NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHILINI NA TANO
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NNE: Naam! kijana Deus akiwa anaamini amesha kaa mbali na sehemu ambayo yupo yule mwanamke mjivuni, siku tatu baadae, mida ya saa mbili, za asubuhi, Deus akiwa ametulia chumbani kwake ana tazama tv, huku mara chache akichat na mwanamke alie msevu kwa jina la pacha, kwenye simu yake, mara akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, akainuka na kwenda kuufungua, hapo akakutana na kijana mmoja wa kiafrika alieshika karatasi mkononi, “mambo vipi rafiki, biko Bien?” alisalimia yule kijana kwa sauti yenye lafudhi ya wenyeji wa pale Congo. …….....
Kijana hakuwa mgeni machoni pa Deus, kwa maana alishamwona mara kadhaa maeneo ya ofisi za MUNUSCO ambazo kwa mkoa wa Ben zipo pale pale air port, ila ilimfanya Deus ahisi kuwa kuna kazi flani ipo mbele yake, na inaweza kuwa kuna sehemu anatakiwa kwenda, “poa tu rafiki niambie, kuna ujumbe wowote kwaajili yangu?” aliuliza Deus, huku akiitazama ile karatasi mkononi kwa yule kijana, “kaka leo umebahatika kwenda Ilingeti, kuona Congo bien (vizuri)” alisema yule kijana wa kicongo, huku anampatia Deus ile karatasi aliyoishika, “dah! afadhari nikapoteze muda, maana nimechoka kushinda ndani siku zote” alisema Deus, huku anaipokea ile karatasi na kutazama kilicho andikwa ndani yake, “lakini hakikisha umeacha vitu vyako bien, visijepotea, maana safari unajuwa ni wakati wa kwenda tu, ila kurudi hiyo ni inshu nyingine” alisema yule kijana huku anaondoka zake, “afadhari leo nikang’aze macho, maana dah!” alisema Deus ambae aliyasikia maneno ya kijana yule, na kuyachukulia juu juu, aliweka lile karatasi kitandani na kuanza kuisoma, huku anaanza kujiandaa.
“Jukumu ni kuendesha gari, safari ni ilingeti, ben kaskazini, lengo ni kuwapeleka madoctor wa WHO na vifaa tiba kwa wananchi, mavazi ni FBO (full battle oder)” alisoma Deus kwa sauti ya chini, huku anaendelea kujiandaa, ambapo alitumia dakika tano tu kujiandaa, na dakika kumi baadae alikuwa ameshasimamisha gari lake, mbele ya ofisi za MONUSCO, ambapo tayari kulikuwa na magari mengine manne, ambayo ni mali ya jeshi la ulinzi la jamuhuri ya demokrasia ya Congo, (FARDC) kama ambavyo unaweza kusema Forces Armées de la République Démocratique du Congo. kwa lugha ya kifaransa, au kama ambavyo ungesema Armed Force of Democratic Republic of Congo, ambayo yalikuwa na kila dalili ya kuwa ni magari ambayo yapo kwenye msafara huo wa WHO.
Haikuwa jambo la kushangaza, kuona jeshi la serikali likishirikiana na umoja wa mataifa, kutokana na aina ya jukumu lililopo la ukurasa wa saba, (capter 7) ni mapigano ya moja kwa moja kuondoa vikundi vyenye silaha nchini humo, baada ya kushindikana kwa makubaliano ya usuluhisi kwa njia ya amani, lakini ukweli ni kwamba, Deus hakuwa na imani na jeshi hilo, ni kutokana na kudumu kwenye mapigano kwa miaka zaidi ya kumi na saba, hii hufanya askari awe na mabadiliko ya kitabia, hivyo kuweza kufanya jambo lolote hata kama ni hatari, inategemea na akili yake inavyo mtuma.
Ni kweli magari hayo yalionekana wazi kuwa yapo kwenye msafara huo wa kuelekea Ilingeti, maana moja kati ya magari hayo manne ambalo ni gari kubwa aina ya KAMAZ la mizigo lililozibwa kote kwa turubai likionyesha kuwa gari hilo lilikuwa limesheheni mzigo, pamoja na gari nyingine tatu ndogo aina ya Toyota land cruzer, moja likiwa lime beba askari wa tano wenye sila nzito, ambazo ukiachilia sub machine gun, pia walikuwa na LMG (Light machine gun) na risasi zake zilizo jaa kwenye mikanda, pia RPG (Rocket Propered Gun) wengi hupenda kuita muanzi, kwa jina la utani, nikutokana na jinsi inavyo fanana, pamoja na makombora yake, ambayo kikawaida hutumika kulipulia majumba makubwa na maadaraja, pia utumika kubomoa magari makubwa ya kubebea askari, mizigo, na pia kulipulia vifaru na vikundi vya askari watembea kwa miguu.
Ukiachilia hilo moja, yale mengine mawili aina ya Toyota, kila moja lilikuwa na askari watatu, mmoja akisimama nyuma ya breach bloack 12 mm ant air craft, kama ambavyo watu toka nchi Urus wanavyoita KAPEVETE, ni maalumu kwaajili ya ulinzi wa mashambulizi toka angani, na pia utumika kushambulia magari yenye ngozi laini, na vikundi vya watu, zilizo sheheni, mikanda ya risasi, huku wale wawili kila gari wakiwa wameshikilia MMG (medium machine gun) kila mmoja, na mkanda wake wa risasi, huku wakiwa wamekalia mabox ya risasi na mabomu, hakika walionyesha kuwa wapo tayari kwa safari, safari ambayo inaweza kutokewa na jambo lolote la kimapigano.
Kwa kulijuwa hilo, Deus ambae alikuwa ametulia ndani ya gari, anasubiri utaratibu wa kwenda kuweka mafuta, akawaza kuhusu usalama wake, endapo itaokea wakatokewa na shambulizi la kushtukiza, maana yeye hakuwa na silaha yoyote, wala body armor (bullet pruff), maana kikawaida waangalizi wa maswala ya kijeshi hawakutakiwa kuwa na silaha, sababu wao kazi yao, haikuwa na jukumu la kuingia moja kwa moja kwenye mapigano, “ila kwa silaha tulizo nazo zikitumika vyema tuna chomoka toka kwenye hatari” aliwaza Deus, na wakati huo huo akashtuliwa na mtu alie gonga kidogo kwenye dirisha la mlango wa dereva.
Deus akageuza uso wake kutazama kwenye kioo, akamwona yule jamaa aliemletea karatasi chumbani, alipomwona akashusha kioo, niambie kaka” alisema Deus, huku anamtazama yule jamaa, “ni safi rafiki, nenda kaweke gas hapo nyuma, mnalaswa kuanza safari sasa hivi, madoctor walishaingia hapa na holex (ni aina flani ya helcoper iendayo kasi na yenye kunyumbulika kwa haraka, nusu saa imeita” alisema yule kijana, kwa sauti yenye lafudhi ya kicongo, huku anaonyesha kwa mkono upande wa nyuma ya jengo moja, linalotazamana na ofisi za Monusco “ok! poa” alisema Deus huku anaingiza gia na kuondoka, maana gari lilikuwa bado lina unguruma, yani halikuwa limezimwa, huku yule jamaa akilifwata moja kati ya magari ya FARDC.
Deus alitembeza gari taratibu, kulifwata jengo lile, na wakati flani alitazama kwenye kioo cha uangalizia nyuma, yani side Mirror, akamwona yule jamaa, akiwa amelifikia gari lile la mizigo, la FARDC, huku askari wote wakishuka toka kwenye gari na kumfwata kijana yule, ungesema labda ni kiongozi wa jeshi, kwa jinsi walivyo miminika kumfwata, lakini wakati Deus anakata kona, kuelekea nyuma ya jengo lile, akamwona yule kijana aliezungukwa na wale askari wa FARDC, alikuwa anaelekeza jambo flani, nao wakimsikiliza kwa umakini mkubwa sana, Deus aliachana nao akihisi kuwa, anawaeleza nao wakaweke mafuta, au anawapaa tetesi flani za kimaslahi juu ya safari ile, hakuwajari sana maana ukizingatia wote ni raia wa DRC, hivyo wanaweza kuwa ni watu wanao fahamiana.
Deus alimaliza kuweka mafuta kwenye gari, akiwa ametumia dakika zaidi ya tano, na kuigia kwenye gari lake, kisha akaliwasha na kuendesha taratibu kuelekea kule alikokuwa amegesha mwanzo, yani kule yalikokuwepo magari mengine, ambapo kwa hakika hakuona dalili ya magari ya jeshi la serikali, kupelekwa kwenye kisima cha mafuta cha MONUSCO, zaidi aliweza kuona askari wale wakiwa wamesimama pembeni ya gari lile kubwa lenye kufunikwa vyema, huku wakilitazama gari la Deus, kwa macho flani ambayo kama akili yako inafanya kazi vyema, lazima ungejuwa kuwa walikuwa wanakuzungumzia.
Deus aliachana nao, alienda taratibu mpaka pale alipokuwa amesimama mwanzo, na kugesha gari, safari hii akalizima kabisa, baada ya hapo akapapasa chini ya seat aliyokalia, ni wazi alikuwa anakagua kitu flani, na alipo jiridhisha kile alichokuwa anakipapasa, akalaza kiegemeo cha seat yake, kisha akatoa simu yake na kuangalia kama kuna ujumbe au simu yoyote iliyopigwa.
Mara tu baada ya kuitazama simu yake, Deus akajikuta akitabasamu peke yake, ni baada ya kuona ujumbe wa Whatsapp, uliotumwa na mtu alieitwa Pacha, “mambo mchoraji wangu” ilikuwa ni salam ya kawaida tu, ila ilitoka kwa mtu ambae mpaka sasa, alikuwa ni kama mtu wake wa karibu sana, japo hakuwahi kumuona anafananaje, “poa Pacha wangu, vipi hujaingia class?” aliandika Deus kisha akaituma kwenda kwenye namba aliuoisave kwa jina la Pacha, kisha akafungua nakilishi ya ramani ya kimtandao, na kuanza kuisaka ramani ya kaskazini mwa mji wa beni, akifuata barabara ambayo wangeitumia muda mfupi ujao, lakini kabla hajafika mbali akasikia simu yake ikiingia ujumbe, akaacha anacho kifanya na kufungua ule ujumbe, uliotumwa kwake kwa njia ya whatsapp.
Ujumbe ulikuwa unatoka kwa Pacha, aliusoma kimya kimya, na kuitimisha kwa tabasamu mwanana, bado sijaingia class” ndivyo ulivyo soma ujumbe huo, ambao ulifuatiwa na ujumbe mwingine, toka kwa Pacha, ambao pia aliufungua kwa haraka, “naona ulikuwa busy na biashara, maana nimekutumia sms muda mrefu, lakini hukujibu” Deus alitabasamu kidogo, huku anaandika ujumbe, “si unajuwa tena jua la Dar, lina changanya kiasi kwamba nasahau, hata kutazama simu” aliandika Deus, na kumalizia kwa kiragosi (emoj) cha kicheko, na wakati anamaliza kuituma kwenda kwa Pacha, ghafla mlango wa mbele wa gari lake, upande wa abiria, ukafunguliwa, hapo Deus akageuza uso wake haraka, kutazama upande ule wa seat ya abiria, huku anainuka na kukaa sawa.
Naam alichokiona Deus kilmshtua sana, maana hakutegemea kwa muda ule wala kwa siku za hivi karibuni, hakika ulikuwa ni mshtuko ulio ambatana na fadhaha, lakini Deus akajitaidi kuzuia mshtuko wake, na kuinua seat yake, akiiweka sawa, “habari yako askari” ilikuwa sauti nyororo ya kike,
Huyu alikuwa ni yule mschana mrembo, ambae Deus alikutana nae Entebe Uganda airport, na kusafiri pamoja kuja DRC, ambae sasa alikuwa anakaa kwenye ile seat ya mbele ya abiria, kwenye gari hili la Deus, “safi tu habari” aliitikia Deus kwa sauti tulivu, huku anawasha gari, na wakati huo huo, milango ya ya nyuma ya gari hilo ikafunguliwa, na kwakutumia kioo cha kati yaani back view, Deus akawaona watu wawili wakiingia ndani ya gari, ni wale ambao, walishuka na mwanadada huyu, kwenye ndege, siku ile pale goma air port, “habari yako kijana, naona tumekutana tena” alisamilia mmoja kati ya wale wanaume wawili, akitumia lugha ya kiswahili, japo hakikuwa kilichonyooka, lakini ilionyesha wazi kuwa wale jamaa, walikuwa wametokea ukanda wa Africa ya mashariki, na lafudhi yake ikifanana kabisa na watu toka Burundi.
Hakika watu hawa wawili waliokaa seat ya nyuma ya gari lake, nikama walimfanya Deus apunguze mshtuko wake, “salama habari zenu” alijibu Deus, huku ametazama mbele yaliko magari mengine, yaani yale ya jeshi la serikali, ambapo alionekana askari mmoja wa jeshi la FARDC, mwenye cho cha major, akiwa amrisha askari waingie kwenye magari, kisha yeye kuingia kwenye lile gari lenye askari watano wenye silaha nzito, huku askari wakiingia kwenye magari kama walivyokuwa mwanzo, huku wakimwacha kijana wa kicongo yule ambae alimletea karatasi chumbani, akiwa amesimama anaazama jinsi mambo yanavyoenda, “poa tu dogo, kumbe na wewe umekuja huku Ben?” aliuliza yule mwingine ambae pia aliongea Kiswahili chenye lafudhi ya watu wa kenya, “yah! Goma tulikaa siku chache sana” alijibu Deus, huku anafunga mkanda seat, na wakati macho yake yakiwa bado yame tazama mbele, ambako alimwona yule kijana wakicongo, akija upande wao usawa wa gari lao.
Naam! Alipo lifikia akaonyesha ishara kwa Deus ambae ndie dereva, kupeleka gari lake, nyuma ya gari alilopanda yule major, ambalo lilitanguliwa na gari moja kati ya yale mawili yenye silaha za 12 mm, lakini licha ya kupewa ishara hiyo, kijana Deus akuonyesha dalili ya kuondoa gari kwenda pale alipoelekezwa, “nadhani umeelewa ulichoambiwa au gari linatatizo?” aliuliza yule mwanamke ambae leo alionekana kuzidi kuwa mzuri, kwa sauti iliyo jawa na mshangao, huku anamtazama Deus kwa macho yenye kuchunguza na kusuta, “samahani naomba fungeni mikanda” alisema Deus, taratibu na kwasauti tulivu, bila kutazama kusoto wala kulia, “sidhani kama ni muhimu kuliko amri uliyopewa” alisema mschana yule ambae licha ya umri wake mdogo kuliko wale wanaume, lakini alionekana kuwa ndie mwenye madaraka makubwa.
Wale wenzie walifunga mkanda mara moja, ila yule mwanamke aliganda kidogo, kisha akafunga mkanda, na ndipo Deus alipo ondoa gari, wakati huo yule kijana wakicongo akiwa amesimama anawatazama, mpaka Deus alipo simamisha gari pale alipoelekezwa, huku gari kubwa lenye mzigo, yani Kamaz, likiwa nyuma yake, likifwatiwa na gari lenye 12 mm KAPEVETE, na ndio wakati ambao Deus alitazama side mirror, pasipo kulega kumtazama mtu yoyote, akajikua amemtazama yule kijana wa kicongo, aliekuwa mita hamsini yuma yao, ambae sasa alionekana akiwa makini sana, na mwenye wasiwasi, anatazama kulia, halafu kushoto, kisha nyuma yake, alipoona hakukuwa na mtu, akaingiza mkono mfukoni mwake, kisha akatoa simu yake, na kubofya namba flani, kisha akaiweka sikioni, ni wazi alikuwa anawasiliana na mtu flani…..unadhani hii safari ina usalama kweli? nini kitawatokea watu hawa, basi endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, unao kujia hapa hapa
jamii forums