Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 237

Aliporudi kwenye kazi zake akakumbuka kuwaandalia ratiba wale wakina Dora kuhusu kuja kuzungumzia bidhaa zao, kwahiyo aliangalia namba zao na kupiga kuwa kashawaandalia barua ya ratiba waende kuchukua.
Baada kama ya lisaa limoja, Dora alikuwa mahali pale kuchukua barua kutoka kwa Erica alisalimiana nae vizuri sana kisha Erica akampa ile barua ila kiukweli Erica hakutaka ukaribu wa haswaa na Dora ila kwa Dora ilikuwa tofauti maana alionyesha kutaka ukaribu zaidi na Erica.
“Erica hongera sana rafiki yangu, umepata kazi sehemu nzuri sana, nani alikuunganishia?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Na mimi Erica, kama kuna aliyekuunganishia na mimi nahitaji”
“Hakuna aliyeniunganishia, mimi nilituma maombi ya kazi tu na kupata”
“Basi na mimi nilete maombi yangu ya kazi, na ukisikia kama kuna nafasi ya kazi uniambie Erica, tafadhali maisha ni kusaidiana”
“Leo ndio unalijua hilo?”
“Erica, ulisema tusahau yote yaliyopita na tuanze mapya”
“Haya yameisha”
“Nashukuru Erica, kwaheri eeh!”
Dora akaaga na kuondoka, Erica alikuwa akiongea na Dora ilimradi tu maana alishamwambia kuwa amemsamehe kwahiyo hakuona kama ni swala zuri kutokuongea vizuri na Dora.
Alipomaliza kazi zake kama kawaida, alienda kumuaga shemeji yake na kukumbushwa swala la kesho yake kutafuta sehemu atakayo somea udereva.
Kwahiyo Erica aliondoka na kwenda kupanda daladala ili kuelekea nyumbani kwao, alipokuwa kwenye daladala ile wakati akiwa na uchovu uchovu sababu ya kukaa kwenye kompyuta kwa muda mwingi, alijikuta tu akisinzia kwenye kiti cha daladala , mara akashtuliwa na mkaka mmoja aliyekuwa pembeni yake,
“Pole sana dada, inaonyesha umechoka sana”
“Asante”
“Samahani dada yangu unaitwa nani?”
“Naitwa Erica”
“Basi mimi naitwa Juma, nimefurahi kukufahamu. Napenda tuwe marafiki, naomba namba zako”
“Umesema unaitwa nani?”
“Naitwa Juma”
“Namba zangu za nini?”
“Nahitaji tuwe tunawasiliana Erica”
“Unikome tena unikome kabisa, sipendi mazoea ya kijinga. Nikome, sihitaji kuzoeana na wewe”
Huyu kaka alimshangaa sana Erica kuwa ana tatizo gani maana kamjibu kwa hasira utafikiri kuna jambo baya amemwambia, hadi mkaka wa watu akajihisi vibaya kuwa pale hajamtongoza je akimtongoza itakuwaje? Alibaki akimshangaa kisha akamwambia,
“Kwani dada tatizo ni nini? Kufahamiana na mtu ni tatizo? Kama hutaki kunipa namba yako si ungesema tu sitaki kuliko kuanza na mada za unikome sijui nini na nini jamani?”
“Tena usinizoee wala usiendelee kuniongelesha, kwenye daladala yote hujaona wadada wa kuwasemesha zaidi yangu? Sitaki mazoea”
Huyu kaka alimshangaa sana Erica ila ilibidi awe mpole tu na kumwambia kwa upole,
“Binadamu hatwendi hivyo Erica, unaweza ukaanguka nikakuinua au mimi nikaanguka ukaniinua. Binadamu hatujibishani vibaya”
“Sikia wewe, sijui Juma sikia nikwambie yani mimi hata ukiniona nakufa hapo niache nife ila mazoea na wewe sitaki”
“Kwanini umekuwa mkali hivyo dada?”
“Nyie wanaume ni watiu wabaya sana, yani hapo utakuwa unajiongelesha sijui namba yako namba yako ila lengo lako ni kunitongoza. Nishakwambia naitwa Erica, na wewe Juma umeona kabisa itikadi zetu hazifanani ila unakazana kutaka namba yangu. Unanitakia nini mimi? Sitaki yani sitaki kabisa, mwisho wa siku ndio uniambie badili dini nikuoe, nikisema nipo tayari ulete propaganda zingine, sitaki na usiniongeleshe tena”
Kituo kilichofuata Erica alishuka sio kwamba alifika ila hakutaka kuendelea kuongea na huyu Juma ndiomana alishuka kituo ambacho sio chake.
Kisha alipanda daladala nyingine na kwenda hadi kituo chake akashuka na kuelekea nyumbani.
 
SEHEMU YA 238


Alifika nyumbani, ila alipokaa na kutafakari kuhusu alichomjibu Yule mkaka wa kwenye daladala aliona yupo sawa kabisa,
“Yani wanaume wana mazoea ya kijinga kabisa, sitaki mazoea na mtu yeyote yule”
Mama yake alimsikia na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, alimueleza mama yake kuhusu mkaka aliyemuongelesha kwenye daladala na jinsi alivyomjibu, alijua mama yake angempongeza maana mama yake alikuwa akitaka mwanae asiwe karibu na wanaume, ila mama yake hakumpongeza kabisa kwa kitendo kile,
“Erica mwanangu, sivyo nilivyokufundisha hivyo. Jifunze kuwa na kauli nzuri kwa watu”
“Sasa mama alitaka namba yangu ya nini kama sio kunitongoza, anajijua kabisa yeye ni Mwislamu na mie ni Mkristo sasa alitaka namba yangu ya nini?”
“Dini sio tatizo, ila tatizo ni utu na ustaarabu. Mtu unamjibu vibaya, hivi leo na kesho ukakutana nae mahali halafu ndio wa kukusaidia unadhani atakusaidia?Huwezi jua mtu huyo utakutana nae wapi tena”
“Hahaha, hujamuona mtu mwenyewe mama. Kwa msaada gani alionao Yule mtu? Hakuna lolote, hawezi kunisaidia chochote. Na siwezi kuhitaji msaada wake”
“Usimdharau usiyemjua Erica”
“Hujamuona mtu mwenyewe mama, anachekesha balaa”
“Watu hatuendi hivyo Erica, huwezi kumuhukumu mtu kwa kosa la mtu mwingine, si mkaka wa watu alikutuma uzae na huyo mwarabu wako. Usipeleke hasira zako kwa watu wasikuwa na hatia, jifunze kauli mwanangu, hatakama mtu humtaki hutakiwi kuongea nae kwa ukali. Mwambie kwa ustaarabu, nina mume wangu siwezi kutoa namba yangu, basi ukiona huwezi kumpa namba yako na sio kumjibu vibaya”
“Sawa mama nimekuelewa”
Alimuitikia mama yake na kuinuka kwenda chumbani ila kuikweli yale maneno ya mama yake hayakumuingia akilini hata kidogo maana yeye aliwaza kuwa njia pekee ya kuwakwepa wanaume ni kuwajibu vibaya, kila alipofikiria mapito yake aliona ni vyema kuwajibu vibaya.

Kesho yake Erica alijiandaa kwaajili ya kwenda kumtafutia mwanae nguo maana hakuona umuhimu wa kutafuta chuo cha udereva sababu tayari alijua kuendesha kwahiyo zile hela aliona ni vyema akamnunulie mwanae nguo, kwahiyo akajiandaa na kuondoka zake hata mama yake hakumwambia kama siku hiyo haendi kazini maana alijua kuwa mama yake angekuwa na maswali mengi sana.
Alifika kwenye duka la nguo za watoto na kununua nguo baadhi kwaajili ya mtoto wake, ila hakutaka kwenda kwenye lile duka la Moses maana hakuwa tayari kumjibu maswali yoyote Tumaini.
Wakati anatoka kwenye lile duka, alishikwa bega kugeuka alimuona Fetty. Alikumbatiana nae kwa furaha maana ni siku nyingi hakuonana nae, toka siku ya mimba.
“Jamani Fetty, toka siku ile ukapotea! Ulikuwa wapi?”
“Nisamehe Erica, kwanza umejifungua mtoto gani?”
“Mtoto wa kike”
“Hongera sana, anaitwa nani?”
“Anaitwa Angel, na wewe ulikuwa wapi kipindi chote hiko hata kuja kuniona jamani!
“Erica, acha tu maisha haya ni kizunguzungu haswaaa. Yani mwenzio nilipatwa na majanga balaa, mapenzi haya yani acha tu”
“Yamekufanyaje tena?”
“Ni historia ndefu ndugu yangu”
“Niambie hata kwa kifupi”
“Nilipata mwanaume wa kuishi nae, nikasafiri nae na kwenda Iringa. Ila yani alichonitenda Yule bwana sitakuja kusahau kamwe, hebu fikiria nimezaa nae mtoto mmoja, eti gafla kasema ndugu zake hawako tayari aoane na mimi kisa yeye Mkristo na mimi ni Mwislamu unajua kanitimua kwake nikiwa sijielewi hata pa kwenda! Nashukuru Mungu nilikuwa nafanya kazi ndio kitu kilichonisaidia, na nimeomba uhamisho na kurudi hapa Dar. Sina hamu na wanaume”
“Mmmh pole sana, sasa wanaume gani wazuri? Wakristo au Waislamu?”
“Wote wabaya ndugu yangu yani mwanaume huwa anokoteza tu sababu na mimi nina mkosi kwakweli natongozwa na Wakristo tu, nawachukia balaa”
“Hata mimi nina mkosi sio peke yako, natongozwa na Waislamu tu”
“Mmmh hadi baba Angel sio Mkristo mwenzio?”
“Sio mwenzangu, nina mkosi tu”
“Ila tusijiombee mikosi, sidhani kama dini ni tatizo ila tunaokutana nao ndio tatizo ndugu yangu. Nitakuja kwenu tuongee vizuri”
Erica akafurahiana pale na Fetty kisha kuagana nae na kurudi nyumbani kwao.
Alirudi na zile nguo alizomnunulia mwanae, mama yake akamuona na kuuliza,
“Erica, hata mwisho wa mwezi haujafika, hizo hela za kumnunulia mtoto nguo nzuri hivi umetoa wapi?”
“Jamani mama, kwani mimi sina hela?”
“Kumbuka, ulikuwa ukilalamika umeishiwa hadi huruma. Haya nguo hizi umezitoa wapi?”
“Mama, kuna siku nilipata daladala na walimpenda sana Angel, wamesema wanahitaji Angel awe balozi wa nguo za watoto ndio leo wamenipigia simu nikachukue nguo hizi”
Mama yake akafurahi sana na kuona mtoto wake ana bahati,
“Unaona sasa, mara nyingine ni vizuri kupanda kwenye usafiri wa jumuiya maana unaonekana”
Erica akacheka tu maana tayari alishamdanganya mama yake.
 
SEHEMU YA 239

Kulipokucha alijiandaa kwenda kazini, na kwenda kama kawaida kisha akaanza kufanya kazi zake, muda kidogo James alitoka ofisini kwake na kwenda kumsalimia Erica,
“Vipi ulipata chuo?”
“Nilipata ndio”
“Basi vizuri, nishaongea na jamaa wa TRA nadhani atafika muda sio mrefu na atakusaidia kuhusu swala la kupata leseni”
“Haya, asante”
James alitoka nje huku Erica akiendelea na kazi zake, muda kidogo Erica alipigiwa simu na James kuwa atoke nje akatambulishwe huyo jamaa wa TRA ambaye ndio atamsaidia.
Erica aliacha shughuli zake na kutoka nje, kufika alipo James ndio akashtuka kuona jamaa mwenyewe ni Yule Juma aliyekutana nae kwenye daladala juzi na akamjibu vibaya.


James alitoka nje huku Erica akiendelea na kazi zake, muda kidogo Erica alipigiwa simu na James kuwa atoke nje akatambulishwe huyo jamaa wa TRA ambaye ndio atamsaidia.
Erica aliacha shughuli zake na kutoka nje, kufika alipo James ndio akashtuka kuona jamaa mwenyewe ni Yule Juma aliyekutana nae kwenye daladala juzi na akamjibu vibaya.
James alimuona Erica alivyosimama na kusita, kwahiyo akamuita,
“Erica, vipi mbona umeganda gafla?”
Erica akasogea ila alikuwa na hofu kupindukia, kisha James akaanza kutambulisha,
“Erica, huyu ni jamaa yangu wa TRA ambaye niliyesema nitaongea nae maswala ya leseni anaitwa Juma. Ndugu yangu Juma, huyu anaitwa Erica, ni mfanyakazi wangu nan i shemeji yangu ndiomana nahitaji umfanyie swala la leseni haraka haraka”
Juma alinyoosha mkono kama ishara ya kusalimiana na kufahamiana na Erica, Erica nae alinyoosha mkono pia na kumpatia ila aligubikwa na aibu ya hali ya juu kwani hakufikiria kama Yule Juma ndiye mtu wa kumsaidia, akakumbuka hadi maneno ya mama yake kuwa huwezi jua utakutana wapi na mtu huyo na atakusaidia nini, alibaki tu kumuangalia Juma kwa aibu na kushindwa hata kusema nae chochote, basi James akamwambia,
“Nenda pale ofisini kwako, kakae na Juma akuelekeze vitu vinavyotakiwa, mimi natoka kidogo. (Kisha akamuangalia Juma na kumwambia) Kwa swala lolote la hela, njoo kwangu.”
Kisha James akaondoka zke na kumuacha Erica akiongozana na yule Juma hadi ofisini.
Kwakweli Erica alikuwa akisikiliza tu kile Juma alichomwambia na alichoagizwa na Juma ndio alichokifanya kwa wakati huo, kisha Juma alivyomaliza alimwambia Erica aandike namba yake na aliandika bila pingamizi na kumuga huku akimwambia,
“Naomba tusahau yote yaliyopita, nisamehe”
“Usijali”
Juma akaondoka zake, kwakweli hii haikuwa siku ya furaha kwa Erica maana alihisi kudhalilika vibaya mno.
 
SEHEMU YA 240

Kwenye mida ya saa kumi jioni, James alimuita Erica na kumpa ruhusa ya kuondoka,
“Yani hata hukumbuki kuwa unatakiwa kwenda chuo?”
“Nilisahau”
“Hebu acha mawazo Erica, fikiria maendeleo yako tu kwasasa, acha mawazo ya kijinga hayo mdogo wangu”
Muda huu Erica alijisikia vizuri sana kuitwa mdogo wangu na James, basi akamuaga pale na kuondoka zake.
Alienda kupanda daladala, ila leo kuna wakaka walikaa pembeni yake na akasikia maongezi yao,
“Yani mademu hawa vimeo vimeo, kuna demu nimekutana nae, ukimuona ni staarabu kumbe ni mbwa tu”
“Yule wa siku ile? Nilikwambia lakini jomba hukunisikia, uliona kama nakuonea wivu ndugu yangu, Yule demu jau yani kimeo cha mwisho”
“Najuta hata kutokufuata ushauri wako, ila mimi nikija kupata demu mwenye upendo wa dhati hakika nitatulia”
“Upendo wa mademu upo kwenye hela, yani ukiwa na pesa utapendwa wewe balaa ila uwe kapuku sasa utajuta yani mademu kwa pesa huwawezi ndiomana mimi sina demu wa kudumu huwa natembea nao na kuwaacha”
Erica aliwasikiliza mpaka alipofika kwenye kituo chake na kushuka ila kwa maongezi yale aliyoyasikia aliona kuwa wanaume wanapenda kuchezea wanawake wakati hata wao walikuwa wanalalamika kuwa wanawake wana matatizo.
Alifika nyumbani kwao na kumsimulia mama yake kuwa Yule mtu alifika ofisini kwao, ila hakumwambia kilichomnfikisha pale Yule mtu,
“Kumbe ni rafiki wa shemeji bhana Yule mkaka”
“Kheee mwanangu ila nilikwambia, kuwa makini na majibu sio kila kitu ni kujibu vibaya”
“Ila mama kama mtu anakutongoza na humtaki?”
“Si nishakwambia, mjibu kiustaarabu kwani ukisema hapana sitaki kuna tatizo gani? Sio unaanza ooh wewe sijui dini nyingine, kimeenda kimerudi sasa ndio nini hapo? Unatakiwa kuwa na jibu moja linaloeleweka”
“Sawa mama nimekuelewa na sitorudia tena mama yangu”
“Ndio usirudie, unanidhalilisha mimi ukifanya ujinga”
Erica aliinuka na kwenda chumbani haraka haraka maana alijua pengine mama yake angemuuliza kuwa mbona kawahi kurudi.
Alikaa chumbani ila wazo la Erick lilimjia kichwani na wakati akimfikiria Erick alipigiwa simu muda huo huo na Erick, kwakweli Erica akatabasamu na kuona ni jinsi gani upendo kati yake na Erick ulivyo mkubwa kiasi kwamba hata Erick anamuwaza vile vile na yeye anavyomuwaza, Erica akapokea ile simu
“Mbona kimya mpenzi wangu hukunitafuta tena?”
“Siku hizi nimeanza kazi Erick, kwahiyo narudi nyumbani nikiwa nimechoka balaa ila nakukumbuka sana tu, yani hata muda huu nimetoka kukukumbuka”
“Vipi facebook siku hizi hutumii?”
“Natumia”
“Mbona huwa sikuoni?”
Erica akakumbuka kuwa alifuta urafiki na erick maana hakutaka kumkwaza Rahim, alimwambia Erick,
“Labda nilitoa urafiki kwa bahati mbaya, ngoja nikuombe tena urafiki ili tuwe tunawasiliana”
“Sawa”
Erica alikata simu na kwa mara hii akachukua ile simu yake na kuingia kwenye mtandao ingawa kwa siku hizo hakupenda kuingia kwani kila alipomuona Rahim alihisi kuumia sana, na leo alikuta Rahim yupo hewani vizuri kabisa ila hakutumiwa ujumbe wowote na Rahim, akamtumia Erick ombi la urafiki na Erick alilikubali muda ule ule na kuanza kuwasiliana nae kwenye mtandao sasa,
“Ila Erick, muda sio mrefu nitalala, maana nimechoka”
“Sawa Erica, ila nakumiss sana na ninatamani siku moja tuishi wote. Subiri tu nirudi kutoka Kusini, ila usinisaliti Erica”
Kidogo Erica alisita kujibu maana kama usaliti kashaufanya sana tu mpaka na mtoto kapata, ila akamjibu kuwa asijali hatomsaliti, bado hakuweza kumwambia Erick kuhusu mtoto aliyekuwa nae maana alihisi kama upendo juu yake utapungua.
Akamuaga Erick kuwa muda huo analala, ila kabla hajatoka hewani alishangaa ujumbe kuingia kutoka kwa Rahim, akaufungua na kuusoma,
“Kweli mwenye asili haachi asili, kwahiyo umemtafuta Erick hadi kuanza tena urafiki nae? Nashukuru Erica, hela zote nilizokuwa nakupa ni kazi bure”
Erica alisoma mara mbili mbili ujumbe wa Rahim bila hata kuelewa kuwa Rahim amejuaje kuwa yeye na Erick wameanza urafiki tena, ila akakumbuka kuwa facebook ina mtindo wa kuandika Fulani na Fulani wamekuwa marafiki, kwahiyo inamaana labda Rahim kaona ujumbe huo ndio kajua kuwa Erica na Erick wamekuwa marafiki tena. Erica hakujua ajibu nini kwahiyo alipotezea huo ujumbe na kulala tu.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 241


Kulipokucha akajiandaa na kwenda ofisini kama kawaida, leo akiwa ofisini akapigiwa simu na Yule Moses mwenye duka la vitu vya watoto na nguo.
“Erica, mbona unaniangusha jamani, hujaipenda ofa yangu? Mpe mtoto nafasi hiyo huwezi jua atakuwa nani ukubwani? Naomba ukubali Erica, mwanao awe balozi wa bidhaa zetu, inamaana bado hujafanya maamuzi?”
Erica akawaza kwa muda kuwa ajibuje kwani kiukweli alikuwa akihitaji sana tu ila sharti alilopewa na Tumaini ndio lilikuwa gumu sana kwake, ila Yule Moses alimuuliza tena,
“Mbona kimya Erica?”
“Nimekubali”
“Wow, lini sasa utakuja kusaini mkataba wetu kisha mwanao aanze kuonekana kwenye matangazo yetu?”
Erica alitamani kuulizia kuwa Tumaini ni nani kwenye lile duka ila hakuweza kuulizia na akawaahidi kwenda kesho yake na mtoto, aliona ni rahisi kwake sababu ni siku yake ya kwenda kliniki.
Alikubaliana nae hivyo na Moses alionyesha kufurahishwa sana na swala hilo.
Kisha Erica alipomaliza kazi zake, kama kawaida akaenda kumuomba ruhusa bosi wake na kumwambia kuwa kesho atampeleka mtoto kliniki kwahiyo hatoweza kufika kazini,
“Hakuna tatizo Erica, yani wewe ukiwa na swala lolote lile usisite kuniambia, sawa eeh!”
“Sawa”
Kisha Erica akataka kuondoka ila James alimzuia kidogo na kumpa laki moja ambayo Erica alikuwa akiikataa,
“Hapana Erica, pokea pesa hii itakusaidia kesho kumpeleka mtoto kliniki. Naelewa shida unayopitia Erica, inaniumiza sana kuona kuna mwanaume mwenye miguu miwili kama mimi na mwenye ufahamu kama mimi ila kaumiza moyo wako, inaniuma sana. Naomba pokea hii pesa, si kwaajili yako ila ni kwaajili ya Angel”
Erica alipokea ile hela na kumshukuru pale kisha kuondoka zake na kurudi nyumbani kwao.
Leo mama yake alimuuliza kuwa mbona karudi mapema,
“Kesho nampeleka Angel kliniki kwahiyo nimeomba ruhusa mapema kwaajili ya maandalizi”
“Kheee makubwa, kuna maandalizi ya kumpeleka mtoto kliniki!”
“Si kama kutafuta kadi lake mama”
“Haya nimekubali ila kishingo upande”
“Sasa mama unafikiria ni nini?”
“Hakuna kitu”
Leo Erica alifanya mambo yake mengine yote ila hakuingia kwenye mtandao kabisa, hadi saa ya kulala alimchukua tu mwanae na kumlaza pembeni yake.
 
SEHEMU YA 242

Kesho yake alijiandaa na kutoka na mwanae, sababu hela alikuwa nayo hakuona tatizo la kukodi gari la kumpeleka kliniki, wakati anatoka kliniki na siku hiyo akagongana tena na Salma ila leo Salma alimpa Erica msonyo huo uliomuacha mdomo wazi kisha akasema,
“Najua umezaa na Rahim, hata ufiche vipi mi naujua ukweli. Ila ngoja nikwambie kitu, kuzaa na Rahim hakutakusaidia chochote maana umezaa mtoto wa kike, kama watoto wakike Rahim anao wa kutosha tu, sio peke yako uliyezaa na Rahim mtoto wa kike. Ila humu kwenye tumbo langu kuna kidume, mrithi wa Rahim”
Erica alimuangalia Salma ila akaona kujibishana nae ni kuweka mzozo tu, kwahiyo akaachana nae na kuondoka zake. Kiukweli roho ilimuuma ila akaona hana sababu ya kuumia kwaajili ya Rahim maana alishaamua kusonga mbele, kwahiyo alitoka pale kliniki na kuelekea stendi kisha kupanda daladala na kwenda kwenye duka la Moses.
Alifika pale na kuonana na Moses kwakweli Moses alifurahi sana, na kumpa ule mkataba ausome kisha asaini maana hakutaka kuchelewesha tena, wakati Erica anasoma ule mkataba na wao walikuwa wakimjaribisha mtoto wa Erica nguo huku wakimpiga picha, Moses alimpenda sana mtoto Yule maana hakuwa mlizi kama watoto wengine na alikuwa na tabasamu muda mwingi, yani walimpiga picha pale na kurudi kwa Erica,
“Kweli huyu ni Angel jamani, mtoto anatabasamu hadi raha. Una mtoto mzuri sana Erica, hongera tena na tena”
Erica alimjibu asante na kumkabidhi mkataba pale maana tayari alishasaini.
“Nimefurahi sana umekubali kusaini mkataba na sisi, huyu mtoto wako atakuwa balozi wetu mzuri sana. Hakuna nguo anayovaa ikamchukiza, angalia hizi picha tulizompiga”
Moses akaanza kumuonyesha Erica zile picha alizopigwa mwanae, kwakweli alipendeza sana hata yeye aliweza kuuona uzuri wa mtoto wake kwenye picha, siku zote walimsifia mzuri mzuri ila yeye alimchukulia kawaida ila kwenye zile picha aliona vizuri kuwa mwanae anastahili kuitwa mzuri na mrembo.
Lile swala la kusaini mkataba lilipoisha, Angel alipewa baadhi ya nguo na kukabidhiwa Erica,
“Sikia, ukimvalisha mpige picha halafu tutumie. Sawa eeeh!”
“Sawa hakuna tatizo”
“Halafu ukamfungulie mtoto akaunti benki ili hela zake tuwe tunaingiza huko, kwa kuanzia tutakuingizia wewe kwenye akaunti yako ila mfungilia ili kila mwezi tuwe tunamuingizia huko maana kila mwezi tutakuwa tunamlipa”
“Oooh nashukuru sana jamani”
“Mshukuru mwanao, maana umepata bahati sana ya kupata mtoto mzuri halafu anajua kutabasamu, mtoto ana pozi kama mtu mzima! Kwakweli kwa mwaka huu huyu ndio mtoto bora kwangu”
Erica akatabasamu na kuendelea kushukuru kisha akahitaji kuondoka, hivyo Moses akamwambia,
“Basi naomba nikupeleke mwenyewe nyumbani kwenu maana ni vyema nikafahamu na kwenu hata leo na kesho iwe rahisi kukupata, mfano tukishusha mzigo mpya tutahitaji mwanao afike, sasa nikipajua kwenu itakuwa rahisi mimi mwenyewe kuja kuwafata”
“Sawa, hakuna tatizo”
Kwahiyo Moses alipanda na Erica kwenye gari yake kisha kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akifata maelekezo toka kwa Erica.
“Ila kumbe una gari, mbona siku ile ulipanda daladala”
“Mfano nisingepanda daladala basi nisingekutana na wewe, unajua kutembea na usafiri wako ni vizuri sana ila kutembea kwenye usafiri wa jumuiya ni vizuri zaidi. Kwanza unaweza kufahamiana na watu usiowatarajia, pili unaweza kupata fursa mbalimbali kwa kusikia mazungumzo ya watu kwenye daladala na pia kuona vitu mbalimbali vinavyotendeka. Sio wote wanaopanda daladala hawana usafiri binafsi, wengine wanao ila wapo kwenye daladala ili kujifunza changamoto mbalimbali.”
“Aaah hapo nimekuelewa”
“Mimi huwa napanda gari binafsi nikiwa na mambo ya haraka ila kama sina haraka basi daladala itanihusu kwanza ni rahisi kujua mahitaji ya watu mbalimbali ukiwa nao karibu”
Erica alimuelewa sana Moses na kumuona ni mtu mwenye uelewa wa hali ya juu.
Walifika kwakina Erica ila Moses hakuingia ndani alimuaga tu pale kisha kuondoka na kumuahidi kuwa ataingia ndani siku nyingine.
 
SEHEMU YA 243

Mama yake Erica kama kawaida alishangaa mzigo wa nguo aliorudi nao Erica ila bado Erica alimwambia swala lile lile kuwa mwanae kachaguliwa balozi kwenye duka la nguo kwahiyo wanampa nguo kama motisha.
“Kheee una bahati sana mwanangu, hapa ndio mtu unaelewa ule msemo wa watu kuwa usimtupe mtoto. Jamani Erica ulikuwa ukilia lia mwanangu na kumuona kama mtoto wako huyu akiwa nuksi kumbe ana baraka zake kwa Mungu. Hongera sana mwanangu”
“Asante mama, ila hongera yetu sote maana ni wewe uliyemlea mtoto huyu vizuri hadi kawa na afya ya kuonekana kupendeza machoni mwa watu. Asante mama, yani Angel ana mwaka tu ila kila anayemuona anampenda yani hadi najisikia raha”
“Ila mwanangu kuwa makini na watu, maana sio wote wanaomsifia mtoto ni watu wazuri. Hata usiwaachie mtoto bila sababu ya msingi eti kwavile mtoto anatabasamu na kufurahi, achana nao yeni ukiwa mahali wewe kuwa makini na mtoto tu, watu wanasifia mzuri mzuri gafla wanatoweka na mtoto, utalia kilio cha mbwa mwanangu, mtoto anauma asikwambie mtu”
“Sawa mama nimekuelewa, naamini maneno yako uliyowahi kuniambia kuwa kila mtoto ni mzuri ila ni vile tu mzazi anavyomuweka. Na umemfanya mwanangu aonekane kwenye muonekano wa kuvutia maana umemuweka vizuri. Asante mama”
Mama yake alitabasamu kwa kuona kuwa Erica amethamini mchango wake kwa mjukuu wake, kisha Erica alienda chumbani kwake ila alijiona kafanya jambo jema kwenda kusaini mkataba mwanae awe balozi,
“Jamani kuna watu wana roho mbaya, sasa Tumaini mapenzi ya kaka yake yanamuhusu nini? Kama kaka yake namdanganya, yeye anaumia na nini? Siwezi kumwambia Erick kwasasa maana nahitaji akili yangu ikae sawa kwanza ndio nimwambie, maana sijui atachukulia vipi. Hapa nilipo ubongo umejaa mawazo halafu nikaongeze na mawazo ya kukataliwa na Erick mwanaume nimpendaye? Hapana kwakweli, siwezi kumwambia kwasasa, na swala la mwanangu kuwa balozi nilikuwa nalihitaji sana kwani kwasasa sina sehemu yoyote ya kusaidiwa kulea mtoto ila kwasaivi itanisaidia, hebu ona hela nilizopata hata itafanya nisipokee tena hela za shemeji ambazo nina mashaka nazo kuwa zinaniingiza matatizoni ingawa mwenyewe anajifanya hana tatizo. Halafu Yule Salma nae ana nini jamani? Sijui kajuaje kama nimezaa na Rahim mmmh! Ila nimefanya vyema kutokumjibu, asinibabaishe sijui mtoto wa kike sijui wa kiume, mtoto ni mtoto asinibabaishe. Kwanza mwanangu kashakuwa balozi, aka mwenyewe naanza kujifaidia matunda ya mtoto akiwa bado mdogo”
Alikuwa akiongea mwenyewe tu huku akitabasamu na kuendelea na shughuli zake zingine. Kisha muda wa kulala ulivyofika alilala tu.
 
SEHEMU YA 244

Kesho yake alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida, ila alipofika tu James alimuita ofisini kwake,
“Vipi jana, ulimpeleka mtoto huku kliniki?”
“Ndio nilimpeleka”
“Vizuri sana, Erica wewe ni mama bora unamjali mtoto wako”
Erica akatabasamu tu, kisha akakumbuka swala la kumfungilia akaunti mtoto wake na kumuomba ruhusa James kuwa aende benki mara moja,
“Unataka kwenda kufanya nini?”
“Nahitaji kumfungulia akaunti mwanangu ili niwe namuwekea pesa kidogo kidogo kwaajili ya elimu yake”
“Aaah nimekupenda bure Erica, wewe ni mama bora. Nakupa ruhusa, tena naomba nikupe nah ii pesa iwe kama kianzio kwenye akaunti ya mwanao”
“Hapana bhana usinipe hela”
“Erica, hii pesa si kwaajili yako ila ni kwaajili ya mtoto wako. Vitu muhimu vya mtoto vyote umebeba?”
“Ndio nimebeba”
“Naomba uchukue hii hela Erica, sio yako hii ni ya mtoto. Ukishamuwekea uniletee na risiti”
Erica akakubali kwani aliona ni kweli James ana lengo la kumsaidia tu. Alipokea zile pesa toka kwa James ambazo zilikuwa laki mbili.
Kisha akaweka kazi zake sawa na kwenda benki kwaajili ya kumfungulia mwanae akaunti.
Alipofika benki wakampa mlolongo mzima sema vitu vyote alikuwa navyo maana alijipanga tangia nyumbani, kwahiyo walianza kufungua hiyo akaunti.
Walipofika kwenye picha za mtoto, mkaka aliyekuwa akishughulikia kumfungulia Yule mtoto akaunti alichukua ile picha na kwenda kuwaonyesha wenzie kisha akarudi,
“Dada, naomba usijisikie vibaya, nimeshindwa kuangalia uzuri wa huyu mtoto peke yangu ndiomana nikapeleka na wenzangu wamuone. Una mtoto mzuri sana”
“Asante”
Alipomaliza, aliombwa kidogo kwa meneja wa benki, kwahiyo akaenda na kuongea nae,
“Dada, tutakuhitaji hivi karibuni kuna mambo tunahitaji utusaidie”
“Mambo gani hayo?”
“Tutakwambia siku hiyo ya kikao, ila tuachie namba yako ya simu hapa mezani. Najua ipo kwenye mitambo yetu ila ni vizuri ukiniandikia kwenye hiki kitabu niwe na kumbukumbu vizuri”
Erica aliandika namba zake kwenye kitabu alichoonyeshwa kisha kuondoka zake na kurudi ofisini ambapo alienda kumpelekea James risiti kuwa ameweka zile pesa kwenye akaunti ya Angel.
“Wow, Erica hata mwanaume atakayekuoa atakuwa ni mwanaume mwenye bahati sana. Una akili sana, sikutegemea kama ungeniletea risiti kweli! Wewe ni mwanamke makini”
Erica alitabasamu tu na kwenda kuendelea na kazi zake na muda ulipofika alienda kuaga na kuondoka zake, bado aliondoka mapema ili kuonyesha kuwa anasoma ila hakuwa akisoma wala nini bali alikuwa akienda nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 245

Siku hiyo alienda kwenye duka la Moses moja kwa moja kumpelekea akaunti namba ambapo Moses alifurahi sana kisha kuagana nae na kumuomba kuwa aende na mtoto Jumamosi kwaajili ya kumpiga picha na nguo zingine. Erica alikubali na kuagana nae pale.
Alirudi nyumbani kwao na kuongea kidogo na mama yake kisha kuingia chumbani kwake na kufanya mambo yake mengine.
Siku hii usiku aliingia kwenye mtandao maana alipokea ujumbe kutoka kwa Erick akimuomba aingie mtandaoni, wakati akiwasiliana na Erick alishangaa Erick kumtumia picha ya mtoto wake.
Erica alishangaa kuwa Erick kaitoa wapi picha ya mtoto wake.

Siku hii usiku aliingia kwenye mtandao maana alipokea ujumbe kutoka kwa Erick akimuomba aingie mtandaoni, wakati akiwasiliana na Erick alishangaa Erick kumtumia picha ya mtoto wake.
Erica alishangaa kuwa Erick kaitoa wapi picha ya mtoto wake.
Alikuwa kimya kwa muda, akashangaa tena kuona Erick akimtumia picha kama tatu za mtoto wake, ikabidi Erica ajibaraguze na kumuuliza Erick,
“Kafanyaje huyo mtoto?”
“Nimekutumia uone uzuri wa huyo mtoto”
“Kweli ni mzuri”
“Erica, nilipoona picha za huyu mtoto nimejikuta nikitamani kuwa na mtoto balaa. Erica tafadhali naomba tuzae”
“Tutazaa tu”
“Erica, usingetoa ile mimba mtoto wetu angekuwa mkubwa sana saivi, natamani mtoto Erica, huwezi amini picha za huyu mtoto nimetumiwa jana basi nimekaa nikiziangalia balaa yani muda wote najihisi nikitaka kumuangalia. Natamani angekuwa mwanangu”
Erica akawaza kuwa pengine Erick alikuwa akimuweka mtegoni ila akajipa moyo kuwa ataukwepa mtego wa Erick, alikuwa kimya tu akisoma jumbe za Erick. Kisha Erick alimuuliza tena,
“Mbona kimya Erica? Husemi chochote kuhusu huyo mtoto?”
“Sasa niseme nini Erick”
“Nimekwambia mwenzako natamani tupate mtoto, wewe hata huchangii kuwa unatamani pia”
“Na mimi natamani, sema upo mbali”
“Nikutumie nauli uje South?”
Erica akawa kimya kwa muda maana aliona akiwa mtegoni zaidi, kisha akamjibu,
“Hapana Erick, kuna kazi ndio nimeanza kufanya, siwezi kuomba likizo mapema hivyo”
“Kwani huko kwenye kazi wanakulipa shilingi ngapi?”
“Mmmh jamani Erick!”
“Niambie tu wanakulipa ngapi?”
“Laki tisa kwa mwezi”
“Basi mimi nipo tayari nikupe mwenyewe kila mwezi hiyo hela, nitakupa na hela nyingine ya matumizi. Erica, natamani tuwe na mtoto”
“Erick, ukirudi nchini tutapanga hayo mambo, hatutakiwi kufanya kwa haraka hivyo”
Erica aliamua kumpooza ila aliogopa kumuuliza kuwa picha za mtoto Yule kazitoa wapi kwa maana alihofia angeanza maneno mengine.
Aliamua kuagana nae tu kwa muda huu na kulala.
 
SEHEMU YA 246

Siku iliyofatia alienda kazini kama kawaida, alifika na kufanya shughuli zake. Muda ulivyofika aliinuka na kwenda kumuaga shemeji yake kwaajili ya kuondoka,
“Kwa siku ulizo jifunza funza bado hauwezi kuendesha hata kidogo Erica?”
“Bado bado”
“Aaaah haiwezekani au wazembe hao!Basi siku za mwisho wa wiki nikufundishe mwenyewe”
“Mmmh nitaelewa tu shemeji usijali”
“Mmmh Erica wewe”
“Usijali shemeji”
Kisha Erica akamuomba kuondoka na kuondoka zake, ambapo moja kwa moja alienda stendi ya daladala ila kabla hajapanda, alishikwa mkono na mtu, kugeuka ni Fetty ambaye alimfurahia na kumkumbatia kisha Fetty akasema kwavile wamekutana tena acha aende naye nyumbani kumuona mtoto, Erica hakukataa na kuanza kwenda nae.
Walifika nyumbani kwakina Erica na kumkuta mama yake ambapo Erica alimsalimia kisha Yule Fetty nae akamsalimia, akaweza kumkumbuka vizuri kutokana na siku ile waliyoondoka kwenda hospitali.
“Karibu sana”
“Asante mama”
Muda kidogo mtoto wa Erica alitoka chumbani na kwenda sebleni, inamaana alikuwa ameamka maana alikuwa amelala, kwahiyo alivyomuona mama yake alionyesha kufurahi sana, kisha Erica alimnyanyua mtoto wake kama ishara ya kumsalimia, na kumpa Fetty amsalimia.
Fetty alimchukua mtoto Yule na kusema,
“Hiiii jamani ni mzuri, uwiiii mzuri sana”
Mama Erica akasema,
“Mmmh taratibu mtoto, huo uzuri mpaka wa kushtuka wa huyo mtoto uko wapi? Mpaka ushangae kweli, kama kusifia si usifie kawaida tu, kwanza ni wa kawaida. Mlete mjukuu wangu”
Ilibidi Fetty ampe mama Erica Yule mtoto ambapo alitoka nae nje, Erica alikuwa amesimama tu akimshangaa mama yake na kushindwa hata kuongea jambo lolote.
Alivyotoka alianza kumuomba msamaha Fetty,
“Fetty, naomba unisamehe mimi. Sijui mama yangu vipi yani mambo yake daha nashindwa hata kuelewa, nisamehe Fetty”
“Hata usijali rafiki yangu, mimi ni muelewa na nimeelewa. Hata hivyo nimeshangaa sana, ila sio kosa la mama ni kosa langu kushangaa sana”
“Jamani Fetty hadi najisikia vibaya”
“Usijisikie vibaya Erica, tena mama hajafanya chochote kibaya. Unajua watoto wengi sana wanazaliwa wazuri, wanapendeza ila huharibika kutokana na maneno ya watu. Kila mtu na mtazamo wake, mwingine anamsifia mtoto kumbe ana kinyongo moyoni, na usiombee awe mchawi basi anaweza kumshika na kumsiriba kimavi”
“Kimavi? Yani anampaka kinyesi?”
“Hapana, ila kimavi ninachosema hakionekani kwa macho ya kawaida ila utashangaa mwanao ni mzuri anapendeza ila hakuna mtu anayetambua uzuri wa mwanao, yani mtoto wako haonekani kabisa. Tena utashangaa vitu vingine anapitwa kupewa, ujue mtoto kapakwa kimavi, yani kuna kipindi kinafika hadi kuna jambo unafanya unashangaa wewe binafsi umemsahau mwanao kwenye jambo hilo na kujiuliza kwanini kumbe mtoto kashapakwa kimavi”
“Ooooh asante kwa kunijulisha, sasa nitajuaje mwanangu anataka kupakwa kimavi?”
“Usimuachie mtoto mtu ambaye umeanza kuingia mashaka nae, na ukiona mtoto ameshaanza kuwa na sifa za kutokuonekana, kutengwa yani unaweza fika kliniki na mtoto, wenzio wakahudumiwa halafu wewe ukaachwa hadi ukamshtua nesi kuwa mbona nipo, yani hapo kuwa na mashaka kuwa pengine ni wewe au mtoto ana kimavi. Kama ni mtu wa jadi, mpeleke mtoto kwa mganga, na kama ni mtu wa maombi basi mpeleke mtoto kwenye maombi”
“Mmmh umenifungua macho Fetty, sasa mama ana mashaka gani na wewe?”
“Mama hajapenda vile nilivyomshangaa mtoto ndiomana kainuka na mjukuu wake ila sio kosa lake inaonyesha mamajo yupo makini sana yani hata mwanao wakimchafua basi mamako yupo makini nae, usione mwanao anapendeza Erica unatakiwa kumshukuru mama yako”
Erica alimsikiliza Fetty maana alijua atakuwa amechukia sana ila ni tofauti, ndio kwanza Fetty alikuwa akimuelekeza tu mambo asiyoyajua, kisha Fetty akaaga kuwa anahitaji kuondoka, ikabidi Erica akaweke mkoba wake ndani na kwenda kumwambia mama yake kuwa Fetty anaondoka.
Mama yake Erica alitoka kwa aibu kidogo maana alijua Fetty ameaga mapema vile sababu ya kumnyang’anya mtoto,
“Nisamehe mwanangu, najua sijafanya vyema”
“Hapana mama, nimekuelewa hata usijali”
Mama Erica alimpa tena mtoto Fetty ili amuaga, ambapo Fetty bila kinyongo alimchukua mtoto Yule na kumuaga kisha kumrudisha kwa bibi yake na kuanza kutoka nje ambapo Erica alimsindikiza.
 
SEHEMU YA 247

Fetty na Erica walikuwa wakisindikizana huku wakiongea mambo mbalimbali,
“Unajua Fetty, wewe ni mtu mzuri sana nashangaa ni kwanini sikuwa na urafiki na wewe wa karibu chuoni”
“Sio kosa lako, kwa mtu ambaye hupendi umbea huwezi kuwa karibu na mimi sana. Mimi ni mbea sana na ninajijua ndiomana wakati nilipokutana na mama yako na anaulizia kwako unapoishi wala sikusita kumleta maana nina asili ya umbea”
Erica alicheka na kusema,
“Yani wewe mbea na unajikubali?”
“Ndio mimini mbea yani najua hilo, kule nilipokuwa naishi na Yule mwanaume nimeachika kwa mengi ndugu yangu. Mume ana mapungufu yake na mimi pia nina mapungufu yangu, ila najua ananimiss sana maana nikishinda nyumbani mimi basi habari za mtaa mzima ninazo. Bora nikienda kazini, ila kazini naenda siku zote halafu Jumamosi na Jumapili napumzika, weee habari zote nazipata yani burudani kwahiyo nikianza kumpa mlolongo wa habari Yule mume anabaki mdomo wazi. Ingawa kanitimua kwa kusikiliza ndugu zake na kusingizia dini ila najua ananimiss sana”
“Hahahaha Fetty wewe, mawifi zako hawakupenda umbea?”
“Basi tu walikuwa na yao, halafu umbea wangu hata sikuwa nafanya nao hata nawashangaa kunichukia. Ila ndugu yangu Erica, mwanaume anayekataa majukumu ya mwanae huwa anaumbuka vibaya tena vibaya sana. Unajua watoto ni baraka njema ambayo Mungu ametupatia, ila ikitokea mtu anakataa majukumu ya ile baraka ambayo Mungu ameitoa basi ujue ipo siku mtu huyo ataumbuka balaa. Yani aibu ya wale viumbe inanukia”
Erica akacheka sana kisha gari likaja na Fetty akapanda na kuondoka.
Wakati Erica anarudi kwao, akakutana na Johari na kushangaana kwa muda,
“Erica kumbe upo kwenu hatuambizani?”
“Majukumu, nisamehee sana”
“Vipi ulishamaliza chuo?”
“Mbona siku nyingi sana”
“Mahafali umefanya kimya kimya hata hatujaalikana”
Erica akanyamaza kwa muda kwani kiukweli hata mahafali yenyewe hajafanya kwahiyo swala la kuambiwa kafanya kimya kimya aliona linamchanganya tu, ikabidi abadili mada,
“Una watoto wangapi saivi Johari?”
“Wawili”
“Kumbe wawili tu? Ulizaa na Yule Yule au?”
“Wawili tu kwani wachache? Wananitosha, natumia uzazi wa mpango mwenzio unajua ukishaharibu maisha yako basi usipende kuendelea kuharibu. Yule mwanaume achana nae, kumbe sikukwambia eeeh! Yule mwalimu bhana kumbe alikuwa na mke wake, kipindi anakuja kuja kuniona mkewe hakuwepo alisafiri kikazi sasa ndio akawa anamalizia shida zake kwangu. Mtoto wa pili sijazaa nae yeye, yupo mkaka amenipenda na mwanangu ndio naishi nae ndiomana siku hizi huku sionekani sana maana naishi huko sehemu nyingine na huyo mwanaume”
“Pole na hongera kwa kumpata huyo anayekujali”
“Na wewe vipi, huna mpango wa kupata mtoto au ndio hadi uolewe? Tupe basi kadi za harusi hiyo”
“Mmmh Johari wewe, nitakwambia tu hata usijali”
Kisha Erica akajifanya anapitia dukani ndio aende kwao, alifanya vile kwasababu hakutaka kwenda kwao na Johari. Kwahiyo waliagana nae, halafu Johari aliendelea na safari yake nay eye kwenda dukani na kununua kitu ambacho wala hakukihitaji kwa wakati huo.
Baada ya hapo, Erica alirudi kwao na jioni ilikuwa imeingia na kigiza nacho kuanza kutanda.
Alivyoingia tu ndani, leo mama yake alikumbuka kuhusu Bahati na kuulizia yuko wapi,
“Erica, hivi Yule muuza samaki aliishia wapi jamani toka siku ile hadi leo kimya!”
“Mmmh! Mama leo ndio unamkumbuka? Kweli umuhimu wa kitu huonekana pale unapokikosa, yani Bahati hayupo tena ndio unamkumbuka wakati siku zote huwa unajifanya humtaki”
“Mmmh Erica jamani ni lazima nimkumbuke, alikuwa anampenda Angel mwenyewe alikuwa anatuletea kuku, samaki nimejifaidia haswaaa. Alikuwa ananiachia hela, jamani lazima nimkumbuke. Akija anashinda na Angel, anacheza cheza nae na mtoto nae anafurahi anakuwa kama watoto wengine wenye baba. Nimemkumbuka sana Yule kijana, yuko wapi?”
Erica akainama chini, hapo kumbukumbu zote za ndoa ya Bahati zilimjia na kujikuta akiumia sana. Alikuwa kimya tu tangu mamake alipokumbushia mazuri ya Bahati, ilibidi mamake amuulize tena,
“Kwani kuna nini Erica? Kwani huyo Bahati yuko wapi?”
“Mama, sielewi kabisa yani sielewi, kweli mwanao mimi ni fungu la kukosa”
“Kwanini unasema hivyo mwanangu?”
“Katika ulimwengu huu hakuna mwanaume niliyejua ananipenda kufa kama Bahati, maana hata nikifanya baya ila kwake ataliona zuri hadi nilijiona ni mwanamke mwenye bahati kama jina lake. Lakini huwezi amini, Yule Bahati aliyenipenda kufa, aliyeonyesha kufanya vyote kwaajili yangu ameoa”
“Ameoa?”
“Ndio ameoa”
“Kwahiyo siku zote alikuwa akija hapa tayari ana mke au?”
“Hapana mama, ila wiki mbili tu baada ya kutoka hapa huwezi amini mama nilimshuhudia Bahati kwa macho yangu akiwa amefunga ndoa. Yani hili jambo sijaambiwa na mtu bali nimelishuhudia kwa macho yangu, Bahati ameoa mama. Hadi nashangaa mama yani kwa wiki mbili tu Bahati ameoa, sikuamini”
“Mmmh yani kwa wiki mbili apate mwanamke mwingine wapange maswala ya ndoa hadi kuoana! Mbona hainiingii akilini hiyo? Au alishakuwa naye huyo mwanamke na walishapanga maswala ya ndoa ila walikuja kwetu kujikosha ili mamake alete maneno ya shombo na tuseme ni mamake kumbe wamejikosha”
“Hata mimi nahisi hivyo mama, kwakweli watu wanajua kuigiza yani Bahati alivyoniigizia ananipenda yani siamini, nashindwa kuamini kabisa. Ndiomana inakuwa ngumu kwangu kuelewa maana ya mapenzi kama mtu anaweza kukuigizia kama Bahati jamani mpaka unaamini unapendwa kumbe hakuna kitu”
“Ila usijali mwanangu, kama ridhiki yako ipo basi ipo tu hata usijali, si unaona saivi sikupigii kelele kuhusu baba wa mtoto ingawa najua kaka zangu wakija hapa ni balaa ila sitaki kuendelea kukuumiza kichwa mwanangu. Usijali, hata mimi sikufikiria kama Bahati anaweza kufanya hivyo”
Erica aliinuka na kuelekea chumbani kwake kwani alijisikia kulia na hakupenda kulia mbele ya mama yake kwahiyo aliingia chumbani na kulia, huko alijikuta akikumbuka mambo mengi sana,
“Hivi mapenzi ni nini? Siyaelewi kabisa, na kwanini yalikuwepo? Niliamini Bahati ananipenda sana ndiomana hela nilizokuwa napewa na Rahim nilimpa Bahati maana nilipenda awe na muonekano wa mwanaume ninayependa kuwa nae, ila ni nini sasa kimenitokea? Bahati nimemkosa, Rahim nae nimemkosa”
Alilia sana hadi mama yake alienda kumgongea,
“Wewe Erica, hebu njoo umchukue mtoto umlaze chumbani”
Erica alifuta machozi na kwenda kumchukua mwanae kisha kuingia nae chumbani, hakutaka kuendelea kuwaza sana badala yake aliamua kulala tu.
 
SEHEMU YA 248


Jumamosi ilipofika Erica aliamka na kujiandaa kisha kumuandaa mtoto wake kwaajili ya kwenda dukani kwa Moses maana alimwambia kuwa ampeleke mtoto Jumamosi hiyo, alikuwa anawaza kuwa siku hiyo apande daladala na mwanae,
“Mmmh kukodi tax kila leo itaniumiza sana, nahitaji kumtunzia mwanangu hela za kumsaidia badae na masomo yake. Mfano ningetunza zile pesa nilizokuwa napewa na Rahim labda ningefanya kitu bora kuliko kumrundikia Bahati ambaye kaniacha na kwenda kuoa msuchana mwingine. Inaniuma kila nikifikiria, namuomba Mungu tu anipe ujasiri”
Wakati analalamika hayo mamake alimsikia, na kutoka kumuuliza kwa hamaki,
“Wewe Erica, usiniambie kuwa ulikuwa unampa hela Bahati?”
Erica akakaa kimya, kisha mamake akaendelea kuongea,
“Yani unampa hela mwanaume? Umepata wapi akili ya kijinga hivyo Erica? Badala mwanaume akupe wewe eti wewe ndio unampa hela mwanaume! Ulimpenda sana eeeh! Nadhani Bahati alikuwa anakubembeleza sababu ya hela ulizokuwa unampa na sio mapenzi. Wewe mtoto ni mjinga sana”
“Ila mama, mbona wanawake huwa tunapewa hela na wanaume? Kwanini iwe ngumu hivyo kwa wanawake kuwapa wanaume?”
“Hebu kuwa na akili kidogo wewe mtoto, tumesomesha kopo tu, uwe unasoma hata maandiko basi, imeandikwa mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho yani mwanaume anatakiwa kutafuta sio wewe utafute umpe ili iweje? Si bora ungenipa mimi mama yako hata nisingekuwa nakusema sana maana hela tumekula wote, ila hela umeenda kuzimwaga kwa tahira Yule, unaona sasa kaona mwanamke mwingine! Mwanaume sio ndugu yako”
“Sawa mama, nimekuelewa”
“Haya, unataka kwenda wapi na mjukuu wangu?”
“Si kule nilipokwambia mama kuwa mjukuu wako amekuwa balozi, sasa ndio leo wanaenda kumpiga picha”
“Mmmh mambo ya kizungu hayo hata siyaelewi, ila ita gari ikupeleke hadi kituoni halafu upande daladala. Usimtembeze mjukuu wangu juani kwa ujinga wako, jua kali hili”
Ilibidi Erica achukue ushauri wa mama yake na kwenda kupanda gari hadi kituoni halafu kupanda daladala.
 
SEHEMU YA 249

Alifika dukani na kwenda moja kwa moja kwa Moses, kama kawaida pale dukani walimfurahia sana mtoto wa Erica, kisha Erica akasogea kuongea na Moses ambapo Moses alionyesha mzigo mpya ambao walitaka kumjaribisha Angel na kumpiga picha, hilo zoezi halikuwa gumu maana mtoto wa Erica alipenda picha sana kwahiyo ilikuwa rahisi sana kwake, kwani aliweka mapozi kama mtu mzima, walipomaliza Moses akamwambia Erica,
“Hiki ndio kitu kinachofanya huyu mtoto awe tofauti na watoto wengine, kuna baadhi ya watoto kuwapiga picha hadi uwavizie maana wakikuona na camera tu ni balaa ila huyu mtoto ana pozi na kutabasamu kabisa. Nampenda sana huyu mtoto”
Moses akamnyanyua Angel huku akimuonyesha baadhi ya vitu vya kuchezea watoto, wakati Erica yupo akitabasamu tu mara alitokea Tumaini na kumuita Erica pembeni, sura ya Tumaini ilionyesha kuchukizwa sana, Erica alimfata nje na kuanza kuzungumza nae,
“Hivi wewe Erica una akili gani? Yani Erick hujamwambia ukweli halafu umenizunguka na kuja kusaini mkataba. Kwanini umefanya hivyo?”
Erica alikuwa kimya na kumfanya Tumaini aendelee kuongea,
“Erica, ngoja nikwambie kitu. Kwa baba tumezaliwa wawili tu yani mimi na Erick, kwa mama yangu tupo sita kwahiyo nina ndugu zangu wengine kwa mama ila Erick kwa mama yake napo yupo peke yake kwahiyo ndugu pekee wa Erick ni mimi tu, Erick anasikiliza ushauri wangu kupita ushauri wowote ule. Sasa wewe umejifanya kiburi, hivi hujui kama naweza kukuharibia? Hujui? Nijibu usinikalie kimya”
Muda huu Erica aliona maneno yamemchosha kwahiyo aliamua na yeye kutoa ya moyoni mwake,
“Tumaini, sikia nikwambie. Ulikuwa mtu mzuri sana kwangu, sikutegemea kama ungekuja kuwa mbogo kiasi hiko. Haya ni maisha ya mwanangu, unaniambia nisisaini mkataba kweli?”
“Maisha ya mwanao? Unajua duka la nani hili?”
“Si la Moses”
Tumaini akabana pua na kumgeza Erica yale maneno,
“Si la Moses, unaongea kama umetoka kufufuka. Si la Moses, unamjua sana Moses wewe? Nilikwambia umwambie ukweli Erick nilikuwa na maana yangu kabisa”
“Sasa hiyo maana yako usiponiambia nitajuaje?”
“Ni duka la Erick hili”
Erica alishangaa kusikia lile ni duka la Erick, kisha Tumaini akaendelea kuongea,
“Endelea kushangaa hivyo hivyo, unadhani Erick atakubali kumuweka mtoto wa kambo balozi?”
“Tumaini nakuomba usimwambie tafadhali, usimwambie Erick”
“Wewe si umejifanya kiburi, eti duka la Moses. Unamjua sana huyo Moses eeeh! Subiri uone sasa kitakachotokea”
Tumaini akaondoka na kumfanya Erica abaki na mawazo, kisha akarudi dukani ili kumchukua mwanae. Moses alimuona Erica alivyonyong’onyea gafla na kumuuliza,
“Tatizo nini Erica?”
“Hakuna tatizo”
“Yani kila ukiongea na Yule Tumaini huwa unarudi umepooza sana, Yule nae sijui anatafutaga nini hapa. Kisa tu duka la ndugu yake ndio kujifanya anakuja mara kwa mara”
Erica alihamaki na kumuuliza,
“Kheee kumbe duka sio lako?”
“Wengi wanajua duka ni langu, ila humu dukani kuna bidhaa zangu pia. Duka hili ni la mtu mmoja anaitwa Erick, ananiamini sana na ana duka lake lingine kubwa kama hili South”
Erica hakuwa na mengi ya kuongea ila alimwambia Moses kuwa anaondoka, Moses akamkodia gari na kumpa baadhi ya nguo kwaajili ya Angel ila hakuelewa ni kwanini Erica kaondoka akiwa amenyong’onyea vile.
 
SEHEMU YA 250

Erica alifika nyumbani kwao akiwa hana raha kabisa, mamake alimshangaa karudi na nguo za mtoto ila hana furaha wala nini. Alienda chumbani kwake, muda huo alimuacha mwanae sebleni na bibi yake alikuwa akitafakari sana,
“Sasa jamani kama lile duka ni la Erick itakuwaje? Ila bora nimeshasaini mkataba maana wakivunja mkataba itabidi wanilipe ila dah inaniuma sana, kwani Tumaini hajawahi kukosea katika maisha yake?”
Wakati anawaza hayo, simu yake ilianza kuita, kuangalia ni Erick alikuwa akipiga, Erica alijishauri kidogo na kupokea. Siku hiyo Erick hakuanza na salamu, moja kwa moja alisema,
“Erica, niambie kuwa sio kweli kwamba una mtoto?”
Erica alikuwa kimya, na kumfanya Erick aendelee kuongea,
“Niambie Erica kuwa nilichoambiwa ni uongo!”
Mara Angel aliingia chumbani kwa mamake huku akisema,
“Mama, mama, mama”
Ile sauti ilisikiwa vilivyo na Erick na akauliza tena kwa mshangao,
“Kumbe ni kweli Erica una mtoto!”


Erica alikuwa kimya, na kumfanya Erick aendelee kuongea,
“Niambie Erica kuwa nilichoambiwa ni uongo!”
Mara Angel aliingia chumbani kwa mamake huku akisema,
“Mama, mama, mama”
Ile sauti ilisikiwa vilivyo na Erick na akauliza tena kwa mshangao,
“Kumbe ni kweli Erica una mtoto!”
Erica alikaa kimya na kukata simu, kisha akamnyanyua mtoto wake na kuanza kulia huku akimuangalia, na mtoto huyu kwasasa alikuwa ni Yule mtoto anayejifunza maneno,
“Mama aiya nini?”
Angel alionekana kumfuta mama yake machozi kwa mikono, Erica aliamua kunyamaza kwani aliona ni kumkosesha mtoto furaha. Aliweka simu pembeni na hakutaka kuisikiliza tena.
Jioni mama yake alimuita na kuanza kuongea nae,
“Hivi Erica redio niliyokupa usikilizage unasikilizaga kweli?”
“Huwa nasikiliza mama”
“Haya niambie, jana alikuwa akihubiri nani na mahubiri yalihusu nini?”
“Ila jana sijasikiliza”
“Wewe mtoto wewe, unajijua kabisa akili yako haipo sawa, kanisani huendi yani upo upo tu na mahubiri nayo kwenye redio usikilizi kweli? Unadhani akili zako hizo mbovu zitaponaje?”
“Nisamehe mama, leo nitasikiliza”
“Hebu acha ujinga, mama yako nakupenda. Waswahili husema mtoto akiunyea mkono sio uukate bali uusafishe, sasa mimi nataka nikusafishe wewe ila wewe ni mbishi balaa unajifanya huelewi ila Erica kuwa makini mwanangu maisha haya, ushaharibu mwanzo usitake kuharibu hadi mwisho, kuwa makini sana”
“Nimekuelewa mama”
Erica alimuitikia mama yake na kumpa mwanae chakula, kisha muda alivyoenda chumbani kulala akaamua kufungua redio kama mama yake alivyomshauri ili kusikiliza mahubiri, alishangaa kuona mahubiri yakimlenga yeye tu.
“Hakuna kitu kibaya katika maisha kama uongo, yani jitahidi uikimbie dhambi ya uongo kumbuka uongo ndio ulifanya Adam na Eva wakala lile tunda, maana walidanganywa na nyoka kwahiyo uongo umetumika hapo. Uongo unatutenga na Mungu, halafu shetani ndio baba wa uongo kwahiyo ukiwa muongo ujue baba yako ni shetani. Kwani ukisema ukweli utapungukiwa na nini? Hata kama utaona kuwa kuna kitu utakipoteza kwa kusema ukweli bora upoteze kitu hiko na Mungu atakusimamia kwenye ukweli unaosema ila uongo utakutesa siku zote za maisha yako. Huwezi kukazana kumuomba Mungu akusaidie wakati katika maisha yako hakuna jambo la kweli yani ni uongo mwanzo mwisho, na uongo hauwezi kukuokoa kamwe. Ondoka sasa kwenye uongo na uwe mtu wa kusema ukweli, kumbuka ukweli humuweka mtu huru”
Erica alizima redio kwani aliona mahubiri yale yanamgusa moyo wake kabisa maana tabia yake ilikuwa imehusishwa moja kwa moja ila alifikiria sana kuwa anawezaje kuacha uongo,
“Ila siku hizi nimepunguza uongo, huwa sidanganyi ila sijibu. Nitawezaje kusema ukweli?”
Akawaza sana na kuamua kulala tu.
 
Patamu hapo !!!!
Tukutane saa 12 jioni... Tuliamshe dude
@@
SEHEMU YA 240

Kwenye mida ya saa kumi jioni, James alimuita Erica na kumpa ruhusa ya kuondoka,
“Yani hata hukumbuki kuwa unatakiwa kwenda chuo?”
“Nilisahau”
“Hebu acha mawazo Erica, fikiria maendeleo yako tu kwasasa, acha mawazo ya kijinga hayo mdogo wangu”
Muda huu Erica alijisikia vizuri sana kuitwa mdogo wangu na James, basi akamuaga pale na kuondoka zake.
Alienda kupanda daladala, ila leo kuna wakaka walikaa pembeni yake na akasikia maongezi yao,
“Yani mademu hawa vimeo vimeo, kuna demu nimekutana nae, ukimuona ni staarabu kumbe ni mbwa tu”
“Yule wa siku ile? Nilikwambia lakini jomba hukunisikia, uliona kama nakuonea wivu ndugu yangu, Yule demu jau yani kimeo cha mwisho”
“Najuta hata kutokufuata ushauri wako, ila mimi nikija kupata demu mwenye upendo wa dhati hakika nitatulia”
“Upendo wa mademu upo kwenye hela, yani ukiwa na pesa utapendwa wewe balaa ila uwe kapuku sasa utajuta yani mademu kwa pesa huwawezi ndiomana mimi sina demu wa kudumu huwa natembea nao na kuwaacha”
Erica aliwasikiliza mpaka alipofika kwenye kituo chake na kushuka ila kwa maongezi yale aliyoyasikia aliona kuwa wanaume wanapenda kuchezea wanawake wakati hata wao walikuwa wanalalamika kuwa wanawake wana matatizo.
Alifika nyumbani kwao na kumsimulia mama yake kuwa Yule mtu alifika ofisini kwao, ila hakumwambia kilichomnfikisha pale Yule mtu,
“Kumbe ni rafiki wa shemeji bhana Yule mkaka”
“Kheee mwanangu ila nilikwambia, kuwa makini na majibu sio kila kitu ni kujibu vibaya”
“Ila mama kama mtu anakutongoza na humtaki?”
“Si nishakwambia, mjibu kiustaarabu kwani ukisema hapana sitaki kuna tatizo gani? Sio unaanza ooh wewe sijui dini nyingine, kimeenda kimerudi sasa ndio nini hapo? Unatakiwa kuwa na jibu moja linaloeleweka”
“Sawa mama nimekuelewa na sitorudia tena mama yangu”
“Ndio usirudie, unanidhalilisha mimi ukifanya ujinga”
Erica aliinuka na kwenda chumbani haraka haraka maana alijua pengine mama yake angemuuliza kuwa mbona kawahi kurudi.
Alikaa chumbani ila wazo la Erick lilimjia kichwani na wakati akimfikiria Erick alipigiwa simu muda huo huo na Erick, kwakweli Erica akatabasamu na kuona ni jinsi gani upendo kati yake na Erick ulivyo mkubwa kiasi kwamba hata Erick anamuwaza vile vile na yeye anavyomuwaza, Erica akapokea ile simu
“Mbona kimya mpenzi wangu hukunitafuta tena?”
“Siku hizi nimeanza kazi Erick, kwahiyo narudi nyumbani nikiwa nimechoka balaa ila nakukumbuka sana tu, yani hata muda huu nimetoka kukukumbuka”
“Vipi facebook siku hizi hutumii?”
“Natumia”
“Mbona huwa sikuoni?”
Erica akakumbuka kuwa alifuta urafiki na erick maana hakutaka kumkwaza Rahim, alimwambia Erick,
“Labda nilitoa urafiki kwa bahati mbaya, ngoja nikuombe tena urafiki ili tuwe tunawasiliana”
“Sawa”
Erica alikata simu na kwa mara hii akachukua ile simu yake na kuingia kwenye mtandao ingawa kwa siku hizo hakupenda kuingia kwani kila alipomuona Rahim alihisi kuumia sana, na leo alikuta Rahim yupo hewani vizuri kabisa ila hakutumiwa ujumbe wowote na Rahim, akamtumia Erick ombi la urafiki na Erick alilikubali muda ule ule na kuanza kuwasiliana nae kwenye mtandao sasa,
“Ila Erick, muda sio mrefu nitalala, maana nimechoka”
“Sawa Erica, ila nakumiss sana na ninatamani siku moja tuishi wote. Subiri tu nirudi kutoka Kusini, ila usinisaliti Erica”
Kidogo Erica alisita kujibu maana kama usaliti kashaufanya sana tu mpaka na mtoto kapata, ila akamjibu kuwa asijali hatomsaliti, bado hakuweza kumwambia Erick kuhusu mtoto aliyekuwa nae maana alihisi kama upendo juu yake utapungua.
Akamuaga Erick kuwa muda huo analala, ila kabla hajatoka hewani alishangaa ujumbe kuingia kutoka kwa Rahim, akaufungua na kuusoma,
“Kweli mwenye asili haachi asili, kwahiyo umemtafuta Erick hadi kuanza tena urafiki nae? Nashukuru Erica, hela zote nilizokuwa nakupa ni kazi bure”
Erica alisoma mara mbili mbili ujumbe wa Rahim bila hata kuelewa kuwa Rahim amejuaje kuwa yeye na Erick wameanza urafiki tena, ila akakumbuka kuwa facebook ina mtindo wa kuandika Fulani na Fulani wamekuwa marafiki, kwahiyo inamaana labda Rahim kaona ujumbe huo ndio kajua kuwa Erica na Erick wamekuwa marafiki tena. Erica hakujua ajibu nini kwahiyo alipotezea huo ujumbe na kulala tu.

ITAENDELEA
:""
 
Back
Top Bottom