Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ALOBAINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA TISA: maana ukiachilia polisi waliokuwepo pale na silaha zao pia kulikuwa na vijana wawili waliovalia kiraia, pamoja na piki piki yao mmoja ambae ni dereva akiwa amevaa kofia ngumu kichwani, huku mwingine akiwa amevalia suruali ya kitambaa viatu vyeusi na tishert aliyo ichomekea na mkononi akiwa ameshikilia kofia nyeusi ni wale wale ambao aliwaona siku ya tukio la Momadou, “kum…make, ni Kisonge, kumbe huyu mshenzi yupo pale MONUSCO kama mamluki” alijisemea Deus, huku anamtazama kijana yule wa kikongo aliekuwa anatoa maelekezo flani kwa polisi hawa wa serikali ya Congo. …..…..….endelea….


Deus hakutaka kujiuliza sana maana alisha rudi tena uchochoroni na kuaendelea kukimbia kuelekea upande ambao aliamini angeibukia moja kwa moja pale kwenye kituo cha mafuta cha MONUSCO, huku kwa mbali akisikia kelele na maongezi ya polisi serikali ya DRC waliokuwa wanaendelea kumsaka.


Deus ambae leo alikuwa amevalia nguo zake za kiraia anatoa simu yake na kuipiga namba ya Feix, ambayo inapokelewa mara moja, “hallow afande kuna msala huku” aliongea Deus kwa sauti ambayo hakika usingeamini kama alikuwa katika shida kubwa kama hii, ilikuwa ni sauti tulivu na ya taratibu, “kuna nini Deus?” aliuliza Felix kwa sauti iliyojawa na mshtuko mkubwa, “nimeingia kwenye mtego wa yule mfanya usafi, lakini nimefanikiwa kuwakimbia” alisema Deus ambae alikuwa katika mwendo mbwa yaani mbio, “ok! fanya unachoweza hakikisha unafika kambini ukiwa salama na gari liwe salama” alisema Felix na kukata simu, ni wazi alikuwa anaenda kufanya maandalizi ya ujio wa Deus ambae alikuwa anaamini kuwa akishalifikia gari basi lazima angefika kambini muda mfupi ujao.


Deus alikimbia kwa uharaka ndani ya chochoro ngeni za mtaa ule mpaka alipoibukia nyuma ya uzio mkubwa wa ukuta wa mawe, ambapo bila kuuliza alitambua kuwa alikuwa ameshalifikia eneo la kituo cha mafua cha MONUSCO.


Kwa tahadhari kubwa sana Deus aliiingia ndani ya uzio huo akitumia gate dogo kwa kuonyesha kitambulisho chake kwamba ni afisa wa UN, kijana wetu anafanikiwa kuingia mle ndani, ana elekea upade wa mbele wa majengo ya MONUSCO kule ambako aliacha gari lake anaona kuwa ni salama kwake analifwaa gari lake kwa haraka.


Alipolifikia na kuingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka kwa mwendo wa taratibu kulifwa lango la kutokea pale MONUSCO, usingedhania kuwa alikuwa katika matatizo makubwa, hata walinzi waliokuwepo pale getini walimfungulia bila shaka lolote.


Naam kijana wetu alipoingia barabarani, na kuikamata barabara ya mavivi akaongeza mwendo na kuanza kutembea kwa speed kali sana kuelekea upande wa kaskazini mwa mji wa ben, huku akiya over take magari mengine yaliyokuwa yanaelekea upande huo, huku kijana wetu akitafakari kitendo alichofanyiwa na kijana yule mkongo, yaani Kisonge, ambae kwa kumbu kumbu za Deus ni kwamba ukiachilia tukio la jaribio la utekaji nyara wa madoctorta, pia Deus alikuwa na uhakika kuwa huyu kijana wa kicongo, ambae amemwona leo kule panasonoc, ndie mtu aliemwona akipiga simu siku ile ya tukio la Momadou na ndie anaehusika kwa asilimia kubwa kuingizwa kwenye mtego.


Dakika saba baadae Deus alikuwa anaingia kwenye lango la eneo la MONUSCO, pale airport Mavivi ambako alimkuta major Felix na wale maafisa wengine, yaani Luten kanali na yule major mwingine, wakiwa wanamsubiri, nae akawasimulia kisa kizima kuanzia siku ya kwanza anakutana na Sonia na kumsaidia kumpeleka bibi yake hospital pamoja na kuwalipia mpaka kile kilichotokea leo hii, kupigiwa kelele za kwamba yeye ni mbakaji, “nenda katulie chumbani kwako” alisema luten kanal na Deus akaenda chumbani kwake na kujilaza kitandani, hofu ikiwa imetanda moyoni mwake, hata alipojaribu kuperuzi simu yake alishindwa hata kujibu sms za pacha wake, zaidi alianza kuwaza kile ambacho kitamtokea muda mchache ujao pengine kingevuruga kabisa malengo ya maisha yake.


Naam kwakifupi muda mfupi baadae, polisi walifika pale Mavivi wakimuhitaji askari toka Tanzania, Deus Frank Nyati anae tuhumiwa kwa ubakaji, iliwashangaza sana kusikia polisi wakitaja majina matatu ya kijana huyo wa kitanzania, ingekuwa vigumu sana kujitambulisha majina yote hayo kwa mschana anae sadikiwa kumbaka.


Polisi wale walihitaji kundoka na Deus, wampeleke kwenye mamlaka hiyo ya kiraia tayari kukabiliana na mashitaka yaliyokuwa yana mkabiri, hata hivyo MONUSCO ikishilikiana na wakina Major Felix, hawa kukubaliana na swala hilo na baada yake walihitaji kumpeleka wao wenyewe kituo cha polisi na walifanya hivyo, walimpeleka Deus kituo cha polisi wakiwa na ulinzi mkubwa wa jeshi la Tanzania na askari wa jeshi la Nepal, ambao ndio walikuwa na jukumu la Military Polisi yaani MP, pale MONUSCO.


Walifika kituo cha polisi, ambako walimkuta Sonia pia alikuwa analia muda wote kuugulia kubakwa na kijana wa kianzania kwa usimamizi wa major Felix, Deus aliandika maelezo yake pale kituo cha polisi ambao baaae walidai kuwa Deus akae mahabusu mpaka siku ya kwenda mahakamani, jambo ambalo lilipingwa vibaya na Felix, na kusema kuwa Deus ataenda kukaa katika mahabusu zilizopo chini ya UN.


Naam polisi wa Congo walikubariana na Felix, japo haikusaidia, maana Deus alichukuliwa na MP toka Nepal na kwenda kuifadhiwa kwenye maabusu yao, huku akinyang’anywa baadhi ya vitu vyake kama vile simu ya mkononi na viatu mkanda na vitu vingine ambavyo mfungwa hakuruhusiwa kuwa navyo.


Taarifa zilifika makao makuu ya MONUSCO, na wakaagiza kuwa kesi ya Deus iendeshwe katika mahakama ya kijeshi chini ya UN, na siyo mamlaka ya kiraia, siku tatu baadae kesi ikaanza kusikilizwa na shitaka likasomwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya kijeshi iliyoendeshwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za MONUSCO pale mavivi, Deus akisomewa kosa la ubakaji, kosa ambalo Deus alilikataa na kufanya mahakama ihailishe kesi mpaka siku inayofwata, huku ikiagizwa kufika kwa mashaidi siku inayofuata, wakati huo tayari taarifa zilikuwa zimesha fika nchini Tanzania katika makao makuu ya jeshi, hakika iliwasikitisha watu wengi sana waliomfahamu Deus, akiwepo kanal Kasuba japo wapo walioamini kuwa Deus amebaka kweli, siku ile ndiyo siku ambayo Deus aliweza kutumia simu yake kwa sekunde chache, hivyo aliwajulisha wazazi wake kile ambacho kilikuwa kimemtokea.


Ukweli mzee Frank Nyati hakuonyesha kushtuka, baada yake alicheka kidogo na kutoa tamko, “hayo ndiyo maisha mwanangu, kumbuka kuwa kila unapozidi kutenda wema ndivyo unavyo jiongezea maadui”.


Siku inayofuata Mashahidi walifika pale mavivi, wakiwepo polisi watatu, Sonia mwenyewe akiwa na bibi yake, wote wakiwa kama mashahidi, maana kesi kama hii katika mahakama ya kijeshi, haina mlalamikaji, unashitakiwa kutokana na vifungu vya sheria.


Upande wa mshatakiwa aliesindikizwa na MP, walikuwepo wakina major Felix, ambao walimsikiliza Deus akianza kuelezea jinsi ilivyokuwa pale alipokutana na mschana huyo na kumsaidia katika matibabu ya bibi yake na mwisho kuanza kumshawishi kingono, huku yeye Deus akikataa kushiriki tendo hilo, na hatimae Sonia kuamua kupiga kelele za kwamba anabakwa.


Baada ya maelezo hayo mwanasheria wa UN, aliekuwa upande wa mashitaka akamuuliza maswali kadhaa kijana wetu, ambae mengine aliyajibu vizuri na mengine alikwama, mfano kuna wakati alimwuliza hivi, “Deus Frank Nyati tayari uliambiwa mgonjwa ametoka hospital kwa maana amesha pona, sasa kwanini uliendelea kwenda nyumbani kwa Sonia au ulihitaji akulipe fadhila kwa msaada uliompatia?” hapo Deus akaanza kujitetea, “mheshimiwa, nililetewa taarifa na bwana Kisonge kuwa Sonia ameagiza niende haraka kwasababu bibi yake amezidiwa, hivyo anaitaji msaada wangu” alijibu Deus kwa sauti ile ile ambayo muda wote husikika kwa utulivu na upole, “umesema kuwa Sonia amekusingizia kubaka je unadhani ni kwanini mschana huyu amefanya hivyo?” aliuliza yule mwanasheria, “mpaka sasa siwezi kusema sababu ya yeye kufanya hivyo, inaweza kuwa alishawishiwa au alishawishika kutokana na tamaa zake” alijibu Deus wakati huo Sonia bibi yake na wale mashahidi wengine walikuwa wamekaa wanasikiliza kwa umakini mkubwa, Sonia uso ameuinamisha chini.


Maswali yakaendelea, “bwana Deus unataka kuiambia mahakama kuwa Sonia alikudanganya kuwa bibi yake ni Mgonjwa na kama ndiyo Sonia alikuwa na lengo gani?” aliuliza mwanasheria, “mheshimiwa nilidanganywa na lengo la kunidanganya, lilikuwa ni kuniingiza mtegoni” alijibu Deus ambae licha ya sauti yake kuwa ya upole lakini alionyesha kujiamini, nikuulize swali la mwisho, je huo msaada ulioutoa kwa familia ya Sonia ulikuwa chini ya mpango wa shirika gani, la UN, UNHCR, WHO, au?” hapo Deus akajikuta anatabasamu, “ni msaada binafsi mheshimiwa” alijibu Deus, “bwana Deus nadhani ulisoma vyema mkataba wa UN kwa MILROB! hivyo basi ulipokuwa unatoa msaada ulijuwa kuwa nikosa kufanya kazi nje ya mkataba wa UN?” aliuliza mwanasheria swali ambalo, Deus, hakuweza kulijibu. …..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ALOBAINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI: lakini alionyesha kujiamini, nikuulize swali la mwisho, je huo msaada ulioutoa kwa familia ya Sonia, ulikuwa chini ya mpango wa shirika gani, la UN, UNHCR, WHO, au?” hapo Deus akajikuta anatabasamu, “ni msaada binafsi mheshimiwa” alijibu Deus, “bwana Deus nadhani ulisoma vyema mkataba wa UN, kwa MILROB! hivyo basi ulipokuwa unatoa msaada ulijuwa kuwa nikosa kufanya kazi nje ya mkataba wa UN?” aliuliza mwanasheria swali ambalo Deus hakuweza kulijibu. …..…..….endelea….


Baada ya hapo akaitwa shahidi wa kwanza, ambae ni Sonia mwenyewe, ambae alianza kwa kuapa kisha kutoa maelezo yake, akidai kuwa ni kweli alisaidiwa na Deus kwa matibabu ya bibi yake, lakini mwisho wa siku akawatembelea na kuanza kumlazimisha ngono ikiwa ni malipo kwa kile alichowasaidia, ilimsikitisha sana Deus ambae alitamani kungekuwa na mtu mwingine ambae angeweza kusema kilicho tokea.


Sasa ukawadia muda wa maswali kitu ambacho wengi hawakutegemea, ni baada ya kuona mwanasheria wa Deus kuwa ni Major Felix, ambae alisimama na kusogea mbele kuja kuuliza maswali kwa shahidi, kila mmoja alishangaa hata Kisonge aliekuwa nje ya jengo lile anafwatilia swala lile alishtuka sana, na kitu ambacho hakuna aliekifahamu zaidi ya luten kanali na yule major mwingine ni kwamba toka siku ya kukamatwa kwa Deus, Felix na wenzake hawakukaa kimya walifwatilia kila kitu kukusanya maelezo na ushaidi.


“Sonia nadhani unanikumbuka vizuri” aliuliza Felix huku akimtazama mschna huyo usoni, ambae mara tu alipomuona Felix akija kumuuliza maswali alitazama chini.*******


Turudi nyuma kidogo, tuanzie siku ya pili baada ya tukio la jaribio la ubakaji wa kusingiziwa wa bwana Deus Frank Nyati, ambapo asubuhi ya siku ile luten kanali aliwaita wenzake, yaani wakina Major Felix, “jamani sawa Deus ni kijana, lakini sidhani kama ni kweli alijaribu kumbaka yule mschana” alisema luten kanali, ambae kwa tukio lile alikuwa anapokea simu nyingi toka Tanzania, ambazo zilikuwa zinataka atoe maelezo yaliyo nyooka juu ya tukio hilo ambalo lilikuwa linaenda kuidhalilisha nchi, “ni kweli afande, Deus hawezi kufanya hivyo huu ni mchezo ambao, umepangwa na watu waliokuwa wanamtafuta, hasa washirika wa IDFNALU” alisema yule major mwingine, “sasa tuna fanyaje jamani maana hapa kisheria hawezi kukwepa makosa yote, akikwepa la kujaribu kubaka basi atapatikana na kosa la kushiriki jambo bila kibali cha UN” alisema luten Kanali na hapo wakaanza kujadiliana kwa kina.


Majadiliano yalidumu kwa muda wa nusu saa, ndipo walipo pata jawabu la kwamba, wajaribu kufuatilia kimya kimya swala la jaribio la ubakaji, pasipo kuishirikisha MONUSCO, maana ukiachilia kufanya kazi pamoja, pia kulikuwa na upinzani flani wa kiutendaji kati ya mataifa ya liyotoka bara la Africa na yale yaliyotoka mabara mengine.


Na aliepewa jukumu hilo alikuwa ni major Felix, ambae moja kwa moja alianzia nyumbani kwa kina Sonia, lengo likiwa ni kuongea na Sonia mwenyewe na akiwa amebeba zawadi nyingi, kwa wanafamilia wale, maana alijuwa udhaifu wa familia nyingi za watu wa eneo lile, alifika pale nyumbani kwa kina Sonia lakini akakuta Sonia hayupo, ila kulikuwa na bibi yake tu! “shikamoo bibi” alisalimia Felix kwa sauti ya upole na unyenyekevu huku mkono wake wa kushoto, ukiwa umeshika simu yake ya kisasa, na mkon wa kulia akiwa ameshika mfuko wenye zawadi mbali mbali kwa familia ile, “jambo Tanzania karibu sana” aliitikia bibi ambae ni wazi alimtambua Felix, kutokana na lafudhi yake ya kishwahili safi, “asante sana bibi pokea hii ni kwaajili yako” alisema Felix huku anakabidhi mfuko wenye mazaga na bibi akaupokea ule mfuko, “asante sana baba, watanzania mnaroho nzuri sana” alisema yule bibi huku anaingia ndani, akiwa na ule mfuko ambako hakukaa sana, akatoka na kiti kidogo cha jikoni yaani kigoda, “karibu baba” alisema bibi huku anaweka kiti chini, “asante bibi nimesha karibia” aliitikia Felix ambae mpaka hapo alisha ona dalili za kupata ushirikiano katika jambo lililomleta pale mtaa wa Pansonic.


Naam baada ya salam, ndipo major Felix ambae muda wote simu yake ilikuwa mkononi, akaanza kuchokoza mada iliyomleta pale, “bibi naona sasa unaendelea vizuri maana nilisikia unaumwa” alisema major Felix, ambae alikuwa amevaa mavazi nadhifu ya kiraia, usinge shindwa kumtambua kuwa ni kutoka kwenye kampuni au shirika kubwa, “nashukuru baba yangu naweza kusema nimepona kabisa hii yote ni kwaajili ya yule mtanzania” alisema yule bibi na hapo ndipo yakaanza maswali na majibu, “pole sana bibi kwa kile kilichomkuta mjukuu wako Sonia, hivi ilikuwaje?” aliuliza Felix huku anainua simu yake na kuisogeza kidogo karibu na bibi, usingejuwa kama kuna jambo analifanya, “baba yangu weee, hatupaswi kupewa pole ni yule mtanzania mwenye roho nzuri ndie wakupewa pole” alisema yule bibi na hapo akaanza kueleza kilichotokea, huku akimsisitiza Felix kumsaidia Deus, asiingie kwenye matatizo yake ya kusingiziwa.


Baada ya maongezi ya lisaa lizima, ambayo yalimpa Felix habari nyingi muhimu ambazo zinge msaidia katika kesi ya Deus, yani kila kitu kilivyokuwa siku ya tukio, Felix akaaga na kuondoka zake, akisisitiza kwa bibi asimweleze mtu yoyote juu ya ujio wake pale nyumbani, huku akiahidi kuja tena kuwatembelea, ahadi ambayo alitimiza siku tatu baaae, ilikuwa mida ya saa nne za asubuhi kwa bahati siku ile alimkuta Sonia, ambae alipomwona tu Major Felix na kumtambua kuwa alikuwa ni mtazania alishtuka kidogo na kutaka kukataa kuongea nae, “usiwe na wasi wasi Sonia mimi ni afisa wa MONUSCO, nime tumwa kuja kukupa salamu za pole kwa kile kilicho kutokea na tutahakikisha kijana yule anapata adhabu anayostahili” alisema major Felix, ambae kama siku ya kwanza, simu yake ilikuwamkononi ambae nikama alimtuliza Sonia na kukaachini kumsikiliza bwana Felix, “hivi mlikutana vipi” aliuliza Felix na hapo Sonia, akaanza kueleza kama ilivyo kuwa yani vile ambavyo hata sisi tume soma katika mkasa huu.


“sasa kwa nini aligeuka na kutaka kukubaka?” aliuliza Felix, kwa sauti ambayo ilijawa na masikitiko, “si alibadilika tu amekuja hapa akaingia ndani na kuanza kunivuta” alisema Sonia pasipo kubabaika japo macho aliyaelekeza chini, “dah! pole mschana, hivi unasema alikutajia jina lake siyo” aliuliza Felix, huku anamtazama Sonia, na simu yake ikiwa mkononi, “ndiyo alinitajia jina lake, anaitwa nani vileeee…. Anaitwa Deus” alijibu Sonia akionyesha kutokulizowea jina hilo, “ni Deus tu, au kuna jina lingine alikutajia?” aliuliza Felix kwa sauti yake ile ile yenye masikitiko, ambayo ingekufanya usitambue kuwa alikuwa katika uchunguzi, “jina jingine ni mimi ndie nilikuwa na mwita mtanzania jina yake ya nguvu sikuweza kuita mara kwa mara” alijibu Sonia namaanisha yeye akukutajia majina matatu kwamba flani bin flani flani?” aliuliza Felix na hapo mara moja Sonia akajibu, “hapana akuniambia anaitwa Deus nani, yeye alinitajia hilo moja tu”


Naam maongezi haya yalichukuwa muda mrefu zaidi,huku Sonia akieleza jinsi polisi walivyokuja haraka pale nyumbani kwao, yalifikia ukomo na kwa Felix kuaga na kuondoka zake kurudi mavivi.*******


Kiukweli Sonia ambae hakutarajia kumwona Felix, akisimama kama mwanasheria upande wa Deus, ghafla alijawa na uoga kubwa sana kiasi cha kuanza kutetemeka, huku mara kwa mara akimtazama bibi yake aliekuwa amekaa kwenye mabenchi kama watu wengine, ambae muda wote alikuwa anamtazama mjukuu wake kwa macho ambayo tafsiri yake ni ngumu, sijuwi alikuwa anamsisitiza nini, “Sonia unamtambua mtu aliejaribu kukubaka hapa ndani ya mahakama?” aliuliza Felix na hapo Sonia akainua uso wake na kumtazama Deus, “ni yule pale” alijibu Sonia, ambae mara tu baada ya macho yake kukutana na macho ya Deus, akatazama chini haraka, “mtabue kwa majina yake matatu” alisema Felix na hapo Sonia akamtazama bibi yake, kisha akamtazama Felix kama vile alitaka kusema jambo flani lakini akasita kisha akatoa jibu sahihi, “nalifahamu jinalake moja tu anaitwa Deus kutoka Tanzania” hilo ndilo jibu la Sonia.


Baada ya hapo maswali mengine yakaendelea, “Sonia umeeleza kuwa bwana Deus alikuwa anapafahamu nyumbani kwenu kwamba kuna siku alifika pale kukuleta bibi yako akiwa hospital, unaweza kuelezea mahakama kwanini hakufanya ubakaji siku ambayo ulijaribu kuvua nguo mbele yake ndani ya gari ukidai kuna joto, wakati kulikuwa na kiyoyozi ndani ya gari” aliuliza Felix, na swali hilo lilikuwa gumu kwa Sonia ambae alimtazama bibi yake kisha akamtazama Deus, halafu akatazama chini kwa kukosa jibu, “haya Sonia, unaweza kutueleza kwa nini Deus alishindwa kukubaka siku mliyokuwa peke yenu wawili na akaamua kukubaka mkiwa pamoja na bibi?” aliuliza Felix, na swali hilo lilikuwa gumu kwa Sonia.


Baada ya maswali mawili matatu, sasa akaingia shahidi mwingine ambae alikuwa ni polisi ambae aliongoza fumanizi la jaribio la ubakaji, Polisi yule mwenye cheo cha inspector, alianza kwa kuapa, kama ilivyo kawaida, kisha akanza kueleza kuhusu tukio lile, “nikiwa kama kiongizo wa kikundi cha doria, wakati tunapita maeneo ya Panasonic, tukasikia raia mschana mdogo akiomba msaada kwamba kuna mtu anajaribu kumbaka, ndio tukaenda mara moja, lakini hatukufanikiwa kumpata kwasababu aliwahi kukimbia” alieleza yule polisi, ambae baada ya kumaliza maelezo yake ndipo Felix, akaanza kuhoji maswali.


Kama kawaida muuliza mswali alikuwa ni major Felix, ambae alisimama kama mwanasheria wa Deus, “Bwana inspector, kwanza kabisa ningeomba uthibitishe kama mtuhumiwa yupo humu ndani na kama yupo mtambue kwa majina yake matatu” alisema Felix na hapo akiwa anajiamini kwa asilimia zote yule insp akaelekeza uso wake pale alipokuwa amekaa Deus, “yule pale, mtanzania anaitwa Deus Frank Nyati” alisema yule polisi huku anaonyesha kidole pale alipokuwepo Deus.


Hapo maswali mengine yakafwatia, “bwana insp, katika maelezo yako unasema mlikuwa katika doria, mkasikia mtu anaomba msaada kwamba anabakwa, na nyie mkaenda mara moja kwenye nyumba ya tukio, je pale nyumbani kulikuwa na mtu mwingine au walikuwa wao peke yao?” aliuliza Felix, huku akiwa anamtazama yule inspector ambae alitulia kwa sekine kadhaa, kama vile anatafuta jibu au anajaribu kukumbuka jambo, “alikuwepo mtu mwingine bibi yake” alijibu inspector, akionekana kama vile ametoa kwa kubahatisha, “bwana inspector, mlikuwa karibu sana, na nyumba ambayo kulikuwa na tukio, je mliona dalili za kutokea kwa tukio hilo toka mwanzo au kushuku jambo eneo hilo au nikisema ni mpango uliokusudiwa kumsingizia bwana Deus kuhusu ubakaji na mlifika pale tayari mkiwa mnayajuwa majina matatu ya mtuhumiwa” alisema Felix, kwa sauti flani yeye kujaa uchokozi.


Naam hapo yule polisi nikama aliupuuzia uchokozi wa major, kwa maana alisha utambua hivyo alitabasamu kidogo, kisha kwa kujiamini akajibu, “hata kwenye maelezo yangu, ll nimeeleza kuwa mschana aliejaribiwa kubakwa, ndie alie taja majina ya mtuhumiwa sababu alikuwa anamfahamu toka muda mrefu” alijibu insp na hapo nusu ya ukumbi ukatabasamu, kasoro watu wachache sana, ambao kama siyo hawakuelewa maana ya jibu la insp, basi hawakupenda jibu la insp, “mheshimiwa, nadhani wewe mwenyewe umeshuhudia shahidi wa kwanza, yaani bi Sonia, akisema kuwa analifahamu jina moja tu la mtuhumiwa, sasa bwana insp anaweza kutueleza ana mkusudia mschana yupi mwingine? hapo ndipo inspector akagonga ngumi kwa nguvu kwenye nguzo ya kizimba alichosimama ikionyesha wazi kuwa, alishtuka kuwa amekosea hatua. …..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Uko wapi sasa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ALOBAINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI MOJA: na hapo nusu ya ukumbi ukatabasamu, kasoro watu wachache sana, ambao kama siyo hawakuelewa maana ya jibu la insp basi hawakupenda jibu la insp, “mheshimiwa, nadhani wewe mwenyewe umeshuhudia shahidi wa kwanza, yani bi Sonia akisema kuwa analifahamu jina moja tu la mtuhumiwa, sasa bwana insp anaweza kutueleza anamkusudia mschana yupi mwingine, hapo ndipo inspector akagonga ngumi kwa nguvu kwenye nguzo ya kizimba alichosimama, ikionyesha wazi kuwa alishtuka kuwa amekosea hatua. …..…..….endelea….


Na kabla yule insp hajaongea chochote, major Felix akawahi kumtazama hakimu, “mheshimiwa sina swali jingine kwa shahidi.” alisema Felix, na hapo hakimu akaita shaidi mwingine.


Na hapo bibi yake Sonia akapanda kizimbani na kuapishwa kisha akaanza kutoa maelezo, “jamani mimi nitasema ukweli tupu” ndivyo alivyoanza kueleza bibi yake Sonia, kishaakaanza kueleza kuanzia siku walipopewa msaada wa kupelekwa hospital na kijana Deus, bibi alieleza jinsi Deus alivyokuwa anawatembelea hospital kila siku, hata alipowalipia fedha ya matibabu na kuwarudisha nyumbani.


Bibi akaendelea kueleza kuhusu siku ya tukio, ambapo Deus alifika na kukaribishwa ndani na Sonia, “wakiwa ndani nikasikia wanabishana, huyo mtanzania alikuwa anakataa vile Sonia alikuwa anataka wafanye, na huyo mtazania alipokuwa anataka kuondoka ndipo nikasikia Sonia anapiga kelele, mimi sikuona wala kusikia wakati huyu mtazania anajaribu kumbaka Sonia” huo ndi ulikuwa mwisho wa maelezo ya bibi yake Sonia.


Hapo kama waida bwana Felix, akasogelea kizimba ambacho kilikuwa kimesimamiwa na bibi yake Sonia, ambae akuonyesha dalili yoyote ya uoga wala wasi wasi, “bibi nadhani unanikumbuka vizuri sana, vipi unaendeleaje na hali yako?” aliuliza Felix, kwa sauti ya upole iliyojaa urafiki, “salama tu baba, naendelea vizuri” alijibu bibi Sonia, huku usowake ukikunjuka kwa tabasamu la matumaini, lililoashiria kufahamiana na Felix, “bibi katika maelezo yako ya mwanzo ni kwamba, unamfahamu,l kijana alie jaribu kumbaka mjukuu wako, je unaweza kumtambua humu ndani mbele ya mahakama kwa sura na majina yake?” aliuliza Felix, kwa sauti ile ile, ya kirafiki, “ni yule pale mtanzania, jina lake nalisahau mara nyingi” alijibu bibi Sonia, huku akimwonyesha kwa kidole kijana Deus.


Hakika hali ile ya kuongea kwa kujiamini na kiurafiki iliwakera baadhi ya watu, ukiachilia wale polisi na baadhi ya watu waliokuwepo mle ndani, ila pia chuki ilijaa kwa kijana Kisonge, aliekuwa nje ya mahakama anafwatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya mahakama, “bibi, unadhani kwanini kijana huyu ambae hukuwa una mfahamu hapo mwanzo aliamua kukusaidia kukupekeka hosptal na kukulipia matibabu, ni kwamba alikuwa anataka kitu flani kwako au kwa mjukuu wako?” aliuliza Felix kwa sauti ile ile ya kirafiki, bibi alianza kwa kutikisa kichwa, kulia na kushoto kabla hajatoa tamko, “hakuitaji kitu na wala hakuonyesha tamaa ya kitu chochote” alisema bibi akionyesha kuamini kile anacho sema, huku Sonia akimtazama bibi yake kama vile hakutarajia kusikia anachokisema bibi yake, “bibi unaweza kueleza mahakama, ni nani kati ya Deus na Sonia, alie kuwa anajaribu kumshawishi mwenzie wakatende tendo la ndoa siku ile ya tukio?” aliuliza Felix, kwa sauti ile ile ya kirafiki, “nilimwona Sonia akimtaka huyo mtanzania kuingia ndani lakini akakataa kuingia mpaka chumbani, ni Sonia nie aliekuwa anamweleza mtanzania wafanye hapo sebuleni, huyo mtanzania akakataa na mwisho akatakundoka zake, ndio Sonia akapiga kelele aseme anabakwa” alieleza bibi yake Sonia, kwa sauti ambayo ukiisikiliza vizuri, nikama alikuwa anajamb jingine la kueleza.


Nikama Felix, aliliona jambo hilo, “bibi unadhani Sonia, kwanini alifanya hivyo kwa mtu ambae alimsaidia bibi yake?” aliuliza Felix, kwa sauti ile ile ya kirafiki, hapo bibi yake Sonia akatulia kidogo, na kumtazama Sonia ambae alikuwa anamtazama kwa machi yaliyojaa huruma na kuomboleza ni kama alikuwa anajaribu kumzuia asiongee jambo flani, bibi alikwepesha macho yake na kumtazama yule insp wapolisi, ambae alikuwa amemkazia macho kama onyo au katazo kwa bibi, bibi akakwepesha macho yake na kumtazama Felix, huku anatabasamu, “baba hii Congo ninaifahamu kama nitaongea ndio utakuwa mwisho wetu mimi na Sonia” alisema bibi, kwa sauti tulivu huku anaachia tabasamu lenye kukata tamaa kitu ambacho kila mmoja alikiona na kuingiwa na simanzi.


Felix akiwa mmoja kati ya watu walioliona tabasamu lile, aligeuka kutazama hakimu, ambae ni mwanajeshi toka Malawi mwenye cheo cha kanali, “mhesimiwa hakimu kama ulivyomsikia shahidi, ni kweli anahitaji ulinzi baada ya kuelekeza kile ambacho anataka kukieleza, je mahakama yako ina mhakikishia ulinzi?” aliuliza major Felix, na hapo hakimu akasema, “ombi limepokelewa, shahidi na mjukuu wake watapewa ulinzi” alisema hakimu na bibi akaruhusiwa kuongea, “siku moja nikiwa hospital na mjukuu wangu, alikuja kijana mmoja wa hapa hapa Congo na kuongea na Sonia mbele yangu, akimtaka kumshawishi Tanzania afanye tendo la ndoa, ili wawafumanie na wao wasema alikuwa anambaka, Sonia alikataa ndipo yule kijana akamweleza mbele yangu, alisema kuwa watamuuwa endapo atakataa kufanya hivyo, watamuua yeye wataniuwa mimi, nilijaribu kumzuia huyu mtazanaia asiwe karibu na Sonia, lakini haikuwezekana, maana nilishindwa kuongea kwa sauti, nilimpa ishara hata siku ile ambayo alikuja tena nyumbani, nilifurahi sana lakini akadanganywa kuwa mimi ninaumwa ili aje wamsingizie na ndivyo ilivyo kuwa” alisema bibi na hapo Sonia akaangua kilio cha wazi, “bibi umeshatuuwa, wale wa Nalu watatuuwa wote” alilia Sonia kabla hajanyamazishwa na kupewa tahadhari kuwa yupo mahakamani.


Naam Felix, alitoa maelezo yake ya hitimisho “mheshimiwa hakimu, naomba kijana Kisonge afikishwe mbele ya mahakama, ili mashahidi wapate kumtambua, maana yeye ndie mshukiwa namba moja, maana ndie alieleta taarifa za uongo kwa mshtakiwa, huku polisi kingozi aliesimamia zoezi hili, pamoja na wenzake waliopo humu ndani washikiliwe kizuizini, ili kuepuka kuvuruga ushahidi na familia ya Sonia na bibi yake wawekwe sehemu salama, nayo ni kambi la MONUSCO” alishauri Felix, na hakimu alikubari ombi lake.


Naam kibari kilitolewa kwamba maafisa wapolisi washikikiliwe kwaajili ya kusubiri hukumu zao, “pia huyo kijana Kisonge, akamatwe popote pale alipo ili ahojiwe kisha kufikishwa mahakamani, kitu ambacho kilimshtua sana Kisonge, ambae alikuwa anasikilizakila kitu kupitia dirishani, hapo akatazama kushoto na kulia na nyuma, japo aliona watu, lakini walikuwa mbali wakiendelea na shuguri zao, hivyo ni wazi hawakuwa wamesikia lile agizo la kukamatwa kwake.


Kisonge akaondoka pale dirishani haraka, na kuelekea upande wa getini, ambako alitokomea huko akiacha mahakama inaendelea kutolewa maagizo, kwamba mahakama itaendelea siku ya pili, baada ya Kisonge kuwa ameshakamatwa.********


Deus alirudishwa mahabusu ya MONUSCO, inayosimamiwa na MP wa Nepal, huku Polisi watatu, ambao walihisiwa kushiriki udanganyifu wa jaribio la ubakaji, nao wakipelekwa kwenye mahabusu ya jeshi hilo la polisi la serikali huko mjini Ben, ambako tayari taarifa za uhalifu wao, zilikuwa zimeshafika, nao wakasimamishwa kazi mara moja.


Siku ya pili saa tatu na nusu, mahaka ikaendelea, huku Kisonge akiwa hajapatikana, na kufanya kesi iahilishwe, na kutangazwa kuwa itaendelea siku tatu baadae, ili kutoa muda kwa jeshi la polisi, na polisi wa Nepal, wamtafute Kisonge, ambae alitafutwa kila kona pasipo kuonekana, huku siku zote Sonia na bibi yake wakiishi kwenye moja ya jengo la askari wakike, pale Monusco Mavivi.


Siku ya tatu, mahakama ili ahilishwa tena, ni baada ya kukosekaa mtuhumiwa namba moja, ambae ni kijana Kisonge, na hivyo kusogezwa tena week moja zaidi, kijana Deus akiendelea kukaa mahabusu pasipo kuwasiliana na pacha wake, japo siku zile za mahakama, alipata nafasi, ya kuwasiliana na wazazi wake, ambapo wakati flani alimweleza ukweli baba yake, kuwa yeye anawasi wasi kmkubwa wa kufukuzwa kazi, maana licha ya kuonekana hakuwa na hatia, kwa ile kesi kuu ya ubakaji, ila tatizo, lilikuwa ni kwenye kufanya kazi nje ya mkataba wa UN.


“baba naweza kuvunjiwa kataba, na kurudishwa Tanzania, ambako lazima nitafukuwa kazi, na ikiwa hivyo, nitakupa plan uniandalie kitu kwaajili ya maisha yangu yajayo” alisema Deus, ambae alitimiza hilo week mbili baadae, ni siku ya mahakama ambayo haikufanyika kutokana na kukosekana kwa kisonge, Deus alitumia nafasi hiyo kutuma mchoro, ambao alikuwa ameiandaa kwa siku zote alizokuwa mahabusu, alizipiga picha na kuzituma kwa njia ya whatsapp, kwenda kwa baba yake.


Mwezi ulio fwata ambao ni mwezi wa kwanza tarehe za mwishoni, bado Kisonge alikuwa hajaonekana, ndipo mahakama ilipoamua kutoa hukumu yake, kwa kueleza kuwa Deus hakuwa na hatia katika shitaka kuu, ila amepatikana na hatia.….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ALOBAINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI MBILI: Mwezi uliofuata ambao ni mwezi wa kwanza tarehe za mwishoni, bado Kisonge alikuwa hajaonekana, ndipo mahakama ilipoamua kutoa hukumu yake, kwa kueleza kuwa Deus hakuwa na hatia katika shitaka kuu, ila amepatikana na hatia.….endelea….


katika kosa la kujihusisha na shughuri nje ya mkataba wa UN, adhabu yake ni kuondelewa hadhi ya kuwa afisa wa UN, “hivyo basi kuanzia tarehe ya 24 january ya mwaka 2014 private Deus Frank Nyati, ameondolewa hadhi ya uafisa wa UN chini ya MONUSCO, hivyo atatakiwa kuelekea makao makuu ya MONUSCO, huko Goma akafanye utaratibu wa kuondoka chini Congo kuelekea nchini kwake.


Wakati huo Sonia na bibi yake, wakipelekwa Kinshasa, ambako wangeishi kwa msaada wa UNHCR,


kama familia masikini yenye kuhitaji msaada, ambako wange pewa makazi mazuri na pia Sonia angepewa mafunzo ya ujuzi fulani, ambao ungemsaidia kujiondoa katika orodha ya familia masikini na kuishi huko huko Kinshasa, ikiwa ni moja ya usalama wa maisha yao, ambayo yangekuwa hatarini kwa kusakwa na mawakala wa IDFNALU.******


Ilikuwa hivyo, Deus ambae aliongozana na wakina Felix, waliokuwa wamesha maliza majuku yao kule Ben, walindoka mavivi saa kumi na moja alfajili ilikuwa ni mapema sana, ambapo walifika Goma mjini kwenye kambi ya askari wa Tanzania, pembezoni mwa Don bosco, mpakani mwa congo na Rwanda, mida ya saa mbili za usiku, walijitahidi sana, maana kikawaida safari ya ben bhutembo libero, virunga, lutchulu, mpaka kibumba kuingia goma kupitia kibhati,l ni ya siku mbili mpaka tatu, lakini hawa walitumia masaa kumi na tano tu.


Siku ya pili saa mbili asubuhi, ikiwa ni siku ya juma tano, Deus pamoja na wakina Felix walifika kwenye ofisi za MONUSCO, wakiwa na mipango tofauti, wakati luten kanali na yule major mwingine, wakiingia kwenye ofisi ya kamanda wa brigedi kutoa riport za majukumu yao ya huko ben, katika mjumuisho, major Felix aliambatana na Deus, ili kumsaidia kukamilisha taratibu zake za mkataba wa UN, ikiwa ni pamoja na malipo yake, ambayo alitakiwa alipwe siku mpaka tarehe ishilini na nane, tarehe ambayo alikuwa anatakiwa aondoke nchini Congo maana atakuwa tayari nje ya mkataba wa UN, kama angeendelea kuwepo Congo basi angeishi kwa gharama zake binafsi.


Naam siku nyingine ya kukumbukwa kwa Deus ilikuwa ni tarehe ishirin na saba, mida ya saa nane mchana, Deus akiwa ndani ya ofisi za MONUSCO, amesha kamilisha taratibu zote, na kupata malipo yake na alisha pata tiketi ya ndege ya mpaka Entebe, ambako agepanda ndege nyingine ya kuelekea Tanzania, Deus aliagana na Felix, kisha akatoka nje ya jengo na kuanza kutembea kuelekea lilipogeti la lakutokea pale nje ya eneo la MONUSCO, akipanga kwenda kuchukuwa pikipiki, ili aende mjini akafanye manunuzi ya vitu ambavyo vingekuwa kama zawadi kwa wazazi wake huko Tanzania, ndio watu pekee ambao, angeweza kuwafanyia hivyo.
.
Deus ambae alikuwa amevalia nguo za kiraia, alitembea taratibu huku anawaza hili na lile, hasa kile ambacho kitaenda kumkuta nchini kwake Tanzania, maana kitende cha kufukuzwa na kuvunjiwa mkataba na UN, nikulipaka matope jeshi lake isingejalisha kama alisingiziwa au alikuwa amefanya kitendo cha ubinadamu, kitu ambacho UN wenywe wamekuwa wakisisitiza sana umanity.


Lakini wakati anaendelea kutembea, mara macho yake yakaelekea kwenye jengo moja la idara ya mipango na Ushirikiano wa jamii, macho yake yakakutana na mtu mmoja mzee makamo, alie kuwa anamtazama kwa macho makali yaliyojaa kitu kama chuki hivi, Deus alishindwa kumuelewa huyu mtu, hivyo akaamua kuachana nae na kuelekeza macho mbele, kule alikokuwa anaelekea lakini baada ya kupiga hatua chache, akajikuta anajiuliza tena kwanini yule mzee amemtazama kwa macho kama yale, hivy akajikuta anageuka na kutazama tena kwenye jengo lile ambako alimuona yule mzee akiwa bado anamtazama.


Naam safari hii macho yao yalipokutana, yule mzee aligeuza uso wake haraka na kutazama upande mwingine, ilimshangaza sana Deus ambae aliendelea kutembea, huku anajiuliza kwa nini yule mzee afanye vile, lakini alikosa jibu na kuendelea kutembea, japo alipokuwa analivuka geti akajikuta ameshawishika kutazama kule alikotoka akamuona yule mzee akiwa anabofya simu yake na kuiweka sikioni, huku macho yake akiyaelekeza huku getini ambako Deus alikuwepo akitoka nje ambae hakumjali, baada yake alitoka nje huku akisalimiana na askari wenzake toka Tanzania waliokuwa wanalinda lile geti.


Deus alitoka zake nje na kusimama mbele ya geti, akatazama upande wa kulia ambako barabara inaenda kukutana na barabara kuu, iendayo gisenyi mpaka Rwanda, kama angeona pikipiki, itakayoweza kumfikisha mjini, lakini hakuona dalili ya pikipi.


Deus akatazama upande wa kushoto, ambako ndiko kuna Linda hotel, iliyopo pembezoni mwa ziwa Kivu, huko aliweza kuona watu wachache na piki piki moja tu, ambayo ilikuwa imesimama mita kama hamsini toka pele getini, lakini ilikuwa na watu wawili mmoja amekalia pikipi amevalia kofia ngumu, mwingine alia valia kofia nyeusi akiwa amesimama pembeni yake anaongea na simu huku wote macho yao wameyaelekeza kwa Deus.


Ukweli nikwamba yule aliekuwa anaongea na simu, alifanana kwa kila kitu na yule aliekuwa anamwonaga kule ben, yaani yule ambae alipiga simu siku ya tukio la Momadou, “Kisonge” alinong’ona Deus, huku anaanza kupiga hatua kuwafwata wawili wale lakini ghafla akashtuliwa na mlio mkali wa honi huku gari likisimama mbele yake.


Deus akashtuka sana kwa ukosefu wake wa umakini, Deus akainua uso na kulitazama gari lile, lilikuwa ni Toyota land Cruizer jeupe lenye nembo ya UN ya rangi ya blue lenye maandishi ya UN WHO, pia ya rangi ya blue, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, nawakati anawaza hayo mara akaona kioo cha gari lile, upande wa abiria wa mbele kikishushwa huku sura ya abiria ikionekana, sura ambayo ilimfanya Deus asijuwe anajisikiaje, yaani aibu au mfadhaiko, hasa kwa habari ya tukio la jaribio la ubakaji la huko ben, “naona una haraka sana Dereva” ilikuwa ni sauti nyororo tulivu iliyotoka kwenye midomo ya mwanamke mrembo, yenye tabasamu angavu lililozidisha uzuri wa mtabasamuji.


Huyu alikuwa ni Doctor wa kike, yule mhabeshi, hapo Deus akabashiri kuwa kichwani kwa mschana huyu mrembo mwenye kujisikia, kumetawaliwa na fikra kuwa yeye ni mtu mwenye tamaa ya ngono kiasi cha kujaribu hata kubaka, akajikuta anavuta pumzi kwa nguvu na kuishusha kama alivyoivuta, hakuwa na jibu alishindwa kumtazama doctor huyu mwenye sura na sauti nzuri za kuvutia, “dereva habari za siku nyingi” ilisikika sauti ya kiume iliyochangamka toka kwenye dirisha la mlango wa nyuma wa gari lile mali ya Monusco, Deus ambae aliitambua sauti hii akageuza uso wake na kutazama kwenye dirisha hilo, “safi tu doctor, kumbe bado hamjaondoka?” aliuliza Deus, akiachana na doctor wakike ambae alikuwa bado anamtazama kwa uso wa tabasamu, “tupo bwana dereva, japo tunatarajia kuondoka muda wowote” alisema doctor toka Burundi, wakati huo huo ikasikika sauti ya doctor toka Kenya, dereva utapatikana wapi jioni ya leo? ni Muhimu sana nikuone” aliuliza doctor toka Kenya, “sasa hivi naelekea mjini ila jioni nitakuwepo kambini” alisema Deus.


Wakati Deus anaendelea kuongea na madoctor wale mara geti la kuingialia kwenye eneo la ofisi za MONUSCO likafunguliwa, na ilikuwa ruhusa waingie, “ni kweli bwana Dereva, ilikuwa muhimu tuonane kabla hatuja ondoka” alisema doctor kutoka Burundi huku gari linaanza kutembea taratibu kuingia ndani, na ndio wakati ambao, ikasikika sauti ya doctor wakike, “ni vyema kama utakuwa makini unapotembea, vinginevyo unaweza kukosa vitu vitamu huko mbeleni” hapo Deus akamtazama tena doctor wa kike, ambae alikuwa pia bado anamtazama huku ameachia tabasamu pana lenye kulevya hata macho yao yalipokutana doctor wa kike akatabasamu na kutazama mbele kule walikokuwa wanaelekea.


Ukweli licha ya kuwa ni mwanamke mwenye kujipa daraja la juu na kuonyesha ubinafsi, lakini ukweli ulibakia pale pale kuwa mschana yule alikuwa na uzuri wa ajabu, hakika kama Sonia angekuwa na uzuri kama wa mwanamke huyu doctor kijana wetu asingenasuka kwenye mtego ule wakina kisonge.


Deus alilisindikiza gari mpaka lilipopotelea ndani ya uzio na geti kufungwa, ndipo akageuka huku anatabasamu sambamba na kutikisa kichwa kwa masikitiko na ndio wakati ambao, alikumbuka kuwa alikuwa anataka kuwakimbilia wakina Kisonge hivyo akatazama haraka kule ambako, Kisonge alikuwa amesimama anaongea na simu, hakika alichokiona kilimshtua Deus.


Nikwamba siyo Kisonge wala yule jamaa mwingine, wote walikuwa wameshandoka na pikipiki yao, “inamaana hawa jamaa wanampango flani hapa MONUSCO au walikuwa wananifuatilia mimi?” alijiuliza Deus huku anaanza Kutembea kuelekea upande wa kushoto kwake akifuata barabara iendayo ziwa kivu na baada ya mita kama mia moja tu, akaingia upande wa kulia, ambako kuna barabara flani ya vumbi iliyoenda kuibukia kwenye shule flani, ambayo Deus hakuielewa kama ni ya msingi au sekondari.


Kapita na kuibukia kwenye makazi ya watu, ambako kila alipozidi kusogea ndipo mtaa ulipozidi kuchangamka, mpaka Deus alipojikuta anaibuka kwenye mtaa mmoja uliochangamka na kuwa kama uswahilini, nyumba ndogo chache zikiwa zime jengwa kwa mawe, lakini nyingi zikiwa zime jegwa kwa mbao na karatasi za nailon, mtaa huu ni moja kati ya mitaa ambayo ina historia kubwa ya mapigano ya M23 na jeshi la serikali ya mwaka 2013 ambapo, wenyewe upenda kuita bengezi, wakifananisha nakile kilicho tokea mji mkuu wa libia, wakati wa anguko la kipenzi cha Africa Ghadafi.


Baadhi ya nyumba Deus aliweza kuona wanawake wakila aina wakiwa wamekaa nje ya nyumba zao hafifu za hali ya chini, waschana wadogo kwa waschana wakubwa, wakati na wazee, waliokuwa wakimtazama kwa macho ya tabasamu huku vijana wengi wakionekana kuingia pale mtaani na kuzama kwenye nyumba zile wakiongozana na wanawake hao, “karibu we kijana” alikaribishwa Deus, ambae hakuitikia, zaidi aliendelea kutembea na kuelekea uapnde wa mjini.


Deus ambae alikuwa anatembea huku anawaza na kufikiria kitu gani ataenda kufanya huko Tanzania maana alikuwa na uhakika kuwa kinachoenda kumkuta ni kupoteza kazi, alipita mtaa mpaka round about ya chukudu, (sanamu ya mtu aliesimama na baskeri ya miti, yenye rangi ya dhahabu, chukudu ndiyo baskeri ya miti), ambako alipata pikipiki, na kuelekea mpaka soko la Virunga akipitia voda, ambapo alifanya baadhi ya manunuzi na kisha kurudi mjini, karibu kabisa na bhilele, ambapo alitembea kwenye barabara za mjini kuja mpaka karibu na uwanja wa mpira wa miguu wa goma, kisha akaendelea kuzunguka akiwa amebeba begi dogo lenye vitenge na nguo mbali mbali kwaajili ya wazazi wake.


Naam sasa basi mida ya saa moja kasoro, giza likiwa limeshaanza kutanda, Deus akiwa anarudi kwenye kambi ambayo ilikuwa inakaliwa na watanzania iliyopo karibu na Don bosco, akipita barabara iendayo kibati, sasa alikuwa anapita kwenye duka ya bilele, pembezoni mwauwanja wa ndege wa goma, mara akaiona pikipiki iliyokuwa inakuja kwa kusuasua nyuma yake, alipoitazama vizuri akaigundua kuwa ni pikipiki ya wakina Kisonge, Deus akatabasamu kidogo, “wacha nikufanyie wepesi kisonge” alisema Deus huku anatazama upande kushoto ambako kuna uwanja wa ndege, akaona kama upande huo siyo mzuri kwake, akatazama upande wakulia akaona chochoro moja yenye giza ya kati ya nyumba na nyumba zile zenye maduka upande huu wa barabara, hapo Deus akakata kona na kuingia upande ule na kupotelea gizani.


Unajuwa nini kilikuwa kinaendelea, basi hebu turudi siku mbili nyumba siku ambayo Deus aliingia ofisini pale MONUSCO, mara baada ya kuingia goma akitokea ben,……… ….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI UNAO kujia hapa hapa jamii forums
 
Hivi kwa matatizo ambayo kisonge kamsababishia deus mpaka kuvunjia mkataba na kuharibiwa ndoto zake unahisi deusi atamfanyaje kisonge?
Basi musilale leo saa 4 tutaona malipo yake kwa kisonge bamutu ba congo 😅😅
 
Ndo episode moja tu.
Nitaendelea kuisoma baada ya wiki mbili.
 
Hivi kwa matatizo ambayo kisonge kamsababishia deus mpaka kuvunjia mkataba na kuharibiwa ndoto zake unahisi deusi atamfanyaje kisonge?
Basi musilale leo saa 4 tutaona malipo yake kwa kisonge bamutu ba congo 😅😅
Hii saa 5 bado bilabila!
 
Sasa hivi sitaki ujinga wa kuifuatilia sijui hadithi au simulizi flani hivi sijui nini.
Hawa wasimuliaji wanatuona sisi kama wajinga flani hivi.
Kumbe wangeleta simulizi zao kwa wakati wangenufaika wao kwa kupata followazi wengi na kufanya biashara yao baadae.
Wasimuliaji kama huyu ni watu wa kuwapotezea tu.
Yako maisha mazuri nje ya hawa wapumbavu
 
Back
Top Bottom