Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THERLATHINI NA MBILI: alisema Deus, kwa sauti yake tulivu, ambae alinekana kuzidi kujiamini, “unaweza kuithibitishia tume hicho unacho kisema kwamba ulikuwa ni mpango wa makusudi?” aliuliza mmoja wa jumbe wale, “ndiyo niliyanasa mawasiliano ya mmoja wa waasi akipewa maelekezo kuwa waondoke haraka, gun ship za UN na Special Force wapo njiani wanakuja eneo la tukio” alijibu Deus na mwisho akaomba kuwakilisha ushahidi. …….endelea….

Na jopo lile likaridhia ombi la Deus Nyati, ambae aliweka ushahidi wa simu aliyoiokota eneo la tukio, ambayo baada ya kuchunguzwa ikabainika kuwa kuna ushirika baina ya baadhi ya askari walikosa uaminifu toka jeshi la FARDC na kudi la waasi wa IFD NALU, katika mpango wa utekaji nyara.

Hakuhojiwa Deus peke yake ila walihojiwa baadhi ya watu waliohusika na safari ile kwa namna moja au nyingine, wakiwemo wale madoctor watatu pamoja na watu walioiratibu ile safari, ambapo ilionekana Deus alikuwa na kila sababu ya kutumia silaha kuokoa maafisa wenzake wa UN, na dawa ambazo zilikuwa zinasafarishwa kwaajili ya wakazi wa Ituli, hivyo kijana huyo mpole na mtaratibu akaonekana kuwa alichukuwa maamuzi sahihi yaliyopo ndani ya sheria.

Uamuzi wa mwisho uliochukuliwa, ni afisa habari wa UN upande wa MONUSCO, kuongea na vyombo ya habari huku pia wakihojiwa madoctor walio okolewa toka matekani ilikuweza kuondoa propagander za kwamba askari wa UN ameuwa raia wa Congo, “lilikuwa tukio la kuhusisha waasi waliotumia makombora mazito kulipua gari la jeshi la serikali, wakatuto kwenye gari huku wakipania kutufanyia vitu vibaya, bahati tulikuwa na askari makini mwenye uwezo wa hali ya juu, akapambana mpaka akatuokoa” alisema mmoja, kati ya wale madoctor.

Hilo lilisaidia kidogo kupunguza tuhuma juu ya kijana Deus, na hata baada ya week mbili kupita, tayari alikuwa amesha sahaulika modomoni mwa watu na wanaharakati wa mchongo, hata maandamano yalikoma kabisa.

Tukio hilo lilimkumbusha mbali sana Frank Nyati, yaani baba yake Deus, ambae licha ya kukubali na kufurahia uwezo mkubwa alio uonyesha kijana wake Deus, lakini pia alikumbuka jinsi serikali ya #mbogo_land ilivyomgeuka na kumwita muasi katika nchi yake, ambayo aliipigania na kuitumikia kwa uadilifu mkubwa.********

Naaam juma mosi moja, mida ya saa mbili za usiku, mtaa wa Jiwe la mwezi, jina hilo lilipatikana kutokana na vipande vya mawe ambavyo viliwai kupatikana miaka ya zaman kwa wingi eneo hilo, miaka ya 1844, wakianini kuwa ni vipande vilivyo meguka toka kwenye mwezi, kutokana na unga’aavu wake, mawe ambayo baadae waligundua kuwa ni madini aina ya Almasi, yaani Diamond ambayo yalikuwa na thamani kubwa sana, na ndiyo sehemu ambayo hapo zamani ilikuwa ndiyo makazi ya mwenye, yaani mfalme kabla ya kuamishia pale GOLDEN EMPIRE, ambako hipo mpaka sasa, historia inasema kuwa kabla hawajafahamu thamani ya madini hayo, walianza kwa kuyatumia kama mapambo kwenye kuta za nyumba zao za udongo zilizo kuwa zina jengwa wakati huo, hasa nyumba za viongozi.

Ila kwa sasa mtaa huu uliotawaliwa na nyumba kumi za kifahari, zenye kilakitu, licha ya kwamba nchi hii, miji yake na vitongoji na mitaa vyote kuwa na viunga vizuri, barabara za lami na zege, lakini mtaa huu ulikaribiana kabisa na makazi ya kiongozi wa nchi, ya GORDEN EMPIRE, au kama wenyewe walivyo zowea kuita, Golden House, ungesema ni kipande cha ardhi au mtaa, ulio nyofolewa huko ulaya, na kuja kupachikwa hapa Mbogo land.

Ndani ya Jumba moja kubwa la kifahali, kati ya yale kumi, yaliyopo mtaani hapo walionekana mfalme wa zamani, King Eric wa pili, akiwa na mfalme wa sasa, yaani King Elvis wa kwanza, kwenye ukumbi wa maongezi wanaongea jambo flani, huku wakishushia kahawa safi inayopatika nchini hapo, “Elvis kiukweli mimi kama mimi, nilikuwa madarakani kama kimvuri tu, babu yako Eugen ndie aliekuwa akiniongoza kwa kiasi kikubwa, ndio maana hata yeye alipozeeka, mimi nikaamua kukuachia madaraka, sababu sikuwa na uwezo wa kuongoza peke yangu, hivyo sielewi chochote na sina uzoefu wa maswala hayo, ambayo kwa kiasi kikubwa niliacha kwa wahusika kama vile mkuu wa usalama wa taifa, na waziri wa ulinzi” alieleza King Eric wa pili, ambae umri wake ulikuwa ni kama miaka hamsini sasa.

Elvis aliekuwa anamsikiliza baba yake, akukubaria na maelezo ya baba yake, “lakini baba lazima unaweza kuwa ulipata hata historia, kama kuna jambo kama hilo liliwahi kutokea na kama lilitokea lilileta madhara gani au sababu ilikuwa nini” alisema Elvis, ambae alikuwa amefanana sana na baba yake, “tatizo ni moja Elvis, sikuwa madadisi wa matukio ya nyuma zaidi nilifwatilia historia ya nchi kwa ujumla, lakini naweza kukushauri, kama una pata muda basi pitia kumbu kumbu zilizoandikwa na wafalme waliopita, unaweza kupata chochote ambacho kita kusaidia, kuliko kumsumbua babu yako Eugen” alisema King Eric.maneno ambayo King Elvis aliyaona kama hayakuwa na msaada kwake, maana licha ya kuwa na tabia ya kusoma kumbu kumbu za wafalme walipita, lakini hakuwahi kuona maandishi yanayofanana na vitu kama hivyo.

Baada ya maongezi yaliyochukuwa lisaa lizima, king Elvi akaaga na kundoka zake, huku akiaidi kwenda kusoma zaidi kumbu kumbu hizo, lakini hakuwa tayari kushirikisha wasaidizi wake, hasa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa #mbogo_land, maana alisha fanya hivyo miezi michache iliyopita, na akiwataka kwenda kuongea na askari ili kufahamu kuna tatizo gani ambalo linawafanya askari kutoroka jeshi, na kitengo cha usalama wa nchi na kazi za siri.*******

Yap! turudi nchini DRC, week nne toka kushindikana kwa jaribio la utekaji nyara, wa madoctor watatu wa WHO, ambalo liliratibiwa na kikundi cha waasi wa IDFNALU, hali ilikuwa imesha tulia, na nikama vile watu walikuwa wamesha sahau kuhusu, tukio hilo, japo MONUSCO walichukuwa tahadhari zaidi kuhusu maafisa wake, hasa wanapokuwa kwenye majukumu na matembezi binafsi, huku Jeshi la ulinzi la Tanzania na raia wake, wakijivunia kuwa na askari mwenye uwezo mkubwa katika mapigano.

Deus akiwa bado yupo kule Mavivi mkoa wa ben, akidhania tayari yupo salama hasa baada ya kuonekana kuwa hakuwa na hatia, kwa shambulizi alilo lifanya aliendelea na maisha yake akifanya majukumu yake vizuri, tayri alisha pata malipo yake ya mwezi wakwanza, kati ya miezi 12 aliyotakiwa kukaa nchini Congo chini ya UN, akiwa anamiliki zaidi ya dollar elfu alobaini na tano, kwa kipindi hicho ilikuwa dollar moja ungebadiri kwa tsh 1800 mpaka 1870, ikiwa ni sawa na dollar 1500 kwa siku, kwamaana hiyo kijana wetu ndoto yake ya kumiliki BWM, ilikuwa inakaribia kutimia, sababu kwa fedha ile aliyokuwa nayo kwa ule mwezi mmoja, ilikaribia million 82 za kitanzania.

Ilimpa moyo Deus wa kukamilisha malengo yake, akiwa na uhakika kuwa atanunua gari analohitaji napengine kujenga nyumba kubwa na mzuri sana, hata kama atachukuwa uamuzi wa kuoa basi atakuwa sahihi, hivyo kijana wetu alitumia wakati wake kupanga mambo yake, huku muda mwingi akiendelea kuwasiliana na mwanamke aliemwita Pacha, ambao urafiki wao ulikuwa unazidi kuongezeka kila kukicha.

Ratiba mpya ya Deus kwa sasa ilikuwa ni kuwapeleka wakubwa wake mjini Ben, kwenye ofisi ya mayor (meya) wa mkoa wa Ben, ambako walikuwa wanavikao vya week mbili na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, ambapo Deus kila alipowa shusha wakubwa wake hao, alienda kwenye ofisi ndogo ya MONUSCO pale Ben na kujaza mafuta, kisha kurudi kwenye ofisi za mayor, na kuegesha gari lake kisha kuanza kutumiana sms na Pacha wake, “hivi mchoraji wangu bishara unafanya saa ngapi, mbona muda mwingi nakuona online?” siku moja mschana ambae Deus alimwita Pacha alimwuliza Deus, wakati wanachati mida ya saa nne hivi, Deus akiwa amekaa ndani ya gari nje ya Jengo la mayor, “sindhani kama biashara inanizuwia kuchat na mtu anaenifanya nisikie baridi chini ya jua kali” aliandika Deus na kutuma, kisha akasubiria jibu.

Ilichukuwa dakika mbili jibu likarudi, ambalo lilikuwa ni vikaragosi kicheko, halafu ikifwatiwa na sms nyingine, “halafu na demu wako atakuwa na kazi gani?” aliuliza mschana ambae Deus alimtambua kama mwanafuzi wa chuo, huko mbeya Tanzania, “wala usiwe na shaka siku nikipata mchumba, kitu cha kwanza nita mweleza kuhusu urafiki wetu” alijibu Deus ambae kiukweli Hakuwa anafahamu hata sura ya mwanamke huyo.

Sekunde chache baadae ukaingia ujumbe wa kikaragosi mchashangao, ikifwatia sms nyingine, “kwahiyo una mwanamke hapo ulipo?” aliuliza pacha, “labda wewe Pacha wangu, ila zaidi ya hapo hata rafiki wa karamu wakike sina” sms hii ilipotumwa, haikuchukuwa hata dakika ikaja sms yenye karagosi kicheko, na kabla haijapoa ikafwaa sms nyingine, “mchoraji wangu tukifunga chuo nitakuja dar nikuone” ile sms ilimfanya Deus atabasamu kidogo, kisha akatulia sekunde kadhaa akitafuta jibu, maana licha ya kuwasiliana na mschana huy kwa muda mrefu, lakini hakudhania kama atatoa wazo kama hilo.

“usijari Pacha, tuombe wote tuwe dar” aliandika Deus, kisha akaituma kwenda kwa Pacha, ambae akutumia muda mrefu kujibu, “unamaana gani, tuombe wote tuwe dar, kwani utasafari?” aliuliza Pacha, hapo Deus akajibu haraka, “huwa situlii sehemu moja, kuna wakati huwa nasafari kwenda Songea kwa wazazi” aliandika Deus na kuituma kwenda kwa Pacha wake wakuzaliwa tarehe moja.*******

Naam siku mbili baadae, mida ya saa mbili asubuhi, Deus aliwashusha wakina Major Felix, nje ya jengo la ofisi za Mayor na kuondoa gari kueleka kwenye mafuta, ambapo ni pembezoni mwa barabara iendayo mavivi, kilomita sita toka kwenye ofisi za mayor, muda aliotumia kuweka mafuta haukuzidi hata dakika kumi, maana gari lilikuwa na mafuta kiasi, hivyo alikuwa kama anajazia tu, na alipo maliza kujazia akaondoa gari kurudi kule kwenye ofisi za mayor, lakini wakati anaikamata njia panda ya Panasonic hotel, akamwona mschaa mmoja mdogo wa miaka kama kumi na saba hivi akiwa amemshika mkono mama mtu mzima alieonekana kuwa katika hali ya uchovu wa mwili ni wazi alikuwa amezidiwa na homa.

Deus alitaka kuwapita lakini roho yake ikasita kidogo na kuamua kusimamisha gari, akidhania kuwa anaweza kutoa hata msaada wa Fedha kwa mschana yule mdogo ili zimsaidie usafiri, pengine ingekuwa bora kama kijana wetu angesikiliza wazo lake la kwanza la kuwaacha wale watu wawili asio wafahamu, unadhani nini kilimtokea kijana wetu, ambae sasa tunamwona akifanya kazi za mipango ya hatari, …..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums

Usiku mwema nyoteeees
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI TATU: Deus alitaka kuwapita lakini roho yake ikasita kidogo na kuamua kusimamisha gari akizldhania kuwa anaweza kutoa hata msaada wa Fedha kwa mschana yule mdogo, ili zimsaidie usafiri, pengine ingekuwa bora kama kijana wetu ange sikiliza wazo lake la kwanza la kuwaacha wale watu wawili asio wafahamu…..…….endelea….
Maana yajayo yana sikitisha, “vipi mdogo wangu, mama anashida gani?” aliuliza Deus baada tu ya kushusha kioo, “bibi anagonjwa namupeleka hospital akatibiwe” alijibu yule mschana ambae kiukweli alionekana wazi anahitaji msaada, maana ukiachilia umri wake mdogo wa kufaa kuwa shule muda ule, pia hata sura yake nzuri ilitia huruma kwa wakati ule.

Hapo Deus Nyati akaona zaidi ya kuwapatia fedha ni vyema angewapelaka hospital kabisa, maana muda ulikuwa bado unaruhusu ukizingatia ndio kwanza ilikuwa saa mbili asubuhi.

Deus akiwa na akili zake timamu, akashuka toka kwenye gari na kufungua mlango wa nyuma wa gari lile mali ya umoja wa mataifa, “ingieni niwapeleke hospital” alisema Deus Nyati, na hakika hapo hata mgonjwa alitabasamu, “Asante baba, mungu akusaidie" alisema yule mama mtu mzima ambae aliitwa bibi na huyu mschana mdogo ambae usingeshangaa kuwa mjukuu wake kwa jinsi walivyo pishana umri.

Mschana mdogo alimsaidia yule mama kuingia ndani ya gari kisha Deus akawasaidia kufunga mlango na safari ya hospital ikaendelea huku mschana yule mdogo, akielekeza njia, ambapo safari iliyotumia dakika kumi na tano ilienda kuishia mbele ya jengo la utawala la hospital ya mkoa wa ben, Deus alishuka na kuwafugulia mlango wagari kisha akamsaidia yule mschana kumshusha bibi yake toka ndani ya gari.

Deus hakuishia hapo, ila aliwapeleka mpaka mapokezi ambako alisimamia malipo ya kumwona Doctor na malipo ya vipimo, ambapo iliishia kwa mgonjwa kupewa kitanda, kwa maana ya kulazwa kwasababu hali yake haikuwa nzuri, hivyo alihitaji uangalizi wa Doctor.

Masaa mawili baadae tayari mgonjwa alisha pumzishwa kitandani na dues akiwa ametumia faranga elfu ishirini na nne, ikiwa ni gharama za kuandisha na kumwona doctor, baada ya hapo Deus akaaga kwa mschana yule mdogo ili arejee kule ofisini kwa mayor, “lakini hatuna chakula, pia natakiwa kwenda nyumbani kuchukuwa nguo nije nikae na mgonjwa” alisema yule binti kwa sauti iliyotia huruma, bila kusita akafungua wallet yake na kutoa noti ya faranga elfu kumi, “itakusaidia, na kesho pia nitakuja kumtazama bibi” alisema Deus huku anamkabidhi yule mschana, ile noti ya elfu kumi.

Hapo Deus akaanza kutembea kuelekea nje ya jengo lile kubwa la hospital, “we mtanzania, hujaniambia unaitwa nani” alisema yule mschana mdogo huku anamkimbilia Deus, na hapo Deus akasimama na kumtazama mschana yule ambae licha ya kumfikia, akaendelea kutembea kuelekea nje, Deus akabaini kuwa mschana huyu alikuwa ana nia ya kumsindikiza kuelekea kwenye gari, “naitwa Deus, wewe inaitwa nani?” aliuliza Deus, huku wanatembea kueleka nje ya jengo hilo la Hospital,”naitwa Sonie, (Sonia) ila unaweza niita Sonii, sijaolewa, naikala na bibi yangu, mama yangu yeye aliondokaga sikumigi, kwa sasa anaikala huko Kampala Uganda” alijieleza Sonia, huku akionyesha sura yenye furaha, tofauti na mwanzo walivyokuwa wanaingia pale hospital.

Waliongea hili na lile mpaka walipofika pale walipoacha gari, wakaagana na Deus akaondoka zake kuelekea ofisi za mayor, ambako alitulia na kuendelea kuchat na rafiki yake Pacha, “hivi Mchoraji wangu, wewe unapenda mwanamke wa aina gani?” aliuliza Pacha, wakati wanaendelea kuchati, “awe mzuri kwangu” alijibu Deus, na kusubiri jibu, ambalo alijuwafika kuwa, lazima litakuja kwa mtindo wa swali.

Nikama alivyo waza, mara baada ya SMS kuingia kwenye simu yake akaitazama na kukutana na swali, “unapenda mwanamke wako aweje?” Deus alitabasamu kidogo kisha akaanza kuandika sms, ambayo ni jibu kwa Pacha wake, “haijarishi atakuwaje japo macho yangu yana ona na nina moyo wa nyama, ila kikubwa ni kwamba, awe ananipenda japo kwa asilimia hamsini, pia tuendane kitabia na mwisho asiwe kikwazo kwa yale niliyo yazowea” alimaliza kuandika Deus kisha akaituma kwenda kwa Pacha, ambapo haikutumia muda mrefu sms ikaingia, Deus akaifungua kwa haraka na kuitazama, “mh! inamaana wewe hujari mwanamke mzuri, mrembo, mwenye shape?” aliuliza Pacha kupitia sms yake, “napenda, lakini sio kwaajili ya tamaa” alijibu Deus ambae hapo hapo akaandika ujumbe, “hivi pacha, unasoma saangapi? mbona muda mwingi unakuwa unachati?” aliuliza Deus kwa sms ikiwa ni kupoteza maswali ya Pacha wake, ambae hata picha yake ya jarida ya Whatsapp ilikuwa ni mauwa rose, “wala haina shida, si unajuwa masomo ya chuo ni juhudi zako mwenyewe” hilo lilikuwa ni jibu la Pacha, ambae siyo tu waliishia kuchat mchana, ila hata usiku wa manane walichati, “nitapungua uzito siku ukiwa na mke, na jua hatuto kuwa pamoja kama hivi” alisema siku moja Pacha wakati wanachati usiku.

Naam Siku iliyofuata Deus baada ya kuwaacha wakina Major Felix pale kwenye ofisi za mayor, akaenda kuchukuwa mafuta kule MONUSCO, ambapo baada ya kuweka mafuta, akaenda hospital kumtazama yule bibi mgonjwa, akiwa ameshapitia sokoni na kununua matunda na vyakula ambavyo vingempa nguvu mgonjwa.

Alimkuta Sonia akiwa na bibi yake, ambae kiukweli alikuwa anaendelea vizuri, mgonjwa alifurahi sana na kumshukuru Deus, “jana nilishindwa kuongea lolote nilikuwa nimezidiwa sana, hakika watanzania mna moyo mzuri sana, asante sana mungu akubariki kijana wangu” mama alitoa baraka zake kwa kijana wetu Deus, ambapo alitumia lisaa lizima kabla ya kuaga na kutoka pale nje kuelekea kwenye gari lake akisindikizwa na Sonia, siku hizo zilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka inakaribia kabisa Chrismass, “naomba unibebe ukaniache kule naenda nyumbani kuandaa chakula cha mchana” alisema Sonia, ambae kiukweli hakuacha kujichekesha, usijari twende nikupeleke, ilinipajuwe nyumbani kwenu” alisema Deus akiwa na nia njema kabisaaaa, kwamba siku mgojwa akitolewa hospital aweze kwenda kumtazama nyumbani.

Waliingia ndani ya gari na kuondoka zao, huku mita chache toka kwenye gate la hospital wakipishana na pikipiki ya kibiashara maarufu kama motor (motoo, inavyo tamkwa) ikiwa imebeba abiria, ambae alikuwa amevaa kofia yenye cap ndefu, aliyoishusha mpaka usawa wa macho, kiasi cha kutufanya tusimwone vizuri, “hebu geuka haraka wafwate hao” alisema abiria, na dereva wa boda boda akafanya kama alivyoagizwa.*******

Naaam nyakati hizo za mwisho wa mwaka ndizo nyakati ambazo, historia mpya ilikuwa imewekwa mshariki mwa Congo ni baaa ya vikosi vya Monusco vya brigade maalumu ya kupambana na waasi wa mashariki mwa congo kufanikiwa kufyeka kikundi kikubwa cha waasi chenye nguvu, cha M23 ikisaidiana na jeshi la serikali, yaani FARDC, ikiongozwa na battalion ya makomando Rejimenti 887, iliyoongozwa na canali mwenye umri mdogo commando Momadou Ndalla wa miaka 33 kwa kipindi hicho. ambae mara baada ya kumaliza mapigano katika ukanda wa kuanzia maeneo ya jirani ya Goma ikiwemo three Tower (minara mitatu) Kibumba, Tchanzo mpaka Lutchuru na Bunagana.

Sasa aliondoka na kikosi chake na kuelekea kaskazini mwa Kivu ya kaskazini, kwaajili ya kupambana na vikundi vingine vya waasi kikiwepo kikundi tishio cha IDFNALU, taarifa hizo za ghafla na za kushtukiza zilipokelewa kwa namna mbili tofauti wapo waliozifurahia, na wapo walioshtushwa na kuchukizwa na ujio huo wa Regiment ya 887, wakiofia ujio wa Momadou Ndalla ambae akuwahi kupoteza vita hata moja, toka ameanza kungoza kikosi hicho cha ma-commando.

“kwahiyo wanakamati wote muwe tayari kwa ujio wa Momadou, ambae kambi yake itakuwa nyuma ya Kambi ya MONUSCO kule Mavivi” alisema Mayor, wakiwa katika kikao cha ulinzi na usalama, na wakina Felix, “lakini mbona kama imekuwa ghafla maana ingekuwa vyema kama angeamabatana na majeshi mengine ya MONUSCO, alisema Felix, ambae anafahamu kuwa licha ya ushindi alioupata Momadou Ndalla, lakini pia alitegemea sana majeshi toka Tanzania, Malawi na South Africa, “hiyo imetushangaza kidogo, lakini nimesha wasiliana na Brigedia thabo tayari baadhi ya kombania za jeshi ya MONUSCO yanafanya maandalizi ya kuondoka Goma, kuja huku” alijibu Mayor, ambae sasa swala hilo aliliacha mikononi mwa maafisa wa jeshi, chini ya MONUSCO.*******

Yap! Deus akiwa njiani na mschana mdogo Sonia, walikatiza mitaa miwili mitatu kabla ya kuingia njia panda ya Panasonic na kukata kulia kueleka mtaani kwa akina Sonia, “nasikia fukuto na mwili unajaa jasho” alisema Sonia ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma ya gari lile, lililopandishwa vioo mpaka juu huku kiyoyozi kikiendelea kupupuma na kuleta kijiubaridi cha kupendeza, “hoo kwa hiyo nizime A/C?” aliuliza Deus, huku anapeleka mkono kwenye kutufe cha hali ya hewa, hakujuwa maana ya fukutobkuwa ni joto, “hapana we acha tu nisikuzumbue” alijibu Sonia, na kumfanya Deus aache kuzima A/C na baada yake akatupa macho kwenye kioo cha kati cha kutazamia nyuma, (back vew) ambapo macho yake yalikutana na kitu ambacho kilimshangaza Deus kiasi kwamba, asingekuwa mahili kwenye kuendesha gari, basi angeivamia moja ya nyumba zlizopo pembeni ya barabara.

Maana kupitia kioo kile cha kati kati, ambacho huwa kina kazi nyingi sana kwenye gari kutokana na aina ya dereva au abiria walio bebwa, Deus hapa akamuona mschana huyu mdogo akiwa anapandisha tishet lake mpaka usawa wa shingoni, na kufanya maziwa yake yaliyotuna na kujaa vyema kifuani kwake, kuonekana wazi wazi, ilishangaza sana, “kumbe unasikia joto, lakini unawezaje kusikia joto wakati kuna baridi kama hii, basi vaa nguo yako ni shushe kioo?” aliuliza Deus kwa mshangao huku akiondoa macho yake kwenye kile kioo kidogo, kwani unadhani mwanamke akisikia joto anasikia baridi?” aliuliza yule mschana mdogo na kumshangaza zaidi Deus, “unazungumzia joto la aina gani hilo Sonia, vaa basi tushushe vioo” alisema Deus huku macho yake yakishindwa kujizuwia kutazama tena kioo kidogo cha kati kumtazama tena Sonia, “usishushe bwana kwani hujuwi joto la mwanamke akiwa na hamu?” aliuliza Sonia kwa sauti tulivu ya kunong’ona, huku akijishika shika chuchu zake zilizochomoza vyema juu ya maziwa yake mtuno na kuziminya minya na kuzivuta kama vile anataka kuzitoa, hiyo ilimshangaza sana Deus, na kutamani wafike haraka nyumbani kwao mschana huyo. ….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa …NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA NNE: “unazungumzia joto la aina gani hilo Sonia, vaa basi tushushe vioo” alisema Deus huku macho yake yakishindwa kujizuwia kutazama tena kioo kidogo cha kati na kumtazama tena Sonia, “usishushe bwana kwani hujuwi joto la mwanamke akiwa na hamu?” aliuliza Sonia kwa sauti tulivu ya kunong’ona huku akijishika shika chuchu zake zilizo chomoza vyema juu ya maziwa yake mtuno kwa kuziminya minya na kuzivuta kama vile anataka kuzitoa, hiyo ilimshangaza sana Deus na kutamani wafike haraka nyumbani kwao mschana huyo. ….endelea…

“Sonia, angalia kama tumefika tusije kupitiliza nyumbani kwenu” alisema Deus huku anakaza macho mbele sasa hakutaka tena kutazama nyuma hata kwa bahati mbaya, hapo Sonia anatazama kushoto na kulia kisha anashtuka kidogo, “tunapia kunyumba, simamisha gari” alipiga kelele Sonia huku anashusha shati lake, na kufunika maziwa yake manono, Deus nae alisha simamisha gari na Sonia baada ya kujiweka sawa akashuka toka kwenye gari kisha Deus akageuza gari na kuondoka zake, huku kichwani akitafakari kitendo cha mschana yule kutoa nguo mbele yake, hakika ilikuwa ni majaribu makubwa.

Ukweli mschana Sonia, licha ya kuwa katika mazingira ya maisha ya chini kidogo lakini kiukweli mschana huyo, alikuwa ni wakuvutia, kuanzia umbo lake na hata sura yake, na kilicho mvutia zaidi Deus ni kile kifua cha mschana huyo mdogo ambae siyo tu kwa sheria za Tanzania na nchi nyingi za Africa, pia hata UN hawa kuruhusu afisa wake kutembea na mschana kama huyo, na siyo tu mschana mdogo, ila UN haikuruhusu afisa wake kushiriki ngono, iwe na afisa mwenzake au mwananchi yoyote wa nchi husika endapo tu siyo mke wake.

Deus akapotezea mawazo hayo na kuendelea kuendesha gari kuelekea barabara kuu ya Mavivi, huku njiani akipishana na bodaboda aliesimama pembeni ya barabara, huku amembeba abiria alieficha sura yake kwa kofia yenye cap ndefu, huku akiitazamisha sura yake pembeni mwa barabara na gari linapopita tu, kijana yule anageuza uso wake, huku anainua kofia yake kulitazama gari na hapo tunaiona sura yake, kuwa ni bwana Kisonge yule mfanya usafi wa MONUSCO Ben Mavivi, “amekwisha huyu mjinga, sasa atajuwa kuwa Congo ni nchi ya wenyewe, na wenyewe ndio sisi”, hviyo ndivyo alivyosema kijana huyu, mfanya usafi wa ofisi za UN kule MONUSCO Mavivi. *******

Yap! Saa sita usiku Deus akiwa anachati na mschana aliemwita Pacha, mara akasikia ngurumo nyingi za magari makubwa kwa madogo yakipita upande wa kulia wa eneo hili la Airport ambalo kwa kiasi kikubwa linamilikiwa UN, sambamba na maongezi ya watu wengine, ni kama walikuwa wanaangalia magari hayo, hata Deus alipochungulia dirishani hakuweza kuona chochote, hivyo akajiinua na kutoka nje kabisa ya chumba chake alichokuwa analala.

Ile Deus anatoka nje, akawaona baadhi ya askari wenzake wakiwa nje wanatazama upande wa magharibi wa eneo hili, ambako kupo wazi kabisa, na pia mchana wake palikuwa pame safishwa na kikosi cha wafilipino, kwaajili ya makazi ya vikosi vya Tanzania Africa ya kusini na Malawi, ambao walitarajiwa kuingia pale muda wowote.

Deus nae akajiunga na wenzake hao, wakiwepo wakina Felix, kutazama upande ule wa magharibi, ambako ukiachilia eneo lililo safishwa , ungekutana na vichaka virefu na miti ya michikichiki, ambako kulionekana msafara mkubwa wa kijeshi la serikali yaani FARDC kikosi namba 887, kilicho ongozwa na Momadou Ndalla, 56
wenye magari makubwa na madogo ukiwa unaingia pale Mavivi, “kazi inahamia huku sasa” alisema Felix, akiwaeleza wenzake ambao walikubariana na msemo wake, “ndiyo hili ni kama shinikizo la nchi za jirani, kwamba MONUSCO itokomeze vikundi vyote vya waasi, yaani IDFNALU na FDRL” alisema mwingine na wakaendelea kuongea, huku wakitazama ule msafara uliokuwa unaendelea kutiririka kutokomea porini, upande wa magharibi.

Wakina Felix wakiwa wanaendelea kuongea, mara akatokea kijana Kisonge, ilimshangaza kidogo Deus, maana Kisonge akiwa kama raia wa kawaida asingepaswa kuonekana ndani ya kambi la jeshi muda ule, “amefuata nini huyu?, au amekuja kwaajili ya kuwapokea hawa wanajeshi? lakini hakuweza kuuliza, baada yake akatulia kimya, “habari za jioni” alisalimia kijana yule ambae kwa umbo ni mwembamba, mwenye kupenda kuvalia suruali yake tumboni, na kukaza sana mkanda wake, “poa dogo mambo vipi?” alijibu luten kanali toka Tanzania, kisha akaendelea kutazama kule yalikoelekea magari, “salama tu naona majeshi ndio yale yanaingia” alisema Kisonge, huku anatazama kule ambako magari yanaelekea, “yes! sasa shughuri inahamia huku, nako kuna hitajika kuwe salama” alisema Felix huku wakiendelea kutazama msafara ule ambao ulikuwa unatembea taratibu, ni kutokana na ile barabara mbovu waliyokuwa wanaitumia, “hakuna usalama hapo, hao wanazidisha machafuko, ni vyema kama wangekaa na waasi na siyo kutumia bunduki” alisema Kisonge kwa sauti kama ya kutokupenda ujio wa FARDC, katika ukanda ule wa Ben.

Iliwashangaza kidogo wakina Felix, na wote wakajikuta wanamtazama Kisonge kwa mshangao, kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akajishtukia, maana aligeuka na kuondoka zake eneo lile, huku wakina Deus wakimsindikiza kwa macho.*******

Naam siku ya pili ratiba ya Deus ilikuwa ile ile ya siku zote, saa moja na robo aliondoka na abiria wake watatu ndani ya Toyota Land Cruizer mali ya MONUSCO, leo msafara uliongezeka kidogo, hawa kuwa peke yao, ila walikuwa na magari mawili ya FARDC, aina ya Toyota Land Cruizer parten yaani nyuma zipo wazi, ambazo kila moja lilikuwa na askari watano wenye silaha nzito pamoja na makambora ya RPG, huku mawili yakati ya hayo likimbeba kanali Momadou, aliekaa seat ya mbele ya abiria.

Saa mbili tayari Deus alisha waacha wakubwa wake pale ofisini kwa Mayor, na yeye akaelekea kwenye mafuta na kisha akaelekea Hospital, ambako alimkuta Sonia akiwa nje ya hospital, akionekana kama mwenye wasi wasi mwingi sana, japo alijitahidi kuficha wasi wasi wake, hata walipoingia ndani kwenda kumwona bibi ambae licha ya kushukuru kwa ujio wa Deus, ambae alibeba matunda na vyakula vingi, lakini nae bibi alionekana kuwa katika hali ambayo ilimshangaza sana Deus.

Maana alikuwa anamtazama kwa jicho flani la wasi wasi na tahadhari kubwa sana, kiasi kwamba, Deus alijishtukia, “bibi kuna tatizo, mbona kama unanitazama hivyo..?” aliuliza Deus ambae kabla hajamaliza kuuliza, Sonia akamkatiza, “Deus twende tuwahi unipeleke kunyumba, nimesahau kuchukuwa nguo za bibi” alisema Sonia huku anamshika mkono Deus, na kuanza kumtoa nje ya ile ward, Deus hakuwa mbishi, akamfwata Sonia, lakini Deus ambae bado alikuwa katika staajabiko la hali ya bibi, alipofika kwenye kizingiti cha mlango, akageuka na kumtazama bibi, ambae pia alikuwa anawasindikiza kwa macho, hivyo macho yao yakakutana na haraka sana yule bibi akaonyesha ishara ya kukataa kwa kutikisa kichwa chache kushoto na kulia, ni wazi bibi kuna kitu alikuwa anakataza, pengine alishajuwa nia ya mjukuu wake ya kutaka kuliwa kitummbua chake na Deus, nadhani ni kwaajili ya kutaka kulipa fadhila kwa kijana huyu.*******

Wakati huo huo ofisini kwa Mayor, kwenye kikao cha makamanda wajeshi na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Ben, leo kulikuwa na ajenda mpya kabisa zilizo badilisha mfumo wa kikao, na utendaji kwa maana kanali Momadou hakuhitaji muda mwingi uishie kwenye vikao vya ndani, baada yake alihitaji kwenda kujiandaa kwaajili ya siku inayofuata na askari waanze kuingia porini, kusaka maficho ya vikundi vya waasi, wazo hilo liliwangwa mkono na wajumbe wote wakikao,

Hivyo ratiba ya kikao ikabadirika, na kuwa mwisho saa nne, na wakati huo huo ikaja taarifa ya kwamba, vikundi vingine vya majeshi ya MONUSCO, vipo njiani vinakuja Ben, na kwamba muda wowote vinaweza kuingia mjini hapo, hivyo nivyema kila mmoja akaenda ofisini kwake akaratibu zoezi linalofwata, na kwamba siku ya pili wakutane asubuhi kama kawaida kupeana mrejesho.

Na wakati kikao kinaendelea ndipo major Felix, akatoka nje kwenda kupiga simu kwa Deus, na kumweleza kuwa leo wanaondoka mapema, hivyo huduma nyingine kama chai watapata mapema sana.********

Deus akiwa na Sonia ambae pia mwonekano wake wa wasi wasi, walifika nje ya jengo la Hospital, pasipo kujuwa kuna watu wanawafwatilia kama ilivyokuwa jana, wao wakaongozana kuelekea kwenye gari, huku Deus bado akiwa anaendelea kutafakari juu ya kile ambacho bibi alikionyesha na Deus kabla ya kufungua mlango akamtazama kwanza Sonia, ambae licha ya umri wake mdogo lakini alijaliwa mambo mazuri, alimiliki umbo pana kiasi, lililoshabihishwa na makalio makubwa kiasi, hips, kifua cha kuvutia na sura yake ya mapokezi. ….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Bora usingeweka kama ndo kipande kimoja tu asee, no mawazo tu usimind
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THERASINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TANO: Deus akiwa na Soniabambae pia mwonekano wake wa wasi wasi, walifika nje ya jengo la Hospital pasipo kujuwa kuna watu wanawafwatilia kama ilivykuwa jana, wao wakaongozana kuelekea kwenye gari huku Deus bado akiwa anaendelea kutafakari juu ya kile ambacho bibi alikionyesha, Deus kabla ya kufungua mlango akamtazama kwanza Sonia, ambae licha ya umri wake mdogo lakini alijaliwa mambo mazuri, alimiliki umbo pana kiasi, lililoshabiishwa na makalio makubwa kiasi, hips, kifua cha kuvutia na sura yake ya mapokezi. ….endelea….

Mh! ilikuwa ngumu kukwepa mtego huo, hasa kwa kijana kama Deus, na ukizingatia alikuwa na muda mrefu hajagusa kitumbua, hivyo akajuwa kuwa endapo ataingia ndani ya gari akiwa na mschana huyo, basi lazima kuna jambo lingelazimika kutokea, Deus akamtazama Sonia ambae sasa alikuwa anashika kitasa cha mlango wa gari tena wa mbele, na kujaribu kufungua nao ukawa mgumu kufunguka, kwa maana ulikuwa umefungwa kwa funguo, “Sonia…” alisema Deus, na kabla hajamaliza kuongea, simu yake ikaita, nae akuzubaa akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa nani, akaona kuwa ni major Felix, hivyo akaipokea haraka, “ndiyo afande” alisema Deus mara baada ya kupokea simu, “vipi umesha toka kwenye mafuta?” aliuliza Felix ambae alionekana wazi kuwa alikuwa nje ya ukumbi, “ndio natoka hapa, vipi mkuu kuna dharura?” aliuliza Deus huku anatoa funguo za gari mfukoni, “yah! kuna mabadiliko kidogo njoo nitakueleza” alisema Felix na kukata simu.

Hapo Deus akaweka simu mfukoni, “Sonia, sitoweza kukupeleka nyumbani maana nimeitwa haraka sana huko ofisini” alisema Deus huku anajipekuwa mfukoni, “lakini huwezi acha kunipeleka natakwenda kuchukuwa nguo za bibi yangu” alisema Sonia kwa kulala mika huku anashika tena kitasa cha gari nakujaribu kufungua, lakini bado mlango haukufunguka, maana Deus alikuwa hajaufungua, “usiwe na wasi wasi Sonia, siwezi kukuacha usiende kumchukulia mama nguo” alisema Deus huku anaingiza tena mkono mfukoni, “mbona sasa hufungui mlango?” aliuliza Sonia huku anajaribu tena kufungua mlango wa gari lakini bado haukufunguka, “sito weza kwenda na wewe, ila chukuwa hii utapanda pikipiki” alisema Deus huku anaibua mkono mfukoni na kutoa dollar tano kisha akampatia Sonia, ambae aliitazama kama vile hakuwa anaihitaji, “lakini..lakini..”alisema Sonia kwa kubabaika, huku akionyesha kukata tamaa, huku akionyesha nia ya kuto kuipokea ile dollar tano.

Hapo Deus hakajuwa kuwa nia ya Sonia ni kwamba yeye aende nyumbani kwao ili akajilie kitumbua, “usijari Sonia nyumbani kwenu tutaenda siku nyingine, nitakaa huko kutwa nzima na nitakula chakula cha mchana” alisema Deus, kwa sauti ya kubembeleza, “sawa lakini ujasema itakuwa lini” alisema Sonia, huku anapokea ile fedha, “nitakujulisha kesho” alisema Deus huku anafungua mlango kwa funguo yake na kuingia kwenye gari kisha akaondoka zake, akimwacha Sonia anamsindikiza kwa macho.*****

Naam saa nne na nusu, tayari wakina Deus walikuwa wameshaingia Mavivi, wakiongozana na magari yale ya FARDC, yaani msafara wa Momadou, njia nzima Deus akiwaza juu ya kile alichokiona kwa bibi yake Sonia na zile dalili za Sonia kutaka kunyanduliwa, lakini bibi amejuwaje, mbona alionyesha ishara ya kukataza, je kunaweza kuwa na tatizo kwa kile ambacho mjukuu wake anakitaka.

Mawazo hayo yaliondoka kichwani kwa Deus, mida ya mchana mara baada ya kuanza kuchat na Pacha wake, ambae sasa alisisitiza kuwa akirudi dar atahitaji wakutane, “nina hamu sana ya kukuona mchoraji wangu” allisema Pacha, kwenye moja ya sms zake, “usijari pacha ila isije kuwa ndiyo mwisho wa urafiki wetu maana unaweza kushtuka kwa jinsi nilivyo wa ajabu ajabu” hilo lilikuwa jibu la Deus, ambae alitumia muda mwingi kuchat na Pacha wake, ambae alimzowea kiasi kwamba hata wakati anapo mkosa hewani, aliona kama amemkosa mtu muhimu sana, kama ilivyokuwa kwa huyo pacha wake ambae alionyesha dalili za wazi za wivu, pale anapo mkosa rafiki yake huyo, “unapokuwa kwenye mambo yako ni bora uwe unaniambia kabisa, siyo kunigandisha hewani” daima Pacha alituma ujumbe wenye maneno makali, “Pacha umesahau kuwa kazi zangu za kuzuruta juani, huwa zina nisahaulisha simu” Deus angedanganya hivyo.

Basi hapo Pacha angetuma ujumbe ukitanguliwa na vikaragosi kicheko, “hoooo! sorry mchoraji wangu, nilisahau, nilijuwa umeenda kukutana na mademu” na Deus pia angerudisha vikaragosi kicheko.*****

Naam siku ya pili ikiwa ni siku moja kabla ya Christmass, Deus hakupata kabisa muda wa kwenda kumwona mgonjwa kule Hospital, maana wakubwa wake yaani wakina Major Felix, hawakukaa sana pale kwenye kikao, wakalazimika kurudi kambini Mavivi, kwaajili ya kuyapokea majeshi ya MONUSCO, hasa lile la watazania wenzao, ambapo walikuwa wepesi wa vitendo, maana licha ya kuingia mida ya saa sita mchana lakini mpaka saa nane, tayari walikuwa wamesha jenga mahema yao ambayo hutumika kama nyumba na tayari walishasimika majiko na chakula kilikuwa kinaendelea kuiva.

Kwaujio wa kikosi hicho cha Tanzania, tayari Deus alishakutana na wenzake aliowazowea, japo ilikuwa ni kama story au kivutio cha utalii kwa baadhi ya askari, ambao walihitaji kumwona na kumuuliza jinsi ilivyokuwa, japo ilikuwa nivigumu sana kumuingia na kuulizia habari hiyo, kutokana na upole wa kijana huyo, japo mara moja moja ungemkuta anaongea na wenzake na kucheka nao kwa pamoja, japo wenzake pia walimwona wa tofauti kidogo ni kuhusu kushiriki mkataba wa umoja wa mataifa akiwa kama Military observer.*******

Siku iliyofwata ilikuwa ni sikukuu, ambapo Deus alitoka kuwapeleka wakina Major Felix mjini, ambako walienda kutembea na kutazama mazingira ya mji wa Ben, ikiwa ni kama kuenjoy Chrismass, na siku ya pili pia ilikuwa hivyo hivyo, japo siku ile walishinda sana kambini kutokana na kwamba makamanda wakuu wa vikosi na wakina major Felix, walikuwa wanakutana na kupanga mikakati ya kuanza kusakama vikundi vya waasi wa IDFNALU.

Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kuendelea na majukumu kama kawaida, siku ambayo ni miongoni mwa siku ambazo siyo tu Deus peke yake ila na wa congo na ukanda mzima wa Africa ya kati hawato zisahau.

Ilikuwa kama kawaida, asubuhi Deus aliondoa gari mavivi akiongozana na magari mengine manne ya MONUSCO, mawili yakiwa ni Amoured Personer Carrier, yaani APC, moja likiwa mbele moja nyuma, ndani kukiwa na askari kumi na moja kila gari, mmoja akikaa kwenye silaha kubwa yenye mzingo wa mm12 yenye kutumia umeme, ukiachilia dereva na mtoa amri wa gari hilo, pia nyuma walikaa askari nane wenye silaha aina SMG modol 81,

Pia ukiachana na magari hayo ya chuma, kulikuwa na gari jingine aina ya Nissan lililowazi nyuma, nalo lilibeba askari watatu, wawili wakiwa na asilaha ndogo aina ya SMG ya mwaka 56, na mmoja akiwa amesimama nyuma ya silaha aina ya MMG, ambayo ilifungwa kwenye kiegemeo chake nyuma ya gari hilo, ikiwa na uwezo wa kuzunguka mzunguko wa 360, huku ikishambulia pia kulikuwa na land rover Pumer, lililombeba mkuu wa kikosi cha askari wa miguu toka Tanzania, pamoja na hayo, lilikuwepo gari la wakina Deus.

Leo katika msafara huo, hapa kuwepo magari ya wakina Momadou, wao tayari walikuwa wameshatangulia muda mrefu na siku ile baada ya kufika eneo husika na kuwashusha vingozi hao, ambao waliingia mkutanoni, magari yote ya UN yakaekelea kwenye mafuta Deus akiwa anawaongoza na kwa kuwa mlolongo wa magari yalikuwa mengi, na yalihitaji kutia mafuta mengi, basi Deus akatumia nafasi hiyo kwenda Hospital kumtazama mgonjwa, ambae alikuta amaesha ruhusiwa lakini amekwama fedha ya kulipia gharama za matibabu na huduma zote alizopewa.

Ilikuwa kama bahati kwao, maana hata walipomwona Deus walitabasamu kwa matumaini na kama walivyotegemea, Deus alilipia matibabu yote na kuwalipia taxi wakaenda nyumbani, nae akahaidi angewatembelea, week inayofwata, kule nyumbani kwao, nae akaondoka zake kurudi kwenye ofisi ya Mayor.********

Yap! ndani ya kikao leo kulikuwa na mpambano mkubwa wa hoja zikiibuka pande mbili zenye mtazamo tofauti kuhusu kuanza kwa operation ya kuwasaka waasi wa IDFNALU, wakati makamanda wa majeshi ya ulinzi yanayounda brigade ya MONUSCO pamoja na kanali Momadou wakisaidiwa na baadhi ya wajumbe wakiraia wakisisitiza kuwa kazi ianze mara moja, huku baadhi ya wajumbe wa kiraia ambao wengi wao ni viongozi wa majimbo ya mkoa huu wa Ben wakisaidiana na baadhi ya makamanda wa jeshi wenyeji wa mkoa huu wa Ben, wakisisitize vikosi visubiri kwanza na itakuwa vyema endapo waasi wakaalikwa kuongea na serikali, ili kujuwa shida yao nini, na serikali itatue shida zao ilikumaliza migogoro na vita ndani ya kivu ya kaskazini.

Lakini licha ya ubishi na ushawishi wa kiasi wa upande wapili, mwisho wakakubaliana kuwa kazi ya msako ianze mara moja, huku kanal momadou, akisema kuwa leo hii baadhi ya vikundi vyake vya kijeshi, vinaelekea starting are, (sehemu ya kuanzia) wakati huo mkuu wakikosi cha Tanzania, akisema kuwa muda mfupi ujao, atatuma kikundi kidogo, kwenda doria ya uchunguzi kwaajili ya kutazama njia za kupisha mizinga na magari ya deraya kwaajili ya kuendelea kusaka waasi, wakati wanasubiri vikundi vya Malawi na afrika ya kusini viwasili Ben.

Air Force nao hawakubaki nyuma, wakasema wataalika gun ship kwaajili ya kuanza kushambulia sehemu shukiwa zote, ili kama kuna waasi, wafie humo, au kujitokeza hadharani na kudhibitiwa kirahisi.******

Naam Deus ambae hakuwahi kujiuliza kwa nini yule doctor wakike hakumwambia hata asante, wala kumsogelea mara baada ya kufika mavivi, aliendesha gari kwa umakini kuelekea kule kwenye ofisi za mayor huku kichwani kwake akiwaza na kuwazua jinsi atakavyokuwa anamiliki gari la ndoto yake yaani BMW, ambalo ataliegesha nje ya jengo moja zuri na kubwa la kifahali, ni mara tu baada ya kurudi Tanzania, pale mkataba wake na UN utakapo kuwa umeisha.*******

Lakini wakati Deus anakaribia ofisi za jiji yaani kwa Mayor wa Ben, ndipo alipoiona pikipiki iliyokuwa imesimama upande wa pili wa barabara pembeni ya safu ya maduka yaliyotazamana na jengo kubwa la ofisi za mayor, ikiwa na watu wawili, mmoja ambae ni dereva akiwa amevaa kodia ngumu na kushusha kioo cheusi cha mbele, nakufunika sura yake huku kijana mwingine, ambae kwa muonekano ni mwembamba, aliekuwa kama abiria kwenye pikipiki ile……..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Shukrani
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI SITA: Lakini wakati Deus anakaribia ofisi za jiji yaani kwa Mayor wa Ben ndipo alipoiona pikipiki iliyokuwa imesimama upande wa pili wa barabara pembeni ya safu ya maduka yaliyotazamana na jengo kubwa la ofisi za mayor ikiwa na watu wawili, mmoja ambae ni dereva akiwa amevaa kofia ngumu na kushusha kioo cheusi cha mbele, nakufunika sura yake, huku kijana mwingine, ambae kwa mwonekano ni mwembamba, aliekuwa kama abiria kwenye pikipiki ile……..….endelea….

Akiwa amevalia suruali ya kitambaa chepesi ambayo mkanda wake aliufungia tumboni, shati alichomekea vyema na kupendezeshwa na viatu vyake vya ngozi vyenye kung’aa kwa rangi ya ngozi ya chatu, kichwani akiwa ameivalia kofia nyeusi ya cap aliyoishusha mpaka usawa wa macho yake…kiasi kwamba hata uso wake usingeweza kuonekana vyema “ni mara ya pili nina muona huyu jamaa” alijisemea Deus huku anaingia kwenye lango la kuingilia kwenye ofisi za mayor.*******

Naam saa nne kasoro ndio mida ambayo kikao kiliisha, makamanda wote wakikubaliana kuwa kazi ya msako ianze mara moja, hivyo mara baada ya kutoka kikaoni, watanzania ambao walitakiwa wakaaandae kikundi cha doria ya kiuchunguzi wakaondoka mara moja kueleka Mavivi kwa mpango wa msafara kama ule wa asubuhi, kasoro gari moja tu la maafisa MILOB (Military Observer) ambao walikuwa wanamalizia baadhi ya mambo pale ofisini kwa Mayor, na dakika kumi baadae msafara wa kanali Momadou nao ukaondoka zake ukielekea njia ile ile ya Mavivi ambako ndiko kikosi chao pia kilifikia.

Lakini wakati msafara wa magari mawili ya kanal Momadou yakiwa yanaondoka pale kwenye viunga vya ofisi za mayor, Deus aliekuwa anawasubiri wakuu wake, akayasindikiza kwa macho huku zikimjia kumbu kumbu za msafara wa WHO, alipokuwa anawapeleka wale madoctor, Deus anakumbuka askari wa jeshi la serikali walikuwa na silaha kama hizi lakini mwisho wake wakaishia kuwatelekeza porini Ilingeti.

Naam wakati Deus aliekuwa anayasindikiza magari yale mawili yaliyobeba wanajeshi wa jeshi la ulinzi la serikali ya jamuhuri ya kidemocrasia, ya watu wa congo yaliyokuwa yanakatiza mbele ya nashika uelekeo wa kulia kuifwata barabara kuu iendayo goma na ilingeti, mara macho yake yakakwama kwa yule kijana, abiria wa pikipiki alievalia kama wale wamusic wa kizamani wa boringo, akiwa anatoa simu haraka na kuibofya kwa haraka kisha akaiweka sikuoni, ambapo hakutumia hata sekunde tano, akawa tayari ameshamaliza maongezi, kisha akaiweka simu mfukoni halafu wakamweleza jambo yule dereva wa boda boda kisha wakapanda piki piki yao na kuondoka zao.

Deus alihisi jambo lisilo la kawaida kwa jamaa yule ambae kiukweli licha ya kuhisi kuwa siyo mgeni machoni pake, pia simu aliyoipiga haikuwa na usalama kwa wenzao, kati ya kundi la kwanza la watanzania au hili la pili la Momadou, Deus kwa kuhisi hivyo alitamani awashe gari na kuifukuzia ile pikipiki ili akamtazame yule jamaa mkanda nje aliejificha sura yake kwa cap ya kofia yake na dereva wake alievalia kofia ngumu.

Lakini wakati Deus anawaza hayo mara wakina Major Ferix wakatoka ofisini na kuingia ndani ya gari ilikuwa ni dakika tatu tu toka msafara wa pili uondoke yani ule wa Kanal Momadou, “samahani afande fungeni Mikanda” alisema Deus, ambae licha ya kuwa ni kawaida yake kumweleza mtu anaepanda gari kufunga mkanda, ila kwa safari fupi au akiwa na wakuu wake mara zote hawezi kuwaeleza swala hilo, hasa ukizngatia kuwa ingekuwa ni sawa na kuwapa amri vingozi wake na hiyo ni utovu wa nizamu kijeshi.

“haya jamani tufungeni mikanda, dereva leo anafwata sheria za chuo” alitania yule luteni kanali huku anafunga mkanda wa seat, yani seat belt, na kwa kuwa yeye ambae ni mkubwa alisha sema, basi wakina Felix wakafwata kufanya hivyo baada ya kuhakikisha wamesha funga mikanda yao, hapo Deus ambae tayari alisha funga mkanda wake akaondoa gari taratibu kutoka kwenye viunga vya jengo la ofisi za mayor, huku wakina Feilix wakijadiri na kuzungumzia jinsi mpambano wa ubishani uliojitokeza kwenye kikao juu ya ufanyike msako au waasi wakae na serikali wamalize tofauti zao.

Lakini story zao hizo hazikuchukuwa muda mrefu, kabla hawajatulia nakuanza kusikilizia mwendo ambao, Deus alikuwa anaendanao, mara baada ya kuikamata barabara hakika mwendo ulikuwa ni mkali sana yani ni mkali kiasi kwamba usingefikiria kuwa wanatembea katikati ya mji, maana walitembea mwendo wa kilomita mia themanini kwa saa huku akipiga honi kwa fujo, kuomba njia, nadhani pia walioko ndani hawakujuwa kuwa amewasha taa kubwa, “mh! Deus vipi mbona kama mwendo ni mrefu utadhani kuna tukio tunaliwahi?” aliuliza luten kanal, huku akimtazama kwa macho ya tahadhari, “ni bora nacho kiwazakiwe tofauti afande” alisema Deus huku anapunguza mwendo kwa gafla na kuingia barabara kuu iendayo mavivi.

Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kilicho sababisha gari kuburuza tairi zake za nyuma, na kuzifanya zisote na kuseleleka huku tairi za gari hilo zikitoa sauti ya mbinja na kuwafanya watu walioshuhudia wapige kelele za shangwe la kishabiki, “Deus unamaana gani?” aliuliza luten kanal kwa sauti ya mshtuko, “kuna watu wanafwatilia msafara wa kanal Momadou nadhani hawana nia njema hata kidogo” alisema Deus huku analiweka gari sawa na kukanyaga mfuta kwanguvu na kulifanya gari lizidi kukimbia, “wapoje hao?” aliuliza Felix, huku wote wakitazama barabara, na macho yamewatoka kwa hofu ya kupata ajari, “vijaa wawili, wapo kwenye piki piki mmoja amevaa kofia nyeusi” alisema Deus ambae muda wote alikuwa makini na barabara na kila waliposogea mbele kuliacha jiji, ndiyo idadi ya magari na vurugu za barabara zilipungua na kufanya gari likimbie bila wasi wasi wowote.

Lakini wakati wanavuka daraja wakawaiona pikipiki ikiwa imelala kati kati ya barabara, huku watu wawili wakiwa wakiwa pembeni ya piki piki hiyo mbele na nyuma ya ile pikipiki, mmoja akiwa amevalia kofia nyeusi kichwani, wakiachia njia ndogo sana upande wa kulia wa barabara, wakijaribu kuinua pikipiki, ilionekana wazi kuwa walikuwa wamepata ajali, “Deus watu wako hao hapo wamepata ajali” alisema luten kanal ambae bila shaka alitegemea kwamba Deus, angepunguza mwendo, ili waweze kufanya jambo linalofaa kama siyo kuwasaidia kutokana na ile ajali basi ni kufanya nao mahojiano kwanini walikuwa wanafwatilia safara, lakini mawazo yake yalikuwa tofauti, maana Deus hakupunguza mwendo wala kuonyesha dalili ya kupunguza mwendo, “ni mtego huo afande inaonyesha kuna tukio huko mbele, hushangai kama ni ajali lakini pikipik haina dalili ya kuharibika popote” alisema Deus ambae wakati huo kwa ufundi mkubwa sana aliyumbisha gari kulia mwabarabara, kuikwepa pikipiki na kufanikiwa kupita kwa speed kali na kumfanya yule jamaa wa upende wakulia wa barabara aruke kwa hofu ya kunusurika kugogwa huku mwenzie alievalia kofia akilisindikiza gari kwa macho ya mshangao, huku wakina Felix wakibakia midomo wazi wasijue wamepitaje kwenye sehemu ile ndogo.

Naam safari iliendelea na gari lilizidi kushika moto, makamanda wamejawa na hofu ya mwendo wakiombea gari lisije kupata hata pacha ya bahati mbaya, maana kingewatokea kitu ambacho kingesababisha wasitambulike walikuwa wangapi na jinsia gani, kwa jinsi ambavyo wange sagika.

Naam dakika tatu baadae wakiwa wanalikaribia, kambi dogo la UN, (Siyo kambi la air port Mavivi), hapo nipo walipo yaona magari mawili ya jesi la serikali ya kiwa mbele yao yanalivuka lile kambi la UN, “jamaa waleee” alisema luten kanal, huku anatarajia kuona gari lao likipinguza mwendo, lakini ndiyo kwanza Deus akazidi kukanyaga mafuta kwenye ile tambalale ya kama mita miatatu kasoro kuwafwata wakina Kanal Momadou, ambao muda wote wakiwa kwenye msafara wao daima hutembea mwendo mkali.

Hapo lazima uelewe yaani licha ya msafara wa Momadou kuwa spee kali, lakini Deus alizidi kuwa sogelea kwa haraka, ungesema walikuwa wamesimama, “Deus hii ni amri, punguza mwendo” alisema luten Kanali kwa sauti ya ukali wa hali ya juu, lakini haikusaidia bado mguu wa Deus ulikuwa umeng’ang’ania kwenye pederi ya mafuta ni kama vile alikuwa ameambiwa aongeze mwendo.

Naam wakiwa wamebakiza mita kama mia mbili kuwafikia mara gafla, ukasikika mlipuko mita chache ndani pori lililopo pembeni ya barabara, ikifwatia mlio kama wa mluzi, ukiambaa hewani, hapo ndipo Deus alipokamata brake za nguvu na kufanya gari lao sitoteshe tairi kwa umbali wa miguu kama ishirini hivi sambamba na kishindo cha “khiiii” huku macho yao wote wanne wakishuhudia mlipuko mkubwa kwenye gari la mbele kabisa uliofuatiwa na milipuko mingine kadhaa ya mfululizo maana kombora moja lili lipua makombora mengine yaliyokuwepo kwenye gari lile la mbele ambalo alikuwa amepanda Kanal Momadou, ambalo ndani ya sekunde kumi tu, lilionekana likiwaka kama kichaka cha nyasi kavu…..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums
 
Imenoga
 
Back
Top Bottom