Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Mbona fupi leo? Yani moja ukaondoka kaka
 
Unajuaga hapa pamefika panono ngoja niwaache na arosto
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TISA: “Tuna BMW S7, sina wasi wasi” alisema Deus, huku anapachika gia na kuondoa gari taratibu, kuingia barabara kuu, usingeweza kudhania kama walikuwa na safari ya mbali kiasi hicho zaidi ya kilomita mia tatu, taratibu gari liliingia barabara ya morogoro na kushika uelekeo wa kushoto ambao ni wa morogoro, likitembea kwa speed ndogo, kama linaishia mzani, wakati huo wapo pale kibaha mpakani hawakujuwa kuwa, mita chache toka pale njia panda ya kisarawe walipokuwepo, kuna askari wa jeshi la polisi alievalia nguo za kiraia alikuwa analitazama gari lile la kisasa lenye mwonekano wa upya…....…….endelea….


Yani jipya haswaaa! ambalo alilitazama likishika uelekeo wa kibaha yaani upande wa kushoto, sambamba na magari mengine yanayoelekea upande huo, yakiwa magari makubwa na madogo ya abiria na yale ya binafsi na mengine ya serikali, ya mizigo na yale ya kibiashara, mabus ya mikoani na maroli ya mizigo yaendayo mikoani na nchi za nje.


Mara akatoa simu mfukoni na kubofya namba flani kisha akapiga simu fulani ambayo haikuita muda mrefu ikapokelewa, “afande gari tunalo litafuta ni kama nimeliona maeneo ya kiluvya madukani na sasa linaelekea upande wa kibaha” alisema yule kijana polisi, ambae kitu kinacho mtambulisha kuwa ni polisi ni unyoaji wake wa nywele na hakuwa na ndevu hata ya dawa, pia ukiachilia tishert aliyovaa na suruali ya jinsi, miguuni alivaa buti nyeusi za jeshi, “ok! subiri hapo niwapigie waliopo mbezi wakukute hapo muwafatilie halafu pia nawapigia waolipo bagamoyo wapitie msata wakawazuwie Lugoba, na kama watapitiliza, basi tutawasiliana na askari wa morogoro wawazuwie, sasa napiga simu picha ya ndege ili na yeye aliangalie hilo gari kama litapita pale” ilisikika sauti iliyo changamka kidogo ikionyesha kuwa na matumaini mapya, “ndiyo afande” alisema yule askari wa jeshi la polisi kabla ya kukata simu na kuiweka mfukoni.


Huyu ni Koplo Cheleji, ni mmoja kati ya askari wa tiifu wa CP Ulenje, ambae kwa uaminifu wake amechaguliwa kufanya jukumu la siri nje ya majukumu yanayotambuliwa na jeshi la polisi, la kufuatilia gari aina BMW 7, ambalo inasemekana lina dhahabu kilo hamsini toka #mbogo_land, dhahabu ambayo inasoko kubwa sana duniani, huku wakiahidiwa fedha nyingi sana endapo watafanikiwa kulipata gari hilo.


Na sasa yeye na mwenzie mmoja walipangwa kwenye vituo vya uchunguzi, yani Kiluvya madukani na picha ya ndege, huku kundi kubwa likiwa mbezi wakiziba barabara ya morogoro na wengine walikuwa njia panda ya msata, pale bagamoyo ili kuzuia barabara ya kuelekea mikoa ya kaskazini huku tayari wakiwa wamesha weka mtego tanga na morogoro.******


Naam! taarifa za kufukuzwa kazi kwa askari alie singiziwa kubaka nchi kongo, zilianza kusambaa kama utani kwenye vyomb vya habari na mitanao ya kijamii, sijuwi hata habari za jeshi zilifikaje kwa wanahabari wa kujitegemea, maana habari zilianza kusagaa kwenye mitandao ya kijamii huku nyingine zikimtambulisha kama shujaa wa UN afukuzwa kazi, wapo walisifia kitendo kile na wapo waliokosoa kitendo kile, wakidai kuwa jeshi la Tanzania hawakuwa na sababu kufukuza shujaa kama huyo kwa kosa ambalo hakulitenda, huku wakipinga kuwa kosa lile halikuwa na maana ya kulichafua jeshi, wakuu mbali mbali wa serikali walihoji kwa mkuu wamajeshi juu swala hilo, wakitaka kujuwa kwanini Deus amefukuzwa kazi.


Mkuu wa majeshi, alikuwa bado yupo ofisini, akiumiza kichwa na kuwaza kile majibu atakayo yatoa kwa rais na waziri juu ya kile kilichotokea, maana ukiangalia shutuma za wanahabari zilikuwa za kweli, Deus Nyati hakuwa na kosa kubwa la kufuzwa kazi, japo utaratibu huo ulikuwepo toka zamani, kwamba askari akileta sifa mbaya kwa taifa hasa akiwa katika majukumu ya kimataifa, nilazima achukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni kufungwa na kufukuzwa jeshi lakini sio kwa huyu ambae alikuwa ametenda kosa akiwa anafanya jambo la kiubinadamu ikiwa ni moja ya kananuni za kijeshi, hasa awapo vitani, kwamba unatakiwa uwe na ubinamu kwa wahanga wa vita, ambao wengi wao ni raia waishio eneo lenye vita na walengwa wakubwa wakiwa ni watoto wakina mama, walemavu na wazee, bila kusahau waliopata madhara ya kivita, kuumia au kujeruhiwa.


Na wakati huo huo ndio wakati ambao, mkuu wa majeshi, alipopokea simu toka kwa waziri wa ulinzi, “ilishindikana kumpatia adhabu nyingine yoyote kati ya zile mnazo peanaga kuliko kumfukuza kazi?” aliuliza waziri wa masuala ya ulinzi alipo mpigia simu mkuu wa majeshi, afande kuna kosa dogo limefanyika ila tunaandaa mwanasheria wa jeshi akate rufaa ili kesi yake iitishwe tena na askari Nyati kubadilishiwa adhabu” alisema mkuu wamajeshi, “hiyo angalau inaweza kuleta maana, yani baada tu ya taarifa hizi, mheshimiwa amepigiwa simu na viongozi wa nchi mbali mbali wanamshangaa kwa maamuzi mulio yachukua” alisema waziri wa masuala ya ulinzi, “afande haukuwa mpango wetu, ila kuna kosa lilifanyika, CDMP alifungua kesi pasipo kutoa taarifa kwa ungozi na kutoa hukumu” alijitetea mkuu wa majeshi, “basi huyo askari atafutwe haraka arudishwe kambini na huyo mkuu wapolisi jeshi, achukuliwe hatua za kinadhamu na hicho kitengo hakimfai tena” alisema waziri, “ndiyo afande” alijibu mkuu wa jeshi, kabla hawajaagana na kukata simu.


Na yeye hakusuburi, akapiga simu kwa CDMP, bwana SS Chawe, simu ambayo haikuita sana, ikapokelewa, “jambo afande” ilisikika sauti ya unyenyekevu iliyojaa wasi wasi toka upande wapili wa simu, “upo wapi Chawe?” aliuliza mkuu wa majeshi kwa sauti ambayo ilionyesha wazi wakati huo haikuhitaji urafiki, “ndio nakaribia nyumbani afande” alijibu brigedia Chawe kwa sauti ile ile, ambayo ilishindwa kuzuia wasi wasi wake, “unaenda nyumbani kupumzika baada ya kumaliza kuharibu mambo?” aliuliza mkuu wa majeshi na wakati Chawe anatafuta jibu, mkuu huyu mwenye cheo cha General, akaongeza swali, “kwahiyo wakati sisi tupo kazini tunahangaika kujibu maswali yako, wewe unaenda kupumzika na mkeo?” aliuliza tena General, hapo Chawe akakosa jibu kabisa, “haya sasa, kesho asubuhi, namuhitaji Private Nyati ofisini kwangu, wakati wewe unajiandaa kwenda kusini Duma South land force Comander, alisema General, na kukata simu.******


Naaam wakati hayo yanazungumzwa, gari aina ya BMW S7 lilikuwa linakatiza maeneo ya TAMCO, kuelekea picha ya ndege ndani ya gari Deus na Sheba walikuwa kimya, kila mmoja akiwaza la kwake, wakati Sheba anawaza juu ya kijana huyu, mwenye umbo la kulea mtoto mzuri, kwanini ameamua kufanya kazi ya hatari kama hii kwa milion 50, huku Deus mwenyewe alikuwa anawaza hatima yake, baada ya kuachishwa kazi aliyoipenda, kazi ya jeshi.


Na wakati anawaza hayo, mara ghafla akakumbuka jambo, “bibie, hujanieleza changamoto ya safari yako, hujanieleza jina lako pia” alisema Deus kwa sauti tulivu, “naitwa Sheba, changamoto ni kwamba tuna fuatiliwa na watu wa serikali, lengo ni kuufikia mpakani tarakea, karibu na Longai, tahadhari ya njiani muda wowote tutavamiwa” alisema yule mschana ambae alimiliki sura ya kitoto japo alionekana kuwa kauzu,


Ukweli Deus alishtuka kidogo, japo sasa ndio alielewa kwanini alilipwa fedha nyingi kiasi kile kwa kazi ya kumfikisha mshana huyu longai, hakutaka kuuliza sana, zaidi alifikiria namna ya kujilinda, “mimi naitwa…” alisema Deus, ambae akabla hajamaliza kujitambulisha, akajikuta akitanguliwa na Sheba, Deus Frank Nyati, askari wazamani wa jeshi la ulinzi” alisema Sheba, ambae hakuonyesha dalili yoyote ya kutabasamu.


Haikumshangaza Deus ambae bado alikuwa anaendesha gari kwa mwendo wa taratibu huku kichwani mwake akitafakari juu ya jukumu hili alilolikubari kwa haraka pasipo kufikiria mara mbili, “kwa uwezo ulionao hupaswi kuwaza sana, maana gari ni bullet proof pia tuna hii” alisema Sheba akipeleka mkono kwenye uvungu wa seat yake na kuibuka na bastora, “itatusaidia mbele ya safari japo mimi sio mtumiaji mzuri kama wewe” alisema Sheba, kwa sauti ile ile isiyo na urafiki, “khaaa bunduki tena?” alinong’ona Deus, akionekana kuto kupendezwa kwa uwepo wa bastora ndani yagari, “vipi hujaipenda?” aliuliza Sheba, huku anairudisha bastora chini ya seat, “ni vyema kama utaisahau mpaka nitakapo shuka toka kwenye gari lako” alisema Deus kwa sauti yake tulivu huku anapunguza mwendo zaidi kuingia picha ya ndege.


Wakati huo tayari walikuwa wamesha vuka makundi mawili ya askari wa usalama barabarani, yani wa pale mzani wazamani na wale wa TAMCO, Deus, nasikia wewe ni Dereva mzuri, lakini toka tumeanza safari, haujagusisha mshale wa speed kwenye themanini, tutafika lini unadhani?” aliuliza Sheba, alieonekana kuchukizwa na mwendo mdogo wa gari lile, “kuna kitu nilikuwa na jaribu, kuhusu muda sina shaka, ni vyema ukabadili makadirio yako, pili kuna jambo bado natazama ili kuthibitisha jambo jingine” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, wakati anasimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu pale picha ya ndege, haya bwana wewe si ndie dereva” alisema Sheba, huku analaza seat yake na kuiegemea vizuri kama mtu anaehitaji mapumziko kwa wakati ule, “na jukumu langu ni kukufikisha longai na sio kuelekezwa mwendo, ni vyema kama utafumba macho na ulale usingizi” alisema Deus, huku anaondoa gari, maana tayari wavukaji wa barabara walikuwa wameshavuka, hawakujua kama kuna mtu amesimama karibu na njia panda ya Tumbi, akilitazama lile gari, huku anapiga simu kwa mtu fulani.******


Naam Brigedia General Salum Said Chawe, akiwa amekosa amani, kutokana na jambo lililotokea, jambo ambalo mwanzo alidhania kuwa ametenda majukumu yake ya kila siku, “lakini ni kweli siku kabisa sikuwa sahihi kuchukuwa maamuzi pasipo kupata maoni toka kwa wakuu” aliwaza Chawe, ambae mpaka sasa hakuwajuwa atampata vipi askari Deus Nyati.


Toka amalize kuongea na mkuu wamajeshi mkuu huyu wa idara ya polisi jeshini, alikuwa kimya kabisa, akiwaza kuhusu maisha mapya huko kusini mwa Tanzania, ambako anaenda kuwa mkuu wa kamandi ya askari wa miguu, yani infanry foces, kanda ya Duma, jambo ambalo mwanzo ndilo lililomuumiza kichwa kuliko lile la kumtafuta Deus Nyati ili kesho afikishwe kwa mkuu wa majeshi, “afande tumeshafika” alishtua yule mpambe wake mwenye cheo cha luten, ambae tayari alikuwa amesha mfungulia mlango. ..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI:Toka amalize kuongea na mkuu wamajeshi mkuu huyu wa idara ya polisi jeshini, alikuwa kimya kabisa, akiwaza kuhusu maisha mapya huko kusini mwa Tanzania, ambako anaena kuwa mkuu wa kamandi ya askari wa miguu, yani infanry foces kanda ya Duma, jambo ambalo mwanzo ndilo lililomuumiza kichwa kuliko lile la kumtafuta Deus Nyat ili kesho afikishwe kwa mkuu wa majeshi, “afande tumeshafika” alishtua yule mpambe wake mwenye cheo cha luten, ambae tayari alikuwa amesha mfungulia lango. ..…….endelea….


Na hapo Chawe akatazama kuchoto kwake, na kuona kuwa ni kweli alikuwa nyumbani kwake, kwamba gari lilikuwa limesha simama muda mrefu, “hooooo! sawa” alisema Chawe kama alie changanyikiwa, huku ana shuka toka kwenye gari tayari mschana wakazi alikuwa ameshatoka kuja kumpokea.


Chawe alipiga hatua chache kisha akasimama na kumtazama mpambe wake ambae alikuwa anamkabidhi dada wa kazi mkoba mdogo wa ngozi kwa dada wakazi, “hebu tafuta namba ya askari Deus Nyati kisha mpigie simu muambie kesho kabla ya saa mbili awe amereport ofisini kwangu pale makao makuu” alisema Chawe kisha akageuka na kuelekea ndani.


Mpambe wa Chawe, akaingia ndani ya gari na Dereva ambae muda wote alikuwa kimya akaondoa gari, “afande inaonekana mkuu amepigwa na kitu kizito, maana siyo kwa mabadiliko ya haraka aliyokuwa nayo” alisema yule dereva, mwenye cheo cha koplo huku anageuza gari tayari kuondoka, “kama sio amepigwa onyo, basi atakuwa amepangiwa kwenda mikoani” alisema yule luten huku anapekuwa simu yake kutafuta namba flani na alipoipata akaipiga.


Simu iliita kwa muda flani kisha ikapokelewa, “jambo afande” ilisalimia sauti ya kike upande wa pili wa simu, “jambo Agness, bado hupo ofisini” aliuliza yule luten, “dah! afande unadhani kuna kuondoka sasa hivi, boss wako ameharibu mambo, simu zinapigwa kila dakika toka wizarani, kuulizia taarifa za Deus Nyati” ilisema sauti ya kike, “duh! hiyo ni hatari, ila fanya kitu kimoja tazama taarifa za huyo askari, nadhani kuna namba yake nitumie” alisema yule luten, “sasa hivi nakutumia afande” alisema Agness, kisha wakakata simu.******


Naam wakati huo huo, Bwana Frank Nyati akiwa songea nyumbani kwake, hakika alionekana kusisimuliwa sana na taarifa za vyombo mbali mbali vya habari, juu ya malalamiko ya wananchi na waandishi wa vyombo hivyo vya habari vya kujitegemea juu ya jeshi kumuachisha kijana wake kazi, mzee huyo ambae sasa alikuwa na umri wa miaka arobaini na nane, mida hii alikuwa ametulia sebuleni akipekuwa kurasa za mitandao ya kijamii na kuganda kwenye ile ambayo ilizungumzia habari za kijana wake, “afadhari sasa wananchi wanaweza kupaza sauti, wanapoona jambo limetendwa sivyo” alisema mzee Nyati akilinganisha na miaka ya nyuma, wakati serikali ya nchini yake ya asili, ilivyokuwa inaendesha operation ya tokomeza waasi ndani ya serikali, “hivi huyu anafahamu kinachoendelea huko mitandaoni kweli?” aliuliza kwa sauti kiasi cha mke wake kumshangaa, “mwenzetu vipi tena, au umepatwa na uchizi kwaajili ya mwanao kufukuzwa kazi?” aliuliza mke wake, huku akisimama mbele ya mume wake, aliekuwa amekaa kwenye kochi, “mh! kimewaka huko, udhani Deus wamchezo mchezo, watu wanahoji huko kwanini amefukuzwa kazi” alisema mzee Nyati huku anaiweka sawa simu yake na piga simu kwa Deus.


Simu iliita kwa sekunde kadhaa, kisha ikapokelewa, “hallow baba, nitakupigia kuna kitu nafanya” ilisikika sauti tulivu ya Deus, toka upande wapili wa simu, “subiri kwanza wewe, hivi umesiki…” kabla mzee Nyati hajamaliza kusema alichokusudia kusema simu ikakatika, “mjinga sana wewe, hebu msikilize baba yako” alisema kwa sauti ya juu mzee Nyati huku anajiandaa kupiga tena simu, “hebu tulia kwanza, pengine mwenzio yupo na mkweo, mpe muda kidogo bwana” alisema mama Deus, na kufanikiwa kumtuliza mzee Nyati, “lakini inabidi afahamu mapema kinachoendelea huko mtaani” alisema Frank Nyati, huku anafungua moja ya kurasa ya mtandao wakijamii, na kumwonyesha mke wake.******


Naam tukiwa pale picha ya ndege, kijana alie kuwa amesimama njia panda ya Tumbi, alilitazama gari aina ya BMW S7, lililokuwa linatembea taratibu kuelekea upande wa kwa Mathius, alipoliona limekaribia darajani, kijana yule mwenye makadirio ya miaka thelathini, akatoa simu na kupiga sehemu, ambapo haaikuchukuwa muda mrefu ikapokelewa, “vipi afande mupo wapi?” aliuliza yule kijana, ambae kwa haraka usigeshindwa kuhisi kuwa ni askari wa jeshi la polisi, “tupo mzani tuna kuja kwa speed, vipi umewaona?” ilisikika sauti ikiuliza upande wa pili wa simu, “nawaona mbele yangu, tena gari linatembea taratibu sana, sijuwi kama wanasafari hawajamaa” alisema yule jamaa huku analitazama lile gari aina ya BMW S7.


Lakini kabla hajasikia lolote toka upande wavpili, mara yule jamaa kwa macho yake akaliona lile gari aina ya BMW jeusi, likimaliza kuvuka daraja na kuacha barabara kuu, kisha likaingia upande wa kushoto wa barabara, ambako kulikuwa na barabara ya zamani ya morogoro inayopitia nane nane, “afande kama nilivyosema naona gari limeingia barabara ya nane nane” alisema yule jamaa huku analitazama lile gari, ambalo lilikuwa bado linatembea taratibu, likitokomea kwenye hiyo barabara ya zamani ya morogoro, “unasema kweli wameingia huko?” iliuliza sauti upande wa pili wa simu, “kweli afande, yani bado nawaona wale wanapotelea nane nane” alisema yule jamaa, huku anatazama upande ule wa nane nane, ambako gari lilikuwa limepotelea, kiasi cha kutokuonekana tena.


“afadhari kama wameingia huko, maana tunaenda kuwakamata sasa hivi” alisikika yule wa upande wa pili ambae aliongea jambo, “sikia sasa, hebu chukuwa boda boda, kisha wafuatilie kwa akili wasikushtukie, tazama wanapoenda kuishia” alisema tena yule wa upande wa pili na simu ikakatwa, huku yule jamaa anatazama kushoto na kulia kuona kama kuna boda boda ya karibu, ambapo alifanikiwa kuipata moja na kuikodi, “wahi nane nane, kunagari nyeusi tuiwahi” alisema yule jamaa na kisha safari ikaanza mara moja, huku akisisitiza mwendo mkali, waliwahi lile gari ambalo sasa lilikuwa limetoweka usoni mwao, lakini waliamini kwa mwendo ule walio uona, wangelikuta kabla Halijafika mbali.******


Naaam luten alipopiga namba ya simu aliyopewa na Agnes, ilimwambia kuwa mtumiaji wa simu anayoipiga, anaongea na simu nyingine hivyo asubiri au ajaribu baadae, nae akaikata kwa maana alichagua kujaribu baadae, ambapo alikaa kama dakika mbili tu, akapiga tena, safari ukasikika ujumbe mwingine kuwa simu anayopiga haipatikani, “mpuuzi, anadhani mimi nimwandishi wa habari” alilalamika yule luten, huku anajaribu tena, kupiga ile namba, ambayo ilimueleza vile vile, “khaaa anajiona nani huyu mpuuzi” alijisemea luten, huku anapiga simu kwa Agnes ambae hakuchekelewa kuipokea, “vipi afande hiyo namba haipatikani?” aliuliza Agness, kwa shahuku, “amenizimia simu, hebu tazama namba ya mtu wa karibu kama ni mzazi wake au, mlezi wake” alisema yule luten na kukata simu.******


Yap! kitu ambacho tunapaswa kukifahamu nikwamba, mara baada ya kukata simu ya baba yake, Deus akiwa anaendesha gari taratibu akaizima kabisa, kisha akakata kona kushoto, kuingia barabara ya vumbi, akiiacha ile morogoro, hata Sheba ambae alikuwa amejilaza kwenye seat yake, alipoona wameingia kwenye barabara isiyo rasmi akainuka na kutazama mbele, “Deus, safari yetu ina miongozo, sidhani kama hii ni njia ambayo umepangiwa” alisema Sheba, huku anamtazama Deus kwa macho ya mshangao na tahadhari, “lengo ni kuelekea longai, iwe kwa njia yoyote ile” alisema Deus, huku anaendesha gari taratibu.


Hapo Sheba akajilaza tena kwenye seat na wakati huo huo simu ya kwenye dash board ikaanza kuita, Sheba akainuka tena na kuitazama ile simu, ambayo ilikuwa inapigwa na mtu mmoja tu, ambae ni Boss Atshen, “enheeeee, boss huyoooooo” alisema Sheba huku anabofya kipokeleo na simu ikajipokea na kuwa katika sauti ya wazi, “wapi unaenda wakati uelekeo ni morogoro road?” ilikuwa ni sauti kali yenye jazba toka kwenye ile simu, “ni vyema ukatulia nikufikishie mtu wako salama, sidhani kama njia ilikuwepo kwenye moja ya sheria zako” alisema Deus kwa sauti tulivu, “lakini unapaswa kutembea kwenye barabara ambayo inakupeleka kaskazini mwa Tanzania” ilisema ile sauti, safari hii ikianza kupoa, “lakini hupaswi kunichagulia njia wakati unafahamu hukuniambia kuwa kuna watu wanatufuatilia” alisema Deus kwa sauti ile ile tulivu, “ok! muda gani utafika point B?” aliuliza boss Atshen kwa sauti iliyopoa, ikiwa imeondoka kwenye hali ya hasira, “masaa manne matano kwa makadirio ya juu” alisema Deus kwa sauti yake ambayo ungesema anaongea utani, “mh! kilomita mia nne kasoro, masaa matano, ukiweza nitakushangaza” alisema boss na kukata simu.


Hapo Deus akakamtazama Sheba, “ni vyema kama utafunga mkanda tuanze safari, alisema Deus, kwa saut yake tulivu ya upole, “sidhani kama ni muhimu, we endesha gari, tena na kushauri ufanye kama ulivyo muahidi boss, inaweza kuwa na faida katika maisha yako mapya nje ya jeshi” alisema Sheba, aliekuwa katika hali ile ile ya ukauzu, Deus hakuongea kitu zaidi ya kukanyaga mafuta zaidi kuongeza mwendo, ambao uliendelea kuongezeka kila sekunde zilvyoenda, huku mshale wa speed ukiinuka toka speed ishirini kilomita kwa saa na kukomea kwenye themanini kwa saa, ambapo licha ya gari kupita kwenye barabara iliyokosa tambalale, lakini bado kwa aliekuwa ndani ya gari asingesikia chochote.


Kilomita moja mbele wakiwa wamesha uvuka uwanja wa nane nane na kuuacha kama mita mia nane hivi, eneo ambalo lilikuwa na uwazi pasipo majengo zaidi ya shamba la miti na jengo moja tu, lililofichwa na msitu huu wa kupandwa upande wa kushoto, wakati upande wa kulia kulikuwa na barabara ndogo dhaifu, iliyoelekea upande wa barabara, Deus alikanyaga brake za ghafla na kuingia upande wa kushoto, akifuata njia ambayo inaenda kwenye ile nyumba katikati ya msitu wa kupandwa na binadamu.


Kitendo ambacho kilizuwa msuko suko kwa Sheba ambae aliyumba kidogo akibakiza nchi chache sana, kujibamiza kwenye kioo cha mbele, kutokana na ile brake, huku akipelekwa pembeni, na kujigonga kwenye mlango halafu akakaa sawa na kugeuza uso wake nyuma kuona anacho kikimbia Dereva wake mpya, lakini hakuona chochote zaidi ya kushuhudia gari likiendelea kutililika kwa speed kuingia kwenye yale makazi, “au huyu nae ni mmoja kati ya watu wanao tufukuzia?” alijiuliza Sheba huku anageuza uso wake kumtazama Deus kwa macho yaliyojaa mashaka, “unadhani unafanya nini Deus?” aliuliza Sheba, huku anapeleka mkono kwenye vungu ya kiti chake na kuikamata bastora.. ..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Haya Sheba anataka kumshikia bastola Deus na sisi tunajua kuwa Dues hapendi tena bastola 🙄
Kesho nishtueni mapemaaaaa tuone ni nini kiliendelea
 
BMW S7
 

Attachments

  • IMG_20250122_084551_498.JPG
    47.6 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…