Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 277

Kesho yake tu alimuaga mama yake kuwa anatoka kidogo na kwenda kushughulikia cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake ambapo aliambiwa kuwa kitatoka baada ya wiki moja.
Yani wakati huo hata aliacha kufatilia mambo ya mkataba wa benki kabisa kwani hakutaka kuwa karibu na mzee Jimmy, ingawa mzee huyo alimtumia ujumbe mara kwa mara kuwa aende benki wakamalizie hatua za mkataba ila Erica hakutaka tena hata alipopigiwa na Yule meneja napo hakutaka kabisa maana alijiona anatosha kwa aliyoyapitia.
Ilimradi Erick kajitolea kumtunza mtoto ilikuwa inamtosha kwakweli.
Siku aliyoenda kufata cheti cha mtoto wake, wakati anarudi alikutana na Yule mama ambaye walikutana dukani akamsaidia kuchukua maji, Yule mama alisimamisha gari yake na kumuita,
“Erica”
Erica alienda kwa Yule mama ambaye alijawa na tabasamu tu, akamsalimia kisha Yule mama akasema,
“Yani nilipoteza namba yako, moyo ukaniuma kweli ila Mungu ni mwema nimekuona tena, ngoja nikuulize swali, una kazi? Yani unafanya kazi?”
“Hapana, nipo nyumbani tu”
“Umesoma mpaka wapi?”
“Chuo, nina shahada ya biashara”
“Jamani, ndio huna kazi kweli binti mzuri kama wewe dah! Sikia, chukua hii kadi yangu ya biashara, wiki ijayo njoo ofisini kwangu na vyeti vyako”
“Asante”
Erica alimshukuru sana Yule mama kwani aliona kama ni kitu cha ajabu ametunukiwa kwa muda huo, kisha akaagana nae na kurudi nyumbani.
Alifika na kujisemea,
“Kweli Mungu ana njia zake za kubariki, nadhani Erick ni baraka tosha katika maisha yangu. Nikijaribu kuunganisha matukio naona wazi kuwa Erick ni baraka tosha kwangu, kwanza Erick alinipigia simu nikawa na kimuhemuhe cha kumpigia na kuamua nikanunue vocha, mama akaamua aniagize na soda ndipo nikakutana na Yule mama mwenye roho nzuri. Haya Erick kasema nifatilie cheti cha kuzaliwa cha mtoto, natoka kukifata nakutana na huyu mama na ananiahidi kazi, wow nadhani Erick ni baraka kwangu”
Alitabasamu maana ilikuwa ni furaha kwake.
Alirudi kwao, kwa kipindi hiko mwanae alikuwa ameanza utundu wa kimya kimya kiasi kwamba alikuwa akirudi tu basi mwanae alichukua mkoba na kuangalia kuwa mama yake kamletea zawadi gani, bibi yake alikuwa akicheka sana na kusema,
“Yani Angel ananikumbusha kipindi kile wakati wewe mdogo, mtu akikuangalia anakuona mtoto mpole kumbe una utundu wa kimya kimya ninaoujua mimi tu, sasa mtu hawezi kudhania kama Angel anaweza fungua mkoba na kupekua ila ona hapo. Hahaha mpaka apate anachotaka”
Kwahiyo Erica alikuwa akinunua matunda mara nyingi ambapo akifika tu anampa mwanae ili mwanae asimpekue mkoba.
Alichukua mkoba wake na kuingia chumbani ambapo aliweka vizuri CV yake na vyeti vyake, aliweka kwenye bahasha nzuri kwaajili ya kuvipeleka kesho kwa Yule mama.
Alipomaliza alimpigia simu Erick kuwa kashapata cheti cha mtoto na picha anazo, basi Erick akamuelekeza mahali pa kupeleka ili mtoto atengenezewe kadi ya bima ya afya, kwahiyo Erica aliona ni vyema afanye vyote kwa pamoja.

Siku hiyo aliondoka asubuhi kwao na kuanza kwenda kwenye ofisi ya Yule mama akifata maelekezo ya kwenye ile kadi aliyopewa na kufika, kisha akaenda mapokezi na kumuulizia,
“Una miadi nae?”
“Ndio”
“Ngoja nimpigie simu, nimwambie unaitwa nani?”
“Erica”
Basi Yule wa mapokezi akapiga simu, Yule mama alipokea ila alionyesha alikuwa na kikao na kuomba kuongea na Erica, ambapo Yule wa mapokezi akamkabidhi simu Erica kisha Yule mama akamwambia aache nakala ya vyeti vyake kwa Yule mtu wa mapokezi, Erica alimshukuru kisha wakakata ile simu na kumuachia Yule wa mapokezi bahasha ya vyeti vyake halafu yeye kuondoka.
Moja kwa moja alienda mahali ambako Erick alimuelekeza kuwa apelike vile vitu kwaajili ya mtoto kupata kadi ya bima ya afya.
Basi alifika kama alivyoelekezwa na moja kwa moja alienda mapokezi na kukutana na mdada ambaye alimsalimia kisha kumuachia vile vitu vya mtoto ambavyo vilikuwa kwenye bahasha iliyoandikwa jina la Erick nje maana ndio maelekezo aliyopewa na Erick,
“Aaaah sawa, basi kikiwa tayari tutakupigia simu uju uchukue”
“Sawa nashukuru”
Basi Erica akaondoka zake, wakati yupo kwenye stendi ya daladala, kuna mdada alifika mbele yake na huyo mdada alionyesha kumfahamu Erica ila Erica alishamsahau, ikabidi Yule mdada aanze kumkumbusha,
“Unakumbuka siku ile umefika kwa Bahati nikakupeleka alipokuwa anaoa Yule Nasma hadi ukaanguka, unakumbuka”
Erica alimtazama huyu mdada na kumjibu,
“Nakumbuka ndio”
“Vipi, uliweza kuacha maisha yaendelee? Mapenzi ndivyo yalivyo mdogo wangu, muda mwingine unaumia hata usipotarajia”
“Nishasahau mie”
“Basi Yule Nasma saivi ni mjamzito, yani Bahati hajachelewesha yupo vizuri huyo”
Erica aliona huyu nae yupo kumchanganya tu wakati yeye ameshaanza kusahau mambo hayo, aliamua kumuaga na kuondoka zake kuelekea kwao, kwani hakutaka kuumiuza kichwa kabisa kwa muda huo kumfikiria tena bahati aliyemshuhudia akifunga ndoa, kwahiyo alipanda basin a kurudi kwao ambapo alimkuta mama yake kama kawaida ila leo mama yake alimwambia,
“Mwenendo wako kwa hivi karibuni umenifurhisha sana, ukienda mahali unawahi kurudi, sijasikia ujinga wa kuleta marafiki wa ajabu ajabu kama Dora. Mwanangu bora umeachana na aina ile ya marafiki, narudia tena, mimi ndio rafiki yako wa kweli. Kama una shida yoyote au una jambo lolote usisite kuniambia mimi rafiki yako wa ukweli”
“Sawa mama”
Basi akafurahi sana maana kwa siku hizo alikuwa akiongea kwa upendo tu na mama yake.
 
SEHEMU YA 278

Siku hiyo akiwa ametulia tu kwao akapigiwa simu kuwa kadi ya mwanae tayari hivyo aende kuichukua, aliahidi kuifata kesho yake, kwakweli Erica alifurahi sana kwani ndio kitu alichokuwa anahitaji kuona mwanae akiishi maisha yasiyompa mawazo kabisa.
Basi kesho yake akajiandaa na kumuaga mama yake kuwa anatoka kidogo kama kawaida, ila alienda moja kwa moja kwenye ile ofisi kwaajili ya kuchukua kadi ya mwanae.
Alimkuta Yule dada wa siku ile ambapo alimsalimia kisha akamwambia asubiri, muda kidogo walikuja wadada wawili na kukaa karibu yake wakati Yule wa mapokezi ameenda kumchukulia kadi ya mtoto.
Mmoja wa wale wadada alimuuliza,
“Samahani dada, erti Erick ni nani yako?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Nimekuuliza kwa maana yangu, nijibu kwanza ni nani yako?”
Huyu mdada alionekana akiuliza kwa shari sana, ila Erica akawa mpole na kumjibu ukweli,
“Erick ni mpenzi wangu”
“Mungu wangu, haiwezekani yani Erick mimi nimsubiri kipindi chote hiki anifanye kama mtoto kweli! Unasema Erick ni mpenzi wako?”
“Ndio ni mpenzi wangu”
“Hapana sikubali”
Yule dada aliinuka na kumkunja Erica, kwakweli Erica alikuwa kwenye mshangao tu kuwa imekuwaje leo akunjwe bila sababu, Yule mwenzie akawa anamzuia kuwa asifanye chochote kibaya,
“Hebu tulia na wewe, hujui inavyouma kuibiwa mpenzi, mimi niibiwe nitulie tu siwezi”
Alikuwa akiongea kwa jazba, Erica hakuweza hata kujitetea toka kwa Yule mdada kwani alionekana ni mkubwa sana halafu alionekana kuwa na nguvu. Kisha Yule dada alimsukuma Erica ambapo Erica alitaka kuanguka chini, sema kuna mdada alitokea nyuma yake akawa kama kamkinga, Erica alipogeuka akamuona Yule mdada kuwa ni Sia yani msichana aliyewahi kuambiwa kuwa ana mahusiano na Erick ila ndio alimsaidia siku hiyo asianguke.


Alikuwa akiongea kwa jazba, Erica hakuweza hata kujitetea toka kwa Yule mdada kwani alionekana ni mkubwa sana halafu alionekana kuwa na nguvu. Kisha Yule dada alimsukuma Erica ambapo Erica alitaka kuanguka chini, sema kuna mdada alitokea nyuma yake akawa kama kamkinga, Erica alipogeuka akamuona Yule mdada kuwa ni Sia yani msichana aliyewahi kuambiwa kuwa ana mahusiano na Erick ila ndio alimsaidia siku hiyo asianguke.
Wakati Erica alikuwa akimshangaa huyu Sia, basi huyu Sia alimvutia Erica nje ya ile ofisi na kumuuliza,
“Kwani umefata nini hapa?”
Kabla hajajibu, Yule msichana aliyekuwa akipambana na erica alitoka nje pia ila Sia alimkingia kifua Erica na kumwambia Yule msichana,
“Ukithubutu kumgusa nitaenda kusema kwa mkurugenzi, najua unajua siogopi”
“Wewe unamtetea huyo kama nani? Unajua nini kuhusu huyo msichana? Kwa kifupi tu, wewe humpati Erick, wala mimi simpati wala yeyote humu ofisini aliyewahi kuwa na Erick maana sasa yupo na huyo msichana”
“Hata kama Linah, bado hutakiwi kumpiga huyu msichana”
Basi Yule dada akachukia sana na kurudi ofisini kisha Yule mwenzie akamfata, halafu Sia akamuomba Erica wasogee mbali kidogo, Erica hakuwa na ubishi ila alimwambia kuwa hapo alienda kufata kadi, na Sia akamuuliza kuwa hiyo kadi nani anampatia,
“Yule secretary ameenda kunichukulia”
“Jiongeze Erica, huyo mtu kafata kadi mbinguni hadi wewe utake kupigwa? Kwanza ilikuwaje maana bado nashindwa kupata muunganiko”
“Nilikuja wiki iliyopita kushughulikia kadi ya bima ya afya ya mtoto, nilielekezwa na Erick kuwa nilete cheti cha kuzaliwa cha mtoto na picha. Nikafanya hivyo, na jana Yule dada alinipigia simu kuwa nije nichukue, nikamwambia nitaenda leo na ndio nilipofika ameenda kunichukulia”
“Pole sana, yani nakupa pole sana. Huyo aliyekushughulikia wiki iliyopita lazima ndio aliyemwambia Yule Linah maana anajua kwa ofisini humu hakuna mwanamke wa Erick mkorofi kama Linah, pia leo hakuwa na sababu ya kwenda kukuchukulia mbali, ni wazi alienda kuwaita wale wakorofi. Sasa swala la kuipata hiyo kadi niachie mimi, ndio nitaifatilia na utakuja kuichukua kwangu, Yule secretary anakuuzisha sura tu”
“Kwahiyo siipati leo?”
“Hebu subiri kidogo”
Erica alisubiri pale nje kisha Sia aliingia kwenye ile ofisi, kwakweli Erica alikuwa akiwaza vitu vingi sana, akakumbuka maneno ya Erick kuwa asimsikilize mtu yeyote Yule zaidi yay eye, na je asisikilize yeyote kweli kwa hali kama hiyo iliyompata siku hiyo? Alikuwa na maswali mengi sana, muda kidogo Sia alirudi na kumwambia,
“Itabidi uje keshokutwa na hiyo kadi nitakukabidhi mimi, ila usimwambie Erick. Nipe namba zako”
Basi Erica akampa Sia namba zake, ila Sia alimwambia kuwa anahitaji kuongea nae haswaa ili amwambie la moyoni mwake, Erica alitulia akimsikiliza, Sia alianza
“Nakumbuka mara ya mwisho ilikuwa ni kunisaidia mimi niweze kuwa na Erick, imekuwaje tena Erick yupo na wewe?”
Erica alikuwa anajiuma uma tu, ila Sia akaongea tena,
“Mimi sio mpambanaji kama Yule aliyepambana na wewe, ila tu nilishtuka kusikia kuwa na wewe ni mpenzi wa Erick. Sijui mlianzaje, najua nilikosea mwenyewe kusema upewe namba za Erick wakati namjua mpenzi wangu vizuri alivyo kuwa kisimpitie mbele. Na ubaya zaidi ni macho ya Erick, najua yanawachanganya wasichana wengi sana maana huwezi kuchomoa akikutazama usoni, sijui wewe na Erick mlianzaje ila Erick bado ni mpenzi wangu.”
Bado Erica alikaa kimya tu, kisha Sia akaendelea kuongea,
“Kwa kifupi, hakuna rangi ambayo Erick hajaiona, hakuna umbile ambalo Erick hajapitia, mnene, mwembamba, saizi ya kati, mrefu, mfupi, mweupe, mweusi, maji ya kunde yani kila aina ya mwanamke unayoijua wewe duniani Erick amepitia. Mimi kuwa na Erick hadi leo nimejitoa muhanga hata wote wanalijua hilo, nishagombana na wengi sana, ila niliwaambia jambo moja tu kuwa mimi siwezi kuachana na Erick hata wafanye nini na wao wajijue kuwa ni wapitaji tu kwa Erick maana mimi ndio wake. Upo? Je upo tayari na wewe kupitiwa tu?”
Erica bado alikuwa kimya huku moyo unamuuma balaa, kisha Sia aliendelea kuongea,
“Usifikirie Erick anagombewa na wanawake sababu ana hela nyingi. Ni kweli wakina Erick kwao ni matajiri, hata yeye ana hela haswaaa ila kinachofanya Erick agombewe na wanawake sio hela ila Erick ni mwanaume wa tofauti sana, ni mwanaume ambaye kila mwanamke atatamani kuwa na aina yake ya mwanaume, Erick anajua kubembeleza jamani kupita mwanaume yeyote uliyewahi kumuona ulimwenguni. Yani kubembeleza kwa Erick ndio mwisho wa matatizo, Erick anabembeleza haswaa na akilitaka lake ni lazima alitimize, anajua kujali Yule mwanaume na anajua kupenda. Mimi nishawahi kumfumania Erick mara nyingi tu tena hivi kwa macho sio kwa kuambiwa, tena muda unamfumania anaweza hata kukutimua ila mkikutana wawili uwiii utaona kama dunia ni mali yako peke yako maana mwanaume atakubembeleza Yule yani utasahau machungu yote ya kumfumania na utaona Yule mwanamke aliyekuwa na Erick ndio mbaya, najua hata ukimueleza haya Erick atakubembeleza wewe hata utasahau kama nishakutana na watu kibao ambao ni wanawake wa Erick”
Muda huu Erica aliamua kuongea kidogo, na kumuuliza Sia,
“Sasa nifanyeje?”
“Cha kukushauri kama hupendi kuumia achana na Erick, mimi nishazoea maudhi ya Erick na kila kitu kwani hadi marehemu baba yangu wakati anakufa aliniambia mwanaume wa kukuoa ni Erick tu maana alimfahamu. Mama yangu nae huwa anamuulizia Erick tu, siwezi kumuacha Erick kwani mara zote mama huulizia kama nawasiliana na Erick, mama yangu uzima wake unategemea furaha iliyopo kati yangu na Erick. Sikia nikwambie Erica, hii ofisi unayoiona ni mali ya baba yake Erick, na Erick ndio kila kitu kwenye hii ofisi japo aliteua wakurugenzi wa kusimamia hii ofisi maana yeye anashughulikia mambo yake mengine South, sikia nikwambie karibia asilimia kubwa ya wadada wanaofanya kazi humu basi wamewahi kutembea na Erick maana ukiona kamtafutia mtu kazi humu ujue ni wake. Narudia tena, cha kukushauri achana na Erick”
Kwakweli hii habari ya leo ilikuwa mbaya sana kwa Erica maana alihisi kama kapigwa ganzi vile mwilini, alijihisi vibaya mno, aliamua kumuaga Sia na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 279


Erica alienda taratibu kama mtu aliyechanganyikiwa, kwanza hakuelewa kuwa huyu Erick amemtakia nini yeye ikiwa ana sifa mbaya kiasi kile, alijiuliza sana moyoni kuwa Erick anafaa kuwa mume wake? Na kama hafai, jina la mtoto kambadilisha ili iweje? Alihisi kizunguzungu haswaaa, aliingia kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alijilaza kwenye siti ya daladala, pembeni yake walikuwa wamekaa wakaka wawili wakizungumza ingawa alikuwa na mawazo sana ila aliweza kusikia mazungumzo ya wale wakaka,
“Sisi wanaume bhana, unaweza ukahangaika na wasichana wa kila aina ila kuna mmoja tu anayekukosha yani kwa huyo hupumui jamani, unajikuta tu huna usemi ila wengine wote hawa huwa unawaambia nakupenda nakupenda, ila kuna mmoja tu kipenda roho”
Mwenzie akawa anacheka sana na kuongezea,
“Ndiomana unaweza kukuta mtu ana wake hata wanne ila kama kipenda roho hayupo kati ya wale wanne bado hawezi kutulia maana bado hajampata Yule anayemuhitaji”
“Na akiwepo lazima wenzie waone wivu maana yeye ndio atasikilizwa sana haijalishi ni mkubwa au mdogo”
Wakawa wanacheka ila yale maneno yao yalimuingia sana Erica, wakashuka, alitamani kujua kuwa unajuaje kama mwanaume huyu kipenda roho wake ni huyu ila akashindwa kuwauliza hadi wameshuka.
Na yeye alivyofika alishuka huku akijiuliza kama kati ya wanawake wa Erick basi ni yeye tu anayependwa au kuna mwingine? Maana kama kubembeleza imekuwa ni sifa ya Erick, je atajua kuwa anapendwa kwa kubembelezwa wakati mwanaume Yule ni kawaida yake kubembeleza? Huo ulikuwa mtihani mkubwa sana kwake, akafika nyumbani kwao amechoka kimawazo na kifikra hata mama yake alimuona hali aliyoingia nayo mwanae na kumuuliza,
“Tatizo ni nini Erica?”
Hakutaka kumwambia ukweli mama yake maana alijua kuwa mama yake kama angejua ukweli basi angemsema sana, kwahiyo akamdanganya tu,
“Nilienda kufanya usahili leo, tumepewa mtihani, maswali yalikuwa magumu sijui kama kazi yenyewe nitapata”
“Mbona hukuniambia mwanangu? Kumbe ulienda kufanya usahili wa kazi! Ila muamini Mungu kuwa anaweza yote hata usijali, kama ridhiki yako ipo basi ipo tu”
Erica alimuitikia mama yake pale kisha akaenda chumbani kwake ambapo mtoto wake naye alikuwa amelala basin a yeye akajilaza pembeni ya mtoto wake huku ana mawazo mengi sana.
 
SEHEMU YA 280

Jioni ya siku hiyo aliamka na kufanya kazi za hapa na pale ila ilimradi tu muda uende, na usiku ulipoingia alienda kulala, ila kabla hajalala alipigiwa simu na Erick, aliitazama na kutamani hata kutokuipokea ila aliipokea tu kishingo upande,
“Erica, mbona unaongea kwa kupooza kiasi hiko? Tatizo ni nini mpenzi?”
“Hakuna tatizo”
“Hapana najua tatizo lipo tu, Erica nimekuzoea haupo hivyo niambie tatizo ni nini eeh! Mimi ndio mpenzi wako na mimi ndio rafiki yako, unaponificha mimi utamwambia nani mwingine?”
Erica alijihisi kama machozi yanamlengalenga na kujikuta akishindwa kukaa na lile swala moyoni, akamwambia,
“Erick, kila siku unasema nakupenda Erica nami naamini hilo. Umeniambia nimbadilishe mwanangu majina niweke yako nami nimefanya hivyo, kweli leo Erick naenda kukutana na msululu wa wasichana zako jamani!”
Erica alikuwa akilia hata Erick alimsikia kwenye simu, kisha Erick akamwambia,
“Kwanza futa machozi yako Erica, hayo machozi yana thamani kubwa sana kwangu, sipendi kuona malkia wangu akilia sababu ya wapumbavu. Sikia Erica, wewe ni msichana pekee nikupendaye hakuna mwingine, ni wewe tu katika maisha yangu. Erica nilikwambia toka siku ile kuwa utasikia stori zisizofaa kuhusu mimi sijui Erick malaya sijui nini na nini ila yote ni sababu ya kutafuta penzi la dhati ambalo lipo kwako Erica. Wewe ndiye uliyefanya mimi niwe malaya, ndiomana hata swala la wewe kuwa na mtoto nimesamehe maana mimi ndiye nimefanya wewe uzae na mwanaume mwingine, Erica sikia nakuomba tufute yote ya nyuma na tuonane wapya, nione Erick wako ni mpya kabisa kwako, na mimi nakuona wewe ni mpya kabisa kwangu, umenisikia Erica mama yangu eeh!”
Erica alinyamaza ila akauliza tena,
“Lakini Erick unajua inaumiza sana, ni kweli sitamani kujua ya nyuma ila inaumiza sana kuona mlolongo wa wanawake zako, na inasemekana hujaachana nao”
“Erica, niamini mimi sina mwanamke mwingine zaidi yako. Wewe ndio maisha yangu, wewe ndio pumzi yangu, wewe ndio kila kitu kwangu, bila wewe siwezi Erica? Unataka nitangetange hadi lini wakati furaha yangu ni wewe? Wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, ni wewe tu Erica, hakuna mwingine zaidi yako”
Erica alitabasamu kwa maneno matamu aliyopewa na Erick na kujikuta akiongea nae kwa furaha sana kwani aliweza kuamini kuwa kweli yeye ni chaguo la Erick, kisha Erick aliendelea kuongea,
“Tafadhali Erica, usisikilize maneno ya watu nisikilize tu mimi mumeo. Na siku nitakayo kuoa wewe hao wanaokupa maneno ya uongo watabaki midomo wazi na hawataamini maana nitamuoa mwanamke nimpendaye, Erica nakupenda sana, usisikilize maneno ya watu”
“Nimekuelewa Erick”
Kwakweli furaha ya Erica iliweza kurejea tena, hadi muda wanatakiana usiku mwema na Erick alikuwa akitabasamu tu. Baada ya hapo aliona kuwa huo muda atalala kwa furaha sana, akapokea na ujumbe toka kwa Erick,
“Mpenzi wangu Erica, lala ukijua kwamba nakupenda sana. Wewe ni wa thamani sana katika maisha yangu, hakuna kama wewe. Mimi ndio rafiki yako, nieleze kila kinachokutatiza, usisite kuniambia, usiondoe furaha yako sababu ya maneno ya watu. Wewe ndio chaguo langu, nakupenda sana”
Erica alitabasamu na kuibusu simu yake huku akiikumbatia na kulala akimuwaza tu Erick kwenye kichwa chake hadi ndoto yake alitamani itawaliwe na Erick tu.
 
SEHEMU YA 281

Asubuhi na mapema aliamka na kufanya shughuli zake za hapa na pale hata mama yake alimshangaa kuwa ndio huyu jana aliyerudi bila furaha ila leo ni anatabasamu muda wote kumbe alikuwa akifurahishwa na maneno ya Erick tu.
Siku hiyo mchana alifika dada yake Mage, alienda kuongea na mama yao kwahiyo alimuacha dada yake aongee na mama yao kisha yeye alienda chumbani akicheza cheza na mwanae maana alikuwa na furaha sana siku hiyo.
Wakati yupo chumbani Erick alipiga simu na kumwambia Erica,
“Upo na Angel hapo karibu, mpee simu niongee na mwanangu. Mwambie babake anataka kumsalimia”
Erica alitabasamu na kumpa Angel simu ambaye alionekana kuchekelea pia, basi Erick aliongea nae vile vile kitoto maana Angel hakujua maneno yote, bado alikuwa kwenye kujifunza kuongea.
Alipomaliza Erica alichukua simu na kutabasamu kisha Erick akamwambia,
“Siku hizi, kila siku jioni nitakuwa napiga simu umpe mwanangu niongee nae, sawa”
“Sawa nafurahi sana”
“Furaha yako ndio furaha yangu, nawapenda sana familia yangu”
Yani Erick alikata simu ila bado Erica alijawa na tabasamu lisiloisha kwani kuna muda mwingine alijiona ni mwanamke mwenye bahati sana ulimwenguni kwa kumpata Erick anayejua kupenda, kwa wakati huo hakutaka tena kukumbuka swala la kuambiwa kuwa Erick kubembeleza ni kawaida yake, alitaka tu kuamini kuwa Erick anampenda basi na si vinginevyo.
Jioni dada yake aliaga, kisha Erica alienda kuongea na mama yake,
“Dada yako kasema mumewe anataka kuja kulipa faini, nimewakubalia maana hata baba yenu alisema wakijifunza basi atakubali. Nimeshamwambia utaratibu wa kumuelekeza mumewe kwahiyo hivi karibuni watakuja, siku hiyo tutakuwa wote hapa kama familia na tutafurahi pamoja. Nitampigia na kaka yenu simu, aache wazimu wake wa kupenda matatizo”
“Ndiomana alisafiri bila kuaga sababu ya kumkatalia kumuoa Dora eeeh!”
“Yani Yule akili zake loh! Alisafiri bila kusema, eti kafika kule ndio ananiambia mama nilisafiri, ila mimi ni mzazi siwezi kumuwekea kinyongo mtoto. Unajua kumuwekea kinyongo mtoto ni kumfungia milango ya baraka eeeh! Nakufundisha wewe sababu ni mzazi pia, usije ukathubutu kumuwekea kinyongo Angel, mpende, msamehe na umthamini”
“Sawa mama”
Basi akapanga pale na mama yake, na namna jinsi watakavyofanya kuwapokea wageni wa dada yake, ila ilikuwa ni furaha tu maana Erica alijawa na tabasamu.
 
SEHEMU YA 282

Siku iliyofuata wakati anafanya shughuli zake za hapa na pale alipigiwa simu na Yule mama aliyekutana nae dukani, akapokea na kumsalimia kisha Yule mama akamwambia,
“Unaweza kuja ofisini muda huu?”
“Ndio naweza mama”
Basi alivyokata simu, Erica alijiandaa haraka haraka maana hakutaka kuchelewa kwenda ofisini kwa Yule mama ukizingatia anauhitaji mkubwa sana wa kazi, akatoka na kumuaga mama yake,
“Wapi tena Erica?”
“Kule nilipofanya usahili ndio wameniita mama”
“Mungu akutangulie mwanangu”
“Asante mama”
Basi Erica aliondoka pale kwao na moja kwa moja kuelekea kwenye ofisi ya Yule mwanamama.
Alifika pale mapokezi na kama kawaida mtu wa mapokezi alimzuia hadi awasiliane na muhusika, ndipo alipoambiwa kuwa amruhusu aende.
Erica alikuwa na kimuhemuhe haswaaa maana swala la kupata tena kazi kwa urahisi vile lilikuwa ni furaha kwake, akafika na kugonga mlango wa ofisi ambapo Yule mwanamama alimkaribisha.
Aliingia akiwa amejawa na tabasamu na kumsalimia tena Yule mama ambaye alimkaribisha kukaa kwenye kiti cha mbele yake,
“Karibu sana Erica, nakupenda, navutiwa na ucheshi wako”
Erica alikuwa akitabasamu tu na kujibu,
“Asante mama”
“Kwakweli inaonyesha kwenu wana furaha sana kwa uwepo wako, sijui kama huwa unachukia. Nimekupenda toka siku ya kwanza, nilikuomba unichukulie maji dukani, ulinichukulia kwa tabasamu, uliniletea kwa tabasamu. Nilipokutana na wewe tena ulikuwa ukitabasamu hata nikiongea na wewe kwenye simu unatabasamu, leo umekuja umejawa na tabasamu. Nitakuita binti tabasamu”
Erica aliendelea tu kutabasamu na tena amepata na sifa basi ndio tabasamu lilionekana vilivyo hadi Yule mama alifurahi zaidi. Kisha akamwambia,
“Nimekuita leo ili tu nikuone, maana ningeweza kukwambia kwenye simu ila nilitaka tu nikuone tena. Sina haja ya kukufanyia usahili wowote, labda nikuulize swali dogo, ungependa mshahara tukulipe kiasi gani?”
Kwakweli hili lilikuwa swali la mtego sana kwa Erica, na alijikuta akishikwa na uoga kujibu ila alijikaza kujibu,
“Mmmh mshahara, mnilipe tu kiasi kile kitakachoendana na kazi yangu”
“Kama kiasi gani?”
“Kiasi mnachoona kinafaa mimi kupatiwa, kulingana na maisha na kazi ninayofanya”
Huyu mama akacheka kiasi na kusema,
“Umeogopa kusema kiasi eeeh! Ila ungekuwa huru tu, basi usijali utalipwa kulingana na kazi kama ulivyosema. Basi wiki ijayo njoo uanze kazi”
“Wow, asante mama yangu”
“Jisikie vizuri tu, wiki ijayo njoo. Ukifika njoo ofisini kwangu moja kwa moja, nikuonyeshe eneo la kazi”
“Asante sana”
“Usijali”
Kisha Erica aliagana na huyu mama halafu yeye akaondoka kurudi kwao.
Moja kwa moja alienda kwenye stendi ya daladala ili apande basi la kurudi kwao, ila akakutana tena na Yule mdada wa siku ile ambaye alikuwa akimueleza habari za Bahati,
“Mambo Erica! Mzima”
“Mi mzima tu”
“Erica, sikia nikwambie kuhusu Bahati”
“Nilishakwambia kuwa hayo mambo nishaachana nayo”
“Hata kama ila ngoja nikwambie hili, unajua nini Yule Bahati inavyoonyesha si mapenzi yake kumuoa Nasma, inavyoonyesha bahati hata hakumpenda Nasma ila kuna uchawi umetumika”
“Uchawi?”
“Ndio uchawi, yani Yule Bahati wamemfanyia madawa inaonyesha ni ndugu wa Bahati wakishirikiana na baba yake Nasma maana hatukuwahi kumuona Bahati akiwa karibu na Yule binti, halafu Yule baba kwa ushirikina ni noma, anasifika sana kwa ushirikina, yani Bahati ile sio akili yake, ile ni limbwata ndiomana ukimuona Bahati tu utajua maana hana furaha na ndoa yake, kwanza amekonda yani badala ya kupendeza sababu kaoa ila Bahati kaisha na kuchukiza. Ana hela ila kama hana hela yani yupo yupo tu mpaka tunamuonea huruma”
“Asante kwa maelezo yako dada, ila kwasasa inatosha sihitaji tena kujua kilichotokea kwa Bahati”
“Sikia nikwambie, ni wewe tu wa kumsaidia Bahati, wewe ndio unaweza kumtoa Bahati kwenye madawa aliyofungwa”
“Nawezaje sasa?”
“Hapo ndio sawa, sasa mimi huwa nipo maeneo haya ya stendi sababu napika chakula. Siku tupange uje mapema nikuelekeze cha kufanya ili kumkomboa Bahati”
Erica akamuitikia tu huyu mwanamke, kisha huyu mwanamke akamuomba Erica namba ya simu ambapo Erica alimpatia na kuondoka zake akielekea kwao.
Alifika na kumkuta mama yake, ambapo baada ya salamu alimuuliza,
“Eti mama, kuna dawa ya mapenzi?”
“Mapenzi hayana dawa mwanangu, kwanini umeuliza?”
“Si watu husema kuna limbwata, na mtu anafanya maamuzi sababu ya limbwata”
“Ni kweli limbwata lipo ila huchukua muda mfupi tu kuisha na likiisha utaomba ardhi ipasuke, penzi la dawa si penzi zuri, penzi zuri ni lile penzi la dhati. Kuna mtu unataka kumfanyia limbwata?”
“Hapana mama siwezi fanya hivyo, nimesikia tu kwa watu ndiomana nikaamua kuuliza”
Basi Erica aliongea na mama yake pale, kisha kufanya shughuli zake zingine.
 
SEHEMU YA 283

Muda wa kulala ulipofika, Erick alipiga simu na Erica alipokea, muda huo mtoto Angel alikuwa macho maana siku hiyo alichelewa kulala, na Erick aliposikia mtoto anaongea ongea akamwambia Erica,
“Mpe simu mwanangu nimsalimie”
Lile neno lilikuwa linamfurahisha sana Erica, akampa simu Angel na Angel nae alikuwa na tabasamu tu maana kila aliposikia sauti ya Erick mtoto alionekana na furaha sana.
Kisha Erica akachukua simu,
“Huwa unaongea vinini na mtoto mbona huwa anacheka muda wote!”
“Jamani huwa namwambia mwanangu jinsi ninavyompenda na kumjali, vipi bima ya afya ya mtoto ushachukua?”
“Bado”
“Kwanini bado wakati waliniambia ni tayari?”
“Sijui ila nilienda wakaniambia bado”
“Au ndio ulienda siku ile uliyoanza kuniuliza yale maswali na kuweka mashaka kwa upendo wangu kwako? Erica, jiamini mama nakupenda sana. Uwe unaniambia kama kuna yeyote kakutenda chochote nitashughulika nae, narudia usisikilize maneno ya watu. Nisikilize mimi tu, nenda kesho ukachukue kadi ya mtoto”
“Sawa”
Erica alikubaliana nae, hata hivyo akakumbuka kuwa siku ile Sia alimwambia aende kesho kutwa ambayo ndio itakuwa kesho, kwahiyo alimuitikia tu Erick na kulala huku akitabasamu kama kawaida.
Palipokucha, alijiandaa kama kawaida na kumuaga mama yake, ila leo mama yake hakumuuliza kuwa anaenda wapi na ile ikawa faraja kwake maana hakujua hata siku hiyo angemwambia uongo gani.
Aliondoka kwao akielekea kwenye ile ofisi ya wakina Erick.

Alifika ofisini ila kabla hajaingia alikutana na Sia mlangoni ambaye alimsalimia kisha akamwambia,
“Kheee una kumbukumbu wewe, yani mi nilishasahau ila subiri hapo nje nikuletee”
Basi Erica alisubiria, baada ya muda mfupi Sia alirudi na kadi ya mtoto ila sura yake haikuwa ya furaha kama mwanzo, kisha akamwambia,
“Tuseme Erica umezaa na Erick? Yani umekuwa na mahusiano nae hadi umezaa nae?”
Erica aliitikia kwa kichwa akimaanisha kuwa amezaa nae, kwakweli Sia hakupendezewa kabisa, alimpa Erica ile kadi huku akilalamika,
“Yani Erick kanitoa mimba ngapi? Na sio mimi tu, ni wasichana wengi kawatoa mimba maana ana daktari wake kwaajili ya hiyo kazi, halafu leo hii kaenda kuzaa na wewe aliyekujua juzi? Aaah hii sio sawa kabisa, Erick sio binadamu, hii sio sawa naumia sana, nadhani unaweza kuelewa jinsi gani naumia. Napenda kukwambia, kuzaa kwako na Erick sio kusema umempata Erick moja kwa moja, ngoja nikukumbushe tu kwamba mimi binafsi siwezi kumuacha Erick, nampenda sana”
Erica aliweka ile kadi kwenye mkoba na aliamua kuondoka tu kwani alijua kukaa pale zaidi ni kuzua mengine, aliondoka na kuelekea kwao.
Kufika kwao kama kawaida, mtoto wake alichukua mkoba na kufungua akabwaga vitu vyote chini, bibi yake alikuwa akicheka tu kama kawaida ila wakati Erica kainama aokote vitu vyake, mama yake aliiona ile kadi ya bima ya afya na kuichukua, akaisoma na kushangaa kisha akamuukliza Erica,
“Wewe si ulisema Angel baba yake ni Rahim! Mbona huku inasomeka Angel Erick?”
 
SEHEMU YA 284

Erica aliweka ile kadi kwenye mkoba na aliamua kuondoka tu kwani alijua kukaa pale zaidi ni kuzua mengine, aliondoka na kuelekea kwao.
Kufika kwao kama kawaida, mtoto wake alichukua mkoba na kufungua akabwaga vitu vyote chini, bibi yake alikuwa akicheka tu kama kawaida ila wakati Erica kainama aokote vitu vyake, mama yake aliiona ile kadi ya bima ya afya na kuichukua, akaisoma na kushangaa kisha akamuukliza Erica,
“Wewe si ulisema Angel baba yake ni Rahim! Mbona huku inasomeka Angel Erick?”
Erica alikaa kimya kwanza kwani hakujipanga kumjibu mama yake kwa wakati huo, mama yake akamuhoji tena kwa ukali,
“Wewe Erica, hebu nijibu hii ina maana gani? Ungeandika jina la marehemu baba yako nisingeshangaa ila umeandika jina la mtu mwingine, hebu nieleze nikuelewe”
“Nisamehe mama”
“Yani wewe Erica ni mwepesi sana wa kuomba msamaha, unajua fika jambo unalofanya si sahihi ila unajua silaha pekee unayotembea nayo ni kuomba msamaha. Sasa siwezi kukusamehe mpaka unipe ukweli wa hili jambo, imekuwaje huyu badala ya kuwa Angel Rahim amekuwa Angel Erick?”
“Kwahiyo mama ningemuandikisha Angel Rahim?”
“Hebu niondolee ujinga wako hapa, huyo Rahim si amegoma kuja hapa nyumbani. Sijakutuma kwenda kumuandikisha jina lolote mtoto, nilikwambia nitamtambua huyo Rahim endapo atafika hapa nyumbani na si vinginevyo, ila nieleze kwanza hii ya Erick imetoka wapi?”
Erica alikaa kimya na kufanya mama yake aongee zaidi,
“Unajua wewe Erica muda mwingine huwa najiuliza kuwa akili zako hizo umezitoa wapi maana huwa unazijua mwenyewe tu. Unafanya kitu unachotaka wewe, nilikwambia kuwa kitu chochote kabla hakijatokea nishirikishe, ila umeamua kwenda kubadilisha jina la mtoto hata bila ya kunishirikisha mama yako. Haya niambie ukweli huyu Erick ni nani na kwanini mtoto aitwe Angel Erick?”
Erica alijifikiria na kutambua kuwa ingawa atapewa lawama na mama yake ila ni lazima amwambie ukweli, aliamua kujitoa muhanga kwa muda huo kuwa liwalo na liwe.
“Mama, ni kweli Angel baba yake ni Rahim na wala sikuongopa kusema baba wa Angel ni Rahim ila kama unavyojua mama huyo Rahim hanijali, wala hajaonyesha uwepo wake toka nina mimba hadi mtoto kakua sasa sijaona tumaini lake lolote ndio kwanza hata kuongea na mimi siku hizi hataki. Kuhusu Erick sasa, ni kijana anayedai ananipenda sana na kaahidi kuja kunioa, aliposikia nina mtoto akamkubali kuwa mwanae pia na kasema atamtunza ndio akaniambia nikamuandikishe mtoto majina yake.”
“Kwanini hukunishirikisha?”
“Nisamehe kwa hilo mama”
“Unajua kama umemuuza mtoto wewe kwa mambo yako ya kijinga, una uhakika gani kuwa huyo Erick atakuoa? Una uhakika gani? Wangapi wamekudanganya? Una uhakika gani anakupenda? Mpaka leo unashindwa kujua uongo wa wanaume Erica? Yani wanaume walivyo halafu kirahisi rahisi tu akubali mtoto, akwambie mbadilishe na jina labda kama kuna kitu cha ziada anachotaka kutoka kwako ila sio mapenzi tu nakataa”
“Nisamehe mama, sasa nitafanyaje?”
“Usiniulize mimi utafanyaje mjinga wewe ila muulize huyo mwanaume uliyemuuzia mtoto kuwa utafanyaje? Mwambie mama yangu kaona kadi ya mtoto kwahiyo itakuwaje? Erica, huwa sipendi ujinga yani sipendi ujinga kabisa ndiomana hukunishirikisha huu ujunga wako maana ulijua wazi ningeukataa na kweli nisingeweza kukubali, ushauza mjukuu wangu sasa mwambie huyo shababi wako aje nyumbani hapa afanye harakati za harusi sio kujimilikisha mtoto wakati hana kitu, shamba walime wengine mazao avune yeye, huo ujinga sitaki kabisa kuusikia.”
“Sawa mama”
“Niitikie tu na ujinga wako huo, kuna muda huwa unaniudhi hadi sijui natamani nini, yani Erica wewe dah!”
Erica aliendelea kumuomba msamaha mama yake kisha kwenda chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 285

Jioni kama ambavyo Erick aliahidi kuwa atakuwa akipiga simu kila jioni aongee na Angel ndivyo alivyofanya na kwa jioni hiyo.
Alipoongea tu na Angel, Erica alishika simu na kuanza kuongea nae,
“Erick, leo nilenda ofisini kuchukua kadi ya mtoto”
“Aaah umefanya vizuri, tena nilitaka nikuulize kuwa hujachukua tu!”
“Ila sio hiko kilichofanya nikwambie kuwa nimeenda, kuna lingine”
“Lipi tena hilo Erica?”
“Kwanza napenda utambue kuwa na mimi ni binadamu nina moyo, nina wivu na kila kitu kwahiyo naumia sana. Ni kweli umesema nisisikilize ya watu ila kuna vitu vinaniumiza sana, Erick nasikia wewe hakuna mwanamke ambaye atakupitia usimuache? Kweli hiyo ndio sifa bora ya mwanaume?”
“Erica, sijakuficha kitu chochote, nilikueleza kila kitu kuwa utasikia mengi kuhusu mimi sijui Erick malaya na mengine kibao ila yote haya ni sababu sikuwa na penzi la dhati. Nilihitaji penzi la dhati, nilihitaji kumpata Yule ninayempenda ambaye ni wewe, kote huku nilikuwa nazunguka kuwa pengine nitapata pumziko la moyo, ila pumziko la moyo wangu lipo kwako Erica. Sikupenda kuwa muhuni, sikupenda kuwa na wasichana wengi ila sababu nilikuwa na stress za mapenzi huku nikiwaza kuwa nitapata pumziko la moyo. Erica ni wewe ndiye nikupendaye, wewe ni mwanamke wa maisha yangu”
“Swala la kunipenda mimi sio mwisho, ila swala ni kuwa hawa wanawake zako utaachana nao lini?”
“Erica, kitendo cha kusema nimekubali kuwa mtoto wako awe mtoto wangu ujue kwamba hao wanawake wote hawana nafasi kwangu. Ni wanawake wangapi wazuri nimekutana nao? Ni wanawake wangapi wenye watoto nimekutana nao? Ni wangapi hawana watoto ila bado moyo wangu upo kwako. Hao wote hawana nafasi kwangu, wewe ndio maisha yangu, nielewe Erica, hivi naanzaje kusema mwanao umuandikishe majina yangu wakati sikutaki? Kumbuka leo na kesho, Angel ana haki kwenye mali zangu maana nimemuhesabia kama mwanangu, na katika vitu vyangu nimeanza kuweka uwepo wake, kwa mfano ningekuwa sikuhitaji hivi nijitoe kwaajili ya mtoto kwa lipi? Erica elewa nakupenda, na nampenda Angel kama mwanangu, kuanzia siku niliyokwambia umuweke Angel jina langu, kwenye moyo wangu kulishabadilika kuwa na mimi ni baba kwasasa, nina mtoto anaitwa Angel. Kitu gani kingine kinakusumbua mama?”
“Kitu kingine, mama yangu ameoana kadi ya mtoto na amesema kama wewe ndio baba wa mtoto basi uje nyumbani ujitambulishe na unioe”
“Wow, hilo ni swala jema sana kwenye masikio yangu, Erica usiwe na mashaka na mimi, maana mimi ndio mume wako. Unatakiwa kuniamini mimi, kuna mambo nayaweka sawa na nitakaporudi utanitambulisha kwa familia yako name nitakutambulisha kwa familia yangu, kisha tutaoana yani hakuna tatizo juu ya hilo kabisa. Mwambie bimkubwa aondoe mashaka, mimi nakupenda nay eye ni kama mama yangu vilevile nampenda”
Maneno ya Erick yalimpa faraja Erica na kujikuta akifurahi na kusahau yote aliyoulizwa na mama yake, kisha akaagana na Erick.

Kesho yake mapema kabisa, alipigiwa simu na Dora, kisha Erica alipokea na kumsikiliza,
“Erica, kumbe ulisimamishwa kazi pale kwa shemeji yako!”
“Ndio, nani kakwambia?”
“Dunia haina siri Erica, nasikia ulifumaniwa unafanya mapenzi ofisini na mfanyakazi mmoja. Kweli Erica ndio unajifanya mtakatifu wakati unafanya mapenzi hadi ofisini!”
“Wewe Dora wewe, umetoa wapi hizo habari jamani? Mambo ya uongo kama hayo huwa mnaenda kuyatunga wapi nyie watu?”
“Erica, mimi siijui ofisi yenu na wala siwajui watu wa pale ofisini ila kuna mtu kaniambia tu kuwa wewe na huyo kaka mmesimamishwa kazi maana mlikutwa mnafanya mapenzi ofisini”
“Basi makubwa”
“Sijakwambia kwa ubaya ila nimekwambia kwa wema tu, Erica unakataa kuwa na watu wenye pesa zao uwe tajiri ila unaenda kuharibu maisha yako na msaka tonge kama wewe. Kweli kabisa hukuona guest au, kwenda kufanya mapenzi ofisini? Tamaa gani hiyo?”
“Inatosha Dora, kwaheri”
Kisha Erica akakata simu maana alihisi inampa tu hasira, alijiuliza sana kuwa ni nani kamuenezea taarifa hiyo ya kufanya mapenzi ofisini, katika mambo yote aliyowahi kuyafanya hajawahi kufikiria kufanya mapenzi ofisini kwahiyo swala la kusambaziwa habari hiyo lilimchanganya kiasi, ila badae alifikiria akaona pengine Dora anatafuta namna ya kuwa nae karibu kwa kutunga habari za uongo maana hakufikiria kwa ofisi ile ya shemeji yake kama kuna mtu wa kusambaza habari za namna ile, kwahiyo aliachana na mambo ya kuambiwa na Dora.
Aliendelea na kazi zake tu, mchana wa siku hiyo mama yake alimuita na kuanza kuongea nae,
“Kuna habari nimepata Erica, kwakweli kama mama yako zimenishtua sana na sitaki ziwe za kweli. Niliahidi kukuamini basi naomba nikuamini kuhusu hili na uniambie ukweli”
“Kitu gani hiko mama?”
“Bite kanipigia simu, amesema mume wake alikuwa akimficha siku zote kisa cha kukusimamisha wewe kazi, ila jana baada ya kumbana bana kaamua kusema ukweli. Hivi kweli kabisa Erica unaweza kufanya hivyo?”
“kufanya nini mama?”
“Nasikia shemeji yako alikufuma kumbe, alikufuma wewe na mfanyakazi mwingine mkifanya mapenzi ofisini, kwakweli sitaki kuamini Erica unanifanyia vitu vya aina hii, unataka niweke wapi sura mama yako?”
Erica alifikiria na kuweza kuoanisha maneno aliyoambiwa na Dora pia, kiukweli ilimchukiza sana ila ilibidi aongee kwa busara na mama yake,
“Mama, napenda nikwambie mimi mwanao siwezi kufanya kitu kama hiko. Sijafikia hatua hiyo maana si kukudhalilisha wewe bali nitakuwa najidhalilisha na mimi pia, ila najiuliza sana hivi huyu James ananitakia nini mimi? Au kwavile ananisingizia vitu na mimi nanyamaza kimya? Huyu mtu nadhani anaelekea pabaya na hashindwi kuniharibia mambo yangu mengi maana ameamua, na mimi nitafanya jambo”
“Unataka kufanya nini Erica? Usiniletee ujinga, Yule ni shemeji yako, unapaswa umuheshimu”
“Hata mimi nahitaji heshima mama, kwanini kila siku anisingizie maneno mabaya? Kwanini anifanyie hivi? Kwakweli sipendi yani sipendi kabisa”
“Hata kama hupendi, mshtakie Mungu tu, ila kama hayo mambo hutendi nashukuru sana. Usitake kuweka ligi na shemeji yako, umenisikia?”
“Sawa mama”
Erica alirudi chumbani kwake huku akifikiria mambo mengi sana,
“Huyu shemeji anataka kunipanda kichwani, ushemeji gani huu kunidhalilisha kila siku maana kila inayoitwa leo ananidhalilisha sasa na mimi nitamdhalilisha tu na atakoma na tabia yake hiyo, kwakweli na mimi nina moyo kama wengine siwezi kukubali kudhalilishwa na uonevu huu siutaki kwakweli”
Akawa anawaza cha kumfanya shemeji yake adhalilike.
 
SEHEMU YA 286


Ulipofika usiku mama yake alimwambia tena,
“Erica usisahau ni Jumamosi hii ndio dada yako Mage na mumewe wanakuja kulipa faini na kukamilisha mambo mengine kwahiyo familia yote itakuwepo. Nishamwambia Tony atakuja Ijumaa yani sijui mambo ya kupika itakuwaje? Maana siku zishaenda, unajua leo ni Alhamisi eeeh! Kwahiyo kesho ni Ijumaa kaka yako atakuja, halafu kesho kutwa Jumamosi yani hata sijui mambo ya chakula nifanyeje?”
“Kwani umealika watu gani mama?”
“Mmmh siwezi kualika watu wengi mwanangu, ni mimi, Mage na mumewe na ndugu wa mumewe watatu kisha watoto wa Mage wote. Bite na mume wake, na Yule mdogo wangu ambaye hajagi kunisalimia ila Jumamosi atakuja, na Yule shangazi yenu maana hao niliwaeleza yote wanajua”
“Aaaah sawa, wajomba je?”
“Tena ukae kimya, niite wajomba zako nizue mapya hapa eeeh! Niliyonayo yananitosha, ukibahatika kuolewa basi wajomba zako watakuja kwenye harusi yako, kwanza hii ni upatanisho tu kwahiyo sio swala la kutaka watu wengi, hao hao wanatosha”
“Sawa mama”
“Sasa nawaza kuhusu chakula”
“Usijali mama, tutapika tu mbona watu sio wengi hao, kwa haraka haraka watu hao hawazidi ishirini, mbona chakula kinapikika tu”
“Utapika wewe eeeh!”
“Hahahah usijali mama”
Basi Erica alitabasamu tu na mama yake ila kichwa chake kilikuwa na mipango mingi sana.
Akaingia chumbani kwake kwa lengo la kulala ila akajiwa na wazo na kuona kuwa asilale bila kufanyia kazi wazo lake, akachukua simu yake na kumpigia shemeji yake James,
“Hallow shemeji nina mazungumzo na wewe ila napenda dada asisikie, sijui upo nyumbani?”
“Ndio nipo nyumbani ila dada yako kalala, ngoja nitoke chumbani nikupigie tuongee vizuri”
Kisha akakata ile simu, Erica akajiandaa maneno ya kuongea na shemeji yake, kisha shemeji yake akampigia simu na Erica akapokea,
“Habari James”
“Wow umeniita James muda huu Erica, nimefurahi sana. Sipendi unavyoniita shemeji”
“Huwa nakuita hivyo ili dada asisikie. Ila kuna jambo nataka kuongea na wewe”
“Jambo gani hilo Erica kipenzi changu?”
“James unanionea sana, unanisingizia vitu vingi sana ambavyo hata sijafikiria kufanya, kweli mimi wa kusema umekuta nafanya mapenzi ofisini jamani! Mbona unataka kunichafulia jina? Lini utaacha kunichafulia jina kama hivi jamani, au unataka nifanye nini?”
“Mbona kitu kidogo erica, nataka kufanya mapenzi na wewe, hivyo tu basi. Nipe tunda uone kama nitakuchafulia jina tena”
“Lakini mimi si mdogo wa mkeo jamani! Mimi ni shemeji yako”
“Ya shemeji ndio tamu, hujui hilo Erica? Kila siku nakuimbia wimbo mmoja kuwa nakupenda sana Erica, yani upendo ninaokupenda wewe hata dada yako hafikii, yani Erica nipe tunda tu nitatulia na hutosikia tena nikikuchafulia popote pale”
“Sawa, nipo tayari kukupa hilo tunda”
“Erica unasema kweli? Hata siamini, kweli Erica?”
“Ndio kweli nipo tayari ila kuna jambo nataka unifanyie kwanza”
“Jambo gani?”
“Jumamosi kuna wageni nyumbani, nimepewa kazi ya kupika na mama ila naona uvivu kwakweli halafu hiyo Jumamosi ndio nitakupa tunda kwahiyo nikipika nitachoka sana. Kwahiyo naomba uandae watu wapike na watuletee chakula tu nyumbani”
“Erica, hilo ni swala rahisi sana kwangu, sema lingine. Walete chakula cha watu wangapi, na vinywaji je? Yani mwambie mama asiwe na wasiwasi kwa swala la chakula na vinywaji, sitaki uchoke kabisa mrembo wangu”
“Sawa, chakula cha watu ishirini. Halfu ombi lingine, nilikuwa naomba uniletee funguo za gari ya dada unajua alininyang’anya eeeh! Wakati ulinipa mwenyewe, tena ukiniletea nikabidhi mbele yake kuwa umejisikia kunipa tu gari maana dada nahisi ameanza kunionea wivu”
“Erica, hilo ni swala dogo sana kwangu, hata gari mpya ungetaka ningekununulia. Niambie kingine unachotaka”
“Nataka uniletee na pesa, unajua pesa hujanipa siku nyingi sana. Nilikuwa sikuombi unanipa mwenyewe ila leo nimekuomba niletee, laki tano uniwekee vizuri kwenye bahasha”
“Erica unanisisimua sana, malizia kingine unachotaka mama”
“Halafu tunda unajua nitakupea wapi?”
“Eeeeh wapi?”
“Sijui, panga wewe”
“Hotelini”
“Tatizo nyumbani nitaaga vipi?”
“Sikia Erica, mimi nitamwambia Bite kuwa nahitaji kwenda na wewe mahali tukachukue mzigo kisha tutaenda zetu hotelini kujilia raha”
“Sasa nyumbani tutawaonyesha mzigo gani tukirudi?”
“Vya kuchukua vipo vingi Erica? Yani wewe niachie mimi, dah natamani hata hiyo Jumamosi ingekuwa kesho, nina hamu na wewe dah!”
“Usijali James umenipata”
“Nakupenda Erica”
Basi Erica akakata ile simu na kufurahi na roho yake pia akafurahi alivyoweza kujikaza kuongea na James maana alichoshwa kutungiwa habari za uongo na kutokusikilizwa kila anapoeleza kuwa anasingiziwa.
Baada ya hapo ndio akaamua kulala sasa maana moyo wake ulikuwa na furaha.
 
SEHEMU YA 287


Kesho yake aliamka na kufanya kazi zake kama kawaida, kisha akamfata mama yake na kumwambia,
“Mama tusihangaike tena kuhusu chakula cha wageni maana shemeji James amesema kuna wapishi wa hotelini wataleta chakula na vinywaji”
“Jamani James, ana moyo wa upendo huyu kijana jamani dah! Mungu amzidishie, si unaona shemeji yako alivyo halafu wewe ulitaka kumuwashia moto jana, kama anakusingizia si yeye mwache akusingizie cha msingi na muhimu anafanya vitu vinavyofaa kwenye familia yetu”
“Sawa mama”
Basi Erica akafanya mambo yake ya siku hiyo hadi kaka yake alipokuja na kumpokea huku wakijiandaa kuhusu kesho kwaajili ya wageni na kufurahi nyumbani
Jioni Tony alimuita mdogo wake ili kuongea nae kidogo,
“Erica, bado una chuki na Dora mdogo wangu jamani?”
“Kaka huyo msichana hafai, unajua hafai yani hafai kabisa. Najua mapenzi hayaingiliwi ila huyo msichana hafai, kama huamini subiri”
Erica alimpigia Dora simu na kuweka sauti kubwa kisha akaanza kuongea nae kiurafiki ili kaka yake aweze kusikia kuwa Dora ni mtu wa aina gani,
“Unajua Dora sina ugomvi na wewe ila swala la kutaka mimi nilale na Yule babu uliyelala nae ndio silipendi”
“Erica kwani tatizo liko wapi? Kwani ukilala na Yule babu anaondoka nayo? Mbona mimi nimelala nae na nipo vilevile? Tena kwa taarifa yako hata jana nimtafuta hadi nimelala nae tena”
“Mmmh Dora jamani, hujionei huruma ujue yani ulibakwa nab ado umemtafuta huyo babu mara mbili kulala nae, akikufanyia kitendo kibovu je?”
“Nikifanyiwa kitendo kibaya na huyu babu haitaniuma sababu mzee ana pesa, sio Yule shemeji yako kanibaka, kaniingilia kimwili hata hela hajanipa nab ado kesi karuka yani Yule shemeji yako amenikera sana. Ila Erica subiri uone mchezo Yule shemeji yako si anajifanya mjanja, nitampata tu mimi na atakaa kwenye kumi na nane zangu na atajuta”
“Unampango wa kufanya nae nini?”
“Subiri Erica, nitakwambia tu. Kanidhalilisha sana, kwani angeniomba kistaarabu ningemnyima? Nisingemnyima nap engine hata ningekuwa nyumba ndogo yake”
“Mmmh Dora, inamaana kaka yangu humtaki tena?”
“Atafute hela kwanza, kipindi kile nilimtaka sababu nilitaka ndoa ila nyie mlivyozingua nikaona bora niwe vilevile kama zamani tu”
Tony akamuomba Erica akate ile simu, ilibidi Erica akate simu kwakweli ilionyesha kumchanganya sana Tony kiasi kwamba hakuongea kitu ila aliamua kwenda kulala tu. Ila kwa upande wa Erica alishukuru kufunguka kwa Dora kwani kumesaidia kaka yake kujua ni mwanamke wa aina gani alikuwa akimng’ang’ania.
Kisha baada ya kukata tu akapigiwa simu na Erick kuwa aongee na Angel kiasi kwamba Angel alizoea kuongea na Erick na alikuwa akifurahi sana anapoongea nae.
Mama yake Erica hakujua kuwa Erica anawaza nini sana ila kumbe Erica bado alikuwa anawaza swala la kumdhalilisha shemeji yake kama ambavyo humdhalilisha yeye kwa kusema maneno ya uongo.
Muda wa kulala ulifika na walienda kulala huku Erica akiwa bado na mawazo ya mambo ya kesho yatakavyokuwa.
 
SEHEMU YA 288


Jumamosi ilifika na Erica aliamka mapema kabisa kufanya usafi na kila kitu, kisha wageni wao kuanza kufika ambapo katika wageni wa shemeji yake wa dada yake Mage yani wale watatu alishangaa kuona mmoja wapo ni mfanyakazi wa James, akamsalimia alikuwa ni mdada na aliitwa Linda.
Baada ya kukaribisha wageni sebleni, Erica alitoka kidogo nje na Yule Linda ili ajaribu kuulizia kuhusu habari juu yake.
“Samahani Linda, samahani kwa kukuuliza hili. Eti kuna habari gani ofisini imeenea kuhusu mimi? Sikujua kama una undugu na shemeji yangu kwa dada Mage, karibu sana, ila naomba niambie ukweli kuhusu hili. Yani kipi kinasikika kuhusu mimi kusimamishwa kazi?”
“samahani Erica, najua mimi na wewe hatujazoeana ila kuna habari pale ofisini hadi kila mtu ameshangaa kuwa wewe umefanya vile ilihali hunaga hata mazoea na mtu”
“Ni habari gani?”
“Tumesikia kuwa, wewe na mlinzi mlifumwa ofisini mkifanya mapenzi. Mmmh kila mtu ameshtuka, ila samahani kukwambia hivi”
“Aaah usijali”
Kisha wakarudi ndani na harakati zingine zikaendelea, ambapo Bite alifika na mumewe na walikuwa na furaha pia wakajumuika na wale wengine huku mambo ya kulipa faini yakiendelea na kila kitu kisha wakaja wale wa chakula na vinywaji, kwakweli watu walikula na kunywa na kusifia sana kwani ilikuwa ni furaha haswaa. Kisha wale wa vyakula na vinywaji wakaondoka na kuacha pale vinywaji na nyama ambazo nazo zilikuwa kwenye bajeti ya kile chakula, kwahiyo waliondoka na vyombo vyao tu maana shughuli zao ziliisha.
Walipomaliza James alimuita Erica na Bite na kumkabidhi Erica funguo za gari huku akisema kuwa ameona vyema Erica kumiliki lile gari, Bite hakupinga hata kidogo maana Yule ni mdogo wake.
Ila Erica akasema na mama yake aitwe ili naye aone mwanae akikabidhiwa hizo funguo, kwahiyo mama yao aliitwa na hakupinga pia kwani kwa siku hiyo alikuwa na furaha sana.
Wakarudi ndani huku wakiendelea kunywa na kula nyama, James alikuwa akimtumia ujumbe Erica kuwa wanachelewa kufanya mambo yao ila Erica akamwambia kuwa wasubiri subiri watu wapungue pungue kwakweli ilikuwa ngumu sana kwa James kwani alikuwa na uchu uliopitiliza, ikabidi amwambie mkewe kuwa kuna mzigo inabidi akachukue na Erica, mama yao alisikia na kuuliza,
“Kwanini asiende na Tony?”
James akasema,
“Hapana mama, inabidi nikachukue na Erica”
Erica alikubali, kisha akainama kama kumnong’oneza James ambapo James kuna bahasha aliitoa mfukoni kwake na kumkabidhi Erica, halafu Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake aliporudi aliwaomba watoto wote watoke nje maana kuna jambo la muhimu anataka kuongea na wakubwa mule ndani, kwahiyo watoto wote walitoka nje.
Erica aliwaomba wale wakubwa watulie na wamsikilize, kisha akasogea kwenye redio yao na kuunganisha simu yake na redio halafu akaanza kusikilizisha sauti ambapo ilikuwa ni sauti yake na ya James, kumbe maongezi ya siku ile yote Erica aliyarekodi kwenye simu yake.
Kwakweli Bite alihisi kama kuzimia kwa yale maongezi.
 
SEHEMU YA 289


Kila mmoja ndani alibaki mdomo wazi, huku James akiinamisha kichwa chini maana alikuwa kadhalilishwa haswaa, akataka kuinuka ili aondoke ila Erica akamshika mkono na kusema,
“Sasa leo, sema ule uongo wako unaotungaga kwaajili yangu kwenye familia yangu. Waambie yale yote unayosemaga kuhusu mimi, sijui niliwahi kukutaka sijui nilikutega yani hakuna cha kukwepa”
James hakujiandaa kwa chochote kwa muda huo kwahiyo hakuweza kujibu chochote alishangaa sana kuwa Erica katoa wapi ujasiri wa kufanya vitu vya namna hiyo maana hakumfikiria kama kuna siku angeweza kumdhalilisha namna hiyo. Kisha Erica akaendelea kuongea,
“Sikuwa na haja na funguo za gari na wala sikuwa na haja na pesa ila nimetaka yote haya ili wajue kuwa wewe una jambo lako kwangu ndiomana huishi kunisingizia mambo mbalimbali”
Wakati Erica anataka kuongea, mama yake akainuka na kumvutia Erica chumbani maana hali ya mwanae Bite ilikuwa inabadilika kila muda toka asikilize yale mazungumzo, kwa wakati huo ni Mage ndio alikaa karibu na Bite huku James akiondoka kwa aibu.
Erica alipelekwa na mama yake chumbani, akaanza kuongea nae,
“Mwanangu, yameisha. Mbona kumdhalilisha hivyo shemeji yako?”
“Mama, hata mimi kazoea kunidhalilisha kila siku kunizulia mapya kwanini? Leo zamu yake, tena nimemuhurumia nilitaka nimdhalilishie chumbani kabisa mmuone ujinga wake, ila nimemuheshimu sana kuwasikilizisha redio tu, aache ujinga wake”
Kisha mama yao alitoka tena na kumchukua Bite kwenda nae chumbani maana Bite alionekana kukosa raha na kutokujitambua kabisa, alipoingizwa chumbani tu alijikuta akianza kulia na alilia kama amefiwa kwahiyo mama yake ndio akafanya kazi ya kumbembeleza.
Kwakweli ilikuwa ni aibu sana ambayo imefanywa na Erica, hakuna aliyefikiria kama Erica angeweza kufanya kitu cha fedheha kiasi hiko tena kwa wageni.

Ilibidi mama Erica aende kusema shughuli imeisha ili kila mmoja aondoke,
“Haya ni mambo ya kifamilia kwahiyo msijali tutayasuluhisha kama familia”
Kwahiyo ilibidi waondoke na wawache pale kama familia tu ambapo hata mume wa Mage ilibidi amuache Mage tu kisha yeye kuondoka na watoto zao.
Kwakweli mama yake Erica aliona aibu sana kwa siku hiyo, wageni walipoondoka walimuita Erica sebleni na kuanza kuongea nae kwa karibu maana Bite alikuwa kachanganyikiwa kabisa huku akibembelezwa tu na mama yao.
Alianza mama yao kumsema Erica,
“Unajua Erica ulichofanya si kitendo cha kiungwana, hata kama shemeji yako mbaya ila sio kumdhalilisha hivi mbele za watu kweli mwanangu!”
“Mama, na mimi ni binadamu unafikiri siku ile umenipiga bila kosa nilifurahi? Nikaacha yapite, khee mtu hakomi anakuja kunizushia na mengine, mtu huyu nimeona sio wa kumchekea maana hashindwi kuharibu hata siku nataka kuolewa, bora ijulikane moja tu. Yeye si alimwaga mboga, basi mimi nimemwaga ugali”
“Sasa hali ya dada yako Bite umeiona?”
“Nimeiona mama, ila Dada Bite anatakiwa kujua anaishi na mtu wa aina gani, tulimfuma siku ile na msichana wa kazi nikamwambia dada kila kitu kuwa shemeji alitaka kunibaka ila dada akaenda kulishwa sumu na shemeji kanichukia hadi mimi, kwakweli kleo sijakubali kabisa. Tena ngoja niwamalizie lingine, Yule Dora alibakwa na James na tena alimuingilia kinyume na maumbile, huyo ndio mume anayeishi na dada”
Walishika vichwa maana hata mama yake aliyembishia siku ile lakini kwa mambo ya siku hiyo hakuwa na jinsi zaidi ya kushangaa na tena kusikia alimuingilia kinyume na maumbile ndio akashangaa zaidi, Mage alisema,
“Kwakweli huyu James hafai, mama hakuna sababu ya kumlaumu Erica tena kafanya vizuri sana maana hata mimi Bite alinipigia simu kuwa Erica kakutwa akifanya mapenzi ofisini, nikasikitika sana na kujiuliza kuwa mdogo wetu kawaje kumbe ni James ndio anamuenezea Erica sifa mbaya, na amemuonea sana sababu Erica nae alikuwa msiri mno kwahiyo James hakufikiria kama ujinga wake tungeujua na uthibitisho kabisa.”
Cha kushangaza wakati wote wanaongea maneno tofauti tofauti, Tony alianza kucheka ikabidi mama yao amuulize,
“Sasa na wewe Tony unacheka nini? Kuna kinachochekesha hapa?”
“Hapana mama, ila nimecheka kwasababu zangu. Kwanza kuanzia leo Erica nitamuita foma kiboko ya uchafu, jamani Erica eeeh mdogo wangu sikutegemea, umemaliza kuniumiza moyo jana, halafu leo umehamia kwa Bite. Natumai mage mumeo yupo vizuri maana kama mchafu wa tabia mtahadhalishe kabisa maana Erica atamsafisha”
“Kwahiyo wewe umefurahi kwa shemeji yako kudhalilishwa na Erica?”
“Mama, Yule hajadhalilishwa wala nini ila tabia yake imejulikana. Ila mdogo wangu Erica nakupongeza sana, jamaa kakupa gari kwa hiyari yake, kakupa laki tano keshi, na leo katulisha tumekula hadi kujimwagia na bado kaumbuliwa. Khaaa niacheni nicheke kabisa, kweli mwanamke hatabiriki, kumbe ulikuwa unamrekosi kaka wa watu Erica jamani! Ngoja nikanyooshe miguu kidogo”
Akainuka na kutoka kwahiyo pale alimuacha mama yao, Erica, Bite na Mage. Na muda kidogo Erica nae akaenda chumbani kwake ambapo mwanae alikuwa amelala tayari kwahiyo alimuacha pale mama yake amalizane na watoto wake.
 
SEHEMU YA 290


Kwa muda huo Erica hakutaka kujiona kama amekosea maana shemeji yake ameshamdhalilisha sana, kwahiyo aliona kafanya sawa kabisa, akachukua simu yake akakuta Erick kashampigia kama mara tatu hivi, na kukumbuka ile ahadi yake ya jioni kutaka kuongea na Angel, ikabidi ampigie simu mwenyewe kwani kwa bahati nzuri alikuwa na salio.
Aliongea nae na kumwambia kuwa Jumatatu anaanza kazi kwahiyo simu awe anampigia usiku kuanzia saa moja,
“Jamani Erica, utakuwa unanikatili mno”
“Sasa nitafanyeje Erick na ndio kazi za watu. Uwe unanitumia meseji kwa sana”
“Utajibu meseji zangu”
“Nitajitahidi niwe najibu”
Kisha Erick aliendelea kumsisitiza Erica kuwa atarudi tu na kufika kwao kujitambulisha, kisha akaagana nae ili alale. Lla alivyokata simu tu akapokea ujumbe toka kwa Rahim na kushangaa sana kuwa bado Rahim anamkumbuka,
“Erica, ingia facebook nina shida na wewe, ni muhimu sana”
Kwakweli Erica hakutaka kuchanganya akili yake kabisa, zaidi zaidi akaweka ile simu pembeni na kujilaza tu kwani hakutaka hata kujua kuwa Rahim anataka amuandikie ujumbe gani, kwa kifupi alishatumbukiwa nyongo na majibu ya Rahim kiasi kwamba hakutaka kumsikia tena.

Kulipokucha, Erica alitoka chumbani kwake na kumkuta mama yake yupo mwenyewe maana hakutoka nje tena toka ule muda alioenda chumbani, akamsalimia na kuanza kuongea nae,
“Mama, kwahiyo wakina dada waliondoka kumbe!”
“Ndio waliondoka”
“Dada Bite je?”
“Alikuwa anakataa ila nikamwambia ndoa ni uvumilivu, si alichagua mwenyewe kuishi na aina ile ya mwanaume, akamvumilie tu yakimshinda atarudi ila hana furaha kwakweli”
“Mama samahani kwa kilichotokea jana, ila mama nilichoka kudhalilishwa na shemeji, na kwa hakika asingeacha kunidhalilisha maana ndio tabia yake, na hapa nyumbani mnamnyenyekea kwahiyo kila anachosema ni ndio. Kwakweli mama sikuweza kuvumilia ule uonevu maana ni uonevu kwangu, mtu kila leo anidhalilishe kwa mantiki gani? Na mimi nimemdhalilisha aone uchungu wa mtu kudhalilishwa, tena bora mimi nimemdhalilisha kwa ukweli wa tabia yake. Ila dah mama mmenisema sana jana kiasi kwamba sikuweza kuvumilia kuwasikiliza na kwenda zangu chumbani, naomba unisamehe tu”
“Erica nawe hujanizoea tu mama yako jamani! Jana nilikuwa nakusema ili Bite aone na mimi nimeumia ila kwa upande wangu nimefurahi sana maana hata mimi sikupenda ile tabia ya kijinga jinga anayoifanya mara akusingizie hiki mara kile mwisho wa siku angeweka uhasama kati yako na dada yako ila kwavile tumejua ukweli wa mambo ni rahisi na nimemfundisha hapa Bite jinsi ya kuishi na mwanaume wa aina ile, walee mtoto bado mdogo Yule”
“Sawa mama, kwahiyo tutamuita Dada Bite ili nimkabidhi zile pesa za mumewe?”
“Weweee tumpe za nini, kitakachorudishwa hapo ni funguo tu, napo hakuna kurudisha mpaka aje kuomba msamaha tena kwangu ndio nitakwambia umrudishie hiyo funguo. Ujinga ujinga sitaki kabisa. Ila pesa iliyotoka hiyo ni malipo ya kukutangazia vibaya mwanangu, hairudishwi hiyo maana kashakutangazia sana vibaya. Haya kachukue laki mbili unipe mama yako”
Erica alicheka sana maana alijua na leo ni kama zile hela za Mzee Jimmy ambazo mama yake alisema warudishe ila za leo kagoma kuwa hazirudishwi, Erica alienda chumbani kwake na kutoa laki mbili kumpa mama yake, huku akimwambia
“Mama mbona za mzee Jimmy ulisema turudishe na hizi umegoma?”
“Mwanangu, Yule mzee humfahamu halafu unataka kula pesa zake si zitakutokea puani. Ila huyu shemeji yako kashakudhalilisha vya kutosha, na umefanya vizuri sana kusema akuletee pesa maana ndio malipo kwa kukusingizia uongo wake. Hiyo ni yako mwanangu, jilie tu”
Erica alicheka tu kisha akaendelea na mambo yake mengine ambapo mama yake alijiandaa na kwenda kanisani.
Erica alibaki nyumbani, na kaka yake Tony nae alirudi na kumkuta dada yake, alikaa nae na kuanza kuzungumza nae,
“Erica, siku uliyoniletea chokochoko kuhusu Dora nilijua mdogo wangu una roho mbaya sana ila sikujua kama ulikuwa unaniponya kaka yako, nashukuru sana mdogo wangu. Dora ananiona nimechoka eti sina hela, angejua vitu nilivyonavyo ni vikubwa mno, hakuna ajuaye ila kwasasa nitamwambia mama yangu”
“Vitu gani hivyo kaka?”
“Hivi unajua kama mimi nina nyumba? Maisha ni nyumba kwanza kabla ya kitu chochote”
“Una nyumba kaka?”
“Ndio nina nyumba, ningemuoa Dora nisingeenda nae kupanga bali ningeenda nae kwenye nyumba yangu, ila yeye kanidharau. Angeonyesha tabia njema hata baada ya kumuacha ningemfikiria ila kumuacha ndio nimempa tiketi ya kufanya uhuni! Bora ameondoka kwangu, angeniua Yule mwanamke. Tatizo wanawake wengi wakiona mtu ana gari ndio wanaona maisha yamekamilika, mimi gari sina ila nina nyumba na mke nitakayempata nitampenda na atafurahi kuwa na mimi”
Basi Erica aliongea ongea pale na kaka yake huku wakishauriana, ila kaka yake aliendelea kumsisitiza kuwa kitendo alichofanya jana hakikuwa kibaya wala nini maana itamsaidia kubadilisha tabia ya shemeji yao na hawezi kumsumbua tena.
Usiku ulifika na kwenda kulala tu na kuacha yaliyopita yawe yamepita.
 
SEHEMU YA 291


Palipokucha, Erica aliamka mapema kabisa na kujiandaa kisha kumuaga mama yake kuwa anaenda kwenye ile kazi,
“Erica, kumbuka na swala la kupata msichana wa kazi hapa nyumbani maana itakuwa ndio yale yale ya kipindi kile. Mtu wa kubaki na mtoto hakuna”
“Sawa mama”
Erica akaenda kazini, alipofika tu alienda ofisini kwa Yule mama ambaye alifurahi kumuona kisha kumuonyesha kazi ya kufanya huku akimpa maelekezo baadhi ya namna ya kufanya, na kumwambia,
“Kuna mtu inabidi ndio awe anakuelekeza maana ndio mtakuwa mnasaidiana nae, ila leo hajaja ofisini, atakuja kesho na utaendelea nae kwenye kazi”
“Sawa asante”
“Kwa leo, fanya hizo chache tu na uwahi tu kutoka maana hakutakuwa na kazi ya ziada mpaka kesho Yule afike kukuelekeza vizuri”
Basi Erica akafanya kazi aliyopewa hadi ule muda wa kuondoka ulivyofika akaondoka zake na kwenda kwao.
Alivyofika alimkuta mama yake na kumsalimia ila leo mama yake alimkalisha chini ili kuzungumza nae tena,
“Unajua Erica bado najiuliza kuhusu huyo uliyemuuzia mtoto, najiuliza sana, huyo kijana ni wa aina gani?”
“Ni kijana mzuri tu mama”
“Uzuri wake hausaidii Erica, hivi ushawahi kuwaza maisha ya badae ya mwanao? Huyo kijana umempa mtoto atampa nini mwanao leo na kesho, yani mtoto wako atakuwa na nini cha kujivunia kuwa na baba kama huyo? Unatakiwa kufikiria Erica, huyu ni mtoto na maisha yake ni muhimu sana kupita unavyofikiria.”
Erica alikuwa kimya tu, kisha mama yake akaendelea kuongea,
“Erica mwanangu sikia nikwambie, mambo ya kuendekeza mapenzi yalipitwa na wakati sijui ananipenda sana sijui nampenda sana, hayo mambo yamepitwa na wakati mwanangu. Umekuwa mtu mzima sasa, baba wa mtoto haeleweki umeamua kutoa mtoto zawadi kwa baba mwingine, je mtoto atafaidika na nini na huyo baba mwingine? Jamani mimi nafikiriaga mbali sana ujue, natamani wote mngekuwa na fikra kama zangu, sipendi watoto wangu mkosee kabisa, maana maisha haya ukishakosea moja ujue mbili itakupiga chenga haswaa, sema mapema ili tufanye kitu. Usimkuze mtoto na jina lisilokuwa na faida kwake, huyo mwanaume ana nini cha maana hadi umemzawadia mtoto?”
“Mama, Erick ananipenda sana na mimi nampenda sana”
“Nishakwambia sitaki kusikia habari za kupendana, niambie ana kipi cha maana kama hana chochote kwakweli nitagharamia tu ukamuweke mjukuu wangu jina la baba yake, najua Yule Mwajuma nitakabana nae koo ingawa sitaki ahisi nina shida nae ila nitamkaba koo tu maana huyu ni mjukuu wake, leo na kesho watamtafuta. Niambie huyo Erick ana kipi cha maana?”
“Mama, kwanza kabisa huyu Erick ndiyo mmiliki wa lile duka la vitu vya watoto ambapo Angel kawa balozi huko na kupatiwa zawadi za nguo na kulipwa kila mwezi, yani unavyomuona angel hapo analipwa kila mwezi sababu ya kuwa balozi kwenye hilo duka. Pia huyu mwanaume ndio kamuandikishia kadi ya bima ya afya mwanangu kiasi kwamba sitahangaika wala nini mwanangu akiumwa, hata nisipokuwa na pesa najua mwanangu atatibiwa. Na kashaniambia kuna vitu amemuandikisha mwanangu kwenye mali zake”
“Erica, unasema kweli!”
“Ndio ni kweli mama?”
“Mmmh hivi inawezekana kweli? Yani kirahisi rahisi tu hivyo, unajua mimi siamini kabisa kama kitu hiko kinawezekana, wanaume wa hivyo wapo kwenye dunia hii kweli? Ikiwa tu mwanaume mwingine hata kununua nguo ya mtoto ambaye si wake ni ngumu halafu unaniambia huyo mwanaume ndio kafanya hivyo! Sikujua, kumbe hata bima ya afya kafanya mpango yeye, aaah sina pingamizi tena mwanangu, acha tu Angel aitwe Angel Erick”
Erica akacheka sana maana mama yake kuna muda anakuwa kigeugeu sana, ila mama yake akasema tena,
“Ila nitachunguza maana bado hainiingii akilini yani mwanaume amthamini hivyo mtoto ambaye si wake mmmh! Nahisi kama kuna kitu nyuma ya pazia, nitachunguza, nitakuwa nakuuliza maswali kila mara maana nataka kujua ukweli”
Erica alimuitikia tu mama yake maana alijua hata akichunguza bado atapata ukweli kuwa Erick na Erica wanapendana.
 
SEHEMU YA 292


Usiku alijiandaa kwaajili ya kulala ila akapigiwa simu na Erick akimsalimia na kumuuliza kuhusu kazini alipoenda amepaonaje kwa siku ile ya kwanza,
“Aaaah ni pazuri tu”
“Kama ni sehemu itakayokuboa niambie Erica, unajua mwanzo sikufikiria kama unauhitaji wa kazi, ila kwavile ushapata sio mbaya, sema kama ni sehemu inayoboa niambie ili nikuunganishie sehemu nyingine”
“Sawa, ila pako sawa kabisa na nimepapenda. Mazingira mazuri, pametulia na panavutia”
Basi wakaongea mengi mengi hadi muda wakaagana na kulala, kwakweli moyo wa Erica ulikuwa umepumzika kwa kipindi hiko maana hakukuwa na kitu cha kuumiza akili yake tena kama mwanzo, ukizingatia kama kazi kapata, na yupo mpenzi anayemjali na kumsikiliza kwahiyo alikuwa na furaha sana.
Kesho yake kama kawaida alijiandaa na kwenda kazini ila napo hakumkuta Yule wa kumuelekeza, na siku hiyo Yule mama alimruhusu mapema zaidi na kumuhakikishia kuwa Yule wa kumuelekeza atafika kesho.
“Unajua nini, lazima Yule awepo maana ndio anajua mlolongo mzima hapa. Hata wiki iliyopita nilikwambia wiki hii ni sababu yake, ila jana nilipompigia alisema kuwa kesho kutwa yani kesho ndio atakuwa hapa ofisini, ni kijana mzuri tu, mstaarabu na utafanya nae kazi vizuri”
“Asante mama”
Kisha aliruhusiwa kuondoka, wakati yupo stendi akisubiri daladala ndipo akakutana tena na Yule jirani wa Bahati ambaye alimuita na kumwambia,
“Tena afadhali nimekuona Erica, twende”
“Wapi?”
“Twende mara moja, kuna mahali nilionyeshwa twende”
Kwakweli Erica alimshangaa huyu dada kuweka mazoea ya karibu hivyo na yeye ila hakupenda kumfanyia dharau kwa kukumbuka kuwa watu wote ni sawa, na usipende kumdharau mtu maana hujui anataka kusema nini.
Akaondoka na huyo dada, kuelekea sehemu anayomwambia waende, kufika mbele walipanda bajaji na kufanya kidogo Erica awe na mashaka na kuhisi pengine huyu dada anampeleka nyumbani kwa Bahati,
“Ila dada si nilishakwambia, mambo ya Bahati sitaki tena”
“Ni kweli hutaki mambo ya Bahati Erica, ila Bahati ile sio akili yake halafu kuna kitu kingine nimeambiwa juu yako ndiomana nimeamua kufanya hivi”
“Kitu gani?”
“Erica, nimeambiwa kuwa wewe kuna kitu umepakwa, tunaita kimavi yani hapo utatanga tanga, utahangaika hangaika ila hutokuja uolewe kamwe. Yani aliyechafua kuhusu Bahati alimalizia tu kuchafua kuhusu wewe, hebu jiulize binti mzuri kama wewe una kasoro gani ya kutokuolewa? Kwanini usiolewe, sikujui Erica ila nilichoambiwa kuhusu wewe kimeniuma kama mzazi pia, utakuwa unajiona huna bahati, mikosi imekuandama kumbe wamekuchafua.”
“Ila mimi nina mchumba wangu”
“Sikatai unae ila unaweza shangaa huyo mchumba anawiwa vigumu sana kutaka kukuoa wewe maana kuna vitu umefungiwa”
“Kwahiyo unataka kunipeleka wapi?”
“Kwa mtaalamu Erica”
Erica alimwambia Yule dereva wa bajaji asimamishe, kisha Yule dereva akasimama halafu Erica akamuuliza,
“Unatudia pesa ngapi?”
“Ya pale hadi hapa?”
“Ndio”
“Elfu mbili”
Erica akatoa elfu mbili na kumpa Yule dereva, kisha akatoa elfu tano na kumpa Yule dada kisha akamwambia,
“Nashukuru kwa kunihurumia, kwaheri”
Erica akaondoka zake, akavuka barabara na kupanda daladala.

Alifika kwao ila hakutaka kufikiria kabisa kuhusu swala la kuambiwa yeye sijui kapakwa kimavi sijui nini na nini hakutaka kabisa kujua maswala hayo hata hakuona kama ni ya msingi kumueleza mama yake, aliingia ndani na kumsalimia na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.
Ila mama yake alimuita na kumueleza yaliyojiri kuhusu shemeji yake,
“Basi nasikia shemeji yako hadi leo hajakanyaga nyumbani kwake, ndio mapya hayo”
“Kheee makubwa, vipi kazini kwake mmeulizia?”
“Bite kasema kauliza kaambiwa kazini ameenda, jana, leo ila nyumbani hajaenda”
“Huyo anatafuta sababu tu, ila atarudi kwake mwenyewe”
Kisha Erica akainuka na kurudi tena chumbani kwake maana tayari alikuwa na mawazo yake ya kumtosha tu.
Mpaka muda analala alikuwa hataki kuweka mawazo ya Yule dada kwenye akili yake ila maneno ya Yule dada yalikuwa yakisikika tu kwenye kichwa chake hadi alipopitiwa na usingizi.
Kesho yake kama kawaida alijiandaa na kwenda kazini, alifika na kwenda kwa Yule mama ambapo Yule mama alimwambia,
“Leo Yule ambaye utafanya nae kazi pamoja amefika, ngoja nimuite nikutambulishe akufahamu”
Kisha Yule mama alipiga simu na kusema neno moja tu,
“Njoo ofisini kwangu”
Baada ya muda kidogo muhusika alifika, Yule mama akamwambia
“Karibu ukae nikutambulishe”
Erica akamuangalia huyu aliyeingia ofisini kwa huyu mama alikuwa ni George Yule aliyewahi kuwa mpenzi wake chuoni, hadi akawa na visasi nae.
 
SEHEMU YA 293


Kisha Yule mama alipiga simu na kusema neno moja tu,
“Njoo ofisini kwangu”
Baada ya muda kidogo muhusika alifika, Yule mama akamwambia
“Karibu ukae nikutambulishe”
Erica akamuangalia huyu aliyeingia ofisini kwa huyu mama alikuwa ni George Yule aliyewahi kuwa mpenzi wake chuoni, hadi akawa na visasi nae.
George alionekana kumuangalia Erica, nae alimuangalia George huku moyoni akiwaza kuwa kwanini wa kufanya nae kazi awe George na si mwingine, basi Yule mama akaendelea kumtambulisha,
“Erica, huyu anaitwa George ndio kijana mtakayekuwa mkisaidiana nae na atakuelekeza kazi za kufanya. George, huyu anaitwa Erica, ndio Yule msaidizi tuliyekuwa tunamuhitaji”
George alimpa mkono Erica wa kumkaribisha, naye Erica alimpa mkono pia, hawakutaka kuonyesha tofauti zao mbele ya bosi wao.
Kisha George akamkaribisha Erica kuwa amfuate eneo la kazi, Erica aliinuka na kufatana nae.
Walipofika kwenye ofisi ambayo wapo wenyewe wawili tu, George akaanza kumuelekeza Erica kazi ambapo kabla ya yote alimuhoji,
“Erica, umemuhonga nini huyu mama hadi kakupa kazi?”
“Kwani hapa kazi watu hupata kwa kuhonga? Na wewe ulihonga nini?”
“Umeanza kuwa na majibu ya shombo hivyo loh! Kumbuka ni mimi ndio wa kukuelekeza kazi hapa, na vilevile mimi nipo juu yako, sasa kuniletea majibu ya shombo hivyo nitaenda kukushtaki?”
“Sikia George, sijaja kufanya kazi nilumbane na mtu, wewe utaniulizaje mimi kuwa nimehonga nini? Kuna cha kuhonga nilichokuwa nacho? Sikia, hayo maswali kamuulize bosi maana ni yeye aliyeniajiri hapa”
“Mmmh sawa, ila ngoja nikwambie. Bosi alisema anatakiwa mtu wa kunisaidia kazi, na tukatangaza kazi na kuchukua watu ishirini kwaajili ya usahili, nilisimamia mwenyewe ule usahili na sikukuona kabisa ila iweje wale wote wamepigwa chini uwekwe wewe! Hainiingii akilini kabisa”
“George, nishakwambia nenda kamuulize muhusika sio mimi”
“Umekuwa na majibu Erica eeh!”
“Tufanye kazi George, maswali ya kijinga jinga hapana kwakweli”
George akamuangalia Erica na kuanza tu kumuelekeza kazi ilimradi siku iende, maana ingekuwa ni ofisi yake kwa majibu yale ya Erica basi angemsimamisha kazi kwa hasira zake maana huwa anapenda anyenyekewe.
Muda wa kazi ulivyoisha, Erica aliondoka zake na kurudi kwao. Leo hakukutana na Yule dada stendi kwahiyo alishukuru tu kwavile hakuonana nae, alipanda daladala na kwenda kwao.

Alifika kwao ila kitendo cha kufanya kazi ofisi moja na mtu aliyewahi kumfanyia vitu vya ajabu maishani mwake alichukia sana, hakupenda kwakweli. Siku hiyo hata mama yake alimuona kama mwanae hakuwa na raha, akamshangaa maana hata jana yake alirudi bila raha. Baada ya salamu akamuuliza,
“Erica unajua tangu jana sijakuelewa kabisa, jana umekuja bila raha na leo tena umerudi bila raha tatizo ni nini na kazi ndio umeanza?”
“Hakuna tatizo mama”
“Lipo, mimi naliona, Erica hata kama unahisi tatizo hilo ni la kijinga niambie mama yake na nitakusaidia kwa vitu vingi tu, kwa ushauri au kwa lolote, niambie mwanangu hata kama unahisi ni la kijinga”
“Sijui nianzie wapi mama”
“Anzia popote tu ila niambie”
“Ila usinifikirie vibaya mama yangu”
“Erica niambie tu tatizo ni nini, mimi ni mama yako lazima tatizo lako liwe kwangu pia, nisipokusaidia mimi atakusaidia nani tena?”
“Mama, kuna mwanamke nilikutana nae jana akasema kuwa mimi nimepakwa kimavi ndiomana siolewi, eti naweza kuona muda bado ila nitatanga tanga ila sitaolewa kamwe maana nimepakwa kimavi”
“Kumbe ndio jambo linalokupa mawazo hilo mwanangu!”
“Ndio mama ila niliona sio la muhimu ndiomana sikukwambia”
“Sikia, lisingekuwa la muhimu basi lisingesumbua akili yako, halafu waswahili husema lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, unajua mambo kama hayo sio ya kuyafumbia macho! Tena nashukuru mwanangu kwa kuniambia maana nitaanza kuombea jambo hilo na kuwaomba watumishi wa Mungu wanisaidie, sikia usipuuze mambo ya muhimu kama hayo ukiambiwa ila unatakiwa uchukue tahadhari mapema sana, hicho kitu sio cha kukikalia kimya, halafu miaka iende ndio tushtuke kuwa kuna tu analisema hivi, kwanini hatukufanyia kazi tulivyoambiwa? Wakati ni huu na wakati ni sasa”
“Ila mama kwani ni muhimu sana mtu aolewe”
“Wewe mtoto usiniletee laana hizo, kuolewa ni muhimu hata maandiko yamesema utawaacha wazazi wako utaambatana na mwenzako na mtakuwa mwili mmoja, mambo ya kusema sijui kwani lazima kuolewa sitaki kuyasikia kabisa, Mungu aliumba mwanaume na mwanamke kwa makusudi kabisa, kungekuwa hakuna umuhimu wa kuoana basi Mungu asingeumba mwanamke maana mwanaume angetosha ila alisema si vizuri mtu huyu awe peke yake, kwahiyo mashetani ya kuniambia sio lazima kuolewa sitaki kuyasikia kabisa. Sema tumuombe Mungu uolewe na mtu anayefaa ila sio swala la kuniambia kwani kuolewa ni lazima, tena nyamaza kabisa”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Ila nashukuru kwa kunihabarisha kuhusu hayo uliyoambiwa maana ni ya muhimu sana kwangu, sisi ni wanadamu huwezi jua ni kitu gani kimefunga huko, huyo mtu namshukuru”
“Ila alisema niende nae kwa mtaalamu kutibiwa”
“Sitaki kusikia na huo ujinga, toka nimekuzaa lini nimekupeleka kwa mtaalamu wewe? Lini? Sitaki hayo mauza uza kabisa, nichanganye maji na mafuta ya nini? Kwani Mungu hasikii? Tumuombe Mungu tu atatusikia ila maswala ya waganga siyataki kwenye nyumba yangu”
“Sawa mama”
Erica alimuitikia mama yake na kwenda chumbani kwake ambapo alifanya shughuli zake zingine, alienda kula na kujiandaa kulala, alipotaka kujilaza tu mwanae aliamka maana alimkuta kalala.
Basi Erica alianza kujigelesha kwa kila hali huku akimbembeleza mtoto ili alale tena nay eye aweze kulala ila mtoto hakulala, hadi saa sita usiku mtoto alikuwa macho, kila Erica alipojaribu kulala mwanae alimfanyia fujo hadi hakuweza kulala, Erica alijitahidi kumbembeleza ila mtoto hakulala, ikabidi aanze kumuuliza kwa taratibu,
“Kwani mwanangu unataka nini leo jamani? Unajua sio kawaida, kweli hadi muda huu hujalala jamani? Unataka nini, eti Angel unataka nini mwanangu?”
Mwanae alimjibu kitu ambacho kilimshangaza sana kwa muda huo,
“Ataka ongea ababa”
“Kheee makubwa, Erick kashaniharibia mtoto”
Ikabidi achukue simu yake ili ampigie Erick, ila simu haikuwa na salio, uwiii Erica aliona sasa atakesha na huyu mtoto, akainuka ili amuombe mama yake simu ampigie Erick.
Akamgongea mama yake na kumuomba simu,
“Erica, simu yangu usiku huu unataka ya nini?”
“Nina shida nayo mama, naomba tafadhali”
“Kuna kivocha change, ukikimaliza kesho ujue kununua”
“Sawa mama”
Erica akachukua simu kwa mama yake na kurudi chumbani, kisha akampigia Erica ambapo kwa muda mfupi tu alipokea,
“Naomba nipigie Erick, mimi Erica”
Kisha akakata simu na baada ya muda kidogo tu Erick alipiga na kusalimiana na Erica,
“Unajua kabisa kitu ulichomzoesha mwanangu jamani Erick halafu humpigii simu!”
“Erica useme mwanao tu, sema mwanetu, huyo ni mtoto wetu sote. Kashalala?”
Muda huo Erica alishang’anywa simu na mtoto wake, kwakweli alicheka tu maana mtoto anavyoonyesha kupenda kuongea na Erick ni balaa.
Baada ya kuongea nae ndio alimpa simu mama yake kisha akasogea akajilaza tena kitandani, Erica akamuuliza Erick,
“Unampaga maneno gani mwanangu wewe hadi leo anigomee hadi aongee na wewe?”
“Usiseme mwanao sema mwanetu, nahitaji anizoee maana mimi ndio baba yake, vipi namba uliyonipigia mwanzo ya nani”
“Ya mama ile”
“Kwahiyo niitunze eeeh!”
“Ifute weee”
“Naitunza, maana siku nisipokupata tu basi nampigia mama”
“Yani wewe loh! Tutaongea kesho basi, saivi ngoja nilale”
Basi wakaagana pale na Erica akalala sasa maana hata mtoto wake alilala.
 
SEHEMU YA 294

Kulipokucha alijiandaa na kwenda ofisini, alifika na kukuta George kashafika alimsalimia na kuanza zile kazi alizomuelekeza jana, ila George akaanza kusema,
“Unachukua muda mwingi sana kujiremba hadi unachelewa ofisini”
Erica hakumjibu na kuendelea na zile kazi,
“Ila unapendeza sana, umekuwa mrembo Erica hadi natamani tena kuwa na wewe”
Bado Erica hakumjibu na kuendelea na kazi, na alipomaliza alimuomba amuelekeze zaidi ili aendelee kufanya kazi,
“Sasa kazi itafanyika vipi kama tunafanya kibubu?”
“Kibubu kivipi?”
“Nakuuliza kitu hunijibu ila ukiwa na shida wewe tu ndio unaniuliza”
“Sikia George, tuulizane mambo ya kazi uone kama sitokujibu. Unaniuliza mambo binafsi kwenye kazi kweli! Nakujibu vipi”
“Kukwambia umependeza ni vibaya? Usinifanyie hivyo Erica, unajua nimekuwa na maisha yangu sasa, na ninaishi mwenyewe nahitaji mwenzangu”
Erica hakumjibu kitu, na kuendelea na kazi hadi muda wa kuondoka ulipofika, alichofanya Erica ni kumuaga tu kuwa wataonana kesho,
“Hapana Erica, subiri nikupeleke kwenu unajua nina usafiri siku hizi eeh!”
“Asante kwa lifti ila napenda zaidi kupanda daladala”
“Erica umekuwaje kwani? Hunitaki tena?”
“Unajua usinichekeshe George, tangu lini nimekutaka? Naomba tufanye kazi”
Erica akaondoka zake na kuelekea stendi, kwakweli George alishangazwa sana na majibu ya Erica, alihisi kuna kitu Erica anajivunia nacho maana hakuona kama ni kawaida kwa Erica kuwa na majibu ya aina ile.
Erica alisimama stendi ili kupanda daladala, ila kabla hajapanda akavutwa na Yule dada, ila kiukweli Erica hakupenda namna ambavyo Yule mdada alimvuta maana ndio alitaka kupanda kwenye gari.
Erica alimuuliza Yule mdada,
“Lipi jipya leo?”
“Erica, usione nakufatilia, napenda maisha yako. Nilienda mwenyewe nikaambiwa kuna mtu unamfahamu utakutana nae, na huyo atahusika sana kuzidi kuvuruga maisha yako ila ninachokwambia kuwa makini, sikulazimishi tena kwenda kwa mtaalamu ila kuwa makini kwa yeyote unayekutana nae. Ni kweli Bahati karogwa yani hasikii wala nini ila dawa zitakapoisha atateseka sana kwani Yule mtaalamu kaniambia kuwa Bahati anakupenda wewe. Erica natamani kukusaidia ila sijui wewe unanifikiriaje, ni hayo tu kwaheri”
Huyu dada aliondoka ni kwavile alijiona tu akitiririka kuelezea wakati hata Erica hakuwa na muda wa kumjibu, kisha Erica alipanda basin a kurudi kwao.
Alipofika kama kawaida alimsalimia mama yake ambapo mama yake alikaa nae na kuanza kuzungumza nae,
“Unajua Erica maneno ya huyo mtu kama yanaanza kuniingia akilini ila najua Mungu ni mwaminifu atatusaidia tu. Sijui ni wapi walikupaka huo ujinga mwanangu ila najua Mungu ni mwema”
Erica alimuitikia tu mama yake na kuingia ndani, leo alipigiwa simu na Erick muda ule ule na alianza kumuuliza kuhusu kazini ila Angel alikuja na kupokonya simu ambapo akaongea kidogo na Erick na alipolizika alirudisha simu kwa mama yake,
“Yani huyu mtoto jamani”
“Muache mtoto Erica, kwani si vibaya kuchukua simu na kuongea na baba yake. Kuna mzigo mpya natuma dukani kwahiyo Jumamosi umpeleke mtoto akajaribishe”
“Sawa hakuna shida”
“Halafu, vipi kazini kwako kupo salama?”
“Ndio kupo salama”
“Umepapenda?”
“Mapema sana Erick kuniuliza hivyo, kumbuka ni wiki ya kwanza hii”
“Sawa ila bado nasisitiza kama unapaona hapako sawa basi acha, mimi nitakutafutia pengine”
“Sawa, nimekuelewa Erick”
Basi akaagana nae na kumalizia mambo yake mengine na kulala tu.

Kulipokucha alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida, siku hiyo aliwahi kushinda George na kuanza kazi zake, muda kidogo George nae alifika na kuendelea na kazi za hapa na pale. Kisha Erica aliitwa ofisini na Yule mama na kuamua kwenda, alipofika alimsalimia kisha Yule mama alimuuliza,
“Unaionaje kazi Erica?”
“Ni nzuri tu mama”
“Ila jitahidi uongeze ubunifu katika kazi, umefikia. Jaribu kuangalia kwa makini anavyofanya George nawe ufanye, najua ni mara yako ya kwanza kufanya kazi hii ndiomana inakuwa sio kwenye ubora ule ninaotaka mimi. Ila kuwa huru, lolote linalokutatiza uje kuuliza, sawa”
“Sawa mama, asante”
“Haya kaendelee na kazi”
Erica alirudi kuendelea na kazi ila kuna kitu alielewa maana alihisi George amfundishi kwa ufanisi, aliendelea na kazi kwa muda kisha akamfata na kumuuliza,
“George, kwanini unaniweke kinyongo mimi hadi leo? Kumbuka mimi ndio natakiwa kuwa na kinyongo na wewe ila sio wewe kuwa na kinyongo na mimi, kumbuka umenifanyia mambo ambayo hayastahili kabisa ila mimi nimenyamaza, kwanini usinielekeze kwa ufanisi sasa”
“Kwani nimekuelekeza vibaya?”
“Ndio, kwanini bosi aniulize kuwa sifanyi kiufanisi wakati wewe unasema umenielekeza vizuri. George haya ni maisha tu, nipo hapa nikitafuta maisha kama wewe ambavyo unatafuta maisha”
“Usijali, ila nikuombe kitu”
“Kitu gani?”
“Naomba unipe mapenzi tena, kwa hakika nitakufurahisha na utapendwa sana”
“George sikia, huwa sili matapishi nikishatapika. Nione kawaida kabisa tena kama dada yako wa tumbo moja, maana hicho ulichosema hakiwezekani na hakitawezekana kamwe”
“Kwanini kisiwezekane Erica, kunipa mara moja tu!”
“Hivi wewe George una matatizo gani? Sitaki”
“Mbona kipindi kile ulinipa?”
“Kipindi kile ulikuwa mpenzi wangu ila sio kwasasa, naomba uachane na habari hiyo kwangu kabisa, sipo hivyo unavyonifikiria”
“Unajifanya mstaarabu sio, wakati masela wengi washakupitia”
“Hivi si wewe ndio ulisema unataka wanawake bikra, sasa bikra imerudi kwangu? Sitaki”
“Wewe Erica, unajifanya keki wakati kipindi kile ulitoa tu”
“George sikia, Erica wa kipindi hiko sio Erica wa kipindi hiki. Nilikuwa natafuta penzi la dhati na sasa nimelipata, sina sababu ya kusaliti penzi langu, unikome na ukiendelea kuniondolea furaha katika kazi sitakaa kimya, nitasema tu kwa bosi”
Ila George alicheka sana, na Erica alienda kuendelea na kazi zake, na alipomaliza alienda kwa bosi wake kumuomba ruhusa ya kutokufika kesho yake kazini,
“Usijali, hata hivyo Jumamosi ni siku fupi hakuna shida.”
Erica alishukuru kisha akajiandaa na kurudi kwao.
Wakati yupo stendi, akamuona Yule mwanamke anayempaga habari za Bahati, kwa muonekano wa Yule mwanamke ni wazi alikuwa akimtafuta Erica, kwavile Erica alikuwa akimkwepa basi gari lililokuwa limekuja ingawa lilijaa ila alipanda hivyo hivyo ili kwa siku hiyo asiongee tu na Yule mwanamke.
Alifika kwao ila hakumkuta mama yake inamaana alikuwa ametoka, akawaza kuhusu mtoto ila naye hakusikika ndani kwamaana hiyo mama yake alitoka nae, baada ya muda kidogo mama yake na mtoto walirudi, akamsalimia na kumuuliza,
“Kheee mama leo ulitoka na Angel?”
“Wee nitamficha mjukuu wangu hadi lini? Kwanza amesifiwa njia nzima, na anavyojua kupokea sifa mwanao yani anatabasamu tu yeye, mtoto huyu kwakweli ana haki ya kupendwa. Halafu leo nimemfananisha na wewe wakati mdogo, hukujua kununa Erica, labda ukubwani ndio unanuna mara nyingine ila udogoni ulikuwa ni mtu wa tabasamu tu”
Erica alitabasamu kwa kufurahia ile sifa aliyopewa na mama yake, kisha akamchukua mtoto kwenda nae chumbani, alipofika tu simu ikaita, kuiangalia ni Erick alikuwa anapiga, Erica akaipokea, ile kusema tu,
“Hallow Erick”
Mwanae alimpokonya simu na kuiweka sikioni kwake, kwakweli Erica alikuwa akicheka na kusema kuna siku ataweka sauti kubwa ili asikie ni maneno gani Erick anaongeaga na mtoto wake kiasi cha kumfanya Yule mtoto kupenda kuongea nae ingawa bado hajui kuongea vizuri.
Kisha Angel alimkabidhi mama yake simu huku akitabasamu tu na Erica akaongea na Erick pale huku akiendelea kumsisitiza kuhusu kesho kwenda dukani,
“Nitamtuma mtu aje awachukue mapema”
“Sawa hakuna tatizo”
Kisha akaagana nae na kuamua kufanya mambo mengine hadi kulala.
 
SEHEMU YA 295

Jumamosi kulipokucha alijiandaa mapema kabisa na mwanae, na gafla alipigiwa simu na Moses akapokea,
“Erica, nipo hapa nje ya nyumba yenu nikikusubiri”
Kwakweli alitabasamu, alijua kuwa Moses kapewa oda tu ya kumfata, kisha akamuaga mama yake na kuondoka ambapo walienda kupanda gari na kuelekea dukani.
Walifika na moja kwa moja Angel alianza kujaribishwa nguo na kupigwa picha maana nyuma ya duka palikuwa na bustani nzuri sana, kwahiyo walitumia eneo hilo kumpiga picha Angel.
Wakati Angel akiendelea kupigwa picha, Erica akaitwa na kutoka nje ili kuona nani anamuita alishangaa kumuona Tumaini siku hiyo akimuita kwa nje, akamfata na kumsalimia,
“Sihitaji salamu yako, msichana ni mbaya sana wewe tena ni mchawi”
“Uchawi wangu nini sasa?”
“Yani uzae na mwanaume mwingine halafu mtoto umbambikizie kaka yangu kweli? Erica unaona ulichofanya ni kizuri? Mwanamke wa kaka yangu umegombana nae na umeharibu mimba yake ambayo ndio ya mtoto halali wa Erick”
“Kwani Tumaini tatizo lako ni nini? Unajua huwa sikuelewi?”
“Tatizo langu ni wewe kumkandamiza kaka yangu kwa uchawi wako, ona sasa ulichofanya kwa wifi yangu? Umeenda kupambana nae ili tum toe mimba aliyobeba ambayo ina mtoto halali wa Erick, wewe ni muuwaji”
“Bado sikuelewi”
“Hunielewi nini, muangalie Yule humtambui?”
Tumaini akanyoosha mkono ambapo Erica aligeuka na kuangalia, alishangaa kuona Yule mwanamke aliyemsukuma ofisini mpaka akadakwa na Sia ndio anakuja.


“Bado sikuelewi”
“Hunielewi nini, muangalie Yule humtambui?”
Tumaini akanyoosha mkono ambapo Erica aligeuka na kuangalia, alishangaa kuona Yule mwanamke aliyemsukuma ofisini mpaka akadakwa na Sia ndio anakuja.
Erica akaona hapo ni balaa kwa upande wake, kwani akikumbuka huyu mdada alivyomsukuma hadi akataka kuanguka ilionyesha kuwa ana nguvu sana, akahofia isije huyu mdada akamchangia na Tumaini na kumfanya awe mboga yao bure kwa muda huo.
Kwakweli hata Tumaini hakuelewa jinsi Erica alivyomtoroka ila alimshangaa tu akiwa mlangoni wa duka akiingia ndani.
Erica alienda kwa Moses moja kwa moja na kumuomba,
“Moses, tafadhali naomba niondoke na mwanangu”
“Ila bado hatujamaliza, tena nilikuwa naanza kukutafuta hapa maana ulitoweka gafla”
“Sipo salama hapa, naomba niende”
“Haupo salama kivipi? Kipi kinakutisha kwani?”
“Tumaini hataki kuniona hapa dukani”
“Kwani Erica wewe na Tumaini kuna nini kinaendelea kati yenu? Unajua huwa sielewi”
“Hamna chochote ila hapendi tu kuniona hapa”
“Erica, Tumaini sio mwenye hili duka hata asikubabaishe. Hebu twende kwanza huko bustanini maana mtoto wako amenuna kwa kutokukuona”
Basi Erica akaongozana na Moses hadi bustanini ambapo Angel kweli alikuwa amekaa pembeni tu hacheki wala nini kumbe tatizo ni hakumuona mama yake, ila alipomuona alifurahi sana na kumkimbilia akamkumbatia huku akimtaka waende nyumbani,
“Bado hatujamaliza mwanangu”
Ila alionyesha aking’ang’ania kwenda nyumbani, Erica akaona dawa ya mtoto wake huyo ni kumpigia Erick ili aongee nae kwani alijua atatulia tu, basi Erica alimpigia simu Erick kisha kumwambia kuwa aongee na Angel, ambapo Erick aliongea nae kidogo na baada ya muda alikubali tena kubadilishwa nguo na kupigwa picha, kile kitendo cha Angel kuongea kwanza na Erick kilimshangaza sana Moses, na baada ya zoezi la picha aliamua kumuuliza Erica,
“Inamaana mwanao kamzoea sana Erick eeeh!”
Erica akacheka tu kisha Moses akaamua kuwabeba kwenye gari yake na kuwarudisha kwao, ambapo Angel alishafungiwa nguo za kurudi nazo nyumbani.
 
Back
Top Bottom