruma sana mdogo wangu”
“Dada, nina wazo”
“Wazo gani?”
“Ongea na Erick akuelekeze anapoishi huyo msichana tumtafute, maana nahisi huyo msichana kuna kitu amemfanyia Erick sio bure”
“Umesema jambo la msingi, sasa tukishampata tutafanya nae nini?”
“Tukishampata najua cha kumfanya wifi, mi nataka Erick arudi kwenye akili sawa na mwanzo. Yani sijui kwanini alikutana tena na huyo shetani”
“Sasa nawaza, hivi Erick atakubali kweli kututajia jina au anapoishi huyo mdada? Atakubali kweli Erick?”
“Hapo pagumu wifi, ila tukimfahamu tu mchezo umeisha”
Erica akaona sasa yupo hatarini ila akayatumia maongezi yale kama nafasi ya yeye kupata namba ya Erick, akatumia uongo wa kuwashawishi ili apewe yeye namba ya Erick,
“Dada nina wazo”
“Wazo gani tena Erica”
“Nipe namba za Erick, niwasiliane nae najua hajanizoea kivile ila nitajaribu kuongea nae hadi anitajie huyo mwanamke, nitamwambia kuwa sitakwambia wewe wala nini ila nitamdanganya mpaka atanitajia”
“Mmmh Erica utaweza kweli? Unajua humjui Erick vizuri eeh tena akijua ni mtu usiyemjua atakuzimia na simu kabisa”
“Sidhani kama anaweza fanya hivyo”
Sia nae akaunga mkono hoja ya Erica, laiti kama angejua ndio mke mwenzio yani asingekubali kabisa.
“Wifi nadhani ungempa tu huwezi jua akamtajia labda, tujaribu tu maana Erick hashikiki kwasasa”
Basi Tumaini akamtajia namba Erica halafu wakaendelea kupanga mipango yao ya kufanya akipatikana huyo kivuruge.
 
SEHEMU YA 89



Erica alirudi kwao akiwa na mawazo sana kuwa laity wakijua kuwa mtu wanayemtafuta yupo karibu yao itakuwaje, yani alihisi kudata kabisa.
Alivyofika tu alianza kupiga ile namba ila iliita bila ya kupokelewa na kujiambia kuwa ataendelea kuipiga kesho yake, ila muda kidogo alipigiwa simu na namba mpya,
“Hallow Erica, mimi ni mrs.Peter sijui unanikumbuka?”
“Nakukumbuka ndio, shikamoo”
“Marahaba mwanangu, umenitupa sana, naomba uje unisalimie jamani”
“Nitakuja mama”
“Naomba uje kesho, nakuomba Erica”
Basi Erica akaongea na Yule mama na kukubaliana nae kuwa kesho yake ataenda kumsalimia.
Kesho yake ilivyofika alijiandaa na kwenda kumsalimia Yule mama, alifika hadi kwa Yule mama na kukaribishwa na Yule mama hadi ndani, tena alionyesha kuwa na furaha sana.
“Erica jamani, nilikukumbuka sana. Mbona ulinitupa hivyo?”
“Nisamehe bure mama yangu”
“Haya nimekusamehe, mwanangu wa kwanza karudi toka uingereza, yani nimetafuta namba yako hatimaye jana nikaipata. Nataka nikutambulishe umjue”
Basi Yule mama aliinuka na kwenda kumuita mwanae, Erica alikuwa ametulia tu pale sebleni na hakuwa na wazo lolote lile.
Yule mama alifika na mwanae, Erica akainua macho yake kumtazama mtoto wa Yule mama, alikuwa ni Rahim Yule ambaye amekuwa akichoma kadi ya mawasiliano nae.
 
SEHEMU YA 90


Yule mama alifika na mwanae, Erica akainua macho yake kumtazama mtoto wa Yule mama, alikuwa ni Rahim Yule ambaye amekuwa akichoma kadi ya mawasiliano nae.
Erica alikuwa ameduwaa tu, hadi Yule mama akamshtua,
“Erica mwanangu jamani una mawazo gani? Huyu ni mwanangu anaitwa Rahim”
“Nashukuru kumfahamu”
“Rahim, huyu ni mwanangu pia anaitwa Erica”
Basi Erica na Rahim wakapeana mikono ya kusalimiana kamavile hawajawahi kuonana sehemu yoyote.
Baada ya salamu, Rahim aliondoka na kurudi chumbani kwahiyo pale alibaki Erica na Yule mama,
“Huyu ni mwanangu wa kwanza”
“Aaah ila mbona yeye kama mpemba mpemba hivi?”
“Hahaha Erica, safari ya ujana ina mambo mengi sana. Baba yake na Rahim ni mpemba kweli ila sikuweza kuoana nae sababu kwao hawakutaka aoe mwanamke ambaye sio sawa na wao, ila nashukuru alimuhudumia mtoto vizuri kabisa na mpaka kawa mkubwa hivyo”
“Na mwanao mwingine ni mpemba pia?”
“Hapana, yeye nilizaa na mwanaume mwingine ila sikuolewa nae kwani alikuwa ni mume wa mtu halafu mimi nilizaa nae bila kujua. Mwanangu, unatakiwa kujua sana hawa wanaume kabla hujajiingiza kwenye mapenzi”
“Asante kwa ushauri, ila umepata bahati ya kuolewa tena”
“Nimepata bahati kweli maana aliyenioa sijazaa nae kabisa ila ana upendo na mimi. Sikia mwanangu nikwambie, linda sana ujana wako. Wewe ni binti wa kike, mzuri, mpole unaonyesha ni mtulivu. Tulia hivyo hivyo mpaka pale utakapopata anayekufaa katika maisha yako, msichana unapozaa mtoto wa kwanza kama bado hujaolewa jua kwamba unajipunguzia nafasi za kuolewa na mwanaume umtakaye. Maana ukiwa hujazaa bado una nafasi kubwa sana ya kuolewa tofauti na ukizaa, ukija kuzaa mtoto wa pili nyumbani, thamani yako inashuka zaidi, watatu na kuendelea utajikuta kuolewa inakuwa ni ndoto kwako au unaolewa na mwanaume usiyemtaka sababu tu amesema atakuvumilia. Inatakiwa uwe makini sana, wanaume waaminifu wapo na wachezeaji wapo”
Maneno haya yalimuingia akilini Erica, wakaongea ongea na huyu mama kisha Erica akamuaga huyu mama kuwa anaondoka ila huyu mama akamuita mwanae Rahim kuwa ampeleke Erica kwao,
“Rahim, hakikisha unamfikisha kwao kabisa”
“Sawa mama, hakuna tatizo”
Basi Erica akaondoka na Rahim kwa kutumia gari ya Rahim.
 
SEHEMU YA 91


Walipokuwa njiani, Rahim alimuuliza Erica kuwa anapendelea kula nini,
“Mmmh napenda sana ice cream”
“Aaah kuna supermarket hapo mbele wanauza nzuri sana, ngoja tupitie mara moja”
Basi Rahim akapeleka gari lake mpaka kwenye supamaketi moja wapo na kushuka pamoja na Erica, kisha wakaingia kwenye lile duka kubwa, wakati wanachukua zile koni kuna mtu alimgusa bega Erica, alipogeuka na kumuangalia alikuwa ni Tumaini, basi akakumbatiana nae kwa furaha,
“Mmmh Erica mdogo wangu ndio upon a shemeji nini?”
Erica akawa anacheka tu, ila Tumaini akamvuta pembeni na kumnong’oneza
“Mdogo wangu unajua kuchagua, mshikilie haswaa unaendana nae”
Kisha Tumaini akawaaga, nao ndio walikuwa wanatoka wakaelekea kwenye gari.
Rahim alihakikisha kweli anamfikisha Erica hadi nyumbani kwao, kisha akamwambia
“Sasa leo itabidi unipe namba zako maana kila siku hunitafuti”
Erica hakuona tatizo kumpa Rahim namba zake kwani alijua hata asingempa basi lazima Rahim angepewa na mama yake, basi akaagana nae pale kisha Erica akaingia ndani kwao.
Alipoingia tu ndani alikuwa anapigiwa simu, na alipoangalia ni namba mpya akapokea
“Erica, ni Rahim hapa. Unajua nishakumiss tayari”
Erica akawa anacheka tu, kisha Rahim aliendelea kuongea,
“Kama hutojali naomba kesho kutwa tuonane Erica, niongee na wewe japo kwa ufupi tu moyo wangu utaridhika”
Erica alikuwa anatabasamu tu na hakuelewa kuwa akubali au akatae, ikabidi akamwambia,
“Basi nitakwambia badae kama itawezekana”
“Naomba iwezekane Erica, please nakuomba”
Basi akaongea ongea nae na kukata simu, Erica akajikuta akiwaza sana, ila akakosa majibu kwani aliona ni jinsi gani Rahim akiingia kwenye moyo wake kiasi kwamba kumtoa ilikuwa ngumu sana ila akakumbuka pia kuwa anampenda Erick ila akawaza kuwa je Erick atampenda tena baada ya ile kushuhudia kuwa alitoa mimba.
Usiku wa siku hiyo alipigiwa simu na Tumaini pia, na alipopokea swala lilikuwa lile lile la kumsifia Rahim kuwa Erica kachagua mwanaume wa maana,
“Yani kama Yule kaka ningemuona miyeyusho ningekwambia pale pale mdogo wangu, ila Yule ni mwanaume tena ni mwanaume haswaa anayeendana na wewe”
“Mmmh dada”
“Kweli mdogo wangu, Yule Rahim ni mwanaume anayekufaa”
Erica alikuwa akitabasamu tu kwani moyoni mwake alimpenda sana Erick ila alivutiwa na huyu Rahim.
Ilipokatika simu ya Tumaini iliingia simu ya Bahati nayo ilimkera sana ila aliamua kupokea maana akili za Bahati alizijua vizuri kuwa asipopokea basi kesho atakuja hapo kwao.
“Nimekumiss Erica”
“Asante”
“Mmmh hata wewe hujanimisi jamani!”
“Sasa unataka nikwambie nini?”
“Niambie kuwa umenimiss pia”
“Kheee makubwa, haya nimekumiss pia”
“Naomba kesho kutwa tuonane mpenzi”
“Aaah hapana, kesho kutwa nipo busy sana”
“Busy na nini Erica wakati chuo mmefunga?”
“Aaah kuna sehemu naenda kesho kutwa, labda tuonane kesho”
“Kesho nitakuwa kazini Erica ndiomana nimekuomba kesho kutwa”
“Basi haitawezekana maana kuna sehemu naenda”
“Jamani Erica, basi nikusindikize”
“Hapana, hairuhisiwi kwenda na mwanaume”
“Duh! Haya bhana”
Akaongea ongea nae na kukata simu huku akichukia jinsi gani Bahati amekuwa akimfatilia vile,
“Sijui yukoje, yani kahisi kesho kutwa nina mtoko anajifanya kutaka kuonana na mimi. Anakera huyu loh!”
Erica alikuwa akichukizwa sana na mwenendo wa Bahati kwani hakupenda kabisa jinsi Bahati alivyokuwa akimfatilia, basi akaamua kulala.
 
SEHEMU YA 92


Kulipokucha baada ya kufanya kazi zake za hapa na pale, alishangaa kutembelewa na rafiki yake na alimkaribisha vizuri sana. Ni muda mrefu sana tangu rafiki yake huyo kumtembelea ni tangu wakati wanasoma sekondari, alikuwa ni Johari.
“Nilikuwa najaribisha tu kama nitakukuta”
“Nipo rafiki yangu, nipo likizo”
“Hongera sana kwa kuchagua njia sahihi ya kusoma rafiki yangu, ila hata mimi nataka nirudi shuleni”
Walishauriana pale umuhimu wa masomo, na baada ya maongezi ya hapa na pale ilibidi leo Erica amuulize vizuri Johari kuhusu Erick kipindi kile.
“Hivi Johari, ni kweli Erick alikuwa muhuni sana kipindi kile?”
“Kwanza nisamehe Erica kuhusu huyo Erick, kiukweli rafiki yako nilisumbuliwa na wivu. Erick hajawahi kunitaka tena hata Manka hajawahi kutongozwa na Erick, kumbe Manka ndio alikuwa anamfatilia Erick”
“Mmmh kumbe, sasa kwanini ulikuwa unaniambia vile kuwa Erick ni muhuni?”
“Sikia Erica, kipindi kile moyo wangu ulikuwa unaendeshwa na wivu yani nilikuwa na wivu sana kiasi kwamba niliona wewe hufai kuwa na Erick, mvulana mzuri vile. Kiukweli Erick alinifata na kuniambia nikwambie kuwa anakupenda sana sababu mimi ni rafiki yako, ila mimi nilirudi na kumwambia kuwa Erica hataki hata kusikia habari hizo na amesema siku ukimtongoza basi atakusemea kwa walimu. Erick alionekana kujisikia vibaya ila alinihakikishia kuwa lazima atakuja kukwambia ukweli kuwa anakupenda. Ndiomana nikatumia njia ya kumchafua Erick kwako kwa kukwambia kuwa ni muhuni sana ili usimkubali”
“Aah Johari jamani, kwanini ulinifanyia hivyo? Umefanya niwe na chuki na Erick kwa kipindi chote jamani Johari!”
“Ndiomana naomba msamaha maana chuki zaidi niliijenga mimi mwenyewe kwa Erick nakumbuka kuwa mimi ndio nilimueleza ukweli mama yako na mimi ndio niliwaeleza ukweli walimu. Na baada ya Erick kufukuzwa shule nilimfata na kumwambia kuwa wewe ndio umesababisha yote, nilisema kwamba umemsemea kwenu na umeenda kumsemea kwa walimu, nilisema maneno mengine hata hayafai ili kuhakikisha tu kuwa Erick hawi karibu na wewe”
“Ndio urafiki huo Johari? Ni urafiki au uuwaji huo? Unajua mara nyingine mtu unapata laana bila ya kujua umepata vipi laana kumbe ni mambo uliyotenda kwa wenzio. Sikia hata kama sikuwa katika rika la kujiunga na mapenzi ila ningetafuta njia bora ya kutokuwa na Erick kwa kipindi kile kuliko njia ambayo umeiweka wewe. Johari, nadhani hujui ila jua kwamba nampenda sana Erick kwahiyo umehusika kuliua penzi la watu waliopendana”
“Nisamehe Erica, hata nikikutana na Erick siku moja nitamwambia ukweli”
Kiukweli Erica hakupenda kabisa vile ambavyo rafiki yake alimfanyia kwa kipindi cha nyuma kwani anaona kama hayo mambo yamechangia yeye kuwa tangatanga wa mapenzi na mwisho wa siku kumpata hadi king’ang’anizi kama Bahati.
Johari baada ya kuona Erica hana furaha tena aliamua kuaga na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 93


Erica aliingia chumbani kwake na kuwaza sana kuwa amekosa penzi la mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwake kwa kusikiliza maneno ya watu kuwa hafai, akachukua tena simu na kujaribu kupiga ile namba aliyoiomba kwa Tumaini ila alipiga weee bila ya kupokelewa na kumfanya azidi kupatwa na mawazo na kukosa raha kabisa.
Muda kidogo akapigiwa simu na Rahim na kupokea,
“Erica natumaini swal la kukutana na wewe kesho bado lipo palepale, tafadhari usibadili mawazo”
Erica akacheka tu na kukubali kuonana nae, kisha wakapanga mahali pa kukutania, baada ya kukata simu akajiambia,
“Usikatae wito, kata neno. Ila mmmh huyu kaka akinitongoza nitaweza kumkataa kweli? Ila bora kuwa na huyu kuliko Bahati maana kumpata tena Erick ni ndoto kwangu”
Wakati anawaza hayo tu iliingia simu ya Bahati na akaona huyu anamzingua sasa hakupokea kabisa na akaamua kuzima simu kabisa baada ya Bahati kumpigia kwa muda mrefu.
Kisha alitoka na kwenda kuongea na mama yake,
“Hivi mama, mimi nafaa kuolewa na mwanaume wa aina gani?”
“Umeshapata mchumba nini?”
“Hahaha hapana mama, si ulisema mpaka nimalize chuo!”
“Sio mpaka umalize chuo mwanangu, ila hata kama bado kumaliza chuo ila ukapata mchumba wa maana mlete nyumbani ajitambulishe na ikiwezekana alipe mahali kabisa, halafu harusi tunaweza tukafanya pia ila kama anaeleweka”
“Sasa ni mwanaume wa aina gani?”
“Erica mwanangu, unatakiwa uolewe na mwanaume msomi, mwenye kazi, awe na pesa, ikiwa ana nyumba na gari itapendeza zaidi. Usije ukaniletea kapuku hapa, nitaweka wapi sura yangu mtaani mimi? Inatakiwa ulete mwanaume wa maana”
“Aaah sawa mama, ikiwa ana pesa je halafu sio msomi?”
“Na wewe huyo asiye msomi unadhani kuna la maana anaweza fanya na hizo hela? Huoni kama ni sifa kuwaambia wenzio mume wangu kamaliza chuo kikuu, ana degree au ana masters au phd huoni kama ni sifa hiyo! Sio kusema mume wangu kaishia form four sijui la saba. Hebu mwanangu ondoa mawazo ya watu ambao hawajasoma, lete msomi hapa nyumbani lakini awe na hela”
“Sawa mama nimesikia”
Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake ila kwa maneno ya mama yake aliona kuwa ni Rahim tu ndiye anayemfaa kwa wakati huo ila sio Bahati maana hana kigezo hata kimoja anachokitaka mama yake.
 
SEHEMU YA 94



Alifikiria sana, hakuwasha simu yake kabisa kwa kuhofia kupigiwa na Bahati wakati amelala na kupata usumbufu.
Asubuhi palipokucha aliwasha simu yake na akapata wazo la kumpigia tena Erick kwani licha ya kwamba alimpenda sana Erick ila alitaka kuongea nae kuhusu swala la yeye kutokutajwa kwa Tumaini kuwa ndiye muhusika maana atamchukia, kwahiyo alitaka kuongea na Erick kuhusu swala hilo na kujaribu tena kumwambia kuwa anampenda, aliipiga tena namba ile ya Erick kwa zaidi ya mara tatu ila haikupokelewa na kumfanya ajihisi vibaya.
Akatoka na kwenda kufanya shughuli zake za hapa na pale huku akisubiria muda ambao Rahim atamwambia kuwa ajiandae waonane, alipomaliza shughuli zake alichukua tena simu yake na kupiga namba ya Erick ila haikupokelewa kama kawaida, kwa wakati huu akaamua kutuma ujumbe kwa Erick,
“Erick, mimi ni Erica. Nina shida sana na wewe, tafadhali pokea simu yangu. Usinichukie Erick”
Akamtumia na kukaa kwa muda ila haikuingia simu yoyote, muda kidogo akapigiwa na Rahim na kumwambia kuwa ameshafika lile eneo ambalo wamepanga kukutana kwahiyo anamsubiri.
Erica aliinuka na kujiandaa kisha kutoka, akamkuta mama yake sebleni
“Eeeh wapi saa hizi!”
“Naenda kwa rafiki yangu mama”
“Mmmh siku hizi sikuelewi kabisa Erica, kama umepata mchumba mlete tu ajitambulishe kuliko kujificha ficha hivyo!”
“Hamna mama, ni rafiki yang utu. Yule dada wa siku ile”
Alimaanisha kuwa ni Tumaini, na kumfanya mama yake kumruhusu bila ya kinyongo chochote.
Erica alitoka na kuondoka zake, ila kitu pekee ambacho hakukijua Erica ni kuwa siku hiyo Bahati alikuwa nje ya nyumba yao akimsubiri amuone anapoelekea kwahiyo alipotoka na kuondoka, Bahati alimfata kwa nyuma bila yay eye kujua chochote.
 
Back
Top Bottom