NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TANO
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NNE: Kijana anatazama barabarani macho yake yana kutana na gari la polisi, hapo ndio anakosa kabisa uwezo wa kujiamini na kuzidi kujawa na wasi wasi,”samahani kaka, nilikuwa ndani ya banda la kuku nafanya usafi ndio maana sikuweza kusikia vizuri” alisema yule kijana kwa sauti ya kuombeleza….endelea….
“acha dharau kwa watu usio wafahamu dogo haya niambie hili gari lililokuja hapa limeenda wapi?” aliuliza Cheleji kwa sauti fulani kavu iliyozii kumtia uoga yule kijana, ambae alishangaa baada ya kuulizwa swali hilo, “gari? …unamaanisha gari gani?” aliuliza yule kijana ambae bado alikuwa katika hali ya wasi wasi, “dogo unarudia makosa, unajuwa sitaki watu waongo, ina maana wewe hujaliona gari lililofika hapa kwenu?” aliuliza Cheleji kwa sauti yenye kitisho, “hapa hakuna gari lilifika ila wakati nafanya kazi zangu, nilisikia gari lina unguruma, nilipo kuja kuchungulia nikaliona gari kule barabarani tena jeusi linageuza na kuingia njia ya upande wa pili, labda hilo, lakini hapa sijaliona gari lolote” alisema yule kijana kwa sauti ile ile ya kuomboleza.
Hapo moja kwa moja bila kuaga, Cheleji alieonekana kugundua jambo akaondoka bila hata kuaga na kuanza kuembea kuwafuata wenzake kule barabarani, walikoegesha gari, ni baada ya kugundua kuwa BMW S7, liligeukia hapo na kurudi barabarani, hivyo kuna uwezekano wametoka nje ya mji kwa kupitia bagamoyo, maana kama wangerudi mjini lazima wangekutana nao njiani.
Naam Cheleji alipolifikia gari, akaingia na kukaa kwenye seat yake, na kutoa simu yake, akapiga kwa CP Ulenje.*******
Naam mzee Frank akiwa nyumbani kwake, alijaribu kupiga simu ya kijana wake kila baada ya dakika tano au kumi, lakini bado haikupatikana, jambo hili lilimchanganya sana mzee huyo, ambae hakuchoka kupiga simu, huku akimlaumu sana kijana wake Deus kwa kuzima simu, we mjinga unapoteza nafasi ya kazi unayoipenda” alipiga kelele za hasira mzee Frank ambae siyo tu kwa yeye kupiga simu kila dakika, pia na yeye alikuwa anapigiwa simu mara kwa mara na Luten Kasian.********
Wakati huo huo, huko Kinyerezi Dar es salaam Monica na binti yake, wakiwa ndani ya gari, sasa walikuwa wanaingia ndani ya lango kubwa la uzio mkubwa ambao kwa vyovyote vile, lazima unge tambua kuwa ni jumba la kifahari, linalokaliwa na watu wenye fedha nyingi sana, gari lile aina ya land rover discover, liliingia ndani nakusimama mbele ya jumba kubwa la kifahari, ambalo muonekano wake ulipendeza, Monica na binti yake Caroline wakashuka na kuelekea ndani, huku wakipishana na wafanyakazi wa ndani, walikuwa wanakimbilia kwenda kushusha mizigo kwenye gari, “ni ajabu sana, sikufikiria kama nitamuona tena kaka Deus” alisema Caroline aliekuwa anatembea sambamba na mama yake, wakielekea ndani ya jumba lao.
Naam wanapoingia ndani wanapokelewa na baba Caroline, ambae alikwa amekaa kwenye kochi, anatazama television ambayo ilikuwa inaonyesha pambano la mpira wa miguu, “naona mmeingia na nyuso za furaha kulikoni jamani?” aliuliza mzee huyo kwa sauti iliyojaa utani, Caroline aliachia kicheko kilicho changanyika na aibu fulani ya kike, wakati mama yake akijibu, “nashiriki furaha ya Carlo si ameiona picha ya yule kijana aliemuokoaga kwenye ajali ya tren wakati ule” alisema Monica akimueleza mume wake, “mh! yule kijana wa miaka ile, hiyo picha ameiona wapi?” aliuliza mzee huyu mwenye muonekano wa kitajiri, japo alikuwa na mwili wa kawaida, yani hakuwa mnene wala mwenye kitambi.
Mama Caroline akaanza kumsimulia mume wake juu ya kisa cha yule kijana, hata baada ya leo kuiona sura ya kijana huyu ikiambatana na habari ya kufukuzwa kazi, “ni habari njema, nakumbuka ulisema ungemzawadia kijana huyo, basi ukimpata nivyema ukitimiza ahadi yako” alisema mzee huyo pasipo kuitazama picha ya kijana yule, ambayo ilitapakaa mitandaoni, nadhani ni kwasababu alikuwa anatazama pambano la mpira wa miguu.******
Saa kumi na mbili na dakika thelathini na tano, ndio muda mbao CP ulenje aliwasiliana na traffic officer wa kituo cha Chalinze na kuagiza kuwa, apewe taarifa ya gari aina BMW S7 nyeusi, kama imekatiza msata, maana waliamini kuwa litakuwa limepitia bagamoyo, “dakika tano afande wacha niwasiliane na traffic waliopo msata” alisema traffic office wa Chalinze, kabla ya kukata simu.
Hata dakika tano hazikutimia kabla simu ya bwana Ulenje haijaita tena na yeye kuipokea, “afande gari limeonekana, lakini bado lina namba za usajili wa muda” alisema traffic officer na hapo Ulenje akaachia tabasamu la mafanikio, “asante sana” alisema ulenje na kukata simu,
Baada ya hapo haraka sana, Uleje akapiga namba ya simu iliyoseviwa, koplo Cheleji, ambae hakuchelewa kuipokea, “ndiyo afande” alisikika sauti ya Koplo Cheleji, yule ambae yupo na wenzake kule kwenye gari, “wasiliana na wenzako haraka waambie wageuze gari kisha nyie wote muelekee Mkata, gari limeonekana linaelekea huko” alisema Ulenje na kukata simu, kisha hapo hapo akapiga namba nyingine ya simu, ambayo iliita kwa mua mfupi sana, ikapokelewa, “jambo afande, naona leo umenikumbuka” ilisikika sauti iliyochangamka toka upende wa pili, “ndiyo bwana Mbuguni, kuna jambo muhimu lililonifanya nikukumbuke” alisema Ulenje, “nakusikiliza afande ni mambo ya kikazi au binafsi?” aliuliza Mbuguni, ambae ni mkuu wakituo cha Mkata, “hii tuifanye binafsi kuna hela ya chai, hebu weka kizuwizi cha muda hapo barabarani, kuna gari dogo jeusi BMW lina kuja huko kwako, hakikisha unalizuia halafu unanipa taarifa mara moja, pia kuna vijana wangu wapo njiani wanakuja” alisema Ulenje kabla ya kukata simu.*******
Mida hiyo hiyo , makao makuu ya jeshi, zilikuwa zina miminika simu kila dakika, kuuliza kama Deus Nyati ameshapatikana kwaajili ya kupewa taarifa za kuja kambini siku inayofuata, lakini ukweli ni kwamba, Deus hakuwa amepatikana, japo mwanzo walipowasiliana na baba yake, waliamini kuwa watampata mapema, lakini sasa hakukuwa na dalili ya kupatikan kwa kijana huyo, ambae hakuwa na mawasiliano ya wazi ambayo yange waounganisha nae, kila mmoja aliingiwa na hofu kubwa juu ya kijana huyo, kwamba ameamua kufanya nini baada ya kuacha jeshi.
Tayari jukumu la kumtafuta Deus, lilisha pelekwa katika idara zote, kuanzia ofisi ya mnadhimu mkuu, mkuu wa mafunzo, usalama na utambuzi, na MP, hata mkuu wa majeshi pia alitoa watu wakushugurikia swala hilo, “kama hajaamua lolote, inakuwaje azime simu” aliuliza major General Mbike, kwa sauti yenye mshangao, mara baada ya kuletewa taarifa kuwa bado simu ya Deus haipatikani, “afande tumejaribu kupiga simu kila dakika, lakini ukweli ni kwamba haipatikani mpaka sasa” alieleza major Salim, ambae alipewa jukumu hilo, “sikia major, nenda kwenye kambi ambayo alikuwa anafanyia kazi mwanzo, mtafuteni mtu wake wakaribu, awaeleze kama alikuwa amejenga au kupanga chumba sehemu, nadhani sasa atakuwa mitaa ya huko” alisema major general Mbike.
“afande hilo tulishalifanya, ukweli nikwamba, yeye alikuwa ni special force, lakini hakukaa kabisa kwenye kikosi chake namba 107 REGMENT, kikosi ambacho kina husisha askari maalumu wenye uwezo mkubwa wa kimapambano, katika mazigira yoyote, yani special force, baada yake muda mwingi alikuwa ameshikizwa hapa makao makuu kwenye tawi lako, sasa kama ni rafiki na watu wakaribu basi ni hapa makao makuu, maana hata watu aliokuwa nao kwenye kambi ya mfunzo ya ulinzi wa amani, wanasema hakuwa na rafiki na wakudumu” alisema yule major, hapo Mbike akachoka kabisa, “ina maana amaeamua kujiweka mbali na jeshi? au kwa kuwa amelipwa izo seti zake za MONUSCO?” aliuliza major general Mbike, kwa sauti iliyo onyesha wazi kutopendezwa na ukosekaji ule wa mawasiliano na askari deus Frank Nyati. .
Naam ilifuatia nusu saa ya majadiliano kati ya General Mbike na yule mwenzie mwenye cheo cha major na mwisho wakakubaliana kuendelea kumtafuta askari huyo, kama idara nyine za makao makuu ya jeshi zinavyofanya.********
Mschana mdogo Carolina, mida hii alikuwa chumbani kwake, amejilaza kitandani, ameshika simu yake ya kisasa mfukoni anaperuzi mitandao ya kijamii akisoma habari zinazo mhusu, kijana Deus, ambae wakati anakutana nae miaka mitano iliyopita yeye akiwa mschana mdogo wa miaka kumi na nne, alivutika sura yake ya upole na kuamini anaweza kuwa mshrika mwenza katika safari ya kutoka makambako kwenda Dar es salaam, kabla kijana huyo hajamsadia kuokoa maisha yake, kwenye ajali kubwa na mbaya ya tren, kisha kupotezana kabisa hadi leo hii alipo shangaa kuona habari zake kwenye mitandao na vyombo vya habari vya mashirika makubwa ya habari duniani, yakizungumzia kuachishwa kazi kwa kijana huyo.
Taarifa ambayo Carolina alikuwa anatamani kuiona ni wapi anapatikana kijana huyo, au mawasiliano, hakuona kama kuna mtu wakaribu wa Deus Frank Nyati, ambae amejitokeza kwenye mitandao, ili aweze kumtumia huyo kumpata kijana huyo, ambae tofauti na miaka mitano iliyopita leo anamtazama kwa macho ya pekee, akitamani kitu zaidi kwa kijana huyo.
Hata hivyo zinapita dakika ishirini pasipo kupata chochote, ambacho kitamsaidia kupata mawasiliano na Deus, zaidi ya kukutana na picha ya kijana Deus, ambae anaonekana kuwa na picha mbili tu, ambazo ziliweza kupatikana, ni wazi hakuwa mtu wa kujionyesha kwenye mitandao, wala kupiga picha mara nyingi, maana ukiachilia kuwa na picha za aina mbili tu, zilizokuwa zinaambatanishwa mitandaoni, pia ata alipojaribu kumtafuta kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii, kama ana account binafsi, katika mitandao hiyo, lakini akuona chochote, wala mtu anae fanana na Deus.
Baada ya kuhangaika bila mafanikio, mwisho akajikuta akitulia anatazama picha ya kijana yule kwa muda mrefu sana, “naamini ipo siku nitakutana na wewe, nitakuambia asante” alijisemea Caroline, ambae aliamini kuwa Deus bado atakuwa anamkumbuka, “hakika haitakuwa katika matatizo au ajali kama wakati ule, naamini safari hii itakuwa siku nzuri kwetu” alijisemea tena Caroline, huku anaachia tabasamu laini, na wakati huo huo simu yake ikaanza kuita na kusababisha ile picha iondoke juu ya kioo cha simu yake na kubakia muonekano wa simu inayo ita, pamoja na jina la mpigaji, ambalo ni Sister.
Caroline akaipokea simu ile na kuiweka sikioni, “hallow dada” aliita Caroline, kwa sauti iliyopoa kidogo, nikama aliona mpigaji amemuondlea picha aliyokuwa anaitazama, “hallow Carlo, mumesha rudi toka mjini?” ilisikika sauti tamu ya kike, “tumesha rudi dada vipi wewe, mbona umechelewa, au ulikuwa na dharula?” aliuliza Carolina, ambae alianza kubadirika na kuwakatika hali ya uchangamfu, “nitarudi saa moja jioni” alisema tena dada yake Carolina, ambae licha ya kuwa na sauti tamu, pia alikuwa na sauti tulivu, “upo na shem eeh..?” alisema Caroline, kwa namna ya kutania, “hapana bwana yeye sijakutana nae ila kuna dharula” ilisikika sauti ya dada, aliongea huku anacheka kidogo, kisha wakaagana na kukata simu.********
Naam Mkata mkoani Tanga, askari wanne wakingozwa na OCS wa kituo hicho cha kitongoji kikubwa cha Mkata walisimamisha gari lao aina ya Toyota landcruizer mali ya jeshi la polisi, kilo mita mbili toka mkata mjini, upande wa kuelekea mkoa wa pwani wakiliegasha gari lao pembeni kidogo ya barabara na kutulia mahali hapo, macho wakiyaelekeza upande huo wa Mkoa wa pwani, hawakuwahi kuonekana kuwa na silaha yoyote mkononi mwao, “hakikisheni ni BMW jeusi, ni maagizo toka dar es salaam…” alisema OCS, ambae hakumaliza kauli yake kabla yeye na askari wake, hawaja shtuliwa na ngurumo nyepesi ya gari, iliyokuwa inatokea upande ule ule wa mkoa wa pwani, ambako wao walikuwa wanatazama, waliliona gari dogo jeusi, lililokuwa linakuja kwa speed kali sana……..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums