Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI: Ukweli simulizi ilikuwa ni yakusisimua, siyo tu kwa Kanal Kasuba, ila pia kwa wengine wote waliokuwa wanasikiliza, “kijana kwanini unaficha utambulisho wako?” aliuliza Kanali Kasuba, huku anamtazama Deus machoni, lakini Deus ambae alikuwa anamtazama Kasuba, alionekana kutoa macho ya mshangao, na kwa kuona kama naweza kuona kitambulisho chako?” aliuliza kanal huku anamtazama Deus, huku amenyoosha mkono tayari kupokea kitambulisho…endelea…..


Hapo Deus mara moja akafungua mfuko mdogo wa begi lake, na kutoa kitambulisho chake cha kupigia kura, kisha akampatia yule kanali, ambae alikitazama kwa sekunde chache, kisha akamtazama Deus, “nahitaji cha kazi bwana Nyati” alisema kanali Kasuba, huku anampatia Deus kitambulisho chake, “nime maliza shule mwaka juzi, bado sija pata kazi yoyote” alijibu Deus huku anapokea kitambulisho chake na kukirudisha kwenye begi, huku kijana huyu anaomba wasije kumkagua na pengine wakaikuta ile bastora Walther P99, iliyopo ndani ya begi lake.


Hapo Kasuba akawatazama wenzake, kwa macho yaliyojaa mashaka, kisha akamtazama tena Deus, “uliwahi kupitia mafunzo yoyote ya kijeshi, kama vile JKT au…?” aliuliza Kasuba, huku anamtazama Deus, ambae kichwani mwake alijuwa wazi kuwa, endapo atasema kuwa aliwahi kufundishwa na baba yake ingemletea matatizo, maana ilikuwa ni kinyume na sheria, “hapana, sikuwahi kuingia JKT, maana nimeishia kidato cha nne” alijibu Deus, pasipo kuonyesha wasi wasi wowote, “vipi kuhusu afya yako” aliuliza kanali Kasuba, akiwa bado anamtazama Deus, huku wenzake wakisikiliza, maswali na majibu, “sina tatizo lolote la kiafya” alijibu Deus na hapo Kasuba akatulia kidogo, kisha akamtaza mmoja kati ya maafisa wajeshi waliokuwepo mahali pale, “kijana anafaa kujiunga na jeshi” alisema kanal Kasuba, huku akimtazama yule afisa ambae alikuwa na nyota tatu mabegani kwake, “nikweli afande, hii ni hazina kubwa katika taifa” alijibu yule afisa huku wenzake wakaitikia kwa vichwa, kuonyesha kuwa, wanakubaliana na mwenzao kuwa, Deus anafaa kujiunga na Jeshi,


Naam baada ya maongezi ya muda mrefu, huku Deus akaeleza kuwa anaishi songea na wazazi wake , na sasa anaelekea dar es salaam ambako, ametumwa na baba yake kwenda kuchukuwa gari ambalo liliagizwa toka Japan, akatoa namba zake za simu kwa Kanal Kasuba, pamoja na namba za baba yake, kisha akaingia wenye gari moja la jeshi na kupelekwa morogoro mjini ili akapate usafiri wa kuelekea dar es salaam, huku Kanal Kasuba akimweleza kuwa ata mtaarifu kipindi cha kuandikisha askari wapya, ili na yeye ajiunge na Jeshi, kitu ambacho Deus alikikubari kwa moyo mmoja, kutokana na kutamani jambo hilo kwa muda mrefu, ila alikosa namna ya kuingia jeshini.*******


Naam taarifa za ajali ya tren zilisambaa kwa kasi ya ajabu, kupitia vyombo mbali mbali vya habari, vya ndani na nje ya nchi, vilieleza kiufasaha jinsi watu sita kati ya nane waliokuwepo ndani ya tren hiyo walivyo nusurika toka kwenye ajali ya Tren, huku mmoja tu kati yao akivujika mguu, na watano wakiwa wazima kabisa, huku wawili wakiwa wamepoteza maisha, na tren kuingia mtoni kama ilivyo, “serikali inatoa pole kwa ndugu wa marehemu wote, na itasimamia mazishi” alisikika waziri wa usafirishaji, kwenye vyombo vya habari.


Wakati huo Deus alikuwa ndani bus, anaelekea dar es salaam kutokea morogoro, hakuna alie fahamu kuwa yeye ni mmoja kati ya watu walio pona kwenye hiyo ajali, ambayo ilikuwa imetawala kwenye vyombo vya habari, “namshukuru kijana Deus aliemsaidia binti yangu kutoka salama, nikimpata kuna zawadi yake” ilisikika sauti ya mwanamke mmoja, kupitia speeker za redio ya gari, ambae alisema kuwa ni mama wa mschana alienusurika toka kwenye ajali, yaani Caroline, aliekuwa anahojiwa na chombo cha habari, ni wazi alikuja kumfwata morogoro baada ya kupata taarifa ya ajali ya Tren, Deus alitamani watu wangejuwa kuwa yeye ndie anaezungumziwa, lakini hakuweza kujitambulisha, maana hakuna mtu ange amini, hivyo alikaa kimya huku safari ikiendelea.


Siku iliyofwaa Deus akiwa Dar es salaam, alienda kwenye kampuni ya magari ya Toyota waliyo itumia kuagiza gari lao, akamaliza taratibu za malipo na kukabiziwa gari, dogo zuri aina ya Toyota colloral c8, lenye uwezo mkubwa na nguvu kubwa sana katika kutembea, ukiachilia kuwa na vinu sita vya kufua nguvu (six cylinder) pia lilikuwa na cc 2490, na speed yake ya kiwango cha juu kabisa ikiwa ni 240 kwa saa.


Lakini basi, wakati anatoka pale Toyota campany, mitaa ya poster mpya, mara akaliona gali fulani dogo, linatoka kwenye jengo kubwa la jirani na Toyota, lililoandikwa BMW campany Ltd, lilikuwa ni dogo jeusi zuri sana, Deus akajikuta anasimamisha gari pembeni ya jengo lile, la BMW, na kuingia ndani, ambako alikuta magari mengi sana, madogo mazuri ya kifahari, akayakagua baadhi, ambayo kiukweli yalimvutia sana, japo alipouliza bei yake, akagundua ni kwanini baba yake akanunua gari lile, badala ya BMW.


Baada ya ukaguzi wake Deus aliondoka pale BMW, huku moyoni mwake akiweka ahadi yake kuwa ipo siku atanunua gari kama lile, yani aina ya BMW, ukweli hiyo ilikuwa ndiyo ndoto yake.*******


Naam Deus alirudi Songea, huku akifika salama na kukabidhi gari kwa baba yake, ambae tayari alikuwa amesha pata taarifa juu ya ajali iliyo tokea na kijana wake akiwa ndani, Deus akamweleza baba yake juu ya kile alichoelezwa na Kasuba, kuhusu kujiunga na jeshi, “una uhakika upo tayari kujiunga na jeshi Deus?” aliuliza mzee Nyati, huku anaendelea kukagua nyaraka za gari lake, “ndiyo baba, ninapenda sana kuwa mwanajeshi, nakumbuka uliniambia kuwa, uliwahi kuwa mwanajeshi huko #mbog_land” alisema Deus, “sawa niliwahi kuwa mwanajeshi, lakini si unajuwa nilipoishia, sasa nipo ukimbizini, kama muasi wa nchi wangu niliyoitumikia kwa nguvu zangu zote” alisema mzee Frank Nyati, safari hii akimtazama kijana wake, “lakini baba hiyo ilikuwa Mbogo Land, siyo Tanzania” alisema Deus ambae alikuwa anaonyesha kuhitaji kujiunga na jeshi.


Hapo Mzee Nyati akamtazama kijana wake kwa sekunde kadhaa, kisha akatazama mezani, zilipo nyaraka, siyo kwamba alikuwa anaendelea kusoma, ila alikuwa anatafakari jambo, “sawa, ila hakikisha utambilisho wako unakuwa ni wa hapa Tanzania” alisema mzee Frank Nyati, kisha akaendelea kupekuwa nyaraka zake, alifanya hivyo kwa sekunde chache kisha akasita kidogo na kumtazama Deus, “Deus, kama utajiunga na jeshi, kumbuka kuwa unatakiwa kuanza upya kila kitu, hata kama unakijuwa, ni hatari sana, kwako kama itabainika kuwa unafahamu mambo mengi kuhusu silaha, na mapigano ya ana kwa ana, pia katika kuruka vikwanzo na sehemu hatarishi” alisema mzee Frank kwa sauti iliyojaa umakini na msisitizo.******


Yap! miezi minne baadae, zilitangazwa nafasi za kujiunga na jeshi, Deus akatulia kusubiri simu ya kanali Kasubi, ya kumwita akajiunge na jeshi, ambapo ilipita miezi mitatu, bila Deus kupigiwa simu yoyote, kiasi cha kuanza kukata tamaa.


Miezi mitatu toka, tangazo la kujiandikisha na jeshi litoke, huku Deus akiwa ameshakata tamaa ya kupigiwa simu na Kanali Kasuba, ndipo siku moja jioni, Deus akiwa kwenye mazoezi ya kujilinda binafsi, ambayo uyafanya uwani pale nyumbani kwao, mara akamwona baba yake anakuja toka ndani, “Deus, siku tatu zijazo inatakiwa uwe umesha fika kwenye kambi ya mafunzo ya mwanzo ya kijeshi, huko Mfinga” alisema mzee Nyati na hapo tabasamu pana likaonekana usoni kwa Deus. ….…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA: Miezi mitatu toka, tangazo la kujiandikisha na jeshi litoke, huku Deus akiwa ameshakata tamaa ya kupigiwa simu na Kanali Kasuba, ndipo siku moja jioni, Deus akiwa kwenye mazoezi ya kujilinda binafsi, ambayo huyafanya uwani pale nyumbani kwao, mara akamwona baba yake anakuja toka ndani, “Deus, siku tatu zijazo inatakiwa uwe umeshafika kwenye kambi ya mafunzo ya mwanzo ya kijeshi, huko Mfinga” alisema mzee Nyati na hapo tabasamu pana likaonekana usoni kwa Deus….ENDELEA….


Naam kijana alisafiri mpaka Mafinga na kupokelewa, kwa maelekezo toka makao makuu ya jeshi, ikiwa ni nafasi ya pekee kabisa, aliyopewa kijana huyu na wenzake ambao waliandikishwa toka JKT, siku za kwanza ilimuwia vigumu sana, kukabiliana na changamoto za pale kambini, moja ikiwa ni kutengwa na wenzake, ambao walikuwa wana fahamiana na wenzao toka kwenye kambi mbali mbali za JKT.


Pili ilikuwa ni changamoto ya masimango, siyo tu kwa wazalendo wenzake, pia kwa wakufunzi ambao ni wanajeshi, waliomwita kuwa ni mpelelezi alietumwa toka makao makuu ya Jeshi, kuja kupeleleza mwenendo wa mafunzo na matukio ya mtu mmoja mmoja.


Deus hakuwa na la kufanya kila aliposimangwa alitabasamu na kucheka, na wakaki mwingine alijibu kwa sauti yake ya upole, “hapana jamani, mimi siyo mpelelezi”


Siku zilienda wanafunzi wakisubiri mafunzo yaanze, huku baadhi ya wanafunzi wenzake na Deus wakianza kumzowea na kujichanganya nae, japo alikuwa na uwezo wa kujikimu kwa mahitaji muhimu binafsi, ukiachilia chakula walichokuwa wanakula bure, na matibabu, lakini wenzake walikuwa wanalipwa kiasi flani cha fedha tofauti na yeye ambae hakuwa na malipo yoyote, sababu hakutokea JKT, ila sasa kila baada ya week alikuwa analetewa baadhi ya mahitaji muhimu na kwa miezi miwili waliyokuwa wakisubiri mafunzo yaanze, alikuwa anapewa kiasi fulani cha fedha, toka makao makuu ya jeshi, ikiwa na kutembelewa na wajumbe mbali mbali toka makao makuu ya jeshi, jambo ambalo liliwafanya wenzie pamoja na wakufunzi, wazidi kuhisi kuwa Deus alikuwa ni askari aliejifanya mwanafunzi, ili ajekupeleleza mwenendo wa mafunzo na utawala, yani kama wanafunzi wanapata wanachostahili.


Naam mafunzo yalianza mwanzoni mwa mwezi wa tatu, toka walipofika pale chuoni, hakika kila mmoja alimwonea huruma Deus, ambae nikama alikuwa analipia vile vitu alivyokuwa anapewa, maana kama wenzake walikuwa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili na mafunzo ya kivita, basi yeye alifanya mara mbili yake, ungeona hata muda wenzake wanapewa mapumziko mafupi yadakika tano au kumi, basi yeye ange kuwa anaruka kichura chura au anapiga push up, huku anasimangwa, “nichore vizuri sasa, wewe siunajifanya mchoraji” ni baadhi ya maneno ya wakufunzi, japo maneno kama hayo yalikuwa yanawakuta kuruti wengi, lakini kwa Deus ilikuwa ni mara mbili yake, na wenzake wanapo maliza mapumziko angejiunga nao, na kuendelea na ratiba kama inavyosema.


Mafunzo yaliendelea, huku Deus akijitahidi kuliko wenzake wengi waliopitia mafunzi yanayofanana na hayo, huko JKT, na akiwa darasani na hata kwenye mazoezi ya nje ya darasa, kama walivyo sema waheanga, kuwa uwezi kuwa mkamilifu kwenye kila kitu, ndivyo ilivyokuwa kwa Deus, ukweli kwenye kwata, yani foot parade, au miguu, ilimuwia vigumu, na kupata shida sana, kwa wakufunzi wake.


Lakini kwa upande mwingine, wa matumizi ya silaha, mbali mbali, utegaji wa mabomu na ufumbuzi wa vikwazo vidogo vidogo katika silaha ay mabomu, ulengaji wa shabaha, na wepesi wa vitendo katika uwanja wavita, na hata uwanja waporini na usomaji wa ramani, alijitaidi sana, na pia alijitahidi katika mazoezi ya utimamu wa mwili, kama vile kuvuka vikwanzo, kukimbia umbali mrefu,


Kipindi cha mafunzo, makao makuu walikuwa wanawafatilia kila hatua ya kijana huyo, ambae mpaka muda huo hawakuwa wanafahamu kuwa ni mwenye asili ya #mbogo_land, maendeleo ya kijana huyu yaliwafurahisha sana wakuu wa jeshi, hasa katika kitengo cha mafunzo na utendaji wa kivita, na licha ya mambo yote ya mafunzo magumu na masimango, lakini pia mkuu wa mafunzo wa chuo hiki cha kuruti, alijivunia sana Deus, na kumtumia kwenye maonyesho mbali mbali mbele ya wageni, mbali mbal waliokuwa wanatembelea shule ile,


Mfano wakati kundi hili la askari la mia nne ishirini, la mwaka 2011, linakaribia kumaliza mafunzo, lilitembelewa na kundi la mabrigedia general, toka nchi za SADEC, ambao walikuja kwenye semina ya week moja, katika chuo cha NDC, yani Nationl Defence Collage, ambao baada ya kumwona Deus, kwenye onyesho la kupita juu kamba, akiwa na begi la uzito wa kilo 25, pamoja bunduki yake aina ya SMG, huku akishuka na kupiga risasi therasini katika alama ya kati ya target, iliyopo umbali wa mita mia moja, katika mikao mbili mbali, ikiwa pamoja na akiwa katika mtembeo wa mbwa, yani mbio, “huyu ni mwalimu au mwanafunzi” aliuliza mmoja kati ya wageni, kwa mshangao, “ni mwanafunzi na bado hajahitimu, alijibu mkuu wa mafunzo na utendaji kivita, wa jeshi la ulinzi la Tanzania.


Iliwashangaza sana Ma- general wale, toka kusini mwa Afrika, “hakika Tanzania imezalisha shujaa mpya” alisema mmoja kati ya wageni wale, akimlenga Deus kuwa ndie shujaa anae mzungumzia,


Naam mpaka mwisho wa mafunzo, Deus ndie aliibuka mshindi wa darasani na porini, hata kwenye vikwanzo na shabaha, yani alipiga malengo, kuliko hata wasimamizi na walimu waliokuwa wanafundisha shabaha, jambo hilo lilifanya kijana huyo apelekwe makao makuu ya jeshi la ulinzi, katika timu maalumu ya shabaha, ambako alikaa miezi sita tu, akapelekwa nchini Cuba, kwenda kupata mafunzo ya mwanzo, ya special force commando, ambako alikaa miezi tisa, na kurudi nchini mwaka 2012 mwezi wa saba, ambapo hakumaliza hata wiki mbili, akapelekwa kwenye mafunzo ya udereva wa kijeshi, ambako alikaa miezi sita tu! ulikuwa ni mwezi wa kwanza ndio mwezi aliomaliza mafunzo, na kurudi makao makuu ya jeshi, ambako ni kikosini kwake.


Pale makao makuu hakukaa sana, ni siku tatu tu, ndizo alizokaa pale makao makuu, kabla hajapoa, akapelekwa Uhuru Cap, kujiunga na mafunzo maalumu ya ulinzi wa amani, akiwa kama mmoja wa kikundi cha special force troop, alifanya mazoezi kwa juhudi na hali ya furaha, akiamini, endapo ataenda safari hiyo ya ulinzi wa amani, japo ina hatari nyingi, lakini ingemletea mafanikio, katika maisha yake, na pengine kutimiza malengo yake ya kununua gari la ndoto yake, yaani BMW kipindi hicho kukiwa na BMW 6, ambayo hata picha ya jarida katika account yake ya whatsapp.


Kijana akiwa katika mafunzo hayo, siku moja usiku akiwa amejilaza kitandani, baada ya mazoezi magumu ya mchana kutwa akapokea sms ya Whatsapp, iliyomtaka atume hadithi, sms ambayo, licha ya kutambua kuwa imekosewa na mtumaji kuja kwake, lakini ikatengeneza urafiki kati yake na mtumaji, ambae alimtambua kuwa ni mwanamke, japo ni kama yeye alieweka picha ya nembo ya kampuni ya magari anayo yapenda ya BMW, yule rafiki yake, ambae siku mbili baadae, aligundua kuwa wamezaliwa siku moja, ya tarehe 26 nwezi wapili ya mwaka 1990, pia aliweka picha ya ua ridi, yani ua rose.


Pasipo kujitambilisha kazi yake, na huku akijuwa kuwa mschana anae wasiliana nae, ni mwanafunzo wa chuo cha usimamizi wa fedha huko Mbeya, Deus aliendelea kuwasiliana na maschana huyo ambae sikuzote alikuwa anamwita pacha, huku wakizidi kuzoweana na kuwa kama watu wanao fahamiana, huku yeye akijitambulisha kama mfanyabiashara ndogo ndogo, za kutembeza mitaani.


Naam miezi tatu minne baadae, Deus Frank akiwa bado katika mafunzo ya ulinzi wa amani, mida ya saa nne, za asubuhi, akaletewa taarifa kuwa anaitwa ofisi kwa afisa utawala, akasomewe simu ya upepo, iliyotumwa kwake toka makao makuu ya jeshi, ukweli mpaka hapo Deus akujuwa kama afurahi au ajisikitikie, maana akujwa barua hiyo inaleta taarifa gani, maana inaweza kuwa chochote, kibaya au kizuri......ilikufahamu kilicho tokea mpaka kijana Deus akaamuwa kuwa kama alivyo sasa, endelea kuwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHILINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MBILI: Naam miezi tatu minne baadae, Deus Frank akiwa bado katika mfaunzo ya ulinzi wa amani, mida ya saa nne, za asubuhi, akaletewa taarifa kuwa anaitwa ofisi kwa afisa utawala, akasomewe simu ya upepo, iliyotumwa kwake toka makao makuu ya jeshi, ukweli mpaka hapo Deus hakujuwa kama afurahi au ajisikitikie, maana uakujuwa barua hiyo inaleta taarifa gani, maana inaweza kuwa chochote, kibaya au kizuri…endelea…..


Maana ni mara nyingi watu huitwa kama hivyo na kusomea simu, zao zinazowaletea taarifa ya kuuguliwa kwa familia zao huko makwao, au pengine taarifa za misiba kabisa, za watu wa karibu, ambao ni tegemezi.


Lakini ilikuwa tofauti kwa Deus, ambae alielezwa kuwa siku inayofwata anatakiwa kwenda kuriport makao makuu, kwenye ofisi ya mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita, kwaajili ya kupangiwa kazi nyingine.*******


Deus Frank Nyati, ambae toka alipo somewa simu hiyo ya upepo, ya kuitwa makao makuu, alikuwa na wasi wasi mwingi, akihofia kuwa, huenda anaitiwa mafunzo mengine magumu zaidi, maana toka alipojiunga na jeshi miaka miwili iliyopita hakuwai kutulia kambini kwake hata mara moja, aliwasili makao makuu ya Jeshi, kwenye kitengo cha mafunzo na utendaji kivita, tawi la kazi za nje ya nchi, ambako alikutana na afisa mwenye cheo cha luten kanal.


Deus alievalia mavazi maalumu ya kivita, yani combat dress, alipiga salut kikakamavu, “jambo afande, mimi ni private Deus Frank Nyati, wa hapa makao makuu, kwasasa nimetokea Uhuru Camp kwenye mafunzo ya peace keeping, nime ambiwa nije nireport hapa” alisema Deus Frank kwa sauti iliyo nyooka, huku mkono ukiwa kwenye usawa wa saluti, “private Deus Frank Nyati, karibu sana” alisema yule afisa, ambae pia, alipiga saluti ikiwa ni jibu la saluti ya Deus, ambae pia alishusha mkono toka mkao wa saluti, “Asante afande” aliitikia Deus ambae alikuwa amesimama mguu sawa, “mguu pande bwana Nyati, pumzisha mwili, baada ya mafunzo mfululizo, sasa unaenda kufanya kazi na wazungu” alisema yule luten kanali, akionyesha sura ya tabasamu.


Deus ambae muda wote alikuwa na wasi wasi, juu ya wito wake pale makao makuu, aliweka mguu pande, huku akiwa anapata uafadhari moyoni mwake, japo hakujuwa anaendaje kufanya kazi na wazungu, “ila Nyati usisahau kurudi na kitenge cha shemeji yako, maana huko kunavitenge vizuri sana” alisema yule luten Kanal huku anatoa karatasi moja kwenye jarida, pale mezani, huku akimwacha Deus akiwa njia panda, japo mwanga ulianza kumjia kuwa anatakiwa kwenda moja kati ya nchi za Africa zenye kulindwa amani, “Private Deus Frank Nyati, dereva Shap shooter sniper, muuwaji wa siri, command special force……” alisema yule kanal, aliekuwa anasoma kwenye lile karatasi, kabla hajasita nakumtazama usoni Deus, kama vile ni kumbe cha ajabu, “sifa zote ni za wewe mmoja tu, au ni kikundi cha watu?” aliuliza yule luten kanal, huku anamtazama Deus, ambae alikuwa amesimama mguu pande, anamtazama kwa macho yake tulivu, na kuishia kutabasamu, pasipo kutamka neno, “ok!” alisema yule luten Kanal huku anatazama tena lile karasi, lililoandikwa mfumo wa mkataba flani.


“Deus Frank umechaguliwa kujiunga na kikundi cha waangalizi wa maswala ya kijeshi, yaani Military Observer MILOB mashariki ya DRC, jimbo la kivu ya kaskazini, chini ya mpango wa UN, MONUSCO, (ni kifupi cha maneno ya kifaransa yanayo someka, Mission de l'Organisation des Nations Unies pour la stabilisation en République démocratique du Congo, ikiwa na maana ya United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo or MONUSCO, kwa kiingereza) ukiwa kama dereva wa maafisa wa MILOB, soma huo mkataba, kuhusu malipo na huduma zote utazo kuwa una pata” alisema yule luten Kanali, huku anampatia nakara ya moja ya karatasi, Deus akakaa mguu sawa, na kupiga salut, “asante sana afande” alisema Deus, na yule kanal akajibu ile salut, kisha wakashusha mikono kwa pamoja, “ukisha soma huo mkataba, nenda hospital kuu ya kijeshi lugalo, kariport kwa afisa utabibu, utakutana na maafisa watatu, ambao mnaenda pamoja huko DRC, mkafanye taratibu za kiafya, kwaajili ya safari, ila kumbuka kuwa wewe ndie askari wakwaza kuwa ndani ya MILOB, ukiwa na cheo kama cha kwako, hivyo nibahati sana, hakikisha unatunza heshima ya jeshi letu na taifa kwa ujumla.


Nikweli ilikuwa bahati kwa askari huyo, nasema bahati sababu haikuwai kutokea askari wa cheo cha chini ya captain yaani nyota tatu, kujiunga na kikundi kama hicho, ambacho, hukusanya maafisa wakuu weye taaluma mbali mbali, kwenda kufanya uangalizi wa shughuli za ulinzi wa amani, nchi mbali mbali, chini ya umoja wa mataifa, yani United Nations.


Ilikuwa bahati kwake, maana alimini kuwa ndani ya maika mitatu aliyo hudumu ndani ya jeshi, angeweza kutimiza malengo yake, ikiwa ni pamoja na kununua gari la ndoto yake, aina ya BMW, aliamini ingewezekana, hasa kutokana na malipo makubwa ambayo angelipwa kwa siku, katika kipindi cha mwaka mzima, kutokana na maelezo ya mkataba wake, angelipwa dolla mia tano kwa siku (sawa na Tsh laki nane kwa mwaka huo wa 2013, ambazo angetakiwa kulipia nyumba ya kulala na chakula, kikawaida nyumba angelipia dolla mia mbili kwa mwezi mzima, na kama asingechangia na mtu, chakula asingeweza kumaliza laki tano kwa mwezi, hivyo malipo ya siku moja yangetosha huduma za mwezi mmoja, (msomaji kumbuka hii hadithi ya kubuni, aina ukweli unao husiana na tukio lolote la kweli, hata yanayo simuliwa ni ya ubunifu tu)


Siku tatu baadae, saa mbili asubuhi, Deus Frank Nyati akiwa na maafisa watatu, wenye vyeo vya meja, walishuka toka kwenye ndege ya shirika la ndege la Tanzania, katika uwanja wa Entebe lnternational nchini Uganda, na kuungana na maafisa kadhaa toka kwenye majeshi ya nchi mbali mbali za Africa, yakiwemo Africa ya kusini (SA ARMY), na Malawi (MAL ARMY) #Mbogo_land (ML ARMY), wote wakiwa ni maafisa wa kuanzia vyeo vya major mpaka luten kanal, katika jinsia toauti, yaki kiume na kike, ambao walionekana kufahamiana, na kuongea pasipo kujari nchi zao, kitu ambacho Deus alikitabiri kuwa, ni kutokana na kuwahi kufanya kazi, au mafunzo flani kwa pamoja sehemu, kilicho watofautisha maafisa hawa ni utofauti wa mavazi yao ya kijeshi, yaani kombati, kila mmoja alivaa nguo za nchi yake, huku akiweka beji ya bendera ya nchi yake, kwenye ukingo wa bega lake la kulia, mwishoni mwa kibebeo cha cheo vyeo vyao.


Hapo kwa kujiona alikuwa peke yake, Deus akatoa simu yake na kutazama kama kuna sms kwenye whatsapp, ambazo ziliingia akiwa Tanzania, kabla ya kuanza safari, na network kukata baada ya kuingia Uganda, ambapo alikuta sms chache sana, kati yake zikiwa zinatoka kwa pacha, yani yule mwanamke ambae amekuwa rafiki yake pasipo kuonana nae, moja kati yake ilikuwa inamsalimia, na nyingine kumwuliza kama ameshaelekea kwenye biashara zake, Deus alishindwa kujibu, maana hakuwa na network.


Yalikatika masaa mawili, wakiwa pale Entebe Air Port, wakiwa wanasubiri ndege nyingine ambayo wangesafiria kwenda Goma Kivu ya kaskazini, nchini DRC, Deus akiwa ametulia peke yake, akiwashuhudia wakubwa wake wakazi, wakiongea na wenzao, wa maitaifa mengine, huku yeye akikosa wa aina yake, maana alioneana kuwa mgeni kuliko yoyote pale Air port, hali hiyo ilimfanya Deus atamani safari iendelee, ili aweze kufika huko DRC akatumikie kwa mwaka mmoja, ili siku akirudi aende likizo akawaone wazazi wake ambao alikuwa na muda mrefu hakuwa amewaona zaidi ya kuwasiliana nao kwa njia ya simu.


Naam hatimae ndege moja kubwa ya shilika la ndege la Ethiopia airline, ikaingia pale uwanjani, japo mwanzo hakujuwa kama ile ndiyo ndege wanayo safiri nayo, lakini baadae wakatangaziwa kuwa, askari wote, yani toka Tanzania na wale wamataifa mengine, wanatakiwa kuingia ndani ya ndege ile kubwa.


Naam wote kwa pamoja baada ya kumaliza kukaguliwa, waliongoza kwenye gazi ya ndege hiyo, na kuingia ndani, ya ndege ile kubwa, ya shirika la ndege la Ethiopia ya daraja la kibiashara, haikuwa ngeni sana kwa Deus, ambae alishawahi kusafiri na ndege kama hizi, alipoelekea nchini cuba masomoni.


Mle ndani ya ndege, mlikuwa na watu wengine, ambao walikuwa wamevalia nguo nadhifu za kiraia, nao wakiwa katika jinsia tofauti yani wakike kwa wakiume, safari hii licha ya kuwaona wale maafisa wajeshi, alio ongozana nao, wakikaa wenyewe kama walivyo kuwa wanapiga story pale nje, na yeye akaamua achague seat moja nzuri ambayo itamfanya aione safari kuwa ni fupi.
Deus akiwa kwenye korido refu la ndege hii ya kisasa, akatazama kushoto na kulia kutazama seat itakayo mfaa, mpaka alipovutiwa na seat moja ya pembeni ya seat ambayo ilikaliwa na mschana mrembo kweli kweli mwenye asili ya Ethiopia, ambae muda huo alikuwa anasoma kitabu, “lazima atakuwa anaongea kiingereza anafaa kuwa kampani yangu huko Congo” alijisemea Deus, huku anaisogelea ile seat, pasipo kujuwa huo ndiyo mwanzo wa kubadiri maisha yake kutoka kuwa askari hodari mpaka kijana anaeshiriki uharifu…….....ilikufahamu kilicho tokea mpaka kijana Deus akaamuwa kuwa kama alivyo sasa, endelea kuwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: Deus akiwa kwenye korido refu la ndege hii ya kisasa, akatazama kushoto na kulia kutazama seat itakayo mfaa, mpaka alipovutiwa na seat moja ya pembeni ya seat ambayo ilikaliwa na mschana mrembo kweli kweli mwenye asili ya Ethiopia, ambae muda huo alikuwa anasoma kitabu, “lazima atakuwa anaongea kiingeleza anafaa kuwa kampani yangu huko Congo” alijisemea Deus, huku anaisogelea ile seat, pasipo kujuwa huo ndiyo mwanzo wa kubadili maisha yake kutoka kuwa askari hodari mpaka kijana anaeshiriki uharifu……ENDELEA……


Deus aliembea taratibu, kuisogelea ile seat ya karibu na yule mrembo, ambae licha ya kufunika nywele zake kwa kitambaa maalumu cha kichwani, lakini zilionekana wazi upande wa mgongoni, jinsi zilivyo nyeusi na ndefu, huku macho yake yakiwa kwenye kitabu alicho kuwa anasoma, huku moyoni mwake kijana Deus, akiwaza namna ya kumkabiri mschana huyu mrembo, kwa lugha ya kiengereza, ambayo yeye alikuwa anaifahamu kwa juu juu, nasiyo kwa undani zaidi.


“Hi” alisalimia Deus huku anakaa kwenye seat ya pembeni ya mschana yule, ambae kimtazamo, ni kama alikuwa na miaka ishirini sita au saba, hivyo angekuwa amemzidi kijana wetu miaka kati ya mitatu au minne, ambae aligeuza uso wake na kumtazama kijana Deus, ambae wakati huo alikuwa amevalia mavazi yake nadhifu ya kijeshi, yaliyomkaa vyema kwenye mwili wake na kufanya umbo lake la mazoezi, lililo shabihishwa na urefu wa kijana huyu wakupendeza vionekane vyema.


Ilitumi kama sekunde nne kwa mschana yule, mwenye mwonekano wa kihabeshi usoni pake, huku umbo lake likiwa la kuvutia, maana alimtazama juu mpaka chini, kisha akapandisha tena uso wake na kumtazama kijana usoni, “mambo” alijibu yule mwanamke kwa lugha adhimu ya Kiswahili iliyo nyooka, kiasi cha kumfanya Deus atabasamu kidogo, “ni bahati kumbe wewe ni mtanzania?” aliuliza Deus akionyesha wazi kufurahia jambo lile, “kwani uwezi kuongea na mtu toka taifa jingine?” aliuliza yule mschana, kwa sauti kavu, huku akimtazama Deus kwa macho ya ukali, akionyesha wazi kuwa hakupendezwa na maneno ya kijana wetu Deus.


Hapo Deus akatuliza akili na kumtazama mschana huyu, akijaribu kuisoma hali yake kwa muda ule, ukweli ukimtazama kwa macho, usingekubali hata kwa viboko, kuwa ni mtanzania, maana mwonekano wake ulionyesha wazi ni raia wa Ethiopia, lakini Kiswahili chake, ndio kinge kuweka njia panda, maana ungesema umekutana nae tegeta au msata.


Deus aligundua kuwa, mschana huyo, alikuwa amechukizwa na kauli ile yenye mtazamo wa kibaguzi, “haaaaa….hapana… ila tu.. niliiii….nilikuwa na hofia kuwa tusinge elewana lugha” alisema Deusi kwa namna ya kujitetea, japo kiukweli hiyo ndiyo sababu halisi ya kufurahi kwake.


Yule mschana mrembo, hakuongea tena neno jingine zaidi akatazama kitabu chake, ambacho jarada lake lilikuwa limeandikwa HELLO DOCTOR, hapo Deus akawa mpole kidogo, na kuanza kuwanza jinsi atakavyo sawazisha makosa yake, japo hakuwa na uzoefu mkubwa wa kucheza na akili za waschana, lakini alijaliwa busara.


Kwanza Deus akatoa simu yake na kuanza kujifanya anaperuzi, wakati hakuwa na network, huku akili yake ikiwa ni ataanzaje kuongea na mschana huyu, ambae siyo tu uzuri wa sura yake, ila pia alionekana kuwa ni mtu mwenye heshima zake, hasa kutokana na mavazi aliyo ya vaa, pia utulivu wake, na hata ukimtazama kwa macho, ungejuwa ni mtu mwenye taaluma flani, kiwango cha juu, maana ukiachilia vijimiwani vyake vya macho alivyo vivaa, pia alikuwa amefunika nywele zake, kwa kitambaa cha rangi ya maziwa, kilichofanana rangi na suit ya kike aliyoivaa, suit iliyo mkaa vyema mwili mwake, huku akiongeza na vito vya thamani alivyo vaa mwilini mwake, kama vile hear ring, pete na mkufu, hata viatu vyake vya kumbukiza, vyeusi vilikuwa vizuri sana.


Baada ya kuwaza kwa muda flani, Deus akapiga moyo konde, na kumvaa yule mschana, “samahani dada naitwa Deus kutoka Tanzania, naelekea DRC, napenda kukufahamu kama hutojari” alisema Deus, kwa sauti tulivu ya upole, huku anamtazama mschana yule kwa macho yake, ambayo siku zote, huwa yanamtambulisha tabia yake ya utulivu na upole.


Yule mschana alifunika kitabu chake, na ukilaza kwenye paja lake pana, kisha akamtazama Deus, “kaka nivyema kama ungeweka mawazo yako kule unakoelekea, kuliko kuanza kuhitaji kujuwa majina ambayo hayatokusaidia” alisema yule mschana mrembo, kwa sauti ya chini tulivu, kisha anageuka na kuchukuwa mkoba wake mdogo, ambao ulikuwa pembeni yake, akaufungua na kutoa simu yake ya kisasa, na ear phone, ambayo aliichomeka masikioni, na kuweka music flani, ambao Deus hakupata bahati ya kuusikia, kisha akafunua kitabu chake, na kuendelea kusoma.


Hapo Deus akaona tayari amesha poteza haki ya kuongea na mschana yule mrembo, hivyo na yeye akainamia simu yake, na kuanza kutazama picha alizopiga akiwa katika mzeozi ya kijeshi, katika vyuo mbali mbali, kabla hajasikia tangazo toka kwenye speeker za ndege ile, ikiwashauri wa funge mikanda, tayari kwa kuanza safari.*******


Naam masaa mawili ambayo ndege ilikuwa hewani, yalimuwia vigumu sana kijana Deus, ambae japo Deus hakuwa mwongeaji sana, ila alijihisi unyonge sana, na kutamani ndege ifike haraka, ashuke, na yule mschana aendelee na safari.


Japo mawazo na matamanio yake yalikuwa tofauti, maana baada ya ndege kutua, katika uwanja ndege wa Goma, jirani kidogo na kitongoji cha bhilelee, pembezoni mwa barabara iendayo kaskazini mwa jimbo la kivu ya kaskazini, yaani mikoa ya Bhutembo na Beni, kupitia mbuga za wanyama za Vilunga, kilomita zaidi ya ishirini toka mlima mrefu wa Volocano, wa nyilagongo, ukanda ambao kwa kiasi kikubwa, ulikuwa umekaliwa na waasi wa M 23


Wakati Deus akiwa anashuka toka ndani ya ndege, akiongozana na wale makamanda wenzake, yani wa kutoka Tanzania, na wale wanchi nyingine, akashangaa kuona yule mschana mrembo wakihabeshi, akishuka toka ndani ya ndege, akiwa ameongozana na wanaume wawili, nao wenye mwonekano wa ki-Africa, ambao walipokelewa mabegi yao makubwa, nakuongozwa, kuelekea upande ambao, kulikuwa na magari mawili, moja likiwa ni bus dogo aina ya Toyota Coster, lenye maandishi makubwa meusi, UN na pembeni yake kukiwa na nembo ya umoja wa mataifa ya rangi ya blue, pamoja na maandishi ya blue, MUNOSCO, huku jingine likiwa ni gari dogo, aina ya Toyota land Cruizer, nalo jeupe, lenye maandishi makubwa ubavuni, kama lile bus, UN lakini hili yalikuwa ya rangi ya blue, na mbele ya maandishi hayo kulikuwa na nembo ya UN WHO, nayo ya blue.


Kitu ambacho kilimfanya Deus ajihurumie nafsi yake, ni pale alipowaona wale watu watatu, wakiongozwa na wale waliowapokea mizigo, wakielekea moja kwa moja, kwenye lile gari dogo, Toyota Land Cruize, na kuingia ndani ya gari hilo, huku yule mschana mrembo akienda kukaa kwenye seat ya mbele upande wa abiria, kisha lile gari kuondoka zake, wakiwaacha wao wanachukuwa mizigo yao na kuelekea kwenye lile bus dogo, yani Toyota Coster, ambalo lilikuja kuwapokea wao, maana hata derva wa gari lile, alikuwa ni askari mwenye cheo cha koplo, toka nchini Nigeria.


Deus aliambatana na wenzake, ambao ni wakubwa wake kwa cheo, kuingia ndani ya gari, na kuanza safari kuelekea, kwenye ofisi za makao makuu ya umoja wa mataifa, pale goma, huku akiombea kuwa, asikuane tena na yule mwanamke, mwenye malingo na dharau, ambae yeye pasipo kujuwa kuwa ni afisa wa UN, alianza kumchombeza kule ndani ya ndege.


Naam Deus alidhania kuwa ni bahati yake, maana alihisi kuwa mambo yameenda kama alivyo tamani yawe, maana week nzima aliyo kuwepo pale Goma, hakuwahi kumwona yule mwanamke wala wale wenzake, na tayari walisha patiwa vitambulisho vya umoja wa mataifa chini ya MUNUSCO, pia yeye kwa upendeleo, akapangiwa kuishi ndani ya kambi moja la jeshi, la pale pale mjini Goma, la MUNIG BASE, lililopo kilomita kama tisa toka mjini, ambalo lilikuwa linakaliwa na askari wa kutoka nchi mbili, wenye jukumu moja, yani platoon mbili za Tanzania, na platoon mbili za kutoka afrika ya kusini.


Bahati aliyokuwa nayo Deus nikwamba, hakutakiwa kulipia nyumba, maana aliishi kama askari wenzake, na hata chakula alipewa kipaumbele na kula chakula cha pekee, pale kambini, na pia tayari alisha kabidhiwa gari, ambalo alikuwa anawaendesha wale maafisa aliokuja nao toka Tanzania, ambalo lilikuwa lina lala pale Munig Base, na alifanya majukumu hayo akiombea asije akakutana na yule mwanamke wa kihabeshi, ambae mpaka hapo hakuwa anajuwa anahusika na nini katika UN.


Sasa tayari kijana Deus alishabadili line ya simu, na kuweka mtandao wa kule Congo, ambao ulimsaidia kupata network ya kuwasilina na wapendwa wake Tanzania, akiwa pamoja na rafiki yake wa simu, Pacha, japo pia aliweza kuwasiliana kwa line yake aliyotoka nayo Tanzania, ila kwaajili ya kupokea simu tu, endapo angepigiwa na mtu toka tanzania.


Deus alizidi kujiona mwenye bahati zaidi, week moja baadae, baada ya kupata safari ya kuelekea mkoa wa ben, kuwapeleka wale maafisa wake, japo barabara ilikuwa ni ngeni kwake, lakini kwa uwezo mkubwa ambao kijana huyu alikuwa nao katika kuendesha gari, alitumia masaa kumi na moja, pasipo kujari ubovu wa barabara ile, kuingia Ben na kisha moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa Ben Mavivi, kwenye kambi ya jeshi chini ya UN, inayokaliwa na majeshi ya MONUSCO, toka nchi za Filipino na India, kilometer kumi toka mjiniBen.


Upande huo, ni upande ambao umezungukwa na misitu mikubwa sana, ya kaskazini mashariki mwa Kongo, ni upande ambao, ulikuwa umetawaliwa na tishio la uwepo wa kikundi cha waasi wa zamani wa Uganda, wa IDFNALU, ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wanahusishwa na matukio yote mabaya ya upande huo wa Congo, kama vile, utekaji nyara, mauwaji ubaki na uporaji wa mali za raia na serikali.


Hapo Deus akajiona kuwa yupo sehemu salama, japo ilimuwia vigumu kuishi na watu mafia mengine ambao hata lugha walikuwa hawaelewani, na ukichulia kuwa wale wakubwa wake, muda mwingi walikuwa maofisini, wanafanya majukumu yao, na mbaya zaidi ofisi zilikuwa pale pale kambini, kiasi kwamba, muda wote yeye Deus alikuwa ametulia kwenye sehemu aliyofikia, akiperuzi mtandaoni, na kuchat na rafiki yake aliemwita Pacha, kutokana na kufanana kwa tarehe yao ya kuzaliwa. maana hakuwa na haja hata ya kuwapeleka wakuu wake ofisini, kutokana na ukaribu wa ofisi.******


Naam! kijana Deus akiwa anaamini amesha kaa mbali na sehemu ambayo yupo yule mwanamke mjivuni, siku tatu baadae, mida ya saa mbili, za asubuhi, Deus akiwa ametulia chumbani kwake anatazama tv, huku mara chache akichat na mwanamke aliemsevu kwa jina la pacha, kwenye simu yake, mara akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, akainuka na kwenda kuufungua, hapo akakutana na kijana mmoja wa kiafrika alieshika karatasi mkononi, “mambo vipi rafiki, biko Bien?” alisalimia yule kijana kwa sauti yenye rafudhi ya wenyeji wa pale Congo. …….....ilikufahamu kilicho tokea mpaka kijana Deus akaamuwa kuwa kama alivyo sasa, endelea kuwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Jinsi inavyoenda mbele ndio inazidu kuwa tamu zaid usiache kufuatilia
 
Hatari
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: lakini hakupata jibu, zaidi ya kuwaona wale wote watatu, wakimtazama kijana mdogo Deus, na wao wakamtazama, ‘eti dogo, mmetokaje ndani ya hii tren, tena mkwa hamja pata majeraha yoyote?” aliuliza yule mwanajeshi wa jeshi la ulinzi wenye cheo cha Canal, huku anamkazia macho Deus, ambae alikuwa tofauti na wale wengine, kwamaana akuonyesha dalili ya wasi wasi, wala taharuki ya ajali….…endelea….


“tuliruka tu, hakuna cha zaidi tulichotumia” alijibu Deus Frank, ambae kama ungemkuta pale usingedhania kama alikuwepo ndani ya ile tren, labda kule kuchafuka kwake ndio ungegundua kuwa alikuwa mmoja wa walionusulika toka kwenye ajali.


Kwa jibu hilo yule Kanali alievalia sare za kijeshi zile za kivita, alimtazama yule kijana toka juu mpaka chini, halafu akatazama Caroline, kabla hajawatazama wale wengine watatu, na kisha akarudisha macho yake tena usoni kijana Deus, “lakini wewe siyo mfanyakazi ndani ya hii tren?” aliuliza yule Kanali, huku anamkazia macho Deus, ambae alitabasamu kidogo, huku anakwepesha macho yake ya upole, “ndiyo mzee huyo na huyu mschana ni abilia waliokosa express, tukawapa lift, ila yeye ndie alietusaidia kuruka toka kwenye Tren” alisema yule dereva wa Tren kwa msisitizo, wakati huo tayari wanajeshi walioenda kusaka miili ya watu walioruka kule nyuma, walikuwa wanarudi huku wamebeba watu wawili pamoja na begi kubwa la mschana Caroline, naamini tutafahamu kwanini waliliacha.


Hapo wanajeshi wote pamoja na wale wa jeshi la ukoaji, wakamtazama Deus kwa mshangao, “kwa hiyo walioumia na kufa hukuwapa maelekezo, au hawakufata maelekezo yako, “aliuliza yule Kanal ambae kwenye shati lake, juu ya mfuko wa kifuani, upande wa kushoto kulikuwa na neno Tanzania, na upande wa kulia kulikuwa na neno JP KASUBA, huku mabegani mwake kukionekana nyota mbili chini ya ngao ya taifa, wengi huiita bibi na bwana, kushoto na kulia, “waliruka mapema, kabla hatuja elezana chakufanya” alisema Deus, kwa sauti yake tulivu.


Wakati maongezi yanaendelea, mara akaja askari wa jeshi la ulinzi, huku akiwa amevalia groves za kitabibu mikononi mwake, ilionyesha wazi kuwa ni muuguzi, alipofika alipiga salut na yule Kanali Kasuba akaitikia kwa salut, “afande tupo tayari kuondoka, kumwaisha yule majeruhi, amevuja damu nyingi sana” alisema yule askari mwenye alama ya yota mbili mabegani mwake, “ok! sawa wachukuwe na hawa wanne, huyu bado nina maongezi nae” alisema Kanal, pasipo kupepesa macho, huku anamtazama kijana Deus, kwa macho kama ya kutaka kubaki pamoja nae, na hapo mschana Caroline pia akamtazama Deus, ambae pia alikuwa anamtazama kwa macho ya tabasamu, “usijali mdogo wangu, tutaonana tu” alisema Deus kwa sauti tulivu, “usijari binti tangulia tu, yeye anakuja, tuaongea mambo ya kikazi” alisisitiza Kanali, safari hii kama vile anamwondoa wasi wasi Caroline, ambae alikubali kuongozana na yule askari pamoja na wale wafanyakazi wa TAZARA, mpaka kwenye gari la wagonjwa, ambako alilikuta begi lake.


Kanali Kasuba pamoja na askari wengine, wakiwa na Deus ambae pia alikuwa na begi lake dogo mgogoni, wakiwa wana wasindikiza kwa macho wakina Caroline, ambao walipolifikia gari, nikama walikuwa hawaamini kilicho watokea, kila mmoja kwa wakati wake aliweza kusimama na kugeuka kutazama kule alipokuwepo Deus, kisha kuingia kwenye gari.


Caroline yeye alivunja record, maana alipogeuka na kumazama Deus, akajikuta anapunga mkono, hata wakina Kasuba wasijuwe anapungiwa nani, “dogo punga mkono” alisema Kasuba akimlenga Deus, ambae alipunga mkono huku anatabasamu, na hapo kidogo Caroline akaachia kijitabasamu, kilicho ambana na simanzi, niwazi alihisi asingeweza kumwona tena kijana huyu, ambae amekuwa msaada mkubwa kwake, katika ajali hii.


Naam wakina Caroline waliingia garini, na gari likaondoka kuelekea mjini, na wakina Kasuba wakilisindikiza kwa macho mpaka lilipotoweka, “imeisha hiyo, niwazi umekuwa muhimu kwao, kiasi kwamba kila mmoja anahitaji muendelee kuwa wote mpaka mwisho wa safari yenu” alisema kanal Kasuba na wote wakacheka kidogo, huku Kasuba anamgeukia Deus, “dogo unaweza kutueleza ilikuwaje ukaweza kuwasaidia hao wote kutoka ndani ya tren?” aliuliza Kasuba, na wenzake wote wakatega masikio macho kumsikiliza kijana Deusi, ambae alianza kutoa maelezo mara moja.*******


Naaam ilikuwa hivi, baada ya kuwatuliza wale wafanyakazi wa TAZARA nao kuacha kila walicho kuwa wanakifanya na kumtazama Deus, huku Tren ikizidi kukaribia daraja, ndipo Deus, akamtazama yule dereva, “mzee kuna namna ya kupanda juu ya behewa?” aliuliza Deus, na yule dereva wa Tren akajibu haraka, “behewa hili hauwezi kupanda labda linalofwata, hilo lipowazi” Deus hakusubiri huyu mzee amalize kujibu, “twendeni haraka, kwenye hilo behewa tumekaribia daraja, alisema Deus, ambae kwa upande wake tayari alikuwa amesha vaa begi lake dogo mgongoni, maana ukiachilia nguo chache zilizo kuwepo, pia kulikuwa na vitu muhimu kwake, kama vile Fedha, vyeti vyake vya shule, na bastora ndogo, ya kisasa aina ya Walther P99, inayotumia risasi yenye mzingo wa mm 6, ambayo anaimiliki kinyume cha sheria, maana hakuwa na kibali cha kumiliki, japo siyo ya kufanyia maovu, hii alipewa na baba yake kwaajili tu, ya kuhakikisha anaitumia kukabiliana na lolote la unyang’anyi litakalo toke akiwa njiani na gari ambalo anaenda kulifwata.


Deus akamshika mkono Caroline ambae licha ya kuwaona wale wafanyakazi wa tren wanaelekea upande wa nyuma wa behewa lile fupi la wafanyakazi wa Tren, yeye alikuwa anamtazama Deus, “begi langu” alisema Caroline, na hapo Deus ambae licha ya kumshangaa mschana huyu kwa kukumbuka begi lake, katika hali ya hatari kama hii, lakini hakumsemesha chochote mschana huyu, zaidi ya kumwachia mkono, na kulishika lile begi kubwa na zito la mschana yule, kisha aka sogea mlangoni akafungua mlango na kulitupa lile begi, pasipo kuangalia lilipo dondokea, kisha akamfwata Caroline, na kumshika mkono kisha kuelekea kule ambako wengine walielekea, ambao sasa walikuwa wamesha fungua mlango na kutoka nje.


Nawalipotoka nje waliwakuta wale jamaa watatu wamesha panda juu ya behewa lenye mbao, na kumsubiri, Deus, ambae alimsaidia Caroline kupanda kwenye mbao za kwenye behewa, huku wale wengine wakimpokea kule juu, kisha Deus nae akapanda juu, ya behewa lile, wakati huo tayari kichwa cha Tren kilikuwa kimebakiza mita kama mia mbili na nusu kuingia darajani, daraja ambalo lilikuwa limesha sombwa na maji, jamani sikilizeni, kosa lolote litagharimu maisha yako au ulemavu wa kudumu, hivyo fanyeni kama niakavyo waeleza” alisema Deus huku anamshika mkono, Caroline, na kuanza kukimbia juu ya mbao, kurudi nyuma zaidi ya Tren, hata wale jamaa watatu pia wakakimbia kuwafwata, mpaka karibu na mwisho ambapo Deus alisimama, akiwa bado amemshika Caroline, nawao wakasimama.


“jamani hatuna muda wakupoteza, mtaruka juu kwa kuelekea nyuma pembeni kidogo ya usawa wa behewa, unapotuwa jilegeze kiasi, mme elewa?” alipiga kelele Deus, “ndiyo” japo walijibu kwa pamoja, lakini kiukweli zilikuwa sauti za chini, ambazo zilikosa matumaini, “haya kila mtu kwa wakati wake, kumbuka kosa moja unapoteza maisha” alisema Deus, na hapo watu hawa kama vile hawaja mwelewa Deus, wote wakamtazama, wakamtazama Deus kisha akamshika Caroline, na kunyanyua kama mtoto, kifuani kwake, kisha akapiga hatua tatu upande wa kulia wa behewa na kuruka juu, Caroline alijikuta akipiga ukelele mkubwa wa uoga, huku anafumba macho kwa uoga, huku akijikuta wakielea kwa sekunde kadhaa hewani, kabla hawaja tuwa chini na kwenye vidimbiwi vidogo vya maji pasipo kupata jeraha hata moja.


Na wale wengine lipoona hivyo, nao wakaruka kama alivyofanya Deus, japo walipata vimichubuko vidogo, wakati huo huo waliweza kuona kichwa cha tren kikiacha njia yake na kutumbukia mtoni, na mkia wake ukifwatia, “baada ya hapo ndio tuka rudi kwenda kuwaangalia wale walioruka mwanzo, pamoja na begi la yule mschana, ambalo tulilikosa, likaja kuonwa na hawa askari” alisema Deus, akimaliza kumweleza Kanali Kasuba.


Ukweli simulizi ilikuwa ni yakusisimua, siyo tu kwa Kanal Kasuba, ila pia kwa wengine wote waliokuwa wanasikiliza, “kijana kwanini unaficha utambulisho wako?” aliuliza Kanali Kasuba, huku anamtazama Deus machoni, lakini Deus ambae alikuwa anamtazama Kasuba, alionekana kutoa macho ya mshangao.


Naweza kuona kitamburisho chako?” aliuliza kanal huku anamtazama Deus, huku amenyoosha mkono tayari kupokea kitambulisho….…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom