Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 108


Alivyofika chuo, alipishana na Dora ambaye alimfata nyuma,
“Erica”
Erica akasimama na kumsikiliza kuwa anasemaje,
“Erica, ulichofanya sio sawa”
“Kitu gani hicho?”
“Yani unasababisha George apigwe na kijana asiyeeleweka halafu polisi unajifanya kumkana George?”
“Sikia Dora, habari za George kwangu zilishafutika hata nashangaa kwa wewe kuzifufua tena, George sina mahusiano nae kwahiyo polisi ningekubali kuwa nina mahusiano na George? Siwezi, na sijamwambia anifatilie kayataka mwenyewe”
“Erica najua humjui George vizuri, ila nikwambie tu George hawezi kuridhika kwa ulichomfanyia na atakukomesha.”
“Usinitishe Dora, kwahiyo atanifanya nini?”
“Sikutishi ila nakwambia ukweli halisi, George huwa hapendi ujinga kabisa, na kwa mambo haya ya kijinga uliyomfanyia utajutia”
“Hebu achana na mimi Dora”
“Sawa ila George atakufanya kitu kibaya wewe, hutakuja kusahau katika maisha yako”
“Nimekwambia achana na mimi Dora, siogopi chochote.”
Kisha Erica akaondoka zake na kuelekea kwenye kipindi, alipomaliza kipindi kuna mkaka alimfata nyuma na kumshika mkono.
“Samahani dada, naitwa Derick sijui wewe unaitwa nani?”
Erica alimuangalia vizuri huyo aliyejitambulisha kwake maana jina kidogo tu liendane na Erick, akamuangalia sana na kumwambia
“Naitwa Erica”
“Nafurahi kukufahamu, naweza kupata mawasiliano yako?”
Katika swala ambalo lilikuwa halimpi shida Erica ni swala la kutoa mawasiliano yake, yani kwa yeyote aliyehitaji mawasiliano yake alimpa ila swala la kutongozwa ndio alikuwa anaangalia sana mwanaume mwenye mvuto ndio amkubali.
Kwahiyo alimpa namba Derick bila ya tatizo lolote lile, naye Derick alimshukuru sana Erica kisha akaagana nae.
 
SEHEMU YA 109


Erica alirudi hosteli na jioni ya siku hiyo alikuwa na kipindi kwahiyo alienda tena chuo, muda anaenda alipigiwa simu na namba mpya na mwenye ile namba alijitambulisha kuwa ni Derick.
“Naweza kuonana nawe muda huu Erica?”
“Hapana nina kipindi”
“Basi ukitoka kwenye kipindi”
“Hapana, nitaenda kulala hosteli”
“Basi naomba nije nikusindikize hosteli tu”
“Hapana, usijisumbue”
Kisha Erica akakata ile simu, na kuingia kwenye kipindi. Alipotoka alishangaa akiitwa na aliyekuwa akimuita alikuwa ni Dora, akasimama na kumsikiliza kuwa amemuitia nini.
“Erica, nakuomba tumalize tofauti zetu”
“Dora, mi nilishamalizana na wewe ila kuwa tena marafiki mimi na wewe hilo haliwezekani na halitawezekana kamwe”
Dora bado alikuwa akimbembeleza Erica huku akimpa maneno mbali mbali, kiasi kwamba kuja kushtukia, chuo kilikuwa kimya kabisa na kuona kamavile kabakia yeye na Dora tu. Ikabidi Erica amuage Dora kuwa anaondoka,
“Huogopi peke yako?”
“Siogopi”
Kiukweli alikuwa anaogopa ila hakutaka kumwambia Dora kwamba anaogopa, Dora akawa anacheka tu maana yeye alikuwa anaishi ndani ya hosteli za chuo ila Erica alikuwa akiishi hosteli za nje ya chuo.
Erica aliondoka pale huku akitembea haraka haraka, alisikia kuna mtu anamuita nyuma yake ila hakutaka kusimama kabisa kwani alikuwa na uoga sana, ila kufika mbele alikuta kuna vijana watatu wamemzingira na kumfanya aogope zaidi, na kabla hajafanya chochote alitokea George mbele yake, yani akiwa ni kijana wa nne.
 
SEHEMU YA 110


Erica aliondoka pale huku akitembea haraka haraka, alisikia kuna mtu anamuita nyuma yake ila hakutaka kusimama kabisa kwani alikuwa na uoga sana, ila kufika mbele alikuta kuna vijana watatu wamemzingira na kumfanya aogope zaidi, na kabla hajafanya chochote alitokea George mbele yake, yani akiwa ni kijana wa nne.
Uoga ulimzidi zaidi Erica, ila George alimsogelea na kumnasa kofi kisha akamkunja na kumwambia,
“Leo nadhani utataja jina la marehemu baba yako, maana leo tunaenda kukubaka wote wane”
Erica machozi yakamtoka, akashtukia akipigwa teke tu na kuanguka chini yani pale pale wale vijana walianza kumvua nguo kwa nguvu sana, huku George akitelemka chini na kuwa wa kwanza kumuingilia, Erica alitamani kupiga makelele ila mkaka mmoja alitumika kumziba mdomo Erica huku mwingine akimshika mikono na mwingine akimkamata miguu na kufanya iwe ngumu hata kufurukuta, Erica alikuwa akiugua moyoni na kumuomba Mungu muujiza utokee. Ila gafla alitokea mtu mbele ya wale vijana akiwa na mbwa na kuanza kuwabwekea huku akimfata George ambaye alikuwa chini na Erica na kumng’ata kwenye makalio, kitendo hiko kilifanya wale vijana wengine wamuachie Erica na wakimbie na George nae alimuachia Erica na kukimbia ambapo yule mbwa alikuwa akiwambiza.
Kisha aliinama Yule kijana aliyeenda na mbwa na kumuinua Erica pale chini huku akimpa pole kwa kilichotokea, kwakweli Erica alishangaa sana moyo wa huyu msamalia ila kwa wakati huo hakumgundua sababu ya mawenge ya kutaka kubakwa, Yule kijana alimsaidia Erica kujisitiri nguo zake kisha kumsaidia kutembea hadi walifika mahali penye mwanga karibu na hosteli, Erica alimtazama Yule kijana kumshukuru, akashangaa sana kuona Yule kijana alikuwa Derick, alimshukuru sana kwakweli na kumuomba akapumzike kwanza kuwa atazungumza nae kesho, ila Derick aliongozana na Erica hadi alipofika kwenye mlango wa chumba cha Erica ndipo akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 111


Erica alienda kubadilisha nguo na kuoga, kisha kurudi kitandani yani siku hiyo hata hamu ya kula hakuwa nayo alikuwa akijitafakari tu,
“Kwahiyo asingetokea Yule Derick ningebakwa na vijana wane leo, duh ningekuwa mtu kweli? Hivi kwanini wanaume wana tabia za hivi jamani, huyu George aliuumiza sana moyo wangu, na ni yeye aliyefanya hadi nimeangukia kwa Bahati sababu ya mawazo, leo hii ananifata tena mimi, anagombana na Bahati halafu anataka kunifanyia mimi mambo ya ajabu. Kwani mimi kibaya nilichofanya kwake ni nini? Hivi amesahau kuwa aliniacha mahali hata nauli ya kurudia sina jamani? Kwanini lakini wanaume wanakuwa hivi?”
Aliwaza sana Erica na kujihurumia, yani siku hiyo hata hamu ya kuwasiliana kwenye facebook hakuwa nayo maana moyo wake bado ulikuwa unatetemeka kwa kile kitendo kilichotokea.
Aliamua kulala tu muda huo maana alikuwa na uoga balaa, asubuhi na mapema aliamka na kilichomuamsha ni simu ya Derick aliikariri namba yake sababu alimpigia jana yake, akaipokea
“Erica samahani ila naomba nikufate twende hospitali ukapime ili uangalie kama wale vichaa hawajakuwekea madhara, na kama kuna madhara basi upate dawa mapema”
Erica aliona ni ushauri mzuri aliopewa na Derick kwahiyo alikubali na kujiandaa kisha Derick akampitia na kwenda hospitali kupima.
Walipima na kukutwa hana maambukizi yoyote ila alipewa dawa tu za kumzuia endapo kuna vilivyokuwemo na kutajiwa siku nyingine ya kuenda tena hospitali.
Waliondoka pale hospitali kisha Derick kumwambia Erica kuwa waende mgahawani wakapate jambo kitu cha kula maana walikuwa hawajala kitu chochote.
 
SEHEMU YA 112



Walikaa mgahawani na kuanza mazungumzo ambapo Erica aliendelea kumshukuru sana Derick na kumuuliza kuwa alijuaje kuwa yupo mashakani,
“Sikia Erica, kwanza utambue kuwa nakupenda na yote haya nimefanya sababu ya upendo wangu kwako”
Erica hakujibu chochote ila aliendelea kumsikiliza,
“Erica, mimi sikukutana na wewe muda ule ulipomaliza kipindi ila nilikuona muda tu na yule rafiki yako, nikakupenda na muda ule kipindi kimeisha nilikufata na kukuomba namba, nashukuru ulinipa. Sasa kuna muda nilimuona Yule rafiki yako uliyekuwa unaongea nae ule mchana, nilimkuta mahali akiongea na mkaka mmoja hivi, nikamsikia akisema nitamgelesha ili achelewe na awe peke yake wakati wa kuondoka na iwe rahisi kwenu. Sikuelewa ila nilihisi kama unaongelewa wewe, nilijiuliza ni kitu gani wanapanga kwako, sikupata jibu ndipo nilipoamua kukupigia simu jioni, nikiwa na lengo la kuzungumza na wewe ila ulisema kuwa una kipindi, nikakuomba kuwa nikusindikize ukitoka kwenye kipindi ila ulikaa, nilijisikia vibaya kwakweli na nikasema niache tu kama ilivyo. Ila kadri nilivyokaa ndivyo moyo ulivyoniuma, nikaamua kupigia simu tena ili nikutahadharishe hata kwenye simu ila sikukupata hewani, nilijua ni sababu ya kwenye kipindi ndiomana umezima ila sikuwa na raha kabisa, nilirudi ninapokaa bado sikuwa na raha, nilipoona ni mida ya kutoka kwenye kipindi nikaamua kuja tena chuoni kukusubiri, nikaona umetoka na Yule rafiki yako akiongea na wewe nilisema sitaondoka hadi nijue mwisho wake, sikutaka kukufata pale sababu nilihisi huwenda ukanishushua, najua ilichukua mud asana hadi wewe kuondoka, ulipokuwa unaondoka nilikuita ila hata nyuma hukugeuka ndio nikashangaa mbele umezingirwa na vijana, nikajua wale ndio walipanga kukufanyia vibaya wewe, nilijua peke yangu nisingeweza ila kwavile mimi huwa naelewana sana na mbwa sababu nishawafuga sana, nilisogea sehemu yenye mbwa na kumpa ishara kisha nikaja nae na kukuokoa wewe”
“Dah! Kwakweli Derick una upendo wa ajabu na una utu sana, nashukuru kwakweli nashukuru sana, maana bila wewe sijui ningekuwa wapi muda huu”
“Asante pia Erica, ila nakupenda sana Erica, tafadhali usinikatae”
“Ila nina mchumba tayari”
Derick akashtuka kidogo na kumuuliza,
“Yuko wapi huyo mchumba?”
“Yupo Marekani”
“Erica, ngoja nikwambie kitu. Unaweza sema naongea tu ila ndio ukweli ulivyo, mwanaume wa mbali utawasiliana nae ndio na atakwambia anakupenda ila hakuna mwanaume anayeweza mahusiano ya mbali hivyo. Lazima huko Marekani ana wanawake ila kwasababu wewe anakuhitaji pia lazima akwambie anakupenda”
“Mmmh!”
“Ndio ilivyo, ila hata hivyo huyo sio mume kwahiyo bado hawezi kunikosesha nafasi ya kuwa na wewe. Huwezi jua Erica, labda mimi ndio Mungu amekupangia niwe mume wako, huwezi jua ni kwanini Mungu amenituma nikufatilie hadi nikuokoe”
“Mmmh!”
“Usigune Erica, nakupenda. Mapenzi mazuri ni mtu umuone, akuonyeshe mapenzi ya dhati sio ya kuwasiliana, nakwambia huyo jamaa atakuliza bure, wanaume wa kweli tupo. Usihangaike kunijibu sasa ila nakupa muda ufikiria na uone jinsi gani Mungu anataka tuwe pamoja”
“Sawa, ngoja nifikirie basi”
“Ila usipange kunikataa Erica, nakupenda sana”
Kisha Erica akamuomba Derick arudi hosteli tu naye Derick alimsindikiza hadi hosteli na kumwambia,
“Erica ukiwa na kipindi cah jioni mpaka usiku uwe unaniambia tafadhali ili niwe nakuja kukusindikiza”
“Sawa”
Kisha akaagana nae na kuelekea kwenye chumba chake.
 
SEHEMU YA 113



Erica aliwaza sana, kwanza aliwaza kuhusu Dora kuwa msichana aliyemuamini kuwa ni rafiki yake siku zote ndio amekuwa adui yake namba moja hata baada ya kuacha urafiki naye, alishangaa kwakweli kuwa hata angepatwa na matatizo Yule rafiki yake angepata faida gani, alishangaa sana. Ila pia alifikiria kuhusu Derick kuwa atamkubali vipi wakati siku hizi mawasiliano yake na Rahim ni motomoto, ndio Rahim ni mpenzi wa kuwasiliana nae tu ila Derick amemsaidia sana na anadai kumpenda sana, je anamkataaje na je atakubali vipi kuwa na mahusiano na wanaume wawili yani alijiona yupo njiapanda kabisa.
Alikuwa na kipindi, akaenda kwenye kipindi ila alipotoka alienda kwa Tuamini maana ni siku nyingi kidogo hakuonana nae, alimkuta na wakaongea mengi sana ila kubwa zaidi lililomshtua ni pale Tumaini alipomwambia habari za Erick,
“Yani nimefurahi kuhusu mdogo wangu Erick”
“Kafanyaje tena?”
“Erick kaachana na Sia, ila sijamlaumu sabau Erick hajawahi kumpenda Sia”
Hii habari ilikuwa nzuri sana kwa upande wa Erica na kutaka kujua zaidi
“Kheee au kampata huyo msichana wake anayempenda?”
“Yule tahira, mama wa marehemu loh! Erick hawezi kumrudia Yule mama wa marehemu hata kwa dawa. Ila huwezi amini, Erick amesema amepata mwanamke kule Afrika kusini na wanapendana sana, amesema akirudi atarudi kumtambulisha kwetu. Amenitumia na picha zao, inaonyesha wanapendana sana yani Erick hataki hata kuongelea habari za mama marehemu, nimefurahi sana kwa mdogo wangu kupata faraja ya moyo”
Kisha Tumaini akafungua simu yake na kuanza kumuaonyesha Erica picha za Erick na huyo mwanamke, Erica alitabasamu tu ila kiukweli hizi habari zilichoma moyo wake, alijihisi wivu uliopitiliza, alihisi kama tumbo lake likiungurumisha, kiukweli alikosa raha kabisa. Muda ule ule aliamua kumuaga Tumaini na kuondoka.
Alirudi hosteli, akaenda chooni na kulia sana, kwani ingawa alikuwa anawasiliana na Rahim ila ukweli kwenye moyo wake ulibaki pale pale kuwa alimpenda sana Erick,
“Yani Erick nimekupigia simu hutaki kupokea, nimekutumia ujumbe hutaki kunijibu jamani Erick kumbe ushaamua kuanzisha maisha na mwanamke mwingine? Erick, nitakuwa na mahusiano mengi kila leo ila ukweli uko pale pale, nakupenda sana Erick, nakupenda sana”
Alikuwa akiongea mwenyewe chooni huku akilia sana kwani hakutegemea kabisa kupata habari kama zile kuwa Erick kashaamua kuwa na mwanamke mwingine na kapanga kumtambulisha akirudi kwao,
“Kumbe ndiomana Erick hutaki kwenu wanijue, yani hata dadako hukutaka ajue kama mimi ni mwanamke unipendaye. Hukunipenda Erick kweli hukunipenda kabisa, umeona huko wasichana wazuri umenisahau kabisa mimi”
Alikuwa akilia huku akiwaza sana, akajikuta kwa muda huo akimchukia hata Rahim,
“Hata Rahim nae ni kama Erick tu, sababu angekuwa muwazi kwa mama yake ila kanificha nisijulikane. Mwanaume pekee aliyenitambulisha kwa ndugu zake ni Bahati, ila simpendi jamani. Nakupenda Erick, kwanini umenifanyia hivi?”
Kila alipokumbuka zile picha alilia sana na kuzidi kukosa raha kabisa, alirudi chumbani na kujifunika shuka kama mtu aliyelala ila kiukweli bado alikuwa akilia, na hapo aliweza kujua ni jinsi gani alimpenda sana Erick na alimuhitaji katika maisha yake. Hakuwa na raha kabisa kiasi kwamba alikuwa na kipindi kingine jioni ila hakwenda maana alijikuta na mawazo kupita maelezo ya kawaida, alimuwaza Erick na alitoa machozi sababu ya Erick.
Erica alilia sana pale kitandani na kulala, hakutaka wale wa kwenye chumba chake wajue ndiomana alijifunika na shuka hadi usoni, na kwavile hakuwa na mahusiano nao ya karibu sana zaidi ya kulala nae kwenye chumba kimoja kwahiyo ilikuwa ngumu sana kwa wao kumuuliza kuwa vipi amelala vile kwa kujifunika na hajatoka kula. Usingizi ulimpitia pale pale.
 
SEHEMU YA 114


Asubuhi kulipokucha alikuwa anapigiwa sana simu na kuamua kuipokea, mpigaji alikuwa ni Derick,
“Mbona unaongea hivyo Erica, unaumwa?”
“Hapana”
“Naomba kuonana na wewe, twende basi tukanywe chai pamoja”
“Basi ngoja nijiandae”
Erica aliinuka pale kitandani na kwenda kuoga, kisha kutoka nje ili ampigie simu Derick, ila alishtuliwa na Yule msichana wa siku ile aliyekuwa anamwambia Erica kuwa ampe ujuzi ili na yeye apiganiwe na wanaume,
“Erica mambo”
“Safi”
“Mbona macho yamekuvimba hivyo?”
Mbele kidogo akatokea Derick kumfata Erica kwahiyo alimuita ili waondoke, ikabidi Erica amuage Yule binti,
“Badae Fetty”
Aliondoka na kumuacha Fetty akimuangalia tu.
Derick alienda kwenye mgahawa na Erica, wakaagiza chakula, akamuangalia Erica usoni naye alimuuliza kwa mshangao,
“Mbona macho yamekuvimba hivyo”
“Aaah sijui, kwani yamevimba sana?”
“Sio sana, ila inaonyesha umelia sana. Nini kilikuwa kinakuliza Erica, kuwa muwazi kwangu. Mimi ni muelewa sana”
Erica aliinama na machozi kidogo yalimtoka, na kumfanya Derick amsogelee na kumuuliza kwa upole kuwa kipi kinamliza,
“Sikiliza Erica, kukaa na kitu moyoni sio suluhisho kwani kitaendelea kuumiza milele. Wote wanaojiua sio kwamba wamependa ila hutokea sababu waliweka vitu moyoni na kushindwa wa kumshirikisha mtu mwishowe wakaona bora wajiue wakati kama wangeeleza matatizo yao wala isingepelekea kujiua. Usiupo moyo wako mateso ya kubeba mizigo ambayo haibebeki, unaposema unaupa moyo wako mwangaza na uhuru yani utajikuta moyo umeachia kabisa. Usipende kitu kikutese moyoni, niambie Erica una tatizo gani?”
“Sikia Derick, kuna mwanaume mmoja nampenda sana tena sana, yupo nje ya nchi ila nimesikia ana mwanamke mwingine”
“Pole Erica? Najua mapenzi yanavyoumiza, ila mimi si nilikwambia, hakuna mwanaume mwenye mapenzi ya dhati anapokuwa mbali. Mimi nikija kuoa, kama natakiwa kusafiri kikazi basi nitasafiri na mke wangu, siwezi kumuacha mke wangu na upweke. Usijali Erica, ndio mapenzi yalivyo. Utamsahau kabisa huyo mtu”
“Hujui tu jinsi gani nampenda, nampenda sana Erick”
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa Erick”
“Wow, ona sasa Mungu alivyo mwema huyo alikuwa anaitwa Erick, na mimi naitwa Derick yani jina langu na lake limetofautiana kwa herufi moja tu yani D. Ila Mungu ana makusudi yake kukuletea mimi, acha huyo aende sababu hakutakiwa kuwa na wewe ila mimi ndio mwenye sifa za kuwa na wewe Erica, yani mfute Erick kabisa katika maisha yako na sasa muwaze Derick tu. Nahitaji ufurahi, huwa unapenda kwenda wapi?”
“Napenda kwenda ufukweni”
“Basi tupange siku, twende tukapunge upepo. Erica, mtoe Erick kabisa katika akili yako, je kuna mwingine anayeisumbua akili yako zaidi ya Erick?”
“Hapana”
“Basi usijali, Derick nipo na nimeletwa kwako ili huyo mtu asikusumbue tena mawazo yako. Mimi ni mwanaume wa tofauti sana,najua kupenda, kujali na kumdekeza mwanamke yani kwangu utapata ambavyo huyo Erick hajawahi kukupatia. Elewa nakupenda sana Erica”
Maneno ya Derick yalikuwa yakimuingia kwenye akili yake vilivyo ingawa kiukweli hakudhania kama anaweza tokea mtu wa kumsahaulisha yeye kumpenda Erick, ukizingatia ni muda mrefu ameanza kumpenda toka wako shuleni na hajaweza kuacha kumpenda.
“Sasa naomba jioni, twende kwenye mgahawa moja tukale, ni mzuri sana yani utaupenda”
Erica alikubali kisha kuagana na Derick na kurudi hosteli, siku hii hakuwa na kipindi chuo kwahiyo alirudi tu hosteli na kukusanya nguo zake chafu na kwenda kufua.
Wakati anafua alienda Yule Fetty na kuanza kumuongelesha Erica huku akimwambia,
“Hongera sana, sijui una kismati gani wewe mdada, majuzi tu wamepigana wakaka kwaajili yako halafu leo nakuona unaondoka na Yule Derick”
“Kwani unamjua Yule”
“Namfahamu ndio”
“Unamfahamu vipi?”
“Namfahamu tu, ila anaonekana yupo romantic sana mmh hongera”
Erica alicheka tu maana hizi hongera alizokuwa anapewa wakati alikuwa akimuwaza Erick tu muda wote huo.
Alimaliza kufua na kuendelea kupiga stori tu na huyu Fetty, kwa siku hizo mbili hakuwa na habari kabisa ya kuingia kwenye mtandao wa kijamii wala hakutaka kujua kama Rahim alimtafuta au la, kwahiyo alikuwa tu akiongea na Yule Fetty pale na kufurahi ili kusogeza siku tu.
“Kumbe wewe Fetty ni mcheshi sana”
“Ndio, si wewe unajiweka peke yako pake yako ndiomana watu wanaogopa hata kukukaribia”
“Hapana bhana, marafiki walinitenda ndiomana sitaki hata kuwa na marafiki wa karibu”
“Ila unatakiwa kuwa na rafiki, kuna mambo yanakupata unaona umuhimu wa kuwa na marafiki sema cha msingi ni kuchagua marafiki wema kwako”
Wakati wanaongea ongea, Derick alifika eneo lile kwa lengo la kumfata Erica na kwenda nae alipomuahidi.
“Mmmh Derick, mbona mapema sana”
“Ndio vizuri mapema”
“Basi ngoja nikajiandae”
Erica aliinuka pale na kumuacha Derick akiwa na Fetty, na baada ya muda alikuwa tayari na kumuaga Fetty kisha akaondoka na Derick.
 
SEHEMU YA 115


Walikuwa wakitembea huku wakipiga stori za hapa na pale sababu Derick alisema sio mbali sana na maeneo yale, kwahiyo waliamua kutembea. Wakati wanaendelea kutembea, Erica alimuona mdada mmoja akija mbele yake, akamkumbuka vizuri huyo dada ni dada yake Bahati, Yule dada alivyofika alipo Erica alimnasa kofi, wakati Erica akigusa pale aliponaswa kofi, alishangaa kuona akinaswa kofi upande mwingine.
 
SEHEMU YA 64


Erica alimuangalia tu huyu Bahati ambaye aliendelea kuongea,
“Asante Erica, asante kwa kunitunzia”
“Sikuelewi”
Hunielewi Erica? Nakushukuru sana, yani siamini kuwa mimi ni mwanaume wa kwanza kwako, asante sana Erica kwa kunitunzia bikra yako”
Erica alimshangaa sana huyu Bahati.
Ila Bahati aliendelea tu kumsifia Erica kuwa ni msichana wa pekee sana, Erica aliamua kumuaga Bahati kuwa anarudi hosteli. Bahati aliinuka na kutaka kumsindikiza Erica,
“Kheee si ulisema unaumwa wewe?”
“Ndio nilikuwa naumwa ila nilikuwa naumwa mapenzi”
Erica alimuangalia Bahati kisha kuanza kuondoka na Bahati alikuwa akimsindikiza, na alimpeleka hadi hosteli.
Muda wote Bahati alikuwa akimsifia Erica kwa uzuri aliokuwa nao,
“Erica mpenzi wangu, wewe ni msichana mrembo sana najua kuna vijana wengi watakufata na kukudanganya kuwa wanakupenda huku wakikusifia kuwa wewe ni mzuri, wakikwambia kuwa wewe ni mzuri na mrembo waambie unajua utaweza kwa kiasi Fulani kuwakata makali yao. Wakikutaka kimapenzi waambie kuwa una mpenzi, Erica sikudanganyi wala sikutanii nakupenda sana”
Erica alikuwa anamsikiliza tu anavyoongea hadi alivyofika hosteli na kuagana nae.


Erica nae [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
SEHEMU YA 116


Wakati wanaendelea kutembea, Erica alimuona mdada mmoja akija mbele yake, akamkumbuka vizuri huyo dada ni dada yake Bahati, Yule dada alivyofika alipo Erica alimnasa kofi, wakati Erica akigusa pale aliponaswa kofi, alishangaa kuona akinaswa kofi upande mwingine.
Ilibidi Derick aende mbele kwa Erica ili kumzuia Yule dada asiendelee kumpiga kofi,
“Sogea wewe kijana”
Yule mdada aliongea kwa ukali sana,
“Kwani tatizo nini dada? Umefika tu na kumpiga, tatizo ni nini?”
“Wewe acha kumtetea huyo Malaya, anajua kila kitu”
Kisha Yule dada alimuangalia kwa jazba sana Erica na kusema,
“Binti mshenzi sana wewe, yani wa kumsababishia mdogo wangu matatizo halafu anaenda jela ila wewe hujali unakula raha tu na wanaume wengine, sogea na wewe nitakuchakaza sasa hivi”
Akamsukuma Derick pembeni na kuanza kumshambulia vizuri Erica ilibidi Derick atumie uanaume wake kumgombelezea Erica,
“Wewe kijana hujui tu, ila mwenzako akinyolewa zako tia maji, huyo binti ni shetani wa mashetani”
Kisha Yule dada akamuangalia Erica na kumwambia,
“Bado sijamalizana na wewe mwanaizaya, siku yako inakuja mwanaharamu wewe”
Yule dada akaondoka huku anasonya sana, kiukweli hata hamu ya kuendelea kula na Derick ilimuisha Erica kwanza alikuwa amechafuka maana Yule dada alimuangusha chini, kwahiyo akaomba kurudi hosteli tu, ikabidi wakodi bajaji iwarudishe hosteli maana ni aibu hata kutembea.

Walifika hosteli, na kwa aibu alishindwa hata kumuaga Derick kwani moja kwa moja alienda chumbani kwao, ila Fetty alimuona na kumfata Derick,
“Vipi tatizo nini?”
“Sijui, yani kuna mwanamke tumekutana nae njiani kaanza tu kumshambulia Erica hata sijui kwanini”
Fetty akacheka kidogo na kupiga makofi kama ya umbea kisha akasema,
“Mapenzi bhana ni kitu cha ajabu sana, yani leo unaweza sababisha wanaume wakapigana sababu yako ila kesho unapigana na mwanamke mwenzio sababu ya mwanaume. Mmh Derick, huyo mwanamke aliyemshambulia Erica humjui kweli? Ni mwanamke wako”
“Kwanza sikuelewi Fetty, unazungumzia nini?”
“Majuzi hapa palitokea gumzo kubwa sana, kulikuwa na vijana wawili wanapigana na chanzo kilikuwa ni Erica halafu leo eti Erica kapigana na mwanamke mwingine, mmmh chanzo ni wewe”
“Unajua bado sikuelewi Fetty, unamaanisha kuna wanaume wamepigana sababu ya Erica?”
“Ndio”
“Mbona Erica mchumba wake yupo nje. Hao waliopigana ni wakina nani?”
“Kalagabao, umeambiwa upo peke yako? Jua kuna wenzako msururu, yani mapenzi ya siku hizi ni ngoma droo, wewe una wanawake msururu na yeye ana wanaume msururu”
Derick hakutaka hata kuendelea kusikiliza haya maneno, aliamua kumuaga Fetty na kuondoka zake huku akitafakari kwa kina yale aliyoyasikia.
 
SEHEMU YA 117



Erica alienda kubadilisha nguo kisha akakaa na kujitafakari ila alipaona hosteli pagumu kwa muda ule, akajiuliza kuwa aende wapi, akaona bora arudi nyumbani kwao hata mama yake akimuuliza maswali amdanganye tu.
Kwahiyo akajitahidi na kuondoka pale hosteli akarudi nyumbani kwao, na kama kawaida mama yake alimuuliza kulikoni amerudi mapema yani sio mwisho wa wiki,
“Mmmh mama hivi hujisikiagi upweke kukaa nyumba yote hii mwenyewe?”
“Najisikia upweke ndio ila napenda usome”
Akaamua amuanzishie mada nyingine ili mama yake asiendelee kumuuliza kuwa kwanini amerudi nyumbani siku ya chuo.
“Mama, najiuliza sana kwa dada Mage kuna wajukuu zako ila kwanini hakuna siku uliyosema waje kukaa hapa nyumbani kama una upweke?”
“Wewe Erica, mada hizo umeanzia wapi?”
“Si nakuuliza tu mama, unajua Yule ni dada yetu tena ni mtoto wako wa kwanza. Kukaa mwenyewe humu ndani kama mkiwa si vizuri, ila angekuwepo hata mjukuu wako mmoja angekuchangamsha.”
“Tayari nimekuelewa”
“Kama umenielewa mama, chukua hatua basi umwambie dada alete watoto wake”
“Erica, tafadhali usinipande kichwani unajua ujinga alioufanyaga dada yako hapa? Wakati baba yenu yupo, Mage alituletea Yule mwanaume wake, tulimkataa kabusa maana hakua anafaa, Yule dadako mjinga kuona vile akaamua kubeba mimba na kujipeleka kukaa kwa mwanaume, ilibidi tumkubali hivyo hivyo ila baba yenu alimkataa kabisa hata mahali yake hakupokea. Sasa unadhani naanzaje kupokea watoto wake hapa nyumbani? Watoto nitakaopokea hapa ni watoto wa Bite tu na wewe ukiolewa ila siwezi kupokea watoto wa Mage”
“Sasa mama, makosa tayari yalishafanyika. Hata ukiwachukia watoto wa dada Mage bado haitasaidia kitu, kwasasa ungesema tu ni kitu gani wafanye ili uwasamehe. Mama dada Mage ni mwanao na hilo halipingiki, kumbuka watoto wake wana haki kwako kama bibi yao, ukiwatenga ni kuwatesa tu. Mama kwasasa ni kusema kitu gani wafanye uweze kuwasamehe”
“Sina kinyongo nao, ila nadhani labda waje upya kujitambulisha. Nitawapokea maana baba ndio hakuwataka kabisa ila hayupo tena, sema hata alipokuwa anakufa alisema kama wakifata taratibu niwapokee ila mpaka leo hawajajiongeza. Ni matahira wale”
“Jamani mama”
“Hata usiniambie habari zao”
Erica alifanikiwa kubadilisha mada kwa mama yake na kwenda chumbani kwake, ila pia alifanikiwa cha kumsaidia dada yake maana alimuona kwa hakika anatia huruma maana naye alionekana kutamani watoto wake wawe wanaenda kwa bibi yao hata likizo ila haikuwezekana sababu ya mambo ambayo alikuwa hajamalizana na mama yao.
 
SEHEMU YA 118


Erica alikaa akijitafakari jinsi yeye alivyo, akaanza kuhesabu idadi ya wanaume aliokuwa nao na kuangalia wapi alipokosea,
“Nilikuwa na Babuu ila huyu alinisaliti, alienda kwa wanawake zake akasingizia kuwa aliwekwa rumande kwa uzurulaji, nikampata George na kuamini kuwa nimempata mume wa maisha yangu ila akaniacha sababu sikuwa bikra, akaja Bahati yani huyu mwanaume sijawahi kumpenda ila nilimkubali sababu nilikuwa na mawazo sana ila ndio amekuwa msumari wa miba kwenye maisha yangu. Alikuja mwanaume niliyempenda kupita kiasi, sikuweza kumkataa sababu nilimpenda sana ila Bahati ndio kaniharibia kwa huyu Erick, kaenda kupigana nae na dada zangu nao wamechangia kwa kunitoa mimba ila ningekuwa nayo hadi leo kwa hakika kusingekuwa na mahusiano mazuri ya mimi na mama yangu sababu anasisitiza nisome siku zote. Haya sasa, Bahati imemkataa, George nae nimemkataa ila wamejifanya wamepigana kwasababu yangu mwisho wa siku wananipangia kunibaka mara dada yake Bahati anipige na kusema nitaona, kwani kosa langu nini jamani? Mbona wananifanyia hivi jamani mpaka najihisi vibaya”
Aliwaza sana yani kwa muda huo hakutaka kumtafuta yeyote Yule na hakutaka mawasiliano na yeyote, alipanga kwenye akili yake kuwa kesho yake aende kwa dada yake Mage bila ya kumwambia mama yake maana atamuaga kuwa anaenda chuo, kwa muda huo alichukua simu yake na kuizima kwani hakutaka kupatikana hewani kabisa.
Muda wa kulala ulipofika akalala, na kulipokucha aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kwa dada yake kama alivyopanga,
“Utakaa huko huko chuoni au utarudi nyumbani?”
“Nitarudi mama”
Aliondoka zake na safari yake kama alivyopanga alienda moja kwa moja kwa dada yake, kwa muda huo alimkuta dada yake pekee maana watoto wa dada yake walienda shule na shemeji yake alienda kwenye shughuli zake, alizungumza na dada yake vile alivyoongea na mama yao.
“U na uhakika mama atatukubali tukifata sharia tu?”
“Mama kasema, mkifata sharia atakubali yani nyie ni kujiongeza tu ila usimwambie kabisa kama mimi ndio nimekwambia”
“Asante mdogo wangu, sikuwahi kufikiria kama ungekuwa na busara kiasi hiki, anachojua Bite ni kuniletea mashtaka tu ila hajawahi kufikiria kuwa naweza kupatana tena na mama kiasi cha kuwakubali wanangu maana huwa nakuja kumsalimia tu, ila umenipa muangaza mdogo wangu kwani hata wanangu nina uhakika watapenda kuwa karibu na bibi yao”
“Usijali dada, tuko pamoja. Nakupenda dada yangu na pia napenda kushirikiana nawe. Ila leo naomba unijibu na mimi nawezaje kumjua mwanaume anayenipenda?”
“Ngoja nikwambie kwa ufupi tu ila ipo siku nitakufundisha kwa undani zaidi”
“Niambie dada hata hiyo kwa ufupi nitaridhika”
“Yani mdogo wangu ipo hivi, mtu anaweza akawa na pesa kupindukia ila asiwe na mapenzi ya dhati na mwingine akawa na pesa na mapenzi ya dhati akawa nayo, ila kuna mwingine ni masikini kabisa ila akawa na mapenzi ya dhati hadi ukaogopa, sasa kuna namna ya kumjua mtu mwenye mapenzi ya dhati”
“Namna ipi hiyo dada?”
“Mtu anayekupenda kwanza kabisa anakujali, anachukulia tatizo lako kama lake, anapenda kukuona ukiwa na furaha, na ukiwa na huzuni atatafuta namna ya kukufanya usijisikie vibaya. Hawezi kukuchukia sababu ya mapungufu yako, na atakusaidia kurekebisha tabia yako kama haiko sawa, mtu wa hivi ana mapenzi ya dhati kwako, hapendi kuona ukiumia”
“Mmmh dada sikuelewi”
“Hunielewi sababu kichwa chako kinafikiria vitu vingi sana, nina uhakika hapo unajiuliza kuwa uliyenaye ana mapenzi ya dhati kwako?”
“Umejuaje dada?”
“Nimejua tu, haya niambie uliyenaye ana sifa gani?”
“Mmmh kusema ukweli dada hata sijielewi, ila kuna kijana simpendi kabisa ila ananifatilia huyo hadi kero yani, hata anikute nimesimama na mwanaume mwingine ananifatilia, ila simpendi”
“Ila hilo ni tatizo, ingekuwa unataka kuolewa ningekwambia utajifunza kumpenda ndani ya nyumba, ila nadhani ni vyema ukimleta nimfahamu huyo kijana, nitakwambia kama anakufaa”
Erica alimuahidi dada yake kuwa atampeleka huyo kijana, kisha muda huo akajiandaa kwenda tena chuoni ila alitaka akaangalie tu mambo yameendaje maana hata kwa siku hiyo hakuwa na kipindi kabisa.
 
SEHEMU YA 119


Wakati anaingia chuo, aliitwa na kugeuka alimuona Derick, ambaye alimsimamisha na kumuuliza,
“Na mbona jana hukupatikana hewani?”
“Simu yangu ilizima chaji”
“Ila nilikuja hosteli hukuwepo”
“Nilienda nyumbani”
“Erica, mbona umekuwa na majibu ya mkato hivyo kwani nimekufanya nini?”
“Hujanifanya chochote”
“Erica, ningekuwa na hasira nawe kwa hakika nisingekutafuta tena, kwanza ulinidanganya kuwa ni mwanaume mmoja tu uliyekuwa naye kumbe kuna wengine walipigana hosteli. Ila Erica mimi sitaki kupigana na yeyote Yule, yani sitaki niwe na ugomvi na yeyote Yule. Kila kitu kifute katika maisha yako na tuanze kurasa mpya ya mapenzi, nakupenda Erica, na napenda tuwe pamoja mpaka mwisho. Sitakuchukia kwa lolote lile maana kwangu ni kama changamoto tu, na kwavile nakupenda basi nataka niwe nawe milele”
Erica alikuwa kimya tu akisikiliza maneno ya huyu Derick ambaye alikuwa akimchombeza vilivyo,
“Erica haijalishi ni wanaume wangapi wamepita kwako na haijalishi wamefanya nini kwako ila bado swala litabaki palepale kuwa nakupenda sana”
“Nimekuelewa Derick, naomba tuongee badae kwasasa kuna mambo nayaweka sawa”
Wakaagana na Derick huku akimuahidi kumfata badae hosteli, wakati akiwa pale chuoni akakutana na Tumaini tena na kusalimiana nae,
“Jamani Erica uliondoka gafla juzi hadi sikukuelewa kabisa, ila unaendeleaje mdogo wangu”
Kabla hajamjibu, simu ya Tumaini ikaanza kuita na Tumaini akamwambia Erica asubiri kidogo aongee na ile simu kwahiyo Erica alikaa pembeni akisubiri Tumaini amalize kuongea na ile simu.
Tumaini alipomaliza kuongea na ile simu alionekana kuwa na furaha sana kiasi kwamba Erica ilibidi amuulize kuwa kitu gani kimemfurahisha,
“Yani Erick kanipigia simu, na kanipa huyo msichana wake niongee nae jamani ana sauti nzuri huyo dada balaa, anaitwa Jack. Oooh natamani nimuone huyo wifi yangu, nimefurahi sana”
“Kwahiyo ndio yupo nae muda huu?”
“Ndio, anasema Yule dada kamwambia mpigie wifi yangu simu ndio kanipigia, jamani nimefurahi sana yani mdada yupo vizuri Yule duh sauti yake tamu hiyo, kwakweli mdogo wangu kabahatika jamani”
Tumaini hakujua kuwa kadri alivyokuwa akisifia kuhusu Yule msichana wa Erick ndivyo alivyozidi kuumiza moyo wa Erica maana muda huo huo Erica aliamua kumuaga kuwa anawahi kipindi ila haukuwa ukweli, kwani alipoondoka pale alijifanya kama anaenda kwenye kipindi ila mbele yake alikatisha na kuanza safari ya kutoka chuo kwani moyo wake ulikuwa na maumivu sana kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 120


Wakati anatoka pale chuo alishikwa bega, na aliyemshika alikuwa ni Derick alijikuta akimkumbatia kwa kilio, na kumfanya Derick atambue kuwa lazima atakuwa ana matatizo na kumfanya ampe ushauri,
“Twende mahali Erica”
Derick alikodi bajaji na kuondoka eneo lile na Erica.
Moja kwa moja alienda na Erica ufukeni na kuanza kuongea nae maneno ya kumpa faraja,
“Najua una matatizo Erica, name nimejitolea kubeba matatizo yako kama yangu. Niambie sasa kinachokusibu ni nini au bado ni kuhusu Erick?”
Erica alitikisa kichwa huku akiendelea kulia, Derick alijitahidi kumpa maneno ya faraja sana mpaka giza liliwakutia palepale,
“Erica, naomba usirudi hosteli kulala ila twende mahali tukacheze, tufurahi usahau kila kitu”
“Wapi huko?”
“Twende club”
“Hapana, sijawahi kwenda club maisha yangu yote. Kwanza kucheza sijui”
“Sio wote wanaoenda disko wanajua kucheza ila hata ile midundo na mziki ukiusikiliza unakuliwaza, twende club Erica tafadhali, hautacheza, tutakaa tu mahali tukitazama watu”
“Basi, ngoja nirudi hosteli nikabadilishe nguo ila hata mavazi ya club sina”
“Hata usiumize kichwa, vaa tu suruali na tisheti basi”
Kisha akaondoka nae hadi hosteli kujiandaa, ambapo Erica alioga na kuvaa alivyoshauriwa kisha kutoka na kuondoka na Derick, ambapo alienda nae kwanza sehemu ya kula ili kupoteza poteza muda.
“Mpaka saa hizi?”
“Ndio, club pananoga muda ukienda enda.Twende sasa”
Walienda disko, kwakwelki ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Erica kujishuhudia watu wakiwa disko na kucheza maana siku zote alisikia tu kwenye stori ila siku hiyo alijionea mwenyewe, walifika mahali na kukaa kisha Derick akaagiza vinywaji, Erica akadakia
“Mimi nataka soda”
“Erica my dear, humu hakuna soda”
“Basi mimi sinywi, situmii pombe kabisa”
“Kwanini hutumii pombe?”
“Sababu ni chungu”
“Aaah sasa kuna kinywaji kimoja hivi kinaitwa Reds kipo humu yani hata sio kichungu na wala hakina mandhari ya pombe, ngoja nikuagizie ukijaribu”
Basi Derick akamuagizia Erica kile kinywaji na kweli Erica alikunywa na kkukipenda, akajikuta anakunywa tu huku akifurahia mziki unavyopigwa na watu wanavyocheza, ilikuwa kikiisha tu Derick anaita kingine kwahiyo Erica alikunywa sana na akaanza kujihisi kizunguzungu huku mara nyingine akilia peke yake, mara amkumbatie Derick na kumwambia anampenda yani pombe ilianza kufanya kazi kwenye akili yake.
Derick aliamua kutafuta chumba maeneo yale ya karibu ili akapumzike na Erica.
 
SEHEMU YA 121


Kulipokucha, Erica alijikuta yupo kifuani mwa Derick akiwa hana nguo kwamaana kwamba alifanya mapenzi na Derick, kiukweli alichukia sana na kumshtua Derick,
“Ndio umefanya nini na mimi sasa?”
“Usinilaumu Erica, tulikuwa tumekunywa wote, ni pombe ndio zimepelekea tukafanya hivi”
“Ulijua fika ndiomana ukanishawishi mimi ninywe zile pombe”
“Ila usijali Erica, huu ni mwanzo mzuri wa mahusiano yetu”
“Kwenda zako huko”
Erica aliinuka na kuanza kuvaa nguo zake,
“Tukaoge basi mpenzi”
“Achana na mimi, nitaenda kuoga hosteli”
Ila akajifikiria akaona ni vyema akaoge kuliko kutembea na mijasho ya mtu mwingine, alienda na nguo zake chooni na kuoga kisha akavalia huko huko. Alipotoka alimkuta Derick ameshavaa,
“Mbona wewe hujaenda kuoga?”
“Nataka niwe nanusa jasho lako mwilini mwangu muda wote”
Erica akamsonya Derick kisha kutoka kwenye kile chumba, Derick alitoka na kufatana na Erica kwa nyuma hadi kwenye kituo cha daladala ndipo alipogundua yale maeneo ni karibu na kwa dada yake Mage, uoga ulimshika wa kukutana na dada yake, ila jambo la bila kutarajia dada yake alitokea mbele yao,
“Kheee Erica, unakuja kwangu kwa kunishtukiza hivi, umeniletea na mgeni jamani! Kwanini hukuniambia?”
Kisha akamuangalia Derick na kumwambia,
“Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana nyumbani”
Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli hakuelewa.
 
Back
Top Bottom