Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHILINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NNE: Naam! kijana Deus akiwa anaamini amesha kaa mbali na sehemu ambayo yupo yule mwanamke mjivuni, siku tatu baadae, mida ya saa mbili, za asubuhi, Deus akiwa ametulia chumbani kwake ana tazama tv, huku mara chache akichat na mwanamke alie msevu kwa jina la pacha, kwenye simu yake, mara akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, akainuka na kwenda kuufungua, hapo akakutana na kijana mmoja wa kiafrika alieshika karatasi mkononi, “mambo vipi rafiki, biko Bien?” alisalimia yule kijana kwa sauti yenye lafudhi ya wenyeji wa pale Congo. …….....


Kijana hakuwa mgeni machoni pa Deus, kwa maana alishamwona mara kadhaa maeneo ya ofisi za MUNUSCO ambazo kwa mkoa wa Ben zipo pale pale air port, ila ilimfanya Deus ahisi kuwa kuna kazi flani ipo mbele yake, na inaweza kuwa kuna sehemu anatakiwa kwenda, “poa tu rafiki niambie, kuna ujumbe wowote kwaajili yangu?” aliuliza Deus, huku akiitazama ile karatasi mkononi kwa yule kijana, “kaka leo umebahatika kwenda Ilingeti, kuona Congo bien (vizuri)” alisema yule kijana wa kicongo, huku anampatia Deus ile karatasi aliyoishika, “dah! afadhari nikapoteze muda, maana nimechoka kushinda ndani siku zote” alisema Deus, huku anaipokea ile karatasi na kutazama kilicho andikwa ndani yake, “lakini hakikisha umeacha vitu vyako bien, visijepotea, maana safari unajuwa ni wakati wa kwenda tu, ila kurudi hiyo ni inshu nyingine” alisema yule kijana huku anaondoka zake, “afadhari leo nikang’aze macho, maana dah!” alisema Deus ambae aliyasikia maneno ya kijana yule, na kuyachukulia juu juu, aliweka lile karatasi kitandani na kuanza kuisoma, huku anaanza kujiandaa.


“Jukumu ni kuendesha gari, safari ni ilingeti, ben kaskazini, lengo ni kuwapeleka madoctor wa WHO na vifaa tiba kwa wananchi, mavazi ni FBO (full battle oder)” alisoma Deus kwa sauti ya chini, huku anaendelea kujiandaa, ambapo alitumia dakika tano tu kujiandaa, na dakika kumi baadae alikuwa ameshasimamisha gari lake, mbele ya ofisi za MONUSCO, ambapo tayari kulikuwa na magari mengine manne, ambayo ni mali ya jeshi la ulinzi la jamuhuri ya demokrasia ya Congo, (FARDC) kama ambavyo unaweza kusema Forces Armées de la République Démocratique du Congo. kwa lugha ya kifaransa, au kama ambavyo ungesema Armed Force of Democratic Republic of Congo, ambayo yalikuwa na kila dalili ya kuwa ni magari ambayo yapo kwenye msafara huo wa WHO.


Haikuwa jambo la kushangaza, kuona jeshi la serikali likishirikiana na umoja wa mataifa, kutokana na aina ya jukumu lililopo la ukurasa wa saba, (capter 7) ni mapigano ya moja kwa moja kuondoa vikundi vyenye silaha nchini humo, baada ya kushindikana kwa makubaliano ya usuluhisi kwa njia ya amani, lakini ukweli ni kwamba, Deus hakuwa na imani na jeshi hilo, ni kutokana na kudumu kwenye mapigano kwa miaka zaidi ya kumi na saba, hii hufanya askari awe na mabadiliko ya kitabia, hivyo kuweza kufanya jambo lolote hata kama ni hatari, inategemea na akili yake inavyo mtuma.


Ni kweli magari hayo yalionekana wazi kuwa yapo kwenye msafara huo wa kuelekea Ilingeti, maana moja kati ya magari hayo manne ambalo ni gari kubwa aina ya KAMAZ la mizigo lililozibwa kote kwa turubai likionyesha kuwa gari hilo lilikuwa limesheheni mzigo, pamoja na gari nyingine tatu ndogo aina ya Toyota land cruzer, moja likiwa lime beba askari wa tano wenye sila nzito, ambazo ukiachilia sub machine gun, pia walikuwa na LMG (Light machine gun) na risasi zake zilizo jaa kwenye mikanda, pia RPG (Rocket Propered Gun) wengi hupenda kuita muanzi, kwa jina la utani, nikutokana na jinsi inavyo fanana, pamoja na makombora yake, ambayo kikawaida hutumika kulipulia majumba makubwa na maadaraja, pia utumika kubomoa magari makubwa ya kubebea askari, mizigo, na pia kulipulia vifaru na vikundi vya askari watembea kwa miguu.


Ukiachilia hilo moja, yale mengine mawili aina ya Toyota, kila moja lilikuwa na askari watatu, mmoja akisimama nyuma ya breach bloack 12 mm ant air craft, kama ambavyo watu toka nchi Urus wanavyoita KAPEVETE, ni maalumu kwaajili ya ulinzi wa mashambulizi toka angani, na pia utumika kushambulia magari yenye ngozi laini, na vikundi vya watu, zilizo sheheni, mikanda ya risasi, huku wale wawili kila gari wakiwa wameshikilia MMG (medium machine gun) kila mmoja, na mkanda wake wa risasi, huku wakiwa wamekalia mabox ya risasi na mabomu, hakika walionyesha kuwa wapo tayari kwa safari, safari ambayo inaweza kutokewa na jambo lolote la kimapigano.


Kwa kulijuwa hilo, Deus ambae alikuwa ametulia ndani ya gari, anasubiri utaratibu wa kwenda kuweka mafuta, akawaza kuhusu usalama wake, endapo itaokea wakatokewa na shambulizi la kushtukiza, maana yeye hakuwa na silaha yoyote, wala body armor (bullet pruff), maana kikawaida waangalizi wa maswala ya kijeshi hawakutakiwa kuwa na silaha, sababu wao kazi yao, haikuwa na jukumu la kuingia moja kwa moja kwenye mapigano, “ila kwa silaha tulizo nazo zikitumika vyema tuna chomoka toka kwenye hatari” aliwaza Deus, na wakati huo huo akashtuliwa na mtu alie gonga kidogo kwenye dirisha la mlango wa dereva.


Deus akageuza uso wake kutazama kwenye kioo, akamwona yule jamaa aliemletea karatasi chumbani, alipomwona akashusha kioo, niambie kaka” alisema Deus, huku anamtazama yule jamaa, “ni safi rafiki, nenda kaweke gas hapo nyuma, mnalaswa kuanza safari sasa hivi, madoctor walishaingia hapa na holex (ni aina flani ya helcoper iendayo kasi na yenye kunyumbulika kwa haraka, nusu saa imeita” alisema yule kijana, kwa sauti yenye lafudhi ya kicongo, huku anaonyesha kwa mkono upande wa nyuma ya jengo moja, linalotazamana na ofisi za Monusco “ok! poa” alisema Deus huku anaingiza gia na kuondoka, maana gari lilikuwa bado lina unguruma, yani halikuwa limezimwa, huku yule jamaa akilifwata moja kati ya magari ya FARDC.


Deus alitembeza gari taratibu, kulifwata jengo lile, na wakati flani alitazama kwenye kioo cha uangalizia nyuma, yani side Mirror, akamwona yule jamaa, akiwa amelifikia gari lile la mizigo, la FARDC, huku askari wote wakishuka toka kwenye gari na kumfwata kijana yule, ungesema labda ni kiongozi wa jeshi, kwa jinsi walivyo miminika kumfwata, lakini wakati Deus anakata kona, kuelekea nyuma ya jengo lile, akamwona yule kijana aliezungukwa na wale askari wa FARDC, alikuwa anaelekeza jambo flani, nao wakimsikiliza kwa umakini mkubwa sana, Deus aliachana nao akihisi kuwa, anawaeleza nao wakaweke mafuta, au anawapaa tetesi flani za kimaslahi juu ya safari ile, hakuwajari sana maana ukizingatia wote ni raia wa DRC, hivyo wanaweza kuwa ni watu wanao fahamiana.


Deus alimaliza kuweka mafuta kwenye gari, akiwa ametumia dakika zaidi ya tano, na kuigia kwenye gari lake, kisha akaliwasha na kuendesha taratibu kuelekea kule alikokuwa amegesha mwanzo, yani kule yalikokuwepo magari mengine, ambapo kwa hakika hakuona dalili ya magari ya jeshi la serikali, kupelekwa kwenye kisima cha mafuta cha MONUSCO, zaidi aliweza kuona askari wale wakiwa wamesimama pembeni ya gari lile kubwa lenye kufunikwa vyema, huku wakilitazama gari la Deus, kwa macho flani ambayo kama akili yako inafanya kazi vyema, lazima ungejuwa kuwa walikuwa wanakuzungumzia.


Deus aliachana nao, alienda taratibu mpaka pale alipokuwa amesimama mwanzo, na kugesha gari, safari hii akalizima kabisa, baada ya hapo akapapasa chini ya seat aliyokalia, ni wazi alikuwa anakagua kitu flani, na alipo jiridhisha kile alichokuwa anakipapasa, akalaza kiegemeo cha seat yake, kisha akatoa simu yake na kuangalia kama kuna ujumbe au simu yoyote iliyopigwa.


Mara tu baada ya kuitazama simu yake, Deus akajikuta akitabasamu peke yake, ni baada ya kuona ujumbe wa Whatsapp, uliotumwa na mtu alieitwa Pacha, “mambo mchoraji wangu” ilikuwa ni salam ya kawaida tu, ila ilitoka kwa mtu ambae mpaka sasa, alikuwa ni kama mtu wake wa karibu sana, japo hakuwahi kumuona anafananaje, “poa Pacha wangu, vipi hujaingia class?” aliandika Deus kisha akaituma kwenda kwenye namba aliuoisave kwa jina la Pacha, kisha akafungua nakilishi ya ramani ya kimtandao, na kuanza kuisaka ramani ya kaskazini mwa mji wa beni, akifuata barabara ambayo wangeitumia muda mfupi ujao, lakini kabla hajafika mbali akasikia simu yake ikiingia ujumbe, akaacha anacho kifanya na kufungua ule ujumbe, uliotumwa kwake kwa njia ya whatsapp.


Ujumbe ulikuwa unatoka kwa Pacha, aliusoma kimya kimya, na kuitimisha kwa tabasamu mwanana, bado sijaingia class” ndivyo ulivyo soma ujumbe huo, ambao ulifuatiwa na ujumbe mwingine, toka kwa Pacha, ambao pia aliufungua kwa haraka, “naona ulikuwa busy na biashara, maana nimekutumia sms muda mrefu, lakini hukujibu” Deus alitabasamu kidogo, huku anaandika ujumbe, “si unajuwa tena jua la Dar, lina changanya kiasi kwamba nasahau, hata kutazama simu” aliandika Deus, na kumalizia kwa kiragosi (emoj) cha kicheko, na wakati anamaliza kuituma kwenda kwa Pacha, ghafla mlango wa mbele wa gari lake, upande wa abiria, ukafunguliwa, hapo Deus akageuza uso wake haraka, kutazama upande ule wa seat ya abiria, huku anainuka na kukaa sawa.


Naam alichokiona Deus kilmshtua sana, maana hakutegemea kwa muda ule wala kwa siku za hivi karibuni, hakika ulikuwa ni mshtuko ulio ambatana na fadhaha, lakini Deus akajitaidi kuzuia mshtuko wake, na kuinua seat yake, akiiweka sawa, “habari yako askari” ilikuwa sauti nyororo ya kike,


Huyu alikuwa ni yule mschana mrembo, ambae Deus alikutana nae Entebe Uganda airport, na kusafiri pamoja kuja DRC, ambae sasa alikuwa anakaa kwenye ile seat ya mbele ya abiria, kwenye gari hili la Deus, “safi tu habari” aliitikia Deus kwa sauti tulivu, huku anawasha gari, na wakati huo huo, milango ya ya nyuma ya gari hilo ikafunguliwa, na kwakutumia kioo cha kati yaani back view, Deus akawaona watu wawili wakiingia ndani ya gari, ni wale ambao, walishuka na mwanadada huyu, kwenye ndege, siku ile pale goma air port, “habari yako kijana, naona tumekutana tena” alisamilia mmoja kati ya wale wanaume wawili, akitumia lugha ya kiswahili, japo hakikuwa kilichonyooka, lakini ilionyesha wazi kuwa wale jamaa, walikuwa wametokea ukanda wa Africa ya mashariki, na lafudhi yake ikifanana kabisa na watu toka Burundi.


Hakika watu hawa wawili waliokaa seat ya nyuma ya gari lake, nikama walimfanya Deus apunguze mshtuko wake, “salama habari zenu” alijibu Deus, huku ametazama mbele yaliko magari mengine, yaani yale ya jeshi la serikali, ambapo alionekana askari mmoja wa jeshi la FARDC, mwenye cho cha major, akiwa amrisha askari waingie kwenye magari, kisha yeye kuingia kwenye lile gari lenye askari watano wenye silaha nzito, huku askari wakiingia kwenye magari kama walivyokuwa mwanzo, huku wakimwacha kijana wa kicongo yule ambae alimletea karatasi chumbani, akiwa amesimama anaazama jinsi mambo yanavyoenda, “poa tu dogo, kumbe na wewe umekuja huku Ben?” aliuliza yule mwingine ambae pia aliongea Kiswahili chenye lafudhi ya watu wa kenya, “yah! Goma tulikaa siku chache sana” alijibu Deus, huku anafunga mkanda seat, na wakati macho yake yakiwa bado yame tazama mbele, ambako alimwona yule kijana wakicongo, akija upande wao usawa wa gari lao.


Naam! Alipo lifikia akaonyesha ishara kwa Deus ambae ndie dereva, kupeleka gari lake, nyuma ya gari alilopanda yule major, ambalo lilitanguliwa na gari moja kati ya yale mawili yenye silaha za 12 mm, lakini licha ya kupewa ishara hiyo, kijana Deus akuonyesha dalili ya kuondoa gari kwenda pale alipoelekezwa, “nadhani umeelewa ulichoambiwa au gari linatatizo?” aliuliza yule mwanamke ambae leo alionekana kuzidi kuwa mzuri, kwa sauti iliyo jawa na mshangao, huku anamtazama Deus kwa macho yenye kuchunguza na kusuta, “samahani naomba fungeni mikanda” alisema Deus, taratibu na kwasauti tulivu, bila kutazama kusoto wala kulia, “sidhani kama ni muhimu kuliko amri uliyopewa” alisema mschana yule ambae licha ya umri wake mdogo kuliko wale wanaume, lakini alionekana kuwa ndie mwenye madaraka makubwa.


Wale wenzie walifunga mkanda mara moja, ila yule mwanamke aliganda kidogo, kisha akafunga mkanda, na ndipo Deus alipo ondoa gari, wakati huo yule kijana wakicongo akiwa amesimama anawatazama, mpaka Deus alipo simamisha gari pale alipoelekezwa, huku gari kubwa lenye mzigo, yani Kamaz, likiwa nyuma yake, likifwatiwa na gari lenye 12 mm KAPEVETE, na ndio wakati ambao Deus alitazama side mirror, pasipo kulega kumtazama mtu yoyote, akajikua amemtazama yule kijana wa kicongo, aliekuwa mita hamsini yuma yao, ambae sasa alionekana akiwa makini sana, na mwenye wasiwasi, anatazama kulia, halafu kushoto, kisha nyuma yake, alipoona hakukuwa na mtu, akaingiza mkono mfukoni mwake, kisha akatoa simu yake, na kubofya namba flani, kisha akaiweka sikioni, ni wazi alikuwa anawasiliana na mtu flani…..unadhani hii safari ina usalama kweli? nini kitawatokea watu hawa, basi endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Hadithi nzuri sana mkuu ,sana tena ila jitahidi makosa madogo madogo yasiwepo sana , kuna wakati unatuaminisha kuwa kisa ni cha muda mrefu miaka ya nyuma sana ghafla inahamia miaka ya 2011, mfano huyo Commando alitumwa akanunue gari Vw beettle kwa miaka hiyo ,lakini ghafla ana simu ya mkononi na ikaja kuonekana anachati na yule binti kwa treni. Ni makosa madogo madogo tu ya kibinadamu,nje ya hapo stori nzuri sanaaa

Tupe mambo ya Ben Maviv hapo😅😅
 
Hadithi nzuri sana mkuu ,sana tena ila jitahidi makosa madogo madogo yasiwepo sana , kuna wakati unatuaminisha kuwa kisa ni cha muda mrefu miaka ya nyuma sana ghafla inahamia miaka ya 2011, mfano huyo Commando alitumwa akanunue gari Vw beettle kwa miaka hiyo ,lakini ghafla ana simu ya mkononi na ikaja kuonekana anachati na yule binti kwa treni. Ni makosa madogo madogo tu ya kibinadamu,nje ya hapo stori nzuri sanaaa

Tupe mambo ya Ben Maviv hapo😅😅
Labda tu umesoma vbaya hiyo ya kuagizwa gari mbona ni kabla ya kujuana na pacha, kwasababu story imeanza kati halafu imerudi nyuma kwaajili ya kuunga matukio yote yalio anzia kati kama ambavyo utaenda kuona
 
Natumai wote muko bien maan sasa tupige kicongo kwasababu dereva wetu yupo huko 😅
 
Natumai wote muko bien maan sasa tupige kicongo kwasababu dereva wetu yupo huko
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI TANO: na ndio wakati ambao Deus alitazama side mirror, pasipo kulega kumtazama mtu yoyote, akajikua amemtazama yule kijana wa kicongo, aliekuwa mita hamsini nyuma yao, ambae sasa alionekana akiwa makini sana na mwenye wasi wasi, anatazama kulia halafu kushoto kisha nyuma yake, alipoona hakukuwa na mtu, akaingiza mkono mfukoni mwake, kisha akatoa simu yake, na kubofya namba flani kisha akaiweka sikioni, ni wazi alikuwa anawasiliana na mtu flani….endelea….


Kilicho mvutia Deus ni namna ambavyo jamaa huyu, alivyoonekana kuwa makini, na kila jambo lililokuwa linaendelea pale, hata jinsi alivyo kuwa makini wakati anaongea na simu ungesema hakutaka mtu mwingine amsikie, lakini Deus hakujari, zaidi akatazama mbele ambako tayari msafari ulikuwa umeanza kuondoka, Deus nae akaondoa gari kufwata gari la mbele yake wakati huo yule mschana mrembo, akitoa kitabu chake na kuanza kusoma.


Safari ilianza taratibu, kwa speed ya ishirini kilomita kwa saa, kutoka nje ya eneo hili, linalomikiliwa na umoja wa mataifa, lililoungana na uwanja wa ndege wa Mavivi, mpaka wanapo ikamata barabara kuu inayotoka mjini, kuelekea Mbao Ilingeti, ndipo magari haya ambayo kwa idadi yapo matano, yana kata kona kushoto, yanapo kamata uelekeo wa kaskazini, yanaongeza mwendo, nakutembea speed ya tisini mpaka mia kilomita kwa saa, huku ndani ya gari mwanadada wa kihabeshi akiwa busy na kitabu chake, na wale jamaa wawili wakionekana kutazama mazingira mazuri ya kijani, misitu minene, japo waliweza kushuhudia baadhi ya majengo katika vijiji walivyo vipita njiani, yakiwa yame bomolewa au kuchomwa moto, ikionyesha ni makombola ndiyo yaliyo tumika kufanya uharifu huo, “nchi ina neema ya mvua, kosa hili janga la vita vya wenyewe kwa wenyewe pasinge kuwa na njaa” alisema mmoja kati ya wale madoctor wawili, huyu ni yule wa kenya “sanaa, na hii neema ndiyo inayo waponza, na kusababisha vita vya mara kwa mara” alisema yule toka Burundi, huku yule mwana dada wa kuoka Ethiopia, akiwa kimya macho, kwenye kitabu chake


Muda wote licha ya kuwa makini na barabara hii, ambayo ni ngeni kwake, lakini pia dereva wetu alikuwa anawaza juu ya mschana huyu, ambae licha ya mikausho yake, ambayo pengine inatokana na kazi aliyo nayo au wadhifa wake lakini alikuwa mzuri na wakuvutia, na kutamanisha kwa mwanaume wa aina yoyote, awe kijana mdogo, au mzee mtu mzima, fukara au tajiri, pengine hata viongozi wa dini wenye nadhiri zao, si unajuwa kuwa macho haya katazwi kuona.


“Sema analinga sana, huyo jamaa yake sijuwi alimpataje, au kwasababu mimi siyo wa aina yake?” aliwaza Deus, huku anazidi kukanyaga mafuta kuyafwata magari mawili aina ya Toyota land Cruzer, mbele kabisa likiwa gari la wapiganaji Fighing Vehicle, likiongoza msafara, na kuhakikisha usalama wa msafara, kwa upande wa mbele, huku likifwatiwa na lile lililombeba mkubwa wa msafara ule, yani Major wa jeshi la FARDC, wakati nyuma yao kulikuwa na KAMZ, lile gari kubwa lenye mizigo, likifwatiwa na gari jingine la wapiganaji, lenye kuhakikisha usalama wa nyuma.


Kuna wakati Deus kwa kutumia ujanja wa hali ya juu, aliweza kumtazama mschana huyu, kwa macho ya wizi, na kuweza kuona uzuri wa mschana huyo, ambae alionekana kuwa busy na kitabu chake, “ni mzuri ila” aliwaza Deus, huku wanaendelea kukatika kwenye misitu minene na mashamba ya michikichi.


Wakati huo walikuwa kati kati ya msitu, na walisha tembea kama kilomita tisa pasipo kukuta nyumba wala sehemu ya wazi, zaidi ya misitu mikubwa na minene, yenye vichaka vipana, hata mbele yao hawakuona dalili ya kuwepo kwa kijiji maeneo ya karibu, akaona magari ya mbele yanapunguza mwendo, na yeye akapunguza mwendo, huku safari inaendelea.


Akiwa na uhakika kuwa mschana huyu yupo busy na kitabu, Deus aligeuza kitakasa macho chake, maana kila baada ya dakika kadhaa alikuwa anamtazama kwa macho ya wizi hata wakati fulani alitazama na kumwona akiwa anatabasamu, nadhani alikuwa anatabasamia kitabu chake, tabasamu ambalo lilimfanya azidi kupendeza, na kuwa mzuri sana, “askari nivyema ukawa makini na barabara kuliko kutazama vitu vingine, nje ya barabara” alisema yule mschana, na hapo Deus alishtuka kidogo maana licha ya mwanamke huyo kuwa busy na kitabu lakini aliweza kugundua kuwa alikuwa anatazamwa.


Deus alijihisi aibu flani kwa tukio lile, lakini akaona kuwa ni lazima afanye jambo ili asionekane dhaifu, “kuna wakati nje ya barabara kuna vitu vya kuvutia sidhani kama ni dhambi kuburudisha macho kwa kutazama uumbaji wa mwenyezi mungu” alisema Deus huku ana yatazama magari ambayo sasa yalikuwa yanapunguza mwendo zaidi, na kufikia speed ishilini kilomiya kwa saa, na yeye akafanya hivyo, huku anatazama side mirror kuona kama kuna gari nyuma yao limepata tatizo au laah, lakini kiukweli yote yalikuwa katika msafara na hakukuwa na dalili za gari lolote kati yao kuharibika “mh! kwanini wanapunguza mwendo, kwenye eneo hatarishi kama hili” aliuliza Deus kwa sauti ya wazi kabisa, ndipo hata wale wengine wakainua nyuso zao kutazama mbele, wakaona ni kweli magari yalikuwa yamepunguza mwendo kwa kiasi kikubwa.


Naam kabla awajapata jibu, juu ya upunguzaji wa mwendo ule, wote wanne wakashuhudia gari la mbele kabisa likisimama, likifwatiwa na gari la yule major lenye askari watano wenye silaha nzito, gari ambalo Deus nae alienda kusimamisha nyuma yake, na yale ya nyuma yakafanya hivyo hivyo, huku lile la mwisho, likiwa limeachia nafasi kubwa sana toka lilipo gari kwa kupeana nafasi.


Naam Deus pamoja na wale madoctor waliweza kuona askari wa gari la mbele kabisa, yani waliopanda mbele na nyuma wale wa kwenye silaha ya 12 mm, wakishuka toka kwenye gari, na kuanza kutembea wakirudi nyuma kuyafwata magari yale ya nyuma ya gari la wakina Deus na madoctor, sambamba na yule askari mwenye cheo cha major toka kwenye gari la pili, nae akashuka na kulifwata gari la wakina Deus, alipo likaribia akasimama, na Deus akashusha kioo, cha upande wake, ambao yule major alikuwa ameusogelea, “Tanzania unapaswa kusubiri ndani ya gari kuna tatizo kwenye gari lanyuma” alisema Major, kwa sauti ya msisitizo, “ndiyo afande” alijibu Deus, huku yule major, akijiunga na wale wengine kuelekea kwenye magari ya nyuma.


“tatizo la magari ya jeshi wakati mwingine yana kwamisha safari” alisema yule mschana kwa sauti ya kulalamika na kukata tamaa huku anageuza shingo yake kujaribu kutazam kule walikokuwa wanaelekea wale askari wa FARDC, “sidhani kama kuna tatizo kubwa la kutuchelewesha, maana naona magari yalikuwa yanataembea bila shida yoyote” alisema Deus, huku na yeye pia akigeuza shingo yake kutazama kule walikoelekea wale askari, ambako hata madoctor waliokaa seat ya nyuma pia walitazama.


Lakini walipo tazama kule nyuma nikama Deus aliona kuna utofauti fulani, maana jambo la kushangaza ni kwamba dereva wa KAMAZ alikuwa bado ndani ya gari, huku mwenzie aliekuwa nae ndani akishuka na kujiunga na wenzake, lakini chakustaajabisha zaidi ni kwamba, askari waliokuwa ndani ya gari la nyuma kabisa ambalo ndilo lenye tatizo, walikuwa bado wapo ndani ya gari, “mh!” aliguna Deus huku anageuza uso wake kutazama mbele ambako ulisikika mgurumo wa gari likitembea, hata wale wenzake pia wakatazama mbele ambako waliliona gari lapili lile ambalo alishuka yule major likigeuzwa na kuanza kutembea kwa mwendo wakawaida kupita ubavuni mwagari lao, yani lile ambalo walikuwepo wakina Deus, likielekea pale lilipokuwepo lile gari la nyuma kabisa.


Deus alishtuka kidogo na kumtazama yule mwanamke aliekaa seat ya mbele, yaani yule doctor ambae bado alikuwa anatazama kule nyuma, na kabla hajauliza anacho taka kuuliza ghafla akasikia gurumo nzito ya KAMAZ kama linaanza kutembea, nae akageuza tena uso wake kulitazama, ambapo aliliona lina sogea na kuingia barabarani, kama linataka kugeuza, lakini kitu cha kushangaza likasimama kwa kukinga barabara, likiwa limeacha nafasi ndogo upande wa kulia wa barabara, yaani upande wapili na wao wakina Deus wakiwa upande wa kushoto wa barabara, kama ujuavyo nchi hii, utembea upande wa kulia, tofauti na Tanzania ambapo utembea upande wakushoto wa barabara.


Mpaka hapo tayari Deus alishagundua kuwa kulikuwa kuna mchezo wamechezewa, “kum… make wametuuza hawa waseng…” alisema Deus sambamba na matusi ya nguoni huku anatazama sehemu ambayo anaweza kupitisha gari kwaajili ya kuondoka, huku wale madoctor akiwepo yule mwanamke, wakimtazama kwa macho ya mshangao, “nini kinaendelea we askari” aliuliza yule mwanamke kwa sauti iliyojaa uoga huku wote wakimtazama kwa macho ya wasi wasi.


Lakini kabla Deus hajajibu au kufanya chochote, ghafla ukasikika mlipuko mita chache toka kichakani upande wakulia wa barabara, ukifwatia na kitu kama mbinja, yani mruzi, “fyuuuuuuuuu) sekunde chache kombola zito likakita kwenye ubavu wa lile gari la mbele, ambalo lilisababisha mlipuko mkubwa wanguvu, kiasi hata gari walilokuwepo wao likatikisika,


Hapo Deus ambae alishajuwa kuwa tayari wameingia kwenye mtego, akawasikia wale madoctor wakipiga kelele za uoga, kila mmoja kwa mtindo wake, “mama na kufaaaa” na wakati huo Deus akasikia magari mawili ya FARDC yakiondoka kwa speed, kurudi yalikotoka, huku wakiliacha lile lenye mizigo, likiwa limezuia barabara, akatoa hand brake ya gari lao, tayari kuondoa gari, lakini kabla hajaondoa gari wakaona watu kumi waliovalia mavazi chakavu ya kijeshi, kila mmoja la aina yake wakiibuka barabarani, kutokea kichani upande wa ule ule wa kulia huku wameshikilia silaha za aina mbali, kama vile AK 47, MMG na mmoja wao alikuwa amebeba kombora aina RPG, huku wengine wawili wakiwa wamebeba vifuko vya makombora ya RPC, zikiwa mikononi mwao, ambazo walikuwa wamezielekeza kwenye gari lao na hapo Madoctor walitoa macho ya kukata tamaa, hasa ukizingatia, walikuwa na askari mmoja, ambae ukiachilia mwonekano wake ambao nikama kijana wakisasa mpole, mtulivu, pia hakuwa na bunduki ya aina yoyote. ..ENDELEA…unazani hii safari ina usalama kweli, nini kitawatokea watu hawa?, basi endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, unayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Ni nzuri sana.
Msimuliaji anaituma hadithi kwa wakati.

Kuna wasimuliaji wanaringa hadi kichefuchefu.

Yaani unaleta hadithi kwa hiyari yako kuthibitisha kipaji chako cha utunzi halafu unaringa nayo.

Ni ukosefu wa maadili ya usimuliaji.
 
Natumai wote muko bien, kuna mambo naweka sawa kisha nashusha cha asubuhi
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI SITA: kama vile AK 47, MMG na mmoja wao alikuwa amebeba kombora aina RPG, huku wengine wawili wakiwa wamebeba vifuko vya makombora ya RPG, zikiwa mikononi mwao, ambazo walikuwa wamezielekeza kwenye gari lao, hapo Madoctor walitoa macho ya kukata tamaa, hasa ukizingatia walikuwa na askari mmoja ambae ukiachilia mwonekano wake ambao nikama kijana wakisasa mpole mtulivu, pia hakuwa na bunduki ya aina yoyote. ..ENDELEA…


Hapo Deus aliwatazama wale askari ambao walikuwa wanakuja kwa kugawanyika wa wanne wakilisogelea gari la wakina Deus, na huku wakiwa wanaanza kulegeza mikono yao na kutazamisha chini mitutu yao ya bunduki, ni wazi walikuwa na uhakika kuwa watu waliopo ndani ya gari hili hawakuwa na silaha ya aina yoyote, wengine sita wakilifwata lile gari lenye mizigo yaani KAMAZ, huko ndio kabisaaa walipachika mikanda ya silaha zao mabegani, huku silaha zao zikiwa zime lala migongoni, “hakuna kuchelewa ndege ya UN itakuja sasa hivi kufanya doria” alipiga kelele mmoja wao akiamrisha kuwa wenzake wafanye haraka haraka ambayo Deus na wenzake hawakujuwa ni ya nini.


Hapo ndipo Deus alipokumbuka maneno ya yule kijana mcongo, aliemletea karatasi, “weka vitu vyako vizuri, visije kupotea, maana safari unajuwa wakati wakwenda tu, wakati wakurudi haijulikani” maneno ambayo hayakuwa utabiri, ni maneno ambayo yalikuwa yamelenga kile kinachoenda kutokea, “inatia hasira” alisema Deus kwa sauti ya kunong’ona, huku anaacha kila anachokifanya na kupeleka mkono chini ya uvugu wa seat yake, masikio yake yakisikia maneno flani yaliyo tamkwa na wenzake kwa sauti za chini ambayo baadae alikuja kugundua kuwa walikuwa wanaomba mungu awaokoe katika mikono ile ya waasi, wakati huo wakamwona mmoja wao ambae nikama mkubwa wao, alikuwa anawekasimu sikioni na kunaza kuongea, hawakuweza kumsikia maana walikuwa wamepandisha vioo mpaka juu ila kwa kumtazama ni kama alikuwa anatoa taarifa fulani.


Hapo Deus akamtazama yule ambae amebeba makombora matatu ya RPG ambayo HE, yaani High Xprosive, ikiwa na maana ina mlipuko mkubwa sana, “jamani mpaka sasa tupo ndani ya mikono ya waasi, na tunahitaji kupigania maisha yetu, hatuwezi kusubiri kuona wanachotaka kutufanyia” alisema Deus huku anapapasa chini ya seat, kisha akatoa mkono ukiwa mtupu, nadhani alishagusa alichopapasa, wakati huo tayari wale jamaa watatu walishalifikia gari lao na kutawanyika,


Wawili wakaenda upande wakulia kwenye mlango wa abiria wa mbele alikokaa yule mwanamke rembo ambae alikuwa anazidi kutetemeka kwa uoga huku akiachia kilio cha chini chini, japo sura yake haiku athirika na mtetemo huo wa uoga, maana bado alikuwa na utamu wake na mwingine akaufwata mlango wa nyuma, aliko kaa doctor toka Burundi, “hatuna namna lazima tuondoke” alisema Deus kwa sauti ya kunong’ona, huku anamtazama yule mmoja alikuwa anakuja upande wa kushoto wa gari.


Magari ya nchi hii mara nyingi ni LHD, pamoja na hili waliopo wakina Deus, yaani left heand driver, ambapo dereva anakaa upande wa kushoto wa gari, yule jamaa moja kwa moja aliuvuka mlango wa dereva kisha akaufwata mlango wa nyuma, yaani alikokaa yule doctor toka Kenya, na wote wakashika vitasa vya milango ya gari na kufungua kwa fujo.


Bahati mbaya milango haikuwekwa lock, hivyo jamaa hawa watatu wote kwa pamoja wakafungua milango yagari lile mali ya umoja wa mataifa MONUSCO, na kuwashika wale madoctor, kisha kuwatoa nje kwa fujo, “yes waambie dollar laki tano masaa sita, vinginevyo tutauwa mmoja mmoja” sasa waliweza kumsikia yule aliekuwa anaongea na simu, ambae ndio kama alikuwa anamaliza maongezi, Deus akamtazama tena yule mmoja kati ya wawili waliobeba makombora, ambae sasa alikuwa amesimama karibu kabisa na wenzake watatu, mmoja kati ya watatu hao akiwa pia amebabe makombora mawili, na mwingine akiwa amebeba mtambo wa RPG wakulipulia makombora hayo, “we askari mshenzi huu ni mpango wenu na wale wenzako” alipiga kelele yule Doctor mrembo kwa sauti kali yenye hasira sambamba na kilio huku anamtazama Deus, nadhani aliwaza hivyo baada ya kuona Deus ameachwa kwenye gari, “ Ni nani kakuambia tuna shirikiana na wapumbavu katika mambo yetu” alisema yule kiongozi wao huku anaweka simu mfukoni na hapo doctor wakike aliekuwa ameshikwa mkono kwanguvu na mmoja kati ya wale jamaa wenye silaha, akamtazama yule jamaa yani kiongozi, “mnataka nini kwetu, sema kama nifedha sio tatizo” alipiga kelele yule mschana, na wale jamaa wakacheka kwa dharau, “mschana mrembo acha kupiga kelele, unajichosha bure tu, unakazi ya kufanya muda mfupi ujao maana katika maisha yangu sijawahi kutomb*… mschana mzuri kama wewe” alisema yule kiongozi aliekuwa anatembea taratibu kwa kulisogelea gari lile la UN, huku anamtazama Doctor wakike kwa macho ya uchu.


Maneno ya yule jamaa nikama yalimvunja nguvu yule doctor wakike, ambae hata Deus hakuwa anamfahamu kwa jina, maana alitoa macho ya huruma kumtazama yule kiongozi, ambae alikuwa ameachia tabasamu la kuchukiza, “tafadhari naomba msinifanyie chochote, mtapata fedha yoyote mnayo hitaji” alisema doctor mrembo, kwa sauti ya kuomboleza iliyo ambatana na kilio cha majuto.


Bahati kilio kile nikama kilikuwa kinazidi kumfurahisha kiongozi huyu wakundi la waasi aliezowea kubaka, nakwamba pasipo mwanamke kulia au kulalamika kwa kufanyiwa ngono unyama yaani manyanyaso ya kingono hakujisikia kama amefanya tendo hilo, alizidi kutamani kufanya ngono na mschana yule, wakati huo Deus alikuwa anawaza namna ya kuondoka eneo lile, maana alijuwa fika kuwa wasinge mwacha, “tena inabidi nimalize shuhuri kabla ya kufika kambini, maana chief akiona lazima na yeye atatamani tu” alisema yule yula jamaa na wenzake wakacheka kizembe, wakati huo tayari kiongozi yule alikuwa anatembea ubavuni mwagari lile la UN, ambalo Deus alikuwa ndani yake, “kwanini huyu hajatolewa ndani ya gari?” aliuliza yule kiongozi, kwa sauti ya ukali na mshangao, “afande mpango ni madoctor watatu, sasa huyo….” alijibu mmoja kati ya vijana wale watatu, aliemshikilia doctor wakike lakini kabla hajamaliza yule kiongozi akadakia, “unajuwa madhara ya kumwachia huyu, atafichua siri ya ushirika wetu na wale FARDC, nao watashikiliwa na kulazimishwa waseme nani anausika, na ikishabainika kabla hatujapata fedha zetu mambo yataharibika” alisema yule kiongozi kwa sauti ya ukali kweli kweli, huku anatembea hatua kadhaa na kusimama pembeni ya gari, kisha akatazama, kule ambako aliwaacha wale askari wengine,


Naam, hapo Deus akajuwa kuwa sasa ndio wakati wa kujikomboa, toka kwenye mikono ya waasi, Deus akageuza uso wake kutazama nani angekuja kumtoa ndani ya gari na ndicho kitu alichotamani, siyo kwamba Deus angeshindwa kutoka mwenyewe kweye gari, hapana ila sijuwi kwanini alikuwa anatamani atolewe.


Deus aliweza kumwona kijana moja ni yule aliekuwa anakagua mizgo kwenye gari la mizigo, akachomoka mbio na bunduki yake mgogoni, akakimbilia kwenye gari upande wa kushoto, alipofika usawa wa mlango wa dereva, akashika kitasa kwa fujo na kufungua mlango kisha akamshika Deus mkono wa kushoto na kumvuta kwa nguvu huku wale wengine pamoja na madoctor wakitazama tukio lile.


Sasa basi, wakati yule jamaa anamvuta Deus kwa nguvu, ndipo Deus alipopeleka mkono chini ya seat ya gari na kuibuka mkono wake kisha akaupeleka kifuani kwa yule jamaa, upande wa kushoto, chini kidogo ya ziwa, akikandamiza kwa nguvu, huku anatoka nje ya gari kwa haraka ungesema anajaribu kujitoa kwa yule jamaa ambae bado alikuwa amemshika mkono, lakini siyo kwa nguvu kama mwanzo, sasa alikuwa analegeza mkono taratibu, huku mkono mwingine akiupeleka kifuani pale kwenye mkono wa Deus.


Kwa macho ya mshangao wale madoctor watatu, kwa pamoja na vijana waasi wenzake walimtazama mwenzao ambae alionekana kukunja sura kwa maumivu, na kabla hawaja jiuliza nini kimetokea, katika hali ambayo hawakuamini kama askari huyu toka Tanzania, anawenza kufanya lolote mbele yao na wakiwa na uhakika hakuwa na silaha yoyote.


Mara wakamwona kijana Deus, akivuta mkono wake upande wa kulia, nakufanya macho yao, yawezekuona kisu kikubwa chenye urefu wa futi moja na makari ya kutisha, huku upande wapili kikiwa na meno kama msumeno kilicho lowa damu, ambacho kilichomolewa kwanguvu, na ghafla, ambacho mtoko wake uliacha uwazi mkubwa chini ya kifua cha muasi huyu, na kufanya baadhi ya viungo vya ndani vya kijana huyo, kama maini na utumbo kuchomoza nje huku zikirusha damu nyingi.


Ile kutahamaki, tayari kisu kilikuwa hewani, kinaelekea kule alikokuwepo Doctor wakike, ambae fumba na kufumbua, tayari kulikuwa kimeshapita cent miter chache karibu na sikio lake na kwenda kukita kwenye shingo la mtu alie mshika usawa wa koo, ile wale jamaa wanashangaa tukio lile la kushangaza, la haraka, tayari Deus alisha msukuma marehemu muasi aliechoma kisu cha kifua na kuelekea kwa yule kiongozi wa waasi, ambae ni kama hakutegemea tukio hilo, maana alikumbwa na marehemu na wote wakaanguka chini.


Deus akushuhudia tukio la kuanguka kwa kiongozi wa waasi maana tayari alikuwa amesha mrukia muasi aliekuwa hatua moja nyuma yake akiwa ameshika yule doctor toka Kenya, nakumtwanga ngumi moja nzito ya uso, ikifwatiwa na ngumi nyingine ya shingo na kumfanya yule jamaa apoteze netwoek na kuyumba kama mlevi, Deus hakuangaika na kule kuyumba yumba kwa yule jamaa, alichukuwa bunduki yake kwa haraka, huku anamtazama yule mmoja aliemshika doctor wa Burundi, ambae sasa alikuwa anamwachia doctor huyu, na kuanza kuangaika kukoki bunduki yake aina ya AK 47.


Hapo Deus akagundua kuwa, waasi wale waliamini kuwa wasingeweza kupata upinzani wowote, kwasabababu walishapewa habari kuwa askari toka Tanzania asingekuwa na silaha yoyote, hivyo yeye kwa haraka na mahesabu ya hali ya juu, akaelekeza bunduki yake aina ya AK47 aliyoipora kwa yule kamanda muasi na kuielekeaza kwa wale askari waliobeba makambola ya RPG, akawona mmoja anapakia kombora kwenye mzinga wa RPG, Deus hakutoa nafasi ya kumalizika kwa upakizi huo maana kitendo cha bila kuchelewa, alikoki ile bunduki aina Automatic Kalashnikov, kwa kifupi AK-47, yenye sifa kubwa ya kuwa na Malengo mazuri, ambayo ilitengenezwa na askari wenye cheo cha sanjent taji, au unaweza kusema staff sagent bwana Mikhal Kalashnikov wa jeshi la Urus, mwaka 1947, na baadae viwanda vya kutoka burgaria na uchina kama vile Norico, nao wakaunda smg kwa mfano wake, japo wenyewe wanasema zinautofauti katika ubora wa Malengo, Asubuhi Njema Mpenzi Somaji Usisahau Kuacha Maoni Yako Hapo Chini ..ITAENDELEA… NYUMA YA MLANGO WA ADUI inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Tuongezee vinyama, tupe epidode za kutosha kama ulivyokuwa unafanya kwenye asali haitiwi kidole
 
Back
Top Bottom