NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THERASINI NA NANE
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI SABA: hapo ndipo Deus alipo kamata brake za nguvu na kufanya gari lao lisoteshe tairi kwa umbali wa miguu kama ishirini hivi sambamba na kishindo cha “khiiii” huku macho yao wote wanne wakishuhudia mlipuko mkubwa kwenye gari la mbele kabisa uliofuatiwa milipuko mingine kadhaa ya mfululizo, maana kombora moja lili lipua makambora mengine yaliyokuwepo kwenye gari lile la mbele ambalo alikuwa amepanda Kanal Momadou, ambalo ndani ya sekunde kumi tu, lilionekana likiwaka kama kichaka cha nyasi kavu…..…..….endelea….
Huku gari la nyuma ambalo lilifanana kwa kila kitu na lile la mbele, likisimama mitachache nyuma ya lenzake na kusababisha baadhi ya vipande vya mabomu vilivyosambaa toka kwenye gari lililolipuka vifike kwenye gari hilo na kusababisha majeraha makubwa kwa askari wa waliokuwepo ndani ya gari hilo.
Ni kama walipuaji walikusudia kuwamaliza kabisa askari hawa wa FARDC, Mara ghafla zikaanza kulindima kulishambulia lile gari la nyuma risasi, zikigonga kwenye ubavu wa kulia wagari hilo, wale majeruhi wa bomu wakaonekana wakijaribu kujiokoa maisha yao, wakijiangishia upande wa kushoto wa barabara, ambako ndiko kulikuwa salama kidogo, ambapo kuna mmoja wao wakati yupo juu anajaribu kutoka kwenye gari akaonekana akitandikwa risasi ya paja na kutupwa kwanguvu nje ya gari.
Hakika hali ilikuwa mbaya na yakutisha, ambayo iliwashangaza na kuwa shtua sana wakina Felix, ambao walipo angalia hawakuona dalili ya msaada wowote wakuwasaidia kupambana na adui ambae hawakujuwa nguvu yake, kutokana na kwamba risasi zilikuwa zinatokea kwenye kichaka kilichopo pembezoni mwa barabara na ukichulia ni kwamba, wao hawakuwa na silaha ya aina yoyote, na mbaya zaidi ni kwamba, gari lao lilikuwa mia chache sana toka kwenye gari lile lililokuwa linashambuliwa kwa risasi, “Geuza gari tuingie hapo kambini” alisema yule Luten Kanali, akimaanisha kwamba Deus ageuze gari wakaingie kwenye lile kambi la UN lililopo jirani.
Lakini ni kama Deus mwenyewe hakusikia alicho ambiwa, “afande piga simu omba msaada” alipiga kelele Deus huku anafungua mkanda wa kiti, yaani seat belt na kutoka nje ya gari, huku wakina Felix, wakimtazama kwa mshangao, wasielewe kijana wao anataka kufanya nini, huku milindimo ya risasi ikiendelea kusikika, tena ilionyesha wazi kuwa zilikuwa zina pigwa na bunduki aina ya MMG zaidi ya moja.
Jibu ambalo walilipata sekunde chache baadae ni mara baada ya kumwona Deus akichomoka toka kwenye gari na kurukia nje ya barabara upande wa kushoto, akiingia kabisa kwenye mtaro wa pembezoni mwa barabara ile ya lami na kuanza kukimbia, akiambaa ambaa kuelekea kwenye lile gari la nyuma la walinzi wa Kanal Momadou, ambalo japo lilikuwa halijalipuka lakini kiukweli lilikuwa lina tobolewa kwa risasi zilizokuwa zina miminika kama mvua.
“Afande tunafanyaje sasa, maana hatuwezi kumwachia Deus peke yake?” aliuliza major Felix, akionekana wazi kuwa anatamani kwenda kumsaidia Deus ambae alionekana analifikia lile gari lililokuwa lina shambuliwa kwafujo na ndio wakati ambao ni kama yule luten kanal alikuwa amezidika toka usingizini, “tushuke toka kwenye gari haraka” alisema luten kanal huku ana fungua mlango na kutoka nje ya gari upande wa kushoto wa gari hilo, akifuatiwa na wenzake ambao pia walishukia upande huo huo wakushoto, kisha kuchukuwa maficho kwenye mtaro wa barabara.
Wakati huo Deus alielifikia gari, ambalo bado lilikuwa lina shambuliwa na risasi mfululizo, ambapo palikuwa na askari saba, walio jeruhiwa vibaya wakiwa wamelala pale chini, huku wanaugulia maumivu ambapo bila kuchelewa, na kusikilizia zile risasi ambazo zilikuwa zina pigwa kwa fujo upande wapili wa gari yaani upande wa kulia, Deus aliwakokota wale majeruhi na kuwa weka mtaroni, hata wakina major Felix walivyoona kitu anacho kifanya Deus na kwamba upande ule ni salama basi na wao wakatembea kwa haraka kusogelea pale alipokuwepo Deus na walipomfikia na kumkuta amesha wasogeza majeruhi mtaroni nao wakaanza kuwapa huduma ya kwanza kwa kuwafunga majeraha yao, kwa kutumia nguo za wale wale majeruhi, huku risasi zikiendelea kulindima.
Naaam wakati wakina Felix wanaendelea kuwashughulikia wale majeruhi mara ghafla risasi zikakoma, ni wazi washambuliaji waliishiwa risasi kwenye mikanda yao, hivyo kulikuwa kunatokea mambo mawili, moja pengine walikuwa wanabadili mikanda ya risasi, pili pengine waliamua kuondoka zao kutokomea porini.
Hapo hapo Deus akaona kuwa huo ndio wakati wa yeye kufanya jambo lake, kitendo bila kuchelewa Deus akaibukia kwenye bodi ya gari, na kunyakuwa SMG, iliyokuwa mle ndani ya gari ikiachwa na wale askari majeruhi, kisha akaielekeza kule kichakani, kule zilikokuwa zinatokea risasi za adui japo hakujuwa maficho sahihi ya adui zake, lakini yeye akapiga risasi tano hovyo hovyo na kwa haraka.
Nikama alipatia, maana akawaona watu kadhaa, waliovalia sare za jeshi la serikali, wakiinuka na kuanza kukimbia hovyo kutokomea porini, na yeye hakuwaacha wafike mbali baada yake aliibana vizuri silaha yake kwenye usawa wabega, na kufumba jicho moja akioanisha kilengeo cha mbele na cha nyuma, kisha akaanza kuwa donyoa mmoja baada ya mwingine, katika mkadilio wa umbali wa mia mia moja mpaka mia mbili, huku akiwaangusha kama vile anaangusha maembe, japo alifanikiwa kuwapiga wanne kati ya saba alio waona, maana wengine walishazama ndani zaidi ya vichaka virefu.
Kundi la kwanza kufika pale ni magari nane, ya jeshi la Tanzania, yakiwepo magari manne ya chuma yasiyopitisha risasi, yaani APC na mengine ya kawaida, yote yakisheheni askari waliokuwa FBO, yaani Full Battle Oder, kuanzia vazi la combat, body armor (bullet proaf ) kofia ya chuma, bunduki mkononi zikiambatana na mikebe mitatu ya risasi, kama haitoshi magari yote yalikuwa na silaha nzito za kivita, aina ya 12 milimita.
Lakini walikuwa wameshachelewa, maana licha ya kuingia porini, na kufanya msako wanguvu, ambapo waliambulia, miili ya watu wanne waliovalia sale za jeshi la serikali, hawa walikuwa tofauti kidogo na wale wa IDFNALLU wakule ituli, sare zao zao zilikuwa ni za mataifa mbali, tena zilizo chakaa, hawa sare zao zilikuwa safi kabisa, na bora zaidi ambao walipatikana pamoja na simu moja na silaha aina ya MMG, mabox ya risasi ya silaha hizo.
Dakika chache baadae, kikaja kikuni kingine cha FARC, ikiwa ni kombania nzima, ambayo haikuishia pale, waligawana na wengine wakaanza kuwa fwatilia wale waliotokomea porini, ambao baadae walirudi na kusema kuwa hawakufanikiwa kuwapata, huku upande wapili, kwa kutumia simu, akabainika mtu mmoja mwenye cheo cha kanal, (sitoweza kulitaja jina lake kwa sababu za kimahakama, ila chukulia kama hadithi au simulizi), ambae alikuwa ni kiongozi wa kitengo flani cha usalama na utambuzi ndani ya jeshi la serikali, ambae alikamatwa baadae kidogo yeye na wenzake.
Sifa ilizidi kuwa upande wa Deus, ambae alionekana kuwa ni askari mwenye uwezo mkubwa, sifa ambazo alipewa na askari wenzake, hasa kutokana na kuwa na uwezo wa kuchukuwa maamuzi ya haraka na kufanikisha lengo pasipo kuleta madhara kwa upande wake na watu wake, kumbuka Deus licha ya kuwa na ufahamu wa matumizi ya silaha toka utotoni mwake, pia alipata mafunzo ya ucommando na ujasusi, katika vyuo vikubwa vya nchi mbali mbali, zenye ulewa na kupasisha kwa kiwango kubwa sana watu wa aina yake ambao walishawahi kusikika dunian kama wakina Fidel Castor, Che guavala, na wengine wengi.
Hakika tukio la kifo cha kamanda aliebeba imani ya wananchi wengi waliotarajia amani katika nchi yao kutokana uwezo wake katika mapigano, kanal Mustafah Momadou Ndalla, aliekufa na askari wake sita mmoja akiwa dereva, na askari mmoja wakike aliekuwa kama mhudumu wake, kilileta huzuni kubwa siyo tu kwa wananchi wa Congo, ila hata kwa watu wengine toka nchi mbali mbali, waliokuwa wanamfahamu, hasa wale waliowahi kufanya nae kazi kwa ukaribu, wengi wao wakiwa ni wanajeshi wa mataifa ya Tanzania, Malawi, #mbogo_land na Afrika ya kusini.
Yaliongelewa maneno mengi sana, huku wengi wakiamini kuwa ni janja ya kuzuwia mipango ya kusambaratisha kikundi cha waasi wa IDFNALU, huku wengine wakisema kuwa serikali ilihofia kuwa kanal huyu kijana, angeweza kuiasi nchi kama walivyofanya watu kama yeye waliowahi kutangulia mfano Sultan Emanuel Makenga, Lawlent Mkunda, na wengine wengi.
Naam zilipita siku tatu, askari wa majeshi yote yakiwa katika utayari wa asilimia mia moja, huku wakina Felix wakiwa wametulia pale Mavivi, pasipo kwenda mjini, ofisini kwa mayor, hata Deus alishinda chumbani kwake muda mwingi akipanga mipango ya matumizi ya fedha zake ambazo atazipata kwa kipindi cha mwaka mzima, huku pia akiendelea kuchat na pacha wake, ambae alikuwa anasisitiza swala la kukutana kwao pale mschana huyo Pacha aliekuwa anaamini kuwa mchoraji wake yupo dar, na yeye atakapo kuwa Dar, (sijuwi ana maanagani aliposema hivyo), maana pengine na yeye yupo Dar.
Siku ya nne, mida ya saa saba mchana Deus akiwa amejipumzisha chumbani kwake, anaendelea kutumiana sms na pacha wake ndipo aliposikia mlango wa chumba chake unagongwa, “ingia” alisema Deus na mlango ukafunguliwa, akaibuka bwana Kisonge, yule kijana wa kicongo mfanya usafi, aliekuwa amevalia suruali ya kitambaa chepesi, viatu vyeusi vya kuchongoka mbele, na tisht aliyoichomekea vizuri kwenye suruali yake, mkononi akiwa ameshikilia kofia nyeusi.
Ukweli ujio wake ni kama Deus hakuupenda, maana alikuwa ameshaanza kumchukia kijana huyu, toka siku ile ya kwanza, ya tukio la Ilingeti, “naona huko bien unajichatisha na mwasie kitoto ya Tanzania” alisema yule Kisonge, huku anajichekesha chekesha, “kwani kila anaechat anachat na demu?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu, na kavu, Kisonge hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kujichekesha.
“tuyaache hayo bwana Dereva, leo nilikutana na mtu moja kule Ben, ni muschana mrembo hivi anasema bibi yake anaumwa sana, na anakuhitaji ukamsaidie” alisema Kisonge, na kisha akatokanje ya chumba, huku akimwacha Deus, anainuka kitandani kwa mshtuko mkubwa sana, maana alisha sahau juu ya familia hii, “inamana ameanza tena kuumwa?” alijiuliza Deus, huku anawaza namna ya kufika mjini, akawaone watu wale ambao aliwachukulia kama ndugu, maskini Deus hakujuwa nini kimeandaliwa kwaajili yake. …..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao unao kujia hapa hapa
jamii forums