Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NNE: Kijana anatazama barabarani macho yake yana kutana na gari la polisi, hapo ndio anakosa kabisa uwezo wa kujiamini na kuzidi kujawa na wasi wasi,”samahani kaka, nilikuwa ndani ya banda la kuku nafanya usafi ndio maana sikuweza kusikia vizuri” alisema yule kijana kwa sauti ya kuombeleza….endelea….


“acha dharau kwa watu usio wafahamu dogo haya niambie hili gari lililokuja hapa limeenda wapi?” aliuliza Cheleji kwa sauti fulani kavu iliyozii kumtia uoga yule kijana, ambae alishangaa baada ya kuulizwa swali hilo, “gari? …unamaanisha gari gani?” aliuliza yule kijana ambae bado alikuwa katika hali ya wasi wasi, “dogo unarudia makosa, unajuwa sitaki watu waongo, ina maana wewe hujaliona gari lililofika hapa kwenu?” aliuliza Cheleji kwa sauti yenye kitisho, “hapa hakuna gari lilifika ila wakati nafanya kazi zangu, nilisikia gari lina unguruma, nilipo kuja kuchungulia nikaliona gari kule barabarani tena jeusi linageuza na kuingia njia ya upande wa pili, labda hilo, lakini hapa sijaliona gari lolote” alisema yule kijana kwa sauti ile ile ya kuomboleza.


Hapo moja kwa moja bila kuaga, Cheleji alieonekana kugundua jambo akaondoka bila hata kuaga na kuanza kuembea kuwafuata wenzake kule barabarani, walikoegesha gari, ni baada ya kugundua kuwa BMW S7, liligeukia hapo na kurudi barabarani, hivyo kuna uwezekano wametoka nje ya mji kwa kupitia bagamoyo, maana kama wangerudi mjini lazima wangekutana nao njiani.


Naam Cheleji alipolifikia gari, akaingia na kukaa kwenye seat yake, na kutoa simu yake, akapiga kwa CP Ulenje.*******


Naam mzee Frank akiwa nyumbani kwake, alijaribu kupiga simu ya kijana wake kila baada ya dakika tano au kumi, lakini bado haikupatikana, jambo hili lilimchanganya sana mzee huyo, ambae hakuchoka kupiga simu, huku akimlaumu sana kijana wake Deus kwa kuzima simu, we mjinga unapoteza nafasi ya kazi unayoipenda” alipiga kelele za hasira mzee Frank ambae siyo tu kwa yeye kupiga simu kila dakika, pia na yeye alikuwa anapigiwa simu mara kwa mara na Luten Kasian.********


Wakati huo huo, huko Kinyerezi Dar es salaam Monica na binti yake, wakiwa ndani ya gari, sasa walikuwa wanaingia ndani ya lango kubwa la uzio mkubwa ambao kwa vyovyote vile, lazima unge tambua kuwa ni jumba la kifahari, linalokaliwa na watu wenye fedha nyingi sana, gari lile aina ya land rover discover, liliingia ndani nakusimama mbele ya jumba kubwa la kifahari, ambalo muonekano wake ulipendeza, Monica na binti yake Caroline wakashuka na kuelekea ndani, huku wakipishana na wafanyakazi wa ndani, walikuwa wanakimbilia kwenda kushusha mizigo kwenye gari, “ni ajabu sana, sikufikiria kama nitamuona tena kaka Deus” alisema Caroline aliekuwa anatembea sambamba na mama yake, wakielekea ndani ya jumba lao.


Naam wanapoingia ndani wanapokelewa na baba Caroline, ambae alikwa amekaa kwenye kochi, anatazama television ambayo ilikuwa inaonyesha pambano la mpira wa miguu, “naona mmeingia na nyuso za furaha kulikoni jamani?” aliuliza mzee huyo kwa sauti iliyojaa utani, Caroline aliachia kicheko kilicho changanyika na aibu fulani ya kike, wakati mama yake akijibu, “nashiriki furaha ya Carlo si ameiona picha ya yule kijana aliemuokoaga kwenye ajali ya tren wakati ule” alisema Monica akimueleza mume wake, “mh! yule kijana wa miaka ile, hiyo picha ameiona wapi?” aliuliza mzee huyu mwenye muonekano wa kitajiri, japo alikuwa na mwili wa kawaida, yani hakuwa mnene wala mwenye kitambi.


Mama Caroline akaanza kumsimulia mume wake juu ya kisa cha yule kijana, hata baada ya leo kuiona sura ya kijana huyu ikiambatana na habari ya kufukuzwa kazi, “ni habari njema, nakumbuka ulisema ungemzawadia kijana huyo, basi ukimpata nivyema ukitimiza ahadi yako” alisema mzee huyo pasipo kuitazama picha ya kijana yule, ambayo ilitapakaa mitandaoni, nadhani ni kwasababu alikuwa anatazama pambano la mpira wa miguu.******


Saa kumi na mbili na dakika thelathini na tano, ndio muda mbao CP ulenje aliwasiliana na traffic officer wa kituo cha Chalinze na kuagiza kuwa, apewe taarifa ya gari aina BMW S7 nyeusi, kama imekatiza msata, maana waliamini kuwa litakuwa limepitia bagamoyo, “dakika tano afande wacha niwasiliane na traffic waliopo msata” alisema traffic office wa Chalinze, kabla ya kukata simu.


Hata dakika tano hazikutimia kabla simu ya bwana Ulenje haijaita tena na yeye kuipokea, “afande gari limeonekana, lakini bado lina namba za usajili wa muda” alisema traffic officer na hapo Ulenje akaachia tabasamu la mafanikio, “asante sana” alisema ulenje na kukata simu,


Baada ya hapo haraka sana, Uleje akapiga namba ya simu iliyoseviwa, koplo Cheleji, ambae hakuchelewa kuipokea, “ndiyo afande” alisikika sauti ya Koplo Cheleji, yule ambae yupo na wenzake kule kwenye gari, “wasiliana na wenzako haraka waambie wageuze gari kisha nyie wote muelekee Mkata, gari limeonekana linaelekea huko” alisema Ulenje na kukata simu, kisha hapo hapo akapiga namba nyingine ya simu, ambayo iliita kwa mua mfupi sana, ikapokelewa, “jambo afande, naona leo umenikumbuka” ilisikika sauti iliyochangamka toka upende wa pili, “ndiyo bwana Mbuguni, kuna jambo muhimu lililonifanya nikukumbuke” alisema Ulenje, “nakusikiliza afande ni mambo ya kikazi au binafsi?” aliuliza Mbuguni, ambae ni mkuu wakituo cha Mkata, “hii tuifanye binafsi kuna hela ya chai, hebu weka kizuwizi cha muda hapo barabarani, kuna gari dogo jeusi BMW lina kuja huko kwako, hakikisha unalizuia halafu unanipa taarifa mara moja, pia kuna vijana wangu wapo njiani wanakuja” alisema Ulenje kabla ya kukata simu.*******


Mida hiyo hiyo , makao makuu ya jeshi, zilikuwa zina miminika simu kila dakika, kuuliza kama Deus Nyati ameshapatikana kwaajili ya kupewa taarifa za kuja kambini siku inayofuata, lakini ukweli ni kwamba, Deus hakuwa amepatikana, japo mwanzo walipowasiliana na baba yake, waliamini kuwa watampata mapema, lakini sasa hakukuwa na dalili ya kupatikan kwa kijana huyo, ambae hakuwa na mawasiliano ya wazi ambayo yange waounganisha nae, kila mmoja aliingiwa na hofu kubwa juu ya kijana huyo, kwamba ameamua kufanya nini baada ya kuacha jeshi.


Tayari jukumu la kumtafuta Deus, lilisha pelekwa katika idara zote, kuanzia ofisi ya mnadhimu mkuu, mkuu wa mafunzo, usalama na utambuzi, na MP, hata mkuu wa majeshi pia alitoa watu wakushugurikia swala hilo, “kama hajaamua lolote, inakuwaje azime simu” aliuliza major General Mbike, kwa sauti yenye mshangao, mara baada ya kuletewa taarifa kuwa bado simu ya Deus haipatikani, “afande tumejaribu kupiga simu kila dakika, lakini ukweli ni kwamba haipatikani mpaka sasa” alieleza major Salim, ambae alipewa jukumu hilo, “sikia major, nenda kwenye kambi ambayo alikuwa anafanyia kazi mwanzo, mtafuteni mtu wake wakaribu, awaeleze kama alikuwa amejenga au kupanga chumba sehemu, nadhani sasa atakuwa mitaa ya huko” alisema major general Mbike.


“afande hilo tulishalifanya, ukweli nikwamba, yeye alikuwa ni special force, lakini hakukaa kabisa kwenye kikosi chake namba 107 REGMENT, kikosi ambacho kina husisha askari maalumu wenye uwezo mkubwa wa kimapambano, katika mazigira yoyote, yani special force, baada yake muda mwingi alikuwa ameshikizwa hapa makao makuu kwenye tawi lako, sasa kama ni rafiki na watu wakaribu basi ni hapa makao makuu, maana hata watu aliokuwa nao kwenye kambi ya mfunzo ya ulinzi wa amani, wanasema hakuwa na rafiki na wakudumu” alisema yule major, hapo Mbike akachoka kabisa, “ina maana amaeamua kujiweka mbali na jeshi? au kwa kuwa amelipwa izo seti zake za MONUSCO?” aliuliza major general Mbike, kwa sauti iliyo onyesha wazi kutopendezwa na ukosekaji ule wa mawasiliano na askari deus Frank Nyati. .


Naam ilifuatia nusu saa ya majadiliano kati ya General Mbike na yule mwenzie mwenye cheo cha major na mwisho wakakubaliana kuendelea kumtafuta askari huyo, kama idara nyine za makao makuu ya jeshi zinavyofanya.********


Mschana mdogo Carolina, mida hii alikuwa chumbani kwake, amejilaza kitandani, ameshika simu yake ya kisasa mfukoni anaperuzi mitandao ya kijamii akisoma habari zinazo mhusu, kijana Deus, ambae wakati anakutana nae miaka mitano iliyopita yeye akiwa mschana mdogo wa miaka kumi na nne, alivutika sura yake ya upole na kuamini anaweza kuwa mshrika mwenza katika safari ya kutoka makambako kwenda Dar es salaam, kabla kijana huyo hajamsadia kuokoa maisha yake, kwenye ajali kubwa na mbaya ya tren, kisha kupotezana kabisa hadi leo hii alipo shangaa kuona habari zake kwenye mitandao na vyombo vya habari vya mashirika makubwa ya habari duniani, yakizungumzia kuachishwa kazi kwa kijana huyo.


Taarifa ambayo Carolina alikuwa anatamani kuiona ni wapi anapatikana kijana huyo, au mawasiliano, hakuona kama kuna mtu wakaribu wa Deus Frank Nyati, ambae amejitokeza kwenye mitandao, ili aweze kumtumia huyo kumpata kijana huyo, ambae tofauti na miaka mitano iliyopita leo anamtazama kwa macho ya pekee, akitamani kitu zaidi kwa kijana huyo.


Hata hivyo zinapita dakika ishirini pasipo kupata chochote, ambacho kitamsaidia kupata mawasiliano na Deus, zaidi ya kukutana na picha ya kijana Deus, ambae anaonekana kuwa na picha mbili tu, ambazo ziliweza kupatikana, ni wazi hakuwa mtu wa kujionyesha kwenye mitandao, wala kupiga picha mara nyingi, maana ukiachilia kuwa na picha za aina mbili tu, zilizokuwa zinaambatanishwa mitandaoni, pia ata alipojaribu kumtafuta kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii, kama ana account binafsi, katika mitandao hiyo, lakini akuona chochote, wala mtu anae fanana na Deus.


Baada ya kuhangaika bila mafanikio, mwisho akajikuta akitulia anatazama picha ya kijana yule kwa muda mrefu sana, “naamini ipo siku nitakutana na wewe, nitakuambia asante” alijisemea Caroline, ambae aliamini kuwa Deus bado atakuwa anamkumbuka, “hakika haitakuwa katika matatizo au ajali kama wakati ule, naamini safari hii itakuwa siku nzuri kwetu” alijisemea tena Caroline, huku anaachia tabasamu laini, na wakati huo huo simu yake ikaanza kuita na kusababisha ile picha iondoke juu ya kioo cha simu yake na kubakia muonekano wa simu inayo ita, pamoja na jina la mpigaji, ambalo ni Sister.


Caroline akaipokea simu ile na kuiweka sikioni, “hallow dada” aliita Caroline, kwa sauti iliyopoa kidogo, nikama aliona mpigaji amemuondlea picha aliyokuwa anaitazama, “hallow Carlo, mumesha rudi toka mjini?” ilisikika sauti tamu ya kike, “tumesha rudi dada vipi wewe, mbona umechelewa, au ulikuwa na dharula?” aliuliza Carolina, ambae alianza kubadirika na kuwakatika hali ya uchangamfu, “nitarudi saa moja jioni” alisema tena dada yake Carolina, ambae licha ya kuwa na sauti tamu, pia alikuwa na sauti tulivu, “upo na shem eeh..?” alisema Caroline, kwa namna ya kutania, “hapana bwana yeye sijakutana nae ila kuna dharula” ilisikika sauti ya dada, aliongea huku anacheka kidogo, kisha wakaagana na kukata simu.********


Naam Mkata mkoani Tanga, askari wanne wakingozwa na OCS wa kituo hicho cha kitongoji kikubwa cha Mkata walisimamisha gari lao aina ya Toyota landcruizer mali ya jeshi la polisi, kilo mita mbili toka mkata mjini, upande wa kuelekea mkoa wa pwani wakiliegasha gari lao pembeni kidogo ya barabara na kutulia mahali hapo, macho wakiyaelekeza upande huo wa Mkoa wa pwani, hawakuwahi kuonekana kuwa na silaha yoyote mkononi mwao, “hakikisheni ni BMW jeusi, ni maagizo toka dar es salaam…” alisema OCS, ambae hakumaliza kauli yake kabla yeye na askari wake, hawaja shtuliwa na ngurumo nyepesi ya gari, iliyokuwa inatokea upande ule ule wa mkoa wa pwani, ambako wao walikuwa wanatazama, waliliona gari dogo jeusi, lililokuwa linakuja kwa speed kali sana……..….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI TATU: kiti ambacho angekiokota moneytalk au woodpecker24 wange nunua mtaa mzima na majumba na mali zote za mtaa na wakazi wa mtaa huo wangewaajili kulima mashamba, na kufanya kazi kwenye viwanda vyao, ambavyo wange vianzisha kwa fedha hiyo hiyo, pia fedha inayo bakia wangeinunua simba na ndio ingekuwa mwaka wao wa kwanza kuchukua club bingwa maana wangetumia fedha hiyo hiyo kuhonga marefa waibebe timu na Doctor G angeacha hiyo kazi akajenga hospital za kwake (hayo ni mawazo ya rafiki yangu Mduku aliyoyatoa siku alipokiona kile kiti cha King Elvis wa kwanza siku tulivyotembelea #mbogoland kwenye ndoa ya Radhia) endelea nayo ….


“Kuna jambo gani tena, au ni lile la askari kuacha kazi?” aliuliza malkia Vaselisa kwa sauti ya unyenyekevu, sauti ambayo mala nyingi huitumia anapohitaji kumuondoa mume wake toka kwenye mawazo ya kiunyonge, “hilo ni moja wapo maana leo nimengundua kuwa kuna baadhi ya askari waliacha jeshi kipindi cha vugu vugu la kundi la UMD, mmoja wao akiwa askari mtiifu na shujaa luten kanal Frank Nyati, alie muokoa mara kadhaa King Eugen wa 25, lakini pia nimegundua kuwa kuna dalili za kurudi kwa kundi la UMD, inawezekana wakina Frank Nyati wanaunda tena kundi hilo?” aliuliza Elvis, sasa akimtazama mke wake ambae pia alionekana kuvuta kumbu kumbu flani.


Uvutaji wa kumbu kumbu ambao ulimfanya achelewe kumjibu mfalme, ambae alimtazama mke wake kwa umakini mkubwa huku akisubiri jibu la mwanamke huyo, ambae kikawaida Elimu yake haikuwa kubwa sana, ila alikuwa na busara zilizo mzidi kimo, “hapa najaribu kuwaza hilo jina nimelisikia wapi halafu siyo muda mrefu” alisema malkia Vaselina huku akijaribu kuvuta kumbu kumbu zaidi, “Nyati…. nyati … Nyati, hoooo! sawa, huyo ni mtazania” alisema Vaselisa, alijaribu kupotezea habari ya huyo ya mtanzania alieitwa Nyati, “amefanyaje huyo mtazania?” aliuliza King Elvis, huku akitazama mke wake.


Mke wake ambae ukiachikia shuguri zake za kusimamia maswala ya jinsia na watoto pamoja na afya, katika nchi ile ya #mbogo_land, akisaidiana na mwanamama Thesilia Martin, mama yake Careen wa kwenye simulizi ya KIAPO CHA FUKARA hiyo ni baada ya kushindwa kuongoza peke yake, kutokana na Elimu ndogo aliyokuwa nayo Malkia huyo, ambae sasa anaendelea kupata Elimu ya chuo baada ya kushauriwa na mama mkwe wake yaani Malkia doctor Irene Simon wa kwenye simulizi ya UMEKOSEA LAKINI TAMU kwamba ajiendeleze Elimu ili awezekuongoza wizara hiyo, ambayo ni lazima kwa mke wa Mfalme.


Pia mwana huyo ambae pia ni mmoja kati ya waschana wadogo kupata kuwa wake wa viongozi wakubwa wanchi alikuwa anapenda sana kuperuzi mitandao ya kijamii ili kuijuwa dunia na kujifunza zaidi, “hukuwahi kusikia habari za Deus Nyati?” aliuliza Vaselisa kwa mshangao, “nisingekuuliza mke wangu, hebu nipe habari zake” aisema King Elivs na kujiweka sawa ili awezekupata habari za mtu huyo ambae mwanzo alihisi anaweza kuwa ndie Nyati ambae alitoweka nchini kwake.


Naam Malikia Vaselisa akaanza kueleza kisa cha askari mtanzania, alie waokoa mdoctor watatu, wa umoja wa mataifa huko nchini Congo na baadae kukutwa na hatia ya jaribio la ubakaji, akishinda kesi kwa kuonekana amesingiziwa na kwamba ulikuwa ni mpango wa IDFNALLU, lakini anaondolewa UN kwa kosa la kufanya jukumu nje ya mkataba na mwisho nchi yake inamfukuza kazi kwa kuliaibisha taifa, “bado sijafanya ujinga huo, hapo lazima ningevunja sheria za nchi yangu, kwa kumuacha askari aendelee na kazi” alisema King Elvis, mwishoni mwa hadithi toka mke wake, “pengine kuna askari wengi wa namna hii, hivyo hawahofii kumpoeza mmoja kwa heshima ya nchi” alisema Vaselisa ambae licha ya kuchanganya damu ya Mmakonde na mwarabu, lakini maisha yake kwa kiasi kikubwa aliishi Dar es salaam.


Waliongea mawili matatu juu ya Deus Nyati, kabla hawaja badili maongezi, pasipo mfalme kufahamu au kulijuwa jina la tatu la askari huyo, shujaa mwenye bahati mbaya.*********


Yap! saa kumi na moja kasoro gari la polisi, lilikuwa kwenye soko dogo maarufu kama mnadani pale kwa matius, njia ya kwenda Efatha, askari saba, wakiwa nyuma ya gari huku koplo Cheleji, akionekana akiwa amesimama kwenye kibaraza cha nyumba moja, pale pembeni ya barabara inayotenganisha nyumba kadhaa upande wa kushoto na soko likiwa upande wakulia mbele yake wakiwa mafundi wa kushona, tume zowea kuwaita mafundi cherehani, mnasema hamjaliona gari dogo jeusi jipya hivi, BMW likipita hapa?” aliuliza Cheleji, akionekana kuishiwa nguvu, baada ya kukosa kile alicho tegemea, “yaani kaka lingepita tunge liona, maana hapa yanapita magari machache sana na yote tumeyaona kama hilo lingepita nalo tungeliona tu” alisema mmoja kati ya wale fundi cherehani wa kiume alieonekana kuwa na umri mkubwa zaidi ya wote, aliekadiriwa kuwa na miaka hamasini na tano, “ok! sie tunaondoka ila kama mtakumbuka chochote au kuliona gari hilo mutatueleza maana tutapia baadae” alisema Koplo Cheleji, wakati anaaga na kundoka kuelekea kwenye gari.


Naam Koplo Cheleji akaingia kwenye gari ambalo wenzake walikuwa wanamsubiri, kisha gari likaondoka kuelekea barabara ya zamani ya Morogoro na walipoikuta wakafuata upande wa kuelekea picha ya ndege yaani kule ambako yule mwenzao aliliona BMW 7 likielekea.


Gari aina ya land rover mia na kumi, lilitembea taratibu huku wote wakiwa makini kutazama kushoto na kulia kama wangeweza kuliona BMW S7, lakini mpaka wanafika pale kwenye msitu, hawa kuwa wameliona gari lile wala dalili ya uwepo wa gari ilo.


Lakini wakati wanataka kukatiza kwenye njia ya kuingia kwenye ile nyumba iliyopo kwenye kichaka cha miti ya kupanda ghafla dereva akasimamisha gari, “afande naweza kuona kuna gari liliingia barabara hiyo njia hapo” alisema dereva wa lile gari la polisi, ambae alikuwa kule mbele ya gari na Cheleji hapo Cheleji nae akatazama kwenye sakafu ya barabara, inayoingia kwenye ile nyumba na kuona alama za tairi za gari akazifuatilia na kuziona zinatokea kwenye ile nyumba, “mh! mbona kama ni gari la ile nyumba” alisema Cheleji, huku anarudisha macho yake upande wa barabara lakini usawa wa sakafu ya barabara ambapo tairi za gari zilizo futika zilionekana kuvuka barabara, “lakini afande unadhani mwenyeji wa eneo hili anaweza kupitisha gari kwenye barabara hii?” aliuliza dereva, huku wakitazama tairi za gari zilizovuka upande wa pili wa barabara.


Naam! hapo nikama Koplo Cheleji alibaini jambo jipya, mh! hebu subiri kidogo, inawezekana hawa washenzi walishtukia kuwa wanafuatiliwa, wakaja kujibanza hapa na Mao alipopita tu wao wakarudi walikotoka na kubadili njia, kama huamini hebu kwanza uone” alisema Cheleji huku anafungua mlango wa gari na kushuka chini, kisha akaelekea kwenye ile nyumba ya kichakani, huku akimuacha dereva anaegesha gari pembeni ya barabara.


Cheleji alitembea kwa haraka kuifuata ile nyumba, huku anatazama kwa umakini alama zile za tairi za gari mpaka alipofika nazo kwenye ile nyumba, na kuziona zikiwa zimeishia ubavuni mwa nyumba, ile ambayo kiukweli ilikuwa kimya kiasi, japo walionekana kuku na bata wakizurula eneo lile la nyumba ile tulivu.


Cheleji akasogelea lango na kugonga hodi mara kadhaa, lakini hakupata mrejesho wowote toka ndani, akarudia tena na tena lakini mambo yakawa vile vile, Cheleji akiwa amekata tamaa ya uwepo wa wenyeji akageuka ili kuondoka, lakini kabla hajapiga hatua hata moja, akasikia michatoka ya vishindo vya mtu upande wa ndani, akiufuata mlango, Cheleji akasimama na kusikilizia kifuatacho.


Nikweli sekunde chache baadae, mlango ukafunguliwa akaibuka kijana mmoja wakati ya umri wa miaka kumi na tisa au ishirini, mwenye uso wa tabasamu na ukarimu, “karibu bro, pole sana maana nilikuwa na jiuliza hii hodi ni huku au?” alisema yule kijana, ambae alionekana wazi kuwa alikuwa ametoka kwenye kazi fulani ngumu, iliyomfanya achafuke nguo zake chakavu, alizokuwa amezivaa, “kwa hiyo ukashindwa kuacha upuuzi wako nakuja kusikiliza mara moja, ukaamua unichomeshe mahindi hapa mlangoni?” aliuliza Cheleji kwa sauti kavu isiyo na utani hata chembe, kiasi cha yule kijana mkarimu kujikuta akibadiri sura yake toka katika hali ya tabasamu, na kuwa katika hali ya uoga na wasi wasi.


Kijana anatazama barabarani, macho yake yana kutana na gari la polisi, hapo ndio anakosa kabisa uwezo wa kujiamini na kuzidi kujawa na wasi wasi,”samahani kaka nilikuwa ndani ya banda la kuku, nafanya usafi ndio maana sikuweza kusikia vizuri” alisema yule kijana kwa sauti ya kuombeleza….endelea…. kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unaoo kujia hapa hapa jamii forums
Big up mkuu
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI TANO: wakiliegesha gari lao pembeni kidogo ya barabara na kutulia mahali hapo, macho wakiyaelekeza upande huo wa Mkoa wa pwani, hawakuonekana kuwa silaha yoyote mikononi mwao, “hakikisheni ni BMW jeusi ni maagizo toka dar es salaam…” alisema OCS, ambae hakumaliza kauli yake kabla yeye na askari wake hawaja shtuliwa na ngurumo nyepesi ya gari, iliyokuwa inatokea upande ule ule wa mkoa wa pwani ambako wao walikuwa wanatazama, waliliona gari dogo jeusi lililokuwa linakuja kwa speed kali sana……..….endelea….


Sekunde tano mbele tayari gari lile dogo lilisha wakaribia kabisa, “ni BMW, lizuwieni” alipiga kelele OCS huku anasogea barabani kwa lengo la kusimamisha gari lile akionekana wazi kuwa alikuwa ameshalitambua gari lile kuwa ndio gari aliloelekezwa na CP Ulenje.********


Naam, sasa tunaenda kaskazini mgharibi mwa mji wa moshi, huko mkoani kilianjaro, mita mia nane toka Samaxi, karibu na maingilio ya eneo maarufu lenye kuchimbwa madini pekee na maalumu ya Tanzanite, ambayo mpaka hadithi hii inakamilika yalikuwa yana patikana Tanzania pekee, japo yalifanana kwa ukaribu na mdini maarufu yenye thamani kubwa la almasi ya Blue, yani blue diamond, yanayopatikana nchi ya jirani na Tanzania, yani #Mbogo_land, kabla hujaingia kwenye kitongoji kikubwa cha Melerani, lilionekana gari aina ya Subaru impreza likitimua vumbi kuelekea njia panda ya KIA, likionekana kama lipo kwenye mashindano ya mbio za magari.


Hatuwezi kulifuata gari hilo kutokana na mbio ambazo lilikuwa linatimka nyuma yake, hivyo tuna lisindikiza kwa macho na kuliona likitokomea upande wa Arusha, dakika saba tatu baadae, inasikika ngurumo kali ya gari likitokea kwenye barabara ya maingilio ya pale kwenye machimbo ya Tanzanite, wakati huo ni kabla ya kujengwa ukuta wa kuzunguka eneo lile, likija mbio na kupita kwa kasi kuelekea upande wa Arusha, yani kule liliko elekea lile Subaru, nikama lilikuwa linajaribu kulifuata lile Subaru kwa malengo fulani.*******


Ilikuwa hivi, Deus akiwa ndani ya BMW S7 na mschana Sheba, amekanyaga mafuta, gari lina soma kuwa linaenda mwendo wa kilomita mia mbili kwa saa moja, ndipo ghafla alipo liona gari la polisi likiwa limesimama pembeni kidogo ya barabara sambamba na askari polisi kadhaa ambao hakujua idadi yao, hakuweza kupunguza mwendo wala kufikiria kufanya hivyo, sababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo, maana sheria ilimruhusu kutembea speed yoyote zaidi ya kilomita hamsini kwa saa.


Lakini wakati anakaribia usawa wa wale polisi, akawaona wameshtuka na mmoja anasogelea barabarani ni wazi alikuwa anataka kuwasimamisha, “mpuuzi” alisema Deus Nyati, huku mguu wake wa kulia ukiwa bado umekanyaga pederi ya mafuta na mshare wa speed uking’ang’ania kuhama toka kwenye mia mbili na kuelekea kwenye mia mbili na kumi.


Kuna mlio fulani sidhani kama unaandikika, yani “vup!” ndivyo ilivyosikika wakati anampita yule polisi ambae wenzie walishika vichwa vyao kwa hofu ya kwamba endapo gari linge mkuta yule mwenzao, ingekuwa vigumu sana kukuta mfupa hata mmoja ambao ni mzima, maana yote ingekuwa imevunjika, “polisi hao” alisema Sheba huku wote wanatazama kwenye side mirror na kuwaona wale polisi wakisogea barabarani kumtazama mwenzao ambae ni kama alishikwa na butwaa, “tuwahi haraka mkata, kabla hawajapiga simu kwa mpuuzi yoyote” alisema Deus, huku anaendelea kuongoza gari lililokuwa katika speed kali sana, “pia jiandae kwa lolote ambalo litatokea mbele ya safari, maana lazima watapiga simu watuzuwie” alisema Sheba, ambae wasi wasi wake juu ya Deus, ulionekana kutoweka kabisa, “hii ni wazi kuwa unatafutwa na polisi na tayari wamesha fahamu kuwa tunaelekea Kilimanjaro” alisema Deus kwa sauti yake tulivu huku anapunguza mwendo kidogo, kuliingia tuta kubwa, mwanzoni mwa kitongoji cha mkata, kisha akakanyaga tena mafuta, mara tu baada ya kulivuka tuta, huku wakishangiliwa na vijana wauza nyama za mbuzi pamoja na boda boda, waliokuwa pembeni ya barabara.


Sekunde kumi tu, zilitosha kwa wao kukatiza kitongoji kile na kutokomea kaskazini zaidi, na kutoweka kabisa wakiacha kelele za nderemo, toka kwa vijana wa pale Mkata.******


Naam CP Ulenye akiwa nyumbani kwake, anasubiri simu toka kwa mkuu wa kituo cha mkata akiwa anaamini kabisa kuwa gari aina ya BMW litakamatwa pale mkata, huku vijana wake wakina Cheleji, waliopo njiani kuelekea mkata, katika makundi mawili kwamaana ya gari na askari watarudi na dhahabu wakiwa tayari wamesha wauwa hao watu wawili, ambao ni kijana wakiume alieonwa na Cheleji, ambae waliamini kuwa ni kijana aliepewa lift, pamoja na mwenzie ambae bado walikuwa hawajamuona na ndie mlengwa wa kuwatelekeza vichakani kisha kuchukuwa gari lao na dhahabu.


Mara ghafla anasikia simu yake inaita na alipotazama kioo cha simu yake akaona kile alicho kitarajia, yani jina la OCS Mkata, akiwa ndie mpigaji "najivunia kuwa na watu kila sehemu" , alinong’ona Ulenje huku anapokea simu yake, na kuiweka sikioni, “niambie mmesha likamata?” hilo lilikuwa ndio neno la kwanza toka kwa Ulenje, “afande ni zaidi ya hatari yani muda mfupi tu, toka upige simu gari limepita hapa mkata kwa speed ya ndege vita inayo jiandaa kuruka” ilisikika sauti toka upande wapili wasimu, “mpuuzi wewe, mmeshindwa kumfukuzia kwa gari lenu?, kama hauna mafuta si ungeniambia” alisema kwa sauti ya ukali Ulenje na pasipo kusubiri kusikia anacho taka kusema yule wa upande wapili akakata simu.


Naam akiwa bado amefura kwa hasira, Ulenje akaboya namba flani kwenye simu yake na kuiweka sikioni, ambapo haikutumia hata sekunde tano tayari akaanza kuongea, “Cheleji, mpo wapi?” aliuliza Ulenje kwa sauti kavu kama ya kushtukiza, sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa hakuhitaji maneno mengi, “afande sasa hivi ndio tuna karibia msata, ila wakina Othman, nimeongea nao dakika kumi zilizopota, tayari walikuwa wamesha pita mzani” ilisikikatoka upande wapili wa simu, “upumbavu mnaendeshaje gari, hebu fanyani haraka, mulipate hilo gari” alisema Ulenje kwa sauti kali na kukata simu.


“khaaa! hawa wapuuzi wanaenda wapi au wanataka kuvuka kwenda Kenya?” aling’aka Ulenje huku anapofya simu yake kupekuwa kitabu cha majina, niwazi alikuwa anatafuta jina fulani, jina ambalo alilipata sekunde chache baadae, lilikuwa ni OC CID Mombo, akaipiga namba hiyo, ambayo iliita muda mrefu kidogo na ikiwa inakaribia kukatika ikapokelewa, “samahai afande nipo kwenye kelele kidogo sikuisikia simu yako, habari za huko Dar?” alisikika mtu toka upande wapili wa simu, “siyo mbaya ila sina muda wakuongea mengi, kuna jambo nataka unisaidie” alisema Ulenje kwa sauti kavu ambayo haikuhitaji mambo mengi.


Ulenje alimweleza Bosco kuwa anahitaji alizuwie gari aina BMW jeusi, “fanya haraka sana, maana muda wowote linaweza kufika hapo kuna hela nzuri sana ukifanikiwa” alisema Ulenje, ambae alimuelekeza Bosco, ambae ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai pale Mombo, kuwa afanye kila linalowezekana atege askari kilomita nne toka Segera njia panda, upande wa kuelekea Tanga mjini na pia wengine wakae upande wa kuelekea moshi kilomita nne toka Mombo, “hakikisha inakuwa sehemu yenye kichaka pasiwe na ushahidi kuna vijana wangu wapo njiani wanakuja kwa haraka” alisisitiza Ulenje kabla ya kukata simu.******


Naam mzee Nyati bado alikuwa katika hali ya sinto fahamu, akijiuliza kwa nini kijana wake amezima simu kwa muda mrefu, maana sasa yalishatimia masaa mawili, simu bado imezimwa, “mama Deus, unajuwa simuelewi mwanao, anawezaje, kuzima simu muda wote huu” alisema mzee Nyati kwa sauti ya kulalamika, “baba Deus, pengine mtoto amezima simu, kwa sababu hataki usumbufu, usikute yupo na mkwe wetu, anampooza baada ya safari na kazi ya muda mrefu huko alikokuwepo na kama ujuavyo toka ameingia jeshini hakuwahi kupumzika” alisema mama Deus kwa sauti iliyojaa mbwebwe, wanawake bhana! haya tuendelee wadau wangu wa JF nawakubali sana.


Ilimshangaza kidogo mzee Nyati, “wewe, ina maana unaunga mkono kitendo cha Deus kuzima simu muda wote huu, kwamba apoteze kazi kizembe hivi?” aliuliza mzee Nyati kwa sauti ya mshangao huku anamtazama mke wake, kwa macho yenye mshangao zaidi kama vile anatazama mzimu, “kwani unadhani Deus anahitaji kurudi kazini, kazi ambayo, imemzungusha bila utulivu katika utumishi wake wote na mwisho wake anaambulia kufukuzwa kazi kwa aibu kwamba ameliaibisha taifa, hawakukumbuka sifa zote alizowaletea kuwa askari shupavu toka nchini kwao” alisema mama Deus, kwa sauti ambayo kiukweli haikuwa na pingamizi kuwa hakutaka tena mwanae arudi jeshini.


Hapo mzee Frank ni kama alikumbushwa jambo fulani, jambo lililotokea miaka ya 1992, jambo ambalo lilimtokea yeye ambae licha ya kumuokoa mfalme mara tatu, kujituma kwenye utendaji wa kazi, mwisho mfalme huyo huyo, alikubaliana kuwa yeye auwawe ya kwamba ni msaliti wa taifa la #mbogo_land, “ni kweli mke wangu, kwanini wamemfukuza na wakati hui huo wanaanza kumuhitaji hapo kuna jambo ambalo linanifanya nizidi kutamani kuwasiliana na Deus, nimueleze kuwa asijekuwasha simu, na aendelee kujificha huenda wanataka kumuondoa duniani moja kwa moja ili asije kuwasumbua hapo baadae kutokana na uwezo wake” alisema mzee Nyati kwa sauti ya ung’amuzi.******


Yap! saa kumi na mbili na robo kwa saa za afrika mashariki gari dogo aina ya BMW S7 lilionekana likikatiza katikati ya mji mdogo wa Mombo kwa mwendo wa kawaida tu, vioo vya giza vimepandishwa mpaka juu, wanje haoni ndani, ila ndani yake, anaonekana kijana Deus na mschana Sheba, wakiwa makini wanatazama nje ya gari kuona kama kuna mtu anawafuatilia.


“sioni kama kuna mtu anatufuatilia hapa tuna weza kutafuta hotel tupate chochote” alisema Seba, aliekuwa ametulia kwenye seat yake, “nita kula Arusha baadae nikishakufikisha salama” alisema Deus, ambae hadithi yetu, inatuonyesha toka alipopata kifungua kinywa akiwa Kampala kwenye hotel ya kina Neela, hakuwa amepata chakula chochote, “unaishije kama roboti unaongea kivivu..” alisema Sheba kwa sauti ya ukali, lakini Deus akamuwahi kwa sauti tulivu, “lakini nina sura ya upole na pia ninatabasamu la upole” alisema Deus na wote wakacheka kicheko hafifu, “haichekeshi Deus, unasura ya upole lakini ni mkorofi sana” alisema Sheba, kwa sauti ya utani, huku anafugua mkebe wa dash board, na kufanya zionekano bando za noti za elfu kumi kumi za kitanzania,


Ananyakuwa bando moja kati ya manne makubwa yaliyopo ndani ya mkebe, “utasimama basi tuchukue maji na soda, upooze koo lako dereva wangu” alisema Sheba huku anachomoa noti mbili na kurudisha lile bando kwenye mkebe, kisha akaufunga, “usijari, japo wewe ndie mwenye kupooza kiu yako” alisema Deus, huku anasimamisha gari pembeni ya barabara karibu na safu ya maduka.


Ile anasimama tu, Sheba akafungua mlango haraka na kushuka, akaelekea kwenye moja ya duka kati ya yale matano yaliyopo pale barabarani, ambako alitumia dakika kama saba au nane, kisha akarudi akiwa na mfuko wenye vinywaji na vitafunwa vikavu, akaingia kwenye gari na safari ikaendelea.


Naam mara baada ya kuacha mji, Dereva akaongeza mwendo kama ilivyo kawaida yake, ndani ya dakika moja tu, tayari gari lilikuwa lina tembea kwa mwendo wa kilomita mia moja themanini kwa saa na kufanya dakika mbili tu, wawe wamesha tembea zaidi ya kilo mita tatu, na wakati gari linaelekea kwenye mwendo wa kilomita mia mbili nao wakainuka kwenye tambalale moja nzuri sana, ambayo Deus aliamini kuwa atatembea zaidi ya kilomita mia mbili kwa saa.


Lakini ile wanakaa sawa tu, ghafla mita kama moja mbele yao, wakaliona gari la polisi likiwa kati kati ya barabara, limesimama kwa mtindo wa kukatiza barabara, yaani kizuwizi, huku polisi sita wakiwa wamesimama pembeni ya gari lile na bunduki mikononi mwao, zikielekea kule waliko kuwa wanatokea wao, huku mmoja wao akiwa amesimama katika kati ya gari, yaani ubavuni mwa gari, amenyoosha mkono mmoja juu, ikiwa ni ishara ya kusimamisha gari lao, “washenzi wametupata” alisema Deus, huku anaanza kupunguza mwendo kwa nguvu, kwaajili ya kusimama.....
Usikose Kufuatia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
mkuu barikiwa sana na endelea kutuburudisha.
 
R.I.P sheba wanajf tulikupenda ila polisi wa mombo wamekupenda zaidi 😭😭
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI SITA: Lakini ile wanakaa sawa tu, ghafla mita kama mia moja mbele yao, wakaliona gari la polisi, likiwa kati kati ya barabara limesimama kwa mtindo wa kukatiza barabara, yani kizuwizi huku polisi sita wakiwa wamesimama pembeni ya gari lile na bunduki mikononi mwao zikielekea kule waliko kuwa wanatokea wao, huku mmoja wao akiwa amesimama katika kati ya gari, yani ubavuni mwa gari amenyoosha mkono mmoja juu, ikiwa ni ishara ya kusimamisha gari lao, “washenzi wametupata” alisema Deus, huku anaanza kupunguza mwendo kwa nguvu kwaajili ya kusimama……….ENDELEA….


Wote wawili walitulia kimya, wakishuhudia gari likiendelea kusotesha tairi kwenye lami kwaajili ya kusimama, hata liliposimama, Deus alikuwa amefanya juhudi ya hali ya juu sana kulisimamisha gari lile pasipo kusababisha ajari.


Hapo Deus aliekuwa anawaza namna ya kumuokoa yule mschana, ili amfikishe sehemu aliyokusudiwa na yeye kupata malipo yake maana hakujua habari ya dhahabu ambayo msomaji unaifahamu, aliwatazama wale polisi ambao walikuwa wanalizunguka gari na bunduki zao mikononi, mitutu wameilekezea kwenye gari, “hivi uliwafanya nini hawa washenzi?” aliuliza Deus, kwa sauti ya upole kama vile hakuna kitu cha hatari mbele yao, “Deus, acha kuuliza maswali na ikiwezekana ufanye jambo tuondoke mahali hapa” alisema Sheba, huku anapeleka mkono chini ya seat yake.
Kabla Deus ajajibu kitu, tayari polisi mmoja alisha ufikia mlango wa dereva na kujaribu kufungua kitasa, lakini mlango haukufunguka, maana ulikuwa umefungwa kwa ndani, yule polisi akainua bunduki yake, akinyoosha usawa wa kioo cha mlango wa dereva, Deus akiwa anamtazama kwa umakini mkubwa, akamtazama mdomo wake ambao ulikuwa unatamka maneno ambayo yeye Deus, hakuyasikia, lakini niwazi alikuwa “anasema fungua mlango” hapo Deus, akafungua mkanda wa kiti na kutoa lock za milango, kisha akafungua mlango, ile anatokeza tu! akashikwa ukosi wa tisheti lake na kuvutwa nje, ukweli kutokana na uwezo alionao katika mazoezi, hakuyumba sana.


Lakini ile anakaa sawa, tayari Sheba alikuwa amesha toka ndani ya gari, sabamba na milipuko mfululizo ya risasi za bastora, kutahamaki tayari Sheba alikuwa amesha washusha askari wa nne, na kubakia wawili walio simama mmoja akiwa bila silaha yoyote na mwingine akiwa na SMG, karibu kabisa na Deus, lakini ile anainua tu, Deus akamuwahi haraka na kumpiga ngumi nzito ya kisogo, ambayo ilimpeleka chini kama mzigo na kumzimisha kabisa, huku yule mwingine akikimbilia kwenye gari, ambalo dereva alikuwa ndani yake, anajaribu kuwasha ili wakimbie, lakini kama vile amepungukiwa na akili, sheba akamimina risasi tatu, ambazo moja ilipiga kwenye bega la yule aliekuwa anakimbilia gari, huku moja ilipiga kwenye kioo cha gari, na kwenda kuchimba kwenye ubavu wa dereva, ambae tayari alikuwa amesha liwasha gari na kuingiza gia namba moja, ambapo kwa msukumo ule wa risasi, akajikuta akanakanyaga mafuta hovyo na kusonga mbele kwa fujo likiingia mtaroni na kushindwa kuendelea na safari, huku dereva aliekuwa anaugulia maumivu akiwa anajitaidi kujitoa kwenye gari.


“sipendi bunduki, hivi nani kakuambia utumie silaha muda huu?” aliuliza Deus, kwa sauti ambayo licha ya utulivu na utaratibu wake, lakini bado ilionyesha kuchukizwa na kitendo kile, “yaani watu saba, hii ni hatari sana tutalazimika kuwakimbia zaidi” alisema Deus akimtazama Sheba, ambae alikuwa anaichomeka bunduki yake kiunoni kwenye pindo ya suruali yake usawa wa kati ya makalio, “kwahiyo unadhani wangekuacha hawa, lazima wangetuuwa kisha kuondoka na gari letu” alijibu Sheba, huku anainama na kuokota mja kati ya SMG zilizoangushwa na wale polisi waliouwawa, “mh! kwanini watuuwe, nani kakuambia watatuuwa?, hebu ingia kwenye gari tuondoke hapa, kabla hatujakutwa” alisema Deus, huku anaingia kwenye gari.


Lakini sasa kabla hajafungu mlango akasikia mlipuko wa kwanza wa risasi, ile kutazama mbele yule jamaa aliekuwa anakimbia bila bunduki alikuwa hewani anaenda chini kama mzigo, huku damu nyungi sana zina vuja kichwani, ni wazi ilikuwa risasi iliyompata ilipiga kichwani, “we mwanamke acha upuuzi, huo ni sawa na ujambazi” alisema Deus, huku anashuka toka kwenye gari, macho yake yapo kwa Sheba, ambae alikuwa anaelekeza silaha kwenye gari la polisi, ambako yule dereva polisi, alikuwa anahangaika kushuka huku anaugulia risasi ya tumbo.


Fumba na kumbua, tayari risasi ilikuwa imesha toka kwenye mtutu wa SMG na kugonga kwenye kioo cha nyuma na kufanya kitawanyike, huku zikifuatia risasi nyingine tano mfurulizo, zilizo ambatana na milipuko yenye kelele mfano wa kiwanja cha majaribio ya shabaha, huku gari likiwa ndio ubao wa shabaha, risasi zilichakaza mwili wa yule askari, “sheba, unaniweka katika wakati mgumu, unadhani nitaishi vipi ndani ya nchi niliyo shiriki mauwaji ya wanausalama wake” alifoka Deus, huku anapokonya silaha toka kwa Sheba, “mbona mgumu kuelewa Deus, unadhani ni wanausalama hawa, hawa ni wanyang’anyi tu, wapo hapa kutuibia” alisema Sheba, huku anageuka na kurudi kwenye gari.


Wakati huo huo, yule askari alie pigwa ngumi ya kisogo, ndio alikuwa anazinduka, akanyoosha mkono taratibu kuchukuwa SMG, yake ili awatandike wakina Deus, lakini kwa bahati mbaya au nzuri Sheba akamuona, hapo haraka akachomoa bastora yake toka kiunoni na kumtandika yule jamaa, “pumbavu, ingia kwenye gari haraka” alisema Deus, huku anatupa ile SMG na kuanza kutembea kuelekea kwenye gari, “nakushauri uchome gari moto, ili kupoteza ushaidi” alisema Sheba, ambae sasa alikuwa anaingia ndani ya gari,


Hapo Deus akageuka kulitazama gari la polisi, halafu akamtazama Sheba, ambae pia alikuwa anamtazama, kisha akaanza kuziokota silaha zilizo kuwa zimezagaa pale chini na kuanza kuitupia ndani ya gari akibakiza moja tu.


Alipomaliza akarudi mita chache nyuma, toka lilipo gari la polisi halafu akaiweka SMG usawa wa bega na kulenga tank la mafuta*******


Wakati hayo yanaendelea, nje ya mji wa Mombo, wakati huo huo barabara hiyo hiyo, maeneo ya njia panda ya Sadan, lilionekana gari aina ya land rover diffender, mali ya jeshi la polisi, lenye askari saba nyuma yake, huku wawili yani Dereva na mwenzie mmoja wakiwa mbele, lilionekana liliembea kwa speed ya mia moja hamsini, kuelekea upande wa Mkata.


Ndani ya gari nyuma palionekana SMG nane zikiwa zimewekwa chini, yani kwenye sakafu ya gari lile ambalo lilibeba askari waliovalia nguo za kiraia pasipo kuzingatia unadhifu, wapo waliovaa tisht na jinsi, wapo waliovaa kodrai na shati za kadet, wengine walivalia kaptura za kaki, na makoti mafupi ya baridi, pia wengine walivalia kofia za sueta maarufu kama mzura.


Gari likukuwa linaenda kasi, ni kweli liilikuwa speed, japo kwa kuwa tumezowea speed ya BMW s7, tunaona kama vile gari hili halikuwa katika speed inayo paswa.


Hata walipo karibia Mkata, wakawaona polisi wenzao wakiwa wamesimama pembeni ya barabara pamoja na gari lao, wakionekana katika mshangao fulani, ni wazi muda mchache uliopita, walikuwa wameshuhudia kitu wasicho kitegemea, na wao hawakusimama, walipita na speed yao hiyo hiyo.
Hilo lilikuwa ni kundi la polisi wa Ulenje, walioongozwa na koplo Othman, wenyewe upenda kumwita Ochu, ambae mawazo na akili yake vilikuwa kwenye kulikamata gari aina BMW jeusi, ambalo aliamini kuwa muda wowote wanalifikia, hawakujuwa kuwa lilikuwa kilomita nyingi mbele yao na kila sekunde lilikuwa lina ongeza umbali katiyao.


Tukiachana na hao, tunaenda maeneo ya Msata, mita mia nne toka kwenye round about ya maungio ya barabara ya bagamoyo na chalinze, ambapo tunaweza kuliona gari kama lile la mbele, yani la polisi nalo likiwa na askari saba nyuma wawili mbele, likitembea kwa speed kuelekea upande wa Mkata, nalo pia lilikuwa katika speed kama ya lile la mwanzo, japo lenyewe lilikuwa lina fikia wakati lina vuka mpaka speed mia moja sitini.


Ili lilikuwa ni kundi la koplo Cheleji, ambae pia kama mwenzie akili na mawazo yake, yalikuwa juu ya kufanikisha kulikamata BMW, maana ukiachilia kujenga sifa na kuaminiwa na Ulenje, pia wangejipatia fedha nzuri sana, hawakujari wala kuwaza juu mwisho wa wale waliopo kwenye gari hilo, ambalo ingetakiwa warudi nalo dar, wao walicho jari nikutekeleza kile walicho tumwa, ambacho ni kuwauwa wote watakao kuwepo ndani ya gari na kurudi na gari na mzigo uliopo ndani yake.


Kwa kuweka kumbu kumbu sawa nikwamba, koplo Cheleji pekee ndie aliemuona Deus, akiingia kwenye gari, hivyo ndie mwenye kuweza kuitambua sura ya kijana huyo, japo haku fahamu wala kujuwa kuwa kijana yule aliemuona pale kiluvya madukani, akiingia kwenye gari lile BMW jeusi ndie askari aliekuwa anazungumziwa Mitandaoni…..…….ENDELEA kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom