Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: “ni upuuzi, hebu fuatilia ni nani aliejichukulia maamuzi hayo kisha nipe jibu kesho saa mbili asubuhi kwenye kikao na huyo askari atafutwe haraka kesho areport hapo ofisini kwako na kufutiwa adhabu hiyo” alisema CDF kwa sauti iliyo onyesha kuwa ilikuwa na hasira kali sana, kisha akakata simu akimwacha COT, yaani Chief Of Treaning akiwa ameacha mdomo wazi kwa mshangao jinsi haya mambo yalivyoenda…..endelea…

Gen Mbike hakutaka kupoteza muda kushangaa, hapo hapo akapiga simu kwenda kwa Chief Of Defance MP, na simu ikaanza kuita mara moja.*****

Wakati huo huo kijana wetu Deus, akiwa ndani ya gari waliingia kiluvya madukani na kwenda kusimama njia panda ya kuelekea kisarawe sehemu aliyoelekezwa na na mtu aliempigia simu.

Deus alilipa kiasi cha Tsh 15000 kama malipo ya usafiri, kisha akashuka na kuchukuwa begi lake kubwa la mgongoni na kusimama pembeni ya barabara iendayo kisarawe kisha akatazama kama angeona kitu chochote ambacho kingempa ishara ya gari au mtu ambae anatakiwa asafiri nae, lakini hakuona dalili yoyote zaidi ya watu waliokuwepo eneo lile wakiendelea na shughuri zao za kibiashara, kama vile boda boda mama ntilie wa mama wauza samaki na wasafiri waliokuwa wanaendelea kusubiri daladala, huku wapiga debe wakiendelea kuwashawishi kupanda magari yale, japo nilazima wangepanda hata bila ushawishi ule wa wapiga debe.

Baada ya kuona hivyo Deus akaona kuwa ule ndio wakati ambao angeutumia kuwasiliana na wazazi wake, kuwaeleza kilichotokea kwake mara baada ya kuingia Tanzania ya kwamba amefukuzwa kazi na pia awajulishe kuhusu mizigo ambayo ameituma kwenye bus, hivyo waende kuipokea siku baada ya kesho, ambayo kwa Kiswahili inaitwa keshokutwa.

Naaam wakati Deus anaendelea kuongea na simu yake mara akaliona gari dogo aina BMW S7 jeus, likiwa linaingia pale njia panda likitokea upande wa kisarawe, macho yalimtoka akilitazama lile gari ambalo kiukweli ndiyo gari la ndoto yake, gari ambalo kuna muda fulani aliliona maeneo ya airport japo hakuwa na uhakika kama ndiyo lile lile au la, ila kwa hakika alikjikuta anazidi kutamani kumiliki gari kama lile, na wakati anaendelea kuongea na simu, mara simu yake ikaanza kutoa ishara ya simu nyingine kutaka kuingia kwenye simu yake, akaitoa sikioni na kutazama mpigaji wa simu ya pili.

Kwa macho yake akaona ile namba ngeni ya nchi za nje, namba ambayo ilitoka kumpigia dakika ishirini na saba au nane zilizopita, “baba subiri kidogo nitakupiga baadae” alisema Deus na kukata simu ya kwanza kisha akapokea ile ya pili.******

Mkuu wa polisi jeshini Brigedia SS Chawe, mida hii alikuwa ndani ya gari la jeshi analotembelea siku zote, ikiwa ni safari ya kuelekea nyumbani kwake huku moyoni akijisifu kwa kumaliza jukumu la kufungua mashitaka na kumaliza kesi ya askari mtovu wa nidhamu, yaani Deus Nyati, ambae kisheria adhabu yake ni kufukuzwa jeshi kwa kulitia aibu jeshi hilo lenye kusifiwa kwa nidhamu, “hivi afande unadhani ni sawa kumfukuza jeshi privae Deus Nyati?” aliuliza msaidizi na mwangalizi (mpambe) wa mkuu wa polisi jeshi, mwenye cheo cha luteni, “hakuna mtu muhimu jeshini, kama amefanya makosa basi sheria lazima ichukuwe mkondo wake” alisema brigedia yule, ambae juu ya mfuko wake wakulia wa shati la kombani, kulikuwa na jina SS Chawe yaani Salum Said Chawe, “lakini afande UN ilibaini kuwa hakuwa na kosa zaidi ya kuvunja taratibu ndogo ambazo askari wengi huzivunja” alisema yule msaidizi.

Hiyo ilimfanya Chawe akasirike, “kwahiyo unanifundisha majukumu yangu” aliuliza Chawe kwa sauti kavu, huku wakitazama jengo la diamond jubilee, kwa maana walikuwa wanakatiza hapo na wakati huo huo simu ya mkononi ya Chawe ikaanza kuita, akaichukuwa haraka na kuitazama, mpigaji alikuwa ni major General Mbike, yaani COT, moyo wa Chawe ukalipuka kwa mshtuko, maana alikumbuka kuwa licha ya kumpokea na kumshtaki Deus, lakini hakuwa amepeleka taarifa yoyote kwa Mkuu wa mafunzo.

Chawe akaipokea haraka simu ile na kuiweka sikioni, “jambo afande” alisalimia brigedia Chawe, “Chawe toka lini umepewa jukumu la kupokea watu wanaotoka operation nje ya nchi?” aliuliza Mbike kwa sauti iliyojilazimisha kuzuwia jazba, “afande huyu ni tofauti kidogo, huyu ni mwalifu, hivyo ni jukumu la MP kwenda kumuweka chini ya ulinzi” alijibu Chawe kwa sauti yenye uzito mkubwa wanidhamu, “uliagizwa na nani brigedia, ofisi yangu si ndiyo yenye jukumu la kukuagiza kuwa fulani akamtwe, maana bado alikuwa chini yangu” aliuliza Mbike, safari hii akiongeza sauti kidogo na kuwa yenye ukali, “afande nadhani msaidizi wangu ndie aliamua kujiongeza baada ya kuona taarifa inachelewa, sababu mimi nililetewa akiwa amesha toka airport” alisema Chawe kwa sauti ya kujitetea “kwahiyo jukumu la kufungua mashaka nalo ulijiongeza au uliagizwa na nani?” aliuliza Mbike, kwa sauti yenye hasira ya wazi na hapo ndipo Chawe alipokumbuka maneno ya huyu msaidizi wake (mpambe)

“afande tulitoa taarifa kwa mnadhimu, tukiomba kibali cha kufungua mahakama, nae akakubali, na sisi tukafanya hivyo” alijibu Chawe, na hapo kikasikika kicheko cha uchungu, “Chawe ulikuwa na maslahi yoyote kwa kumshtaki Deus, mbona ulikiuka sheria na nidhamu ya kijeshi ambayo unaisimamia kila siku, ni kweli ulitakiwa uende kwa mnadhimu kabla yangu? wewe ndie ulietakiwa ukampokee Deus airport na siyo mimi, hata jukumu la kumshtaki Deus, lilikuwa la kwangu, hakika hii imekuchafua, anyway jiandae kwa kile kitakacho kutokea kwa kosa la kufukuza askari ambae bado jeshi lilikuwa linamuhitaji” alisema Mbike na kukata simu, akimuacha Chawe ameshikilia simu huku macho ameyatoa kama vile amefumaniwa.******

Yap! Saa nane na nusu, ndio muda ambao, Sheba alisimamisha gari maeneo ya kiluvya madukani, akitokea upande wa kisarawe kupitia barabara ya tondoroni mpaka mdidimue, Sheba kama alivyoelekezwa na boss wake Atshen akasimamisha gari mita chache toka barabara hiyo iendayo Morogoro, ambapo aliambiwa kuwa atampata mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuendesha gari na pia ni mpiganaji mkubwa sana mwenye uwezo mkubwa.

Sheba akatazama kushoto na kulia mwa barabara ya vumbi ya kiluvya madukani kama angemuona mtu analifwata gari lile, lakini hakuona mtu yoyote anae lifuata gari lake, zaidi aliwaona watu wengi wakiwa wanaendelea na shughuri zao, wakiwa wauza samaki, mama nitilie wapiga debe wa daladala, pia madereva wa boda boda na watu waliokuwa wanafika pale kutafuta mahitaji au usafiri wa kwenda maeneo mbali mbali ya mji.

Wakati Sheba anatazama kushoto na kulia, mara macho yake yakakwama kwa kijana mmoja mrefu wa wastani, mwenye umbo fulani ambalo lilimtambulisha kuwa ni kijana aliependa mazoezi, au kufanya mazoezi kwa muda mrefu siku za hivi karibuni, ambae alikuwa amebeba begi kubwa mgongoni mwake, “mh! mbona sikuwhai kuona kijana mtanzania mwenye kufanana na wewe” aliwaza Sheba, ambae sio kwaajili ya lile begi, ila ni kwaajili ya uso wa upole wakijana huyu, ambae sasa alikuwa anaongea na simu, huku macho yake anapepesa kushoto na kulia na mwisho macho yake yakaganda kwenye gari lake, ambalo alilitazama kwa muda mrefu kidogo huku anaendelea kuongea kwa simu yake.

Dakika moja baadae, akamuona kijana yule, akibofya simu yake na kuiweka tena sikioni, ilionyesha wazi kuwa kuna simu nyingine ilikuwa imeingia wakati akiwa anaongea na hata alipoongea na ile simu ya pili alionekana akitazama tena gari la Sheba, na kuanza kutembea kulifuata, mpaka alipolifikia gari lile, hapo Sheba akajikuta anatabasamu, maana alishajuwa kuwa kijana huyu mwenye umbo la pekee, ndie mtu aliekusudiwa kuwa dereva na mlinzi wake katika safari mpya ya kuelekea kaskazini mwa Tanzania,

Kijana yule alipolikaribia gari, Sheba akafungua mlango na kushuka akiliacha lina unguruma, na kuzunguka upande wa kushoto wa gari, akaingia kwenye upade huo kwa maana seat ya abiria wa mbele na Deus nae hakujiuliza, akausogelea mlango wa abiria wa nyuma na kuufungua mlango ule akaliona begi dogo ambalo hakulijali, yeye akaweka begi lake na kuufunga mlango ule, kisha akaingia kwenye seat ya dereva, ambayo mlango wake ulikuwa wazi.

Baada ya kuingia akafunga mlango na kumtazama Sheba, “habari yako dada” alisalimia Deus kwa sauti yake ya upole, “nzuri, nadhani maelekezo unayo, mzigo wako huo hapo seat ya nyuma” alisema Sheba, huku akionyesha lile begi dogo lililopo seat ya nyuma, Deus alilitazama lile begi dogo, kisha akalinyoosha mkono na kulichukuwa, halafu akafungua lile begi, ambalo ndani yake kulikuwa na bando za fedha za kitanzania, noti za elfu kumi kumi, akafunga na kulirushia tena kule nyuma, “ok! boss wako yupo vizuri, anaenda na muda na mkweli anatimiza ahadi” alisema Deus, huku anatazama dash board ya gari lile ambao leo ni mara yake ya kwanza kuingia ndani yake, “una uhakika tutafika salama?” aliuliza Sheba kwa saut ya kutilia mashaka, maana kwa muonekan wa sura na muonekano wa Deus, upole wake na uongeaji wake, usingemuweka katika kundi kama hili.

“Tuna BMW S7, sina wasi wasi” alisema Deus, huku anapachika gia na kuondoa gari taratibu, kuingia barabara kuu, usingewaza kama walikuwa na safari ya mbali kiasi hicho, zaidi ya kilomita mia tatu, taratibu gari liliingia barabara ya morogoro na kushika uelekeo wa kushoto, ambao ni wa morogoro, likitembea kwa speed ndogo, kama linaishia mzani, wakati huo hapo, pale kibaha mpakani hawakujuwa kuwa, mita chache toka pale njia panda ya kisarawe walipokuwepo, kuna askari wa jeshi la polisi alievalia nguo za kiraia alikuwa analitazama gari lile la kisasa, lenye mwonekano wa upya…....…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
Mbona fupi leo? Yani moja ukaondoka kaka
 
Unajuaga hapa pamefika panono ngoja niwaache na arosto
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TISA: “Tuna BMW S7, sina wasi wasi” alisema Deus, huku anapachika gia na kuondoa gari taratibu, kuingia barabara kuu, usingeweza kudhania kama walikuwa na safari ya mbali kiasi hicho zaidi ya kilomita mia tatu, taratibu gari liliingia barabara ya morogoro na kushika uelekeo wa kushoto ambao ni wa morogoro, likitembea kwa speed ndogo, kama linaishia mzani, wakati huo wapo pale kibaha mpakani hawakujuwa kuwa, mita chache toka pale njia panda ya kisarawe walipokuwepo, kuna askari wa jeshi la polisi alievalia nguo za kiraia alikuwa analitazama gari lile la kisasa lenye mwonekano wa upya…....…….endelea….

Yani jipya haswaaa! ambalo alilitazama likishika uelekeo wa kibaha yaani upande wa kushoto, sambamba na magari mengine yanayoelekea upande huo, yakiwa magari makubwa na madogo ya abiria na yale ya binafsi na mengine ya serikali, ya mizigo na yale ya kibiashara, mabus ya mikoani na maroli ya mizigo yaendayo mikoani na nchi za nje.

Mara akatoa simu mfukoni na kubofya namba flani kisha akapiga simu fulani ambayo haikuita muda mrefu ikapokelewa, “afande gari tunalo litafuta ni kama nimeliona maeneo ya kiluvya madukani na sasa linaelekea upande wa kibaha” alisema yule kijana polisi, ambae kitu kinacho mtambulisha kuwa ni polisi ni unyoaji wake wa nywele na hakuwa na ndevu hata ya dawa, pia ukiachilia tishert aliyovaa na suruali ya jinsi, miguuni alivaa buti nyeusi za jeshi, “ok! subiri hapo niwapigie waliopo mbezi wakukute hapo muwafatilie halafu pia nawapigia waolipo bagamoyo wapitie msata wakawazuwie Lugoba, na kama watapitiliza, basi tutawasiliana na askari wa morogoro wawazuwie, sasa napiga simu picha ya ndege ili na yeye aliangalie hilo gari kama litapita pale” ilisikika sauti iliyo changamka kidogo ikionyesha kuwa na matumaini mapya, “ndiyo afande” alisema yule askari wa jeshi la polisi kabla ya kukata simu na kuiweka mfukoni.

Huyu ni Koplo Cheleji, ni mmoja kati ya askari wa tiifu wa CP Ulenje, ambae kwa uaminifu wake amechaguliwa kufanya jukumu la siri nje ya majukumu yanayotambuliwa na jeshi la polisi, la kufuatilia gari aina BMW 7, ambalo inasemekana lina dhahabu kilo hamsini toka #mbogo_land, dhahabu ambayo inasoko kubwa sana duniani, huku wakiahidiwa fedha nyingi sana endapo watafanikiwa kulipata gari hilo.

Na sasa yeye na mwenzie mmoja walipangwa kwenye vituo vya uchunguzi, yani Kiluvya madukani na picha ya ndege, huku kundi kubwa likiwa mbezi wakiziba barabara ya morogoro na wengine walikuwa njia panda ya msata, pale bagamoyo ili kuzuia barabara ya kuelekea mikoa ya kaskazini huku tayari wakiwa wamesha weka mtego tanga na morogoro.******

Naam! taarifa za kufukuzwa kazi kwa askari alie singiziwa kubaka nchi kongo, zilianza kusambaa kama utani kwenye vyomb vya habari na mitanao ya kijamii, sijuwi hata habari za jeshi zilifikaje kwa wanahabari wa kujitegemea, maana habari zilianza kusagaa kwenye mitandao ya kijamii huku nyingine zikimtambulisha kama shujaa wa UN afukuzwa kazi, wapo walisifia kitendo kile na wapo waliokosoa kitendo kile, wakidai kuwa jeshi la Tanzania hawakuwa na sababu kufukuza shujaa kama huyo kwa kosa ambalo hakulitenda, huku wakipinga kuwa kosa lile halikuwa na maana ya kulichafua jeshi, wakuu mbali mbali wa serikali walihoji kwa mkuu wamajeshi juu swala hilo, wakitaka kujuwa kwanini Deus amefukuzwa kazi.

Mkuu wa majeshi, alikuwa bado yupo ofisini, akiumiza kichwa na kuwaza kile majibu atakayo yatoa kwa rais na waziri juu ya kile kilichotokea, maana ukiangalia shutuma za wanahabari zilikuwa za kweli, Deus Nyati hakuwa na kosa kubwa la kufuzwa kazi, japo utaratibu huo ulikuwepo toka zamani, kwamba askari akileta sifa mbaya kwa taifa hasa akiwa katika majukumu ya kimataifa, nilazima achukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni kufungwa na kufukuzwa jeshi lakini sio kwa huyu ambae alikuwa ametenda kosa akiwa anafanya jambo la kiubinadamu ikiwa ni moja ya kananuni za kijeshi, hasa awapo vitani, kwamba unatakiwa uwe na ubinamu kwa wahanga wa vita, ambao wengi wao ni raia waishio eneo lenye vita na walengwa wakubwa wakiwa ni watoto wakina mama, walemavu na wazee, bila kusahau waliopata madhara ya kivita, kuumia au kujeruhiwa.

Na wakati huo huo ndio wakati ambao, mkuu wa majeshi, alipopokea simu toka kwa waziri wa ulinzi, “ilishindikana kumpatia adhabu nyingine yoyote kati ya zile mnazo peanaga kuliko kumfukuza kazi?” aliuliza waziri wa masuala ya ulinzi alipo mpigia simu mkuu wa majeshi, afande kuna kosa dogo limefanyika ila tunaandaa mwanasheria wa jeshi akate rufaa ili kesi yake iitishwe tena na askari Nyati kubadilishiwa adhabu” alisema mkuu wamajeshi, “hiyo angalau inaweza kuleta maana, yani baada tu ya taarifa hizi, mheshimiwa amepigiwa simu na viongozi wa nchi mbali mbali wanamshangaa kwa maamuzi mulio yachukua” alisema waziri wa masuala ya ulinzi, “afande haukuwa mpango wetu, ila kuna kosa lilifanyika, CDMP alifungua kesi pasipo kutoa taarifa kwa ungozi na kutoa hukumu” alijitetea mkuu wa majeshi, “basi huyo askari atafutwe haraka arudishwe kambini na huyo mkuu wapolisi jeshi, achukuliwe hatua za kinadhamu na hicho kitengo hakimfai tena” alisema waziri, “ndiyo afande” alijibu mkuu wa jeshi, kabla hawajaagana na kukata simu.

Na yeye hakusuburi, akapiga simu kwa CDMP, bwana SS Chawe, simu ambayo haikuita sana, ikapokelewa, “jambo afande” ilisikika sauti ya unyenyekevu iliyojaa wasi wasi toka upande wapili wa simu, “upo wapi Chawe?” aliuliza mkuu wa majeshi kwa sauti ambayo ilionyesha wazi wakati huo haikuhitaji urafiki, “ndio nakaribia nyumbani afande” alijibu brigedia Chawe kwa sauti ile ile, ambayo ilishindwa kuzuia wasi wasi wake, “unaenda nyumbani kupumzika baada ya kumaliza kuharibu mambo?” aliuliza mkuu wa majeshi na wakati Chawe anatafuta jibu, mkuu huyu mwenye cheo cha General, akaongeza swali, “kwahiyo wakati sisi tupo kazini tunahangaika kujibu maswali yako, wewe unaenda kupumzika na mkeo?” aliuliza tena General, hapo Chawe akakosa jibu kabisa, “haya sasa, kesho asubuhi, namuhitaji Private Nyati ofisini kwangu, wakati wewe unajiandaa kwenda kusini Duma South land force Comander, alisema General, na kukata simu.******

Naaam wakati hayo yanazungumzwa, gari aina ya BMW S7 lilikuwa linakatiza maeneo ya TAMCO, kuelekea picha ya ndege ndani ya gari Deus na Sheba walikuwa kimya, kila mmoja akiwaza la kwake, wakati Sheba anawaza juu ya kijana huyu, mwenye umbo la kulea mtoto mzuri, kwanini ameamua kufanya kazi ya hatari kama hii kwa milion 50, huku Deus mwenyewe alikuwa anawaza hatima yake, baada ya kuachishwa kazi aliyoipenda, kazi ya jeshi.

Na wakati anawaza hayo, mara ghafla akakumbuka jambo, “bibie, hujanieleza changamoto ya safari yako, hujanieleza jina lako pia” alisema Deus kwa sauti tulivu, “naitwa Sheba, changamoto ni kwamba tuna fuatiliwa na watu wa serikali, lengo ni kuufikia mpakani tarakea, karibu na Longai, tahadhari ya njiani muda wowote tutavamiwa” alisema yule mschana ambae alimiliki sura ya kitoto japo alionekana kuwa kauzu,

Ukweli Deus alishtuka kidogo, japo sasa ndio alielewa kwanini alilipwa fedha nyingi kiasi kile kwa kazi ya kumfikisha mshana huyu longai, hakutaka kuuliza sana, zaidi alifikiria namna ya kujilinda, “mimi naitwa…” alisema Deus, ambae akabla hajamaliza kujitambulisha, akajikuta akitanguliwa na Sheba, Deus Frank Nyati, askari wazamani wa jeshi la ulinzi” alisema Sheba, ambae hakuonyesha dalili yoyote ya kutabasamu.

Haikumshangaza Deus ambae bado alikuwa anaendesha gari kwa mwendo wa taratibu huku kichwani mwake akitafakari juu ya jukumu hili alilolikubari kwa haraka pasipo kufikiria mara mbili, “kwa uwezo ulionao hupaswi kuwaza sana, maana gari ni bullet proof pia tuna hii” alisema Sheba akipeleka mkono kwenye uvungu wa seat yake na kuibuka na bastora, “itatusaidia mbele ya safari japo mimi sio mtumiaji mzuri kama wewe” alisema Sheba, kwa sauti ile ile isiyo na urafiki, “khaaa bunduki tena?” alinong’ona Deus, akionekana kuto kupendezwa kwa uwepo wa bastora ndani yagari, “vipi hujaipenda?” aliuliza Sheba, huku anairudisha bastora chini ya seat, “ni vyema kama utaisahau mpaka nitakapo shuka toka kwenye gari lako” alisema Deus kwa sauti yake tulivu huku anapunguza mwendo zaidi kuingia picha ya ndege.

Wakati huo tayari walikuwa wamesha vuka makundi mawili ya askari wa usalama barabarani, yani wa pale mzani wazamani na wale wa TAMCO, Deus, nasikia wewe ni Dereva mzuri, lakini toka tumeanza safari, haujagusisha mshale wa speed kwenye themanini, tutafika lini unadhani?” aliuliza Sheba, alieonekana kuchukizwa na mwendo mdogo wa gari lile, “kuna kitu nilikuwa na jaribu, kuhusu muda sina shaka, ni vyema ukabadili makadirio yako, pili kuna jambo bado natazama ili kuthibitisha jambo jingine” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, wakati anasimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu pale picha ya ndege, haya bwana wewe si ndie dereva” alisema Sheba, huku analaza seat yake na kuiegemea vizuri kama mtu anaehitaji mapumziko kwa wakati ule, “na jukumu langu ni kukufikisha longai na sio kuelekezwa mwendo, ni vyema kama utafumba macho na ulale usingizi” alisema Deus, huku anaondoa gari, maana tayari wavukaji wa barabara walikuwa wameshavuka, hawakujua kama kuna mtu amesimama karibu na njia panda ya Tumbi, akilitazama lile gari, huku anapiga simu kwa mtu fulani.******

Naam Brigedia General Salum Said Chawe, akiwa amekosa amani, kutokana na jambo lililotokea, jambo ambalo mwanzo alidhania kuwa ametenda majukumu yake ya kila siku, “lakini ni kweli siku kabisa sikuwa sahihi kuchukuwa maamuzi pasipo kupata maoni toka kwa wakuu” aliwaza Chawe, ambae mpaka sasa hakuwajuwa atampata vipi askari Deus Nyati.

Toka amalize kuongea na mkuu wamajeshi mkuu huyu wa idara ya polisi jeshini, alikuwa kimya kabisa, akiwaza kuhusu maisha mapya huko kusini mwa Tanzania, ambako anaenda kuwa mkuu wa kamandi ya askari wa miguu, yani infanry foces, kanda ya Duma, jambo ambalo mwanzo ndilo lililomuumiza kichwa kuliko lile la kumtafuta Deus Nyati ili kesho afikishwe kwa mkuu wa majeshi, “afande tumeshafika” alishtua yule mpambe wake mwenye cheo cha luten, ambae tayari alikuwa amesha mfungulia mlango. ..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WATSAPP: 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: “ok! nipe hali ya uzito wa mzigo, daraja la mzigo, na usalama wa usafirishaji” aliuliza kijana wetu, ambae alikuwa anaendelea kuendesha gari kwa speed kama vile analazimika kwenda na muda flani, wakati huo walikuwa wanakaribia njia panda ya Moroco, “uzito, haufiki hata kilo, usalama ni mkubwa sana, thamani yake laki mbili” alijibu yule mwanamke kwa sauti ile ile, ambayo kama unauwezo wa kujaji mtu kupitia sauti ungejuwa kwa, uzuri wa mwanamke huyu, siyo wataratibu, na ni mwanamke wa mjini, mwenye maisha ya hali ya juu. endelea

Hapo dereva wetu akashusha pumzi ndevu ya kuchoka, maana yeye amezowea kusafirisha mizigo ya hatari, lakini sasa anaambiwa kuwa, mzigo hakuwa na hatari yoyote, na thamni yake ni laki mbili, hapo akaona kuwa ni utani, lakini kutokana na utaratibu wake namba 7, hakutakiwa kudharau kitu wala mtu, “ok! malipo elfu hamsini, utanipatia nikifisha mzigo, lakini utatakiwa kuzingatia kuwa, hakuna ujanja, huo ni utaratibu namba 5” alisema dereva, akitaja elfu hamasini kwa kutegemea kuwa mwanamke huyu, angeona bei kubwa, na kughairi mpango, “wala usiwe na wasi wasi, natukienda sawa, nita kuongezea mala dufu ya elfu hamsini” alisema yule mwanamke, huku akizidi kuipooza sauti yake, “ok! mpango umekubaliwa” alisema dereva na kukata simu, wakati huo, anapunguza mwendo kuingia njia panda ya Moroco, na kukata kushoto kuelekea barabara ya mwenge, kisha akaongeza mwendo, pasipo kujari sms zilizokuwa zinaingia kwenye ile simu yake nyingine, muda wote mschana mdogo Zamda akiwa anamtazama kijana huyu, kwa macho ya viulizo, na kushindwa kupata jibu.*******

Yap! wakati kama huu, kusini mashariki mwa Tanzania, pembezoni mwa mto Ruvuma, kaskazini mashariki mwa msumbiji, ndani ya nchi ndogo ya kifalme, nchi iliyosaahulika katika ramani ya dunia, kutokana na kuchelewa kutambuliwa na umoja wa mataifa, nchi ya mbogo #land_land, inayoongozwa na mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mwenye makazi yake katika ngome ya dhadhabu, kwamaana ya Golden Castle, iliyopo ndani ya jiji la Treanch Town, kwa maana ya Treanch Town City.

Tuachane na King Elvis, twende kusini mwa mji huu wa TT, mpaka nje kidogo ya jiji Hilo la Trench Town, ni pembezoni mwa barabara ya kuelekea upande wa msumbiji, katika kitongoji kidogo cha Mmajile, (mmemaliza), mji ulikuwa umechangamka kwa burudani, kama ujuwavyo mji huu, jioni na nyakati kama hizi, watu hutumia muda wao na familia zao, au wapenzi wao, kupata burudani katika bustani za viunga vya jiji, huku wakipata vinywaji na vitafunwa mbali mbali.

Hayatuhusu hayo, sisi twendeni moja kwamoja mpaka kwenye jengo moja kubwa, la ghorofa kumi na mbili, ambao lilikuwa alijamaliziwa ujenzi wake, lililokuwa limezungushiwa uzio wa mabati, kama wafanyavyo wakandarasi wengine wanapofanya ujenzi mkubwa kama huu.

Ndani ya uzio huo yana onekana magari nane ya kifahari, ni jambo la kawaida kwa nchi hii kuona magari kama haya, maana wanachi wengi ni mtajiri, lakini licha ya magari hayo nane, pia kulionekana vijana kumi na tano, walio valia nguo nyeusi, kwa maana ya suruali nyeusi za jinsi, na tishert nyeusi, zilizo kamata miili yao, kichwani kofia nyeusi za cap, waswaili uita kapelo, mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya HECKLER &KOCH G95 toka GERMANY ASSAULT RFLE 5.56MM, H K G 95, yaani hecler & koch G 95, iliyotengenezwa nchi germany assault refle yenye mtutu wa mzingo mill miter 5.56, kwa faida ya msomaji, ni aina ya silah iliyotumika kumuuwa Osama bin laden mwaka 2011.

Wakionekana kuwa makini sana, katika ulinzi wa eneo hilo, lenye mwanga hafifu, vijana hawa walionekana wakiwa wamejipanga kwa kuachiana nafasi ya mita kati ya kumi mpaka kumi natano eneo lote la mbele.

Achana na eneo ili kwa nje, huko ndani katika moja kumbi za jengo hilo, lenye giza, zilionekana taswira za vimvuli vya giza, vya watu kama sita hivi, ambao kiukweli usingeweza kuona sura zao, walionekana kuwa katika mpango flani mzito sana, “bwana James Carvin, alitoroka nchini mwaka 1988, na kukimbilia tanzania, ambako anaalianzisha tena biashara zake na kuwa mfanyabiashra mkubwa na tajiri” alisema mmoja wao, aliekuwa amesimama mbele yao, huku wengine watano, wakiwa wamesima kwa kutengeneza nusu mwezi, huku wakionekana kumsikiliza kwa umakini mkubwa sana.

“bwana James Carvin, ambae kwa sasa anamiliki viwanda vikubwa vya vyakula unga na vinywaji, huko Tanzania, alikimbia nchini, akikwepa tuhuma za uhaini, alionekana kuwa alikuwa anafadhiri kikundi cha kijeshi cha waasi wa zamani, kilicho fahamika kwa jina la harakati za uhuru kwa damu” alisema tena yule ambae walikuwa wanamtazama, ambae kwa haraka alionekana kuwa na umri mkubwa zaidi yao, “naamini bwana James atakuwa na hasira kali sana na serikali, hivyo akielezwa anachotakiwa kufanya juu yetu, lazima ataungana na sisi, na kutusaidia kulipia kontena ishirini za silaha mabomu na risasi, kwaaajili ya mapinduzi, pamoja na kutusaidia chakula kwaajili ya askari wetu waliopo msituni” alisema yule jamaa, ambae licha ya kuwa gizani, na rangi yake kuwa nyeusi, pia alikuwa amevalia koti refu jeusi, suruali nyeusi, viatu vyeusi, na kofia ya duara yeusi yenye kuziba uso wake.

“Lakini mheshimiwa, itakuwaje kama atakataa, maana Jemes nikama mtu wa kufata sheria pia” aliuliza mmoja kati yao, ambae alionekana kuvalia nguo zinazofanana na wale vijana wa nje, “sikia bwana Tambwe, fanya kama nilivyo kuagiza, mweleze kwamba, mimi nimesema, kuwa, endapo tutachukuwa nchi hii, yeye atakuwa huru kuchimba dhahabu, kufanya biashara bila ushuru wowote, pia atapewa eneo kubwa sana la kufungua biashara yake na pia atapewa kandarasi ya kuchimba gass na mafuta, lazima atakubari tu, na kumbukeni kuwa mzigo hupo njiani, sikutatu baadae unatia nanga Queen Irine Bay, lazima tuwe na fedha ya kulipia kwa wale jamaa watukabidhi mzigo wetu” alisema yule alie itwa Mheshimiwa, safari hii akionyesha msisitizo mkubwa, “lakini mheshimiwa, nadhani itakuwa vizuri kama tukiwa na mpango mwingine, maana uwezi kujuwa James atasemaje” safari hii alishauri mtu mwingine, na siyo yule alie itwa Tambwe, huyu alikuwa amevaa suit nyeusi na kofia nyeusi.

Hapo mheshimiwa akatulia kidogo kama sekunde tano hivi, kisha akamtazama yule alie shauri, “sasa nimekuelewa, bwana Kadumya, mpango wapili upo, na utatekelezwa muda mchache sana baada ya huu wa kwanza kushindikana” alisema mheshimiwa ambae mpaka sasa hatuja mfahamu kwa jina, huku wale wengine wakimsikiliza kwa umakini mkubwa sana, “Kadumya hakikisha vijana wako wanafwata maelezo, ikiwa pamoja na endapo huu wakwanza utashindikana, wamuuwe James, kisha watahamia kwenye mpango wa pili, ambao nita wapa muda mfupi baada ya mpango wa kwanza, japo sitegemei kama James akiona mitutu ya bunduki usoni mwake, ataweza kusema hapana” alisema Mheshimiwa akionekana kuwa mwenye uhakika zaidi.

Naam baada ya hapo hawa kutumia muda mrefu mahala pale, wakaagana, “Kadumya, hakikisha vijana wako, wanapanda ndege kesho mapema, kuelekea Tanzania, nguo na silaha watazikuta huko huko, kwa bwana Mbwambo, kule temeke kaburi moja” alielekeza Mheshimiwa, kabla hawajaondoka zao, kwa namna ya siri kama vile Hawakuwa pamoja.******

Naam turudi kigamboni, ambako tayari polisi walisha kagua magari yote yaliyokuwa yana subiri kuingia kwenye kivuko yani Pantoni, pasipo kuliona BMW jeusi, na kuamua kurudi walikotoka, huku CP Ulenje akitoa maagizo askari wasambae maeneo yote kulisaka gari ilo, na yeye pamoja na askari watano wakaelekea upande wa mji mwema, kwenda kumwona bwana Songoro.

Ilikuwa ni safari ya dakika kumi na tano, mpaka kufika kwenye nyumba ya bwana Songoro, iliyo jitenga ndani ya eneo moja kubwa lililozingikwa na vichaka vifupi na minazi mirefu, sehemu ambayo walipofika tu, wakapokelewa na bwana Songoro alie simama sambamba na yule mwanamke, ambae sasa alikuwa amevalia chupi aina ya bikini na sidilia kifuani kwake, kati kati ya eneo la mbele la ile yumba kubwa, huku wakionekana watu waliokuwa wanagala gala chini kwa maumivu makali, huku wengine wakiwa wamepoteza fahamu zao, idadi yao ikifika zaidi ya kumi, huku zikionekana silaha mbali mbali zajadi na zile za kisasa, yani visu mapanga na bastora, vikiwa vimetawanyika eneo lile, huku baadhi ya ya watu hao wakionekana kuvujwa na damu , toka kwenye majelaha mbakubwa, katika sehemu mbali mbali za miili yao.

CP Ulenje alitoa macho kwa mshangao, “Songoro unasema alikuwa kijana mmoja tu?” aliuliza CP Ulenje kwa mshangao, “ukweli sikuwai kufikiria kama kuna mtu anaweza kuwa kama yule kijana, hakika namwitaji na tena namwitaji nimkate kiungo kimoja baada ya kingine” alisema Songoro kwa sauti iliyo jaa chukizo na kasiriko, “vijana tayari wapo kazini, naamini muda siyo mrefu watamtia nguvuni” alisema Ulenje, wakati huo wanaingia ndani, na kukagua watu wengine walio kuwa bado wanagala gala kwa maumivu, wapo waliolalamikia mbavu wapo waliolalamikia nyuso zao, na wapo walio lalamikia miguu yao, ilimradi kila mmoja wao alipata anacho stahili, “unampango gani na hawa watu Songoro” aliuliza Uledi , wakati wanaendelea kukagua mle ndani, “wajinga hawa wanawezaje kupigwa na mtoto mrembo kama yule” alisema Songoro ambae hakuonyesha dalili ya kuwa saidia vijana wake, waliokuwa wanataabika pale chini, “huyo kijana atakuwa tatizo hapa mjini, inabidi apatikane haraka sana” alisema CP Ulenje, huku anatoa simu, kubofya namba kisha akaipiga na kuweka sikioni.

Simu haikuita muda mrefu, ikapokelewa, “OCD mambo ni mazito, kuna uvamizi mkubwa umetokea huku mji mwema kigamboni, kwa mfanyabiashara Songoro, agiza gari la wagonjwa lije huku, pia peleka taarifa vituo vyote vya polisi, hapa mjini, msako mkali uendelee, malengo ni BMW jeusi, kamata kila anae hisiwa mpaka apatikane, na taarifa itolewe kuwa ni mtu hatari sana huyo” alisema CP Ulenje, mara tu baada ya simu kupokelewa, “sawa mkuu inatekelezwa” alijibu OCD, na hapo Ulenje akakata simu, kisha akamtazama Songoro, “hakiki hakikisha unaondoa hizo silaha hapo nje” alisema Ulenje, kwa msisitizo.*******

Naam barabara ya bagamoyo, mtaa wa tegeta, njia panda ya kwasharifu, linaonekana gari moja jeusi aina ya ford ranger likiwa limesimama pembeni ya barabara hiyo, huku mtu mmoja, mwenye mwonekano wa miaka 40, akiwa amesimama ubavuni mwa gari ilo, huku uso wake, ukionekana kujawa na mashaka mengi, mara kwa mara alikuwa anatazama saa yake, na kisha kutazama upande wa mjini, ni wazi alikuwa anatarajia kuona mtu au gari likitokea upande huo….. hivi huyo mzee James atakubari mpango wa mheshimiwa, ebu tuone kitakacho tokea. basi… endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums[/
[/QUOTE]
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI:Toka amalize kuongea na mkuu wamajeshi mkuu huyu wa idara ya polisi jeshini, alikuwa kimya kabisa, akiwaza kuhusu maisha mapya huko kusini mwa Tanzania, ambako anaena kuwa mkuu wa kamandi ya askari wa miguu, yani infanry foces kanda ya Duma, jambo ambalo mwanzo ndilo lililomuumiza kichwa kuliko lile la kumtafuta Deus Nyat ili kesho afikishwe kwa mkuu wa majeshi, “afande tumeshafika” alishtua yule mpambe wake mwenye cheo cha luten, ambae tayari alikuwa amesha mfungulia lango. ..…….endelea….

Na hapo Chawe akatazama kuchoto kwake, na kuona kuwa ni kweli alikuwa nyumbani kwake, kwamba gari lilikuwa limesha simama muda mrefu, “hooooo! sawa” alisema Chawe kama alie changanyikiwa, huku ana shuka toka kwenye gari tayari mschana wakazi alikuwa ameshatoka kuja kumpokea.

Chawe alipiga hatua chache kisha akasimama na kumtazama mpambe wake ambae alikuwa anamkabidhi dada wa kazi mkoba mdogo wa ngozi kwa dada wakazi, “hebu tafuta namba ya askari Deus Nyati kisha mpigie simu muambie kesho kabla ya saa mbili awe amereport ofisini kwangu pale makao makuu” alisema Chawe kisha akageuka na kuelekea ndani.

Mpambe wa Chawe, akaingia ndani ya gari na Dereva ambae muda wote alikuwa kimya akaondoa gari, “afande inaonekana mkuu amepigwa na kitu kizito, maana siyo kwa mabadiliko ya haraka aliyokuwa nayo” alisema yule dereva, mwenye cheo cha koplo huku anageuza gari tayari kuondoka, “kama sio amepigwa onyo, basi atakuwa amepangiwa kwenda mikoani” alisema yule luten huku anapekuwa simu yake kutafuta namba flani na alipoipata akaipiga.

Simu iliita kwa muda flani kisha ikapokelewa, “jambo afande” ilisalimia sauti ya kike upande wa pili wa simu, “jambo Agness, bado hupo ofisini” aliuliza yule luten, “dah! afande unadhani kuna kuondoka sasa hivi, boss wako ameharibu mambo, simu zinapigwa kila dakika toka wizarani, kuulizia taarifa za Deus Nyati” ilisema sauti ya kike, “duh! hiyo ni hatari, ila fanya kitu kimoja tazama taarifa za huyo askari, nadhani kuna namba yake nitumie” alisema yule luten, “sasa hivi nakutumia afande” alisema Agness, kisha wakakata simu.******

Naam wakati huo huo, Bwana Frank Nyati akiwa songea nyumbani kwake, hakika alionekana kusisimuliwa sana na taarifa za vyombo mbali mbali vya habari, juu ya malalamiko ya wananchi na waandishi wa vyombo hivyo vya habari vya kujitegemea juu ya jeshi kumuachisha kijana wake kazi, mzee huyo ambae sasa alikuwa na umri wa miaka arobaini na nane, mida hii alikuwa ametulia sebuleni akipekuwa kurasa za mitandao ya kijamii na kuganda kwenye ile ambayo ilizungumzia habari za kijana wake, “afadhari sasa wananchi wanaweza kupaza sauti, wanapoona jambo limetendwa sivyo” alisema mzee Nyati akilinganisha na miaka ya nyuma, wakati serikali ya nchini yake ya asili, ilivyokuwa inaendesha operation ya tokomeza waasi ndani ya serikali, “hivi huyu anafahamu kinachoendelea huko mitandaoni kweli?” aliuliza kwa sauti kiasi cha mke wake kumshangaa, “mwenzetu vipi tena, au umepatwa na uchizi kwaajili ya mwanao kufukuzwa kazi?” aliuliza mke wake, huku akisimama mbele ya mume wake, aliekuwa amekaa kwenye kochi, “mh! kimewaka huko, udhani Deus wamchezo mchezo, watu wanahoji huko kwanini amefukuzwa kazi” alisema mzee Nyati huku anaiweka sawa simu yake na piga simu kwa Deus.

Simu iliita kwa sekunde kadhaa, kisha ikapokelewa, “hallow baba, nitakupigia kuna kitu nafanya” ilisikika sauti tulivu ya Deus, toka upande wapili wa simu, “subiri kwanza wewe, hivi umesiki…” kabla mzee Nyati hajamaliza kusema alichokusudia kusema simu ikakatika, “mjinga sana wewe, hebu msikilize baba yako” alisema kwa sauti ya juu mzee Nyati huku anajiandaa kupiga tena simu, “hebu tulia kwanza, pengine mwenzio yupo na mkweo, mpe muda kidogo bwana” alisema mama Deus, na kufanikiwa kumtuliza mzee Nyati, “lakini inabidi afahamu mapema kinachoendelea huko mtaani” alisema Frank Nyati, huku anafungua moja ya kurasa ya mtandao wakijamii, na kumwonyesha mke wake.******

Naam tukiwa pale picha ya ndege, kijana alie kuwa amesimama njia panda ya Tumbi, alilitazama gari aina ya BMW S7, lililokuwa linatembea taratibu kuelekea upande wa kwa Mathius, alipoliona limekaribia darajani, kijana yule mwenye makadirio ya miaka thelathini, akatoa simu na kupiga sehemu, ambapo haaikuchukuwa muda mrefu ikapokelewa, “vipi afande mupo wapi?” aliuliza yule kijana, ambae kwa haraka usigeshindwa kuhisi kuwa ni askari wa jeshi la polisi, “tupo mzani tuna kuja kwa speed, vipi umewaona?” ilisikika sauti ikiuliza upande wa pili wa simu, “nawaona mbele yangu, tena gari linatembea taratibu sana, sijuwi kama wanasafari hawajamaa” alisema yule jamaa huku analitazama lile gari aina ya BMW S7.

Lakini kabla hajasikia lolote toka upande wavpili, mara yule jamaa kwa macho yake akaliona lile gari aina ya BMW jeusi, likimaliza kuvuka daraja na kuacha barabara kuu, kisha likaingia upande wa kushoto wa barabara, ambako kulikuwa na barabara ya zamani ya morogoro inayopitia nane nane, “afande kama nilivyosema naona gari limeingia barabara ya nane nane” alisema yule jamaa huku analitazama lile gari, ambalo lilikuwa bado linatembea taratibu, likitokomea kwenye hiyo barabara ya zamani ya morogoro, “unasema kweli wameingia huko?” iliuliza sauti upande wa pili wa simu, “kweli afande, yani bado nawaona wale wanapotelea nane nane” alisema yule jamaa, huku anatazama upande ule wa nane nane, ambako gari lilikuwa limepotelea, kiasi cha kutokuonekana tena.

“afadhari kama wameingia huko, maana tunaenda kuwakamata sasa hivi” alisikika yule wa upande wa pili ambae aliongea jambo, “sikia sasa, hebu chukuwa boda boda, kisha wafuatilie kwa akili wasikushtukie, tazama wanapoenda kuishia” alisema tena yule wa upande wa pili na simu ikakatwa, huku yule jamaa anatazama kushoto na kulia kuona kama kuna boda boda ya karibu, ambapo alifanikiwa kuipata moja na kuikodi, “wahi nane nane, kunagari nyeusi tuiwahi” alisema yule jamaa na kisha safari ikaanza mara moja, huku akisisitiza mwendo mkali, waliwahi lile gari ambalo sasa lilikuwa limetoweka usoni mwao, lakini waliamini kwa mwendo ule walio uona, wangelikuta kabla Halijafika mbali.******

Naaam luten alipopiga namba ya simu aliyopewa na Agnes, ilimwambia kuwa mtumiaji wa simu anayoipiga, anaongea na simu nyingine hivyo asubiri au ajaribu baadae, nae akaikata kwa maana alichagua kujaribu baadae, ambapo alikaa kama dakika mbili tu, akapiga tena, safari ukasikika ujumbe mwingine kuwa simu anayopiga haipatikani, “mpuuzi, anadhani mimi nimwandishi wa habari” alilalamika yule luten, huku anajaribu tena, kupiga ile namba, ambayo ilimueleza vile vile, “khaaa anajiona nani huyu mpuuzi” alijisemea luten, huku anapiga simu kwa Agnes ambae hakuchekelewa kuipokea, “vipi afande hiyo namba haipatikani?” aliuliza Agness, kwa shahuku, “amenizimia simu, hebu tazama namba ya mtu wa karibu kama ni mzazi wake au, mlezi wake” alisema yule luten na kukata simu.******

Yap! kitu ambacho tunapaswa kukifahamu nikwamba, mara baada ya kukata simu ya baba yake, Deus akiwa anaendesha gari taratibu akaizima kabisa, kisha akakata kona kushoto, kuingia barabara ya vumbi, akiiacha ile morogoro, hata Sheba ambae alikuwa amejilaza kwenye seat yake, alipoona wameingia kwenye barabara isiyo rasmi akainuka na kutazama mbele, “Deus, safari yetu ina miongozo, sidhani kama hii ni njia ambayo umepangiwa” alisema Sheba, huku anamtazama Deus kwa macho ya mshangao na tahadhari, “lengo ni kuelekea longai, iwe kwa njia yoyote ile” alisema Deus, huku anaendesha gari taratibu.

Hapo Sheba akajilaza tena kwenye seat na wakati huo huo simu ya kwenye dash board ikaanza kuita, Sheba akainuka tena na kuitazama ile simu, ambayo ilikuwa inapigwa na mtu mmoja tu, ambae ni Boss Atshen, “enheeeee, boss huyoooooo” alisema Sheba huku anabofya kipokeleo na simu ikajipokea na kuwa katika sauti ya wazi, “wapi unaenda wakati uelekeo ni morogoro road?” ilikuwa ni sauti kali yenye jazba toka kwenye ile simu, “ni vyema ukatulia nikufikishie mtu wako salama, sidhani kama njia ilikuwepo kwenye moja ya sheria zako” alisema Deus kwa sauti tulivu, “lakini unapaswa kutembea kwenye barabara ambayo inakupeleka kaskazini mwa Tanzania” ilisema ile sauti, safari hii ikianza kupoa, “lakini hupaswi kunichagulia njia wakati unafahamu hukuniambia kuwa kuna watu wanatufuatilia” alisema Deus kwa sauti ile ile tulivu, “ok! muda gani utafika point B?” aliuliza boss Atshen kwa sauti iliyopoa, ikiwa imeondoka kwenye hali ya hasira, “masaa manne matano kwa makadirio ya juu” alisema Deus kwa sauti yake ambayo ungesema anaongea utani, “mh! kilomita mia nne kasoro, masaa matano, ukiweza nitakushangaza” alisema boss na kukata simu.

Hapo Deus akakamtazama Sheba, “ni vyema kama utafunga mkanda tuanze safari, alisema Deus, kwa saut yake tulivu ya upole, “sidhani kama ni muhimu, we endesha gari, tena na kushauri ufanye kama ulivyo muahidi boss, inaweza kuwa na faida katika maisha yako mapya nje ya jeshi” alisema Sheba, aliekuwa katika hali ile ile ya ukauzu, Deus hakuongea kitu zaidi ya kukanyaga mafuta zaidi kuongeza mwendo, ambao uliendelea kuongezeka kila sekunde zilvyoenda, huku mshale wa speed ukiinuka toka speed ishirini kilomita kwa saa na kukomea kwenye themanini kwa saa, ambapo licha ya gari kupita kwenye barabara iliyokosa tambalale, lakini bado kwa aliekuwa ndani ya gari asingesikia chochote.

Kilomita moja mbele wakiwa wamesha uvuka uwanja wa nane nane na kuuacha kama mita mia nane hivi, eneo ambalo lilikuwa na uwazi pasipo majengo zaidi ya shamba la miti na jengo moja tu, lililofichwa na msitu huu wa kupandwa upande wa kushoto, wakati upande wa kulia kulikuwa na barabara ndogo dhaifu, iliyoelekea upande wa barabara, Deus alikanyaga brake za ghafla na kuingia upande wa kushoto, akifuata njia ambayo inaenda kwenye ile nyumba katikati ya msitu wa kupandwa na binadamu.

Kitendo ambacho kilizuwa msuko suko kwa Sheba ambae aliyumba kidogo akibakiza nchi chache sana, kujibamiza kwenye kioo cha mbele, kutokana na ile brake, huku akipelekwa pembeni, na kujigonga kwenye mlango halafu akakaa sawa na kugeuza uso wake nyuma kuona anacho kikimbia Dereva wake mpya, lakini hakuona chochote zaidi ya kushuhudia gari likiendelea kutililika kwa speed kuingia kwenye yale makazi, “au huyu nae ni mmoja kati ya watu wanao tufukuzia?” alijiuliza Sheba huku anageuza uso wake kumtazama Deus kwa macho yaliyojaa mashaka, “unadhani unafanya nini Deus?” aliuliza Sheba, huku anapeleka mkono kwenye vungu ya kiti chake na kuikamata bastora.. ..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Haya Sheba anataka kumshikia bastola Deus na sisi tunajua kuwa Dues hapendi tena bastola 🙄
Kesho nishtueni mapemaaaaa tuone ni nini kiliendelea
 
BMW S7
 
Attachments

  • IMG_20250122_084551_498.JPG
    IMG_20250122_084551_498.JPG
    47.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom