Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Naam barabara ya bagamoyo, mtaa wa tegeta, njia pnda ya kwasharifu, linaonekana gari moja jeusi aina ya ford ranger likiwa limesimama pembeni ya barabara hiyo, huku mtu mmoja, mwenye mwonekano wa miaka 40, akiwa amesimama ubavuni mwa gari ilo, huku uso wake, ukionekana kujawa na mashaka mengi, mara kwa mara alikuwa anatazama saa yake, na kisha kutazama upande wa mjini, ni wazi alikuwa anatarajia kuona mtu au gari likitokea upande huo…..
“baba Zamda, umesema Zamda analetwa, sasa mbona simwoni mwanangu” ilikuwa ni sauti ya kike toka ndani yagari, iliyoambatana na kilio cha chini chini, “mama Zam we tulia, ata mimi nina wasi wasi juu ya binti yetu, lakini bosco, amesema yule kijana alie mpigia simu, lazima atarudi na Zamda, ilimradi tu tumkabidhi fedha yake” alisema yule mzee ambae sasa tuna gundua kuwa ndie mzee Simba, yani baba yake Zamda, “kwakweli baba Zamda kama mtoto hatorudi ninaenda kukutolea taarifa kituo cha polisi, na kwenye vyombo vya habari, ilimradi wewe na wenzako wote mkamatwe na mwangu nimpate, nilikuambia achana na hiyo biashra ya dawa za kulevya, tafuta biashara nyingine, lakini wewe hukunisikia” aliendela kulalamika mwanamke alie kuwa ndani yagari.


Hapo Mzee Simba akaachia msonyo mrefu, “lakini hizi fedha ndizo tulizo, mtibia mama yako, na hizi ndizo zinazotufanya tuishi vizuri, halafu nani kakuambia unaweza kuacha ghafla hivyo, unazani wangeniacha hai wakina Songoro?” aliuliza bwana Simba, kwa sauti ya ukali kidogo, na hapo akasikia sauti ya kilio kikiongezeka toka ndani yagari, “sijuwi mwanangu wanamfanyaje huk jamani” hakika ilitia huruma na kuchukiza kwa wakati mmoja.


Lakini kabla hata mzee Simba ajaongea neno lolote, mara wakaliona gari aina BMW 7, likija na kusimama karibu kabisa na gari lake, kisha milango miliwi ya gari ikafunguliwa, hapo mzee Simba akamwona binti yake akiwa anatoka kwenye gari, huku amevikwa shuka kwa mtindo wa kuviligwa mwilini mwake, “mwanangu upo salama kweli” aliuliza mzee Simba, huku anamtazama binti yake kwa macho ya ukaguzi, na swali ilo ndilo lilo mshtua mke wake, ambae alichomoka ndani gari kwa speed ya haraka, usingesema kuwa ndie alikuwa amezimia masaa kadhaa yaliyopita, “jamani mwanangu, hawajakuumiza kweli” alisema mama Zamda huku anamkumbatia binti yao, huku wote wakilia kwa furaha, muda wote kijana wetu derva ambae bado atuja mfahamu kwa jina, akiwatazama kwa macho ya kuvutiwa na tukio lile, “hapana mama, hawajanifanya chochote, dereva aliwai kabla ajanifanya” alisema Zamda huku wote wawili, yani yeye na mama yake wanageuka kumtazama kijana huyu mwenye sura ya upole, ambae mara baada ya macho yao kukutana anatabasamu kidogo.


Hapo Mzee Simba nae akakumbuka anachotakiwa kufanya, hivyo ana fungua mlango wa nyuma wa gari ili, na kutoa begi, “kijana kuna zaidi ya million hamsini, ni za kwako, sina muda wakusubiri wacha nikimbie mji” alisema mzee Simba, huku anampatia begi dereva, ambae alilipokea na pasipo kuongea neno, akalifungua lile begi na, kuchukuwa bunda moja la noti za elfu kumi kumi, na kukagua, kisha akapapasa mabunda mengine, alafu akamtazama mzee Simba, “sikunyingine tukutane kwa yale yaliyomema, siyo kuuza mtoto kwa dawa za kulevya, nitakuwa wa kwanza kukuadhibu” alisema Dereva kisha akamtazama Zamda ambae bado alikuwa ameshikana na mama yake wakimtazama, “nawatakia safari nje, kaeni mbali na watu wale” alisema Dereva kisha akaingia kwenye gari na kuondoka zake, huku akimwacha mzee samba na familia yake wakiingia ndani yagari na kuondoka zao pia, wakati Dereva anageuza gari kurudi mjini, mzee simba alikuwa anaelekea upande wa bagamoyo.*******


Msako ulishika kasi ndani ya jiji la dar es salaam, polisi walizagaa jiji zima, na vitongoji vyake, wakilisaka gari jeusi aina ya BMW, ambayo waliyaona mengi sana, lakini siyo kama lile lililotajwa, na hata dereva hakuwa kama yule waliyoelekezwa, maana pengine wangekuta BMW 3 au 1, tena anaendesha mtu mzima, au kijana mnene au mfupi, pengine mweupe sana, au mweusi sana, au wakati mwingine wange mkuta anaendesha mwanamke.


Lakini msako huo wenye faida kwa askari wajeshi la polisi, haukukoma, uliendelea kushika kasi, huku raia wazurulaji na wachelewaji wa kurudi nyumbani, wakikumbana na dhahama ya polisi hao, ambao walijipatia fedha toka kwa wazurulaji, ambao walilazimika kutoa chochote, ili wasipelekwe mahabusu, ambako kutoka kwake ni gharama kubwa zaidi, wakati huo taarifa zikizidi kusambaa kwenye kamandi nyingine za mikoa ya kipolisi ambayo iliundwa kwa mtindo wa kanda, katika pande kuu nne, yani kaskazini, kusini, mashariki na magharibi, yani pande za temeke, mbezi ya kimara, upende wa ilala, na upande wa mwenge mpaka tegeta.


Taarifa hizo zilifanya askari wengi zaidi waigie barabarani, na kuendeleza msako, wa BMW jeusi, huku wakielezwa kwamba, dereva wa gari ilo ni mtu hatari sana, na askari wanapaswa kuwa makini sana watakapo kabiliana nae, huku akitajiwa kuwa mtu hatari.*******


Usiku huo huo linaonekana gari aina ya Toyota Wish, likiingia Kinyerezi mwisho, kutokea mbezi, kupitia malamba mawili, linaishana na polisi wengi njiani, na linapofika stendi ya kinyerezi, lina ingia upande wa kushoto, na kufwata barabara ya vumbi inayopita chini ya nguzo kuu za umeme, mpaka linapofika mtaa mpya wa njia panda, ambapo linaenda moja kwa moja kwenye lango la uzio mkubwa wa kuta, wenye vitu mbali mbali vya usalama, yani waya wa umeme, na camera za ulinzi.


Licha ya kuwa na vitu vya usalama kama hivyo lakini inashangaza kuona lango la uzio huu likiwa wazi, pasipo mlinzi wala mtu yoyote, na cha kushangaza zaidi ungeweza kuona jumba kubwa la kifahari, ambalo kwa majumba ya kifamilia kwa hapa dar es salaam, ningeweza kusema ni moja kati ya majumba machache yanayoweza kumilikiwa na watu bnafsi, lakini hapa kuwa na umeme wala kandiri, kwa maana hiyo, palikuwa na giza nene la kutisha.


Gari linaingia ndani kwa mwendo wa taratibu sana, dereva akionekana kuwa katika umakini wa hali ya juu, na kwenda kusimama mbele ya jumba hilo la kifahari, huku taa za gari lile likimulika magari jumba lile, ambalo alikuonyesha dalili ya kuwepo kwa watu ndani.


Pasipo kuzima gari wala taa, mlango wa dereva unafunguliwa, kisha anashuka mwanamke mmoja mrembo sana, alie kuwa anaongea na simu, mwenye urefu wa wastani umbo la kuvutia, lenye kila kitu ambacho wanaume wengi utamani kuona kwa mwanamke, pengine ata wanawanawake wenye kutamani kuwa navyo, yani ukiachia sura nzuri aliyokuwa nayo maschana huyu, alie valia suruali nyeusi ya kitambaa chepesi, na shati fupi jeupe, chini akimaliza kwa kiatu cha mikanda chenye unyayo msawazisho yani flat, lakini pia alikuwa na umbo moja matata sana, yani hips pana za wastani, makalio yenye ukubwa wa wastani, na tumbo dogo, lililobebwa na kiuno uzuri cha kufaria nguo yoyote ikaonekana, kifua kilicho beba maziwa yaliyo chaa vyema, na chuchu za kutoboa sidilia, na mbaya zaidi ukiachilia usowake wa duara la yai, mcho makubwa kiasi, pua ya kisomari, lips pana za kulambia vanilla, pia alikuwa na kijimwanya flani, kwenye meno yake ya juu, na tatizo jingine, alikuwa anajisi sima flani kwenye mashavu yake, ambayo kuviona kwake ni mpaka acheke au atabasamu, na wakati mwingine akiwa anakula,


Mschana huyu anatazama ile nyumba kubwa ya kifahari kwa mshangao, huku simu yake bado ikiwa sikioni, “samahani J nitakupigia baadae maana hapa nyumbani hata sipaelewi, yani geti lipo wazi hakuna umeme, wala dalili ya kuwepo mtu” alisema yule mwanamke na kukata simu, kisha akapekuwa namba nyingine ambayo ilikuwa imeandikwa baba, anaipiga lakini haipatikani, ana piga nyingine iliyoandikwa mama, nayo haipatikani, ana jaribu ya dada wakazi, nayo ikaita bila kupokelewa, geukia gari na kuinama kwaajili ya kuchukuwa kitu flani ndani, hapo ungweza kuona jinsi msambwanda wake wakuvutia ulivyoonekana kwa nyuma.


Yule mschana anashika koti moja jeupe la kidoctor lililokuwepo kwenye seat ya gari, na kuanza kulipekuwa kidogo, lakini niwazi alikosa anachokiitaji, anahamia kwenye mkebe wa dash board na kuanza kupekuwa, hapo tunaweza kuona vitu kadhaa, kikiwepo kitambulisho, cha kazi, chenye jina la dr Veronica James Carvine, anapekuwa kwenye ule mkebe na kutoka na tochi ndogo, anajaribu kwa kuiwasha, inatoa mwanga wa kuridhisha, anatoka nakuegesha mlango wagari, ambalo bado lilikuwa linaendelea kuunguruma, yeye akaanza kuelekea kwenye jumba kubwa tena kwa mwendo wa tahadhari. endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa, jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Yule mschana anashika koti moja jeupe la kidoctor lililokuwepo kwenye seat ya gari, na kuanza kulipekuwa kidogo, lakini niwazi alikosa anachokiitaji, anaamia kwenye mkebe wa dash board na kuanza kupekuwa, hapo tunaweza kuona viu kadhaa, kikiwepo kitamburisho, cha kazi, chenye jina la dr Veronica James Carvine, anapekuwa kwenye ule mkene na kutoka na tochi ndogo, anajaribu kwa kuiwasha, inatoa mwanga wa kulizisha, anatoka nakuegesha mlango wagari, ambalo bado lilikuwa linaendelea kuunguruma, yeye akaanza kuelekea kwenye jumba kubwa tena kwa mwendo wa tahadhari. endelea……


Huku moyoni mwake akizidi kushikwa na uoga mkubwa, ukiachilia tabia yake ya kuogopa giza toka utotoni, pia mschana huyu Veronica, aliuunganisha tukio la kuwaona polisi wakizagaa mtaani, na mazingira aliyo yakuta pale nyumbani kwao.


Lakini baada ya kupiga hatua kadhaa, Veronica anakumbuka jambo, hivyo ana simama na kutazama upande wa kushoto wa jumba lile, macho yake yanakutana na magari sita yote ya kifahari, japo moja lilikuwa limefunikwa kwa turubai jeupe, lakini haimshangazi sana, maana licha ya kuyafahamu yale matano pia ni kawada kwa baba yake kununua gari lolote wakati wowote.


Veronica anayatazama kwa sekunde kadhaa magari yale, kama vile anatafakari jambo, kisha ana toa simu yake na kuipiga namba iliyoandikwa, J simu inaita mpaka inakatika bila kupokelewa, mpaka inapo katika, “jamani J si tumetoka kuogea sasahivi, sasa mbona hupokei simu?” alijisemea Veronica, kwa sauti ya chini, yenye wasi wasi mwingi sana, huku anapiga tena ile simu, ambayo ni kama mwanzo, inaita mpaka inakatika bila kupokelewa.*******


Mji wa Kisarawe mida hii ulikuwa umechangamka kiasi, ni wazi baadhi ya watu walisha elekea majumbani mwao, ndio wakati ambao lilionekana BMW 7 jeusi likikatiza taratibu sana eneo lile la mjini, kama vile dereva alikuwa anatazama jambo flani pale mtaani.


Lakini ukweli ni kwamba, dereva huyu, hakuwa anatazama kitu chochote, zaidi ya kumakinika na barabara, huku akifwata sheria ya speed hamsini kwa saa, kila unapo pita mjini, au kwenye kwenye kijiji, music laini ukisikika mle ndani ya gari, seat ya abiria wa mbele kukiwa na vijifuko kadhaa vilivyosheni vitu mbali mbali, chini ya seat hiyo sehemu ya kuwekea miguu, likioneana begi dogo.


Dereva huyu mwenye uso wa upole, aliekuwa anaendasha gari kwa mkono wa kushoto, huku mkono wa kulia ukiwa umekita kiwiko chake, kwenye mlango, wagari ilo, lililopandisha vioo vya giza mpaka juu, na kiganja chake cha mkono kikiwa usawa wa shavu na kidevu, kama vile ameshika tama, ni wazi, alionekana ku tuliza akili yake, na kuipeleka kwenye kumbu kumbu flani iliyo muumiza kichwa.


BMW 7 lina iacha njia panda ya kati kati ya mji, na kunyoosha kuelekea barabara inayoelekea mkoani, yani Kibaha, kwa mwendo ule ule, wa taratibu, ungesema kuwa huo ndio mwendo ambao, gari hili linge tembea nao, mpaka mwisho wa safari, kama linavyoonkana, likitembea kuelekea nje ya mji.


Naam wakati dereva wetu anamaliza mji, na kukanyaga clutch kwaajili ya kupachika gia, mara anasikia simu yake ikianza kuita, niile simu ya kawaida simu ambayo anawasiliana kwa mambo ya kawaida, yani ile ambayo alikuwa anachart na mtu alie mwandika Pacha, dereva anatabasamu kidogo, tayari kisha nimiss kumbe bado tu hajaacha mambo yake, nilidhani atakuwa amesha pata mwanaume wakumliwaza” alijisema Dereva huku anagairi kuongeza gia na kutafuta sehemu ya kuegesha gari, ili apokee simu ile na ukichukulia alikuwa amesha uacha mji huu wa kisarawe.


Jambo ambalo Kijana huyu hakujuwa ni kwamba, kuna vijana wanne waolikuwa wamesimama pembeni ya banda moja la biashara, na pikipiki zao mbili, wakiachia tabasamu zao katika nyuso zao ngumu, nibaada ya kuliona BMW 7 la kisasa lenye kutunzwa vizuri, likisimama mita chache toka mwishoni mwa mji huu mdogo wa kisarawe.*******


Turudi kwa Doctor Veronica, ambae baada ya kuwakosa watu ambao wange mfanunulia juu ya ukimya na hali aliyoikuta pale nyumbani kwao, mara anapata wazo jingine, anapiga namba nyingine, iliyoandikwa mchoraji, na kuipiga, nayo inachukuwa muda kidogo bila kupokelewa, anapati wasi wasi, ni wazi namba hii huwa haiachwi kupokelewa labda isiwe hewani kabisa, kama ilivyo kuwa kwa mezi zaidi ya mitatu iliyo pita, ambapo ilipotea kabisa hewani, na kama haikupokelewa lazima ingepokelewa, tofauti na namba ya mchumba wake kijana John Joseph Daud, ambae siyo mara moja au mbili, amekuwa akiacha kupokea simu yake kutokana na ubusy wa kazi, na asikumbuke kupiga mara anapopata nafasi, jambo ambalo lilisha wahi kuwa gombanisha mara kadhaa, jambo ambalo lime fanya mambo kuwa magumu sana katika mahusiano yao mapya.


Kama alivyo tegemea Veronica, simu inapokelewa, hapo Veronica anashusha pumzi nzito, “niambie wangu dakika chache hizi tayari umesha nimiss, si nilikuambia nitakupigia nikifika nyumbani” ilisikika sauti tulivu ya kiume toka upande wapili wasimu, yenye utani kiasi flani, “sikia, hii siyo utani, mwenzio kuna kitu sikielewi hapa nyumbani…” alisema Veronica kwa sauti ya chini yenye dalili zote za uoga, lakini kabla hajamaliza tayari ilishakakatizwa na upande wapili, “sasa unadhani mimi nitayaelewa hayo mazingira ya nyumbani kwenu, ikiwa hata sijuwi unaishi wapi?” iliuliza sauti upande wapili wasimu, “sikia bwana, mala zote umekuwa ukinisaidia japo hatujawai kukutana wala kuonana, naamini na leo utanisaidia japo kwa ushauri, si unakumbuka ahadi yako” alisema yule mwanamke ambae ndie doctor Veronica James, kwa sauti ya chini ya yenye uoga mwingi.


“yah lakini ahadi yangu haikusema kuhusu ushauri wa mapenzi” iliongea ile sauti ya kiume kwa utani, “unaweza kuacha utani, ukanisikiliza kidogo mchoraji?” aliongea Veronica, kwa sauti iliyo onyesha msisitizo, “ok! nakusikiliza” ilisikika ile sauti ya kiume ambayo ilisikika sambamba na music laini ulio pigwa kwa sauti ya chini, “mwenzio nimefika nyumbani, lakini sioni dalili ya mtu yoyote, halafu kuna giza mpaka naogopa kusogelea nyumba yenyewe” alieleza doctor Veronica, kwa sauti iliyoonyesha uoga na wasi wasi.


Lakini kitu cha ajabu, ndio kwanza akasikia kicheko toka kwa mtu aliempigia simu, “he! unacheka tena baada ya kunishauri cha kufanya?” aliuliza Veronica kwa mshangao, na kuchukia, “tatizo lako upo kama kuku, yaani umeshasahau kuwa leo ni birth day yako, hiyo ni surprise mama” alisema yule mwanaume, upande wapili wa simu, na hapo Veronica akaachia tabasamu laini, lililofanya dmples zake zionekane, nakuazidi kuonyesha uzuri wake, “una akili nyingi sana mchoraji wangu, sijawai kujuta kukufahamu, yani nilikonda ulipotoweka hewani, safari hii, huwezi kunikwepa lazima nikuone” alisema Veronica, kwa sauti iliyoanza kuchangamka.


Upande wapili kikasikika kicheko, cha taratibu, “nenda kasherehekee huko, shemeji anakusubiri” ilikuwa ni sauti tulivu iliyoambatana na kile kicheko, cha taratibu, “hayo mengine haya kuhusu, ngoja niwafanyie surprise wao wenyewe, usiache kunichek ukifika nyumbani” alisema Veronica kwa sauti ya chini, na kukata simu, kisha akaanza kutembea kwa haraka na kujiamini, kuufwata mlango wa jumba lile kubwa.


Naam hatua ya kwanza, yapili ya tatu, mala ghafla umeme ukawaka, na kuangaza eneo kubwa lote la nje, na kumshtua sana Veronica, ambae kabla hajakaa sawa, anasikia kelele za shangwe toka upande wa kulia wa jumba lao, “surpriseeee” Veronica anatazama upande ule uliotokea kelele, “akawaona watu kama kumi hivi anao wafahamu, wakiwa wamependeza sana kwa mavazi yao, wakiwepo rafiki zake wachache, wazazi wake yani mama baba na wadogo zake wawili, pia alikuwepo John Joseph, ambae ni mpenzi wake,


Wote walionekana kuwa katika nyuso za furaha, huku wakiwa wamesimama kwenye eneo lililopambwa kwa mapambo mbali mbali maalumu kwaajili ya sherehe, kama vile Maputo ya rangi mbali mbali, huku meza moja kubwa ikionekana kujawa na vyakula vya aina mbali mbali, na pembeni yake kukiwa na meza nyingine ndogo yenye keki moja kubwa ya pink.


Japo mschana huyu mrembo Veronica, alijuwa kuwa hii ni surprise kama alivyo julishwa na mchoraji, lakini alishtuka kwa furaha isiyo na kifani, na kujikuta akishika midomo yake kwa aliyo iachamisha kwa staajabiko la furaha, tofauti na vile alivyo panga kuwastua wenyewe, maana ukiachilia kuwaona wazazi na marafiki zake pamoja na wadogo zake, pia alishangaa zaidi kumwona mpenzi wake John Joseph, aliezowea kumwita kwakifupi J, akiwepo pale nyumbani kwao.


Siyo tu kuhusu simu aliyotoka kuongea nae, akimweleza kuwa yupo ofisini, ila pia, ni ratiba ngumu ya kijana huyo hasa mida ya jioni, ukweli sikuzote kijana huyo ambae amekutana nae miezi michache iliyopita, utumia jioni kufanya kazi, hakika kumwona hapa leo mida kama hii, ni jambo la furaha sana kwake, ilionyeshakuwa ammpa umuhimu mkubwa sana, kwa kuacha shughuli zake za ofisi na kuja kuungana nae katika sherehe hii


Jambo lingine ni kwamba, licha ya kijana huyu, alielelewa na mjomba wake, baada ya kupoteza wazazi wake, kutambulishwa kwa wazazi wa Veronica, na kuanza taratibu za kuharalisha penzi lao kwaajili ya kuoana, lakini ukweli ni kwamba John au J, hakuwa na mazowea ya kuja hapa nyumbani,


“hongera Vero kwa kwa kutimiza miaka 25” alikuwa ni mama yake Veronica, alie sema hivyo huku anamkumbatia Veronica, wadogo zake wawili wakike wakisubiri pembeni yao, huku baba na marafiki wengine wakiwa wamewazunguka, wanapiga makofi, ya kuwashangilia, “asante mama” alisema Veronica huku anaachia tabasamu mwanana na furaha sambamba na machozi ya furaha.


Wakiwa bado wamekumbatiana, mama yake akasogeza mdomo wake sikioni kwa Veronica, “tumekuandalia zawadi, ya nyumba na gari jipya range rove, hiyo hongera kwa kujitunza mpaka umri huo, pasipo kukutana na mwanaume, siyo tu umetunza heshima yetu, pia umedumisha mila ya nchini kwetu #Mbogo_land” alisema mama Vero, hapo veronica akainua usowake kumtazama baba yake, ambae alikuwa ameshika funguo mbili, moja ya nyumba na nyingine ya gari.


Mzee huyu mwenye mwili wa kawaida ambao uwezi kudhania kuwa ni tajiri mkubwa sana, anatanua mikono yake kwaajili ya kumkumbatia binti yake, ambae anamwacha mama yake na kumkumbatia baba yake, “asante sana baba” anasema Veronica, kwa sauti iliyojawa na furaha kiasi cha kububujisha machozi, machoni mwake, “ni jukumu langu mwanangu, angalia kule kwenye park” alisema mzee James, tajiri mkubwa mwenye asiri ya watu wa #mbogo_land, huku anatazama kule kwenye magari.


Siyo Veronica pekee alie tazama upande ule, ata watu wengine waliokuwepo eneo lile, pia walitazama kule ambako mzee James alimwelekeza binti yake atazame, ambako kwa msaada wa taa za pale nje, ambazo sasa zilikuwa zimesha washwa, wote kwa pamoja waliweza kumwona mtu mmoja alie valia sare za kampuni moja ya ulinzi, akifunua gari lililokuwa limefunikwa canop jeupe.


Hakika Veronica alishindwa kujizuwia, baada ya kuliona gari aina ya Range Rover rangi ya dhahabu, jipya kabisaaaaa, aliruka juu na kumgeukia tena baba yake kisha akamkumbatia kwa furaha, asante sana baba na mama” alisema Veronica kwa furaha, kabla jamwachia baba na kumrudia mama, na kwenda kumkumbatia kwa mara nyingine.


Naam wakati Veronica anamkumbatia mama yake, ndio wakati ambao, mzee James akasikia simu yake ikiita, mzee huyu tajiri asie na utamaduni wa kudharau simu, akaitoa mara moja na kutazama jina la mpigaji.


Hapo mzee James anaonekana kushtuka vibaya sana, anaikodolea simu kwa sekunde kadhaa, huku anajiuliza jambo, licha ya namba iliyompigia kutokuwa ngeni, lakini huyu alie mpigia alikuwa anaitaji nini kwake, “ Chitopelah kwanini ampigie usiku kama huu?” alijiuliza bwana Jemes, ambae mshtuko wake unaonekana wazi kabisa usoni mwake…#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Hapo mzee James anaonekana kushtuka vibaya sana, anaikodolea simu kwa sekunde kadhaa, huku anajiuliza jambo, licha ya namba iliyompigia kutokuwa ngeni, lakini huyu alie mpigia alikuwa anaitaji nini kwake, “ Chitopelah kwanini ampigie usiku kama huu?” alijiuliza bwana Jemes, ambae mshtuko wake unaonekana wazi kabisa usoni mwake…endelea…..


Mara nikama mzee huyu anagutuka, na kutazama watu wapembeni, kuona kama kuna mtu yoyote alie kuwa ameuona mshtuko wake, kila mmoja anaonekana kuwa busy na tukio la birth day, labda kijana John pekee, ambae alikutana macho na mzee James, yaani baba mkwe wake, ambae hakumjari sana, baada yake anamsogelea mke wake na kumnong’oneza jambo, kisha anaelekea upande wa ndani ya jumba ili la kifahari, huku kijana John Joseph, ambae kwasasa tuta mwita JJD, akimsindikiza kwa macho, mkwe wake mtarajiwa.********


Naam saa tano na za usiku, maeneo ya mjimwema Kigamboni, gari mbili za polisi zilikuwa zinaondoka kwa kasi kuekelea upande wa kongowe mbagala, zikiwa zimebeba watu waliojeluhiwa vibaya sana, huku CP Ulenje akisisitiza kuhusu usiri wa safari hiyo ya kuwapeleka watu hao, kwenye hospital ya siri, ambayo imekuwa ikitoa matibabu ya siri, kwa vijana wa bwana Songoro.


Baada ya magari kutoweka CP Ulenje akageuka na kumtazama Songoro, “sasa kaka wacha mimi nikasimamie msako wa huyo mpuuzi” alisema Ulenje, huku anatazama saa mkononi mwake, “sawa bwana Ulenje, we nenda mimi naanda posho kwa askari wako, pia natakiwa kuwasiliana na Eze naamini atanipatia vijana ambao watanisaidia kwa siku mbili tatu, kabla wa wengine hawakaa sawa” alisema Songoro, huku anatoa simu mfukoni mwake, na kuanza kuibofya akielekea ndani, yule mwanamke akimfwata nyuma yake kuingia nndani ya jumba lile.


Ulenje na askari wake, wakaingia kwenye magari, na kuelekea kivukoni, wakiwaacha Songoro na yule na yule mwanamke wakipotelea ndani, huku Songoro akipiga simu na kuiweka sikioni.


Yap! mwishoni mwa mji wa kisarawe, wanaonekana vijana wanne waliovalia makoti meusi, na kukaa kama vile wameifadhi vitu flani mle ndani ya makoti yao, ya baridi, japo kulikuwa na joto, wakiwa wamesimama pembeni ya piki piki mbili, wakilitazama gari dogo jeusi aina ya BMW 7, gari la kisasa kabisa, ambalo kwa hapa Tanzania yalikuwa machache sana, lililosimama mita kama mia mbili toka pale walipokwepo wao, huku wakivuta kitu mfano wa sigara lakini haikuwa na kishungi, ungesema tubambu la kienyeji, lakini harufu yake, ndiyo ambayo ingekufanya kupigane na mawazo yako.


“oya bro tuna subiri nini, twendeni tuka chukuwe chuma ile” alisema mwenzao huku anaingiza mkono wa kulia kwenye mfuko wa koti lake la baridi, “tulia dogo, pale ni karibu sana, tuta msubiri hapo chini kwenye kona, tunaweza kukinukisha, halafu polisi wakatuotea” alisema mmoja wao, huku anapokea ile tumbaku yenye harufu kali, toka kwa mwenzie na kuiweka mdomoni, ambako anaivuta pafu moja na nakutoa moshi huku macho yake yanamtazama yule kijana alie mwita dogo, “lakini kwani wao hawajuwi michongo yetu, isitoshe mpaka wajipange waje kwenye tukio, sisi tumesha kiamsha, na ukichukulia lile gari linakimbia sana” alisema yule kijana huku anatoa mkono wake toka ndani ya koti, uliokuwa umekumbatia bastora, ambayo anaikoki na kuirudisha mfukoni, “ok! twendeni kazini, hakuna kushangaa kazi moja nzuri tunatoweka” alisema yule jamaa alievuta mara ya mwisho, kisha na yeye akaingiza mkono wake kwenye mfuko wakoti na kuibuka na bastora ambayo aliikoki na kubaki nayo mkononi.


Wakati huo wale wengine wawili wakiwasha pikipiki zao na kupanda juu yake, wakifwatiwa na wale wengine wawili, kisha wakaondoka kuelekea kule liliko gari aina ya BMW 7, “leo mwisho wake umefika, atajuta kutumia hii barabara huyu mpuuzi” alisema mmoja wao, ni yule aliembeba huyu alieonekana mwenye amri juu yao, kwamba ndie kiongozi wao, “tena hili jamaa ameahidi mkwanja mrefu sana” alisema yule kiongozi wao, wakati huo walikuwa tayari wamesha lifikia gari lile na kusimama ghafla mbela yake, huku waliokaa nyuma wakishuka haraka na kuwa milango ya gari, mmoja akiwa wa dereva na mwingine wa abiria, wa nyuma, na kushika vitasa vya gari lile wakinyonga kwa kujalibu kufungua.


Lakini milango ikawa migumu, kufunguka ikionyesha kuwa milango gari lile ambalo bado lilikuwa lina unguruma, na kuacha mwanga afifu wa taa za mbele, ilikuwa imefungwa kwa ndani, kwa kuligundua hilo, haraka sana, yule kiongozi akakimbilia mbele ya gari, akiwa na bastora yake mkononi, “fungua mlango vinginevyo napasua kichwa chako” alisema yule jamaa huku anainua bastora yake na kuonyeshea kwenye kioo usawa wa kiti cha dereva, hapo hapo wakasikia mlango wa dereva ukifunguliwa, “nachukia bunduki, unaweza kuacha kuionyesha kwangu” ilisikika sauti ya taratibu ya kiume, huku mlango ukizidi kufunguliwa, “acha ujinga achia gari, na ukileta ubishi risasi zote zilizopo humu zitaishia mwilini mwako” alisema yule kijana alie kuwa mbele ya gari, na wakati huo, yule kijana mwingine mdogo, aliekuwa mlango wa nyuma, akawahi na kwenye mlango wa dereva na akiwa na bastora yake mkononi.*******


Naam, sasa twendeni #mbogo_land, mashariki mwa TT City, yani jiji la Treanch Town, mtaa Shining stone, mtaa tulivu wenye majengo makubwa sana ya kifahari, ambayo nje yake, yanaonekana magari yakifahari, huku katikati ya mtaa huo wenye nyumba ishirini, kukiwa na uwanja mdogo uliojengwa kwa zege, wenye alama ya H, iliyomaanisha helpad, yani eneo la kutuwa helicopter.


Mtaa huu tulivu uliomulikwa na taa kila kona kiasi cha kukusahaulisha kuwa ni usiku, ni mtaa unaokaliwa na viongozi wakuu wa serikali ya kifalme ya nchi hii ndogo na tajiri, wengi wao wakiwa mawaziri.


Tuachane na fahari za mtaa huu, twende kwenye moja kati ya majumba ya mtaa huu, jumba linalokaliwa na waziri wa ulinzi wa nchi wa hii, MHE Dickson Chitopelah, ambae mida hii alikuwa ndani ya ofisi yake ndogo, iliyopo ndani ya jumba lile la kifahari, “nashukuru umepokea simu yangu bwana James, maana ni muhimu na yenye faida kwako” alisema mzee huyu, ambae kiukweli ndani ya nyumba ile hakukuwa na miwngine aliekuwa macho zaidi yake, “ukweli hata mimi nimeshangaa, zaidi ya shutuma zote mlizo nipatia wakati ule, nakunifanya niikimbie nchi yangu, leo hii unanipigia, bila shaka utakuwa na habari njema baada ya kuthibitisha kuwa shutuma hazikuwa za kweli” ilisikika sauti ya bwana James tajiri mkubwa ukanda wa afrika mashariki kusini na kati.


Hapo kikasikika kicheko cha kifahari, na kujiachia toka kwa bwana Chitopelah, “bwana James usitegemee kitu kama hicho, yaani baraza zima lime kuwa gumu kukubari kuwa wewe na wenzako hamjausika na kikundi cha HUD (yani Harakati za Uhuru kwa Damu) ukweli hata mimi imeniuma sana, yani nime jaribu sana kukutetea, hata hivyo sijapiga simu ili kuzungumza jambo hilo, nimekupigia ili tuongee kuhusu biashara” alisema Chitopeah, ambae ni waziri wa ulinzi wa #mbogo-land.


Hapo kikasikika kicheko cha furaha na raha toka upande wapili wa simu, yaani kwa bwana James Carvin, “itakuwa safi sana nikipata mshirika wa kibiasha huko mbogo land, maana itakuwa ni nafsi ya kujisafisha, na kurudisha imani kwa Mfalme, na pengine kunisamehe kabisa japo sikutenda kosa” alisema bwana James, kwa sauti iliyojaa furaha.


Hapo ungemwona Chitopelah, akijitabasamulia kimya kimya, “kuna ziadi ya ilo bwana James, chakufanya kesho kutakuwa na mkutano wa biashara, sito kuwepo ila kuna kijana naomba ukutane nae, yeye anampango wangu wa kibiashara, nimuhimu sana wewe ukimsikiliza, na kukubaliana nae, maana yeye anasimama baada yangu, na kila atakachosema nimesema mimi, eneo ni SistaFada Hotel shekilango Dar es salaam, muda ni saa mbili usiku, kikao cha kwanza kitakuwa cha siri, hakikisha unaenda mwenyewe kikaoni” alisema Chitopelah na kumfanya mzee James azidi kuachia kicheko cha furaha, “sawa mheshimiwa, hakuna tatizo, nitafanya kama ulivyoagiza, hii inaweza kuwa safari mpya ya matumaini mapya, maana licha ya utajiri nilionao, bado nina tamani sana kurudi nchini mwangu” alisema bwana James, kwa sauti iliyochangamka kabla hawajakata simu.


Baada ya kukata simu, Mhe Chitopelah aliachia tabasamu pana sana, tena ni tabasamu la ushindi, “mambo yanaenda kukaa sawa, ninaenda kuwa mtu mkubwa sana na tajiri mkubwa duniani” alisema Chitopelah, huku anainuka toka kwenye kiti cha ofisi, na kutoka nje ya ofisi yake.


Huyo ni bwana Dickson Chitopelah, ambae aliwahi kuwa askari wa jeshi la Mbogo Land, ambalo linajulikana kwa jina la ML ARMY, akifika mpaka cheo cha kanari, ambapo aliteuliwa kuwa msimamizi mkuu, wa walinzi wa mfalme Eric wa pili, baba yake mfalme Elvis wa pili, na sasa King Elvis amemteuwa kuwa ni waziri wa ulinzi, kutokana na uaminifu aliojijengea kwa mfalme huyo.********


Naam hapo yule kijana mdogo akamwona dereva, ambae ni kijana mwenye uso wa upole, aliekuwa anamtazama kwa macho yaliyojawa na huruma, “oyaaaa! usinitazame kwa macho ya huruma, hebu shuka haraka” alisema yule kijana mdogo, huku akinyoosha mkono wake wenye bastora kichwani kwa yule kijana, wakati huo yule alie simama mbele ya gari akilifwata gari, na wale wengine wawili wakirudi kwenye piki piki zao wakijuwa kuwa tayari kazi imeisha, “kwanini uelewi dogo” ilikuwa ni sauti kali yenye kuchukia toka kwa yule dereva wa BMW 7, ambayo ilienda sambamba na kitendo cha kuchomoka kwa ghafla toka kwenye gari, huku bwana dogo anashuhudia ngumi mbili zikija usoni kwake, kwa kasi ya umeme, huku moja ikija, na kutua, usawa wa mgongo wa pua yake, huku nyingine ikikita shingoni, na kumfanya yule bwana mdogo atupwe mita kadhaa nyuma, na katika hali ya kuanguka akajikuta akiminya trigger ya bastora yake na kusababisha kutoka kwa risasi moja, iliyoenda hewani na kuwafanya wenzake watoe macho kwa mshangao, huku yeye mwenyewe akijipiga kwanguvu chini na bastoora ikimtoa mkononi mwake na kuangukia pembeni.


Hapo yule aliekuwa analisogelea gari, akajuwa kuwa, tayari mambo yamesha haribika na kinachotakiwa ni kumpiga risasi dereva, kisha waondoke na gari haraka, lakini ile anajiandaa kuinua bastora yake, tayari dereva alikuwa mbele yake ameshika mkono wenye bastora, “nilisha sema sipendi bunduki husikiii?” alisema dereva sambamba na kumi nzito kidevu, hapo tayari vijana hawa wakajuwa kuwa wanapambana na mtu hatari, hivyo wanatakiwa kufanya jambo la haraka ili wafanikishe malengo yao.


Hapo sasa wakati huyu alieshikwa mkono, akisikilizia ngumi nzito ya chini ya kidevu, kwenye ngumi za kulipa wanaita upper cut, waswahili wanaita, ngumi funua, wale wawili walishuka toka kwenye piki piki zao, na kutoa vipande vya magongo kwenye makoti yao, na kumsogelea kwa haraka dereva, wakati huo yule dogo akiwa anajaribu kujiinua lakini anajikuta anarudi chini, kwa kizungu zungu kikukali kilicho mwandama, hivyo anatulia chini, na kuanza kupapasa bastora yake ambayo ilipo achia risasi pia ilimtoka mkononi, na anapoikosa anatulia na kutazama kule walikokuwepo wenzake.


Huko anachokiona kinamfanya ajute kuzaliwa jambazi, maana kwanza kabisa aliwaona wale wenzake wawili wanamfwata dereva ambae alikuwa amemshika yule mkubwa wao na kumnyang’anya bastora, ambayo aliitupa chini, kijana mdogo anawaona wale wawili, wanamfikia dereva na wote kwa pamoja wanainua yale marungu yao juu, na kuya shusha kwanguvu, kuelekea kichwani kwa dereva, ambae kwa haraka sana, anakwepa yale marungu, huku akimvuta yule mwenzao, kwanguvu, na kusabaisha yale marungu yanatua kichwani kwa mwenzao.


Siyo dogo peke yake anaeshangaa, hata wale waliotekeleza shambulio wanashangaa kilicho tokea, na hilo ndilo kosa ambalo wanalifanya, maana wakati wanashangaa, tukio lile na kumtazama mwenzao aliekuwa anaenda chini kama mzigo, dogo anashuhudia kitendo cha haraka sana, yule jamaa anarusha ngumi kama tano mfurulizo, kuelekea usoni kwa mmoja kati ya wale vijana wawili, huku ngumi ya sita ikielekea shingoni kwa yule mwingine, na wote wanaenda chini, kama vifurushi, lakini katika hali ya kushangaza, yule kiongozi wao, akiwa pale chini anaiokota bastora na kuielekeza kwa yule dereva, ambae anaichukua na kukuta kifuniko cha mitambo ya bastora ile, wenyewe wanaita reciver cover, kitendo kinacho sababisha spring ishindwe kukaa sehemu yake na kuchomoka huku ikifwatiwa na postone, inayojitoa kwenye slide base yake, hata huyu mwamba anapo minya trigger hammer inagonga hewani, maana firing pin imeondoka na breach.


Wakati wanashangaa hilo na kujuwa kuwa huyu kijana mwenye sura ya upole ambae walimviazia kwa muda mrefu, wampole gari lake la kisasa, ni mtu hatari sana, tena zaidi ya walivyo mfikilia hapo mwanzo, ndipo walipo staajabu, maana kuna kushangaa na kustaajabu.


Maana wakati mitambo ya bastora ikitawanyika kwenye ile bastora ya kiogozi wao, ghafla kijana huyu alie kuwa ameshikilia kile kibati ambacho ni kifuniko cha mitambo, akakizamisha kwanguvu shingoni mwa yule mkubwa wao, na kusababisha damu zivuje kwa fujo, huku mtu yule akitapa tapa kama kuku aliechinjwa, kuona hivyo wale jamaa wakaona hii sehemu haikuwafaa tena, ni vyema kama wange kimbia.


Lakini ile wanainuka tu, tayari kijana wetu, yaani dereva alisha kanyaga gongo moja kati ya mawili ya wale vijana, na kulibetua kama vile cheza mpira, na kulifanya liruke juu, kisha akalidaka na kulishusha kichwani kwa mmoja wao, alie achia ukelele wa “chwiiiii” kama kitimoto, alie kutana na rungu la mtu ambae sijuwi nimwite nani, mchinjaji au muuwaji, “wajinga, nimesema, sipendi, bunduki” ilisema yule kijana, kwa kituo uku kila neno likienda sambamba napigo la rungu, akiwatandika vijana awa wawili, ambao kiukweli hakuwaacha mpaka alipohakikisha wamegeuka sakafu ya bucha….…#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE: Lakini ile wanainuka tu, tayari kijana wetu, yani dereva alisha kanyaga gongo moja kati ya mawili ya wale vijana, na kulibetua kama vile cheza mpira, na kulifanya liruke juu, kisha akalidaka na kulishusha kichwani kwa mmoja wao, alie achia ukelele wa “chwiiiii” kama kiti moto, alie kutana na rungu la mtu ambae sijuwi nimwite nani, mchinjaji au muuwaji, “wajinga, nimesema, sipendi, bunduki” alisema yule kijana, kwa kituo huku kila neno likienda sambamba napigo la rungu, akiwatandika vijana hawa wawili, ambao kiukweli akuwaacha mpaka alipohakikisha wamegeuka sakafu ya bucha….…endelea….


Naam yule kijana mdogo, alie shuhudia wale wanzake wakiuwawa kinyama, sasa alimwona yule jamaa, yani dereva anatembea taratibu, kuja upande ambao yeye alikuwa amelala chini, kijana akaanza kupapasa kwa haraka kutafuta bastora yake, ambayo hakuwa na uhakika kama imeangukia eneo la karibu na pale alipokuwepo, lakini mpaka jamaa anamfikia, alikuwa bado hajaiona, hakuwa na lolote la kufanya zaidi ya kumtazama dereva kwa macho ya huruma, “dogo nadhani sasa umeelewa kwanini nilikuwa na kutazama kwa macho ya huruma. nilikuwa nahurumia kile ambacho umekiona kimetokea, lakini siyo mbaya, nakupa nafasi nyingine, rudi shuleni, achana na ujinga huu” alisema dereva, na wakati huo huo, wakasikia ngurumo ya gari likija upande ule, tena kwa speed ya hatari.******


Naam muda ulikuwa umezidi kusonga, jiji la dar es salaam lilionekana kuanza kutulia, hata watu walikuwa wanaonekana kwa uchache, kama ilivyokuwa kwa magari, baadhi ya kumbi za starehe zilikuwa zimesha fungwa, magari ya polisi na polisi wenyewe ndio walio onekana kutawala kila kona ya jiji, hasa mtaa huu wa kimara, ambao sasa tunaenda kuuangazia.


Tunaenda moja moja kimara mwisho, tukitokea mjini, yani upande wa ubungo, tunakata kona upande wa kulia, tunaacha upande wa DAWASCO, na kuelekea kichungwani, mita kama mia mbili toka njia panda, ya kichungwani, ndani ya uzio mkubwa wa jumba moja kubwa sana, la kifahari, alionekana watu sita wakiume, watano wakiwa ni wenye kujazia miili yao, iliyo jaa kimazoezi, wakiwa wamesimama mita kadhaa toka, aliposimama mzee mmoja mnene, mfupi, na mwenye sharubu kama pembe za zagamba (ng’ombe mkubwa wa kienyeji) aliekuwa anaongea na simu, “dah! umeanza kuzeeka bwana Songoro, yani mtu mmoja anakusumbua, imeanza lini hiyo tabia ya kukubali kusumbuliwa na mjinga mjinga mmoja?” aliuliza yule mzee kwa sauti ya mshangao, na yenye dharau.


Hiyo ilikuwa ni mara tu baada ya Songoro kumaliza kusimulia kulicho mtokea, “sikia bwana Eze, nisaidie hao vijana, maana mpaka sasa hapa nipo mwenyewe, tena waje sasa hivi” alisisitiza Songoro, “usijari kaka, umenitoa mbali sana, siwezi kukuacha peke yako, muda mfupi ujao vijana watakuwa hapo” alisema huyu mzee mfupi akijitaidi kumpa uhakika kwa bwana Songoro, “na kuaminia kaka, sasa nifanye utaratibu wa kuongeza vijana wengine” alisema Songoro na kisha akakata simu.


Mara tu baada ya kukata simu, hapo hapo bwana Ezekel Ndimbo anaanza kupekuwa kitabu cha majina cha simu yake, na kwa kuangalia simu zilizopigwa siku hiyo, na kubaini kuipata namba iliyoandikwa Mama P, anaipiga mara moja, ambapo simu inaita kwa sekunde chache na kupokelewa, “niambie baby, mbona usiku sana jamani” ilikuwa ni sauti ya chini ya taratibu iliyojaa uvivu, na uchovu wa usingizi, ni wazi alipokea simu ile ikiwa ni sekunde chache baada ya kuamka.


Hapo Eze anaonekana kuachia tabasamu pana, “hoooo mamaaa, mbona umelala mapema sana, leo ukutoka hata kidogo na rafiki zako?” aliuliza bwana Eze kwa sauti ya chini kidogo, ni kama hakutaka mtu flani asikie, “nitatoka na nani baby wakati mwenyewe, muda wote upo na mkeo” ilisikika sauti ile ya kivivu ya mwanamke, upande wa pili wa simu, “hapana mamaaa, ujuwe siku chache hizi nipo busy sana, ila siyo mbaya kesho jioni tutakutana napengine tulale pamoja, au unasemaje mamaa?” alisema Eze kwa sauti yachini yenye kubembeleza, “hooooo bahati mbaya baby, kesho kuna sehemu naenda, hatuwezi kuonana” alisema Mama P, kwa sauti ile ile ya kudeka.


Ukweli kauli hii nikama ilimshtua kidogo Ezekiel Ndimbo, ambae anageuka na kuwatazama wale, vijana walio simama mita adhaa pembeni yake, “unaenda wapi, inamaana hata ukirudi hatuwezi kuonana mpenzi?” aliuliza Eze, kwa sauti ya kubembeleza, “mhhhh! sizani baby, tufanye kesho kutwa bwana” alisema mama P, kwa sauti ya kubembeleza zaidi, “ok! hakuna shida, tuta wasiliana, basi” alisema Eze, kabla hawajagana na kukata simu, kisha Eze akatazama chini, huku uso wake umekunjika kwa mashaka juu ya mpenzi wake huyo, “mh! huyu mwanamke anataka kunichezea sasa” alisema Eze, huku anashika kiuno chake, kwa mikono yake miwili.


N wakati huo wale vijana watano baada ya kuona tayari boss wao amemaliza kuongea na simu, wakamsoglea pale alipokuwepo, na ndipo Eze aliekuwa katika mawazo mazito ya kushuku mama P kuwa anamsaliti, akagutuka, “Inno, piga simu kwa Side, mwambie achague watu kumi waende mji mwema kwa Songoro, watafanya kazi huko mpaka utaratibu mwingine utakapo fanyika” alisema Eze kwa sauti ambayo nikama ilikuwa imekosa amani, kwa safari ya ghafla ya mpenzi wake huyo, ambae kila anapokuwa na safari au dharura yoyote humjulisha mapema, na isitoshe yeye alikuwa na hamu, kubwa ya kunyanduana na mpenzi wake huyo, siku yakesho.


Inno, alitekeleza maagizo mara moja, na wakati anaendelea kuongea na Side, Eze akatoa maagizo kwa wale wengine, “kuna kazi nataka mnifanyie, nataka mumfwatilie mama P, kuanzia kesho asubuhi, mpaka usiku, asinifanye mjing…” kabla hajamaliza kuongea, mara ghafla mlango wa nyumba kubwa ukafunguliwa na kuwafanya wote washtuke, ungesema kuna boss mkubwa zaidi aliku anatarajiwa kutoka ndani ya jumba ile kubwa.


Lakini akatokea mama mmoja mrefu na mpana, “Eze, usiku sasa, nakutaka chumbani” ilikuwa sauti iliyojaa ukali, toka kwa huyo mama alie simama pale mlangoni, “nakuja mke wangu” alijibu mtu mfupi mnene mwenye sharubu yani bwana Eze Ndimbo, huku anatazama pembeni na kubetua midomo kwa chuki, kabla hajawageukia wakina Inno na kuagana nao, huku akiwasisitiza kuhusu kesho kumfwatilia mpenzi wake mama Space, au kama wanavyoita kwa kifupi mama P, kisha mtu mfupi huyu, akaondoka zake kuelekea kwenye jumba kubwa, ambako bado mke wake alikuwa anamsubiri mlangoni.


Kitu ninachokiona baada ya wiwili hawa kusogeleana, ni picha ya kushangaza sana, maana kiukweli, kimo cha Eze, kwa mke wake, kiliishia usawa wakifua cha mama huyu, nakutengeneza picha ya mama alie ongozana na mtoto wake kuingia ndani, siyo mimi tu, hata wakina Inno walichekea tumboni mara baada ya kuona walicho kiona, kwa boss wao na mke wake.*******


Nyumbani kwa tajiri mkubwa mwenye fedha na mali, viwanda na magari, bwana James Cervin, bado sherehe ndogo, ya maazimisho ya kutimiza miaka ishirini na tano binti yao mpendwa, doctor Veronica, ilikuwa inaendelea, sasa watu walikuwa wanapata vinywaji, huku kila mmoja kwa wakati wake, akimpatia hongera zake mschana mrembo Veronica, ambae sasa alikuwa amesimama pembeni kidogo na mpenzi wake yani mchumba wake, kama siyo mume mtarajiwa, kijana John Joseph Daud, ambae alijitambulisha kwa Veronica kuwa anafanya kazi idara ya ardhi.


Wawili hawa walionekana kuzama kwenye maongezi mazito, “lakini baby, si tumesha kubariana kuwa, ni mpaka tuowane” alisema Veronica kwa sauti ya chini yenye kubembembeleza, huku anachezea vidole vyake, “ndiyo tulikubariana hivyo, lakini Vero, ujuwe mwenzio ninapitia wakati mgumu sana, ungefanya lolote ambalo linaweza kunisaidia na mimi nipunguze kidogo” alisema JJ nae pia kwa sauti ya kubembeleza yenye kutia huruma, “J kwanini tusiharakishe kufunga ndoa, maana kinyume na hapo, nitakuwa nimewakosea sana wazazi wangu” alisema Veronica kwa sauti iliyojaribu kumshawishi kijana JJ, “sikia Vero, siyo lazima tufanye kabisa, lakini kuna njia nyingine tuna weza kutumia mpaka kila mmoja wetu akaridhika” alisema JJ, huku anapandisha mikono yake mabegani kwa Veronica, ambae aliinua uso wake na kumtazama JJ kwa macho ya mshangao, “mh! J, inawezekana vipi, au unamaanisha kujichua, hujuwi kama ni kitu hatari sana kwa afya yako?” aliuliza Veronica kwa sauti ya chini yenye kuonya, “hapa siyo hivyo, kuna michezo tutacheza sisi wawili, na mwisho wake tutajikuta tumelizika kabisaaaaa” alisema JJ, kwa sauti ya taratibu, huku anaramba ramba midomo yake.


Hakika kijana huyu, ni mtanashati, kuanzia mavazi ngozi ya mwili wake, hata mtindo wa unyoaji wa nywele na ndevu zake, pia uongeaji na mipozo yake wakati anaongea na vitendo vya taratibu, “mh! basi tutapanga siku, nione hiyo michezo” alisema Veronica, huku anapeleka mikono yake kifuani kwa mpenzi wake, “hoooo! tupange siku tena, mimi nilidhania kuwa tunajaribu leo?” aliuliza JJ kwa sauti ya kulalamika, “hapana J, haiwezi kuwa ghafla hii jamani, bora hata tukifanya kesho kutwa, kesho nitaaga kazini halafu keshotwa siku nzima ya kwako” alisema Veronica kwa sauti yenye kumbembeleza na kuomba J amwelewe.


Naam wakati wakiwa katika mjadara mzito, na wakati huo huo wakamwona baba yake Veronica akiwa anatokea upande wa nyumba kubwa, na kuelekea alikokuwepo mama Veronica, huku uso wake ukiwa ni wenye furaha kubwa, furaha ambayo anamshirikisha mama Veronica, baada ya kuanza kumweleza kilicho mfuraisha, JJ na Veronica wanaacha kuongelea mpago wao, wanamtazama mzee James, alie kuwa anaongea kwa furaha na mke wake, “baba sijuwi kafurahi nini” alisema Veronica, huku anacha kuwatazama wazazi wake, tofauti na JJ ambae alikuwa anaendelea kuwatazama, “baba yako ni mfanya biashara mwenye mafanikio, na sasa anaendelea kufurahia mafanikio yake” alisema JJ, huku anato simu mfukoni na kutazama muda, “saa sita hii, wacha niende nyumbani” alisema JJ, huku anaanza kutembea kuelekea kule waliko wazazi wa Veronica, huku Veronica mwenyewe akimfwata.


“jamani J, mbona imekuwa ghafla hivyo, au nimekuudhi?” aliuliza Veronica, kwa sauti yenye kutia huruma, “hapana Vero, ila si nilikuambia kuwa mjomba wangu ana sheria zake za kuingia pale nyumbani kwake, hasa linapokuja swala la kuchelewa” jibu la JJ, lilimfanya Veronica atabasamu kidogo, “usujari J, baba amenipatia nyumba, utaanza kuishi huko, wakati tunasuburi kufunga ndoa” tofauti na alivyotegema Vero kwamba JJ angefuraia habari ile, lakini ndiyo kwanza akazidi kutembea kwa haraka kuwasogelea wazazi wa Veronica.


Ukweli Veronica alishindwa kumwelewa JJ, aambae alitembea kwa haraka na mara baada ya kuwakaribia, akapunguza mwendo, na kutembea taratibu sana, huku wakiweza kuyanasa maongezi ya mama na baba Veronica, “huu ni mwanzo wa sisi kurudi nchini kwetu, Mheshimiwa lazima atasimamia ilo” alisema mzee James, kwa sauti iliyojaa furaha, “yani sipati picha, hata watoto wetu sasa watafaidi matunda ya nchi yao” alisema mama Veronica, ambae pia alijawa na furaha, kabla awajageuka na kuwatazama wakina Veronica waliokuwa wamesha wakaribia….…. …#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa Jamii Forums
 
Haya tuwe sambamba sasa hvi utaelewa nini kinaendelea
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Ukweli Veronica alishindwa kumwelewa JJ, aambae alitembea kwa haraka na mala baada ya kuwakaribia, akapunguza mwendo, na kutembea taratibu sana, huku wakiweza kuya nasa maongei ya mama na baba Veronica, “huu ni mwanzo wa sisi kurudi nchini kwetu, Mheshimiwa lazima atasimamia ilo” alisema mzee James, kwa sauti iliyojaa furaha, “yani sipati picha, ata watoto wetu sasa watafaidi matunda ya nchi yao” alisema mama Veronica, ambae pia alijawa na furaha, kabla hawajageuka na kuwatazama wakina Veronica waliokuwa wamesha wakaribia….….ENDELEA……


“Hoooo! John, vipi ndio unataka kuaga mwanangu” aliuliza mama Veronica, huku yeye na mume wake wakiwatazama watoto wao, “ndiyo mama naona muda umeenda sana, na kesho nahitajika kazini” alisema John Joseph, huku anaachia tabasamu usoni kwake, “ok sawa bwana John, karibu sana, karibu muda wowote, usiogope kuja hapa wewe sasa ni mwanafamilia pia” alisema mzee James, alie onyesha kujawa na furaha ya wazi kabisa, “asante mzee, nitakaribia” alijibu JJ, kabla ya kuaga kwa Vero na kuondoka zake, akaingia kwenye gari yake ndogo, aliyo iegesha nje ya uzio wa wakina Vero, na kuondoka zake, akiwaacha wazazi wa Veronica wanamsimulia binti yao mpango wa biashara mpya kati ya baba yake na waziri wa ulinzi wa #mbogo_land.********


Huko kisarawe mambo haya kuwa madogo, mara baada ya kusikia mlindimo wa risasi, polisi waliingia kwenye magari, na kuwahi mlio wa risasi ulikotokea, ambako ni upande wa barabara ya kuelekea kibaha mkoani, ambako walitembea mita kama miambili tu! toka nyumba ya mwisho ya kisarawe mjini, wakaona pikipiki mbili zikiwa zime simamishwa pembeni ya barabara, huku ikionekana miili ya watu watatu, iliyolala kwenye vijibwa vya damu, kando kando ya barabara, wakionekana mfano wa watu walipatwa na ajari kubwa, na mbaya ya gari.


Kuona hivyo polisi hawa wakasimamisha gari ambalo lilikuwa na polisi watatu nyuma yake, na wenye bunduki zao aina ya SMG zilizo tengenezwa mwaka 56, wakashuka toka nyuma yagari huku mmoja wao mwenye cheo cha sajent akishuka toka seat ya gari upande wa abiria, akimwacha dereva anageuza gari vizuri na kuangazia eneo lile kwa kutumia taa kali za gari.


Polisi walianza kuzunguka eneo lile kwa taadhari kubwa kuhakikisha usalama wao, huku buduki zao zikiwa mikononi tayari kwa lolote, ambalo lingetokea mahali pale, maana hali waliyo iona iliwashangaza na kuogofya.


Baada ya kuhakikisha hakuna kitu chochote kingine, wala mtu yoyote mwingine, zaidi ya wale walio lala pale chini, wanavuja damu, wawili wakasogelea miili ya watu watatu, walio kuwa wamelala chini kwa utulivu, huku askari wengine wawili wakigawana pande za ulinzi, kuhakikisha hakuna hatari itakayo watokea, “nani ameweza kuwa zibiti hawa jamaa” aliuliza kwa mshangao yule sajent baada ya kumtambua yule jamaa, alie chomwa na kibati cha bastora shingoni, ukiachia wale wengine, ambao walikuwa wamepondeka pondeka sura zao, kweli paka amenasa kwenye mtego wa panya” alisema mwingine, kabla yule sajent hajatoa maamuzi, “hakuna la ziada ni kubeba miili na kuipeleka hospital” alisema yule sajent huku anatoasimu na kupiga kwa OCD.


Simu sekunde kadhaa kabla ya kupokelewa, “habari za saa hizi afande” alisalimia yule sajent, mara tu baada ya simu kupokelewa, “safi sajent, vipi kuna lolote huko” iliuliza sauti iliyojawa na shauku ya kutaka kujuwa, toka upende wapili wa simu, “afande tumefika eneo la tukio, kuna watu watatu wameuwawa, ila ni waharifu tuliokuwa tuna watafuta kwa muda mrefu” alisema yule sajent, “umaanisha ni wakina Nondo?” aliuliza OCD kwa sauti iliyojaa mshangao, “ndiyo afande, lakini cha kushangaza ni kwamba, tumekuta bastora yao pamoja na marungu yaliyotumika kuwa shambulia, ila haijulikani wameuliwa na nani” alisema sajent akionekana kushangazwa na jambo lile lililo tokea, “hakika kila mti na shoka lake, haya wapelekeni hosptali wakaifadhiwe, na ukaandike riport, lakini hakikicheni mna fahamu alie fanya hivyo, ni wazo kuwa huyo ni mtu hatari zaidi ya wakina Nondo” alisema OCD, kabla ya kukata simu.


Wakati huo tayari askari walisha maliza kupakiza miili ya wale jamaa watatu, yaani wakina Nondo, na kuingia kwenye gari, kisha kuondoka zao, pasipo kujuwa kuwa, mita kadhaa ndani ya kile kichaka, yule kijana mdogo alikuwa anawatazama, huku anatetemeka sana kwa kile alicho kishuhudia kikiwatokea wenzake, toka kwa mtu yule, ambae siku zote walimchukulia kama mtu dhaifu, ambae wange mnyang’anya gari kirahisi kabisa, lakini kilicho watokea ni zaidi ya kukutana na simba au chui, au mbogo aliejeruiwa.*********


Naam saa sita na nusu usiku mita nne toka barabara ya kisarawe kwenda kibaha, eneo la tondoroni, kando kando ya barabara ya treni ya kati, BMW 7 linaonekana likisimama mbele ya nyumba moja ya tofari yenye ukubwa wa wastani, ambayo licha ya kujengwa kwa tofari za sement, lakini, ilikuwa haijamaliziwa kuwa katika hali ambayo mtu anaweza kishi, tunaitaga finishing, yani licha kuezekwa vizuri, lakini milinga na madirisha yalikuwa wazi karibu nyumba nzima, kasoro chumba kimoja tu, ambacho madirisha yake kwa nje yalionekana kuzibwa kwa vipande vya mabati chakavu, kama ilivyo kuwa kwenye mlango wa chumba hicho, ambao
ulionekana kuwa umechoka choka, lakini ilicho pendeza zaidi kwenye nyumba hii garge ya kulazia gari, ambayo ilikuwa imejengwa upande wa kulia wa jengo hilo. ikionekana ni madhubuti zaidi, kuliko hata nyumba yenyewe.


Utashangaa kuona jengo hili, lililopo eneo hili ambalo umeme ni kitenda wili, gate la kulazia gari lilijifungua lenyewe, ni wazi lilikuwa linatumia umeme, na gari linaingia ndani, kisha dakika chache baadae anaonakena dereva wetu akitokea mle ndani, ya lile banda, akiwa amebeba mifuko miwili, begi, na simu zake nne, akaingia kwenye ile nyumba ambayo haijamalizika, moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba chenye mlang wa bati lililochoka, anachukuwa funguo, toka mfukoni, na kufungua kufuri ambalo kiukweli hata sijuwi kwanini analiweka kwenye ule mlango dhaifu, ambao mtu akisukuma unangoka wote.


Dereva wetu ambae mpaka sasa hatuja mfahamu vizuri, wala kulijuwa jina lake, anapoingia ndani ya kibanda hicho kilichotawaliwa na giza nene, giza ambalo analiondoa kwa mwanga watochi ya simu, ambacho inafanya mle ndani muonekane vizuri.


Tunaona meza ndogo ya mbao, mita moja toka kwenye kitanda cha futi sita kwa mbili na nusu, kilicho tandika vizuri, hakika mle ndani hakukuwa na vitu vingi sana, zaidi ya meza na kitanda, kulikuwa na sanduku chakavu, na nguo chache zilizo tundukwa ukutani.


Kabla ujajiuliza kwa nini kijana mtanashati kama huyu, anae miliki gari lenye thamani ya nyumba nne kubwa za kisasa, anaishi maisha ya hali ya chini kama haya, hapo hapo tuna mwona kijana wetu, akisogeza mguu wake chini ya uvungu wa kitanda, usawa wa tendegu (mguu wa kitanda) la kushoto, ambako ndiko kwenye mto yani anakoweka kichwa, anakanyaga kwa nguvu kidogo.


Hapo kitanda kijipindua taratibu, kikilalia ubavu, kwa kuegemea upande huu aliosimama kijana, hatuoni upande wapili una nini, ila tuna mwona kijana wetu anazunguka upande wapili wa kitandani, yani sehemu ambayo kitanda kikikaa sawa kunakuwa uvunguni, ambae taratibu anaonekana akitembea na kuzidi kuwa mfupi, mfano mtu anaeshuka ngazi, na anapo malizikia, hapo hapo tuna ona kile kitanda kikirudi tena na kukaa sawa kama kilivyo kuwa mwanzo, hakika inashangaza sana.********


Yap! ndani ya ngome ya dhahabu, yaani Gorden Empire, inayokaliwa na King Elvis, mfalme mwenye elimu kubwa sana, alipata kuitawala nchi hii ndogo yenye utajiri mkubwa, alikuwa chumbani kwake, anajaribu kupitia, nyaraka mbali mbali za mipango na kumbukumbu za siri, zilizowahi kuandikwa na kuifadhiwa na baadhi ya wafalme waliopita, akiwepo baba yake king Eric wa pili, na babu yake king Eugen wa 25, kitu ambacho mpaka sasa yeye mwenyewe hajawai kukifanya, kutokana na kuwa na mipango mingi ya kuitekeleza iliyojaa ndani ya kabati hilo, lililopo ndani ya chumba chake cha kulala.


Elvis anatazama vyema kabati lile kubwa na kuhesabu baadhi ya nyaraka alizowahi kuzipitia, ambazo nyingi alisha zitekeleza, mpaka macho yake yanapo tua kwenye bahasha moja ndogo, ambayo siyo mara yake ya kwanza kuiona, na kuisoma, lakini hakuwai kuelewa maana ya maneno yaliyoandikwa na babu yake king Eugen wa 25 “mume wangu mpendwa, nivyema kama ungelala, kesho nayo siku” ilisikika sauti nyororo tamu toka kitandani, “malikia wangu mpendwa, najuwa unanihitaji sasa, nakuja kwako” alisema Elvis, kwa sauti iliyojaa utani, huku anapeleka mkono wake na kuichukuwa ile bahasha ya kaki iliyofungwa kwa jikamba chekundu, na kuifungua, kisha akatoa karatasi lililopo ndani yake, na kuanza kusoma maandishi yaliyoandikwa kwa wino mwekundu wakuchovya, ni wazi karamu iliyotumika ilikuwa ni nyoya la mwewe, “jamani Elvis, unasema unakuja wakati nakuona unatoa tena ilo karatasi” alisema kwa kulalamika mke wa mfalme Elvis, mwenye asili ya Tanzania, mwanamke ambae alichukuwa nafasi aliyokuwa anaitamani mama wa dhahabu, (soma hadithi ya #KIAPO_CHA_FUKARA.


Elvis nikama alipuuzia lalamiko la Mke wake, na kuweka umakini wake, kwenye lile karatasi, ambalo lilisomeka katika mtindo wa nukuu, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini, lakini siwezi kuibadilisha akili yako, kabla sija kamatwa na kuuwawa, wacha leo niikimbie nchi yangu ninayoipenda, lakini nakuahidi, uwe wewe au kizazi chako, kitakumbuka maneno yangu, nikiweza nitaipigania nchi yangu, mimi au kizazi changu” ukweli yalihitaji tafakari kubwa sana, siyo kwamba hakuelewa maana yake, nini kilifichika ndani ya maneno haya, na aliyaongea nani, hicho ndicho kitu ambacho kilimuumiza kichwa Elvis, na kumfanya awe anarudia mara kwa mara, kusoma maneno haya. ambayo yalikuwa muhimu sana, kwake kuyafahamu undani wake, hasa katika kipindi hiki cha tetesi za kurudi kwa kundi la uasi la UMD.


Wakati Elvis anaendelea kuumiza kichwa, mara akasikia mke akimkumbatia toka nyuma, “aya mfalme wangu, niambie sasa, kitugani kinakufanya unikimbie kitandani” alisema Malkia Vaselisa, huku anamaliza kwa kumkisi mume wake shingoni, na kumfanya mfalme huyu msomi aheme kwa nguvu kutokana na msisimko mkubwa alioupata, “hebu tazama hii Lisa, inawezekana inahusiana na matukio yanayoendelea hivi sasa, hapa nchini kwetu?” aliuliza King Elvis wa kwanza, huku anamwonyesha mke wake huyu, ambae ana shahada ya uchumi, aliyoipata nchini kwao Tanzania.


Hapo Lisa, alie valia gauni jepesi la kulalia, lililoangaza maungo yake ya ndani, anaichukuwa ile karatasi iliyoandikwa kwa mtindo wa nukuu, na kuisoma kwa sauti akitamka kilicho andikwa, “mh! kwani aliandika nani hii?” aliuliza Malkia Vaselisa, huku anaenda kukaa kwenye meza ndogo yenye makasha kadhaa, “iliandikwa na mfalme Eugen wa 25, mwaka 1992, wakati wa tetesi za uasi wa kwanza ujio wa UMD hapa nchini” alijibu King Elvis, na kumfanya mke wake atabasamu kidogo, “sina ufahamu mkubwa kuhusu vita na usalama wanchi, lakini unaonaje ukiongea na babu, anaweza kukueleza chochote” alishauri Vaselisa, huku anaweka ile karatasi kwenye bahasha yake, na kuifunga kama livyo kuwa, kisha ana inuka na kuiweka kwenye kabati, “ni wazo zuri sana Lisa, ndio maana sijawai kujuta kukuoa” alisema Elvis huku ana mgeukia mkewake aliekuwa amesimama mita chache mbele yake.


Vaselisa akaachia tabasamu pana la furaha, “nakuamini mume wangu Elvis, ndio maana najivunia kuwa na wewe, japo mwanzo nilidhania utaniacha mara baada ya kujuwa kuwa Careen (mke wa Peter Jacob, #kiapo_cha_fukara) alikuwa anakupenda sana, zaidi ya kuwa marafiki” alisema Malikia Lisa, huku anamkumbatia mume wake, ambae pia alizungusha mikono yake kwenye kiuno cha mke wake huyo, “mwache rafiki yangu sasa afaidi maisha yake ya ndoa” alisema Elvis huku anacheka kidogo, wakiwa bado wamekumbatiana, “lakini nao wamepitia kwenye misuko suko, mpaka kufunga ndoa, na sasa wanaendelea vizuri na maisha yao” alisema Queen Lisa, huku wanaachiana toka kwenye kumbatio, na kushikana mikono, kuelekea kitandani.********


Naam mwanadada Velonica, akiwa kitandani amejilaza, anawaza juu ya mshangao wa kushtukiza, juu ya birth day, yake na taarifa za baba yake kuhusu kuwa na uwezekano wa kuanza kufanya biashara katika nchi ya asili yao, nchi ambayo baba yake aliondoka kama mkimbizi, mara mawazo hayo ya kupendeza yakamezwa na kumbu kumbu za uondokaji wa mpenzi wake John Joseph, “mbona kama aliondoka akiwa amekasirika” aliwaza Veronica ambae kama siyo lile shuka lake, basi machoyetu, yangeweza kupata kitu zaidi cha kuelezea, maana zaidi ya shuka lile, hakukuwa na kitu chochote, katika mwili wa mwanamke huyu mrembo kuliko hata mke wa mfalme wa mbogo land.


Nime mtaja Queen Lisa, kutokana na uzuri wake, urembo wake, na uvaaji wa vito vya thamani, na ndie ambae anaetajwa na vyombo mbali mbali vya habari na mitandao vya kijamii, changanya na majarida makubwa ya urembo duniani, kuwa licha ya kuwa ndie mwanamke mrembo zaidi, katika wake wa viongozi wa nchi pia nimiongoni mwa wanawake kumi wazuri zaidi duniani, changanya wote unaowafahamu hapo mtaani kwenu, “kwanini ghafla hivi amekuwa na haraka ya kutaka tufanye mapenzi kabla ya ndoa” alijiuliza tena Veronica James, “au ana nia ya kunichezea kisha aniache?” alijiuliza Veronica, ambae kiukweli alisha wahi kuachana na wanaume kadhaa kutokana na tabia kama hii, watatu kati yao, wakiwa tayari alisha wakaribisha nyumbani kwao, na kuwatambulisha kwa wazazi wake…. #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: “kwanini ghafla hivi amekuwa na haraka ya kutaka tufanye mapenzi kabla ya ndoa” alijiuliza tena Veronica James, “au anania ya kunichezea kisha aniache?” alijiuliza Veronica, ambae kiukweli alisha wahi kuachana na wanaume kadhaa kutokana na tabia kama hii, watatu kati yao, wakiwa tayari alisha wakaribisha nyumbani kwao, na kuwatambulisha kwa wazazi wake….


Lakini moyoni mwake alikili kuwa, JJ alikuwa tofauti kabisa na wanaume wengine, hasa katika kukutana kwao, hebu nikujuze kidogo, mwaka mmoja uliopita, mida ya saa mbili usiku, siku ambayo Veronica alihisi machungu ya penzi ambalo ndio kwanza lilikuwa na week tatu, huyo alikuwa ni kijana Elenest, ambae mwanzo alikutana nae shuleni, wakati wanasoma kidato cha sita, na baadae kukutana siku ambayo kijana yule alikuja pale hospital ya mkoa wa pwani, ambako yeye anafanyia kazi,


“hoooo Vero mambo vipi” alisalimia Elenest mara tu walipokutana kwenye valanda la hospital, “hooo! Elenest huyo, poa tu za miaka” aliitikia Veronica, ambae kipindi wapo shule, ilikuwa ni vigumu sana kwa mtu kuipata salamu yake, “namshukuru mungu tupo vizuri, naona unakoti jeupe, inamaana siku hizi ni doctor?” aliuliza Elenest kwa mshangao, “yah! nina mwezi wa sita sasa, vipi wewe hupo wapi siku hizi?” aliuliza Veronica kwa sauti ya uchangamfu, na tabasamu, ambalo lilikuwa linamzidishia uzuri wake usoni, “nipo TRA mwaka wa pili sasa” alisema Elenest, huku macho yake yakikosa utulivu, kwa kumkagua mschana huyu mrembo, “ok! hongera sana, haya sasa nakuona hapa hospital vipi unaumwa au unakuja kikazi, maana nyie watu wa mapato mnamambo yenu” alisema Veronica akimaliza kwa kicheko, “hapana… hapana..mmhh, nime mleta mgonjwa?” alijibu Elenest huku anatazama mlango wa chumba kimoja kilicho andikwa doctor wa uzazi, “hooo hongera naona tayari ndoa imejibu” alisema Veronica kwa utani, huku anacheka kidogo, “hapana sijaoa bado, nime mleta dada yangu, shemeji ameniomba ni fanye hivyo kwasababu yeye gari lake limezigua kidogo” ilo ndilo lilikuwa jibu la Elenest lililotoka haraka sana, ungesema aliulizwa na polisi, “wewe ndie ulieiba” hebu waza jibu lingetokaje.


Basi maongezi yao yaliisha kwa kupeana namba za simu, namba ambazo zilianza kutumika usiku wa siku ile ile, kwa kutakiana usiku mwema, elenest akiwa mchokozi, na ikiwa ndiyo tabia yao kwa kuwasiliana kila siku, mara kwa mara, na kujikuta ndani ya week mbili wamesha tengeneza urafiki mkubwa ulioanza kuzalisha penzi, kwa ahadi ya kufunga ndoa, na yeye akiongeza sharti lake kwamba, hakuna kitumbua bila ndoa.


Jumapili ya week ya tatu, Veronica alimkaribisha Elenest nyumbani kwao, akimtambulisha kama rafiki yake, mbele ya baba yake na huku akimwita mama yake na kumwomba amtathimini mpenzi wake huyo, “anakufaa mwanangu, maana kuchagua sana utaokota kilichooza” alijibu mama mtu, na kumpatia furaha kubwa Veronica, ambae alikuja kuyaona machungu, siku ya alkhamis siku ambayo Veronica alimwona Elenest akija na pale hospital akiongozana na mwanamke flani, ambae yeye alimtambua kuwa ni dada mtu, ambae alikuwa na ujauzito mkubwa tu, wa pata miezi saba au nane.


Kwanza alishangaa kuona mpenzi wake huyo, amekuja pale hospital bila kumjulisha, lakini akaona siyo mbaya kwenda kumsalimia yeye na wifi yake, lakini pia alipokuwa anawasogelea, akaona kama vile wanabishana kitu, “sikiliza Sara, mimi nina kazi nyingi ofisini, siwezi kukaa sana hapa, ukimaliza panda bajaji” alisikika Elenest ambae ni wazi kabisa, hakuwa amemwona Veronica, “lakini mume wangu, unakumbuka doctor alisema kuwa nisitumie usafiri mwingine zaidi ya gari, kuepuka kuharibika kwa ujauzito” alilalamika yule mwanamke, maneno ambayo yalimshtua sana, Veronica, ambae pasipo kujiuliza aligeuka na kurudi ofisini kwake.


Ile anakaa tu, akasikia simu yake inaita, akaitazama na kuona kuwa mpigaji alikuwa ni Elenest, akaikata na kuizima kabisa ile simu, akaiweka kwenye mkoba wake na kubakia na simu ndogo zaidi pale mezani kwake, simu ambayo Elenest hakuwa na namba yake, mara nyingi huitumia kuwasiliana na wazazi wake tu, baada ya hapo akatoka ofisini na kuelekea kwa mganga mkuu, ambako alienda kuomba ruksa kwamba anadharula, alipo kubaliwa akaondoka zake, nakuelekea kwenye gari, akimkwepa Elenest, ambae alikuwa anatembea kuifwata ofisi yake.


Veronica aliingia kwenye gari lake na kuondoka zake, huku moyoni mwake akiwa amejawa na machungu makubwa sana, maana hakujuwa mwanamume yule alikuwa na niagani na yeye, kwamba amwache mke wake amuoe yeye, au lengo ni kuonja kitumbua chake kisha waachane.


Sasa basi usiku wa siku hiyo, Veronica akiwa mwenye machungu makubwa moyoni, akakumbuka kuwa mara nyingi akikosa amani upenda kwenda kusoma hadithi za mwandishi mmoja anae penda sana kusimulia hadithi za nyumbani kwao #mbogo_land, hivyo akachukuwa simu yake aliyoizima na kubadiri chip yake, kisha akaiweka ile nyingine maana haikuwa smart, halafu aka pekuwa haraka haraka namba ya mtu huyo maarufu wa nchini Tanzania, lakini akuiona namba yake, hasa kwenye sehemu ya whatsapp, ujuwe kitu ambacho mwandishi huyu hakijuwagi ni kwamba anawasiliana na watu wengi mashuhuri, na waschana werembo, pasipo yeye kujuwa, maana mara nyingi huwa haitaji utambulisho wao.


Naam licha ya kupekuwa pekuwa sana toka kwenye simu yake, lakini namba ya mtunzi huyo toka Hadithi za Mbogo Edgar, zilikosekana kwenye simu ile kubwa ya kisasa na gharama kubwa ya doctor Veronica, ni wazi iliondoka na ile line iliyotolewa, ndipo alipoingia kwenye Facebook, na kutazama namba ya mwandishi huyu, kwa lengo la kuchukuwa namba, ili wawasiliane nae kwa njia ya whatsapp, kwamba amtumie hadithi kwa kiasi cha fedha ambacho wangekubaliana.


Veronica alifanya hivyo, na baada ya kunakili namba kichwani, akaiweka whatsapp na kuandika ujumbe, “habari mwandishi wangu” akatuma ujumbe, ambao haukutumia hata dakika moja, ukajibiwa, “nzuri tu! lakini samahani umekosea namba mimi siyo mwandishi” ndivyo jibu lilivyosema, na kumfanya Veronica atabasamu kidogo, akijuwa kuwa mwandishi anamfanyia masihara, “kama siyo mwandishi wangu utakuwa nani basi, ebu nitumie story initoe kwenye mawazo” aliandika Veronica akiweka na vile vikatuni (emoj) vya kucheka, kisha ikatumwa na kwenda kwa mtu huto aliedhania kuwa ni mwandishi.


Naam zilipita sekunde chache sana, jibu likaja, “labda unadhani nakutania, ukweli mimi siyo mwandishi wako, labda niwe mchoraji wako, ili nikutoe mawazo” iliandikwa hivyo sms iliyoingia, na kumfanya Veronica acheke kidogo, “haya nimeshindwa mimi, sasa utanitumia au hutaki?” aliandika Veronica na kuituma hiyo sms, kisha kusubiri jibu, “ok! inaonyesha kuwa na uhitaji sana story, unataka nikusimulie kwa mdomo au nikuandikie kwa sms?” jibu hilo lilimshtua sana, Veronica na kuamua kurudi tena Facebook kutazama kama kweli namba aliyoitumia ni yenyewe au siyo yenyewe, ukweli alirudia kufanya hivyo mara kadhaa, mpaka alipobaini kuwa alichanganya namba za kampuni.


Hapo akarudi haraka whatsapp na kuandika ujumbe kwa yule alie kuwa anadhania kuwa ni mwandishi “samahani ndugu yangu, nilikosea namba, naomba sana unisamehe” aliandika Veronica na kutuma ujumbe huo, ambao ulitumwa kwenda kwa mtu yule ambae kwenye picha yake ya jarida aliweka picha ya gari aina ya BMW, mtu ambae alimchukulia kama mstaarabu na mvumulivu sana, mtu ambae mpaka dakika hii, hakuwa ametambua kuwa ni mwanamke au mwanaume.


Sekunde chache baadae Veronica akiwa anasuiri jibu, huku akiwa amesahau kuwasilina na mtu wa hadithi, mara ukaingia ujumbe, kwenye simu yake hiyo, akaufungua na kuusoma, “nilisha kusamehe ndugu yangu, maana binadamu tuna mambo mengi sana yanayo tuandama, haipaswi kuchukia au kumjibu vibaya mtu mwingine maana huwezi kujuwa yupo katika hali gani” ndivyo ulivyosomeka.


Hakika alijikuta akivutiwa na ustaarabu wa mtu huyo, hivyo akajiuliza ajibu nini kwa mtu huyu mstaaabu, alie enda sambamba na hisia zake, lakini wakati anawaza hilo, mara ujumbe mwingine ukaingia, Veronica akaufua ujumbe ambao nikama ulimkosesha amani, “nikutakie usiku mwema” hapo Veronica akaandika ujumbe kwa haraka, “ok! nawe pia, ila siyo mbaya nikikuuliza kitu mchoraji wangu” aliandika Veronica akimalizia na vile vikaragosi vya kucheka, na kuituma kwenda kwa huyo jamaa, halafu akasikilizia jibu, ambalo lilipo ingia alilifungua haraka, kama sms ya pesa, “uliza tu, hakuna shida, lakini siyo kuhusu uandishi” ndiyo ilivyosema, na hapo Veronica akaandika ujumbe wake, “naona tume tumia zaidi ya nusu saa kuchat lakini sijajuwa kama nachat na mwanaume au mwanamke?” kisha akaituma kwenda kwa mchoraji wake,


Ilitumia dakika mbili, mpaka kurudi kwa jibu, “kuna umuhimu wa kujuwana jinsia, ok! mimi ni mwanaume” alijibu mchoraji, na baada ya kuisoma ile sms Veronica akajikuta anatabasamu peke yake, huku anaandika ujumbe, “mimi ni mwanamke kama unaona inafaa kufahamu” na baada ya hapo akaandika ujumbe mwingine, “nikutakie usiku mwema” lakini wakati anatuma kwenda kwa huyo jamaa, na huku ujumbe mwingine ukaingia kwenye simu yake, “ok! nimefurahi kusikia hivyo, nikutakie usiku mwema mrembo, unahitaji kulala mapema, kutunza urembo wako” ujumbe huo ulimfanya Veronica acheke sana, kiasi kwamba hata mlinzi wao huko nje alisikia, “huyu mtu anaonekana mtundu sana, yani anachekesha sana” alisema Veronica, huku anaisave ile namba kwa jina la Mchoraji wangu, kisha akaiweka simu yake kwenye kijimeza kidogo, na bofya switch ya taa pembeni ya kitanda, na giza likatawala mle ndani. #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: “ok! nimefurahi kusikia hivyo, nikutakie usiku mwema mrembo, unaitaji kulala mapema, kutunza urembo wako” ujumbe huo ulimfanya Veronica acheke sana, kiasi kwamba hata mlinzi wao huko nje alisikia, “huyu mtu anaonekana mtundu sana, yani anachekesha sana” alisema Veronica, huku anaisave ile namba kwa jina la Mchoraji wangu, kisha akaiweka simu yake kwenye kijimeza kidogo, na bofya switch ya taa pembeni ya kitanda, na giza likatawara mle ndani.ENDELEA…….


Yap! zilipita siku tatu, pasipo wawili hawa kuwasiliana, lakini siku ya nne, siku ambayo, ilikuwa ni siku ya kumbuku ya kuzaliwa kwa Veronica, mida ya saa nne za usiku, baada ya kuisha kwa kwa hafla iliyoandaliwa na wazazi wake kwaajili yake, akiwa kitandani anasoma jumbe mbali mbali toka kwa watu waliokuwa wanampongeza kwa kutimiza miaka ishirini na tatu, wakijibu status aliyoituma kwenye whatsapp yake, mara akafungua ujumbe toka kwa mchoraji wangu.


Veronica alijikuta anatabasamu kidogo, kisha akafungua ujumbe huo, ambao pia ulijibiwa kwenye status, aliyo iweka usiku ule, mida ya saa mbili, “hongera msomaji wangu, kumbe umezaliwa leo?” ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo, na yeye Veronica akatabasamu, na kuandika wa kwake, “ndiyo, tena sasa nina timiza miaka ishilini na tatu” alipomaliza kuandika akautuma, akutegemea kama kungekuja jibu jingine toka kwa mchoraji wake, lakini haikupita hata sekunde tano, ukaingia ujumbe, “kumbe pacha” ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo, ulimtabasamulisha kidogo Veronica, ambae wakati huo huo akaandika ujumbe “una maana gani pacha?” aliuliza Veronica, na kutuma ujumbe huo kwenda kwa mchoraji.


Ukweli Veronica nikama alichoka kujibu sms za kijana huyu, ambae alionekana kuwa na tudalili za utapeli wa mapenzi, hivyo akataka kuweka simu mezani ili alale, lakini kabla hajaiweka ujumbe ukaingia, nae akalazimika kusoma akipanga kuwa ni ujumbe wa mwisho kuusoma kwa usiku ule, “tumezaliwa siku moja mwezi mmoja, mwaka mmoja” ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo, hapo Veronica akaona wazi kuwa, huyo mchoraji wake anahitaji kublokiwa, maana anaweza kuwa ana nia ya kumteka kihisia ili kumwingiza penzini, na kula kitumua chake, kama zilivyo tamaa za wanaume wengi wanao mfahamu.


Lakini kabla hajafanya hivyo, akakumbuka kitu, “atakuwa amenionea wapi, mpaka atake kunichezea akili” alijiuliza Veronica ambae toka ajiunge na whatsapp hakuwai kuondoa picha ya uaridi, aliyoiweka kama picha ya jarida, “hebu kwanza, alisema Veronica huku anatazama sehemu ya status, na kuanza kukagua status za watu, kilenga status ya mtu alie msave kama mchoraji wangu, ambayo aliikuta chini chini kabisa, ikionekana kuwa yalipita masaa mengi, kabla hajaiposta hiyo status, ambayo Veronica aliifungua, nakuona picha ya mtu mkubwa ilio kolea kwa ukijani,sambamba na maneno yaliyo someka kama ifuatavyo, “kwa mara nyingine nasema asante baba na mama, nimeongeza mwaka mmoja, wakati sasa naweza kusimama mwenyewe” ujumbe huo ulionyesha ulitumwa saa moja za asubuhi, ulimshangaza sana Veronica, na kumfanya agundue kuwa ni kweli mchoraji alizaliwa siku kama aliyo zaliwa yeye.


Haraka sana akarudi sehemu ya ujumbe, ambako alikuta kuna ujumbe kwenye namba ya mchoraji, “naona upo busy, usiku mwema” ilimuuma Veronica, ambae aliandika haraka ujumbe na kuutuma, “hapana nilikuwa bafuni” kisha akautuma kwenda kwa mchoraji, ambako ulionyesha kuwa umeenda lakini haukupokelewa, kwa maana mtumiaji wasimu alikuwa amezima data, Veronica alijihisi mbinafsi sana, roho ilimuuma, akarudi kwenye status na kutuma ujumbe, kupitia posta ya mchoraji, “happy birth day mchoraji wangu” baada ya hapo, akaweka simu mezani na kuzima taa ya pembeni ya kitanda, “atakuwa amechukia pengine ameona nimemdharau kwa kuchelewa kujibu sms” aliwaza Veronica, huku anajifunika shuka mpaka kifuani.


Siyo kwamba alipata usingizi moja kwa moja, alitumia muda mrefu sana kupata usingizi, kulikosababishwa na kuwaza mambo yanayo mtokea kwenye mahusiano yake, ambayo alijipa pongezi kwa kuto kuimbilia dudu, kitu ambacho siyo kwamba akukihitaji, la hasha, kuna wakati alikuwa anajisikia kiu ya kupata dudu, lakini alijizuwia kufanya hivyo, kwa kuzingatia ushauri wa mama yake, katika kutunza mila na tamaduni za kwao #mbogo_land.*****


Naam siku ya pili, Veronica akiwa canteen anapata chakula, ndipo alipochukuwa simu yake, ambayo hakuwa ameishika kwa muda mrefu na kutazama kama kuna ujumbe au missed call yoyote, akakuta jumbe nyingi sana Whatsapp, ambazo nyingi zilikuwa zina mtakia heri ya siku ya kuzaliwa, nae akaanza kujibu moja baada ya nyingine, mpaka alipo ikuta sms ya mchoraji, sijuwi kwanini, Veronica alijikuta anapata na hali mbili kwa wakati mmoja, yani tabasamu la furaha, na hali ya kukosoa kwa kumwona mchoraji ni mmoja kati ya wanaume matapeli wa mapenzi, “mh! yani jana alipokuwa na mke wake, alizima data haraka haraka, halafu sasa hivi ndio kanitumia ujumbe” aliwaza Veronica, huku anaufungua ujumbe huo toka kwa mchoraji, “asante sana msomaji wangu, pia hongera kwa kuwa mtu wakwanza kunitakia heri ya kuzaliwa zaidi wazazi wangu” ndivyo ulivyo sema ujumbe ujumbe huo.


Hapo Veronica akajikuta anatabasamu kidogo, “mshenzi sana huyu, yani ana maneno ya ulaghai” alisema Veonica huku anaandika ujumbe, “mh! ina maana hata mkeo hajakuwish happy birth day?” aliandika Veronica, akimalizia na kiemoj chenye kutoa macho ya mshangao, kisha akaituma kwenda kwa mchoraji wake, ujumbe ulienda lakini uliweka alama ya kujitiki kimoja cheusi, ikionyesha kuwa mtumiaji alikuwa nje ya mstari, yani hakuwa online.


Veronica aliingiwa na kitu kama unyonge hivi, hivyo akaweka simu yake mezani na kuendelea kupata chakula, huku akitafakari mchoraji, ambae kiukweli alijikuta tu akimchukulia kama ndie kipoozeo chake cha mawazo, “sijuwi anaishi wapi na anafanya kazi gani” aliwaza Veronica, huku anachukuwa tena simu yake na kutazama kama ujumbe umepokelewa, akaona bado una kijitiki kimoja cheusi, “au ameishiwa vocha” aliwaza Veronica mtoto wa tajiri mkubwa sana hapa nchini Tanzania, huku anaiweka mezani, na kuendelea kula.


Katika hali iliyo mshangaza hata yeye wenyewe Veronica, akajikuta anakosa utulivu juu ya kutokuwepo hewani kwa mchoraji wake, ambae kiukweli licha ya kuanzisha mawasiliano nae siku nne zilizopita, lakini hakuonyesha dalili za tamaa ya mapenzi, “au yupo na mke wake ndio maana amezima data?” alijiuliza Veronica, huku ana chukuwa tena simu yake na kuitazama, akaona hali ni ile ile, ya kijitiki kioja, hapo akatazama muda wa wisho kwa mchoraji kuwa hewani, akaona ni saa nane usiku, inamaana hata ujumbe wake aliujibu usiku, siyo kama alivyo alivyodhania kuwa alizima data usiku kucha kwaajili ya kuwa na mwanamke, “mh! hebu ngoja” alisema Veronica kwa sauti ya chini, huku anaingia sehemu ya kupiga kawaida, na kupiga namba ya mchoraji wangu, ambayo ilianza kuita mara moja.


Veronica akatulia na simu yake sikioni, huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi, sijuwi alihofia nini, ila ukweli licha ya kupiga simu ile, lakini hakujuw atamweleza nini mchoraji wake, na wakati anawaza hayo, mara simu ikapokelewa.


Kwanza kabisa Veronica alikutana na sauti za ukelele wa watu, ambao nikama walikuwa kwenye mkusanyiko flani mkubwa kiasi, “hallow pacha, mambo vipi?” ilisikika sauti tulivu, toka upande wapili wasimu, Veronica akajikuta anatabasamu, “poa tu, samahani, nilitaa nikujulie hali, maana toka usiku sijakuona hewani, nikajuwa unatatizo” alisema Veronica kwa sauti tulivu, huku tabasamu likiwa limeganda usoni kwake, “hooo asante kwa kunijali, mimi nipo fresh” alijibu mchoraji toka upande wapili wasimu, kwa sauti ile ile tulivu, japo alionyesha kuwa kwenye kelele nyingi sana.


Ukweli nikama Veronica alikosa chakuongea, maana hakuwa na chakuongea, lakini hakukosa cha kuongea, “naona upo kwenye kelele nyingi, vipi unaweza kuwasha data, tukachati, au upo busy?” aliuliza Veronica, huku anajichekesha kidogo, “mh… siyo mbaya… ila ukiona nachelewa kujibu, usishangae maana hapa nipo kazini” alisea mchoraji na kukata simu, akimwacha Veronica anajiuliza kwa mshangao, “mh! kazi gani hiyo sehemu yenye kelele kama hizo” alijiuliza Veronica, huku anaenda kwenye sehemu ya whatsapp, ambako alikuta kumchoraji amesha ingia hewani, na sasa anacharaza, (type) mcharazo ambao haukutumia muda mrefu, ukafwatiwa na kuingia kwa ujumbe.


Veronica ambae akuangaika kusoma sms za watu wengine, akafungua ujumbe ule mara moja na kuusoma, “maisha yenyewe yapo wapi, huyo mpenzi anahitaji matunzo” lilikuwa jibu la ujumbe alioutuma mara ya mwisho, lililomfanya atabasamu kidogo, lakini wakati anajiandaa kuandika ujumbe mala ukaingia wingine, “ninaposema wewe wa kwanza kunitakia heri ya kuzaliwa, nina maana kwamba toka nizaliwe, ukiondoa wazazi wangu, wewe ndio wa kwanza” safari hii baada ya kuusoma ujumbe huo, Veronica akajikuta akianza kuamini alichoa mbiwa.


Hivyo akaandika ujumbe wake, kwenda mchoraji, “usijari kila mwaka nitakuwa nakutakia heri ya kuzaliwa kwako” alipomaliza kuandika akatuma kwenda kwa mchoraji, jibu alikukawia sana, likaingia, “nita nenepa sana” alijibu mchoraji, na hapo Veronica akatania kidogo, “usije kuota kitambi nikakukimbia bure” aliandika hivyo akimalizia kwa vikaragosi vya kucheka, na kuituma kwa mchoraji, ambae alijibu kwa vikaragosi vya kucheka.


Veronica akajikuta anapenda kumfahamu zaidi kijana huyo, “kama haito kuudhi, unaweza kuniambia unaishi wapi na unafanya kazi gani, mchoraji wangu?” aliuliza Veronica na kwenye ujumbe alioutuma, kwenda kwa mchoraji wake, na kisha kutulia kusubiri jibu lake, na muda huo alikuwa amesha maliza kula, dakika tatu zilitimia kabla ya jibu kurudi, tayari Veronica alikuwa amesha nawa, na sasa alikuwa anapata juice tamu ya matunda.


Dakika ya tano, ujumbe ukaingia kwenye simu yake, haraka akaichukuwa simu yake na kutazama ujumbe unatoka kwa nani, akaona kuwa unatoka kwa mchoraji, hivyo akaufungua kwa shahuku, “mimi ni mfanyabiashara ndogo ndogo, nina zunguka kila kona ya jiji la dar es salaam” hilo jibu lilimshangaza kidogo Veronica, ambae alitazama simu yake kwa sekunde kadhaa, kama vile anajiuliza alichoambiwa ni kweli au anataniwa, na wakati anaendelea kujiuliza, mara ukaingia ujumbe mwingine, “wewe je, msomaji wangu, unaishi wapi na unafanya nini?” ndivyo ulivyosomeka ujumbe ule, Veronica alijiuliza dakika nzima, kama kuna umuhimu wa kujibu au laa, maana mtu anae chat nae hakuwa na hadhi yake, hata robo katika robo ya robo, wakati anajiuliza hilo mara akaona ujumbe unaingia, kwenye simu, akaufungua kivivu na kuutazama, “msomaji, bado upo, au hupendi kuchati na wauza vyombo, ok! mchana mwema” ndivyo ilivyosema ile sms.


Ukweli ujumbe ule ulimshtua sana Veronica, na kusisimka kwa jinsi kijana huyu, anavyoweza kusoma hisia zake kwa haraka, “hapana mchoraji wangu, nilikuwa na nawa, siunajuwa hii ni mida ya lunch” alindika Veronica na kuituma, kisha akaandika nyingine kwa haraka, “mimi ni mwanafunzi wa chuo cha biashara mbeya, nipo mwaka wa kwanza, wazazi wangu wapo dar es salaam” kisha akaituma, na kutazama kama zote zimepokelewa, ila ukweli hazikupokelewa, maana zilikuwa na tik moja nyeusi, ambayo kiukweli ilionyesha alisha zima data.


Ukweli jambo hilo lilimuumiza sana Veronica na kujikuta akikosa amani moyoni mwake, maana alijiona kuwa mkosaji, na mbinafsi, kwa kumdharau mchoraji, mara kwa mara alitazama kama ujumbe umepokelewa lakini wapi, hata mida ya usiku, saa nne ndipo alipo uona ujumbe ukiingia kwenye simu yake, ulikuwa unatoka kwa mchoraji, “mambo msomi wa kibiashara?” ilikuwa ni salamu. katika hali ya furaha Veronica akajikuta ameandika asicho kitarajia, “jamani mchoraji wangu, nusu uniuwe kwa pressure kwanini ulitoka hewani ghafla” ungesema ujumbe ule umetumwa kwenda kwa mpenzi wake.


Veronica hakujari hilo, ila alisubiri jibu lake, alipolipata alijikuta anatabasamu peke yake, “pole pacha, wateja walikuwa wengi, si unajuwa tunapambana, ili tusikimbiwe na warembo kama nyie” katika hali ambayo Veronica akujitambua, akajikuta anatamani kumpigia mchoraji wake, katika kuhakikisha kama kweli hakuwa na mke, au alikuwa anadanganya.


Veronica akapiga simu kwa mchoraji, simu ambayo ilipokelewa mara moja, tena bila hata kusubiri, “hallow naona umeshindwa kuchat, ukaona unipigie” ilikuwa sauti nzito, tulivu yenye kusisimua toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo ilimsisimua Veronica, na kumfanya atamani kuendelea kuisikia…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa, jamii forums
 
Taratiiibu sasa muunganiko wa matukio umeanza kuupata umeona dokta vero alivyozama kwa mchoraji ambae hajawah hata kumuona alikosea namba tu, basi usikae mbali nam ujue nn kilijiri
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI: Veronica akapiga simu kwa mchoraji, simu ambayo ilipokelewa mara moja, tena bila hata kusubiri, “hallow naona umeshindwa kuchat, ukaona unipigie” ilikuwa sauti nzito, tulivu yenye kusisimua toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo ilimsisimua Veronica, na kumfanya atamani kuendelea kuisikia…..ENDELEA……


Ukweli jibu lilikuwa mbali kidogo, kwa Veronica, maana ukweli alicho tarajia sicho alicho kutana nacho, “hapana …. nimekupigia nikutakie usiku mwema, maana nimechoka, nataka kulala” alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyojawa na kigugumizi cha aibu, “hoooo! nashukuru kusikia sauti yako Pacha, hakika usiku wangu utakuwa wenye kubarikiwa sana” ilisikika ile sauti tulivu nzito ya kiume, toka upande wapili wa simu, na hapo Veronica akajikuta anacheka kivivu, tena kicheko laini, “yani wewe kwanini unasema hivyo?” aliuliza Veronica, kwa sauti laini sambamba na kile kicheko laini, “si vyema sana kukueleza, lakini sio vyema pia kutumia mali ya mtu bila kumweleza, hakika Pacha unasauti nzuri sana, ungekuwa doctor nadhani wagonjwa wako wangekuwa wanaanza kupona mara tu unapoanza kuwahoji” ilisikika ile sauti nzito na tulivu.


Hapo Veronica akashindwa kujizuwia akacheka tena taratibu na kivivu, “mchoraji wangu unavisa wewe, lakini hata wewe unasauti nzuri” alisema Veronica, na hapo kikasikika kicheko, cha taratibu, toka upande wapili wa simu, “nani kakuambia mwanaume anasauti nzuri, bora ulale mapema, kesho usije kusinzia darasani” alisema mchoraji wa Veronica, na hapo Veronica akakumbuka kuwa alijitambulisha kuwa ni mwanafunzi, kwa kijana huyu, “hilo kwangu siyo tatizo, labda kama wewe unaogopa wifi atakufuma unaongea na mimi” alisema Veronica ikiwa ni kipimo cha uthibitisho, kama kijana huyu, ambae siyo tu kumwona, hata jina halisi hakuwa analifahamu, “kwahilo ondoa shaka Pacha, piga simu muda wowote, tuma sms muda wowote, hata kama ningekuwa na mwanamke asingeweza kunitenga na marafiki” “ilizungumza ile sauti nzito ya upole.


Hakika siyo sauti pekee ila hata maneno ya mtu huyo yali mvutia na kumsisimua doctor Veronica, “mh! inawezekanaje?” aliuliza Veronica, ambae siyo kutaka jibu, ila pia alihitaji kuendelea kuongea na kijana huyu, aisikie sauti yake, “unajuwa mapenzi ni hatua ya mwisho kabisa katika urafiki, na usipo owana na mpenzi wako kinachofwata ni kuachana, lakini urafiki wa kawaida unabakia pale pale, sasa mtu amenikuta na marafiki zangu wanao nisaidia na kuliwaza ninapo kuwa mpweke, halafu yeye aje anitenge nao ili iweje?” japo ilikuwa ni sauti tulivu, lakini ilionyesha kumaanisha kile kilicho tamkwa, “wewe ni mwanaume watofauti sana, natamani siku moja nikuone” alisema Veronica, akiwa anamaanisha kile anachokisema, “usijari, ukirudi likizo nijulishe” alijibu yule kijana.


Naam licha ya kuagana lakini waliongea kwa muda mrefu sana, yakadiliwa masaa mawili yalikatika wakiongea, mpaka Veronica alipoanza kusinzia, wakaagana, na Veronica kupitiwa na usuingizi.


Naam huo ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wa simu , na kijana huyo, alie mpatia jina la mchoraji wangu, urafiki ambao ulizidi kukuwa siku baada ya siku, huku Veronica akishindwa kukuta na kijana huyo ambae licha ya kutamani kumwona, alihofia kugundulika kwa utambulisho wa uongo alioutoa, kwa kijana huyo mfanya biashara wa mitaani, yani machinga, kijana ambae licha ya kuwasiliana nae mara kwa mara na kuongea mengi sana, lakini hakuwai kuomba kukutana na Veronica.


Urafiki wao ulizidi kuwa mkubwa sana, na kufiakia hatua ya kupeaana ushauri, hata Veronica alipopatwa na jambo ambalo lilihitaji kuliwaziwa aliona kimbilio ni mchoraji wake, ilifikia hatua ya kwamba asipo mpata ndani ya lisaa limoja basi angejisikia huzuni kubwa sana, na pengine angeshusha lawama kubwa kwa Mchoraji pindi angempata hewani, ungesema kuwa ni mpenzi wake, urafiki wa simu huo ulikuwa ni wa wazi kabisa, kiasi hata wazazi wa Veronica hasa mama yake aliutambua, lakini hakuutilia mashaka.


Miezi sita baadae, Urafiki ukiwa umekolea kwa wote wawili, siku moja Veronica akiwa anatoka kazini kwake, yani kibaha hospital, alipofika maeneo ya mbezi, akasimamisha gari mbele ya maegesho ya CRDB na kuchukuwa mkoba wake, wenye simu na pochi ya fedha, kisha kuelekea usawa wa madukani, lakini wakati ana pita sehemu flani, kwenye mchanganyiko na mkusanyiko wa watu, mara akajikuta amekumbana na mwanamke mmoja kwanguvu sana, kiasi ha mkoba wake kuanguka chini, “uwe unatazama unakoenda bwana” alisema huyo nwanamke ambae ungemtazama kwa haraka, kutokana na uvaaji wake, ungegundua kuwa hakuwa sawa, ni kama mtumiaji wa uraibu wa dawa za kulevya, maeneo ya mbezi, alisimamisha anaelekea dukani kununua kitu flani.


Ukweli Veronica akuthubutu hata kujibu neno lolote, japo yule mwanamke alionekana kumkumba kwa makusudi, Veronica aliokota mkoba wake na kuelekea dukani, huku akiwa ameingiwa na kitu kama hofu flani hivi, maana tukio lile japo ni lakwaida kutokea sehemu kama hizi, lakini kwa mwonekano wa yule mwanamke ulimtisha sana, akaikumbuka hata ile sauti yamikwaruzo ya kilevi, na hata jinsi alivyo vaa.


Veronica alipo fika dukani, ndipo alipogundua kuwa ameibiwa ni baada ya kukosa pochi na simu zake kwenye mkoba, fedha haikuwa tatizo, tatizo ni kadi za benk, vitambulisho passport za kusafiria na simu zake, hivyo ndivyo vilivyo muumiza na kumletea machungu.


Kwanza alienda moja kwa moja kutoa taarifa kituo cha polisi, ambako wali mfungulia jarida la upotevu, huku wakimshauri kwenda kituo cha redio au television kutoa tangazo, maana waliamini kuwa mwizi asingevitupa vitu ambavyo hakuwa na uhitaji navyo, mfano line za simu, vitambulisho na passport ya kusafiria, ushauri ambao Veronica aliufanyia kazi, kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, hivyo akapanga aende siku ya pili.


Naam siku ya pili alienda kazini, mida ya saa mbili asubuhi, kwa lengo la kuomba luksa, ya kwenda kwenye kituo cha television cha shirika la habari la taifa, lakini alipokuwa katika harakati za kuomba luksa, mara akaambiwa kuna mgeni wake ofisini kwake, “jamani leo sipo kazini nina dharula” alijibu Veronica, ambae ni wazi alionekana kuchanganyikiwa, “dictor ni muhimu ukamwona mgeni wako, ni wazi anajambo muhimu la kukueleza kuhusu vitu vyako vilivyopotea” alielezwa na mjumbe huyo alie mletea taarifa za ugeni.


Kusikia hivyo Doctor Veronica akakimbilia ofisini kwake mara moja, ambako alikuta kijana mmoja mtanashati mwenye wingi wa tabasamu, alie kaa kwenye kiti mbele yameza kubwa ya ofisini kwake, na bahasha moja kubwa iliyo tuna tuna ikiwa mezani, ukweli Doctor Veronica alikuwa kama chizi, alinyakuwa ile bahasha bila kuuliza wala kuambiwa lolote, na kuifungua, na alipoitazama ndani, alijikuta anamtazama yule kijana kwa macho yaliyo jaa tabasamu, “jamani, umevipataje hivi vitu we kaka” aliuliza Doctor Veronica kwa sauti iliyo jawa mshangao huku usowake ukiwa umetawaliwa na tabasamu nono, “hata sija jitambulisha doctor Veronica, hebu tulia kwanza nitakueleza kila kitu” alisema yule kijana, ambae alionekana kuwa mwenye uso wa tabasau pia,.


Hapo Veronica akacheka kidogo, “lazima nichanganyikiwe kaka yangu, yani hapa nilikuwa naomba luksa ya kwenda kwenye vyombo vya habari kutangaza” alisema Veronica, huku anakaa kwenye kiti chake, “ok! naitwa John Joseph Daud, unaweza kuniita JJ” alijitambulisha yule kijana, ambae mwonekano wake ni wakisasa, na utanashati, “nimefurahi kukufahau kaka JJ, yani hata siamini kwa msaada ulionipa, ilikuwaje mpaka ukavipata hivi toka kwa yule dada mwizi?” aliuliza Veronica kwa sauti yenye shahuku ya kujuwa, huku anakagua kitu kimoja baada ya kingine, na kuona kila kitu kipo sawa, mpaka fedha zilizokuwepo kwenye pochi.


Hapo kijana yule mtanashati, yani JJ, akaanza kumsimulia kulichotokea, ya kwamba jana ile jioni, wakati anakatiza mitaa ya mbezi, akamwona yule mwanamke teja, akimkumba yeye Veronica na kumwibia, pasipo Veronica kujuwa kama anaibiwa, hivyo yeye JJ akaamua amfwatilie mschana huyo, mpaka alipo ingia chochoroni na kumkamata akimdanganya kuwa ni polisi, hivyo arudishe vitu alivyoiba la sivyo angempeleka kituoni, ndipo mwanamke yule alipo rudisha kila kitu, “nikajaribu kukufwata kule ulikoelekea lakini sikukuona, lakini bahati nzuri, nikaona kitambulisho chako cha sehemu unayofanyia kazi, ndio nikaona leo nije hapa kukuletea” alieleza JJ, “jamani asante, nimepata kila kitu” alisema Veronica, huku anapekuwa simu yake na kuona missed call na jumbe nyingi za whatsapp, zikiwa zina msubiri, “basi dada yangu, nadhani kazi yangu imeisha, nikuache uendelee na kazi” alisema JJ, huku anainuka toka kwenye kiti, “jamani kaka yangu asante sana, ila siyo mbaya kama utaenda kupata soda” alisema Veronica huku anachapua noti kumi, za elfu kumi kumi, toka kwenye pochi yake, na kumpatia JJ.


Ukweli JJ alionyesha jambo la ajabu sana kwa vijana wakisasa, “hapana dada yangu, siwezi kupokea, nitaonekana kama nimefanya hivyo kwaajili ya kuhitaji fedha, naomba uwe na amani” alisema JJ, huku anaanza kuondoka, “ok! samahani kaka yangu, unaishi wapi, na unafanya kazi gani?” aliuliza Veronica, akiwa na maana kama JJ asingekuwa na kazi basi ange msaidia kupata kazi kwa baba yake.


Hapo JJ alisimama na kugeuka kumtazama Veronica, huku anatabasamu, “kuna umuhimu wa kufahau hayo, ok! lakini siyo mbaya, maana binadamu siyo milima” alisema kijana yule, na kuanza kujitambulisha, “naishi temeke kaburi moja, kwa mjomba wangu, nina miezi miwili toka nimeanza kazi kwenye shirika moja la mawakala wa usafirishaji, la jamaa moja anaeitwa Santana Kibona” alisema JJ, ambae akuonyesha dalili ya kuitaji chochote kwa Veronica, “hooo! baba yangu ni mfanyaboashara mkubwa, na weza kuwaunganisha akatumia kapuni yenu, wakati mwingine” alisema Veronica katika nia ya kumsaidia JJ, ilikurudisha Fadhila.


Hapo Veronika akajitambulisha kiundani na kwa mara ya kwanza akaweka wazi utambulisho wa wazazi wake, kuwa ndie James Carvine, mmiliki wa mkapuni ya JC, “hoooo! kumbe, wewe ni mtu kubwa hivi, siyo mbaya nikipata namba yako, unaweza kuwa msaada huko mbeleni” alisema JJ mara baada ya kusikia utambulisho huo. na hapo wakapeana namba ya simu, na kisha JJ akaaga na kuondoka.


Naam hiyo ndiyo ikawa sababu ya Veronica kufahamiana na JJ, na kuanza kutengeneza mawasiliano mapya kabisa, huku akipunguza mawasiliano na kijana mchoraji, na miezi mitatu baadae wakati mawasiliano na Mchoraji yakikoma ghafla, huku wawili hawa wakianzisha mahusiano ya kimapenzi, na kukubaliana kuowana, hivyo Veronica anamtamburisha JJ kwa wazazi, ambao walimpokea kwa mikono miwili.


Siku zilienda pasipo kupokea ujumbe wowote toka kwa mchoraji, wala kuona kama alikuwa hewani, hata miezi sita ikapita, pasipo mchoraji kuwa hewani, sasa leo mida ya saa mbiili usiku, katika siku yake hii ya kuzaliwa, Veronica akiwa kazini, anapost status, ya birth day yake, ndipo alipoiona stastus ya mchoraji, ikiwa na picha ya nembo ya kampuni ya magari ya BMW toleo la 7, kama profile picha yake, na stastus ikiwa na picha ya kijani na maandishi mekundu, “happy birth day kwangu” Veronica akajikuta akitabasamu mwenyewe, “huyu mshenzi leo nime mnasa, sijuwi alipotelea wapi” alijisemea Veronica.*******


Tuachane na Veronica, sasa turudi miaka ishirini na nne nyuma kabisa, ulikuwa ni usiku wa saa saba, ndani ya msitu mnene, giza nene lilikuwa lime tawara kwenye anga la nchi ya #mbogo_land, mvua kali sambamba na vimeta vya radi, zilizo ambatana na ngurumbo za kutisha za radi hizo, ambazo zlikuwa zina sikika toka kwenye milima ya kalio la Semi (jina la milima iliyopewa jina kutoka na mwonekano wake, uliofanana na mwamke maarufu sana, mwenye makalio makubwa, aliepata kuisi miaka ya nyuma enzi za mfalme eugen wa tatu huko #mbogo_land) …..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Taratiiibu sasa muunganiko wa matukio umeanza kuupata umeona dokta vero alivyozama kwa mchoraji ambae hajawah hata kumuona alikosea namba tu, basi usikae mbali nam ujue nn kilijiri
Sahii
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: Tuachane na Veronica, sasa turudi miaka ishirini na nne nyuma kabisa, ulikuwa ni usiku wa saa saba, ndani ya msitu mnene, giza nene lilikuwa lime tawala kwenye anga la nchi ya #mbogo_land, mvua kali sambamba na vimeta vya radi, zilizo ambatana na ngurumbo za kutisha za radi hizo, ambazo zilikuwa zina sikika toka kwenye milima ya kalio la Semi (jina la milima iliyopewa jina kutoka na mwonekano wake, uliofanana na mwamke maarufu sana, mwenye makalio makubwa, aliepata kuishi miaka ya nyuma enzi za mfalme eugen wa tatu huko #mbogo_land) …..ENDELEA…..


Wananchi wa Mbogo Land usiku huu, walikuwa wamejifungia ndani ya nyumba zao, wakisikiliza kelele za mvua na radi toka nje, japo ni kawaida kwa mvua na radi kama hizi, hasa kipindi hiki cha masika, lakini safari hii hawakuwahi kuzowea hali kama hii, ambayo kikawaida hudumu hata kwa miezi minne, na ukwamisha mambo mengi waliyo ya zowea.


Wakati huo huo magharibi mwanchi hii, kilomita sita toka mpaka wa Tanzania, anaonekana kijana mmoja mwenye umri wa pata miaka 32, alieshika panga moja kubwa, lenye kung’aa, mkono wake wakulia, huku mkono wa kushoto, akiwa amemshika mwamke mrembo, alie beba na mtoto mdogo wa wakiume, mwenye mkadirio wa miaka miwili, akiwaongoza kukatiza kwenye vichaka vinene vya miti na nyasi ndefu, wakati mwingine wakivamia madimbwi makubwa ya maji na yeye kusamdia mwanamke na yule mtoto kujikwamua, kisha kuendelea na safari.


Japo watatu hawa walikuwa katika sura za taharuki na kwa kile kilicho watokea, lakini hakuna alieonekana kutokwa na machozi wala kuangua kilio, siyo yule mwanaume wala mwanamke au huyu mtoto, na mtoto huyo ndie ambae, leo ndio tutapata kumfahamu vyema, huyu anaitwa Deus Frank Nyati, ndie Dereva wa BMW 7 jeusi.


Hiyo ilikuwa ni mwaka 1992, Deus akiwa na miaka miwili, zina zagaa tetesi za harakati za kimapinduzi, zilizo ongozwa na kikundi cha Harakazi za Uhuru kwa Damu, kilicho ongozwa na askari mtoro alie asi jeshi la MLA, (Mbogo Land) huyu ni Erasto Kadumya, alietoroka jeshini akiwa na cheo cha kanal, japo ilisadikiwa kuwa yeye amechaguliwa kama mtendaji mkuu, wa kikundi hicho cha UMD, ambacho kilianzishwa kwa kusudia la kuondoa utawala wa kifalme, na kuleta mfumo wa uongozi wa kawaida, ya ni uongozi wa kuchaguliwa, ule wa kuwa na Rais, wabunge na mawaziri.


Lakini kuna watu walikuwa nyuma ya hilo, tena ni watu wenye nafasi na hesima kubwa ndani ya nchi hii, ndogo nzuri yenye utajiri mkubwa, na serikari kwa kulijuwa hilo, likatumia kikundi chake maalumu cha MLSA (Mbogo Land Secret Agent), chini ya usimamizi wa Agent mpya aliechukuliwa toka MLA, Major Dickson Chitopelah, likaanza kuwasaka wahusika na mamluki waliopo ndani na nje ya serikali, wanaoshirikina na kikundi hicho, ambacho kilikuwa ndani ya misitu minene ya Kalanga Njete, misitu mikubwa, inayo ungana mistu ya nchi za jirani za Tanzania upande wa kusini, na msumbiji upande wakaskazini, misitu yenye sifa za kuwa na wanyama wa kila aina, misitu ambayo nchi zote tatu, hutumia kama sehemu ya utalii.


Naam kazi ya MLSA, wenye watu kila idara, ndani ya nchi hii, ilifanikiwa ndani ya muda mfupi sana, ungesema kuwa tayari walikuwa wanawafahamu toka mwanzo watuhumiwa wao, ambao walipo wakamata tu, walipewa adhabu kali, na mwisho kuuwawa kwa mateso makubwa, vifo ambayo vilimshtua kila mmoja, wakiwepo MLSA wengine.


Mfano, mtuhumiwa mmoja alichukuliwa na kufungiwa kwenye pipa la chuma, lenye mfuniko mkubwa na mzito wa chuma, ambao ulipigwa kufuri kubwa ya chuma, na kisha kuwekwa juu ya jiko kubwa la makaa ya mawe, ambalo utumika kuyeyushia dhahabu, au vyuma na vitu vingine vingumu, huku mtuhumiwa akiwa ndani ya jungu ilo la chuma, maarufu kama iron port.


Achana na hiyo sasa kuna ile ambayo, mtuhumiwa alie maliza kuhojiwa, ange chukuliwa na kufungwa mikono na mikuu, kisha kuwekwa ndani ya chumba kidogo chenye panya wengi wenye njaa, ambao wangeanza kumtafuna taratibu, ambapo siku ya tatu, tayari mtu huyo angekuwa amesha poteza maisha, na kama haitoshi mkuu wa operation, aliamuru familia za wahusika na watu wao wakaribu nao pia kuteketezwa, yani ndani ya weeke mbili, tayari familia sita zilikuwa zime toweka, na kitu cha kusikitisha na kushangaza ni kwamba, watu wengi walio uwawa ni watu ambao kwa namna mmoja au nyingine, walikuwa ni nguzo muhimu katika vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi ile, ndogo na tajiri.


Mbaya zaidi ni kwamba, wengi walio kamatwa na kuuwawa hawakuwa na hatia, yani hawakuwa washirika katika mapinduzi ya UMD (Uhuru kwa Mapinduzi ya Damu), na katika hali ambayo ilimshangaza bwana bwana James Carvie, ambae ni mfanyabiashara mkubwa pale #Mbogo_land, ni kuletewa taarifa ya siri toka kwa mtu ambae hakumfahamu, kuwa na yeye ni mmoja kati ya wa tuhumiwa, na kwamba anashutumiwa kufadhiri kikundi hicho chenye lengo la kufanya mapinduzi, kwa njia ya umwagaji damu.


Ukweli hakutumia hata masaa ishirini na nne, kutoa fedha zake kwenye account zake za benk, na kutoa kila alichokiona kuwa kitamsaidia huko aendeko, na kisha kukimbilia nchini Tanzania, akiwa na mke wake na mtoto wake mmoja wakike, mbako alipokelewa na kupewa kibari cha kuishi kama mkimbizi wa kiasa, huku nchini kwake, yani ndani ya nchi aliyoipenda, zikianza kuzagaa habari za kwamba, bwana James Carvine, ndie mfadhiri mkuu wa kundi la UMD, na kwamba anasakwa na serikali ya nchi ya Mbogo Land popote alipo, jambo ambalo siyo yeye pekee, ila liliwashangaza watu wengi sana, wakiwepo baadhi ya viongozi wa nchi ya Mbogo Land, na nchi jirani, huku wakipiga simu kwa king Eugen, wakimtaka atazame upya namna ya kuendesha operation yake, japo haikusaidia, yeye alikuwa anafanya kila linalowezekana kabla hajakabidhi nchi kwa kijana wake Eric, ambae sasa alikuwa anasoma huko nchini Tanzania (soma UMEKOSEA LAKINI TAMU)


Shutuma hizo zilienda pia kwa watu wengi wengi sana, ambao walikamatwa na kuuwawa, wakiwepo askari wengi ndani ya jeshi la MLA, pia baadhi ya walinzi wa ikulu, ya golden empire, jambo ambalo lilimshtua sana, askari mtiifu na mlinzi hodari wa Mfalme, na kumfanya atilie mashaka juu ya operation iliyokuwa inaendelea pale nchini Mbogo Land, hivyo akaenda moja kwa moja kwa mkuu wa operation ile.


Naam kweli bwana Frank Nyati, alimkuta Kanal Chitopelah, ofisini kwake, na kumpa salamu zote za heshima, alizostahili kuzitoa kwa kamanda huyo, ambae aliitikia kwa namna flani ambayo haikumpendeza Frank, “eleza shida yako, nina mambo mengi” alisema Chotepelah, pasipo kumtazama usoni bwana Frank Nyati, “mkuu samahani, nadhani kwa heshima na sifa ya nchi yetu, nivyema kama ukitazama upya namna ya kuendesha hili zoezi la kuwasaka waasi, ni vyema ukawafanyia mahojiano ya siri, ilikubaini kama taarifa ulizonazo ni sahihi au siyo sahihi” alishauri bwana Frank Nyati, ambae kipindi hicho alikuwa na cheo cha luten kanal, ambae aliongea kwa sauti yenye nidhamu kubwa na unyenyekevu.


Lakini ilikuwa tofauti kidogo kwa bwana Chitopelah, ambae aliinu uso wake na kumtazama Frank kwa jicho kali, lenye maonyo, na hasira, “kwahiyo unajaribu kukosoa maamuzi yangu, unajuwa ukinikosoa mimi, ni sawa ume mkosoa alienipa mamlaka haya?” aliuliza Chitopelah, kwa sauti ya taratibu, lakini iliyojaa hasira, huku bado amekazia macho Frank, “samahani afande sijakosoa, nimeshauri, maana naona kama vijana wanakamata watu ambao ndio nguvu kuu ya ulinzi na usalama, nikama tuna mrahisishia adui kuja kufanikiwa kile anacho kusudia” alisema Luten kanal, Frank, pasipo kubabaishwa na mwonekano wa Chitopelah, jinsi alivyo kuwa anamtazama kwa jicho la ukali lenye chuki na hasira.


Ukweli kwamba kujiamini kwa Frank, hakukumpendeza Chitopelah, ambae alionyesha kuchukizwa zaidi, “ok! kwahiyo wewe ndio unaijuwa nguvu ya nchi siyo, basi utakuwa unajuwa mambo mengi zaidi, nadhani itakuwa vyema kama utakuja kutueleza unacho kijuwa zaidi” alisema Chtopelah, kwa sauti ile ile yenye chukizo, japo safari hii, ilikuwa na hasira ndani yake, lakini ilikuwa tofauti kwa Frank, ambae aliachia tabasamu, lenye uchungu ndani yake, “ingekuwa vyema kama ukianza kuhoji watu wako, kabla hujanifikia mimi” alisema kisha akaweka mkono wake kifuani, na nakuinama kidogo, kama ishara ya kuaga na kisha akaondoka zake, akiufwata mlango wa kutokea na kutoka nje, kisha akaondoka zake mazima, huku kichwani mwake akitafakari jambo, juu ya majibu ya Chitopelah.


Frank alipofika kazini kwake, yani ndani ya makazi ya mfalme, akatulia na kuwaza sana juu ya mwonekano wa Chotopelah, na vile alivyokuwa anatoa majibu, kama vile alichukizwa na hakupenda kile ambacho alimweleza, ukweli Frank alitamani kuongea na Mfalme juu ya jambo lile lile alilo ongea na Chitopelah, lakini hakupata nafasi, maana Mfalme alikuwa katika vikao na wazee wa baraza.


Naam usiku saa tano, mvua kubwa ikiwa inanyesha, Frank Nyati, akiwa chumbani kwake na mke wake, alie kuwa anambembeleza mtoto Deus alale, mala ghafla umeme ukakatika, mwanzo flank alijuwa ni kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, ndio maana umeme umekatika, lakini alishtuka baada ya kuona mwanga wa taa za umeme, kupitia nyumba za jirani, uliokuwa unaendelea kuwaka, hapo Frank, akajuwa kuwa kuna jambo halipo sawa, pengine sasa Chotopelah, amekuja kumchukuwa, ili wakafanye mahojiano.


Naam haraka sana Frank akakimbilia dirishani, na kuchungulia kwa tahadhari, akawaona watu kadhaa wakiwa wanaisogelea nyumba yake kwa kwa mwendo wa tadhari, huku mikononi mwao, wakiwa na silaha, ambazo kwa haraka haraka hakuweza kuzitambua kutokana na giza lililotanda maeneo ya nyumbani kwake, japo kwa urefu wa mitutu ya bunduki zile zilizo fanana na Uzi gun, ni wazi zilikuwa na viwambo vya sauti, hapo Frank, akarudi haraka kitandani, “baba Deus kunani…?” kabla mke wake ajamaliza kuuliza akamziba mdomo, “shiiiii” Frank alionyesha ishara kwa mke wake ya kukaa kimya, kisha akamshikatoka kitandani na kukimbilia kwenye moja ya kabati, lililopo mle chumbani, akapeleka mkono juu ya kabati ilo, na kuibuka na panga moja refu, lenye kung’aa sana, kutokana na makali yake, kiasi wamba licha ya giza lililotanda ndani, lakini ungeweza kuliona.


Mama Deus au mke wa bwana Frank, alimwona mume wake akiusogelea mlango kwa tahadhari kubwa, na kutoka nje, kisha akafunga mlango, akiwaaca yeye na mtoto wao wapekee yani Deus, wakiwa kitandani wanashangaa kinachotokea, uoga ume watawala, kiasi cha kutetemeka miiliyao, maana hawakujuwa A wala B. …..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Mama Deus au mke wa bwana Frank, alimwona mume wake akiusogelea mlango kwa tahadhari kubwa, na kutoka nje, kisha akafunga mlango, akiwaaca yeye na mtoto wao wapekee yani Deus, wakiwa kitandani wanashangaa kinachotokea, uoga ume watawara, kiasi cha kutetemeka mmiliyao, maana hawakujuwa A wala B. endelea……..


Wakati mama Deus aliekuwa ameshikwa na uoga mkubwa, anashangaa na kujiuliza, mara akasikia kishindo kikubwa cha kuvunjwa kwa mlango, kilicho fatiwa na kelele za vilio vya maumivu, toka kwa binadamu wa kiume, huko sebuleni sambamba na vishindo vya panga, ambayo vilidumu kwa kwa dakika nzima, kisha ukapita ukimya mfupi, uliovunjwa sekunde chache baadae.


“usiniuwe.. usiniuwe Frank sisi tumetumwa na Chitopelah” ilisikika sauti ya mwanaume akilalamika, “umetumwa kujakufanyanya” aliuliza Frank kwa sauti kavu ya kikatili, ambayo mama Deus hakuwahi kuisikia hata siku moja, “tume ambiwa tukuuwe wewe na familia yako yote, namba usiniuwe Frank, ningekataa ningeonekana muasi, na mimi ningeuwawa na Familia yangu” alilalamika huyo mtu toka sebuleni, “ok! kwahiyo wewe na wenzako mnafahamu anacho kifanya Chitopelah siyo?” aliuliza Frank, kwa sauti ya ukali, “ndiyo…. hapana ….hapana sijuwi chochote, yeye anatutuma tu” alisikika huyo mwanaume akiongea kwa haraka haraka, katika hali ya kujitetea, hapo kikafwatia kishindo kiukubwa cha kupigwa kwa mtu, kikifwatia na anguko la mtu mzima, “puuuuh!”


Hapo vikafwatia vishindo vya mtu vikija upande wa chumbani, yaani chumba ambacho alikuwepo mama Deusi na mwanae, ambae sasa alikuwa amemziba mwanae mdomo kwa kuofia kupiga kelele, maana hakujuwa kama aliekuwa anasogelea chumba ni mume wake, au yule mwingine mwenye kuomba msamaha, hata mlango ulipofunguliwa chumba ulipofumuliwa, ilibakia kidogo amwage mikojo kitandani, “mjinga sana, Chitopelah, hawezi kutufanya wajinga muda wote” alisema Frank, huku anasogelea kwenye meza yenye simu, kipindi hicho simu zilikuwa za mezani, ambazo utumia umeme wake zenyewe, “wakina nani hapo baba Frank” aliuliza mama Deus kwa sauti iliyo jawa na uoga, akiwa pale pale kitandani, “mawakala wa siri wa usalama wa taifa, niwazi wanampango mbaya juu ya taifa, wacha nitoe taarifa hii kwa mfalme, vinginevyo wataipindua nchi muda siyo mrefu” alisema kwa haraka bwana Frank, huku anakamata mkonga wa simu, na kuanza kubofya namba flani flani, kisha akaweka sikioni.


Naam simu haikuchukuwa muda mrefu ikapokelewa, “nijulishe Chitopelah, vipi tayari Frank amesha kamatwa?” ilisikika sauti toka upande wapili, sauti ambayo ilimshtua na kumshangaza Frank, ambae aligeuka na kuitazama familia yake, kwa macho yaliyojaa fadhaha, “hallow! nani mwenzangu, mbona kimya?” iliuliza sauti toka upande wapili wasimu, sauti ambayo, Frank hakuwa na shaka kuwa, anaeongea nae alikuwa ni mfalme mwenyewe Eugen, maana namba za simu hiyo, ni namba ambazo walikuwanazo watu wachache sana, katika serikali, simu ambayo hupokea mfalme mwenyewe, simu ambayo hutumika kutokea taarifa za siri, inamaa mfalme anafahamu, na amebariki swala la yeye kukamatwa na kuuwawa.


Ukweli ilimvunja nguvu bwana Frank, ambae alikumbuka baadhi ya matukio ambayo aliyafanya, katika ulinzi wa taifa lake, pasipo kupewa tuzo yoyote, wala kukumbukwa kama shujaa, na matokeo yake leo anahesabika kama muasi katika taifa lake pendwa, “Ni mimi Frank, mtukufu mfalme, mfuasi wako mtiifu, ambae nimekutumikia muda wote, kwa utihifu na kujitolea, pasipo kukiuka wala kujali maslahi yangu” alisema Frank kwa sauti ya kikakamavu, huku machozi yakimtoka macho pake.


Hapo ikasikika sauti ya pumzi ndefu ikishushwa, ukweli Mfalme hakutegemea kama Frank angepiga simu muda ule, “Frank, kwanini sasa umegeuka na kuamua kusaliti nchi yako Frank, eti kisa hujahesabiwa kama shujaa?” aliuliza mflame, kwa sauti ya ukali, na kuzidi kumtoa machozi Frank, “sijawai kuisaliti nchi yangu, wala kufikilia kuisaliti nchi yangu, najuwa hujuwi kuwa unashiriki kuisaliti nchi ya babu zako, ambayo unatakiwa kuikabidhi kwa mwenyew kijana Eric” alisema Frank kwa sauti ile ile ya kikakamavu, huku machozi yakiendelea kumtoka machoni pake, “unamaanisha nini Frank, unajaribu kunivuruga akili, ili wewe na wenzako muweze kufanikisha mapinduzi?” aliuliza mfalme Eugeni kwa sauti ya ukali.


Swali na namna ya uulizaji wa mfalme Eugen vilimuumiza sana Frank, ambae alieugulia maumivu moyoni mwake, “hicho ndicho kinachofanywa na watu unao waamini, lakini siwezi kuibadirisha akili yako, kabla sija kamatwa na kuuwawa, wacha leo niikimbie nchi yangu ninayoipenda, lakini nakuahidi, uwe wewe au kizazi chako, kitakumbuka maneno yangu, nikiweza nitaipigania nchi yangu, mimi au kizazi changu” alisema Frank, na kukata simu, halafu akasogelea lile kabati la nguo, na kulisogeza pembeni kwa nguvu zake zote, maana lilikuwa zito sana, baada ya hapo, akafukua kidogo pale alipoondoa kabati, na kubomoa kipande cha sakafu.


Mama Deus anamwona mume wake, akifukua kwenye ile sehemu aliyobomoa, na kisha kuibuka na kijifuko kidogo sana cha ngozi, mfano wa pochi za kale, akaingiza mkono ndani yake na kuibuka na vipande kadhaa vya mawe vyenye kung’aa, halafu akavirudisha ndani ya kile kifuko cha ngozi, halafu akafungua moja kati ya drow za lile kabati na kuchukuwa kibunda cha fedha, cha noti za 1oo ML sh, fedha yanye nguvu na thamani ukanda wa afrika mashariki na kusini na kati, na sehemu nyingi duniani.


Baada ya kuziweka mfukoni, akamgeukia mke wake na mwanae, waliokuwa kitandani, “mama Deus hapa siyo sehemu salama kwetu, mchukue mtoto nifwateni” alisema bwana Frank, kisha yeye akasogelea dirisha na kuchungulia tena nje, akawaowa watu zaidi ya kumi, ambao walivalia mavazi tofauti na sare na MLSA, ni kama wale ambao walikuja mwanzo.


Watu hao kama wale wamwanzo, waliobeba bunduki zao fupi, zenye mitutu mirefu, walionekana wakitembea kwa tahadhari kubwa, katika mvua kubwa na ya kutisha, kuifwata nyumba yake, “wapuuzi” alisema Frank Nyati kwa sauti ya chini, huku anaufwata mlango na kutoka haraka sana kuelekea sebuleni, huku mke wake, aliembeba mtoto wa miaka miwili akimfwata.


Naam, mke wa bwana Frank, yaani mama Deus, anawona mume wake anaokota bunduki toka kwa mmoja kati ya watu waliolala chini, pale sebuleni, halafu ana mtazama mke wake na kumpa ishara ya kwamba warudi chumbani, na hapo mama Deusi anafanya hivyo, yaani anarudi chumbani haraka sana, akiwa na mwanae mkononi.


Baada ya kuhakikisha mke wake na mwanae wamesha rudi chumbani, Frank alijibanza pembeni ya mlango, akiwa na Uzi Gun yenye kiwambo cha sauti, kisha akachungulia nje, kwa umakini mkubwa sana, akawaona wale jamaa wanaoisogelea nyumba yake, wakiwa umbali wa mita kama ishirini, wakija kwa tahadhari kubwa, na silaha zao mikononi, mitutu wameielekezea kwenye nyumba ya bwana Frank.


Frank aliweza kuona mmoja wao, akionyesha ishara ya kuwa watawanyike na kuizunguka nyumba ile, hapo Frank akaishika ile Uzi Gun na kufungua mtutu wa kuzuwia sauti, silent barrel, yani kiwamba sauti, na alipoitoa akaikoki ile Uzi Gun kisha aka itupia nje ya nyumba.


Kuna jambo hapo inabidi ulielewe, kwa itendo hiki alicho kifanya Frank, nikwamba silaha hii aina ya Uzi, Uzi ni jina la kiebrania lenye kutamkwa U-zi, ni mfumo wa bunduki ndogo za mitambo ya bolt, iliyoanza kutetengenezwa na Major Uzel Gal, wa jeshi la ulizi la Israel (IDF), mwishoni mwa miaka ya 1940, na kuanza kutumika, mwaka 1950 na majeshi ya IDF, (Israel Defence Force) ,ikiwa ni miongoni mwa silaha za kwanza kabisa, kutumia mtindo wa kuweka risasi kwenye mikebe, yani Magazine yenye uwezo wa kubeba risasi 25, ina uzito wa kilo nne kama itawekewa na mkebe wenye risasi 25.


Silaha hii ndogo na fupi yenye kubebeka kirahisi, inauwa vizuri ndani ya mita hamsini mpaka mia moja, na ni nzuri kwa mapigano ya kwenye maeneo yenye majengo, yani FIBUA, (Fighting In Bulding Area) hasa kwa umbali wa mita mia moja mpaka mia moja hamasini, mwanzo ilitumika kupigania mstari wa mbele, lakini baadhi ya majeshi, wameitoa kwenye mapigano ya ana kwa ana, na sasa uitumia kwa uvamizi wa siri, au hutumiwa na askari wa uchunguzi. huku wakiiboresha na kuiwekea silent barrel, iwe rahisi kwa kazi za kuvizia.


Ukiachana na tabia hizo za Uzi Gun pia kuna sifa moja kama siyo mapungufu ya silaha hii, ambayo haikuwekwa kwenye Orodha ya sifa na tabia za silaha hii, japo hutolewa kama tahadhari ya kwamba, usi idondoshe ikiwa au kugongesha sehemu ngumu silaha hii, ikiwa na risasi kwenye chamber (chemba) maana bolt yake ni nyepesi kusukuma nyundo, ambayo ugonga pin ya kupigia kitako cha risasi, na kama ujuwavyo, hii pia ni kama AK 47 au SMG, ni automatic sub machine gun, hivyo basi kila risasi inapolipuka na kichwa kuondoka, kupitia mtutu, mitambo kurudi nyuma kutokana na hewa nzito ya baruti iliyo ungua, kutoa ganda na kusababisha mtikisiko, ambao ungeifanya ile silaha, kuruka kidogo, na kujibamiza tena chini, na kutokea kitendo kama kile cha mwanzo, hivyo kuendelea kufyetua risasi paka zitakavyoisha kwenye mkebe wake, au endapo litatokea tatizo la missed fire, yani risasi kutokulipuka, kutoka na baruti kuganda kwenye ganda la risasi.


Hiyo ndiyo akili aliyoitumia bwana Frank, ambae baada ya kuitupa ile silaha na yeye akakimbilia upande wa jikoni, na kuufungua mlango wa kutokea nje, halafu akarudi ndani, na kuelekea kule alikoielekezea familia yake, yani chumbani, huku silaha aina ya Uzi, ikiendelea kukooa, na kitu kingine ambacho ulikuwa hukifahamu ni kwamba silaha hii ikiwa bila kiwamba sauti inatoa mlio flani wa kupendeza masikioni mwa watu wanaopenda vita.


Frank akaingia chumbani na kumkua mke wake, akiwa amejibanza kwenye kona karibu na kabati, huku amemshika mtoto Deus, “nifwate” alisema bwana Frank, huku anafungua mlango wa chumba bafuni, na mke wake akamfwata, huku amembeba mtoto, wakati huo milindomo ya risasi ikiendelea kusikika toka nje, maana hata wale jamaa pia walianza kupiga risasi hovyo hovyo.


Bafu lilikuwa lenye upana wa futi sita kwa nane, ukiachilia sink la choo, pia kulikuwa na sehemu yenye bomba la mvua, na sink la kunawia, Frank akasogelea sink la kunawia, ambalo lilikuwa lime nasishwa ukutani, akagusa chini ya sink lile, na baada ya hapo akalikamata lile sink na kulivuta hapo nalo likavutika na kipande cha kama ukuta, ambacho ukitazama vizuri, unagundua kuwa ni mlango mdogo, uliotegenezwa kwa kipande chuma.


Japo kulikuwa na giza, na sehemu ile ilikuwa na giza zaidi, lakini kitu ambacho siyo mimi peke yangu, hata mke wa bwana Frank, alishangaa, kuona sehemu ambayo kila siku alikuwa anatumia kupigia mswaki, na kunawa uso, kumbe kuna mlango, na wakati mama Deus anaendelea kushangaa, huku nje ya nyumba milindimo ya risasi ikikoma, na ukimya mkubwa kutawala, mama Deus aliweza kumwona mume wake akiingiza mkono ndani ya kile kimlango chenye ukubwa wa dirisha la choo, na kuibuka na tochi mbili, akaiwasha ya kwanza na kumkabidhi mke wake, “ingia haraka” alisema bwana Frank, kwa sauti ya kunong’ona, huku ana mchukuwa mtoto Deus toka kwa mama yake, wakati huo walikuwa wanasikia vishindo vya watu, wakiingia ndani ya nyumba, huku mvua ikiendelea kunyesha kwanguvu.


Mama Frank akiwa na tochi mkononi, akaingia ndani ya kijimlango kile, kwa kutanguliza miguu, ambapo miguu yake iligusa ngazi, na baada ya hatua mbili, akakanyaga aridhi, “mpokee huyo” alisema bwana Frank, huku anampatia mtoto Deusi, ambae muda wote alikuwa anatazama kila kilichokuwa kinatokea usiku ule, hakika ilikuwa jambo geni na la kutisha sana kwake, lakini uwezi kuamini ujasiri wa mtoto huyu, ambae akuonyesha uoga wala wasi wasi, uso macho yake yakiwa makavu kabisa, pasipo dalili ya machozi wala kilio. …..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom