Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI SITA: Lakini wakati Deus anakaribia ofisi za jiji yaani kwa Mayor wa Ben ndipo alipoiona pikipiki iliyokuwa imesimama upande wa pili wa barabara pembeni ya safu ya maduka yaliyotazamana na jengo kubwa la ofisi za mayor ikiwa na watu wawili, mmoja ambae ni dereva akiwa amevaa kofia ngumu na kushusha kioo cheusi cha mbele, nakufunika sura yake, huku kijana mwingine, ambae kwa mwonekano ni mwembamba, aliekuwa kama abiria kwenye pikipiki ile……..….endelea….

Akiwa amevalia suruali ya kitambaa chepesi ambayo mkanda wake aliufungia tumboni, shati alichomekea vyema na kupendezeshwa na viatu vyake vya ngozi vyenye kung’aa kwa rangi ya ngozi ya chatu, kichwani akiwa ameivalia kofia nyeusi ya cap aliyoishusha mpaka usawa wa macho yake…kiasi kwamba hata uso wake usingeweza kuonekana vyema “ni mara ya pili nina muona huyu jamaa” alijisemea Deus huku anaingia kwenye lango la kuingilia kwenye ofisi za mayor.*******

Naam saa nne kasoro ndio mida ambayo kikao kiliisha, makamanda wote wakikubaliana kuwa kazi ya msako ianze mara moja, hivyo mara baada ya kutoka kikaoni, watanzania ambao walitakiwa wakaaandae kikundi cha doria ya kiuchunguzi wakaondoka mara moja kueleka Mavivi kwa mpango wa msafara kama ule wa asubuhi, kasoro gari moja tu la maafisa MILOB (Military Observer) ambao walikuwa wanamalizia baadhi ya mambo pale ofisini kwa Mayor, na dakika kumi baadae msafara wa kanali Momadou nao ukaondoka zake ukielekea njia ile ile ya Mavivi ambako ndiko kikosi chao pia kilifikia.

Lakini wakati msafara wa magari mawili ya kanal Momadou yakiwa yanaondoka pale kwenye viunga vya ofisi za mayor, Deus aliekuwa anawasubiri wakuu wake, akayasindikiza kwa macho huku zikimjia kumbu kumbu za msafara wa WHO, alipokuwa anawapeleka wale madoctor, Deus anakumbuka askari wa jeshi la serikali walikuwa na silaha kama hizi lakini mwisho wake wakaishia kuwatelekeza porini Ilingeti.

Naam wakati Deus aliekuwa anayasindikiza magari yale mawili yaliyobeba wanajeshi wa jeshi la ulinzi la serikali ya jamuhuri ya kidemocrasia, ya watu wa congo yaliyokuwa yanakatiza mbele ya nashika uelekeo wa kulia kuifwata barabara kuu iendayo goma na ilingeti, mara macho yake yakakwama kwa yule kijana, abiria wa pikipiki alievalia kama wale wamusic wa kizamani wa boringo, akiwa anatoa simu haraka na kuibofya kwa haraka kisha akaiweka sikuoni, ambapo hakutumia hata sekunde tano, akawa tayari ameshamaliza maongezi, kisha akaiweka simu mfukoni halafu wakamweleza jambo yule dereva wa boda boda kisha wakapanda piki piki yao na kuondoka zao.

Deus alihisi jambo lisilo la kawaida kwa jamaa yule ambae kiukweli licha ya kuhisi kuwa siyo mgeni machoni pake, pia simu aliyoipiga haikuwa na usalama kwa wenzao, kati ya kundi la kwanza la watanzania au hili la pili la Momadou, Deus kwa kuhisi hivyo alitamani awashe gari na kuifukuzia ile pikipiki ili akamtazame yule jamaa mkanda nje aliejificha sura yake kwa cap ya kofia yake na dereva wake alievalia kofia ngumu.

Lakini wakati Deus anawaza hayo mara wakina Major Ferix wakatoka ofisini na kuingia ndani ya gari ilikuwa ni dakika tatu tu toka msafara wa pili uondoke yani ule wa Kanal Momadou, “samahani afande fungeni Mikanda” alisema Deus, ambae licha ya kuwa ni kawaida yake kumweleza mtu anaepanda gari kufunga mkanda, ila kwa safari fupi au akiwa na wakuu wake mara zote hawezi kuwaeleza swala hilo, hasa ukizngatia kuwa ingekuwa ni sawa na kuwapa amri vingozi wake na hiyo ni utovu wa nizamu kijeshi.

“haya jamani tufungeni mikanda, dereva leo anafwata sheria za chuo” alitania yule luteni kanali huku anafunga mkanda wa seat, yani seat belt, na kwa kuwa yeye ambae ni mkubwa alisha sema, basi wakina Felix wakafwata kufanya hivyo baada ya kuhakikisha wamesha funga mikanda yao, hapo Deus ambae tayari alisha funga mkanda wake akaondoa gari taratibu kutoka kwenye viunga vya jengo la ofisi za mayor, huku wakina Feilix wakijadiri na kuzungumzia jinsi mpambano wa ubishani uliojitokeza kwenye kikao juu ya ufanyike msako au waasi wakae na serikali wamalize tofauti zao.

Lakini story zao hizo hazikuchukuwa muda mrefu, kabla hawajatulia nakuanza kusikilizia mwendo ambao, Deus alikuwa anaendanao, mara baada ya kuikamata barabara hakika mwendo ulikuwa ni mkali sana yani ni mkali kiasi kwamba usingefikiria kuwa wanatembea katikati ya mji, maana walitembea mwendo wa kilomita mia themanini kwa saa huku akipiga honi kwa fujo, kuomba njia, nadhani pia walioko ndani hawakujuwa kuwa amewasha taa kubwa, “mh! Deus vipi mbona kama mwendo ni mrefu utadhani kuna tukio tunaliwahi?” aliuliza luten kanal, huku akimtazama kwa macho ya tahadhari, “ni bora nacho kiwazakiwe tofauti afande” alisema Deus huku anapunguza mwendo kwa gafla na kuingia barabara kuu iendayo mavivi.

Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana kilicho sababisha gari kuburuza tairi zake za nyuma, na kuzifanya zisote na kuseleleka huku tairi za gari hilo zikitoa sauti ya mbinja na kuwafanya watu walioshuhudia wapige kelele za shangwe la kishabiki, “Deus unamaana gani?” aliuliza luten kanal kwa sauti ya mshtuko, “kuna watu wanafwatilia msafara wa kanal Momadou nadhani hawana nia njema hata kidogo” alisema Deus huku analiweka gari sawa na kukanyaga mfuta kwanguvu na kulifanya gari lizidi kukimbia, “wapoje hao?” aliuliza Felix, huku wote wakitazama barabara, na macho yamewatoka kwa hofu ya kupata ajari, “vijaa wawili, wapo kwenye piki piki mmoja amevaa kofia nyeusi” alisema Deus ambae muda wote alikuwa makini na barabara na kila waliposogea mbele kuliacha jiji, ndiyo idadi ya magari na vurugu za barabara zilipungua na kufanya gari likimbie bila wasi wasi wowote.

Lakini wakati wanavuka daraja wakawaiona pikipiki ikiwa imelala kati kati ya barabara, huku watu wawili wakiwa wakiwa pembeni ya piki piki hiyo mbele na nyuma ya ile pikipiki, mmoja akiwa amevalia kofia nyeusi kichwani, wakiachia njia ndogo sana upande wa kulia wa barabara, wakijaribu kuinua pikipiki, ilionekana wazi kuwa walikuwa wamepata ajali, “Deus watu wako hao hapo wamepata ajali” alisema luten kanal ambae bila shaka alitegemea kwamba Deus, angepunguza mwendo, ili waweze kufanya jambo linalofaa kama siyo kuwasaidia kutokana na ile ajali basi ni kufanya nao mahojiano kwanini walikuwa wanafwatilia safara, lakini mawazo yake yalikuwa tofauti, maana Deus hakupunguza mwendo wala kuonyesha dalili ya kupunguza mwendo, “ni mtego huo afande inaonyesha kuna tukio huko mbele, hushangai kama ni ajali lakini pikipik haina dalili ya kuharibika popote” alisema Deus ambae wakati huo kwa ufundi mkubwa sana aliyumbisha gari kulia mwabarabara, kuikwepa pikipiki na kufanikiwa kupita kwa speed kali na kumfanya yule jamaa wa upende wakulia wa barabara aruke kwa hofu ya kunusurika kugogwa huku mwenzie alievalia kofia akilisindikiza gari kwa macho ya mshangao, huku wakina Felix wakibakia midomo wazi wasijue wamepitaje kwenye sehemu ile ndogo.

Naam safari iliendelea na gari lilizidi kushika moto, makamanda wamejawa na hofu ya mwendo wakiombea gari lisije kupata hata pacha ya bahati mbaya, maana kingewatokea kitu ambacho kingesababisha wasitambulike walikuwa wangapi na jinsia gani, kwa jinsi ambavyo wange sagika.

Naam dakika tatu baadae wakiwa wanalikaribia, kambi dogo la UN, (Siyo kambi la air port Mavivi), hapo nipo walipo yaona magari mawili ya jesi la serikali ya kiwa mbele yao yanalivuka lile kambi la UN, “jamaa waleee” alisema luten kanal, huku anatarajia kuona gari lao likipinguza mwendo, lakini ndiyo kwanza Deus akazidi kukanyaga mafuta kwenye ile tambalale ya kama mita miatatu kasoro kuwafwata wakina Kanal Momadou, ambao muda wote wakiwa kwenye msafara wao daima hutembea mwendo mkali.

Hapo lazima uelewe yaani licha ya msafara wa Momadou kuwa spee kali, lakini Deus alizidi kuwa sogelea kwa haraka, ungesema walikuwa wamesimama, “Deus hii ni amri, punguza mwendo” alisema luten Kanali kwa sauti ya ukali wa hali ya juu, lakini haikusaidia bado mguu wa Deus ulikuwa umeng’ang’ania kwenye pederi ya mafuta ni kama vile alikuwa ameambiwa aongeze mwendo.

Naam wakiwa wamebakiza mita kama mia mbili kuwafikia mara gafla, ukasikika mlipuko mita chache ndani pori lililopo pembeni ya barabara, ikifwatia mlio kama wa mluzi, ukiambaa hewani, hapo ndipo Deus alipokamata brake za nguvu na kufanya gari lao sitoteshe tairi kwa umbali wa miguu kama ishirini hivi sambamba na kishindo cha “khiiii” huku macho yao wote wanne wakishuhudia mlipuko mkubwa kwenye gari la mbele kabisa uliofuatiwa na milipuko mingine kadhaa ya mfululizo maana kombora moja lili lipua makombora mengine yaliyokuwepo kwenye gari lile la mbele ambalo alikuwa amepanda Kanal Momadou, ambalo ndani ya sekunde kumi tu, lilionekana likiwaka kama kichaka cha nyasi kavu…..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums
imefika patamu mwandish uwe una tuwekea vpnd 2 asubuh
 
Hapo lazima uelewe yaani licha ya msafara wa Momadou kuwa spee kali, lakini Deus alizidi kuwa sogelea kwa haraka, ungesema walikuwa wamesimama, “Deus hii ni amri, punguza mwendo” alisema luten Kanali kwa sauti ya ukali wa hali ya juu, lakini haikusaidia bado mguu wa Deus ulikuwa umeng’ang’Niania kwenye pederi ya mafuta ni kama vile alikuwa ameambiwa aongeze mwendo.

Naam wakiwa wamebakiza mita kama mia mbili kuwafikia mara gafla, ukasikika mlipuko mita chache ndani pori lililopo pembeni ya barabara, ikifwatia mlio kama wa mluzi, ukiambaa hewani, hapo ndipo Deus alipokamata brake za nguvu na kufanya gari lao sitoteshe tairi kwa umbali wa miguu kama ishirini hivi sambamba na kishindo cha “khiiii” huku macho yao wote wanne wakishuhudia mlipuko mkubwa kwenye gari la mbele kabisa uliofuatiwa na milipuko mingine kadhaa ya mfululizo maana kombora moja lili lipua makombora mengine yaliyokuwepo kwenye gari lile la mbele ambalo alikuwa amepanda Kanal Momadou, ambalo ndani ya sekunde kumi tu, lilionekana likiwaka kama kichaka cha nyasi kavu…..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums
Noumaaaaa
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THERASINI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI SABA: hapo ndipo Deus alipo kamata brake za nguvu na kufanya gari lao lisoteshe tairi kwa umbali wa miguu kama ishirini hivi sambamba na kishindo cha “khiiii” huku macho yao wote wanne wakishuhudia mlipuko mkubwa kwenye gari la mbele kabisa uliofuatiwa milipuko mingine kadhaa ya mfululizo, maana kombora moja lili lipua makambora mengine yaliyokuwepo kwenye gari lile la mbele ambalo alikuwa amepanda Kanal Momadou, ambalo ndani ya sekunde kumi tu, lilionekana likiwaka kama kichaka cha nyasi kavu…..…..….endelea….

Huku gari la nyuma ambalo lilifanana kwa kila kitu na lile la mbele, likisimama mitachache nyuma ya lenzake na kusababisha baadhi ya vipande vya mabomu vilivyosambaa toka kwenye gari lililolipuka vifike kwenye gari hilo na kusababisha majeraha makubwa kwa askari wa waliokuwepo ndani ya gari hilo.

Ni kama walipuaji walikusudia kuwamaliza kabisa askari hawa wa FARDC, Mara ghafla zikaanza kulindima kulishambulia lile gari la nyuma risasi, zikigonga kwenye ubavu wa kulia wagari hilo, wale majeruhi wa bomu wakaonekana wakijaribu kujiokoa maisha yao, wakijiangishia upande wa kushoto wa barabara, ambako ndiko kulikuwa salama kidogo, ambapo kuna mmoja wao wakati yupo juu anajaribu kutoka kwenye gari akaonekana akitandikwa risasi ya paja na kutupwa kwanguvu nje ya gari.

Hakika hali ilikuwa mbaya na yakutisha, ambayo iliwashangaza na kuwa shtua sana wakina Felix, ambao walipo angalia hawakuona dalili ya msaada wowote wakuwasaidia kupambana na adui ambae hawakujuwa nguvu yake, kutokana na kwamba risasi zilikuwa zinatokea kwenye kichaka kilichopo pembezoni mwa barabara na ukichulia ni kwamba, wao hawakuwa na silaha ya aina yoyote, na mbaya zaidi ni kwamba, gari lao lilikuwa mia chache sana toka kwenye gari lile lililokuwa linashambuliwa kwa risasi, “Geuza gari tuingie hapo kambini” alisema yule Luten Kanali, akimaanisha kwamba Deus ageuze gari wakaingie kwenye lile kambi la UN lililopo jirani.

Lakini ni kama Deus mwenyewe hakusikia alicho ambiwa, “afande piga simu omba msaada” alipiga kelele Deus huku anafungua mkanda wa kiti, yaani seat belt na kutoka nje ya gari, huku wakina Felix, wakimtazama kwa mshangao, wasielewe kijana wao anataka kufanya nini, huku milindimo ya risasi ikiendelea kusikika, tena ilionyesha wazi kuwa zilikuwa zina pigwa na bunduki aina ya MMG zaidi ya moja.

Jibu ambalo walilipata sekunde chache baadae ni mara baada ya kumwona Deus akichomoka toka kwenye gari na kurukia nje ya barabara upande wa kushoto, akiingia kabisa kwenye mtaro wa pembezoni mwa barabara ile ya lami na kuanza kukimbia, akiambaa ambaa kuelekea kwenye lile gari la nyuma la walinzi wa Kanal Momadou, ambalo japo lilikuwa halijalipuka lakini kiukweli lilikuwa lina tobolewa kwa risasi zilizokuwa zina miminika kama mvua.

“Afande tunafanyaje sasa, maana hatuwezi kumwachia Deus peke yake?” aliuliza major Felix, akionekana wazi kuwa anatamani kwenda kumsaidia Deus ambae alionekana analifikia lile gari lililokuwa lina shambuliwa kwafujo na ndio wakati ambao ni kama yule luten kanal alikuwa amezidika toka usingizini, “tushuke toka kwenye gari haraka” alisema luten kanal huku ana fungua mlango na kutoka nje ya gari upande wa kushoto wa gari hilo, akifuatiwa na wenzake ambao pia walishukia upande huo huo wakushoto, kisha kuchukuwa maficho kwenye mtaro wa barabara.

Wakati huo Deus alielifikia gari, ambalo bado lilikuwa lina shambuliwa na risasi mfululizo, ambapo palikuwa na askari saba, walio jeruhiwa vibaya wakiwa wamelala pale chini, huku wanaugulia maumivu ambapo bila kuchelewa, na kusikilizia zile risasi ambazo zilikuwa zina pigwa kwa fujo upande wapili wa gari yaani upande wa kulia, Deus aliwakokota wale majeruhi na kuwa weka mtaroni, hata wakina major Felix walivyoona kitu anacho kifanya Deus na kwamba upande ule ni salama basi na wao wakatembea kwa haraka kusogelea pale alipokuwepo Deus na walipomfikia na kumkuta amesha wasogeza majeruhi mtaroni nao wakaanza kuwapa huduma ya kwanza kwa kuwafunga majeraha yao, kwa kutumia nguo za wale wale majeruhi, huku risasi zikiendelea kulindima.

Naaam wakati wakina Felix wanaendelea kuwashughulikia wale majeruhi mara ghafla risasi zikakoma, ni wazi washambuliaji waliishiwa risasi kwenye mikanda yao, hivyo kulikuwa kunatokea mambo mawili, moja pengine walikuwa wanabadili mikanda ya risasi, pili pengine waliamua kuondoka zao kutokomea porini.

Hapo hapo Deus akaona kuwa huo ndio wakati wa yeye kufanya jambo lake, kitendo bila kuchelewa Deus akaibukia kwenye bodi ya gari, na kunyakuwa SMG, iliyokuwa mle ndani ya gari ikiachwa na wale askari majeruhi, kisha akaielekeza kule kichakani, kule zilikokuwa zinatokea risasi za adui japo hakujuwa maficho sahihi ya adui zake, lakini yeye akapiga risasi tano hovyo hovyo na kwa haraka.
Nikama alipatia, maana akawaona watu kadhaa, waliovalia sare za jeshi la serikali, wakiinuka na kuanza kukimbia hovyo kutokomea porini, na yeye hakuwaacha wafike mbali baada yake aliibana vizuri silaha yake kwenye usawa wabega, na kufumba jicho moja akioanisha kilengeo cha mbele na cha nyuma, kisha akaanza kuwa donyoa mmoja baada ya mwingine, katika mkadilio wa umbali wa mia mia moja mpaka mia mbili, huku akiwaangusha kama vile anaangusha maembe, japo alifanikiwa kuwapiga wanne kati ya saba alio waona, maana wengine walishazama ndani zaidi ya vichaka virefu.

Kundi la kwanza kufika pale ni magari nane, ya jeshi la Tanzania, yakiwepo magari manne ya chuma yasiyopitisha risasi, yaani APC na mengine ya kawaida, yote yakisheheni askari waliokuwa FBO, yaani Full Battle Oder, kuanzia vazi la combat, body armor (bullet proaf ) kofia ya chuma, bunduki mkononi zikiambatana na mikebe mitatu ya risasi, kama haitoshi magari yote yalikuwa na silaha nzito za kivita, aina ya 12 milimita.

Lakini walikuwa wameshachelewa, maana licha ya kuingia porini, na kufanya msako wanguvu, ambapo waliambulia, miili ya watu wanne waliovalia sale za jeshi la serikali, hawa walikuwa tofauti kidogo na wale wa IDFNALLU wakule ituli, sare zao zao zilikuwa ni za mataifa mbali, tena zilizo chakaa, hawa sare zao zilikuwa safi kabisa, na bora zaidi ambao walipatikana pamoja na simu moja na silaha aina ya MMG, mabox ya risasi ya silaha hizo.

Dakika chache baadae, kikaja kikuni kingine cha FARC, ikiwa ni kombania nzima, ambayo haikuishia pale, waligawana na wengine wakaanza kuwa fwatilia wale waliotokomea porini, ambao baadae walirudi na kusema kuwa hawakufanikiwa kuwapata, huku upande wapili, kwa kutumia simu, akabainika mtu mmoja mwenye cheo cha kanal, (sitoweza kulitaja jina lake kwa sababu za kimahakama, ila chukulia kama hadithi au simulizi), ambae alikuwa ni kiongozi wa kitengo flani cha usalama na utambuzi ndani ya jeshi la serikali, ambae alikamatwa baadae kidogo yeye na wenzake.

Sifa ilizidi kuwa upande wa Deus, ambae alionekana kuwa ni askari mwenye uwezo mkubwa, sifa ambazo alipewa na askari wenzake, hasa kutokana na kuwa na uwezo wa kuchukuwa maamuzi ya haraka na kufanikisha lengo pasipo kuleta madhara kwa upande wake na watu wake, kumbuka Deus licha ya kuwa na ufahamu wa matumizi ya silaha toka utotoni mwake, pia alipata mafunzo ya ucommando na ujasusi, katika vyuo vikubwa vya nchi mbali mbali, zenye ulewa na kupasisha kwa kiwango kubwa sana watu wa aina yake ambao walishawahi kusikika dunian kama wakina Fidel Castor, Che guavala, na wengine wengi.

Hakika tukio la kifo cha kamanda aliebeba imani ya wananchi wengi waliotarajia amani katika nchi yao kutokana uwezo wake katika mapigano, kanal Mustafah Momadou Ndalla, aliekufa na askari wake sita mmoja akiwa dereva, na askari mmoja wakike aliekuwa kama mhudumu wake, kilileta huzuni kubwa siyo tu kwa wananchi wa Congo, ila hata kwa watu wengine toka nchi mbali mbali, waliokuwa wanamfahamu, hasa wale waliowahi kufanya nae kazi kwa ukaribu, wengi wao wakiwa ni wanajeshi wa mataifa ya Tanzania, Malawi, #mbogo_land na Afrika ya kusini.

Yaliongelewa maneno mengi sana, huku wengi wakiamini kuwa ni janja ya kuzuwia mipango ya kusambaratisha kikundi cha waasi wa IDFNALU, huku wengine wakisema kuwa serikali ilihofia kuwa kanal huyu kijana, angeweza kuiasi nchi kama walivyofanya watu kama yeye waliowahi kutangulia mfano Sultan Emanuel Makenga, Lawlent Mkunda, na wengine wengi.

Naam zilipita siku tatu, askari wa majeshi yote yakiwa katika utayari wa asilimia mia moja, huku wakina Felix wakiwa wametulia pale Mavivi, pasipo kwenda mjini, ofisini kwa mayor, hata Deus alishinda chumbani kwake muda mwingi akipanga mipango ya matumizi ya fedha zake ambazo atazipata kwa kipindi cha mwaka mzima, huku pia akiendelea kuchat na pacha wake, ambae alikuwa anasisitiza swala la kukutana kwao pale mschana huyo Pacha aliekuwa anaamini kuwa mchoraji wake yupo dar, na yeye atakapo kuwa Dar, (sijuwi ana maanagani aliposema hivyo), maana pengine na yeye yupo Dar.

Siku ya nne, mida ya saa saba mchana Deus akiwa amejipumzisha chumbani kwake, anaendelea kutumiana sms na pacha wake ndipo aliposikia mlango wa chumba chake unagongwa, “ingia” alisema Deus na mlango ukafunguliwa, akaibuka bwana Kisonge, yule kijana wa kicongo mfanya usafi, aliekuwa amevalia suruali ya kitambaa chepesi, viatu vyeusi vya kuchongoka mbele, na tisht aliyoichomekea vizuri kwenye suruali yake, mkononi akiwa ameshikilia kofia nyeusi.

Ukweli ujio wake ni kama Deus hakuupenda, maana alikuwa ameshaanza kumchukia kijana huyu, toka siku ile ya kwanza, ya tukio la Ilingeti, “naona huko bien unajichatisha na mwasie kitoto ya Tanzania” alisema yule Kisonge, huku anajichekesha chekesha, “kwani kila anaechat anachat na demu?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu, na kavu, Kisonge hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kujichekesha.

“tuyaache hayo bwana Dereva, leo nilikutana na mtu moja kule Ben, ni muschana mrembo hivi anasema bibi yake anaumwa sana, na anakuhitaji ukamsaidie” alisema Kisonge, na kisha akatokanje ya chumba, huku akimwacha Deus, anainuka kitandani kwa mshtuko mkubwa sana, maana alisha sahau juu ya familia hii, “inamana ameanza tena kuumwa?” alijiuliza Deus, huku anawaza namna ya kufika mjini, akawaone watu wale ambao aliwachukulia kama ndugu, maskini Deus hakujuwa nini kimeandaliwa kwaajili yake. …..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NANE: “tuyaache hayo bwana Dereva, leo nilikutana na mtu moja kule Ben, ni muschana mrembo hivi, anasema bibi yake anaumwa sana, na anakuhitaji ukamsaidie” alisema Kisonge na kisha akatoka nje ya chumba huku akimwacha Deus anainuka kitandani kwa mshtuko mkubwa sana, maana alisha sahau juu ya familia hii, “inamana ameanza tena kuumwa?” alijiuliza Deus huku anawaza namna ya kufika mjini akawaone watu wale, ambao aliwachukulia kama ndugu, maskini Deus hakujuwa nini kimeandaliwa kwaajili yake. …..…..….endelea….

Baada ya kuwaza kwa muda mfupi, Deus akapata wazo la kwenda kuaga kwa major Felix na ukichukulia kuwa yeye hakuwa na kizuwizi chochote cha kutoka nje ya kambi kama ilivyokuwa kwa askari wengine, hivyo hata alipofika kwa major Felix na kuaga kwamba anaenda kuembea mjini, hakukuwa na kipinga mizi chochote, “siyo tatizo ni vyema ukatumia gari letu maana ukanda huu changamoto ni usafiri” alishauri Felix na Deus akauchukuwa ushauri huo, kisha akajiandaa na kuelekea mjini.

Saa tisa za jioni, tayari kijana huyu alikuwa ameshafika maeneo ya kituo cha mafuta cha MONUSCO, akiwa ameshapitia pia sokoni na kununua baadhi ya vitu ambavyo hupenda kuwanunulia wakina Sonia ambapo aliacha gari pale na kuelekea njia panda ya Panasonic hotel, ni kama mwendo wa dakika kumi endapo utatembea kwa mguu tena taratibu kwa hiyo dakika kumi baadae, tayari kijana wetu alikuwa ameshafika njia panda, na sasa akaingia upande wa kushoto na kuelekea mtaani kwa kina Sonia, akiwa na mfuko uliojaa vitu vingi alivyo wabebea wakina Sonia na bibi yake.

Mchezo wakushangaza unaanza pale Deus alipofika nyumbani kwa kina Sonia na kumkuta bibi yake Sonia, akiwa amekaa nje ya nyumba yao akionekana mzima wa afya, hiyo ilimfanya deus acheke kidogo, “bibi ni wewe au macho yangu yana sema uongo?” aliuliza Deus akiwa amebakiza hatua chache kumfikia bibi yake Sonia aliekaa kwenye kibaraza cha nyumba yao, lakini jambo la kushangaza bibi hakujibu chochote zaidi ya kumkazia macho Deus pasipo kuonyesha dalili ya kwamba amefurahia ujio wake.

Ilimshtua sana Deus, “bibi ni mimi umesahau?” aliuliza Deus ambae sasa alikuwa amesha mkaribia kabisa yule bibi, safari hii bibi akataka kuongea kitu, lakini ile anafungua mdomo tu, Sonia akaibuka toka ndani ya nyumba yao, huku akiwa amevalia kitenge kimoja alicho kifungia kifuani, “hoooo! Tanzania umenikumbuka leo” alisema Sonia, huku anamsogelea Deus na kumshika mkono pasipo kupokea ule mfuko, Karibu munyumba” alisema Sonia, huku anamwongoza Deus ndani ya nyumba ambayo Deus hakuwahi kuingi humo ndani hapo mwanzo.

Deus akiwa katika mshangao kwa hali aliyomkuta nayo bibi ambae aliambiwa kuwa anaumwa sana, kwa jinsi alivyomwona kama vile akuupenda ujio wake, “sijui hapendi nije hapa kwao?” alijiuliza Deus wakati anavuka kizingiti cha mlango kuingia ndani ya nyumba hii, huku anageuza uso wake kumtazama bibi yake Sonia, ambae pia alikuwa anamtazama kijana huyo na macho yao yalipokutana bibi akatikisa kichwa kushoto na kulia ikiwa ni ishara ya kukataza jambo.

Ilimshangaza Deus ambae hakujuwa maana halisi ya katazo la bibi yake Sonia, “wala asijari natoka sasa hivi?” aliwaza Deus ambae sasa alikuwa ndani ya nyumba hii ambayo ukichilia makochi chakavu na kongwe kama ulivyo mwonekano wa meza ndogo iliyopo mbele ya makochi hayo, pia kila klichoonekana machoni pa Deus kilikuwa ni cha hali ya chini sana, hata kitanda kidogo cha futi sita kwa tatu na nusu, kilicho tandikwa matandiko chakavu pale sebuleni kilionekana wazi kuwa kinamilikiwa na mtu mwenye maisha ya hali ya chini sana, “Sonia, mbona uliagiza kuwa bibi anaumwa wakati haumwi hata kidogo?” aliuliza Deus wakati kwa mshangao huku akiwa bado ameshikwa mkono na Sonia ambae sasa alikuwa anaufwata mlango wa chumbani, “nilidanganya ili ukuje mbio maana unafanya masiku mingi na haukuji” alisema Sonia ambae alievalia kitenge kimoja tu, alicho kifungia kifuani.

Wakati huo walikuwa wanasimama mbele ya mlango ambao ulionyesha wazi kuwa ni wa chumba cha kulala, na Sonia akashika kitasa tayari kufungua mlango na hapo ndipo Deus akakumbuka katazo la bibi, akaunganisha na kitendo cha kudanganywa kuwa bibi anaumwa, halafu akajumlisha kitendo cha kupelekwa chumbani.

Hapo mbuzi akagoma kuingia buchani, “hapana Sonia hapa sebuleni pana tosha” alisema Deus huku anageuka na kuelekea kwenye kochi lilipo, huku Sonia akiuachia mkono wa Deus na kusimama akimtazama kwa macho ya kujiuliza, kwamba afanyaje ili aeleweke mbele ya kijana huyu, ambae sasa alikuwa anaweka mfuko mezani na kukaa kwenye moja kati ya makochi yale matatu, “jamani Deus mwenzio naona baridi, basi ukuje unipatie fukuto (joto) kidogo” alisema Sonia kwa sauti iliyotokea puani huku anamsogelea Deus na kusimama mbele yake.

Ilimshtua kidogo Deus, kwa kuona mschana mdogo kama huyu, anahitaji dudu kwa kuomba yeye mwenyewe, “mh! hapana Sonia siyo leo, tutapanga siku nitakuja” alisema Deus huku anainuka toka kwenye kochi nikama alitaka kuondoka zake kwa kuzingatia lile katazo la bibi, “hapana bwana siwezi kungoja tena, haitachukuwa lisaa lizima” alisema Sonia huku anaishika ile nguo yake eneo la kifuani na kuitegua ikifwatia na kitendo cha nguo ile kushuka kama bendera iliyo funguka kamba kwa bahati mbaya na kwena kukwama sakafuni.

Naam macho ya Deus yaliweza kuhushudia mwili mtupu uliohamasisha ngono, maziwa yaliyotuna na kujaa vyema, tumbo dogo kiasi, kiuno kipana kilichobeba hips nene, hatari zaidi ni kitumbua mtuno kilicho pambwa vizuri kwa nywele za wastani, huku kunde ziikionekana kuchomoza kama vile korongo anae meza samaki, “hapana Sonia siyo leo” alisema Deus na kuanza kutembea kufwata mlango wa kukea nje.

Maskini Deus hakufanikiwa kuufikia mlango, maana kabla hata hajapiga hatua ya tatu ghafla ukasikika ukelele toka nyuma yake, “jamanieeeee….. nisaidieni, ananibaka huyu mwanaume…..,niachie we mtanzania, jamani ananibakaaaa…..ananibakaaaaa” ilikuwa ni sauti ya Sonia Sauti iliyo mshangaza na kumshtua sana kijana wetu Deus, ambae aligeuka na kumtazama Sonia ambae alikuwa bado amesimama uchi wa mnyama akiendelea kupiga kelele za kwamba anabakwa, “nisaidieni jamani.. huyu mtanzania ananibakaaaa” alipiga kelele Sonia, ambae hakuonyesha dalili ya kuwa anatania.

Hapo Deus akakumbuka katazo la bibi, hivyo jambo hili siyo la ghafla, ila ni lakupangwa na hatari zaidi ni kwamba, kuwa ujio wake huku kwa akina Sonia unafahamika kwa Kisonge ambae ndie aliempatia ujumbe wa kuwa bibi yake Sonia, anaumwa sana, na kwamba wanamuhitaji aende, kwa kumbu kumbu hizo, Deus akajuwa kuwa yupo kwenye hatari kubwa ni vyema kama angetafuta njia ya kulimaliza swala lile, ukweli kutafua suluhu kwa njia ya kumbembeleza Sonia kwamba atulie isingewezekana, hasa kama ule ulikuwa ni mtego wa makusudi, hivyo njia pekee nikufika sehemu salama ambayo ni kambini.

Hivyo basi kwa kujuwa kuwa kama ule ulikuwa ni mtego basi lazima kuna watu waliokuwa karibu na eneo lile na wanakaribia kumnasa, Deus akamtazama Sonia kwa macho ya kumpa ujumbe kuwa sio rahisi kihivyo kisha akageuka na kutazama mlangon ambako tayari kulianza kusikika vishindo vya watu wakija mbio mbio, kuifwata nyumba ile ya wakina Sonia.

Kwa akili za haraka sana Deus akatazama kushoto na kulia, mwa ile sebule, akauona mlango mwingine wa kuelekea jikoni, aliutambua kwa kuwa ulikuwa ni vizingiti tu, hakukuwa na mlango hivyo akakimbilia upande huo, anakimbilia upande wa jikoniiii” alipigakelele Sonia, na hii ilionyesha wazi kuwa mschana huyu hatari alikuwa anafahamu kuwa kuna watu walikuwa wanasubiria apige kelele tu nao waje haraka kumkamata Deus.

Deus hakujari kelele za mschana huyu, akaingia jikoni haraka ambako aliona mlango wa kutokea nje ukiwa umefungwa kwa kuegeshwa na wakati huo akasikia vishindo vya watu wakiingia sebuleni, “yuko wapi huyo mbakaji?” ilikuwa ni sauti ya kiume yenye hasira.

Deus hakutaka kuzubaa akaufungua mlango wa kutokea nje na kujikuta akiibukia uwani, uwa uliozungukwa na uzio wa mabanzi ya mti, lenye mlango mwembamba uliokuwa umefungwa nusu, Deusi akatoka mbio kuufwaa ule mlango, ile ana ukaribia akasikia vishindo vya watu, kwa ukaribu zaidi vikija mbio mbio, vikiwa vimesha ufikia ule mlango na kwa bahati alifanikiwa kuwaona wawili waliokuwa wanaingia ndani, walikuwa ni polisi, wa serikali ya DRC wakiwa na silaha aina ya SMG mkononi mwao.

Hapo Deus hakujiuliza mara mbili akajuwa kuwa yupo kwenye hatari zaidi ya ile ambayo aliidhania mwanzo, hivyo kijana wetu aliona kuwa ni lazima atoke nje na kijana huyu mwenye mafunzo ya hali ya juu, hakutaka kubadiri njia, alilenga upande ule ule ambao watu walikuwa wanakuja mbio mbio, na wakati wanaufikia mlango ule uliofunguliwa nusu tayari polisi wa kwanza alikuwa anaingia ndani huku bunduki yake ikiwa mkononi, huku mwingine akifwatia nyuma yake hapo huwezi amini hata kama ungeshuhudia kwa macho, kitu ambacho alichokifanya kijana Deus.

Kwa uharaka wa hali ya juu, Deus ambae alisha juwa kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni na kwamba kutoka hapa salama ndiyo kipaumbele chake, aliruka juu na kukita mguu wake wakushoto kwenye kifua cha yule polisi alie tangulia ambae alitupwa nyuma na kwenda kumgonga polisi mwezie aliekuwa nyuma yake, huku Deus akiruka juu na kushika banzi moja, kati ya yale yaliyotengeneza wigo ule kisha akarukia nje ambako ile anatuwa tu, akakutana na polisi mwingine ambae pia alikuwa na SMG, Deus akumkawiza akamzibua ngumi moja nzito ya usoni usawa wa pua,ngumi ambayo ilimtia wenge polisi huyo ambae aliyumba kidogo na kabla hajakaa sawa, Deus akakimbia kuingia ndani ya chochoro za mtaa ule bahati ikawa upande wake, maana hakukuwa na mtu yoyote aliemfuata, hivyo akaamini kuwa tayari amesha wakimbia polisi wale, kilichobakia ni kutafua njia ya kuelekea kule kwenye kituo cha mafuta.

Naam Deus akiwa anaamini kuwa tayari amesha waacha wale polisi, alitembea umbari kama wa mita mia moja hivi na kujikuta akiibuka kwenye njia ya panasonc, ambapo alichungulia kwa tahadhari kuona kama anaweza akaitumia njia hiyo lakini ile anachungulia tu, akajikuta anashtuka na kubakia mdomo wazi, siyo kwa kuona polisi waliokuwa wamesimama kama vile walijuwa lazima atumie njia ile, ila ni kwa kumuona mtu aliekuwa pamoja na polisi wale, wakielezana jambo flani.

maana ukiachilia polisi waliokuwepo pale na silaha zao, pia kulikuwa na vijana wawili waliovalia kiraia pamoja na piki piki yao, mmja ambae ni dereva akiwa amevaa kofia ngumu kichwani huku mwingine akiwa amevalia suruali ya kitambaa, viatu vyeusi, na tishert aliyo ichomekea na mkononi akiwa ameshikilia kofia nyeusi ni wale wale ambao aliwaona siku ya tukio la Momadou, “kum…make ni Kisonge kumbe huyu mshenzi, yupo pale MONUSCO kama mamluki” alijisemea Deus huku anamtazama kijana yule wa kicongo aliekuwa anatoa maelekezo flani kwa polisi hawa wa serikali ya Congo. …..…..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NI bonge moja LA story ila Leo ndo mwisho kuisoma kuna nyingine tena alileta ina itwa asali ikawaga mapigo say aya aya nkajikuta tu nimeipotezea na ilikuwa nzuri sana pia inasikitisha na hii pia inabid niipotezee, yaan kipande kimoja after all this tym sitaki arosto siku izi, jamaa jifunze ebu kwa brodree
 
ubaya ubwela asipoileta tunaenda youtube ipo yote
 
NI bonge moja LA story ila Leo ndo mwisho kuisoma kuna nyingine tena alileta ina itwa asali ikawaga mapigo say aya aya nkajikuta tu nimeipotezea na ilikuwa nzuri sana pia inasikitisha na hii pia inabid niipotezee, yaan kipande kimoja after all this tym sitaki arosto siku izi, jamaa jifunze ebu kwa brodree
Dah usifanye tujutie kuisoma hii hadithi shusha mistari ndugu yangu
Inakuja
 
Back
Top Bottom