Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
- Thread starter
- #201
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ALOBAINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA NANE: Deus alimuhesabia hatua kijana huyu, huku anapapasa eneo lile la mguu na kukamata kisu chake, “nadhani umenisikia vizuri kaka wenzenu washa kufa bado nyie” alisema Deus kumghadhibisha zaidi yule jamaa, “unasemaje we mjinga usinilazimishe nikuuwe” alisema yule jamaa ambae sasa alimfikia Deus na kuvuta mguu wake kisha akapeleka teke la nguvu kuelekea usawa wa ubavu wa Deus, hakika lilikuwa ni kosa kubwa sana kwake, maana hakujuwa kile anachokofanya ndicho Deus alichokihitaji….. …….endelea…. Comment yako na like yako ndio itanifahamisha kuwa hii simulizi kuna watu wanaifuatilia hapa jamii forums, jambo hilo litanipa hamasa ya kupost kwa haraka tofauti na ukikaa kimya no Comment no like itanitia uvivu kwasababu siwezi kujua kama kuna watu wanaoifuatilia... twende pamoja sasa...
Maana kabla hata teke lile halijaufikia ubavu wake, ghafla Deus akaukamata mguu ule kwa mkono wa kushoto na kuufyetua halafu akauvuta kwa haraka na kumfyetua yule jamaa ambae hakuwa amejiandaa kwa tukio lile, na kujikuta akienda hewani mzima mzima na kujibwaga chini, akifuatiwa na mkito wa kisu cha shingo, ambacho hakikusubiri hata sekunde mbili pale shingoni kikachomolewa kwa haraka huku kijana Deus akiinuka kwa uharaka na kupitisha kisu shingoni kwa kijana mwingine aliekuwa amesimama karibu na Deus.
Kisonge pamoja na wenzake wakiwa wameduwaa wasiamini wanachokiona waliweza kuona mmoja kati ya vijana wale akigeuza bunduki yake na kuitumia kama vifimbo au gongo, ambay aliinua juu na kuishusha usawa wa kichwa cha Deus, ambae aliona mapema kitendo kile na kuikwepa ile bunduki huku anazamisha kisu tumboni kwa kijana yule na kukichomolea kwa pembeni akichana sehemu kubwa ya tumbo la kijana huyu, “mpigeni risasi” alisikika Seveline akipiga kelele, wakati huo huo akishuhudia ngumi nzito ikitua usoni kwa Kisonge ambae ilimyumbisha na kumtupa chini, na kabla hajapoa, Seveline mwenyewe akapigwa teke la tumbo lililomtupa mpaka kwenye ukuta wa Don Bosco na kujibwaga chini.
vijana wawili waliobakia, kila mmoja akakoki bukundi yake kwa haraka lakini Deus alikuwa zaidi ya haraka, maana ile mmoja wao anainua bunduki kuelekea kwa Deus, tayari Deus alikuwa ameshamfikia na kuikaata ile bunduki yake akiitazamisha kwa yule mwingine ambae pia alikuwa anaminya trigger kuruhusu risasi itoke.
Ni vitendo pacha, bunduki zote zilitoa risasi kwa pamoja na wale wote wakitandikana risasi bila kutegemea, tukio ambalo Kisonge alilishuhudia kwa macho yake, hakikika lilimtisha na kumuogopesha, maana baada ya vijana wale kupigana risasi na wote kupoteza maisha, Kisonge akamwona Deus akimsogelea Seveline, ambae alipomwona Deus anamsogelea akataka kuinuka na kukimbia, lakini hakufanikiwa hata kusimama, tayari alikuwa amesha fikiwa na Deus, “nadhani kesho utakuwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbali mbali” alisema Deus na bwana Seveline ambae alijaribu kusema jambo, “Tanzania hauko na roho mbay….” lakini Deus hakumpa nafasi ya kumalizia kauli yake, akazamisha kisu kwenye ubavu wa kushoto wa Seveline ambae alitoa mguno wa maumivu.
Kuona hivyo, Kisonge akaona ni vyema kama hatofanya jambo basi na yeye lazima afe, na ukweli ni kwamba, asingeweza kukimbia mbele ya Deus zaidi ya kutumia ujanja na maarifa, “Safi sana bwana Deus, huyo ndio chanzo cha yote haya, umefanya bien kumuuwa mshenzi, alisema Kisonge huku anasimama na kujifuta vumbi kwenye nguo zake, ungesema ni kweli alikuwa anakimaanisha kile alichokuwa anakisema, “nivyema ukatumia muda huu kuomba msamaha wa dhambi zako kuliko kutumia uongo kuongeza siku za kuishi” alisema Deus kwa sauti yake ya taratibu lakini ya kutisha huku anatembea taratibu kumsogelea kijana huyu.
Hapo Kisonge akaona kuwa mambo ni magumu, akawaza akimbie akaona kuwa hawezi kufikambali mbele ya huyu mwanajeshi toka Tanzania hivyo akawaza apige kelele, akaona kuwa kelele hazito msaidia kitu zaidi zita mpunguzia muda wa kuishi na zitamfanya huyu jamaa amuuwe haraka, hivyo, akaona jambo jema ni kutumia ujanja wa kauli kumlegeza Deus achelewe kumuuwa mpaka polisi au jeshi la serikali litakapo kuja na kumuokoa maana aliamini kuwa mpaka muda huo majeshi yatakuwa njiani kufuata mlio wa mlipuko wa risasi ulikosikika, “papaa sisemi uongo nikweli kabisa, hawa watu walitishia familia yangu, ikabidi niwe nao, lakini leo umeniokoa kabisa” alisema Kisonge kwa sauti ya kuomboleza.
Wakati huo tayari Deus alikuwa amesha mfikia Kisonge, “yaani unadhani nitakuacha licha ya yale yote uliyonifanyia” alisema Deus huku anamshika Kisonge kwa mkonoo wa kushoto na kuvuta kisu kwa nguvu lakini kabla hajakipeleka kwenye ubavu wa Kisonge mara kwa ghafla, wakamulikwa na mwanga mkali wa taa za gari, toka upande wa barabara kuu sambamba na gari lililokuwa linakuja upande wao likiwa umbali wa mita kama mia tatu,l toka pale walipo.
Hapo Kisonge akaachia tabasamu moja pana sana, “haya sasa Mtanzania sasa utajibu makosa yako kwa kuuwa afisa wa MONUSCO” alisema Kisonge huku tabasamu la kebehi na dharau , likiwa bado mdomoni mwake macho yake yakimtazama Deus kuona jinsi atakavyokuwa ameingiwa na wasi wasi na pengine kuanza mipango ya kutoroka.
Lakini kitu cha ajabu Kisonge akamwona Deus ambae bado alikuwa amemshika nae anatabasamu, tabasamu ambalo mwonekano wake ni kama tabasamu la simba, “unamzungumzia afisa wa MONUSCO aliefia katikati ya kundi la waasi…..?” aliuliza Deus, huku anasukuma mkono wake wakulia, ulioshika kisu kwanguvu kwenye ubavu wa Kisonge, ambae alisikia kisu kikipenya kwenye mbavu zake changa za upande wakushoto, alitamani kupiga kelele kuomba msaada, lakini sauti haikuweza kutoka akageuza shingo kutazama gari lililokuwa linakuja kwa speed na sasa lilikuwa limekaribia kuwafikia akashtuka kisu kikichomolewa na kupitishwa shingoni mwake.
Hapo hata yeye hakujuwa nini kilifuatia ila sisi tunaweza kumwona Deus akiachilia mwili wa Kisonge ukianguka na kisha yeye kukimbilia kwenye chochoro iliyopo jirani yake, ambapo ile anatokomea tu, tayari risasi zikaanza kumiminwa pasipo kifikiria madhara ambayo yangewapata wakazi wanyumba za jirani.
Gari lilisimama wakashuka askari wa jeshi la serikali, wasiopungua kumi wote na silaha mbali mbali zikiwepo smg na makombora kipimo cha kati yaani RPG, na kuona jinsi miili ya watu ilivyotapakaa pale chini ikiwa na majeraha makubwa miilini mwao, pamoja na silaha zao, tena marehemu wakiwa na mwonekano wa kijeshi tena wanajeshi watoro ni kutokana na mavazi yao, wawili ambao mmoja alitambuliwa kuwa ni afisa wa MONUSCO pale Goma, hakika ilikuwa inasikitisha sana, hasa kwa tukio kama lile kutokea maeneo ya mjini kama haya.
“msakeni huyo muuwaji mpaka tumpate” alisema mmoja kati ya wale wanajeshi wa jeshi la serikali, yani FARDC, wenyecheo cha major ambae alikuwa ameshuka toka seat ya abiria wa mbele, na bila kuchelewa askari wakatokomea vichochoroni kumsaka kijana yule ambae mwanzo alionekana akikimbia kuingia humo vichochoroni.
Naam msako ulianza kwa kasi na mbwembwe za kila namna, lakini hawakumpata kijana yule, zaidi ya kukuta miili mingine mitatu ya watu wanaofanana na wale, yaani wenye muonekano wa kiaskari watoro, ukiachilia wale wawili ambao mmoja alitabulika kuwa ni mfanyakazi wa MONUSCO.
Msako ulizidi kutanuka, na askari kuongezeka, mpaka kufikia msako wa jiji zima la Goma, taarifa zilifika MONUSCO na baadhi ya maafisa wakaenda kuutambua mwili wa bwana Seveline, pamoja na mtu aliekuwa anatafuta na MONUSCO, kwa uchochezi na mipango ovu, yaani kijana Kisonge hakuna alietambua chanzo cha mauwaji haya ya hovyo, wakapanga kufanya uchunguzi.
Wakati MONUSCO wanaendelea na uchunguzi, huku FARC wakiendelea na msako, masako ambao ulidumu usiku kucha, hata kulipokucha msako uliendelea uchunguzi pia uliendelea.******
Saa tatu asubuhi wakati Deus anasindikizwa na major Felix, kuelekea air port kuchek in, bado waliweza kuwaona FARDC wakizunguka ndani ya mitaa ya jiji la Goma, “Deus umeusika na hili?” aliuliza major Felix aliekaa seat ya mbele ya abiria, huku macho yake ameyaelekeza mbele, walikokuwa wanaelekea, yaani upande liliko lango la kuigilia airport lango maalumu la maafisa wa UN, major Felix alionekana wazi kusikia kile kilichotokea jana usiku, mitaa ya bilele hatua chache toka pale walipo, “ningeidhurumu nafsi kama ningeliacha lipite” alijibu Deus kwa ile sauti yake tulivu, Major Felix akatabasamu kidogo, “kazi mzuri” alisema Felix wakati huo gari linasimama mbele ya lango la airport na wakati huo huo likafunguliwa na askari wa SA ARMY na wao wakaingia.
Deus alifanya taratibu za kiusafiri ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa passport mizigo na mwili kisha akaingia ndani ya ndege kusubiri muda wa kuondoka wakati huu tayari major Felix alikuwa amesha ondoka zake kuelekea makao makuu ya MONUSCO.*******
Felix na dereva wake walienda moja kwa moja mpaka ofisini, ambako alikuta mjadala mzito mkubwa juu ya kilichokea jana usiku, kamanda na maafisa wa usalama wakiumiza vichwa vyao kwa maswali magumu, kwanini bwana Seveline, auwawe katikati ya kundi la waasi na kwanini Kisonge ambae alikuwa ametoweka miezi kadhaa iliyopita nae imekuwaje auwawe na wale waasi, na kwanini muuwaji akuchukuwa silaha wala risasi za waasi.
“inakuwaje kama yule askari mtanzania anahusika na hili?” aliuliza mmoja wa maafisa wa MONUSCO, upande wa jeshi huku anacheka kidogo, ilionyesha alifanya utani kidogo, “inawezekana maana mpaka sasa alieonekana eneo la tukio alikuwa ni kijana mmoja tu” alijibu mwingine na hapo wote wakatulia na kutazamana kana kwambavkuna jambo fulani wanalijadiri vichwani mwao, “hilo lipo wazi kabisa je tunaweza kupata habari kwake?” aliuliza mmoja wao huku anamtazama luten kanal toka Tanzania, ambae mpaka hapo alikuwa anaamini kuwa tayari Deus amesha ondoka congo,maana tayari major Felix ambae alimsindikiza Deus airport alikuwa ameshaingia ukumbini, “mh! sidhani kama atapatikana maana tayari yupo safarini, pia hakuna ushaidi ambao unaonyesha kuwa private Deus Nyati anahusika juu hili, maana jana jioni mpaka tunaenda kulala tulikuwanae” aliejibu ni alikuwa ni major Felix na siyo luten kanal.
Hapo makamanda na maafisa wengine wa UN wakatazama kwa macho ya kushuku ukweli wa maelezo ya major Felix, ila kwa kuwa hawakuwa na ushahidi, hawakuwa na lakufanya juu ya Deus, ambae walikuwa na uwezo wa kumzuwia Deus pale Uganda, yaani Entebe airport na kumleta tena Goma, au kutuma watu wafanye nae mahojiano pale pale Entebe.******
Ukweli nikwamba nusu saa ilikatika Deus akiwa ndani ya ndege anasubiri muda wa kuondoka, ukweli ni kwamba aliingia mapema sana kuliko abiria wengine ambao sasa walianza kuingia mmoja baada ya mwingine kwa kuona kwamba amekaa peke yake muda mrefu akahitaji kuchungulia simu yake, lakini ile anatoa simu tu akaona kuna mtu akisimama pembeni yake, hakushangaa wala kujiuliza maana ndege ile ndogo ina safu mbili tu za viti, kushoto na kulia, na kila safu ina muunganiko wa viti viwili viwili, hivyo yeye akatoa simu yake na kuibofya ili awashe data, “habari yako Deus” ilikuwa ni sauti tamu ya kike, ambayo sio kumshtua Deus ila pia ilimsisimua na kumfanya Deus amtazame msalimiaji, ambapo Deus alijikuta akitoa macho kwa mshangao wa kustaajabu.
“hooo nzuri tu mambo… habari za leo….” alisalimia Deus kwa kubabaika, huku bado ametoa macho kwa mshangao akimtazama usoni msalimiaji mwenye kusisimua, ambae sasa alikuwa anaweka vizuri gauni lake na kukaa kwenye seat ya pembeni ya seat aliyokaa yeye.
Huyo alikuwa ni doctor wakike yule ambae majibu yake siku zote hayajawahi kuwa mazuri kwa Deus, “kwa mara nyingine tena ndani ya ndege seat moja safari ya Uganda” Doctor wakike, huku tabasamu pana likiwa limetawara usoni mwake…….…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums